Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kauli ya TFF Kuhusu Watu Wanaotaka kuchoma Kadi za Chama Flani cha siasa Uwanja wa Taifa Leo

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limeonya vikali na kupiga marufuku watu kuingiza siasa katika mchezo wa leo kati ya Simba na Yanga

Akiongea leo na waandishi wa habari,Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa wamepata taarifa kuna watu fulani leo wanataka kuchana kadi za chama fulani, wengine wanataka kuchoma bendera za chama fulani kupitia mchezo wa leo kati ya Simba na Yanga, hivyo wameonya vikali watu wasijaribu kuingiza siasa zao kwenye michezo na kusema kwa yoyote atakayejaribu yatakayompata asije kuwalaumu TFF

"Kuna watu tumesikia na kuthibitishiwa kwamba kuna watu leo wanataka kuchana kadi za chama fulani cha siasa uwanja wa Taifa mbele ya mashabiki wa Simba na Yanga.

"Kuna wengine wamepanga kuzichoma moto, wako wale wengine wamepanga kuchoma hata bendera za chama hicho, wengine wanasema watafanya ndani ya uwanja wengine nje ya uwanja.

"Nitumie nafasi hii kuwaambia kwamba taarifa tunazo na tunatoa onyo kali kwa yoyote atakaye thubuti kufanya hayo wanayotaka kufanya kwani litakalo mtokea lisijekuwa lawama kwa TFF" alisema Alfred Lucas.


IKULU Yakanusha taarifa FEKI Inayosambazwa Mitandaoni kuhusu Rais Magufuli

$
0
0
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ametahadharisha umma kuhusu habari hii bandia inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii.

Msigwa ameandika kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa taarifa hiyo si ya Ikulu na kuwa imetengenezwa na wahalifu wa mitandao hivyo kwa kuwataka wananchi kuipuuza.

Hii ndo Taarifa ya uongo inayosambazwa 

Bodaboda Dar es Salaam mwisho saa 6 usiku

$
0
0
Jeshi ya Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limetoa wito kwa madereva bodaboda katika Jijini la Dar es salaam, kuacha kufanya shughuli hiyo ifikapo majira ya saa 6 usiku ili kupunguza uhalifu.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro, amesema kuwa jeshi hilo limebaini wahalifu wengi hutumia mwanya katika muda huo kutenda uhalifu ikiwa ni pamoja na kuwadhuru waendesha pikipiki.

Aidha, Kamanda Sirro, amesema, kuanzia Februari 18 hadi 23 Jeshi la Polisi Usalama Barabarani limefanikiwa kukusanya kiasi cha shilingi milioni 460 kutokana na makosa mbalimbali ya barabarani pamoja na kukamata pikipiki 1,280 kati ya hizo pikipiki 30 zimekamatwa kutokana na kupita katika njia ya mabasi yaendayo haraka huku madereva 27 wakifikishwa mahakamani.

Kuhusu suala la dawa za kulevya, Sirro aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mpaka sasa limefanikiwa kukamata jumla watuhumiwa 257 pamoja na kete za dawa za kulevya 1,526, puli 112 na misokoto ya bangi 247 kutokana na oparesheni inayoendelea.

Alisema baadhi ya watuhumiwa bado awajafikishwa mahakamani kwani upelelezi bado haujakamilika na mara baada ya upelelezi kukamilika watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili

Rais Magufuli Ateua VIGOGO Wapya Mamlaka ya BIMA, NHC

Simba Yaitandika Mabao 2 Yanga Uwanja wa Taifa Leo

$
0
0
Klabu ya Yanga ilianza vyema mchezo ndani ya dakika za mwanzo kabisa na kupelekea mchezaji Obrey Chirwa mwenye jezi namba 7 mgongoni kufanyiwa madhambi ndani ya kumi na nane na mchezaji wa Simba Novat Lufunga na kupelekea Yanga kupata penati ndani yaya dakika 4 za mchezo na kupigwa vyema na mchezaji Simon Msuva wa Yanga.

Yanga iliendelea kuongoza kwa bao hilo la kwanza huku wakiwa na moto wa kutafuta goli la pili, katika dakika ya 23 Yanga walipata kona ya kwanza ambayo ilipigwa na mchezaji Haruna Niyonzima lakini kipa wa Simba aliweza kuicheza vyema na kuondoa hatari ya Yanga kupata goli la pili ndani ya dakika za mwanzo mwanzo.

Kocha wa Simba Omug alipoona kikosi chake hakina mwenendo mzuri ndani ya dakika 27 alimtoa Luizio na kumuingiza Said Ndemla ambapo hapo kidogo mchezo kwa upande wa Simba ulibadilika na kuanza kufanya mashambulizi, huku wakijaribu

Ndani ya dakika 32 Goli kipa wa Yanga Deogratius Munishi alidaka mpira na kukaa nao kwa muda na kupeleka faulo ambayo ilipigwa na Said Ndemla wa Simba lakini Ndemla alikosa na kupoteza nafasi ya kusawazisha goli la kwanza.

Yanga iliendelea kufanya vyema na kujaribu mara kadhaa katika lango la Simba bila mafanikio, ndani ya dakika 43 Simba ilibahatika kupata faulo nyingine tena ambayo ilipigwa na mchezaji Ajib lakini mpira huo ulikwenda nje.

Mchezo uliendelea kwa kasi na mashambulio kwa timu zote mbili, na ilipofika dakika ya 47 mchezaji wa Yanga Thabani Kamusoko alitoka nje baada ya kupata majeraha na kuingia Said Juma Makapu.

Mpaka muda wa mapumziko Yanga ilikuwa ikiongoza kwa bao moja dhidi ya Simba huku ikiwa imetawala mchezo kwa asilimia 51 na Simba ikitawala mchezo kwa asilimia 41.

Baada ya kurudi kwa kipindi cha pili timu zote mbili zilikuwa na hamasa ya mchezo na ushindi hamasa hizo zilipelekea mchezaji wa Yanga, Endrew Vicenti alipata kadi ya njano ndani ya dakika 56 mchezaji wa Simba alipigwa kadi nyekundu na kutoka nje ya uwanja na kuwaacha Simba wakiwa pungufu uwanjani.

Katika kipindi cha pili baada ya kuingia mchezaji Kichuya Simba ilibadilika na kuanza kufanya mashambulizi ya mara kwa mara na kuonyesha uwezo katika kucheza mpira jambo lililopelekea mchezaji Mavugo wa Simba ndani ya dakika 66 kupata goli la kwanza kwa Simba na kuweza kusawazisha na kuwa bao moja kwa moja.

Mpka dakika ya themanini ya mchezo Simba kupitia kwa mchezaji wake Shiza Ramadhan Kichuya aliiandikia Simba goli la pili dhidi ya Yanga huku timu hiyo ikiwa pungufu uwanjani.

Mpaka mpira umekwisha Simba 2-1 Yanga (Mavugo 66, Kichuya 81 : Msuva 5)

Picha 8 za Mbowe, Lowassa , Nape na Wema Sepetu Walivyoshuhudia Yanga Ikitandikwa Mabao Mawili na Simba

$
0
0
Baadhi ya Viongozi wa Serikali na Siasa leo walikuwa miongoni mwa watu walioshuhudia mpambano kati ya watani wa jadi Simba na Yanga katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, ambapo mnyama Simba ameibuka kidedea kwa kuibamiza Yanga goli 2-1 licha ya kuwa pungufu kwa muda mrefu.

Viongozi hao ni pamoja Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu Chadema na Aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamal Malinzi na Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya February 26

Rais Museveni atembelea viwanda vya Bakhresa jijini Dar leo.....

$
0
0
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).

 Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz.

 Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).
 Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni(mweneye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa  Bw. Salim Aziz akimtambulisha Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.  
 Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akimwelezea jambo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni  na  Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Bakhresa  Bw. Salim Aziz.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiangalia namna Juisi ya Azam inavyotengenezwa alipofanya ziara katika Kiwanda hicho leo Jijini Dar es Saalam. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles Mwijage.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kundi la Makampuni  ya Bakhresa wakifurahia ugeni wa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni(hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo.

Rais Museveni Awakaribisha Watanzania Kuwekeza Nchini Uganda

$
0
0
 Na. Immaculate Makilika na Lilian Lundo- MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini Uganda.

Rais Museveni ametoa kauli hiyo leo wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni ya Bakhresa vinavyozalisha Unga na Juisi vya Buguruni na Vingunguti jijini Dar es Salaam.

“Nawakaribisha wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira” alisema Rais Museveni.

Kauli hiyo ya Rais Museveni imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji wa Kitanzania Said Salim Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano nchini humo.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani amesema kwamba Kampuni hiyo iko mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani 2,000 kwa siku nchini Uganda.

Aidha, amesema kutokana na uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya Waganda 650 wamenufaika na ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.

Kwa upande wa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania zimeingia makubaliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya viwanda.

Amesisitiza Watanzania wanaweza kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo wanalima tani milioni 4 za mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini humo.

“Tunawahamasisha wafanyabiashara wa Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili kuzalisha , bidhaa na ajira za kutosha kwa wananchi” alisema Waziri Mwijage.

Waziri Mwijage alitoa Wito kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kufanya uzalishaji wa bidhaa zinazotumika viwanda mfanio kwa kulima matunda au mbogamboga.

Rais Yoweri Museveni aliwasili nchini jana kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo akiwa nchini alifanya mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na kutembelea Viwanda vya Said Salim Bakhresa vya Tazara na Vingunguti.

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi TTCL na Kumuapisha Kamishna Jenerali Wa Jeshi La Zimamoto Na Uokoaji Pamoja Na Mabalozi Wanne

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Bw. Omary Rashid Nundu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Bw. Omary Rashid Nundu umeanza tarehe 24 Februari, 2017.

Bw. Omary Rashid Nundu anachukua nafasi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTCL Prof. Tolly Salvatory Augustine Mbwete.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Thobias Emir Andengenye kuwa Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Kamishna Jenerali Thobias Emir Andengenye anachukua nafasi ya Kamishna Jenerali Pius M. Nyambacha ambaye amestaafu.

Pia, Mhe. Rais Magufuli amewaapisha Mabalozi wanne walioteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali kama ifuatavyo;

Mhe. Dkt. Pindi Hazara Chana ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Nairobi, Kenya ambako anachukua nafasi ya Mhe. John Haule ambaye amestaafu.

Mhe. Silima Kombo Haji ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Khartoum, Sudan ambako anakwenda kufungua Ubalozi.

Mhe. Abdallah Abas Kilima ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Muscat, Oman ambako anachukua nafasi ya Mhe. Ali Ahamed Saleh ambaye amestaafu.

Mhe. Matilda Swila Masuka ameapishwa kuwa Balozi wa Tanzania Seoul, Korea Kusini ambako anakwenda kufungua Ubalozi mpya

Aidha Mhe. Rais Magufuli ameshuhudia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Mabalozi wote wanne wakila kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa ummakilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba na viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Pindi Chana kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya, tukio lililofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Silima Kombo Haji kuwa Balozi wa Tanzania nchini Sudani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Abdallah Kilima kuwa Balozi wa Tanzania nchini Oman, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Balozi Matilda Masuka kuwa Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akila kiapo cha Ahadi ya Uadilifu pamoja na Mabalozi Pindi Chana, Balozi Silima Kombo Haji, Abdallah Kilima pamoja na Balozi Matilda Masuka mara baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam.

PICHA NA IKULU

Rais Magufuli na Museveni Wakubaliana Kutosaini Mkataba wa EPA......Wadai EPA ni Ukoloni Mpya Kwa Waafrika

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Museveni kwa pamoja wamekubaliana kutosaini mkataba wa mahusiano ya kiuchumi na kibiashara kati ya nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA).

Makubaliano hayo yamefanyika jana Ikulu, Jijini Dar es Salaam ambapo  Rais Yoweri Museveni yuko nchini Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia tarehe 25 – 26  Februari, 2017.

Akiongea na waandishi wa habari Rais Magufuli amesema kuwa mkataba wa EPA hauna faida bali ni aina nyingine ya ukoloni ambao unataka kurejeshwa kwa nchi za Afrika.

“Nimeongea na Rais Yoweri Museveni amekubali kutosaini mkataba wa EPA, nitawaagiza wataalamu waliosaidia kutupa maelezo juu ya madhara ya mkataba huo kwenda pia Uganda kuwapa maelezo ambauo waliyatoa kwa Tanzania,” alifafanua Dkt. Magufuli.

Kwa upande wake, Rais Yoweri Museveni amesema kuwa ameongea na Rais Magufuli na wamekubaliana kutosaini mkataba huo na kuongeza kuwa suala la EPA ni lazima lijadiliwe na nchi zote za Afrika Mashariki ili kuwepo na msimamo wa pamoja kwa nchi zote za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha Rais Museni amempongeza Rais Magufuli kwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa kununua ndege mpya Sita, hivyo amekaribisha shirika hilo kutoa huduma za usafiri wa anga nchini Uganda kutokana na nchi hiyo kuwa na uhitaji wa huduma hiyo.

Vilevile amempongeza Rais Magufuli kwa ujenzi wa Reli ya Kiwango cha Kimataifa (Standard Gauge Railway) kutoka Dar es Salaa mpaka Mwanza na Isaka mpaka Rwanda ambapo itapelekea ujenzi wa bandari kavu katika mkoa wa Mwanza hivyo wafanyabiashara wa Uganda kunufaika na bandari hiyo ambayo itakuwa karibu zaidi kuliko ilivyo kwa Dar es Salaam.

Wakati huohuo Mawaziri wa Nje kutoka Tanzania na Uganda Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Oryem Henry Okello wamesaini makubaliano ya uhusiano katika mambo ya Diplomasia baina ya nchi hizo mbili.

Taarifa Muhimu: TCU yatolea ufafanuzi uhakiki wa wanafunzi wasiokuwa na Sifa Vyuoni

$
0
0
Tume ya Vyuo  Vikuu  Tanzania (TCU)  inapenda kuuarifu umma kuwa, uhakiki wa ubora wa wanafunzi wa elimu ya juu
hufanyika kwa mujibu  wa Kifungu  5(1)(b)(c)  cha Sheria ya
Vyuo Vikuu Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania.
 
Katika kutekeleza jukumu hili Tume ilianza zoezi la uhakiki kuanzia mwezi Agosti 2016. Hadi kufikia Februari 2017 zoezi
hilo lilikuwa limekamilika kwa vyuo 67 kati ya 84 vinavyotoa shahada ya kwanza. 

Hii ni mara ya kwanza uhakiki wa sifa za wanafunzi wa vyuo  vyote nchini kufanyika kwa wakati mmoja.  Lengo  la uhakiki lilikuwa kujiridhisha kuwa wanafunzi waliopo vyuoni ni wale waliodahiliwa kwa mujibu wa  sheria na taratibu  na kwamba wanakidhi vigezo  stahiki.
 
Uhakiki ulifanyika kwa kulinganisha taarifa za TCU na zile zilizowasilishwa na vyuo.  Uhakiki huo  ulihusisha jumla ya wanafunzi 131,994 waliopo vyuoni kwa mwaka wa masomo 2016/17.
 
Baada ya kulinganisha orodha zilizowasilishwa na vyuo na ile ya TCU ilibainika kuwa wanafunzi 123,827 sawa na asilimia 93.8  wanasifa stahiki.  Aidha jumla ya wanafunzi 8,167 sawa na asilimia 6.2 tu walibainika kuwa na kasoro  katika taarifa za sifa zao.

Kufuatia hali hiyo, Tume ilitoa taarifa kwa umma kuwaomba wanafunzi kurekebisha dosari hizo  kwa kuthibitisha taarifa zao  kupitia vyuo  husika ifikapo  tarehe 28  Februari 2017  ili kuweka kumbukumbu sahihi za mwanafunzi.
 
Hata hivyo  imebainika kuwa taarifa hiyo  imepokelewa kwa mtazamo na hisia tofauti na hivyo kusababisha mkanganyiko vyuoni. Umma unaarifiwa kwamba haikuwa nia wala lengo la Tume kusababisha mkanganyiko huo.
 
Kwa kuwa uhakiki wa sifa za wanafunzi ni kazi endelevu ya Tume na kutokana na maombi ya wadau  mbalimbali,  Tume sasa  itaendelea kuwasiliana moja kwa moja na vyuo  katika kukamilisha zoezi hilo. 

Hivyo  wanafunzi wote waliokuwa wameorodheshwa katika taarifa iliyotolewa awali wanaombwa kuwa watulivu  na kuendelea na masomo  yao kama kawaida.
 
Aidha ifahamike kuwa wanafunzi waliokuwa wameorodheshwa siyo kwamba wamethibitika kuwa hawana sifa stahiki bali kuna dosari katika taarifa zao. Ndiyo sababu Tume iliwaomba kuthibitisha taarifa zao  ili kuondoa dosari hizo.
 
Imetolewa na
Kaimu Katibu Mtendaji
24 Februari 2017

Kikwete: Siasa ni shule isiyokuwa na mwisho

$
0
0
Mbunge wa Chalinze mkoani Pwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Ridhiwan Kikwete, amesema siasa ni shule ambayo haina mwisho na ndiyo maana anaendelea kujifunza mengi kutoka kwa wanasiasa wenzake husani waliomtangulia bila kujali chama.

Kikwete alitoa ujumbe huo jana  mara baada ya kukutana na kuteta na aliyekuwa mgombea urais kupitia CHADEMA katika uchaguzi wa mwaka 2015, Edward Lowassa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wakati wa mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga.

Kikwete ambaye ni mwanachama na kiongozi ndani ya klabu ya Yanga, alimfuata Lowassa alipokuwa amekaa na kufanya naye mazungumzo ambayo hajayaweka wazi, na kisha kurudi sehemu yake huku akishuhudia timu yake ya Yanga ikilala mabao 2-1.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kikwete ameandika "Siasa ni shule ambayo haina mwisho. nahisi bado niko shule ya msingi na ninaendelea kujifunza".

Pia mbunge huyo alitumia fursa ya mchezo huo kukutana na mbunge wa Hai ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na kuzungumza naye mawili matatu.

Kikwete na Mbowe wote ni wapenzi wa Yanga, kwahiyo bila shaka wote waliondoka uwanjani hapo wakiwa na majonzi ya kipigo kutoka kwa Simba.

Mbali na hao, mechi hiyo pia iliwakutanisha mahasimu wengine katika siasa za Bongo, ambao ni Nape Nnauye na Edward Lowassa waliokuwa wamekaa katika eneo moja, ambapo Nape ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika mchezo huo

Vigogo Shirika la Posta watenguliwa nafasi zao.....Wengine wasimamishwa kazi

$
0
0
Taarifa kamili ya bodi hiyo kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wake, Dk. Haruni Kondo jijini Dar es Salaam jana.

  ***
Kwa kuzingatia maendeleo ya mageuzi makubwa yanayojitokeza katika sekta ya mawasiliano, Shirika la Posta Tanzania kama mtoa huduma kwa umma (Public Postal Operator), linawajibika kuhakikisha kuwa huduma za kisasa zinazozingatia vigezo vya ubora, usalama, uadilifu katika utendaji na uwajibikaji zinawafikia watu wengi zaidi katika maeneo yote ya nchi.
 
Kwa hivi sasa Bodi ya Wakurugenzi pamoja na Menejimenti imechukua hatua katika maeneo yafuatayo:-
 
1) KUPAMBANA NA UHALIFU WA MADAWA YA KULEVYA.
Shirika la Posta Tanzania limechukua hatua kadhaa ili kuhakikisha linashiriki na kuchangia kikamilifu jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano za kupambana na uhalifu, ikiwa ni pamoja na usafirishaji, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya, usafirishaji na utakatishaji wa fedha haramu, ugaidi, udanganyifu katika utambulisho pamoja na uhalifu mwingine wa kimtandao wa Kitaifa na Kimataifa.
 
Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika imedhamiria kuongeza msukumo na kasi ya usimamizi ili kupambana na uhalifu huu ambao una madhara makubwa kwa jamii.
 
Hatua mojawapo zilizochukuliwa na Shirika ni kusimika mfumo wa kisasa wa kudhibiti usalama na kurahisisha utambuzi wa vitu na matukio hatarishi na haramu yanayopitishwa au kujitokeza kupitia mtandao wa Shirika.
 
Mfumo huu uliogharimu zaidi ya shilingi milioni mia mbili (200) ambao unajumuisha ufungaji wa kamera za kiusalama (CCTV) katika Posta Kuu ya Dar es Salaam, tayari mzabuni aliyeusimika ameshakamilisha kazi yake na ataukabidhi kwa Shirika wiki ijayo na utazinduliwa rasmi wakati wowote kuanzia hapo.
 
Aidha, tumesimika mifumo ya kisasa ya kiusalama ikiwa ni pamoja na mashini za ukaguzi wa mizigo (baggage scanners) katika Ofisi zenye uwezekano wa kuwa uchochoro wa uhalifu wa aina hii ikiwa ni pamoja na Ofisi za Zanzibar, Kigoma, Dar es Salaam na Arusha.
 
Hatua hii imechukuliwa kwa kuzingatia kuwa matukio ya uhalifu uliopangwa (organized crimes) yamekuwa ni changamoto kubwa kwa Mashirika ya Posta Duniani na hivyo tumedhamiria kuhakikisha kuwa, mtandao wa Shirika wa Kitaifa sio uchochoro wa uhalifu huu.
 
Vitu visivyoruhusiwa kusafirishwa katika mtandao wa Posta kwa mujibu wa sheria ni pamoja na madawa ya kulevya, bidhaa za kemikali zenye sumu, silaha za moto na milipuko, wanyama hai, nyara za Serikali, vifaa vya mionzi, vyakula vinavyooza, betri za aina mbalimbali, vimiminika, fedha haramu, utakatishaji wa fedha na vitu vyovyote hatarishi.
 
Katazo la vitu hivi kusafirishwa katika mtandao wa Posta limezingatiwa katika sheria na taratibu mbalimbali za Kitaifa ikiwa ni pamoja na sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki na Posta (EPOCA) ya mwaka 2010, Umoja wa Posta Duniani (UPU), Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga (ICAO) na Shirika la Forodha Duniani (WCO).
 
Kwahiyo, Shirika la Posta Tanzania kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usimamizi wa sheria, kwa hivi sasa limeimarisha uhakiki wa mifumo yake na pia ukaguzi wa barua, vifurushi, vipeto na mizigo ili kujiridhisha juu ya usalama na uzingatiaji wa sheria.
 
2)   UANZISHWAJI WA JAMII CENTRE
Hatua nyingine iliyochukuliwa ni uanzishwaji wa kituo cha kisasa cha huduma ya Jamii Centre katika Posta Kuu ya Dar es Salaam iliyoko mtaa wa Azikiwe.
 
Maandalizi ya Ofisi ikiwa ni kaunta za kutolea huduma, mifumo ya mawasiliano, samani kwa wateja, mafunzo ya wahudumu na vifaa vya kazi tayari vimefungwa ili vitumike na kituo kiko tayari kwa uzinduzi, wakati wowote kuanzia sasa.
 
Kituo kinatoa huduma jumuishi za kimtandao katika sehemu moja (One Stop Community Centre) ili kuwapunguzia wananchi usumbufu wa kufuata huduma hizo maeneo mbalimbali tofauti.
 
Huduma zinazotolewa kwa njia ya mtandao kwa sasa ni pamoja na:-
  1. Malipo ya wastaafu (NSSF)
  2. Malipo ya gawio (dividends) za makampuni mbalimbali
  3. Malipo ya usajili wa Baraza la Mitihani
  4. Huduma za kibenki- CRDB
  5. Moneygram
  6. Maxmalipo (Road lincense), Luku, Ving’amuzi n.k
  7. Huduma mbalimbali za Posta.
Bodi imeelekeza Menejimenti kuendelea na ushawishi kwa makampuni na taasisi nyingine kama RITA, NHIF, NIDA, Mabenki n.k ili kujiunga na mfumo huu wa kisasa.  Hapo baadae zichukuliwe hatua za kufungua vituo vingine katika miji/mikoa ya Zanzibar, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Arusha na Morogoro kabla kufikia mwisho wa 2017.
 
3)   USIMAMIZI WA KADA ZA UONGOZI NA RASILIMALI WATU
Baada ya Bodi kufanya tathmini yake juu ya utendaji wa Wafanyakazi wa Shirika, imeelekeza Menejimenti ichukue hatua stahiki kwa kada zote za Wafanyakazi kuanzia hapa Makao Makuu, Zanzibar, Mikoani, Wilayani hadi Vijijini.
 
Bodi inatambua kuwa ufanisi wa Shirika hili utatokana na utendaji wa Rasilimali watu iliyopo. Kwa hivi sasa Shirika lina Wafanyakazi wenye ajira ya kudumu wapatao 1,082 hadi kufikia Disemba 2016 lakini, baadhi yao wanafanya kazi kwa mazoea na lazima sasa wabadilike.
 
Menejimenti iendelee kusimamia uwajibikaji wa Viongozi na Watumishi wa kada zote ndani ya Shirika ili kujenga nidhamu ya kazi, kujituma, kuheshimu kanuni na taratibu, kuongeza ubunifu na kufanya kazi kwa ufanisi wenye tija kwa Shirika.
 
Bodi inatambua jitihada za Menejimenti za kuwa na mkakati wa kuimarisha usimamizi na udhibiti wa nidhamu za Wafanyakazi hususani katika kuwaongezea uwezo, kutokana na mafunzo wanayopewa kulingana na uhitaji wa soko, utii, uaminifu na hamasa katika utendaji wa kazi.
 
Ili kuthibitisha hilo, Wafanyakazi wanapoajiriwa wanakula viapo vya utii na kutunza siri katika utendaji kazi wao na tunapenda kuendelea kuajiri Wafanyakazi wenye uwezo na fuzu sahihi ili kuendana na mabadiliko ya soko na Wafanyakazi waendelee kupewa mafunzo ya mara kwa mara ili kuongeza ufanisi na dhana ya kumjali mteja.
 
Aidha, kwa wakati huu kuna mwelekeo mzuri kwani Shirika limeanza kuwapima Wafanyakazi kwa kutumia mfumo wazi wa kazi (OPRAS) kwa kuanzia mwaka huu wa fedha 2016/2017, na itakapobainika kuwa wapo Wafanyakazi ambao hawakufikia viwango vya utendaji lazima wawajibishwe.
 
Kwa kuzingatia yote hayo, katika kikao chake cha jana  tarehe 24/2/2017 Bodi ilipitia kwa makini utendaji, uwajibikaji na nidhamu na uwezo wa watendaji wakuu katika Shirika hilo ambao wanatakiwa kuwa mfano bora wa uongozi wa utendaji mzuri .
 
Imebainika na kujiridhisha kuwa baadhi ya watendaji wakuu Makao  Makuu ya Posta wamekuwa kikwazo katika dhana ya uwajibikaji, weledi, na kujituma katika kutekeleza wajibu na majukumu yao ili kulifanya Shirika la Posta kuwa mfano bora wa Mashirika yenye ubora katika kutoa huduma.
 
Aidha, kuna baadhi ya vitendo kwa baadhi ya watendaji vinadhihirisha tabia ya umangimeza, urasimu, kufanya kazi kwa mazoea ubadhirifu na wizi.
 
Bodi imeamua kufanya mabadiliko ya uongozi wa juu wa Shirika la Posta kwa kutengua nafasi za watendaji wakuu:
1)   Meneja Mkuu Menejimenti ya ya Rasilimali za Shirika Ndg. James M. Sando na kumteua Ndugu Macrice Mbodo kukaimu nafasi hiyo.
2)   Meneja Mkuu uendeshaji wa Biashara Bi. Janeth Msofe na kumteua aliyekuwa Meneja Mkoa Shinyanga Ndugu. Hassan Mwang’ombe.
3)   Imemsimamisha kazi Ndugu. Jasson Kalile aliyekuwa Meneja Msaidizi Mail and Logistic.
4)   Imemsimamisha Kazi Ndugu Ambrose John aliyekuwa Senior Motor Transport Officer.
 
IMETOLEWA NA:-
MWENYEKITI
BODI YA WAKURUGENZI
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
DAR ES SALAAM

Mbunge Paulina Gekul anusurika Kifo......Alazwa ICU, Ziara yaahirishwa

$
0
0
Mbunge wa jimbo la Babati mjini Paulina Gekul amenusurika kifo baada ya gari lake lenye namba za usajili T 189 BHQ kuacha njia na kupinduka vibaya ambapo mbunge huyo alikuwa katika msafara wa naibu waziri wa Mazingira Luhaga Mpina wilayani Babati mkoa wa Manyara.

Baada ya ajali hii kutokea mmbunge Paulina Gekul ambaye ni mmbunge wa babati mjini akakimbizwa hospitali ya mkoa wa manyara na kulazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi I.C.U huku wanahabari wakikatazwa kuingia katika chumba hiki na madakatari ambao wanamuhudumia mbunge huyo 
 
Hata hivyo baada ya ajali kutokea naibu waziri wa mazingira amelazimika kuahirisha ziara yake ya kutembelea maeneo mbalimbali ndani ya mji wa babati huku mpina akiipongeza halmasahauri ya mji wa babati kwa kutambua umuhimu wa kutunza mazingira katika hali ya usafi baada ya kununua gari kwaajili ya kubebea taka lenye thamani ya zaidi ya milioni 200.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 27

CHADEMA Wamwandalia Sherehe Wema Sepetu.......Wapambe Wake 500 Wanaomuunga Mkono Kumfuata

$
0
0
Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), kimesema kipo kwenye maandalizi ya kumkabidhi kadi mrembo wa Tanzania mwaka 2006, Wema sepetu, pamoja na kundi lake lenye zaidi ya watu 500.

Wema alikuwa mmoja kati ya wanachama maarufu wa CCM katika kundi la wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka juzi kwa kaulimbiu ya ‘mama ongea na mwanao’.

Akiwa kama kiongozi wa wasanii, alishiriki kumnadi Mgombea Mwenza wa CCM ambaye kwa sasa ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Katika mkutano wake na wanahabari mwishoni mwa wiki,  Wema  alisema kwa sasa ameamua kuvaa magwanda na yupo tayari kwa mapambano.

Mkuu wa Idara ya Habari wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema), Tumaini Makene jana alisema   wapo kwenye maandalizi na kabla ya Machi 5, mwaka huu watamkabidhi Wema kadi ya uanachama   na kundi lake linalomuunga mkono.

“Wema atakabidhiwa kadi kwa utaratibu maalumu maana ameonyesha heshima na nia ya kujiunga kwenye mapambano ya kweli.

“Kwa kweli Chadema tunafarijika sana na kuja kwake maana kuna timu kubwa inayomuunga mkono pia wanataka kujiunga na chama.

“Tena na wengine wanatoka katika mashirikisho mbalimbali  ikiwamo TFF.  Kwa hiyo hapo unapata picha ya Wema ni mwanachama mpya wa Chadema mwenye mvuto wa aina yake na huwezi kubeza hata kidogo kuja kwake,” alisema Makene

Alisema   wakati wowote chama hicho kitatangaza lini mwanachama huyo atakabidhiwa kadi ya Chadema, tukio ambalo alisema litakuwa la aina yake.

Akizungumza nyumbani kwao Sinza, Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Wema alisema amechukua uamuzi wa kuhama CCM baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, kumtaja katika orodha ya watu wanaotumia dawa za kulevya.

Alisema kitendo hicho kilimdhalilisha kwa kiwango kikubwa.

“Nimeamua kufanya uamuzi wa kuhama CCM na sasa nahamia Chadema.  Sitaki nionekane labda nimepata hasira kulingana na tuhuma zinazonikabili, lakini nataka nionekane nimefanya uamuzi kama binadamu yeyote angeweza kufanya.

“Nimekubali na nimekiri kwamba nilisema nitakufa nikiwa CCM lakini ya Mungu mengi. Natamani ningejua awali, nasema sijachelewa, naamini uamuzi wangu nilioufanya ni sahihi na nimeingia kwenye vita.

“Nipo tayari kupigana, nina imani kwamba kutakuwa na watu wengine wapo nyuma yangu wengi watanifuata,” alisema.

Wema aliyekuwa na mama yake mzazi, Miriam Sepetu ambaye naye   alitangaza kuhama CCM na kuhamia Chadema, alisema alipokuwa kada wa CCM alikuwa mwaminifu na kwa kipindi chote alikipigania kwa uwezo wake wote.

“Nimetuhumiwa hivi karibuni na nilivyokuwa kama kada nilijitoa maisha yangu, utu wangu, nilipoteza muda wangu kupigania kile ambacho nilikiamini ni sahihi lakini siku moja kisinitupe na kinithamini kwa kile nilichokifanya lakini tofauti na nilivyokuwa natarajia havikutokea.

“Sisemi kama nilikuwa nafanya ili nije kubebwa kama princess (binti wa mfalme) ama queen (malkia) kwa sababu Wema ulikuwa unajitoa basi hata ukikosea usiadhibiwe au ukiwa unatuhumiwa usichukuliwe hatua, hapana, sijamaanisha hivyo,” alisema.

Alisema baada ya kushutumiwa aliamua kukaa kimya muda mrefu kwa kuwa alikuwa anatafakari alipokosea.

“Nimekaa kimya muda mrefu si kwamba nimefurahia kilichotokea, nilikuwa bado natafakari na kutathmini where did I go wrong (wapi nilikuwa nimekosea).

“Ni kitu gani ambacho nimekosa na kufanyiwa hichi nilichofanyiwa, nilichogundua ni kitu ambacho najua mwenyewe siwezi kusema nafurahia,” alisema.

Wema alisema kitendo cha kutuhumiwa bila wahusika kuwa na uhakika na tuhuma kimemnyong’onyeza na kumvunja moyo kwa kiasi kikubwa.

“Wanasema wenyewe ‘tenda wema nenda zako usingoje shukrani’, lakini siku ya mwisho siwezi kuwa mnyonge kwa sababu naamini there is something called democracy (kuna kitu kinaitwa demokrasia) katika nchi yangu na hicho ndicho nataka kukipigania,” alisema.

Alisema  uamuzi aliouchukua ni mgumu lakini hatarudi nyuma na anaamini kuna kundi kubwa la watu wasiopungua 500 watamfuata.

Kikwete aitamani nafasi ya Kinana CCM

$
0
0
Mbunge  wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amesema hatamani kuwa rais bali anataka siku moja awe Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam juzi  alipohojiwa katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds.

Jibu hilo la Ridhiwani lilitokana na swali aliloulizwa na watangazaji wa kipindi hicho kama ana ndoto za kuwa rais wa nchi.

“Sijawahi kutamani kuwa rais ila muda ukifika natamani kuwa Katibu Mkuu wa CCM,” alisema.

Ridhiwani alisema mafaniko yake hadi hapo alipofikia ni kutokana na mchango wa baba yake ambaye ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

“Malezi yangu, kuzaliwa na kiongozi kumenisaidia kufika hapa, nisingezaliwa huko labda ningekuwa mtu tofauti na nilivyo, mzee wangu ana mchango mkubwa hata jimboni, ananipa changamoto, ananielekeza, ana nafasi ya kunishauri,” alisema.

Pia alisema katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda, tayari Mkoa wa Pwani una viwanda 164 vikiwamo vinavyojengwa na vilivyokamilika, huku 84 vikiwa ni vikubwa.

Alisema uwekezaji wa viwanda hivyo umegawanyika katika sehemu mbili, chini ya Sh bilioni tano na ule ulio juu zaidi.

“Sehemu kubwa ni viwanda vya kuchakata malighafi, kuna vya matunda, marumaru, nondo, korosho, mabati, saruji na malighafi ya nyumba na vinavyofanya kazi nikivitaja ni zaidi ya 40,” alisema.

Ridhiwani alisema jimbo lake na mkoa wote wa Pwani, unafanya jitihada kuhakikisha bidhaa zilizokuwa zikipatikana China ziweze kupatikana Chalinze ili kuepuka gharama za usafirishaji.

Alisema uwekezaji wa kiwanda cha Twyford Tanzania Ceramics kilichotembelewa wiki hii na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, uligharimu Dola za Marekani milioni 158.

Ridhiwani alisema kiwanda hicho kinachotarajia kukamilika katika kipindi cha Julai hadi Agosti, kitakuwa na uwezo wa kutoa kontena 28 hadi 30 kwa siku.

Alisema kupitia kiwanda hicho, wananchi watapata faida kwa kufanya biashara na kuongezeka kwa ajira.

“Kitakuwa na ajira zaidi ya 2,000 zilizo rasmi, huku zisizo rasmi zikiwa ni zaidi ya 4,000. Hata hivyo, bado nasisitiza ajira izingatie wazawa kwa sababu wananchi tayari wanalalamikia upendeleo katika kupeana ajira, walioajiriwa pale wengi si wakazi wa Chalinze, hata Waziri Mwijage nilimwambia,” alisema.

Pamoja na jitihada hizo, alisema utekelezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda unaweza ukakwamishwa kutokana na uwezo wa kutafsiri neno na nia nzuri ya Rais Dk. John Magufuli.

“Rais hawezi kujenga viwanda peke yake, wasaidizi tutoe tafsiri sahihi ya nia yake nzuri, tutekeleze. Sitokubali kumdhalilisha rais, akisimama mwaka 2020 akiulizwa kuwa viwanda viko wapi aseme viko Pwani, atoe mfano Chalinze,” alisema.

Kamanda Sirro Asimulia Anavyosumbuliwa na Wanawake Usiku

$
0
0
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Kamishna, Simon Sirro amesema miongoni mwa changamoto anazokutana nazo ni pamoja kupigiwa simu za vishawishi na wanawake hasa usiku wa manane, wakidhani anapata pesa nyingi kwenye kazi yake.

Kamishna Sirro amefichua siri hiyo hivi karibuni akiwa kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, ambapo amesema pamoja na changamoto hizo, anajitahidi kukabiliana nazo kwa kuwa tayari amekwishawazoea.

Amesema kuwa kuna wanawake wengine wakiona amependeza kwenye tukio fulani, wanajua lazima atakuwa na pesa za kuwasaidia katika maisha yao hivyo wakati mwingine humpigia simu usiku, na yeye akidhani kuwa ni taarifa za uhalifu, lakini hukutana na vishawishi vikiambatana na sifa kedekede.

“Mwigine anaweza kukupigia simu tu usiku, kama unavyojua hawa wadada wa mjini, wakiniona wanajua niko vizuri, mwingine anakupigia anakuambia mzee tulikuona umevaa kofia vizuri, mjini kuna namna nyingi ya kuishi”. Amesema Kamanda Sirro

Aidha, Sirro ametaja changamoto nyingine ambazo hukutana nazo kuwa ni pamoja na suala la askari wake kulalamikiwa jambo linaloonesha dhahiri kama kiongozi ameshindwa kuwasimamia vijana anaowaongoza  na mara nyingi huwa anachukua hatua.

Hata hivyo, Lingine ni uhalifu kuzidi katika eneo fulani na hufanya wananchi kuwa na uoga, na kupoteza imani kwa Jeshi la Polisi jambo ambalo linamfanya yeye ajisikie vibaya zaidi kuliko hata wananchi, huku nyingine ikiwa ni viongozi wa mitaa kutowajibika katika kudhibiti uhalifu pamoja na kuletewa

Hashim Rungwe Amjulia Hali Godbless Lema Gerezani

$
0
0
Mwenyekiti  wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chauma), Hashim Rungwe, amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chadema), ambaye   bado yuko mahabusu katika Gereza la Kisongo mkoani Arusha.

Akizungumza na waandishi wa habari  mjini Arusha jana baada ya kuonana na mbunge huyo, Rungwe alisema baadhi ya matatizo yanayotokea kwenye jamii yanasababishwa na baadhi ya watawala.

Alisema hali hiyo imekuwa ikiibua chuki miongoni mwa wananchi   jambo ambalo si zuri na linahitaji kukemewa.

Kiongozi huyo alimtembelea Lema    akiwa  amefuatana  na viongozi mbalimbali akiwamo Makamu Mwenyekiti wa Chauma, Kayumbo Kabutali  na wabunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare na Moshi Vijijini, Antony Komu,  wote wa Chadema

“Historia ya zamani inatufunza matatizo yanayotokea katika jamii yanachangiwa na mambo yanayotendwa na baadhi ya watawala  ambayo yanaleta chuki.

“Na chuki siyo kitu kizuri kwa sababu inazidi kuwa kubwa kwenye mioyo ya watu hata kama wako kimya,”alisema na kuongeza:

“Hili limewahi kutokea enzi za mitume hata Nelson Mandela aliwekwa ndani na alipotoka dunia nzima iliamka hivyo tunaona kuna baadhi ya watu wanawekwa ndani bila sababu ya msingi, natoa wito kwa wenye mamlaka kuangalia suala hili.”

Mwenyekiti huyo alisema ni wakati wa watanzania wote kwa ujumla kupigia kelele suala hilo kwa vile  Mbunge ambaye ni mwakilishi wa wananchi, anazuiliwa kwa makosa yenye dhamana jambo la kukemewa.

“Tumekuja Arusha   kumuangalia Lema kwa sababu ni mwenzetu na tuna masikitiko na kama walifikiri wakimuweka Lema ndani wanamsimamisha au kumkomesha, wanamkomaza kisiasa.

“Anapata ujasiri wa aina Fulani kwa sababu  haelewi kwa nini yuko ndani, wangemkuta na malori matatu ya silaha sawa,” alisema.

Mbunge wa Bukoba Mjini alisema ameridhishwa na kupata matumaini na hali ya mbunge huyo kwa vile  ni yuleyule na ameongeza ujasiri wa kulisema lile analoamini.

Naye Mbunge wa Moshi Vijiji, Antony Komu,  alisema Lema ameomba wabunge wote bila kuangalia itikadi za vyama vyao wanapaswa kuwa makini wakati wa utungaji wa sheria.

Alisema   kutokana na baadhi ya upungufu wa sheria kuna watu wako gerezani kwa muda mrefu.

Alisema  katika gereza hilo asilimia kubwa wako gerezani kwa muda mrefu kutokana na upungufu wa sheria mbalimbali.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images