Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Jipatie BANDO Ambalo HALICHACHI Toka Tigo Pekee

$
0
0
Sasa unaweza kutumia dakika za maongezi, sms, na MB's zako bila presha ya muda mpaka ziishe. Bando lako #Halichachi

Watumishi Wawili Wa Tra Wakamatwa Kwa Tuhuma Za Kujihusisha Na Biashara Haramu Ya Dawa Za Kulevya

$
0
0
Oparesheni za kuwakamata watuhumiwa wanaojihusisha na dawa za kulevya nchini imefanikiwa kukamata watuhumiwa wawili waliohusika kupitisha kemikali bashirifu za dawa hizo aina ya ephedrine huku wengine wawili wakiwa bado wanasakwa na polisi

Akitoa taarifa hiyo leo Jijini Dar es Salaam Kamishna wa Oparesheni wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Mihayo Msikhela amesema watuhumiwa hao ni wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na wamegundulika baada ya kufanya uchunguzi wa ripoti ya majina iliyokabidhiwa kwao na uongozi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Kamishan Msikhela amesema taratibu zinazotumika kwa sasa za kuwakamata watuhumiwa wa madawa ya kulevya ni za kiusalama zaidi ili kuzuia watuhumiwa wasipoteze ushahidi.

Aidha, Kamishna Msikhela amesema katika operesheni ya kupambana na dawa za kulevya inayoendelea nchini mikoa ya Simiyu, Mara na Lindi inaongoza katika uteketezaji wa madawa ya kulevya ya bangi na mirungi kwa kipindi cha siku nne.
.

Waziri Mkuu: Kuanzia March 1 pombe za VIROBA Marufuku Kuuzwa Hapa Nchini

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia Machi mosi, 2017 Serikali itapiga marufuku matumizi ya pakiti za plastiki kufungashiwa pombe kali maarufu kwa jina la ‘viroba’.

“Tumekaa na wenye viwanda na kukubaliana kuwa wanaotengeneza Pombe waziweke katika ukubwa unaokubalika. “Sasa hivi viroba vimeenea kila kona hata watoto wa shule za msingi wanatumia kwa sababu ni rahisi kuweka mfukoni na kutembea navyo. Kuanzia tarehe moja Machi, tutakayemkamata ameshika pombe ya viroba, sisi na yeye.”

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 16, 2017) wakati akizumgumza na maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Mererani, wilayani Simanjiro akiwa katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Manyara.

Amesema agizo hilo linaenda sambamba na vita dhidi ya dawa za kulevya kwani mji wa Mererani unaongoza kwa matumizi ya dawa hizo haramu.

“Tutawakamata wanaosambaza, wanaouza na wanaokula. Hapa Mererani kuna bangi, kuna mirungi, cocaine na heroine. Mkuu wa Mkoa hapa panahitaji operesheni kupambana na dawa za kulevya. Piteni kwenye vijiwe na kukagua wale waliolegealegea, kisha tuwapime,” alisisitiza.

Akifafanua suala la uwekezaji kwenye eneo la Shambalai kutokana na ujumbe ulioandikwa kwenye mabango, Waziri Mkuu alisema katika eneo hilo zimetengwa ekari 500 kwa ajili ya EPZA ili kujenga miundombinu mbalimbali.

“Hilo eneo ni la uwekezaji kwa ajili ya ujenzi wa viwanda, masoko na maduka makubwa (malls). Sote tunafahamu kuwa Tanzania hivi sasa inaweka msisitizo juu ya ujenzi wa viwanda. Pale tunataka tuwe na viwanda vya nyama, vya kushona nguo na kuchakata madini ya Tanzanite ili kjongeza thamani,” alisema huku akishangiliwa.

Alisema kama kuna mtu ana uhakika kuwa nyumba yake bado haijalipwa fidia katika eneo lile, aende akaonane na Mkuu wa Mkoa huo, Dk. Joel Bendera lakini taarifa alizopewa ni kwamba hakuna mtu ambaye hajalipwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewaita wakurugenzi wa kampuni ya Tanzanite One ili wampatie taarifa juu ya malalamiko yanayotolewa na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwamba hali ilikuwa nafuu wakati kampuni hiyo ikimilikiwa na wazungu kuliko hivi sasa.

“Nikimaliza ziara ya mkoa huu, nataka tarehe 27 Februari, Wakuu wa hii kampuni waje ofisini kwangu na taarifa kuhusu shughuli za uendeshaji wa madini. Nitawashirikisha na wabunge wenu ili waje waseme kwa nini mzungu ni bora kuliko Mtanzania,” alisema.

“Serikali hii inatarajia kuona Watanzania wakinufaika na rasilmali zao. Haiwezekani tukahimiza uwekezaji wa ndani halafu leo anasifiwa mzungu kuliko mzawa,” alisema.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 17, 2017.

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Wageni Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 17 Februari, 2017 amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayeshughulikia masuala ya nishati Bw. Amadou Hott ambaye yupo hapa nchini kwa mazungumzo na wataalamu na viongozi yenye lengo la kuboresha sekta ya nishati hususan uzalishaji wa umeme.
 
Bw. Amadou Hott amekuja nchini ikiwa ni utekelezaji wa mazungumzo yaliyofanywa kati ya Mhe. Rais Magufuli na Rais wa AfDB Bw. Akinwumi Adesina Mjini Addis Ababa nchini Ethiopia tarehe 31 Januari, 2017 ambapo viongozi hao walikubaliana kuongeza ushirikiano kati ya AfDB na Tanzania katika maendeleo huku mkazo ukielekezwa kupata majawabu ya kuongeza uzalishaji wa umeme na wa gharama nafuu.
 
Bw. Amadou Hott ameelezea kuguswa na dhamira ya Mhe. Rais Magufuli juu ya kuongeza uzalishaji wa umeme na wenye gharama nafuu kwa ajili ya kufanikisha mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa viwanda, na ameahidi kuwa Benki hiyo itahakikisha dhamira hiyo inafanikiwa.
 
Kwa Upande wake Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia Bw. Amadou Hott kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote itakapohitajika ili kufanikisha dhamira hiyo.
 
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bharti Enterprises inayomiliki kampuni ya simu ya Airtel Duniani Bw. Sunil Bharti Mittal ambapo viongozi hao wamezungumzia utendaji kazi wa kampuni ya simu ya Airtel Tanzania ambayo Serikali ya Tanzania inamiliki asilimia 40 ya hisa za kampuni hiyo.
 
Baada ya mazungumzo hayo, Bw. Sunil Bharti Mittal ameelezea utayari wake wa kuingiza kampuni ya Airtel Tanzania katika soko la hisa la Dar es Salaam ili Watanzania wapate fursa ya kumiliki kampuni hiyo kwa kununua hisa.
 
Katika hatua nyingine, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapa nchini Mhe. Jean Pierre Tshampanga Mutamba Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais , IKULU
Dar es Salaam
17 Februari, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya February 18

Vurugu za mgambo na machinga zaibuka tena Jijini Mwanza

$
0
0
Vurugu na mvutano mkali umeibuka jana kati ya mgambo wa jiji la Mwanza na wamachinga wanaofanya biashara katika eneo la Makoroboi baada ya kutakiwa kuondoka mahali hapo. 

Eneo hilo lipo katikati ya msikiti unaomilikiwa na watu wenye asili ya Asia wa Swaminarayan na Shule ya watoto wadogo ya Tample. 

Uamuzi huo umekuja wakati tayari Rais John Magufuli alishaonya kutowavumilia viongozi wa mikoa watakaowaondoa wamachinga kwenye maeneo yao, kabla hawajawatafutia maeneo mbadala ya kufanyia biashara. 

Katika vurugu hiyo iliyotokea asubuhi jana inadaiwa kuwa mgambo mmoja alijeruhiwa baada ya kushambuliwa na wamachinga hao wakipinga kuondolewa eneo hilo. 

Hata hivyo, walipotafutwa viongozi husika kuzungumzia tukio hilo hawakupatikana kwa madai wapo kwenye vikao. 

Hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba aliwatangazia wamachinga wote ambao wapo katika maeneo yasiyo rasmi waondoke kufikia Februari 9, mwaka huu na kwamba atakayekaidi ataondolewa kwa nguvu. 

Wakizungumza katika eneo la tukio, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema hatua hiyo ilijitokeza baada ya kutakiwa kuondoka katika eneo hilo.

 “Tulipofika hapa asubuhi tulikuta, sehemu tunayopanga bidhaa zetu kuna mgambo wa jiji wakisema hakuna mtu kuingia wala kufungua biashara eneo hilo, mgambo walianza kutufukuza,” alisema Ally Erick. 

Shuhuda mwingine alisema kutokana na hasira waliyoipata watu hao walilazimika nao kujihami kwani mgambo hao walishindwa kutumia busara baada ya kutaka kuwaondoa kwa kuwapiga virungu. 

Alisema baada ya kuzidiwa walilazimika kuomba nguvu mpya kutoka kwa askari wa kutuliza ghasia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema yupo kwenye kikao na Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Hosiana Kosiga alisema naye yupo kwenye kikao.

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Merry Tesha alisema hayupo eneo lake la kazi badala yake atafutwe Mkuu wa Wilaya ya Ilemela anayekaimu nafasi hiyo, Dk Leonal Masale,hata hivyo alipopigiwa simu iliita bila kupata majibu.

Mwanamke asimulia alivyobakwa na askari Msumbiji

$
0
0
Wakati Serikali ikiahidi kufanya uchunguzi wa vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu katika kutimua Watanzania nchini Msumbiji, mwanamke mmoja amesema alibakwa na askari watatu kabla ya kuwekwa mahabausu ambako alikaa siku tatu bila kula. 

Mwanamke huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Halima (si jina lake halisi) ni mmoja kati ya zaidi ya Watanzania 180 ambao wamekuwa wakitimuliwa nchini Msumbiji tangu mwanzoni mwa wiki na wengi wakidai wana hati halali za kuishi nchi hiyo jirani na wengine kulalamikia vitendo vya ukiukwaji haki wakati wa utekelezaji wa operesheni hiyo. 

Tayari Serikali imesema kuwa itafanya uchunguzi wa madai hayo, ambayo yanaweza kuharibu uhusiano wa muda mrefu wa Tanzania na Msumbiji. 

Halima anasema walianza kufukuzwa usiku wa Jumamosi ya Februari 11, muda ambao askari hao waliutumia kumfanyia kitendo hicho. 

Halima anasema kuwa alisikia watu wakivunja geti la nyumba waliyokuwa wakiishi na kudhania ni majambazi, kumbe walikuwa ni askari ambao waliwalazimisha kutoa nyaraka zao zote za kuishi Msumbiji pamoja na pesa. 

“Niliwasikia wakivunja geti nikamwambia mume wangu watakuwa ni majambazi kumbe askari, mume wangu akajificha chini ya uvungu, lakini wakamtoa na baadaye kututoa ndani na kuanza kutupiga.” 

Anasema baada ya kipigo walilazimishwa kuzoa mali zao kutoka ndani na zikawekwa kwenye gari la polisi na kisha kuwafunga mikono na baadaye kuwapeleka mahabusu. 

“Cha kushangaza tulibebeshwa vitu wenyewe kuweka kwenye gari pasipo kuelezwa sababu baada ya hapo askari akanivuta nyuma ya nyumba na kuniingilia kimwili. Nikajua ni mmoja, lakini waliendelea hadi wakafikia watatu,” alisema. 

“Ninaona aibu walinibaka kwa njia ya kawaida tofauti na taarifa za wengine wanaosema tulibakwa kinyume na maumbile, si kweli. Nawaomba waelewe hatukubakwa kinyume na maumbile kama wanavyosema ilikuwa kawaida.” 

Hata hivyo anaeleza baada ya hapo waliwekwa mahabusu kwa siku tatu pasipo kula, hali iliyowalazimu kunywa maji yaliyokuwa yamewekwa chooni. 

“Tulikaa mahabusu siku tatu, hamna kula wala kunywa, chooni tulienda kwa mtutu tukalazimika kunywa maji ya chooni kwa sababu hakukuwa na jinsi na njaa ilizidi. Kwa hiyo inabidi useme unakwenda chooni ili ukanywe maji,” alisema Halima. 

Kutokana na hali hiyo, Halima anashangazwa na kauli ya Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Susan Kolimba kwamba waliorudishwa hawakuwa na nyaraka huku kaimu balozi wa Tanzania nchini Msumbiji akiwatangazia wengine kuondoka ndani ya siku tano. 

“Kweli mtu utathubutu vipi kuishi nchi ya watu bila kibali? Hata kaimu balozi na yeye anatukana, kwamba hatujaingia na documents (nyaraka)? Ilibidi atutetee lakini katukana. Mungu atatulipia,” alisema. 

Mwanamke mwingine aliyewekwa mahabusu kabla ya kurudishwa nchini, Mary Makundi anasema askari wa kiume walimwambia awape fedha na alipowajibu kuwa hana, walimpekua na kuzikuta. 

Anasema walizichukua fedha hizo pamoja na simu kabla ya kumpiga na kutaka kumbaka.

“Walivunja mlango wakanikuta. Wakaniambia niwape nyaraka zangu. Nikawapa nikijua wanazikagua tu na kuniacha, lakini cha kushangaza walizichana mbele yangu na kunitaka niwape pesa na simu. Nikawaambia sina wakanipiga na kunikagua hadi sehemu za siri na kuchukua pesa na simu,” alisema Mary. 

“Baada ya hapo walinipiga kwanza kabla ya kunifunga mkono. Askari mmoja akataka kunibaka, nikamwambia kuwa hata kama hawatutaki nchini kwao, hawawezi kuniingilia bila kinga. 

“Nilipoona hali imekuwa mbaya, nilisema wacha nigombane nife kwa silaha, lakini si kubakwa.” 

Mtanzania mwingine Mohamedi Said ni mmoja wa wafanyabiashara walioambiwa waondoke pasipo kuchukua chochote na anadai kuacha mali zake zote pamoja na nyumba aliyojenga. 

“Polisi walikuja ghafla wakatuambia wageni wote tunatakiwa tuondoke. Hapa nina vibali vyote mpaka leseni ya biashara, lakini imebidi niondoke kwa sababu ya usalama wangu,” alisema Said. 

“Hakuna anayejua sababu mpaka sasa. Nimekuja nyumbani kufuatilia haki yangu kwa sababu mpaka kibali cha kujengea ninacho. 

“Mpaka sasa amekuja kaimu balozi kutoka ubalozi wa Tanzania na amesema kwa ripoti aliyopewa ametupa siku tano tuondoke. Hatujui kwanini siku tano. Utahamishaje vitu kwa siku tano au kumtafuta mnunuzi wa nyumba kwa siku tano kwa sababu imenibidi niache duka kubwa na gari,” alisema Said. 

Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani na Msumbiji, Mohamed Mkama alisema wananchi wa kijiji chake wamekuwa wakishirikiana na wanakijiji wa vijiji jirani vya Msumbiji, lakini tukio hilo limewashangaza. 

Amesema mara nyingi wamekuwa wakitembeleana na hata wengine kutoka upande wa Msumbiji kuja kutibiwa Tanzania kutokana na ujirani mwema uliopo. 

“Kijiji changu kina vitongoji vitano ambavyo tumekuwa tukishirikiana na kijiji cha upande wa pili kwa muda mrefu na wengine wana vitambulisho vya uraia mwema, lakini tunashangaa kwanini wanarudishwa pasipo kuelezwa sababu,” alisema Mkama. 

Ofisa uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama alisema idadi ya Watanzania waliorudi na kusajiliwa katika mpaka wa Kilambo ni watu 221 hadi kufikia jana mchana. 

Serikali yajipanga kuzuia uvutaji sigara hadharani

$
0
0
Wizara ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema ipo katika hatua za mwisho za kutayarisha mwongozo wa kupiga marufuku matumizi ya uvutaji wa sigara hadharani ili kudhibiti maradhi yasiyoambukiza yanayotokana na sigara.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu uvutaji wa sigara hadharani katika sehemu za mkusanyiko na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi.

Alisema tayari Wizara ya Afya imewasilisha muswada wa kulinda afya ya jamii ambao moja ya kazi yake kubwa ni kupambana na matumizi ya sigara katika jamii na sehemu za mkusanyiko.

Akifafanua zaidi, alisema utafiti uliofanywa kuhusu maradhi yasiyoambukiza unaonesha kwamba upo kwa asilimia 38 ambayo yanahusishwa na uvutaji wa sigara.

Kombo alisema mwongozo huo ukikamilika utaletwa mbele ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na wajumbe kutoa maoni yao kabla ya kufanya kazi na kuwa sheria inayotakiwa kutekelezwa na kusimamiwa.

Alisema yapo matumizi mabaya ya uvutaji wa sigara hadharani ikiwemo sehemu za mikusanyiko ya watu kama hospitalini na sehemu za kusubiri usafiri wa abiria na kusababisha madhara makubwa ambayo hayaonekani kwa mara moja.

Manji alazwa tena Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete

$
0
0
Baada  ya kupata dhamana ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu juzi, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, amelazwa tena kwenye Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyoko katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na Ofisa Uhusiano wa Taasisi hiyo jana, Anna Nkinda, Manji alifikishwa hospitalini hapo juzi jioni ikiwa ni muda mfupi baada ya kupata dhamana dhidi ya kesi ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin inayomkabili.

“Ni kweli Manji yupo hapa, aliletwa jana jioni (juzi) kwa matibabu ambapo hadi leo (jana) ninavyoongea na wewe bado yupo hapa amelazwa anaendelea na matibabu kama kawaida,” alisema Anna.

Hii ni mara ya pili kwa Manji ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu, kulazwa kwenye taasisi hiyo.

Mara ya kwanza ilikuwa ni Februari 12, mwaka huu alipolazwa hapo akitokea katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, alipokuwa ameshikiliwa tangu Februari tisa akifanyiwa mahojiano.

Mfanyabiashara huyo alifika mwenyewe kwenye kituo hicho cha polisi kutokana na wito uliotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliyetaja majina 65 ya watu aliodai wanajihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Mbali na Manji, baadhi ya watu wengine waliotajwa na Makonda na kutakiwa kufika kituoni hapo ni Mchungaji wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, Mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azzan ambao tayari wamehojiwa polisi huku Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, akiwa bado hajahojiwa licha ya kutajwa kwenye orodha hiyo.

Juzi Alhamisi, Manji alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo shauri lake lilisikilizwa na Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Cyprian Mkeha.

Karani wa mahakama hiyo, Sarah Mulokozi, alimsomea mshtakiwa shtaka lake ambapo alidai kuwa kati ya Februari 6 na 9, mwaka huu eneo la Upanga Sea View jijini Dar es Salaam, Manji alitumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Mtuhumiwa huyo alikana shtaka hilo na Mkurugenzi wa Mashtaka Msaidizi (ADPP), Osward Tibabyekomya, alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuiomba Mahakama kupanga tarehe nyingine ya kutajwa.

Upande wa mawakili wa utetezi ambao ni Alex Mgongolwa na Hudson Ndusyepo, waliiomba Mahakama kumpa mshtakiwa dhamana  kwa sababu ya mashtaka yanayomkabili yanadhaminika.

Hakimu Mkeha alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kutakiwa kusaini hati ya dhamana ya Sh milioni 10 pamoja na mdhamini mmoja wa kuaminika ambapo Katibu Mkuu wa Klabu ya Yanga, Charles Mkwasa, alimdhamini Manji, ambaye aliachiwa kwa dhamana hadi Machi 16.

Mara baada ya kupata dhamana, Manji aliondoka mahakamani hapo saa 9:40 akiwa kwenye gari yenye namba T670 BBX aina ya Hummer.

Waziri Mkuu Awazuia Kuwatangaza Hadharani Watuhumiwa wa Dawa za Kulevya Kabla ya Kuwachunguza Kwanza

$
0
0

Wakati Serikali ikiendelea kujipanga kwa vita dhidi ya dawa za kulevya, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa na wilaya kutotangaza majina ya watuhumiwa kabla ya kufanyika uchunguzi na kujiridhisha. 

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kulaumiwa na watu tofauti kwa kitendo chake cha kutangaza majina ya watu aliotaka kufanya nao mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya. 

Wengi waliokosoa kitendo hicho, hasa wabunge, walisema kutangaza majina ni kuharibu uchunguzi na pia kunachafua watu kabla ya kuthibitika kuwa wanajihusisha na dawa hizo na kwamba chombo pekee kinachoweza kumtia mtu hatiani ni mahakama. 

Watu walioitwa kituo cha polisi jijini Dar es Salaam, wakiwemo wanasiasa, wafanyabiashara wakubwa, viongozi wa dini na wasanii walihojiwa na baadhi kupekuliwa majumbani na ofisini kwao kabla ya kwenda kupimwa. 

Baadhi ya watuhumiwa hao ni  kiongozi wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji na msanii nyota wa filamu, Wema Sepetu. 

Akizindua Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya uliofanyika ofisi ya waziri Mkuu jana, Majaliwa alisema wakuu wa mikoa wana nafasi nzuri ya kushiriki katika vita hiyo kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu. 

“Wakuu wa mikoa mna kazi kubwa katika vita hii. Mkiwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama, mpo kwenye nafasi nzuri ya kuendesha vita hii kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu,” alisema Waziri Mkuu mbele ya mawaziri ambao ni wajumbe wa Baraza la Taifa la Kudhibiti Dawa za Kulevya na wakuu wa mikoa. 

“Jiepusheni kuwatangaza watuhumiwa kabla hatujafanya uchunguzi. Itakapotokea uchunguzi umekamilika na kuwakamata watuhumiwa, msisite kuwatangaza kwenye vyombo vya habari, msiogope. Serikali inawategemea na itaendelea kuwaunga mkono,” alisema.

Pamoja na hayo, Majaliwa alisema Serikali haitawavumilia watendaji wa mamlaka watakaochukua rushwa kwa lengo la kuwasaidia wahusika wa dawa za kulevya. 

Alisema anafahamu kuwa mapambano dhidi ya dawa za kulevya ni vita kubwa na hilo linatokana na kuhusisha wafanyabiashara wakubwa na watu maarufu. 

“Watendaji wa mamlaka kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kufahamu kuwa mmeaminiwa, hivyo muwe waadilifu kwani mmekabidhiwa makubwa yanayohitaji uangalifu wa hali ya juu,” alisema.

 Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kuendelea kuimarisha mapambano dhidi ya udhibiti wa dawa hizo nchini na hilo litafanyika bila uonevu wala upendeleo. 

“Dawa za kulevya ni tatizo kubwa. Tanzania imekuwa ikitumika kama njia ya kupitishia dawa hizo, hivyo mapambano yanapaswa kufanyika kwa nguvu kubwa. Sheria ya udhibiti isimamiwe kikamilifu; masharti yote yaliyotajwa yatekelezwe bila kumuonea mtu,” alisema Majaliwa ambaye kwa nafasi yake anakuwa mwenyekiti wa baraza hilo. 

Alisema baraza hilo lina wajibu wa kusimamia utekelezaji wa sera ya udhibiti wa dawa za kulevya nchini. 

“Jukumu hili ni kubwa. Sisi kama wajumbe wa baraza tunatakiwa kulitekeleza kwa uadilifu na umahiri mkubwa. Sina shaka na wajumbe,” alisema.

"Nisingejiingiza kwenye kutumia dawa za kulevya ningekuwa tajiri sana-" TID

$
0
0
Msanii Khalid Mohamed maarufu kwa jina la  TID, amekiri kuwa kujihusisha kwenye utumiaji wa dawa za kulevya kumemrudisha nyuma kiuchumi.

Akiongea kwenye kipindi cha XXL, kupitia Clouds FM Ijumaa hii, Mnyama ambaye alikiri hadharani kuwa mmoja wa mastaa walioathirika na matumizi ya dawa hizo, alisema hadi sasa angekuwa na utajiri wa kushangaza. Anasema dawa hizo zina gharama kubwa.

“Nadhani ningekuwa nimenunua kama magari mengine manane, ningekuwa nimefanya video za muziki kadhaa zenye kiwango kikubwa. Lakini nilitumia hela nyingi sana hasa pale ninapoenda kujirusha ningetumia hela nyingi sana,Lakini hii imefikia mwishoni,"alisema TID.

Staa huyo amedai kuwa dawa zilimfanya awe na mtazamo tofauti katika vitu vingi ambavyo alivichukulia rahisi rahisi.

“When you are high you think you are on top, nobody can touch you sababu you are under influence unaanza kugombana na watu, ukawajibu watu vibaya, but when you are clean unaweza ukafanya vitu, you can save a lot of money, you can be a better person, you can even marry a good girl, you can fall in love,” amesema Mnyama ambaye amejitolea kuwa balozi wa vita dhidi ya matumizi ya dawa za kulevya.

“It’s over now.”

Kwenye show hiyo TID aliachia wimbo mwingine uitwao Woman ambao amedai kuwa remix yake atamshirikisha Diamond.

Habari Zilizopo Karika Magazeti Ya Leo Tarehe 19, February

Tiba ya Tatizo la Nguvu za Kiume, Maumbile Madogo na Kuchelewa Kufika Kileleni

$
0
0
Tatizo la nguvu za kiume limekua kubwa sana kwa wanaume wengi pia hata maumbile kuwa madogo sana.  

Lakin tatizo hilo kupitia  kampuni ya NATURAL BEAUTY COSMETIC limepata uvumbuzi wa matatizo hayo na kuyapatia dawa. 

Kwa tatizo la nguvu vipo vidonge ambavyo tunauza @120,000/=  Na tatizo la maumbile tunayo dawa ya kupaka yenyewe ni @130,000/= 

Pia ipo mashine original ya HANDSOME UP.Hiki ni kifaa ambacho unatumia kulingana na size unayohitaji wewe. Mashine hii inapatikana kwa @170,000/= 

Pia ipo spray ambayo ni dawa  kwa ajili ya kuchelewesha wakati wa tendo la ndoa, inapatikana kwa @110,000/=. 

Pia zipo zingine nyingi au unaweza kutufollow us Instagram @natural2162.  

Ununuapo bidhaa kampuni ya NATURAL BEAUTY COSMETIC hakikisha unapewa na risiti,pia bidhaa zetu zote ni guarantee ili kukuhakikishia mafanikio yako. 

Wasiliana nasi kwa namba.  0759-029968 au 0659-618585 popote ulipo utapata huduma zetu karibu sana.

Amiri Jeshi Mkuu Rais Magufuli Atunuku Kamisheni Kwa Maafisa Wapya 165 Wa JWTZ Ikulu Jijini Dar Es Salaam

Mbowe Asakwa na Polisi Kila Kona.....Apewa Masaa 48 Ajisalimishe Mwenyewe Kwa Sirro. Masogange, Chid Benz Mahakamani Kesho

$
0
0
Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro amesema endapo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti kituoni kesho (saa 48 tangu jana), atatafutwa kwa namna ambayo jeshi hilo litaona inafaa.

Mbowe ni miongoni mwa watu mashuhuri waliotajwa hivi karibuni katika orodha ya watu 65 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wanaodaiwa kujua taarifa za wanaojihusisha na dawa za kulevya. 

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamishna Siro alisema Mbowe kupitia kwa baadhi ya viongozi aliwajulisha angeripoti Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, Jumatano ya Februari 15, lakini alikuwa hajaripoti hadi jana 

“Jumatatu asiporipoti kutakuwa hakuna namna ya kulizuia tena Jeshi la Polisi kutafuta namna ya kumuhoji,” alisema. 

“Mheshimiwa Mbowe tunamheshimu sana kama kiongozi wa chama kikubwa cha siasa na hata akiwa bungeni ameonekana akipinga kwa nguvu suala la dawa za kulevya na anasikitika kuona vijana wa Kitanzania wanateketea. 

"Asitafute namna nyingine, tunamuhitaji kwa ajili ya kumuhoji kutokana na hizi tuhuma za dawa za kulevya,” alisema Siro. 

Alisema kiongozi kama Mbowe hatakiwi kuwa mtu wa kuta- futwa. ”Jeshi la Polisi lisingependa kuwa na mvutano na yeye, najua anajua kuwa tunamtafuta. 

"Jana (juzi) tumejitahidi kumtafuta kwa simu hajapatikana, tumekwenda nyumbani kwake hatujampata na hata tulipokwenda mahali ambapo inasemekana anaishi sasa hatukumpata,” alisema. 

Kamanda Siro alisema hafahamu ni kwanini Mbowe haja- ripoti wakati yeye mwenyewe anapinga biashara ya dawa za kulevya, hivyo baada ya taarifa yake ya jana, anamuomba ajitahidi aende waonane, tofauti na hapo ni lazima atakamatwa na kuhojiwa kwa kuwa ndiyo wajibu wa jeshi hilo.

 Hata hivyo, Februari 10 akiwa mjini Dodoma, Mbowe alise- ma hatafika polisi kwa kuitwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda lakini yupo tayari kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola endapo utaratibu wa kisheria utafuatwa. 

Wengine kortini 
Katika hatua nyingine, Kamishna Siro alisema operesheni ya dawa za kulevya inaendelea vizuri na kesho watuhumiwa Agnes Gerald ‘Masogange’, Rashid Said ‘Chid Mapenzi’ na Walid Nasher watapelekwa mahakamani. 

Hata hivyo, Kamanda Siro alitoa kauli mbili zinazokinzana, mwanzo alisema watuhumiwa hao watashtakiwa kwa kutumia dawa za kulevya, lakini baadaye akasema walipatikana na dawa hizo. 

Alisema operesheni inayoendelea tangu Februari 16 imewezesha kukamatwa watuhumiwa 73 wa makosa mbalimbali, yakiwamo ya wizi wa kutumia nguvu. 

Pia, ilikamatwa mitambo mitano ya kutengeneza pombe haramu aina ya gongo na puli 250 za bangi. Kamishna Siro alisema juzi walimkamata mtuhumiwa anayejifanya askari magereza akiwa na sare za jeshi hilo.

Alisema mtuhumiwa huyo, Elias Msingwa aliwahi kuwa askari wa jeshi hilo kabla ya kuachishwa kazi Desemba mwaka jana, akiwa na cheo cha Koplo lakini amekamatwa akiwa na sare zikiwa na cheo cha Sajenti. 

Akizungumzia tukio hilo katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, akiwa na pingu mkononi, Msingwa alisema alikuwa askari katika Gereza la Keko jijini Dar es Salaam na alifanya kitendo hicho baada ya kukosa nauli ya daladala. 

“Ninakaa Kivule jana (juzi) nilikuwa sina nauli ya kuja mjini ndiyo maana nikavaa sare hizi ili niweze kusafiri bure, ninaomba radhi kwa Watanzania na kuwashauri wenzangu wasije wakafanya hivi na baada ya hapa nitazirudisha sare hizi,” alisema Msingwa. 

Kamishna Siro alisema sare hizo zilivaliwa kinyume na sheria, huku zikitumika kuwababaisha wananchi hivyo upelelezi unaendelea utakapokamilika jalada lake litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.

Mwanamke Aishia Mikononi mwa Polisi Baada Ya Kukutwa Akifukua Maiti ya Mwanaye........Aliamini Atafufuka Baada ya Siku 3

$
0
0
Mwanamke aliyekuwa akiamini kuwa mtoto wake angefufuka siku ya tatu baada ya kufariki dunia Februari 15, jana alizua kizaazaa baada ya kufukua kaburi na kutoa maiti hiyo, hali iliyosababisha wananchi wafanye vurugu na kuichoma nyumba yake. 

Mtoto huyo, Baraka Mwafongo (22), aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu, alizikwa siku iliyofuata lakini maiti yake ilifukuliwa usiku wa kuamkia jana na kuwekwa katika pagala ikiwa imevishwa suti kumsubiri mchungaji aifufue. 

Mwanamke huyo, Ruth Segeleti (52), anayeishi Mtaa wa Shigamba, Mbalizi, hakutaka kuzika maiti ya mwanawe akieleza kuwa mtoto wake angefufuka baada ya siku tatu, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari. 

Alisema polisi waliona kuwa huenda hana uwezo ndipo walipomsaidia kuzika, lakini usiku wa kuamkia jana alipata vijana wawili waliomsaidia kufukua kaburi na kuchukua maiti hiyo ambayo waliipeleka kwenye pagala na kuiweka ikiwa imevishwa suti. 

Baada ya wakazi kubaini kaburi la mtoto huyo limefukuliwa, kundi la watu lilijitokeza makaburini na kusababisha polisi kufyatua mabonu ya machozi 

Wananchi waligundua kuwa kaburi lilikuwa wazi majira ya saa 3:00 asubuhi baada ya majirani kumuona mwanamke ambaye walijua alikuwa na msiba wa mtoto wake Jumamosi akiwa na jembe mkononi na furushi la nguo akitokea makaburini. 

“Nilipomsemesha, hakutaka kunijibu,” alisema mkazi wa mtaa huo, Mariam Mwakisepile ambaye ni jirani wa mwanamke huyo. 

“Nililazimika kuwaarifu majirani wengine ambao walikwenda makaburini ambako walikuta kaburi la Baraka likiwa limefukuliwa.”

 Shuhuda mwingine wa tukio hilo, Christina Nyopelo alisema walipiga simu kituo cha polisi cha Mbalizi na kuwaarifu.

“Baada ya muda mfupi polisi waliwasili na wakiwa makaburini waliona sanduku ndani ya kaburi, lakini mwili haukuwapo,” alisema Nyopelo.

 “Polisi kwa kushirikiana na wananchi waliamua kukagua maeneo ya makaburi na hatimaye walifanikiwa kuukuta mwili ukiwa umelazwa kwenye banda lililopo karibu na eneo hilo.” 

Habari hizo zilisambaa na kukusanya kundi la watu kutoka mji wa Mbalizi na kusababisha polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya. 

Alisema baadaye polisi walikwenda nyumbani kwa mwanamke huyo na kumkamata, pia waliupeleka mwili wa Baraka, Hospitali Teule ya Ifisi kwa ajili ya kuuhifadhi.

Kamanda Kidavashari alisema mtuhumiwa alipelekwa Kituo cha Polisi Mbalizi kuhojiwa. 

Umati wa watu pia ulijazana Mtaa wa Shigamba na kusababisha polisi walipue mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu. 

Jitihada hizo zilizaa matunda kwa muda mfupi, lakini ilipofika saa 8:00 mchana watu wasiofahamika waliichoma moto nyumba ya mwanamke huyo. 

Katika kukabiliana na tukio hilo, polisi waliwatawanya wananchi kwa kupiga baadhi ya watu waliokutwa eneo la tukio. Kamanda Kidavashari alisema polisi wanawasaka watu waliohusika kuchoma moto nyumba ya mwanamke huyo.

Maneno ya Profesa J baada ya kwenda gereza la Ukonga alipofungwa Mbunge Lijualikali

$
0
0
January 11 2017 Mbunge wa Jimbo la Kilombero Morogoro kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo ‘CHADEMA’ Peter Lijualikali alihukumiwa na Mahakama ya wilaya kifungo cha miezi sita jela bila kulipa faini kwa kosa la kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

Leo February 19 2017 Mbunge wa Mikumi Joseph Haule maarufu Profesa J amekwenda kumtembelea gerezani Ukonga Dar es salaam na baada ya kutoka hapo akaandika yafuatayo.

‘Nimetoka gereza la Ukonga kumwona Mh. Lijualikali na Patron wa mkoa wa Morogoro kamanda Zinga na wapiga kura wangu watatu kutoka kata ya TINDIGA walifungwa miaka 30, wana afya njema na wanawasalimia sana ila wanalalamika tu hali sio nzuri kabisa kule ndani.. Mungu AWASAIDIE 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 20

Kiwanda Cha Minjingu Chamchefua Waziri Mkuu......Akitaka Kimuombe Radhi Rais Magufuli

$
0
0
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema haridhiki na hali aliyoikuta kwenye Kiwanda cha kutengeneza mbolea cha Minjingu, baada ya kubaini kuwa wanatumia mifuko yenye nembo ya Kenya wakati mbolea hiyo inazalishwa hapa nchini.

Kutokana na hilo, Waziri Mkuu amewataka wamiliki wa kiwanda hicho waandike barua kwa Rais Dk. John Magufuli kabla hajamaliza ziara yake Jumatano, awe amepata nakala ya barua hiyo.

Agizo hilo alilitoa jana baada ya kutembelea kiwanda hicho kilichopo Wilaya ya Babati akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake mkoani Manyara. Waziri Mkuu alirejea Babati akitokea Dar es Salaam ambako alikuwa na ratiba za kitaifa.

“Nilikuja kukagua kiwanda baada ya kupokea malalamiko kuwa mbolea hii haikubaliki huko vijijini. Watafiti wameonyesha kuwa ikitumika inasaidia kutoa mazao mengi. Lakini wakati niko kiwandani nimekerwa kukuta mifuko ya kupakia mbolea hii ina anuani ya Nairobi, Kenya wakati mali ghafi inatoka Tanzania.

 “Ni kwa nini mifuko hii ina anuani ya Kenya? Hapa tulipaswa tuone anuani ya Babati! Je mlipata kibali kutoka serikalini? Tena kuna lebo ya TBS. Kwa nini Tanzania haionekani? kwani malighafi iko Kenya? haiwezekani, ni lazima uandike barua na uombe radhi kwa Mheshimiwa Rais Magufuli. Yeye anahimiza ujenzi wa viwanda ndani ya nchi, halafu ninyi mnafanya hivyo?,” alihoji.

Akiwa ndani ya kiwanda hicho, Waziri Mkuu alikuta baadhi ya mifuko ya mbolea ikiwa imeandikwa: ‘County Government of Bungoma’, ina nembo ya Serikali ya Kenya na anuani ikionesha kuwa mbolea hiyo imetengenezwa na kiwanda cha mbolea cha Minjingu lakini anuani inasomeka P. O Box 2941 – 00200 Nairobi, Kenbro Industrial Park, Mombasa Road; namba ya simu +254-20-6000-970 lakini mifuko hiyo pia ina muhuri wa TBS.

Baadhi ya mifuko ilikuwa ikipakiwa ndani ya lori tayari kwa kusafirishwa kwenda kwa wateja.

Alisema atamwagiza Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage kwenda kiwandani hapo na wanasheria wake pamoja na wataalamu kutoka Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) ili waangalie hatua gani zinapaswa kuchukuliwa.

“Kwa staili hii hii tumeona watu wakinunua kahawa yetu na kwenda kuipakia upya huku wakiweka lebo za kwao. Leo hii hata Tanzanite pia inasemwa imetengenzwa India. Hatuwezi kukubali hali hii iendelee,” alisema

“Tukiruhusu hali hii, watu watajuaje kuwa mbolea hii ambayo ni first class duniani kuwa inapatikana Tanzania? Kiwanda chetu, ardhi yetu, suala la kutangaza nchi yetu kwa kutumia bidhaa zetu litafanikiwa kwa njia hii kweli?,” alisema na kuhoji

Akitoa maelezo kuhusu hali hiyo, Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Tosky Hans alimweleza Waziri Mkuu kwamba wametumia lebo hiyo kutokana na makubaliano na wanunuzi jibu ambalo Waziri Mkuu hakulikubali na kusisitiza kuwa anapaswa aombe radhi.

Wawili wapoteza maisha Jijini Mwanza kwa kukosa dawa za kulevya

$
0
0
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga amesema watu wawili wameripotiwa kupoteza maisha mkoani Mwanza kwa sababu ya kukosa dawa za kulevya mtaani kama walivyozoea.

Kamishna Sianga amesema taarifa hiyo ameipata kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, hali inayomaanisha mafanikio ya mapambano ya dawa hizo, ambapo kwa sasa usambaaji wake umepungua mtaani kwa kiasi kikubwa.

"Nimeongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ameniambia kwamba kuna watu wwili wamefariki sababu walikuwa drug addict na sasa dawa hizo hazipo mtaani" Amesema Sianga

Sianga amesema mara baada ya kupokea kijiti cha mapambano kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, Mamlaka hiyo imeendelea na moto huo huo, na kwamba kwa hivi sasa timu yake hailali, ikiendelea na mapambano kila siku na kwamba hata jana, kuna mtuhumiwa mkubwa wa dawa za kulevya amekamatwa.

"Leo (jana) asubuhi tumemkamata mtuhumiwa mmoja mkubwa wa dawa kulevya, tupo naye tunaendelea kumuhoji, mengi yataibuka" alisema Kamishna Sianga

Kuhusu kuendelea kutumia mbinu iliyokuwa ikitumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam paul Makonda ya kutaja majina hadharani,, Kamishna Sianga alisema hatatumia njia hiyo kwa kuwa kutaja majina ya watu hadharani kunaweza kuiingiza serikali katika matatizo maana kuna watu wengine wanaweza kutoa majina ya watu kwa sababu ya chuki binafsi.

Amesema njia anayoitumia ni kuwakamata na kuwahoji kimyakimnya na wakishajiridhisha hatua nyingine za kisheria zinafuata.

Katika hatua nyingine, Sianga amesema Tanzania iko makini katika kuwashughulikia wahusika wakubwa wa dawa za kulevya duaniani tangu miaka mingi iliyopita, akitolea mfano mtuhumiwa mmoja wa kike ambaye ni gwiji katika biashara hiyo au 'King Pin', ambaye hivi sasa amefungwa katika magereza ya Tanzania tangu mwaka 2010

"Tulimkamata mmoja kati ya watu waliokuwa wametajwa kama king pin wa dawa hizo nchini Marekani, alikuwa ameshindikana, na huko Marekani alikuwa na kesi zaidi ya 40, lakini alikamatwa hapa na amefungwa tangu mwaka 2010, yuko gerezani nafikiri kama siyo Keko, ni Segerea". Amesema Sianga.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images