Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Dkt Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. Justin Ntalikwa kuanzia leo tarehe 26 Machi, 2017.

Nafasi ya Katibu Mkuu wa wizara hiyo itajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

26 Machi, 2017

Alichokisema Mkuu wa Majeshi Kuhusu Deni la Tanesco

$
0
0

Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Venance Mabeyo amesema Jeshi lake lipo tayari kupunguza deni linalodaiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) Bilioni 3, huku akiahidi kesho Jumatatu kuanza kwa kupunguza deni hilo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Makao Makuu ya Jeshi (Ngome) Jijini Dar es Salaam amesema deni hilo limetokana na matumizi makubwa ya umeme, ukubwa wa jeshi lenyewe na mgawanyiko wake nchi nzima, zana wanazotumia huku nyingine zikilazimika kuwashwa muda wote kwa saa 24 kwa lengo la kulinda na kuimarisha ulinzi wa Taifa.

"Baada ya kupokea maelezo ya Tanesco na kufuatia tamko la Rais, Jeshi la Wananchi limetafakari na limefanya jitihada kupata fedha za kupunguza deni hili, tunadaiwa fedha kiasi kinachozidi kidogo Sh3 bilioni na Tanesco peke yake, tayari nimeagiza watendaji wetu watafute kiasi cha Sh 1 bilioni na wahakikishe kesho Marchi 27, cheki inawafikia Tanesco haraka ili huduma hiyo iendelee kutumiwa." Alisema Mabeyo

Pamoja na hayo Mkuu huyo amesema ufinyu wa bajeti umekuwa changamoto kubwa kwao katika kukabiri mahitaji makubwa katika jeshi hilo.

Kwa upande mwingine Mabeyo ameshauri na kusisitizia kwa Taasisi nyingine za Serikali kulipa deni ili kuongezea Tanesco uwezo wa kutoa huduma bora zaidi sekata za utumishi pamoja na kwa wananchi kwa ujumla ambao mpaka sasa wanashida ya umeme.

Bunge laahidi kuunda timu maalum kuchunguza biashara ya usafirishaji wa mchanga wa dhahabu

Polepole atolea ufafanuzi mabadiliko ya CCM ili kuondoa uzushi Kuhusu Kumpata Mgombea wa Urais 2020

$
0
0
Na Humphrey Polepole
Mabadiliko ya Katiba ya CCM 2017 yamegusa maeneo gani?
Hivi karibuni kumekuwapo maneno ya upotoshwaji juu ya Mabadiliko ya Katiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yaliyofanyika tarehe 12 Machi 2017. Napenda kufafanua kwa uchache maeneo ambayo yamefanyiwa Mabadiliko ili kuanzia sasa ieleweke bayana kwamba msingi wa Mabadiliko haya ni Mageuzi Makubwa ambayo yanafanywa na Chama chetu ili kuongeza tija, ufanisi, uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kupiga vita rushwa na ubadhirifu wa mali za umma.
 
Mageuzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yanalenga kutizama Uongozi (Leadership), Muundo/Mfumo (Structure/System) na Utawala (administration). Chama chetu kimetimiza miaka 40 mwaka huu (2017) tangu kuanzishwa kwake na kipindi hiki tumeazimia kwa kauli moja kukiimarisha, kukijenga na kukifanya madhubuti. Kazi hii ya Mageuzi ya CCM ilianzishwa na Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokaa katika Mkutano wake wa mwenzi Desemba 2016 na baadaye kupitishwa kwa sauti moja na Mkutano Mkuu Maalum wa Machi 2017.
 
Ikumbukwe kwamba mabadiliko haya ya Katiba yangaliweza kupendekezwa na kuanza kutumika pasina ya kuitisha Mkutano Mkuu, lakini hekima ya Uongozi wa Chama chini ya Mwenyekiti Ndugu Magufuli na Katibu Mkuu Ndugu Kinana ikatuongoza kwamba Mabadiliko haya ambayo yanajenga msingi wa Mageuzi ya Chama chetu lazima yashirikishe wanachama wetu.
 
CCM kama chama cha siasa ili kifanye kazi yake vizuri na yenye matokeo makubwa chanya, ilikusudiwa lazima kihuishwe ili kiweze kwenda na wakati na kutekeleza matakwa ya wanachama, kwa kuzingatia ukweli kuwa lengo kuu la chama chochote cha siasa ni kushika dola.
 
Mabadiliko ya Kikatiba ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) yana lengo la kukiimarisha chama chetu ili kuziteka hisia, mioyo na fikra za watanzania wengi, kwa nia ya kukiunga mkono katika lengo lake la kushika dola na kuleta maendeleo endelevu kwa watanzania.
 
Katiba ya CCM imekuwa ikifanyiwa marekebisho mara kwa mara tangu ilipotungwa mwaka 1977, kwa madhumuni ya kuiboresha ili iendane na wakati uliopo. Kwasababu hiyo, yamekuwepo matoleo 12 ya Katiba hii hadi mwaka 2012. Katiba ambayo imepitishwa na Mkutano Mkuu Maalum tarehe 12 Machi 2017 jijini Dodoma, inakuwa toleo la 14.
Mabadiliko haya yanalenga kurekebisha Muundo, Mfumo, Uongozi, Utendaji na mengineyo.
 
Mambo muhimu ambayo yamezingatiwa katika marekebisho haya ni yafuatayo; –
 
MFUMO WA CHAMA
Mfumo wa Chama, una sura ya serikali na utawala na kuwa na ngazi nyingi ya vikao vya uamuzi. Hali hii inafanya gharama ya kukiendesha Chama kuwa kubwa, vikao haviitishwi na maamuzi ya chama hayawafikii walengwa. Hivyo basi yafuatayo yanazingatiwa,
 
Kupunguza wingi wa vikao vya nadharia na badala yake kuwa na vikao vichache vinavyofanyika, vyenye maamuzi yenye tija na kujenga uhai wa chama.
 
Kupunguza idadi ya wajumbe au wawakilishi ili wawe wachache lakini wenye umakini na uwezo wa kusimamia sera, itikadi, maamuzi ya chama pamoja na kuondoka urasimu na kupunguza gharama za uendeshaji pasina kuathiri ubora wa uwakilishi.
 
Muundo wa Wilaya za Chama uendane na uundo wa sasa wa wilaya za Serikali
Uzito mkubwa umewekwa katika kuimarisha chama katika ngazi ya shina, eneo ambalo ndilo waliko wapiga kura. Kwa kufanya hivyo, chama kitakuwa karibu na watu na watakiona kuwa ni chama chao.
 
Uendeshaji wa shughuli zote za jumuia za chama na mali zake uwe chini ya usimamizi wa Chama cha Mapinduzi na Baraza la Wadhamini la Chama cha Mapinduzi.
 
VIONGOZI
Viongozi wachache wamekuwa na tabia ya kujilimbikizia nafasi nyingi za Uongozi, utendaji na uwakilishi katika Chama na Serikali. Hali hii hushusha ufanisi na kupunguza tija. Nafasi nyingi kwa mtu mmoja ni kushindwa kuleta ufanisi katika vikao husika.
 
Hapa imezingatiwa kuwa; ukiacha wale wanaolazimishwa kikatiba kuwa na nafasi zaidi ya moja kwa mujibu wa mamlaka yao, kuanzia sasa nafasi za Uongozi katika chama zitakuwa si zaidi ya moja.
 
KURA YA MAONI
Mfumo wa kura za maoni hukusudia kuimarisha demokrasia ndani ya chama na kuashiria nafasi ya mgombea anayeonekana kukubalika zaidi. Hata hivyo, eneo hili limekuwa na matokeo mabaya ya kukithiri kwa rushwa na kupata viongozi wasio na imani ya kweli ya chama wanaosaka maslahi, wafanyabiashara wenye malengo binafsi na mamluki.
 
Mapendekezo ya kuimarisha udhibiti wa kura za maoni; –
Katiba ya CCM ya Mwaka 1977 Toleo la 2012 Ibara ya 61A(1-3) inaelekeza kura za maoni za ubunge na uwakilishi zitapigwa kwenye mikutano mikuu ya jimbo na si kwa wanachama wote matawini kama ilivyofanyika mwaka 2015.
 
Imependekezwa ili kudhibiti taratibu za kura za maoni jimboni, kuepusha migawanyiko, kuziba mianya ya rushwa na kuepusha wapiga kura mamluki, inapendekezwa kufanya mabadiliko ya upigaji kura za maoni za ubunge na uwakilishi pamoja na kufuata utaratibu ufuatao wa kuwajadili wanaogombea;
 
Wagombea ubunge/uwakilishi watachukua fomu na kurudisha kwa Katibu wa CCM wa Wilaya inayohusika. Fomu zote za wagombea ubunge/uwakilishi zitajadiliwa na kutolewa mapendekezo katika ngazi ya wilaya, mkoa na Taifa kabla ya kupigiwa kura za maoni.
 
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa itateua majina yasiyozidi matatu ambayo yatawasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu wa Jimbo kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni. Mkutano Mkuu wa Jimbo utapiga kura za maoni kumpendekeza mwanachama mmoja awe mgombea wa ubunge/uwakilishi katika jimbo hilo.
 
Mara ya baada ya kura za maoni, mapendekezo ya uteuzi yataanzia kwenye Kamati ya Siasa Jimbo (kwa Zanzibar), Kamati ya Siasa ya Wilaya (Tanzania Bara), Mkoa, Kamati Maalum (Kwa Zanzibar), Kamati Kuu na hatimaye Halmashauri Kuu ya Taifa itafanya uteuzi wa mwisho.
 
Utaratibu huu hautawapa fursa wagombea kutengeneza makundi na kutoa rushwa kwasababu hakuna anayejua kama atakuwepo kwenye orodha ya wagombea. Wale wana CCM wenye tabia ya kujiandaa na vyama zaidi ya kimoja, kwa utaratibu huu hawataweza kujiandaa mapema kuhamia vyama vingine. Utaratibu huu pia utasaidia kuondoa urasimu na migawanyiko isiyokuwa na sababu.
 
Aidha, utaratibu huu utahakikisha anapatikana mgombea mwenye msimamo thabiti wa Chama na ni utaratibu halisi kwa chama kuusimamia ipasavyo.

Habari Zilizop Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 27

Rais Magufuli ateua Makamishna sita wa Jeshi la Uhamiaji

$
0
0
Rais John Pombe Magufuli amewapandisha vyeo maafisa sita wa Uhamiaji kuwa Makamishna kuanzia februari 28, mwaka 2017 na kuwateua kushika nyadhifa mbalimbali katika Jeshi hilo.

Wateule hao ni Mrakibu wa Uhamiaji (SI) Edward Peter Chogero kuwa Kamishna wa Divisheni ya Fedha na Utawala pamoja na Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Samwel Rhobby Magweiga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Udhibiti na Uongozi wa Mipaka.

Wengine ni Mrakibu Mwandamizi (SSI) wa Uhamiaji Gerald John Kihinga kuwa Kamishna wa Divisheni ya Pasipoti na Uraia, Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Musanga Mbusuro Etimba ambaye anakuwa Kamishna wa Divisheni ya Hati za Ukaazi na Pasi.

Aidha Mrakibu Mwandamizi wa Uhamiaji (SSI) Hennerole Morgan Manyanga ameteuliwa kuwa Kamishna wa Divisheni ya Sheria.

Rais amemteua pia naibu Kamishna wa Uhamiaji Mourice David Kitinusa kuwa Kamishna Chuo cha Uhamiaji  cha kikanda (TRITA)

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Meja Jenerali Projest Rwegasira, amesema kuwa uteuzi huo unaanzia februari 28, mwaka 2017.

CCM yateua Makatibu wa Mikoa 31, wa Wilaya 155. ......Yaeleza msimamo wa chama kuhusu Makonda

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kuendelea kufanya mageuzi ya uongozi, muundo na mfumo, kimefanya uteuzi wa makatibu wa mikoa 31 wakiwamo wapya 20, na wa wilaya 155 ambao uteuzi wao unaanza mara moja kuanzia jana.

Pia chama hicho kimekiri kufanya mabadiliko ya kikatiba yanayolenga maeneo matatu ambayo ni misingi ya uongozi, muundo na mfumo pamoja na utawala na utendaji kwa lengo la kukijenga zaidi chama hicho, na hakuna sehemu yoyote kwenye Katiba hiyo iliyobadilishwa inayohusu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema kati ya makatibu hao walioteuliwa wa mikoa 11 ni wale waliopandishwa hadhi kutokana na utendaji wao na 20 ni wapya kabisa.

Alisema katika orodha ya makatibu hao walioteuliwa, chama hicho kilizingatia sifa hizo ikiwemo maadili, weledi, jinsia na mpango wa kuachiana vijiti kwa kuzingatia rika.
 
Uteuzi wa Makatibu wa CCM Mikoa…
  1.     Arusha- ­ Elias Mpanda
  2.     Dar es Salaam-­ Saad Kusilawe
  3.     Dodoma- ­ Jamila Yusuf
  4.     Geita- ­ Adam Ngalawa
  5.     Iringa- ­ Christopher Magala
  6.     Kagera­- Rahel Degeleke
  7.     Katavi­- Kajoro Vyahoroka
  8.     Kigoma-­ Naomi Kapambala
  9.     Kilimanjaro-­ Jonathan Mabihya
  10.     Lindi­- Mwanamasoud Pazi
  11.     Manyara- ­Paza Mwamlima
  12.     Mara- ­Innocent Nanzabar
  13.     Mbeya- ­Wilson Nkhambaku
  14.     Morogoro-­ Kulwa Milonge
  15.     Mtwara- ­Zacharia Mwansasu
  16.     Mwanza-­ Raymond Mwangala
  17.     Njombe-­ Hossea Mpagike
  18.     Pwani-­ Anastanzia Amasi
  19.     Rukwa-­ Loth Ole Nesere
  20.     Ruvuma­- Amina Imbo
  21.     Shinyanga- ­Haula Kachambwa
  22.     Simiyu-­ Donald Etamya
  23.     Singida-­ Jimson Mhagama
  24.     Tabora-­ Janeth Kayanda
  25.     Tanga-­ Allan Kingazi.
“Makatibu wengi (20) tuliowateua ni wapya, hatuwezi kufanya mageuzi ya kuwa na CCM mpya na upya huo usionekane. Mageuzi ni fikra” amesema Polepole.

Lakini pia alisema katika orodha hiyo ya makatibu wa wilaya wa CCM 155, makatibu 76 ni wapya kutokana na vigezo vipya vilivyowekwa na chama hicho.

Aliwataja baadhi yao kuwa ni Mussa Matoroka anayekwenda Arumeru, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba ‘Gaddafi’ (Longido), Joyce Mwenda (Namtumbo), Kombo Kamote (Bagamoyo), Grevas Ndaki (Momba), Othman Dunga (Hanang), Pili Augustino (Dodoma Mjini) na Martin Mwakitabu (Chamwino).

Wengine ni Aveline Ngwada (Bukombe), Nuru Ngeleja (Chato), Michael Mbaga (Iringa Mjini), Afidu Luambano (Temeke), Joyce Mkaugala (Ilala), Hanaf Msabaha (Kinondoni), Salum Kali (Ubungo), Robert Kalenge (Kigamboni), Ramadhan Dallo (Arusha) na Gulisha Mvanga (Monduli).

Kuhusu suala la Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam, Polepole alisema, kwanza napenda kusema kuwa uhusiano wa CCM na vyombo vya habari ni wa kihistoria’… CCM inapenda kufuata utaratibu na ndio salama yetu kama yupo kiongozi wa chama amefanya jambo tuna utaratibu mzuri wa kuchunguza. Lakini pili, Mkuu wa Mkoa ni mteule wa Rais na anapomteua anamteua yeye peke yake na halazimiki kushauriana na mtu, hivyo badala ya kukaa na kumpangia Rais kitu cha kufanya, tumuache afanye kazi’.. “

Aidha, Humphrey Polepole akitolea ufafanuzi madai yanayoenezwa kuwa wamefanya mabadiliko kuwa Rais Magufuli ndiye atakayegombea 2020 bila kupingwa amesema kuwa, mabadiliko ya katiba waliyoyafanya katika mkutano mkuu maalum, hayakuhusu mchakato wa kumpata mgombea wa uchaguzi mwaka 2020. Hivyo tunawaomba wanachama wetu na watanzania wapuuze habari nyingine zinazoenezwa.

Katibu wa CCM itikadi na Uenezi ­Taifa

Sakata la Nape Kutishwa a Bunduki: Mgeja Amtaka Waziri Mkuu Aombe Radhi kwa Niaba ya Serikali

$
0
0
Mwenyekiti  wa Taasisi ya Tanzania Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja, amelaani kitendo cha kutishiwa kwa silaha ya moto aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Vijana, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Amesema kwamba, kitendo kilichofanyika dhidi ya Nape ni ukiukwaji wa haki za kibinadamu na utawala bora ambacho hakiwezi kuvumiliwa.

Mgeja, ambaye alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, kabla hajahamia Chadema mwaka juzi, alitoa kauli hiyo jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Kigoma.

Pamoja na hayo, alimuomba Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, asimame hadharani kuwaomba radhi Watanzania kwa niaba ya Serikali.

“Mbali ya kuwaomba radhi Watanzania, waziri mkuu achukue hatua mara moja ya kukomesha vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, ikiwamo kuheshimu misingi ya demokrasia kwa kuzingatia katiba ya nchi, sheria, kanuni na taratibu,” alisema Mgeja.

Akifafanua zaidi, mwanasiasa huyo alisema tukio la Nape kutishiwa silaha ni moja ya matukio ya ukandamizaji wa haki za binadamu yanayoendelea kutokea nchini na kwamba yanatakiwa kukemewa kabla hayajaleta madhara zaidi kwa wananchi.

“Kwa kweli mimi binafsi pamoja na taasisi yangu ya Tanzania Mzalendo Foundation, tunalaani vikali kitendo kilichotendwa hadharani na mmoja wa walinzi wa raia.

“Yaani kitendo cha kumtisha raia kwa silaha ya moto kwa lengo tu la kumzuia asizungumze na wanahabari hakikubaliki, tukio hili limetushtua na kutusikitisha Watanzania.

“Matukio haya ni ishara ya wazi ya ukandamizaji wa demokrasia na ni matumizi mabaya ya madaraka ambayo yameanza kushika kasi miongoni mwa viongozi wa Serikali.

“Wananchi wengi hivi sasa hawatendewi haki, angalieni yanayotokea kwa wafugaji, ikiwamo tukio la hivi karibuni ambalo vijana wawili wa kifugaji kule Bagamoyo walipigwa risasi na kufariki.

“Wananchi wanyonge hivi sasa wanajiuliza iwapo mtu aliyekuwa waziri wa Serikali na kada maarufu ndani ya chama tawala na aliyekipigania kiweze kupata ushindi japokuwa kwa goli la mkono, leo anafanyiwa vitendo vya aina hiyo.

“Kwa kuwa sikufurahishwa na tukio hilo, namshauri Waziri Mkuu Majaliwa, asimame hadharani kwa niaba ya Serikali ya CCM, awaombe radhi Watanzania.

“Tena awahakikishie matukio ya aina hiyo hayajirudii tena kwa sababu yeye na viongozi wengine, waliapa kuilinda Katiba na siyo kuivunja,” alisema Mgeja.

Basata Wasema Wimbo wa Nay wa Mitego Umejaa Matusi

$
0
0
Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) limeeleza kuwa wimbo wa Nay wa Mitego uliosambaa kwenye mitandao hivi karibuni ukiwa na jina la ‘Wapo’ una matusi na haufai.

Katibu Mkuu wa Basata, Godfrey Mngereza ameeleza kuwa Baraza liliusikiliza wimbo huo na kubaini kuwa ni wimbo usiofaa kwa jamii na zaidi unachochea vurugu.

“Ule wimbo tumeusikiliza, kama Baraza tunasema ule wimbo hauna maadili, ni wimbo ambao una matusi, ni wimbo ambao unachochea vurugu, ni wimbo ambao haufai kwa jamii,” alisema.

Aliongeza kuwa vyombo vyote vya habari ambavyo vitaucheza wimbo huo vitakumbwa na mkono wa sheria kutoka kwa vyombo husika.

Nay wa Mitego alikamatwa na Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro majira ya saa nane usiku, na lifikishwa Dar es Salaam anakoshikiliwa kwa mahojiano na Jeshi la Polisi.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei alithibitisha kukamatwa kwa msanii huyo usiku wa kuamkia jana.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, wakili Peter Kibatala amesema kuwa atasimamia kesi dhidi ya msanii huyo na kwamba tayari ameshamjulia hali katika kituo cha kati jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria maarufu Alberto Msando Ammwagia Sifa msanii Harmorapa

$
0
0
Baada ya msanii Harmorapa kupata Ubalozi wa kinywaji kinachoitwa cider ‘swala’, Mwanasheria maarufu Alberto Msando ambaye amekuwa akizishughulikia kesi za wasanii maarufu kama Wema Sepetu na wengineo, ametoa pongezi kwa msanii huyo.

Msando ametoa pongezi hizo kwa Harmorapa kupitia ukurasa wake wa Instagram akimpongeza kwa hatua aliyopiga na kujitahidi kutengeneza umaarufu ambao wengi wameshindwa.

"I really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi hawawezi.

"Wengi wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu. Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider ‘swala’. Its a big step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby 😂😂😂😂
 
"Kisa tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama wengine. #TheDon#HarmoMbio #HarmoBastola#KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa 😂😂#NusuUsoNusuPua"
I really like this guy. @harmorapatz1 sio kwamba ana kipaji kikubwa cha kuimba. Nimesikiliza wimbo wake mmoja. ILA ameweza kutumia fursa. Na kikubwa kuliko vyote AMETHUBUTU. Ameweza kufanya kile ambacho wengi hawawezi. Wengi wanasubiri sana kufanya maamuzi. Wengi wanaogopa au wanaona aibu. Nimefurahi leo kuona amepata endorsement ya cider 'swala'. Its a big step. Hawa ndio vijana ambao tunawataka. Kila nikimuangalia sura yake namkumbuka marehemu Remmy Ongala. Na kuna mtu anamuita baby 😂😂😂😂. Kisa tu ameweza kuwa na kipato na anaendelea kuwa maarufu. Sitashangaa kusikia wale mastaa wa bongomovie ambao hatujui movie zao wakianza kuvizia malipo ya endorsement!! Na ndio litakuwa anguko lake. Kama wengine. #TheDon #HarmoMbio #HarmoBastola #KiherehereMbeleYaBastolaKinazaaWoga #SuraMkunjo #PuaSasa 😂😂#NusuUsoNusuPua
A post shared by Msando Alberto (@albertomsando) on

Serikali Yaagiza Nay wa Mitego Aachiwe Huru na Wimbo Wake Uendelee Kuchezwa Redion

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo wa ‘WAPO’ na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Akiongea na Wandishi wa Habari Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa Kodi, wauza Unga, wanaotumia dawa za kulevya pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

VIDEO:Msikilize Waziri Mwakyembe Akiagiza Nay wa Mitego Aachiwe Huru

$
0
0
Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe ameagiza Polisi nchini kumuachia msanii wa Bongofleva Nay wa Mitego aliyekuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutoa wimbo usio na maadili.

Waziri Mwakyembe amesema Rais ameshauri wimbo wa ‘WAPO’ auboreshe kwa kutaja na wakwepa kodi.

==>Msikilize hapo chini Akiongea

Rais Magufuli Atoa agizo kwa CAG kukagua sekta ya madini

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 27 Machi, 2017 amepokea ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Ripoti hiyo imewasilishwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Prof. Mussa Juma Assad katika hafla iliyohudhuriwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Ripoti hiyo imegusa maeneo mbalimbali yakiwemo ukaguzi wa hali ya hesabu za Serikali, misamaha ya kodi, ukusanyaji wa kodi na maduhuli ya Serikali, uandaaji na utekelezaji wa bajeti, hali ya deni la Taifa, usimamizi wa rasilimali watu, usimamizi wa mali na madeni ya Serikali na usimamizi na uendeshaji wa taasisi za umma zikiwemo taasisi muhimu za kifedha na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Prof. Mussa Juma Assad amesema pamoja na hatua kubwa iliyopigwa na Serikali katika kuzingatia taratibu za fedha bado kuna mapungufu mbalimbali ambayo yameendelea kujitokeza na ameshauri hatua zichukuliwe kukabiliana nayo ikiwemo kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za umma katika madini, kuiepusha TANESCO kununua umeme wa gharama kubwa, matumizi mabaya ya misamaha ya kodi na kuongeza mashine za kutoa risiti (EFD).

Akizungumza baada ya kupokea ripoti hiyo, Mhe. Rais Magufuli ameipongeza Ofisi ya CAG kwa kazi nzuri inayofanya na ameahidi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana kwa karibu na ofisi hiyo ili kukabiliana na mianya yote inayosababisha upotevu wa fedha za umma.

Hata hivyo Mhe. Rais Magufuli amemuagiza CAG kufanya ukaguzi wa kina katika sekta ya madini na kubaini mianya yote ambayo inasababisha nchi kukosa mapato makubwa hususani katika misamaha ya kodi, mikataba mbalimbali na ulipaji wa kodi.

“Haiwezekani Watanzania wanakosa dawa hospitali wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa maji wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa umeme wakati dhahabu zao zinaondoka, Watanzania wanakosa barabara wakati dhahabu zao zinaondoka, nataka ukakague kwa kina hii sekta ya madini ili watanzania wajue chao nini na kama kinapatikana sawasawa?” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Dkt. Magufuli pia amemuagiza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Majaliwa kuitisha kikao cha pamoja kitakachomkutanisha CAG na Mawaziri wote, Makatibu Wakuu wa wizara zote, Gavana wa Benki Kuu na Wakuu wa taasisi za umma ili kila mmoja aambiwe hali ya hesabu katika taasisi yake na kuchukua hatua.

“Mhe. Waziri Mkuu ukaongoze hicho kikao na wewe CAG uwaambie kila mmoja katika eneo lake juu ya dosari zake, sitaki kuona dosari zinajirudia zilezile kila wakati” amefafanua Mhe. Rais Magufuli.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, CAG anapaswa kuwasilisha ripoti ya hesabu za Serikali kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kabla ya tarehe 31 Machi ya kila mwaka, na baada ya hapo ripoti hiyo huwasilishwa bungeni katika kikao kinachofuata.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

27 Machi, 2017

Ripoti Yathibitisha Faru John alikufa kwa kukosa matunzo

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amepokea taarifa rasmi ya uchunguzi wa kifo cha Faru John kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Prof. Samwel Manyele ambaye alikuwa akiongoza tume maalum iliyoundwa na Waziri Mkuu.

Akisoma taarifa hiyo mbele ya Waziri Mkuu, Prof. Manyele amesema tume yake ilifanya uchunguzi wa kifo cha Faru John kwa kupima vinasaba vya sampuli mbalimbali vikiwemo mzoga, fuvu, mifupa, pembe, damu, ngozi na kinyesi kilichokaushwa ambapo ilibainika kuwa vyote ni vya mnyama mmoja, aina ya faru mweusi ambaye ni dume.

Prof. Manyele amesema matokeo hayo yamethibitisha kuwa faru John alikufa katika hifadhi ya Sasakwa Grumeti kwa kukosa matunzo na uangalizi wa karibu.

“Maabara iliyotumika ni ya Chuo Kikuu cha Pretoria, Afrika Kusini chini ya usimamizi wa timu ya wataalamu kutoka Tanzania, wachunguzi wa Serikali, chini ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali. Sababu za kifo chake zilichangiwa na kukosa matunzo na uangalizi wa karibu, kukosa matibabu alipoumwa, mazoea yanayotokana na kutofuata taratibu zilizowekwa kisheria na mapungufu ya kiuongozu kwa Wizara husika, hifadhi na taasisi zake,” amesema.

Prof. Manyele amesema mapungufu waliyoyabaini kutokana na uchunguzi huo ni kutokuwepo kwa kibali rasmi cha kumhamisha Faru John; kukosekana kwa mkataba wa kupokelewa kwa Faru John hifadhi ya Sasakwa Grumeti na kutofuatiliwa kwa afya na maendeleo ya Faru John baada ya kuhamishwa. 

Mengine ni uchukuaji holela wa sampuli za wanyama pori kwa lengo la utafiti na kuzisafirisha nje ya nchi; migongano ya kimaslahi kati ya watumishi waliolenga kusimamia taratibu na wale wenye kusimamia maslahi binafsi na uwepo wa taasisi nyingi zenye mamlaka sawa juu ya masuala ya uhifadhi wa wanyamapori.

“Pamoja na kwamba mawasiliano yanaonyesha zoezi hilo liliridhiwa na Wizara, hapakuwepo na kibali rasmi kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori cha kuruhusu kumhamisha Faru John kutoka NCAA kwenda Grumeti,” amesema Prof. Manyele katika ripoti yake. 

Kwa upande wake Waziri Mkuu ameishukuru timu ya uchunguzi iliyokuwa chini ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kazi iliyoifanya ikiwemo kuainisha udhaifu uliokuwemo ndani ya Wizara ya Maliasili na Utalii na taasisi zake.

“Ofisi yangu itaipitia taarifa hii ambayo ni kubwa kiasi na kuifanyia kazi. Matokeo ya kazi hiyo, tutayatoa hivi karibuni ili kuonyesha Serikali imeamua kufanya nini juu ya mapendekezo yaliyotolewa.”

Amemtaka mkurugenzi Msaidizi wa Kitengo cha Kupambana na Ujangili wa Wanyamapori, Bw. Robert Mande, afuatilie mapendekezo yaliyoainishwa na tume hiyo na wayafanyie kazi mapema iwezekanavyo

Picha na Kauli ya Nay wa Mitego baada ya kuachiwa na polisi

$
0
0
Mwanamuziki Nay wa Mitego ameachiwa huru kutoka katika Kituo cha Polisi cha Kati Dar es Salaam ikiwa ni saa chache tangu Rais Dkt Magufuli aliporuhusu kuchezwa redioni kwa wimbo wake uliokuwa umefungiwa na BASATA.

Agizo hilo la Rais Magufuli limetolewa leo na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe alipokuwa akizungumza na waandishi habari mkoani Dodoma.

Waziri Mwakyembe alisema kuwa Rais Magufuli amesema wimbo huo ni mzuri, na kumshauri Nay wa Mitego aongezee mambo mengine kama  kuwataja watu ambao wanakwepa kodi, watumiaji wa dawa za kulevya.

Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.

Baada ya kutoka, Nay wa Mitego amezungumza na waandishi wa habari na kuwashukuru wale wote waliojitokeza na kumsaidia kwa namna yoyote ile.

Amewashukuru Watanzania wote lakini pia wasanii waliokwenda kumuona na kumtumia jumbe za kumpa moyo, lakini pia mawakili wake waliopambana kwa muda wote kuhakikisha kuwa haki yake inakuwepo na kulindwa.

"Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki, walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana". Amesema Nay wa Mitego 


Waziri Mwigulu Awaasa Askari Kutowabambikizia Watu Kesi

$
0
0
Askari na Maafisa wa jeshi la Polisi nchini wameaswa kutotumia madaraka yao vibaya kwa kuwabambikizia wananchi kesi kwani kufanya hivyo ni kushindwa kusimamia dhamira njema ya Mhe Rais ya kuwapatia wananchi wanyonge haki zao stahiki.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe Mwigulu Nchemba wakati akifungua kikao cha kazi cha Siku tatu cha mwaka 2017 kwa maafisa waandamizi wa Polisi na Makamanda wa Mikoa/Vikosi kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa LAPF Mjini Dodoma.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya kuwabambikizia kesi, Kuwabadilishia watu kesi zao za msingi kwa sababu ya kushindwa kutoa rushwa hivyo kikao hicho kinapaswa kuwa na maamuzi na maadhimio yenye dira na taswira njema kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Amesisitiza pia Askari na Maafisa wa Polisi kutotumia taarifa za watu wanaohasiana kuwa ndio chanzo pekee cha msingi wa shtaka badala yake kufanya uchunguzi kwa kina na kujiridhisha vyema ili kufikia hukumu yenye tija Na haki kwa mtuhumiwa kwani kufanya hivyo kutaimarisha amani na jeshi la Polisi kupata taarifa nyingi za uhalifu kutoka kwa wananchi endapo watajikita katika haki.

Akizungumzia Vita dhidi ya Dawa za Kulevya Mhe Nchemba alisema kuwa serikali imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kukamata na kuziteketeza Dawa za kulevya zilizopo mashambani ambapo ametilia msisitizo zaidi kwa Askari na Maafisa wa Jeshi la Polisi kuendelea kupambana ili kuzikamata Dawa za kulevya zilizopo katika viwanda.

Amesisitiza pia Jeshi la Polisi kuendelea kupambana na kubaini uhalifu sambamba na kushirikiana na vyombo vingine ili kuhakikisha lengo mahususi la serikali ambalo ni kuzuia uhalifu linafanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mhe Mwigulu amesema kuwa kauli mbiu ya Mwaka 2017 inayosema “ZINGATIA MAADILI TUNAPOPAMBANA NA UADILIFU ILI KUIMARISHA USALAMA KWA MAENDELEO YA TAIFA” endapo kama itatekelezwa kwa vitendo itaijenga nchi na kuzidi kudumisha zaidi amani iliyopo kwa wananchi.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi nchini Ernest Mangu alisema kuwa kikao hicho cha kazi kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kina dhamira kubwa ya kufanya Tathmini ya utendaji wa mwaka 2016 na kuandaa mikakati mizuri ya mwaka 2017 na kupata fursa ya kubadilika kiutendaji kwa kuzingatia dhamira ya serikali ya awamu ya Tano inayoongozwa na Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Hata hivyo amesisitiza zaidi askari wote nchini kutofanya kazi kwa mazoea, Kuacha Urasimu na kujenga uaminifu na weledi katika kazi.

Mangu amesema matendo ya Askari Polisi nchini yanapaswa kuwa mfano bora wa kuigwa katika jamii hivyo askari Polisi hapaswi kuwa chanzo cha vurugu au kujihusisha na matendo ovu yasiyostahili katika jamii.

Ameongeza kuwa miongoni mwa mambo yatakayopewa kipaombele kwa kujadiliwa katika Kikao hicho itakuwa ni pamoja na Vita dhidi ya Dawa za Kulevya, Vita dhidi ya Magendo, Vita dhidi ya ujangili na Uvuvi sambamba na Vita dhidi ya Ubambikizaji wa kesi kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Jordan Lugimbana akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma kabla ya kumkaribisha Waziri Mwigulu Nchemba kuzungumza na askari hao amelipongeza jeshi la Polisi kwa kazi kubwa linayofanya ambapo pia ameeleza mpango wa Mkoa katika kupambana na migogoro ya ardhi kwa kuanzisha kamati maalumu ya wataalamu wa sheria kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) Kupitia na kushauri ili kuweza kumaliza haraka migogoro hiyo.

Naye Makamu wa kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela alisema kuwa jambo la msingi ambalo askari Polisi wanapaswa kulifanya ni pamoja na kuhakikisha kila mwananchi anapata Uhuru wake na kama jambo hilo likitekelezwa ipasavyo Fikra za Hayati Mwalimu J.K Nyerere zitakuwa zimeenziwa kwa weledi.

Nape Nnauye: Matumizi ya Nguvu sana Hayalipi

$
0
0
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote.

“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!"
Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao unaikashifu serikali. 

Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, leo mchana alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi  kumuchia huru msanii huyo na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uendelee kuchezwa  kwenye vyombo mbalimbali,


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 28

Aliyemtishia Nape kwa bastola sio polisi- Waziri Mwigulu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amesema mtu aliyemtishia kwa bastola aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye si askari wa Jeshi la Polisi, lakini ameshapatikana na atashughulikiwa kwa mujibu wa utaratibu wa ulinzi na usalama.

Mwigulu alisema hayo baada ya kufungua mkutano wa kazi wa mwaka wa maofisa waandamizi wa polisi, makamanda wa mikoa na wakuu wa vikosi wa Jeshi la Polisi ambao unafanyika mjini hapa.

“Ameshapatikana (aliyemtishia Nape) na atashughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za ulinzi na usalama ambazo zimekuwa zikifanyika ndani, lakini hazitangazwi,”alisema.

Hata hivyo, Mwigulu alikataa kuelezea kwa undani kuhusu mtu huyo kwa kubainisha anatoka taasisi gani wala jina la mtuhumiwa kwa madai kuwa ni kwa sababu ya usalama wake.

Baadhi ya taasisi za ulinzi na usalama nchini ni Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Usalama wa Taifa na Takukuru.

Mtu huyo alifanya kitendo hicho wakati Nape, ambaye alikuwa Waziri wa Habari, alipokuwa anaelekea Hoteli ya Protea alikopanga kuzungumza na waandishi wa habari baada ya mbunge huyo wa Mtama kuachwa katika mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri.

Mtu huyo alikuwa pamoja na wenzake wawili ambao kwa pamoja walikuwa wakimlazimisha arudi kwenye gari lake na kuondoka, lakini Nape alibisha na ndipo mtu huyo aliporudi nyuma, kuchomoa bastola kutoka kiunoni na kisha kumtishia kabla ya kutulizwa na mwenzake.

Watu hao walitoweka eneo hilo muda mfupi baadaye.

Siku moja baada ya tukio hilo Mwigulu alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi, Ernest Mangu kumtafuta mtu huyo.

Mwigulu aliandika katika ukurasa wake wa twitter akisema:

“Mh Nape sio jambazi, hana record za uhalifu. Kitendo cha kutolewa bastola si cha Kitanzania na si cha kiaskari. Nimemuagiza IGP achukue hatua.”

Tukio hilo lilitokea siku chache baada ya RC Paul Makonda kuvamia kituo cha televisheni cha kampuni ya Clouds Media, akiwa na askari wenye silaha za moto na kulazimisha arekodiwe mahojiano baina ya watangazaji wa kipindi cha Shirika la Wambeya Duniani (Shilawadu) na mwanamke anayedai kuzaa na Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ambaye ameibukia kuwa mpinzani wa kiongozi huyo.

Hadi sasa, Jeshi la Polisi halijaeleza kuhusu askari hao waliojumuika kufanikisha uvamizi huo.

Polisi Wanaodaiwa Kuiba Mafuta Ya Ndege Wafikishwa Mahakamani

$
0
0
Askari  wawili wanaotuhumiwa kuiba mafuta ya ndege ya Kampuni ya ATCL, kwa kushirikiana na walinzi, wameondolewa kazini na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi.

Washtakiwa hao na wenzao wawili walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa.

Akisoma mashtaka Wakili wa Serikali Mwandamizi, Nassoro Katuga aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Koplo Bahati Msilimini (33), PC Benaus (34), Iddi Nyangasa (42) na fundi wa ndege, Ramadhani Mwishehe (52).

Katuga alidai washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka  mawili, shtaka la kwanza kula njama na shtaka la pili hujuma dhidi ya Serikali.

Alidai katika shtaka la kwanza washtakiwa wanadaiwa kati ya Machi mosi na Machi 17 mwaka huu maeneo ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere walikula njama ya kutenda kosa la uhujumu uchumi.

Katika shtaka la pili washtakiwa wote wanadaiwa kati ya tarehe hizo, wakiwa na nia ya kuhujumu manufaa ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, bila uhalali walitoboa na kuchota mafuta ya ndege lita 280.6 kutoka kwenye ndege JET A1 ya ATCL yenye namba za usajili 5H\MWF-8Q-300.

Katuga alidai kitendo hicho kilizuia utoaji wa huduma muhimu ya usafiri wa ndege.

Hata hivyo wakili huyo alidai upelelezi haujakamilika na hakuna kibali chochote kutoka kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Wakili wa utetezi, Martin Rwehumbiza aliiomba mahakama ikubali kuwapa dhamana wateja wake kwa sababu mashtaka yanayowakabili yanadhamana.

Alidai thamani ya mafuta wanayodaiwa kuchota haizidi Sh milioni 10 hivyo mahakama hiyo ina mamlaka ya kutoa dhamana.

Akijibu hoja hiyo Katuga alipinga washtakiwa hao kupewa dhamana kwa madai kwamba wataingilia upelelezi hivyo aliomba wakae ndani kwa muda.

Akitoa uamuzi Hakimu Nongwa alisema sheria inaruhusu Mahakama ya Kisutu kushughulikia dhamana kwa makosa ambayo thamani yake haizidi Sh milioni 10.

“Sirahisi kujua mafuta yalikuwa na thamani gani sababu hayakuwekwa katika hati ya mashtaka, hakuna hati ya kuzuia dhamana kutoka kwa DPP, wangeona washtakiwa wakiwa nje kwa dhamana wataingilia upelelezi wangeweka hati ya kuzuia dhamana zao.

“Dhamana ni haki ya washtakiwa hakuna zuio lolote, mahakama inaona ni vyema washtakiwa wakapewa dhamana, hawawezi kuingilia upelelezi sababu walishaondolewa kazini,”alisema Hakimu Nongwa.

Washtakiwa wote walipata dhamana na wadhamini walitakiwa kuhakikisha washtakiwa hao wanafika mahakamani kila kesi itapokuwepo. Kesi hiyo iliahirishwa hadi Aprili 27 mwaka huu kwa kutajwa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images