Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mdogo wake Askofu Gwajima aibuka na kumshambulia kaka yake kwa kutaka vyeti vya Makonda

$
0
0
Baada ya Askofu Josephat Gwajima kutumia zaidi ya wiki tatu kuzungumzia suala la dawa za kulevya na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa ametumia cheti cha mtu, ndugu yake kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kumshambulia akimtaka aache mamlaka husika zifanye kazi yake.

Mwanasheria Methusela Gwajima ambaye ni mdogo wake Askofu Gwajima akizungumza na waandishi wa habari leo amehoji, kwanini suala la elimu ya Makonda limeibuliwa wakati huu ambapo amevalia njuga suala la vita dhidi ya dawa za kulevya. 

"Watu hawa wanaozungumzia elimu ya Makonda walikuwa wapi? Tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hawakusema chochote ila amegusa dawa za kulevya ndio wameibuka na kuanza kumshambulia?"

Methusela amesema hamaanishi kuwa mabaya  ya Makonda yasinguzumzwe, lakini kwanini yamekuja wakati huu?

"Kwanini wanataka kutuhamisha kwenye ajenda yetu iliyopo mezani?. Yani sasa Watanzania tumehamishwa tukaacha kujadili suala la dawa za kulevya na kwenda kujadili cheti cha mtu. amesema Methusela.

Mwanasheria huyo ametahadharisha kuwa kama vita hii dhidi ya dawa za kulevya itashindwa, huenda asiibuke mtu mwingine mwenye ujasiri kama Makonda kwa sababu kila mmoja atakuwa anahofia kufanyiwa kama alivyofanyiwa Makonda. Na haya yatakapotokea basi wahusika wa biashara ya dawa za kulevya ndio watakuwa wameshinda.

Wakati huo huo, amemshambulia kaka yake kwa kugeuza suala la dawa za kulevya na elimu ya makonda kuwa sehemu ya mahubiri kanisani kwake.

“Wewe umeshatuhumiwa, umeitwa Polisi, hivi kwanini usisubiri uchunguzwe? Kama wewe huhusiki si utaambiwa basi. Wameitwa watu wengi, wameitikia wito, kwanini sasa yeye amegeuza kuwa ajenda? Mbaya zaidi imekuwa ni ajenda kanisani. Kwa hiyo kanisa limegeuzwa kuwa kijiwe cha siasa na watanzania wamekaa kimya hawasemi,” alieleza Methusela

"Kama Gwajima anadhani kuwa ameonewa aende mahakamani badala ya kukaa na kulalamika. Kwanini basi anakwepa mahakama na kufanya kanisa ndio sehemu ya kuzungumzia, kila Jumapili ni Makonda, Makonda, Makonda, vyeti, vyeti"  amehoji Methusela.

Mwanasheria Methusela amesema ni lazima watanzania wajiulize ni kundi gani lililopo nyuma ya Askofu Gwajima ambalo ndilo linamsukuma kuendelea kumshambulia Mkuu wa Mkoa na kusababisha kuachwa kwa ajenda ya msingi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aisifu Tanzania

$
0
0
Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres ameisifu Serikali ya Tanzania kwa jitihada zake za kutafuta amani nchini Burundi.

Guterres alitoa pongezi hizo wakati aliposimama kwa muda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wa jijini Dar es Salaam akitokea Kenya.

Katibu Mkuu huyo mpya wa UN alisimama kwa ajili ya kufanya mazunguzmo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga.

Pamoja na mambo mengine Guterres alitumia fursa hiyo kutoa pongezi kwa serikali kwa juhudi zake za kutafuta amani nchini Burundi kupitia kwa Msuluhishi wa mgogoro huo, Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa.

“Tanzania imekuwa kinara wa amani Afrika na duniani na naipongeza kwa dhati katika jitihada zake inazozifanya za kutafuta amani ya Burundi na katika nchi nyinge za ukanda huu,” alisema Guterres.

Aidha alisema anatambua mzigo mkubwa inaoupata kama nchi kutokana na kuendelea kupokea wakimbizi kutoka Burundi, na kuahidi UN kuendelea kuunga mkono jitihada za kutafuta suluhu ya kisiasa nchini humo.

Kwa upande wake; Balozi Mahiga aliwasilisha salamu maalum kutoka kwa Rais John Magufuli kuhusiana na hatua iliyofikiwa ya usuluhishi wa mgogoro wa Burundi na ushiriki wa Tanzania katika vikosi vya Umoja wa Mataifa vya ulinzi wa amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Balozi Mahiga pia alisema Tanzania imefurahishwa na ujio wake na Rais amempa mwaliko rasmi wa kufanya ziara nchini.

Aidha alimweleza kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), katika mkutano wao ujao wana mpango wa kuwasilisha hoja maalum kuhusu hali ya kisiasa nchini DRC.

Mbali na kufanya ziara nchini Kenya, Katibu Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa alitembelea Somalia na kukutana na Rais mpya wa nchi hiyo, Hassan Sheikh Mohamud, ambapo aliagiza Jumuiya ya Kimataifa kuchukua hatua kuepusha balaa la njaa nchini humo, kutokana na hali mbaya ya ukame.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya March 10

Hakimu Atishia Kuifuta kesi ya Jamii Forums

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imetishia kuifuta kesi inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa JamiiForums, Maxence Mubyazi Melo na mwanahisa wa kampuni ya Jamii Media Co Ltd, Mike William ikisema haifurahishwi na mwenendo wa shauri hilo. 

Hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo, Thomas Simba alisema hayo jana mara baada ya Wakili wa Serikali, Hamis Said kueleza kuwa wakili anayeendesha kesi hiyo ni mgonjwa na kwamba jana ilikuwa siku ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali. 

“Haya mambo ya kuahirishaa- hirisha kesi siyafurahii. Wakati mwingine (kama) kesi haiendelei, nafuta,” alisema Hakimu Simba baada ya wakili huyo wa Serikali kuomba kesi hiyo iahirishwe hadi Machi 20. 

Hakimu Simba aliiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 3, siku ambayo washtakiwa hao watasomewa maelezo ya awali katika kesi hiyo ambayo washtakiwa wanadaiwa kuzuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi. 

Washtakiwa hao wanaotetewa na mawakili, Tundu Lissu, Jeremiah Mtobesya, Tika Hamis, Hassan Kihangio, Fedrick Kihwelo na Masoud George, watasomewa maelezo hayo ya awali baada ya upande wa mashtaka kukamilisha upelelezi wa kesi hiyo. 

Katika kesi hiyo, namba 456/2017, inadaiwa kuwa kati ya Aprili Mosi na Desemba 13 mwaka jana, wakiwa Mikocheni, wakiwa wakurugenzi wa Jamii Media ambayo inaendesha tovuti ya Jamiiforums walishindwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi ambalo lilikuwa likichunguza mawasiliano ya kimtandao yaliyochapishwa katika tovuti yao. Washtakiwa hao wapo nje kwa dhamana.

TANESCO Yaipa Zanzibar Wakati Mgumu

$
0
0
Hatua ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kutoa siku 14 kwa Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) na taasisi za Serikali kuhakikisha wanalipa madeni yao ya umeme la sivyo watakatiwa umeme, vitaipa wakati mgumu Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). 

Jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanesco, Dk Tito Mwinuka aliwaambia waandishi wa habari kwamba shirika lake linadai wateja hao jumla ya Sh275 bilioni. 

“Tunadai kiasi kikubwa sana cha fedha kutoka kwa wateja wakubwa na wadogowadogo, mpaka Zeco, hivyo tunatoa notisi ya siku 14 kuanzia leo (jana) walipe deni lao kwani baada ya hapo tutasitisha huduma pamoja na kuchukua hatua nyingine za kisheria,” alisema Dk Mwinuka.

 Katika kiasi hicho, Zeco inadaiwa Sh127 bilioni ambacho ni sawa na asilimia 15 ya Bajeti ya Serikali ya Zanzibar kwa mwaka 2016/17 ambayo ni Sh841.5 bilioni. 

Pia kiasi hicho ni kikubwa karibu mara nne ya kile kilichotengwa katika bajeti hiyo kwa ajili ya mikopo ya ndani ambacho ni Sh33.0 bilioni hali inayoonyesha kwamba Zeco na SMZ watalazimika kuandaa mpango mkakati wa kulipa deni hilo ambao utamaanisha kujifunga mkanda ili kulimaliza. 

Alipoulizwa kuhusu notisi hiyo ya kulipa deni, Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira wa Zanzibar, Salama Aboud Talib ambaye alikuwa ziarani Pemba alisema hadi jana hakuwa amepokea barua kutoka Tanesco hivyo asingeweza kuzungumza chochote. 

Wiki iliyopita, akiweka jiwe la msingi katika kituo cha kupoza umeme cha njia ya Kv 132 mkoani Mtwara, Rais John Magufuli aliiagiza Tanesco kuwakatia umeme wadaiwa wote sugu ikiwamo Zanzibar. 

Alisema shirikia hilo halipo kisiasa, hivyo wadaiwa wote wakatiwe umeme. Sambamba na hayo, alilitaka shirika hilo kutoingia mikataba na kampuni zinazoweza kusababisha au kuongeza madeni, badala yake mwekezaji yeyote akitaka kuwekeza azalishe umeme wake na kuuza mwenyewe.

Wadaiwa wengine 
Kuhusu wadaiwa wengine, Dk Mwinuka alisema hadi kufikia Januari, shirika hilo lilikuwa linazidai wizara na taasisi za Serikali kiasi cha Sh52 bilioni huku kampuni binafsi na wateja wadogo wakidaiwa jumla ya Sh94 bilioni. 

Alisema malimbikizo hayo ya madeni yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya shirika kwa wakati ikiwamo uendeshaji, matengenezo ya miundombinu pamoja na miradi mbalimbali. 

Alisema kulipwa kwa malimbikizo hayo ya madeni kutaisaidia Tanesco kujiendesha kiushindani na kwa ufanisi zaidi, hivyo kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme nchini. 

Alipoulizwa kuhusu mashirika na taasisi za umma zinazodaiwa malimbikizo hayo ambayo Tanesco haikuyataja, Msemaji wa Serikali, Dk Hassan Abbas alisema mashirika hayo yanatakiwa kuanza kutekeleza agizo hilo kwa kulipa deni kama wanavyodaiwa.

Rais Magufuli alivyoirudia mistari ya wimbo wa ‘Muziki’ wa Darassa

$
0
0
Rais Magufuli amekuwa akisifika kutokana na utendaji kazi wake lakini pia ni moja kati ya viongozi ambao wanaweza kuongea na wananchi na kuchombeza na maneno ya utani.

Licha ya kuwa Rais Magufuli ni mtu makini na mkali kwa watumishi wasiotekeleza majukumu yao lakini alifurahisha umati wa watanzania alipokuwa akiongea nao na kugusia wimbo wa ‘Muziki‘ wa Darassa katika sehemu ya hotuba zake kwa kunukuu mistarii kadhaa

==>Msikilize hapo chini

Tundu Lissu, Masha wataka kujumuishwa kesi ya Kupinga uchaguzi TLS

$
0
0
Wanasheria wawili wa jijini Dar es Salaam, Tundu Lissu na Lawrence Masha wamesema wataiomba mahakama kuwajumuisha kama wadaiwa katika kesi za kupinga uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) walizodai zimefunguliwa jijini Dar es Salaam na Dodoma. 

Lissu, ambaye ni mbunge wa Iramba na mwanasheria wa Chadema, na Masha (mwanachama wa Chadema na waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani) wamedai kuwa kesi hizo mbili zimefunguliwa Mahakama Kuu na Godfrey Wasonga mjini Dodoma na Onesmo Mpinzile jijini Dar es Salaam, wakitaka uchaguzi huo uzuiliwe.

Mawakili hao wamewahi kupambana katika kesi mbili tofauti zilizohusu vyama vya CCM na Chadema.

Wasonga aliwahi kupambana na Lissu katika kesi iliyofunguliwa na wanachama wawili wa CCM mjini Dodoma waliopinga ushindi wa mbunge huyo wa Singida Mashariki katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010, wakati Mpinzile alipambana na mwanasheria huyo wa Chadema aliyekuwa akimtetea mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali ambaye amehukumiwa miezi sita jela. 

Hata hivyo, Wasonga alisema jana kuwa hajafungua kesi ila anakusudia kufanya hivyo.

Hatua ya Lissu, ambaye ni mwanasheria mkuu wa Chadema, kuchukua fomu ya kuwania urais wa TLS akisema imechagizwa na kauli ya Rais John Magufuli dhidi ya mawakili, ilibadili upepo wa uchaguzi huo na kumlazimu Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe kuuzungumzia akisema Serikali haitavumilia kuona chama hicho kinajiingiza katika siasa.

TLS imekuwa ikafanya uchaguzi kila mwaka, lakini umekuwa hauna harakati kubwa kama ulivyo wa mwaka huu. Tayari TLS imepitisha wagombea urais, wakiwamo Lissu na Masha.

Mbali na kuwa mawakili, Masha na Lissu, ambao wote wanawania urais, ni wanachama wa Chadema, jambo linaloonekana kuchochea mjadala wa siasa kuingia katika chama hicho.

Lakini, mgombea mwingine, Godwin Mussa Mwapongo, pia ni kada wa CCM aliyechukua fomu za kuwania kupitishwa na chama hicho kugombea urais mwaka 2015 ingawa hakufanikiwa. Mgombea mwingine ni Victoria Mandari.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Lissu alisema wamepata wasiwasi kuwa huenda kukawa na njama za washtakiwa katika kesi hiyo, ambao ni TLS na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kutojitetea vya kutosha na hivyo kukubali mashtaka ili uchaguzi huo uzuiwe.

Alisema ili hali hiyo isijitokeze, wataiomba masjala ya Mahakama Kuu iliyopo Dar es Salaam, iwaunganishe katika kesi hizo kama wadaiwa.

“Uchaguzi ukizuiwa, maslahi yetu sisi tunaogombea yatakuwa yamevurugwa kwelikweli. Kwa sababu hiyo na kwa mujibu wa taratibu zinazoruhusiwa kisheria, sisi ambao tunagombea na wapigakura wanaotaka, tutapeleka maombi haraka ili tuunganishwe kwenye kesi zile kama wadaiwa,” alisema Lissu.

“Tutanunua ile kesi, kusije kukawa na njama za uongozi wa sasa wa TLS kuendelea kuongoza baada ya muda wao wa kikatiba kuisha na kusije kukawa na njama ya kuzuia uchaguzi na wale ambao wanataka kuvuruga TLS wakafanikiwa.”

Lissu alisema lengo jingine ni kutaka masuala ya uchaguzi huo yasije yakaamuliwa nyuma ya migongo yao au juu ya vichwa vyao na hivyo wanataka kupata fursa kamili ya kuiambia mahakama kwanini maombi hayo ya kuzuia uchaguzi hayana msingi wowote.

Aliongeza kuwa mawakili hao walioamua kuweka mapingamizi ni wanachama wa TLS na walikuwa na nafasi ya kuweka mapingamizi baada ya kamati ya uteuzi kutangaza majina ya wagombea.

“Kulikuwa na kipindi cha karibu wiki mbili cha kuweka mapingamizi dhidi ya wagombea walioteuliwa, fursa hiyo mwisho wake ilikuwa Machi 15 mwaka huu, lakini hakuna hata mmoja wao aliyeweka mapingamizi hayo. Itabidi tuwahoji,” alisema.

Kwa upande wake, Masha alisema hakuna mtu hata mmoja kati ya wagombea wote wa urais aliyeamua kuingia na kugombea kwa sababu za kisiasa.

Masha alisema licha ya kuwa hana nafasi ya uongozi Chadema, ni mwanachama aliyekuwa wa kwanza kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya urais kabla Lissu hajachukua fomu hiyo.

Alisema kama kungekuwa na mbinu za kisiasa, yeye na Lissu wasingechukua fomu ya kuwania nafasi moja.

“Lissu alikuja kuchukua fomu baada ya muda wa kushiriki katika uchukuaji wa fomu kuongezwa, kama tungekuwa na njama ya kisiasa isingekuwa rahisi kwa Lissu na mimi wote kuchukua fomu kugombea nafasi moja,” alisema waziri huyo wa mambo ya ndani wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Masha alisema chama hicho kinaongozwa kwa mujibu wa sheria na kwamba hakina uhusiano wowote katika masuala ya kisiasa.

Kuhusu matukio yaliyojitokeza Lissu alisema anashangaa kuona Serikali inaingilia suala la uchaguzi wa TLS, akisema hii ni mara ya kwanza tangu kuundwa kwake, zaidi ya miaka 60 iliyopita.

“Ni mara ya kwanza kwa Serikali kuingia moja kwa moja katika suala la nani anapaswa kuwa kiongozi wa chama hiki. Hii haijawahi kutokea tangu TLS ilipoanzishwa 1954,” alisema.

Alisema chama hicho kinaongozwa kwa mujibu wa sheria na kwamba kuwa wanachama au viongozi wa vyama vya siasa, hakuna maana yoyote ile TLS.

“Linapokuja suala la uchaguzi wa TLS nafasi zangu zote nilizonazo hazina maana. Kitu pekee chenye maana ni je wewe ni wakili mwenye sifa zote zinazotakiwa ili kuweza kugombea nafasi unayotaka kugombea katika chama cha mawakili,” alisema Lissu.

“Nadhani Dk Mwakyembe anayafahamu haya, kama atakuwa hayafahamu ni bahati mbaya sana. Wapiga kura ndio waamuzi wa mwisho kwenye uchaguzi huu. Hatutaki baraka za yeyote.”

Jinsi Ya Kuandaa Na Kutayarisha Lishe Maalumu Kwa Wanaume Wenye Tatizo La Ukosefu Na Upungufu Wa Nguvu Za Kiume

$
0
0
 Ukosefu  na/au   upungufu  wa  nguvu  za  kiume  ni  tatizo  linalo wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani. 

Kufahamu  mambo  yanayo  sababisha  tatizo  la  ukosefu/ upungufu  wa  nguvu  za  kiume, dalili  za  mwanaume  mwenye  tatizo  la  ukosefu na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, viashiria  vya  tatizo  la  ukosefu/upungufu  wa  nguvu  za  kiume, athari za  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, tafadhali  tembelea : http://neemaherbalist.blogspot.com/2015/07/uhusiano-kati-ya-damu-na-tatizo-la.html

LISHE  MAALUMU  KWA WANAUME  WENYE  TATIZO  LA  UKOSEFU NA/AMA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME
Hii ni  Tiba-Lishe  maalumu  kwa  wanaume  wenye  kusumbuliwa  na  tatizo  la  ukosefu na  upungufu  wa  nguvu  za kiume. Tiba –lishe  hii  inajumuisha  vyakula,matunda, mimea mbalimbali, pamoja  na  dawa  ya  asili  iitwayo  Jiko.
 
JINSI  YA  KUANDAA  NA  KUTAYARISHA  LISHE  MAALUMU  KWA  WANAUME  WENYE  TATIZO  LA  UKOSEFU NA /AMA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME
 
Mahitaji
1.     Dawa  asilia  ya  Jiko
2.     Juice  ya msafisha  tumbo
3.     Supu  ya  nyanya  chungu
4.     Vitunguu  swaumu/vitunguu maji
5.     Juice  ya  rozera
6.      Vumbi la Kongo ( Congo Dust )
7.     Pink salt   ( Chumvi  ya pinki ) au  Himalayan Salt
8.     Pilipili manga

MAANDALIZI , MATAYARISHO  NA  MATUMIZI
Jinsi  Ya  Kuandaa, Kutayarisha  na  Kutumia  dawa asilia ya  Jiko.

Chukua  vijiko  vidogo   viwili  vyenye  dawa  ya jiko, kisha  tia  kwenye  kikombe chenye  maji  ya  moto  ambacho  ujazo  wake  ni  milimita  mia  mbili  hamsini ( 250mills ). Iache  kwa  kama  dakika  kumi, kisha  koroga  halafu  tumia  kunywa pamoja  na  machicha  yake. Utafanya  hivyo  mara  mbili kwa  siku, asubuhi  na  jioni  kwa  muda  wa   siku  thelathini. 
 
AU  Chukua  vijiko  vidogo  viwili  vyenye  dawa  yako  halafu chemsha  pamoja  na  maji  robo  lita  hadi itokote kabisa, kisha  ipua  halafu  tumia  kunywa  dawa  pamoja  na  machicha  yake. Utafanya  hivyo  mara  mbili  kwa  siku, asubuhi  na  jioni  kwa muda  wa  siku  thelathini

VUMBI  LA  CONGO ( CONGO DUST ) :   Katika  kipindi  cha  siku  thelathini  za  matumizi  ya  tiba  asilia  ya  Jiko. Unashauriwa  kutumia  vumbi  la  congo  walau  mara  moja  kwa  wiki  kwa  muda  wa  wiki nne. Yani  wiki ya  kwanza, utumie  mara  moja, wiki ya  pili  utumie  maara  moja, wiki  ya tatu  utumie  mara  moja, na  wiki  ya  nne  utumie  mara  moja.

MATAYARISHO   NA   MATUMIZI  YA  VUMBI  LA  CONGO
Chukua  dawa  yako  kiasi  cha kujaa  kwenye  kidole, kisha changanya  kwenye  mafuta  ya  kujipaka  halafu  tumia  kupaka  kwenye  kichwa  cha  uume  wako.  Utafanya  hivyo, nusu  saa  kabla  ya  kushiriki  tendo  la  ndoa.

LISHE   MAALUMU   YA   KUTUMIA   PAMOJA   NA   DAWA   YA   JIKO
Pamoja  na  dawa  ya  Jiko, unashauriwa  kutumia  lishe  maalumu  kama  ifuatavyo:

1.     SUPU   YA  NYANYA  CHUNGU  AMA  NGOGWE : Unashauriwa  kutumia  supu  ya  nyanya  chungu  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni kwa  siku thelathini.

Mahitaji :    
·Robo  kilo  ya  nyanya  chungu  (  Tumia nyanya chungu  zenye  rangi  ya  kijani kwani  ndio  zenye  virutubisho  vinavyo hitajika.
·Nusu  kijiko  kidogo  cha  chumvi  ya  pinki  (  Pink  Salt), au  Himalayan  salt  pamoja  na  maji  lita  mbili.  (  Kama  utakosa  hizo  chumvi  utatumia   nyanya  chungu  peke  yake  bila kuongeza  chochote  )

Matayarisho :  Baada  ya  kuziosha  nyanya  zako  bila  kutoa  vikonyo vyake, ziweke  kwenye  maji  kiasi  cha  lita  mbili, ndani  ya  maji  hayo ongeza  nusu  kijiko  kidogo  cha  chumvi  ya  pink, au  Himalayan Salt  ( Kama  hauna  hizo  chumvi   chemsha nyanya  zako  peke  yake  bila  kuchanganya  na  chochote), kisha  chemsha hadi  itoe  supu. Baada  ya  hapo, ipua kisha  tumia  kula  supu  yako  pamoja  na  kutafuna  nyanya  chungu  zote   ulizo  chemsha.  

Utafanya  hivi  mara   mbili   kwa  siku,asubuhi  na  jioni  kwa  muda  wa  siku thelathini.  Asubuhi  utatumia  muda  wwowote  kati  ya  saa  kumi na  mbili  alfajiri  na  saa nne  asubuhi  na  usiku  utatumia  muda  wowote  kati  ya  saa  moja  usiku hadi  saa  nne  usiku. )

N.B :KABLA  YA  KUTUMIA  SUPU  YA NYANYA  CHUNGU,  WEKA  TOFAUTI  AMA  INTERVAL  YA DAKIKA  KUMI   HADI  KUMI  NA  TANO TANGU UMETUMIA  DAWA  YA  JIKO. KWA MFANO  KAMA  UMETUMIA  DAWA  YA  JIKO  SAA  MBILI  KAMILI,ASUBUHI,  BASI  SUPU  YA  NYANYA  CHUNGU  ITUMIE  SAA  MBILI  NA  DAKIKA  KUMI AU  NA  DAKIKA  KUMI  NA  TANO . UTAFANYA VIVYO   HIVYO   WAKATI WA  USIKU.

Pia  kama, utakosa  nafasi  ya   kuchemsha  nyanya  chungu, basi unashauriwa  kutafuna  nyanya  chungu  zikiwa  mbichi  pamoja  na  maji  ya  uvugu  vugu  lita  moja  na  nusu, mara  mbili  kwa  siku  asubuhi na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.

3. JUICE  YA  ROZERA :  Unashauriwa  kutumia  juice  ya Rozera  mara kwa  mara, kila  upatapo  nafasi.. Unashauriwa  kutumia  lita  moja  hadi  mbili  ya juice  ya  Rozera kila  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini  mfululizo. Unatakiwa kutumia  lita  hiyo  moja  ya  juice  ya   Rozera  kwa  wakati  mmoja. Kama  ni mchana  utakunywa  lita nzima  ya  juisi  ya  Rozera, na  kama  ni  jioni, utakunywa  lita  nzima  ya  juisi ya  Rozera. Unatakiwa  kuinywa  bila  ya  kuchanganya na  kitu  chochote  kile. Na  muda  mzuri  wa  kuinywa, ni  kati  ya  saa  sita mchana     hadi  saa  saa  2   kamili  usiku.

Matayaraisho  Ya  Juice  Ya  Rozera :  Chukua  vijiko  vikubwa  vinne  vya  rozera  iliyo kaushwa, kisha  loweka  kwenye  maji  lita  mbili, iache  kwa  muda wa  dakika  thelathini, kisha  chemsha  hadi  itokote.  Itakapo tokota, ipua, chuja, makapi  weka  pembeni, baki  na  juisi  yako ambayo  utaitumia  kwa  kunywa  yote . Utafanya  hivyo  mara  moja  kwa  siku  kwa  muda  wa  siku  thelathini. Unaweza  kuinywa  ikiwa  ya  moto, ama  ikiwa  imepoa. Ila vizuri zaidi  uinywe  ikiwa ya  moto.

4.  JUICE  YA  MSAFISHA TUMBO : Unashauriwa  kunywa  walau  lita  moja ya  juisi  ya  dawa  asilia  ya  MSAFISHA TUMBO mara  moja  kwawiki  katika  kipindi  cha  wiki  nne utakazo  kuwa  unatumia  dozi ya  dawa  ya  Jiko.   Hii  ina  maana  kuwa  ndani  ya  wiki  nne  za  dozi  ya  Jiko,  utatumia  lita  nne  za  juisi  ya  Msafisha  Tumbo, lita  moja  kila wiki, kwa  muda  muda  wa  wiki  nne.

Matayarisho  Ya  Juisi  Ya  Msafisha  Tumbo:  Chukua  vijiko  vitatu  vidogo  vyenye  dawa  ya msafisha  tumbo,,  kisha  weka  kwenye  lita  moja  ya  maji, halafu chemsha  hadi  itokote, ikisha  tokota, ipua  chuja, makapi  weka  pembeni, ubaki  na  juisi  yako  ambayo  utaitumia  kwa  kunywa  yote. Unatakiwa  kuinywa  ikiwa  ya  moto  na  muda  mzuri  wa  kuinywa  ni  saa  kumi  na  mbili  jioni.

5.  VITUNGUU  MAJI  NA  VITUNGUU  SWAUMU:  Katika  kipindi  chote  utakacho  kuwa  unatumia  dozi  ya  dawa  ya  Jiko, unashauriwa  kutumia  kwa  wingi sana, vitunguu  maji  na  vitunguu  swaumu.

NJIA  ZA  KUTUMIA  VITUNGUU  MAJI  NA  VITUNGUU  SWAUMU
Zipo njia  kuu tatu  za  kutumia  kitunguu  maji  na  kitunguu  swaumu  kama lishe  maalumu  kwa  mwanaume  anaye  tumia  tiba  ya  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.

A. MCHANGANYIKO   WA   JUICE  YA  KITUNGUU  MAJI  NA  KITUNGUU  SWAUMU
Unashauriwa  kutumia  mchanganyiko  huu, walau  mara  moja  kwa  wiki.Lakini  kama  utaweza  kutumia  mara  mbili  au  tatu  kwa  wiki, sio mbaya  pia.
 
Mahitaji :   Kitunguu  swaumu  kiasi  ha  robo  kilo, kitunguu
maji  robo  kilo.
Matayarisho :  Blend au  saga  robo  kilo  ya  kitunguu  swaumu kupata  juisi  yake. Ukisha  saga, weka  juisi  yako  kwenye  sufuria
safi.  

Kisha  saga  robo  kilo  ya  kitunguu  maji  kupata  juisi
yake, ukisha  pata  juisi  ya  kitunguu  maji, changanya  pamoja  na ile  juisi  ya  kitunguu  swaumu  halafu  chemsha  hadi  itokote.
 
Ikisha  tokota, ipua  iache  ipoe.  Ikisha  poa  tumia  kunywa
mchanganyiko  wako  wote. Utakunywa  mara  moja  tu  kwa  siku.
 
Kama  utapenda, unaweza  kuchanga  na  asali  robo  lita  na  kuchemsha pamoja, kisha  ikisha  tokota, ipua  iache  ipoe  na  utumie  kunywa.

B.  KACHUMBARI   YA   KITUNGUU  MAJI  NA  KITUNGUU  SWAUMU
Chukua    vitunguu  maji  vikubwa vinne, kisha  vimenye  na  kuvikata  kata, kama  vitunguu  vya kachumbari. Halafu  chukua  punje  kumi  na  sita  za  vituu  swaumu, vikate  kate  na  uvichanganye  pamoja  na  vitunguu  maji  ulivyo vikatakata.   

Tumia  kula  mchanganyiko  wako  wote. Utafanya  hivyo mara  moja  tu  kwa  siku. Unaweza  kuongeza na  chumvi  ya  kawaidakidogo  kama  utapenda.  Tumia kachumbari hii  mara  nyingi  kadri  utakavyo  weza.
MENGINEYO

  Kama  ni  mtumiaji  wa  chai, penda  sana  kutumia  chai  iliyo ungwa  kwa  pilipili  manga  na  tangawizi.  Na  kama  unaatumia  uji, penda  sana  kutumia  uji  ulioungwa  kwa  pilipili  manga

 Jenga  mazoea  ya  kutumia  nyanya  chungu  katika  kila  mlo  wako. Kwa  mfano, kamaunakulala  ugali  na  nyama, basi  nyanya   chungu  pia  ziwepo  pembeni ( NYANYA  CHUNGU  ZINAZO HITAJIKA  HAPA  NI  ZILE  ZENYE  RANGI  YA  KIJANI KIBICHI )
 
vi.  Jenga  mazoea  ya  kuwa  unajumuisha  kitunguu  swaumu  kwenye  mlo  wako. Nyanya  chungu  iwe  kiungo  kisicho  kosa  katika  mlo  wako. Mfano, kama  unakula  ugali  na  nyama, basi  katika  mchuzi  ya  mboga  yako, kitunguu  swaumu  kiwe miongoni  mwa  viungo.

Kwa mahitaji  yako ya  dawa  ya  JIKO  pamoja  na  vumbi  la  kongo, wasiliana  na NEEMA  HERBALIST, duka  la  kuuza  dawa  mbalimbali  za  asili. Tunapatikana  Ubungo  jijini  Dar  Es  Salaam, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO   NATIONAL  HOUSING, nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.
 
Kwa  wateja  waliopo  jijini  Dar  Es  Salaam, wasio na  muda  au  nafasi  ya  kuja  ofisini  kwetu  Ubungo, tunayo  huduma  ya  kuwafikishia  dawa  mahali  walipo ( HOME & OFFICE  DELIVERY)
 
Kwa wateja  waliopo  nje  ya  mkoa  wa  Dar  Es  Salaam, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya usafiri  wa  mabasi mbalimbali. Wateja  waliopo  Zanzibar  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri wa  boti, wateja waliopo  Nairobi  watatumiwa  dawa  kwa  mabasi  ya  DAR EX PRESS, wateja  waliopo  MOMBASA  watatumiwa  dawa  kwa  mabasi  ya  TAHMEED, na  wale  wa ughaibuni  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU NAMBA  0766 53 83 84.

Na  kwa  taarifa  zaiddi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku kwenye  blogu yetu:

www.neemaherbalist.com

Kigogo mwingine wa CCM ajiuzulu

$
0
0
Ikiwa ni siku nne tu zimepita tangu Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT), Sophia Simba kusema kuwa hana mpango tena wa kugombea nafasi hiyo katika uchaguzi ujao, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM naye amesema kuwa miaka mitano aliyotumikia nafsi hiyo inatosha, hivyo ni wakati wake kupumzika.

Alhaji Abdallah Bulembo alitangaza uamuzi huo wa kujiuzulu jana wakati akifungua kikao cha dharura cha jumuiya hiyo walipokuwa wakijadili mapendekezo yaliyotolewa na Halmahsauri Kuu wa CCM iliyokutana Disemba mwaka jana.

Bulembo aliwaambia wajumbe hao kuwa anajiuzulu na nafasi hiyo na kuwa sababu si kwa vile ameteuliwa kuwa mbunge bali yeye anaamini ni muda wa kupisha mtu mwingine. 

Aidha, aliwataka viongozi hao kujipima kuona kama kuna ambaye anaona kuwa anaweza kuongoza jumuiya hiyo agombee.

Lakini aliwaasa wote watakaogombea kuwa, yeye hatompigia mtu kampeni na wala asiwepo mtu atakayesema kuwa amekubaliana naye jambo lolote, hivyo kila mgombea ajinadi mwenyewe.

Pia Bulembo alisema kwa muda wote ambao ameingoza jumuiya hiyo, amefanikiwa kwa asilimia 75 kwa yote aliyoyaahidi kwani wakati anaingia madarakani jumuiya hiyo ilikuwa katika hali mbaya hadi mwenyekiti aliyekuwepo, Dkt Kikwete akataka kuifuta. 

"Tangu nimeingia madarakani hatujawahi kuomba hata shilingi mia kwa ajili ya kuendesha vikao vyetu, "alijisifu Bulembo.

Hata hivyo amesema ataendelea na majukumu ya nafasi hiyo hadi mwezi Oktoba atakapokabidhi ofisi kwa mwenyekiti mpya atakayechaguliwa.

Maaskofu Watoa Waraka Mzito

$
0
0
Jumuiya  ya Kikristo Tanzania (CCT) imetoa waraka uliojumuisha mambo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwataka viongozi kutenda haki, kutokuwa na upendeleo, kuheshimu Katiba na sheria za nchi.

Pia jumuiya hiyo imewataka Watanzania kwa ujumla kuliombea taifa na viongozi wake, ili wawe walinzi wa Katiba na sheria za nchi kama walivyoapa.

Waraka huo ulisambazwa jana katika vyombo vya habari, ukiwa umetiwa saini na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Fredrick Shoo na Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania (KAT), Dk. Jacob Chimeledya.

Wengine ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Moravian Tanzania (KMT), Dk. Isaac Nicodemo na Askofu Mkuu wa Kanisa la African Inland Church in Tanzania (AICT), Silas Kezakubi.

“CCT inatoa maelekezo kwa Wakristo wa makanisa wanachama na Watanzania wote kwa ujumla, kuendelea kulinda na kuheshimu misingi ya haki za binadamu na kuliombea taifa na viongozi wake ili waendelee kuwa na hofu ya Mungu na waadilifu.

“Watende haki, wasiwe na upendeleo na waheshimu na kuwa walinzi wa Katiba na sheria za nchi kama walivyoapa,” ilisema sehemu ya waraka huo.

CCT ilieleza pia kusikitishwa na vitendo vya ujambazi na matumizi ya silaha katika jamii na kukemea matukio ya ukatili na yale ya watu kupotea katika mazingira ya kutatanisha.

 “CCT inasikitishwa na vitendo vya ujambazi na matumizi ya silaha katika jamii yaliyofikia kiwango cha kuua askari polisi."

Aidha, CCT inakemea matukio ya ukatili unaondelea katika jamii.

“Yapo matukio ambayo yamedhihirisha ushirikiano hafifu kati ya polisi na wananchi na kuendelea kujitokeza kwa matukio yanayoashiria chuki za kidini na kikabila.

 “CCT inatoa wito kwa Serikali kuhakikisha misingi ya umoja na mshikamano wa kitaifa inaheshimika na utawala wa kisheria unafuatwa,” ilisema taarifa hiyo.

Dawa za Kulevya
CCT ilisema ili vita dhidi ya dawa za kulevya ifanikiwe, ni muhimu Serikali ikalenga kutokomeza kiini cha tatizo kwa kuwapata wahusika wakuu wa biashara hiyo bila kujali wasifu wao na nafasi walizonazo katika jamii.

Kutokana na hilo, CCT ilisisitiza kuwa Serikali izingatie misingi ya sheria, haki na usawa katika kuwakamata, kuwapekua na kuwafikisha katika vyombo vya sheria bila kuonea mtu wala kusukumwa na misingi yoyote ya imani au itikadi ya mtu.

 “CCT inaunga mkono vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya na viroba iliyoanzishwa na Serikali. Hata hivyo, CCT inasisitiza kuwa ili vita hii ifanikiwe, ni muhimu sana Serikali ilenge kutokomeza kiini cha tatizo kwa kuwapata wahusika wakuu wa biashara hii bila kujali wasifu wao, nafasi zao wala nafasi walizo nazo katika jamii.

“Katika kufanya hivyo, ni muhimu Serikali izingatie misingi ya sheria, haki na usawa katika kuwakamata, kuwapekua na kuwafikisha katika vyombo vya sheria bila kuonea wala kusukumwa na misingi yoyote ya imani au itikadi ya mtu.

“Ni muhimu kwa Serikali kuendelea kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kupata ajira na kuendesha shughuli za ujasiriamali ili kujiepusha na vitendo viovu vikiwemo matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe kali.

“CCT inayaelekeza makanisa wanachama, wazazi na walezi kuendelea kuwalea vijana wao katika misingi ya kidini ili wasijiingize katika matumizi ya dawa za kulevya na pombe kali.

“Wakati huu wa Kwaresma, tunawaombea na kuwaomba wale wote ambao kwa njia moja au nyingine wanajihusisha na dawa za kulevya au unywaji wa pombe kali, watubu na kuyaacha maovu yao na Mungu atawarehemu,” walisema maaskofu hao.

Hali ya Chakula
Kuhusu hali ya chakula nchini, CCT ilisema kuwa pamoja na mvua kuanza kunyesha, Serikali na wengine wawezeshe usambazaji wa chakula kutoka mikoa yenye ziada kwenda mikoa yenye uhaba wa chakula ili bei ya chakula iweze kushuka.

“Tunaiomba Serikali kupitia idara yake inayohusika, iratibu na kusaidia utekelezaji wa jambo hili, ili wananchi waweze kumudu bei, mfano mahindi hayo yakisambazwa, bei ishuke kutoka zaidi ya Sh 100,000 ifikie angalau Sh 60,000.

“Pia tunawaomba wakulima wasitumie njaa hii kutekeleza usemi ya kwamba ‘kufa kufaana’, hivyo kwao kipindi hiki kigumu kwa Watanzania wengine wakakifanya kipindi cha kupandisha bei ili kupata faida kubwa.

“Sambamba na wito huu, tunawaekeleza wanachama wetu kupitia vitengo vya maafa na misaada ya kibinadamu, waendelee kuwasaidia wananchi wenye upungufu mkubwa wa chakula wakipate kwa bei nafuu kwenye maeneo yao,” ilisema.

CCT iliwataka Wakristo wote kuendelea kumwomba Mungu ili mvua zinazoendelea kunyesha ziwe za neema na zisilete madhara.

Katika hilo, wameiomba serikali kutoa unafuu wa bei ya gesi ya kupikia ili wananchi wengi wapunguze au kuachana kabisa na matumizi ya kuni na mkaa.

Elimu
CCT ilisema pamoja na nia njema ya Serikali kutoa elimu bure, lakini iangalie masilahi ya walimu na kuwe na mpango mkakati unaotekelezeka wa kuimarisha miundombinu ya kufundishia.

 “Serikali haina budi kuendelea kutoa elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu dhana ya elimu bila malipo, ili kuepusha migogoro inayokabili sekta ya elimu kwa dhana hiyo kutoeleweka kwa vizuri kwa baadhi ya wananchi.

“Pia mabadiliko ya mitaala na miongozo mingine ya kufundishia ya mara kwa mara imekuwa ikiathiri elimu ya Tanzania kwa kila awamu ya uongozi na kuwafanya wahitimu wetu kukosa ushindani kikanda na kimataifa,” ulisema waraka huo.

Kupitia waraka huo, maaskofu waliishauri Serikali kuwa na será ya elimu isiyobadilika badilika kila uongozi mpya unapoingia madarakani.

Upelelezi Kesi Ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake Wasubiri Ushahidi Kutoka Ulaya

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa upelelezi uliokuwa ukifanywa ndani ya nchi ya Tanzania katika kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Kamishna Mkuu Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake umekamilika.

Hayo yameelezwa na wakili wa Jamuhuri Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.

Hata hivyo Wakili Wilson amedai kuwa huyo bado wanasubiri upelelezi unaofanywa nje ya nchi ambao bado haujakamilika.

Mbali na Kitilya washtakiwa wengine ni Miss Tanzania, 1996, Shose Sinare na Sioi Graham Solomon.Wanadaiwa kutenda makosa nane likiwemo la utakatishaji wa fedha wa kiasi cha USD milioni sita.

Baada ya taarifa hiyo ya upelelezi, Wakili wa utetezi Majura Magafu aliiomba mahakama kuwaleza upande wa jamuhuri waeleze hali ya upelelezi ikoje na siyo kuleta lugha za ujanja ujanja.

“Tunaomba upande Jamuhuri watupe majibu yenye muelekeo, waache lugha za ubabaishaji, kama upelelezi haujakamilika waseme basi siyo suala la kutueleza umekamilika ndani ya nchi lakini nje bado, haileti maana yoyote.”Amesema Magafu.

Akijibu hoja hizo,Hakimu Mkeha amesema kitendo cha kesema upelelezi wa ndani umekamilika inaonyesha kesi imepiga hatua kwa kiasi fulani hivyo ameuagiza upande wa jamuhuri ukija tena ueleze hali ya upelelezi huko nje ikoje.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 24,mwaka huu.

Mbali na shtaka la utakatishaji wa fedha, watuhumiwa hao wanakabiliwa na tuhuma za kula njama, kutoa nyaraka za uongo na kughushi.

Wanadaiwa kutenda makosa hayo katika tarehe tofauti kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa Mkopo wa USD 550 wa Serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard ya Uingereza.

VIDEO: Rais Magufuli Aongoza Kikao Cha Usalama Na Maadili Ya CCM Mkoani Dodoma

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Machi, 2017 ameongoza Kikao cha Usalama na Maadili cha chama kilichofanyika Chamwino Mkoani Dodoma.

Kikao hicho kimehudhuriwa na wajumbe wake wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambaye ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Ndg. Philip Mangula, Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Idd.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza jambo wakati wa kikao cha Usalama na Maadili kilichoongozwa na Rais Dkt Magufuli,Chamwino mkoani Dodoma.

 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma,pichani kati ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na  Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein mapema leo,Chamwino mkoani Dodoma.

Kamanda Siro aongea kuhusu kukamatwa kwa Vanessa Mdee na Rummy

$
0
0
Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema jeshi hilo bado linawashikilia Wasanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya akiwemo Vanessa Mdee ambaye alikamatwa juzi (Jumatano) na Rummy Shaeli kwa tuhuma za matumizi ya dawa za kulevya.

Akiongea na wana habari Ijumaa hii ofisini kwake kamanda amesema jeshi hilo bado linawashikilia watu hao mpaka uchunguzi utakapo kamilika.

“Juzi tulimkamata Vanesa Mdee napia tunamshikilia Rummy Shaeli taarifa zinaonyesha ni watumiaji na wasambazaji lakini upelelezi unaendelea na ukikamilika tutawafikisha mahakamani au tutamuachia. Na sio hao tu wapo wengine ambao tuna majina baadhi tumewakamata inasemekana huwa wanasafirisha dawa hizo kwenda Afrika Kusini,” amesema Siro.

Vanessa alikuwa miongoni mwa watuhumiwa wa matumizi ya dawa za kulevya waliotajwa na Mkuu mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda katika orodha yake ya pili na kuwataka kuripoti katika kituo cha kituo kikuu cha polisi. Hata hivyo Vanessa hawakuweza kufika kituoni hapo kwa wakati kwa sababu wakati agizo hilo likitolewa alikuwa nje ya nchi na kumtuma mwanasheria wake kumwakilisha.

Jaji Warioba Atoa Kauli Nzito Kuhusu Tatizo la Njaa Nchini

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Jaji Joseph Warioba amewataka watanzania wote kuungana na kujiaandaa kukabiliana na baa la njaa ambalo huenda likatokea, huku akikiri kuwa tatizo la upungufu wa chakula kwa mwaka huu, ni kubwa kuliko kawaida.

Akizungumza leo wakati akizindua kongamano la 'Wanawake na Uongozi' katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Dar es Salaam, Jaji Warioba amesema hakuna haja ya watanzania kubishana na kulumbana kama kuna njaa au upungufu wa chakula, bali kujiandaa ikiwa ni pamoja na kujifunza kujifunza katika nchi ambazo tatizo hilo limetokea ikiwemo Kenya na Somalia.

"Haijalishi kama njaa ipo au kuna upungufu wa chakula kinachotakiwa ni kuungana  na kujiandaa kwa pamoja ili kujua ni jinsi gani tutaweza kukabiliana na baa la njaa endapo litatokea kama jinsi inavyosemwa, tujifunze kupitia Kenya na Somalia. Siyo sawa kurushiana maneno huyu anasema hivi huyu anamjibu vile, tuungane kwa pamoja" Amesema Warioba ambaye pia alikuwa ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba a kuongeza “Serikali ijiandae kukabiliana na njaa kwa sababu ingawa tumezoea kwamba kila mwaka zipo sehemu zenye upungufu wa chakula, mwaka huu tatizo ni kubwa”

Kuhusu vita dhidi ya dawa za kulevya, Warioba ametaka elimu itolewe kwa watu wanaojishughulisha na dawa za kulevya hususani wanaolima bangi lakini pia wasaidiwe wapate njia mbadala za kuweza kujikimu ili kuachana na shughuli hizo ambazo zinaathiri asilimia kubwa ya vijana.

Ameongeza kuwa tatizo la dawa za kulevya linaripotiwa kawaida kama siyo tatizo kwa sababu limefanywa kama jambo la siasa

"Tatizo la dawa za kulevya linazungumzwa kama jambo la kawaida, badala yake tumetafuta mchepuo wa kisiasa, ambao ndiyo unazungumzwa, Karibu kila siku utaona taarifa kwamba wameenda askari wameharibu dawa za kulevya katika mashamba ya bangi, inaripotiwa tu kama tukio halafu basi. 

"Tuseme hapana matumizi ya madawa, madawa ni mengi sana yanayoingia , tunajua madhara yake, tuyazuie yanayoingia kutoka nje pamoja na yanayolimwa, tujitahidi kuwasaidia vijana walioathirika. Tunahitaji kujenga nguvu za pamoja" Amemalizia jaji Warioba.

Kongamano hilo lililoandaliwa na Mtandao wa Wanawake na Katiba, ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, na limetumika pia kuzindua kitabu chenye jina 'Nguvu zetu, Sauti zetu, Ajenda katika mchakato wa katiba mpya' kilichoandaliwa na mtandao huo jijini Dar es salaam,

Maamuzi ya Mahakama kwa maafisa wa zamani wa TFF katika kesi ya rushwa

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru watumishi wawili wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Martin Chacha na Juma Matandiko  baada ya kuwaona hawana kesi ya kujibum. Uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi.

Akisoma uamuzi huo, Hakimu Shahidi amesema kuwa amewaachia huru washtakiwa baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na kuona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha pasipo kuacha shaka kuwa washtakiwa wametenda kosa.

Washtakiwa Matandika na Mecky wanatuhumiwa kwa kuomba rushwa ya Shilingi milioni 25.

Awali ilidaiwa kuwa Februari 4 mwaka jana, washtakiwa hao wakiwa waaajiriwa wa TFF walishawishi kuomba rushwa ya kiasi hicho cha pesa kutoka kwa Salum Kulunge na Constatine Morandi ambao ni maofisa kutoka Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Geita na Klabu ya Mpira wa Miguu Geita.

Ilidaiwa kuwa watuhumiwa hao waliomba rushwa hiyo kama kishawishi kwa TFF na Idara ya Uhamiaji Tanzania kutoa uamuzi dhidi ya klabu ya Mpira wa Miguu Polisi Tabora ili kuisaidia klabu  ya Geita kupanda katika ligi kuu ya Tanzania.
 
Akitoa uamuzi huo, Hakimu Shahidi alisema katika ushahidi uliotolewa na mashahidi wa upande wa mashtaka unaonesha hakuna mtu aliyeenda Takukuru kulalamika juu ya washtakiwa kuomba rushwa zaidi ya sauti ya CD kusambaa katika mitandao.

Amesema upande wa mashtaka haukuonesha kama kweli washtakiwa walitoka Geita kuja Dar Saalam.

Kuhusu sauti zilizotambuliwa za Mecky na Matandiko kupitia CD, Hakimu Shaidi amesema watu wana sauti za kufanana na hata kuigizana hivyo hauwezi kujikita kwenye ushauli kuwa ni washtakiwa wenyewe ndio wanaosikika kwenye hiyo CD.

Amesema, ni wajibu wa upande wa mashtaka kuthibitisha pasipo kuacha mashakama kuwa washtakiwa walitenda kosa hilo.

Hakimu Shahidi ameenda mbali na kueleza kuwa kwa mujibu wa ushahidi ulitolewa mahakamani hapo, imedaiwa kuwa kanuni za TFF zinaeleza wazi kuwa, mchezaji akibainika kudanganya ndiye anayepaswa kuadhibiwa lakini si timu kunyang'anywa pointi.

"Hawa hawakuwa na mamlaka ya kunyang'anya pointi, hivyo wasingeshtakiwa kwa kuomba rushwa na hata kama walitenda kosa basi wangeshtakiwa na tuhuma zingine, labda utapeli", amesema.

Kutokana na upungufu wa ushahidi, Hakimu Shaidi aliwaachia huru washtakiwa kwa sababu hawana kesi ya kujibu.

Kesi hiyo ilikuwa inaendeshwa na Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru),Leonard Swai.

Godbless Lema Afanya Mkutano wa Kwanza Baada ya Kutoka Gerezani......Wema Sepetu naye Alipewa Nafasi ya Kuwasalimia Wananchi

$
0
0
Na,Vero Ignatus ,Arusha.
Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoka rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho. 

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamilisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.

Amewataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma
Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la Arusha
Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo leo jijini Arusha.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya March 11

Macho Yote Yaelekezwa Dodoma Leo.....CCM Iliyosukwa Upya Yasubiriwa

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kinafanya vikao viwili vikubwa kwa mkupuo vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mjini Dodoma.

Vikao hivyo vitafanyika kwa siku moja, baada ya Kamati Kuu kutofanyika jana. Badala yake siku nzima ya jana, ilitumika kwa ajili ya kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya chama.

Kikao hicho cha Kamati ya Usalama na Maadili cha jana, kiliangalia maadili ya wanachama wake na kiliongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, Rais John Magufuli.

Pamoja na mambo mengine, kikao hicho hujadili nidhamu za viongozi na baadhi ya wanachama waliokwenda kinyume na maadili ya chama hicho.

Kamati hiyo huhoji wanachama na viongozi na mapendekezo yake, hupelekekwa Kamati Kuu kwa ajili ya hatua zaidi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole alisema, vikao hivyo vitafanyika leo, ambapo Kamati Kuu itakutana asubuhi.

Alisema baada ya Kamati Kuu kumaliza kikao chake, mchana Halmashauri Kuu itafanya mkutano wake, ambao ndio utakaoandaa ajenda kwa ajili ya Mkutano Mkuu Maalumu wa chama hicho, utakaofanyika kesho, ambao utafanya mageuzi makubwa katika chama.

Baadhi ya mageuzi hayo ni kubadilisha Katiba na Kanuni za chama pamoja na jumuiya zake, ikiwemo kupunguza wajumbe wake ili kuwa chama cha ufanisi zaidi.

Polepole aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kutoka mikoa yote nchini, kuwasili mjini Dodoma na kuhudhuria kutokana na maandalizi yake kukamilika.

“Nawaomba wajumbe wa Mkutano Mkuu wafike mjini Dodoma kutokana na maandalizi yote kukamilika ili kufanikisha mkutano huo ambao ni muhimu katika kufanya mageuzi katika chama,” alisema Polepole.

Jina la Mama Salma Kikwete Latumika Kutapeli

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu uwepo wa Chama cha Akiba na Mikopo (Saccos), inayotapeli watu fedha kwa kutumia majina ya watu maarufu nchini.

Tahadhari hiyo ilitolewa jijini Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Alisema Saccos hiyo yenye jina maarufu la Focus Vicoba kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook na tovuti inayojulikana kwa jina “http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz. wapka-mob, hutumia majina ya viongozi serikalini na watu maarufu, kwa nia ya kuwatapeli wananchi.

Alisema majina ya viongozi yanayotumiwa na matapeli hao ni pamoja na jina la mke wa Rais mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Nne, Salma Kikwete, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi.

Aliongeza kuwa matapeli hao, hutumika kufungua akaunti za facebook na tovuti mbalimbali, ambazo hutumia kuwarubuni watu kwa kuwaaminisha kuwa wanaweza kupata mikopo yenye masharti nafuu na haraka zaidi kwa njia hiyo ya mtandao.

Alisema katika ufuatiliaji wa suala hilo, kitengo cha upelelezi wa makosa ya mtandao cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kimebaini kuwa katika tovuti “http://www.vicobaloanstz. wapka-mob” www.vicobaloanstz. wapka-mob picha na jina la Mama Salma, limetumika huku kwenye ukurasa wa Facebook wakitumia jina la Mengi, likiwa ni pamoja na namba za simu 0757 308381 na 0768 199359 ambazo si za Mama Salma wala Mengi.

Aidha, alisema katika ufuatiliaji wa jambo hilo, Desema 16 mwaka jana alikamatwa mtu aliyefahamika kwa jina la Boniface Ojwando (27) baada ya kubainika kuwa anahusika katika mtandao huo wa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu kupitia mitandao hiyo ya kijamii, ambapo mpaka sasa mtuhumiwa ameshafikishwa mahakamani ili kujibu mashtaka hayo yanayomkabili.

“Nitoe onyo kwa wale wote wanaondelea kufanya udanganyifu huu wa kujipatia fedha kwa njia isiyo halali kupitia mitandao ya kijamii kuacha mara moja, kwani sheria iko wazi na pindi watakapokamatwa, watachukuliwa hatua kali,”alisema Sirro.

Alitoa rai kwa wananchi wote, kutokuwa wepesi kukubali matangazo ya mikopo, yanayotolewa kwenye mitandao ya kijamii, bila kufika katika ofisi husika ili kujiridhisha kuhusu utolewaji wa mikopo hiyo, ili kuepuka kutapeliwa fedha na mali zao.

Godbless Lema Asimulia Maisha ya Gerezani na Jinsi Alivyopewa Cheo cha Nyapara Kuwaongoza Wafungwa Wenzake

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) ameibuka na kueleza mambo mbalimbali, aliyokumbana nayo katika kipindi cha miezi minne akiwa mahabusu katika Gereza la Kisongo mkoani Arusha, kutokana na kukosa dhamana katika kesi ya uchochezi.

Aidha, amesema akiwa katika mahabusu hiyo, alipewa cheo cha nyapara na kuweza kuwaongoza wafungwa wenzake, jambo lililomfanya kufahamu matatizo na manyanyaso mbalimbaliwa, wanayofanyiwa wafungwa.

Lema alisema hayo katika Viwanja vya Ngarenaro jijini Arusha jana, alipokuwa akiwahutubia wakazi wa jimbo lake katika mkutano wa hadhara.

“Kwani nimekosa nini? Kutoa maoni ndio nifanywe hivi kweli? Nilikuwa naomba sana kwa Mungu tangu nilipowekwa ndani hadi siku nilipotoka. 

“Na Mungu aliniambia endelea kuomba na usubiri uone miujiza yangu, lakini akaniambia wasamehe wote waliokukosea kwa kukuweka gerezani bila kosa.”

Akizungumzia kosa alilolifanya la kutoa kauli ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli; Lema alisema; “Nilivyosema nimeona maono walidhani mimi ni kichaa, lakini Mungu ndiye atakayethibitisha maono haya, kama yalikuwa ni feki au la.

“Dhambi mbaya na kubwa kuliko zote duniani ni uoga, kinachotesa nchi hii si polisi, ni uoga, angalia kilichotokea juzi mahakamani, nimekaa ndani miezi minne halafu nilipotoka wananchi walikamatwa na kupigwa, kisha wakafunguliwa kesi ya mkusanyiko usio halali, jambo ambalo ni la uonezi,” alisema Mbunge huyo.

Akitoa ushauri kwa polisi, Lema alisema; “ Nawaomba polisi muwe na utu, kwani damu mnayoimwaga itawarudia, hakuna dhambi itakayopandwa ikavuna haki, kwanini mnawapiga watu? Nasema Mungu yupo.”

Alisema Idara ya Mahakama, haipo huru na kwamba kielelezo cha Serikali kuingilia mhimili wa mahakama ni hatua ya hivi karibuni ya Rais Magufuli kumteua Kaimu Jaji Mkuu badala ya Jaji Mkuu.

Alisema lengo la uteuzi huo, aliodai si sahihi, ni kuifanya Serikali icheze na sheria na kwamba tafsiri iliyo ni kuilazimisha Mahakama icheze wimbo wa serikali.

“Hili ni jambo la hatari sana, kwani watu wakijua kuwa Mahakama inayumbishwa na haijasimama imara, haki itatafutwa mitaani. Mateso niliyoyapata Magereza, yamenitengeneza kuwatetea waliopo magerezani.

“Nakuomba Mbunge mwenzangu James Millya (Mbunge wa Simanjiro – Chadema), tukienda bungeni turekebishe sheria, maana tulipozitunga, tulidhani sisi haitugusi kumbe inatugusa, hivyo tuombe ifanyiwe marekebisho.”

Alisema pia akiwa jela, alishuhudia mambo mbalimbali, ikiwemo kufungwa kwa vijana wadogo wenye umri wa miaka 14 kinyume cha sheria za nchi.

Aliongeza;“Umri huo ni mdogo sana na ninaposema Magereza, lazima mjuwe hali halisi iliyopo magereza."

Alisema pia alishuhudia kuwekwa mahabusu kwa watu wengine kwa muda mrefu, bila kufikishwa mahakamani au kupewa dhamana, jambo alilosema ni kukiuka sheria za nchi.

Alisema kutokana na uzoefu alioupata mahabusu kwa kipindi cha miezi minne, anaandika kitabu kuhusu wafungwa wanavyoteseka magerezani.

Alisema pia akiwa mahabusu, ameweza kukutana na watu wanaoitwa magaidi zaidi ya 65 wakiwa wamekaa kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka minne; huku wengine wakiwa wamekatwa miguu, lakini cha ajabu ni kuwa hawajahukumiwa kutokana na kutokuwepo kwa ushahidi.

“Unapochelewesha kesi za ugaidi, unajenga tabaka kati ya dini na dini, kama ni magaidi, malizeni upelelezi ili wahukumiwe, lakini kwa upelelezi wangu na uchunguzi wangu sijaona kama hao watu ni magaidi.

“Natoa agizo, mmalize upelelezi kabla sijaenda Bungeni, hii haitakuwa noma ndogo, itakuwa noma kubwa nikienda Bungeni. 

“Kama mimi Mbunge mmeninyima dhamana, kila siku mnaweka mapingamizi narudi gerezani, hali ikoje kwa watu wasioandikwa kwenye magazeti ambao hawajulikani, ni wazi kuwa wananyanyaswa sana,” alisema mbunge huyo.

Kabla ya kuanza kuhutubia, Lema alimpa nafasi msanii, Wema Sepetu ambaye alimtaja kuwa ni mwanamke jasiri na kuwa ana uhakika atashinda katika kesi yake ya kudaiwa kukutwa na dawa ya kulevya.

Akihutubia, Wema alisema ana imani na Mungu na kuwa mitihani ya maisha, anayokumbana nayo ni mipango ya Mungu katika kumfikisha mahali alipo hivi leo.

Alimuomba Lema kusamehe kila analofanyiwa na kutolipiza kisasi ili kupata baraka za mwenyezi Mungu.

Naye, Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini, Derick Magoma alisema Chadema wilaya Arusha, ipo imara haijayumba wala kutetereka wakati Lema alipowekwa mahabusu kwa kipindi cha miezi minne.

“Hatumpi mtu yoyote kura, bali ni Lema hadi 2020 au zaidi ya hapo, tumefanya maendeleo kwa kipindi cha miaka miwili na wananchi wote mnajua kuwa maendeleo yameletwa na Chadema” alisema.

Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro, alieleza furaha aliyonayo kutokana na kitendo cha kuachiwa kwa Lema. Alisema kwamba miezi minne aliyokaa mahabusu, si jambo la mchezo.

“Mbunge najua walikuweka ndani sababu ya kudhoofisha maendeleo ya Jiji la Arusha, lakini kwa sababu una Meya na madiwani bora wa Baraza la Madiwani, hatukuweza kutetereka” alisema Lazaro.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images