Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

VIROBA Marufuku Kuanzia Leo

$
0
0
Mtakumbuka tarehe 20 Februari 2017 Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa tamko la Serikali la utaratibu utakaotumika kutekeleza agizo la kusitisha utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe kali zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki (viroba)kuanzia tarehe 1 Machi 2017. 

Utekelezaji wa katazo hili utazingatia Ibara ya 8(1) (b) na 14, Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004 na Kanuni zake zilizotungwa kupitia kifungu 230 (2) (f) cha sheria hiyo, na Sheria ya Leseni za Vileo Namba 28 ya mwaka 1968 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2012.

Napenda kusisitiza na kuujulisha umma wa Tanzania kuwa utekelezaji wa maamuzi haya ya Serikali kuhusu usitishaji uingizaji, uzalishaji, uuzaji na matumizi ya vifungashio vya plastiki vya kufungia pombe kali utaanza rasmi tarehe 01 Machi, 2017, katika Mikoa yote ya Tanzania Bara.

Operesheni ya kukagua utekelezaji wa agizo la serikali la usitishaji utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki itaendeshwa nchini kote kuanzia tarehe 2 Machi 2017 kwa kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama na Kamati za Mazingira katika ngazi ya Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji na Mtaa. 

Kamati hizi zitawajibika kuwasilisha taarifa za operesheni wakati na baada ya operesheni hiyo Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na nakala Ofisi ya Makamu wa Rais.

Mnamo terehe 24 Februari 2017, kiliitishwa kikao cha Mawaziri na viongozi wa taasisi za Serikali kujadili mpango wa utekelezaji wa zuio hili. Katika kikao hicho, Wizara na taasisi za Serikali zilipewa majukumu mbalimbali, kama ifuatavyo:

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa kuzingatia umuhimu wa ujazo katika utozaji kodi, imeanzisha mfumo wa stempu za Kielektroniki ili kudhibiti ujazo wakati wa uzalishaji kwa ajili ya kupata mapato stahiki. Aidha, Mamlaka itahakikisha kwamba wazalishaji na waingizaji nchini wa malighafi ya pombe kali (ethanol) wamesajiliwa na kwamba mfumo wa ufuatiliaji wa usambazaji malighafi hiyo unawekwa.

Wazalishaji na waingizaji wa malighafi hiyo watawauzia wale tu ambao wamepewa kibali na pia watatakiwa kutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu (3) ya kiasi cha ujazo kilichouzwa na wateja waliouziwa ambao wamesajiliwa. Uuzaji wa malighafi kwa watengezaji wa pombe kali ambao hawajasajiliwa itakuwa ni kosa la jinai kulingana na Sheria.

Mkemia Mkuu wa Serikali ambaye ndiye msajili wa kemikali za viwandani na majumbani, atasajili makampuni na taasisi zinazoingiza kemikali za viwandani na majumbani nchini ikiwa ni pamoja na Ethanol. 

Msajili atawajibika kutoa taarifa sahihi za majina ya makampuni na watu binafsi na taasisi zinazohusika, kiasi kilichoingizwa na kimetumika, pamoja na madhumuni ya matumizi.

Kulingana na sheria ya Leseni ya Vileo Na 28 ya Mwaka 1968 na marekebisho yake ya mwaka 2012, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika operesheni hii itaratibu zoezi hili katika mikoa, wilaya, tarafa, kata, vijiji na mitaa yote Tanzania bara kwa kuhakikisha kuwa wanaofanya biashara ya pombe ya kawaida na pombe kali (spirit) na watumiaji kinyume na masharti ya leseni za vileo wanakamatwa na kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS), katika operesheni hii watakukagua viwanda vyote vinavyojihusisha na uzalishaji wa vileo na vifungashio vya aina mbalimbali vya kufungia pombe kali kama vimekidhi viwango vya kitaifa Ukaguzi katika viwanda vya plastiki utachunguza kama kuna mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kwa ajili ya pombe kali.

Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki kama haitumiki kwa kuzalisha bidhaa zingine katika kiwanda husika, mwenye kiwanda atalazimika kutoa ufafanuzi wa hatima ya mitambo hiyo. Mitambo ya kuzalisha vifungashio vya plastiki itakayokutwa inaendelea kuzalisha pombe kali na kufungashia vifungashio vya plastiki itakamatwa na kutaifishwa na wahusika watashtakiwa.

Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Watoto na Wazee, kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na mabwana afya katika operesheni hii watatoa elimu kwa umma na kukagua maeneo yote yanayotumika kuhifadhia, kuuza na kusambaza vileo vya aina zote, na kushiriki kukamata vileo ambavyo vipo kinyume cha sheria na kanuni.

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kupitia Idara ya Habari Maelezo, itasaidia kutoa elimu kwa umma kuhusu suala hili. 
 
Wizara ya Mambo ya Ndani, kupitia Jeshi la Polisi, na vyombo vingine vya ulinzi na usalama, itashiriki katika operesheni, ikiwemo kwenye masuala ya inteligensia.

Ofisi ya Makamu wa Rais na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira, wataratibu operesheni.

Kama tangazo letu la tarehe 20/2/2017 lilivyoonesha muda wa nyongeza unaweza kutolewa kwa wazalishaji halali ambao wataonyesha ushahidi wa kuelekea kuhamia kwenye teknolojia ya chupa, na kwamba watahitaji muda mchache kufanya hivyo, na ambao watatimiza masharti kadhaa na kupata kibali maalum kabla ya tarehe 28/2/2017. 

Hadi sasa Serikali imepokea maombi ya wazalishaji 9. Tutangaza kesho iwapo kuna ambao wamekidhi masharti au la. Kanuni za upigaji marufuku pombe hizi zipo tayari.

Pia tumepokea malalamiko kwa wazalishaji wengi kwamba zoezi hili limekuja ghafla na wengine wana malighafi na bidhaa kwenye maghala. Ukweli ni kwamba Serikali ilitoa taarifa Bungeni, kuanzia mwezi Mei 2016, na mara kadhaa baada ya hapo, na rekodi zipo, kuhusu hatua hizi.

 Vilevile, taarifa ya Serikali iliyotangaza kupiga marufuku pombe za viroba ziliripotiwa kwa ukubwa stahiki kwenye vyombo vya habari, ikiwemo kwenye ukurasa wa kwanza wa gazeti la Mwananchi, mwezi Agosti 2016. 

Katika taarifa zote za nyuma, Serikali ilitangaza kwamba hatua hiyo itaanza tarehe 1 Januari 2017. Hatua hizi zimechelewa kwa miezi miwili. 

Iwapo, baada ya taarifa hizo za Serikali, kuna mzalishaji ameagiza malighafi au kutengeneza au kuhifadhi pombe za viroba, au kuchukua mkopo kwa ajili hiyo, atakuwa amefanya hivyo akijua madhara yake.

Mwisho napenda kutoa wito kwa wananchi wote kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa zoezi hili la upigaji marufuku matumizi ya pombe zinazofungashwa katika vifungashio vya plastiki (viroba) kwa kutoa taarifa kwa vyombo husika ili wale wanaozalisha na kuuza au kuhifadhi waweze kuchukuliwa hatua stahiki. Zawadi itatolewa kwa watakaotoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watakaokiuka zuio hili.

OFISI YA MAKAMU WA RAIS
28/02/2017

Waziri Nape: Nitajiuzulu Uwaziri Kama Itabainika Natoka Kimapenzi na Wema Sepetu

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, amesema atajiuzulu uwaziri endapo mtu atampelekea ushahidi wa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii yeyote.

Kauli hiyo ya Nape inakuja ikiwa ni takriban wiki tatu tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aseme watu wanaotetea wale aliowataja hadharani kwa kuhusika na dawa za kulevya wengine ni wapenzi wao.

“Wengine wanaumia tunagusa wapenzi wao, wawasaidie waache si kupiga kelele tu, ujumbe umefika,” alisema Makonda katika moja ya mikutano yake.

Ingawa katika mkutano huo Makonda hakumtaja mtu kwa jina, lakini aliitoa kauli hiyo siku chache baada ya Nape kupinga mfumo wake wa kutaja majina ya watu hadharani, hususani wasanii na kuwatuhumu kuhusika na dawa za kulevya.

Nape alisema kuwataja watu bila ushahidi ni kuwachafulia majina yao waliyoyatengeza kwa muda mrefu.

Mbali na Nape, Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Msukuma (CCM), alizungumza mara kadhaa bungeni akimpinga Makonda kwa mfumo wake aliokuwa akitumia, kutaja majina ya watu wanaojihusisha na dawa za kulevya.

Akizungumza katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na kituo cha luninga cha ITV juzi, Nape alieleza kushangazwa na kitendo cha kuhusishwa kuwa na mahusiano na wasanii.

“Ila kama mtu ana ushahidi alete hapa mezani aseme Nape hili unalofanya, unafanya kwa sababu una uhusiano, na mtu akileta najiuzulu uwaziri.

“Hii ni katika watu ambao wanakosa hoja halafu wanasingizia hoja ambazo hazina msingi, ningefurahi mtu akisema Nape hana sababu ya kutumia busara, twende na hoja hii nyingine ni upuuzi,” alisema Nape.

Akizungumzia kuhusu kutajwa kuhusishwa kuwa na mahusiano ya kimapenzi na msanii nyota wa filamu, Wema Sepetu, Nape alisema wasanii wengi ni wadogo zake akiwamo Wema.

“‘Majority’ ya wasanii hawa ni wadogo zangu. Wamezungumza habari ya Wema, sasa nieleze ukweli kwamba baba yake, mzee Sepetu (Isack) na baba yangu (Moses Nnauye) ni mtu na kaka yake, kwa hiyo Wema ni mdogo wangu sana sana.

“Mama yake anatoka Singida, mama yangu naye anatoka Singida, ni mtoto mdogo lakini mtu akiamua apoteze ‘direction’ (mwelekeo) ya mjadala anaweza kuja na hoja nyingi sana.

“Mimi nimeanza kufanya kazi na wasanii, nimefanya nao kazi kwa miaka 16, hii ya uwaziri imekuja juzi tu. Pia msisahau hawa wasanii tuliwatumia kwenye kampemi ya CCM, mimi ndiyo nilikuwa Katibu wa Uenezi wa CCM.

“Ukizungumza burudani, hamasa na ‘publicity’ mimi ndio nashughulika nayo, hivyo kuwaingiza wasanii kwenye kampeni haikuwa kazi rahisi, sasa nikiwa nao karibu dhambi inatoka wapi, maana ndio nilipewa dhamana ya kuwasaidia. Hizi hoja zingine ni za kijinga kabisa,” alisema Nape.

Pamoja na mambo mengine, Nape alisema utaratibu uliokuwa ukitumiwa na Makonda kwa kutaja majina ya watu hadharani una madhara makubwa kwani unajenga chuki katika jamii.

Nape ambaye pia ni mbunge wa Mtama mkoani Lindi, alisema hakuna mahali popote duniani vita ya dawa za kulevya ilishinda kwa kupiganwa hadharani.

 “Tutajenga chuki kubwa sana kwenye jamii kama tukianzisha utaratibu wa kila mtu anasimama anamtaja mtu hadharani, ukishamtaja anaandikwa kwenye mitandao.

“Nchi itaingia kwenye vurugu kubwa bila sababu na wale wenye chuki zao watapitia hapo kuanza kutajana majina, tukitajana majina hadharani, hii vita hakuna mahali walipigana hadharani wakashinda popote duniani, haipo,” alisema.

Aidha alisema watu wasihukumiwe bila kosa bali haki itendeke na sheria na taratibu zifuatwe.

“Namshukuru Rais (Dk. Magufuli) ametumia busara namna ya kuli-handle (kulishughulikia) hili suala, amemteua kamishna na amemkumbusha waziri mkuu kwamba yeye ndie mwenyekiti wa hii kamati na mawaziri wako ndio wajumbe, sasa ameweka vita hii katika chombo salama.

“Pia namshukuru kamishna mwenyewe kasema tusitaje majina hadharani, lakini tufuate sheria na akasema hakuna jiwe litabaki juu ya jiwe, tutahakikisha tunasimamia sheria,” alisema Nape.

Adhabu za kikatili mashuleni zapigwa marufuku

$
0
0
Serikali imepiga marufuku tabia ya baadhi ya waalimu kutoa adhabu kali na za kikatili kwa wanafunzi na badala yake waalimu wameelekezwa kutoa adhabu kulingana na taratibu na sheria zilizowekwa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. George Simbachawene kupitia hotuba yake iliyosomwa na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais katika uzinduzi wa ripoti ya elimu ya msingi nchini amesema, kumekuwa na tabia ya baadhi ya waalimu kutoa adhabu kinyume cha taratibu.

Naye Mratibu wa Mtandao wa Elimu nchini ambao ni wasimamizi wa utafiti huo Bi. Cathrene Sekwao na mtafiti Bw. Jacob Kateri amesema wameamua kufanya utafiti huo ili kuweza kujua hali ya elimu ikoje ili serikali iweze kuona nini kifanyike kuboresha sekta ya elimu ambapo pia wameitaka serikali kupitia mapendekezo yao.

Mahakama Kuu Kuamua Dhamana ya Lema Ijumaa Hii

$
0
0
Hatima ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), itajulikana Ijumaa wiki hii baada ya shauri hilo kurudishwa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa utekelezaji wa uamuzi wa Mahakama ya Rufaa.

Hatua hiyo imekuja baafa ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa Tanzania kufuta rufaa mbili za Mkurugenzi wa Mashitaka(DPP), dhidi ya  mbunge huyo juzi mjini hapa.

Mmoja wa mawakili anaomtetea mbunge huyo, Adam Jabir, alisema shauri hilo litaamuliwa Machi 3, mwaka huu mbele ya Jaji Salma Maghimbi kutokana na rufaa ya Jamhuri namba 135 ya mwaka jana, inayopinga uamuzi wa Novemba 11, mwaka jana wa Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha kumpa Lema haki ya dhamana.

Novemba 11 mwaka jana, Wakili Mwandamizi wa Serikali Paul Kadushi, alisimama wakati hakimu huyo akijiandaa kuandika masharti ya dhamana na kuieleza mahakama hiyo kuwa wameshasajili notisi ya kusudio la kukata rufaa Mahakama Kuu wakipinga uamuzi wa hakimu huyo kumpa Lema dhamana.

Hata hivyo,uamuzi huo wa dhamana haukuweza kutekelezwa kwa sababu ya nia ya kukata rufaa waliyoitoa mawakili hao wa Serikali.

Hakimu Kamugisha alishindwa kuendelea na mahsarti ya dhamana kwa mshitakiwa huyo ambapo,alikubaliana na upande wa Jamhuri na kusema kuwa notisi ina hadhi sawa na maombi ya rufaa yaliyowasilishwa Mahakama Kuu hivyo mwenendo na uamuzi wake utasimama mpaka uamuzi utakapotolewa na Mahakama Kuu.

Januari 4 mwaka huu, Jaji Maghimbi alitarajiwa kusikiliza na kutoa uamuzi kuhusiana na dhamana ya Lema ila ilikwama baada ya  mawakili wa Serikali kukata Rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania,kupinga Jaji huyo  kusikiliza rufaa yao wenyewe.

Jaji Magimbi alitarajiwa kutoa uamuzi juu ya rufaa iliyowasilishwa na upande wa Jamhuri wakipinga Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kumpa Lema haki ya dhamana.

Uamuzi huo ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu na wakazi wengi wa jiji la Arusha,hasa ikizingatiwa mbunge huyo anashikiliwa katika mahabusu ya Gereza Kuu la Kisongo kwa zaidi ya miezi mitatu,tangu akamatwe na polisi nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Novemba 2, mwaka jana.

Aidha uamuzi huo ulikuwa unatarajiwa kutoa tafsiri ya kisheria ya notisi ya nia ya kukata rufaa iliyowasilishwa na na mawakili hao wa Jamhuri,notisi iliyosababisha Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi kutokuendelea na hatua ya kuweka masharti ya dhamana.

Akiahirisha uamuzi huo mahakamani hapo,Jaji huyo alisema kuwa mikono yake imefungwa na hawezi kusikiliza na kutoa uamuzi  kutokana na mawakili wa Serikali,kusajili nia ya kusudio la kukata rufaa Desemba 30 mwaka jana,katika Masijala ya Mahakama ya Rufaa Tanzania iliyopo mkoani hapa, kupinga asisikilize rufaa hiyo.

Awali kabla ya mawakili wa serikali kukata rufaa Mahakama ya Rufaa Tanzania kupinga kusikilizwa kwa rufaa yao Mahakama Kuu, Jaji Maghimbi,aliwataka mawakili wa Jamhuri  kuwasilisha hoja zao za rufaa Disemba 29,huku mawakili wa Lema wakitakiwa kujibu hoja hizo Disemba 30 kabla ya mahakama hiyo kutoa uamuzi wa rufaa hiyo jana.

Lema anakabiliwa na kesi mbili za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kesi namba 440 na 441.

Wasanii Wamkaanga Wema Sepetu.......Wakanusha Madai ya Kuidai CCM

$
0
0
Baadhi  ya wasanii wa kundi la Mama Ongea na Mwanao, waliokuwa katika kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka 2015 za mgombea mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mama Samia Suluhu, wamekanusha madai ya kutolipwa wala kukidai chama hicho madeni yoyote wakati na baada ya kampeni hizo kumalizika.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam leo, Makamu Mwenyekiti wa muda wa kundi hilo, Yobnesh Yusuph maarufu Batuli, alisema madai hayo si kweli kwani wasanii wote walilipwa na mikataba wanayo.

“Nikiwa kama Makamu Mwenyekiti wa ‘group’ hili la Mama Ongea na Mwanao kwa muda, ni kweli kuna uvumi ulienea katika mitandao kwamba wasanii tulioshiriki kampeni na Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu hatujalipwa, si kweli nakanusha taarifa hizo kuwa si za kweli.

“Ingawa kwenye msafara wa mamba kenge hawakosekani, wapo wanaoshawishiwa kulichafua kundi letu, kumchafua Makamu wa Rais na kuichafua CCM, mimi nakataa, wasanii wote tulilipwa na mikataba ipo.

"Haiwezekani wewe staa mkubwa unakaa mbele ya vyombo vya habari unaongea uongo kwamba wasanii hatujalipwa wakati wewe ndiyo ulikuwa unawalipa hicho kitu hakiwezekani,” alisema Batuli aliyekuwa ameongozana na baadhi ya wasanii wa kundi hilo.

Hivi karibuni msanii nyota wa filamu na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu ambaye alitoka CCM na kuhamia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema wasanii hao wanadai malipo yao ambapo hakutaja kiasi wanachodai na kwamba wamekuwa wakizungushwa pindi wanapoulizia madeni hayo.

Rais Magufuli Asali Ibada Ya Jumatano Ya Majivu Katika Kanisa Katoliki La Mtakatifu Petro (St Peter) Oysterbay Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokia ya  Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa wakiwatakia heri ya Masista katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.




Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akijiandaa Kumpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.
Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akimpaka majivu kichwani Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa katika Ibada hiyo ya Jumatano ya majivu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa mara baada ya Ibada hiyo ya jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Taasisi ya TWAWEZA Yatoa Ripoti Kuhusu hali ya Chakula nchini.

$
0
0
Utangulizi
Wiki na miezi iliyopita kumekuwepo na mijadala mizito ya kisiasa na kitaifa juu ya masuala ya upungufu wa chakula Tanzania.

Taaarifa za upungufu wa chakula mwanzoni zilikataliwa na viongozi wa juu wa serikali lakini baadae walikiri kuwepo kwa upungufu wa chakula nchini. Mwishoni mwa mwezi Januari 2017, Waziri wa Chakula, Mifugo na Uvuvi, Dk. Charles Tizeba aliliambia bunge kwamba utafiti uliofanywa na Wizara kwa kushirikiana na wadau kadhaa 1 , umegundua kwamba Wilaya 55 (kati 169 za Tanzania Bara na Visiwani) zilikumbwa na njaa, na tani “35,491 za nafaka zinahitajika kusambazwa kati ya mwezi wa pili na wa nne mwaka 2017 ili kukabiliana na upungufu huo uliowakumba watu 1,186,028” 2 katika Wilaya hizo.

Waziri Tizeba alilalamikia kupanda kwa bei za vyakula katika maeneo mengi na alisema hii inasababishwa na wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia mianya ya njaa, pamoja na uhitaji mkubwa wa mahindi katika nchi jirani. Matokeo yake ni kusababisha bei za ndani kupanda. Aliongeza kwamba “Serikali imeanza kuchukua hatua kudhibiti hali hiyo ambayo ni pamoja na kutoa chakula kutoka hifadhi za taifa na kuuza kwa bei nafuu katika maeneo yaliyo athirika.”

Sintofahamu hii juu ya hali ya chakula nchini imetokea katika kipindi ambacho uchumi wa Tanzania umekua kwa kasi nzuri ya asilima saba kwa mwaka. Lakini ukuaji huu haujafanikiwa kuondoa umasikini kwa kiwango kilichotarajiwa na wengi. Asilimia 68 ya wananchi bado wanaishi chini ya kiwango cha umasikini cha $1.25 kwa siku 3 . Pamoja na hayo kiwango cha udumavu kimeendelea kuonekana kwa watoto chini ya miaka 5 4 , ukiachilia mbali mafanikio madogo yaliyopatikana katika miaka ya karibuni kwenye utoaji wa lishe nchini. Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Tanzania (NBS) na UNICEF wanakadiria kuwa robo tatu ya watoto wote wa Tanzania asilimia 74) wanaishi kwenye umasikini mkubwa 5 .

Muhtasari huu unawasilisha takwimu za maoni ya wananchi na uzoefu wao katika hali ya upungufu wa chakula na sababu zake. Ni kaya ngapi na jamii zipi ambazo zimekumbwa na njaa? Ni vyakula vipi vilivyo adimu kupatikana? Na ni kwa namna gani bei za vyakula zimepanda ikilinganishwa na miezi michache iliyopita?

Takwimu za muhtasari huu zimetokana na utafiti wa Twaweza wa Sauti za Wananchi. Sauti za Wananchi ni utafiti wenye uwakilishi mkubwa unaotumia simu za mkononi. Uwakilishi huu ni wa Tanzania bara. Maelezo zaidi juu ya utafiti huu yanapatikana katika tovuti ya www.twaweza.or.tz/sauti. Takwimu za muhtasari huu zilikusanywa katika awamu ya pili ya kundi la pili la Sauti za Wananchi.

  1. Wahojiwa 1,800, awamu ya 13 ya kupigiwa simu kwa kundi hili la wahojiwa, kati ya tarehe 14 - 26 Septemba 2016.
  2. Wahojiwa 1,610, awamu ya 16 ya kupigiwa simu kwa kundi hili la wahojiwa, kati ya tarehe 9 - 15 Februari 2017.
Matokeo makuu ni:
  • Kaya nane kati ya kumi (asilimia 80) zimeripoti kwamba kipato chao hakikidhi mahitaji yao ya kila siku.
  • Kaya nane kati ya kumi (asilimia 79) huweka akiba ya chakula kwa ajili ya kijitosheleza ifikapo vipindi vya njaa.
  • Wahojiwa wengi wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wanaripoti upungufu wa chakula katika maeneno wanayoishi
  • Bei ya mahindi imepanda mara mbili katika kipindi cha miaka miwili na kusababisha ongezeko la bei katika bidhaa.
  • Kaya saba kati ya kumi (asilimia 69) zilihofia kukumbwa na njaa katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
  • Hali ya upungufu wa chakula imekua mbaya zaidi katika kipindi cha mwezi wa Septemba mwaka 2016 hadi Februari, 2017.
Mambo nane muhimu kuhusu hali ya chakula Tanzania

Jambo la 1: Kaya nane kati ya kumi zimeripoti kwamba kipato chao hakikidhi mahitaji yao ya kila siku.

Mwezi Septemba mwaka 2016 kaya nane kati ya kumi (asilimia 80) ziliripoti kuwa na kipato kisichokidhi mahitaji yao ya kila siku. Takwimu hizi zinatofautiana kidogo katika kaya za mijini na zile za vijijini au kati ya kaya masikini na kaya tajiri.

Kielelezo cha 1: Je kipato kinachopatikana katika kaya kinatosha kukidhi mahitaji ya kila siku ya nyumbani?

1.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba 2016)

Kaya tano kati ya sita (asilimia 85) zinasema kwamba kipato kinapopungua wanalazimika kubana matumizi. Idadi ndogo inasema watakopa bidhaa (asilimia 6) na wengine huripoti kwamba watakopa fedha zaidi (asilimia 2).

Walipoulizwa kukadiria ni kiasi gani cha fedha kingetosha kwa ajili ya mahitaji ya kaya ya kila siku, wastani wa makadirio yote yalikua shilingi 1,777 kwa mwanakaya au shilingi 10,662 kwa kila kaya 6 . Kwa mwanakaya anaeishi mjini makadirio yalikuwa juu kidogo (shilingi 2,247) kuliko kijijini (shilingi 1,579). Makadirio pia yalikuwa makubwa zaidi kutoka kwenye kaya zenye uwezo (asilimia 20 ya waliokuwa na utajiri wa juu sana - Shilingi 2,304) ukilinganisha na kaya masikini (asilimia 20 ya waliokuwa na umasikini wa chini kabisa - Shilingi 1,577).

Jambo la 2: Wananchi tisa kati ya kumi wanaona ni jukumu lao wenyewe kuhakikisha wana fedha za kutosha za kukidhi mahitaji ya kaya zao

Idadi kubwa ya wananchi (asilimia 87) wanasema iwapo watakosa fedha za kukidhi mahitaji ya chakula kwa ajili ya familia zao, hawatarajii watu wengine kulichukua jukumu hilo. Hata hivyo, asilimia 17 ya wanawake na asilimia 9 ya wanaume wangetarajia msaada kutoka nje.

Kielelezo 2: Iwapo ungekuwa huna pesa za kukidhi mahitaji ya chakula kwa ajili ya familia yako pamoja na kaya yako, je unadhani ni jukumu la mtu kukusaidia au ni jukumu lako mwenyewe?

2.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba 2016)

Miongoni mwa wale wananchi wachache (asilima 13) wanaofikiri kwamba ni jukumu la mtu mwingine kuwasaidia katika hali hiyo, nusu yao (asilimia 49) wamesema ni wajibu wa serikali kutoa msaada. Idadi ndogo wamesema ni wajibu wa wanandugu (asilimia 36) au marafiki na majirani (asilimia 7).

Jambo la 3: Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kaya moja kati ya nne imepokea fao, faida au pesa kutoka kwenye miradi ya serikali

Katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kuanzia mwezi wa tisa 2015 mpaka mwezi wa tisa 2016, asilimia 25 ya kaya zimepokea fao, faida au pesa kutoka katika vyanzo vifuatavyo:
  • Sare za shule, kadi ya matibabu, chakula na kadhalika kutoka kwenye Mpango wa Watoto Wanaoishi kwenye Mazingira Magumu
  • Nafaka za bure kutoka kwa viongozi wa kijiji na Wakala Wa Taifa Wa Hifadhi Ya Chakula (NFRA)
  • Chakula cha shule kinachotolewa na Mpango wa Chakula Shuleni
  • Kazi za jamii zinazotolewa na Tanzania Social Action Fund (TASAF)
  • Pesa zinazotolewa na TASAF kwa ajili ya kunusuru kaya masikini
  • Vocha za mbolea/mbegu zinazotolewa na Mpango wa Taifa wa Ruzuku na Kilimo
  • Malipo ya mafao kutoka Mfuko wa Pensheni wa Taifa (NSSF)
  • Malipo ya mafao kutoka Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF)

Kielelezo 3: Mafao au faida zilizopokelewa ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita
(Asilimia ya kaya zinazopokea mafao haya)
Screenshot from 2017-03-01 12:03:22.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba 2016)

Jambo la 4: Kaya nane kati ya kumi huweka akiba ya chakula

Kaya nane kati ya kumi (asilimia 79) zimeripoti kwamba wana hifadhi chakula kwa ajili ya dharura au kuepukana na njaa. Wananchi wengi zaidi wa vijijini huhifadhi (asilimia 87) kuliko wa mijini (asilimia 61) na kaya masikini huhifadhi kuliko kaya tajiri. Uhifadhi wa chakula pia uko juu kwa kaya ambazo hutegemea zaidi kilimo kama sehemu kubwa ya kipato chao (asilimia 92) kuliko kaya ambazo hutegemea vyanzo vingine vya mapato kama vile biashara au ajira (asilimia 49).

Kielelezo cha 4: Je, kaya yako huhifadhi chakula kwa ajili ya matumizi wakati wa dharura au njaa?
(Asilimia iliyojibu ndiyo)
4.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 16 (Februari 2017)
Jambo la 5: Wahojiwa wengi wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) wanaripoti upungufu wa chakula katika maeneo wanayoishi.

Asilimia 78 ya wahojiwa wa Sauti za Wananchi waliripoti kuwa upungufu wa chakula ulikuwepo katika maeneno wanayoishi. Hali hii ilijitokeza zaidi kati maeneo ya vijijini (asilimia 84 wakisema kuna upungufu wa chakula) kuliko mijini (asilimia 64 wakisema hivyo).

Kielelezo cha 5: Je eneo unapoishi lina upungufu wa chakula?
(Asilimia iliyojibu ndiyo)
5.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 16 (Februari 2017)

Jambo la 6: Bei ya mahindi imepanda sana katika kipindi cha miaka miwili.

Kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania 7 bei ya mahindi imepanda kutoka shilingi 400 kwa kilo mwanzoni mwa mwaka 2015 mpaka shilingi 852 kwa kilo kufika mwezi Desemba 2016. Bei ya mahindi imepanda kwa kiwango cha juu sana ikilinganishwa na kiwango cha mfumuko wa bei wa kipindi hiki, Pamoja na mfumuko wa bei, hii inawasilisha kuongezeka mara mbili zaidi kwa bei ya mahindi katika kipindi hiki 8 .

Wahojiwa wa Sauti za Wananchi wameripoti kuwa bei hizi zimeongezeka zaidi baada ya Benki ya Tanzania kutoa takwimu zake hadi kufikia 1,253 kwa kilo moja. Hata hivyo, ni lazima ifahamike pia kwamba takwimu hizi zimejikita katika bei zilizoripotiwa kwenye masoko ya ndani, wakati takwimu za Benki ya Tanzania zimejikita katika bei halisi za wasambazaji wa jumla.

Kielelezo cha 6: Bei ya mahindi kwa kilo
6.png
Chanzo cha takwimu: Ripoti za Benki Kuu ya Tanzania (Januari 2015 – 2017) Sauti za Wananchi - Awamu ya 16 (Februari 2017)

Kaya mbili kati ya tatu (asilimia 68) zimeripoti upungufu wa mahindi katika maeneo yao kuliko upungufu wa mchele ama maharage (asilimia 4). Uchambuzi wa takwimu hizo za bei toka Benki kuu ya Tanzania zinaonesha kwamba bei za mchele na maharage hazijapanda sana katika kipindi hicho hicho cha miaka miwili tangu mwanzoni mwa 2015. (haijaoneshwa kwenye kielelezo.)

Jambo la 7: Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita, kaya saba kati ya kumi zimepata hofu ya kupungukiwa na chakula.

Katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita (Novemba 2016 mpaka Februari 2017) kaya saba kati ya kumi (asilimia 69) zimepata hofu ya kupungukiwa na chakula.
Matokeo pia yanaonesha kwamba:
  • Asilimia 50 ya wananchi wamelazimika kupunguza idadi ya milo kutokana na kukosa fedha au rasilimali zingine.
  • Asilimia 51 wamepungukiwa na chakula au.
  • Asilimia 50 wamelazimika kushinda na njaa kabisa.
Katika hali zote hizi, kiwango cha upungufu wa chakula ni mkubwa katika sehemu za vijijini
kuliko mjini.

Kielelezo cha 7: Ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita ....
(Asilimia iliyojibu ndiyo)
7.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu 16 (Februari 2017)

Jambo la 8: Hofu ya kupungukiwa na chakula imeongezeka sana kati ya Septemba 2016 na Februari, 2017

Mwezi Septemba mwaka 2016, asilimia 45 waliripoti hofu ya kupungukiwa na chakula. Hata hivyo, ilipofika Februari 2017, idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia asilimia 65 wakiripoti hofu ya kupungukiwa na chakula. Ongezeko hili katika kipindi cha miezi mitano ni kubwa.

Mwezi Septemba 2016, kaya nne kati ya kumi (asilimia 43) ziliripoti kuwa, katika kipindi cha miezi kumi na mbili ya awali, zilikumbwa na upungufu wa chakula. Miezi mitano baadae, (Februari 2017) kaya tano kati ya kumi (asilimia 51) ziliripoti kukumbwa na upungufu mkubwa wa chakula kati ya Novemba 2016 na Februari 2017.

Jedwali la 8: Upungufu wa chakula mwezi Septemba 2016 na Februari 2017 (Asilimia iliyojibu ndiyo)
Je, ndani ya siku saba zilizopita, je ulipata hofu yoyote kwamba kaya yako haitokuwa na chakula cha kutosha?

8.png
Chanzo cha takwimu: Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 13 (Septemba 2016) Utafiti wa Sauti za Wananchi - Awamu ya 16 (Februari 2017)

Pamoja na hayo, katika kipindi cha miezi sita kabla ya Septemba 2016, kaya moja kati ya tano (asilimia 21) iliripoti kwamba mtu mmoja ndani kaya hiyo alikuwa amelala njaa kutokana na ukosefu wa chakula.

Katika kipindi cha miezi mitatu kabla ya Februari 2017, kaya moja kati ya tatu (asilimia 35) iliripoti kupatwa na hali hiyo.

Katika matukio yote matatu, takwimu zinaonesha kuongezeka kwa hali ya upungufu wa chakula kwa kiasi kikubwa kati ya Septemba 2016 na Februari 2017.
 Hitimisho

Takwimu zinazowasilishwa katika muhtasari huu zinashabihiana na tamko la Wizara ya Chakula, Mifugo na Uvuvi, pamoja na wadau wake, kwamba kwa sasa kuna tatizo la upungufu mkubwa wa chakula nchini Tanzania. Aidha, takwimu zilizotolewa na Benki Kuu ya Tanzania zinaonesha kwamba bei ya mahindi imepanda kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita. Habari zilizoelezwa na wananchi ni kwamba upungufu wa chakula ni tatizo kubwa kwa sasa na hii ilijidhihirisha pale ambapo wahojiwa wengi wa Sauti za Wananchi (asilimia 78) waliripoti upungufu wa chakula katika maeneno waliyokuwa wakiishi.

Hali ya upungufu wa chakula imeonekana kuwa mbaya zaidi katika miezi ya hivi karibuni. Hii inajidhihirisha pale ambapo kaya zilizoripoti kupata hofu ya kukosa chakula zilipanda kutoka asilimia 45 hadi asilimia 65 kati ya Septemba 2016 na Februari 2017. Vivyo hivyo, idadi ya kaya zilizopungukiwa na chakula ziliongezeka kutoka asilimia 43 Septemba 2016 hadi asilimia 51 Februari 2017. Kaya ambazo zilikuwa na angalau mtu mmoja aliyeshinda siku nzima bila kula nazo ziliongezeka kutoka asilimia 21 hadi asilimia 35 katika kipindi hicho hicho.

Upungufu huu wa chakula umesababishwa kwa kiasi fulani na umasikini wa kipato unaofanya kaya maskini ziwe katika hali tete. Kaya nane kati ya kumi ziliripoti Septemba 2016 kwamba kipato chao hakikidhi mahitaji yao ya kila siku, na walihofu kupungukiwa na chakula katika kaya zao.

Tamko la serikali la hivi karibuni kwamba kuna upungufu wa chakula Tanzania ni jambo linalotia matumaini. Serikali inatambua kuwa jitihada zinahitajika kukusanya na kugawa chakula katika sehemu zenye uhitaji mkubwa. Hata hivyo, hata baada ya uhaba huu kupunguzwa, tatizo la msingi – sintofahamu ya mara kwa mara kuhusu uhakika wa kupata chakula – bado litakuwepo. Tunahitaji utafakari kwa kina namna tutakavyotatua tatizo sugu la umasikini wa kipato ambazo zimewaacha wananchi wengi katika hali tete isiyo na kikomo.

Makato Bodi ya Mikopo: TUCTA Yatoa Siku 14 kwa Serikali Kuwarudishia Wafanyakazi Fedha Walizokatwa Kinyume na Mkataba wa 8%

$
0
0
Shirikisho  la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), limetoa siku 14 kwa Serikali kurejesha fedha za makato ya mikopo ya asilimia 15 zilizokatwa kikamakosa kupitia Bodi ya Mikopo, likisema sera inayotumika imejaa utata.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Rais wa TUCTA, Tumaini Nyamhokya, alisema  Serikali lazima irekebishe sheria hiyo ya Bodi ya Mikopo kupitia Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi Stadi kutokana na kuwajumuisha wafanyakazi wote katika makato ya asilimia 15 wakati imetungwa hivi karibuni.

Nyamhokya alisema kuwa wakati sheria hiyo inatungwa, baadhi ya wafanyakazi walikwishaingia makubaliano mengine ya kukatwa asilimia 8 katika mishahara yao.

Alisema wamesikitishwa na hatua hiyo ya Serikali, ingawa wanaamini haitalifumbia macho suala hilo.

Aidha Nyamhokya alisema kuna milolongo mingi ya makato katika mishahara ya wafanyakazi ambayo ni zaidi ya asilimia 57, huku pia mazingira ya kufanyia kazi yakiendelea kuwa magumu na Serikali ikishindwa kuongeza mishahara wala kuwapandisha vyeo kwa muda mrefu.

Aidha alisema kwa kawaida mtumishi mwenye mkopo serikalini analipa kwa makubaliano maalumu, lakini mtindo wa bodi hiyo kukusanya fedha za wanufaika kabla ya kuanza kwa sheria husika kumeleta athari kwa watu wengine.

Rais Magufuli Amteua Mama Salma Kikwete Kuwa Mbunge

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamis ya March 2

Jeshi la Polisi Arusha lakamata bunduki 10 na risasi 59

$
0
0
Na Rashid Nchimbi, Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limefanikiwa kupata jumla ya bunduki kumi za aina nne tofauti zikiwemo Sub-Machine Gun sita baada ya operesheni ya wiki mbili iliyoanza tarehe 15.02.2017 katika wilaya ya Ngorongoro.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jana asubuhi, Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha Naibu Kamishna (DCP) Charles Mkumbo alisema silaha hizo zilipatikana katika vijiji vya Olorieni Magaiduru, Oldonyosambu na Sale vilivyopo katika tarafa za Loliondo na Sale.

Alisema mafanikio hayo yalitokana na taarifa fiche ambazo zilibainisha kwamba kuna baadhi ya watu wanamiliki silaha za kivita hivyo mahojiano makali baina ya askari wa Jeshi la Polisi na Viongozi wa Kimila na kuwataka wasalimishe silaha popote pale ambapo walikuwa wanaamini kwamba silaha hizo zitawafikia Jeshi la Polisi.

Akibainisha vijiji ambavyo silaha hizo zilipatikana kuwa ni Olorieni Magaiduru zilipatikana silaha aina ya Chinese 56 SMG moja yenye namba MT. 70B 1 2730021 na risasi 21 pamoja na silaha aina ya Semi Automatic Rifle (S.A.R) yenye namba KN 250374 ikiwa na risasi nne.

Katika kijiji cha Oldonyasambu ilipatikana silaha aina ya Mark IV yenye namba ZKK 5602 pamoja na silaha nne aina ya Chinese 56 Sub-Machine Gun (SMG) zikiwa na risasi 19. Silaha hizo nne ni Chinese 56 SMG yenye namba RT 7663, bunduki ya pili namba yake ni 563631144 na bunduki mbili nyingine hazikuwa na namba.

Kamanda Mkumbo alisema katika kijiji cha Sale silaha aina ya Chinese 56 SMG yenye namba 89020539 ikiwa na risasi 15 kwenye magazine ilipatikana pamoja na silaha nyingine mbili tofauti ambazo ni S.A.R yenye namba 25032534 na Mark III yenye namba 263126.

Aidha kamanda Mkumbo aliwataka wananchi wanaomiliki silaha za moto kinyume cha sheria wazisalimishe mara moja kwenye ofisi za mitaa, vijiji na hata vituo vya Polisi vyovyote vilichopo karibu huku akitoa onyo kwa wale ambao watakaidi na wakikutwa nazo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao. Alisema Operesheni hiyo ni endelevu na itakuwa katika maeneo tofauti ya mkoa huu na si wilaya ya Ngorongoro pekee.


Polisi Watinga Nyumbani kwa Gwajima....Mwenyewe Agoma Kufungua Mlango

$
0
0
Jeshi  la Polisi kwa mara nyingine jana lilizingira nyumba ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, kwa kile lilichodai kuwa lilifika kufanya uangalizi.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Askofu Gwajima mwenyewe, zinaeleza kuwa polisi walifika nyumbani kwake wakiwa katika gari lao.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, polisi hao walipojaribu kutaka kuingia nyumbani kwa askofu huyo, walizuiwa mlangoni kwa sababu hawakuwa na kibali chochote wala maelezo yanayojitosheleza ya kutaka kukutana na kiongozi huyo wa kiroho.

Askofu Gwajima  jana alikiri polisi hao kumfuata nyumbani kwake na hivyo kulazimika kumtafuta wakili wake mara moja.

“Ni kweli walikuja wakiwa na gari la polisi, lakini walipofika nami nilimpigia mwanasheria wangu ambaye aliniambia tuwaulize wametumwa na nani na kama wana ‘search warrant’ (kibali cha kufanya upekuzi) au ‘arrest warrant’ (kibali cha kukamata),” alisema.

Askofu Gwajima alisema walipowauliza, walimtaja Afande Kingai kama ndiye mtu aliyewatuma, lakini hawakuwa na kibali chochote.

Kwa mujibu wa Askofu Gwajima, mwanasheria wake alifanya mawasiliano ya simu na Afande Kingai ambaye amepewa jukumu la kuwafuatilia wale wote waliotuhumiwa katika sakata la dawa za kulevya na kumuuliza sababu za kumfuata nyumbani.

“Afande Kingai amemweleza mwanasheria wangu kuwa walikuwa wamekuja kwa ajili ya ‘observation’ (uangalizi) tu, kwa hiyo mwanasheria wangu akasema kama ni ‘observation’ tu tusiwaruhusu kuingia ndani kwa sababu sheria ya hivyo hakuna, na sisi tumewazuia hawakuingia ndani,” alisema Askofu Gwajima.

Alipoulizwa kama kufuatwa kwake sasa na polisi kuna uhusiano wowote na kauli alizozitoa kanisani kwake hivi karibuni kuhusu elimu ya Paul Makonda ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Askofu Gwajima alisema huenda ikawa hivyo, lakini akasisitiza kuwa hana uhakika kwa sababu hajazungumza na askari waliomfuata.

Na alipoulizwa kama anadhani ujio huo pia unatokana na andiko ambalo linasambaa kwenye mitandao ya kijamii ambalo linasema Jumapili ijayo mwalimu aliyemfundisha mtu mmoja anayetajwa kwa jina la Bashite atakuwapo kanisani kutoa ushuhuda, Askofu Gwajima alikana akisema andiko hilo si lake.

Pamoja na hayo, Askofu Gwajima alikwenda mbali na kuhoji: “Hata kama ni kweli, sasa unaogopa mwalimu kuja… kanisani kwangu wapo watu wengi waliosoma naye Bashite kuanzia shule ya msingi na Sekondari ya Pamba… vyeti kama huna huna tu.”

Alipoulizwa haoni kauli yake kwamba Rais Magufuli ni tofauti kabisa na Makonda ilikuwa na nia ya kuwatenganisha viongozi hao, Askofu Gwajima alisema aliyemtaja kwa kumshambulia ni Makonda na si Rais.

“Aliyenitaja kwa kunishambulia katika sakata la dawa za kulevya ni Makonda na si Rais, mimi nimemuongelea Makonda, mimi ni mtumishi wa Mungu siwezi kuongozwa kwa ‘speculation’, si unajua hata Yesu alisema kama wewe huna dhambi basi uwe wa kwanza kushika jiwe,” alisema Askofu Gwajima.

Alipoelezwa kuwa katika mahubiri yake ni kama anaonekana kumshtaki Makonda, askofu huyo alisema:“Nilisema nitamshtaki kwa mahakama iliyo juu yake na nilisema Makonda aombe radhi, angekuwa mstaarabu baada ya sakata lile yeye mwenyewe angenipigia simu na kuniambia Gwajima nilikengeuka, lakini hajafanya hivyo.”
 
Pamoja na hayo, Askofu Gwajima alisema kwa aliyoyafanya Makonda tayari amekwishamsamehe na ndiyo maana hajampeleka mahakamani.

Kauli ya Ridhiwani Kikwete Baada ya Mama Yake Kuteuliwa Kuwa Mbunge

$
0
0
Mbunge wa Jimbo la Chalinze mkoani Pwani Ridhiwan Kikwete amefunguka baada ya mama yake jana kuteuliwa na Rais Magufili kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ridhiwan Kikwete amesema kuwa mama Salma Kikwete ni mwanamke wa shoka kwani amewezesha wasichana wengi nchini Tanzania kupata elimu na amekuwa mtetezi wa haki za wanawake hivyo anaamini kupata nafasi ya kuwa Mbunge itakwenda kuwezesha mapambano kuwa sheria rasmi.

"Umekuwa mtetezi wa haki za wanawake na usawa wa kijinsia, umewezesha wasichana kupata elimu. Wewe ni mwanamke wa Shoka. Hongera sana kwa uteuzi‬. Imani sasa umepata sehemu ya kuwezesha mapambano kuwa sheria. Mungu akutangulie Mama yangu , Mheshimiwa Mbunge. Hongera tena" aliandika Mhe. Ridhiwan Kikwete

Rais Magufuli aanza ziara katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mhe. Dkt.  John Pombe Magufuli, leo tarehe 02 Machi, 2017 ameanza ziara ya kikazi ya siku 4 katika Mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Katika ziara hiyo Mhe. Rais Magufuli atafungua miradi mbalimbali ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika mikutano ya hadhara.

Leo asubuhi Mhe. Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Tanzania Goodwill Ceramic Tiles Ltd. kilichopo Mkuranga Mkoani Pwani na baadaye ataelekea Mkoani Lindi.

Kesho tarehe 03 Machi, 2017 Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake Mkoani Lindi na keshokutwa tarehe 04 Machi, 2017 atafanya ziara yake Mkoani Mtwara.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

02 Machi, 2017

CCM yamjibu hivi Mjane wa Kapteni Komba kuhusu mafao ya mumewe

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Mjane wa Marehemu, Kapteni Komba, Bi. Salome Komba kufuatilia malipo ya mafao ya mumewe kwa uongozi wa kundi la Tanzania One Theatre (TOT) ambako ndiko alikokuwa akifanyia kazi.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), Rodrick Mpogolo, ametoa maelekezo hayo ikiwa ni siku moja tu baada ya Salome kukaririwa  akimuomba Mwenyekiti wa CCM, Rais John Magufuli aingilie kati kumsaidia ili alipwe mafao ya marehemu mume wake yanayofikia Shilingi Milioni 75.

Mpogolo amesema ofisi yao haiwezi kulizungumzia suala hilo kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi.

“Ofisi yao haiwezi kulizungumzia kwa sababu masuala yanayohusu fedha yanapaswa kufafanuliwa vyema na uongozi wa kundi lao la TOT ambako Komba alikuwa akifanya kazi,” amesema.

Kwa mujibu wa Bi. Salome, hadi sasa wakati mumewe akitimiza miaka miwili tangu afariki dunia, CCM imemlipa Shilingi Milioni 4.5 tu ikiwa ni sehemu ya malipo hayo huku akifuatilia kwa muda mrefu bila mafanikio kupata kiasi kilichobaki cha Shilingi milioni 70.5 bila mafanikio.

Komba aliyezaliwa mwaka 1954, alifariki dunia Februari 28, 2015 na kuzikwa Mkoani Ruvuma ambako enzi za uhai wake alijizolea umaarufu mkubwa kutokana na umahiri wake katika kutunga na kuimba nyimbo mbalimbali za kwaya, hasa za kukipigia debe chama chake (CCM) wakati wa kampeni mbalimbali za uchaguzi.

SORRY MADAM -Sehemu ya 37 & 38 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWAILIPOISHIA

ILIPOISHIA
Wapelelezi waliopo nje ya chumba hicho walizidi kuyafwatilia mazungumzo hayo kwa vinasa sauti walivyo weza kuvifunga ndani ya chumba hicho.

“Siwezi kumfahamu mtu gaidi kama wewe. Niambieni ni nini alicho kuambia baba yangu Eddy”
Shamsa alizungumza kwa hasira huku akimwagikwa na machozi, Briton kwa dharau akatabasamu kisha akajivuta kidogo kwenye kiti na kumtazama usoni Shamsa
“Baba……..baba gaidi kama Eddy. Ohoooo mimi ndio niliye weza kumuua, sahamani kwa hilo”
Shamsa akasimama kwa hasira na kumrukia Briton na wote wakaanguka chini na kuanaza kumshindilia ngumi za hasira Briton aliye fungwa pingu miguuni na mikononi.

ENDELEA
Wapeleezi wawili wa kike wakaingia ndani ya chumba hicho na kumtoa Shamsa juu ya mwili wa Briton anaye zidi kupigika na binti huyo. Ikawalazimu kumtoa kabisa nje ya chumba hicho na kumpeleka katika chumba chake walicho mpatia na chenye ulinzi mkali sana.

“Mwanangu mbona umekuwa hivyo?”
Mama Pudensia alizungumza huku akimtazama Shamsa machoni anaye mwagikwa na machozi akionekana dhahiri kwamba ana hasira kali iliyo mpanda, kwani kifua chake kiliweza kutanuka kiasi, mishipa yake ya shingo inaoenekana vizuri, uzuri wa sura yake umebadilika sana.

Mambo yote yakiwa yanaendelea, Bwana Mgwira aliweza kushuhudia tukio hilo akiwa katika chumba cha kusikilizia mazungumzo yaliyo kuwa yanafanywa kwenye chumba hicho.

‘Hakikisha hii siku haipiti lazima awe amesha kufa’
Bwana Mgira alimtumia meseji mmoja wa wapelelezi alio kuwa nao ndani ya chumba hicho kisha yeye akatoka na kuondoka zake.
                                                                                                        ***
   Kitu kilicho zidi kumuumiza kichwa Raisi Praygod ni wapi alipo Eddy, ambaye wananchi wengi wote wanafahamu kiongozi huyo amefariki. Anashindwa hata kuwatangazia wananchi kwamba Eddy ndio amehusika na vifo vya wanajeshi hao.

“Sasa hapatunafanyaje?”
Raisi Praygod alimuuliza mshauri wake bwana Mgwira, wakiwa ndani ya ofisi ya yake.
“Muheshimiwa hapo kusema kweli hatuwezi kufanya chochote zaidi ya kumtafuta kimya kimya, pasipo wananchi kuweza kulitambua hilo. Pia itakuwa ni nafasi ya kipekee kuweza kumuua, pasipo watu wengine kuelewa”

“Etieee?”
“Ndio muheshimiwa, kwa maana wananchi wanajua kwamba amekufa. Tunacho kifanya mwili wa yule mshenzi kule Muhimbili, unazikwa na jeshi kwa madai kwamba ni gaidi, hakuna muandishi wa habari atakaye karibia jeneza na kuipiga picha sura ya Eddy”
“Lakini tukiwabana waandishi wa habari wasifanya kazi yao, kunaweza kuzuka mambo ya kitata. Tuwape nafasi tuone itakavyo kuwa”
“Sawa muheshimiwa. Tuachane na hayo, vipi uchaguzi ndio mwaka huu, umejipangaje kaka”

“Kama kawaidia, miaka mitano ijayo ipo mikononi mwangu”
Raisi Praygod alizungumza kwa kujiamini, kwani anatambua kwamba wananchi wengi wa Tanzania wanamchukulia kwama kiongozi imara na sahihi katika maisha yao, ila nyuma ya pazia ni kiongozi katili asiye paswa kushikilia hata hiyo miaka mitano ya awamu ya pili.
                                                                                                   ***
“Priscar twende kule kwenye handaki”
“Sawa mdama”
Priscar akazidi kujikaza kuliendesha gai hilo, kwani wote wawili kila mmoja ana uchungu wake kwa upande wake, yeye anamlilia Samson, ila bosi wake anamlilia Eddy. Kwa mwendao wa lisaa moja na nusu wakawa wamefanikiwa kufika kwenye handaki ambalo ndipo yalipo kuwa maficho ya Rahab na kikundi cha wezake walio kuwa wakidili na maswala ya ujambazi, wa kuua watu kazi hiyo ikiwa ni amri kutoka kwa raisi Praygod wao wakiifanya pasipo kujua kwamba ni kazi ya kiserikali,
Wakashuka wote wawili, huku Rahab akionekana kuwa na Shahuku kubwa ya kutaka kwenda kumuona Eddy akiwa ndani ya handaki hilo.

Wakafika ndani, hapakuwa na mtu wa aina yoyote, Rahab akafungua kila chumba kuhakikisha kwamba ni kweli hakuna mtu, ila ndivyo jinsi macho yake yalivyo weza kushuhudia kwamba hakuna mtu wa aina yoyote katika handaki hilo, akarudi eneo la sebleni akiwa amechoka, akamkuta Priscar akiwa ameshika karatasi nyeupe akiwa anasoma yaliyo andikwa humo ndani huku machozi yakimwagika, alipo maliza taratibu akamkabidhi Rahab aweze kuisoma karatasi hiyo.

{Madam R. Samahani sana kwa kile kilicho weza kujitokeza zidi ya wanajeshi hao, sikuwa na jinsi zaidi ya kuweza kuwaangamiza ili wasiweze kumdhuru mwanaume unaye mpenda kwa dhati.

Rahab natambu ya kwamba mapenzi yanauma sana pale unapo mkosa yule umpendaye, ndivyo jinsi hata wanafamilia wa wanajeshi nilio waua, ndivyo wanavyo umia kwa sasa. Madama, asante sana kwa kuweza kunipa nafasi ya pili ya kuweza kuishi, ila nikiwa kama si binadamu wa kawaidi, hali hii inadhidi kunidhuru siku hadi siku pale ninapo mwaga damu za watu, huwa natamani kila muda na kila mara niweze kumwaga damu za watu, natambua maamuzi ninayo yachukua ni magumu sana ten asana.

Ningependa niyachukue mimi kama mimi mwenyewe na nisimshirikishe mtu yoyote. Nitakufa kwa ajili ya kuto ua zaidi kwani kila nikiua ndivyo jinsi ninavyo zidi kupata nguvu, za kuendelea kuua. Namuacha Eddy ndani ya handaki hili ukija hakikisha hali yake inakuwa salama kwani bila ya hivyo anaweza kufariki muda na saa yoyote. Nakutakia kazi njema. Samson}

Ujumbe huo wa Samson ukazidi kumchanganya Rahab akajikuta akitoka mbio ndani ya handaki hilo na kuanza kuita kwa sauti kubwa huku na huko akiliita jina la Eddy. Milio ya ndega pamoja na upepo unao vuma ndani ya msitu huo havikutosha kuweza kusikia sauiti yoyote ya mtu akiliitikia jina lake. Uchungu mkali ukazidi kumtawala ndani ya moyo wake, akazidi kuita jina la Eddy ila hapakuwa na majibu ya aina yoyote.

Akajaribu kuweza kuvuta hisia, ila picha halisi ambayo inamjia kichwani ni jinsi Samson alivyo weza kuaondoka katika eneo hilo na gari lake, akiwa amefika eneo la barabara kuu, kuna mzee wa makamo alimsimamisha na kumuomba lifti, japo Samson kwa mara ya kwanza aliweza kukataa, ila mzee huyo alijaribu kuweza kumsihi sana kwamba anahitaji lifti. Samson ikambidi kumfungulia mlango mzee huyo mwenye mvi nyingi kichwani mwake, kisha akaondoka naye.

Mwendo kasi wa gari anayo iendesha Samson kukamfanya mzee huyo kuanza kumuomba Samson aweze kupunguza mwendo huo, ila Samson hakuhitaji kuweza kupunguza, zaidi na zaidi ndivyo jinsi alivyo zidi kuongeza mwenda kasi hadi mzee huyo akaanza kumwagikwa na machozi.

Simu ya Samson ikaanza kuita, alipo ona ni jina la Rahab, akaiacha simu hiyo iite hadi ikakatika, ikapigwa tena, ikaita hadi ikakatika, ikapigwa kwa mara kadhaa ila Samon hakuweza kuipokea zaidi alipo ona inampigia kelele, akafungua kioo cha upande alipo kaa mzee huyo, kisha akaitupia kwanye nyasi nyingi zilizopo kandokando ya barabara, kurudisha macho yake barabarani, kufumba na kufumbua gari yake ikagongana uso kwa uso na gari la mafuta, likauburuzwa kwa urefu fulani, huku tanki lake la mafuta likiwa limetoboka na kumwaga mafuta. Mikwaruzo ya ya vyuma vyuma kwenye lami, vikazalisha cheche, zilizo ingia kwenye mafuta ya petrol na kusababisha mlipuko mkubwa, ulio pelekea gari hiyo kurushwa pembeni ya barabara na kuendelea kuteketea kwa moto.

“Am sorry madam” (Samahni bibie)
Yalikuwa ni maneno ya mwisho ya Samson kabla hajafariki kabisa. Kwa hasira Rahab akajikuta akipiga kelele kali, hadi miti ikatingishika, huku ndege wakipupuruka kwa woga wa sauti hiyo ambayo hawakuwahi kuisikia.  Priscar naye akajikuta akianguka chini na kupoteza fahamu, kwani hakuweza kustahimili mtingisho na nguvu ambayo inazunguka ndani ya msitu huo.

***
      Kwa kupitia kifaa maalumu kilichomo ndani ya mwili wa Briton, maeneo ya mgongoni mwake, vijana wanne wa Al-Shabab waliweza kugundua ni jengo gani ambalo Briton yupo. Kila mmoja akiwa na simu yake yenye uwezo ya kuonyesha alama nyekundu sehemu Briton alipo, wakajigawa wawili wawili, kwenda kulisoma jengo hilo kabla hata wajafanya uvamizi majira ya usiku, kwani muda wa sasa ni jioni.

Pasipo kustukiwa wakalichunguza gorofa hilo, walipo hakikisha kwamba ulinzi wa eneo hilo umeimarishwa sana, ikabidi warudi kwenye nyumba ya wageni walipo fikizia kuendelea kupanga mipango yao.

Kila mmoja alihakikisha anajiandaa vizuri, kwani hawakuhitaji zoezi hilo liweze kuwachukua muda mrefu, wakiwa katika kutazama luninga iliyomo ndani ya chumba hicho, wakaona taarifa ikiwaonyesha binti waliye agizwa akiwa kwenye ulinzi mkali wa askari na kuingizwa kwenye gari.
“Watakuwa wamempelea kwapi?”
“Nahisi kwenye kituo kikubwa cha polisi”
“Una uhakika huo?”
“Ndio kwa maana hawezi kupelekwa eneo jengine lolote zaidi ya kuwa katika kituo kikuu cha polisi”

“Basi nyinyi wawili mutaenda katika kituo cha polisi usiku huu, kisha na sisi wa wili tutakwenda kumkomboa bosi”
“Sawa mkuu”
Mipango ya vijana hao wanao jiamini kupita maelezo ikakamilika vizuri majira ya saa mbili usiku wakatoka vijana wana kwenda kwenye kituo cha polisi, wakiwa na lengo la kwenda kuhakikisha kwamba wanatoka na Shamsa, wakiwaancha wezao wanao kwenda kwenye jengo la alilo shikiliwa Briton.

Mahakama Kuu Dar yatupilia mbali ombi la Freeman Mbowe

$
0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania leo March 2, 2017, imetoa uamuzi wa pingamizi la Serikali dhidi ya maombi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Freeman Mbowe aliyeiomba Mahakama ilizuie Jeshi la Polisi kumkamata akituhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Mbowe alifungua kesi ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamishna  wa Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Mkuu wa Upelelezi kanda maalum na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Jopo la majaji wakiongozwa na Jaji Sekieti Kihiyo wameutaka upande wa mleta ombi hilo kufanyia marekebisho ya kifungu kwenye maombi ya Freeman Mbowe kuzuia kukamatwa na Jeshi la Polisi na kumuweka  ndani wakati kesi ya msingi ikiendelea

Baada ya uamuzi huo, kiongoz wa jopo la mawakili wa upande wa Freeman Mbowe, Jeneral Ulimwengu alisema nje ya Mahakama baada ya maamuzi hayo kuwa,

“Ombi limekataliwa kwa sababu hatukuwa na kifungu  ambacho katika sheria zetu kinafanya kazi katika nchi na maelekezo hayo ni kwamba kwa sababu tuna ‘import’ sheria zetu kutoka Uingereza. Tutafute kifungu ambacho kinaweza kusaidia kuendesha mashtaka, hiyo kazi itafanyika kati ya leo au kesho kwa sababu kesi ya msingi bado ipo na itasikilizwa March 8.” alisema Jenerali Ulimwengu.

Naye Mweneyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe baada ya maaamuzi hayo ya Mahakama alisema jopo la mawakili litahamia mjini Arusha kwenye kesi inayomkabili Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema.

Rais Magufuli: Marufuku kusafirisha mchanga nje ya nchi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepiga marufuku usafirishaji wa mchanga wa madini nje ya nchi na ametaka mchanga wote ufanyiwe uyeyushaji hapa hapa nchini.

Rais Magufuli ametoa katazo hilo leo wakati akiweka jiwe la msingi la kiwanda cha kutengeneza vigae (Tiles) cha Kampuni ya Goodwill Tanzania Ceramic Limited kilichopo katika Wilaya ya Mkuranga Mkoani Pwani.

Akizungumza baada ya kutembelea kiwanda hicho, Mhe. Rais Magufuli ameishukuru Menejimenti ya kiwanda hicho kwa uwekezaji huo na ameelezea kufurahishwa kwake na kutumika kwa teknolojia ya kuyeyusha mchanga wa kutengenezea vigae.

"Nchi hii tumechezewa vya kutosha, sasa nyinyi hapa mnayeyusha mchanga kwa kuuchemsha hadi nyuzi joto 1,000 wakati wengine wanasafirisha mchanga nje ya nchi wakati uchemshaji wake hauhitaji kufika hata nyuzi joto 1,000, naiagiza Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji na Wizara ya Nishati na Madini kuwa kuanzia sasa ni marufuku kusafirisha mchanga nje ya nchi" amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Kiwanda hicho kikubwa Afrika Mashariki na Kati ambacho ujenzi wake umegharimu Dola za Marekani Milioni 50 kwa awamu ya kwanza kitakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za mraba 80,000 za vigae kwa siku, kitazalisha ajira za moja kwa moja 1,000 na ajira zisizo za moja kwa moja 2,000.

Akizungumza kabla ya kuweka jiwe la msingi la kiwanda hicho Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru amesema pamoja na kiwanda hicho, tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani jumla ya viwanda 2,169 vinavyojumuisha viwanda vidogo, vya kati na vikubwa vimesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na vipo katika hatua mbalimbali za kukamilika.

Naye Balozi wa China hapa nchini Mhe. Dkt. Lu Youqing amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kutilia mkazo juhudi za kukuza uchumi zilizowezesha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokuwa kwa kasi kubwa Barani Afrika na amebainisha kuwa China itaendelea kushirikiana na Tanzania kuendeleza uwekezaji nchini Tanzania ikiwemo kujenga viwanda.

"Mhe. Rais kwa mujibu wa takwimu za TIC mpaka mwisho wa Juni 2016 uwekezaji wa moja kwa moja kutoka China umefikia Dola za Marekani Bilioni 6.6 na umezalisha ajira za moja kwa moja kwa Watanzania 150,000 na zisizo za moja kwa moja 450,000 na kiwanda hiki cha Goodwill Tanzania Ceramic Limited kimejengwa na wawekezaji kutoka China, vipo viwanda vingine vingi vinajengwa, Mbunge wa Mkuranga ameniambia kuwa kuna viwanda zaidi ya 50 vya Wachina vinavyojengwa hapa Mkuranga, nimefurahi sana kuona karibu kila sekta Watanzania wanafurahia ushirikiano wa Tanzania na China" Amesema Balozi Dkt. Lu Youqing.

Magufuli: Serikali haitatoa chakula cha bure kwa wenye njaa

$
0
0

Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameendelea kusisitiza kuwa kuwa Serikali haitatoa chakula cha msaada kwa watakaopatwa na njaa ilihali wanaweza kuzalisha chakula katika maeneo yao.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo leo katika ziara yake mkoani Pwani, wakati akizungumza na wananchi wa Somanga, Nangurukuru na Mchinga Moja, ikiwa ni ziara yake katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.

Amepokea kero za wananchi katika maeneo hayo nakuwataka  kufanya kazi kwa bidii ikiwemo kuzalisha mazao ya chakula cha kutosha

"Najua mmezoea kusikia maneno mazuri mazuri kuwa hakuna atakayekufa kwa njaa, sasa mimi nasema usipofanya kazi, usipolima mazao na kupata chakula wakati mvua inanyesha Serikali haitatoa chakula cha bure kwa wenye njaa, ni lazima tufanye kazi, sasa hivi mvua zinanyesha limeni mazao ya chakula" amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Pia Rais Magufuli amezungumza na wananchi wa Ikwiriri na kupokea kero zao ambapo amewaagiza Mamlaka ya Maji katika Mji huo kuhakikisha mradi wa maji uliojengwa na kukamilika tangu mwaka 2015 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 5, unaanza kutoka maji kabla ya mwisho wa Mwezi huu na pia amepiga marufuku utozaji wa ushuru kwa wafanyabiashara wadogowadogo wa mazao.

Aidha, Mhe. Dkt. Magufuli amewaagiza viongozi wa Mkoa wa Lindi kushughulikia migogoro ya wakulima na wafugaji iliyoanza kuibuka mkoani humo na ameahidi kutoa Shilingi Milioni 20 kusaidia ujenzi wa Zahanati ya Somanga.

Mbali na hayo Rais Magufuli amewaagiza Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kujenga kituo cha mabasi cha Nangurukuru na pia amemuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Lindi kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Hamidu Bobali kuhakikisha anapeleka Daktari katika kijiji cha Mchinga Moja ili kutatua kero ya wananchi kukosa huduma ya matibabu.

Mhe. Rais Magufuli ataendelea na ziara yake kesho tarehe 03 Machi, 2017 hapa Mkoani Lindi

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya February 3

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images