Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sophia Simba atangaza kung’atuka UWT

$
0
0
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanwake Tanzania (UWT), Sophia Simba ametangaza kutogombea tena nafasi hiyo kwenye uchaguzi wa Chama hicho unaotarajiwa kufanyika mwaka huu.

Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na  wanawake wa umoja huo wakati wa maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani yaliyofanyika jijini Dar es salaam.

“Mimi Sophia Simba, nimeamua kutogombea kwa hiari yangu mwenyewe nimeamua kutogombea nafasi ya Mwenyekiti wa Wanawake Taifa UWT katika uchaguzi ujao,”amesema Sophia Simba.

Sophia Simba ametaja sababu zilizomfanya asigombee kuwa ni azma yake ya kuutumikia umoja huo kwa muda wa vipindi viwili tu na si zaidi ya hapo.

Aidha, amesema kuwa akiwa ndani ya UWT amebahatika kushika nafasi mbalimbali za uongozi kwa sababu alianzia nafasi ya ukatibu wa tawi la Kaskazini NDC.

Hata hivyo amesema kuwa anamshukuru mungu kwa kumjalia kushika nafasi mbalimbali kwa kuwa amekuwa mbunge kwa muda wa miaka 22.

Makonda: Nisemeni, Mkichoka Mtanyamaza

$
0
0
Mkuu  wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kelele zinazoendelea dhidi yake ni dalili za mafanikio katika vita dhidi ya dawa za kulevya.

Makonda ameyasema hayo jana alipokuwa mgeni rasmi katika tamasha la Twendezetu Kigamboni lililofanyika katika wilaya.

Amesema, mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni ya kufa au kupona.

“Mfahamu kuwa tunapambana kati ya mauti na uzima, kelele, mwangwi vinavyoendelea sasa ni dalili njema kwamba tunaendelea kunyooka,” amesema Makonda.

Makonda alisema Dar es Salaam ya sasa anaifananisha na chuma kilichopinda na sasa kiko katika hatua ya kunyooka hivyo lazima zitokee kelele nyingi kama ambavyo zinaendelea sasa.

“Huwezi kufanya kazi ya kunyoosha chuma bila kusikia mwangi, kelele na maumivu kwa sababu kazi ya kukomboa vijana dhidi ya dawa za kulevya si rahisi,” amesema Makonda.

Amesema katika kipindi hicho ambacho amekiita kuwa ni cha kulinyoosha Jiji la Dar es Salaam ni lazima kelele zisikike, uonekane moto unaoacha maumivu makali na baada ya hapo ije picha ya chuma kilichonyooka ambayo ndio picha ya Jiji la Dar es Salaam itakayokuwa imenyooka.

Amesema kelele hizo zitapita na mwisho lazima kufika ng’ambo ya pili pasipo na dawa za kulevya, kwenye taifa lililojengwa na uchumi imara.

Amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kuhakikisha dawa za kulevya zinatokomezwa ambapo alisema hivi sasa katika Jiji la Dar es Salaam dawa hizo zimepungua.

“Nitoe pongezi kwa Jeshi la Polisi dawa za kulevya zimepungua sasa Dar es Salaam na pia niwapongeze pia vijana ambao wanaendelea kutoa taarifa,” alisema Makonda.

Aliwaasa wananchi kushirikiana na Rais John Magufuli ambaye anafanya jitihada kuijenga Tanzania ya kesho iliyo bora. Kuhusu Kigamboni alisema anatarajia kuiona Kigamboni ikiwa mji wa mfano ambao haujaharibiwa na matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na uhalifu na vijana walioharibika kutokana na matumizi ya dawa za kulevya badala yake kuwe na vijana wachapakazi.

“Watu watakapokuja Kigamboni wakute ni mji msafi, salama, uliopangika unaofaa kupumzika… mji ulio salama usio na uhalifu,” amesema Makonda.

Amewataka wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Hashim Mgandilwa na viongozi wake katika kutimiza ndoto hiyo ya kuifanya Kigamboni tulivu na salama.

Amewaasa wazazi kuhakikisha wanafuatilia mienendo ya watoto wao kuhakikisha hawajiingizi katika matumizi ya dawa za kulevya na pia vijana kuchungana wao wenyewe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Mgandilwa alisema lengo la tamasha hilo ni kuzitambulisha fursa zilizopo katika wilaya hiyo, kuwakutanisha vijana kupiga vita dawa za kulevya na pia kuiunga mkono serikali katika kufanya mazoezi.

Tamasha hilolilihudhuriwa pia na Mbunge wa Jimbo hilo, Dk Faustine Ndungulile Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Rahel Mhando na Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo.

Mama Wema Sepetu akamatwa na Polisi

$
0
0
Mama mzazi wa Wema Sepetu, Mariam jana alikamatwa na Polisi jijini Dar es Salaam akituhumiwa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyiffu kutoka kwa mfanyabiashara, Alex Msama.

Kwa mijibu wa gazeti la Mwananchi, Mariam alikamatwa majira ya saa nne asubuhi na kufikishwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay jana ambapo alifunguliwa jalada la kesi inayomkabili. 

Baadaye aliachiwa kwa dhamana saa 12 jioni baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili.

Inadaiwa kuwa chanzo ni kuwa, Mariam alikubali kumuuzia Msama nyumba iliyopo Sinza, Dar es Salaam baada ya benki ya TIB kutaka kuipiga mnanda kufuatia mama Wema Sepetu kumdhamini mtu katika benki hiyo ambaye hakurejesha mkopo wake.

Kwa sababu Msama hakuwa na fedha ya kutosha kwa wakati huo, aliendelea kutafuta fedha katika benki na wakati huohuo akimpa Mariam fedha kidogo ambazo zilifikia TZS milioni 14. 

Mariam baada ya kuona mchakato wa Msama unachelewa, aliuza nyumba ile kwa mtu mwingine bila kumtaarifa Msama aliyekuwa tayari amechukua fedha zake.

Aidha, jana wakati wa mahojiano Kituo cha Polisi, Mariam alikiri kupewa TZS milioni 8 ambazo zipo kimaandishi na kusema hatambui fedha nyingine zaidi.

Msama alipoulizwa kuhusu kumshtaki Mariam alikiri na kusema kuwa yeye anataka kulipwa fedha zake zote.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu alithibitisha kushtakiwa kwa kada huyo na kusema aliandika maelezo ya awali kuhusu suala hilo na kuachiwa.

Askofu Gwajima asema yeye ni mashine....Ukiweka Mguu Lazima Akusage. Msikilize Hapa LIVE Akihubiri Kanisani

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema yeye ni sawa na mashine ya kusaga na kukoboa ambayo ukiweka miguu unageuka sembe.                      

Gwajima amesema hayo leo asubuhi katika ibada inayoendelea kanisani kwake hivi sasa akieleza kuwa, "Baba wa familia amechokozwa kuwa anavuta unga watoto wamechachamaa wanataka baba ampige adui yake, nitaendelea kupiga bila kuogopa chochote."                   

"Watu wananiambia niache kumpiga mbona hawakumwambia yeye aache kunipiga, nitampiga tu na bado kazi inaendelea."

==>Msikilize LIVE Hapo chini

VIDEO: Rais Magufuli Akerwa na Matapeli....... Atoa Siku 7 Dangote Apewe eneo la kuchimba makaa ya mawe

$
0
0
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini impe mfanyabiashara Aliko Dangote eneo la kuchimba makaa ya mawe na agizo hilo liwe limetekelezwa ndani ya siku saba kuanzia leo.

Ameiagiza kuwa, makaa ya mawe yakiisha kwenye eneo atakapopewa Dangote, apewe eneo lingine.

Ametoa maagizo hayo leo mkoani Mtwara kabla ya kuzindua magari 580 ya Dangote yatakayokuwa yakibeba saruji kutoka kiwandani.

“Nia yangu nataka kiwanda hiki kifanye kweli ili ikiwezekana ujenge viwanda vingine…ujenge hata kumi” amesema Rais Magufuli.

Amemruhusu Dangote auze makaa hayo kwa watu wengine ili Serikali ipate fedha.


Ameiagiza Wizara ya Nishati na Madini kukusanya mapato ya uchimbaji wa makaa hayo kwa Dangote mwenyewe.

Rais amemhakikishia Dangote kuwa, ndani ya siku saba atakuwa amepata kibali cha kuchimba makaa ya mawe kwa ajili ya kiwanda cha saruji kilichopo Mtwara.

Ameiagiza menejimenti ya kiwanda cha Dangote iwasiliane na serikali moja kwa moja badala ya kupitia kwa watu wengine.

Rais amesema, dunia inakwenda haraka sana hivyo uamuzi kuhusu changamoto zilizopo lazima ufanywe haraka ili Tanzania iendane na kasi hiyo.
.

==>Msikilize Rais Magufuli akizungumza alipokuwa kwenye kiwanda cha Cement cha Dangote

Matokeo ya operesheni maalum ya kutokomeza viroba iliyoendeshwa jijini Dar es Salaam kuanzia Machi 1-3, 2017

$
0
0


1.      UTANGULIZI
Kama mnavyofahamu unywaji wa pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zimechangia kwa kiasi kikubwa uchafuzi wa mazingira, kupotea kwa nguvu kazi ya taifa, ajali na vifo zivyosababishwa na unywaji uliokithiri wa pombe hizi, kuongezeka kwa vitendo vya uhalifu na kupotea kwa mapato yanayosababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu. Madhara haya ndiyo yaliyopelekea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa kutoa tamko tarehe 16 Februari, 2017 akiwa Mererani, Mkoani  Manyara kuhusu kusitisha uzalishaji, usambazaji,  uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) kuanzia tarehe 1 Machi 2017; Baadaye tarehe 20/2/2017 na tarehe 28/2/2017 nilitoa maelezo na ufafanuzi kuhusu ufuatiliaji wa agizo hilo.

Ili kutekeleza kwa ufanisi agizo hili serikali imeunda Kikosi Kazi cha Kitaifa kwa ajili ya kuratibu Operesheni Maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya serikali na kuchukua hatua stahiki.

Kikosi Kazi hicho kiko chini ya uratibu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, na kinajumuisha Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Fedha na Mipango,  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Ofisi ya Waziri Mkuu, Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani wa Biashara (FCC), Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Idara ya Uhamiaji na Jeshi la Polisi.

Operesheni maalum ya utekelezaji wa maelekezo ya Serikali inaendelea kutekelezwa nchini kote  kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa na  Wilaya pamoja na Kamati za Mazingira za Mikoa na Wilaya.  Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Makamu wa Rais. Majumuisho ya taarifa ya nchi nzima yatafanywa baada ya Kikosi Kazi kuendesha Operesheni maalum katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii inatokana na kuwepo kwa Viwanda vingi na wasambazaji wengi wa Pombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets).

Ofisi ya Makamu wa Rais iliratibu operesheni maalum  katika Jiji la Dar es Salaam kwa siku tatu mfululizo kuanzia tarehe 01 hadi 03 Machi 2017. Operesheni hii ilitokana na kuwepo  kwa viwanda vingi vinavyozalisha pombe kali za aina mbalimbali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki (sachets)  ambazo hazikidhi vigezo mbalimbali vya Sheria.

Kikosi Kazi maalum katika Operesheni hii  tulikielekeza kufanya yafuatayo:-

i) Kukagua na kuzuia (seize) pombe kali zilizofungashwa katika viroba (sachets) kwenye viwanda na kuorodhesha idadi ya pombe za viroba zilizopo, vifungashio (packaging materials), mitambo mahususi kwa ajili ya kufungashia pombe za viroba na mitambo ya kutengeneza vifungashio;

ii)Kukagua na kuzuia pombe kali zilizofungashwa katika viroba (sachets) kwenye maghala (warehouse /store), na maduka ya jumla (whole sale) na kuorodhesha idadi ya pombe kali zilizofungashwa katika viroba na vifungashio (packaging materials) tupu vilivyopo;

iii)Kubaini iwapo kuna mapungufu yoyote kwenye ufungashaji pombe kali;

iv)Kukagua viwanda vya kutengeneza vifungashio vya sachets kubaini kama kuna ukiukwaji wa Sheria;
 
v)Kukagua uhalali wa vibali na nyaraka za uzalishaji / uendeshaji wa kiwanda / msambazaji husika (mfano vibali na vyeti vya TFDA na TBS, EIA, stempu za kodi za TRA, leseni za biashara, leseni za vileo);

vi)Kukagua nyaraka zinazoonesha kumbukumbu za uzalishaji na nyaraka za usambazaji (sehemu bidhaa zilipouzwa kwa jumla) ili kujua kama uzalishaji na usambazaji unafanyika;

vii)Kufanya tathmini ya Operesheni, kuboresha mapungufu na kuandaa ripoti ya Operesheni; na

viii)Kuchukua hatua yeyote inayolenga kuboresha Operesheni na hali inayojitokeza

2. UKAGUZI ULIVYOFANYIKA
Jumla ya  wakaguzi 58 walishiriki katika zoezi hili na kugawanywa katika  timu tatu (3) kulingana na mikoa ya kikodi ya TRA Dar es Salaam, ambayo ni Temeke, Kinondoni na Ilala. Aidha, timu hizo pia zilijumuisha askari polisi na wanahabari.Katika operesheni hii, TFDA na TBS waliainisha viwanda vinavyozalisha pombe kali, na Manispaa ziliainisha  maduka, maghala  na baa zinazofanya biashara ya pombe kali kinyume na sheria.

Sheria mbalimbali za udhibiti ikiwa ni pamoja na Sheria ya Chakula, Dawa na Vipodozi Sura, 219; Sheria ya Viwango Namba 2 ya mwaka 2009, Sheria ya Vileo ya mwaka 1968 (ilirejewa mwaka 2012), Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura, 191 na Kanuni ya Kukataza Uzalishaji, Uingizaji na Matumizi ya Vifungashio vya Plastiki kufungia Pombe Kali, iliyochapishwa katika Gazette Serikali Namba 76 ya mwaka 2017 zilitumiwa katika kutekeleza Operesheni hii.

3.MATOKEO YA UKAGUZI
Jumla ya viwanda 16 vya kuzalisha pombe kali, maduka ya jumla 18, maghala manne, baa tatu na kiwanda kimoja cha kuzalisha bidhaa za plastiki ikiwemo vifungashio vya plastiki vya kufungashia pombe kali (viroba) vilikaguliwa ambapo matokeo ya ukaguzi ni kama ifuatavyo:-

(i)Jumla ya carton  99,171 za pombe kali zilizofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba) zimekamatwa  Kati yake vyenye ujazo wa mililita 50 ni carton 69,045 na milita 100 ni carton 29,344 za milliita 90 ni 782  Aidha,  chupa zenye ujazo wa mililita 100 ni 10,625.  Thamani yake  ni Tshs bilioni 10.83

(ii) Chapa mbalimbali za pombe kali za virobakama vile Red Wine, Banjuka, Officer’s Cane Spirit, Flash Ginna Dragon  zilikuwa hazikidhi viwango na zilikuwa hazijasajiliwa na TFDA hapa nchini

(iii)Makampuni yote yaliyokamatwa hayana Vyeti vya Tathmini ya Athari kwa Mazingira (EIA). Makampuni mengine yalikuwa hayajalipa kodi TRA na  hayakuwa na cheti cha TFDA na wala   cheti cha TBS.

(iv)Makampuni mawili  yalikutwa yanazalisha na kusafirisha mizigo usiku

(v) Viroba vyenye thamani ya jumla ya Tshs 235 millioni vimekutwa vimefichwa  kwenye maghala ya duka la jumla chini ya jengo la ghorofa (handaki) Kariakoo.

(vi)Baadhi yapombe kali aina mbalimbali zilizofungashwa katika viroba na chupahazikuwa na namba ya matoleo (batch numbers) na tarehe za uzalishaji kwenye lebo (label);

(vii) Baadhi ya pombe kali zilizoonekana wakati wa ukaguzi wa viwanda, maghala, baa na maduka ya pombe kali hazikuwa na stickers sahihi za TRA na nyingine zilikuwa na stickers ambazo zilihisiwa na TRA kuwa  bandia, na hivyo kuhitaji uhakiki zaidi;

(viii) Viwanda saba (7) vilikutwa  vinafanya marekebisho kutokana na kusimamishwa awali  na TFDA kwa kosa la kutoweka kabisa namba za matoleo na tarehe ya kuzalishwa kwa bidhaa au kuweka taarifa husika katika bidhaa chache walizozalisha hadi hapo watakapokidhi masharti ya TFDA;

(ix)Baadhi ya pombe kali kwenye baadhi ya viwanda, maghala, maduka na baa zilikuwa zimefungashwa kwenye chupa zenye ujazo wa chini ya mililita 200 ambavyo ni rahisi kubebeka kama viroba.

4.HATUA ZILIZOCHUKULIWA

Hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na:-
(i) Bidhaa za pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki zenye ujazo mdogo zenye thamani ya takriban Tshs 10.8 billionizimekamatwa na kuzuiliwa (seized) katika store za viwanda, maduka ya jumla, baa na maghala ya wasambazaji;

(ii) Idara ya Uhamiaji imeagizwa kushughulikia raia wa kigeni wasio na vibali vya kuishi nchini ambao walikutwa kwenye baadhi ya viwanda wakati wa ukaguzi;

(iii) Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeelekezwa kuvifuatilia na kuvichukulia hatua viwanda vyote vilivyokaguliwa na kugundulika kufanya kazi bila kuwa na cheti cha Tathmini ya Athari kwa Mazingira (Environmental Impact Assessment) au Cheti cha Ukaguzi wa Mazingira (Environmental Auditing);

(iv)  Mamlaka ya Mapato Tanzania imelekezwa kufuatilia na kuchukua hatua stahiki kwa viwanda na maghala yote yaliyoonekana kuwa na bidhaa zenye stickers za TRA zinazosadikika kuwa bandia.

(v)TFDA na TBS wameelekezwa kufuatilia kwa karibu usitishaji wa ufungashaji wa pombe kali katika mifuko ya plastiki (viroba) na  na chupa za ujazo mdogo chini ya 200mls; na

(vi)Bidhaa zote zilizokamatwa zitabaki hivyo hadi Serikali itakapoelekeza hatua ya baadae.

5.  HATUA ZINAZOFUATA
(i) Kuendelea na na Operesheni hii nchi nzima kwa kasi zaidi. Aidha, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mkoa, Wilaya hadi ngazi ya Vijiji zihakikishe   agizo hili linatekelezwa nchini kote. Wenye viti wa Mitaa na vijiji wahusike pia kwa kushirikiana na kamati hizi. Aidha, Kamati za Ulinzi na Usalama za Mikoa zinawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni Ofisi ya Makamu wa Rais kila mara kwa kufuata maelekezo yatakayotolewa.

(ii) Kufungua kesi mahakamani dhidi ya wafanyabiashara waliokiuka katazo hili ili adhabu kali kutolewa

(iii) Viroba vyote vilivyokamatwa  pamoja na mizigo mingine itabaki chini ya ulinzi kwa sheria zilizotumika na mtu yeyote haruhusiwi kufanya chochote hadi maelekezo zaidi yatakapotolewa na serikali.

(iv) Kwa walioomba muda wa nyongeza kuhamia kwenye teknolojia ya chupa, maombi hayo yatashughulikiwa baada ya Operesheni ya kuondoa pombe kali ambazo zimezalishwa na zinauzwa kinyume cha Sheria.

6.  WITO
Operesheni ya utekelezaji wa kuzuia uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya  pombe kali zilizofungashwa katika vifungashio vya plastiki nchini ni endelevu na ina lengo la kuimarisha afya ya jamii, kudhibiti ukusanyaji wa mapato na hifadhi ya mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo. Katika kutimiza azma ya operesheni natoa wito ufuatao: -

(i)  Kila mwananchi ashiriki katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali  kwa kutoa taarifa zitakazowezesha kubaini wanaokaidi agizo la Serikali la kuzuia uzalishaji, usambazaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki na katika ujazo mdogo. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa taarifa ya wanaohusika na tutahakikisha usiri wa hali ya juu;

a.Kwa atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu anayezalisha, anayeuza au kutumia stempu feki za TRA, atapata zawadi ya shilingi milioni moja;

b.Mtu atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote mwenye kiwanda/mtambo wa kuzalisha pombe za viroba ambao hautambuliki na Serikali au mwenye mtambo wa kutengeneza viroba au kuchapisha chapa za viroba kinyume na sheria, atapata zawadi ya shilingi milioni moja.

c.Mtu yoyote atakayetoa taarifa itakayowezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote mwenye ghala au aliyehifadhi shehena ya pombe za viroba kinyume cha Sheria atapata zawadi ya shilingi laki 5.

d.Mtu yoyote atakayetoa taarifa ya kuwezesha kukamatwa kwa mtu au watu wanaoingiza nchini pombe za viroba kutoka nje ya Tanzania kinyume na Sheria na utaratibu atapata zawadi ya shilingi laki 5.

e.Mtu yoyote atakayetoa taarifa ya kuwezesha kukamatwa na kushtakiwa mtu yoyote anayehamisha au kusafirisha pombe za viroba kinyume na Sheria na maelekezo ya Serikali atapata zawadi ya shilingi laki 5.

Taarifa hizi zitolewe kwa njia ya ujumbe mfupi (SMS) au Whatsapp au kwa kupiga simu kwenye simu nambari 0685 333 444 au kwa Afisa yoyote kwenye Operesheni hii.

(ii)Wafanyabiasharana wananchi waliokuwa wanajihusisha na uzalishaji, usambazaji, uuzaji na uingizaji wa pombe kali zinazofungashwa katika viroba wanatakiwa kutii  maelekezo haya ya Serikali mara moja;

(iii) aasisi za TFDA, NEMC na TBS zinaelekezwa kushiriki kikamilifu katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali ili kufikia malengo yanayotarajiwa; na

(iv) Serikali za Mitaa kupitia Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji / Mtaa na Kata washiriki katika kuwatambua na kutoa taarifa ya watu au kikundi cha watu wanaojihusisha na uzalishaji, usambazaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zilizifungashwa katika viroba; na

(v) Kuhakikisha wafanyabiashara wote waliokamatwa na watakaokutwa wameshindwa kulipa kodi wanalipa kodi stahiki mara moja.

                                                                                       
January Makamba (Mb)
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
5 Machi 2017

NECTA yawasihi wananchi kuendelea kuwapa taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

$
0
0
Na Eleuteri Mangi, MAELEZO
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.

Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.

Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za kazi.

Tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake.

Wema Sepetu Atembelea Godbless Lema Baada ya Kutoka Gerezani

$
0
0
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye hivi sasa amehamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametimiza hadi yake kwenda kuonana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema ambaye amepata dhamani siku ya Ijumaa na kutoka gerezani.

Wema Sepetu juzi alisema atakwenda Arusha kuonana na Mbunge huyo ambaye amekaa ndani kwa zaidi ya miezi mitatu na kusema ni faraja kwao saizi kuona ametoka na kuja kuendeleza mapambano

"Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano, kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho (jana) i'll be in Arusha kuonyesha Solidarity" alisema Wema Sepetu

Baada ya Wema Sepetu kufanikiwa kuonana na Mbunge wa Arusha Gobless Lema amefunguka na kusema saizi anajisikia furaha na amani kuwa ndani ya chama hicho
"Finally Met my brother, aisee Chadema inanipa furaha mimi. Nina amani ya moyo... Ona Venye nacheka .... It was A Good Day...." aliandika Wema Sepetu

Raisi Magufuli: Hata mkeo anaweza asikupende siku nyingine, cha muhimu ni kuchapa kazi

$
0
0
Rais Magufuli leo mkoani Mtwara wakati akiweka jiwe la msingi katika kituo cha kupooza umeme njia ya KV 132 amelipongeza Shirika la Umeme nchini Tanesco na kumpongeza Waziri wa Nishati na Madini, kwa juhudi zake katika kazi.

Rais Magufuli amesema aliamua kumteua Sospeter Muhongo kuwa Waziri kutokana na ukweli kwamba alikuwa anaona uchapaji wake wa kazi kipindi ambacho yeye ni Waziri wa Ujenzi.

"Lengo lililokuwa kwenye ilani ya Uchaguzi kwa mwaka jana ilikuwa asilimia thelathini na kitu nyinyi mkafika mpka asilimia arobaini, na sasa hivi mko zaidi ya asilimia 46 sasa nisipowapongeza nitakuwa mtu mbaya wa moyo mbaya.

" Na mimi na moyo mzuri kweli ndiyo maana nawapongeza wizara pamoja na Tanesco haya matatizo mengine ambayo yanatokea ni kwa sababu tuliingia mikataba ya hovyo huko nyuma, ya kulipia capacity charges ninajua mnayashughulikia na tunajaribu kutafuta pesa za mikopo tulipe haya madeni twende na Tanesco mpya" alisema Rais Magufuli

Mbali na hilo Rais Magufuli alimsihi Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo

"Nilipoteuliwa kuwa Rais sikuona mtu mwingine anayefaa kama Muhongo, nikamrudisha hapa hapa sababu mimi nilipokuwa nikihesabu kilometa za barabara yeye alikuwa anaesabu kilometa za nyaya, kwa hiyo nilifahamu kazi yake na saa zingine ukifanya kazi vizuri unakuwa kama hupendwi pendwi hivi, lakini kwa nini wakupende? Hata mke wako anaweza asikupende siku zingine, wewe chapa kazi" alisisitiza Rais Magufuli

Rais Magufuli aliendelea kusisitiza kuwa katika maisha ya kila siku huwezi kupendwa na kila mtu

"Hata ndugu yako anaweza asikupende, saa zingine hata baba yako au hata mdogo wako anaweza asikupende, huwezi ukapendwa na kila mmoja, hata mitume hawakupendwa na wote na wengine walisulubiwa pamoja na kwamba walifanya mazuri. 

"Kwa hiyo Prof. Muhongo wewe fanyakazi tena usihangaike hata kusoma ile mitandao, mimi sisomagi hiyo mitandao achana nayo watandae huko huko wenyewe wewe chapa kazi" alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya March 6

Kauli ya Rais Magufuli kuhusu Watanzania waliofukuzwa Msumbiji

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 05 Machi, 2017 amemaliza ziara yake ya kikazi ya siku 4 katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Kabla ya kuondoka Mjini Mtwara na kurejea Jijini Dar es Salaam Mhe. Rais Magufuli alifanya mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mashujaa Mjini Mtwara ambapo alisema Serikali ya Awamu ya Tano imejipanga kuhakikisha inasukuma maendeleo ya Mtwara na Lindi kwa nguvu kubwa kwa manufaa ya wananchi.

Alisema Serikali imedhamiria kutilia mkazo juhudi za uendelezaji wa bandari ya Mtwara, ujenzi wa barabara, uimarishaji wa miundombinu ya nishati ya umeme, ujenzi wa viwanda vikubwa na usimamizi mzuri wa shughuli za kilimo ambavyo vitasaidia kukuza uchumi, kuzalisha ajira na kuboresha maisha ya watu.

Mhe. Rais Magufuli aliwapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa mafanikio yaliyopatikana katika soko la korosho lililopita na ameagiza wale wote waliohusika kufuja fedha za wakulima wachukuliwe hatua.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli alisema Tanzania itaendeleza uhusiano na ushirikiano wake mzuri na nchi jirani ya Msumbiji na ametaka suala la wahamiaji haramu wanaoondolewa nchini humo wakiwemo Watanzania lisikuzwe huku akisisitiza kuwa Serikali haiwezi kuwatetea watu wanaoishi katika nchi nyingine bila kufuata sheria.

Kuhusu Mkoa wa Mtwara kufanya vibaya kielimu, Mhe. Rais Magufuli amewataka wananchi wa Mtwara kubadilika kwani juhudi za Serikali kuwapelekea maendeleo hazitakuwa na maana kama wananchi watakuwa hawana elimu.

“Nimeambiwa hapa watu wanapenda sana disco na ngoma, watoto badala ya kusoma wanacheza disco, hapo tunakwenda pabaya” alisisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Mkutano wa Mhe. Rais Magufuli Mjini Mtwara ulidhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi, Waziri wa Nishati na Madini Prof. Sospeter Muhongo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Fedha na Mipango Dr. Philip Mpango, Wabunge na viongozi wa taasisi.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU


Gazeti la MAWIO laibwaga Serikali Mahakamani. Kurejea mtaani Alhamisi wiki ijayo

$
0
0
Hatimaye gazeti la MAWIO lililofutwa na serikali ya Tanzania na kuacha kuchapishwa kwa zaidi ya mwaka mmoja, limerejea mtaani kwa uamuzi wa Mahakama Kuu.

Serikali ililifuta gazeti hilo na kulizuia kuchapishwa kwa njia yoyote ile Januari 15, mwaka jana- 2016.

Uamuzi wa Mahakama Kuu uliotolewa Jumanne , umetupilia mbali amri ya serikali ya “kuliua na kulizika kabisa” gazeti hilo lililokuwa likitoka kila wiki – Siku ya Alhamisi.

Mahakaka Kuu ilisema kuwa amri ya serikali kuliua MAWIO haikuwa sahihi, hivyo “gazeti hilo lilionewa.”

Jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Sakieti Kihiyo, limesema gazeti la MAWIO halikupewa nafasi ya kujitetea kabla ya hatua ya serikali ya kulifuta kutoka orodha ya msajili wa magazeti nchini.

Msajili wa magazeti nchini ni Idara ya Habari Tanzania (MAELEZO).

Jaji Ignas Kitusi ndiye alisoma uamuzi wa Mahakama kuu – kwa niaba ya jopo siku ya Jumanne, wiki iliyopita (Februari 28). Jaji mwingine aliyekuwa kwenye jopo hilo, ni Jaji Ama-Isario Munisi.

Serikali ililifuta gazeti la MAWIO tarehe 15 Januari 2016 baada ya kudaiwa kuandika ilichoita habari na makala za “kichochezi.”

Utawala wa Kampuni ya Victoria Media Services Limited, wachapishaji wa gazeti la MAWIO, uliamua kufungua kesi mahakamani. Hii ni kesi Na. 15 ya mwaka 2016.

Wakili wa MAWIO, Dk. Rugemeleza Nshalla, amesema kuwa hatua ya serikali iliegemea falsafa ya “…Nyonga kwanza na sikiliza baadaye.”

Dk. Nshalla amesema katika mazingira yoyote yale, sharti walalamikiwa wapate nafasi ya kujieleza na kusiklilizwa na mahakama kwanza kabla ya hukumu kutolewa.

Mkurugenzi Mtendaji na Mhariri Mkuu wa gazeti la MAWIO, Simon Mkina amesema alishangazwa sana na hatua ya serikali kufuta alichoita “mdomo wa wananchi.”

“Kufuta chombo hiki au kingine kama hiki, ni kukiri kuwa serikali haipendi kusikia kutoka kwa wananchi…” amesema Mkina

Mkina amesema MAWIO limekuwa gazeti linalozingatia maadili na kufuata weledi wa hali ya juu katika kuandika na kuchapisha habari na makala na kuongeza kuwa limekuwa gazeti pekee linalotoa uwanja mpana kwa wananchi kuandika mawazo yao ili kuchochea uwajibikaji wa viongozi wa serikali.

Mkina amesema kufuatia uamuzi huo wa Mahakama Kuu, MAWIO litarejea mtaani Alhamisi ya wiki hii na kuahidi kuwapa wasomaji wake habari zilizofanyiwa kazi ya ziada.

“Kwa muda wa zaidi ya mwaka mmoja, wakati gazeti halipo mtaani – likiwa limefutwa na serikali, pamoja na kupoteza ajira za watu na kuingia katika hasara kubwa, bado tulikuwa na kazi ya kujiuliza ni wapi tulikosea na je, lini tutapewa haki yetu? Bahati nzuri haki yetu imefika,” aliongeza Mkin.

Uamuzi na hatua ya kulifuta MAWIO, lililokuwa likichapishwa kila Alhamisi, ulitangazwa na Nape Nnauye, Waziri wa habari, vijana, utamaduni, sanaa na michezo.

Tangazo lililotolewa katika gazeti la serikali, Na. 55 la Januari 15, 2016, lilisema serikali inachukua uamuzi wa kulifuta kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kupitia Sheria ya Magazeti ya 1976; sura ya 229 kifungu cha 25(1).

Credit: FikraPevu

Mabasi Happy Nation na Abood yagongana na lori Mlima Kitonga na Kujeruhi Watu 12

$
0
0
Watu 12 wamejeruhiwa na watatu kati yao wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa baada ya kutokea ajali iliyohusisha magari mawili ya abiria na lori moja, katika eneo la Mlima wa Kitonga wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akizungumza  baada ya kutokea kwa ajali hiyo ,  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Julius Mjengi alisema magari yote matatu yaliyohusika kwenye ajali hiyo yalikuwa yakienda jijini Dar es Salaam.

Ameyataja mabasi yaliyohusika kwenye ajali hiyo kuwa ni ya Kampuni ya Happy Nations, Abood na gari moja la mzigo.

Mjengi amesema katika ajali hiyo watu 12 walipata majeraha na watatu kati yao wamefikishwa Hospitali ya Rufaa ya mkoani Iringa kwa matibabu na tisa kati yao walitibiwa na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Kamanda huyo ametaja chanzo cha ajali kuwa ni dereva wa gari la Abood lililokuwa nyuma ambaye aliligonga basi la Happy nations ambalo nalo liligonga gari lilikuwa mbele yake na kusababisha magari yote kuserereka na kutoka pembeni mwa barabara.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL   BEAUTY COSMETICS

Ni kampuni inayotoa bidhaa original na zenye matokeo mazuri bila madhara wala kemiko ya aina yoyote. Bidhaa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda. Tunawaletea punguzo la bei la %10 bidhaa tulizonazo ni kama zifuatazo.
 
     👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 170,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 100,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 110,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @100,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @100,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima kwa vidonge au dawa ya kunywa @150,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11 Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo la ndoa @120,000
12.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
13. kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @100,000/=
15. Kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake @100,000/= NK. [ Bidhaa zetu zote ni garantii pia hakikisha unapewa risiti ununuapo bidhaa kampuni hii popote ulipo utapata huduma zetu]
 
     WASILIANA NASI KWA NAMBA
        {065 9618585 au 0759029968.}
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
                               Karibu sana

Breaking News: Mbunge Tundu Lissu akamatwa na Polisi akitoka mahakamani

$
0
0
Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu baada ya kuachiwa huru na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Lissu aliachiwa leo asubuhi na Hakimu Mkuu Mkazi, Huruma Shahidi baada ya upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili Paul Kadushi kuwasilisha hati ya kuondoa shtaka hilo.

Kadushi aliwasilisha hati hiyo chini ya kifungua namba91 (1) cha makosa ya jinai akionyesha DPP hana haja ya kuendelea na kesi, mahakama ikaridhia na kumuachia.

Muda mfupi baada ya kuachiwa na kutoka nje ya mahakama alikamatwa tena na askari waliokuwapo mahakamani hapo na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi.

Lissu alikuwa anashtakiwa kwamba Januari 11, mwaka huu katika kampeni za uchaguzi jimbo la Dimani aliwashawishi watu wasiridhike na wawe na nia ovu dhidi ya utawala.

Wema Sepetu Adai Kutishiwa Kuuawa

$
0
0
Mwigizaji  na mrembo wa taji la Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu, amedai anapokea vitisho vya kupotezwa kama ataendelea na msimamo wake wa kuitumikia Chadema.

Wema amesema yeye hatishwi na chochote, ameshaamua na hakuna mtu yeyote atakaebadili mawazo yake kwa kuwa anachohitaji ni amani ya moyo wake na kuwa huru kwani alikokuwa aliona nchi ilikuwa inaenda kubaya.

“Ninatishiwa sana, napigiwa simu na kutumiwa  ujumbe mfupi wa maneno kwenye akaunti zangu na kwenye mitandao ya kijamii.

“Mimi siogopi, nimeshaamua na hakuna wa kunizuia kwa hilo, kwani tangu nimeingia katika chama hiki nina amani ya moyo na ninahisi nimetua mzigo mzito  niliokuwa nimeubeba,” amesema Wema.

Amedai kuwa baadhi ya vitisho anavyopata ni matusi ya nguoni ambapo anaweza kupigiwa simu na kutukanwa, wengine kumtumia ujumbe mfupi wakidai watampoteza lakini anauhakika anayeweza kupoteza maisha yake  ni Mungu.

Amesema anajua amepata maadui ila anauhakika ni wachache sana kwani wengi wanamuunga mkono na ukizingatia watu wake wa karibu  wote wako naye bega kwa bega hivyo hana sababu za kuogopa na anauhakika yuko kwenye chama makini kinachojua nini maana ya demokrasia.

“Hakuna mtu muhimu kama mzazi wako kama anakupa sapoti ya kutosha basi hakuna mwingine atakayeweza kuzuia hilo, nashukuru wamejua nini ninakihitaji na ninataka kuonyesha nini nilichokuwa nacho ambacho nilikokuwa hawakukiona,” amesema Wema Sepetu.

Kwa sasa Wema  yuko katika ziara ya kutambulishwa  mikoa yote kwa wanachama na wapenzi wa Chadema na jana ameanzia Arusha kumtia moyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, anayekabiliwa  na kesi ya uchochezi.

VIDEO: Godbless Lema Kampa Ujumbe Mzito Wema Sepetu.....Kasema Akiamua Anaweza Kuwa hata Rais

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wikendi iliyopita alitumia muda wake kufanya mazungumzo na kada mpya wa chama hicho, Wema Sepetu ikiwa ni siku mbili tangu aachiwe kwa dhamana baada ya kukaa gerezani kwa takribani miezi minne.

Lema alimtia moyo na kumpa somo mrimbwende huyo, akimtaka kuwa imara na kujitoa bila kujali ni watu wangapi wanaomuunga mkono.

“Hatuhitaji taasisi kupigania righteousness (haki), tunahitaji watu makini ndani ya taasisi. hauhitaji kampani kubwa sana, unahitaji commitment (dhamira), sacrifice (kujitoa) na determination (uamuzi wa ari).

Lema alimtaka Wema kufikiria vitu vikubwa zaidi na kuwa na ndoto kubwa hata ya kuwa rais wa nchi siku moja.

“Wewe unaweza kuwa kitu cha ajabu, unaweza hata kuota kuwa Rais wa nchi hii… nani ajuaye?” alisema.

Mbunge huyo machachari alimtaka Wema kujichukulia kama mwanamke shupavu na kusahau yaliyopita huku akimtia moyo kuwa hata kesi aliyofunguliwa mahakamani itakwisha pia.

Wema alitangaza kujiunga na Chadema akitokea CCM siku chache baada ya kutoka katika selo za polisi jijini Dar es Salaam alipokuwa akishikiliwa kwa siku zaba akituhumiwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya aina ya bangi. 

Alifunguliwa kesi baada polisi kudaiwa kukukuta msokoto wa bangi nyumbani kwake baada ya kumfanyia upekuzi.

==>Msikilize Lema Akimpa Ujumbe hapo Chini

Makonda Amwaga machozi kanisani.....Ni katika Ibada ya Maombi ya Vyeti na Ajira

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alimwaga machozi mbele ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kimara wakati wa ibada ya Jumapili.

Mkuu huyo wa Mkoa ambaye alikuwa ni mmoja wa watu waliohudhuria ibada ya siku hiyo, alijikuta akibubujikwa na machozi baada ya kupewa nafasi ya kuwasalimia waumini wa kanisa hilo.

Kabla ya kuanza kulia, Makonda alikuwa ametumia muda wake madhabahuni kueleza nia yake ya kuendelea na mapambano ya dawa za kulevya jijini.

Misa ya jana katika Usharika wa Kimara ilikuwa ni mahsusi kwa ajili ya kuombea vyeti vya kuzaliwa, vya masomo na mikataba ya ajira kwa Wakristo wa hapo.

Wakati wa akitoa salamu hizo, Makonda alisema nchi kupitia Dar es Salaam imekuwa ndiyo mlango wa kuingiza na kutoa dawa za kulevya hivyo hatoweza kukaa kimya na kushuhudia watoto na taifa vikiangamia.

“Hizi ni dalili kwamba kazi ninayoifanya katika ulimwengu wa roho inalipa, hakuna aliyemcha Mungu anayeweza kuacha kusimama katika kusudi zuri ambalo Rais wetu ametuelekeza akabaki kupiga kelele hizo ndogondogo.

“Sijui kama unafahamu baba mchungaji wamefikia hatua ya kusema sasa hata mke wangu si raia wa Tanzania…vita hii haipiganwi kienyeji ni lazima uwe umekaa sawasawa,” alisema Makonda.

Alisema historia ya vita vya dawa za kulevya haijawahi kumuacha mtu salama ndani ya Taifa na kwamba hata sasa maswali yamekuwa mengi juu yake.

“Kila aliye jaribu ama alikufa, alifungwa, alipata kila aina ya msukosuko na hatimaye jambo hilo likafanya waovu, wauaji wapate mali kwa njia isiyokuwa halali. Wakapata nguvu na kutengeneza hofu ya kwamba yeyote yule ajaribuye kushughulika nao atashughulikiwa.

“Ndio maana mara kadhaa nimekuwa nikisema ni lazima uwe unamjua Mungu, uwe na uhakika na Mungu unayemwamini na kama huna uhakika usithubutu kuingia kwenye mapambano haya,” alisema.

Aliwabeza wanaoendelea kumjadili na kusema kuwa ukuu wa mkoa si tatizo bali hoja ni namna gani ameitumia nafasi aliyopewa kutekeleza kusudi la Mungu hapa duniani.

“Maswali yamekuwa mengi juu ya njia lakini unapotaka kuwavusha watu kwenda ng’ambo ya pili hakuna mjadala juu ya njia.

“Kuwa mkuu wa mkoa si tatizo, tatizo umeikamilishaje kazi ya Mungu aliyokupa hapa duniani, hapa tuko kwenye vita na vita hii si ya ulimwengu wa mwili bali ni ya ulimwengu wa roho.

“Wananchi wa wamechanganyikiwa, kila wakipita mahala wanaona watoto wanatumia dawa za kulevya na wakiangalia nyuma wanaona wale wauzaji wakubwa hawashikiki, wanatisha, hawajui wapite wapi,” alisema.

Alisema Jiji la Dar es Salaam ndilo lango kuu la uchumi ambapo asilimia 80 ya mapato yanayokusanywa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) yanatoka Dar es Salaam. Hata hivyo limekuwa lango la uchumi mbadala wa kuingizia dawa za kulevya na kuangamiza taifa.

“Rais hawezi kutoa elimu bure kuanzia msingi hadi sekondari ama kuwakopesha watoto wasome halafu wakaendelea kuvuta bangi ama kutumia dawa za kulevya je, ni mzazi gani mwenye akili timamu atakaye furahia hilo, kiongozi gani mwenye ufahamu wa kimungu anayefurahia hilo?

“Mcha Mungu gani anaweza akakaa kwenye mkoa kama huu akaruhusu madawa yapite halafu watoto wanateketea, mcha Mungu anaweza akaruhusu uovu uendelee kutawala halafu anajiita anamtumikia Mungu?

“Mcha Mungu gani huyo…nikisema mtamjua, sikatai dini yake na wala sitaruhusu akatize katika anga la utawala nililopewa, nimepewa bendera ya Tanzania, nimepewa mamlaka nina ‘operate’ kutoka kwenye mamlaka ya juu sana. Nitasimama hadi mwisho kuhakikisha jina lipitalo majina yote linainuliwa,” alisema Makonda huku akishangiliwa.

Mara kwa mara katika mahubiri yake alikuwa akitoa mifano kwa kutumia baadhi ya maneno kutoka katika kitabu cha Biblia na kushangiliwa na waumini wa usharika huo.

“Vita tuliyonayo ni kazi ya mauti na uzima, kuhakikisha tunamtoa mtoto fulani kwenye makucha ya shatani na hii kazi yesu alishaifanya…ukitaka kujua kaifanya wapi soma.

“Shetani anafitinisha, anachonganisha, anaharibu, anateketeza lakini yesu amekuja kurejesha kilichopotea na ndio kazi tunayoifanya sisi,” alisema.

==>Tazama Video hapo chini

Gwajima Azindua Opareshi Mpya ya Kumkabili Makonda

$
0
0
Askofu Mkuu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, amezindua operesheni mpya aliyoipa jina la ‘Operesheni 81Mzizima’ huku akimtaka mtu anayeitwa Daud Bashite ajitokeze hadharani kuthibitisha uhalali wa vyeti vyake.

Hivi karibuni, Askofu Gwajima alihubiri kanisani kwake na kusema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, anatumia vyeti vya mtu anayeitwa Paul Christian, wakati jina lake halisi ni Daud Albert Bashite.

Akizungumza wakati wa ibada kanisani hapo, Ubungo jijini Dar es Salaam jana,  Askofu Gwajima alisema operesheni hiyo mpya ni vita ya mwisho ya kumshikisha mtu adabu.

Alisema, tangu aanzishe hoja hiyo, hadi sasa wahusika hawajajitokeza hadharani kujibu tuhuma hizo, jambo ambalo alisema linaonyesha alichokisema ni kweli.

“Tangu niibue hoja ya Makonda anatumia vyeti vya Daud Albert Bashite, hakuna aliyejitokeza hadharani kukanusha madai yangu.

“Mimi naamini nilisema ukweli kwani kitendo cha kukaa kimya kinaonyesha wazi kuwa ni kweli ninachokisema na kama anabisha, aje hadharani kukanusha akiwa na vyeti vyake na mimi nitakuja na vyangu…

“Kuna baadhi ya watu wananisihi sana niache kumchambua eti wanasema, Gwajima acha, hiyo inatosha.

“Mbona wakati Makonda aliponihusisha na dawa za kulevya hakuna aliyejitokeza kumwambia aache?

“Hii ni vita ya mzizima ya kushikisha adabu iitwayo hold the final battle of good manners,”alisema Askofu Gwajima.

“Hizi ni salamu tu ili ajue kuwa ukimshambulia baba wa imani, hauwezi kubaki salama kwa sababu viongozi wa dini wanapigana vita mbalimbali ikiwamo majini na mashetani, lakini wanashinda kwa jina la Yesu.

“Nina uhakika na nina ushahidi usio na shaka kuhusiana na suala hilo, labda ajitokeze na kuniomba msamaha.

“Nina material na mazagazaga kibao kuhusu Daud Bashite, niseme,” alihoji Gwajima huku waumini wake wakiitikia semaaa.

“Lakini, kwa leo sitaki nimwongelea sana, kwa sababu namwonea huruma, ila ninachotaka kumwambia ni kwamba, usiweke miguu yako kwenye mashine ya kusaga na kukoboa, utageuka sembe.

“Akumbuke kuwa, baba wa familia akiguswa, hata watoto wanaamka, ndicho kilichojitokeza katika maisha yangu kwani baada ya kushambuliwa sana, waumini wameongezeka tofauti na awali.

“Hata wale waliokuwa hawaji kanisani, hivi sasa wanakuja,”alisema. 

Katika mahubiri hayo, Askofu Gwajima alisema kuna wakati Mungu huwainua watu wake kwa makusudi maalumu ili kutimiza kusudio lake.

“Sasa nataka kumwambia kuwa, hizi ni salamu tu, nimerusha ka kipande tu… kuhusu Bashite, lakini kelele kibao.

“Hapa sitaki maigizo wala ngonjera, ninachotaka ni samahani tu, lakini anapaswa kujua kuwa, ukimshambulia baba wa imani, awe askofu, mchungaji, padri au wa dini yoyote, hauwezi kubaki salama, lazima na wewe utashambuliwa tu,”alisema.

Pamoja na hayo, alisema kama ataamua kukaa kimya kama anavyoombwa na baadhi ya watu, akikaa kimya Mungu atawainua watu wengine ili waweze kuzungumza kwa niaba yake.

Kwa mujibu wa Gwajima, hana nia ya kumchafua mtu kwenye suala hilo wala hana mgogoro na hana tatizo, ila aliamua kusema alichokisema kwa sababu alichokozwa.

“Nilichokozwa na siwezi kunyamaza kwa sababu ninachokisema ni kweli na wala hakiwezi kubadilika leo, kesho wala keshokutwa.

“Sijawahi kumpiga mtu bila  kunichokoza na wala sijawahi kumchokoza muumini wangu kanisani, awe muislamu au mtu mwingine.

“Sisi ni wakristo, lakini waislamu ni ndugu na marafiki zetu. Hivyo, basi hakuna mshale utakaoweza kunipiga mimi na vita kwangu haijaanza leo wala jana,”alisema.

Pia, Askofu Gwajima alisema ana historia ndefu inayoanzia Oktoba 21, mwaka 1996 wakati alipoanzisha kanisa lake na kupitia changamoto mbalimbali ambazo alizishinda kwa nguvu za Mungu.

Alisema kwamba, hadi sasa ana makanisa 400 yaliyopo maeneo mbalimbali ndhini na mengine 300 yaliyopo katika nchi mbalimbali duniani.

Katika mabuhiri hayo, Askofu Gwajima alimtolea mfano Erick Shigongo kwa kile alichosema kuwa ni miongoni mwa watu wa kuigwa kwani wanatafuta mafanikio kadri wawezavyo.

“Mtu ukipata mafanikio kunakuwa na chuki kibao zinazotolewa ili wakuvunje moyo badala ya kukaa na kuanza kutafakari ili kuona umewezaje ili wakuige.

“Mwisho naamini utafiti unapingwa kwa utafiti, hivyo basi kauli yangu kwa Daudi itapingwa kwa vielelezo ili na mimi niweze kutoa vielelezo vyangu,” alisema Askofu Gwajima.

Wiki iliyopita Jeshi la Polisi kwa mara nyingine lilizingira nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa kile lilichodai kuwa lilifika kufanya uangalizi.

Vurugu za machinga zajeruhi watu 9 Jijini Mwanza wakiwemo mgambo wa jiji.

$
0
0
Watu tisa (9) wamejeruhiwa katika vurugu wakati wa kuwaondoa wafanyabiashara wadogowadogo sehemu zisizo ruhusiwa wilayani Nyamagana, mkoani Mwanza

Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa w Mwanza DCP Ahmed Msangi imesema kwamba tukio hilo limetokea mnamo tarehe 05.03.2017 majira ya saa15:45hrs katika mtaa wa Buhongwa Center ambapo watu tisa wakiwemo askari mgambo wa jiji la mwanza saba (07), afisa mazingira mmoja (01) na dereva wa jiji mmoja (01) walijeruhiwa.

Amesema watu hao walijeruhiwa kwa kupigwa na mawe sehemu mbalimbali ya miili yao na wafanyabiashara wadogowadogo waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya barabara wakishirikiana na watu wengine waliokua wakishabikia wakati wakiendelea na zoezi la kuwaondoa wafanya biashara wadogowadogo katika maeneo yasiyo ruhusiwa haswa kwenye hifadhi ya barabara ya mwanza kwenda shinyanga.

Aidha, Msangi amesema katika harakati za kudhibiti vurugu hizo askari walifanikiwa kuwakamata watu tisa ambao inadaiwa kuwa walikuwa wakihusika katika vurugu hizo kwa ajili ya mahojiano na uchunguzi utakapokamilika, watafikishwa mahakamani.

Majeruhi wote wapo hospitali ya mkoa ya Sekou Toure wakiendelea kupatiwa matibabu na hali zao inaendelea vizuri.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images