Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Video Mpya : Diamond Platnumz f/ Ne-Yo – Marry You

$
0
0
Baada ya kusubiriwa kwa muda mrefu, video ya Diamond Platnumz ya wimbo wake, Marry You aliomshirikisha Ne-Yo imetoka. Kwa mara ya kwanza video hii imewekwa kwenye channel ya Vevo ya staa huyo.

Universal Music Group (UMG) watangaza rasmi kumsainisha Diamond

$
0
0
Hatimaye record label kubwa duniani, Universal Music Group (UMG), imemtangaza rasmi kumsainisha Diamond Platnumz.

Anakuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kusainishwa kwenye label hiyo.

Wimbo wake, Marry You akiwa na Ne-Yo ni wa kwanza kutoka chini ya mwamvuli wa Universal Music.

“He’s a star, he is talented and full of energy and creatively he’s on par with any international artist I’ve worked with,” anasema Mkurugenzi Mtendaji wa label hiyo Afrika, Sipho Dlamini.

“He’s focused and determined to succeed. He’s passionate about his country, his people , his language and his culture and I love that. He is a first class performer on stage, his new material is authentic, fresh and African, yet it will touch people across the globe. Artists like him are the reason we do what we do.”

Kitwanga Aibuka Bungeni....Atishia Kuongoza Wananchi Kung'oa Mitambo ya Maji Ziwa Victoria

$
0
0
Mbunge  wa Misungwi (CCM), Charles Kitwanga, amesema yuko tayari kuwahamasisha wananchi wa jimbo lake kwenda kuing’oa ama kuizima mitambo ya kusukuma maji Ziwa Victoria kupeleka mkoani Shinyanga ikiwa maji hayatafika jimboni kwake.

Kitwanga alitoa kauli hiyo bungeni jana alipokuwa akiuliza swali la nyongeza.

Mbunge huyo alisema wananchi wa jimbo lake katika Vijiji vya Ihelela Kashwasa, walishapewa ahadi tangu mwaka 2008 kuwa wangeunganishiwa maji kutoka katika mtambo wa kusukuma maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Shinyanga, lakini hadi sasa ahadi hiyo haijatekelezwa.

“Ahadi hii ilitolewa na aliyekuwa Rais wa wakati huo, Jakaya Kikwete, lakini kila siku ni ahadi bila utekelezaji. Kweli nitawasindikiza wananchi wangu kuzima mitambo ili maji yasipelekwe Shinyanga, nasema kweli nitafanya hivyo,” alisisitiza Kitwanga.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Isaack Kamwelwe, alikiri kuwa Rais wa awamu ya nne alitoa ahadi hiyo mwaka 2008 kwamba wananchi wa maeneo ya Ihelela wataunganishiwa maji kutoka bomba la Ziwa Victoria.

Hata hivyo, Kamwelwe alimuomba mbunge huyo asihamasishe watu kuzima mitambo hiyo wakati wowote badala yake wavute subira.

Katika swali la msingi la Mbunge wa Kasulu Mjini, Daniel Nsanzugwako (CCM), alitaka kujua Mto Malagarasi una ujazo gani wa maji na kama yanatosheleza mahitaji.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri Kamwelwe alisema serikali imepanga kutekeleza miradi mbalimbali kwa kutumia Mto Malagarasi ikiwamo mradi wa maji kwa ajili ya miji ya Urambo, Kaliua pamoja na kilimo cha mwagiliaji na uzalishaji umeme wa megawati 44.5.

“Wakati wa masika, mto huo unakuwa na maji yanayotiririka kwa mita za ujazo 55 kwa sekunde na wakati wa kiangazi unakuwa na mita za ujazo 40 kwa sekunde," alisema.

Picha: Wema Sepetu na wenzake watua Central Polisi Dar......Walitakiwa Wajisalimishe Leo Kwa Kujihusisha na Madawa ya Kulevya

$
0
0
Kufuatia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kuwataka baadhi ya mastaa wanaoshukiwa kujihusisha na matumizi na biashara ya madawa ya kulevya kuwasili kituo cha polisi cha kati siku ya leo baadhi ya mastaa wametii agizo hilo na kuwasili.

Wema Sepetu ambaye alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotuhumiwa na Mkuu wa Mkoa wa Da es salaam Paul Makonda kwamba anatumia Madawa ya kulevya, amewasili kituoni hapo  huku akiwa amevalia vazi la  hijab.

Wasanii wengine waliofika kituoni hapo ni pamoja na TID, Nyandu Tozzy pamoja na mtangazaji wa Clouds TV Babu wa Kitaa. 
TID akiwa kituoni hapo

Makonda Amtaja Na Vee Money na Tunda Ishu ya Madawa ya Kulevya....Waliokaidi Agizo Lake Leo Kukamatwa

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ameagiza kukamatwa kwa watu aliowataja jana kuhusika na dawa za kulevya ambao hawajajisalimisha kituo cha polisi leo, kama alivyoagiza

Makonda aliyefika katika Kituo Kikuu cha Polisi, amesema watu wao ambao hawajajisalimisha, wasakwe kokote waliko, na wawekwe ndani.

"Kuna watu tuliwaita, baadhi nimeambiwa hawajafika, ambao hawajafika nimeagiza wakachukuliwe wakae ndani mpaka siku ya Jumatatu" Amesema Makonda.

Amesema kati ya watu waliotajwa jana, ni wasanii watano pekee ndiyo wamejisalimisha siku ya leo katika kituo hicho wakiongozwa na aliyewahi kuwa Miss Tanzania Wema Sepetu, Nyandu Tozi (Hamidu), TID, Babuu wa Kitaa.

Pia kwa mujibu wa taarifa ya jeshi hilo, jumla ya polisi 7 wamekwisha kamatwa huku watatu wakiendelea kutafutwa na wengine wawili ambao hawako katika jiji la Dar es Salaam watakamatwa ndani ya muda mfupi ujao.  

 Katika hatua nyingine, Makonda ametaja orodha nyingine tofauti na aliyoitaja jana ya watu wanadaiwa kuhusika katika dawa za kulevya akiwemo msanii bongo fleva Vanessa Mdee, mwanamitindo anayefahamika kwa jina la Tunda.

Mbali na wasanii hao, makonda amewataja pia askari wengine watatu wa Jeshi la Polisi Tanzania ambapo amedai kuwa askari hao wanatuhumiwa kwa kupokea pesa kiasi cha shilingi bilioni 1 hivi karibuni kutokana na kuhusika na dawa za kulevya pamoja na kukamata dawa za kulevya kisha kuziuza tena.

Pia amemtaja anayejulikana kwa jina la Omari Sanga kuwa ni mmoja anayehusishwa na uletaji wa dawa ya kulevya na amesababisha asilimia 60 ya watanzania kufungwa katika magereza ya china.

Makonda amesema "Waliofika tutajadiliana nao kuona namna gani wanatupatia yale tunayoyataka kuyafanyia kazi kutokana na taarifa tulizo nazo. Vita hii ya dawa za kulevya haiishi leo, inaisha pale dawa zinapokuwa zimeisha"

Naye Kamanda Wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam kamishna Simon Sirro amesema kuwa Jeshi hilo limeunda tume ya kushughulika na mapambano dhidi ya dawa za kulevya mkoani humo

Serikali Yatolea Ufafanuzi Madai Ya Walimu na Riba Kubwa Katika Mabenki

$
0
0
Dodoma, Ijumaa, 3 Februari, 2017:Serikali imetolea ufafanuzi kuhusu kero mbalimbali za Wabunge ikiwemo kuhusu maslahi ya walimu nchini na kadhia ya riba kubwa katika mabenki. Ufafanuzi huo umetolewa leo wakati wa vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini hapa.

Stahili za Walimu
Serikali imesema kuwa ni kweli inadaiwa na walimu madeni yasiyo ya mishahara yanayofikia  shilingi 26,042,581,697 hadi kufikia Desemba,2016. Naibu Waziri, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo amesema deni hilo litaanza kulipwa hivi karibuni kwa kuwa deni hilo lote limeshahakikiwa.

Kuhusu madeni ya mishahara, Naibu Waziri Jafo ameliambia Bunge kuwa uhakiki wa deni la shilingi 10,034,495,540 umekamilika na kinachosubiriwa ni kulipwa kupitia akaunti ya mtumishi anayedai. Ameongeza kuwa, deni linalobaki ni shilingi 8,067,922,773 ambalo linaendelea kuhakikiwa ili nalo liweze kulipwa.

Upungufu wa Vyumba vya Madarasa na Maabara
Akijibu hoja kuhusu mkakati wa Serikali wa kupunguza tatizo la vyumba vya madarasa na maabara, Naibu Waziri Jafo amesema kuwa, Serikali katika bajeti ya mwaka 2016/17 imetenga jumla shilingi bilioni 29.3 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 3,306 kwa shule za msingi na shilingi bilioni 16.3 zimetengwa kujenga vyumba vya madarasa 1,047 kwa shule za sekondari.

Ameliambia Bunge kuwa utekelezaji wa malengo hayo pia utafanywa kupitia Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Sekondari (MMES II) ambako pia zimetengwa shilingi bilioni 23.6 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa vyumba 1,642. Upande wa maabara Serikali imetenga shilingi bilioni 18.9 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba 2,135.

Kumuinua Mwanamke Kiuchumi
Serikali imesema kuwa hadi kufikia Desemba, 2016 Benki ya Wanawake imeshafungua matawi katika mikoa saba (7) ya Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Iringa, Njombe, Mbeya na Ruvuma ambapo huduma mbalimbali za kuwainua akina mama kiuchumi zimetolewa. Katika huduma hizo, dirisha la kuhudumia maeneo ya Iringa na Makambako pekee hadi kufikia Desemba, 2016 jumla ya Wajasiliamali 6,850, wanawake 5,350 na wanaume 1,500 walipatiwa.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis Kigwangalla ambapo aliongeza kuwa Benki hiyo imefungua vituo vya kutolea mikopo 252 kufikia Desemba 2016.

Riba Kubwa katika Mabenki
Serikali imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) haiwezi kuweka ukomo wa riba za mabenki kwani si tu inapingana na jukumu lake la msingi la kusimamia mabenki, bali pia hilo liinapingana na mfumo wa uchumi wa soko huria. Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe.Dkt. Ashatu Kijaji ametoa kauli hiyo wakati akijibu hoja inayohusu uwepo wa riba kubwa katika mabenki.

Dkt.Kijaji ameeleza kuwa, suala la Benki Kuu kutoa maelekezo kwa mabenki kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuyachukulia mabenki hatua endapo yatapata hasara kwa kutumia riba ambayo Benki Kuu imeelekeza. “Benki Kuu haina mamlaka kisheria ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na mabenki katika kutoa mikopo,” alisema.

Hali ya Kituo cha Biashara cha Taifa Nchini Uingereza
Serikali imesema kuwa imekifunga rasmi Kituo cha Biashara cha Taifa kilichopo mjini London, Uingereza kutokana na changamoto mbalimbali za kituo hicho ikiwemo ufinyu wa bajeti pamoja na upungufu wa rasilimali watu.

Akijibu hoja hiyo Bungeni leo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji amesema, badala yake, shughuli zote za kituo hicho zimehamishiwa Ubalozi wa Tanzania uliopo mjini London.


Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.

Wakuu wa Mikoa na Wilaya Wapewa Rungu la Kutumbua Watumishi

$
0
0
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  George Simbachawene amesema kuwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Simbachawene ameyasema hayo leo Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la  nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Chemba Juma Nkamia kuhusu Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa wababe katika maeneo yao ya kazi.

“Wakuu wa Mikoa na Wilaya wanasimamia maeneo yao kwa mujibu wa sheria na wana haki ya kuwachukulia hatua watumishi ambao hawatekelezi majukumu waliyopewa,” alifafanua Simbachawene.

Aliendelea kwa kusema kuwa, hata kama kuna Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambao ni wababe katika maeneo yao ya kazi hauwezi kusema kila Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyechukua hatua dhidi ya mtumishi ambaye hawajibiki katika kazi yake ni mbabe au muonevu.

Aidha, Simbachawene amesema kuwa ni wakati sasa wa watumishi wa Umma kutekeleza wajibu wao na kuacha kufanya kazi kwa mazoea. Kwani hakuna kiongozi ambaye ataweza kumchulia hatua mtumishi ambaye anawajibika na kazi zake kama alivyopangiwa.

Vile vile amesema kuwa, wakuu hao wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakifanya kazi nzuri katika maeneo wanayoyasimamia, kutokana na watumishi wengi wa Serikali walikuwa wamejisahau kutekeleza wajibu wao na kufanya kazi kimazoea.

Benki Kuu haina mamlaka kupanga riba kwenye mikopo ya taasisi za kifedha (benki)

$
0
0
Benny Mwaipaja-WFM, Dodoma
SERIKALI imesema kuwa Benki Kuu ya Tanzania haina mamlaka kisheria ya kuweka ukomo wa riba au riba elekezi itakayotumiwa na taasisi za fedha nchini zikiwemo benki katika kutoa mikopo.

Kauli hiyo imetolewa Bungeni mjini Dodoma, Februari 3, 2017 na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, wakati akijibu maswali ya msingi yaliyoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Mbagala, Mhe. Issa Ali Mangungu, aliyetaka kujua kama serikali inaweza kuandaa utaratibu maalumu wa riba elekezi itakayowawezesha wanawake na vijana kupata mikopo kwenye benki kwa riba nafuu ili waweze kujikwamua kiuchumi

Aidha Mbunge huyo alitaka kufahamu kama Serikali inaweza kuziagiza benki za biashara kulegeza masharti ya dhamana kwa vijana na wanawake ambayo amedai yanarefusha mchakato wa upatikanaji wa mikopo kwa makundi hayo.

Dkt. Kijaji amesema kuwa viwango vya riba katika benki na taasisi nyingine za fedha hupangwa na taasisi husika kwa kutegemea mambo mengi ikiwemo nguvu ya soko, sifa za mkopaji, ushindani katika soko, gharama za upatikanaji wa fedha, mwenendo wa riba za dhamana za serikali, gharama za uendeshaji na matarajio ya mfumuko wa bei.

Amesema kuwa Benki Kuu imepewa mamlaka kisheria kusimamia Benki na Taasissi nyingine za fedha hivyo haiwezi kuingilia upangaji wa riba za mikopo kwenye taasisi hizo kwakuwa jambo hilo linapingana na mfumo wa uchumi wa soko huria.

“Kutoa maelekezo kwa benki na taasisi za fedha kutumia viwango fulani vya riba katika biashara zao, kutaifanya Benki Kuu kukosa nguvu na mamlaka ya kuzichukulia hatua endapo zitapata hasara kwa kutumia riba iliyopangwa ama kuelekezwa na Benki Kuu” alisisitiza Dkt. Kijaji

Naibu Waziri huyo wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amesema kuwa Benki Kuu imeendelea na jukumu lake la msingi la kuhakikisha kuwa mfumo huo unaendeshwa kwa kuzingatia sheria zilizowekwa ili kulinda maslahi ya Taifa na uchumi kwa kusimamia ongezeko la ujazi wa fedha ili kuhakikisha linakwenda sambamba na mahitaji halisi ya uchumi ili kudhibiti mfumuko wa bei.

Ameyataja majukumu mengine ya BOT kuwa ni kuhakikisha kuwa ongezeko la mikopo ya benki haliathiri uzalishaji mali kulingana na malengo ya ujazi wa fedha, kuhakikisha kuwa soko la dhamana la serikali linaendeshwa kwa ufanisi ili liweze kutoa riba elekezi kulingana na hali ya soko na uchumi kwa ujumla.

MWISHO

Alichoandika Afande Sele kuhusu mkakati wa RC Paul Makonda wa kotokomeza dawa za kulevya jijini Dar es Salaam.

$
0
0
Afande Sele ni miongoni mwa wasanii wa siku nyingi Tanzania ambao wamekua wakifatilia pia na ishu za siasa na mengine yanayoendelea ambapo leo hii ameandika  kuhusu ishu ya  dawa za kulevya iliyotangazwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda.

Afande ameandika "Katika hili sakata la MAPAPA na MAPUNDA ya Unga kama kweli braza Paul yupo serious na sio ‘Matango Pori’kama tulivyoona ktk masakata mengine,huenda hata wale WASAFI wakaonekana wachafu…kila la kheri Mr Paul….RiP Da Amina…wacha parry ianzeee"

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya February 4

Waturuki Kujenga Reli ya Kisasa.......Treni Itatumia Saa 1;30 Kutoka Dar hadi Moro. Dar Hadi Mwanza ni Masaa 7 tu

$
0
0
Serikali ya Tanzania na kampuni za ujenzi za Uturuki na Ureno, zimesaini mkataba wa ujenzi wa Reli ya Kati kwa kiwango cha kimataifa (standard gauge) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro wenye thamani ya dola za Marekani bilioni 1.21 (Sh trilioni 2.66).

Kati ya fedha hizo, dola za Marekani bilioni 1.21 (Sh trilioni 2.2) ndiyo gharama halisi ya ujenzi wa kipande hicho na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni dola milioni 1.85 (Sh bilioni 406).

Mradi huo unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili na nusu, utaifanya Tanzania kuwa nchi ya pili barani Afrika yenye reli kama hiyo ambayo inaweza kupitisha treni ya umeme inayotembea kwa mwendo wa kasi.

Akizungumza kabla ya kutilia saini mkataba huo jana, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, alisema kwa sasa barani Afrika, Morocco ndiyo yenye reli kama hiyo inayopitisha treni inayotembea kasi ya kilomita 200 kwa saa.

Kukamilika kwa kipande cha reli ya Dar es Salaam mpaka Morogoro, treni inayotembea kwa kasi ya kilomita 160 kwa saa itaweza kupita.

Profesa Mbarawa alisema hali hiyo itafanya safari ya kutoka Dar es Salaam kwenda Morogoro kuwa saa 1:30.

Kukamilika kwa awamu ya pili ya reli hiyo kutoka Morogoro mpaka Dodoma kutaifanya safari ya treni hiyo ya umeme kutoka Dar es Salaam kwenda makao makuu ya nchi kwa kutumia saa 2:30 huku kitakapomalizika kipande cha Dar es Salaam mpaka Mwanza, kutaifanya treni hiyo kusafiri kutoka Dar es Salaam mpaka mkoa huo wa Kanda ya Ziwa kwa saa 7:30.

Kampuni zilizotia saini ujenzi wa reli hiyo ni Yapi Merkenzi Instant Ve Sanayi A.S ya Uturuki ambayo imeungana na Mota-Engil, Engenharia E and Construcao S.A ya Ureno.

Awamu ya kwanza ya reli hiyo kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro itakuwa na urefu wa kilomita 300 kati yake kilomita 205 ni njia kuu na 95 ni njia za kupishania treni.

Ujenzi huo utahusisha pia uzio wa usalama kutokana na reli hiyo kutumia umeme pamoja na ujenzi wa vivuko kwa watu na wanyama.

Profesa Mbarawa alisema:“Wakati tunafikiria ujenzi wa reli hii tuliwatuma vijana Kenya, Ethiopia na Nigeria kuangalia namna ambavyo wenzetu wamefanikiwa, tulilenga kuepuka makosa ambayo wenzetu waliyafanya ili tusiyarudie.

“Tuligundua nchi hizi treni yao inakwenda kilomita 120 kwa saa, tukajiuliza kwanini tusipate inayokwenda 160? Sasa tumepata inayokwenda kasi zaidi. Ya Kenya na Nigeria zinatumia mafuta, tukaenda Ethiopia tukakuta wao wanatumia umeme, tukaona kwanini na sisi tusije na inayotumia umeme? Sasa tumefanikiwa.”

Alisema reli hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba mzigo wa tani 35 kwa excel moja, ikilinganishwa na sasa ambapo reli ya zamani (meter gauge) ina uwezo wa kubeba tani 14 kwa excel moja.

Reli hiyo itakuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 17 za mizigo kwa mwaka kutoka tani milioni tano za sasa, hivyo kuifanya kuwa daraja la uchumi wa nchi kwa kuiunganisha na nchi za jirani ambazo hazina bandari.

“Tumeamua kufanya mradi huu kwa kasi na kuzingatia kiwango cha ubora wa reli yenyewe lakini pia gharama za ujenzi. Usafiri wa reli ni nafuu na inabeba mizigo mingi,” alisema Profesa Mbarawa.

Alisema itakapokamilika reli hiyo, itarahisisha usafiri ambapo mtu anaweza kuishi Dodoma au Morogoro na akafanya kazi Dar es Salaam.

Alisema gharama ya ujenzi huo inategemewa kushuka kwa eneo la kuanzia Morogoro hadi Mwanza kwani eneo hilo si la mwinuko kama ilivyo kutoka Dar es Salaam mpaka Morogoro.

Aliongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha 2016/2017, Serikali itaongeza fedha za ujenzi wa reli hiyo ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo kutoka kwa wahisani ili kuhakikisha wanaiunganisha Tanzania na kuifanya kuwa karibu zaidi tofauti na ilivyo sasa.

Alisema jumla ya kampuni 40 ziliomba zabuni ya kujenga reli hiyo lakini YAPI ya Uturuki inayoshirikiana na Mota ndiyo iliyorudisha zabuni.

Akizungumzia kuhusu kampuni za China kutopewa zabuni ya ujenzi wa reli hiyo alisema ni kwasababu hazikurudisha zabuni zao.

Wakati huo huo Waziri Mbarawa alisema tayari Serikali imetangaza zabuni ya ujenzi wa reli hiyo kuanzia Morogoro hadi Makutupora kilomita 336, Makutupora hadi Tabora 294, Tabora hadi Isaka 133 na Isaka hadi Mwanza 248.

“Tunaikaribisha kampuni yoyote inayotaka kujenga na hakuna kampuni tutakayoionea ila uwezo wa kampuni na gharama za ujenzi zitaangaliwa,” alisema Waziri Mbarawa.

Akizungumza katika utilianaji saini huo Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Profesa Norman King, alisema kuanza kwa ujenzi wa reli hiyo ni kutimia kwa ndoto za Rais Dk. John Magufuli za kuona Tanzania inakamilisha ujenzi wa reli ya kiwango cha kimataifa.

“Pamoja na kuonekana kwa wengi tumechelewa lakini kuchelewa huku ni kuzuri kwa sababu tumeua ndege wawili kwa jiwe moja kwa kupata treni inayokwenda kasi na ya umeme,” alisema King.

Nape Aipongeza Serengeti Boys Kwa Kufuzu Fainali Za AFCON Gabon 2017

SORRY MADAM -Sehemu ya 27 & 28 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
‘Hawanijui hawa’
Eddy alizungumza huku akishuka kwenye gari bastola yake akiwa ameichomeka kwa nyuma.
“Nyinyi ni wakina nani?”
Eddy aliwauliza huku akijiweka sawa kwa lolote litakao kwenda kujitokeza, ukimya wa barabara hiyo inayo elekea ikulu na majira haya ya usiku iliwafanya Lube na wezake kuweza kuilisikia swali hilo walilo ulizwa. Hapakuwa na aliye jibu zaidi ya wao kuanza kujitawanya na kumzingira Eddy na kumuweka kati tayari kwa kumshambulia.

ENDELEA
Eddy akawatazama kwa huku akiwahesabu jinsi walivyo kaa, taratibu akalivua shati lake na kubaki tumbo wazi, Lube akamuamrisha mwenzake mmoja kufanya shambulizi kwa Eddy anaye onekana kujiamini sana. Kitendo cha jamaa kumfikia Eddy, akakutana na teke zito lilotua kifuani kwake na kumuangusha chini kama mzigo. Ikawabidi wengine kushanga kwani kila mmoja hakuamini kama kiongozi huyo anaweza kufanya tukio la aina hiyo.

Wote watatu walio bakia wakamvamia Eddy kwa kasi, kila mmoja akijaribu kupiga sehemu yake anayo iweza kupiga katika mwili wa Eddy, ila kila walivyo jaribu kupambana, ndivyo jinsi walivyo weza kukutana na mapigo makali yaliyo wachanganya kiasi cha kuwafanya kila mmoja kujikuta akiwa na maumivu upande wake. Lube alipo gundua Eddy amewazidi kila jambo. Kwa bahati nzuri akaona gongo moja pembezoni mwa barabara. Akarudi nalo hadi sehemu wanapo endelea kupambana wezake, huku gongo hilo akiwa amelificha nyuma ya mgongo wake.
“EDDYYYYYYYYY……..”
Lube akamuita Eddy kwa sauti ya juu na kumfanya Eddy ageuke kutazama mtu anaye muita, ila gafla gongo zito likatua, kichwani mwake na kumfanya Eddy kuyumba, kijana mmoja akamsindikiza na teke zito lililo muangusha Eddy chini na kupoteza fahamu.

“Mbebeni haraka haraka”
Lube alizungumza, kabla hata hawajamnyanyua mwanga mkali wa gari ukawamulika, na kuwafanya wasimama kulitizama gari hilo ni la nani majira hayo ya usiku. Gari hiyo ikafunga breki na kusimama, akashuka mtu ambaye wote wanamfahamu.
“Huyu Samson amefwata nini hapa”
Mmoja wao alizungumza kwa sauti ya chini huku wakimtazama Samson akitembea na kuwafwata sehemu walipo.
“Bosi tufanyaje?”
Mmoja wao aliuliza huku kila mmoja akijiweka sawa. Samson akawatazama kisha akawakazia macho, wote wakajikuta wakishikwa na woga mkali kwani macho ya Samson yalibadilika na kutisha sana

***
    Agnes na Jaquline wakashuhudia jinsi Halima na wezake wanavyo pata mateso gerezani. Video hizo zikawamfanya Agnes kumwagikwa na machozi ya uchungu, uzuri wa wezao hao wote umepotea, alama nyingi za makovu zimetawala kwenye miili yao.

“Munaweza kuamua sasa, kufanya kazi na sisi au wezenu waendelee kupata mateso na mwisho wa siku hukumu ya kuuawa itakuwa dhidi yao”
Kabla hawajajibu mlio wa simu ukalia kutoka kwenye mfuko wa mmoja wa walinzi, akaitoa simu hiyo na kuipokea kisha akaiweka sikioni mwa John
“Ndio mkuu”
“Leo ninakuja mako makuu kila kitu ukiweke sawa”
“Sawa mkuu”
Simu ikakatwa John akashusha punzi kidogo, kwa taarifa aliyo weza kuipata kwa mkuu wake Mzee Godwin. Akaagiza ulinzi uzidi kuimarishwa na vijana waweze kujiandaa kumpokea mkubwa wao huyo anaye tokea barani Afrika.

“Tumekubali, ila kwa sharti moja”
Jaquline alizungumza huku akimtazama John machoni huku akiwa amemkazia macho, John akatingisha kichwa chake kumruhusu Jaquline kuendelea kuzungumza.
“Hatuta weza kufanya kazi yoyote na nyinyi hadi pale tutakaopo waokoa wezetu”
“Mmmmmmm, nitarifikiria”
“Waandalieni sehemu inayo stahili wao kuwepo”
John akatoa agizo lake kwa vijana wake, wakawachukua Jaqulne na Agnes na kuwapeleka kwenye moja ya chumba kilicho na huduma za kila kitu wakisubiria juu ya jibu watakalo pewa na John.

Mzee Godwin akaagana na bwana Abdulah Mohamed mkuu wa kikosi cha kigaidi cha Al-Shabab, wakaingia kwenye ndege ya kifahari aina ya Jet inayo ingia abiria watano pamoja na marubani wawili. Tom na Manka tayari walisha ingia kwenye ndege hiyo wakimsubiria baba yao aliye kuwa akipiga stori za hapa na pale na kiongozi huyo waliye aihidiana kupanga baadhi ya mipango takayo kuwa kabambe katika kutawala baadhi ya maeneo kwa kutumia nguvu.
“Mumemechoka ehee”
Mzee Godwin aliwauliza wanae hao huku akijiweka vizuri katika siti aliyo kaa
“Ahaa kidogo tu”
Tom alijibu
“Mmmm mimi nimechoka sana tu baba, hapa natamani tufike huko tunapo kwenda”
“Musijali haita chukua masaa mengi tutakuwa tumefika”
                                                                                           ***
Mihemo mizito pamoja na mingurumo anayo itoa Samson ikawafanya Lube na wezake kuzidi kutetemeka, mmoja wao akachomoa bastola yake na kumfyatuia baadhi ya risasi kwa Samson, ila jambo la kushangaza risasi hizo ziliingia mwilini mwa Samson ila katika sehemu zilipo ingia jeraha lake likapona ndani ya sekunde chache.

Kwa kasi ya ajabu Samson akamkimbilia jamaa aliye mpiga risasi, akamkamata shingo, kwa mkono mmoja akamnyanyua juu, huku akizidi kukoroma na macho yake yakiwa yamebadilika na kuwa kama simba aliye na hasira kali.

“Ondokeni hapaaa”
Samson alizungumza kwa sauti nzito, huku akimuachia aliye mpiga risasi hakuhitaji kumdhuru na kuwafanya Lubne na wezake wote kuondoka katika eneo hilo, wakaingia ndani ya gari lao na kuondoka kwa mwendo wa kasi kila mmoja akiwa haamini alicho weza kukiona kwa binadamu huyo wanaye mtambua kama Samson.

Samson akambeba Eddy begani na kumuingiza kwenye gari lake na kuondoka naye.
“Madam nimempata”
John alizungumza kupitia simu yake huku akiwa amesimamisha gari lake pembezoni mwa barabara huku Eddy akiwa amemlaza siti ya nyuma.
“Safi sasa hakikisha unampeleka kwenye eneo ambalo si rahisi kwa mtu kuweza kutambua”

“Sawa madam”
Samson akakata simu na kuendelea na safari, Samson kitu alicho weza kukumbuka ni moja ya handaki ambalo Rahab alimueleza kwamba yalikuwa ni maficho yao kipindi walipo weza kukutana kwa mara ya kwanza, na handaki hilo lipo nje ya mji. Usiku huo huo akafunga safari hadi nje ya jiji la Dar es Salaam, akifwatisha maelekezo anayo tumiwa kwa njia ya meseji na Rahab aliyopo ndani ya ikulu
“Mke wangu leo unachati sana”
Raisi Praygod alimuuliza Rahab, mara baada ya kuingia ndani ya chumba chao dakika kadhaa zilizo pita, ila mapokezi ya leo yapo tofauti sana na siku nyingine za nyuma, kwani alisha zoea kufanyi mapokezi ya mabusu motomoto.

“Kuna taarifa ninaisoma hapa”
“Taarifa gani ambayo raisi siifahamu?”
“Aihusiani na Tanzania”
“Mmmm saw………..”
Raisi Praygod hakuimalizia sentesi yake simu yake ikaita, akaitoa kwenye mfuko wa koti lake la suti na kukuta Lube ndio anaye mpigia, akamtazama Rahab kwa macho ya kuiba kisha akaipokea.
“Mmmmmm”
“Mkuu tumeshindwa Samson sio binadamu”
Raisi Praygod akashindwa kuzungumza chochote zaidi ya kutoka ndani ya chumba chake cha kulala na kwenda kuzungumzia sebleni, na kumpa nafasi Rahab ya kumpigia simu Samson.
“Sio binadamu kivipi?”
“Yaaani yaani macho yake yamekuwa kama, samba”
“Ahahaa Lube hembu pangilia sentesi zako nikuelewe”

Tunda Man adai amepokea simu nyingi baada ya jina Tunda kutajwa kwenye list mpya ya Mtandao wa Madawa ya Kulevya

$
0
0
Msanii wa muziki Tunda Man amedai jana alipokea simu nyingi baada ya Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kutangaza list mpya ya majina ya watu wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya ilikiwemo jina la Tunda ambaye ni video queen.

Baadhi ya waandishi kwenye mitandao ya kijamii waliandika jina Tunda bila kutolea ufafanuzi ni Tunda gani, hali ambayo iliwafanya wasiohusika kupigiwa simu nyingi akiwemo msanii wa muziki Tunda Man.

Tunda Man amedai wengi ambao ulikuwa wanampigia simu walitaka kujua kama kweli ni yeye ndiye aliyetajwa au ni Tunda mwingine.

“Jaman Tunda alietajwa na Mh Paul Makonda ni huyu sio mie maaana simu zimekuwa nyingi @soudybrown na wewe hujui au umeamua tu kunipigia,” aliandika Tunda Man Instagram huku akiwa amempost dada huyo.

Pia kwenye list hiyo mpya alitajwa mwanadada Vanessa Mdee ambaye pia anatakiwa kuripoti makao makuu polisi Jumatatu.

Jeshi La Polisi Lawasimamisha Kazi Askari 12 Waliotuhumiwa Kujihusisha Na Biashara Ya Madawa Ya Kulevya

$
0
0
Kufuatia tuhuma zilizotolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda zikiwahusisha baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewasimamisha kazi Askari 12 waliotuhumiwa ili uchunguzi ufanyike dhidi yao.

Akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi uliopita, IGP Mangu alisema ni lazima Jeshi la polisi lichukue hatua kali dhidi ya yeyote atakayebainika kujihusisha na vitendo hivyo, hata kama ni Askari.

"Jeshi la Polisi linachukua hatua madhubuti za kuwachunguza Askari na Wasanii wote waliotuhumiwa na baada ya uchunguzi kumamilika hatua za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakayethibitika kwa uhalifu huo" alisema IGP Mangu.
 
Pia IGP Mangu ameiomba jamii kuendelea kutoa taarifa za uhalifu wa aina yeyote ili nchi iendelee kuwa salama. Hapo chini ni Majina ya Askari wanaotuhumiwa kujihusisha na biashara ya Madawa ya kulevya, ambao wamesimamishwa kazi.

CCM Yabadili Gia Angani

$
0
0
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema chama hicho siku ya kesho tarehe 5 mwezi wa pili kitakuwa kikitimiza miaka 40 toka kimezaliwa, kimefanya mabadiliko katika kusherehekea siku hiyo kwa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii

Polepole amesema toka chama hicho kimeanzishwa kimekuwa ni chama cha wananchama na chama ambacho kinashughulika na masuala ya watu watu pamoja na matatizo yao, hivyo mwaka huu wameamua kusherehekea siku hiyo kwa namna tofauti kwani hawatukuwa na sherehe kama desturi yao bali watasherehekea kwa kushiriki shuguli za kijamii.

"Maadhimisho ya mwaka huu yatakuwa tofauti kidesturi kama ambavyo yamefanyika hapo mwanzoni hivyo hatutakuwa na sherehe kama ilivyodesturi ya mikutano mikubwa ya hadhara , kwa maana ya uzinduzi na kilele isipokuwa mwaka huu tutafanya shughuli za maadhimisho ya CCM kwa namna kuu mbili, moja ni kwa kushiriki shughuli za kijamii, shughuli ambazo moja kwa moja zinagusa maisha ya watu wetu, jambo la pili ni mikutano ya ndani na hapa wanachama wote wa CCM watashiriki mikutano ya ndani kuanzia mikoa, ngazi ya wilaya, ngazi za majimbo, ngazi za kata na ngazi za matawi kwa kushirikisha mashina yetu kote nchini Tanzania."

Mbali na hilo Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole amesema kuwa maadhimisho ya miaka 40 ya CCM kwa mwaka huu yatafanyika kwa mwaka mzima huu wa 2017.

Ikumbukwe kuwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kilizaliwa tarehe 5 Februari, 1977 kutokana na kuvunjwa kwa vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) na Afro-Shirazi Party (ASP).

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya February 5

Mawaziri: Mageuzi ya Rais Magufuli Yanazaa Matunda

$
0
0
Dodoma, Jumamosi, 4 Februari, 2017
Serikali imesisitiza kuwa, utekelezaji wa Bajeti kwa kipindi cha robo ya kwanza yanaakisi dhamira ya kimageuzi iliyoanza kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano. 

Wakijibu hoja zilizotokana na mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti na maoni ya Wabunge Bungeni leo, Mawaziri wa sekta mbalimbali wamesisitiza kuwa kuna mabadiliko makubwa katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Dhamira ya Rais Iko Wazi
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mhe. January Makamba, amesema kuwa ikiwa ni miezi 15 tu madarakani, kuna mabadiliko makubwa katika kila eneo la utendaji wa Serikali ya Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli. Alisema hali hiyo inatokana na dhamira safi na ya wazi ya Mhe. Rais Magufuli kuenzi misingi aliyoiacha Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. 

Waziri Makamba amesema miezi 15 baadaye, na Bunge likiwa linajadili takwimu za robo ya kwanza tu ya Bajeti ya sasa, hata kama wapo watu ambao huenda wameumizwa na mageuzi yanayoendelea, kwa vyovyote vile, hakuna hoja wala ushahidi wa kulalamika kuwa nchi inarudi nyuma.

Biashara Zashamiri
Wizara ya Fedha imetoa takwimu kuonesha kuwa biashara nchini zinashamiri tofauti na baadhi ya watu wanaotumia takwimu za kufungwa kwa baadhi ya biashara hizo. Wakichangia hoja, Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Phillip Mpango na Naibu wake, Mhe. Dkt Ashatu Kijaji, wamefafanua kuwa mapato ya Serikali yameongezeka na hali ya biashara inakwenda vyema. 

Akifafanua kuhusu kushamiri kwa biashara nchini, Naibu Waziri Dkt. Ashatu amesema wakati takwimu zinaoonesha kuwepo kwa biashara 4,183 tu zilizofungwa, watanzania wengi zaidi wamefungua biashara. Amesema kuwa takribani biashara 139,554 zimefunguliwa katika mwaka mmoja uliopita. 

Idadi ya Watalii Yaongezeka
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Prof. Jumanne Maghembe amesema kuwa,ubunifu wa kodi mpya zilizoanzishwa na Serikali haujapunguza idadi ya wataliinchini. Alisema sekta hiyo inayochangia asimilia 17.5 ya pato la Taifa kwa mwaka
baada ya kuanza kukata kodi mpya ya ongezeko la thamani katika sekta hiyo. 

“Mheshimiwa Spika pamoja na Tanzania kuanza kutoza kodi hii mpaka sasa ninayofuraha kuwajulisha kuwa hatujaona ushahidi wa kodi hii kupunguza idadi ya watalii wanaokuja nchini,” alisema Prof. Maghembe.

Mfumo Mpya wa Mbolea
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhe. William Tate Ole-Nasha, amesema Serikali itaanzisha mfumo mpya utakaosaidia kuboresha upatikanaji na usambazaji wa mbolea nchini. 

Amedokeza kuwa, katika mfumo mpya, Serikali itaanza kununua mbolea kwa ununuzi wa pamoja kama ilivyo katika ununuzi wa mafuta. Ameongeza kuwa pia Serikali imebaini changamoto ya kuwepo kwa tozo nyingi katika sekta ya kilimo na kuahidi kuwa itawasilisha Bungeni hoja ya kupunguza baadhi ya kodi hizo. 

Imetolewa na:
Idara ya Habari-MAELEZO.

Hivi Ndivyo CCM Ilivyosherehekea Miaka 40 Ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ya Longido Kata Ya Namanga.

$
0
0
Katika kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Sherehe  ya Kutimiza Miaka 40 ya Chama Cha Mapinduzi,  Wanaccm Wilaya ya Longido Kata ya Namanga Jana tar. 04/02/2017 Wamekutana na kufanya Shughuli za Jamii ikiwemo kufanya Usafi wa Mazingira Katika Hospitali ya Serikali iliyopo Kata ya Namanga.

Aidha Juzi pia waliwatembelea watoto Yatima Wanaolelewa na kituo Cha Masai Foundation Kata ya Namanga Chini ya Msimamizi wake  Mama Kabati. 

Waliweza kutoa  msaada wa vitu mbalimbali vya kuwasaidia watoto hao ikiwemo chakula. Wanaccm hao kupitia Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Mama Esuphati Naikara alisema CCM inatambua Changamoto mbalimbali zinazowakabili Watoto Yatima Wanaolelewa na Vituo Vya Watoto Yatima hivyo  wameamua Kwa Umoja weo  kuwasaidia wanyonge hao.

"Leo katika Kumbukumbu tunawakumbuka Waasisi wa CCM Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Hayati Mzee Aboud Jumbe ( Mungu azidi kuwarehemu na Kupumzisha Roho zao kwa Amani ) Kwa Mchango wao Mkubwa ktk Kuunda CCM Imara & Madhubuti ambayo Leo inaongozwa na  Mzee wa Hapa Kazi tu Mwenyekiti CCM Taifa na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania Mh.  Dkt. John Pombe Magufuli ambaye ni Mchapa Kazi hodari kwelikweli, Mwenye Mapenzi mema na Nchi yetu, Mwenye kutetea Wanyonge,  Mwenye nia ya dhati ya Kuwatumikia Watanzania..Watanzania & Wanaccm kwa Ujumla  tunampongeza sana na Kumuombea kwa Mungu azidi kumlinda ili akatuongoze vyema."Alisema  Katibu wa CCM Wilaya ya Longido Mama Esuphati Naikara

Katika Hatua nyingine Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg.Robert PJN Kaseko amekabidhi Kiasi Cha Tsh. 100,000/= Kwa Katibu wa CCM Kata ya Namanga Ndg. Moody S.Jumaa Kwa ajili ya Chama hicho Cha Mapinduzi ili Kuwawezesha Viongozi Kutimiza Majukumu yao vizuri ya Ujenzi wa Chama. Fedha imepokelewa  Mbele ya Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Longido Ndg.Laraposh Laizer na Wanaccm.

CCM Hoyeeeeeeeeeeee. Kidumu Chama Cha Mapinduzi. 
Wana CCM Wilaya ya Longido Kata ya Namanga wakifanya Usafi wa Mazingira Katika Hospitali ya Serikali iliyopo Kata ya Namanga Jana. 

Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg.Robert PJN Kaseko akikabidhi Pesa Kiasi Cha Tsh. 100,000/= Kwa ajili ya CCM ili Kuwawezesha Viongozi Kutimiza Majukumu yao vizuri ya Ujenzi wa Chama.

Wanaccm Wilaya ya Longido Wakiwa katika picha ya Pamoja na watoto Yatima Wanaolelewa na kituo Cha Maasai Foundation Kata ya Namanga. 


Wana CCM Wilaya ya Longido Kata ya Namanga wakiwa katika Picha ya Pamoja Baada ya Kufanya Usafi wa Mazingira Katika Hospitali ya Serikali iliyopo Kata ya Namanga Wilayani Longido. 
 
 

Kamanda Sirro: Wema Sepetu, Nyandu Tozzy na TID bado wanashikiliwa na jeshi la polisi

$
0
0
Wakati macho na masikio ya Watanzania wakisubiri kusikia hatma ya wasanii wanaodaiwa kujihusisha na dawa za kulevya, wasanii wanne waliofika Kituo Kikuu cha Polisi bado wanashikiliwa na jeshi hilo kwa mahojiano zaidi.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro amesema kuwa bado wasanii hao Wema Sepetu, Dogo Hamidu, Khalid Mohamed (TID), na mtangazaji maarufu wa Clouds TV Babuu wa Kitaa bado wanashikiliwa na jeshi hilo.

“Bado tunawashikilia kwa mahojiano zaidi,” amesema Sirro kwa kifupi.

Wasanii wengine waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ambao wanatakiwa kufika kituoni Jumatatu ni Vanessa Mdee, Tunda na watu wengine Halidali Kavila, Amani, Kashozi na Omry Sanga.

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images