MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA
ILIPOISHIA
Shamsa akajikuta akistuka baada ya kumuona Phidaya akimfwata katika sehemu alipo shikiliwa na polisi.
“Hawa ndio majambazi eheee?”
Phidaya alizungumza kwa sauti ya ukali, askari mmoja akamuitikia, Phidaya bila hata kujiuliza mara mbili, akamzaba kofi Shamsa, aliye kuwa akimshangaa, pasipo kuamini kwamba huyo ni Phidaya au laa, kwa maana wamefanana kila kitu. Ilibidi baadhi ya askari wamzuie Phidaya asiendelea kuwashambulia majambazi hao walio ivamia hospitali yake.
ENDELEA
Shamsa na majambazi wengine watatu wakaingizwa ndani ya gari tatu tofauti za polisi, tukio hilo Sa Yoo aliweza kulishuhudia ila hakujau ni kitu gani kimetokea hadi Shamsa kukamatwa na askari, isitoshe akiwa katika mavazi ya unesi, wakati si mavazi ambayo alikuwa nayo.
Gari za polisi zilizo beba wahalifu zikaondoka Sa Yoo naye akaingia kwenye gari lake na kuzifwatilia hadi kituoni. Shamsa na waalifu wengine wawili wakaingizwa mahabusu, kusubiria mahojiano yatakayo fwanywa dhidi yao.
Akilini mwa Shamsa kumbukumbu za Phidaya, zilizidi kujirudia kichwani mwake. Hakuelewa ni jambo gani ambalo limetokea hadi Phidaya kuwa hai.
“Au sio yeye?”
Alijiuliza mwenyewe, huku akiwa amesimama kwenye moja ya kona ya mahabusu, huku mahabusu wezake wengine wakike wakiwa wamejilaza, kwenye sakafu.
“Kwa usiku huu hautaweza kumuona”
Askari mmoja alimueleza Sa Yoo, ambaye alihitaji kukutana na rafiki yake ili amuhoji kuhusu jambo lililo jitokeza muda mchache ulio pita. Sa Yoo kwa haraka akampigia simu daktari wa Shamsa, akamueleza kila kitui kilicho tokea, daktri hiyo aliye kabidhiwa jukumu la kumuangalia Shamsa, kwa haraka akafika kituo cha polisi akiwa ameongozana na mwanasheria wake kuhakikisha kwamba Shamsa anaachiwa huru.
***
Maisha ya madam Mery yalizidi kuwa mazuri kadri siku zilivyo zidi kwenda, jeraha la risasi aliyo pigwa na Manka lilisha pona muda mrefu sana. Maisha yake aliamua kuyahamishia mkoani Mwanza, ambapo alifanikiwa kufungua mgahawa mmoja mkubwa wa kisasa, ambao kwa siku una uwezo wa kuhudumia wateja mia tisa hasi alfu moja kwa siku.
Umaarufu wa mgahawa wake uliendana moja kwa moja na jina lake, jumba kubwa la gorofa la kifahari, lililopo maeneo ya majango mapya. Aliliwekea ulinzi mkali kutoka katika mashirika mawili tofauti yanayo jishuhulisha na ulinzi. Uzuri wake uliwanyima usingizi wanaume wengi wa jijini Mwanza, umri wa miaka arobaini na moja alio nao, kwa haraka haraka ukimtazama utahisi ni msichana mwenye umri wa miaka ishirini na tano.
Kwa siku hiyo, madam Mery alijawa na furaha sana moyoni mwake, pale alipo toka katioka banki ya Bacrays, na kukuta kiasi cha miliomi moja dola za kimarekani zikiwa zimeingizwa kwenye akaunti yake hiyo.
“Ranjiti nitakutesa hadi kufa kwako”
Madam Mery alizungumza baada ya kupokea risiti yake inayo onyesha kiasi hicho kikubwa cha pesa kikiwa kimeingizwa kwenye akaunti yake. Kwa mwendo wa madaha akaanza kutembea huku mlinzi wake wa kike akiwa ameibeba pochi lake kubwa. Wakaingia kwenye gari, walipo muacha dereva wake.
“Nirudishe nyumbani nahitaji kupumzika kwa sasa”
“Sawa madam”
Safari ya kutoka benk hadi nyumbani kwake iliwachukua dakika ishirini, geti kubwa linalo funguliwa na umeme likafunguka. Gari yake aina ya Hammer, likaingia na dereva akalisimamisha kwenye maegesho ya magari, ambapo kuna gari nyingine nne za kifahari zikiwemo, Range rover sport, Aud Q7, Ferrari spider na BMW X6. Milinzi wake kwa haraka akashuka na kumfungulia mlango.
“Lete tu pochi pumzika”
Madam Mery alizungumza huku akiichukua pochi yake kwa mlinzi wake huyo, akaelekea ndani, alipo pokelewa na mfanyakazi wake wa ndani.
“Mama utakula nikuandalie chakula?”
Hapana sijisikii kula”
Kwa furaha ambayo madam Mery anayo, hakutamani siku hiyo kuweza kuingiza kiu chochote mdoni mwake, kwani utajiri wake unazidi kuongezeka mara dufu, akaingia chumbani kwake, ajitupa kwenye tanda lake kubwa linalo nesa nesa.
“Mery sasa hivi mimi ni milionear”
Alizungumza huku akiliachilia tabasamu lake pana, akakaa kitako, akaichukua rimoti ya Tv yake kubwa ilipo ukutani, akaiwasha na kuanza kutafuta chaneli ambayo ina kipindi kizuri cha kutazama. Chaguo la chaneli likaangukia katika chaneli ya ITV, ambapo amekuta mwenyekiti wa chama cha upinzani cha TDPP(Tanzania Democras People Party), bwana Kibwila, akizungumza na waandishi wa habari.
Masikio na macho ya Madam Mery yote yakaelekea kwenye Tv yake, mapigo ya moyo yakaanza kumdunda pale alipo muona Manka akiwa pembeni ya kiongozi huyo.
“Huyu mtoto amefwata nini kwenye hichi chama?”
Madam Mery aalijiuliza huku akiongeza kidogo sauti ya Tv hiyo. Mwenyekiti wa chama hicho bwana Kibwila, akafikia wakati wa kumtangaza mgombea uraisi wa chama chake.
“Mgombea wetu atakaye ipeperusha bendera ya chama chetu atakuwa ndugu Godwin, gererali mstaafu wa jeshi la wananchi Tanzania”
Madama Mery, akahisi kizunguzungu kikali kikitaka kumchukua, baada ya kulisikia jina la Mzee Godwin, kwa kudhibitishiwa kwamba mwenyekiti huyo hajakosea kabisa, akaonyesha picha ya Mzee Godwin, hapo ndipo furaha yote ya Madam Mery ikayeyuka kama barafu liwekwapo juani.
***
Taratibu Rahab akamfikia Raisi Praygod kwenye mlango alipo simama, kwa haraka akamkumbatia, na kuanza kumwagikwa na machozi jambo lililo mshangaza raisi Praygod.
“Mume wangu nisamehe”
Rahab alizungumza huku machozi yakimwagika, raisi Praygod, alizidi kuendelea kushangaa, kumuona Rahab akiwa amerejea katika hali ya kawaida. Rahab, hakusita kuanza kuzinyonya lipsi za mume wake, joto la hisia za kimapenzi likaanza kupanda katikati yao. Kila mmoja akajikuta akiwa na hamu ya kupata penzi la mwenzake, ambalo walilikosa kwa kipindi fulani. Ndani ya dakika kadhaa wote wawilili wakajikuta wakiwa hawana nguo katika miili yao.
Kila mmoja alipo hakikisha kwamba amemuandaa mwenzake vya kutosha, mechi ikaanza, si raisi wala Rahab aliye onekana kuchoka, kila mmoja alihakikisha kwamba anampa mwenzake kile kitu roho inapenda, huku wote wakiwa wamejawa na furaha mioyoni mwao.
***
Iliwalazimu Black Shadow kuhamishiwa katika chumba kingine cha siri, kilichopo chini ya ardhi ndani ya hospitali hiyo. Kazi hiyo ilifanywa na dokta Ranjiti na wasaidizi wake, usiku huo huo, baada ya tukio la uvamizi kutokea katika hospitali yake. Polisi wakatoa tamko kwa watu ambao walijitokeza kumuombea shujaa huyo, kwamba warudi majumbani kwao na kuanzia siku hiyo watu hawata ruhusiwa kuja kujazana katika hospitali hiyo, hadi pale afya ya Black Shadow itakapo imarika.
Lilikuwa ni pigo kwa mashabiki wa Black Shadow, ila hawakuwa na jinsi, ni lazima waweze kutii tamko hilo la askari. Ulinzi ukazidi kuimarishwa kwenye hospitali hiyo, hata dhiara ya raisi, ikakatishwa hadi pale mambo yatakapo kuja kuwa sawa ndipo raisi aweze kumtembelea mpiganaji huyo.
Uwepo wa Black Shadow katika chumba cha siri ulijilukana kwa watu wachache tu akiwemo Sabogo, ambaye yeye pekee ndiyo alipewa ruhusa ya kwenda kumuona Black Shadow katika chumba hicho. Asubuhi na mapema, Sabogo akawa yupo ndani ya chumba hicho cha siri kilicho jaa taa nyingi zenye mwanga mweupe.
Sabogo akatoa kinyago kingine kilicho tengenezwa, kwa ajili ya Black Shadow, akamvua kinyago cha mwanzo na kumvalishi kingine kipaya lilicho mkaa vizuri, alipo hakikisha rafiki yake yupo salama, akatoka ndani ya chumba hicho na kurudi kwa daktari mkuu wa hospitali bwana Ranjiti.
“Itamchukua muda gani hadi kupata fahamu?”
“Itamchukua kipindi kidogo, ila kutokana bado tunaendelea kumuangalia kwa usalama mkubwa, basi tumuombe Mungu, kila jambo litakwenda sawa”
“Sawa dokta ila hakikisha kwamba hakuna mtu ambaye atagundua kwamba yupo chumba cha siri”
“Usijali kwa hilo”
Yote yakiwa yanazungumza ndani ya ofisi ya dokta Ranjiti Phidaya aliweza kuyasikia akiwa nje ya mlango, moyo wake ulizidi kumsumbua kila alipo fikiria juu ya donge nono ambalo polisi walilitangaza kwa mtu ambaye angelisaidia jeshi hilo kumkamata Eddy.
Phidaya akarudi kwenye ofisi yake akiwa na mawazo mengi, akilini mwake akaanza kulifikiria tukio la jana alipo weza kuiona sura ya Black Shadow, pili akafirikiria jinsi, majambazi walivyo vamia kwenye hospitali yake, na kutaka kumuua Black Shadow.
“Ina maana wanamjua kwamab ni Eddy nini?”
Phidaya alizungumza huku akinyanyuka kwenye kiti chake na kuanza kuzunguka zunguka ndani ya ofisi yake.
“Ngoja nikamueleze kila kitu mume wangu”
Phidaya alizungumza, kwa haraka akaanza kupiga hatua hadi mlangoni kwake, akavuta kitasa cha mlango huo, akaufungua na kuanza kutembea kuelekea katika ofisi ya mume wake.
***
Baada ya Sabogo kutoka ofisini kwake, dokta Ranjiti, akawasha Tv yake, moja ya taarifa aliyo ikuta ni jinsi hospitali yake ilivyo vamiwa. Ila kati ya majambazi walio kamatwa, mmoja wao akamstua kidogo. Akajikuta akisimama kabisa na kwenda kuikodolea macho Tv hiyo. Jina la Shamsa Eddy, ndio kabisa zikazidi kumpagawisha. Na moja ya picha ikapita kwenye taarifa hiyo ya habari jinsi mke wake alivyo mtandika kofi jambazi huyo wa kike.
‘Mungu wangu siri inakwenda kufichuka’
Dokta Ranjiti alizungumza huku kijasho kikianza kumpiga na mapigo yake moyo yakizidi kwenda mbio. Akaanza kujipapasa kuitafuta simu yake ya mkononi sehemu alipo iweka, kwa bahati nzuri akaikuta kwenye koti lake, akaichomoa kwa haraka na kuminya baadhi ya namba kisha akaiweka sikioni, baada ya muda ikapokelewa upande wa pili.
“Ehee mkuu habari yako bwana”
‘Salama vipi dokta nikusaidie nini?’
“Naamini hao majambazi walio kuja kuvamia hospitalini kwangu wapo mikononi mwako”
‘Ndio na wanaendelea kufanyiwa mahojiano, ila huyu mmoja wa kike hana hatia ndio tumemuachia mida hii’
“Mungu wangu…….!!!”
‘VVipi kuna tatizo kwani?’
“Aha…ahaaa hapana”
‘Basi kila litakalo kuwa linaendelea nitakujulisha’
“Sawa mkuu”
Dokta Ranjiti baada ya kukata simu alipo maliza kuzungumza na mkuu wa kituo cha polisi, akili yake ikaanza kufanya kazi kama compyuta pale inapo tafuta, majina yaliyo hifadhiwa kwenye kumbukumbu zake. Kwa haraka mkumbukumbu zake zikatua kwenye moja ya mtu ambaye kazi zake ni umafia na huzifanya kazi za matajiri wengi ndani na nje ya Japani, pasipo kukosea wala kukamatwa na askari polisi kutokana na kujibadilisha badilisha sura na yeye huwa mara nyingi huwa ndio mtu anaye mfanyia upasuaji wa kumbadilisha sura.
“Ndio Kim upo wapi?’
‘Yokoma, vipi kuna tatizo dokta?’
“Ndio kuna tatizo bwana, kuna binti anaitwa Shamsa Eddy nahitaji uweze kumuondoa dunia”
‘Amekufanyaje tena dokta?’
“Ni binti ambaye anaitambua siri ya yangu juu ya mke wangu Phidaya, si unatambua kwamba huyu Phidaya ni mwanamke niliye mpora waziri mmoja nchini Tanzania”
‘Yap nalitambua hilo ulisha wahi kuniambia’
“Ndio basi binti huyo ni kati ya wale majambazi walio kamatwa jana na polisi na yeye anamtambua vizuri Phidaya kutokana ni mama yake”
Mazungumza ya simu ya dokta Ranjiti yakamfanya Phidaya kusimama nje ya mlango, aliweza kusikia kila kitu alicho kizungumza mume wake, ila hakuweza kusikia mazungumzo na mtu wa pili.
‘Phidaya kutokana ni mama yake’
Maneno hayo yakaanza kujirudia kwa nguvu akilini mwake, machozi yakaanza kumlanga lenga Phidaya, hakuona haja ya kuendelea kukaa mlangoni mwa mume wake kwa haraka akaanza kutembea kurudi ofisini mwake. Akaufunga mlango wake kwa ndani, akavuta kiti chake, akawa kama mtu aliye changanyikiwa mara kadhaa akijiuliza maswali mengi kuhusiana na kitui alicho kisikia.
“Shamsa Eddy”
‘Ni binti ambaye anaitambua siri yangu juu ya mke wangu Phidaya’
Phidaya akajikuta akizidi kuyakumbuka maneno ya mume wake bwana Ranjiti, kiu na hamu ya kumuona Shamsa, ikaanza kumjaa moyoni mwake, kwani anatambu ni kati ya majambazi ambao walikamatwa jana na ni yule aliye mtandika kibao jana usiku. Kwa haraka Phidaya akavua koti lake na kuvaa koti la baridi, akajifutamachozi usoni mwake, wala hakuhitajki tena kuzungumza na mumewe kwa kitu alicho wahi kukiona. Kwani roho ya kumchukia mwanume huyo ilianza kumvaa. Swali ambalo mara kwa mara alijiuliza kichwani mwake, kwamba yeye ni nani, taratibu alihisi linaanza kupata jibu.
“Lazima nijijua mimi ni nani”
Phidaya alizungumza peke yake huku akitembea kwenye kordo ya kuelekea nje ya hospitali.
***
Kwa juhudi za mwana sheria aliye msimamia Shamsa, kwenye mahojiano kati yake na polisi, yalizaa matunda, kwani hadi inatimu alfajiri tayari Shamsa alionekana kwamba hana hatia kutokana na maelezo yake aliyo yatoa. Uchunguzi ulio fanywa kwa nesi ambaye aliuawa na Shamsa, ulionyesha kwamba hakuwa ni nesi wa hospitali hiyo kutokana na kukutwa na michoro mingi(tattoo) mwilini mwake.
Pia katika kubanwa kwa waalifu wawili wa kiume walio kamatwa, walidhibitisha kwamba Shamasa sio mwenzao, hilo pia lilichangia kwa Shamsa kuachiliwa huru.
“Inabidi sasa twende nyumbani ukapumzike”
Sa Yoo alizungumza mara baada ya Shamsa kuachiliwa huru, kwani naye pia alishinda kituoni hapo kuhakikisha kwamba rafiki yake anaachiwa huru.
“Hapana nahitaji kwenda hospitali kumuona Black Shadow ndio niweze kwenda nyumbani’
Kutokana Shamsa ni mtu wa kung’ang’ania maamuzi yake mwanzo mwisho, Sa Yoo na daktari hawakuwa na hiyana zaidi ya kuanza safari kuelekea katika hospitali aliyo lazwa Black Shadow. Akilini mwa Shamsa hakumfikiria Phidaya kutoka alihisi labda alimfananisha, isitoshe tayari walisha mzika mama yeka huyo. Kutokana ni asubuhi, barabara ilijaa foleni nyingi, kwa hiyo iliwachukua muda mwingi sana hadi kuweza kufika katika hospitali hiyo. Wakiwa getini, wakapishana na gari aina ya Aud A4. Hakuna aliye weza kuifwatilia sana, haswa Shamsa ambaye muda wote alimuwaza Black Shadow wake.