Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Magufuli Awapa Makavu Wabunge Wa CCM Wanaompinga Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais Dkt John Pombe Magufuli juzi akiwa yupo mkoani Dodoma, alipata nafasi ya kufanya kikao na wabunge wa chama hicho ambapo alizungumza mambo mbalimbali ambayo hafurahishwi nayo kama kiongozi mkuu wa chama.

Rais Magufuli alikutana na wabunge hao katika Ikulu ndogo ya Chamwino Mkoani Dodoma ambapo miongoni mwa mambo mengi aliyozungumza nao ni pamoja na kuwaambia kuwa anafahamu baadhi ya wabunge wanampinga Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

"Nafahamu baadhi yenu mnampinga Waziri Mkuu na mnataka aondolewa kwa kura ya kutokuwa na imani naye, naomba niwaambie kuwa hamtafanikiwa. Mimi namuunga mkono msaidizi wangu huyuo kwa asilimia 100 kwa nimejionea mwenye namna anavyoweza kufanya kazi, "alisema Rais Dkt Magufuli na kuongeza.

"Hata mkimuondoa, nikija kuteua mwingine nitamleta huyu huyu na endapo mtamkataa basi nitavunja bunge wote mrudi kwenye uchaguzi."

Mbali na hilo kiongozi huyo alitoa onyo kwa wabunge wa CCM ambao wanagawa muda wao wa kuzungumza na kuwapa wabunge wa upinzani pindi wanapokuwa kwenye vikao vya bunge. 

Kauli hii imekuja baada ya Mbunge wa Jimbo la Bunda (CCM), Boniface Getere kumpa dakika tano mbunge wa Serengeti (Chadema), Marwa Ryoba kutoka kwenye muda wake wa kuchangia ambao ni dakika 10.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti Dkt Magufuli amewaambia kuwa anakerwa na baadhi ya wabunge kufifisha jitihada za serikali katika kupambana na dawa za kulevya huku akimtuhumu mbunge mmoja kutoa siri na kuzipeleka upinzani.

Kuhusu matangazo ya bunge kutokurushwa mubashara, Mwenyekiti wa CCM aliwaambia wabunge hao kuwa yeye ndio aliamua iwe hivyo kutokana na wabunge wengi kuwa wapiga porojo tu.

Credit: Mwananchi

Kauli ya Godbless Lema kuhusu wabunge CCM waliokwenda kumsalimia gerezani kuitwa wasaliti

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameibuka na kueleza kushangazwa na kauli ya Rais Dk. John Magufuli kwamba wabunge wa CCM waliotaka kwenda kumwona gerezani walikuwa wasaliti.

Lema alisema anatarajia Spika wa Bunge, Job Ndugai, atatoa msimamo juu ya kauli ya kiongozi huyo wa nchi.

Kauli hiyo ya Lema imekuja siku moja baada ya Rais Dk. John Magufuli, kuripotiwa na chombo kimoja cha habari  kwamba alishangazwa na hatua ya baadhi ya wabunge wa CCM waliounda kamati ya kutaka kwenda kumtembelea Lema gerezani.

Katika mkutano wake na wabunge hao juzi uliofanyika Ikulu ndogo ya Chamwino mkoani Dodoma, Rais Magufuli alisema amekuwa akielezwa kuwa kamati hiyo ilikuwa imepanga safari za kutaka kwenda kumwona Lema alipokuwa gerezani jambo ambalo alilifananisha ni sawa na usaliti kwa chama chake.

Katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, Lema alisema kitendo cha wabunge hao kutaka kumtembelea si usaliti bali ni upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yeyote pale anapokuwa na matatizo.

Lema alikaa gerezani kwa muda wa miezi minne kwa kukosa dhamana kutokana na mashtaka yaliyokuwa yakimkabili.

“Mheshimiwa Rais Magufuli nakusalimu. Nimetoka gerezani hivi karibuni ambako nilikuwa huko kwa zaidi ya miezi minne kwa kunyimwa masharti ya dhamana kwa dhamana iliyokuwa wazi.

“Nimeona kwenye vyombo vya habari leo kwamba wale wabunge waliokuwa wanataka kunisalimia nilipokuwa magereza ni wasaliti wa chama cha CCM.

“Mheshimiwa Rais wengi walinisalimia wakiwemo wachungaji, masheikh, wabunge na viongozi mbalimbali, sidhani kama hatua hii ilikuwa ni usaliti isipokuwa upendo ambao ni muhimu kwa binadamu yeyote pale anapokuwa na matatizo.

“Mheshimiwa  Rais nimeogopa sana kwa kauli hii, je Taifa linakwenda wapi? Hivi kweli sisi wabunge ni maadui? Kama viongozi tutafikiri utengano ni moja ya njia ya kuimarisha vyama vyetu, bila shaka tutakuwa tunalitendea Taifa ubaya,” alisema Lema.

Mbunge huyo alisema dhambi hiyo ikikomaa ni wazi kwamba lugha za kidini, ukanda na ukabila hazitaacha kukomaa.

Alisema ni muhimu sasa wakajenga utamaduni wa kuhimiza mshikamano wa kitaifa bila kujali itikadi kama kweli wanapenda masikini na wanyonge.

“Nawaomba wabunge wenzangu walionijali wakati niko gerezani wasijisikie vibaya kwani walifanya jambo jema na muhimu kwa wakati muhimu sana katika maisha yangu ninatarajia kuwa Spika wa Bunge atatoa neon juu ya kauli hii ya Rais.

“Mheshimiwa Rais wakati wa msiba wa Christina Lissu dada yake na Tundu Lissu, nilikuona katika msiba ule wewe na mama yetu mke wako, je wewe ulikuwa unasaliti chama chako?

“Meshimiwa Rais neno la Mungu linasema wapendeni maadui zenu, waombeni wanaowadhi, wabarikini wanaowaonea kwani kufanya hivi ni kuishi kwa thawabu za Mwenyezi Mungu,”alisema Lema.

Mbunge huyo alisema pamoja na hali hiyo ya kuzuiwa lakini aliwashukuru wabunge wa CCM kwa kwenda kumjulia hali, akiwa nyumbani kwake baada ya kutoka gerezani.

“Sina la kusema katika hili kama Rais alikuwa anajua hawakuja kuniona gerezani lakini niwashukuru wabunge wa CCM wote waliokuja kunijulia hali nyumbani. Sisi kama nchi tunatakiwa kuwa na umoja badala ya kuanza kubaguana kwa itikadi zetu za vyama.

“Mdogo wangu wa kike amepata mchumba lakini familia ya huyo mchumba wake inatokana na CCM je tuvunje vikao vya harusi kwa sababu ya tofauti ya vyama?

“Jibu ni hapana sisi ni Watanzania ni lazima tuishi kwa kupenda na kwa umoja kama ambavyo utamaduni wetu unatutaka na si vinginevyo,” alisema.

Lema alikamatwa Novemba 2, mwaka jana mjini Dodoma nje ya viwanja vya Bunge na kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Novemba 4 mwaka jana akikabiliwa na kesi mbili namba 440 na 441 za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Katika kesi ya kwanza ya jinai namba 440, anadaiwa kati ya Oktoba 22 mwaka jana maeneo ya Kambi ya Fisi, Kata ya Ngarenaro, katika mkutano wa hadhara alitoa maneno yenye kuleta tabaka miongoni mwa jamii kwa kutoa matamshi yenye chuki, kuibua nia ovu kwa jamii.

Katika kesi ya pili namba 441, alidaiwa kwamba, Oktoba 23, mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja vya Shule ya Sekondari Baraa, Lema  alitoa maneno kuwa:

“Kiburi cha Rais kisipojirekebisha, Rais akiendelea kujiona yeye ni Mungu, nimeota  Mwaka 2020 haitafika Mungu atakuwa ameshamchukua maisha yake,”.

Februari 27,  mwaka huu, Mahakama ya Rufaa Tanzania ilifuta rufaa mbili za Jamhuri dhidi ya Lema baada ya mawakili wa Serikali kuieleza mahakama  hiyo kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), hana nia ya kuendelea na rufaa, hivyo kuiomba mahakama kuzifuta rufaa hizo zilizokuwa zinahusu dhamana ya mbunge huyo.

Kilichoendelea Leo Mahakamani Kuhusu Kesi ya Madawa ya Kulevya Inayomkabili Wema Sepetu

$
0
0
Kesi ya Dawa za kulevya inayomkabili muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Wema Sepetu iliyokuwa isikilizwe leo, imeahirishwa hadi Aprili 11 mwaka huu baada ya upande wa mashtaka kudai kuwa upelelezi haujakamilika.

Muigizaji huyo ni mmoja kati ya wasanii ambao walitajwa kwenye list ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda yawatuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Katika upelelezi wa awali ambao ulifanywa na jeshi la polisi, walidai wamekuta msokoto wa bangi nyumbani kwa muigizaji huyo.

Mwaka Mmoja ya Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kuwa madarakani.......Yote Aliyoyasema Yako Hapa

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda leo Machi 15, 2017 anatimiza mwaka mmoja tangu ateuliwe kuwa Mkuu wa Mkoa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Machi 13, 2016 na kuapishwa Machi 15, 2016.

==>Haya ni Baadhi ya Maneno Yake

1.Namshukuru Rais Magufuli kwa kusikiliza kauli ya Mungu na kunikabidhi mamlaka ktk mkoa huu wa Dar.

2.Navishukuru sana Vyombo vya Habari kwa kuwa daraja kati ya Serikali ya Mkoa na wananchi. Wamefanya kazi kubwa!

3.Nawashukuru sana vijana tuliowakamata wa mwanzo(TID na wenzake), wamekuwa mfano mzuri kwa wenzao na Mungu awasaidie

4.Mwaka wangu wa II nikiwa kama RC wa Dar, kasi itaongezeka maana nimekomaa sasa. Nitahakikisha jiji linarudi kwny mstari.

5.Kuna makampuni ya barabara mawili nimeshayapiga marufuku kwa sababu ya kujenga barabara chini ya viwango.

6.Katika vitu nimeweka msingi mzuri ni kinondoni, kesi za ardhi zinasikilizwa mpaka jumamosi

7.Kazi hii nimepewa na Mungu, acha idadi ya wanaomchukia Makonda waongezeka lakini niwe na uhakika na Mungu wangu

8.Tumeamua kufanya vitu hadharani kwa sababu hatutaki kupokea rushwa wala fedha haramu

9.Hatuna kisasi na mtu, ndio maana upande huo wanapigana sisi tunacheka

10.Kupitia fedha za dawa za kulevya, watu wamejenga maghorofa yanakwenda kwa kasi sana na wamefanya hata thamani ya viwanja ipande

11.Fedha hizi za dawa za kulevya zinaenda kukauka DSM ili kila mtu ale kwa jasho lake

12.Tutaanza mfumo wa kutumia kadi ili tukusanye kodi yetu na kila mtu ale kwa jasho lake, kuna watu wanaficha fedha

13.Kipindi hiki ni cha kazi. Nawapongeza wote wanaofanya kazi kwa bidii na kuifanya Serikali isimame kidete

14.Changamoto mojawapo niliyokutana nayo ni MUDA! Muda hautoshi, nahitaji hata miaka kadhaa ili kumsikiliza kila mwananchi

15.Changamoto nyingine ni mazoea ya Watendaji wa Serikali ktk kutoa huduma. "Njoo kesho" imekuwa kero kwangu na kwa wananchi

16.Kuzungushwa kwa wananchi kunapelekea changamoto katika za Serikali za Mitaa kuletwa ofisini kwangu. Hili nalo ni tatizo!

17.Nampongeza sana Kamishna Sirro na Awadhi (wa Usalama barabarani) kwa kusimamia ulinzi na usalama jijini Dar

18.Milio ya risasi ilikuwa kawaida Dar, watu waliogopa hata kwenda Mlimani City kwa hofu ya kuporwa. Tumeyakomesha yote hayo

19.Mtu anataka nikae kimya wakati wananchi wangu Dar wanateseka kwa matumizi ya DawazaKulevya... Nauliza "Wewe ni NANI?"

20.Tunapambana kupigania ndoto za vijana na matumaini ya wazazi wao. Haijalishi tumechelewa kiasi gani lakini hatutoacha!

21.Wapiga dili wa Bandarini jijini Dar wamekuwa wakisumbua kwa fedha zisizo halali na kuwasumbua wafanyabiashara halali

22.Sibabaishwi na watu wanaonichukia wakati nikitekeleza majukumu niliyopangiwa na Rais Magufuli kama Mkuu wa Mkoa.

23.Bureau de Change zinatumika kufichia pesa haramu. Wiki ijayo moto utawaka, lazima tushughulikie maficho haya.

24.Sasa foleni jijini Dar imepunguzwa kwa kiwango kikubwa na askari. Ukifurahishwa na trafiki toa shukrani zako, tuwape moyo.

25.Mwaka huu wa pili tutakazia sana kwenye utumishi. Nitaanzia kwenye Serikali za Mitaa nione jinsi wanavyowasaidia wananchi.

26.Nataka mwananchi apate majibu kamili aendapo Ofisi ya Umma. Kama hawawezi kumsaidia waende wao ofisi ya juu sio mwananchi.

27.Wanaoishi mabondeni jijini Dar na wana hati halali nitawapa viwanja. Watendaji waliotoa hizo hati nitawashughulikia!

28.Najua wengi wanaoishi mabondeni wamepangishwa na waliolipwa fidia. Huwezi kuwa na akili timamu ukakubali kupanga bondeni

29.Hivi karibuni nitaelekeza wapi showroom za magari zinatakiwa ziwe jijini Dar. Nataka magari yote yauzwe eneo moja

30.Ninawashukuru wanasheria wetu 35 wanaotoa msaada na ushauri wa kisheria bure kwa wananchi wa jiji la Dar wasio na uwezo

31.Tumepewa eneo kubwa la kujenga kambi kwa ajili ya wahanga wa DawazaKulevya. Hii itatusaidia kufuatilia mienendo yao

32.Hadi sasa tuna watu 11,854 jijini Dar waliokubali kuacha matumizi ya DawaZaKulevya kwa hiari. Haya ni mafanikio makubwa

33.Wengine tukiwaita Kituo cha Polisi wanatumia Colgate na Chumvi ili wasigundulike ktk vipimo. Tuna mbinu mpya za kuwapima

34.Kuna wanaowatumia watoto wadogo kufanya uhalifu na kabla ya hapo wanawavutisha bangi. Tunawasaka na tutawakamata!

==> Bonyeza play kumsikiliza LIVE Hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya March 16

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge)

Kiroba Champonza Padri wa Kanisa Katoliki....Polisi Wamtia Mbaroni

$
0
0
Polisi  mkoani Ruvuma inamshikilia Padri wa Kanisa Katoliki Parokia ya Kitanda wilayani Namtumbo, Gislary Tweve kwa tuhuma za kumshambulia mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kitanda, Adolf Nyoni (34) baada ya kukataa kulipa kinywaji aina ya Konyagi, kilichokuwa katika kifungashio cha plastiki (kiroba) alichokunywa katika duka la kanisa hilo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Zuberi Mwombeji alisema padri huyo anadaiwa kutenda kosa hilo Machi 10, mwaka huu, saa mbili usiku katika duka la Parokia ya Kitanda.

Kamanda Mwombeji alisema Padri Tweve alimpiga Nyoni kichwa na makofi, kisha kumrukisha kichura kwa kile kinachodaiwa kukataa kulipa pombe hiyo ambayo imekatazwa kisheria, lakini duka hilo bado limekaidi na kuendelea kuuza pombe hiyo.

Alisema Polisi inaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo na mara utakapokamilika, mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.

Aidha, Jeshi la Polisi limetoa rai kwa wakazi wa Mkoa wa Ruvuma, kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa makosa mbalimbali katika vyombo vya dola, badala ya kujichukulia sheria mkononi na kuachana na biashara iliyopigwa marufuku ya pombe kali zilizofungwa kwenye vifungashio vya plastiki.

Kuanzia Machi mosi, mwaka huu, serikali imepiga marufuku utengenezaji, usambazaji, uuzaji na unywaji wa pombe zilizowekwa katika vifungashio vya plastiki maarufu kwa jina la viroba, na kuibainisha kuwa itatoa adhabu zikiwemo faini za hadi Sh milioni tano, kifungo jela au vyote kwa pamoja, kwa watakaokiuka marufuku hiyo.

Serikali imechukua hatua hiyo baada ya kubainika kwamba mbali ya kuikosesha mapato serikali yanayofikia Sh bilioni 600 kwa mwaka, pombe hizo za kwenye viroba zimekuwa zikitumiwa isivyo kutokana na ufungashaji wake wa kirahisi.

Wasonga, Tundu Lissu Nusura Watwangane Ngumi Mahakamani

$
0
0
Mawakili maarufu nchini Tundu Lissu na Godfrey Wasonga jana nusura wazipige kavukavu na kama si busara za mawakili wengine waliokuwa wamefurika katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma na hasa Deus Nyabiri, huenda hali ingekuwa tofauti.

Katika mahakama hiyo, ambayo ilifurika umati mkubwa wa mawakili na wasikilizaji, wawili hao waliibua mzozo wakiwa kwenye korido walipokuwa wakisubiri kuingia kwenye chumba cha mahakama kuanza kusikilizwa kwa kesi mbili, ya kwanza namba 12/2017 ya kupinga uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) ambayo ilifunguliwa na Wasonga, na nyingine ni namba 13 na 14/2017 ambazo Lissu na wenzake walipeleka maombi ya kuunganishwa katika kesi hiyo ya Wasonga.

Sakata lilianzia kwa Lissu, ambaye aliwashawishi wenzake kumuunga mkono kabla ya kuanza kesi hiyo kuwa wamuombe Jaji Awadh Muhamed abadilishe chumba cha kusikilizia kesi hizo kutokana na umati uliokuwa umefurika akisema eneo alilopanga lilikuwa ni dogo.

Hoja hiyo ilipingwa na Wasonga ambaye alimtaka Lissu kunyamaza kwa kuwa si mhusika ndipo wakaanza kurushiana maneno makali na kutaka kupigana huku kila mmoja akiwa ameshikiliwa na watu.

“Nitakufanya kama nilivyokufanya kule Singida na sijui kama umesahau... nitakushughulikia mimi si wa mchezo mchezo ,” alisema Wasonga huku akiwa ameshikwa na mawakili wanne.

Wakati huo, Lissu aliyekuwa ameshikwa mkono na Nyabiri alikuwa akirusha maneno kwa Wasonga akimweleza kuwa hawezi kumfanya kitu.

Kelele hizo zilimfanya Jaji Muhamed aliyekuwa akiendelea na kesi nyingine kuhoji sababu za kuwapo kelele nje hivyo kumtuma askari magereza ambaye aliwaambia jaji anahoji sababu ya kelele hizo.

Baada ya angalizo hilo, Nyabiri aliwasihi wanyamaze lakini Wasonga alionekana bado ana hasira hivyo mawakili wenzake kumtoa.

Nje ya mzozo huo, katika kesi mbili ambazo ziliwafikisha mahakamani hapo jana, Lissu ambaye ni mgombea urais wa TLS na mgombea umakamu wa rais, Godwin Ngwilimi walisema wanamwakilisha mgombea mwingine wa urais, Lawrence Masha kutaka mahakama ikubali ombi lao la kuingizwa katika kesi namba 12/2017 ambayo ilifunguliwa na Wasonga.

Katika kesi namba 12, Jaji Muhamed alianza kusoma barua ya Wasonga ya kutaka aiondoe mahakamani kwa kuwa ilifunguliwa kimakosa lakini akasema anayo hati ya kufungua upya baada ya marekebisho.

Alipomaliza kusoma barua hiyo, jaji akaomba muda wa kuitafakari huku akiwaomba mawakili wakubali kuhamisha chumba cha mahakama kutokana na idadi kubwa ya watu.

“Hii barua ya kuondoa kesi ndiyo nimeipata muda huu, naomba mnipe muda ili nitafakari, baada ya dakika 15 tukutane mahakama ya wazi maana hapa naona hapatoshi, lakini siyo lazima mje na majoho kwani mnajulikana,” alisema.

Baada ya dakika 20 wakiwa katika mahakama ya wazi, Jaji Muhamed aliwaita mawakili wa pande zote na kuzungumza nao kwa dakika 22 ndipo wakarejea saa 5:40 asubuhi. Kesi hiyo iliendelea tena huku kila upande ukipewa dakika sita ukianza na upande wa waliopeleka maombi ya kutaka waunganishwe katika kesi hiyo.

Mawakili hao; Lissu, Fred Kalonga, Paul Kaunda na Ngwilimi waliamua kumpa dakika zao Lissu na akazitumia kuwasilisha kile walichokiita hati ya haki.

Lissu alisema waliamua kuomba nafasi ya kuunganishwa katika kesi hiyo kwani wanajua kuwa kama hawataunganishwa, kwa vyovyote haki yao inaweza kupotea na hasa kwa wagombea.

“Mheshimiwa jaji, mimi Tundu Lissu na Lawrence Masha ni wagombea wa nafasi ya rais wa TLS, lakini pia yupo mwenzetu Godwin Ngwilimi ambaye anagombea nafasi ya makamu wa rais, kwa pamoja tunaomba kuunganishwa katika kesi hii kwa kuwa tuna masilahi na tunaweza kupoteza,” alisema Lissu na kuongeza:

“Kanuni ya 14 ya Mwenendo wa Mashtaka inaruhusu mtu mwenye masilahi kuomba aingizwe. Katika kanuni hiyo kifungu cha 1 na 2 vinaruhusu mheshimiwa Jaji, na hati ya maombi inajieleza yenyewe.”

Baada ya kueleza hayo ilikuja zamu ya Wasonga ambaye alisema,“Mheshimiwa Jaji, hakuna mahali ambapo mawakili hawa wanaweza kuingia na sheria inawaondolea uhalali hata wa kuleta maombi ya aina hii.”

Wasonga alihoji kati ya wagombea wote ni kwanini hao watatu ndiyo waliamua kwenda mahakamani Dodoma kutaka waunganishwe wakati wako wengi na akahoji kama ni gharama mbona wote walikuwa wameziingia.

Kuhusu ombi lake la kupinga uchaguzi, alisema kanuni za uendeshaji ni mbovu na haziwezi kuwafanya viongozi wake kuwa halali.

Mawakili Deus Nyabiri na Elias Machibya ambao walisimama kwa niaba ya TLS, walikubaliana na hoja za waleta maombi Lissu na wenzake kwamba wanazo sababu za msingi za kuomba kuingizwa katika kesi hiyo huku wakisema Wasonga alifanya uamuzi kwa kukurupuka na kwamba ana lengo la kuivuruga TLS.

Machibya alisema hoja zote za Wasonga hazikuwa na mashiko, akaiomba mahakama kutupilia mbali utetezi wa wakili huyo na waombaji waingizwe na ili waje kumdai gharama.

Machibya alisema kanuni alizozipinga Wasonga ni nzuri kwani zilianza kutumika Januari Mosi, 2016 na kwamba viongozi wa sasa waliingia kwa kutumia kanuni hizo.

Mvutano uliendelea huku Jaji akisisitiza wapeane nafasi ya kueleza bila kurushiana maswali ndipo Ngwilimi alipohitimisha kwa kumuomba Jaji awaruhusu waingizwe kwenye kesi na bila ya kufanya hivyo, watakuwa wamepoteza haki zao zote kwani walishatumia gharama kuwashawishi watu wawachague.

Baada ya hoja hizo, Jaji Muhamed aliahirisha kesi hiyo kwa muda na ilipotimu saa 8:00 mchana alisema akirejea atatoa uamuzi wa kama waombaji wanastahili kuingizwa kwenye madai hayo au hawana sifa.

Aliporejea saa 8:13 mchana, Jaji hakutoa uamuzi huo kama alivyokuwa ameahidi kwani malumbano yaliendelea kwa kiasi kikubwa baada ya Wasonga kukiri kuwa alikuwa amekosea katika shtaka la awali, lakini akasema anayo hati nyingine ya kuwasilisha kwa kuifungua upya.

Ilichukua zaidi ya saa mbili kwa mawakili kuwasilisha hoja za kumpinga huku wakimpiga vijembe Wasonga ambaye hata hivyo alionekana kuwa imara kwa kujibu mashambulizi kila alipopewa nafasi.

Wakili wa Serikali, Angaza Mwipopo aliungana na hoja za upande wa Lissu na TLS kuwa Wasonga alikuwa amekosea na kumtaka akubali kuondoa kesi yake mahakamani na kulipa gharama.

Hata hivyo, Wasonga alipinga hoja ya kulipa gharama akisema atawasilisha ombi jingine lililo sahihi alimradi ahakikishe uchaguzi wa TLS haufanyiki.

Kesi zote mbili zitatolewa uamuzi leo mchana na Wakili Wasonga alisema baada ya uamuzi huo atafungua kesi nyingine hapohapo ambayo tayari alishafanya marekebisho ya vipengele vyake.

Wakati hayo yakitokea Dodoma, jijini Dar es Salaam jana mahakama ilieleza kuwa hatima ya kesi dhidi ya TLS itajulikana leo wakati itakapotoa uamuzi wa pingamizi lililowekwa na Serikali pamoja na TLS.

Kesi hiyo ya kikatiba imefunguliwa na wakili wa kujitegemea, Onesmo Mpinzile katika Mahakama Kuu Masjala Kuu Dar es Salaam dhidi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG).

Katika kesi hiyo, Mpinzile anapinga kanuni za uchaguzi za TLS za mwaka 2016, akiiomba mahakama itamke kuwa ni batili kwa madai kuwa zilisainiwa na kupitishwa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka katika TLS.

Hata hivyo, juzi AG na TLS waliwasilisha pingamizi la awali wakiiomba Mahakama iitupilie mbali kesi hiyo, wakidai kuwa mdai hana haki ya kisheria kufungua kesi hiyo na kwamba hati ya kiapo inayounga mkono maombi yake ina dosari za kisheria.

Hoja hizo za pingamizi la Serikali na TLS zilisikilizwa na jana mdai kupitia kwa wakili wake, Emmanuel Makene, alimalizia kujibu hoja hizo za pingamizi huku naye akiiomba mahakama itupilie mbali mapingamizi hayo ya Serikali na TLS.

Baada ya kukamilisha usikilizwaji wa hoja za pande zote jana, kiongozi wa jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo, Rose Teemba aliiahirisha hadi leo kwa ajili ya uamuzi. Mbali na Jaji Teemba, majaji wengine katika kesi hiyo ni Beatrice Mutungi na Ignas Kitusi.

Tundu Akamatwa Na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma

$
0
0
Mbunge Tundu Lissu amekamatwa na jeshi la polisi asubuhi hii nyumbani kwake na kupelekwa ofisi ya Kamanda wa Polisi mkoani Dodoma.
 
==>Huu ni Ujumbe wa Tundu Lissu alioutumia mtandaoni
Wandugu wapendwa. Ninaandika haya nikiwa nyumbani kwangu Dodoma. Najiandaa kwenda mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa Mahakama Kuu juu ya kesi ya kutaka kuzuia Uchaguzi wa TLS.

Ninawapa taarifa kwamba nimefuatwa nyumbani na askari wawili kutoka ofisi ya RPC Dodoma. Sijazungumza nao bado lakini ni wazi wana maagizo ya kunikamata na kunizuia kuja Arusha kwenye Uchaguzi wa TLS. Wameshindwa kuzuia uchaguzi wetu mahakamani. Sasa, kama kawaida ya serikali za kidikteta kila mahali, wanatumia mabavu ya kijeshi.

Wito wangu kwenu mawakili wa Tanzania:
Nendeni Arusha mkachague viongozi wa TLS watakaopigania haki za binadamu, utawala wa sheria na demokrasia. Msipofanya hivyo hakuna mtu yeyote, hata ninyi mawakili, atakayepona kwenye utawala wa aina hii.

Kumbuka, kama Nimrod Mkono anaweza kufungiwa ofisi na TRA ni wakili gani mwingine aliye salama??? Kama wakili anaweza kukamatwa mahakamani kwa kufanya kazi yake ya uwakili, ni nani miongoni mwetu aliye salama??? Nendeni mkapige kura kukataa mfumo wa aina hii.

Mimi naenda mahabusu, na pengine, gerezani. Nawaombeni kura zenu ili niweze kuwaongoza katika kipindi hiki kigumu. 

Hiki sio kipindi cha kuwa na viongozi wanaojipendekeza kwa wanaokandamiza haki za watu wetu na haki za mawakili wetu. 

Hiki ni kipindi cha kuwa na viongozi watakaopigania haki zenu na haki za watu wetu. Mnanifahamu. Nipeni jukumu hili la kuwaongoza kwenye giza hili nene. Msikubali kuyumbishwa.

Na wachagueni pia Makamu wa Rais, Mweka Hazina wajumbe wa Governing Council watakaokuwa na msimamo kama wa kwangu.

Nawatakieni kila la kheri. I'll think of you all wherever they'll take me to, wherever I'll be incarcerated. This too shall pass. The race of man shall rise again. It always has. Nimemwambia na mke wangu naye aende Arusha akapige kura. So, everybody to Arusha. Go vote your consciences.

All the best.

TL

UPDATES: Tundu Lissu Asafirishwa Kuelekea Dar es Salaam Akidaiwa Kuruka Masharti ya Dhamana

$
0
0
Mbunge Tundu Lissu(CHADEMA) amekamatwa na Polisi asubuhi ya leo nyumbani kwake Dodoma na kupelekwa Ofisi ya Kamanda wa Polisi na sasa anasafirishwa kwenda Dar es Salaam kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana.

Hashim Rungwe amvaa Dkt. Mwakyembe.....Amtaka asiivuruge TLS

$
0
0
Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe kuacha kuingilia mambo yanayohusu chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) hasa kwenye suala uchaguzi wa kumsaka Rais wa chama hicho

Akijibu maswali ya wananchi kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa katika ukurasa wa Facebook EATV, Mh. Rungwe amesema kuwa TLS ina utaratibu wake wa kuendeshwa na kamwe haiwezi kupelekwa kama jinsi waziri anavyotaka kwani chama hicho kinaongozwa kwa sheria na kanuni.

“Yeye kama Waziri maoni yake ni muhimu, lakini  anasema vijana hawa wawili wana maoni ya kisiasa yaani Lissu na mwenzake lakini wakati huo huo yeye ni waziri na mpaka amefika hapo yupo ndani ya chama cha kisiasa. na amevaa kofia mbili. TLS  haiwezi kuendeshwa kama anavyotaka yeye, huwezi kutengeneza utaratibu nje ya utaratibu. Tuheshimu pia taaluma za watu." Rungwe alifunguka.

Aidha Rungwe ambaye pia ni Wakili wa Mahakama Kuu na Mwanachama wa chama hicho ameongeza kuwa katika chama hicho hakuna sheria ambayo inamzuia mwanasiasa yoyote kugombea nafasi na kuongeza kwamba kuwazuia upinzani wakati waliomo kwenye chama tawala wanaruhusiwa ni kutengeneza chuki ndani ya jamii na nchi kwa ujumla

"Kutengeneza chuki kwa makusudi it's a great crime, hasa chuki ikitengenezwa na viongozi waliopo madarakani, ambao wamepewa dhamana ya kuwaongoza wananchi yeye atuache na TLS yetu, kama itaonesha watu hawa hawaruhusiwi kugombea basi watazuiliwa kwasababu watu wanaochuja wagombea ni sisi wenyewe". Amesema

Hivi karibuni Waziri huyo wa Sheria na Katiba alinukuliwa akisema kuwa serikali haiwezi kuona (TLS) ikinajiingiza katika siasa na kuongeza kuwa kama wanataka hivyo, basi serikali haitasita kuifuta Sheria ya TLS Sura ya 307 iliyoanzisha chama hicho cha wanasheria.

Mawakili wa Manji wawasilisha ombi Mahakamani Kuhusu kesi yake kwamba sio Raia wa Tanzania

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu Yusuf Manji amewasilisha hati ya kuiomba Mahakama Kuu iwaagize maofisa Uhamiaji wamfikishe mahakamani ili kesi yake isikilizwe kwa mujibu wa sheria.

Manji yuko kwenye matibabu Hospitali ya Aga Khan jiji hapa akiwa chini ya ulinzi baada ya kuachiwa kwa dhamana. Februari 20 mwaka huu, alipelekwa ofisi ya Uhamiaji mkoa na kuhojiwa kwa madai ya kuingia nchini kinyume cha sheria.

Katika kesi hiyo wajibu maombi hayo ni Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG) na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Wakili wa Manji, Hudson Ndusyepo aliyefungua kesi ya maombi hayo, anataka Mahakama iagize maofisa uhamiaji na polisi kumfikisha mahakamani ili iamue uhalali wa kushikiliwa kwake na kuagiza aachiwe.

Katika hati ya maombi hayo, Ndusyepo anadai kuwa alimtembelea mteja wake hospitali ya Aga Khan Februari 17 mwaka huu na kukuta maofisa wa Uhamiaji wakimsubiri mteja wake wampeleke kwa ofisa Uhamiaji wa mkoa kwa mahojiano dhidi ya tuhuma kuwa siyo raia wa Tanzania.

Kwa mujibu wa Ndusyepo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Quality Group Limited na Diwani wa Mbagala Kuu, Amedai kuwa alitoa maelezo kwa maofisa Uhamiaji na alirudishwa Aga Khan ambako yupo chini ya ulinzi hadi leo.

Mahakama Kuu Yatupilia Mbali Kesi Ya Kuzuia Uchaguzi TLS

$
0
0
Mahakama Kuu imetupilia mbali kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Wakili Onesmo Mpinzila pamoja na mambo mengine akipinga Kanuni za Uchaguzi za Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) za mwaka 2016.

Kesi hiyo imetupiliwa mbali baada ya Mahakama kukubaliana na hoja za mapingamizi ya TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao ndio waliokuwa wadaiwa katika kesi hiyo.

Hoja hizo ambao Mahakama imekubaliana nazo ni pamoja na kwamba mdai hakuwa na mamlaka kisheria kufungua kesi hiyo na kwamba hati yake ya kiapo kilichokuwa kikiunga mkono madai yake ilikuwa na kasoro za kisheria.

Uamuzi huo umesomwa na Jaji Ignasi Kitusi kwa niaba ya jopo la majaji watatu waliokuwa wakisikiliza kesi hiyo. Majaji wengine walikuwa ni Rose Teemba(kiongozi wa jopo) na Beatrice Mutungi.

Rais Magufuli atembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Dodoma na kufyatua matofali

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 16 Machi, 2017 ametembelea eneo la ujenzi wa Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma na kuwahakikishia wananchi kuwaatahamia Dodoma hivi karibuni kama alivyoahidi.

Mhe. Rais Magufuli ambaye ameongozana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenister Joakim Mhagama na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amesema pamoja na majengo ya Ikulu Serikali itajenga miundombinu mingine zikiwemo reli na barabara za lami zitakazounganisha maeneo ya vijiji vinavyozunguka Ikulu na mji wa Serikali.

Pia Mhe. Dkt. Magufuli amewahakikishia wananchi kuwa wote watakaoguswa na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya Serikali na wanaostahili kulipwa fidia watalipwa, na ametoa wito kwa wananchi hao kutumia fedha za fidia watakazolipwa kujenga makazi bora na kujipanga kufanya shughuli zenye manufaa kwao.

“Hapa sasa watakuja watu wengi, wafanyakazi na wageni maana tayari Mabalozi wa nchi mbalimbali nao watajenga ofisi zao hapa, sasa na nyinyi mjipange kufanya biashara, mtapata soko la kuuza mazao na bidhaa nyingine, mkipata fedha ziwasaidie kwa manufaa na sio kuzichezea” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Kwa upande wake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa amesema utekelezaji wa Serikali kuhamia Dodoma unakwenda vizuri ambapo mpaka sasa viongozi wakuu wa wizara zote na wafanyakazi 2,069 wameshahamia Dodoma na wengine wanaendelea kuhamia Dodoma.

Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa atasimamia utekelezaji wa maagizo ya Mhe. Rais Magufuli aliyeagiza kujengwa kwa reli itakayounganisha eneo la Bwigili na Dodoma mjini ili kurahisisha usafiri wa watu pamoja na kuharakisha ujenzi wa barabara za kuzunguka mji wa Dodoma na barabara za kuunganisha mji wa Serikali na Dodoma Mjini.

Wakiwa katika eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli na Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa wameshiriki ufyatuaji wa matofali yatakayotumia katika ujenzi wa majengo ya Ikulu.

Mapema kabla ya kutembelea eneo hilo, Mhe. Rais Magufuli amepokea taarifa ya mapendekezo ya ujenzi wa Mji wa Serikali wa Makao Makuu Dodoma kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Mhandisi Paskasi Muragili na kuagiza ujenzi wa Mji huo uzingatie maslai ya Taifa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chamwino

16 Machi, 2017

Meya wa Ubungo kufungua kesi ya jinai dhidi ya RC Makonda kwa kuwa na Vyeti FEKI

$
0
0
Meya wa Ubungo, Boniphace Jacob amesema Jumanne wiki ijayo atafungua kesi ya jinai dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutokana na madai ya kuwa na vyeti feki.
 
Jacob pia amesema, atamshtaki Makonda katika sekretarieti ya maadili ya utumishi wa umma, tume ya haki za binadamu pamoja na utawala bora.
 
Jacob ameeleza kuwa kesi hiyo itasimamiwa na mawakili maarufu Tundu Lissu ambaye ni Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA na Peter Kibatala..

Kesi hiyo itafunguliwa wiki ijayo baada mawakili hao kumaliza mchakato wa uchaguzi wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Machi 18 mwaka huu ambapo Tundu Lissu ni mmoja wa wagombea wa kiti cha urais


Rais Magufuli amtumbua Vita Kawawa na kuvunja Bodi ya Tumbaku Tanzania.....Waziri Mkuu Kaagiza viongozi wa 'WETCU' Wakamatwe Haraka

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa  Tabora kuwakamata viongozi wanne wa Chama Kikuu cha Ushirika wa Tumbaku (WETCU) pamoja na kufunga ofisi za chama hicho kupisha uchunguzi wa tuhuma za ubadhirifu.

Pia Waziri Mkuu amevunja Bodi ya WETCU pamoja na  Bodi ya Tumbaku Tanzania  - TTB kwa sababu ya kushindwa  kusimamia zao hilo pamoja na matumizi mabaya ya fedha za umma.

Waziri Mkuu ametoa maagizo hayo leo jioni katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Isike Mwanakiyungi mkoani Tabora, ambapo amesema Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa TTB, Bw. Vita Kawawa pamoja na Mtendaji Mkuu wa Bodi hiyo Bw. Wilfred Mushi.

Viongozi wa WETCU ambao Waziri Mkuu ameagiza wakamatwe ni Mwenyekiti Bw. Mkandara Mkandara, Makamu Mwenyekiti Bw. Msafiri Kassim, Mkaguzi wa Ndani na Mhasibu  Mkuu. Pia amewasimamisha kazi watumishi wa kitengo cha uhasibu wa chama hicho hadi uchunguzi utakapokamilika.

“Kuanzia sasa watumishi wote wa kitengo cha uhasibu pamoja menejimenti nimewasimamisha kazi pamoja na Mrajisi wa mkoa wa Tabora Deogratius Rugangila. Kamanda hakikisha ofisi hazifunguliwi kuanzia sasa hadi hapo timu ya ukaguzi  itakapokamilisha kazi yake,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesema kwa muda mrefu wakulima wameteseka na zao hilo kukosa tija kwa sababu ya usimamizi mbovu wa viongozi wa ushirika na Bodi ya Tumbaku Tanzania jambo ambalo Serikali haiwezi kulivumilia.

Amesema“Hatuwezi kuwa na ushirika ambao hauwasaidii wanachama. WETCU walipokea sh. bilioni 15 ambazo walizikatia risiti na hazijaonekana. Pia waliwalipa wazabuni sh, bilioni 10 ambazo hawajazikatia risiti,”.

“Wakati wanachama ambao ni wakulima wakiendelea kutesema WETCU walinunua gari la sh. milioni 269 kinyume na maelekezo ya Mkutano Mkuu wa wadau ambao ulipitisha zitumike Shilingi milioni 40 tu,” amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa chama hicho kimesababisha kupungua kwa uzalishaji kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na menejimemti mbovu jambo ambalo limechangia wakulima wa tumbaku kukosa tija.

Amesema WETCU kimekithiri kwa matumizi mabaya ya fedha ambapo alitolea mfano suala la ukarabati wa ofisi tatu ikiwemo ya makao makuu ambayo ilipangwa ikarabatiwe kwa sh. milioni 33 wakatumia sh. milioni 170 na ofisi za Tabora na Urambo zilipangiwa sh. milioni tano kila moja na hazikukarabatiwa.

Pia Waziri Mkuu amepiga marufuku ununuzi wa mbolea kutoka nje ya nchi wakati ikiwa inazalishwa hapa nchini.

Aidha, alimepiga marufuku matumizi ya kwa dola katika sekta ya tumbaku na badala yake zitumike fedha ya Kitanzania kwa sababu kitendo hicho kimekuwa kiwanyonya wakulima.

Serikali yapiga marufuku kufunga ndoa bila cheti cha kuzaliwa

$
0
0
Serikali  imepiga marufuku watu kufunga ndoa bila kuwa na cheti cha kuzaliwa kuanzia Mei Mosi, mwaka huu.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo leo akiwa katika ziara yake mkoani Morogoro na kuongeza kuwa serikali imeamua kufanya hivyo ili kupata takwimu sahihi za wananchi wake zitakazosaidia kupanga mipango ya kimaendeleo sanjari na kuzuia wageni kuingia kinyemela nchini.

Pamoja na mambo mengine, Dk.Mwakyembe amewataka Wakala wa Usajili wa vizazi na Vifo (RITA), kuhakikisha inasimamia sheria ya usajili ambapo amesema kuwa bila kuwa na  takwimu sahihi  za  vizazi na vifo ama ndoa  inasababisha nchi kushindwa kusonga mbele kimaendeleo.

“Wenzetu nchi zilizoendelea suala la usajili wamelipa kipaumbele lakini sisi bado tuko nyuma, kwa mfano Mkoa wa Morogoro  kwa mujibu wa sensa  ya watu na makazi ya mwaka 2012, inaonyesha kuna jumla ya wakazi milioni 2.2, lakini waliosajiliwa na kuwa na vyeti  vya kuzaliwa ni asilimia 11 pekee huku wengine wakiwa bado hawasajiliwa,” amesema.

Dk. Mwakyembe pia ametumia nafasi hiyo kuwaonya watendaji wa mahakama watakaolalamikiwa na wananchi kufanya kazi kinyume na maadili ikiwamo upokeaji wa rushwa ama kutotenda haki na kutumia  mahakama kugeuza kesi za madai kuwa kesi za jinai.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 17

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL   BEAUTY COSMETICS

Ni kampuni inayotoa bidhaa original na zenye matokeo mazuri bila madhara wala kemiko ya aina yoyote. Bidhaa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda. Tunawaletea punguzo la bei la %10 bidhaa tulizonazo ni kama zifuatazo.
 
     👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 170,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 100,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 110,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @100,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @100,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima kwa vidonge au dawa ya kunywa @150,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11 Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo la ndoa @120,000
12.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
13. kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @100,000/=
15. Kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake @100,000/= NK. [ Bidhaa zetu zote ni garantii pia hakikisha unapewa risiti ununuapo bidhaa kampuni hii popote ulipo utapata huduma zetu]
 
     WASILIANA NASI KWA NAMBA
        {065 9618585 au 0759029968.}
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
                               Karibu sana

Taarifa kutoka Ofisi ya Bunge la Tanzania kuhusu uchaguzi wa Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EAC).

$
0
0
Uchaguzi wa Wajumbe Tisa (9) watakaoiwakilisha Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA) unatarajiwa kufanyika katika Mkutano wa Saba wa Bunge unaotarajiwa kuanza  Aprili 4 mwaka huu.

Uchaguzi huo utakaofanyika Dodoma, utazingatia maisha  ya bunge hilo lililoingia madarakani mwaka 2012 ambalo litafikia ukomo wake Juni 4 mwaka huu.

Taarifa iliyoletwa kwa vyombo vya habari na Kitengo cha Bunge cha Habari, Elimu na Mawasiliano imeeleza kuwa uchaguzi huo utasimamiwa na Katibu wa Bunge ambaye atatoa tangazo kwenye gazeti la serikali la leo.

“Katibu wa Bunge atatoa tangazo kwenye Gazeti la Serikali kesho( leo ) tarehe 17 Machi, 2017 linaloainisha siku ya uteuzi wa wagombea kuwa tarehe 30 Machi, 2017 saa kumi kamili jioni na siku ya uchaguzi kuwa ni tarehe 4 Aprili, 2017 mara baada ya kipindi cha maswali na majibu Bungeni.” Ilisema taarifa hiyo

Katika taarifa hiyo, msimamizi wa uchaguzi alitoa wito kwa Watanzania wenye sifa za kugombea na kuchaguliwa wajitokeze.
==
 
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images