Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Huzuni Yatawala Mahakamani Wakati Daktari Akitoa Ushahidi Dhidi ya Scorpion

0
0
Daktari  Bingwa wa Macho wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Christine Mataka ambaye alimpokea na kumhudumia, Said Mrisho anayedaiwa kutobolewa macho na Salum Njwete maarufu Scorpion akiwa shahidi wanne katika kesi hiyo upande wa serikali, ametoa siri nzito ya tukio hilo.

Dokta Mataka amesema alikuwa daktari wa kawaida kwa muda mrefu lakini alitunukiwa digrii ya pili (Master’s) na kuwa daktari bingwa wa matatizo ya macho miaka 14 iliyopita.

Akiongozwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nasoro Katuga bingwa huyo alisema macho ya Said hayakutobolewa kama inavyosemwa na watu kwenye vyombo vya habari isipokuwa yamenyofolewa na kuondolewa kabisa.

Majeruhi alifika hospitali macho yake yakiwa yamenyofolewa na kubaki hukohuko,hospitali hakufika hata na mabaki ya goroli.

Akielezea kitaalamu Dokta Mataka alisema kwa kawaida mtu anapotobolewa macho na kitu chochote ni lazima ukute goroli zikiwa zimepasuka na utete wenye utelezi unakuwa umetapakaa machoni lakini kwa majeruhi huyo goroli za macho yote mawili zilikuwa hazipo kabisa.

"Ukweli hiyo hali ilinishangaza sana kwa miaka 14 nikiwa kama daktari bingwa wa macho sijawahi kukutana na tukio kama hilo hivyo baada ya kupigwa na butwaa niliwapigia mabingwa wenzangu waje kujionea hali hiyo na tushauriane jinsi ya kufanya.

"Hata wao walivyofika wote walishangaa na kuniambia nao hawajawahi kukutana na hali hiyo.

"Nilimtibia majeruhi wakati huo huo nilikuwa nikimuongelesha na kumuuliza yaliyomsibu ambapo aliniambia wakati akinunua kuku pale Buguruni ndiyo akatokea mtu na kuanza kumshambulia.

"Nikamuuliza kama anamfahamu hiyo mtu aliniambia akimuona atamtambua.

"Baada ya matibabu nilimpeleka wodini na kumuandikia tarehe za kuhudhuria kliniki na nilimuambia kuwa katika maisha yake hawezi kuona tena hivyo ajifunze kuishi maisha ya mtu asiye na macho.

"Baadae alipoanza kuja kliniki aliniambia kuwa mama yake alikuwa akitaka kumpa jicho lake moja lakini nilimueleza ukweli kuwa hilo haliwezekani.

"Huwezi kulihamisha jicho halafu likawa hai hiyo huduma haipo hapa duniani.

Baada ya kutoa ushahidi wake mbele ha Hakimu Frola Haule kesi hiyo iliahirishwa mpaka Februari 22 mwaka huu itakapotajwa tena mahakamani hapo ambapo daktari bingwa wa tumbo ambaye nae alimtibu majeruhi huyo anatarajiwa kutoa ushahidi wake kwa upande wa serikali.

Sakata la Dawa ya Kulevya: Askofu Gwajima atema cheche

0
0
Gwajima:- Namuomba Rais ambadilishie Kazi Makonda, hii ya Ukuu wa Mkoa kutawala na kuongoza hata watu usiowapenda imemshinda. Sisemi amfukuze hapana nasema ambadilishie Kazi.

Gwajima : Makonda ana chuki na wivu na mimi

Gwajima : alikasirika hata niliposhuka na helkopta yangu siku ya mechi ya viongozi wa dini na wabunge dodoma.

Gwajima : nilichelewa kidogo nikaamua kupanda helkopta yangu mpaka uwanjani kabisa.

Gwajima : mimi nilicheza namba kumi Makonda namba tisa, jicho alilokuwa ananiangalia ni la chuki mpaka nikawa nashangaa.

Gwajima : hii hapa picha niko na Makonda, naibu spika na viongozi wengine tukichangia ujenzi wa taifa mbona hajanikamata hapa kama ninauza unga? .

Gwajima : Makonda alikuja kanisani kwangu na marehemu sitta na akapanda mazabauni je hakujua kama nauza unga? 

Gwajima : hili ni shambulio kwa kanisa sio kwa Gwajima

Gwajima : hili ni shambulio kwa wote walio okoka tuonekane hatufai

Gwajima : hili ni shambulio kwa maaskofu wote na wachungaji wote

Gwajima : kwa sababu Gwajima ana kanisa kubwa

Gwajima : kwa sababu Gwajima ana waumini zaidi ya elf sabini kanisani kwake na makanisa zaidi ya 400 nchi nzima.

Gwajima : nilikuwa mkali Sana kwa serikali ya awamu ya nne na kikwete

Gwajima : nilikemea sana kupotea kwa ndovu kila siku

Gwajima; Makonda anafanya hivi kwa maslahi ya Nani? .

Gwajima : Makonda anafanya hivi kufurahisha serikali iliyopita ionekana nimekomolewa.

Gwajima : Hili ni shambulio kwa Ukristo. Rais wangu mpendwa mbadilishie Kazi Makonda.

Gwajima : Makonda hajatumwa na Rais kufanya anayoyafanya

Gwajima : mimi namfahamu vizuri Rais, hawezi kumtuma Makonda kufanya hivi.

Gwajima : Makonda atavuka mipaka sasa, atakemea Polisi, atakemea jeshi, atakemea wabunge

Gwajima : Makonda atakemea mpaka waziri mkuu.

Gwajima; wenzetu wabunge wameungana kutumia sheria na kanuni zao watamuhoji.

Gwajima : sisi raia wa kawaida tusio na sheria wala kanuni za kututetea tutashtaki wapi? .

==>Msikilize Hapo Chini Akiogea

PICHA: Wema Sepetu na Tundu Lissu Walivyofikishwa Mahakamani Mchana Huu

0
0
Mbunge wa Singida Mashariki na Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA Tundu Lissu pamoja na Mwigizaji Wema Sepetu wamefikishwa Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu mchana huu  kujibu tuhuma zinazowakabili.

Tundu Lissu anakabiliwa na kesi ya uchochezi.Kesi inayomkabili Wema Sepetu ni kukutwa na msokoto wa bangi nyumbani kwake

Tundu Lissu Kapandishwa Kizimbani LEO na Kusomewa Mashitaka Manne ya Uchochezi

0
0
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.
 
Lissu amepandishwa kizimbani saa 6:25 na kusomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa.
 
Mutalemwa amesema upelelezi wa kesi hiyo bado lakini akawasilisha maombi ya kupinga dhamana ya mshtakiwa.
 
Katika maombi hayo amesema mshtakiwa Lissu anakabiliwa na kesi nyingine tatu mahakamani hapo na kwamba ingawa yuko nje kwa dhamana lakini amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.
 
Hata hivyo maombi hayo yalipingwa na Wakili wa Lissu Peter Kibatala akisema kuwa mashtaka yake yanadhaminika.
 
Amesema kiapo cha kupinga dhamana kilichotolewa na mkuu wa upelelezi wilaya ya Ilala, ASP Denis Mjumba kina dosari za kisheria kwani hakikidhi masharti ya viapo.
 
Mabishano bado yanaendelea, Wakili Kibatala bado anatoa hoja kabla ya Hakimu Huruma Shaidi kutoa uamuzi.

Wema Sepetu Kaachiwa Huru Kwa Dhamana ya Sh. Milioni 5

0
0
Msanii wa filamu  nchini na Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, mchana huu  amepandishwa kizimbani kwenye mahamaka ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Akisomewa mashtaka na wakili wa serikali Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba imeelezwa kuwa msanii huyo alikutwa na kiwango kidogo cha dwa za kulevya aina ya bangi 

Wakili Nassoro Katuga amesema mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa Wema Sepetu mnamo tarehe 4 mwezi wa pili mwaka 2017 katika eneo la Kunduchi Ununio watuhumiwa watatu akiwemo Wema Sepetu walitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya kuzuia na kupambana na dawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) (a) cha makosa hayo.

Msanii huyo na wenzake wameachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na wadhamini wawili na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 22 Februari 2017 itakapotajwa tena na kwamba bado uchunguzi unaendelea

VIDEO: Yusuph Manji Arudishwa Ndani ya Polisi Baada ya Kutaka Kutoka

0
0
Mfanyabiashara Yusuph Manji leo amefika kituo cha polisi kati kama alivyoahidi jana baada ya kutajwa kwenye orodha ya watu 65 na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Yusuph Manji alifika asubuhi kwenye kituo cha Polisi cha kati ambapo baadaye alionekana akiwa anatoka nje ya kituo  kuondoka lakini ghafla akazuiwa na Polisi na kumwambia anahitajika ndani ten.

==>Litazame tukio zima hapo chini

Picha: Askofu Gwajima Naye Kaamua Kwenda Polisi Leo Badala ya Kesho Kuitikia Wito wa Makonda

0
0
Askofu Josephat Gwajima mchana huu amefika katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kuhojiwa baada ya kutajwa na RC Paul Makonda katika orodha ya wahusika wa dawa za kulevya.

 Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima,Mchungaji Gwajima akionekana kufurahia jambo wakati akiwasili kituo cha polisi kati majira ya saa 7:30 mchana akiwa ameongoza na wafuasi wake,kutii agizo la Mkuu wa Mkoa Paul Makonda,ambaye watuhumiwa wote 65 aliowataja jana katika sakata la dawa za kulevya,aliwataka kufika kesho Ijumaa saa 5 asabuhi kituo cha Polisi kati kwa mahojiano zaidi.
Wafuasi wa Askofu Gwajima wakiwa wanawasili kituo cha Polisi kati
 Polisi wakiwatawanya wafuasi hao wa Askofu Gwajima na kuwataka  kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi
 Polisi wakiwatawanya wafuasi hao wa Askofu Gwajima na kuwataka  kukaa umbali wa mita 100 kutoka kituo cha Polisi

Mahakama Yatupilia Mbali Pingamizi la Serikali......Yampa Tundu Lissu DHAMANA Ya Milioni 20

0
0
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.

Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi.

Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa Ya February 10

Waziri Mkuu Amuagiza CAG kuchunguza Mapato ya shirika la Ndege Tanzania ATCL

0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema atamuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kuchunguza ukusanyaji mapato ya Shirika la Ndege Tanzania(ATCL)

Ameyasema hayo jana  alipotembelea Makao Makuu ya shirika hilo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujionea mwenendo wa uendeshaji wake.

“Nitamuagiza CAG  aje aangalie mwenendo wa ukusanyaji wa mapato ya shirika hili kuanzia mwaka jana lilipoanza kufanya kazi hadi sasa,” alisema Majaliwa.

Alisema kuwa Serikali haiko tayari kuona shirika hilo linakufa tena, hivyo amewataka viongozi wake wahakikishe linaendeshwa kwa mafanikio kwa manufaa ya Taifa.

Pia aliwataka waache kukusanya mapato kwa kutumia  risiti za kuandika kwa mkono na badala yake waanze kutumia mfumo wa kieletroniki ili kuzuia upotevu wa mapato hayo.

Katika hatua nyinginre, Waziri Mkuu amemtaka Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Witness Mbaga ajiridhishe na fedha zinazokusanywa katika eneo la mizigo kama ziko sahihi, lengo ni kudhibiti upotevu wa mapato.

Aidha,  Waziri Mkuu aliwataka viongozi wa shirika hilo kuhakikisha wanazingatia ratiba ya njia na muda wa safari ili wasipoteze wateja.

Agizo wa Rais Magufuli uwanja wa ndege Dar laanza kutekelezwa

0
0
Shughuli za ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) jana tarehe 09 Februari, 2017 zimeendelea kama ilivyoagizwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyefanya ziara ya kushtukiza jana tarehe 08 Februari, 2017.

Wafanyakazi 850 wameendelea na kazi mbalimbali za ujenzi wa uwanja huo ikiwa ni pamoja na ujenzi wa njia za kuingia na kushuka kwenye ndege, mifumo ya ujazaji wa mafuta ya ndege, maeneo ya kuegeshea ndege, sehemu ya kuingia na kutoka jengoni, mifumo ya viyoyozi na ujenzi wa nguzo.

Pia, timu ya wataalamu wanaosimamia ujenzi huo imefanyiwa mabadiliko ambapo wataalamu wengine 9 kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wamepelekwa na kuanza kazi mara moja.

Mkandarasi ambaye ni kampuni ya BAM International ya Uholanzi, Mhandisi Mshauri ambaye ni kampuni ya ACE ya Misri na wafanyakazi walioajiriwa katika mradi huo wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa hatua alizochukua zilizowezesha shughuli za ujenzi kuendelea.

Katika ziara ya juzi, Mhe. Rais Magufuli alielezea kusikitishwa na utekelezaji wa mradi huo uliopangwa kugharimu Shilingi Bilioni 560 kiasi ambacho ni kikubwa mno ikilinganishwa na jengo linalojengwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa Mnyaa alikiri kuwepo kwa dosari na kuahidi kuchukua hatua.

Mhe. Rais Magufuli ameahidi kuwa Serikali inafanya juhudi za haraka kutoa malipo ya Mkandarasi na Mhandisi Mshauri yaliyosababisha kusitishwa kwa ujenzi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Idd Azzan awasili kituo cha Polisi kuitikia wito wa RC Makonda

0
0
Aliyewahi kuwa Mbunge wa jimbo la Kinondoni, Idd Azzan ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi kuhojiwa kuhusu tuhuma za kuhusika na Dawa za Kulevya.

Viongozi wengine waliotakiwa kufika polisi kuhojiwa ni  Askofu Josephat Gwajima na  Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, ambao waliripoti jana kisha wakaondolewa na kupelekwa kusikojulikana

Freeman Mbowe Kagoma kwenda Polisi Kuitikia Wito wa Makonda......Kasema Lazima Amshitaki Kwa Kumchafulia Jina

0
0
Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Aikaeli Mbowe amesema kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda hana mamlaka ya kumuita kwenda Kituo cha Polisi.

Mbowe ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma kufuatia kutajwa katika orodha ya watuhumiwa 65 wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kutakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam leo saa tano asubuhi.

Mbowe amekanusha vikali tuhuma hizo za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya na kusema kuwa anachokifanya RC Makonda ni kuwaepusha watuhumiwa wa kweli wa dawa za kulevya na mikononi mwa sheria.

Aidha, Mbowe amesema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi muda wowote endapo njia sahihi zitakapofuatwa. 

Pia amesema atamfungulia mashtaka RC Paul Makonda kwa kumchafulia jina lake kufuatia kumtuhumu kwa biashara ya dawa za kulevya.

Kiongozi huyo wa Kambi ya Upinzani Bungeni amesema kuwa wao hawana ugomvi wowote na Jamhuri bali Paul Makonda binafsi.

Wakati huo huo, Kiongozi wa Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mbunge wa jimbo la Hai,  Freeman Mbowe amekutana na kufanya mazungumzo na Wabunge kutoka Bunge la Ulaya, David Martin, Gerrard Quille, Balozi wa Umoja wa Ulaya Tanzania, Roeland Van De Beer  na Waziri Kivuli wa Mambo  ya Nje, Afrika Mashariki na Kikanda,Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, mjini Dodoma leo Ijumaa 10/02/2017.

Zitto Kabwe amkingia kifua Mbowe....Msikilize Hapa Akiongea

0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye pia ni Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amemkingia kifua Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na kusema kuwa anaamini Mbunge huyo wa Hai hajawahi kujihusisha na dawa za kuleva kwa namna yoyote

Zitto ambaye ameambatana na Mbowe katika mkutano wake na wanahabari leo mjini Dodoma, amesema kilichofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kumtaja Mbowe katika sakata la dawa za kulevya ni sawa na kutangaza vita na chuki dhidi ya chama hicho.

Amesema kuichafua CHADEMA ni sawa na kuuchafua upinzani hivyo na yeye hawezi kukaa kimya kuona upinzani ukishambuliwa, na ndiyo sababu ya kuongeza nguvu kwa kuungana naye.

==>Msikilize hapo chini akiongea

Jeshi la Polisi Dar Lamjibu Mbowe......Lasema Kama Hataripoti Polisi, Basi Litamfuata Popote Alipo.

0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema kama Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hataripoti bila kutoa taarifa yoyote ya udhuru atafuatwa kwa kuwa jeshi hilo linahitaji  kumhoji.

Kamanda wa kanda hiyo, Simon Sirro amesema hayo leo muda mfupi baada ya Mbowe kueleza kuwa hataripoti polisi kutokana na wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

Amesema operesheni dhidi ya mihadarati bado inaendelea na kuanzia sasa hawataruhusu tena mkusanyiko wa watu katika kituo cha polisi kati na wale watakaoonekana watashughulikiwa hivyo asije kulalamika mtu kwani taarifa imeshatolewa.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ametangaza rasmi kutofika kituoni hapo kwa madai kuwa hawezi kwenda polisi kwa wito wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda isipokuwa pale tu taratibu za kisheria zitakapofuatwa.

Yusuf Manj na Askofu Gwajima Kuendelea Kusota Selo.....Sirro Asema Upelelezi Bado Unaendelea

0
0
Kamanda Sirro amesema  bado wanamshikilia mwenyekiti wa Yanga, Yusuph Manji pamoja Askofu wa kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya na upelelezi dhidi yao bado haujakamilika.

Watuhumiwa hao wawili waliripoti kituoni hapo jana mchana na siyo leo kama walivyoagizwa na RC Paul Makonda.

Kamanda Sirro amesema atatoa taarifa Jumatatu kueleza nini kinaendelea kuhusu watuhumiwa hao.

Mpaka wakati anazungumza na waandishi wa habari kamanda huyo alisema walioripoti kituoni hapo ni watuhumiwa 4 kati ya 65 .

Walioshuhudiwa na waandishi wa habari wakiripoti kituoni hapo ni Iddi Azzan, Hussain Pamba Kali pamoja na bosi Sea Cliff.

Rais Magufuli ateua Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya

Anaswa na mzigo wa dawa za kulevya chumbani..... RPC Mwanza asimulia Sakata Zima

0
0
Mtu mmoja anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza kwa kosa la kupatikana na dawa za kulevya yanayodhaniwa kuwa heroine kiasi cha pinchi 240 na ndonga mbili.

Taarifa ya jeshi hilo iliyotolewa leo, imedai kuwa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Kassim Hemed Kesi mwenye umri wa miaka 43,  amekamatwa majira ya saa 6 usiku wa kuamkia leo katika mtaa wa Kanyerere kata ya Butimba wilaya ya Nyamagana Jijini Mwanza

Taarifa hiyo imedai kuwa mtu huyo ni  mfanyabiashara wa spear za magari katika mtaa huo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Ahmed Msangi amesema kuwa awali polisi walipata taarifa za mtuhumiwa huyo kuwa anajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, hivyo askari walikuwa wakiendelea na upelelezi pamoja na uchunguzi kuhusiana na  tuhuma hizo.

Aidha wakati askari wakiendelea na upelelezi dhidi ya tuhuma za mfanyabiashara huyo, jana tarehe 09.02.2017, polisi walipokea taarifa kutoka kwa raia wema kwamba mtuhumiwa huyo ameingiza mzigo mkubwa wa madawa ya kulevya kutoka Dar es Salaam na ameanza kuusambaza mtaani.

Tukio lilivyokuwa
Askari walianza kufanya ufuatiliaji wa haraka kuhusiana na taarifa hizo, ndipo ilipofika majira ya saa sita usiku askari walifika hadi nyumbani anapoishi mtuhumiwa na kuizingira nyumba yake yote na kumuona kupitia dirisha akiendelea kufunga madawa hayo kwenye vikete vidogovidogo maarufu kama pichi.

Wakati askari wanataka kuingia ndani ya nyumba mtuhumiwa alishtuka na kukimbiza mzigo huo wa madawa ya kulevya chooni ili kupoteza ushahidi.

Aidha askari waliona kitendo kile kupitia dirishani na baadhi YA askari waliingia ndani na kufanikiwa kukuta pinchi 240 zikiwa chooni lakini bado hazikuwa zimetumbukia shimoni na kufanikiwa kuzitoa kwenye tundu la choo.

Msangi amesema wakati huohuo askari wengine waliokuwa nje walikwenda kuvunja bomba linalopitisha uchafu/choo linalokwenda kwenye shimo na kuweka kizuizi hapo na kufanikiwa kupata ndonga 2 za dawa za kulevya huku nyingine zikibebwa na maji .

 Polisi wanaendelea na mahojiano na mtuhumiwa ili kuweza kubaini mtandao wa watu aliokuwa akijihusisha nao katika biashara hiyo ya madawa ya kulevya.

Habari Zilizopo Katika Magazeto ya Leo Jumamosi ya February 11

Zitto Kabwe: Sasa kukamata wabunge hovyo hovyo mwisho

0
0
Mbunge wa Kigoma mjini Zitto Kabwe amefunguka na kusema ile hali ya polisi kuwakamata wabunge hovyo sasa mwisho baada ya jana Ndugai kutoa uamuzi kuwa Afisa yoyote wa Serikali ambaye atakuwa akimuhitaji mbunge ni lazima kwanza atoe taarifa kwa spika

Hali hii imefikia baada ya Jumatano bunge kupitisha azimio la kutaka kwanza ruhusa ya spika wa bunge pale vyombo vya dola kama polisi wanapokuwa wanamuhitaji mbunge yoyote kwa jambo lolote.

"Leo (jana)  Spika wa Bunge ametoa uamuzi wa Spika kwamba Afisa wa Serikali anapomtaka mbunge kwa jambo lolote lile lazima kwanza kupata kibali chake. Mabunge yote ya Jumuiya ya Madola hulinda kwa wivu mkubwa hadhi yake kama mhimili. Sasa kukamata kamata wabunge hovyo mwisho. Lazima mihimili iheshimiane. Sasa tuone kama Sirro atamfuata Mbunge wa Hai kama alivyosema" alisema Zitto Kabwe

Mbali na hilo Mhe. Zitto Kabwe ametoa pongezi kwa wabunge wote pamoja na Spika wa bunge kwa kuonyesha msimamo na kupigania heshima ya bunge

"Nawapongeza wabunge wote kwa kuonyesha msimamo katika jambo hili na ninampongeza sana Spika Ndugai kwa kusimamia heshima ya bunge lake" Alimalizia Zitto Kabwe
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images