Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

LIVE: Mkutano wa RC Paul Makonda Katika Awamu ya Tatu ya Madawa ya Kulevya

0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda muda huu yupo katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere ambapo atatangaza list mpya ya majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya.

Hii itakuwa list ya tatu ya mkuu huyo baada ya mbili kupita.

Katika list zilizopita vigogo mbalimbali walitajwa kama Yusuph Manji, Iddi Azzan, askofu Gwajina na wengine.

Pia mkutano wa leo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja viongozi wa usalama. 

==>Angalia tukio zima hapo chini

Rais Magufuli Akutana Na Kufanya Mazungumzo Na Wageni Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam

0
0
Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa ya kujenga uchumi wa Tanzania na amewaomba wananchi wa Tanzania na Afrika Mashariki kuunga mkono mfano mzuri unaooneshwa na kiongozi huyo.

Mhe. Daniel Kidega amesema hayo leo tarehe 13 Februari, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya kukutana na Mhe. Rais Magufuli na kufanya nae mazungumzo yaliyojikita kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya nchi wanachama, kuinua hali ya uchumi na kutatua matatizo yanayozikabili baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya.

“Nikueleze kitu kimoja, Tanzania na Afrika Mashariki tumebahatika sana kupata kiongozi kama Rais Magufuli ambaye anatuongoza vizuri, analeta maendeleo na mabadiliko, naomba watu wote wa Tanzania na Afrika Mashariki wamuunge mkono, kwamba kiongozi kama yeye ndiye tunayemtaka, tuangalie viongozi wanaoleta maendeleo na mabadiliko kwa watu wetu ili tuwe vizuri” amesisitiza Mhe. Daniel Kidega.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Cooke ambapo viongozi hao wamezungumzia namna Tanzania na Uingereza zitakavyoimarisha uhusiano na ushirikiano katika uwekezaji na biashara, mapambano dhidi ya Rushwa na dawa za kulevya, kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kuimarisha huduma za usafiri wa anga.

Kwa upande wake Mhe. Dkt. Magufuli amemshukuru Mhe. Sarah Cooke na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wake wa kihistoria na Uingereza katika kujenga uchumi imara wa Tanzania, kupambana na rushwa na dawa za kulevya na amemshukuru Uingereza kuongeza fedha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayosaidia maendeleo hapa nchini.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi Mpya wa Shirika la Fedha Duniani (IMF) Bw. Bhaswar Mukhopadhyay ambapo viongozi hao wamezungumzia juu ya shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofanywa kwa ushirikiano wa Tanzania na IMF.

Bw. Bhaswar Mukhopadhyay amempongeza Rais Magufuli kwa hatua kubwa na muhimu anazochukua kuimarisha uchumi, zilizowezesha kiwango kizuri cha ukuaji wa uchumi na kudhibiti mfumuko wa bei za bidhaa.

Halikadhalika Mhe. Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Balozi Liberat Mfumukeko.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

13 Februari, 2017

Waziri Mkuu Majaliwa Akutana Na Maofisa Wa Magereza

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamishna Mkuu wa Magereza, Dk. Juma Malewa asimamie zoezi la upimaji wa maeneo yanayomilikiwa na Magereza kote nchini na kuhakikisha yanawekewa mipaka.

Ametoa agizo hilo leo mchana (Jumatatu, Februari 13, 2017) katika kikao baina ya Kamishna huyo mpya na Maafisa Magereza wa Mikoa yote na maafisa wanaoshughulikia kilimo na viwanda alichokiitisha ofisini kwake mjini Dodoma.

“Magereza yetu mengi yako kwenye maeneo ambayo hayajapimwa. Baadhi ya maeneo kuna migogoro kwa sababu wananchi wamejenga karibu kabisa na maeneo ya Magereza. Lazima tupime maeneo yote na kuyawekea alama mipakani ili kubainisha maeneo yetu,” amesisitiza.

Mbali ya maeneo ya Magereza, Waziri Mkuu amesema, jeshi hilo lina mashamba makubwa ambayo pia hayajapimwa hali ambayo amesema imechangia baadhi ya wananchi kulima ndani ya maeneo ya jeshi hilo.

“Natambua kuwa jeshi hili lina mashamba makubwa lakini nayo pia hayajapimwa. Kila RPO ni mjumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wake, tumieni wapima ardhi kutoka kwenye Halmashauri zenu na mhakikishe kuwa maeneo hayo yanapatiwa hati,” amesema.

Makonda aagiza mume wa muigizaji Shamsa Ford ( Chidi Mapenzi ) akamatwe

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ameagiza kukamatwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Chidi Mapenzi ambaye ni mume wa msanii maarufu wa filamu nchini Shamsa Ford kwa ajili ya mahojiano kuhusu dawa za kulevya.

Makonda ametaja jina la Chidi Mapenzi leo wakati akihitimisha mkutano wa uzinduzi wa awamu ya tatu ya vita dhidi ya dawa za kulevya katika mkoa wa Dar es Salaam, ambayo imeambatana na kukabidhi orodha mpya ya majina ya watuhumiwa wengine 97 kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Dkt. Rogers William Sianga.

Mara baada ya kupokea majina hayo, Kamishna Sianga amesema kuwa atayashughulikia na atahakikisha kila mtu anakamatwa na kushughulikiwa bila kumuonea mtu kwa mujibu wa sheria iliyounda mamlaka hiyo.

Jina lingine lililotajwa leo ni Mfaume Kiboko, ambapo Kamishna Sianga ameagiza pia akamatwe na apelekwe kwake haraka iwezekanavyo.

Katika hotuba yake, Mh. Makonda pamoja na kuweka wazi kuwa moto wa vita hiyo ndiyo unaanza kuwaka sasa, amewaonya watu wote ambao wanakaidi amri yake ya kuripoti polisi na kuwatangazia vita zaidi, huku akisema yeye kama mkuu wa mkoa ana mamlaka yote ya kumuita mtu yeyote na ikiwezekana kumfukuza kwenye mkoa wake.

"Ukiitwa polisi nenda, hizi mbwembwe nyingine achana nazo, hizo mbwembwe siyo kwenye utawala huu wa Magufuli, na siyo kwenye utawala na Makonda, Mwingine anasimama kabisa na kifua chake eti hawezi kwenda kwa sababu eti Makonda ni kijana mdogo, sasa kama Makonda ni mdogo hawezi kukuita wewe, atapajua shimoni ni wapi, Pia nina mamlaka ya kukufukuza kwenye mkoa wangu endapo nitajiridhisha kuwa wewe ni hatari kwenye mkoa wangu" Amesema Makonda 

Makonda amesema atatumia sheria mpya ya mwaka 2015 kuwashughulikia wote wanaohusika bila kujali ni nani, na kufafanua kuwa sheria hiyo inaelekeza pia adhabu kwa watumiaji na kuwataka watu wanaokosoa uamuzi wake wa kutaja majina waungane naye, kwa kuwa wao ndiyo waliotaka majina hayo awali

"Sheria mpya ya mwaka 2015 inasema mtumiaji wa dawa za kulevya atafungwa jela miaka mitatu, kuna wengine hakuna sheria ya kumuadhibu mtumiaji, hawahui sheria........Kuna wengine wakati ule wa Kikwete, aliposema ana majina walitaka ayataje, sasa leo Makonda anataja wanaanza kelele, nale ninayo majina mengine 97, na haya ndiyo yana watu wazito zaidi, na yataleta mtikisiko zaidi"

Pia ametaja baadhi ya mbinu mpya ambazo hutumiwa na wasambazaji wa dawa za kulevya kuwa ni pamoja na kutumia mitungi ya gesi, pamoja na kuwatumia wauza vitumbua mitaani.

Kwa upande wake Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Simon Sirro, amesema tangu Februari 01 hadi 12 mwaka huu, jumla ya watuhumiwa 311 wamekamatwa na kuhojiwa wakiwemo 77 waliotajwa na Makonda.

Amesema kati ya hao 311, watuhumiwa 117 walikutwa na vielelezo.

TID Awaomba Radhi Watanzania Kwa Utumiaji Wa Dawa Za Kulevya

0
0
Msanii TID amefunguka na kuwaomba radhi Watanzania kutokana na tabia yake ya kutumia dawa za kulevya kwani anaamini kuwa akiendelea kutumia dawa hizo hatakuwa mfano bora hata kwa mtoto wake.

TID anasema anaamini kutokana na matumizi ya dawa hizo huenda akawa amewakwaza watu au kufanya mambo ambayo si mema katika jamii hivyo anaomba kusamehewa kwani alikuwa akifanya kwa nguvu ya dawa za kulevya na si yeye.

"Nimekuwa muathirika na matumizi ya dawa za kulevya, leo sipo hapa kusema kwanini nimeingia huku, nimekuja hapa kama kijana niliyepotea njia. Kutoka moyoni, nimekuja kukiri kuwa nimeikosea sana familia yangu, mama yangu, ndugu jamaa na marafiki hivyo nimekuja kuwaomba msamaha wote niliowakwaza under influence ya dawa za kulevya" alisema TID

Mbali na hilo TID anasema ameamua kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaan Mhe. Paul Makonda katika vita dhidi ya madawa ya kulevya na kusema hata kama watu wanaweza kumuona mnafiki si mbaya maana yeye, ameamua kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya.

"Nimesimama hapa kama kijana shupavu, mpambanaji, mnyama. Vita hii inabidi uwe mnyama kama Paul Makonda ili uweze kushinda, hakuna anayejua nimepitia mangapi mpaka nimefika hapa, natangaza rasmi kujiunga kwenye vita hii" alisema TID

Wema Sepetu afunguka kwa mara ya kwanza tangu atoke mahabusu

0
0
Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu leo amefunguka na kuwashukuru mashabiki wake kwa kumpa faraja na kumuombea katika kipindi chote ambacho alikuwa matatizoni

"Mimi na familia yangu tunapenda kuchukua fursa hii kutoa shukrani zetu za dhati kwa wote mlioshirikiana nasi kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu tulichopitia. Najua wengi mlikua mnaniombea, nashukuru kwa sala na dua zenu kwani zimenisaidia kwa kunipa nguvu wakati nikiwa kwenye wakati mgumu sana kwenye maisha yangu". Aliandika Wema Sepetu

Wema aliendelea kutoa shukrani zake kwa wasanii pomoja na mwanasheria wake ambao walikuwa naye katika kipindi hicho kigumu katika maisha yake.

"Napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote duniani kwa kuniamini na kusimama na mimi kwa kipindi chote hiki, pia napenda kuwashukuru wasanii wenzangu wote. Asante sana kwa mwanasheria wangu Alberto Msando kwa kunisimamia na kuwa na mimi bega kwa bega wakati huu mgumu. Nakuombea kwa Mungu akupe moyo huohuo wa kuwatetea wanyonge". Aliandika Wema Sepetu

Orodha Ya Mahakimu Na Majaji Waliovuruga Kesi Za Madawa ya Kulevya Kupelekwa Kwa Jaji Mkuu

0
0
Vita dhidi ya Dawa za Kulevya sasa imeshika kasi, mara baada ya Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Dkt. Rogers William Sianga kutangaza kuanza na majaji na mahakimu waliovurunda kwenye kesi zinazohusu dawa za kulevya

Sianga aliyeapishwa jana na Rais Magufuli, ametoa tamko hilo leo wakati kupokea kijiti kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Poul Makonda ikiwa ni pamoja na kukabishiwa majina ya watu 97 ya wafanyabiashara wakubwa, wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.

Kamishna Sianga amesema kuna mahakimu na majaji ambao wamekuwa wakivuruga kesi za watuhumiwa wa dawa za kulevya ambapo pia amesema watapitia kesi zote za madawa ya kulevya ili kuwabaini na kisha watapeleka orodha kamili katika mamlaka husika ili hatua zichukuliwe.

Akitolea mfano wa kesi ambazo amedaia zilivurugwa na mahakimu, amesema kuna kesi moja ambapo ushahidi ulikuwa wazi kuwa mtuhumiwa amemeza dawa za kulevya, lakini hakimu akasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na matatizo ya vidonda vya tumbo.

Pia Sianga ameagiza kukamatwa kwa maafisa wa polisi waliosaidia kuingiza viwatilifu vya kutengeneza dawa za kulevya nchini kiasi cha takriban tani 21.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Poul Makonda amesema katika mkoa huo kuna bandari bubu 54 huku 27 zikiwa zinatumika kupitishia dawa za kulevya.

Pia amesema kuna takriban nyumba 200, hoteli 67, Club 20 na vijiwe 107 vinavyotumika kusambaza na kuuza dawa za kulevya huku akibainish kuwa kwa utafiti alioufanya, kila siku katika jiji hilo, kati ya kilo 10 hadi 15  husambazwa na kumalizika kila siku.

Mkutano huo wa mapambano ya dawa za kulevya uliofanyika kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam ulihudhuriwa pia na viongozi wa kidini, wanasiasa, wabunge, madiwani, wakuu wa idara mbalimbali katika halmashauri za mkoa wa Dar es Salaam, wadau mbalimbali wa mapambano ya dawa za kulevya pamoja na waathirika wadawa za kulevya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya February 14


Mama Akataa dhamana ili akae rumande na hausigeli wake

0
0
Mkazi wa Sitakishari Dar es Salaam, Christina Thomas (28), amekataa kudhaminiwa ili arudi rumande na msichana wake wa kazi ambaye alishindwa masharti ya dhamana.

Christina jana alifikishwa Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa tuhuma za kumpiga mtoto wake wa miaka miwili na kumsababishia majeraha makubwa, kuzimia na kushindwa kumpeleka hospitalini.

Mwendesha Mashitaka Hilda Kato, alidai mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Ritha Tarimo kwamba mshitakiwa siku isiyofahamika Januari, alimpiga kwa fimbo mtoto huyo na kumsababishia majeraha.

Kato alidai katika mashitaka ya pili, mshitakiwa huyo ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo na msichana wake wa kazi, Blanka Benjamin kwa uzembe walimwacha mtoto huyo bila kumpeleka hospitali huku akiwa na hali mbaya ambayo ilisababishwa na mama mzazi.

Baada ya kusomewa mashitaka, mama huyo alijibu kuwa hakumbuki, huku mshitakiwa wa pili ambaye ni msichana wa kazi akikana mashitaka yake.

Mwendesha Mashitaka alimwambia Hakimu Tarimo kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika, lakini dhamana yao iko wazi kama watakidhi masharti. 

Hakimu alitoa masharti ya dhamana kwa washitakiwa kuwa na wadhamini wawili wa kuaminika mmoja akiwa mtumishi kwenye taasisi inayofahamika na kusaini dhamana ya Sh 800,000 kila mmoja.

Baada ya kusomewa masharti hayo ya dhamana mshitakiwa namba moja alikidhi masharti ya dhamana huku wa pili akishindwa kutokana na wadhamini kuchelewa.

Hata hivyo, mshtakiwa huyo wa kwanza ambaye ni mama wa mtoto alisema hawezi kuwa nje kwa dhamana akimwacha mshitakiwa wa pili rumande hivyo kumwomba hakimu warudi wote ndani hadi kesho watakapotimiza masharti ya dhamana pamoja.

Hakimu alimwambia mshitakiwa huyo kwamba kwa sababu yeye ana mtoto mdogo hivyo angeweza kutoka na kumwacha mshitakiwa wa pili na kesho (leo) angepata dhamana, lakini akasema mtoto wake ataondoka na baba yake, na yeye atarudi rumande hadi watakapopata dhamana wote wawili.

Makonda amkumbusha Spika kuwapima wabunge kilevi

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amemkumbusha Spika wa Bunge. Job Ndugai, kuhusu kusudio lake la kuanza kuwapima wabunge kubaini kama wametumia kilevi kabla hawajaiingia kwenye ukumbi wa chombo hicho cha kutunga sheria.

Siku chache baada ya Rais Magufuli kutengua uteuzi wa Charles Kitwanga, kwenye baraza lake la mawaziri kutokana na kuingia bungeni akiwa amelewa, Ndugai alisema kuwa kuna wabunge kadhaa huingia bungeni wakiwa wametumia vilevi vikali zaidi vikiwemo bangi, viroba na unga’

Aidha kutokana ba hatua hiyo, Spika huyo alisema wanafikiria kuweka vifaa maalumu vya kupima ulevi kwa watunga sheria hao na kutafuta wataalamu wa kutoa ushauri nasaha wa kisaikolojia, utaratibu huo haujaanza kutolewa bungeni licha ya kwamba ni miezi tisa ipite,

Jana katika hafla maalum ya kukabidhi orodha mpya ya watuhumiwa wa biashara haramu ya madawa ya kulevya Kumkaribisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kupambana na Kuzui Dwa za Kulevya, Rogers Siang’a, Makonda alimkumbusha Spika Ndugai kusudio lake la kuanzisha utaratibu wa kuwapima wabunge ulevi.

“Na utaratibu huu wa kuwapima wabunge wetu utakuwa mzuri sana, na ninakumbuka kuna kipindi Spika aliwahi kutangaza kuanzisha lakini sijui ukaishia wapi, nitoe tena rai kwake afikirie tena kuanzisha utaratibu huu ili tuweze kuwabaini wabunge kama wanatumia kilevi ama la,”alisema Makonda.

Ulinzi waimarishwa Taasisi ya Moyo Muhimbili Ambako Yusuf Manji amelazwa

0
0
Hali ya ulinzi imeimarishwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) alikolazwa mfanyabiashara Yusuf Manji baada ya kuugua ghafla akiwa polisi alikokuwa akihojiwa.

Manji aliyekuwa akihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi jijini hapa alipelekwa hospitalini hapo juzi jioni akiwa ndani ya gari la wagonjwa aina ya Toyota Land Cruiser lenye nembo ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) huku gari lake aina ya Range Rover likifuata kwa nyuma.

Askari wenye sare na wengine wakiwa na mavazi ya kiraia nje ya wodi aliyolazwa mwenyekiti huyo wa klabu maarufu nchini ya Yanga walionekana wakiimarisha ulinzi.

Ilipofika saa 4:13 asubuhi mfanyabiashara huyo alitoka kwenye chumba hicho na kuongozwa kuelekea upande mwingine wa jengo hilo.

Akiwa amevalia nguo za wagonjwa zenye rangi ya kijani, Manji alitembea taratibu kuelekea upande aliokuwa akielekezwa.

Alipoulizwa kuhusu uwapo wa Manji hospitalini hapo, Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Profesa Mohamed Janabi alisema hawezi kuzungumzia taarifa za mgonjwa.

Februari 8, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alitoa orodha ya watu 65, akiwamo Manji ambao aliwataka wafike Polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu masuala ya dawa za kulevya.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya February 15

Hakimu, Karani Kortini Kwa Tuhuma Za Rushwa

0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)  mkoani Mara imewapandisha kizimbani Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo mjini Musoma, Swalala Mathayo (40) na karani wa Mahakama hiyo, Charles Masatu (56) kwa tuhuma za kudai na kupokea rushwa.

Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Musoma, Richard Maganga, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Marshal Mseja, alidai  watuhumiwa hao kwa pamoja wanadaiwa  kuomba na kupokea rushwa ya Sh 200,000.

Alidai   Hakimu Mathayo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kuomba na kupokea rushwa,wakati karani Masatu anatuhumiwa kushiriki katika kuiomba rushwa hiyo.

Mseja  alidai chanzo cha madai hayo ya rushwa ni kuwa hakimu huyo alitoa hukumu ya kifungo cha miaka miwili  kwa Magdalena Aloyce (29) mkazi wa mtaa wa Makongora mjini Musoma.

Alidai kwa vile mtuhumiwa alifungwa   akiwa na mtoto mdogo   wa miezi 10 na kuwaacha  wengine wawli bila  uangalizi, ndugu zake walimfuata mkuu wa gereza na kuomba mfungwa huyo apewa kifungo cha nje   aweze kuhudumia familia yake ambayo inamtegemea.

Ndugu walipewa maelekezo  na mkuu wa magereza kwenda kwa ofisa wa ustawi wa jamii na walipofika walihudumiwa na kujaziwa fomu namba 12 kwa mujibu wa Sheria ya Kutumikia Jamii,  alisema.

Alisema  fomu hiyo ilitakiwa kuidhinishwa na hakimu aliyetoa hukumu hiyo.

Mseja alidai hakimu huyo hakuweza kufanya hivyo bali alitengeneza mianya ya kudai rushwa kwa kumuhusisha karani wake na hapo ndipo ndugu hao walipotoa taarifa Takukuru na kuwekwa mtego na hatimaye kukamatwa na rushwa hiyo ya Sh 200,000.

Watuhumiwa hao  walikana  mashitaka na wapo nje kwa dhamana hadi   Machi 21 mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

Majanga Yaendelea Kumwandama Yusuf Manji.......Iadara ya Uhamiaji Yasema Itamfungulia Mashitaka Kwa Kuajiri Wafanyakazi Wageni

0
0
Idara  ya Uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam imesema inakusudia kumfungulia mashtaka mfanyabiashara maarufu Yusufu Manji kwa kosa la kuajiri wafanyakazi wageni 25 wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini kupitia Kampuni ya Quality Group.

Wakati Uhamiaji wakisema hivyo, Julai 15 mwaka jana Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Yusuph Manji alitoa taarifa kwa umma kupitia vyombo vya habari , akieleza kuwa amestaafu rasmi nafasi hiyo.

Katika taarifa hiyo Manji alisema baada ya kustaafu atabakia kuwa mshauri huku akitaja  sababu za kufanya hivyo kuwa ni utaratibu uliokuwa umewekwa na waasisi wa kampuni hiyo wa kuwa na ukomo wa uongozi usiozidi miaka 20.

Katika taarifa hiyo alieleza kuwa ameshatumikia nafasi hiyo kwa miaka mingi na ni muhimu kutoa fursa kwa kiongozi mwingine ili aweze kujishughulisha na shughuli nyingine ikiwamo kufundisha katika vyuo vikuu ujasiriamali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kamishna wa Idara hiyo, John Msumule alisema kazi hiyo itafanyika baada ya mfanyabiashara huyo kutoka hospitali alikolazwa akiendelea na matibabu ambapo ataunganishwa  na kesi hiyo na lazima afikishwe mahakamani.

“Jumla ya wafanyakazi walikuwa 128, kati yao wawili walikimbia nchi na kubaki 126 na baada ya ukaguzi tuliwabaini wengine 25 wakiwa hawana vibali vya kufanya kazi nchini.

“Taratibu zetu ni kuwafungulia mashtaka waliokamatwa lakini pia tutamfikisha mahakamani muajiri wao kwa kufanya makosa hayo huku akijua ni kinyume na sheria,” alisema Musumule.

Alisema walianza kufanya ukaguzi katika kampuni hiyo  Ijumaa ya wiki iliyopita lakini hawakupewa ushirikiano ambapo walimkamata msaidizi wake.

“Siku ya Jumamosi walikuwa na passport hapa lakini wafanyakazi wawili walikimbia nchi na ndipo tulipogundua kuna 25 wanaofanya kazi katika kampuni hiyo bila kuwa na kibali,”alisema Musumule.

Mbali na hilo alisema wamefanikiwa kumkamata raia wa Uganda, Asha Talib ambaye alikuwa na makosa ya kuishi nchini bila kibali, kuhondhi hati za kusafiria 15 za raia wa Uganda na tatu za Madagaska.

Mtuhumiwa huyo alipokuwa akihojiwa mbele ya waandishi wa habari alidai kuwa alikuwa anafanyakazi katika kampuni inayoshughulika na maombi ya viza kwa njia ya mtandao ambapo bosi wake raia wa Tanzania alikimbia.

“Kazi tuliyokuwa tunafanya ni kuwapatia watu mbalimbali viza baada ya kufanya maombi kwa njia ya mtandao na kisha kuwatumia viza hizo za kusafiria huko waliko,” alisema Talib.

Aidha katika hatua nyingine Kamishna Musumule alisema kuwa kuna baadhi ya watumishi wa idara hiyo wasiokuwa  waminifu ambao wamekuwa wakishiriki katika kughushi hati mbalimbali za kusafiria.

“Wiki ijayo nendeni Makao Makuu ya Idara ya Uhamiaji ambapo tutawatangazia hatua ambazo tumezichukua juu ya watumishi hao ambao si waaminifu,”alisema Musumule.

Alisema katika operesheni hiyo,  walikamata vibali bandia nane vya raia wa China wa Kampuni ya Global Leader na ukaguzi uliofanyika katika jengo la Diamond Plaza walibaini Kampuni ya Luck Spin.

“Pia tumefanikiwa kumkamata mwajiri raia wa Tanzania kwa kumwajiri mgeni kutoka nchini Malawi katika kampuni ya ulizi kinyume cha sheria,” alisema Musumule.

Swali La Tundu Lissu Lazua Ubishi Mahakamani

0
0
Mbunge  wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, amemtaka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Salum Hamdani, kueleza anachofahamu juu ya Katiba ya Zanzibar na kama Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar , Salum Jecha ana mamlaka ya kufuta matokeo ya uchaguzi au laa.

Lissu alihoji hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati Hamdani alipokuwa akitoa ushahidi katika kesi ya uchochozi inayomkabili Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio.

Mshtakiwa Lissu aliomba kujiwakilisha mwenyewe mahakamani hivyo baada ya ushahidi alimuhoji maswali shahidi kulingana na ushahidi wake.

Swali hilo la Lissu lilimfanya Wakili wa Serikali, Paul Kadushi, kupinga akitaka shahidi asijibu kwa sababu si mtaalamu wa sheria wala Katiba.

Kadushi alidai shahidi hawezi kutoa tafsiri ya Katiba ya Zanzibar na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kusikiliza masuala ya kikatiba.

Akijibu pingamizi hilo, Lissu alidai halina msingi wowote kwa sababu suala la Serikali ya Zanzibar ni halali na  limeletwa na upande wa mashtaka wenyewe katika shtaka la pili na la tatu hivyo wakabiliane nalo.

Wakili Peter Kibatala alidai mahakamani hapo kuwa shahidi huyo anapaswa kueleza yeye mwenyewe kama hawezi kulijibu swali hilo na si vinginevyo na kwamba katika kuandika uamuzi wake mahakama ipende isipende ni lazima itajibu swali hilo.

Hakimu Simba baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili aliahidi kutoa uamuzi leo iwapo shahidi aeleze anachokifahamu kuhusu Katiba ya Zanzibar ama la.

Kabla ya kufikia katika malumbano hayo Lissu alitaka kujua yeye na washtakiwa wenzake walikula wapi kuchapisha huo uchochezi.

Alihoji wao watu wanne waliwasiliana kwa maandishi, email ama simu na saa ngapi, maswali hayo yalijibiwa na shahidi kwamba hafahamu.

Awali akihojiwa na Wakili Kibatala kuhusu wapi alipata taarifa za kuwapo kwa mikusanyiko ya watu katika sehemu za kuuzia magazeti , Hamdani alidai alizipata kwa RCO wa Kinondoni, Temeke na Ilala na kwa upande wa Zanzibar alipata kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Diwani Athumani.

Shahidi alidai katika Gazeti la Mawio la Januari 14 mpaka 20 kulikuwa na habari yenye kichwa cha habari Machafuko yaja Zanzibar na kwamba maneno hayo yangeweza kuleta chuki, uvunjifu wa amani, uchochezi na hofu.

Alidai baada ya kuona hivyo na kulinua gazeti hilo alifungua jalada la uchunguzi kisha aliteua wapelelezi ili kuona kama kuna kesi ya jinai na walipoona waliwafikisha washtakiwa mahakamani.

Mchekeshaji Eric Omondi Karudia kuiigiza sehemu ya movie ya Adam na Eva

0
0
Mchekeshaji wa Kenya Eric Omondi amekuwa na utundu wa  kuzirudia na kuziigiza movie na nyimbo za mastaa mbalimbali ambapo wakati huu ameirudia sehemu ya movie ya Adam na Eva wakiwa kwenye bustani ya Eden.

==>Itazame hapo chini

Vita dhidi ya dawa za kulevya: Masogange adaiwa kukamatwa na polisi

0
0
Taarifa zinadai kuwa mrembo Agnes ‘Masogange’ Gerald amekamatwa na polisi usiku wa kumkia leo, ikiwa ni sehemu ya msako wa watu wanaohusishwa na biashara ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa Jamii Forums, Masogange anashikiliwa kwenye kituo kikuu cha polisi jijini Dar es Salaam. 

Mrembo huyo anakuwa staa mpya kuingizwa kwenye orodha ya mastaa wengine waliohusiswa na sakata hilo.

 Kwenye mazungumzo yaliyovuja hivi karibuni na kusambaa mtandaoni, Wema Sepetu aliyekuwa ameshikiliwa pia kituoni hapo kwa sakata kama hilo, alisikika akimtaja Masogange kuwa mmoja wa mastaa wanaoshukiwa kujihusisha kwenye biashara hiyo.

Hiyo sio mara ya kwanza kwa Masogange kushikiliwa na polisi kwa tuhuma hizo. August 2014, Kikosi Kazi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya nchini kilimhoji kwa zaidi ya saa 10 mrembo huyo kuhusiana na tuhuma za kukamatwa na dawa aina ya crystal methamphetamine huko Afrika Kusini, Julai mwaka 2014.

Masogange alitawala vyombo mbalimbali vya habari nchini mwaka 2014 baada ya kukamatwa Afrika Kusini akiwa na nduguye Melisa Edward wakiwa na ‘mzigo’ wa dawa hizo zenye thamani zaidi ya Sh6.8 bilioni. 

Wasichana hao walinaswa baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo, Afrika Kusini wakitokea Tanzania.

Katika mahojiano hayo, Masogange alidai kuwa alipewa dawa hizo na mtu ambaye hamfahamu kwa jina lakini anaikumbuka sura yake.

Naibu Waziri wa Afya kuweka hadharani majina ya mashoga Dar es Salaam

0
0
Naibu Waziri Wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa atawaweka hadharani wanaume wote wanaojihusisha na mapenzi ya jinsi moja (mashoga) ambao hufanya biashara hiyo kupitia mitandao ya kijamii.
 
Naibu Waziri aliyasema hao jana usiku kupitia ukurasa wake wa Twitter ambapo alieleza kuwa yupo katika ziara jimboni kwake na mara atakaporejea jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamia Dodoma rasmi ataiweka orodha hiyo hadharani.
 
Aidha, amesema kuwa wale wote wanaodhani kuwa vita dhidi ya wanaume wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja ni mzaha, wataona hali itakavyokuwa kwani vita hiyo ni kubwa sana na wataishinda.
 
Kigwangalla ambaye pia ni mtaalamu wa afya alisema kuwa suala la mtu kuwa shoga si suala la kibaolojia (asili) bali ni watu tu kujiendekeza na hivyo watakahikikisha wanalikomesha.
 
Sheria ya ndoa ya Tanzania inapinga watu wa jinsia moja kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi, lakini pia ni kitu kilichozuiliwa katika vitabu vitakatifu vya dini.


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 16

Wafanyakazi 25 wa Maji Kujieleza Leo

0
0
Wafanyakazi 25 wa Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na  mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuf Manji, wanaodaiwa kutokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini, leo wataanza kujieleza kwa maandishi katika ofisi za uhamiaji.

Ofisa uhamiaji wa mkoa, John Msumule  amesema uhamiaji haijawakamata wafanyakazi hao, isipokuwa inashikilia hati zao za kusafiria.

“Kesho (leo) tunatarajia kuanza kuwahoji ili watoe maelezo yao, ikiwa ni hatua ya maandalizi ya kuwapeleka mahakamani Jumatatu ili kuwezesha hatua nyingine za kisheria kuchukua nafasi yake.”

Mbali na wafanyakazi hao, Manji anasubiriwa na sekeseke jingine la uhamiaji baada ya kuitwa ili aunganishwe na wafanyakazi hao kushtakiwa kwa madai ya kuajiri wageni wasiokuwa na vibali vya kufanya kazi nchini.

Manji amekuwa akishikiliwa na polisi tangu Februari 9 alipoitikia wito wa mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wa kuripoti kituo kikuu cha polisi kwa ajili ya mahojiano kuhusu matumizi na biashara ya dawa za kulevya.

Ofisa uhusiano wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Anna Nkinda amesema Manji aliruhusiwa hospitali jana saa 10:00 jioni baada ya kupatiwa matibabu kwa siku tatu. Hata hivyo haikufahamika alikokwenda.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images