Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sakata la Madawa ya Kulevya: Wema Sepetu Kawatoa Hofu Mashabiki Wake

$
0
0
Mwigizaji wa Tanzania Wema Sepetu ambaye mwishoni mwa wiki iliyopita alifika kwenye kituo kikuu cha Polisi kati Dar es salaam baada ya kutajwa kwenye orodha ya wanaotuhumiwa kufanya  biashara ya dawa za kulevya, amewatoa hofu Mashabiki zake.

Wema amesikika kwenye sauti aliyoiweka kwenye mitandao akisema: 'Nadhani natakiwa kusema kitu sababu najua nina mashabiki, nina watu wananipenda na kunifatilia…. nina watu wanani-support, nina watu wana hofu kuhusu mimi.

"Nina watu ambao wananijali sana na nina uhakika yani wana wasiwasi sana lakini nataka tu niwaambia kwamba msiwe na wasiwasi"

==>Msikilize hapo chini

Kampuni ya Mo Dewji, Lamada Hotel ni mdaiwa sugu wa kodi.....maofisa Ardhi wavamia ofisi, Watoa Notisi ya Siku 14

$
0
0
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeanza oparesheni maalumu ya kukusanya Kodi ya Pango la Ardhi kutoka kwa wadaiwa sugu wa Makampuni, mashirika ya kiserikali na watu binafsi kwa kuwafuata katika maeneo yao.

Katika hatua ya kwanza Wizara kwa kushirikiana na Manispaa za  mkoa wa Dar es salaam imetoa notisi kwa wadaiwa sugu wa kodi ya pango la Ardhi wakiwemo Mohammed Enterprises anaedaiwa Shilingi milioni 73, Lamada  Hotel anaedaiwa Shilingi milioni 54, Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) anaedaiwa Shilingi milioni 144 na Tanganyika Motors anaedaiwa Shilingi milioni 22.

Makampuni hayo yamepewa notisi ya siku 14 ili kulipa kodi hizo wanazodaiwa na endapo hawatalipa watafutiwa umiliki au mali zao kwa kupigwa mnada ili kufidia gharama wanazo daiwa.

Serikali kwa kutumia kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment imeendesha oparesheni hiyo kwa kufika katika ofisi za wamiliki wa viwanja na mashamba makubwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Akiongea kwa kusisitiza, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Wizara imepanga kukusanya Sh. bilioni 111.77 kutokana na Kodi ya Pango la Ardhi.

Wizara haitaweza kufanikisha malengo hayo endapo itaendelea kuwaachia wadaiwa sugu ambao hawataki kulipa kodi. Kwani kwa miaka mingi sasa mapato mengi ya serikali yamekuwa yakiachwa kutokana na kushindwa kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi Kayandabila alisisitiza.

Baadhi ya watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment na baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa nje ya Ofisi ya Mohammed Enterprises iliyopo jingo la Golden Jubilee mara baada ya wafanyakazi wa Mohammed Enterprises kukimbia.

Wafanyakazi wa Lamada Hotel (kushoto) wakiangalia kwa makini Notisi ya madai ya kodi ya Ardhi wakati ikiwasilishwa na watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment.

Watumishi kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kushirikiana na kampuni ya Udalali ya Msolopa Investment wakiwa nje ya ofisi Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje (EPZA) ili kuwasilisha notisi ya madai ya kodi ya ardhi. 

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Yamungu Kayandabila akiongea na waandishi wa habari kwamba Serikali kupitia Wizara yake haitamuacha mtu au kampuni yoyote inayodaiwa kodi ya Ardhi hata kama ni Taasisi ya serikali.

Hassan I. Mabuye
Information Officer
The Ministry of Lands, Housing
and Human Settlements Development

Dar es salaam, Tanzania

Rais Trump Apata Pigo.....Mahakama Yatengua Amri Yake

$
0
0
Jaji mmoja wa Marekani amesimamisha kwa muda utekelezaji wa amri ya Rais Donald Trump ya kuwazuia raia kutoka mataifa saba, yaliyo na raia wengi wa imani ya Kiislamu kuingia nchini Marekani.

Jaji wa Seattle alipuuzilia mbali sababu zilizotolewa na mawakili wa Serikali na kusema kuwa amri hiyo inaweza kusimamishwa mara moja huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa mahakamani.

Serikali inatarajiwa kukata rufaa ya dharura dhidi ya uamuzi huo wa mahakama, ambao ni changa moto kubwa kwa utawala wa Trump.

Serikali ya Marekani inasema kuwa makumi ya maelfu ya visa zimefutiliwa mbali tangu rais Trump kutia sahihi amri ya kupunguza idadi ya watu wanaopaswa kuingia nchini Marekani juma lililopita.

Kutokana na hatua hiyo, Idara ya Forodha ya Marekani imeyaambia mashirika ya ndege kwamba waruhusu abiria kupanda ndege kuelekea Marekani abiria ambao walinyimwa ruhusa baada ya Rais Trump kutoa amri kwamba watu kutoka nchi saba zenye Waislamu wengi, wakataliwe kuingia Marekani.

Wakati huohuo waziri Mkuu wa zamani wa Norway, Kjell Magne Bondovik, alisema kuwa alizuiwa katika uwanja mmoja wa ndege mapema juma hili, katika tukio alilosema ni la uchokozi, kwa sababu eti alikuwa na visa ya Iran katika paspoti yake.

Waziri Nape aingilia kati sakata la wasanii wanaotuhumiwa kwa Madawa ya Kulevya......Ataka Busara Itumike

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameingilia kati na kutaka busara itumike katika zoezi la kutaja wasanii wanaohusika na dawa za kulevya linalofanywa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda

Nape ametoa ushauri huo leo Mjini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu sheria mpya wa huduma za habari, ikiwa ni siku nne tangu mkuu huyo wa mkoa aanze kutaja wahusika wa dawa za kulevya wakiwemo wasanii wa bongo fleva na filamu.

Baadhi ya waliotajwa na kutakiwa kuripoti polisi kwa mahojiano ni pamoja na Vanessa Mdee, Wema Sepetu, Nyandu Toz, Chidi Benz, TID, Tunda, Babuu wa Kitaa n.k

Nape baada ya kuulizwa swali na wanahabari kuhusu suala hilo amesema kuwa wizara yake inakiri kuwa tatizo hilo ni kubwa, na ilifikia hatua ya kuwasaidia baadhi ya wasanii kwenda kupata matibabu akiwemo msanii Ray C na kwamba wanaunga mkono jitihada zozote za kupambana na tatizo hilo.

Amesema tatizo lipo kwenye namna ya kuwaadhibu wanaogundulika kutumia dawa za kulevya, kwa maana ya sheria ipi itumike kuwashitaki, lakini pia tatizo lingine ni busara inayotumika kuwataja na kuwakamata watu ambao tayari wamekwisha athirika na dawa kulevya badala ya kuwasaidia.

Kwa mtazamo wake nape amesema hilo ni tatizo la jamii nzima, na kushauri jamii yote ya watanzania kushiriki katika kujenga maadili ya watoto.

Profesa Lipumba Akanusha Kuwa 'Kibaraka' wa Serikali

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba amekanusha tuhuma za kuwa na ukaribu unaotia shaka kati yake na serikali na kutolea ufafanuzi ishu mbalimbali zinazoashiria ukaribu huo ikiwemo ya kuchepusha ruzuku ya chama.

Mwenyekiti huyo anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa amesema kinachodaiwa kuwa ni ukaribu wake na serikali, siyo sahihi kwa kuwa yeye huwa anaalikwa tu kwenye matukio mbalimbali ya kitaifa ambayo hawezi kukataa mwaliko.

"Kwa mfano ukikaribishwa kwenye shughuli ya serikai, labda Rais anazindua kitu, au sherehe za kitaifa na Rais yupo utakataaje" Amesema Lipumba.

RUZUKU
Suala la ruzuku ya chama hicho kuchepushwa pia ni jambo linalodaiwa kuwa ushahdi wa Prof Lipumba kuwa karibu zaidi na serikali, ambapo amesema ilikuwa ni lazima iwe hivyo kutokana na uamuzi wake kama Mwenyekiti wa chama wa kutengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Fedha, ambaye ndiye aliyekuwa mtia sahihi katika masuala ya fedha.

Pia sababu nyingine ya kuchepusha fedha za ruzuku amesema ni mahitaji ya chama kwa kuwa kilikuwa kinaingia kwenye uchaguzi hivyo kilihitaji fedha kwa ajili ya shighuli mbalimbali.

" Kuhusu ruzuku, nilikuwa nimetengua uteuzi wa mkurugenzi wa fedha, bwana Bashange, kwahiyo hakuwa tena signatory wetu, kwa nafasi yangu kama mwenyekiti niliona hafai, tukajitahidi kufungua akaunti nyingine lakini haikuwezekana. Ikabidi Naibu Katibu Mkuu ambaye ndiye anayeshika nafasi ya Katibu Mkuu anapokuwa hayupo ofisini, aandike barua ya kuomba ruzuku kwa ajili ya mahitaji tuliyokuwa nayo" Ameeleza Lipumba

Lipumba ameendelea kusema "Tukapeleka taarifa kuomba ruzuku. Kwahiyo Naibu Katibu Mkuu akaandika barua kwenda kwa Msajili kuwa tunaomba ruzuku na ipitie kwenye akaunti nyingine, na hilo likafanyika"

MIKUTANO
Kuhusu yeye kuruhusiwa kufanya ikutano, huku Katibu Mkuu wake akizuiliwa, hususani tukio lililotokea mkoani Mtwara, Lipumba amesema hata yeye alipokwenda Mtwara hakuruhusiwa kufanya kilichokuwa kimempeleka, na badala yake aliishia kufanya mikutano ya ndani, huku akibainisha kuwa kilichomkwamisha Maalim Seif ni kwenda bila kutoa taarifa kwa kiongozi wa wilaya.

"Nimekwenda Mtwara, nilikaribishwa na viiongozi wa wilaya, kazi yangu ilikuwa ni kufungua matawi, lakini polisi wakanizuia kuwa sitakiwi kufanya mikutano ya nje, nikafanya mikutano ya ndani...Lakini Maalim Seif alikwenda bila kumtaarifu kiongozi wa wilaya". Amesema

ULINZI
Lipumba aliyekuwa katika mahojiano na kituo kimoja cha TV, amekanusha taarifa za kupewa ulinzi na serikali na kufafanua tukio la kupigiwa saluti na askari, akisema kuwa siku hiyo hakupigiwa yeye saluti bali diwani wa eneo ambalo yeye alishiriki kufanya usafi.

"Pale Buguruni, tulikuwa katika usafi, na tulikuwa na diwani wa eneo lile, askari walikuwa wakiangalia usalama, na alipotokea diwani wa eneo lile, askari walimpigia yeye kwa kuwa ndiye mkuu wa eneo lile, siyo mimi"

Kitendo kilichodaiwa kuwa ni askari kumpigia saluti Prof Lipumba

Katika hatua nyingine, amesema anaendelea kumtambua Maalim Seif kama Katibu Mkuu halali wa CUF,  huku akimtaka amfuate ili wamalize tofauti zao na kufanya kazi kwa pamoja.

Kauli ya Vanessa Mdee Baada ya Kutajwa na RC Makonda Kwenye Listi ya Wahusika wa Madawa ya Kulevya

$
0
0
Iliwashangaza wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na biashara ya madawa ya kulevya. 

Ni shutuma nzito, na hata kabla uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza kuonekana katika maisha yao.

Wito huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot tamthilia ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na kurudi Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya kesho.

Pamoja na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha yaendelee kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na katika ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress from @asos #FILA.

Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”

Kwenye picha hizo amezima comments ili kuepuka maneno ya kejeli kutoka kwa baadhi ya watu ambao tayari wamefanya hivyo kwenye picha zingine. Vee anaungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Wema Sepetu, Mr Blue, TID na wengine kwenye orodha hiyo.

Serikali yatangaza ‘Diploma’ ndiyo kigezo cha chini cha elimu kwa waandishi wa habari

$
0
0
 
Serikali imetangaza kuwa kiwango cha chini cha taaluma anayopaswa kuwa nayo mwandishi wa habri kuwa ni 'Diploma ya Uandishi wa Habari' kwa mujibu wa kanuni za sheria mpya ya hunda za habari zilizokamilika utungaji wake hivi karibuni.

Akizungumza na wana habari leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo , Nape Nnauye amesema kuwa kanuni zimeshaundwa na zimechapishwa kwenye gazeti la serikali tangu Februari 3 mwaka huu baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali.

"Tumesoma, tumechambua maoni ya wengi, wapo waliotaka iwe cheti, wengine diploma, wengine digrii, wapo waliotaka PhD na wapo waliotaka iwe mtu yeyote nayejua tu kusoma na kuandika. Serikali imesimama katikati ya maoni hayo. Sifa ya chini kabisa kwa kuanzia itakuwa ni diploma ya uandishi wa habari” Amesema Nape

Waziri Nape amesema pia kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika tangu Desemba 31 mwaka 2016, ambapo yeye kama Waziri mwenye dhamana alishatoa tangazo katika gazeti la serikali.

Aidha kuhusu wasio na sifa hiyo, Waziri Nape amesema kuwa serikali imetoa kipindi cha mpito cha miaka mitano ili waandishi wasiokuwa na sifa hiyo, waliopo sasa na watakaoingia kwenye taaluma hiyo, wakasome ili wawe wamepata sifa hiyo.

Amesema katika utekelezaji wa sheria hiyo, kuna taasisi ambazo tayari zipo, zitaongezewa majukumu au kazi zake kuhuishwa, pia kuna vyombo vipya vitaanzishwa na kuna taratibu mpya za kiutendaji zitaandaliwa.

Kuhusu manufaa ya sheria hiyo, Nape amesema kuanza kutumika kwa sheria hiyo ni jambo muhimu kwa tasnia hiyo kwa kuwa ni ruhusa ya kuanza kwa mchakato wa kuifanya taaluma ya habari kuwa taaluma kamili yenye sifa mahsusi na  maadili yaliyokamilika pamoja na kuwa na vyombo vya kusaidia utekelezaji wake.

Sheria hiyo ilisainiwa na Rais Magufuli Novemba 16 mwaka 2016, na siku mbili baadaye ilichapishwa kwenye gazeti la serikali baada ya muswada wake kupitishwa na Mkutano wa 5 wa bunge mwezi Novemba 2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya February 6


Kinana: Mwisho wa Viongozi Madalali CCM Umewadia

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama  Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana, amesema kwa sasa viongozi madalali  wanaouza viongozi ndani ya chama hicho hawatakiwi, huku akiwataka watafute kazi nyingine za kufanya.

Kutokana na hali hiyo amesema sasa wamejipanga kuhakikisha CCM inaendelea kutawala maisha yote huku akiwataka wenyeviti wa kata, wilaya na mikoa kutokuwa  sehemu ya malalamiko na badala yake wawe sehemu ya kusimamia Serikali kama anavyofanya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dk.  John Magufuli.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya miaka 40 ya CCM yaliyofanyika katika ukumbi wa Dodoma Convention Centre, ambao unamilikiwa na chama hicho, ambapo Kinana awalitaka viongozi wa chama hicho kuacha kuwa walalamikaji na badala yake wawe sehemu ya kuisimamia Serikali katika kutimiza wajibu wake.

“Sasa hatutaki kuwa na viongozi madalali ndani ya chama, kwa hiyo kama wapo wajitafakari wenyewe. Ndiyo maana hata sisi tumekubaliana maadhimisho sio sherehe lazima tuachane na tabia za sherehe ukisema sherehe itabidi pia mlipane na posho jambo ambalo halikubaliki,’’ alisema Kinana.

Akielezea sababu za kuendelea kushinda kwa chama hicho katika chaguzi mbalimbali, Kinana alisema wamekuwa wakisimamia na kupigania haki za wananchi huku akidai kwa sasa kuna viongozi wamekuwa madalali ndani ya chama hicho.

“CCM ni chama chenye nguvu wana CCM wamekuwa wamoja na hiyo ndiyo imetufanya tumekuwa tukiendelea kuaminiwa na wananchi na sababu zipo wazi ni kusimamia na kupigania haki zao hakuna mwenye kauli wana CCM wanamuunganiko.

“Sababu nyingine ya kuendelea kuaminiwa ni uwepo wa demokrasia pana na yenye kina kwa kila mwanachama kuwa na uhuru wa mawazo kwa kusema na hata kushauri.

“Wanaoamua ndani ya chama ni wanachama wakisema ndiyo ni ndiyo na wakisema hapana ni hapana katika uchaguzi mwanachama ana haki ya kuchagua na ana uhuru wa kuchukua fomu na kugombea,’’ alisema Kinana.

Alisema kwa sasa vipo vyama vitatu pekee duniani ambavyo vinaoongoza kwa maandiko mazuri na yenye tija  ambapo alivitaja vyama hivyo kuwa ni Chama cha Kikomunisti cha China, CCM na ANC cha Afrika Kusini.

Kinana  alisema mwaka 2015 chama hicho kilifanya tathmini kwa miezi 12 kuanzia katika shina mpaka taifa lengo likiwa ni kupunguza urasimu na umangimeza, ambayo iliwasaidia kujua upungufu na marekebisho wanayotakiwa kufanywa.

Kuhusu suala la Serikali kuhamia Dodoma, alisema Serikali inatakiwa iungwe mkono japo alikiri kwamba mwanzo utakuwa mgumu.

Pia aliwataka wanachama wa chama hicho kuchagua viongozi wenye kazi zao katika uchaguzi mbalimbali utakaofanyika.

“Muwachague viongozi bora waadilifu wenye shughuli zao zisizotokana na CCM awe na shughuli ya kufanya,’ ’alisema.

Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula, alisema CCM kimehusika kwa asilimia kubwa katika kuleta amani na utulivu nchini huku akiponda vyama vingine kuhusika na maandamano kila kukicha.

“Hivi vingine ni vyama vya maandamano tu, amani na utulivu imeletwa na CCM kumbukeni zamani tulikuwa tunasema chuo kikuu sasa hivi tunasema vyuo vikuu  Udom pekee wanamaliza wanafunzi 36,000,’’ alisema Mangula.

Maadhimisho ya miaka 40 kwa mwaka huu yamekuwa ya aina yake ambapo yamehudhuriwa na wabunge wote wa chama hicho, wakiwamo mawaziri wakuu wastaafu, John Malecela na Mizengo Pinda pamoja na Spika wa Bunge, Job Ndugai.

Tanzania na Malawi zasaini kushrikiana katika mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga

$
0
0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Kikao cha Tume ya Kudumu ya Pamoja ya Ushirikiano (JPCC) kati ya Tanzania na Malawi kimeweka mazingira mazuri ya kushughulikia mgogoro wa mpaka katika Ziwa Nyasa ambapo juhudi za kutafuta suluhu zilisimama kutokana na mabadiliko ya uongozi nchini Malawi.
 
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt, Augustine Mahiga (Mb) wakati alipokuwa anasoma hotuba ya kufunga kikao hicho jijini Lilongwe siku ya Jumapili tarehe 05 Februari 2017.
 
Mhe. Waziri alieleza kuwa kikao hicho kimefanyika kufuatia maelekezo ya Waheshimiwa Marais wa Tanzania na Malawi ambao walifanya mazungumzo walipokuwa Ethiopia katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Umoja wa Afrika na kutoa wito kwa jopo la viongozi wa zamani wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) kuongeza kasi ya kutafuta suluhu ya mgogoro huo. 

Jopo la viongozi wa zamani wa SADC lililopewa dhamana ya kushughulikia suala hilo linaundwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais wa zamani wa Msumbiji; Mhe. Thabo Mbeki, Rais wa zamani wa Afrika Kusini na Mhe. Festus Mogae, Rais wa zamani wa Botswana.
 
Waziri Mahiga alieleza kuwa japo Tanzania na Malawi zinatofautiana katika mpaka wa Ziwa Nyasa lakini tofauti hizo sio kikwazo kwa nchi hizo kushirikiana katika maeneo mbalimbali kwa ajili ya faida ya wananchi wa pande zote mbili.
 
Alisema kikao hicho cha JPCC kinatoa fursa kwa pande mbili kujadili na kukubaliana maeneo mbalimbali ya ushirikiano na kuweka utaratibu wa utekelezaji.
 
Aidha, katika kikao cha JPCC, wajumbe wanakitumia kubuni mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji wa maeneo ya ushirikiano yaliyoafikiwa.
 
“Nafurahi kusikia mmejadili na kukubaliana maeneo mengi ya ushirikiano ikiwemo biashara, kilimo, utalii, tehama, utangazaji, utunzaji wa mazingira na usafiri wa anga”. “Ni jambo la kupongezwa katika majadiliano yenu pia mmependekeza iundwe Kamati ya Makatibu Wakuu ambayo itakuwa inakutana kila baada ya miezi sita ili kutathmini utekelezaji wa maeneo yaliyoafikiwa kwa mujibu wa muda uliokadiriwa”.
 
Mhe. Mahiga alitoa maelezo namna Serikali ya Awamu ya Tano inavyoboresha miuondombinu ya Bandari ya Dar Es Salaam, barabara na mipango ya kuboresha Reli ya TAZARA kwa kushirikiana na China ili Malawi iweze kusafirisha bidhaa zake kwa urahisi.
 
“Ni jukumu letu na pia ni wajibu wa kimataifa kuzihudumia nchi zisizokuwa na bandari. Hivyo, Tanzania ambayo imezungukwa na nchi nane zisizokuwa na bandari itaboresha miundombinu ili nchi hizo ziweze kusafirisha bidhaa zao bila usumbufu wowote.
 
Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Malawi, Mhe. Francis Kasaila alisisitiza umuhimu wa kuimarisha miundombinu ya bandari, barabra na reli ili Serikali ya Malawi na wafanyabiashara waweze kusafirisha bidhaa kwa urahisi. 

Alisema ili vituo vya mizigo vya Malawi vilivyopo Dar es Salaam na Mbeya vifanye kazi kwa ufanisi hakuna budi kuboresha Bandari ya Dar es Salaam, Reli ya TAZARA, barabara ya Dar es Salaam hadi Mbeya na kujenga Kituo cha Pamoja cha kutoa Huduma mpakani.
 
Kikao hicho kilimalizika kwa kushuhudiwa uwekaji saini wa mikataba ya makubaliano katika Mashauriano ya kisiasa na kidiplomasia na usafiri wa anga.
 
Mhe. Waziri kabla ya kurejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu amepangiwa miadi ya kuonana na Rais wa nchi hiyo, Mhe. Prof. Peter Mutharika ambapo amepanga pamoja na mambo mengine kujadili suala la Watanzania wanane wanaoshikiliwa katika gereza kuu la Mzuzu kwa tuhuma za kuingia kinyume cha sheria katika mgodi wa urani wa Kayerekera.
 
Imetolewa na: Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki
Tarehe 06 Februari 2017

Polisi Waingilia Kati Mzozo wa Kanisa la Anglikana.......Wamzuia Askofu Mokiwa Kushiriki Ibada

$
0
0
Polisi  wameingilia kati mvutano ndani ya Kanisa la Anglikana baada ya kumzuia Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam, Dkt. Valentino Mokiwa kushiriki ibada ya kumsimika Askofu mpya wa Dayosisi ya Lweru.
 
Askofu Mokiwa amekuwa katika mvutano na Askofu Mkuu wa Anglikana Tanzania, Dkt. Jacob Chimeledya tangu alipotangaza kumvua  uongozi wa Dayosisi ya Dar es Salaam, akidai mkuu huyo hakufuata utaratibu na kwamba hana mamlaka ya kuchukua uamuzi huo.
 
Aidha Askofu Mokiwa aliwasili makao makuu ya Dayosisi ya Lweru mjini Muleba mkoani Kagera na alitarajiwa kuungana na maaskofu wengine kumsimika Godfrey Mbelwa kuwa askofu mpya wa dayosisi hiyo.
 
Lakini taarifa zilizopatikana  zimesema Askofu Mokiwa alichukuliwa na polisi na kuhojiwa katika kituo cha Muleba, kutokana na kuhofu kuwa kuwapo kwake kungeweza kusababisha vurugu katika ibada iliyokuwa iongozwe na Dkt. Chimeledya kutokana na mvutano uliopo.
 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera Augustino Ollomi,amesema kuwa jeshi hilo halikumkamata Askofu Mokiwa na kumhoji, badala yake amesema walichukua hatua haraka baada ya kupata taarifa za kiintelijensia kuhusu masuala ya usalama.
 
“Ni wajibu wetu kufuatilia, tulimuonya kuhusu suala la kuhudhuria ibaada kwa sababu kulikuwa na viashiria vya uvunjifu wa amani lakini ilikuwa ni hiari yake kutohudhuria, huo utakuwa ni uamuzi wake,” amesema Ollomi.
 
Kamanda Ollomi amesema walimuita Askofu Mokiwa juzi saa moja usiku kwa ajili ya kumpa ushauri wa kutohudhuria sherehe hizo kwa kuwa mgogoro uliopo katika kanisa hilo ungeweza kusababisha uvunjifu wa amani.

"Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani sakata la madawa ya kulevya" - Rama Dee.

$
0
0
Rama Dee ni mmoja kati ya wasanii bora wa Rnb ambaye mara nyingi amekuwa na misimamo tofauti na wasanii wengi ambao wanafanya aina hiyo ya muziki.

Katika kile ambacho kinaendelea juu ya sakata la madawa ya kulevya, Rama Dee ameingia katika kundi la wasanii wachache ambao wameweka mitazamo yao hadharani juu ya ukamataji wa wasanii na kuwekwa ndani.

Rama Dee amesema “Mimi kama msanii,Siungi mkono wasanii kuwekwa ndani Ila ninge muunga mkono Kama angeweza kuziba mirija ya Wauzaji Papa kuwafikia wasanii na watanzania kwa ujumla!

"Toka nipo mdogo wauza unga wanafahamika na majina yao yapo kwenye mitandandao lakini sijawahi ona wakikamatwa wala kuonyeshwa kwenye vyombo vya habari! Hata hao polisi pia sijaona picha zao!

"Wasanii ni watu Kama watu wengine tu…so unapo anza kuaribu biashara zao kwa sababu tu upo na power ya uongozi sidhani kama ni busara! :

"Ushauri wangu kaa na viongozi wenzio ambao walikutangulia kwenye uwongozi uliza why walishindwa then anzia hapo!

"Unajuwa haya mambo unaweza ona ya kawaida Ila yanaweza kuharibu maisha ya watu kuliko hata huwo Unga! Haswa wasanii. :

"Namuunga mkono Nape kuwa kuna njia za kutumia ambazo zinalinda sheria ya mtuhumiwa! Ila ukitumia nguvu bila Akili ni sehemu mojawapo ya kuwapatia pesa Wanasheria bila msingi wowote! :

"Kukamata watu kwa kuhisi ni utaratibu mbaya sana! Kumbuka kuna watu wapo na chuki za maendeleo ya watu wengine.Unaweza ukasikia hata Tale anauza unga ambae ni rafiki yako, sijuwi utafanyaje hapo.

"Mimi naona plan yako imeanzia sehemu si sahihi rudi nyuma Anza tena ni hayo tu, halafu hakuna movement nzuri Kama movement ya kutumia power ya wasaniii na jamii kiujumla.

"Fanya kazi yako Mh. makonda waache wasanii watafute mkate wao wa kila siku! Rama Dee!"

Mwisho.

Uporaji wa Kutumia Bunduki Watikisa Jiji la Mbeya

$
0
0
Wamiliki wa maduka, bodaboda na grosali jijini Mbeya wamekumbwa na hofu baada ya kuibuka kwa kundi la watu wanaodaiwa kuwa majambazi ambao wamekuwa wakipora fedha na pikipiki katika maeneo tofauti tangu mwishoni mwa Januari.

Mitaa iliyoonja adha ya wavamizi hao ni ya Mafiati, Mwanjelwa, Mabatini, Soweto na Mabanzini ambako vikundi hicho kilivunja maduka matano.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema wanashikilia watu watatu kuhusiana na matukio hayo.

Kamanda Kidavashari alisema upelelezi wa awali unaonyesha kundi hilo limetokea Tunduma mkoani Songwe na kwamba lilipokewa na wenyeji ambao huwaongoza katika uporaji huo.

‘’Mpaka sasa tunamsaka kijana anayeitwa Frank Senior au Frank Popo wa Mtaa wa Iyela kwa madai ya kuhusika kusaidia uhalifu huo,’’ alisema.

Awali, mwenyekiti wa wa Chama cha Waendesha Bodaboda Kanda ya Soweto, Joseph Patrick alisema hivi karibuni kuna watu walifika eneo hilo saa 3:00 usiku wakawavamia madereva na kuwapora fedha, kisha wakavamia Mtaa wa Block Q walikopora pikipiki mbili.

Aliwataja walioporwa kuwa ni Saimon Nkwandi na Msafiri Jumanne. Patrick alisema waporaji hao pia walimpiga risasi dereva mwingine aliyemtaja kwa jina la Peter Hans baada ya kukataa kuwakabidhi pikipiki.

Mkazi wa Mafiati, Betweli Mwakitabu alidai waporaji hao walivamia grosari zaidi ya tano na kupora fedha kwa wamiliki na wateja. Tukio kama hilo lilitokea pia Mtaa wa Mabanzini.

Mwanza Yatoa Msaada wa Chakula Kwa Kaya 231 Zilizoathiriwa na Mvua

$
0
0
Serikali wilayani Nyamagana Mkoani Mwanza  imetoa msaada wa vyakula kwa watu ambao nyumba zao ziliezuliwa paa na mvua iliyonyesha wiki iliyopita iliyoambatana na upepo. Mvua hiyo iliathiri kaya 231 zenye watu 800 ambao mpaka sasa hawana makazi. 

 Vyakula vilivyogawiwa ni kilo 3,760 za unga na kilo 1,000 za maharagwe vyote vikiwa na thamani ya Sh7.3 milioni. 

Akizungumza baada ya kukabidhi vyakula hivyo kwa nyakati tofauti, mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Marry Tesha alisema msaada huo umetolewa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine. 

Alisema vyakula katika Kata za Mahina waligawa kwa kaya (94), Butimba (64), Nyegezi (61) na Mkuyuni (12). Mkuu huyo wa wilaya aliwataka viongozi wa maeneo hayo kuhakikisha msaada huo unatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Pia, alito wito kwa wananchi kujenga nyumba imara zinazoweza kuhimili mikikimikiki, kwa kuwa nyingi zilizobomoka, hazikuwa imara. 

Ally Juma, ofisa mtendaji wa Kata ya Mahina ambako nyumba za kaya 94 ziliezuliwa, alisema wamiliki wameshindwa kupaua upya kutokana na uduni wa kipato. 

 Ofisa Mtendaji Kata ya Nyegezi, Charles Musa alitoa wito kwa wananchi kupanda miti kwenye makazi yao ili kuepuka madhara yatokanayo na upepo mkali. 

Naye Amina Rashid, ambaye ni muathirika wa mvua hizo anayeishi Mahina, aliiomba Serikali iendelee kuwasaidia kwa sababu madhara waliyoyapata ni makubwa na uwezo wengi ni mdogo. 

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS ni kampuni inayoongoza kwa kutoa bidhaa original za asili zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote pia tunatoa punguzo la bei la %10 kwa ajili ya Xmas and new year pata bidhaa kwetu uweze kufurahia matokeo mazuri kwa bidhaa original.

     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
 
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
 
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @10,000/= vidonge maalum @150,000
 
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @130,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
 
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
 
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @90,000/=
 
12.kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=

     WASILIANA NASI KWA NAMBA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma zetu. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti unapewa ili kuhakikisha mafanikio yako
           Follow us 
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Kutana na Maajabu ya Maalim Hussein .....Anatoa Dawa za Biashara, Dawa za Uzazi, Anasafisha Nyota, Anarudisha Mali Iliyopotea au Kuibiwa

$
0
0
Kutana na Maajabu ya Maalim Hussein Mtaalm wa Tiba Asili na Mtabibu wa nyota za binadamu Africa na dunia nzima.
 
Anatoa TIBA MAENEO YOTE NCHINI, KWA WALE WENYE KUHITAJI TIBA ANATIBU YAFUATAYO,
1.Husafisha NYOTA na kutoa PETE za BAHATI na kwa wale waliosumbuka kwaajili ya matibabu na hawakufanikiwa njoo ujionee muujiza wa papo kwa papo-
 
2. Humpa mtu JINI la  MALI kwa yule anaetaka  KUMILIKI UTAJIRI Bila masharti yoyote.
 
3.Anatibu MAGONJWA yalio SHINDIKANA
 
4.Mpenzi/MUME/MKE Aliekukimbia ANAKURUDISHIA Ndani ya saa 72 tu.
 
5.Pia tunatoa dawa za Nguvu za KIUME na Kurefusha kwa saizi unayo Taka
 
6.Anatoa Dawa za BIASHARA NA MVUTO
 
7.Tunatoa Dawa za Uzazi kwa kina Mama kwa wale wenye Tatizo Sugu
 
8.Anatoa Zindiko ya Nyumba,Mwili, na Mvuto kazini.

9.Tunamaliza kesi zilizo kaa muda Mrefu bila kumalizika.

10.Tung'arisha Nyota na Cheo kazini. 

11.Tunarudisha Mali zilizopotea au Kuibiwa.

12. Humaliza Kabisa Tatizo la  CHUMA ULETE
-Love Spell
-Money Spell Casting
-Traditional Healer
-Protection Rituals
-Marriage Spells( to heal Marriage Problems and restore Affection)
-Traditional bad luck Removal
-To Prevent Devorce and bind lovers together

Whatsapp +255674835107
Call-+255746757102 
 
PIA ANATIBU KWA NJIA YA SIMU UKIWA POPOTE PALE DUNIANI

Ajali Yaua Watu 7 Mkoani Kilimanjaro Wakiwemo Waandishi wa Habari

$
0
0
Watu saba wamekufa na wengine wanne wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo Mwika, mkoani Kilimanjaro. 

Akizungumza jana katika eneo la tukio, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa alisema ajali hiyo ilitokea saa 11. 00 jioni ikilihusisha lori, gari dogo na pikipiki. 

Alisema lori hilo lilikuwa linatoka Rombo kwenda Dar es Salaam, likiwa limepakia ndizi.

“Breki za lori zilishindwa kufanya kazi na ndipo lilipoligonga gari dogo aina ya Toyota Surf lililokuwa likipishana nalo,” alisema. 

Alisema kabla ya kuanguka lori hilo pia liligonga pikipiki na taarifa za awali ni kuwa watu saba walikuwa wamepoteza maisha. 

Alipoulizwa kuhusu taarifa za kina kuhusu majeruhi na waliopoteza maisha, alisema,“Tuko eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia majeruhi ili kuwapeleka katika Hospitali ya KCMC.” 

Habari kutoka eneo la tukio zilisema gari dogo lilikuwa mali ya kiongozi wa Chama cha Walimu mkoani humo na lilikuwa limewabeba watu watano, wakiwamo waandishi wa habari. 

Wabunge wacharuka matumizi ya fedha za wafadhili

$
0
0
Wabunge wameitaka Serikali kutoa maelezo ya dola 300 milioni za Kimarekani (sawa na Sh570 bilioni) zilizotolewa na wahisani kwa ajili ya kusaidia miradi ya afya, lakini hazijatumika. 

Fedha hizo zilitolewa na Global Fund kwa ajili ya kugharamia miradi ya Ukimwi, malaria na kifua kikuu (TB) na zinatakiwa hadi kufikia Desemba mwaka huu ziwe zimeshatumika. 

Mjadala huo ulizuka jana katika semina ya wabunge wa kamati tatu za Bunge kuhusu afya ya wanawake, watoto na vijana iliyoandaliwa na Umoja wa Mabunge ya Dunia (IPU) na Bunge la Tanzania. 

Semina hiyo ilishirikisha Kamati ya Bajeti, Huduma na Maendeleo ya Jamii na ya masuala ya Ukimwi. 

Akizungumza katika semina hiyo, mbunge wa viti maalumu (Chadema), Suzan Lyimo alisema bila kuwa na bajeti ya kutosha, malengo ya pambano dhidi ya Ukimwi hayawezi kufikiwa. 

“Tunasikia kuna wadau wengi waliokuwa wanasaidia eneo hili wamejiondoa. Nataka kufahamu wanasemaje kuhusu hili?” alihoji. 

Akijibu hoja hiyo, Marianna Balampama kutoka Kundi la Washirika wa Maendeleo (DPG), alisema wafadhili hawajajitoa kusaidia miradi hiyo. Alisema wafadhli hao kama Marekani na Global Fund wanaendelea kutoa misaada. 

Hata hivyo, alisema muda wa dola 300 milioni za Kimarekani zilizotolewa na Global Fund unakaribia kuiisha, lakini hazijatumika. 

Alisema kutokana na masharti mapya ya Global Fund, muda wa kutumika ukimalizika, kama hazijatumika hutakiwa kurudishwa. 

Hali hiyo iliwafanya wabunge wengine kuanza kuguna na wengine kunong’ona. Kutokana na maelezo hayo, Deogratius Rutatwa, ambaye ni ofisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (Nacopha), aliiomba Serikali kuchukua hatua za haraka ili fedha hizo zisirudishwe. 

Hata hivyo, Dk Nemes Irya kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) aliwatoa hofu wabunge kuwa fedha hizo haziwezi kurudi kwa wafadhili.

 “Huwa fedha hizi zinakuja kwa mafungu kama tunavyotekeleza miradi,” alisema. 

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema Serikali ilikuwa na mazungumzo na Global Fund ya jinsi ya kutumia kiasi hicho cha cha fedha hizo katika kuboresha miundombinu. Waziri Ummy alisema ameiam- bia Global Fund kuwa Serikali inataka iwe na uamuzi kwa asilimia 15 ya fedha zinazotolewa. 

“Mwaka huu nimewambia Global Fund, kati ya hizo Dola 380 milioni za Kimarekani mnazotupatia, asilimia 15 nizitenge mimi. Niamue tunazitumiaje, wasitu lazimishe tuzitumie kwaajili ya Ukimwi na malaria tu, bali nizitumie kuboresha mifumo.” Ummy Mwalimu

Rais Magufuli Amwapisha Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi

$
0
0
Rais John Magufuli leo amemuapisha Mkuu mpya wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo Ikulu jijini Dar es Salaam.

Jenerali Mabeyo aliteuliwa na Rais Magufuli Alhamisi iliyopita kushika wadhifa huo baada ya Jenerali Devis Mwamunyange kustaafu.

Jenerali Mabeyo alikuwa Luteni Jenerali kabla ya kupandishwa cheo kuwa Jenerali.

Kabla ya kuapishwa Jenerali huyo, Rais John Magufuli alimvalisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo cheo kipya na kuwa Jenerali.

Pia, Rais Magufuli amemuapisha Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Luteni Jenerali James Mwakibolwa akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo.

Rais Magufuli apigilia msumari Sakata la Madawa ya Kulevya......Ataka Polisi Wasiangalie Umaarufu wa Mtu, Asema hiyo sio Vita ya Makonda Pekee

$
0
0
Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata wanaohusika na Dawa za Kulevya bila kuangalia umaarufu au cheo cha mtu.

Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza  mara  baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Vanance Mabeyo pamoja na viongozi wengine wa majeshi, na mabalozi.

Katika hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Magufuli alianza kwa kumpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Ernest Mangu kwa hatua nzuri aliyoichukuwa ya kuwasimamisha kazi Askari Polisi 12 waliotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya ili kupisha uchunguzi.

Rais Magufulia amesema hakuna wa kuachwa hata akiwa mkewe Mama Janet Magufuli, na kuongeza kuwa wakamatwe bila ya kujali majina yao.

"Najua IGP Mangu watu walikupigia simu wanakupa ushauri kuhusu Dawa za Kulevya, ungewasikiliza leo usingekuwa IGP.

"Vita ya dawa za kulevya haina cha umaarufu, haijalishi ni mtoto wa nani anahusika, hata kama ni mke wangu mkamateni.

"IGP nakuagiza kamata watuamiaji wote wa dawa za kulevya hao watakwambia wanapozipata, haiwezekani ziuzwe kama njugu."Amesema Rais Magufuli

Akizungumzia suala la uendeshaji wa kesi za dawa kulevya, Rais Dkt Magufuli amemwambia Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania,  Jaji Prof. Ibrahim Hamis Juma kuwa kesi hizo zinaendehswa taratibu sana huku akitolea mfano wa mfanyabiashara mmoja maarufu wa dawa za kulevya aliyekamatwa mkoani Lindi lakini hakuwahi kufikishwa mahakamani. 

"Kuna mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya alikamatwa mkoani Lindi lakini sijawahi kusikia amefikishwa mahakamani" Amesema Rais Magufuli.

Rais  Magufuli amesema kuwa vita ya dawa za kulevya si ya Paul Makonda peke yake bali ni ya Watanzania wote huku akivitaka vyombo mbalimbali vya ulinzi na usalama kushirikiana kutokomeza tatizo hili linalopelekea kupoteza nguvu kubwa ya taifa.

Kauli hii ya Rais Magufuli inakuja ikiwa ni siku chache tangu Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda atangaze vita dhidi ya watu wanaohusika na dawa za kulevya akianza kwa kutaja majina yakiwemo ya askari na ya wasanii maarufu wa muziki na filamu akiwemo Wema Sepetu, Chid Benz, Vanessa Mde n.k.

Siku tatu baada ya Makonda kuwataja watuhumiwa hao, IGP Ernest Mangu alichukua hatua ya kuwasimamisha askari  12 waliotajwa na kuahidi kuchukua hatua zaidi, jambo ambalo limepongezwa na Rais Magufuli na kumueleza kuwa endapo asingechukua hatua hiyo, angejua kuwa na yeye anahusika.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images