Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Afanya Ziara Ya Kushtukiza Bandarini Na Kuzuia Makontena 20 Yenye Mchanga Wa Madini Uliokuwa Usafirishwe Nje Ya Nchi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Machi, 2017 amefanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa maelekezo aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kudhibiti udanganyifu wa mizigo inayoingia na kutoka nchini kupitia bandari hiyo ikiwemo usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi.

Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia makontena 20 ya mchanga wenye madini kutoka kwenye migodi iliyopo kanda ya ziwa ambayo yamezuiliwa kusafirishwa nje ya nchi tangu alipotoa agizo la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga nje ya nchi tarehe 02 Machi, 2017.

Pamoja na kushuhudia makontena hayo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP - Ernest Mangu na vyombo vingine vya dola kuhakikisha mchanga wa madini unashikiliwa popote ulipo, mpaka hapo uchunguzi wa kina utakapofanyika kubaini ukweli.

“Nataka niwaambie nchi yetu inachezewa mno, nimekuja kuyaona haya makontena kama yapo, na kweli nimeyaona, sasa utaratibu utakapokamilika nataka Watanzania na dunia nzima ione kilichomo humu ndani kama ni mchanga kweli ama dhahabu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Akiwa bandarini hapo Mhe. Dkt. Magufuli pia ameshuhudia udanganyifu mwingine unaofanywa na wafanyabiashara wanaoagiza mizigo kutoka nje ya nchi baada ya kuoneshwa makontena ambayo nyaraka zinaonesha yamebeba mitumba ya nguo na viatu wakati ndani yake kila kontena moja limebeba magari matatu ya kifahari.

Maafisa wa bandari ya Dar es Salaam na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wamemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa kufuatia maelekezo aliyoyatoa ya kuhakikisha mizigo yote inakaguliwa kwa mitambo ya mionzi (Scanning Machines) wamefanikiwa kubaini udanganyifu mwingi unaofanywa na wafanyabiashara wanaoingiza nchini na kusafirisha nje ya nchi mizigo mbalimbali yakiwemo makontena 10 ambayo yamepatikana yakiwa na magari ya kifahari ilihali nyaraka zake zikionesha yana mitumba ya nguo na viatu.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza maafisa na wafanyakazi wa bandari ya Dar es Salaam na TRA kwa kazi nzuri wanayofanya kudhibiti upotevu wa fedha za umma bandarini hapo na amewataka kuendelea kutekeleza wajibu wao kwa uzalendo na kujiepusha na rushwa.

Leo mmenifurahisha sana, ninawatia moyo endeleeni kuwakamata wote wanaofanya udanganyifu huu na muwachukulie hatua kali za kisheria, lakini msimuonee mtu na msipokee rushwa, tunataka watu wajifunze kuwa hapa sio shamba la bibi” amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha, ametoa wito kwa vyombo vyote vinavyoshughulikia udhibiti wa mizigo inayoingia na kutoka kupitia bandari ya Dar es Salaam na bandari nyingine hapa nchini, kuendelea kushirikiana ili kukomesha vitendo vyote vya udanganyifu ambavyo vinasababisha nchi kupoteza mapato mengi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

23 Machi, 2017

Gwajima: Mimi ndo chanzo cha Nape Nnauye Kutumbuliwa na Rais

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Josephat Gwajima amesema kuwa yeye ni sababu kubwa ya  kutenguliwa kwa Waziri wa habari,utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Nnauye.

Akizungumza leo (Alhamisi) baada ya kutembelea Ofisi za kituo cha redio cha Efm,Gwajima amesema    Mkuu wa Mkoa alivamia  ofisi za  Clouds kwa lengo la kutaka wamchafue Askofu huyo lakini baada ya Nape kuunda tume iliyofanya uchunguzi kumesababisha kutenguliwa kwake.

"Labda niseme kuwa sababu za Nape kutenguliwa zinanihusu sana mimi.Cha kujiuliza ni kwamba ni nani alikuwa nyuma ya Mkuu wa Mkoa alipovamia Clouds hadi Nape atenguliwe?”alihoji.

Gwajima alifika Ofisini hapo saa 4:06 na kukutana na viongozi na wafanyakazi huku akiwapa pole na kuwatia moyo na kwamba watayashinda majaribu yanayoikumba tasnia ya habari.

VIDEO: Msanii Harmorapa Alivyotimua Mbio Baada ya Polisi Kutoa Bastola Kumdhibiti Nape Nnauye

$
0
0
Leo Rais Magufuli ametengua uteuzi wa Nape Nnauye na nafasi yake amepewa Dr. Mwakyembe.

Baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na waandishi wa habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano.

Saa chache baadae Nape Nnauye alifika eneo hilo lakini alizuiwa na askari huku wakimrudisha ndani ya gari.

Katika sakata hilo, Askari mmoja aliamua kutoa bastola na kuielekeza kwa Nape. Msanii Harmorapa alikuwepo jirani na Nape wakati tukio hilo likitokea...

==>Mshuhudie hapo chini alivyotimua mbio baada ya bastola kutolewa

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL   BEAUTY COSMETICS

Ni kampuni inayotoa bidhaa original na zenye matokeo mazuri bila madhara wala kemiko ya aina yoyote. Bidhaa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda. Tunawaletea punguzo la bei la %10 bidhaa tulizonazo ni kama zifuatazo.
 
     👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 170,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 100,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 110,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @100,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @100,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima kwa vidonge au dawa ya kunywa @150,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11 Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo la ndoa @120,000
12.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
13. kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @100,000/=
15. Kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake @100,000/= NK. [ Bidhaa zetu zote ni garantii pia hakikisha unapewa risiti ununuapo bidhaa kampuni hii popote ulipo utapata huduma zetu]
 
     WASILIANA NASI KWA NAMBA
        {065 9618585 au 0759029968.}
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
                               Karibu sana

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 24

Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba Aagiza aliyemtolea bastola Nape Nnauye Achukuliwe Hatua Kali za Kisheria

$
0
0
Kufuatia tukio la mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni Askari kumtishia Mbunge Nape Nnauye kwa kutumia bastola, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi amesema tukio lile halikuwa sahihi na kuagiza hatua zichukuliwe.

Waziri Mwigulu Nchemba ambaye ndiye mwenye dhamana ya kusimamia usalama wa raia na mali zao amesema kuwa, Nape Nnauye si jambazi, hakuwahi kuwa na taarifa za uhalifu, sasa kwanini mtu amtishe kwa bastola tena mbele ya umati mkubwa uliojaa waandishi wa habari?

“Mh.Nape Moses Nnauye sio jambazi, ni mtanzania, ni mbunge, mjumbe wa NEC wa CCM, hana record ya uhalifu. Kitendo cha mtu kumtolea Bastola, Sio cha kiasikari, sio cha kitanzania na sio cha ki Mungu, kama mtu ameweza kutoa Bastola mbele ya Kamera nawaza mbali ingekuwa kwenye uchochoro angefanya nini.”

Aidha, Waziri Nchemba amesema kuwa amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kumbaini mtu huyo aliyefanya kitendo hicho na kumchukulia hatua stahiki.

“Nahusika na Usalama wa Raia wote wa Tanzania, nimemwelekeza IGP atumie picha kumsaka mtu yule aliyeinua kufanya kitu cha kihalifu kwa kofia ya uaskari. Na kama ni Askari basi sheria zinazoongoza taasisi husika zichukue mkondo wake.”

Nape Nnauye alitishwa na bastola hiyo jana alipofika katika Hoteli ya Protea Dar es Salaam kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari baada ya Rais Dkt John Pombe Magufuli kumvua Uwaziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

==>Tazama video hii kuona ilivyokuwa

Ufafanuzi Kutoka Mahakama Ya Tanzania Kuhusu Habari Ya "Utata Wa Jaji Mkuu"

Alichokiandika Nape Nnauye Leo Kupitia Ukurasa wake wa Twitter

$
0
0
Jana Rais Magufuli alitengua uteuzi wa Nape Nnauye na nafasi yake akapewa Dr. Mwakyembe.

Baadaye Nape Nnauye alitoa taarifa kuwa atazungumza na waandishi wa habari lakini Meneja wa Hotel ambayo mkutano ulitakiwa ufanyike alisema ameagizwa kuwaambia waandishi watawanyike na hakutakuwa na mkutano.

Nape alilazimika kuzungumza akiwa juu ya gari lake.Hata hivyo, polisi waliingilia kati

Leo asubuhi kupitia ukurasa wake wa twitter, ametoa ujumbe kwa wanahabari nchini ambapo ameandika: "Wanahabari mme GUSA sana moyo wangu!Sikujua kama mnanipenda na kunithamini kiasi KILE!Nawashukuru SANA kwa kujitolea kwenu!Nawapenda SANA!"

CCM Yakanusha taarifa kuwa Katibu Mkuu wa CCM Komrade Kinana Ataongea na waandishi leo

$
0
0
Tumekuwa tunapokea simu nyingi kutoka kwa waandishi wa habari, na pia kuna wengine wamefika mpaka ofisini, kuuliza au kuja kuhudhuria kikao baina yao na Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Abdulrahman Kinana, asubuhi hii.

Napenda kuwafahamisha kwamba hata sisi wenyewe tumesoma tu tangazo hilo kwenye moja kati ya post za humu, hivyo naomba msihangaike nalo kwa sababu ni uzushi.

Katibu Mkuu mwenyewe yupo safarini nje ya nchi karibu wiki nzima hii.

Nawasilisha kwenu kwa taarifa sahihi.

Charles Charles
Idara ya Itikadi na Uenezi

Tarehe 24 Machi, 2017

VIDEO: Rais Magufuli Katoa ONYO Kwa Wamiliki wa Vyombo vya Habari Wakati akiwaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi, Ikulu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John P. Magufuli, leo amewaapisha Dr Harrison Mwakyembe na Prof Palamagamba Kabudi pamoja na mabalozi kadhaa Ikulu Jijini Dar.

Mwakyembe ameapishwa kuwa Waziri mpya wa habari, Profesa Kabudi kaapishwa kaapishwa kuwa waziri wa Katiba na Sheria.

==>Haya ni mambo machache aliyoyasema Rais Magufuli Leo

1.Kuna wengine walisema Kinana leo angezungumza na waandishi, wakati nimemtuma India ambapo atakuwa kwa zaidi ya siku 10

2.Tunataka kuitoa nchi katika hali ya mazoea kuipeleka katika mstari ambao ni sahihi

3.Ukiangalia siku iliyofuata baada ya Rais wa Benki ya Dunia kuja, magazeti yote yaliandika habari nyingine tofauti-

4.Niwatake waandishi wa habari muwe wazalendo, Tanzania ikiharibika na nyie pamoja na wanaowatuma muandike wote mtaharibikiwa

5.Hata magazeti ya leo yana picha ya mtu mmoja ambaye amefanya kosa moja, utadhani kosa ni linaungwa mkono na serikali

6.Niwatake wamiliki wa vyombo vya habari muwe waangalifu, kama mnadhani mna uhuru wa namna hiyo, kuweni makini sana

7.Kuna vyombo vingine vya habari sehemu yenye ugomvi ndio wanapeleka kamera na habari hizo zinapewa muda mrefu, 'watch out'

8.Vyombo vingine haviandiki mazuri ya mtu, lakini wakipata mabaya yake ndiyo yanajaza kurasa

==>Tazama hii Video kumsikiliza Rais Magufuli akiongea Pamoja na walichoongea wateule wa Rais


Kutana na MAALIM HUSSEIN Mtabibu wa Nyota za Binadamu.........Anafungua Kizazi, Pete za Bahati na Kusafisha Nyota

$
0
0
MAALIM HUSSEIN Anaupeo wa Kubaini Tatizo lako Kupitia Wasaa Punde Utakapo Fanya Mawasiliano Kwa wale wenye MATATIZO kupitia UWEZO na KUBRI Alionayo"INSHALLAH YATATUKUKA" 

 MAALIM HUSSEIN Anauzoefu wa Zaidi ya miaka 19 Katika kutoa huduma ya UTABIBU WA NYOTA NA TIBA ASILI KATIKA NCHI 37. 

 MAALIM HUSSEIN HUTIBU KUPITIA VITABU VYA QUR-AN, Dawa za Asili ya Africa, DAWA ZA KIARABU NA MAJINI... Kwa Matatizo Yafuatayo》》
☆☆ 
☆Kutafsiri Ndoto 
☆Mfarakano wa Ndoa 
☆Kufungua Kizazi(kwa walifungwa kwa njia ya Kishirikina) ☆Nguvu za Kiume 
☆Kusafisha NYOTA 
☆BAHATI NASIBU(Kubashiri Timu za Kushinda) 
 ☆Pete za Bahati 
 ☆Kinga ya Mwili & Biashara 
☆Zindiko ya Nyumba & Kiwanja ☆ Humaliza Kesi za muda mrefu 
☆Hurudisha MALI ILIOPOTEA 
 ☆Humaliza tatizo la CHUMA ULETE HUTOA JINI LA MALI (Kwa wale tu wanaohitaji Kufanikiwa bila mashaarti) Na DUAH MAALUM KWA WAHITAJI WOTE (Na Mengine Mengi ya Siri) 

Kwa Ushauri na Tiba Whatsapp/Calls +255 674835107 +255 746757102

Kauli ya Waziri Dkt Mwanyekembe kuhusu madai ya RC Makonda kuvamia Clouds

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, jana baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam, amekiri kuwa anafahamu kuhusu tukio la uvamizi lililofanyika katika ofisi za Clouds Media Group.

Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mwakyembe aliyechukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema kuwa yeye kwa sasa hawezi kulizungumzia tukio hilo wala kutoa uamuzi wowote kwa kuwa hajapata ushahidi unaojitegemea.

“Ninachokijua kuhusu hilo tukio kinatokana na taarifa za vyombo vya habari, taarifa za magazeti, za redio, za televisheni, na sidhani kama taarifa hizo zinatosha kwa mimi kutoa uamuzi wowote.”

Ameongeza kuwa bado suala hilo ni la kuchunguzwa zaidi kwani picha inayotolewa ni ya upande mmoja.

“Mlalamikaji hapa ni Clouds, anayetupa taarifa kuhusu suala hili zima ni Clouds na wenzake. Kwa hivyo naipata picha hii kwa upande mmoja…”

Aidha kwa mujibu wa ripoti iliyokuwa imetolewa na kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ilisema kuwa wamesikiliza upande wa mlalamikaji (Clouds Media Group).

Lakini walipokwenda kwa ajili ya kuusikiliza upande wa mlalamikiwa (RC Paul Makonda) hawakufanikiwa kumpata. 

Hii ni baada ya wao kusubirishwa kwa muda mrefu  nje ya ofisi yake na baadae kuambiwa kuwa Makonda ameondoka na hatoweza kurudi kwa siku hiyo. Jambo hili liliwafanya wajumbe hao kujiaminisha kuwa Makonda hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo na aliamua kuwatoroka.

Hata hivyo ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ili aifikishe katika mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.

CHADEMA Kuwasha Moto Bungeni

$
0
0
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema matukio yaliyotokea hivi karibuni likiwamo la aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kutolewa bastola, yanaweza kubadili upepo wa Bunge linalotarajiwa kuketi siku chache zijazo.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliwaambia hayo waandishi wa habari jana waliotaka kufahamu mipango ya chama hicho katika kutumia mhimili wa Bunge kutokana na uwepo wa matukio ya uvunjaji wa sheria.

Katika hilo, Mnyika alisema Watanzania watarajie Bunge lijalo la Bajeti kuwaka moto.

“Sisi ndio tunaongoza Kambi Rasmi ya Upinzani na ambacho ninaweza kuwaambia Watanzania ni kwamba watarajie Bunge la Bajeti kuwaka moto juu ya utendaji wa Serikali. Sasa kuwaka moto namna gani na kuhusu nani ni masuala ambayo yataonekana katika hatua ya baadaye. Naamini safari hii haitakuwa wabunge wa Chadema, Ukawa pekee, naamini Bunge litakuwa kitu kimoja katika kuchukua hatua,” alisema Mnyika.

Chadema Yanunua Ugomvi wa Nape
Katika hatua nyingine chama hicho kimemtaka Rais Dk. John Magufuli ajitokeze waziwazi na kusema sababu za kumwondoa aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.

Pamoja na hilo, kimetaka Rais Dk. Magufuli aseme iwapo alitoa maelekezo kwa vyombo vya usalama waliovamia ofisi za Clouds Media Group na yule aliyemtolea bastola Nape alipokuwa akizuia asizungumze na vyombo vya habari juzi.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, aliyezungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, kuhusu ajenda mbili zilizozungumzwa katika kikao cha Kamati Kuu Maalumu ya chama hicho kilichoketi Machi 22 na 23, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

“Ni vyema Rais akaeleza kwa kuwa taarifa za Ikulu hazikufafanua kwanini amemwondoa Nape. Aeleze waziwazi sababu za kumwondoa Waziri katika kipindi ambacho taarifa ya kamati iliyoundwa imetolewa ambayo imeeleza wazi makosa yaliyofanywa na mteule wa rais katika siku chache tu baada ya kumkingia kifua.

“Imeonekana matumizi mabaya ya wazi ya watumishi wa vyombo vya usalama ikiwamo waliovamia kituo cha Clouds kwa bunduki, aliyemtolea Nape bastola, rais ndiye msimamizi wa vyombo vyote vya ulinzi na usalama, awaeleze Watanzania iwapo askari na wanausalama hao wamefanya kazi kwa maelekezo yake,” alisema Mnyika.

Alisema kama sivyo ni hatua zipi ameelekeza zichukuliwe kwa wahusika wa mambo hayo.

Mnyika alisema chama hicho kinapinga mwenendo wa matumizi mabaya ya madaraka ikiwa ni pamoja na kulindwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na matukio ya hivi karibuni yanayogusa uhuru wa vyombo vya habari ikiwemo kuvamiwa kwa kituo cha Clouds Media Group pamoja na kitendo cha Nape kutolewa bastola.

“Uamuzi wa kumlinda Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa gharama hata ya kumwondoa Waziri wake ni wazi ni matumizi mabaya ya madaraka. Na matumizi haya mabaya ya madaraka yamejipenyeza sasa hayamhusu Rais tu pekee bali pia watendaji wake na vyombo mbalimbali,” alisema Mnyika.

Alisema nchi imeanza kuwa ya kipolisi na matumizi ya vyombo vya dola katika masuala ambayo havipaswi kutumika.

“Tunatoa pole kwa wanahabari kwa mambo hayo pamoja na Nape kwa haya yanayomkuta,” alisema Mnyika.

Alisema haki inapovunjwa mahali popote na kwa raia yeyote, wao kama chama hawasiti kutoa kauli ya kukemea.

Mnyika aliwataka Watanzania kuungana kupinga mabaya yanayofanywa na Serikali ili kulinusuru Taifa na hatari zinazoikumba na zitakazoendelea.

“Taarifa nilizonazo kutoka vyanzo vyangu serikalini ni kwamba, Rais ameamua kumlinda RC kwa sababu eti Chadema kupitia kwa Mwenyekiti Mbowe ilitoa msimamo wa kumtaka amchukulie hatua. Watu ndani ya Serikali wanasema kama atamchukulia hatua eti Rais ataonekana amekidhi matakwa ya Chadema,” alisema Mnyika.

Alisema chama chao kina wajibu wa kuikosoa Serikali iwapo haifanyi kazi sawa sawa na Rais anawajibika kwa wananchi na si Chadema.

Mnyika alikumbusha kuwa wakati walipotangaza Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta), waligusia kauli kuwa; anapoonewa yeyote, unapokuwa kimya, haki inapovunjwa kwa mtu mmoja ukadhani kwamba haikuhusu, ikaenda kuvunjwa kwa mtu mwingine ukanyamaza kimya ukadhani kwamba haikuhusu, ipo siku jambo litakukuta mwenyewe na hakutakuwa na mtu wa kupaza sauti kwa niaba yako.

Alisema kauli hii ilionekana kuwahusu upinzani pekee lakini hivi sasa imejidhihirisha tofauti kutokana na athari zinazojitokeza kwa raia, vyombo vya habari na baadhi ya wanaCCM.

Rais Magufuli ateua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 25 Machi, 2017 amemteua Bw. Charles Edward Kichere kuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Kabla ya Uteuzi huo Bw. Charles Edward Kichere alikuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA.

Bw. Charles Edward Kichere anachukua nafasi ya Bw. Alphayo Kidata ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ikulu.

Kufuatia uteuzi huo, nafasi ya Naibu Kamishna Mkuu wa TRA itajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

25 Machi, 2017

TPA yakamata makontena mengine 262 yenye mchanga wa madini Bandari kavu Dar

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imebaini makontena mengine 262 yenye mchanga wa dhahabu yaliyokuwa yamehifadhiwa katika bandari kavu ya MOFED (zamani ZAMCARGO) iliyopo Kurasini jijini Dar es salaam yakisubiri taratibu za kiforodha kabla ya kusafirishwa kwenda nje ya nchi kupitia kitengo cha makontena kinachoendeshwa na kampuni binfasi ya TICTS.

Kubainika kwa makontena hayo kumekuja siku tatu tu baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kutembelea bandari ya Dar es salaam na kukagua makontena 20 yenye shehena ya mchanga wa madini kutoka migodi mbalimbali iliyopo Kanda ya Ziwa.

Mhe. Rais Magufuli alifika bandarini siku hiyo kukagua utekelezaji wa agizo lake la kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini kutoka migodini.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mhandisi Deusdedit Kakoko, amesema makontena hayo yaliyokuwa katika hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kiforodha yamebainika leo tarehe 25 Machi, 2017 katika msako mkali unaoendeshwa na Mamlaka yake.

Mhandisi Kakoko amesema makontena yote hayo yalikuwa na lakiri (seals) za Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA), na yalikuwa yanashughulikiwa na kampuni ya usafirishaji wa mizigo ya Freight Forwarders Tanzania Limited iliyopo Dar es salaam.

Mhandisi Kakoko amesema jumla ya makontena 256 yalikuwa katika bandari kavu ya MOFED, wakati makontena mengine sita yalikuwa tayari yameshaingizwa bandarini tayari kwa kusafirishwa.

Ametoa wito kwa makampuni yote ya madini yenye shehena za mchanga yajitokeze yenyewe na kuonesha mizigo yao popote ilipo nchini kabla haijabainika katika msako kabambe unaondeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali nchi nzima.

Orodha ya makontena hayo yaliyobainika inaonesha yalifika bandarini hapo katika nyakati tofauti kutoka migodi ya Buzwagi na Pange Mines.

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Bandari Bw. Ramadhani Mungi amesema bandari zote nchini ziko salama na kwamba ulinzi na usalama umeimarishwa kwa kuwekwa askari na vifaa vya kisasa vya ulinzi zikiwemo kamera.

Habari Zikizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili a March 26

Nay wa Mitego akamatwa na polisi Morogoro..... ni kutokana na wimbo wake unaoikosoa serikali

$
0
0
Mwanamuziki  Emmanuel Elibariki maarufu Nay wa Mitego amekamatwa na Polisi leo asubuhi mkoani Morogoro na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero mkoani humo.

Nay wa Mitego amekamatwa akiwa hotelini Morogoro baada ya kuamaliza shughuli zake zilizompeleka ambapo alitakiwa kuongozana na polisi hao hadi kituo cha polisi.

“Nimekamatwa kweli. Muda Huu nikiwa hotel Morogoro baada ya kumaliza Kazi yangu iliyo ni leta. Napelekwa Mvomelo Police. Nawapenda Watanzania wote. ✊🏿✊🏿 #Truth #Wapo.” Ameandika Nay wa Mitego kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Licha ya kuwa mwanamuziki huyo hajaeleza sababu ya kukamatwa kwake, au Jeshi la Polisi kutoa taarifa, lakini inaaminika kuwa sababu kubwa ni wimbo wake alioutoa siku za hivi karibuni unaokwenda kwa jina la Wapo.

Wimbo huo umezungumzia mambo mengi hasa ya kisiasa yanayoendelea nchini kwa sasa ikiwa ni pamoja na tuhuma zinazomkabili Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, uhuru wa vyombo vya habari na  masuala ya sanaa.

SORRY MADAM -Sehemu ya 43 & 44 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Eddy taratibu akapanga foleni ya kutokea nje, huku kila abiria akikaguliwa kutoka kwenye uwanja huo. Ikafika zamu yake ambapo akampatia dada mmoja mkaguzi hati yake ya kusafiria{Passport). Dada huyo akaipitisha kwenye mashine maalumu, akayanyanyua macho yake na kumtazama Eddy kwa umakini. Dada huyo akanyanyua simu yake na kuzungumza kitu ambacho Eddy hakukielewa, gafla Eddy akaona kundi la polisi likimfwata wakiwa na mbwa pamoja na bundiki.

Kwa mara ya kwanza alipo watazama alijifariji labda kuna mtu wanaye mfwata tofauti na yeye. Ila kadri walivyo zidi kuja ndivyo wlivyo zidi kumlenga yeye huku macho yao yote wakimtazama, na ndani ya dakika wakawa wamemzingira Eddy na kumuweka kati, asitambue sababu ni nini ya askari hao kumzunguka.

ENDELEA
Karibia watu wote walio Karibia na eneo hilo, macho yao waliyelekezea eneo walipo simama askari pamoja na Eddy aliye wekwa kati.
"Upon chini ya ulinzi"
Askari mmoja alizungumza kwa lugha ya kingereza na kumfanya Eddy amkodolee macho pasipo kuelewa haswa ni nini kosa alilo litenda hadi akamatwe.

"Kwa kosa gani?"
"Una haki ya kukaa kimya, na si kuuliza maswali. Mpigeni pingu mpelekeni chumba cha mahojiano"
Kutokana na kuziheshimu sheria za nchi hiyo ambazo ni kali kwa waalifu wake, Eddy akakubali kipigwa pingu mikononi mwake. Hakuhitaji askari hao wamsumbue, kwa mwendo wa taratibu wakatembea kuelekea katika chumba cha mahojiano.

Begi la Eddy likawekwa juu ya meza aliyo ikuta ndani ya chumba hicho. Wakaanza kulipekua, wakakuta nguo pamoja na pesa ambazo Eddy alihitaji kuzitumia akiwa katik nchi hiyo. Cha kushangaza aksari hao watano wakagawana pesa yake pasipo kumueleza Eddy jambo lolote.
"Hembu niambieni basi kwa nini mumenikamata?"
"Utajua muda mchache ujao ni kwanini tumekukamata wewe kaa kimya"

Ikamlazimu Eddy kubaki kimya. Hazikupita dakika nyingi akaingia mwanamama mweusi aliye panda juu kiasi.
"Mambo Eddy"
Mwanamama huyo alitabasamu huku akivuta kiti na kukaa. Eddy akajaribu kuvuta hisia zake ni wapi alipo muona mwana mama huyo, ila hakupata kumbukumbu yoyote kwenye kichwa chake, isitoshe mwana mama huyo anazungumza kiswahili vizuri ikiashiria kwamba yeye ni muafrika tena Mtanzania.

"Mimi ni balozi wa Tanzania hapa Japana ninaitwa mama Ngoi"
"Wewe ndio umeagiza nikamatwe?"
"Hapana ila ni amri kutoka iku. Unatakiwa uweze kurudi nyumbani ukaendelee na majukumu yako ya kikazi"
Eddy akatabasamu kwa kejeli. Akamtazama mama huyo kuanzia kichwani hadi kwenye tumbu, sehemu ya chini ya mwili wake hakuweza kuiona kutokana na kuzibwa na meza kwa chini.
"Kazi eheeee?"
"Ndio nchi ipo hatarini na katika vitisho vya kulipuliwa kwa bomu la nyuklia. Wewe ndio unaye hitajika kurudi katika nafasi yako ya uwaziri.

Matukio ya kijambazi yanatokea kila kukicha, isitoshe hata mke wa raisi mwenyewe ametekwa inapata miezi minne sasa"
Eddy akastuka kusikia Rahab ametekwa, akajiuliza maswali kadhaa kichwani mwake. Ila hakuhitaji kuonyesha mstuko wake huo kwa maana anatambua kwamba huo ni uongo kwa Rahab kuweza kutekwa.

"Nisikilize mama. Sina kitu nilicho kibakisha Tanzania. Sina familia sina chochote kwa hiyo sihitaji kurudi. Tafadhali waambie kuwa sihitaji kurudi Tanzania"
"Tayari maandalizi ya kukurudisha Tanzania yanaendelea huko nje ya uwanja wa ndege. Tafadhali hii ni kwaajili ya usalama wako na nchi"
"Hembu kwanza nifungulieni hizi pingu. Hauwezi kuzungumzw eti na kiongozi wako ukiwa umenifunga pingu kama muhalifu"

Ushawishi huo wa Eddy ukamfanya mama huyo, kumuamrisha askari mmoja kufungua pingu za Eddy pasipo kufahamu kwamba ana dili na mtu wa aina gani. Akili ya Eddy ikafanya kazi haraka haraka akifikiria kashfa mbaya inayo endelea ndani ya Tanzania kwamba yeye ni gaidi aliye teka jengo la Mlimani City.

Moja kwa moja akatambua kitendo cha yeye kurudi Tanzania nikwenda kuhukumiwa. Kifungo cha maisha kwani mauaji aliyo yaona ni makubwa sana. Kazi yake ikaanza kufikiria ni jinsi gani anaweza kutoroka pasipo kujua ataoroka vipi ikiwa yeye bado ni mgeni katika nchi ya Japan.

***
Kitendo cha Briton kuendelea kunyonywa uume wake, kilizidi kumkera ila kwa jinsi biti huyo anavyo zidi kumnyonya ndivyo jinsi alivyo jikuta mwili ukimsisimka hadi uume wake ukasimama kabisa. Cha kushangaza Dada huyo wa kikenya akaanza mushangilia akiamini mambo yake yanazidi kuwa mazuri.

Akamuamrisha msichana huyo kuondolewa katika chumba hicho na kubaki yeye na Briton. Dada huyo pasipo kuwa na aibu, akaanza kujnyonya uume wa Briton, akazidi kwenda mbali na hapo kwani akaanza kufanya ngono na Briton pasipo ridhaa yake. Hasira ya Briton ilizidi kumpanda ila hakuwa na uwezo wa kufanya jambo lolote kwajinsi alivyo fungwa hakuweza kufanya jambo lolote.

Dada huyo alipo maliza matakwa yake, amawaamuru watu wake kumfungulia Briton, wakambeba mzoga mzoga hadi ndani ya chumba kimoja kikubwa, ambapo Briton akamuona mzee wa makamo mwenye miaka kati ya arobaini na tano hadi hamsini na tano akiwa amesimama na bomba la sindano, huku akiwa amevalia koti jeupe ikiashiria kwamba huyo ni daktari. Briton akiwa ameshikiliwa hivyo hivyo na majamaa hayo yaliyo gawanyika kwa misuli mingi. Akachomwa sindano ya shingoni, ndani ya dakika mbili mbeleni, usingizi mzito ukamchukua na kulala fofofo asijue ni nini kinacho endelea.

***
Majira ya saa kumi na mbili jioni. Barabara ya kuelekea mikoni, kuanzia Ubungo na kwenda mbele maeneo ya kimara zote na mbezi mwisho. Imetulia huku askari wa usalama barabarani, wakifanya kazi ya kusimamisha magari yote yanayopita katika barabara hiyo. Wakazi wengi wanao itumia barabara hiyo walisikika wakilaani kitendo hicho ambacho kinawachelesha wengi wanao toka makazini, wamisubiria msafara wa raisi uweze kupita.

Foleni ikazidi kuwa kubwa kiasi cha magari yanayo tokea, Kariakoo, Mwenge na Tabata kushindwa kwenda. Ving'ora vya pikipiki za polisi pamoja na magari hayo vikaanza kusikika jirani kabisa na mataa ya Ubungo yalipo. Wananchi ambao walikuwa wamechukia walijikuta wakichomoza vichwa vyao kwenye magari kutazama msafara huo ambao mara nyingi husifika kwa gari zake kwenda kasi na katika mtindo wa kupanua barabara.
"Raisi jioni hii anakwenda wali?"
Mmoja wa wananchi alisikika akimuuliza mwezanke wakiwa ndani ya basi lao dogo linalo tokea kariakoo.
"Mmmm nitajulia wapi ndugu yangu wakati hata ikulu yenyewe sipajui"

Magari hayo yakazidi kupita kwa mwendo wa kasi huku askari aliye simaama kwenye eneo hilo la mataa akiyaelekeza magari hayo yanapo hitajika kwenda. Msafara huo wenye magari kumi na saba, ukapita ila gari nyengine yenye namba za ikulu, ikiwa imewasha taa zake ikaongezeka kataka msafara huo na kuongeza idadi ya magari na kufikia kumi na nane.
"Mkuu gari zinatakiwa kuwa ngapi?"
Askari huyo wa usalama barabarani alizungumza kwa simu yake ya upepo akimtaarifu kiongozi wa msafara, baada ya kuitilia shaka gari hiyo iliyo ongezeka.

"Kumi na saba. Over"
"Kuna gari moja ya ikulu imeongezeka muheshimiwa. Una taarifa nayo?"
"Hapana, tutaichukulia uangalizi. Over"
Askari huyo akaanza kuruhusu gari za abiria na wananchi wa kawaida kuendelea na safari zao.
"Madam nimesha jiunga kwenye msafara"
Priscar alizungumza na Rahab kulitia simu ya mkononi.
"Umestukiwa?"
"Sidhani, kwa maana niliuwahi msafara"
"Poa kila kitu kinakwenda kwenye mlango"
"Sawa madam"

Simu ikakatwa na Priscar akazidi kuongeza mwendo kasi wa gari yake.Taarifa ya kuongezeka kwa gari katika msafara wa raisi. Akielekea katika handaki alilo pata habari kwamba mke wake ndipo alipo shikiliwa. Ikaanza kumchanganya, madereva wote taarifa hiyo wakawa nayo. Mchezo walio ufanya ni wote kutanua barabara, kisha gari ya Raisi Praygod Makuya, ikapita mbele kwa mwendo wa kasi kisha hizi nyingine zikaziba kwa nyuma jambo lililo amza kumpa wasiwasi Priscar.

***
Kutokana na nguvu aliyo kuwa nayo kwenye kikosi cha Al-Shabab, Shamsa akamuomba bwana Abdulah Mohamed kuanzisha oparesheni ya kumtafuta Briton. Hakuficha chochote kwa bwana Abdulah Mohamed. Akamuelezea hisia za mapenzi ambazo anazo kwa Briton.

Vikosi vya kigaidi vya kundi hilo vikiongozwa na Shamsa, akiwa amerudi upya kwenye kazi hiyo kwa lengo la kumtafuta mpenzi wake. Vikaanza oparesheni ya kuteka meli ambazo zinakatiza katika ukanda wa Somalia. Kila meli iliyo kamatwa ilifanyiwa upekuzi wa mu mmoja baada ya mwengi. Kuhakikisha wanamtafuta Briton kwa udi na uvumba. Zoezi hilo lilizidi kudumu takribani mwenzi mzima, ila hakufanikiwa kuweza kumtia machozi Briton.

Wazo la Briton kufa maji likaanza kutawala moyo wake na akili. Kumbukumbu ya ajali waliyo weza kuipata kipindi walipo kuwa wanatoroka. Ikazidi kumuogopesha. Unyonge ukaanza kumtawala na kujiona ni msichana asiye na bahati. Muda mwingi akawa anautumia katika kunywa pombe kali na kulewa chakari.

Hali hiyo ikazidi kumsikitisha bwana Abdulah Mohamed. Ikamlazimu kumtafutia Shamsa madaktari wa saikolojia kutokea Japan. Madaktari hao baada ya kumfanyia Shamsa uchunguzi wa kina wakatambua, akili yake inakwenda kuchanganyikiwa kwa ajili ya mapenzi.

Wakamuomba bwana Abdulah Mohamed, kumruhusu Shamsa waende naye Japan kwa ajili ya matibabu. Ombi hilo kwa mara ya kwanza likawa gumu sana kwa Bwana Abdulah Mohamed. Ila kwa jinsi ali ya Shamsa ilivyo zidi kuwa mbaya hadi kiafya ikamlazimu kumruhusu waondoke naye, ila akiwa na walinzi wangine wawili wakike. Kwa usafiri maalumu wa ndege ya Jeti ya kifahari inayo milikiwa na kikundi hicho ikaanza, kuelekea Japan.

***
Eddy hakuhitaji kufanya makosa ya kurudi Tanzania kwa wakati huo. Akawatazama askari waliomo ndani ya kiwanja cha ndege hiyo.

"Naomba niende haja ndogo"
Eddy alimuomba Mama Ngoi ambaye yupo na baadhi ya askari wa Japan pamoja na Tanzania wanao mlinda. Eddy akasindikizwa hadi chooni na askari wawili wa kijapan ambao walibaki nje ya mlango kumsubiri. Eddy akakuta vijana wawili masharo baro waliomo ndani ya choo hicho, kutokana hakuwa na haja ya kwenda kwenye haja zinazo takiwa kufanyika chooni.

Alicho kifanya, nikuwasogelea vijana hao walio simama kwa pamoja wakikojoa katika sehemu mbili maalumu zinazo fanana. Pasipo kuwauliza akawapiga maeneo ya nyuma ya shingoni kwa kutumia viganga vyake vilivyo komaa kwa mazoezi.Vijana hao wakapoteza fahamu. Kwa haraka Eddy akaanza kumvua nguo mmoja wao. Akazivaa akachukua koti la mmoja wao na kulivaa vizuri, akachukua na kofia iliyo mficha vizuri sura yake.

Alipo jitizama kwenye kioo akatabasamu kwani, amebadilika kwa kiasi kikubwa na si rahisi kwa askari alio waacha nje ya mlango kumtambua. Akajipapasa kwenye mifuko ya nguo za kijana aliye mchukulia nguo. Akakuta noti mbili za dola mia mia za kimarekani. Akampapasa mwengine na kumkuta na yen kumi, pesa ya kijapani.

Pasipo kupoteza muda akatoka katika choo hicho na kuwakuta askari wakiendelea kumsubiria. Akawapita kwa kujiamini, askari hao wala haku shuhulika naye waliendelea kupiga stori zao.

Maalim Seif azipiga kufuli akaunti za CUF, Lipumba Alalamika

$
0
0
Mwenyekiti wa CUF anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama Siasa, Prof. Ibrahim Lipumba amelalamikia kitendo cha Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharrif Hamad kuzifunga  akaunti zote za chama hicho za wilaya.
 
Ameyasema hayo wakati wa kikao cha baraza la uongozi linaloongozwa na upande wake. Profesa Lipumba amesema kutokana na uamuzi huo ruzuku ya chama kutoka serikalini wameikosa.
 
“Wajumbe nawashukuru kwa kuja ili kupata fursa ya kujenga chama. Chama chetu kipo ndani ya mtihani ambao kwa kweli chanzo chake ni Katibu Mkuu wetu kutoheshimu katiba yetu na kutoheshimu taratibu za kidemokrasia,” amesema Prof. Lipumba.
 
Aidha, Prof. Lipumba amesema kuwa Maalim Seif alitakiwa kuhudhuria kikao hicho na alipewa taarifa lakini hakuweza kufika, hali iliyosababisha majukumu yake kusimamiwa na Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara. Magdalena Sakaaya.
 
Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Zanzibar), Nassor Mazrui amesema kuwa hatua ya kufunga akaunti za benki imelenga kulinda fedha ya chama ili zisitumiwe vibaya na upande wa Profesa Lipumba.
 
Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa bado anamtambua Prof. Lipumba kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho kwa kuwa hakuwa na taarifa kuhusu uamuzi wake wa kujiuzulu.

Jeshi la Polisi Morogoro latoa sababu kukamatwa kwa Nay wa Mitego

$
0
0
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro, Kamanda Ulrich Matei amethibitisha kukamatwa kwa msanii Nay wa Mitego usiku wa kuamkia leo mkoani Morogoro.

Kamanda Ulrich Matei ametoa sababu kubwa ya kukamatwa kwa msanii huyo ni kutokana na kutoa wimbo unaofahamika kwa jina la 'Wapo' ambao anadai unaikashfu Serikali iliyopo maradakani.

Kamanda Matei amesema shauri la Nay wa Mitego lipo jijini Dar es Salaam hivyo msanii huyo atasafirishwa na kupelekwa Dar es Salaam kuhojiwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa mkoa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images