Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kauli ya Jeshi la Polisi Kuhusu Kumkamata Zitto Kabwe Bungeni

$
0
0
Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe jana alijificha ndani ya ukumbi wa bunge mjini Dodoma  kwa hofu ya kukamatwa na Jeshi la Polisi mara tu atakapotoka nje ya ukumbi huo.

Zitto Kabwe kupitia ukurasa wake wa Twitter aliandika  kuwa Polisi wa bunge wamemwambia kuwa watamkakata kwa kosa la uchochezi ambalo yeye mwenye hafahamu ni lipi


Akizungumzia taarifa hizo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Lazaro Mambosasa  amesema si kweli kwamba Polisi walikuwa Bungeni kumsubiri Zitto atoke wamkamate.

 “Hiyo taarifa yeye mwenyewe ndio anajitangazaia akamatwe lakini sisi hatumkamati kwasababu hatuna ishu nae

“Unajua watu wanafikia mahali wanatafuta umaarufu wakamatwe ili wapige mayowe… hatuna mpango wowote wa kumkamata kwasababu hajatenda kosa la jinai” Amesema Kamanda Mambosasa.

Wafanyabiashara wa Pombe za kienyeji watakiwa kuwa na leseni

$
0
0
Wafanyabiashara wa Pombe za Kienyeji wanatakiwa kuwa na leseni ya kufanya biashara hiyo ambayo hutolewa na Halmashauri.

Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo aliyasema hayo jana  Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Najma Giga juu ya Serikali imejipangaje kukabiliana na tatizo la ulevi wa kupita kiasi kwa pombe za kienyeji pamoja na sheria ya vileo ya mwaka 1969 kuwa ya zamani hivyo kutokidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo.

“Pombe za kienyeji zimeanishwa katika kifungu cha 2 cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77 ambapo kwa mujibu wa sheria hiyo, wafanyabiashara wote wanatakiwa kuwa na leseni ambayo inatolewa na Halmashauri,” alifafanua Jafo.

Aliendelea kwa kusema kuwa, biashara hiyo hairuhusiwi kufanyika katika muda wa kazi. Muda unaoruhusiwa kisheria ni kuanzia saa 12:00 jioni hadi saa 5:00 usiku kwa siku za Jumattu hadi Ijumaa na kuanzia saa 05:00 asubuhi hadi saa 06:00 usiku kwa siku za Jumamosi, Jumapili na Sikukuu.

Vile vile  alisema kuwa unywaji wa pombe kupita kiasi ni tabia ya mtu ambayo inawezekana kabisa haitokani na mapungufu ya Sheria.

Hata hivyo Wakuu wa Mikoa na Wilaya wameagizwa kusimamia taratibu za uendeshaji wa biashara za vileo na kuchukua hatua kwa watumiaji na wafanyabiashara wanaobainika kukiuka Sheria hiyo.

Aidha alisema kuwa, endapo ipo haja ya kuifanyia marekebisho Sheria ya vileo, Serikali itakuwa tayari kupokea mapendekezo kwa eneo ambalo litaonekana kuwa na mapungufu ili kufanyiwa marekebisho kupitia Bunge.

Jafo alitoa wito kwa Watanzania wote kutumia muda wao kufanya kazi kwa bidii ili kujiletea maendeleo kwa ustawi wa Taifa zima. Aidha Serikali haitasita kuchukua hatua kwa wanywaji pombe wasiozingatia utaratibu pamoja na wazururaji wakati wa kazi.

Mbunge Amvaa Makonda Kuhusu Utajiri wa Mali Alioupata ndani ya Kipindi Kifupi.......Ataka Vyombo vya Dola Vimchunguze

$
0
0
MBUNGE wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma, amemlipua bungeni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa kudai kuwa anastahili kuchunguzwa kutokana na mali kibao anazomiliki ndani ya kipindi kifupi ikiwamo jengo la ghorofa, viwanja na magari ya kifahari.

Akizungumza bungeni jana, mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM katika Mkoa wa Geita, alisema Makonda hakuwa na utajiri alio nao sasa mwaka 2015, na hivyo akataka achunguzwe ni kwa namna gani amebadilika ghafla baada ya kushika nafasi za ukuu wa wilaya na baadaye ukuu wa mkoa, huku akisisitiza kuwa yeye yuko tayari kuvisaidia vyombo vya dola kuonyesha utajiri aliojilimbikizia mkuu huyo ndani ya kipindi kifupi.

Alitaja sababu nyingine za kumchunguza Makonda kuwa ni pamoja na kufanya ukarabati ofisi yake kwa Sh. milioni 400 na pia akayataja magari ya kifahari anayomiliki katika kipindi hicho kifupi kuwa ni pamoja na la aina ya Lexus alilodai lina thamani ya Sh. milioni 400 na lingine la thamani kubwa alilolitaja kuwa ni V8.

Aliposimama bungeni, Msukuma ambaye kabla ya jana alishagusia tuhuma dhidi ya Makonda kwa kuzungumzia safari alizokwenda Marekani, Dubai na Jiji la Paris nchini Ufaransa, jana alianza kwa kuomba mwongozo kwa Spika akitumia kanuni ya 68(7), akisema anashangaa ni kwa namna gani mawaziri wanaosimamia masuala ya utawala bora wamepigwa ganzi kiasi cha kushindwa kushughulika na Makonda na kumsubiri Rais.

“Mheshimiwa Spika, nasimama kwa kanuni ya 68(7) kuhusu jambo lililojitokeza jana (juzi) wakati wa mjadala wa Bunge…naomba mwongozo wako.

"Mimi binafsi naunga mkono jitihada za Rais kukamata wauza dawa za kulevya, lakini dalili ya kwanza ya kuanza kumhisi mtu kama anajishughulisha na biashara ambazo hazieleweki, kwanza ni mwenendo wa mtu yeyote…siyo mbunge wala siyo nani,” alisema Musukuma.

Alisema mkuu huyo wa mkoa, mwaka 2015 alikuwa akiishi kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, lakini sasa wakati amekuwa Mkuu wa Mkoa, anatumia magari ya kifahari, ana jengo la ghorofa Mwanza na pia anamiliki viwanja maeneo mbalimbali.

“Anatumia Lexus ya petroli ya Sh. milioni 400, lakini imekarabatiwa ofisi (yake) ya RC Dar es Salaam kwa zaidi ya Sh. milioni 400 bila kufuata utaratibu wa manunuzi wa serikali.

“Ana ma-V8 na Mwanza amejenga jengo la ghorofa…ni kina nani wanaotakiwa kujadiliwa na kufanyiwa uchunguzi?” Alidai Musukuma kabla ya kuongeza:

“Na hawa mawaziri tulionao humu, kwa nini wamepigwa ganzi? Utawala bora, Mambo ya Ndani na Waziri wa Sheria…kwa nini mmepigwa ganzi?”

Musukuma aliongeza: “Kwa nini mmepigwa ganzi? Mnalifanya suala hili ni la Rais, kuanza kuhangaika na Mkuu wa Mkoa…na hata kama anachangiwa na wahisani, Sheria ya Maadili inatutaka anayekuchangia umtangaze.Lini amemtangaza aliyemchangia fedha?”

Musukuma alisema anaomba mwongozo kama wengine wanafanya mambo ya ovyo na wanakuwa na kinga na mawaziri wakapigwa ganzi na hawataki kufuatilia.

“Tunataka RC achunguzwe mali zake alizonazo… kwa mwaka mmoja huwezi kumiliki magari ya kifahari, ukajenga Mwanza, ukaenda Marekani, ukanunua maviwanja.

"Wala siyo suala la kuogopa. Mimi nasema nipo tayari kuwasaidia mawaziri na vyombo vya usalama tuwaonyeshe,” alisema Musukuma.

Msukuma ametoa kauli hizo ukiwa ni mwendelezo wa kumtuhumu Makonda baada ya kufanya hivyo bungeni juzi aliposema anashangaa kuona Taifa linaifanyia kazi taarifa ya mkuu huyo wa mkoa juu ya wauza dawa za kulevya, wakati mawaziri wa zamani wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Charles Kitwanga, wamewahi kusema wana orodha ya watu wanaouza dawa za kulevya na hakuna hatua zilizochukuliwa.

“Wauza dawa za kulevya wanajulikana na hata walio mstari wa mbele kukamata wenzao wanashinda nao na kuwasafirisha nchi mbalimbali kama Marekani.

“Kwanini vyombo vya ulinzi na usalama visimchunguze Makonda maana anasafiri sana Ulaya, Ufaransa na Dubai, hivi anasafiri kwa mshahara upi alionao?

“Tunaambiwa juu ya vita ya kupambana na dawa za kulevya halafu tunawakamata akina Ray C na Chidi Benz wakati hao ni wagonjwa.

“Kama Rais Magufuli amesema kama mkewe Mama Janet anahusika na dawa za kulevya akamatwe, kwanini Makonda naye asihojiwe kwa sababu amewapangisha watu nyumba wakati wanajihusisha na dawa za kulevya?”
alisema Msukuma. 

Hivi karibuni, Makonda aliongoza kasi katika vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kuamuru watu kadhaa wanaodaiwa kujihusisha na dawa hizo jijini Dar es Salaam waripoti polisi wakiwamo wasanii Wema Sepetu, Khalid Mohamed ‘TID’, Dogo Hamidu na Tunda.

Aidha, aliwataja askari polisi kadhaa wanaohusishwa pia na dawa za kulevya akiwamo aliyewahi kuwa Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime. Askari hao walisimamishwa kazi na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu, ili kupisha uchunguzi wa kina dhidi yao kuhusiana na tuhuma alizoziibua Makonda.

Ufafanuzi wa Naibu Spika
Akifafanua mwongozo huo, Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson, alisema Mbunge huyo amezungumza jambo ambalo ni kinyume cha kanuni za chombo hicho cha kutunga sheria.

“Mheshimiwa Mbunge, umetoa maelezo mengi siwezi kuyarejea hapa…maana nitakuwa kama natoa msisitizo, jambo ambalo kanuni zetu zinakataza, kwa maana mambo aliyoyataja, yule mtu aliyemtaja na wengine waliohusika, kama jambo alilolisema si sahihi, wanaweza kuja bungeni,” alisema Dk. Tulia.

Naibu Spika huyo alisema kwa mujibu wa kanuni ya 68 (7), mwongozo unatakiwa kuombwa kwa jambo lililotokea bungeni mapema na kwamba, kama ni jambo la juzi, atumie kanuni nyingine kuleta hoja yake.

CUF Mambo Bado.....Habibu Mnyaa Atimuliwa Uanachama

$
0
0
 MOHAMED HABIBU MNYAA AFUKUZWA UANACHAMA

Tarehe 7/2/2017 Mkutano Mkuu wa Tawi la Chanjaani, Jimbo la Mkoani wilaya ya Mkoani-Pemba, umefanya maamuzi ya kumfukuza uanachama wa CUF Mohamed Habibu Mnyaa  kutokana na kukiuka katiba ya chama Ibara ya 12 (6)(7)(16) kutokana na kuwa na mwenendo usiofaa wa kuwagawa wanachama, kueneza taarifa za upotoshaji dhidi ya viongozi na Chama, kufanya vitendo vya hujuma za kutaka kukidhoofisha Chama, kudharau na kushindwa kuhudhuria na kutoa ushirikiano kwa tawi lake kila alipotakiwa kufanya hivyo. Mkutano Mkuu wetu wa leo umehudhuriwa na wajumbe halali 112 kati ya wajumbe wote halali 113.

Wajumbe wote 112 wamepiga kura za ndio kuazimia kumfukuza uanachama kwa mujibu na mamlaka ya kikatiba yaliyoelezwa katika katiba ya CUF ukurasa wa 29 ibara ya 18(1)(ix) kuhusu wajibu wa Mkutano Mkuu wa Tawi kama ilivyoeleza kuwa;

 “Kumchukulia hatua za nidhamu mwanachama au kiongozi yeyote wa tawi hilo, ikiwa ni pamoja na kumpa onyo, karipio, karipio kali, kumsimamisha uanachama au uongozi wa Chama kwa muda, na hata kumuachisha au kumfukuza uanachama wa Chama”

Mohamed Habibu Mnyaa alijiunga na CUF katika tawi hilo tarehe 28 septemba mwaka 1999 na kukabidhiwa kadi yenye Namba ya usajili 029033. Mohamed ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Mkanyageni kwa muda wa vipindi viwili 2005-2015, amekuwa na mwenendo huo mbaya na usiofaa kwa Chama na viongozi wake tangu alipokosa ridhaa ya wanachama na Maamuzi ya vikao vya Chama kumpitisha kugombea kwa mara nyingine tena katika nafasi ya ubunge mwezi August, mwaka 2015. Mohamed amefukuzwa uachachama akiwa ni mwanachama wa kawaida wa tawi la Chanjaani asiyekuwa na wadhifa wowote mwingine ndani ya Chama.

Kwa mujibu wa Katiba ya CUF ibara ya 108(5) kuhusu Nidhamu ya chama na Muda wa kukata Rufaa inaeleza kuwa;

“ Mwanachama au kiongozi yeyote aliyeamua kukata Rufaa kwa jambo lolote lile, basi atafanya hivyo kwa ngazi iliyo juu ya kikao kilichotoa maamuzi ambayo hakuridhika nayo katika kipindi kisichozidi siku kumi na nne (14) tokea siku uliotolewa uamuzi huo”  ni hiyari yake kuona kama inafaa kukitumia kifungu hiki au kutokitumia.

Tunatoa wito kwa wanachama wote wa tawi la Chanjaani, kuzingatia wajibu wao wa kikatiba na kuheshimu taratibu, kanuni na kulinda nidhamu na heshima ya Chama chetu ndani ya Chama na ndani ya jamii kwa ujumla. Uongozi wa tawi hautasita kutekeleza matakwa ya katiba pale itakapobainika kwa mwanachama yeyote kwenda kinyume na maamuzi na misimamo ya Chama. 

HAKI SAWA KWA WOTE

KOMBO MOHAMED MAALIM
KATIBU WA TAWI LA CHANJAANI, JIMBO LA MKOANI-PEMBA
Mawasiliano: 077 815 3414

Mrema Awatuhumu Polisi Kusambaza Dawa za Kulevya

$
0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustino Lyatonga Mrema ameibuka na kusema kuwa wapo baadhi ya polisi wanagawa na kusambaza dawa za kulevya pia wanawasaidia baadhi ya waathirika wa dawa hizo waliopo magerezani kuzipata.

Augustino Mrema anasema vita ya dawa za kulevya inawezekana kumalizika kama watawatumia watumiaji na wauzaji wadogo wadogo kuwapata wale wauzaji wakubwa ambao ndiyo tatizo zaidi katika jamii.

"Vita hivi vitawezekana kumalizika kama tutatumia hawa wadogo wenye kete mbilimbili, na siyo kuwapeleka magerezani, wamenionesha na njia wanazotumia kuwapa dawa waathirika waliopo magerezani, tusitumie nguvu nyingi kuwakamata hawa dagaa wadogo wadogo, bali tuwatumie hawa tupate chain nzima, kwa njia hiyo tutapeleka watu wanaostahili magerezani" alisema Augustino Mrema

Mbali na hilo Augustino Lywatonga Mrema anasema kama polisi walikuwa wanasambaza na kugawa madawa ya kulevya hivyo basi wao ndiyo walikuwa wakiendesha hivyo vijiwe na kuwajua wahusika wa madawa ya kulevya.

"Sasa kama polisi ndiyo anasambaza na kugawa madawa kwa hiyo vijiwe vile vilikuwa vinaendeshwa na wao, hivyo wanawajua wanaogawa, na wanaotumia sasa huu mtandao ukikamatwa hii nchi itapona" alimalizia Mrema.

Jana Tundu Lissu Kalala Sero Baada ya Kunyimwa Dhamana.....Mbowe Alaani

$
0
0
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, linamshikilia Mbunge wa Singida Mashariki ambaye pia ni mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu kwa madai ya kutoa kauli za uchochezi.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam jana, Kamanda wa Kanda Maalumu, Kamishna Simon Sirro, alisema Lissu alikamatwa juzi mjini Dodoma wakati alipokuwa akitoka katika vikao vya Bunge.

Alisema baada ya kumkamata, walilazimika kumsafirisha hadi Dar es Salaam ambako inadaiwa ndiko alikotolea kauli hizo ambazo wanadai zinaweza kuhatarisha amani ya nchi.

“Tumemkamata Tundu Lissu juzi mjini Dodoma na kusafirishwa usiku hadi Dar es Salaam ili aweze kufikishwa kituoni kwa ajili ya kuhojiwa kutokana na kutoa kauli zake za kichochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi,” alisema Sirro.

Alisema si mara ya kwanza kwa kiongozi huyo kutoa kauli hizo na kuitwa kituoni kwa ajili ya kuhojiwa, lakini kinachofanyika baada ya kuruhusiwa amekuwa akiendelea kuzitoa tena.

Sirro alisema kutokana na hali hiyo, jeshi hilo linaendelea na mahojiano na kwamba uchunguzi utakapokamilika watamfikisha mahakamani kwa hatua zaidi.

Alisema kutokana na hali hiyo, kesho (leo) atatoa taarifa kamili kuhusu matamshi hayo yanayodaiwa ya kichochezi ili wananchi waweze kujua.

Naye Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, amesema anasikitishwa na vitendo vya kukamatwa wabunge wakiwa ndani ya vikao, huku Ofisi ya Bunge ikikaa kimya bila kutoa tamko.

Akizungumza jana baada ya kumtembelea Lissu, ambaye yuko mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam, Mbowe alisema Ofisi ya Bunge inajua wabunge wana kinga ya kisheria, lakini wamekuwa hawachukui hatua wala kutoa kauli yoyote.

“Tunasikitishwa na vitendo vya kukamata wabunge wakiwa ndani ya vikao vya Bunge na hasa wabunge wa upinzani, wanaendelea kukamatwa wengine wanafungwa na wengine wanapotezewa muda wao wa Bunge.

“Wabunge wanakamatwa Dodoma wanasafirishwa usiku wa manane kama vibaka halafu wananyimwa dhamana, viongozi wa Bunge hawatoi kauli yoyote… haya mambo yanayotokea si ya kawaida,” alisema Mbowe.

Alisema Lissu amehojiwa kwa kauli zake zinazodaiwa kuwa za uchochezi, wakati akijadili suala la njaa katika Taifa.

“Sasa Lissu kama viongozi wengine wa Chadema, vyama vingine vya siasa na madhehebu mbalimbali ya dini, walitahadharisha hali ya kuwapo kwa njaa katika Taifa. Lakini ndani ya Bunge kauli ya Serikali iliyotolewa na Waziri wa Kilimo ilithibitisha kwamba watu zaidi ya milioni 1.5 wanakabiliwa na njaa na karibu 200,000 wana shida kali ya njaa.

“Kauli alizoongea Lissu zimeshathibitika si za uongo na tunashangaa mwezi mmoja umepita na Serikali imeshatoa kauli ya kuthibitisha shutuma zilizotolewa na viongozi wa dini, kisiasa na hata wa kijamii, lakini bado wamemshika Lissu na wamekataa kumpa dhamana,” alisema.

Mbowe alisema viongozi wa chama hicho watakutana na wanasheria wao kutafakari kwa kina hatua za kuchukua.

 “Wamesema hawawezi kutoa dhamana katika hatua ya sasa, jalada lake litapelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na ndiye atakayetoa maamuzi kuhusiana na kesi yenyewe. Tumeelekezwa tufuatilie dhamana yake kesho (leo),” alisema.

Video: Msikilize RC Paul Makonda akitaja majina mapya 65 ya watuhumiwa wa Dawa za kulevya Akiwemo Mbowe, Na Gwajima

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda leo ametaja majina mengine ya watu wanaotuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya ambapo pia watahojiwa na Jeshi la Polisi.

RC Paul Makonda amesema kuwa watu hao wanatakiwa kufika katika Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Majina hayo mengine 65 ameyataja leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo miongoni mwa wengi waliotajwa ni pamoja na Mwinyi Machapta, aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan, Askofu Josephati Gwajima, Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Aikaeli Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji.

Hapa chini ni video RC Paul Makonda akitaja majina ya watuhumiwa wa dawa za kulevya.

Makonda Kataja Majina Mengine 65 ya Wanaohusika na Madawa ya Kulevya......Yumo Freeman Mbowe, Yusuph Manji, Askofu Gwajima

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametaja majina ya watuhumiwa wengine 65 wa madawa ya kulevya, wakiwemo Mwenyekiti wa Chadema na Mbunge wa Jimbo la Hai, Freeman Elikael Mbowe, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Askofu Josephat Gwajima na Mbunge Mstaafu wa Kinondoni, Idd Azzan.

Makonda amesema hii ni awamu ya pili ya oparesheni ya kusaka watuhumiwa wa mtandao wa biashara haramu ya madawa ya kulevya, ambapo amesema awamu hii itakuwa ngumu ikilinganishwa na ile ya kwanza iliyohusisha polisi na wasanii kukamatwa.

Makonda amewataka watu wote 65 waliotajwa, kuhakikisha wanaripoti kwenye Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam (Sentro) siku ya Ijumaa saa 5 asubuhi kwa mahojiano zaidi.

Akizungumza na wanahabari ofisini kwake, Makonda amesema kuwa, waliokamatwa awali ndiyo waliofanikisha kupatikana kwa orodha hiyo mpya.


Kauli ya CHADEMA baada ya Mbowe kutuhumiwa kwa biashara ya dawa za kulevya

$
0
0
Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kutaja orodha ya majina 65 ya watuhumiwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeibuka na kukosoa utaratibu unaotumiwa na kuongozi huyo.

CHADEMA kimekosoa utaratibu unaotumiwa wa kutangaza majina hadharani ambapo wamesema kuwa baadhi ya wanaotajwa ni viongozi wa ngazi za juu wa kitaifa.

Mkutano huo ulioongozwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Vicent Mashinji umekuja saa chache baada ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Aikaeli Mbowe kutajwa miongozi mwa watuhumiwa hao 65.

“Majina mengi yaliyotajwa kuna jina la Mwenyekiti wa chama Mbowe, suala la utetezi wake au maelezo hilo ni suala binafsi sababu kilichotajwa ni jinai lakini kimsingi tunachukua nafasi hii kulaani jinsi tusivyoweza kuendesha utawala wa sheria kwenye nchi yetu na jinsi tusivyofuata kanuni zilizowekwa dhidi ya sheria.

"Mh. Mbowe ni kiongozi wa kitaifa, ni kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, ni Mbunge wa Hai…. kwahiyo kuna taratibu za kufata unapokua na kusudio la kumuita.”

Katibu huyo alisema kuwa si sahihi kutaja majina ya viongozi wakubwa hadharani kwa tuhuma tu ambazo hata hazijathibitishwa. Dkt Mashinji amesema kuwa huko ni kukosa utashi na busara za uongozi.

Katika orodha hiyo ya awamu ya pili iliyotolewa na RC Makonda leo mchana imejumuisha viongozi wengine kama, Askofu Josephat Gwajima, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, Aliyekuwa Mbunge wa Kinondoni, Iddi Azan

Kamanda Sirro aeleza hatma ya Wema Sepetu

$
0
0
Wema Sepetu bado anaendelea kushikiliwa na polisi jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za dawa za kulevya ambapo jana baadhi ya watuhumiwa wenzake walifikishwa mahakamani na kuachiwa kwa dhamana.

Leo February 8, 2017 Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa jeshi lake bado linamshikilia Wema na wenzake saba ambao walikamatwa na vielelezo na kuwa jalada lao limepelekwa kwa wakili wa selikali alipitie ili aone ushahidi uliopo pamoja na kupata majibu kutoka kwa mkemia mkuu wa selikali kubaini kama kweli ni mtuamiji wa madawa ya kulevya.

Amesema upelelezi ukikamilika na wao watapelekwa Mahakamani.

Yusuf Manji Aapa Kumshitaki Makonda Kwa Kumchafulia Jina......Kasema Yupo Tayari Kupimwa na Kupekuliwa Kama ni Kweli Anatumia Madawa ya Kulevya

$
0
0
Manji: Nimesikia wakisema natakiwa kufika kituo cha Polisi siku ya Ijumaa.

Manji: Mimi nina nafasi mbili kwenye jamii, Mimi ni mtoto wa baba yangu na nafasi yangu ya pili mimi ni mwenyekiti wa Yanga na nyote mnajua ninavyoheshimiwa.

Manji: Na chaguzi zilizopita mimi nilichukuahukua fomu peke yangu ya kugombea Yanga hivyo naheshimika.

Manji: Huwezi kunitangaza kupitia radio kwamba niende kwenye kutuo cha polisi saa tano. Makonda ni mdogo kwangu kiumri.

Manji: Na katiba inasema kila mtu ana haki yake, Ukinichafua mimi kama Mwenyekiti wa Yanga unachafua Yanga nzima.

Manji: Ukinishutumu mimi ni mpumbavu tu wewe.

Manji: Kama unataka mimi nikusaidie kutaja wauzaji ni kuniweka kwenye hatari.

Manji: Mimi nitaenda Kituo cha Polisi kesho sisubiri hiyo Ijumaa.

Manji: Kifungu cha 66 katika katiba kinaeleze haki zangu na kufungu 32 pia. Vinanilinda.

Manji: Nataka nimshitaki Mahakamani na vyombo vyote vilivyoandika kunituhumu na madawa.

Manji: Kesho naenda Polisi asubuhi nihojiwe baada ya hapo naanza kutafuta haki yangu. Huwezi kuniita kaka huku unanitaja kwenye mambo mabaya.

Manji: Wapo watu kwenye mtandao wameanza kuandika vitu, Alichofanya mkuu wa mkoa ni kosa siwezi kukubali.

Manji: Na Wanayanga kama mnaona mimi sifai na kama hamna imani na mimi hata kesho naondoka Yanga. Siwezi kuchafua Club kubwa.

Manji: Kwanini RC Makonda hajamuita Askofu Pengo au Mashehe wamsaidie?

Manji: Hiwezi kuniita mimi kama mbwa njoo, Hii ni kutafuta masifa. Kesho utanikuta mimi kwenye gazeti na wengine 65 watasahaulika. Hii sio haki.

Manji: Zipo njia za kushughulikia vitu, Tukienda Comoro tunaenda na bendera ya Tanzania.

Manji: Kama unataka msaada omba msaasa sio unaagiza msaada, Unaniita na watu 65 nikae kwenye foleni, watu 65 watamaliza saa ngapi? Saa tano usiku nitoke? Sina kazi nyingine za kifanya?

Manji: Yupo mzee mmoja na wenyewe mnamjua, alinitukana nikamdai shilling moja. Unanihusisha mimi jina langu nloachiwa na baba kwenye huu upumbavu halafu unathubutu kiniita kaka yako?

Manji: Hii itanifanya nishindwe kwenda Comoro na Klabu ya Yanga sababu Wanacomoro watasema nimepeleka madawa. Wananichafua sana.

Manji: Hivi ni vita na wanahitaji msaada haraka na kama wana shutuma au ushahidi au huo msaada wanieleze. Kama vita kwanini isiwe leo wasubiri ijumaa. Mimi naenda kesho.

Manji: Kesho nyie watu wa magazeti na habari msitoe habari kwa upande mmoja.

Manji: Ambao hawatabalance habari. Cybercrime inasema ukiweka habari ya uongo unafungwa. "Ambaye ataandika makonda manji dawa za kulevya" kesho namshitaki.

Manji: Wakina Amina Chifupa walitaja majina, yalienda wapi? Hii jitihada hakuna mtu anakataa. Hata unayemchunguza humtaji kwenye vyombo vya habari. Hata TAKUKURU hawawataji wanaowachunguza. Mimi siwezi kwenda kutaja mshahara wa mfanyakazi. Nitakiwa namvunjia heshima.

Manji: Mimi nipo tayari kupimwa na kusearchiwa na Makonda naye apimwe kama anatumia na wamsearch pia.

Manji: Mimi sitaki kuchanganya vitu viwili kwenye mkutano mmoja. Kesho au keshokutwa ntafanya mkutano kuanzia PSPF, Coco Beach nk. Leo nakaa kwenye point moja tu ya madawa.

Manji: Mkuu wa mkoa kunasehemu nimegongana naye oysterbay na nlienda kuonanana naye kama diwani wa mbagala kuu kumuomba mkuu wa majeshi atakayekuja ahamishe kambi ya jeshi kutoka mbagala na kupelekwa nje ya mji. Kama diwani siwezi kumuandikia rais.

Rais Magufuli apokea hati za utambulisho wa Mabalozi wa nchi sita

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 08 Februari, 2017 amepokea hati za utambulisho za Mabalozi 6 kutoka nchi mbalimbali walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi wote wana makazi yao hapa Jijini Dar es Salaam na wamekabidhi hati zao za utambulisho kwa Mhe. Rais Magufuli Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Mabalozi hao ni Balozi wa Ufalme wa Kiarabu wa Saudi Arabia Mhe. Mohamed Ben Mansour Al Malek, Balozi wa Ufalme wa Morocco Mhe. Abdelilah Benryane, Balozi wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Benson Keith Chali, Balozi wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo, Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mhe. Mousa Farhang na Balozi wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Gervais Abayeho.

Pamoja na kupokea hati zao za utambulisho Mhe. Rais Magufuli amewakaribisha Mabalozi hao hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi zao katika nyanja mbalimbali hasa uchumi kwa manufaa ya pande zote.

“Mhe. Balozi najua kuwa Saudi Arabia imekuwa ikishirikiana na Tanzania kutekeleza miradi mingi ya ujenzi wa miundombinu na bado kuna miradi mingi tutashirikiana, naomba umfikishie salamu zangu nyingi Mhe. Mfalme wa Saudi Arabia kuwa tutaendelea kushirikiana” amesema Mhe. Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Mhe. Balozi Mohamed Ben Mansour Al Malek.

“Nitafurahi sana kuona Cuba inakuja kujenga viwanda vingi vya kuzalisha dawa hapa Tanzania, tunataka kuondokana na uagizaji wa dawa kutoka nje ya nchi ili kupunguza gharama kubwa ambazo Serikali inabeba kwa sasa kwa kuagiza dawa kutoka nje” Mhe. Rais Magufuli amemueleza Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Lucas Domingo Hernandez Polledo.

Balozi wa Morocco hapa nchini Mhe. Abdelilah Benryane amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na mambo mengine ambayo nchi hiyo inaendelea kushirikiana na Tanzania tayari imeanza mchakato wa kutekeleza ahadi ya Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI ya kujenga uwanja wa mpira Mjini Dodoma.

Akizungumza na Balozi wa Zambia hapa nchini Mhe. Benson Keith Chali Mhe. Rais Magufuli amesema anatarajia ujio wake pamoja na mambo mengine utasaidia kuharakisha mchakato wa kuimarisha utendaji kazi na ufanisi wa reli ya TAZARA na bomba la mafuta la TAZAMA kwa manufaa ya nchi hizi mbili.

Kwa Balozi wa Burundi hapa nchini Mhe. Gervais Abayeho, Mhe. Rais Magufuli amemhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na nchi hiyo kama ndugu na marafiki wa kihistoria na kwamba anaamini kuwa juhudi zinazoendelea kufanywa na Mpatanishi wa Mgogoro wa kisiasa nchini humo Mhe. Benjamin William Mkapa ambaye ni Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu nchini Tanzania zitazaa matunda.

Mabalozi wote wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa hatua anazochukua kujenga uchumi wa Tanzania, kukabiliana na rushwa, matumizi mabaya ya madaraka na kusimamia uwajibikaji wa viongozi na watumishi wa umma.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

08 Februari, 2017

Makonda azijibu tuhuma zilizotolewa na Wema Sepetu kuhusu Masogange

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya.

Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, “Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia kama vile unajitahidi kuhama.”

“Hebu wewe kama una taarifa za mitandao sahihi tuambie tu, ndio maana nimesema tunapokea kwa wenyeviti wa mitaa, tunapokea wapi, wewe kama una taarifa sahihi wewe tuambie tu. Lakini usiibue taarifa kwa sababu wewe una jambo la kujibu ukaibua taarifa nyingine tena siyo rasmi, tena nimeeleza hapa ukiwa kwenye mahabusu au popote pale chini ya usimamizi hata simu huruhusiwi kuwa nayo,” ameongeza.

“Kwahiyo bado vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kucheki pia utaratibu gani uliotumika kwa mtu kujirekodi na kuanza kutoa matangazo wakati upo sehemu sahihi ya kutoa hizo taarifa.”

Majina 65 ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya yametajwa kwenye orodha ya awamu ya pili yakiwemo majina makubwa nchini Freeman Aikaely Mbowe, Yusuf Manji, Mchungaji Josephat Gwajima, Iddi Azan na Hussein Pambakali.

Kamanda Sirro Kaeleza Kinachoendelea Baada ya Kumkamata Tundu Lissu

$
0
0
Kamanda wa kanda maalumu ya Dsm,Kamanda Sirro amewaambia waandishi wa habari kuwa bado wanaendelea kumshikilia Tundu Lissu katika  kituo kikuu cha Polisi ikiwa ni siku ya tatu bila dhamana.

Lengo la kuendelea kumshikilia ni kuendelea kufanya upelelezi wa matamshi yake na kujihakikishia pasi na shaka kuwa Tundu Lissu ana kesi ya kujibu.

Hadi pale upelelezi huo utakapokamilika,basi Tundu Lissu atafikishwa mahakamani. 

==>Msikilize hapo chini akiongea

Makonda Aitwa Bungeni Kujieleza......Ni Baada ya Kutoa Kauli za Dharau Dhidi ya Bunge

$
0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limewaita mbele ya Kamati yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kudharau Bunge.

Maamuzi hayo ni sehemu ya maazimio manne ya  Bunge yaliyopishwa usiku huu dhidi ya viongo wanaoteuliwa na Rais hasa wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo azimio lingine ni kumtaka Waziri wa TAMISEMI kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutoingilia majukumu yasiyo yao.

Hatua hiyo inafuatia hoja iliyotolewa bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.

Pia Mwita amedai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wkuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.

Baada ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge, wabunge wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto Kabwe, Saed Kubenea na Joseph Musukuma wamepata fursa ya kuchangia ambapo kwa kiasi kikubwa wote wameoneshwa kukerwa na  kauli hiyo inayodaiwa kutolewa na Paul Makonda, pamoja na utaratibu wa wabunge kukamatwa bila utaratibu.

Wakati mbunge Zitto Kabwe akipendekeza kuitwa mbele ya kamati viongozi waliotuhumiwa, Ester Bulaya amepasua jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho aliodai umetoka kwa kiongozi mmoja aliyeteuliwa na Rais.

Akichangia mjadala huo, Waziri anayehusika na Bunge pamoja na sera Mh. Jenista Mhagama amewataka wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa yanayofanywa na viongozi aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ana majukumu yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wao, hivyo kama kuna RC au DC anakwenda kinyume na sheria au kuingilia Bunge, anapaswa kuwajibishwa mwenye.

Baada ya mjadala huo, Chenge amewahoji wabunge wanaokubaliana na mapendekezo ya mtoa hoja, ambapo wabunge wote wameitikia kuunga mkono mapendekezo hayo manne na kuwa maazimio rasmi ya Bunge.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya February 9

Rais Magufuli AMTUMBUA Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha)....Ni Baada ya Jana Kufanya Ziara ya Kushtukiza

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana  tarehe 08 Februari, 2017 alifanya ziara ya kushtukiza katika mradi wa ujenzi wa jengo jipya la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam (Terminal 3) na kuagiza shughuli za ujenzi wa uwanja huo ziendelee kuanzia  leo.

Awali Mkandarasi anayejenga uwanja huo ambaye ni kampuni ya BAM International alitangaza kusitisha ujenzi kuanzia jana kutokana na kutolipwa madai yake na Mhe. Rais Magufuli ameahidi kulipa fedha hizo haraka.

Hata hivyo, Mhe. Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa kwake na namna mradi huo unavyotekelezwa ikiwemo Serikali kukubali gharama kubwa za mradi ambazo ni Shilingi Bilioni 560 kiwango ambacho ni kikubwa ikilinganishwa na jengo linalojengwa.

“Hivi kulikuwa na sababu gani za nyinyi wataalamu wa Serikali kukubali gharama kubwa namna hii, hivi hili jengo linafanana na Bilioni 560?

“Halafu mlikuwa na haraka gani kuidhinisha kuanza awamu ya pili ya ujenzi kabla ya kumaliza awamu ya kwanza?” amehoji Mhe. Rais Magufuli alipokuwa akiwauliza Wahandisi wa Wizara ya Ujenzi wanaosimamia ujenzi huo.

Kufuatia hali hiyo, Mhe. Rais Magufuli amemuagiza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof. Makame Mbarawa Mnyaa aliyeongozana nae kuunda timu ya wataalamu watakaofanya tathimini ya utekelezaji wa mradi huo ikiwa ni pamoja na kuzungumza na Mkandarasi anayejenga uwanja huo na Mhandisi Mshauri ambao wamekubali kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

“Serikali italipa fedha ambazo Wakandarasi wanadai lakini, nataka Waziri uunde timu ya kufanya tathmini upya, ni lazima hii gharama ipungue, hatuwezi kumaliza fedha zote hizi wakati jengo halifanani na thamani hiyo” alisisitiza Dkt. Magufuli.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli ambaye ameonesha kutofurahishwa na dosari zilizoanza kujitokeza katika baadhi ya maeneo ya jengo hilo, amemuagiza Mhe. Waziri Mbarawa kuunda upya timu ya Wahandisi watakaosimamia mradi huo na ambao watafanya kazi kwa uzalendo na kusimamia ubora.

Kabla ya kuondoka uwanjani hapo Mhe. Rais Magufuli alikutana na wafanyakazi walioajiriwa katika shughuli za ujenzi wa uwanja huo na kuwahakikishia kuwa Serikali imechukua za kuhakikisha mradi huo unaendelea na kwamba kuanzia leo  wataendelea na kazi kama kawaida.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemsimamisha kazi Kaimu Katibu wa Tume ya Mipango (Wizara ya Fedha)Bi. Frolence Mwanri aliyeidhinisha kuanza kwa awamu ya pili ya ujenzi wa jengo hilo jipya la Uwanja wa Ndege kabla ya kumalizika kwa awamu ya kwanza ili kupisha uchunguzi.

Mhe. Dkt. Magufuli ameviagiza vyombo vinavyohusika kufanya uchunguzi katika mradi huo.

Kauli ya Freeman Mbowe Baada ya Makonda Kumtaja kwenye Orodha ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya

$
0
0
Muda mfupi baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuwaita polisi kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali, baadhi ya walioitwa wamelaani hatua hiyo wakisema inalenga kuwachafulia majina na heshima mbele ya jamii.

Miongoni mwa waliotwa ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ambaye amezungumza na kueleza kutofurahishwa na hatua hiyo.

Mbowe aliyekuwa safarini kwenda bungeni Dodoma, alisema ameshangazwa kutuhumiwa kwa jambo asilolijua.

“Kama amemtaja mbunge wa Hai anajulikana ni mmoja, hata kama asingesema Freeman, Mbunge wa Hai anajulikana ni Freeman Mbowe.

“The only thing (kitu pekee) ninaweza kusema nchi haiendeshwi hivyo. Yametajwa majina mengi ambayo sijui Makonda ana evidence (ushahidi) gani!

“Anasema tukiwaita tukiridhika na maelezo yao tutawaachia. Huwezi kusema tu, yaani kwa kusema ni Mbowe... mimi ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, mimi ni mbunge, mimi ni mzazi, nina wanachama, maaskofu, mapadri, mashehe na viongozi mbalimbali.

“Unapokuwa unamhusisha kiongozi na ‘drug trafficking au drug business’ (usafirishaji wa dawa au biashara ya dawa za kulevya), sijui ana ushahidi gani hadi akanihusisha na jambo hilo, mimi sielewi, kwa hivyo siwezi kusema kwa kitu ambacho sielewi,” alisisitiza Mbowe.

Mbowe aliendelea kusema kuwa kesi za dawa za kulevya hazina dhamana, hivyo alimtaka Makonda awe na ushahidi wa kutosha anapowataja watuhumiwa.

“Tuache habari ya kuitwa, wewe umepata tuhuma, hujafanya uchunguzi, hakuna mtu aliye juu ya sheria, lakini unatakiwa kufanya uchunguzi ili ukimkamata mtu unamshtaki, siyo unataja mtu unachafua hadhi yake. Halafu ukija kusema hatuna ushahidi juu yako umeshaharibu jina lake,” alisema na kuongeza:

“Mimi sijui kama jeshi la polisi linafanya kazi hii au ni Makonda amejipa kazi ya kuwa mpelelezi. Au labda yeye kwa kuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ndiyo amejipa kazi ya kutaja majina kwenye mambo yenye kashfa kama haya? Sielewi. This is very wrong precedence (Hii ni rejea mbaya) kwa utawala wa sheria.”

Mbowe alisema inawezekana ni mikakati ya Serikali kuendelea kukandamiza upinzani kwa kuwakamata viongozi wake.

“Sijui kama kuna watu wanaolengwa, lakini tumeona viongozi wetu wanakamatwa hawapewi dhamana, (Tundu) Lissu amekamatwa, (Godbless) Lema amekamatwa ... mtu anakaa miezi minne, kwa hiyo wanaweza kufanya lolote. Inawezekana ni mkakati wa kutesa wapinzani. Wamenitafuta kwenye biashara wameona haitoshi... sina uhakika lakini sioni kama wana nia njema na sisi,” alisema Mbowe.

Alipoulizwa kama ataitikia wito wa Makonda, Mbowe alisema bado anawasiliana na wanasheria wake kabla ya kuchukua hatua.

Tundu Lissu Kagoma Kula Hadi Polisi Wamfikishe Mahakamani

$
0
0
Wakati Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akigoma kula hadi afikishwe mahakamani, wakili wake amepeleka maombi Mahakama Kuu kuomba apewe dhamana baada ya polisi kuendelea kumshikilia kwa siku ya tatu.

Wakili wa mbunge huyo, Peter Kibatala alisema mteja wake amefikia hatua hiyo, baada ya Jeshi la Polisi linalomshikilia kumnyima dhamana bila sababu.

“Hakuna sababu za msingi za kumnyima dhamana na tangu jana Lissu hajala na amesema hatakula hadi afikishwe mahakamani,” alisema Kibatala na kuongeza:

“Kosa analodaiwa kulifanya lilifanyika Januari 4 na hadi Februari 6 ni mwezi, kama ni muda wa kuchunguza kosa hata hati ya mashtaka ingekuwa tayari,” alisema Kibatala.

Alisema mteja wao (Lissu) analalamikia kuanzia ukamatwaji wake ulipoanza, alipokamatwa eneo la Bunge bila Spika kuwa na taarifa.

Kibatala alisema polisi waliokwenda kumkamata aliwatambua njiani na alikamatwa bila kuwapo kibali cha kukamata (arrest warrant).

Yusuf Manji kawasili Polisi Leo badala ya Kesho Kuitikia Wito wa Makonda

$
0
0
Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.

Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.

Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.

Manji amewasili na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi huku akiwa na mawakili wake kadhaa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images