Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Yoweri Museveni Amaliza Ziara Yake Ya Siku Mbili Nchini Na Kurejea Nyumbani

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni amemhakikishia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwa yupo tayari kuweka jiwe la msingi la mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga nchini Tanzania.

Mhe. Rais Museveni amesema hayo jana tarehe 26 Februari, 2017 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati akiagana na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli baada ya kumaliza ziara yake rasmi ya kiserikali ya siku 2 hapa nchini na kurejea Uganda.

“Tulikuwa na mazungumzo mazuri na Mhe. Rais Magufuli, tumejadili mambo mengi hususani kuhusu mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta, tumekubaliana na Mhe. Rais mambo mengi, na sasa tutakwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi huo” alisema Mhe. Rais Museveni.

Mhe. Rais Museveni aliwasili hapa nchini juzi asubuhi tarehe 25 Februari, 2017 ambapo alifanya mazungumzo na mwenyeji wake Mhe. Rais Magufuli na jana alitembelea viwanda viwili vinavyomilikiwa na kampuni ya mfanyabiashara wa Tanzania Bw. Said Salim Bakhresa ambavyo ni kiwanda cha uzalishaji wa unga wa ngano kilichopo Buguruni na kiwanda cha uzalishaji wa juisi kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam.

Licha ya kuwekeza nchini Uganda Mfanyabiashara huyo pia amekuwa akipeleka bidhaa zake kwa wingi nchini Uganda.

Pamoja na Mhe. Rais Magufuli viongozi wengine waliokuwepo wakati wa kumuaga Mhe. Rais Museveni ni pamoja Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa na Viongozi wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Lori laporomoka mlimani, laua wafanyabiashara 6 na Kujeruhi 12

$
0
0
Wafanyabiashara sita wamekufa papo hapo na wengine 12 kujeruhiwa, baada ya lori lililokuwa likiwapeleka mnadani kuacha njia na kuporomoka kwenye mlima wenye kona nyingi zinazofikia 99 wilayani Lushoto

Taarifa zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba zilisema ajali hiyo ilitokea jana Jumapili jioni katika mlima wenye idadi hizo za kona zinazoanzia Mng’aro hadi Mlalo wilayani Lushoto, baada ya lori aina ya Mitsubishi Fuso Canter kuporomoka. 

Watu walioshuhudia ajali hiyo walisema lori hilo lilikuwa likitokea Kijiji cha Mng’aro kilichopo uwanda wa chini lilipokuwa likipanda mlima kuelekea Mlalo kwa ajili ya kuwahi soko siku inayofuata. 

Walisema lori hilo lilipofika katikati ya mlima liliacha njia na kurudi nyuma hatimaye likaporomoka bondeni, huku mizigo ikiwaangukia watu hao. 

Kamanda Wakulyamba aliwataja waliokufa kuwa ni Jamal Hemed (40), mkazi wa Mlalo, Hassan Rashid (33) wa Nyasa, Bisura Seif wa Kifungilo, Hadija Said wa Mhelo, Zuena Juma wa Kwedege na Husna Athumani wa Hemtoye. 

Alisema majeruhi wa ajali hiyo walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa matibabu. Kamanda huyo alisema dereva wa lori hilo, Nassoro Athumani (25) anatafutwa kwa kuwa alitoroka baada ya ajali. 

Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva na ubovu wa gari. 

Jenerali Ulimwengu Aiomba Mahakama Imuunganishe Katika Kesi ya Mbowe Dhidi ya Makonda

$
0
0
Mwanahabari nguli Jenerali Ulimwengu, leo anatarajia  kuwasilisha maombi Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, akiomba kuungana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe  katika kesi ya katiba iliyofunguliwa hivi karibuni.

Ulimwengu anaomba kuunganishwa katika kesi ya katiba namba 1 ya 2017 kama mdai dhidi ya wadaiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalumu ya Dar es Salaam.

“Maombi ya kumuunganisha yameandaliwa na kesho(leo) yatakuwa mahakamani kuomba naye awe mdai. Anaomba kujiunga kwa kuwa mambo anayopigania Mbowe naye ana maslahi nayo kwa sababu ni mambo muhimu ya katiba,” alisema mmoja wa jopo la Mawakili kutoka Kurugenzi ya Katiba Sheria na Haki za Binadamu ya Chadema, Peter Kibatala.

Katika kesi hiyo ya katiba, Mbowe anaomba Mahakama Kuu itamke   kuwa Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya kudhalilisha na kukamata.
 
Mbowe pia anaomba mahakama itengue vifungu vya 5 &7 vya Sheria ya Tawala za Mitaa kwa kuwa ni batili na vinakiuka haki ya katiba.

Mbowe alifungua kesi hiyo akidai Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekiuka sheria na taratibu katika kushughulikia watuhumiwa wa biashara ya dawa za kulevya nchini.

Kesi hiyo ya katiba inasikilizwa na majaji watatu, Jaji Sakieti Kihiyo, Jaji Lugano Mwandambo na Jaji Pellagia Khaday.

Baada ya kufungua kesi hiyo Mbowe pia aliomba mahakama itoe amri asikamatwe mpaka maombi yake ya zuio yatakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.

Mahakama ilitoa zuio la muda kwa Jeshi la Polisi  kutomkamata Mbowe hadi maombi yake ya kupinga kukamatwa aliyowasilisha mahakamani yatakaposikilizwa.

Maombi hayo yalitakiwa kusikilizwa mwishoni mwa wiki lakini upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Gabriel Malata uliwasilisha pingamizi, ukiomba mahakama iyatupilie mbali kwa sababu  hana msingi katika sheria.

Upande wa mdai ulijibu hoja za kupinga maombi yao na Mahakama ilisikiliza hoja za pande zote mbili na kupanga kutoa uamuzi wa pingamizi hilo Machi 2, mwaka huu.

AUDIO: Askofu Gwajima aelezea sakata zima la Makonda kutumia vyeti vya mtu mwingine

$
0
0
Siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo.

Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni la mwenye vyeti hivyo.

Aidha, Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako atalifumbia macho jambo hili. 

Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.

Hapa chini ni sauti ya Askofu Gwajima akihubiri kanisani kwake.

Mahakama yaicharukia serikali kesi ya Godbless Lema......Yahoji sababu za mbuge huyo kunyimwa dhamana.

$
0
0
Mwenyekiti wa kikao cha jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, kinachoendelea Arusha, Bernard Luanda, leo amegeuka mbogo kwa wanasheria wa serikali kwa kitendo cha kumnyima Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema dhamana kwa lengo la kumnyima haki.

Akizungumza Mahakamani hapo leo mbele ya majaji wenzake Stella Mugasha na Jaji Kipenka Mussa, Luanda amesema haipendezi na haingii akilini mtu (Lema) kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki.

“Tunaomba ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikai (DPP) muwe makini sana maana mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua Mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushitua sana,” alisema huku akishauriana na wenzake mara kwa mara kwa masikitiko.

Aliendelea kusema kuwa ofisi ya DPP inaitia najisi taaluma hiyo, kitu kipo wazi ila wanafanya vitu vya ajabu na havipendezi.

Alihoji jaji Luanda kuwa“Tumesoma faili lote tunashangaa hivi kweli ofisi ya mwanasheria mkuu ina wanasheria kweli na kama wapo kwa nini huyu mtu (Lema) awe ndani mpaka leo?”.

Alisema kwa kuwa mikono yao kisheria imefungwa hawawezi kufanya chochote kwa leo na kuwataka Mawakili upande wa Lema kurudi Mahakama Kuu, kuendelea na maamuzi ya dhamana.

Hali hiyo ilitokana na Wakili wa serikali Faraja Nchimbi kusimama mahakamani hapo na kuomba kuiondoa rufaa hiyo kwa madai kuwa ipo nje ya uwezo wake.

“Waheshimiwa Majaji baada ya timu yetu ya wanasheria kupitia kwa kina rufaa hii kwa sababu zisizozuilika tumeona hatupo tayari kuendelea na rufaa hii, maana hatukupeleka kusudio (Notisi) kwa msajili muda ulipita, hivyo tunaomba kuiondoa na uamuzi wa kuiondoa rufaa hii tumeufikia Ijumaa muda uliisha kuja mahakamani,”. Alisema Nchimbi.

Baada ya kuwasilisha ombi hilo, Wakili wa Lema Peter Kibatala, alisimama na kusema upande wao hawana pingamizi ila waliomba hoja za awali za rufaa hiyo ziondolewe Mahakamani hapo bila kunakiliwa.

Baada ya ombi hilo Jaji Kipenka Mussa alipokea kwa niaba ya Majaji wenzake na kukubali ombi la kuiondoa rufaa hiyo namba 9/2017.

Aidha Jaji Luanda alimkaribisha jaji Stella Mugasha pia kuongea kwa niaba yao ambapo alisema mahakama imekubali ombi la pili la kuiondoa rufaa namba 10/2017, baada ya Wakili Paul Kadushi kuomba kuiondoa pia.

Wakili wa Lema Peter Kibatala, alilazimika kusimama tena Mahakamani hapo kusema kuwa upande wao unasikitika kuona ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP wanatumia Mahakama kwa njia ya kumnyima haki mteja wao, hivyo aliomba mahakama hiyo iwatatulie tatizo la kisheria lililojitokeza hadi mteja wao awe ndani hadi sasa.

Kibatala aliongea hayo huku akishindwa kujizuia na kumwaga chozi la huzuni mahakamani hapo mbele ya Majaji hao.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya February 28

Wafanyakazi wengine Wawili wa Quality Group ya Yusuf Manji Wafikishwa kizimbani

$
0
0
Wafanyakazi wengine wawili wa Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na Yusuf Manji ambao ni raia wa India wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka ya kuzuia maofisa wa Uhamiaji kutimiza majukumu yao.

Washitakiwa hao ni Jose Kiran (40) ambaye ni Meneja Miradi wa kampuni na Prakash Bhatt (35) ambaye ni Katibu Muhtasi wa kampuni hiyo ambao wameongezwa katika kesi inayowakabili wafanyakazi 14 wa kampuni hiyo, raia wa India wanaokabiliwa na mashitaka matatu likiwamo la kughushi viza ya biashara.

Wakili wa Serikali, Method Kagoma alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo kinyume cha Kifungu Namba 30 (1) (f) na Kifungu Namba 2 cha Sheria ya Uhamiaji ya Mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na Sheria Namba 8 ya Mwaka 2015.

Kagoma alidai washitakiwa hao wawili, Februari 20 mwaka huu katika Kampuni ya Quality Group waliwazuia maofisa Uhamiaji kutimiza majukumu yao baada ya kukataa kuripoti kwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Dar es Salaam, kwa kujaribu kukimbia nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mpaka wa Horohoro.

Washitakiwa wote walikana mashitaka ambapo upelelezi wa kesi hiyo umekamilika hivyo upande wa mashitaka unaomba tarehe kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.

Hata hivyo, washitakiwa waliachiwa huru baada ya kutimiza masharti ya dhamana yaliyowataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini dhamana ya Sh milioni tano.

Hakimu Mkeha alisema kesi hiyo itatajwa Machi 7 mwaka huu kwa ajili ya washitakiwa kusomewa maelezo ya awali. 

Mbali na washitakiwa hao, wengine katika kesi hiyo ni Rajat Sarkar (35), Jagadish Mamidu (29), Niladri Maiti (41) Divakar Raja (37) ambao ni washauri wa kampuni hiyo, huku Mohammad Shaikh (44) mhasibu na Pintu Kumar (28) ambaye ni Meneja msaidizi wa kampuni.

Pia wapo ni Bijenda Kumar (43), Prasson Mallik (46), Nipun Bhatt (32), Anuj Agarwal (46), Varun Boloor, Arun Kateel (46), Avinash Chandratiwari (33) na Vikram Sankhala (50) ambao wote ni washauri wa kampuni hiyo. Kagoma alidai katika mashitaka ya kwanza washitakiwa walitenda kosa hilo Februari 13, mwaka huu maeneo ya Kampuni ya Quality Group, Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Alidai kuwa washitakiwa wote wakiwa ni raia wa nchini India, walikutwa na visa zilizoghushiwa kinyume na kifungu namba 31 (1) (e) na Kifungu Namba 2 cha Sheria ya Uhamiaji ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho na sheria namba 8 ya mwaka 2015. Kagoma alidai katika mashitaka ya pili kuwa washitakiwa wote kwa pamoja katika tarehe hiyo hiyo, mwaka huu, maeneo ya Kampuni ya Quality Group, walikutwa wakiishi nchini kinyume na sheria.

Pia katika mashitaka ya tatu, inadaiwa washitakiwa wakiwa katika Kampuni hiyo, huku wakijua kuwa wao ni raia wa India walikutwa wakifanya kazi nchini kinyume na kifungu namba 9 (i) (e) na kifungu namba 3 cha sheria ya ajira namba 1 ya mwaka 2015.

Hivi karibuni, Ofisi ya Uhamiaji ilitaja wafanyakazi 25 wa Yusuf Manji kwamba wanafanya kazi nchini bila ya kuwa na kibali na kukusudia kumfungulia mashitaka mfanyabiashara huyo ambaye pia anakabiliwa na kesi ya kutumia dawa za kulevya, kwa kosa la kuajiri wafanyakazi kutoka nje ya nchi wasio na vibali.

Waziri Lukuvu Amnyang'anya Ardhi Makonda

$
0
0
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ametangaza kumchukulia hatua mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Mohamed Iqbal aliyempa Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda eneo la ukubwa wa ekari 1,500 ili kujenga viwanda vidogo, wakati linamilikiwa na serikali na si mali ya mfanyabiashara huyo.

Jumanne iliyopita mfanyabiashara huyo alimkabidhi Makonda eneo la ukubwa wa ekari 1,500 Kigamboni, kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vya wafanyabiashara.

Ekari hizo zilitolewa na Kampuni ya Azimio Estate inayojihusisha na ujenzi wa majengo na uendelezaji wa ardhi na kukabidhiwa kwa Makonda.

Kampuni hiyo pia iliwahi kutajwa katika ripoti za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu ushiriki wake katika miradi ya ujenzi wa nyumba za Shirika la Tafa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ambao unadaiwa uligubikwa na ufisadi.

Alipotembelea eneo hilo lililopo Kigamboni, Makonda aliipongeza kampuni hiyo kwa kukubali kutoa eneo lao na kusema wameonesha nia ya kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli za nchi kuwa ya viwanda, hasa kwa kuwa wenye viwanda vidogo wana changamoto nyingi za maeneo na wengine kulazimika kuweka katika maeneo ya watu.

Mkurugenzi wa Azimio Estate, Iqbal alisema baada ya kupata maombi kutoka kwa mkuu wa mkoa waliamua kutoa ardhi hiyo ili kusaidia juhudi za serikali za kuwa na viwanda.

“Tulipokea ombi na tumeamua kutoa eneo hili ambalo naamini litasaidia katika juhudi hizi za ujenzi wa viwanda vidogo katika mkoa huu, tutaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha wanafikia lengo,” alisema Iqbal.

Lakini katika mkutano wake na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Lukuvi alisema eneo hilo ni la serikali na kwamba wizara yake itamshughulikia mfanyabiashara huyo kwa kumdanganya mkuu wa mkoa.

Lukuvi alisema mfanyabiashara huyo aliidanganya serikali pamoja na kumdanganya mkuu wa mkoa Makonda ambaye ndiye aliyekabidhiwa eneo hilo kwa niaba ya serikali. Mbali na kosa la kuidanganya serikali, Lukuvi pia amesema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki ardhi kinyume cha sheria.

Alisema tayari amekwishafanya mawasiliano na mkuu huyo wa mkoa na kumuelewesha kuwa alidanganywa kwa kuambiwa kuwa anapewa eneo kwa ajili ya viwanda, huku eneo lenyewe likiwa ni mali ya serikali.

“Sitaki ardhi itumike kama sehemu ya wafanyabiashara kutakatishia fedha zao chafu,” alisema Lukuvi na kuwataka watu wote wanaomiliki maeneo mijini kujisalimisha kwa maofisa ardhi wa wilaya wa ajili ya uhakiki.

“Hilo eneo ni mali ya serikali, halijawahi kuwa mali ya mtu huyo aliyetajwa na kumkabidhi mkuu wa mkoa. Amemdanganya mkuu wa mkoa, na sisi hatukubali, tutamshughulikia kwa niaba ya mkuu wa mkoa,” alieleza Lukuvi, baada ya kuwapo madai ya wananchi kulalamika kuwa wameporwa ardhi yao.

Aidha, wizara hiyo imetayarisha hati 214 kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliosalimisha ofa zao za umiliki wa ardhi kwenye wizara hiyo ili wamiliki ardhi hizo kihalali.

Lukuvi alisema ni rahisi kwa wananchi wenye umiliki wa ofa kutapeliwa kuliko wakiwa na umiliki wenye hati ambazo ni halali hivyo ili kuondoa changamoto hiyo wizara ilitoa muda kwa wananchi kupeleka ofa hizo ili watayarishiwe hati halali.

“Kuwa na umiliki halali wa ardhi ni jambo kubwa kwa usalama wa wananchi wenyewe, nataka ifike siku Tanzania iwe haina mtu anayemiliki ardhi kwa kutumia ofa kwa sababu sasa hivi wizara haitoi ofa, ofa hizo zilishakoma siku nyingi,”
alisema Lukuvi.

Aliongeza kuwa ingawa muda wa kusalimisha ofa hizo za umiliki umekwisha, lakini wizara hiyo inatoa muda zaidi kwa watu ambao bado hawajapeleka ofa zao katika halmashauri zao za wilaya kupeleka ofa hizo ili wamiliki ardhi hizo kwa hati.

Aidha, akizungumzia utayarishaji wa teknolojia itakayohusika na masuala yote ya ardhi inayojulikana kama ‘Mfumo Unganishi wa Ardhi’, Lukuvi alisema tayari Kampuni ya Kifaransa iliyoshinda zabuni inaendelea na kazi na Julai mosi mwaka huu hati ya kwanza ya kielektroniki ya mfano itatolewa.

Tayari jengo litakalotumika kwa ajili ya shughuli hizo limeshakamilika na mfumo huo bado unaendelea kutengenezwa ili kuwezesha wananchi wote wanaomiliki ardhi Tanzania wanamilikishwa hati za kielektroniki
.

Mbunge Awaomba Wananchi Wampige Mawe

$
0
0

Mbunge wa Korogwe Vijijini, Stephen Ngonyani maarufu Profesa Majimarefu, ametoa ruhusa kwa wakazi wa jimbo lake kumwadhibu kwa kumpiga mawe iwapo atashindwa kutekeleza ahadi alizoahidi wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Majimarefu aliyasema hayo wakati akizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mikutano ya hadhara na wananchi wa Vijiji vya Kwemshai, Ngulu na Mlungui, katika ziara yake jimboni mwake.

Alisema licha ya kuwa nje ya nchi kwa matibabu, lakini baada ya afya yake kuimarika amerejea nchini akiwa tayari kutatua kero za umma.

Aidha, amewaomba wapigakura wake kuendelea kushirikiana naye huku wakimpatia muda kumwezesha kuwatatulia kero hizo.
 
“Nawashukuru kwa kuniombea pale nilipokuwa nikiugua, nilikuwa nje ya nchi kwa matibabu sala zenu zimeniwezesha kuungana nanyi leo," alisema.

Aliwaeleza wananchi wa Kijiji cha Mlungi kuwa tatizo la maji na umeme viko mbioni kutatuliwa ndani ya mwaka huu na kwamba wale wanaoeneza maneno kuwa hakutafanyika kitu wanajidanganya kwa vile mambo yanakwenda sawa.

Majimarefu alisema katika kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo, ameamua kumkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mhandisi Robert Gabriel kusimamia Mfuko wa Jimbo kusaidia miradi.

Katika hatua nyingine, Majimarefu aliwashukia mahasimu wake wa kisiasa aliodai wanatumia mbinu chafu kumchafua kuhusu afya yake tangu alipougua na kwenda kutibiwa nje.

“Kuna mahasimu wangu wa kisiasa wanapita kila kijiji kuzungumzia afya yangu kwamba nimepoteza fahamu na kukatwa mguu, siyo kweli myapuuze,”alisema.

Majimarefu alisema wananchi wapuuze uzushi huo usiokuwa na msingi kwani una lengo la kuwavunja moyo kwa manufaa yao ya kisiasa.

Hata hivyo, alisema kuwa hatavunjika moyo kwa maneno hayo na badala yake yamekuwa changamoto kwake kutekeleza ahadi zake na hafanyi hayo kwa lengo la kujipatia umaarufu kama inavyodaiwa na baadhi ya watu ila ni moja ya utekelezaji wajibu wakekwa wananchi waliomchagua.

Majimarefu aliwaeleza wananchi hao kuwa wakati wa watu kufanya fitna umekwisha na uliobaki ni ule wa kusema ukweli akiwahimiza kufanya kazi sambamba na kulinda rasilimali misitu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Gabriel, alisema kwamba kazi yake ni kusimamia rasilimali za umma, hivyo atahakikisha kwamba yale yote yanayoanzishwa na mbunge huyo anayalinda.

Chadema yaweka ulinzi mkali nyumba ya mama Wema......Ni Baada ya Nyumba Hiyo Kupigwa Mawe Usiku

$
0
0
Nyumba ya mama Wema Sepetu, Mariam Sepetu, iliyopo Sinza Mori jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia jana imepigwa mawe juu ya bati kwa muda wa saa moja na nusu.

Kutokana na tukio hilo viongozi wa Chadema wamechukua hatua ya kuweka ulinzi mkali nyumbani hapo na kuzungumza kuwa wamegundua kitu ambacho hawatakiweka wazi kwa sasa.

Baada ya tukio hilo kutokea mama Sepetu aliwasiliana na mwanae Wema Sepetu pamoja na viongozi wa Chadema, ambapo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob alifika na kuangalia hali ya mama huyo na kuamua kuweka ulinzi.

”Tumeshaangalia mazingira yote tumegundua kitu ambacho hatuta kiweka wazi kwa sasa ila tutaweka ulinzi mkali na atakaye jaribu shauri yake hatuta kubali suala hili liendelee kumkuta kamanda wetu na mimi mara kwa mara nitafika kuangalia mazingira” amezungumza hayo Meya wa Ubungo, Boniface Jacob.

Meya alifafanua kuwa ulinzi huo hautaishia nyumbani kwa mama Wema bali hata nyumbani kwa Wema Sepetu ulinzi utaimarishwa kwani amegundua wanachama hao wapya wamekuwa wakiwindwa na watu wasiojulikana.

Wema alipohojiwa amesema, ” Mama yangu ameteseka usiku kucha kwa kukosa amani, amelia na kukosa hata hamu ya kula tumefika tumemkuta katika hali mbaya, najua yana mwisho ila tutazidi kufanya dua ya kumwomba Mungu atuepushie na mabaya yote,”.

Mama nae alihojiwa na kusema,” sikuweza kutoka nje kwa kuwa najua mbaya wangu amekaa wapi na amekusudia kufanya nini,”.

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL   BEAUTY COSMETICS

Ni kampuni inayotoa bidhaa original na zenye matokeo mazuri bila madhara wala kemiko ya aina yoyote. Bidhaa zetu zote zimetengenezwa kwa mimea na matunda. Tunawaletea punguzo la bei la %10 bidhaa tulizonazo ni kama zifuatazo.
 
     👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 170,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 100,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 110,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @100,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @100,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima kwa vidonge au dawa ya kunywa @150,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11 Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo la ndoa @120,000
12.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
13. kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @100,000/=
15. Kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake @100,000/= NK. [ Bidhaa zetu zote ni garantii pia hakikisha unapewa risiti ununuapo bidhaa kampuni hii popote ulipo utapata huduma zetu]
 
     WASILIANA NASI KWA NAMBA
        {065 9618585 au 0759029968.}
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
                               Karibu sana

Ridhiwani Aanika uhusiano wa Jakaya Kikwete na Lowassa.....Asimulia Jinsi Aliyopigiwa Simu na Baba Yake Baada ya Kupiga Picha na Lowassa

$
0
0
Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ambaye pia ni mtoto wa rais mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete ameeleza uhusiano uliopo kati ya baba yake na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuwa bado ni maswahiba.

Ridhiwani ametoa ufafanuzi huo kutokana na imani iliyojengeka kuwa kuna uhasama kati ya Dkt. Kikwete na Lowassa ambao awali walikuwa maswahiba wakubwa kabla ya siasa kuingiza doa kwenye uhusiano huo.

 Uhasama huo uliaminika kuwepo na kuongezeka hasa baada ya Dkt. Kikwete kuongoza kamati ya maadili ya CCM iliyoliondoa jina la Lowassa katika orodha ya waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais, hali iliyopelekea mwanasiasa huyo kuhamia Chadema na kugombea nafasi hiyo.

Akizungumza wikendi hii na mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo baada ya kuenea mitandaoni picha inayomuonesha akisalimiana na kuteta na Lowassa, Ridhiwani alieleza kuwa hakuna uhasama kati ya baba yake na mwanasiasa huyo mkongwe kama wengi wanavyoamini.

Aliongeza kuwa amewahi kuwashuhudia wakizungumza na kuwasiliana kama kawaida kwa njia ya simu mara kadhaa.

“Kwanza hakuna ugomvi kati ya watu hawa wawili. Unajua watu wanashindwa kuelewa kwamba hakuna urafiki katika masuala ya kazi. Kwa mfano suala lile la kumtafuta rais, jambo la kutafuta rais sio jambo la Jakaya peke yake,” alisema Ridhiwani.

“Ukweli wa mambo ni kwamba Bwana Lowassa na bwana Kikwete ni watu wanaosaidiana katika mambo mengi sana,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Ridhiwani alieleza kuwa baba yake alipoona picha yake na Lowassa wakisalimiana baada ya kukutana Jumamosi iliyopita Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya watani wa jadi, Simba na Yanga alimpigia simu kutoka Ethiopia na kumtaka kuendelea na hali hiyo kwani siasa sio vita.

“Kwa mfano hata jana jioni alinipigia simu, of course alikuwa yuko Ethiopia, akaniambia ‘bwana nimeona kwenye picha uko na bwana Edward [Lowassa] ilikuwa wapi hapo?’, nikamwambia nimekutana nae uwanja wa Taifa tulikuwa tunaangalia mpira,” “[Akasema] ‘aah naye alikuja kuangalia mpira’ nikasema ndio. Akasema ‘okay hayo ndio mambo mnayotakiwa kufanya, msifike sehemu mkaona kama siasa ni vita’.

“Kwahiyo ndio maana mimi baada ya kuongea naye akaniambia siasa sio vita, na mimi niliposhika simu yangu Instagram yangu nikaandika kwamba ‘tunaendelea kujifunza…. Lakini basically najifunza kutoka kwa maneno ya mzee wangu ambaye ameniambia kwamba ‘siasa sio vita na kwamba na ninyi katika umri wenu inabidi muendelee kujifunza’ kwahiyo hata mimi comment yangu kwenye Instagram, actually sababu yake kubwa ni hiyo,” alifafanua.

Ridhiwani alieleza kuwa alimuona Lowassa baada ya kipindi kirefu kupita hivyo aliamua kumfuata na kumsalimia ambapo pamoja na mambo mengine, Lowassa alimuuliza alipo Dkt. Kikwete na akampa salamu zake amfikishie na familia kwa ujumla.

Lowassa alilazimika kujiuzulu nafasi ya uwaziri mkuu mwaka 2008 katika Serikali ya Awamu ya Nne iliyokuwa inaongozwa na Dkt. Kikwete kutokana na sakata la Richmond.

Zitto Kabwe Atoa Kauli Nzito Kuhusu Sakata la Godbless Lema....Ataka ofisi ya DPP iwajibishwe

$
0
0
Kitendo cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini Mh. Zitto Zuberi Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe

Katika mtandao wake wa kijamii Mh. Zitto amedai kuwa kitendo cha  Mbunge huyo ambaye ni muwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana  ni siasa za ukomoaji ambazo zinajenga chuki kwenye jamii na chuki huwa zinazaa visasi.

"Haitoshi majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi" Ameandika Zitto Kabwe

Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja mapema jana baada ya  majaji watatu  kutoka mahakama ya rufaa kuitaka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipendezi na haingii akilini mtu  kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki ya dhamana.

"Mnatufanya wanasheria wote hatuna akili na mnachafua mpaka  mahakama, kwa hali ya kawaida mtu mumshikilie kwa misingi ya kisheria, lakini katika kesi hii tumepitia jalada hatujaona kitu chochote cha kumshikilia Lema hadi leo na imetushtua sana". Alisema Jaji Stella Mugasha.

Adama Barrow amtimua kazi mkuu wa majeshi Gambia

$
0
0
Rais wa Gambia Adama Barrow amemuachisha kazi mkuu wa majeshi wa nchi hiyo Ousman Badjie.

Hatua hiyo ya Rais Barrow imekuja kutokana na Badjie kutangaza mwezi Disemba mwaka jana baada ya uchaguzi mkuu kuwa atafuata amri ya Rais aliyepita Yahya Jammeh ambaye alishindwa katika uchaguzi huo.

Hata hivyo wanajeshi wa Gambia hawakuweza kutii amri kutoka kwa mkuu huyo wa majeshi ambaye alikuwa chini ya Jammeh ambaye baada ya muda alikubali kuachia madaraka hayo na kukimbilia nchini Equatorial Guinea.

Na sasa Masanneh Kinteh ambaye aliwahi kufanya kazi nchini Cuba anachukua nafasi hiyo ya Badjie. Baada ya kuteuliwa katika nafasi hiyo, Kinteh alitaja jambo lake la kwanza ambalo atalifanya katika jeshi lake ni kuwafanya wajiamini ili waongeze hamasa yao.

“My immediate priority as chief of defence staff is to bring back the confidence in the troops to lift their morale,” amesema Kinteh.

Mkuu wa shule Mkoani Singida ajinyonga hadi Kufa

$
0
0
Mkuu wa Shule ya Sekondari Tumuli katika Wilaya ya Mkalama, mkoani Singida, Richard Makala (58) amejinyonga kwa kamba kutokana na kile kinachodhaniwa ni upweke.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Debora Magiligimba, amesema mjini Singida kuwa Mkamala alikutwa amejinyonga kwa kutumia kamba iliyotengenezwa kwa vipande vya chandarua iliyofungwa juu ya mti umbali wa mita 130 kutoka nyumbani kwake.

Aidha kamanda huyo alisema chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na kwamba hakuna mtu au watu wanaoshikiliwa kutokana na tukio hilo na kuongeza kuwa polisi inaendelea na upelelezi kubaini kilichomsibu mwalimu huyo.

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya shule hiyo, Mabruki Ng’ui ameliambia gazeti la Habarileo Jumatatu hii kuwa mwalimu huyo alikuwa anaishi peke yake kwa muda mrefu baada ya mkewe ambaye ni Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Tanzania (KKKT) Kitusha wilayani Iramba kuamua kutengana naye kutokana na unywaji pombe.

“Huyu bwana amekuwa kwenye ndoa ya jina tu maana mke wake amekuwa akiishi mbali naye kwa kipindi kirefu sana, amekuwa mpweke kwa muda mrefu mno huenda hicho ndicho kilichosababisha ajitoe roho yake,” amesema Mjumbe huyo wa Bodi.

Marehemu Makala ni mzaliwa wa kijiji cha Ndago, wilayani Iramba na anatarajiwa kuzikwa leo nyumbani kwake, ameacha mjane na watoto watano.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa afungua mkutano wa watendaji Wakuu wa Mashirika ya umma,Ikulu

$
0
0
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa  mapema leo 28 Februari 2017, ameongoza mkutano wa siku moja wa watendaji wakuu na wenyeviti wa bodi za mashirika ya umma, unaojadili nafasi za mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili ya Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21), Unaofanyika Ikulu Jijini Dar e Salaam.

Mkutano huo ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazina,Waziri Majaliwa amewapongeza wakuu hao ambapo amewataka kuhakikisha wanaongeza juhudi na maarifa katika mashirika yao ili kusonga mbele.

Akisoma hotuba ya ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Mkuu Majaliwa amewataka wakuu hao kuongeza ubunifu zaidi ili kuongeza maarifa katika mashirika yao hii ni pamoja na kujiendesha kwa faida ili kuipunguzia Serikali mzigo wa kujiendesha.

Majaliwa amelipongeza Shirika la Nyumba NHC ambalo kwa miaka ya nyuma lilikuwa likiendeshwa kwa hasara, hata hivyo baada ya kuongeza ubunifu na kuingia kijana mzawa, wameweza kupiga hatua na sasa wamekuwa wa mfano wa kuigwa huku pia akipongeza baadhi ya mifuko ya Maendeleo ya Jamii pamoja na mabenki mengine kwa ikiongozwa na benki kuu, kutokana na kuwa na menejimenti nzuri, ubunifu na kutumia wataalamu waliobobea  katika fani zao, wameweza kufanya mambo makubwa.

“Kumekuwa na dhana potofu kwamba Mashirika ya Umma hayatakiwi kufanya biashara,  na kwamba yakifanya biashara lazima yapate hasara inaendelea kubaki kuwa ni dhana potofu. Ipo mifano mbalimbali” ameeleza Majaliwa huku akitolea mifano ya nchi zilizofanikiwa kwa mashirika ya Umma  kufanya vizuri  mfano

Mashirika kama Petrobras la Brazil, Statoil la Norway, CNOOC la China ambayo ni makubwa na yameweza kuwekeza nje  ya mipaka ya nchi zao.

Majaliwa amesema mpaka sasa Serikali imeweza kuwa na Mashirika ya umma 264 ambapo kati ya Mashirika hayo, Mashirika 65 ni Mashirika ya Kibiashara, Mashirika 187 ni mashirika ya  huduma wakati mashirika 12 ni udhibiti. Kati ya Mashirika 65 ya kibiashara, Mashirika 8 yanaendeshwa kwa ruzuku ya Serikali, wakati Mashirika 57 hayategemei ruzuku ya Serikali.

Awali akifungua mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi, Profesa Joseph Semboja amesema malengo ya mkutano ni kukusanya maoni ya viongozi kuhusu nafasi ya mashirika ya umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano, kuzungumzia changamoto tarajiwa katika utekelezaji wa majukumu haya na kutoa mapendekezo ya namna ya kukabiliana na changamoto hizo.

“Mashirika ya Umma yana nafasi na uwezo mkubwa wa kufanikisha utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2016/17–2020/21 wenye kaulimbiu ‘Maendeleo ya Viwanda kwa Mabadiliko ya Kiuchumi na Maendeleo ya Watu’,” amesema Profesa Semboja.

Profesa Semboja aliongeza, “Katika kuunga mkono jitihada za Serikali ya Rais John Magufuli, mkutano huu umewezakutanisha viongozi kutoka serikalini na mashirika ya umma kwa lengo la kubadilishana maarifa na uzoefu wa jinsi mashirika haya yatakavyoiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda kwa maendeleo endelevu.”

Mkutano huo unajadili namna ya kuboresha mifumo ya kiutendaji ndani ya mashirika na uhusiano miongoni mwa mashirika na taasisi za serikali, kufungamanisha mipango ya mashirika ya umma na Mpango wa Pili wa Maendeleo, kutathmini kiwango na aina ya rasilimali zinazohitajika kuwezesha utekelezaji wa mipango na; kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango.

Jumla ya washiriki 100,  kutoka wizara, mashirika ya umma na mamlaka za udhibiti takribani 52 nchini.

TFDA Yatoa Ufafanuzi Kuhusu Uvumi Wa Dawa Aina Ya P-500 (Paracetamol).

Waziri Nape: Sikupinga vita dhidi ya biashara ya dawa za kulevya bali nilishauri busara itumike

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa ufafanuzi juu ya kauli iliyonukuliwa ikionyesha kuwa alipinga vita dhidi ya dawa za kulevya iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda. Amedai kuwa hakupinga vita hiyo bali alitaka busara itumike kwa washukiwa.

Waziri Nape alitoa ufafanuzi huo katika kipindi cha dakika 45 cha ITV, alipoulizwa swali na mtangazaji wa kipindi hicho kutaka kujua kuhusu kauli yake iliyoonesha kupinga utaratibu uliotumika wa kuwakamata au kuwapata watuhumiwa wa dawa za kulevya.

“Niseme kwanza ilitokea nilikuwa na mkutano na waandishi wa habari, ukienda leo ukanitaja Nape ukaniambia baada ya siku mbili njoo kituoni, hata kama nilikuwa na madawa ya kulevya nyumbani kwangu hivi unayakutaje? 

'Kwasababu kwa vyovyote vile nitayachukua, ntayaficha, ntakuja kituoni ntaripoti utanibana ntakwambia twende nyumbani kwangu ukakague mnaenda mnakagua mnakuta hamna, si basi! 

"Kwahiyo nikawa na wasiwasi kwamba inawezekana kabisa nia ilikuwa njema lakini nilidhani pangeweza kutengenezwa utaratibu bora zaidi ya namna ya kuwapata, kwasababu hapa kuna watumiaji, kuna wauzaji na wale ambao wanaleta sasa madawa ya kulevya,” alisema Nape.

Aliendelea, “Ukishughulika na mtumiaji huyu ukadhani ndiye mhalifu wako unakosea, kwasababu huyu ni muathirika na muathirika anahitaji dawa anahitaji huduma ameshaathirika, hapa wahalifu wetu nikuanzia huyu anayemletea halafu kuna huyu anayempa yule aliyemletea, sasa ili uwapate hawa wawili lazima umtumie huyu vizuri ili akupeleke kwa hawa wawili. Lakini ukimkamata huyu ukamtia ndani sasa hawa wawili watakimbia.”

“Kwahiyo mimi nikaona kwamba tunaivuruga vita yenyewe, anayeingiza madawa ya kulevya na anayesambaza kwa maana ya kuyauza, hawa ndiyo tatizo letu. Na ndio maana nikasema hebu tutumieni busara, watu wakadhani nimepinga. 

"Tena mimi nilisema mara nyingi sana tumieni busara namna ya kuiendesha vita hii. Madhara ya kutotumia busara katika vita hii ni makubwa sana, kwasababu ukimweka huyu mtu mmoja ndani hawa wengine wataendelea kuwaathiri wengine na ndiyo maana nasema hii vita tutumieni busara. 

"Hii vita ni ya kupigana kimya kimya kwasababu wanaofanya biashara hii hawaifanyi hadharani wanafanya kwa kificho. Shughulika nao kwa kificho, hii vita hakuna mahali ambapo wameshawahi pigana hadharani, tukitajana hadharani hata wenye chuki watatajana humo humo,” alisisitiza.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya March 1

Waziri Mkuu Anusa Madudu Minada Ya Madini.......Amuagiza Kamishna wa Madini aende Mererani

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema anafuatilia kwa makini minada ya madini inayofanyika nchini kwa sababu anazo taarifa za kukiukwa utaratibu kwenye minada hiyo.

Amesema ukiukwaji huo unachangia kutobadilika kwa mapato ya mauzo yatokanayo na mnada hata kama kuna vito viliyokakatwa au havijakatwa.

Ametoa kauli hiyo juzi jioni (Jumatatu, Februari 27, 2017) wakati akihitimisha kikao alichokiitisha kwenye makazi yake Oysterbay jijini Dar es Salaam kilichojumuisha Mawaziri wa Fedha pamoja na Nishati, Mkuu wa Mkoa wa Manyara na watendaji wake, Mbunge wa Simanjiro, wamiliki wa mgodi wa Tanzanite One, watumishi waliofukuzwa kazi na wachimbaji wadogo.

Alisema licha ya kuwa Kitengo cha Uthaminishaji wa Madini ya Almasi na Vito cha Wizara ya Nishati na Madini (TANSORT) kinasifiwa kwa kuongeza mapato ya madini, bado kuna kazi ya ziada inabidi ifanyike kwenye minada hiyo ili Serikali iweze kunufainika na madini hayo.

“Uzoefu wa kwenye minada ya korosho unaonyesha kuwa wanaushirika ndiyo wanaiba fedha za wakulima. Nimekuwa ninafuatilia kwa muda sasa uendeshaji wa hii minada na sijaridhishwa na uendeshaji wake. Hakuna tofauti ya bei madini ya Tanzanite yanapokuwa yamekatwa au la,” alisema.

Kwa mujibu wa wataalamu wa madini na vito, inapotokea kuna madini yamekatwa bei inapaswa kuwa juu ikilinganishwa na madini ghafi yanapouzwa moja kwa moja.

Amemuagiza Kaimu Kamishna wa Madini, Bw. Benjamini Mchwampaka (ambaye alihudhuria kikao hicho kwa niaba ya Kamishna wa Madini) aende Mererani na kufuatilia utendaji kazi wa mgodi wa Tanzanite One na suala zima la teknolojia zinazotumika kiwandani hapo.

Waziri mkuu aliitisha kikao hicho kufuatia ahadi aliyoitoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mererani, wilayani Simanjiro, mkoani Manyara Februari 16, 2017 kwamba akimaliza ziara ya mkoa huo ataitisha kikao na wawekezaji wa Tanzanite One baada ya kupokea malalamiko kwamba hali ya watumishi ilikuwa nafuu wakati kampuni hiyo ilipokuwa inamilikiwa na wazungu kuliko ilivyo hivi sasa.

Ili kuhakikisha ukusanyaji wa mapato katika sekta ya madini unaongezeka, Waziri Mkuu amemwagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato (TRA) aimarishe ukaguzi kwenye viwanja wa ndege vya Arusha na Kilimanjaro (KIA),

“Kamishna wa TRA na watu wako inabidi mjipange kwa sababu kuna njia nyingi za ukwepaji kodi zinafanyika kwenye sekta ya madini wakiwemo hata hawa wachimbaji wadogo. Simamieni utaratibu wa kufuatilia kodi, nendeni kule walipo, msisubiri waje kuwaletea malipo ofisini. Wasipokuja je? Au wakija wakakuta mmetoka ofisini je?” Alihoji Waziri Mkuu.

Akizungumzia kuhusu uelewa wa sheria miongoni mwa wachimbaji wadogo, Waziri Mkuu alisema Wizara ya Nishati na Madini kupitia kwa Kamishna wa Madini wanapaswa kutoa elimu na uelewa wa kisheria kwa wachimbaji hao ili kupunguza migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza kwenye maeneo mengi nchini.

“STAMICO na Kamishna wa Madini fanyeni kazi pamoja, waelewesheni wachimbaji wadogo kuwa uwepo wa vitalu maana yake kuna mipaka ambayo pia inajumisha utoaji wa leseni kwa wenye vitalu hivyo. Kwa hiyo, waelimisheni kuwa mtu hapaswi kwenda upande wa pili wa mtu mwenye leseni, akifanya hivyo atakuwa anavunja sheria.”

“Ninyi ni wadau wakubwa wa sekta hii kwa hiyo mnapaswa kushiriki katika zoezi la kutoa elimu. Mnayo maeneo mengi ya uchimbaji lakini yana migogoro, mfano ni kule Ngaka na Kiwira. Maeneo yote haya yanahitaji usimamizi mzuri. Mnayo Bodi, Mwenyekiti yupo kwa hiyo mnatosha kuifanya kazi hii,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa mgodi wa Tanzanite One waboreshe mahusiano yao na vijiji vilivyo jirani na mgodi huo. “Kuweni karibu na wananchi ili wajue umuhimu wenu na uwepo wenu na waweze kusaidia kulinda mali zenu. Shirikianeni na Halmashauri na Baraza la Madiwani, tangazeni kazi zenu za CSR ili wananchi wajue mmechangia nini katika kusaidia maendeleo yao,” alisema.

Kuhusu suala la watumishi waliofukuzwa kazi kwenye mgodi huo, Waziri Mkuu amemwagiza Katibu Mkuu (OWM-Kazi, Ajira na Vijana), Bw. Erick Shitindi asimamie suala lao na kuwapatia majibu kuhusu hatma ya suala hilo.

Watumishi hao walikuwa wanawakilisha wenzao 201 ambao walifukuzwa kazi Februari 8, 2016 kwa sababu ya kufuatilia maslahi yao vikiwemo malipo ya saa za kazi za ziada (overtime), mishahara ya miezi miwili, malipo ya NSSF, vitendea kazi na usalama wa kazi migodini.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images