MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
“Mungu wangu…..!! Umezinduka?”
Phidaya alizungumza huku akipiga magoti chini, akakinyanyua kichwa cha Black Shadow, akakiweka kwenye mapaja yake, akijaribu kumpa huduma ya kwanza mgonjwa, macho ya Eddy yaliyo jaa machozi ya maumivu makali ya mbavu zake zilizo piga chini, alipo kuwa akijaribu kunyanyuka kitandani ili kumuona mwanamke mwenye sauti ya inayo fanana na Phidaya, yakatua usoni mwa nesi huyo, akajikuta akistuka kwani ni Phidaya mwenyewe, ndiye aliyepo mbele yake akimuhudumia.
ENDELEA
Kwa haraka Phidaya, akakiweka kichwa cha Black Shadow chini, akamnyoosha ili asiendelee kujikunja na kusabaisha nyuzi alizo shonwa kwenye mbavu kuachia. Akatoa simua yake na kumpigia daktari msaidizi wa dokta Ranjiti, akamuelezea hali ya mgonjwa aliyo kuwa nayo.
“Phidaya……”
Black Shadow akajitahidi kumuita Phidaya na kumfanya astuke na kumtazama mgonjwa wake.
“Unalijua jina langu…..?”
“Phid….aa…ya mk……”
Black Shadow hakumalizia sentensi yake akatulia kimya akazimia tena. Phidaya akazidi kuchanganyikiwa ndani ya dakika moja mbeleni daktari akafika akiwa na dawa maalumu za kupunguza maumivu, wakasaidia na Phidaya kumnyanyua Black Shadow na kumrudisha kitandani mwake. Dokta akamfantia uchunguzi wa haraka, cha kumshukuru Mungu hapakuwa na itilafu iliyo weza kujitokeza kwenye mshono wake.
“Amepoteza fahamu kutokana na muumivu makali sana”
Dokta Yan alimuambia Phidaya aliye onekana kuwa na wasiwasi mwingi.
“Ila dokta Yan, huyu mgonjwa anaonekana kama kunijua mimi”
“Kukujua wewe kivipi?”
“Ameniita jina langu la Phidaya”
Dokta Yan akabaki akiwa na mshangao asijue ni kitu gani kinacho endelea. Kila mara Phidaya akajikuta akijifuta jasho usoni mwake na kitambaa chake, mapigo ya moyo wake hayakutulia kabisa kiasi cha kumfanya ahisi kuna jambo ambalo Black Shadow analitambua, isitoshe maneno yake ya mwisho yaliyo katika katika alipokuwa akizungumza ndio yalizidi kumchanganya.
“Hivi atazinduka kweli?”
“Ndio nesi atazinduka, ila itamchukua kama masaa mengine tisa hadi kumi, kwa maana sindano nilkiyo mchoma inapunguza mumivu taratibu taratibu”
“Isije akawa akaka kwa muda mrefu kama alivyo kaa?”
“Hapana atakuwa salama tu nesi, ila nikuulize swali?”
“Uliza tu”
“Mbona una wasiwasi mwingi sana juu ya huyu mgonjwa tofauti sana na mara ya kwanza?”
“Kusema kweli dokta Yan mimi sielewi kabisa kichwa change, nahisi kuna kitu ambacho najaribu kukikumbuka ila nashindwa kujua ni kitu gani hicho”
Macho yakamtoka dokta Yan, wasiwasi mwingi na yeye ukamtawala ila akajikaza asiweze kuuonyesha mbele ya Phidaya. Akamuomba Phidaya aondoke akaendelee na kazi zake. Phidaya hakuwa na hiyana yoyote kwa daktari huyo msaidizi wa mume wake. Akaondoka na kuelekea ofisini kwake akamuacha Phidaya akiwa amesimama jirani kabisa na kitanda cha Black Shadow.
Phidaya kwa mara nyingine, akajikuta akianza kumvua Black Shaodow kinyago alicho kivaa, akafanikiwa kumaliza kukivua kinyago hicho na kukishika katika mkono wake wa kushoto. Sura nzuri ya Black Shadow, ikamfanya aitazame kwa muda mwingi sana zaidi ya dakika kumi.
Wazo moja likamjia kichwani mwake, akatoa simu yake na kuingia upande wa kamera kisha akampiga Black Shadow picha nne, alipo maliza akamvalisha kinyago chake kama kilivyo kuwa na kutoka zake ndani ya chumba hicho.
***
“Ndio dokta kuna jambo nahitaji kukuambia”
Dokta Yan, alizungumza kwenye simu yake mara ya kuingia ofisini kwake na kujifungia kwa ndani. Simu hiyo iliyopo hewani, anazungumza na dokta Ranjiti akiwa ndani ya gari akirudi kutoka kwenye mgahawa alipo kwenda kuonana na Kim.
“Jambo gani hilo?”
“Ni kuhusiana na mke wako”
“Amefanyaje?”
“Nahisi anaanza kuutafuta ukweli juu yake”
“Umelijuaje hilo?”
“Anadai kwamba yule mgonjwa mpiganaji amezinduka, na amemuita jina lake”
“U…uuu..nasema mpiganaji amezinduka…..?”
“Ndio amezinduka na amemuita mkeo jina lake na hapa kunaonekana kuna kufamiana”
“Sasa umefanyaje wewe”
Dokta Ranjiti alizungumza huku akionekana kama amechanganyikiwa kwa taarifa aliyo pewa.
“Ilinibidi nimchome sindano ya usingizi, ili hadi utakapo rudi tuweze kujua tunafanyaje”
“Kazi nzuri Yan, nipo njiani nakuja sasa hivi”
Dokta Yan akakata simu na kukaa vizuri kwenye kiti chake akimfikiria mgonjwa waliye muweka katika chumba cha siri, kwani yeye ni mtu wa karibu wa dokta Ranjiti na anafhamu kila kitu ambacho kimetokea kati ya Phidaya na Ranjiti.
***
Mawazo ya Shamsa yote yakahamia kwa Phidaya, mwanamke aliye mchukulia kama mama yake, ambaye alimpatia upendo mkubwa kama alivyo kuwa amepatiwa kwa marehemu mama yake. Tangu aweze kuishi na Phidaya kwa miaka zaidi ya mitatu, alitokea kumpenda mama huyo, kwani wote asili zao zimeenda na ilikuwa ni vigumu sana kwa watu kuwatofautisha hao kama si mtu na mama yake. Asili yao ya kihidi ndio ilizidi kuwafanya wafanane japo si sana.
“Shamsa una waza nini?”
Sa Yoo alimuuliza Shamsa aliye jilaza kwenye sofa ndani ya sebule yao, huku miguu yake akiwa ameiweka juu ya meza kubwa ya kioo iliyopo jirani naye. Shamsa akashusha pumzi kidogo kisha akaishusha miguu yake kwenye meza na kukaa sawa.
“Namfikiria yule nesi kule hospitalini”
“Sasa ndio anakufanya uwe katika mawazo kiasi hicho, kama ni ugomvi si ulisha isha”
“Hapana si hivyo Sa Yoo”
“Ila ni nini?”
Ýule ni mama yangu”
Sa Yoo macho yakamtoka kama ameona kitu cha kushangaza sana na chakutisha, taratibu Sa Yoo akajiweka vizuri kwenye sofa alilo kaa na kuendelea kumtumbulia macho Shamsa.
“Mbona unanitumbulia macho yako hivyo, unaniogopesha bwana”
“Hamna Shamsa, nashangaa, inakuwaje yule nesi awe mama yako?”
“Kweli ni mama yangu, ila cha kushangaza tulisha mzika, yeye, bibi na mdogo wangu wa kiume anaitwa Junio”
“Sasa, Shamsa unataka kuniambia siku hizi watu wanaweza kurudi kutoka wafu au….?”
“Sa Yoo sio hivyo hata mimi nashangaa kwanini imekuwa hivyo”
“Ahahaa hapana Shamsa bado hujanishawishi”
“Hembu lete Laptop”
Sa Yoo akanyanyuka na kuichukua Laptop ilipoto kwenye meza ya chakula akarudi nayo na kukaa kwenye sofa alilipo Shamsa. Akaiweka mezani na Shamsa akaifungua na kuiwasha, wakasubiria kwa sekunde kumi na tano ilipo waka, Shamsa akaingia kwenye mtandao wa ‘google’ akaandika jina lake, haikuchukua sekunde jina lake likawa limejitokea kwenye kioo cha laptop hiyo akaingia kwenye sehemu ya picha, zikafunguka picha nyingi, picha ya kwanza kabisa kuonekana ni yake akiwa na Phidaya pamoja na Junio. Macho yakamtoka Sa Yoo.
Akaivuta laptop karibu kudhibitisha picha anayo inaoa kweli nesi aliye muoana anafanana kabisa na mtu anaye muona amesimama na Shamsa. Mwanga wa Laptop hiyo ukaanza kufifia huku taa nyekundu ndogo ikiwaka chini kidogo ya kioo hicho.
“Ohoo inaisha chaji, hujaichomeka kwenye kebo ya umeme hembu inama uivute hiyo kebo”
Sa Yoo alizungumza na Shamsa akafanya kama alivyo ambiwa, gafla Laptop hiyo ikarushwa mbali na kuangukia chini, huku kioo cha dirisha la karibu walipo kaa, likipasuliwa na risasi ambayo imeingia na kumkosa Shamsa aliye inama chini kuvuta kebo hiyo na kutua kwenye laptop.
“Sa Yoo inama chini”
Shamsa alizungumza kwa sauti kali, Sa Yoo bila hata kuuliza akalala chini kabisa ya sakafu.
“Shamsa ni nini hicho”
“Ni risasi hiyo”
Risasi mfululizo zikaanza kumiminika ndani ya sable yao, meza ya kioo ikapasuliwa, kila mmoja akawa amelala chini na kujibanza kwa chini kwenye sofa walilo kuwa wamelalia.
***
Kim baada ya kukabidhiwa kazi na dokta Ranjiti ya kumuua Shamsa hakuona haja ya kupoteza muda wala kujipanga kwani mtu ambaye anakwenda kumuu kwake ni sawasawa na siafu mdogo ambaye anaweza kuminya minya chini kwa kidole chake kimoja.
Akarudi nyumbani kwake na kuingia kwenye compyuta yake, akalisaka jina la Shamsa Eddy, akafanikiwa kulipata, kwa utaalamu wake alio kuwa nao kwenye maswala ya mtandao akafanikiwa kufahamu hadi nyumba anayo ishi binti huyo alipo, hakikisha kwamba amefanikiwa kumpata, akafungua droo lake kubwa, ambapo akachukua budnuki yake aina ya L115A3 AWM yenye uzito usio pungua kilo 16 ikiwa na risasi zake tano ndani ya magazine.
Akaiingiza kwenye begi lake kubwa, akachukua na bastola zake mbili, akazichomeka kwa kiunoni kwa nyuma, akajiweka sawa na kutoka nje ya nyumba yake. Akaliweka begi lake ndani ya gari lake aina ya Range Rover, na taratibu akaanza kuondoka kuelekeaeneo la tukio.
Lee Si, aliweza kumuona Kim akiwa anatoka nyumbani kwake, kama alivyo agizwa na bosi wake Madam Phidaya, akaendelea kumfwatilia mtu huyo ambaye amepewa kazi na dokta Ranjiti.
Kim hakustuka kwamba anafwatiliwa hadi alipo fika katika eneo la karibu kabisa na nyumba ambayo anaishi Shamsa. Kwa uzuri karibu na nyumba hiyo kuna moja ya dorofa linalo endelea kujengwa ila ni takribani wiki mbili ujenzi wa jengo hilo umesimamishwa kutokana na uchunguzi unao fanyiwa mkandarasi wa gorofa hilo.
Kim akapanda hadi gorofa ya tano akiwa na begi lenye bunduki yake hiyo kubwa, ambayo mara nyingi anaitumia kwa mauaji ya mtu mmoja mmoja. Akaitoa bunduki yake hiyo na kuifunga, akaiweka sawa kwenye moja ya dirisha linalo elekea kwenye nyumba ya Shamsa.
Kwa kutumia Lensi ya bunduki hiyo akafanikiwa kuwaona mabinti wawili wakiwa wamekaa kwenye sofa huku wakionekana vichwa kwa nyuma. Kitu kilicho mchanganya hakujua kati ya hao mabinti wawili yupi ni muhusika anaye paswa kuuawa.
Akamlenga shabaha binti wa kwanza upande wa kushoto kwake, ila binti huyo alipo inama kidogo aliweza kuina sura yake, na kutambua kwamba sio ambaye anatakiwa kumuu. Akaihamishia shabaha yake kwa binti wa kulia kwake, alipo hakikisha kwamba amemuweka vizuri kwenye tageti, akafyatua risasi, ila binti huyo aliinama chini kabla ya risasi hiyo kufika na kutua kwenye laptop ambayo hapo mwanzo binti huyo alikuwa ameiziba.
”Shitii…….”
Kim alizungumza huku akiwa ameyakaza meno yake, kwani tangu aanze kuifanya kazi ya mauaji hakuwahi kumkosa shabaha yule aliye kusudia kumuua, hata iweje, ila kwa huyu binti sijui imekuwaje. Binti wa pili naye akapotea kwenye tageti yake na risasi aliyo kuwa amemlenga ikatua kwenye meza ya kioo na kupasuka pasuka. Sofa ndilo lililo haribu mpango mzima wa Kim kumuua Shamsa, kila alipo jaribu kuwatafuta hakuweza kuwaona.
Lee Si, alishushudia mpango mzima ukiwa unaendelea kwa muuji na wanao paswa kuuliwa, akiwa amekaa ndani ya gari lake mbali kidogo na nyumba ambayo ishi Shamsa.
“Hapa ndipo atakapokuwa anaishi yule binti”
Lee Si alizungumza huku akitazama jinsi Kim akipiga risasa zinazo toka kimya kimya kutokana na bunduki anayo itumia kufungwa kiwambo cha kuzuia risasi.
“Hapana naweza kufanya kitu”
Lee Si akawasha gari lake, akakanyaga mafuta kwa kasi na kwenda kulipaki mbele ya mlango wa nyumba ya Shamsa, kwa utaalamu mkubwa akajirusha nje ya gari baada ya kulisimamisha, akaupiga teke mlango huo na ukafunguka, jambo lililo washangaza Sa Yoo na Shamsa, hata Kim mwenyewe akashangaa kuona gari nyekundu ikiwa imesimama nje ya mlango wa Shamsa.
***
“Vipi mwenzetu tulisikia kwamba unaumwa?”
Halima alimuuliza Rahab huku akijipangusa machozi ya furaha yaliyo mtiririka usoni mwake.
“Yaa kweli nilikuwa ninaumwa?”
“Nini zaidi”
Fetty alimuuliza Rahab huku akiwa ameupitisha mkono wake mmoja mabegani mwa Rahab.
“Ahaa ni malaria tu ilinishika nusu iniue”
Rahab aliongopea
“Doo pole sana”
“Sasa mke wa raisi inakuwaje anaumwa Malaria hadi ikulu kuna mbu kweli?”
Anna alitania huku akicheka, wote wakajikuta wakiangua kicheko, wakamkaribisha Rahab na kuketi naye kwenye masofa yaliyomo ndani ya chumba chao.
“Vipi unatumia kilevi, au ndio umestaarabika Mrs President”
“Hapana jamani, bado nina dozi musije mukaniua mwana wa mwenzenu. Haya niambieni yaliyo wakuta kwa maana nasikia mulikufa nyinyi?”
“Ni kweli kama tetesi ulivyo sizikia kwamba tumekufa ila ndivyo dunia inavyo jua, ila ukweli hatujakufa”
Fetty akaanza kuadisia mkasa wa wao tangu walipo achana, wakiamini kwamba rafiki yao huyo alikamatwa kwenye tukio la mwisho la wao kuvamia benki hadi wao walivyo pitia matatizo mengi pamoja na mateso. Hawakumficha ujuzi walio upata kwa bwana Rusev, na jinsi alivyo watelekeza na kuangukia mikononi mwa Wamarekani. Mateso makali waliyo pitia wakiwa gerezani hadi kuokolewa na Mzee Godwin na kurudi tena Tanzania.
Machozi yakamwagika, Rahab, kwani historia hiyo iliyo wapata wezake imemsikitisha kupita maelezo, na yeye akawaadisia mambo yote yaliyo mpata kwenye maisha yake hadi kuolewa na raisi Praygod, ila kitu alicho waficha wezake na nguvu zake za ajabu alizo kuwa nazo.
“Ila unampenda huyo mumeo”
Agnes aliuliza huku akiwa amekazia macho Rahab.
“Ahaaa hivyo hivyo tu maisha yanasonga”
“Mmmmm ila kunaonekana ikulu ni kuzuri, mwenzetu huna hata doa”
Wote wakacheka, Rahab akatambulishwa kwa Jaquline na Manka. Wakaendelea kupiga piga stori kuhusiana na mpango wao wa kuingia ikulu kupitia kura za wananchi.
“Musijali nitahakikisha munaingia ikulu na si munatambua raisi Praygod ni mmoja wa target yetu ambaye bado hatujafanikiwa kuiangusha?”
Rahab alizungumza huku akiwatazama wezake wote ndani ya chumba, Fetty akatingisha kichwa akimaanisha kwamba anakumbuka.
“Basi nitakuwa nikiwaeleza kila kitu ambacho kitakuwa kinaendelea ndani ya ikulu”
Wote wakampigia makofi Rahab, kila mmoja akaamini ushindi wa Mzee Godwin kuingia ikulu upo karibu kuiva.
***
Dokta Ranjiti akasimamisha gari lake eneo la maegesho na kushuka kwa haraka, akaanza kutembea kwa kasi kueleka ofisini kwake, akili yake alihisi inakwenda kuchanganyikiwa, swali kubwa alilo jiuliza, imekuwaje Black Shadow, alitambue jina la mke wake. Kila alipo jaribu kuhisi labda Black Shadow, aliweza kusoma koti la mke wake, ambalo kila mfanya kazi wa hospitalini kwenye nguo yake ya kazi huwa kuna jina.
Hilo nalo halikumuingia kabisa akilini, akafungua ofisi yake na kukaa kwenye kiti chake cha kuzunguka, kwa haraka akampigia simu dokta Yan, ndani ya dakika tatu akawa amefika kwenye ofisi ya dokta Ranjiti.
“Hembu nieleze ilikuwaje kuwaje?”
Dokta Ranjiti alizungumza kwa sauti ya chini ya kunong’oneza, kwani swala hilo ni nyeti sana na halikupaswa mtu yoyote kuweza kulisikia.
“Kwa madai yake amesema kwamba mgonjwa alimuita baada ya kuzinduka”
Naye dokta Yan alizungumza kwa sauti ya chini.
“Sasa huyo Black Shadow amemjuaje mke wangu?”
“Hata mimi sitambui dokta, au anaweza kuwa ni rafiki wa karibu wa huyo mume wake uliye niambia?”
“Yaweza kuwa, au unaonaje tukamfunue sura yake, kwa maana najishangaa tumemfanyia mgonjwa upasuaji hata kuiona sura yake”
“Hapo kweli umenena dokta”
Dokta Ranjiti akashusha pumzi nyingi, huku akimtazama dokta Yan, rafiki yake wa muda mrefu sana. Kwa pamoja wakanyanyuka, na kutoka ndani ya ofisi kuelekea katika chumba cha siri walipo mlaza Black Shadow.
Phidaya akaitazama picha ya Black Shadow kwenye simu yake, akayafumba macho yake kwa muda mrefu, huku akihakikisha kwamba anajaribu kumkumbuka mtu huyo, kwani kila alipo jaribu kuitazama picha hiyo mapigo yake ya moyo yalimuenda kasi sana.