Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Zitto Kabwe Awatuhumu Usalama wa Taifa Kwa Kuhusika na Utekaji Wa Wananchi.......Huu ni Mchango Wake Alioutoa Bungeni

$
0
0
[Sehemu ya 3 ya Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kwa mwaka 2017/18]

Mheshimiwa Spika

Kuna kijana wa kitanzania, ndugu Ben Saanane amepotea kwa zaidi ya miezi mitano sasa. Hajulikani alipo. Wazazi wake na rafiki zake wamemtafuta na kutoa malalamiko bila mafanikio. Wamefikisha taarifa kwa jeshi la polisi na wamepaza sauti bila kuchoka. Kuna nyakati suala hili lilionekana la siasa na ndio maana wengine tulikaa pembeni. Lakini sasa ni miezi 6, kuna taarifa juu ya suala hili, nimeona nisikae kimya juu ya hili.

Taarifa zinatoka chini chini, sio rasmi, kwamba huyu kijana 'ametoweshwa'. Kwamba alishikiliwa na watu wa Idara ya Usalama na amepotezwa. Jeshi la Polisi wana taarifa za mawasiliano ya mwisho ya Ben Saanane kwa kutumia simu yake ya mkononi, ambayo inaonekana simu ilipoteza mawasiliano akiwa maeneo ya Buguruni siku aliyotekwa tarehe 15/16 Novemba 2016 na tangu siku hiyo hapakuwa na mawasiliano tena.

Siku hiyo simu yake ilisoma maeneo ya Tabata asubuhi, kisha Mikocheni na Mwenge muda mwingi wa mchana. Saa mbili usiku alikuwa Mburahati na saa nne usiku ilizimwa akiwa Buguruni. Polisi wanajua kuwa wenzao wa Usalama wa Taifa ndio waliomteka kijana huyu lakini hawawezi kuchukua hatua dhidi yao. Hivyo wameamua kukaa kimya wakiamini kuwa Watanzania tutasahau.

Jambo hili linasikitisha na kuumiza sana, Ben ni kijana wa kitanzania, ni mtoto, mjomba, baba, kaka, anayo familia, siwezi hata kufikiria ni namna gani familia yake inaumia kwa miezi hii sita bila kumuona ndugu yao, bila kujua alipo, bila kujua hatma yake. Inaumiza sana, inaumiza mno, ni jambo gumu sana kulivumilia, si jambo rahisi kulipuuzia na kusahau tu. Watanzania hatupaswi kukalia kimya kuhusu jambo hili, tukisahau hili hakuna atakayepona.

Kumekuwa na matukio ya namna hii mabaya kabisa huko nyuma; ndugu Absalom Kibanda, aliyekuwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri alivamiwa na kuumizwa vibaya sana na leo jicho lake moja halioni mwaka 2013. Pia ndugu Yona wa Temeke alitekwa na kuumizwa na kutupwa huko mbweni jijini Dar es salaam na hakuna mtu yeyote aliyekamatwa juu ya matukio yote hayo. Orodha ya matukio ya namna hii ni ndefu.

Watanzania wamesahaulishwa yote haya, Polisi mpaka Leo hawajamkamata hata mtu mmoja juu ya yote hayo. Sababu kubwa ni ukimya wetu. Sisi wabunge tumepewa ridhaa na wananchi wenzetu kuyasema haya, tumepewa mamlaka ya kuihoji serikali juu ya mambo ya wananchi, na Usalama wao na mali zao ni jambo la kwanza la msingi kabisa, wananchi wetu wakiwa na mashaka juu ya usalama wao, shughuli za uzalishaji mali zitakuwa duni, uchumi wa Taifa utadorora zaidi. Tunao wajibu wa kuhakikisha Usalama wa wananchi wetu, ni wakati wa kuibana Serikali juu ya hili.

Mheshimiwa Spika,

Naomba kulikumbusha Bunge lako Tukufu na wananchi Kwa ujumla kwamba Usalama wa Taifa hawana mamlaka yeyote kisheria kukamata mtu yeyote yule Kwa mujibu wa kifungu cha 5(2) cha sheria ya usalama wa Taifa ya mwaka 1996 Kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kadhaa. Kwa hiyo Askari wa Usalama wa Taifa waliokwenda Clouds Media na silaha, Askari wa Usalama aliyemtolea silaha Mbunge wa Mtama, ndugu Nape, na kikosi cha utekaji na utesaji cha Usalama wa Taifa kinachohusishwa na utekaji wa watu wanavunja sheria ya usalama wa Taifa.

Hata askari wa Usalama wa Taifa waliomkamata Mbunge wa Geita Vijijini, ndugu Msukuma, Mbunge wa Nzega, ndugu Bashe na Mbunge mstaafu, ndugu Malima walivunja sheria ya Usalama wa Taifa. Kuna viashiria vyote kuwa hali si nzuri kabisa.

Lakini kuna jambo moja muhimu sana juu ya jambo hili, MTAZAMO HASI wa Watanzania juu ya Idara ya Usalama wa Taifa. Idara Nyeti, Muhimu na ya Kuheshimiwa mno kwa Taifa letu, inaniuma leo kusimama hapa Bungeni kuisema Idara ya Usalama wa Taifa. Mimi niko Bungeni mwaka wa 12 huu, hatuzungumzii mambo ya Usalama wa Taifa humu bungeni, jambo hilo ni 'Taboo', lakini kwa hali ilivyo sasa imenibidi niseme.

Mambo haya maovu yanayohusishwa na Idara hii yanaondoa uhalali wa Taasisi hii kwa wananchi, yanaondoa heshima, hadhi na uaminifu juu ya idara hii, yanajenga chuki na taswira hasi ya Wananchi kwa idara hii, hili si jambo jema kwa Taifa. Ni wakati sasa wa kuchukua hatua. Ni lazima Bunge liamke na kukomesha hali hii.

Kwa mujibu wa Kanuni ya 120(2) ya Kanuni za Bunge natoa Taarifa kwamba nitatoa hoja binafsi kutaka Bunge lako Tukufu kuunda Kamati Teule kufanya uchunguzi kuhusu vitendo vya utekaji, uteswaji na hata mauaji dhidi ya raia (suala la Ben Saanane likiwemo).

Pamoja na mambo mengine, Kamati teule hiyo pia nitapendekeza iangalie namna ya kufanya mabadiliko makubwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa ili kuiondoa kuwa Idara ya utesaji na badala yake kuwa idara ya kulinda Wananchi, Rasilimali za nchi na Ulinzi wa Katiba ya nchi.

Naamini wabunge wenzangu mtaniunga mkono kwenye hili.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Dodoma
Aprili 11, 2017

Zitto Kabwe: Hali ya Uchumi ni Mbaya, Watanzania Wamepoteza Matumaini

$
0
0
[Sehemu ya 1 ya Hotuba ya ndugu Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto (MB) kuhusu Mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Kwa mwaka 2017/18]

Mheshimiwa Spika,

Tangu mwezi Novemba mwaka 2015 nchi yetu ilipata Serikali mpya iliyoanza kazi kwa kasi kubwa haswa katika maeneo ya kupambana na rushwa, ufisadi na kuongeza mapato ya Serikali. Wananchi walikuwa na matumaini makubwa sana kutokana na mwanzo huu, na hata ufanisi katika utendaji wa kazi Serikalini ulianza kuboreka.

Bahati mbaya, leo tunapokutana kujadili utendaji wa Serikali wa mwaka uliopita na kupanga Bajeti ya mwaka unaofuata wa fedha matumaini hayapo tena, kuna hali kubwa ya kukata tamaa miongoni mwa wananchi.

Maeneo mengi ya nchi kuna uhaba mkubwa wa chakula na badala ya Serikali na hasa Rais kuwa matumaini Kwa wananchi akiwa Comforter In Chief, kumekuwa na maneno makali ya kuwakatisha tamaa wananchi. Bei za vyakula nchini zimepanda mno kiasi cha wananchi kushindwa kumudu chakula ili waweze kufanya kazi na kukuza Uchumi.

Taarifa za Serikali kupitia ripoti za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake juu ya hali ya Uchumi ya nchi yetu (Quartely Economic Review na Monthly Economic Review) kwa mwezi wa Disemba 2016 zinaonesha kuwa kuna mfumuko mkubwa mno wa bei za Vyakula, hasa Chakula Kikuu kwa Watanzania - Mahindi, ambapo bei ya chakula hicho kikuu nchini imepanda kwa zaidi ya 30% na kupandisha mno gharama za maisha za wananchi wote nchi nzima.

Leo bei ya kilo moja ya mahindi nchini iko sawa au ni zaidi ya bei ya kilo moja ya mchele kwenye miji mbalimbali nchini, sukari bei juu, mafuta ya kula bei juu nk. Kwa wakazi wa mjini hata bei ya gesi kwaajili ya kupikia majumbani imepanda, wananchi wamerudia matumizi ya mkaa, tujiandae na uharibifu wa misitu nchini.

Jana Ofisi ya takwimu ya Taifa imetoa Taarifa ya kuonyesha kuwa Mfumuko wa Bei umepanda kwa kasi na sasa umefika asilimia 6.4 Kwa mwaka unaoishia Machi, 2017. Ibara ya 20 ya Hotuba ya Waziri Mkuu iliyosomwa bungeni inaonyesha mfumuko wa bei wa asilimia 5.2 kwani wametumia takwimu za mwezi Desemba, 2016.

Ukuaji wa sekta binafsi umedorora na kushuhudia biashara maelfu kwa maelfu zikifungwa na kusababisha ajira nyingi kupotea na ajira chache kutengenezwa. Katka Ibara ya 26 ya Hotuba ya Waziri Mkuu inaonekana kuwa ajira 418,000 zilizalishwa mwaka 2016/17. Lakini Waziri Mkuu hakulieleza Taifa kuwa Hivi sasa Watanzania 1.6m wanaingia kwenye soko la Ajira kila mwaka. Pia Waziri Mkuu hakueleza Taifa ni ajira ngapi zimepotea Kwa viwanda kufungwa au kupunguza uzalishaji na biashara kufungwa. Manispaa ya Ilala peke yake imefunga biashara 2900 na hivyo kupoteza chanzo cha mapato ya Manispaa. Lakini hata mikopo ya Kibenki kwa sekta binafsi imepungua mno, ikiwa ni kiashiria cha mdororo wa sekta binafsi.

Matamko ya viongozi wakuu wa Serikali kuhusu mwelekeo wa Uchumi yanatuma ujumbe hasi kuhusu uwekezaji wa mitaji nchini, na hivi sasa kila mwekezaji kwenye macho ya Serikali anaonekana mpiga dili. Juhudi zote za kuhamasisha uwekaji wa mitaji nchini zilizofanywa tangu Serikali ya awamu ya tatu, zimefutwa katika mwaka Mmoja tu wa Serikali ya awamu ya tano. Hali ni ya kusikitisha sana.

Tatizo jengine kubwa ni suala la ajira, ukiondoa ajira zilizopotea kwa mdororo wa sekta binafsi, lakini pia hakuna ajira mpya serikalini tangu awamu ya tano iingie madarakani. Vijana mbalimbali waliomaliza masomo yao ya Ualimu, Utabibu, Maafisa Kilimo, Mifugo na Uvivu bado wako mtaani bila ajira kwa mwaka sasa. Hata walioajiriwa mwanzoni ajira zilisitishwa kwa kisingizio cha uhakiki wa watumishi wa Umma.

Yote hayo yana athari kwenye uchumi wa nchi, yamepunguza kipato cha wananchi, yamechangia ugumu wa maisha. Yamefuta matumaini waliyokuwa nayo watanzania na yamewakatisha tamaa. Bunge letu lina wajibu wa kuhakikisha Serikali inarelebisha hayo.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Mbunge - Kigoma Mjini (ACT Wazalendo)
Bungeni Dodoma
April 11, 2017

Juma Nkamia Kamshangaa Waziri Mwakyembe Kuhudhuria Mkutano wa Roma......Kasema Akiambiwa Ndiye Aliyemteka Atakaataje?

$
0
0
Mbunge wa Chemba Juma Nkamia leo alipata nafasi ya kusimama Bungeni Dodoma  katika kuchangia maoni kuhusu mapitio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2017/2018.

Katika vitu alivyoongelea  Nkamia ni kitendo cha Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe kwenda katika mkutano wa msanii Roma mkatoliki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana.

Amesema: Jana nilipata nafasi ya kuangalia Press Conference ya Roma. Najiuliza, Waziri wa habari alienda kufanya nini? Akiambiwa ndo alimteka Roma atakataa?

"Mtu alitekwa, serikali ndo inamwandalia press conference na kuisimamia? Ivi kesho mkiambiwa ndo mlihusika kumteka mtakataa? Najua ukweli unauma, lakini lazima tuseme.

"Serikali wakati mwingine mnaingia kwenye mitego wenyewe na mnamgombanisha Rais na wananchi.

"Nimesema ukweli, wengine wataanza kuwaza labda ni kwa sababu nilikosa uwaziri.....No, lazima tuseme ukweli."

==>Msikilize Hapo chini akiongea 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Aril 12

Rais Magufuli kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Reli ya kisasa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli leo  anatarajia kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge) katika eneo la Pugu Jijini Dar es salaam.

Hayo yalisemwa  jana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda alipotembelea eneo la mradi huo lililopo Pugu Jijini Dar es salaam. Alisema kuwa mradi huo utazalisha ajira nyingi katika kada mbalimbali.

Aidha, aliongeza kuwa mradi huo utakapokamilika utarahisisha usafiri wa kutoka Dar es salaam hadi katika mikoa ya Morogoro, Dodoma na Mwanza.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kutarahisisha shughuli za usafiri na usafirishaji kwa kuwa safari ya Dar es salaam hadi Morogoro itatumia muda wa saa 1:16, huku Dar es salaam hadi Dodoma itatumia masaa 2:30 na safari ya Dar es salaam hadi Mwanza itatumia masaa 7:30.

Mradi huo ambao uko chini ya Kampuni za Merkezi ya Uturuki na Mota-Engil Afrika ya Ureno, kwa awamu ya kwanza utaanza na kipande cha kilomita 300 kati ya Dar es salaam hadi Morogoro kwa gharama za dola bilioni moja za Marekani.

TAKUKURU Yakabidhi Ripoti kwa Rais Magufuli.....Yaokoa Bilioni 53 ndani ya Mwaka Mmoja

$
0
0
Rais Magufuli amepokea ripoti ya mwaka 2015/2016 ya utendaji kazi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) iliyowasilishwa kwake  jana na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Kamishna Valentino Mlowola.

Katika maelezo yake mafupi kwa Mhe. Rais Magufuli, Kamishna Mlowola katika kipindi cha tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani fedha za umma zilizookolewa na   TAKUKURU zimeongezeka kutoka Shilingi Bilioni 7 hadi kufikia Shilingi Bilioni 53 huku kukiwa na mafanikio makubwa katika kudhibiti mianya ya ukwepaji wa kodi na matumizi mabaya ya fedha za miradi ya maendeleo.

Amesema kutokana na nia thabiti ya Serikali ya Awamu ya Tano kukabiliana na rushwa wananchi wameitikia kwa wingi kutoa taarifa za vitendo vya rushwa na kumekuwa na ongezeko kubwa la kesi za rushwa ambazo zinafikishwa mahakamani.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU kuhakikisha wote wanaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa wanachukuliwa hatua zinazostahili na kwamba kama kuna mapungufu ya kisheria ishirikiane na vyombo husika kurekebisha sheria hizo.

“Rushwa tukiiacha iendelee tutakwama, kwa hiyo niwaombe Watanzania na vyombo vyote vinavyohusika vitoe ushirikiano mkubwa kwa TAKUKURU, lakini nitoe wito kwenu TAKUKURU, sijaona watu wakifungwa sana kwa makosa ya rushwa.

"Mtu anashikwa na ushahidi lakini akipelekwa mahakamani ushahidi haupelekwi au unafichwa kwa makusudi au anayeendesha kesi anaamua kutokuusema halafu aliyeshikwa na rushwa anaachiwa, wananchi wanawajua wanaojihusisha na rushwa, ifike mahali watu wanaokutwa na makosa ya rushwa wafungwe” alisisitiza  Rais Magufuli.

Rais Magufuli Aipa Majukumu Mazito Kamati ya Pili ya Kuchunguza Madini Katika Mchanga Unaopelekwa Nje ya Nchi

$
0
0
Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli,  jana tarehe 11 Aprili, 2017 amewaapisha wajumbe wa Kamati Maalum ya pili ya wachumi na wanasheria itakayochunguza mchanga wenye madini ulio katika makontena yaliyopo maeneo mbalimbali nchini.

Walioapishwa ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Prof. Nehemiah Eliachim Osoro na wajumbe wake ambao ni Prof. Longinus Kyaruzi Rutasitara, Dkt. Oswald Joseph Mashindano, Bw. Casmir Sumba Kyuki, Bw. Andrew Wilson Massawe, Bw. Gabriel Pascal Malata, Bw. Usaje Bernard Usubisye na Bi. Butamo Kasuka Philip.

Akizungumza baada ya kuwaapisha wajumbe wa kamati hii, Mhe. Rais Magufuli alisema ameunda kamati hiyo ili ifanye uchunguzi wa kina utakaobaini aina ya madini yaliyo ndani ya mchanga huo, thamani yake, kiwango cha kila aina ya madini, uzito wa mchanga unaowekwa ndani ya makontena na pia kujua ni makontena mangapi yamepitishwa tangu mwaka 1998.

“Kafuatilieni makontena mangapi yametoka hapa nchini na kupelekwa nje ya nchi tangu mwaka 1998, na kama hayo makontena yana madini aina ya dhahabu, shaba na silva mkafuatilie tujue zimepelekwa tani ngapi za dhahabu, tani ngapi za shaba na tani ngapi za silva, je makontena mangapi yanapita kila mwezi? Makontena 1,000 au mangapi? na je zilikuwa na thamani ya kiasi gani? Je tumelipwa kiasi gani cha fedha?

“Na nyie wanasheria mfanye uchunguzi juu ya kinachofanyika na muone sheria zinasema? Tujue utekelezaji wa sheria kama unafanyika inavyotakiwa? Tunataka hoja hizi zipate majibu” alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli alisisitiza kuwa wakati umefika kwa Tanzania kunufaika na rasilimali zake na kwamba Serikali haiwezi kukubali madini yaendelee kuondoka bila kuleta manufaa kwa wananchi.

Serikali kudhibiti biashara ya vyuma chakavu

$
0
0
Na Daudi Manongi-MAELEZO, DODOMA
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji imeandaa Rasimu ya Muswada wa Sheria itakayoweka bayana taratibu na mfumo wa usimamizi na udhibiti wa bishara ya chuma chakavu katika hatua mbalimbali za uzalishaji, ukusanyaji, usambazaji, uuzaji na uyeyushaji wake kwa kuzingatia uhifadhi na usimamizi wa mazingira kwa manufaa ya Taifa.

Hayo yalisemwa  jana na Waziri wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge Mjini Dodoma.

"Biashara ya Chuma chakavu imeshamiri hapa nchini na duniani kwa ujumla na hili limetokana na mahitaji ya vyuma chakavu ambapo kumetumiwa na wahalifu kuharibu miundombinu iliyojengwa kwa vyuma kwa nia ya kupata chuma ili waiuze kama chuma chakavu" Alisema Mwijage.

Alisema ili kukabiliana na hujuma hizi Mamlaka husika zikiwemo TANESCO, TANROADS na RAHCO wamekuwa wakifanya kazi kwa karibu na jeshi la Polisi ikiwemo kutumia walinzi wa Taasisi husika ili kulinda rasilimali hizo.

Alisisitiza kuwa Muswada huu umeweka wazi na bayana adhabu itakayotolewa kwa mtu atakayebainika kuharibu miundombinu.

Aidha Mhe.Mwijage alitoa wito kwa watanzania kutoa taarifa pindi waonapo mtu anayehujumu miundombinu kwa namna yote ile.

“Natoa wito kwa wenye viwanda na wafanyabiashara wa vyuma chakavu  jiepusheni na ununuzi wa vyuma ambavyo asili yake ina mashaka na tutaharakisha sheria hii ili kutatua tatizo hili,” aliongeza Mwijage.



Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora watoa tamko kulaani watu kutekwa

$
0
0
Jana  Jumanne Aprili 11, 2017 Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga ametoa tamko lililoambatishwa kwa vyombo vya habari kuhusiana na matukio ya watu kutekwa na kupotea.
 
Soma hapa tamko hilo la Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Bahame Tom Nyanduga :
 
Katika siku za karibuni kumekuwepo  na taarifa katika vyombo vya habari, ikiwemo mitandao ya kijamii, kuhusu matukio ya kupotea au kutekwa kwa wananchi katika mazingira yenye utatanishi, suala ambalo limeibua mijadala katika jamii.
 
Siku ya Jumatano tarehe 5 Aprili, 2017 msanii wa muziki wa kizazi kipya, Bw. Ibrahim Mussa a.k.a Roma Mkatoliki na wenzake watatu walitekwa wakati wakiwa katika studio za Tongwe Records, eneo la Masaki jijini Dar es Salaam, baada ya kuvamiwa na kundi la watu wasiojulikana. Tarehe 10 Aprili 2017 Bw. Ibrahim Mussa alieleza mbele ya vyombo vya habari jinsi walivyotekwa na kuteswa.
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inalaani vitendo hivyo, kwani vinaashiria kuwepo kwa makundi yanayoendesha matendo ya utekaji watu kinyume cha sheria.
 
Matukio ya hivi karibuni ya kuvamia kampuni za tasnia ya habari na mawasiliano au kuwateka watu, yanaashiria kutoweka kwa uvumilivu wa uwepo wa maoni tofauti katika jamii kuhusu mambo mbalimbali.
 
Kuna matukio yaliyowahi kutokea huko nyuma, kwa mfano, mwandishi wa habari wa Mwananchi Communication Ltd. (MCL) na Deutsche Welle (DW), Bi. Salma Saidi, tarehe 19, Machi 2016, alitekwa na watu wasiojulikana Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu  Julius Nyerere, akitokea Zanzibar, na inasemekana aliteswa na kuachiwa baada ya siku kadhaa.  
 
Pia kumekuwepo taarifa za kutekwa Mkuu wa Idara ya Utafiti na Sera wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Msaidizi wa Mwenyekiti wa chama hicho, Bw. Bernard Focus Saanane a.k.a Ben Saanane, aliyetoweka nyumbani kwake eneo la Tabata jijini Dar es Salaam Novemba 18, 2016 na mpaka sasa hajulikani alipo.
 
Wakati Bi. Salma Saidi na Bw. Ibrahim Mussa na wenzake watatu walionekana baada ya muda mfupi, Bw. Ben Saanane bado hajulikani alipo, yapata miezi mitano sasa.
 
Uchambuzi wa Tume unaonyesha kuwa waliotekwa wamefanyiwa hivyo kutokana na tasnia yao, au kutumia haki yao ya msingi ya uhuru wa maoni na kujieleza, haki ambazo zimeainishwa na kulindwa katika Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1977), Ibara ya 19 ya Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa (1966), na Ibara ya 9 ya Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (1986).
 
Tanzania ni nchi ambayo imeridhia na kuafiki mikataba hiyo, na matamko mbalimbali ya kimataifa yanayosisitiza haki hizo. Haki ya kujieleza inaweza kuhojiwa iwapo tu itatumika kinyume na hadhi ya mtu mwingine, au  maslahi ya taifa, kiusalama, kiafya au kimaudhui, na itahojiwa kwa taratibu za kisheria zinazokubalika katika jamii inayoheshimu demokrasia, kwa kuzingatia Katiba ya nchi na mikataba ya Kimataifa.
 
Tume inapenda kusisitiza kwamba katika nchi yenye demokrasia, serikali ina wajibu na jukumu la kuzilinda haki hizi, na pia kuwalinda wananchi dhidi ya matendo yanayodhalilisha utu wao, utesaji, na matendo yote yanayowanyima uhuru na haki zao za msingi, ikiwemo haki ya maoni na uhuru wa kujieleza.
 
Kujirudia kwa matukio ya kutekwa watu bila ya serikali kuwakamata wale wanaotekeleza matendo hayo, na kuwapeleka katika vyombo vya sheria, ni jambo la kushangaza, na la aibu kwa taifa. 
 
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inasikitishwa kuwepo kwa vitendo hivyo katika nchi yetu ambayo imejengeka katika misingi ya haki na demokrasia. Tume inapenda kutoa tahadhari kwamba vitendo kama hivyo na uwepo wa makundi ya kihalifu yanayotekeleza utekaji, utesaji,na mauaji ya watu, yaani (forced disapperance, torture, extra judicial and summary executions) hutokea katika nchi ambazo zinaashiria kuvunjika kwa utawala wa sheria. Vitendo hivi havitakiwi kuvumiliwa kabisa, na Tume haipendi kuamini kwamba nchi yetu inaelekea huko.  
 
Hivyo basi, Tume inashauri mambo yafuatayo:
  1. Vyombo vya dola, hususan Jeshi la Polisi, vifanye uchunguzi wa kina kuhusiana na matukio hayo, na kuchukua hatua zipasazo za kisheria kuhakikisha kwamba waliohusika na kupotea kwa Bw. Bernard Saanane, na utekaji wa Bi. Salma Saidi, Bw. Ibrahim Mussa na wenzake wanapatikana na kuchukuliwa hatua za kisheria.
  1. Tume inapenda kuvitaka vyombo vya dola vya ulinzi na usalama, kuwahakikishia wananchi kwamba, watu wahusikao na matukio haya siyo watu walioko miongoni mwa vyombo hivyo vya ulinzi na usalama.
  1. Ili kuhakikisha hilo ni vema Jeshi la Polisi likatangaza mapema hatua lilizochukua juu ya mtu aliyeonekana na silaha akimtishia Mhe. Nape Nnauye. Kutosikika kwa hatua zilizochukuliwa kuhusu mtu huyo kunazidi kuacha hisia katika jamii kwamba analindwa asichukuliwe hatua za kisheria.
  1. Tume inawaasa wananchi washirikiane na vyombo vya dola kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kupatikana kwa Bw. Bernard Saanane, na zitakazofanikisha kuwapata watekaji wa Bi. Salma Saidi, Bw. Ibrahim Mussa na wenzake.
  1. Mwisho kabisa Tume inapenda kuwakumbusha wananchi wote na vyombo vyote vya serikali, umuhimu wa kufuata taratibu za kisheria iwapo kuna malalamiko yoyote kuhusu matumizi mabaya ya uhuru wa maoni na haki ya kujieleza, na siyo kuendekeza utekaji na utesaji wa watu, kwani kufanya hivyo ni kujichukulia sheria mkononi na ni ukiukwaji wa sheria, ni matendo yanayotishia amani, na ni kinyume cha haki za binadamu na utawala bora nchini.

Je, Umeathiriwa na Punyeto Kiasi cha Kushindwa Kurudia Tendo la Ndoa???.....Bofya Hapa Kupata Tiba, Pia Tuna Handsome Up ya Kuongeza Maumbile

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETIC ni kampuni inayotoa bidhaa ORIGINAL zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote. Pata punguzo la bei kwa bidhaa hizi. 
 
1.HANDSOME UP ni kifaa kinachoongeza maumbile ya kiume  kwa 99% kwa size uipendayo wewe na kuimarisha misuli ya uume kwa @170,000/= tuu. 
 
2.MEN GELY kupaka. Hii inaongeza kwa wastani wa inch 6.5 na inapatikana kwa @120,000/=.  
 
3. MAX MAN 2. Ni vidonge kwa ajili ya nguvu ambavyo vinasaidia sana hata kwa watu wenye kisukari na waliokua wakifanya sana masturbation. Pia huongeza hamu ya tendo la ndoa kwa @130,000/=tu.     
 
Tupo DAR ES SALAAM  kariakoo na kinondoni kanisani.

Kwa mawasiliano zaidi piga  0759029968 au 0659618585.
Popote ulipo utapata huduma zetu.
 
Follow us
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
 
     Bidhaa zetu zote ni garantii na unapewa risiti
              Karibu

LIVE: Mshuhudie Rais Magufuli Akizindua ujenzi wa Reli ya kisasa Dar hadi Moro

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo April 12, 2017 anaweka jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa Reli ya kisasa (Standard Gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.

==>Tazama tukio zima hapo chini

Gwajima Aachiwa Huru Baada Ya Kutiwa Mashtaka ya kutoa lugha chafu

$
0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeifuta kesi ya kutoa lugha chafu inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima.
 
Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha aliifuta kesi hiyo leo chini ya kifungu cha 225 cha sheria ya Mwenendo wa Makosa ya jinai (CPA).
 
Kesi hiyo imefutwa baada ya Wakili wa Serikali, Joseph Maugo kueleza kuwa hawakuwa na shaidi na kuomba wapewe ahirisho.
 
Katika uendeshwaji wa kesi hiyo upande wa mashtaka uliita shahidi mmoja kwa miezi 14.
 
Katika kesi hii, Gwajima anadaiwa kuwa kati ya Machi 16 na 25,2015 Tanganyika Packers Kawe alitumia lugha chafu na kumdhihaki Muhadhama wa Kanisa Katoliki Askofu Kardinal Polcarp Pengo.

Rais Magufuli Akizindua Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Dar hadi Moro....Haya ni Baadhi ya Mambo Aliyoyasema

$
0
0
Rais Magufuli amezindua Rasmi ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa ya Kimataifa ambayo treni ya kisasa inayotumia umeme itaweza kusafiri kwa mwendokasi wa kilomita 160 kwa saa.

==> Haya ni baadhi ya mambo aliyoyasema
21.Unapokuwa dereva wa lori na unapopakia abiria hutakiwi kuwauliza wasimame waangalie sehemu gani, dereva mzuri anangalia kufika salama

20.Niwaombe tuangalie TZ kwanza siasa baadae, muiache Serikali ya CCM iliyoaminiwa na Watanzania itekeleze wajibu wake tutakutana 2020
 
19.Watanzania wanataka maendeleo, hakuna anayekula siasa kwa hiyo Tanzania kwanza siasa baadae

18.Tanzania tunaweza kwa hiyo tunapoyafanya haya tunafanya kwa sababu tuna wajibu wa kufanya, na haya ni malipo yangu kwenu

17.Niko kwa niaba yenu, tumeonewa sana, Tanzania ni tajiri hatutakiwi kuwa ombaomba

16.Mlinituma nifanye haya, au niwaulize ndugu zangu haya yote ninayoyafanya kweli ni mabaya?

15.Nazuia hata michanga ya madini, ninafanya kazi hii kwa niaba yenu, kwani nashindwa kusema nipelekee hiyo michanga nitaikuta Ulaya?

14.Wanasema samaki mkunje akiwa mbichi, fisadi mkunje akiwa mbichi akishakomaa mvunje, nafuu walalamike wachache, Watanzania wafurahi

13.Vita ya kupambana na ufisadi ni ngumu na hasa unapowabadilisha watu wachache waliozoea maisha fulani kwa miaka 50

12.Nataka mhandisi amalize mradi wa reli ya kisasa kabla ya miezi 30, na ikiwezekana siku ya kufungua twende bure mpaka Dodoma

11.Tunajua tunapoenda pasitokee mtu wa kubadilisha ajenda tuanze kuzungumzia ajenda ambazo hazipo kwenye ilani ya uchaguzi

10.Hivi karibuni tumepata mkopo wa kuanza kujenga barabara za mwendokasi katika awamu ya tatu na ya nne

9.Tanzania imekuwa kwa uchumi 7%, ushahidi wa kukua kwa uchumi ndio hii miundombinu tunayoijenga

8.Kazi tunazozifanya mara nyingi utakaowaona wanapiga kelele ni wale ambao walizoea kupiga dili, na mimi nataka waendelee kupiga kelele

7.Nawahakikishia Watanzania mimi ni dereva mzuri nawahakikishia lori litafika kule tunakokwenda na hili ni lori la maendeleo
 
6.Wale wataalamu wa kusoma kwenye mitandao wakaangalie ni nchi gani imejenga reli ya namna hii kwa pesa zake watakuta ni Tanzania
 
5.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30

4.Mradi huu wa ujenzi wa reli ya kisasa unatarajiwa kutoa ajira kwa watu takribani 600,000

3.Ujenzi wa reli hii ya kisasa utasaidia kutunza barabara zetu, barabara zetu zinaharibika kwa sababu zinasafirisha mizigo mikubwa

2.Ujenzi wa reli ya kisasa utakuza sekta zingine nchini, itawezesha malighafi mbalimbali kusafirishwa kwenda kwenye maeneo ya viwanda
 
1.Ujenzi wa reli huwa ni gharama kubwa, reli hii itakuwa inabeba uzito mkubwa na spidi kubwa, watu watalala Moro na watafanya kazi DSM

==>Hapo chini kuna video ya tukio hilo

Mbunge wa Nkasi Kaskazini , Ali Mohamed Keissy Achekelea Kitendo cha Roma Kutekwa......Kataka Wasanii Wote Wanaomkashifu Rais Wafanyiwe Hivyo

$
0
0
Mbunge wa Nkasi Kaskazini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ali Mohamed Keissy amefunguka na kusema wasanii ambao wanaandika nyimbo za kumtukana na kumkashfu Rais Magufuli wanapaswa kupata kibano zaidi ili waache tabia hiyo

Mbunge huyo amesema hayo leo bungeni na kusema angeaachiwa yeye dakika mbili tu wangeona ni nini angewafanya, hivyo kuendelea kuwatetea wasanii hao ni jambo ambalo si sawa, na kusema wasanii hao wajaribu kwenda Rwanda au nchi za kiarabu waone jinsi watakavyonyongwa.

"Mtu anaimba wimbo wa matusi kumtukana Rais mwanzo mpaka mwisho halafu anaachiwa nchi gani hii? Utawala gani huu? Wewe mtu unamtukana Rais unaachiwa?, aende Rwanda kule au nchi za kiarabu watakunyonga. Unamtukana Rais wa nchi wewe umekuwa nani? Uhuru gani huu, Demokrasi gani hii? Unaimba wewe nyimbo na mtu wa studio anarekodi ama kweli huu si utawala wangeniachia mimi dakika mbili ili niwaoneshe hawa" alisema Mbunge Kessy

Keissy anasema ni jambo ambalo haliwezekani mtu kumuimba Rais anamtukana na wewe kuendelea kushabikia  huku akidai kuwa yeye ameusikiliza wimbo wa Roma na kusikitishwa na kile kilichoimbwa.

"Ukiusikia huo wimbo wa Roma Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu sana, haiwezekani mtu na akili yako unasikia wimbo kama ule halafu unashabikia mtu, haiwezekani kusema kweli ni makosa, ni kukosa adabu Rais wa nchi hatukanwi popote pale haiwezekani nendeni nchi zingine, nenda Rwanda hapo nenda Burundi nenda DRC Congo ukaangalie watakushugulikia, nyinyi mnacheka cheka hapa. Rais haiwezekani kumchezea namna hii huu ni utovu wa nidhamu" alisisitiza All Keissy

Video: Godbless Lema Atoa ONYO Kali kwa Waliopanga Kumteka

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewaonya watu aliodai kuwa wamemuweka kwenye orodha ya wabunge kumi na moja wanaotakiwa kutekwa.

Akizungumza leo na waandishi wa habari mjini Dodoma, Lema amedai kuwa yeye haogopi vitisho vya kutekwa na kwamba wanaopanga kumteka wanapaswa kufahamu kuwa hawatafanikiwa na kwamba hakuna atakayeweza kusababisha kifo chake isipokuwa Mungu pekee.

“Ninawaonya watekaji, kwamba ninamjua Mungu ninaemwamini, kwamba hawataliona kaburi langu wala mauti yangu kwa sababu Mungu ninayemuamini najua nguvu zake na najua uwezo wake,” alisema Lema.

“Kwahiyo mimi kutekwa haitawezekana, kuuawa na mtu haitawezekana kwa sababu namtumaini Mungu kwa nguvu zangu zote,” aliongeza Mbunge huyo.

Kauli hiyo ya Lema imekuja kufuatia kauli ya Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe aliyeeleza jana Bungeni kuwa alionywa na baadhi wa watu wakiwemo mawaziri kuwa yeye ni miongoni mwa wabunge kumi na moja walio kwenye mpango wa kutekwa na genge la watu wasiojulikana.
 
==>Msikilize hapo  chini  akiongea

VIDEO: Msikilize Mbunge Ally Kessy Akiongelea Sakata la Roma Kumtukana Rais

$
0
0
Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy amedai kuwa msanii Roma Mkatoliki amerekodi wimbo ambao una lugha ya matusi dhidi ya Rais, na kulaani kitendo hicho.

Akizungumza leo bungeni mjini Dodoma, Kessy ambaye alionesha kuumizwa na kitendo cha kuandika na kurekodi nyimbo zenye lugha za kuudhi dhidi ya Mkuu wa nchi alihoji uhuru na demokrasia inayotoa nafasi hiyo.

“Wewe unamtukana Rais wa nchi umekuwa nani? Uhuru gani, demokrasia gani hii. Unaimba wimbo na mtu wa studio anarekodi, ama kweli huu sio utawala… wangeniachia mimi dakika mbili niwaoneshe hawa,” amesikika Kessy.

“Haiwezekani, Mkuu wa nchi anatukanwa. Ukiusikia huo wimbo wa Roma sijui Mkatoliki ndugu zangu ni wimbo wa aibu. Haiwezekani mtu anaachia wimbo kama ule halafu unamshabikia tu,” aliongeza.
 
==> Msikilize hapo chini akiongea

Mbuge wa Igunga (CCM) Dk. Dalaly Peter Kafumu Awaponda Wabunge wa CCM naa Wasaidizi Wegine wa Rais

$
0
0
Mbuge wa Igunga Dk. Dalaly Peter Kafumu amefunguka na kusema kuwa wasaidizi wa Rais wakiwemo wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mawaziri, na wabunge wa upinzani na washauri wa karibu wa Rais wamekuwa wanafiki na kushindwa kumshauri

Dalaly ametoa kauli hiyo kwa madai ya kushindwa kumshauri vizuri Rais Magufuli katika mambo ya msingi ambayo yanaweza kuleta maendeleo katika taifa

Dkt. Kafumu amesema hayo bungeni wakati akichangia Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, mbunge huyo anasema viongozi hao wanashindwa kutumia vyema sifa kuu tatu za Rais Magufuli ambazo ndizo zilikuwa zinahitajika kwa muda mrefu.

"Tumepata Rais ambaye sifa zake tatu zilikuwa zinahitajika sana, sifa ya kwanza ana nia thabiti ya kuleta maendeleo kwa wanyonge, sifa ya pili anaamua papo kwa papo hacheleweshi, sifa ya tatu anataka watu wafanye kazi, sifa hizi sisi baadhi yetu tumezitumia vibaya tumeshindwa kuzitumia vyema ili nchi yetu isonge mbele. Baadhi yetu wabunge wa upinzani na CCM, baadhi yetu mawaziri siyo wote na baadhi yetu wasaidizi wa Rais tumeshindwa kusema kweli, tumeshindwa kushauri kwa ukweli tumekuwa wanafiki na hili jambo litatuua sana" alisema Kafumu

Kafumu anadai wengi wao wamekuwa wakitengeneza ushauri nusu nusu kwa Rais jambo ambalo linafanya zile sifa zake tatu kuu zitumike vibaya, kwa kufanya maamuzi kwenye jambo ambalo huenda halijakamilika.

"Rais anaamua pale pale unafikiri kitatokea nini? tunahitaji uchambue ushauri wako, uupime, uutengeneze ushauri uende umekamilika, na Rais wetu huyu anayefanya papo kwa papo akiamua nchi inasonga mbele, sasa hivi haya yote tunayoyaona ni kwa sababu ya unafiki umezidi miongoni mwetu" alisema Kafumu

Serikali yatoa ajira kwa walimu 3,081.....Yasema upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati ni 60%.

$
0
0
Serikali imesema jumla ya walimu 3,081 wakiwemo walimu 7 wa shule ya Sekondari Omumwani Kagera, wameajiriwa, hivyo bado kuna nafasi ya walimu 1.048 kati ya nafasi 4,129 za walimu wa Sayansi na Hisabati zilizotolewa kibali cha ajira.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene alipokuwa  akizungumza na Waandishi  Habari,ofsini kwake ambapo amewataka walimu wote walioajiriwa wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia tarehe 18 hadi 25 mwezi huu.

Amesema walimu walioajiriwa  wamepangwa moja kwa moja na TAMISEMI katika halmashauri zote nchini ambazo zina upugufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati.

Simbachawene amesema kati ya walimu hao walioajairiwa walimu 1,537 ni wa Shahada  na walimu 1,544 ni wa Stashahada.

“Sehemu kubwa ya walimu wa Shahada wamepangwa  kwenye shule za kidato cha tano na sita na wachache kwenye shule za kidato cha kwanza hadi cha nne’’ alisema.

Simbachawene amekiri  kuwa kuna upungufu wa walimu 26,026 wa masomo Sayansi na Hisabati katika shule mbalimbali za sekondari nchini.

“Moja ya changamoto kubwa ambazo zinaikabili sekta ndogo ya elimu ya sekondari ni upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati upungufu uliopo  katika shule 3,602 ni 26,026 sawa na asilimia 60.14 ya walimu 43,248 wanaohitajika” amesema Simbachawene

Amesema walimu wanaohitajika kwa masomo hayo ni walimu 43,248 lakini waliopo kwa sasa ni 17,252 pekee.

Amesema kwa sasa serikali ina shule za sekondari 3,602 na kati ya hizo shule 333 ni za kidato cha tano na sita huku zingine 54 za kidato cha tano zimeanzishwa .

Aidha amesema shule hizo za sekondari kwa upande wa masomo ya Sanaa ina ziada ya walimu 7,463 ambapo waliopo ni walimu 63,240 na wanaohitajika ni walimu 55,777.

“Kutokana na ziada hiyo ya walimu wa Sanaa serikali imeanza kuchukua hatua yawahamisha walimu hao katika shule za msingi ili kuziba upungufu wa walimu katika shule hizo’’ alisema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya April 13

Rais Magufuli Ampigia Simu Mwana FA na Kumpongeza

$
0
0
Msanii wa Hip hop Tanzania Hamis Mwinjuma maarufu kama mwana FA jana alielezea alivyofurahishwa na simu aliyoipokea kutoka kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John pombe Magufuli akizisifia kazi zake.
 
Mwana FA katika ukurasa wake wa twitter aliandika kuwa “Nimefurahi kupokea simu ya Mheshimiwa Rais Magufuli kunisalimia na kuniambia kuwa yeye ni mpenzi wa kazi zangu”
katika kuthibitisha furaha yake, Mwana FA aliandika ujumbe mwingine ambao ni mstari ulioko katika wimbo wake wa iliobamba wa ‘Dume Suruali’ unaosema ‘utoe hela kwani ina TV ndani’ kwa lafudhi ya kisukuma huku akitilia mkazo kwa kuweka herufi kubwa katika neno ‘heRA’ ikiwa ni namna ya kuigiliza anavyoongea Mheshimiwa Rais.

Siyo mara ya kwanza kwa Rais Magufuli kupiga simu kwa wasanii na kuwapongeza kwa kazi zao. Amekuwa na kawaida ya kupongeza pia vituo vya redio na televisheni na kutoa michango mbalimbali katika kuhamasisha ukuaji wa sanaa nchini.
 
Amewahi kupiga simu Clouds tv kupitia kipindi chao cha ‘Clouds 360’ kinachorushwa kila siku asubuhi na kile cha ‘SHILAWADU’ kinachorushwa siku ya Ijumaa kuanzia saa 3 usiku akiwapongeza watangazaji kwa juhudi wanazozifanya na kuwapongeza.
 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images