Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

News Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Aprili 13, 2017 muda huu

$
0
0
Fuatilia hapa matangazo ya moja kwa moja kutoka Bungeni Dodoma ambapo leo Aprili 13, 2017 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea na Mkutano wa Saba. 

==>Tazama hapo chini  yote yanayojiri muda huu.

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Yasema Nafasi ya Sophia Simba Iko Wazi na Itajazwa Hivi Karibuni

$
0
0
Tume  ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi ya ubunge wa Viti Maalumu iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba, ambaye alifukuzwa uanachama hivi karibuni.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa tume hiyo, Jaji Semistocles Kaijage, ilieleza kuwa kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343,  Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa baada ya Sophia kufukuzwa uanachama wa CCM Machi 11, mwaka huu, nafasi hiyo  yake bungeni iko wazi.

Alisema kwa mujibu wa Ibara ya 67 (1) (b) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ili mtu ateuliwe au achaguliwe katika nafasi ya ubunge, ni lazima awe mwanachama aliyependekezwa na chama chake husika cha siasa.

“Kwa kuwa Sophia Simba amefukuzwa uanachama wa chama kilichomdhamini, Ibara ya 67 (2) (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inaelekeza kuwa amepoteza sifa za kuteuliwa au kugombea ubunge.

“Kutokana na kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge wa Viti Maalumu, taratibu za kujaza nafasi hiyo zinaendelea kwa kuzingatia kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, sura ya 343,” alisema Kaijage.

Sophia na wenzake saba walifukuzwa uanachama baada ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa CCM Machi 11, mwaka huu mjini Dodoma huku wengine wakipewa onyo kali.

Waliopewa adhabu sambamba na Sophia ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida, Jesca Msambatavangu (Iringa), huku Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Emmanuel Nchimbi akipewa onyo kali kwa kosa la kukisaliti chama wakati wa mchakato wa uteuzi wa mgombea urais mwaka juzi.

Mahakama Yabariki Kina Shikuba Kupelekwa Marekani

$
0
0
Mahakama  imekubali maombi ya aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Harrison Mwakyembe ya kutaka Watanzania watatu washikiliwe wakati wakisubiri kibali cha kusafirishwa kwenda Marekani kujibu mashtaka ya kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya nchini humo.

Uamuzi wa kuyakubali maombi hayo ulitolewa jana na   Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Cyprian Mkeha, baada ya kujiridhisha na ushahidi na vielelezo vilivyotolewa mahakamani.

Kabla ya Hakimu Mkeha kutoa uamuzi huo, Shikuba alisema ni bora wakapelekwa Marekani kwa sababu  wanaweza kupata haki yao.

“Ni bora tukapelekwa Marekani tunaweza kupata haki yetu, watu watatu tunatuhumiwa kwa kilo 1.78 za heroine, kweli hiyo?

“Tunaishi kama wahujumu uchumi, hatujabadilisha nguo siku ya tatu, kesi Lindi nimefutiwa na kilo 200 za heroine nakuja kushtakiwa Marekani kwa kilo moja.

“Sina hata viatu, nimetolewa Lindi hivyo hivyo… nitakuwa mtu wa kwanza kuingia Marekani nikiwa nimevaa ndala,”alidai Shikuba wakati akisubiri Hakimu aingie mahakamani.

Kifungu cha 8(3) cha Sheria ya Kusafirisha wahalifu  kinasema hakimu akishajiridhisha na ushahidi uliofikishwa mahakamani anampa taarifa Waziri wa Katiba na Sheria kwa ajili ya kutoa kibali cha kuwasafirisha.

Hakimu Mkeha akisoma uamuzi baada ya kusikiliza hoja za pande mbili, alisema mahakama kabla ya kuamua ilijiuliza maswali kadhaa ikiwamo kama mashtaka wanayohusishwa nayo wajibu maombi yako katika utaratibu wa kubadilisha wahalifu.

Pia mahakama ilijiuliza kama kuna mkataba kati ya nchi husika ambako baada ya kuangalia imebaini kwamba kuna makubaliano ya kubadilishana wahalifu kati ya nchi hizo mbili.

“Mahakama imekubaliana na maombi yaliyowasilishwa na Waziri wa Katiba na Sheria, mahakama inatoa amri ya kuwashikilia wajibu maombi mpaka   waziri atakapotoa kibali cha kuwasafirisha kwenda Marekani,”alisema.

Hakimu Mkeha alisema kama wajibu maombi watakuwa wanapingana na uamuzi huo, mahakama inawapa nafasi ya kukata rufaa ndani ya siku 15.

Mwakyembe aliwasilisha maombi Februari 15 mwaka huu, akiomba mahakama hiyo kuamuru  Kiongozi wa Taasisi ya Kusambaza Dawa za Kulevya nchini, Ally Haji, maarufu Shikuba, Iddy Mfuru na Tiko Adam washikiliwe wakati wakisubiri kibali cha kuwasafirisha kwenda Marekani kujibu tuhuma za kula njama kusafirisha na kusambaza dawa za kulevya nchini humo.

Jamhuri iliwakilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Edwin Kakolaki na katika kuiridhisha mahakama iliwasilisha maombi pamoja na ushahidi dhidi ya wajibu maombi, wa kuonyesha kujihusisha kwao katika matukio hayo.

Ushahidi ulionyesha kwamba Marekani iliwachunguza wajibu maombi kwa miaka minne na walitumia Dola za Marekani 10,000 kununua dawa hizo kutoka kwa taasisi yao ili kubaini ukweli..

Wajibu maombi ilibainika walikuwa wakisafirisha heroine kwa kutumia magari, wakifikisha dawa hizo Marekani na kuwatumia watu kusambaza kwa kutumia ndege binafsi na Shikuba ndiye kiongozi wa taasisi hiyo.

Kakolaki alidai maombi yaliambatana na kiapo kilichoapwa na Richard Magnes ambaye katika kiapo chake anadai wajibu maombi wanatuhumiwa kuingiza dawa za kulevya zaidi ya kilo 1.78 Marekani.

Alidai ushahidi katika kiapo hicho unadai aliwahi kukamatwa mbeba dawa(punda) mwaka 2012, alizitoa kwa njia ya haja kubwa na alipohojiwa alimtaja Shikuba kuwa alimpa dawa hizo.

Kakolaki alidai tangu mwaka 2005 wajibu maombi wanatajwa na watuhumiwa mbalimbali   Marekani kwamba ndiyo wanaosambaza dawa hizo kwa kutumia taasisi yao inayoongozwa na Shikuba.

Ushahidi huo wa kiapo unadai Shikuba aliwafundisha miongoni mwa watuhumiwa waliokamatwa, jinsi ya kubeba dawa hizo na kusafirisha na kwamba dawa hizo zilikuwa zikiingia Tanzania kwa meli kupitia mwambao   kwa maelekezo ya Shikuba.

Majibu ya hoja za Wabunge yaliyotolewa na Waziri Mkuu bungeni

$
0
0
1.0.      UTANGULIZI

Mheshimiwa Spika,
  • Naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema kwa kutupa Afya njema hadi leo ninapohitimisha Majadiliano ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.
Mheshimiwa Spika, ninapohitimisha hoja yangu, katika siku ambayo Taifa letu liliondokewa na aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Moringe Sokoine, aliyezaliwa tarehe 1 Agosti 1938 na kufariki kwa ajli ya gari siku kama ya leo mwaka 1984. Ninalazimika kuwakumbusha Watanzania wote kumuenzi mpambanaji huyo wa haki za wanyonge kwa kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na rushwa na ubadhilifu wa mali za umma. Namuomba Mwenyezi Mungu aendelee kumpumzisha kwa amani Edward Moringe Sokoine. Amen.
 
Natoa shukrani zangu za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria; Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kwa michango yao mizuri kwenye Hoja yangu.
 
 Kipekee ninakushukuru sana wewe Mheshimiwa Spika, Naibu Spika na Wenyeviti wote wa Bunge kwa kusimamia kwa umahiri mkubwa majadiliano ya Hotuba ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Taasisi zake na Mfuko wa Bunge.

Ninawashukuru pia Waheshimiwa Wabunge kwa pongezi  zenu kwa Serikali na kwa michango yenye dhamira njema ya kuboresha mipango na kazi zilizokusudiwa kutekelezwa na Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. Mjadala huu umedhihirisha namna ambavyo Bunge linaendelea kuimarika na kutekeleza wajibu wake wa Kikatiba kuishauri na kuisimamia Serikali kikamilifu.
 
Ninawashukuru Makatibu Wakuu wote, Makamishna na watumishi wote wa Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Wizara nyingine walioshiriki kuandaa taarifa hii.
2.0.      WACHANGIAJI
Mheshimiwa Spika,
  • Mjadala huu, ulichangiwa na Waheshimiwa Wabunge 148, ambapo Waheshimiwa Wabunge 99 walichangia kwa kuzungumza moja kwa moja hapa Bungeni na Waheshimiwa Wabunge 49 wamechangia kwa njia ya maandishi.
Ninawashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia Hoja yangu. Hata hivyo, kutokana na muda naomba uridhie nisiwataje na majina yao yaingizwe katika Hansard.

Niko mbele yenu kuomba ridhaa yenu ili tupitishe bajeti hii tuweze kufanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini.
  • Serikali imejibu hoja hizo kupitia Mawaziri na Naibu Mawaziri. Hoja zilizosalia zitajibiwa kwa maandishi. Aidha, baadhi ya hoja zitajibiwa na Mawaziri wa sekta husika watakapowasilisha bajeti zao.
3.0.      UTENDAJI WA SERIKALI KWA UJUMLA
Mheshimiwa Spika, kabla ya kuanza kujibu Hoja za Waheshimiwa Wabunge, naomba uniruhusu nibainishe baadhi ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi thabiti wa Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan na Mheshimiwa Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein kwa namna wanavyoendelea kuiongoza nchi yetu kwa uzalendo uliotukuka na dhamira njema isiyotiliwa shaka.
 
Mheshimiwa Spika, nina hakika Watanzania wote ni mashuhuda wa kazi nzuri inayofanywa na Mheshimiwa Dkt. John P. Magufuli katika kuiongoza Nchi yetu kwa     weledi mkubwa na kwa mipango iliyo imara ili kuboresha maisha ya Watanzania. Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake tumeshuhudia kuanza kwa miradi mikubwa na yenye tija kwa nchi yetu.
 
A:      HUDUMA ZA KIJAMII
Elimu bila malipo
Mheshimiwa Spika, chini ya Serikali ya Awamu ya Tano ambapo watoto wote wa Tanzania wanapata elimu ya Msingi na Sekondari bila malipo. Kila mwezi Serikali inapeleka shilingi bilioni 18.77 kwenye shule zote za Serikali nchini Tanzania. Aidha, ni chini ya Serikali hii, kiasi cha shilingi bilioni 3.3 zinatolewa kila mwezi kwa Walimu Wakuu na Wakuu wa Shule kama motisha kwa viongozi hao na kufanya kila mwezi kutuma shilingi bilioni 22.7.  Tunajua zipo changamoto zilizojitokeza, hasa uandikishaji mkubwa uliosababisha uhaba wa madawati. Kipekee, ninawashukuru Waheshimiwa Wabunge kwa kujitolea kusimamia suala hili kwa dhati.
 
Mheshimiwa Spika, huu ni utekelezaji wa Ilani ya CCM wenye lengo la kuhakikisha kila mtoto wa Kitanzania anapata urithi ulio bora, ambao ni elimu.
 
Maboresho kwenye Sekta ya Afya
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano inatoa kipaumbele kikubwa kwenye sekta ya afya. Tunatambua kwamba jamii yenye afya njema ndiyo inayoweza kuzalisha kwa tija. Kutokana na ukweli huo, Serikali imeendelea kuboresha huduma za afya kwa kuongeza bajeti ya kununua vifaa tiba na dawa kutoka shilingibilioni 31 mwaka 2015/2016 hadi shilingibilioni 251 mwaka 2016/2017. Hadi leo, tumenunua ambulance 67, tumeanza kuzigawa kwenye Kanda ya Ziwa. Pia tumeagiza kila Halmashauri hapa nchini, zitenge fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba moja ya mganga, nyumba ya muuguzi na maabara ya damu.
 
Aidha, Serikali imebuni utaratibu wa kununua dawa na vifaa tiba moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya kununua kutoka kwa wasambazaji. Pia, Serikali imeanzisha utaratibu wa kujenga maduka ya madawa ya MSD kwa lengo la kuwezesha upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa bei nafuu kwa wananchi. Tayari maduka manane (8) yamejengwa na mengine yanaendelea kujengwa kote nchini.
 
Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuboresha huduma za afya nchini, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amefanya uamuzi wa kusambaza magodoro 25, mashuka 50  na vitanda 25 vya hospitali katika Halmashauri zote 184 nchini. Kati ya vitanda hivyo, 5 ni kwa ajili ya wajawazito. Pia Serikali imetoa seti tano za vifaa tiba katika kila Halmashauri. Serikali itaendelea kuboresha huduma za afya nchini, ikiwemo kusambaza watumishi katika sekta ya afya.

B:      SEKTA ZA UZALISHAJI
 
Ujenzi wa Reli ya Kati
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea na jitihada za kuimarisha reli ya kati kwa lengo la kurahisisha usafiri na usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi. Katika mwaka wa fedha 2016/2017 Serikali ilitenga shilingitrilioni moja kwa ajili ya maandalizi ya ujenzi wa reli hiyo. Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, leo hii tarehe 12 Aprili, 2017 Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha standard gauge. Ujenzi wa reli ya kati ambayo ni mradi wa kipaumbele katika Dira ya Taifa ya Maendeleo, kuchochea ukuaji wa uchumi na ujenzi wa uchumi wa viwanda nchini.
 
Ujenzi wa Viwanda
Mheshimiwa Spika, Serikali pia inaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuvutia uwekezaji nchini. Ndani ya mwaka mmoja jumla ya viwanda 2,169vimesajiliwa, ikiwa ni pamoja na viwanda vya mbolea, saruji, chuma na usindikaji wa mazao. Uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda nchini ni dhahiri na tayari tumeanza kuona matokeo. Kwa mfano, Mkoa wa Pwani pekee una viwanda vikubwa 83 na vingine vidogo vidogo zaidi ya 200. Huu ndio mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano.
 
Maboresho kwenye Sekta ya Usafiri wa Anga
Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Tano inaendelea na jitihada za kulifufua Shirika la Ndege la Tanzania kwa kununua ndege mpya sita, ambazo zinawasili kwa awamu mbalimbali. Serikali imekamilisha upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dodoma pamoja na kuendelea kujenga jengo la tatu la abiria (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mwanza na ukarabati wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro na Uwanja wa Songwe – Mbeya.
 
Vilevile, Serikali inaendelea na ujenzi wa uwanja wa ndege  wa Mkoa wa Geita na kukamilisha maandalizi kwa ajili ya upanuzi na ujenzi wa viwanja vya ndege vya Tabora, Kigoma, Sumbawanga, Lindi na Shinyanga. Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa viwanja vya ndege vya Musoma, Mtwara, Iringa na Songea.
 
Jitihada hizi ni kudhihirisha dhamira ya dhati ya kuboresha usafiri wa anga ili kurahisisha usafiri kwa wananchi pamoja na kuchochea utalii nchini.
 
Miradi ya Barabara
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kukarabati na kuboresha barabara zinazounganisha mikoa nchini.  Aidha, Serikali inaendelea kuimarisha barabara kote nchini ikiwa ni pamoja na kujenga barabara zitakazofungua fursa za kiuchumi katika maeneo mbalimbali. Baadhi ya barabara hizo ambazo ziko katika hatua mbalimbali za ujenzi  ni Barabara ya Itoni – Mkiu – Ludewa – Manda (km 211);Barabara ya Tabora – Sikonge – Ipole- Koga – Mpanda (km 259);Barabara ya Mbeya – Makongorosi – Rungwa – Itigi – Mkiwa  (km 528);Manyoni – Itigi – Tabora (km 259.7);Barabara ya Dodoma – Babati  (km 261); Barabara yaIringa – Dodoma (km 260); Barabara ya Masasi – Songea – Mbamba Bay (km 866.7); Barabara ya Makutano – Nata – Mugumu – Loliondo – Mto wa Mbu (km 338); na Barabara ya Kigoma – Kidahwe – Uvinza- Kaliua – Tabora (km 491);
 
Madeni ya makandarasi, wazabuni, watumishi na watoa huduma:
Mheshimiwa Spika, baadhi ya Waheshimiwa Wabunge, wamejadili kuhusu madeni ya makandarasi, wazabuni, watumishi na watoa huduma wanaoidai Serikali kwa muda mrefu.
 
Mheshimiwa Spika, nataka niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kuwa Serikali inatambua umuhimu wa kuwalipa wakandarasi na wadeni wote wa Serikali. Hata hivyo, kabla ya kufanya malipo hayo, Serikali inabidi kujiridhisha kuhusu uhalali wa madeni hayo, na mara moja tunapokuwa tumejiridhisha kuhusu uhalali wa madeni hayo tumekuwa tukilipa bila kusita. Hadi kufikia mwezi Desemba, 2016 jumla yashilingi bilioni 2,934.2 zilikuwa zimehakikiwa, ambapo shilingi bilioni 555.2zililipwa. Ninawaomba makandarasi, wazabuni, watumishi na watoa huduma wote wanaoidai Serikali, watuwie radhi na watuvumilie wakati tunapojiridhisha kuhusu madeni yao. Serikali isingependa mdeni wake apunjwe lakini pia ingependa Serikali ilipe madeni halali.
 
Napenda kuliarifu Bunge lako tukufu kuwa Serikali imeongeza shilingi bilioni 21 kwa shughuli za Bunge ili liweze kufika tarehe 30 Juni, 2017.
 
Mheshimiwa Spika, niliona ni vyema nianze mjadala huu kwa kubainisha masuala muhimu yaliyofanywa na Serikali ili kuweka kumbukumbu vizuri kutokana na baadhi yetu kuchangia kana kwamba hakuna jambo lolote lililofanywa na Serikali tangu iingie madarakani.
 
4.0.      MAJIBU YA HOJA
          Mheshimiwa Spika,
  • Kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, Kanuni ya 99 (13) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari 2016, naomba nitumie nafasi hii kujibu na kufafanua baadhi ya hoja za Waheshimiwa Wabunge kama ifuatavyo:
  1. HOJA
Serikali itoe maagizo kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri kutengeneza ajira angalau 20,000 kila mwaka katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri zao, na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo iwe inatolewa kila mwaka kwenye Bunge la Bajeti.
 
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni); Mheshimiwa Juma Hamidu Aweso (Pangani)
 
JIBU:
Mheshimiwa Spika,
Napenda, kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015 Ibara ya 59 inazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa zote nchini kuzingatia viashiria vya ukuzaji ajira katika mipango ya maendeleo ya ngazi husika pamoja na kutoa taarifa za mwenendo wa ajira kila robo mwaka.
 
Aidha, maelekezo haya, yanazingatiwa katika Mwongozo wa kuandaa Bajeti ya Serikali unaotelewa na HAZINA kila mwaka unaozitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi zote kubainisha fursa za ajira zinazotarajiwa kupatikana kila mwaka kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Vilevile Mwongozo huo unazitaka Taasisi hizo kutoa taarifa za ajira zinazozalishwa kutokana na utekelezaji wa Miradi hiyo kila robo mwaka. Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi zote ziendelee kuzingatia maelekezo haya.
  1. HOJA: Kuhusu hali ya upatikanaji wa chakula nchini.
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Kunti Yusuph Kajala (Viti Maalum); Mheshimiwa Zuberi Zitto Kabwe (Kigoma Mjini); Mheshimiwa Ridhiwani Jakaya Kikwete (Chalinze)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema kwenye hotuba yangu ya Bajeti ya 2017/18 ukurasa wa 21, katika msimu wa kilimo 2016/17 hali ya upatikanaji wa mvua katika Mikoa inayopata mvua za vuli haikuwa ya kuridhisha na hivyo kusababisha ukame na upungufu wa mavuno katika baadhi ya maeneo. Ili kukabiliana na hali hiyo, Serikali inahamasisha sekta binafsi kununua mazao ya chakula kutoka maeneo yenye ziada na kuyauza katika maeneo yenye uhaba hasa kwenye wilaya 55 tulizozibaini.
 
Aidha, wafanyabiashara waliohifadhi nafaka katika maghala, wazisambaze katika masoko ya ndani. Katika kuunga mkono juhudi hizo, Serikali imesambaza tani 1,969 za mbegu bora za mazao yanayostahimili ukame kwenye Halmashauri mbalimbali. Natoa wito kwa wakulima kuendelea kutumia vizuri mvua zinazonyesha katika msimu huu wa masika kwa kupanda mazao yanayokomaa kwa muda mfupi na kutumia mbegu bora za mazao ya kilimo zinazostahimili ukame.
  1. HOJA:
Kutokana nchi yetu kuwa na mipaka mingi yenye vipenyo vingi pamoja na ukanda mrefu wa bahari ambavyo hufanya udhibiti wa uingizaji wa dawa za kulevya kuwa mgumu, Serikali imeshauriwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa kutoa elimu kwa jamii zinazoishi mipakani ili zishirikiane na vyombo vya dola hatua ambayo itasaidia udhibiti wa uingizwaji wa dawa hizo hatari nchini.
 
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeshaanza kutoa elimu kwa Kamati za Ulinzi na Usalama katika maeneo ya mipaka ya Tunduma, Kasumulo, Namanga, Horohoro na Mtukula ili kuweza kutoa elimu juu ya athari za dawa za kulevya kwa jamii inayoishi mipakani. Aidha, elimu hii itatolewa kwa wananchi kadri hali itakavyo ruhusu ili wananchi wote kwa pamoja washiriki katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya badala ya kuviachia vyombo vya dola pekee.
  1. HOJA: Mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kulinda watoa taarifa na pendekezo la kutaifisha mashamba ya bangi.
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI); Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq (Viti Maalum)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, tatizo la dawa za kulevya ni janga kubwa la kitaifa linaloathiri ustawi wa Nchi yetu. Serikali imedhamiria kwa dhati kupambana na mtandao wa dawa za kulevya nchini. Mafanikio katika mapambano ya dawa za kulevya yanahitaji ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wananchi. Hivyo, napenda kulihakikishia Bunge lako Tukufu kwamba, watoa taarifa za wahusika wa dawa za kulevya wanaendelea kulindwa na watalindwa kwa mujibu wa Sheria ya Kulinda Watoa Taarifa na Mashahidi ya Mwaka 2015 (Whistleblower and Witness Protection Act of 2015).
 
Mheshimiwa Spika, Serikali inalipokea pendekezo la kutaifisha mashamba ya bangi na itaendelea kutafakari utekelezaji wake. Pale tutakapojiridhisha kuwa adhabu hii itatoa fundisho kwa wananchi wanaojihusisha na kilimo cha bangi, Serikali haitasita kuleta Bungeni muswada wa mabadiliko ya sheria ili kuongeza suala hilo.
  1. HOJA: Kuongeza vituo vya tiba ya Methadone na Sober Houses za Serikali angalau moja kila Mkoa.

MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI); Mheshimiwa Abdallah Ali Mtolela (Temeke)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, uanzishwaji wa vituo vya tiba kwa kutumia Methadoneunategemea ukubwa wa tatizo la matumizi ya dawa za kulevya na uwepo wa miundombinu ya msingi katika Mkoa husika. Hadi sasa kuna vituo vya Methadonekatika hospitali za Muhimbili, Mwananyamala na Temeke – Dar es Salaam. Vilevile, Serikali inakusudia kufungua vituo kama hivyo katika Mikoa ya Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Mbeya, Morogoro, Mwanza, Pwani naTanga.
 
Kwa kuwa matibabu ya Methadone yanawasaidia watumiaji wa dawa za kulevya aina ya Heroin pekee, Serikali inatarajia kuanzisha nyumba za upataji nafuu (Sober Houses) kila Mkoa. Huduma hii itakuwa ni kwa ajili ya kuwasaidia waraibu (addicts) wengine wa aina zote za dawa za kulevya, badala ya kuwaachia watu binafsi ambao mpaka sasa wanaendesha nyumba 17 za upataji nafuu nchini. Vilevile, Serikali imeandaa Mwongozo wenye lengo la kusimamia na kuratibu Sober Houses za watu binafsi.
  1. HOJA: Serikali iongeze vituo vya afya, vifaa tiba, wahudumu wa afya wenye weledi na kupunguza umbali wa kupata huduma kwa Wanaoishi na Virusi vya UKIMWI (WAVIU). 
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI);
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, Ilani ya Uchaguzi ya CCM na Sera ya Maendeleo ya Afya ya Msingi vinaelekeza Serikali kuboresha huduma za afya ya msingi kwa kujenga zahanati kila kijiji, kituo cha afya kila kata na Hospitali kila Wilaya. Aidha, Serikali ina mkakati wa kuongeza idadi ya wataalam wa afya nchini kote. Kupitia mikakati hii, wananchi wakiwemo WAVIU watapata huduma karibu na maeneo wanayoishi.
  1. HOJA: Serikali itoe elimu ya kujikinga na VVU kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo elimu kwa njia ya Sinema na kuanzisha vilabu vya mapambano dhidi ya VVU katika shule zote kuanzia msingi pamoja na kuandaa mitaala ya elimu ya UKIMWI katika ngazi zote za elimu (elimu ya msingi hadi vyuo vikuu).
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI);
 
JIBU:
Mheshimiwa Spika,
Nia ya Serikali ni kuona elimu ya UKIMWI inawafikia wote wanaostahili. Serikali ina magari ya Sinema katika mikoa ishirini ya Tanzania Bara ambayo hutoa elimu ya UKIMWI kwa njia ya sinema. Tanzania Visiwani nayo sasa inapatamagari ya sinema katika mikoa yake yote. Wizara ya elimu imetoa mitaala ya kufundisha wanafunzi kuhusiana na elimu ya UKIMWI shuleni.
 
Serikali inatoa wito kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmashauri kuyatumia ipasavyo magari hayo na kuhakikisha Walimu wapya wanapitishwa vyema katika mitaala hiyo pamoja na kuanzisha klabu za kuhamasisha mapambano dhidi ya UKIMWI katika shule na vyuo vyote nchini.
  1. HOJA: Serikali ibuni chanzo mahususi cha kutunisha Mfuko wa UKIMWI (AIDS TRUST FUND) kama ilivyo kwa mifuko mingine kama vile REA na maji, ili kufanikisha mapambano dhidi ya UKIMWI.
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI);
 
JIBU:
Mheshimiwa Spika,
Ushauri uliotolewa umepokelewa na Serikali itaufanyia kazi.
  1. HOJA: Kuweka utaratibu wa kufuatilia fedha zinazotolewa na wafadhili kwenye Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NGOs) zinazojihusisha na masuala ya UKIMWI.
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Dkt. Haji Mponda (Kamati ya Kudumu ya Bunge, Masuala ya UKIMWI);
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kufuatilia fedha zinazotolewa kwenye NGOs upo na tumekuwa tukisisitiza ufuatwe. Mathalan, nilipofanya ziara Mkoani Arusha hivi karibuni nilirudia wito wa kuzifanyia kaguzi za mara kwa mara NGOs zinazofanya kazi nchini. Hivyo, ushauri wa Kamati kuhusu hitaji la kufanya ukaguzi kwenye NGOs zinazoshughulikia UKIMWI utaendelea kuzingatiwa.
 
Natoa wito kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri waendelee kuhakikisha wadau wa UKIMWI wanaofanya kazi kwenye maeneo yao wanakaguliwa kulingana na Sheria ya UKIMWI ya mwaka 2008 na Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali ya mwaka 2002. Nia yetu ni kujua wanapata nini, kwa ajili ya huduma zipi ili wanufaika waweze kujulishwa.
  1. HOJA: Serikali ijiridhishe kuhusu masuala ya kitaalam na kufanya mapitio na maboresho ya Sheria stahiki katika kutekeleza Mpango wa kuunganisha Mifuko ya Pensheni.
MTOA HOJA: Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama (Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, zoezi la kuunganisha Mifuko ya Pensheni linafanyika kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu. Katika kutekeleza jukumu hilo, Mifuko yote ya Pesheni imefanyiwa tathmini (Actuarial Valuation), ambayo pamoja na mambo mengine, imebainisha kuwa kuunganisha Mifuko ya Pensheni ndio njia bora ya kuimarisha Sekta ya Hifadhi ya Jamii nchini.
 
Aidha, Serikali imeandaa Andiko la mapendekezo ya kuunganisha Mifuko. Kazi hii imefanyika kwa kushirikisha wadau muhimu katika Sekta husika. Serikali itaendelea kutoa taarifa za mara kwa mara kwa hatua zinazofikiwa.
  1. HOJA: Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.
MTOA HOJA:  Mheshimwia Zuberi Kuchauka (Liwale)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, uwekezaji ni kazi mojawapo ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Lengo la uwekezaji ni kulinda thamani ya michango ya wanachama pamoja na kukuza uwezo wa Mifuko kulipa mafao kwa wanachama wake pale wanapopatwa na majanga mbalimbali yanayowasababishia kukosa kipato. Majanga hayo ni kama vile maradhi, uzee na kifo. Kwa msingi huo, uwekezaji kwenye viwanda unaofanywa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa una manufaa mtambuka kwani pamoja na kulinda thamani ya fedha za michango ya wanachama, uwekezaji huu unakuza mapato ya Serikali, unatoa fursa za ajira na hivyo kusaidia kuongeza idadi ya wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii. Serikali itaendelea kuhakikisha kwamba uwekezaji unaofanywa na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii unazingatia Miongozo ya Uwekezaji ili mifuko hiyo isiweze kupata hasara.
  1. HOJA: Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na utoaji wa Elimu ya Mpiga Kura.
MTOA HOJA:  Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama (Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu la kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Katika Mwaka wa Fedha 2017/2018 Tume ya Taifa ya Uchaguzi itaweka kipaumbele katika uboreshaji wa Daftari la Wapiga kura.
 
Aidha, Tume ya Taifa ya Uchaguzi imepewa jukumu la kutoa elimu ya mpiga kura Nchi nzima na kusimamia na kuratibu Asasi, Taasisi au watu wanaotoa elimu ya mpiga kura. Tume imeendelea kutoa elimu ya Mpiga Kura kwa njia mbalimbali ikiwemo kutumia Redio, Televisheni, kukutana na wadau kupitia maonyesho mbalimbali, pamoja na kushiriki mikutano katika ngazi za Mikoa na Halmashauri.
  1. HOJA: Mgogoro wa Uongozi ndani ya CUF
MTOA HOJA: Mheshimiwa Joseph Kizito Mhagama (Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria) Mheshimiwa Freeman Aikaeli Mbowe (Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni); Mheshimiwa Cecilia Danel Paresso (Viti Maalum); Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah (Tumbe); Mheshimiwa Khatibu Said Haji (Konde); Mheshimiwa Juma Kombo Hamad (Wingwi); Mheshimiwa Masoud Abdallah Salum (Mtambile)
 
JIBU
Mheshimiwa Spika, Hoja hii imejadiliwa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Waheshimiwa Wabunge mbalimbali.
 
Serikali haifurahishwi na migogoro ndani ya vyama vya siasa, kwani inadumaza demokrasia nchini na kusababisha mifarakano isiyokuwa na tija. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kama mlezi wa vyama vya Siasa imekuwa ikishiriki kikamilifu katika kuhakikisha migogoro ndani ya vyama vya siasa inatatuliwa kwa majadiliano.
 
Mheshimiwa Spika, Katika mgogoro uliopo ndani ya chama cha CUF, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ilitoa ushauri kulingana na taratibu zilizopo. Hata hivyo, wakati usuluhishi ukiendelea baadhi ya wanachama wa CUF ambao hawakuridhika na usuluhishi uliofanywa na Msajili walipeleka shauri Mahakamani, ili kudai haki kwenye Mhimili wa Mahakama ikiwa ni pamoja na suala la ruzuku ambalo Mahakama imetoa zuio la muda mpaka shauri la msingi lililoko mahakama itakapolitolewa uamuzi. Kwa kuwa masuala hayo yapo Mahakamani, ni vizuri tukaiacha Mahakama ifanye kazi yake. Hiyo ni rai yangu.
 
5.0.      HITIMISHO
Mheshimiwa Spika, Kama nilivyosema hapo awali, muda usingeweza kutosha kujibu hoja zote zilizotolewa na Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia hoja. Tumejifunza mambo mengi kutoka kwenye michango yenu, na tupo tayari kuendelea kujifunza zaidi kutoka kwenu Waheshimiwa Wabunge.
 
Mheshimiwa Spika, Nchi hii ni yetu sote, na kila mmoja wetu anao wajibu wa kulisukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu. Kila mchango wa Mheshimiwa Mbunge una thamani kubwa sana kwetu, na ninawashukuru sana kwa ushauri, maangalizo na mafunzo. Endeleeni kutoa ushauri kwa Serikali, hata kwa maandishi siyo lazima kusubiri Bungeni, nasi tutaupokea na kuona namna bora ya kufanyia kazi.
 
Mheshimiwa Spika, kila Mtanzania ikiwemo Waheshimiwa Wabunge, anawajibika kuiacha Tanzania ikiwa ni nchi bora zaidi ya alivyoikuta. Ili kuifikia azma hiyo, inabidi tuanze kuwa tayari kujinyima mambo mazuri tuliyoyazoea, angalau kwa muda, ili kuimarisha misingi ya ujenzi wa Tanzania yetu. Ninawasihi waheshimiwa Wabunge wenzangu muielewe dhamira ya Serikali na mtuamini katika kusimamia rasilimali za nchi yetu kwa manufaa yetu na vizazi vijavyo. Serikali imejipanga vizuri katika kulinda maslahi ya nchi hii na wananchi wake, hivyo nawaomba muendelee kutuunga mkono kwa kupitisha Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu.
 
Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naomba kutoa hoja.

Dkt. Ngwale ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo (TBA)

$
0
0
Waziri wa Ujenzi, Uchukukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa (Mb), kwa mamlaka aliyopewa kwa mujibu wa Sheria ya Wakala wa Serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake kupitia Sheria Na. 13 ya mwaka 2009 amemteua Dkt. Edward Wilson Ngwale kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe 10.04.2017.

Mhe. Prof. Mbarawa amemteua Dkt. Ngwale kushika nafasi hiyo kwa kipindi kingine cha miaka mitatu katika nafasi ya Mwenyekiti wa Bodi baada ya uteuzi wa awali kufika ukomo.

Aidha, sambamba na uteuzi huo Prof. Mbarawa amewateua Wajumbe watano (5) wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo Tanzania kuanzia tarehe 10.04.2017 kama ifuatavyo:-

1.Eng. John Bura – Mkandarasi  kupitia Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB)
2.Arch. Pius P. Tesha – Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
3.Prof. Bakari M. M. Mwinyiwiwa – Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
4.Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya – Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
5.Eng. Amiri N. Mcharo – Wizara ya Fedha na Mipango.

Imetolewa na;

Eng. Joseph M. Nyamhanga
KATIBU MKUU (UJENZI)

12.04.2017

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza taarifa za ajira kutolewa kila robo mwaka

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza mamlaka ya serikali za mitaa, wizara na taasisi zote zitoe taarifa za ajira zinazozalishwa kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo kila robo mwaka.

Ametoa agizo hilo leo jioni (Jumatano, Aprili 12, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akitoa maelezo ya kuhitimisha majadiliano ya bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2017/2018.

Waziri Mkuu alikuwa akijibu hoja ya Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mhe. Freeman Mbowe ambaye aliitaka Serikali itoe maagizo kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri kutengeneza ajira angalau 20,000 kila mwaka katika miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri zao, na taarifa ya utekelezaji wa agizo hilo iwe inatolewa kila mwaka kwenye Bunge la Bajeti.

“Napenda, kumtaarifu Mheshimiwa Mbunge kuwa Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015, Ibara ya 59 inazielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa zote nchini kuzingatia viashiria vya ukuzaji ajira katika mipango ya maendeleo ya ngazi husika pamoja na kutoa taarifa za mwenendo wa ajira kila robo mwaka,” amesema.

Waziri Mkuu amesema maelekezo hayo, yanazingatiwa katika Mwongozo wa kuandaa Bajeti ya Serikali unaotolewa na HAZINA kila mwaka ambao unazitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi zote zibainishe fursa za ajira zinazotarajiwa kupatikana kila mwaka kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Vilevile mwongozo huo unazitaka taasisi hizo kutoa taarifa za ajira zinazozalishwa kutokana na utekelezaji wa miradi hiyo kila robo mwaka. Ninatoa agizo, Mamlaka ya Serikali za Mitaa, Wizara na Taasisi zote ziendelee kuzingatia maelekezo haya,” amesema.

Akizungumzia kuhusu ujenzi wa viwanda, Waziri Mkuu amesema ndani ya mwaka mmoja, jumla ya viwanda 2,169 vimesajiliwa vikiwemo viwanda vya mbolea, saruji, chuma na vya usindikaji wa mazao.

“Serikali pia inaendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuvutia uwekezaji nchini. Uhamasishaji wa ujenzi wa viwanda nchini ni dhahiri na tayari tumeanza kuona matokeo. Kwa mfano, mkoa wa Pwani peke yake una viwanda vikubwa 83 na vingine vidogo vidogo zaidi ya 200. Huu ndio mwelekeo wa Serikali ya Awamu ya Tano,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama alisema Programu ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji Thamani na Huduma za Fedha Vijijini (MIVARF) ilipanga kukarabati barabara zenye jumla ya kilomita 148.5, kujenga masoko manne na kukarabati kituo kimoja cha mafunzo ya utunzaji mazao baada ya kuvuna.

Akijibu hoja za utekelezaji wa programu hiyo kwa upande wa Pemba na Unguja, Waziri Mhagama alisema miradi ya ujenzi na ukarabati wa barabara ilianza Agosti na Novemba 2014 na kazi hiyo kwa Pemba ilikamilika Desemba 2015 wakati kwa upande wa Unguja ilikamilika Januari 2016.

“Kazi za ujenzi wa masoko ya Kinyasini na Mombasa (Unguja) pamoja na Konde na Tibirinzi (Pemba) zilianza Desemba 2016 na zinatarajiwa kukamilika Julai 2017. Wakandarasi wamehimizwa kuhakikisha wanakamilisha kazi hizo katika muda uliopangwa ili kuendana na ratiba iliyopangwa,” alisema.

Akijibu hoja kuhusu uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma, Waziri Mhagama alisema uamuzi wa kuhamia Dodoma na kuifanya Makao Makuu ya Serikali ilikuwa ni ndoto ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alitaka kuona Dodoma ikistawi na Serikali kuweza kuhamia huko ili kutekeleza kwa vitendo dhana ya Mji Mkuu.

Alisema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma siyo suala la kisiasa kama baadhi ya watu wanavyodai bali ni utekelezaji wa maamuzi kamili kama yalivyoelekezwa kwenye Ibara ya 151 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015 na kama ilivyotamkwa kwenye GN namba 273 ambayo ni tamko la Serikali na sheria halali.

Naye Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Vijana, Mhe. Anthony Mavunde alisema kila mwaka vijana kati ya 800,000 hadi milioni moja wanaingia kwenye soko la ajira wakati soko la ajira ni dogo.

Hata hivyo, Naibu Waziri Mavunde alisema Serikali imeanza kubadilisha mtazamo wa vijana kuhusu ajira kwani wengi wao hudhani kwamba kuwa na ajira ni lazima mtu avae tai, awe na ofisi yenye meza na kiti kinachozunguka.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma yakubali mashtaka matano dhidi ya RC Paul Makonda

$
0
0
Ndugu waandishi wa habari, kwa heshima kubwa ya kutambua nafasi yenu muhimu kwenye jamii, nimewaita hapa ili tushirikiane kuujuza umma kwamba tupo kwenye wakati mzuri wa haki kuonekana ikitendeka dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambae kwa vielelzo vyote anatambulika kama Daudi Albert Bashite lakini wengi wanamfahamu kama Paul Makonda.

Ndugu waandishi wa habari, huu ni mwanzo, na kwa hakika ni mwanzo mwema wenye kuashiria kuwa mwisho wa Daudi Bashite umewadia.

Ndugu waandishi wa habari, mtakumbuka kuwa 22 Machi 2017 mwaka huu, niliwasilisha mashitaka yangu dhidi ya Daudi Bashite kwa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, kutaka achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kukiuka maadili ya utumishi wa umma na kukosa sifa yakuwa kiongozi si tu DSM bali Tanzania kwa ujumla.

Mashtaka yangu tume yalikuwa ni yafuatayo;

1. Kugushi vyeti vya kitaaluma kuliko fannywa na RC makonda huku akijua fika kuwa vyeti anavyotumia vya taaluma si vyake wala si muhusika hivyo kujiita PAUL CHRISTIAN MAKONDA huku akijua fika kuwa yeye ni DAUDI ALBERT BASHITE, amekiuka sheria za nji nakutenda jinai.

2. Kula kiapo cha utii na uaminifu mbele ya Mheshimiwa Rais kwa uhusika wa kugushi ni kosa kubwa sana kisheria,huku akijua fika kuwa Rais alipaswa amuapishe yeye kama DAUDI ALBERT BASHITE na siyo PAUL CHRISTIAN MAKONDA.

3.Kujipatia Mali kama magari na vinginevyo kinyume na maadili ya viongozi wa umma, ambapo zawadi zote unazopokea unapaswa kutangaza hadharani, ikiwemo kupata mali hizo kwa wahusika ambao amekuwa akiwatangaza hadharani na kuwatuhumu kujihusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.

4.Kukiuka Misingi ya utawala bora haki za binadamu na utawala wa sheria kwa kutuhumu watu ovyo hadharani kuwa walijihusisha na biashara ya madawa ya kulevya kabla ya kukutwa na hatia na kisha wengine kuachiwa huru baada ya kubainika hawakutenda makosa hayo; kinyume kabisa na sheria ambapo mtu anatakiwa kutangazwa hadharani anapokutwa ametenda makosa.

5. Shitaka la mwisho lilikuwa ni la Uvamizi wa kituo cha kirusha matangazo ya redio na runinga cha Clouds media, ambapo akijua kuwa maadili ya viongozi wa umma, hayaruhusu kiongozi kushurutisha au kulazimisha jambo lolote kwakutumia madaraka yake kama kiongozi, ambapo mtuhumiwa alitenda kosa la kutaka kutumia nguvu kurusha kipindi cha kumkashifu Kiongozi wa dini wa Maknisa ya Ufufuo na Uzima almaarufu kamam Askofu Josephat Gwajima.

Ndugu waandishi wa habari, jana Aprili 12, nilipokea barua kutoka kwa Kamishna wa Tume, Jaji Harold R Nsekela akinijulisha kuwa Tume ya maadili ya viongozi wa Umma imekubali Mashtaka yangu dhidi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, na kunitaarifu kuwa wameanza kuyafanyia kazi mashitaka yote.

Ndugu waandishi wa habari, taarifa hiyo ya Kamishna wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imetoa mwanga mkubwa kwamba HAKI ambayo wengi wamekuwa wakiiomba, sasa Mwanga umeanza kuonekana.

Hivyo niwaombe wapenda haki wote popote walipo tushirikiane kwa hili ambalo mkuu wa mkoa amekuwa ni kero jijini Dar es salaam, Tupeane ushirikiano wa kuniongezea vielelezo vingine zaidi ya vile nilivyowasilisha Tume yaani vyeti na nakala zingine za mali kama nimesahau jambo lolote.

Mimi mlalamikaji na mashahidi wangu muhimu tupo tayari, mbali na matukio ya utekwaji na upoteaji wa watu lakini tumeendelea kutaka kuona mwisho wa kero hii jijini Dar es salaam, hivyo wakati wowote shauri litakapo anza kusikilizwa kwenye baraza la maadili ya viongozi wa umma, tutakuwa mstari wa mbele kutaka haki itendeke.

Wenu
Katika upiganiaji haki

BONIFACE JACOB
MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO

Orodha ya majina ya Walimu wa Sayansi na vituo vya kazi walivyopangiwa

$
0
0
Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imetangaza ajira mpya kwa Walimu wa masomo ya Hisabati na Sayansi leo tarehe 12 Aprili, 2017.

Majina ya Walimu yaliyotangazwa yanatokana na tangazo la nafasi ya kazi ya Ualimu lililotolewa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia mnamo tarehe 01 Desemba, 2016.
 
Jumla ya Walimu wapya wapatao 3,081 wakiwemo 1,544 ni wa ngazi ya Shahada na Walimu 1,537 ni wa Stashahada.
 
Walimu hao watatakiwa kuripoti kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri na baadaye kwenye Shule walizopangiwa kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi tarehe 25 Aprili, 2017. Walimu wote waripoti wakiwa na vyeti halisi vya taaluma vya kidato cha nne (IV) na kidato cha sita (VI), vyeti halisi vya kitaalaam vya kuhitimu mafunzo ya Ualimu ngazi ya Stashahada na Shahada na Cheti cha kuzaliwa.
 
Angalizo :
i. Walimu waliopangiwa vituo ni wa masomo ya Hisabati na Sayansi waliohitimu hadi mwaka 2014/2015.

ii. Kituo cha kazi cha mwalimu ni shule aliyopangiwa na sio makao makuu ya Halmashauri.
 
iii. Mwalimu atakayeripoti na kuchukua posho ya kujikimu na baadae kuondoka atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
 
iv. Walimu wote watakiwa kuripoti katika vituo vyao kuanzia tarehe 18 Aprili, 2017 hadi 25 Aprili, 2017, watakaochelewa nafasi zao zitajazwa na mwalimu mwingine.
 
v. Hakutakuwa na uhamisho ndani ya Mkoa au Halmashauri.
Majina ya Walimu hao yanapatikana katika tovuti ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI ya www.tamisemi.go.tz
 
Imetolewa na:
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais TAMISEMI

==>Orodha ya Walimu wa Shahada wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.


<<Bonyea hapa kudownload>>

==>Orodha ya Walimu wa Ajira Mpya kwa Masomo ya Sayansi na Hisabati.



Jeshi la polisi latoa tahadhari msimu huu wa sikukuu ya Pasaka

TCRA yazitoza faini kampuni za simu, Zadaiwa kutozingatia vigezo vya utoaji huduma

$
0
0
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imezipiga faini zaidi ya milioni 65 kampuni tisa za simu nchini kwa kosa la kushindwa kukidhi baadhi ya vigezo vya ubora wa huduma kinyume na matakwa ya kanuni ya  9,10 na 11 ya kanuni za ubora wa huduma za 2011

Akiongea jana na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba alizitaja kampuni hizo kuwa Benson Informatics Limited Smart, Airtel Tanzania, Vodacom Tanzania, Zanzibar Telecom Limited Zantel, Mic Tanzania Limited, Tigo, Viettel Tanzania limited, Halotel, na Tanzania Telecommunications Company Limited, TTCL huku akizitaka kampuni hizo kuhakikisha zinatoa huduma bora.

"TCRA inawakumbusha watoa huduma wote wa mawasiliano nchini kuhakikisha mnatoa huduma zinazokidhi ubora wa sauti na upakuaji wa hali ya juu (Kudownload) pamoja na kufuata sheria za huduma ya mawasiliano ya mwaka 2011". Alisema Kilaba

Aidha Mhandisi huyo alisema wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaoshindwa kukidhi vigezo vya ubora wa huduma kama ilivyo agizwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya April 14

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Yaibua Madudu

$
0
0
Ripoti  ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ya mwaka 2015/16 imeanika madudu kila kona, huku deni la Taifa likizidi kupaa.

Pamoja na hali hiyo ripoti hiyo imeeleza kwa kina namna vitendo vya ukwepaji kodi katika taasisi mbalimbali za Serikali ikiwemo migodi ya dhahabu ambayo haijalipa kodi kwa kipindi cha miaka 10.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini hapa baada ya kuwasilisha ripoti hiyo bungeni, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad, alisema ukaguzi huo umehusisha taasisi 543 kati yake 222  zikiwa za Serikali kuu, 171 Serikali za mitaa na 150 ni mashirika ya umma kati ya 200 yaliyopo.

Pamoja na hali hiyo Prof. Assad, aligusia pia suala la bajeti iliyopita jinsi ilivyotekelezwa  ambapo aliishauri Serikali kupanga bajeti inayoweza kuitekeleza badala ya kupanga kiasi kikubwa ambacho hakina uhalisia.

Hata hivyo ripoti hiyo haina tofauti na ripoti nyingine za nyuma zilizotolewa na CAG, ambapo madudu mengi yamekuwa yakiripotiwa, lakini hakuna mabadiliko katika kudhibiti ubadhirifu huo.

Ripoti hiyo pia inaonesha hati zilizotolewa kwa Serikali, Bunge na Mahakama ni 505, kati yake 436 sawa na asilimia 86.34 ni hati safi, 60 sawa na asilimia 11.88 ni  zenye shaka na nne sawa na asilimia 0.79 haziridhishi na tano sawa na asilimia 0.99 ni mbaya.

Mchanganuo wa hati zilizotolewa, unaonesha mamlaka ya Serikali za Mitaa ilikuwa na jumla ya hati 171, kati yake hati inayoridhisha ni 138, hati yenye shaka ni 32, hati isiyoridhisha ni moja huku kukiwa hakuna hati mbaya.

Msahama wa kodi tishio
Ripoti hiyo inaonyesha, taarifa ya uchunguzi ya Mei, 2016 ilibaini matumizi mabaya ya msamaha wa kodi wa Sh bilioni 3.46 ambao ulitolewa kwa walengwa wawili walioagiza magari 238.

Alisema magari hayo yalisajiliwa kwa majina tofauti na wale waliopewa msamaha huo.

“Walengwa wote waliopewa misamaha hiyo walikana kuhusika na magari hayo, hali inayoonyesha kuwa bado kuna uhitaji wa kuboresha udhibiti na ufuatiliaji wa masuala ya misamaha ya kodi,” alisema.

Misahama kwa migodi
Kuhusu tathimini ya misamaha ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya migodi, alisema ukaguzi ulibaini lita za mafuta 4,248,802 yaliyosafirishwa kutoka Dar es Salaam kati ya Oktoba, 2014 na Desemba 2015 kwa ajili ya matumizi katika migodi ya Buzwagi, Bulyankulu na Geita.

 Prof. Assad, alisema ukaguzi huo ulibaini kuwa lita 20,791,072 za mafuta yenye msamaha wa kodi wa Sh bilioni 10.17 kwa ajili ya Mgodi wa Buzwagi kwa kipindi cha miezi 18 yalisafirishwa kwenda kwa Kampuni ya M/S Aggreko na  mkandarasi msaidizi ambaye hakuwa muhusika katika msamaha huo.

 “Naishauri Serikali pamoja na TRA kufanya uchunguzi wa mafuta yote ambayo hayana ushahidi kama yamesafirishwa katika vituo vya uchimbaji madini na kukusanya kodi inayodaiwa kiasi cha Sh bilioni 1.599,” alisema.

Alisema ni lazima Serikali ihakikishe kodi ya Sh bilioni 10.17 katika mafuta yote yaliyosamehewa kodi na kupelekwa kwa wakandarasi wasiohusika na msamaha huo kama M/S Aggreko inakusanywa.

“Serikali pia ihakikishe kuwa usimamizi unaimarishwa juu ya matumizi ya misamaha inayotolewa kwa mujibu wa sheria ili kuepusha hasara kwa serikali kutokana na matumizi mabaya ya misamaha ya kodi hizo,” alisema.

Licha ya hali hiyo alisema ukaguzi ulibaini kuwa kiasi cha lita 3,874,263 chenye kodi ya Sh bilioni 2.45 kilichoingizwa nchini pasipo ushahidi wa taarifa za malipo ya kodi husika.

“Katika nyakati tofauti, sikupatiwa nyaraka za ukusanyaji wa kodi kiasi cha Shilingi bilioni 2.42 kutoka kwenye lita 3,234,420 za mafuta yaliyoingizwa nchini na kampuni 24 za mafuta na kuchukuliwa na wamiliki kati ya Januari Mosi hadi Juni 30, 2016. Hii inaonesha upungufu katika ukusanyaji kodi zitokanazo na uingizwaji wa mafuta,” alisema.

Kutokana na hali hiyo, aliishauri Serikali ifanye uchunguzi ili kubaini usahihi wa matumizi ya mafuta hayo na ikibainika hayakutumika ipasavyo, kodi husika zitozwe pamoja na riba.

“Pia serikali iboreshe mifumo ya kusimamia uagizaji wa mafuta ili kuzuia matatizo haya kujitokeza katika siku zijazo,” alisema.

Akizungumzia usimamizi na ufuatiliaji usioridhisha wa madeni ya kodi na tozo, alisema baada ya kupitia orodha ya madeni ya Idara ya uchunguzi, kodi za ndani na walipa kodi wakubwa pamoja na vielelezo vingine na kugundua kuwa Sh bilioni 588.83 (Tax Investigation Sh bilioni 92.03, DRD Sh bilioni 425.83 na Ltd  Sh bilioni 70.97) kilikuwa hakijakusanywa na mamlaka kutoka kwa walipakodi mbalimbali.

 “Hii inaonyesha udhaifu katika ufuatiliaji na ukusanyaji wa madeni ya kodi na tozo.

“Nilipitia pia sampuli ya majalada ya walipa kodi na kubaini kodi iliyokadiriwa na kukusanywa na TRA ilikuwa pungufu kwa Sh bilioni 9.45,” alisema.

CAG alisema hiyo inaashiria kuwa mamlaka haikufanya uchambuzi na upitiaji wa taarifa ya mapato ya walipakodi na vielelezo vyake ipasavyo.“Hivyo, kutoa mwanya kwa wakadiriaji kufanya tathmini ndogo kwa walipa kodi na kuikosesha Serikali mapato,” alisema.

Alisema ukaguzi wa ukusanyaji wa kodi ya forodha umebaini mamlaka haikukusanya tozo ya maendeleo ya reli Sh bilioni 9.27, kodi ya bidhaa na mafuta na riba ya ucheleweshaji malipo Sh bilioni 3.3, ushuru wa forodha Sh bilioni 9.3 kutokana na bidhaa 9,942,810 ambazo hazikuwepo kwenye maghala ya forodha na utokusanywa kwa kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) kwenye maziwa yaliyosindikwa Sh bilioni 2.96 ambayo yaliingizwa nchini.

“Hivyo, jumla ya Shilingi bilioni 613.6 hazikukusanywa na mamlaka ingawa tathmini ya kodi ilifanyika kwa hoja zote zilizoeleza hapo juu,” alisema.

Madudu Tanzanite
Profesa Assad alisema katika ukaguzi huo wamebaini kuwa kampuni ya Sky Associates ambayo ilinunua hisa za umiliki wa Kampuni TML inayoendesha Mgodi wa Tanzanite One kutoka kwa Kampuni ya Richland Januari 30 mwaka 2015 imekuwa ikiuzia madini Tanzanite Kampuni Tanzu ya Sky Associates bila kumshirikisha mbia mwenzake ambaye ni Stamico.

Pia imebaini kuwa TML inatafuta masoko na kuuza Tanzanite bila kupata kibali cha mshirika wake STAMICO ambayo ni kinyume cha kifungu cha 15.1 (b-d) cha makubaliano ya ubia kati ya Stamico na TML.

Ufisadi NIDA
Profesa Assad alisema ukaguzi umejiridhisha kuwa uongozi na watoa huduma na wazabuni wameshiriki kwa namna moja au nyingine katika ubadhirifu na udanganyifu kwenye matumizi ya fedha katika mradi wa kuboresha vitambulisho vya Taifa.

“Mradi huu unajumuisha mikataba ya manunuzi ya vifaa vya kuboresha vitambulisho vya Taifa, ununuzi wa vifaa vya Tehama kama vile IPad, programu na vifaa vya kompyuta, upatikanaji wa vibarua, bima za magari na gharama za kusafirisha na kufunga vifaa vya kusajili ambapo Sh bilioni  4.5 zilikuwa na udanganyifu,”alisema.

Alisema kutokana na hali ya usajili na kutoa vitambulisho vya Taifa kuwa mpya hali hiyo ilisababishwa na maandalizi hafifu kwa uongozi wa mamlaka ya juu ya kuamua jinsi mfumo ambao ungeweza kutumika vizurio

Alisema hali hiyo ilisababisha mabadiliko ya maelekezo yaliyogharimu Serikali kupitia manunuzi yasiyona tija na wakati huo huo wadanganyifu kutumia mianya iliyopo kujinufaisha wenyewe kinyume na taratibu.

Michango ya mifuko ya jamii
Profesa Assad alisema uhakiki wake amebaini kuwa makato ya kisheria yenye jumla ya Sh bilioni 284 yanayolipwa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya yalicheleweshwa kati ya siku 30 hadi siku 90 baada ya malipo ya mishahara ya mwezi.

“Ucheleweshaji huu ulihusisha madai ya Mfuko wa Pesheni wa Watumishi wa Umma PSFPF kwa Serikali michango ya kabla ya mwaka 1999 pamoja na madai ya miaka ya nyuma kwa mifuko mingine ya Hifadhi ya Jamii.

“Matokeo yake nimebaini ucheleweshaji wa mkubwa wa ulipaji wa mafa kwa wastaafu waliokuwa wakichangia kwenye mifuko wa pesheni kwa watumishi wa umma mwaka huu,”alisema.

Aliishauri Serikali kulipa malimbikizo ya madeni na michango yake kwa wakati kwa mifuko ili kuiwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kuiwezesha mifuko ya hifadhi ya jamii kutimiza majukumu yake ipasavyo na wastaafukupata stahili zao kwa wakati.

Tanesco hasara
Kwa upande wa Shirika la Umeme nchini (Tanesco), ukaguzi umebaini shirika lina madeni katika manunuzi ya umeme kutoka kwa watengenezaji huru wa nishati  (IPPs), na watengenezaji wa dharura wa nishati (EPPs).

Inaonesha madeni hayo yamesababishwa na Tanesco kununua uniti moja ya umeme kwa wastani wa Sh 544.65 kutoka kwa  IPPs na EPPs na kuuzia wateja umeme kwa Sh 279.35 hivyo shirika kupata hasara ya Sh 265,30 kwa kila uniti.

Ili kumaliza hali hiyo, ripoti inashauri jitihada zaidi zifanyike katika kuongeza vyanzo vya umeme wa maji na gesi na kuachana na ule wa wazalishaji binafsi wanaozalisha nishati hiyo kwa mafuta.

Uwekezaji mifuko ya pensheni
Ripoti hiyo inasema, ukaguzi umebaini kushuka kwa mapato ya uwekezaji kwa kiasi kikubwa kwenye mifuko pensheni, NSSF, PPF, PSPF, na LAPF.

Alisema hali hiyo inatokana na kutokuwepo kwa ufanisi wa menejmenti katika kusimamia mikopo iliyotolewa kwa vyama vya ushirika wa kuweka na kukopa.

Mbali na hilo ilielezwa kwamba usimamizi hafifu wa kuratibu shughuli za uwekezaji, umechangia kutokusanywa madeni ya muda mrefu ikiwa ni pamoja na Sh trilioni 1.6 kutoka serikalini.

Ushuru wa bilioni 15 wayeyuka bandari
 Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Ukaguzi Maalum kuhusu ushuru wa bandari (Wharfage), katika Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), ambao ulilenga kubaini waliohusika na ukwepaji kodi bandarini, ulibaini ushuru wa Sh bilioni 15.02 haukukusanywa na TPA kutokana na ubadhirifu wa makampuni ya kutoa mizigo bandarini, wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato (TRA) na watumishi wa mabenki.

Usimamizi wa rasilimali watu
Profesa Assad alisema udhaifu katika usimamizi wa rasilimali watu umeendelea kujitokeza, ambapo malipo ya mishahara ya Sh bilioni 7.3 na makato ya kisheria ya Sh bilioni 2.5 yalifanyika kwa watumishi walioacha kazi au kufariki.

“Ukaguzi wangu umebaini kuwa mishahara ya watumishi walioacha kazi, waliofariki au waliostaafu wameendelea kulipwa mishahara kupitia akaunti zao. Vilevile fedha za makato ya mishahara ya watumishi hao zimeendelea kupelekwa kwenye taasisi husika.

“Jumla ya Sh bilioni 1.2 kililipwa kwa sampuli ya watumishi 260 katika taasisi 919 za Serikali Kuu na Sh bilioni 6.1 zililipwa kwa watumishi katika Halmashauri 108 zilizokaguliwa,”alisema Profesa Assad.

 Alisema udhaifu mwingine uliojitokeza katika usimamizi wa rasilimali ni kushindwa kujiridhisha kuhusu urejeshwaji wa mishahara katika akaunti ya Hazina Sh bilioni 4.33.

Alifafanua kuwa katika sampuli ya taasisi 8 za Serikali Kuu na mamlaka za serikali za mitaa 53, ofisi yake ilibaini jumla ya Sh bilioni 4.33 hazikulipwa kwa wafanyakazi.

Kutokana na hili, aliishauri serikali kuweka mfumo wa mrejesho ambapo mamlaka za serikali za mitaa wakati wote zitakuwa na uwezo wa kupata taarifa za zuio la malipo.

Alitaja udhaifu mwingine kuwa ni malimbikizo ya madai ya wafanyakazi Sh bilioni 14.4, ambapo katika sampuli 7 ofisi yake ilibaini malimbikizo ya madai ya wafanyakazi yanayofikia Sh bilioni 8.2 kwa kipindi cha kuanzia mwaka mmoja hadi kumi.

Usimamizi wa mali, madeni
Alisema ukaguzi wake umebaini ongezeko la idadi ya magari yaliyotelekezwa katika taasisi mbalimbali za Serikali Kuu kutoka magari 675 mwaka 2014/15 hadi kufikia magari 1,272 mwaka 2015/16 sawa na ongezeko la asilimia 88.

Kwa upande wa Serikali za Mitaa, alisema jumla ya magari, pikipiki na mitambo inayofikia 652 yalitelekezwa pasipo hatua zozote kuchukuliwa na menejimenti.

“Kwa upande wa idara na wakala wa Serikali jumla ya magari 92 yalitelekezwa. Hata hivyo, menejimenti ya taasisi husika haikuchukua hatua yoyote. Uwepo wa mali hizi kwa muda mrefu pasipo kuuzwa, unaweza kusababisha hasara itokanayo na wizi wa vifaa na uchakavu,”alisema Profesa Assad.

Alisema kwa upande wa ukaguzi wa miradi ya maendeleo, uhakiki wa dawa zilizonunuliwa kupitia fedha za mfuko wa kimataifa wa kupambana na Malaria, Ukimwi na Kifua Kikuu uliofanyika kwenye ghala la Bohari Kuu ya Dawa, umegundua uwepo wa dawa zilizokwisha muda wake zenye thamani ya Sh bilioni 10.19.

Ofisi za Ubalozi
Alisema kama alivyobaini katika ukaguzi wake uliopita, serikali haijachukua hatua zozote kufanya ukarabati wa baadhi ya nyumba katika Balozi za Tanzania nje ya nchi.

“Kati ya balozi 34, balozi 12 zinamiliki nyumba 37 zilizo katika hali mbaya na zinahitaji marekebisho. Wakati huo huo serikali inamiliki viwanja 10 katika balozi mbalimbali ambavyo havijaendelezwa hivyo viko katika hatari ya kunyang’anywa,”alisema.

Profesa Assad alisema uhakiki wa matumizi ya miradi ya maendeleo iliyokamilika kwa baadhi ya halmashauri ulibaini miradi yenye thamani ya Sh bilioni 4.2 ambayo haijaanza kutumika kutoa huduma kama ilivyokusudiwa.

“Walengwa waliokusudiwa hawakupata faida iliyotarajiwa. Mfano wa miradi hiyo ni ya maji ya visima na bomba ambayo ilikamilika tangu mwaka 2013/14,”alisema.

Bil 24/-  bila ushindani
Profesa Assad alisema ukaguzi wake umebaini manunuzi yaliyofanyika bila ushindani kwa Serikali Kuu Sh bilioni 24.2.

“Manunuzi yaliyofanyika bila mkataba kwa Serikali Kuu kwa taasisi kumi Shilingi  bilioni 11.2, manunuzi kufanyika kwa  wazabuni wasioidhinishwa na mamlaka husika kwa Serikali Kuu kwa taasisi 14 Shilingi  bilioni 7.3.

“Manunuzi yaliyofanyika bila ushindani kwa Serikali za Mitaa Shilingi bilioni 2.1, manunuzi kufanyika kwa wazabuni wasiodhinishwa na mamlaka husika kwa serikali za mitaa halmashauri 28 Sh bilioni 1.2,”alisema Profesa Assad.

Mafuta na gesi
Profesa Assad alisema ukaguzi wake ulibaini kuwa matumizi ya bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam ni kiwango cha chini cha ujazo kwa asilimia 94 huku Tanesco akiwa ndiye mteja pekee akitumia wastani wa futi za ujazo milioni 46.61.

“Futi hizo za ujazo ni sawa na asilimia 6 tu ya ujazo wa bomba husika licha ya kuwepo makubaliano kati ya TPDC na Tanesco ya kusambaza futi za ujazo milioni  138.8 katika vituo sita vya kuzalisha umeme vya Tanesco.

“Pia nilibaini, mkataba wa Ubia wa Uzalishaji Gesi (PSA) baina ya TPDS na Kampuni ya Pan African Energy Tanzania Limited (PAET) umetengenezwa kwa namna ambayo gawio la Serikali kutoka kwenye mauzo ya gesi asilia litakuwa linapungua kadiri uzalishaji unavyoongezeka,”alisema.

Kutokana na hilo, alipendekeza kufanyika upya kwa makubaliano ya mgawanyo wa uzalishaji (PSA) ili kuiwezesha serikali kunufaika zaidi pindi uzalishaji unapoongezeka.

Pamoja na hilo, alisema ukaguzi ulibaini kifungu cha 13.1 (a) cha ibara ya XIII ya mkataba wa ushirikiano wa uchimbaji gesi ya eneo la Songosongo kinaitaka PAET kulipa kodi ya ziada ya faida.

  “Sambasamba na hayo, nilibaini PAET haijawahi kuwasilisha ripoti ya kodi ya zaidi ya faida (statements of additional profit tax).

“Hata hivyo, Sheria ya Kodi ya Mapato ya mwaka 2004 haikuwa na kipengele cha kodi la ongezeko la faida, mawasiliano na uongozi wa TRA yameonyesha kuwa sheria hii bado inaandaliwa,”alisema Profesa Assad.

Vyama vya Siasa
Profesa Assad alisema katika ukaguzi wa vyama vya siasa vinne kati ya 19 vilivyosajiliwa havikuwa na taarifa za fedha na hivyo kumfanya ashindwe kujiridhisha kuhusu usahihi wa taarifa hizo.

Alivitaja vyama hivyo ambavyo havikuwasilisha taarifa hizo kama kifungu cha 14(1) cha Sheria ya Vyama vya Siasa inavyoeleza kuwa ni NRA, UPDP, Chauma na UMD.

Alisema wafanyakazi wa vyama vya siasa walibainika kuwa hawana mikataba huku vyama vitatu vikibainika kutokuwa na akaunti benki.

Alivitaja vyama ambavyo vilikosa akaunti benki kuwa ni Demokrasia Makini, Alliance for Democracy na Chama cha Kijamii (CCK).

Pia alisema vyama vinne havikuandaa taarifa ya fedha kwa ajili ya ukaguzi kama kifungu cha 14(1) cha sheriaya vyam avya siasa ambapo alivitaja kuwa ni NRA, UPDP na Chauma na UMD.

Askari Polisi 8 Wauawa na Majambazi.....Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi

$
0
0

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za vifo vya Askari Polisi 8 waliouawa kwa kushambuliwa na watu wenye silaha jana jioni katika eneo la Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Askari Polisi hao walikuwa wakitoka kubadilishana doria na wameshambuliwa kwa kupigwa risasi wakiwa wanasafiri kwa gari katika barabara ya Dar es Salaam – Lindi.

Mhe. Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP-Ernest Mangu, familia za askari wote waliouawa, Askari Polisi wote na Watanzania wote walioguswa na vifo hivyo.

“Nimeshtushwa na nimesikitishwa sana na vifo vya askari wetu 8 ambao  wamepoteza maisha wakiwa wanalitumikia Taifa, naungana na familia za marehemu wote, Jeshi la Polisi na Watanzania wote katika kipindi hiki kigumu cha huzuni na majonzi ya kuondokewa na vijana wetu shupavu.

“Namuomba Mwenyezi Mungu atupe moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amelaani tukio hilo na matukio yote ya kuwashambulia askari polisi ambao wanafanya kazi kubwa na muhimu ya kulinda raia na mali na ametaka Watanzania wote watoe ushirikiano katika kukomesha vitendo hivyo.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Majambazi Yaliyoua Polisi 8 kwa Risasi Nayo Yameuawa

$
0
0
Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.

Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.

Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.

Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.

Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.

Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.

"Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kwenye oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati” amesema Marijani

Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi

Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

Rais Magufuli Kuzindua Mabweni Mapya Chuko Kikuu cha Dar es Salaam


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) yalaani mauaji ya Askari Polisi 8 Mkoani Pwani

$
0
0
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imepokea kwa masikitiko taarifa ya kuuwawa kwa askari wanane (8) wa Jeshi la Polisi, katika tukio lililotekelezwa na watu wasiofahamika jioni ya Aprili 13, 2017 katika kijiji cha Jaribu Mpakani, Wilaya ya Kibiti Mkoani Pwani.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vikali mauaji haya ya kikatili ya askari polisi waliokuwa kazini na wasiokuwa na hatia. Aidha, tunaungana na Watanzania wengine kuwapa pole familia za wafiwa na Jeshi la Polisi kwa ujumla.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa matukio ya mauaji ya askari polisi na wananchi wengine maeneo tofauti Mkoani Pwani tangu mwaka 2015 yamekuwa yakiongezeka na kusababisha uvunjifu wa haki za binadamu, hususan haki ya uhai inayolindwa na Katiba ya nchi, na madhara mengine kwa familia za wahanga, kwa jamii na taifa kwa ujumla.

Haki ya kuishi kama zilivyo haki nyingine, inalindwa kisheria, na pia inalindwa na mikataba mbalimbali ya kimataifa na kikanda ambayo Tanzania imeridhia. Hakuna mtu anayepaswa kuporwa haki hii ya msingi kiholela. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977) Ibara ya 14, kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata kutoka katika jamii hifadhi ya maisha yake, kwa mujibu wa sheria.

Ikumbukwe kwamba askari polisi wanapokuwa kazini wanatekeleza majukumu muhimu ya kulinda raia na mali zao, kwa hiyo usalama wao unategemewa na Watanzania wote. Yeyote yule anayewaua askari polisi siyo tu anataka kuwachonganisha askari polisi na raia, bali pia anawaweka raia hao katika hofu kubwa ya usalama wao na mali zao.

Hivyo basi, kwa mara nyingine, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inashauri kwamba:

1. Katika kuhakikisha kuwa haki ya kuishi ya askari polisi na wananchi wote inalindwa, Jeshi la Polisi na Serikali kwa ujumla wafanye uchunguzi wa kina ili kubaini sababu za mauaji haya kutokea kwa kujirudia Mkoani Pwani, na kuhakikisha wahusika wote wanapatikana na wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria, ili sheria ichukue mkondo wake.

2. Tume inawakumbusha wananchi kuwa vitendo vya ukatili, mauaji, na matendo yote yanayokiuka Sheria yanayofanywa na raia wasio wema ni ukiukwaji wa Sheria, haki za binadamu na misingi ya utawala wa sheira; Hivyo Tume inakemea matendo haya na kutaka yapigwe vita.

3. Aidha, inawataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kuhakikisha upelelezi wa matukio hayo unakamilika ili hatua za kisheria zichukuliwe kwa watakaobainika kuhusika na matukio haya.

Imetolewa na:
Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Aprili 14, 2017

Mchungaji Getrude Rwakatare ateuliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum

Ahukumia Jela Miaka 30 na Viboko 5 Ka Kosa la Ubakaji

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Hai imemhukumu Daudi Maulid (22) mkazi wa Kijiji cha Longoi, Kata ya Masama Rundugai, kutumikia kifungo cha miaka 30 jela na viboko vitano baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi na kumsababishia ujauzito.
 
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Arnold Kirekiano baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi watano uliotolewa mahakamani.
 
Miongoni mwa mashahidi hao ni mwanafunzi huyo, Dawati la Jinsia na Watoto na daktari.
 
Hakimu alisema anatoa adhabu hiyo ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye nia ya kutenda kosa kama hilo katika jamii.
 
Alisema kwa kosa la kubaka atatumikia kifungo cha miaka 30 jela na viboko vitano na kosa la kumpa mimba mwanafunzi atatumikia kifungo cha miaka mitatu na kulipa fidia ya Sh500,000.
 
Awali, mwendesha Mashtaka wa Polisi, Valeria Banda alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Oktoba 7, 2015 katika kijiji hicho huku akijua anafanya kosa.
 
Mshtakiwa alidaiwa kumbaka mwanafunzi huyo aliyekuwa na miaka 16 ambaye alikuwa anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Patmos iliyopo wilayani hapa na kumpatia ujauzito.
 
Kabla ya hukumu kutolewa, upande wa mashtaka uliiomba Mahakama kutoa adhabu kali dhidi ya mshitakiwa.

Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Aman Mwasote Ahukumiwa Kifungo cha Nje cha Miezi 6

$
0
0
Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, imemuhukumu kifungo cha nje cha miezi sita na kulipa faini ya Sh1 milioni, Aman Mwasote baada ya kutiwa hatiani kwa kumwita mtoto wa miaka tisa kuwa mchawi.
 
Mwasote, ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za Injili alishtakiwa kwa kutoa kauli kuwa mtoto huyo huwaloga wanafunzi na walimu alipokuwa kwenye mkutano wa injili.
 
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi, Venance Mlingi aliyesema mahakama imeridhishwa na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri kwamba, Mwasote alitenda kosa hilo.
 
Awali, Wakili wa Serikali, Xaveria Makombe alidai mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 20, mwaka jana eneo la Shule ya Msingi Kalobe, akiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Injili.
 
Hakimu Mlingi alisema mshtakiwa atatumikia kifungo cha nje kwa kufanya shughuli za kijamii na Aprili 20 atatakiwa kufika mahakamani ili apangiwe shughuli ya kufanya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya April 15

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images