Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli Afanya Mazungumzo Na Rais Wa Zanzibar Dkt. Shein, Mjini Dodoma Leo

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Machi 2017, amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.

Dkt. Magufuli amesema katika mazungumzo yao wamezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kumtakia heri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia leo kuwa siku yake ya kuzaliwa.

Kwa upande wake Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kumtakia heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.

''Siku ya kuzaliwa ni siku ya furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana  na leo nimefurahi sana'' amesema Dkt. Shein.

Dkt.Shein amesema ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli ili waweze kubadulishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma

13 Machi, 2017

Makonda azindua barabara Jijini Dar es Salaam Leo

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema jiji la Dar es Salaam linatakiwa kubadilika  katika kufikia viwango vya majiji ya kimataifa.

Makonda ameyasema hayo leo wakati akikabidhiwa barabara ya kurasini iliyojengwa kwa zege yenye urefu wa Kilomita moja, amesema  barabara hiyo ndio kiungo kikubwa kwa upande wa bandari.

Mwaka jana RC Makonda katika harakati za kutatua kero za wananchi alipewa kero ya barabara hiyo na yeye kuikabidhi kwa kampuni ya ukandarasi Grant Tech Company ambayo ilijitolea kuikarabati barabara hiyo kwa kiwango cha zege.
 

Akiongea katika makabidhiano hayo Operation Manager wa kampuni hiyo, Bw. Maswingo alisema anayofuraha kumkabidhi mkuu wa mkoa barabara hiyo ya kimometa 1 ambayo inaonganisha katika ya Kurasini na Kilwa Road ikiwa imejengwa kwa kiwango cha hali ya juu kutokana na aina ya magari ambayo yanatumia barabara hiyo.
 

“Hii barabara aliizindua mkuu wa mkoa mwaka jana mwezi 12 na sasa hivi tunamkabidhi ikiwa imekamilika. Barabara hii ni kiungo muhimu katika eneo hili bila shaka itachangia kuchochote maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa ni barabara hii ni kiungo muhimu,” alisema Mwaswingo.
 

Kwa pande wa mkuu wa mkoa Dar es salaam, Paul Makonda alisema barabara hiyo itakuwa chachu ya maendeleo kwa mkoa wa Dar es salaam kwa kuwa itawarahishia wafanyabiashara kutoa mizigo yao bandarini kwa urahisi.

Mkuu wa Mkoa ametoa onyo kwa kampuni za ukandarasi zinazofanya shughuli zao hapa jijini chini ya viwango ya kuwa  kuanzia sasa kampuni hizo pale zitakapotambuliwa zitatakiwa kurudia miradi hiyo kwa gharama zao binafsi na kupewa adhabu ya kufungiwa kandarasi yoyote hapa jijini  kwa miaka mitatu.

"Wananchi wamechoka kutengeneza magari kila mara kutokana na ubovu wa barabara, wakina mama wamekuwa wakijifungulia barabarani hasa nyakati za mvua kama hizi kutokana na ubovu wa barabara zilizojengwa hata miezi sita haijapita" amesema Makonda .

Makonda amesema miundombinu ya barabara ni moja ya nyenzo ya ukuaji wa kiuchumi kwa taifa lolote lile. Makonda ameelekeza manispaa zote zisimamie vyema fedha za barabara ili kupunguza adha za usafiri kwa  wananchi wa Dar es salaam ambao wamechoka kupita kwenye barabara zenye mashimo zinazoleta hitilafu hata kwa vyombo vyao vya usafiri.

Makonda amemshukuru mkandarasi huyo kwa uzalendo wake na kujitoa kwake kuijenga Dar es salaam kwani kwa kufanya hivyo ni  ndoto ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ya kukuza uchumi na kufikia Tanzania ya viwanda  inaendelea kutimia.

Picha 10 za Muonekano wa Jiji la Dar Baada ya Mvua Kubwa Kunyesha

Taarifa ya TANESCO kuhusu mvuaKubwa zinazonyesha Dar es Salaam

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya March 14

Vanessa Mdee Kaachiwa Kwa Dhamana

0
0
Mwanamuziki Vanessa Mdee maarufu Vee Money ameachiwa kwa dhamana na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam baada ya kuwa ameshikiliwa kwa takribani wiki moja kufuatia tuhuma ya dawa za kulevya inayomkabili.

Mdee aliachiwa jana jioni ambapo anatuhumiwa kutumia na kusambaza dawa za kulevya. Alishikiliwa na Polisi tangu juma lililopita baada ya kwenda kuripoti kufuatia kutajwa kwenye orodha ya watuhumiwa wa dawa hizo iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Slaam, Paul Makonda.

TPDC, Dangote wakubaliana mauzo ya gesi asilia

0
0
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limefikia makubaliano na Kampuni ya Dangote Group of Industries kuhusu bei ya mauzo ya gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya kiwanda chake cha saruji kilichopo mkoani Mtwara.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar  jana, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Kapulya Musomba alisema makubaliano hayo yanahusu kuunganisha miundombinu ya kusafirisha gesi asilia kutoka kwenye bomba kubwa kwenda kiwandani hapo na kukamilisha mkataba wa awali kwa ajili ya mauzo ya gesi kwa matumizi ya kiwanda hicho. 

Alisema makubaliano hayo ni utekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli. Desemba mwaka jana, Rais Magufuli alipokutana na mmiliki wa kiwanda hicho, Aliko Dangote jijini hapa alimtaka kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC badala ya kutumia watu wa kati wenye nia ya kutengeneza faida binafsi. 

Mwakilishi wa Kampuni ya Dangote, Sada Ladan-Baki alisema gharama za kuunganisha bomba hadi kiwandani zitabebwa na kampuni hiyo na siyo Serikali ya Tanzania. 

“Tutagharamia ujenzi wa bomba, mwanzo hadi mwisho na tutaanza ujenzi mwezi ujao,’’ alisema. 

Alimshukuru Rais Magufuli kwa kuwaruhusu kununua gesi nchini akisema hatua hiyo itatoa ajira kwa Watanzania wengi. 

Wafanyakazi 9 wa TBC wasimamishwa kazi kwa kutangaza habari ya uongo kuhusu Rais Magufuli

0
0
Wafanyakazi tisa wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) wamechukuliwa hatua za kinidhamu kufuatia kurusha habari ya uongo kuhusu Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Wafanyakazi hao wamesimamishwa kazi kufuatia kurusha taarifa ya uongo kutoka tovuti ya fox-channel.com ambayo ilidai kuwa Rais wa Marekani, Donald Trump  amempongeza Rais Dkt John Pombe Magufuli kwa utendaji wake mkubwa na vita dhidi ya dawa za kulevya. Tovuti halali ya Fox ni foxnews.com na si hiyo iliyonukuliwa na TBC.

Mkurugenzi wa TBC, Dk. Ayoub Riyoba amethibitisha kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa wafanyakazi hao kufuatia kosa hilo walilolifanya.

“Ni kweli watu kadhaa wamesimamishwa kazi kutokana na suala hilo.”

Wafanyakazi tisa waliosimamishwa ni pamoja na Elizabeth Mramba, Gabriel Zacharia, Prudence Constantine, Dorothy Mmari, Ramadhani Mpenda, Leya Mushi, Alpha Wawa, Chunga Ruza na Judica Losai.

==>Hii ndo taarifa ya uongo iliyosomwa TBC.

Mahakama Yampa ONYO Halima Mdee

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemwonya na kumwambia Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), kwamba kadi za onyo kwa ajili yake zimeisha kutokana na kushindwa kuhudhuria mahakamani siku ya kesi.

Kauli hiyo ilitolewa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya kubaini kwamba ilitolewa hati ya kumkamata mbunge huyo kwa kushindwa kufika mahakamani.

Halima Mdee alipotakiwa kujitetea aliinuka na kujieleza kuwa amefika mahakamani hapo akiwa na nyaraka za safari ikiwamo tiketi na VISA na kwamba taarifa za safari alimpa wakili.

Kwa upande wa wakili wao, Hekima Mwesiga aliieleza mahakama kuwa nyaraka za kuiarifu mahakama juu ya safari ya Halima Mdee nje ya nchi kwa bahati mbaya hakuziwasilisha, alikuwa nazo Peter Kibatala ambaye alikuwa akiendesha kesi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

“Tutaonana wabaya katika hili ni lazima unapofanya kitu adabu yake ifuatwe, Wakili hakufuata taratibu na Halima kabla ya kusafiri ulipaswa kutoa taarifa mahakamani ili uweze kupata ruhusa ya mahakama lakini haukufanya hivyo.

“Sasa nafikiri wote tufuate taratibu za kuhudhuria mahakamani, Halima Mdee kadi zako  za kukuonya zimeisha tafadhali,”alisema Hakimu.

Mdee na wabunge wengine wa Chadema, Mwita  Waitara, Saed Kubenea  na makada wao wanatuhumiwa kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Theresa Mmbando.

Kabla ya onyo hilo, mahakama ilisikiliza ushahidi wa upande wa mashtaka uliotolewa na Mrakibu wa Polisi, ambaye pia ni Msaidizi wa Operesheni Ilala, Eugen Mwampondele.

Mwampondele alidai siku ya tukio alimwona Rafii Juma na Halima Mdee wakimkunja Theresa Mmbando ili awape nyaraka.

Shahidi huyo alidai waliompiga Mmbando hawapo mahakamani. Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mbunge wa Jimbo la Ubungo, Saed Kubenea, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema (56), Halima Mdee (37) na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (40).

Wengine ni mfanyabiashara na kada wa chama hicho, Rafii Juma (21)pamoja na Diwani wa Kata ya Saranga, Ephreim Kinyafu (33).

Inadiwa kuwa Februari 27, 2016 katika Ukumbi wa Karimjee Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam watu hao walimjeruhi Theresia na kumsababishia majeraha mwilini wakati wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Aondolewa na Kurejeshwa Jeshini

0
0
Aliyekuwa  Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi, ameondolewa katika wadhifa huo na kurejeshwa jeshini.

Akithibitisha habari hizi, Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu (DAS), Titus Mughuha, amesema Kanali Mkisi alitoa taarifa za uhamisho huo katika kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama na kusema kuwa, anarejea makao makuu ya jeshi alikokuwa awali kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.

‘Ni kweli Kanali Martin Mkisi amepata barua ya kurudi makao makuu ya jeshi, uhamisho huo ni wa kawaida na haupaswi kuhusishwa na uzushi ama sababu zozote,” alisema Mughuha.

Kutokana na mabadiliko hayo, Mkuu wa Wilaya ya  Buhigwe mkoani humo, Kanali Marko Gaguti, atakaimu nafasi hiyo hadi uteuzi mwingine utakapofanyika kujaza nafasi hiyo.

Kanali Martin Mkisi amedumu katika nafasi hiyo kwa kipindi cha miezi tisa, akitokea makao makuu ya Jeshi la Wananchi (JWTZ), kutokana na uteuzi wa Rais, Dk. John Magufuli kwa wakuu wa wilaya 139 alioufanya Juni, mwaka jana.

Credit: Mtanzania

Dr. Makongoro Mahanga Atoweka.....Polisi Waendelea Kumsaka

0
0
Aliyekuwa  Naibu Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Dk. Makongoro Mahanga, anayesakwa na Jeshi la Polisi ametoweka nyumbani kwake.

Mahanga anasakwa na polisi kutokana na amri ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, iliyoamuru akamatwe kwa kushindwa kumlipa Kainerugaba Msemakweli zaidi ya Sh milioni 11 za kesi ya madai aliyomshinda.

Mahakama hiyo ilitoa amri ya kukamatwa Machi 7, mwaka huu na kutoa nyingine mwishoni mwaka wiki ambapo alitakiwa kufikishwa mahakamani jana. Hata hivyo hakupatikana.

“Makongoro Mahanga hajaja mahakamani na nyumbani kwake hayupo, anaendelea kutafutwa,” alisema Msajili wa Wilaya wa Mahakama Kuu, Ruth Masambu.

Hadi jana, Mahakama Kuu ilishatoa hati mbili kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ilala, ikielekeza Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani.

Msemakweli ambaye ni mlalamikaji, alikabidhiwa hati hiyo na kutakiwa kumkabidhi Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni, ili aweze kutekeleza amri hiyo.

Hamduni alikiri kupokea hati hiyo na kusema mdaiwa hajapatikana hivyo wanaendelea kumtafuta.

Dk. Mahanga, anatakiwa kumlipa mwanaharakati huyo baada ya kesi aliyofungua ya kashfa dhidi yake kufutwa mahakamani.

Rais Magufuli amepiga simu Clouds Tv na kuzungumza na mwanamuziki Diamond Platnumz baada kusikia maombi yake

0
0
Mwanamuziki Diamond Platnumz amepata nafasi ya kuzungumza na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kuhusu hali ya wasanii ilivyo nchini na kuomba serikali kuunga mkono juhudi zao ili kulisaidia taifa kuongeza pato na wasanii kupata faida kutokana na kazi wanazozifanya.

Diamond amezungumza na Rais Magufuli kupitia kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa katika kituo cha runinga cha Clouds Tv na kumwambia wamekuwa wakifanya jitihada lakini zaidi wanahitaji msaada wa serikali ili wapate kipato ambacho kinastahili kutokana na kazi wanayoifanya.

“Mkuu tunaomba utusaidie sana maana tunaamini wewe ni Rais ambaye unatetea wanyonge na kusaidia wanyonge na sisi vijana wako kwa unyonge wetu tunaomba utusaidie kwasababu utakuwa umesaidia familia nyingi, sababu tuna familia tuna watoto na watu wengi tunategemea mziki ili tujiajiri na kuliingia pato taifa,

“Nafikiri tuweke system nzuri ya kulipa kodi kama mimi ni mlipa kodi mzuri na wengine nimeweka mfumo wafate hivyohivyo nafikiri itasaidia sana kuliingizia pato taifa na sisi pia atleast kupata riziki na kujenga nchi  yetu,”
alisema Diamond.

Rais Magufuli alimjibu kwa kumpongeza kwa kazi nzuri ambayo wasanii wanaifanya ya kuitangaza Tanzania kimataifa, “Asante sana nimekusikia lakini pia nakupongeza na uzidi kuitangaza Tanzania katika muziki na hata wasanii wengine hata wale wanaoigiza nawapenda kama shilawadu na kadhalika.”

Lakini awali akizungumza na mtangazaji wa kipindi hicho Babbie Kabae alisema kuwa amepanga kukutana na wasanii ili kusikiliza changamoto zinazowakabili, “Maombi yake nimeyasikia nimepanga siku moja kukutana na hao wasanii ili tuone jinsi gani tunawasadia.”


==>Tazama Video hapo chini

Waziri Nape Atishia Kuwatumbua maafisa habari wa serikali

0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amemtaka Mkurugenzi wa Habari maelezo kufuatilia utendaji kazi wa maafisa habari na mawasiano wote ili kuona utendaji kazi wao kama unaleta maendeleo kwa jamii.

Waziri huyo ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumza na maafisa habari na mawasiliano wakati akifungua kikao kazi cha 12 cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina ndogo Mkoani Dodoma.

Amesema kuwa wao ndiyo chanzo cha kuwafanya viongozi wao kukimbia vyombo vya habari kutokana na maafisa hao kushindwa kuwaandaa vyema badala ya kutoa habari zinazotakiwa kwa jamii.

Amesema kuwa maafisa habari na viongozi wa umma nchini wanapaswa kutekeleza sheria hasa zinazowataka kutoa habari na taarifa kwa kuhakikisha vyombo vya habari na wananchi wanapata habari kwa wakati bila urasimu.

“Nataka niiagize ofisi ya mkurugenzi wa habari maelezo kuhakikisha kuwa mnafuatilia utendaji kazi wa kila afisa habari na mawasiliano ili kujiridhisha kama wanafanya kazi zao kwa mujibu wa sheria au la na kama tutabaini kuna afisa habari ambaye hatekelezi majukumu yake ipasavyo tumuombe atupishe”. Alisema Nape

Aidha Waziri huyo aliwasisitizia maafisa hao kutoa ushirikiano mzuri kwa waandishi wa habari pindi wanapofika katika ofisi zao kuwapa taarifa sahihi na kwa wakati ili jamii iweze kupata ufumbuzi ya matatizo yao.

Kauli ya Profesa Jay kuhusu wasanii walioenda jimboni kupinga Ubunge wake

0
0

Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia CHADEMA ambaye pia ni msanii wa 'hip hop', Joseph Haule (Profesa Jay) amesema hana kinyongo na wasanii  wote waliokwenda jimboni kwake kipindi cha uchaguzi oktoba 25, 2015 kwa ajili ya kumpinga.

Msanii huyo kupitia ukurasa wake wa kijamii instagram ameandika maneno machache yanawagusa moja kwa moja wasanii wenzake waliokuwa nje ya chama hicho kuwa amewasamehe ila amewataka wajiongeze kwa maana sanaa inahitaji umoja.

"Nilishawasemehe wasanii wenzangu waliokuja jimboni kupinga Ubunge wangu mabasi kwa mabasi,  jiongezeni wanangu. Asante wana Mikumi kwa kuwa na imani kwangu, sanaa yataka umoja nitakubeba ukianguka". Ameandika Profesa Jay

Kwa upande mwingine msanii huyo amewataka mashabiki na wapenzi wa muziki wake wakae tayari kupokea mzigo mpya siku ya kesho Jumatano unaotarajiwa kupewa jina la 'kibabe'.

Mafuriko Yaua Mtu Mmoja Jijini Dar es Salaam......Jeshi la Polisi Latoa Tahadhari

0
0
Na Regina Mkonde
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam jumanne ya Machi 13, 2017 katika eneo la Mongo la Ndege, limeokota mwili wa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Imelda Ngonyani (13) aliyekufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Msimbazi.

Akizungumza na waandishi wa habari Machi 14, 2017, Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro amesema marehemu huyo kabla ya kufa maji alikuwa pamoja na wenzake watano walionusurika kifo wakielekea shule ya Msingi ya Mongo la Ndege.

“Mwanafunzi huyo alikufa maji wakati akijaribu kuvuka mto Msimbazi akiwa na wenzake ambao walinusurika kifo wakiwa njiani kuelekea shule ya Mongo la Ndege,” amesema.

Sirro ametoa wito kwa wananchi kuwa makini katika kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha, na kuwataka wananchi wanaoishi karibu na mto msimbazi kuondoka kwa hiari ili kujiepusha na athari za mafuriko.

Katika hatua nyingine, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi mnamo Machi 12, 2017 maeneo ya Zimbwini kata ya Vijibweni Manispaa ya Kigamboni lilifanikiwa kukamata watuhumiwa wawili wenye umri kati ya 25 hadi 30 wakiwa na bastola moja aina ya Bereta yenye risasi sita ndani ya magazini.

“Majambazi hao walijeruhiwa vibaya ndipo wakakimbizwa hospitali ya vijibweni, walipofikishwa hospitalini hapo walibainika kuwa wamefariki dunia wakiwa njiani. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa silaha hiyo iliyokamatwa ni mali ya Pato Sixtus Nyagali mkazi wa Kijichi, upelelezi unaendelea kufanyika ili kumpata mmiliki huyo na kuhakikisha mtandao wote wa uhalifu unafikishwa katika mkono wa sheria,” amesema. 

Sambamba na hilo, Sirro amesema Kikosi cha Polisi Usalama Barabarani cha kanda hiyo, kimekusanya 319,350,000 za faini kwa ajili ya makosa mbalimbali ya barabara kuanzia Machi 10 hadi 13, 2017.



Habari Zilizopo Katika Magazeti ya leo Jumatano ya March 15

Ridhiwani Kikwete ahojiwa kwa tuhuma za dawa za kulevya

0
0
Mbunge wa Chalinze Mkoa wa Pwani, Ridhiwani Kikwete amehojiwa kwa muda wa saa tatu na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya.

Ridhiwani Kikwete alitajwa katika orodha ya majina 97 ambayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliyakabidhi wa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga.

Kiongozi huyo alihojiwa Jumatatu Machi 6, 2017 ambapo alifika katika ofisi hiyo majira ya 5:09 asubuhi akiwa amefuatana na watu wengine watatu.

Ridhiwani Kikwete baada ya kufika ofisini hapo alipelekwa kwenye chumba maalumu cha mahojiano ambapo alihojiwa kwa saa tatu ambapo inaelezwa kuwa alibainika kuwa si muuzaji wala mtumiaji wa dawa hizo, lakini tatizo ni rafiki zake ambao yupo karibu nao.

Katika taarifa yake aliyoitoa Jumanne hii, Ridhiwani amesema ameshukuru kuona haki imetendeka katika sakata hilo lililokuwa likimkabili.

“Ni kweli niliitwa na kuhojiwa. Serikali yangu chini ya Kamisheni ya Madawa ya kulevya inasimamia haki na nimeona ikitendeka. Niko huru toka kwenye tuhuma/kashfa,” Ridhiwani aliandika Instagram na kuongeza.

“Tuunge mkono juhudi hizi. Tuunge mkono hatua zinazochukuliwa ili kuokoa vijana wetu na kulinda nguvu kazi ya Taifa #vitadhidiyaMadawa #magufulinikazitu #tanzaniakwanza #miminikazitu #chalinzenikazitu,” 

Yusuf Manji Mahakamani Tena Kesho

0
0
Kesi inayomhusu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ya juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine, inatarajiwa kusikilizwa tena kesho Alhamisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuahirishwa kwa mara ya mwisho Februari 16, mwaka huu.
 
Manji anatuhumiwa kutumia madawa hayo kinyume na sheria ya mwaka 2015 ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) namba 5 ambapo inadaiwa Manji alitumia dawa hizo Februari 6 na 9, mwaka huu.
 
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Osward Tibaloyekomya huku upande wa Manji ukiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa.
 
Baada ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kesi hiyo, Manji alikataa mashtaka hayo na kuachiwa nje kwa dhamana ya milioni 10 iliyotolewa na Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa.
 
Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kusikilizwa kwa kesi hiyo bila ya Manji kuwepo kutokana na kuumwa kwani kwa sasa amelazwa kwenye Hospitali ya Aga Khan ambapo anasumbuliwa na tatizo la moyo.

Ratiba ya Uchaguzi Mkuu wa CCM Mwaka 2017

Sophia Simba: Sina Mpango wa Kuiunga na Chama Chochote cha Upinzani

0
0
Aliyekuwa mwanachama mkongwe wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Sophia Simba ambaye alifukuzwa uanachama kwa usaliti, amezungumzia hatua aliyoichukua baada ya uamuzi huo dhidi yake.

Wikendi iliyopita, CCM ilitangaza kumvua uanachama Mwanasiasa huyo baada ya kumtia hatiani, ambapo taarifa zinadai kuwa yeye alibainika kwenda nyumbani kwa aliyekuwa mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa hata baada ya uchaguzi mkuu akiwa amevalia hijabu kujificha. Hali iliyotafsiriwa kuwa alikuwa akimpelekea siri za chama.

Baada ya uamuzi huo wa CCM kutangazwa, Lowassa alimkaribisha Sophia Simba na wenzake 12 waliofukuzwa, kujiunga na Chadema huku akiwaita mashujaa waliokuwa wanatetea demokrasia ndani ya chama hicho tawala.

Hata hivyo, Sophia Simba amesema kuwa hana mpango na hatahamia katika chama chochote kwani maisha yake yote yametokana na kuitumikia CCM. 

Mwanasiasa huyo ambaye alijiunga na CCM tangu ilipozaliwa mwaka 1977 na kushika nyadhifa mbalimbali baadae, amesema kuwa atabaki kuwa mkereketwa wa chama hicho.

“Napenda kuwaeleza Watanzania wote, wafahamu kuwa sina mpango wowote wa kujiunga na upinzani. Na unajua CCM ina makundi mawili, la kwanza ni wanachama wenye kadi na la pili wakereketwa ambao ni wengi. Na mimi nitaingia katika kundi hilo na sio kuhama,” Sophia Simba anakaririwa na Mtanzania.

Aidha, alikanusha taarifa zilizokuwa zimeripotiwa kwenye baadhi ya mitandao kuwa amekutana na mwanasiasa mmoja wa upinzani. Alisisitiza kuwa hakufanya hivyo na hana mpango huo.

Akizungumzia tuhuma za kukisaliti chama hicho zilizopelekea kung’olewa kwake, alikana kuwa msaliti wa chama hicho ingawa alisisitiza kuwa hataki kulizungumzia kwa undani bali anamuachia Mungu anayeiona nafsi yake.

“Sitaki kuzungumzia kwa udani suala la usaliti ila kwa ufupi, Mungu anaishuhudia nafsi yangu. Jamani, hivi kweli nikisaliti chama changu ambacho kimenilea katika maisha yangu yote!”

Katika hatua nyingine, alisema kuwa hana mpango wa kwenda mahakamani kutafuta haki ya kurejea ndani ya chama hicho kwani kufanya hivyo ni kukosa fadhila kwa jinsi ambavyo chama hicho kimempa maisha. 

Mwanasiasa huyo mkongwe alisema kuwa amepokea adhabu aliyopewa kwa mikono miwili na kwamba hana kinyongo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images