Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mwanamke Atoa Tangazo Gazetini Baada ya Kugundua Mumewe Anachepuka Nje ya Ndoa

$
0
0
Mtandao wa TUKO umeripoti kuhusu huyu Mwanamke aliyewaaacha wengi na mshangao baada ya kutumia njia isiyo ya kawaida kumzuia mumewe kuchepuka na kuchukua Mwanamke mwingine.

Mwanamke huyo Mkenya aliyetambulika kwa jina la Wanjiru Kamami ama Shiro alichapisha tangazo kwenye gazeti moja la Kenya akitaka kujuzwa habari na yeyote atakayemwona mumewe akiwa na ‘mpango wa kando’ au Mchepuko.

Katika kitendo cha Mwanamke huyo kuonyesha kwamba yuko serious akaamua kuandika na jina la mume wake pamoja na namba ya simu kwenye hilo tangazo lililosomeka "Hii ni kuwajulisha kwamba huyu aliye kwenye picha ni Mume wa Wanjiru Kamami toka mwaka 1982

"Ukimuona anadanganya Wasichana wa shule, Wanawake wengine au kina mama wa sokoni, mwambie aende nyumbani kwa mke wake au piga simu au sms kwenye 0751 993 571"

Bunge Lapitisha Muswada wa Sheria Kuwasaidia Wasio na Uwezo wa Kuwalipa Mawakili

$
0
0
Hatima ya wasaidizi wa kisheria pamoja na huduma ya msaada wa kisheria kwa watu wasiokuwa na uwezo wa kumudu gharama za mawakili, sasa iko mikononi mwa Rais John Magufuli, baada ya Bunge kupitisha bila pingamizi Muswada wa Sheria ya Huduma ya Msaada wa Kisheria wa mwaka 2016.

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe aliwasilisha muswada huo bungeni mjini Dodoma juzi wenye lengo la kuwa sheria itakayosimamia na kuratibu utoaji wa huduma ya msaada wa kisheria kwa watu wasiokuwa na uwezo, kuwatambua wasaidizi wa kisheria na mambo mengine yanayohusu utoaji wa msaada wa kisheria nchini.

Wakati akitoa majumuisho waziri huyo, alikubali kuufanyia marekebisho baadhi ya vifungu vya muswada huo baada ya kupokea maoni na ushauri kutoka kwa wabunge mbalimbali ikiwemo Kambi ya Upinzani.

Alisema muswada huo ukiwa sheria rasmi, utakuwa mkombozi kwa watanzania katika eneo la sheria, kwani wengi wao hawajui kusoma na kuandika, lakini pia wengi hawana uwezo wa kumudu gharama za kuajiri mawakili.

Alisisitiza kuwa sheria hiyo, itasaidia pia kupambana na kusaidia wale wote wanaoathirika na utekelezwaji wa mila na tamaduni potofu, zinazoendelea kutekelezwa nchini.

“Kuna mila na desturi zilizopitwa na wakati ambazo hazitambuliwi kisheria, lakini bado mila hizo zinatumika na kuumiza watu wengi sana kwa mfano masuala kama vile talaka, ndoa, watoto na mirathi haya ni mambo ambayo kupitia sheria hii yatakuwa na ahueni sasa,” alibainisha.

Alisema wananchi wengi wamekuwa wakikosa haki zao kisheria kutokana na kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya sheria; na mbaya zaidi sheria zilizopo, hazitambui kama mhusika ana uelewa gani wa kisheria.

Pamoja na kwamba, Dk Mwakyembe alichukua na kuyafanyia kazi baadhi ya maoni ya Kambi ya Upinzani, yaliyowasilishwa bungeni hapo juzi na Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Tundu Lissu, alikosoa namna mbunge huyo alivyotumia mifano ya Marekani katika suala zima la huduma ya msaada wa kisheria.

Alisema anasikitishwa na kitendo cha mbunge huyo, kuifanya Mahakama Kuu ya Marekani kuwa ni mfano wa kuigwa na Tanzania wakati mahakama hiyo ndio iliyokuwa inaongoza kwa muda mrefu tangu miaka ya 1800 hadi 1960 kukandamiza haki za watu weusi.

“Kwa muda mrefu kumekuwa watu humu ndani kazi yao ni ku google na kunukuu Kiingereza tu humu ndani bila kuangalia context. Kwa mfano kipindi alichotolea mfano mheshimiwa Lissu cha miaka 1800 kulikuwa na ubaguzi wa rangi wa kupindukia,” alisema.

Alisema mfano huo hauendani na hali halisi ya Tanzania, kwani nchi hiyo ilipata Uhuru tangu mwaka 1961 na kuanzia hapo, kila mtu akiwemo mhindi, mwarabu na mwafrika aliyepo nchini humo, alikuwa na uhuru hadi wa kupiga kura.

Alipendekeza wabunge kuhakikisha wanatumia mifano hai, inayoendana na hali halisi ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kutolea mifano ya wazee na waasisi waliopo. “Wapo akina Mkwawa na kina Kinjekitile, hawa wamezungumzia mengi kuhusu masuala ya haki,” alisema.

Ridhiwani Kikwete Afafanua Sakata la Diamond Kupewa Bendera Ya Taifa

$
0
0
Mwimbaji Mtanzania Diamond Platnumz alikabidhiwa bendera ya taifa na Waziri wa michezo na sanaa Nape Nnauye baada ya kualikwa kutumbuiza kwenye ufunguzi wa michuano ya soka ya Afrika 2017 kwenye taifa la Gabon.

Baada ya hapo Ridhiwani aliandika kuhusu timu ya taifa ya soka ambapo wengine waliitafsiri post yake kama amechukia Diamond kupewa bendera lakini leo kupitia The Beauty TV amehojiwa na kutoa ufafanuzi.

"Kwanza watu wanatakiwa kuelewa kwamba ile post haikuwa kwasababu ya Diamond na hata ukisoma kwenye maandishi yangu hakuna sehemu Diamond ametajwa isipokua msg iliyo pale inaweza kuwa inamgusa Diamond.

"Kilichonifanya niandike ile msg ni ule wivu wa kuona kwamba mashindano yanayokwenda kufanyika ni ya mpira wa miguu, sisi tunayo timu ya taifa ya mpira wa miguu lakini kilichotushangaza badala ya kutoa bendera kwa timu ya mpira wa miguu tunawapa Waburudishaji kina Diamond

"Matarajio yetu sisi watu wa mpira ni kuona Nahodha wa timu ya taifa akipokea Bendera, aliyepaswa kupokea bendera ni captain wa timu ya taifa……. hii pia lakini ni kuwapa changamoto TFF, je wao wanashangilia kuona Diamond amepewa bendera?

"Mtazamo wangu mkubwa ulijikita huko na sio mtazamo wa kwamba Diamond sijui nani………. NO NO… Diamond yeye nampongeza sana kwa hatua aliyofika, anafanya kazi nzuri na ndio maana watu wamemuona wamempa nafasi ya kwenda kutumbuiza lakini kikubwa ni nini ajenda kubwa Gabon? ajenda ni mpira wa miguu.

"Diamond sio mcheza mpira wa miguu, hata kama anashabiki atakua ni mshabiki tu…. sisi kama Mashabiki  wa soka tunaona wenzetu wanajiandaa kuhakikisha timu zao zinafuzu kwenda kucheza katika hatua ile, sisi kwetu tunaandaa Wanamuziki kwenda kuburudisha, ni jambo la kusikitisha sana"

Mkuu wa Mkoa Amgomea Waziri Maghembe

$
0
0
Uamuzi uliofanywa wiki iliyopita na Waziri wa Maliasili na Utalii, Professa Jumanne Maghembe wa kuagiza kuendelea mchakato wa kulitenga eneo la pori tengefu la Loliondo umepingwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Badala yake, RC Gambo ameagiza Kamati ya wataalamu iliyoundwa kwa maelekezo ya Waziri Mkuu, Khasimu Majaliwa inayochunguza chanzo cha mgogoro wa Loliondo iendelee na kazi iliyopewa na hatimaye itoe mapendekezo yake ya namna ya kumaliza mgogoro huo uliodumu kwa miongo miwili.

Gumbo alikuwa akizungumza jana katika mkutano wa wadau wa vyombo vya habari   katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

Alisema hakuna kiongozi yeyote mwenye mamlaka ya kukosoa au kusimamisha maagizo ya Waziri Mkuu isipokuwa Makamu wa Rais na Rais. 

RC Gumbo alionekana dhahiri kuwa amekerwa na kukasirishwa na uamuzi wa Waziri Maghembe wa kufanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Loliondo na   kutoa maagizo ya kugawa eneo la kilometa za mraba 1500  kuokoa Hifadhi ya Serengeti.

Alisema uamuzi uliotolewa na waziri  huyo ni ushauri kwa kamati yake na jambo linalozusha sintofahamu juu ya mwenye mamlaka zaidi kati ya Waziri na Mkuu wa Mkoa . 

“Hakuna kiongozi mwingine yeyote mwenye kukosoa maagizo au maelekezo ya Waziri Mkuu isipokuwa Makamu wa Rais na Rais.

“Sisi kauli ya waziri tunaichukulia kama ushauri ambao unaweza kutolewa na mwananchi yeyote, ” alisema.

Alisema ni lazima kamati ya wataalamu aliyoundwa ikamilishe kazi yake ikiwa ni pamoja na kujiridhisha kuhusu mipaka, vyanzo vya maji, maeneo ya ufugaji, uhifadhi, mipaka ya vijiji na hatimaye  kuwasilisha mapendekezo yake serikalini   yafanyiwe kazi na si vinginevyo.

Mkuu huyo wa Mkoa alishangazwa na uelewa na umakini wa Wizara ya Maliasili na Utalii katika kulitambua na kufuatilia eneo la pori tengefu.

RC Gumbo alisema inaelekea  wataalamu wa wizara hawana uelewa wowote kuhusu kinachoendelea Loliondo.

“Wizara inazungumzia pori tengefu lakini tayari kuna mji pale, hata eneo la kilometa za mraba 1500 wanazosema tumewauliza inaanzia wapi na kuishia wapi hawajui.

"Hata aliyechora ramani naye hajui mipaka ndiyo maana nasema tuache kamati imalize kazi yake," alisema.

Mbunge Ahoji Viongozi wa Kisiasa Kuvaa Sare za JWTZ

$
0
0
Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amesema kitendo cha makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya kuvaa sare za Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakati wa utekelezaji wa majukumu yao, ni kinyume na Katiba ya nchi na kwamba ni dalili ya nchi kuendeshwa kijeshi.

Tangu alipoapishwa Novemba 5 mwaka juzi, Rais John Magufuli amekuwa na utaratibu wa kuteua maofisa JWTZ katika nyadhifa mbalimbali jambo ambalo wabunge wa Upinzani wamekuwa wakilipinga mara kwa mara.

Waitara alitoa kauli hiyo bungeni jana wakati akiomba Mwongozo, baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu, akisisitiza kuwa wanajeshi hao kufanya shughuli za kisiasa si sawa.

Huku akitumia kanuni ya Bunge ya 68 (7) na kurejea taarifa ya habari ya Shirika la Utangazaji (TBC) alisema: “Wakati naangalia taarifa ya habari nikamwona Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Meja Milanzi (Meja Jenerali, Gaudence) akifanya shughuli zake huku amevaa kijeshi kinyume cha Ibara ya 147 ya Katiba yetu.”

Baada ya kikao cha Bunge kuahirishwa saa 7 mchana, Waitara alisema kuwa ni kawaida kwa wateule wa Rais kuvaa sare hizo na kusisitiza: “Wakuu wa mikoa ni wanasiasa na ndani ya CCM ni wajumbe wa kamati za siasa za mikoa. Mkuu wa Wilaya ni mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya, sasa wanaanzaje kuvaa au kujihusisha na mavazi ya kijeshi?”

Akiwa bungeni, Waitara alisisitiza kuwa siku za karibuni Mkuu wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndaga naye alionekana akifanya shughuli zake huku amevaa sare hizo.

“Ukisoma Katiba pamoja na mambo mengine, inapiga marufuku wanajeshi kujihusisha na siasa. Hawa viongozi wanaovaa nguo za kijeshi wanawatisha wananchi wanapokwenda kusikiliza matatizo,” alisema.

Ibara ya 147 (3) inasema: “Itakuwa marufuku kwa mwanajeshi kujiunga na chama chochote cha siasa, isipokuwa tu kama atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii”.

Mbunge huyo alihoji: “Inakuwaje wengine wanavaa sare za Jeshi na vyeo juu wakati wamestaafu?”

Akijibu Mwongozo huo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alisema kwa mujibu wa kanuni ambayo Mbunge huyo aliombea Mwongozo, hoja aliyotoa ni suala ambalo halijatokea ndani ya Bunge wakati likiendelea na shughuli zake, hivyo asingeweza kutoa majibu yoyote.

Wakuu Wa Shule za Dar Ambazo Zimeshika Mkia Matokeo Kidato cha Nne Watumbuliwa

$
0
0
Matokeo ya mtihani wa kidato cha nne  kwama 2016 yametoka na miongoni mwa Shule 10 zenye Wanafunzi waliofeli zaidi Tanzania, 6 zinatoka Dar es salaam na hiyo imemfanya Mkuu wa wilaya ya kigamboni Hashim Mgandilwa kufanya uchunguzi kwenye hizo shule.

Baada ya uchunguzi wake Mkuu huyu wa wilaya ameagiza kushushwa vyeo kwa Wakuu wa shule mbili za za Sekondari ambazo ni Kidete na Somangila Day na ametoa sababu mbili za kuchukua uamuzi huo.

Amesema sababu ya kwanza ni kufelisha na pili kuna mmoja amepata ukuu wa shule katika namna ambayo ina ukakasi na inaonekana kwa namna moja ama nyingine kuna Watu walimtengenezea kukipata hicho cheo

"Hiyo ilileta mvutano shuleni na baadhi ya Walimu walimuunga mkono na wengine hawakumuunga mkono hivyo ikasababisha Walimu takribani 7 kuihama shule hiyo kwa muda wa miezi miwili hadi mitatu." Amesema  DC Mgandilwa

Miiko Elfu Moja Na Moja( 1001) Ya Wafu

$
0
0
Msimuliaji :  Dokta. mungu  wa  kabili …….0744 000  473
Asalaam Aleykum Ndugu zanguni.  Habari za mwaka mpya  wa  2017.

Ni matumaini yangu kuwa Mwenyezi Mungu amewavusha salama.

Niende  kwenye  mada  ya  leo, Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikipata kesi za watu ambao nikiwatazama katika jicho la rohoni, nagundua ya kwamba, matatizo yao yanahusiana moja kwa moja na kutofuata ama kutozingatia miiko ya jinsi ya kushughulika na  habari  za  wafu.

Ninapo zungumzia  habari  za   wafu, namaanisha   masuala yoote yanayo husiana na wafu, kuanzia makaburi, maiti, vyumba vya kuhifadhia maiti, taratibu za kumuandaa na kumuosha marehemu, taratibu za maziko na mazishi, taratibu  za  matanga & maombolezo,  nguo za marehemu, masuala ya mirathi ya marehemu, jinsi ya kuishi na yatima walio achwa na marehemu, mke au wake za marehemu , mali za marehemu nakadhalika.

Watu wengi wana pata nuksi, mikosi au hata vifo visivyo vyao, kwa sababu ya kutozingatia taratibu za namna ya kushughulika na wafu.

Somo hili lina muhusu kila mmoja wetu, kwa  sababu  kila  mtu  anaweza  kupata  msiba  wa  ndugu, jamaa  au  rafiki  wakati  wowote  ule.

Pamoja  na  kwamba, hakunaga  mtu  mwenye  uzoefu  wa  kufiwa. ( Yaani  kuzoefu  uchungu  wa  kufiwa  kwa  sababu  umeshapata  misiba  mizito mingi ), lakini  linapokuja  suala  la  kufahamu  kuhusu  miiko  na  taratibu za  namna  ya  kushughulika  na  habari  za  wafu, kila  mtu  anapaswa kuwa  na  uzoefu   wa  kutosha, kwa  sababu  msiba  unaweza  kuja  wakati wowote.

Ni muhimu sana kujua taratibu na miiko ya namna ya kushughulika na habari za wafu ili usije kupata madhara yasiyo ya lazima, kwa sababu ya kutokujua nini cha kufanya pale unapokuwa una shughulika na habari za wafu.

Kwa bahati mbaya sana, nyakati za siku hizi hata watu wazima nao hawajui namna ya kushughulika na habari za wafu. Kupitia mfululizo wa makala haya, nitakuwa nikielezea kuhusu miiko mbalimbali ya namna ya kushughulika na habari za wafu.

 Fuatilia makala haya mwanzo hadi mwisho, ili upate kuzijua taratibu hizo na hivyo kujiepusha na madhara mbalimbali yanayo weza kukupata kutokana na kutokujua kwako.

1. KAMA UMEJIFUNGUA MTOTO AMBAE AMEZALIWA AKIWA AMESHA KUFA TAYARI

Moja kati ya mambo ambayo unapaswa kuwa nayo makini sana, ni  pale unapokuwa una shughulika na mazishi ya kichanga, hususani kile kilicho zaliwa kikiwa kimekufa tayari.

Hii ni kwa sababu, maiti ya vichanga, pamoja na eneo vinapozikwa vitoto vichanga ni hazina kubwa sana katika ulimwengu wa wachawi na walozi.

Katika ulimwengu wa wachawi na walozi, watoto wachanga walio zaliwa wakiwa wamekufa tayari, hujulikana kama “ WATU WALIO PITA DUNIANI BILA KUONEKANA” .

Wachawi wanapo sikia mwanamke amejifungua kitoto kichanga kikiwa kimefariki dunia, hukusanyika na kufanya karamu kubwa ya kichawi, kwa sababu , maiti ya kitoto kichanga kilicho zaliwa kikiwa kimefariki dunia, ina maana kubwa sana  katika shughuli zao.

Wachawi hutumia vitovu vya watoto wachanga walio zaliwa wakiwa wamekufa, kama malighafi ya kutengeneza aina mbalimbali za ndumba za kichawi, mfano; kutengeneza ndumba ya kuwafanya wasionekane na maadui zao, kutengeneza uchawi wa kuiba na kufunika nyota ya mtu au biashara ya mtu na kumfanya mtu huyo pamoja na biashara yake visonekane hadi anaingia kaburini, kutengeneza mafuta yajulikanayo kama mafuta ya usiku, ambayo hutumiwa na wafanyabiashara hasa wafanya biashara ndogo ndogo katika kuvuta wateja kwenye biashara, kutengeneza filimbi ya kichawi ambayo hutumika kuwaita wachawi kwenye mikutano yao ya kichawi.

Wachawi hutumia kufanya matambiko mazito kwenye makaburi yaliyo tumika kuzika vitoto vichanga ambayo mara nyingi huwa yanakuwa majumbani.

Matambiko hayo ya kichawi, huwa na madhara makubwa sana kwa watu wanaoishi katika nyumba hiyo, hususani wazazi pamoja na ndugu wa hicho kichanga.

Endapo wachawi watafanikiwa kutumia katika  shughuli zao za kichawi, maiti ya kichanga kilicho zaliwa kikiwa kimekufa, mabalaa, nuksi na mikosi mbalimbali itaiandama familia ya kichanga hicho, kwa sababu moja kati ya maunizi yanayo fanywa na wachawi, huwa ni pamoja na kuwatupia mikosi wazazi wa kichanga hicho, hususani mama wa kichanga hicho.

 Wachawi watatumia tambiko la kitoto hicho kichanga kama lango la kichawi la kuingia katika familia ya wazazi wa kitoto hicho na kuifanya kama watakavyo.

Moja kati ya dalili kwamba, wachawi wametumia  katika shughuli zao za kichawi, kitoto chako kilicho zaliwa kikiwa kimekufa, ni pamoja na kutopata ujauzito , kubeba mimba zinazochoropoka, au kuendelea kuzaa vitoto vilivyo kufa, katika kila ujauzito unao upata.

NINI CHA KUFANYA : 1. Kwanza unapokuwa mjamzito unatakiwa kuchukua tahadhari ya hali ya juu sana ili kuepuka kuzaa kitoto ambacho kimekufa, kwa sababu wachawi huwa wanawafunga wanawake wajawazito wajifungue vitoto vilivyo kufa ili waweze kuvitumia katika mambo yao ya kichawi.

Hivyo unapokuwa na mke mjamzito, hakikisha unampa kinga madhubuti ambayo itawazuia wachawi kumfunga na kusababisha kichanga hicho kisicho na hatia, kuzaliwa kikiwa kimepoteza maisha. 2. Kama tayari umejifungua kitoto ambacho kimezaliwa kikiwa kimeshakufa, unatakiwa ufuate taratibu maalumu za kukifanyia maziko maalumu, pamoja na wewe mwenyewe kufanyiwa tambiko maalumu la kukusafisha na kukukinga dhidi ya jambo  kama hilo, katika siku zako zijazo.

Taratibu za maziko ya vitoto vichanga vilivyo zaliwa vikiwa vimekufa, zinategemea na mambo makuu yafuatayo : jinsia ya mtoto, siku aliyo zaliwa mtoto, mtoto amezaliwa peke ake au wamezaliwa mapacha, kama ni mapacha wamekufa wote au mmoja amepona, na kama mmoja amepona, zipo pia taratibu za namna ya kumfanyia tambiko na ibada maalumu ili kumuepusha na jicho la maadui wa kichawi.

Kitu kingine, inategemea na mtoto aliyezaliwa ni NZAO ama UZAO wa ngapi wa mwanamke aliye jifungua. Kama ni uzao wa kwanza, kuna taratibu zake, na kama ni uzao wa mwisho kuna taratibu zake pia.

Taratibu hizi zisipo fuatwa, basi madhara makubwa sana yatatokea kwa familia husika.

2. KAMA MAMA AMEFARIKI NA MTOTO AMEBAKI HAI

Kama utapatwa na mtihani huu, unapaswa kuwa makini sana na kuzingatia taratibu na kanuni za kufuata.

Ninaposema kuwa makini namaanisha uwe makini kwelikweli, kwa sababu wachawi wana siri kubwa sana na mwanamke aliye jifungua na kufariki dunia.

Kuwa makini sana na watu watakao enda kuuosha mwili wa mke wako ,au dada yako n.k ambae amefariki wakati anajifungua, kwani baadhi yao watakuwemo wachawi ama mawakala wa wachawi ambao watachukua baadhi ya vitu vya mke wako na kwenda kuviuza kwa wachawi.

Vitu hivyo ni pamoja na nywele, nywele za sehemu za siri, kucha, na maji yaliyo tumika kumuoshea.

Vitu hivyo hutumiwa na wachawi kutengeneza ndumba za aina mbalimbali, kama vile kuwafunga wanafunzi wanao soma, wafanyakazi, wafanya biashara nakadhalika.

3. KAMA MAMA NA MTOTO WOTE WAMEFARIKI:

 Kama kwa bakti mbaya umepatwa na mtihani mzito kama huu, unapaswa kuwa makini na kuchukua tahadhari kama ilivyo elezwa hapo juu.

4. KAMA NDUGU YAKO ALIYE FARIKI ALIKUWA KICHAA AU MWENDAWAZIMU

Kama ndugu yako aliyefariki alikuwa kichaa au mwendawazimu wakati wa uhai wake na alifariki dunia akiwa katika hali hiyo unapaswa kuzingatia yafatayo :

Kwanza maiti yake isilale ndani. Itoke moja kwa moja mochwari hadi makaburini. Nguo zake zote zichomwe moto siku ya saba baada ya maziko.

Kuweni makini sana na watu watakao enda kuosha mwili wake.

Ikiwezekana awepo mwanafamilia anae aminika, wakati wa zoezi la kuuosha mwili wa ndugu yenu, kwa sababu watu walio kufa wakiwa wendawazimu ni hazina kubwa sana kwa wachawi, kuanzia sehemu za miili yao, hususani nywele na kucha, nywele za siri , sanda iliyo tumika kuwavisha, nguo  walizokuwa  wamevaa  wakati  wa  kupatwa  na  umauti pamoja na kaburi lililo tumika kuwazika.

Wachawi hutumia vitu hivyo katika kutengeneza uchawi na ulozi wa aina mbalimbali.

 Kwa mfano, nywele za marehemu ambae alikuwa mwendawazimu wa jinsia ya kiume, hutumika kutengeneza ndumba ya kichawi ya kumtuliza kimapenzi mwanaume na kumfanya awe kama mwendawazimu kwa mwanamke aliye mfanyia uchawi huo.

Vivyo hivyo, nywele za mwanamke aliyefariki akiwa mwendawazimu hutumika kutengeneza uchawi wa kuwapumbaza wanawake kimapenzi na kuwafanya kuwa kama wendawazimu kwa waume zao.

Kama hiyo haitoshi, wachawi huchukua nywele za marehemu mwendawazimu wa kiume, huchanganya na nywele za mwendawazimu mwanamke, nywele za mtu aliyekufa akiwa msukule, mafuta ya msukule pamoja na ndumba nzingine, ili kutengeneza uchawi wa kuwapumbaza na kuwafunga wafanyakazi hususani wale wanao fanya kazi kwenye kampuni za watu binafsi.

Uchawi huu hutumiwa sana na matajiri wanao miliki maduka, hoteli, migahawa  au kampuni zao binafsi.

Mtu aliye fanyiwa uchawi huu mara nyingi huwa na uwezo mkubwa na wa kipekee katika kazi yake, na bosi wake anakuwa hayupo tayari kupoteza huduma yake, basi anacho kifanya ni kumlisha uchawi huu na kumpumbaza katika maisha yake yote.

Vilevile, wachawi hutumia vitu vya mwendawazimu kutengeneza uchawi wa biashara hususani biashara ya chakula .

Mtu ukishakula tu chakula kilicho wekwa uchawi huu basi utakuwa kama mwendawazimu kwenye chakula cha kwenye mgahawa au hoteli hiyo.

Huwezi kula chakula sehemu nyingine yoyote ile isipokuwa kwenye mgahawa huo tu, hata yatokee mabadiliko gani.

Uchawi huu pia hutumiwa na wafanyabishara wa biashara nyinginezo kama vile nguo nakadhalika. Kumpumbaza mteja. Mteja huweza kununua nguo ambayo thamani yake ni sh elfu kumi, kwa shilingi laki moja.

Uchawi huo ndio unao tumiwa sana na akina dada katika kuwapumbaza wanaume na kuwafanya wawape kila kitu wanacho kitaka. Endapo utaruhusu wachawi watumie vitu vya marehemu ndugu yenu ambae amefariki akiwa mwendawazimu, basi mikosi na mabalaa makubwa yataiandama familia yenu.

5. KAMA NDUGU YAKO ALIYE FARIKI ALIKUWA KIPOFU !

Unapaswa kuwa makini sana, pale unapopatwa na msiba wa ndugu yako wa damu ambae alikuwa na ulemavu wa kutokuona yaani kipofu.

Hii ni kwa sababu wachawi wanaweza kutumia katika shughuli zao za kichawi baadhi ya vitu vya ndugu yenu na matokeo yake kuiacha familia yenu ikiwa kwenye mabalaa na mikosi isiyo elezeka.

Kuweni makini sana na aina ya watu watakao pewa jukumu la kuosha mwili wa ndugu yenu.

Nawashauri badala ya kuwapa kazi hiyo watu wa mochwari, ifanye ninyi wenyewe ili kuhakikisha kuwa hakuna ufisadi wowote unao fanyika hapo.

 Kwani endapo hamtafanya hivyo, basi mtatoa nafasi kwa wachawi pamoja na wakala wao kuchukua baadhi ya vitu vya ndugu yenu huyo kwa ajili ya kufanya shughuli zao za kichawi.

Vitu hivyo ni pamoja na nywele, nyusi,nywele za siri,kucha, nguo alizokuwa amezivaa marehemu wakati anaaga dunia, kama alikuwa anatumia gongo la mti, nalo ni dili kubwa sana kwa wachawi, maji yaliyo tumika kumuosha nakadhalika.

Pamoja na mambo mengine, vitu vya marehemu ambae wakati wa uhai wake alikuwa na ulemavu wa kuona yaani upofu ( Hasa Yule aliye zaliwa na upofu ), hutumiwa na wachawi kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile uchawi wa kuwafunga maadui zako wasi kuone, uchawi wa mapenzi kumfanya mpenzi wako asimuone mtu mwingine yoyote Yule isipokuwa wewe tu, kufunga nyota ya mtu isionekane na yoyote Yule. Kwenye kaburi la marehemu aliyekuwa na ulemavu wa kuona, hufanyika tambiko la kuzika na kufunga kesi, kuifanya isionekane.

Pia vitu hivyo hutumika kuwaloga wanawake wajawazito kuzaa watoto wenye ulemavu wa macho

6. KAMA NDUGU ALIYE KUFA ALIKUWA NA ULEMAVU WA KUTOSIKIA :

Wachawi hutumia vitu vya mtu aliye fariki ambae wakati wa uhai wake alikuwa na ulemavu wa kusikia, kutengeneza uchawi wa aina mbalimbali kama vile; Mapenzi; kumfanya mpenzi asisikie jambo la mtu yoyote Yule, isipokuwa wewe tu, kumroga mtoto wa mtu kumfanya asiwasikie wazazi wake, kumroga mke au mume wa mtu kufanya asiwe na masikizano na mwenzi wake nakadhalika.

Vitu vinavyo tumika hapo ni pamoja na nywele, nyusi, kucha, nywele za siri, nguo zake, maji yalotumika kumwosha pamoja na kaburi lake.

Unapopatwa na msiba wa ndugu ambae wakati wa uhai wake alikuwa na tatizo la ulemavu wa kusikia, basi unapaswa kuwa makini sana.

7. KAMA NDUGU YENU AMEKUFA MAJI  : Kama mmepata taarifa kuhusu msiba wa ndugu yenu ambae amekufa maji, eidha alikuwa anaogelea, au amepata ajali kwenye mashua au jahazi au meli, zipo taratibu na miiko ya kufuata wakati wa maziko yake.

Moja ya miiko hiyo ni pamoja na “ msichimbe kaburi kabla hamjaupata mwili wa marehemu”.

Hakikisheni kwanza mmeupata mwili wake ndio mchimbe kaburi na kumzika kwa kufuata taratibu zote za kumzika mtu aliye fariki kwenye ajali ya maji.

 Msichimbe kaburi kabla hamjauona mwili wa marehemu. Endapo mtachimba kaburi kabla ya kuuona mwili wa marehemu halafu ikatokea bahati mbaya msiupate mwili wa marehemu, basi  kwanza, mmoja  kati  ya  ndugu  wa  karibu  katika  familia  ya  marehemu, atafariki  dunia ndani  ya  mwaka  huo  huo. Idadi  ya  ndugu  watakao  fariki  ndani  ya  mwaka  mmoja, itategemeana  na  idadi  ya  siku  ambazo  hilo  kaburi  limekaa  wazi.

Kama  hiyo  haitoshi, pili , mtakuwa mmewapa faida kubwa  sana  wachawi.

Wachawi wataenda kulitumia kaburi hilo kutengeneza uchawi mkubwa na wenye nguvu sana.

Makaburi ya namna hiyo hapa Afrika mashariki yapo machache sana, na yanapatikana zaidi nchini Congo DRC na Tanzania hususani kanda ya ziwa na kanda ya kusini katika mkoa wa Lindi.

 Kanda ya ziwa makaburi hayo yapo katika mikoa ya Mwanza, Shinyanga na Simiyu, na mengi kati yao ni yale ya wahanga wa ajali ya meli ya MV Bukoba ya mwaka 1996, ambapo mamia ya miili ya abiria waliokuwa kwenye meli hiyo haikuweza kupatikana, ilihali ndugu, jamaa na marafiki walisha chimba makaburi.

 Huko nchini Kongo, idadi kubwa ya makaburi hayo ni yale ya wale mabinti bikira, walio kufa kwenye ajali ya meli iliyotokea mto Kongo miaka ya 70.

Katika ajali hiyo hakuna, mwili uliopatikana hata mmoja na idadi kubwa ya ndugu, jamaa na marafiki wa mabinti hao ilikuwa tayari imeshachimba makaburi kwa ajili ya kuwahifadhi wapendwa wao hao. LAWAMA NYINGI KUHUSU AJALI HIYO ZILIELEKEZWA KWA ALIYE KUWA RAIS WA KONGO KIPINDI HICHO, MOBUTU SSESESEKO AKIDAIWA KUWATOA KAFARA MABINTI HAO KWA MAELEKEZO YA KAMATI YAKE YA UFUNDI ( Miiko yangu ya kazi, hainiruhusu kutoa maoni yangu kuhusu jambo hili )

8. MSICHIMBE KABURI HALAFU LIKALALA BILA KUZIKWA : Kaburi huwa halilali njaa, hakikisheni siku mtakayo chimba kaburi  hilo, iwe ndio siku mtakayo mzika marehemu wenu.

Kamwe msichimbe kaburi kabla mwili haujafika nyumbani.

Endapo mtakiuka jambo hilo, basi misiba itaiandama familia yenu kwa mwaka mzima.

Mtakuwa  mmeiunganisha  familia  yenu  na  kaburi  lililo  lala  wazi  kwa  hiyo  siku  moja. Tumbo la kaburi hilo  litadai malipo yake ya kulala bila chakula chake kwa siku nzima.

9. MSIACHE KABURI WAZI WAKATI MNAENDA KUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU

 Mkishamaliza kuchimba kaburi, msilitelekeze peke yake. Wekeni watu kadhaa wa kulinda kaburi ambao watakaa huko kaburini hadi pale mwili wa marehemu utakapo letwa kuzikwa.

10. MWANAMKE MJAMZITO ASIHUDHURIE MAZISHI Mwanamke mjamzito hatakiwi kuhudhuria kwenye maziko ( makaburini ).

Endapo atafanya hivyo basi, roho ya marehemu itamuingia mtoto aliyeko tumboni, na hivyo kusababisha bahati mbaya na mikosi kwa mwanamke huyo wakati wa kujifungua na endapo atajifungua salama, basi mtoto atakae zaliwa anaweza kupoteza uhai, au endapo ataishi basi, mama  huyo  atafariki  na  kumuacha  motto na  motto  atakuwa kwa taabu sana na ataandamwa na mikosi.

Kama itatokea mwanamke huyo akalazimika kuhudhuria kwenye mazishi ( Mfano labda aliyefariki ni mtu wake wa karibu sana kama vile mama yake,baba yake, mume wake, kaka yake, dada yake au mtoto wake ), basi anatakiwa ASITAZAME MWILI WA MAREHEMU wakati wa kuaga.

Endapo atafanya hivyo, basi ile roho ya marehemu itaishaishawishi roho ya mtoto aliyepo tumboni, kwenda kwenye nchi ya wafu, jambo ambalo litasababisha matatizo makubwa sana kwa mama wa mtoto wakati wa kujifungua.

Uwezekano wa kujifungua mtoto aliyefariki, utakuwa kwa asilimia mia.

11.  Unapopita kwenye eneo la makaburi mida ya saa saba mchana au saa moja usiku, usiache mdomo wako wazi wala kupiga miayo. Endapo utafanya hivyo, roho za wafu zitakuingia na kusababishia matatizo makubwa.

12. Mnapomzika marehemu, kichwa kiangalie upande wa magharibi na miguu iwe upande wa mashariki.

14. Mara tu kifo kinapotokea, kitu cha kwanza, unacho takiwa ni kuondoa ama kufunika picha na vioo vyote vilivyomo kwenye chumba alichopo marehemu. Ni nuksi kubwa sana kuacha taswira ya mwili wa marehemu ionekane kwenye kioo. Kama hiyo haitoshi, ni nuksi kubwa sana kutazama taswira yako kwenye kioo hicho, mpaka mwili wa marehemu uatakapo kuwa umeondolewa. Ukitaka kuamini ninacho kisema, jaribu kuingia na kioo kwenye chumba alimo lala marehemu halafu jitazame kwenye hicho kioo. Utakacho kiona, uje ukisimulie hapa.

15. Naweni mikono kwa dawa maalumu baada ya kubeba jeneza lenye mwili wa marehemu.

16. Oga dawa mara baada ya kutoka kaburini.

17.  Kama marehemu amefariki akiwa nyumbani, mnapoenda kuutoa mwili wake, miguu itangulie kutoka, kamwe msifanye kosa mkatanguliza kichwa.

18. Kama watu wawili katika nyumba moja, wanaumwa sana, halafu ikatokea mmoja wao akafariki dunia, basi hiyo ni ishara kwamba huyo mwingine atapata nafuu kubwa.

19. Kuna ndege mmoja anapatikana porini ( SIMTAJI KWA SABABU ZA KIMIIKO), ukichukua nyoya la huyo ndege halafu ukaliweka kwenye mto wa kitanda anacho lalia mgonjwa, basi mgonjwa huyo atakufa wala hatopona. Nyoya hilo hilo likiwekwa kwenye kitanda anacholalia mtoto mdogo, litamzuia mtoto huyo kukua.

20. Kitanda anacho lalia mgonjwa mahututi, kitazame mashariki na magharibi, na kamwe sio kaskazini na kusini. Kichwa kiangalie magharibi na miguu itazame mashariki.

21. Jina la mwisho kutajwa na marehemu wakati anakaribia kukata roho, litakuwa jina la mtu atakae fuatia kufa baada ya marehemu.

22. Endapo mtu anae karibia kukata roho, atakun’gata, basi na wewe utamfuata baada ya muda mfupi. Ili kujiepusha na kifo cha namna hiyo, basi unatakiwa na wewe umng’ate katika sehemu ile ile aliyo kun’gata.

23. Kama kiongozi wa familia atafariki dunia, basi mnatakiwa kusimamisha saa kubwa ya ukutani inayo kaa sebuleni, vinginevyo wanafamilia walio baki nao watamfuata ndani ya kipindi kichache, vitatokea vifo mfululizo vya wanafamilia.

24. Baada ya kuuosha mwili wa marehemu, na kuuvisha nguo zake, unatakiwa kuweka punje moja ya chumvi kwenye kifua cha marehemu ili kuwafukuza roho na majini wabaya.

25. Kama marehemu atakuwa akiwa ameacha macho wazi , hiyo ni ishara mbaya sana. Maana yake ni kwamba,anatafuta watu ( ndugu zake ) wa kwenda nae kaburini. Kujiepusha na hilo, funikeni macho yake kwa kutumia sarafu .

26.  Usifagie chumba cha marehemu kabla marehemu hajatolewa. Endapo utafanya hivyo, basi amini nakwambia wewe ndie utakae mfuata marehemu.

27.  Msitoe shuka wala nguo yoyote iliyopo kwenye kitanda alicho kilalia marehemu, na ambacho umauti ulimkuta. Endapo mtakiuka hilo, basi mwanafamilia mwingine atafariki ndani ya mwaka huo huo.

28. Endapo Kundi la wanandugu, jamaa na marafiki, mtaenda kuuchukua mwili wa marehemu halafu ghafla mkaona anatoa damu kwenye tundu za pua, basi mjue kuwa marehemu amekufa kwa mkono wa mtu, na aliye husika na kumuua, yu miongoni mwenu,ndani ya chumba hicho hicho.

29. Kwa mara nyingine tena narudia, mwili wa marehemu unapotolewa kwenye jengo lolote lile, iwe nyumbani, kanisani, au msikitini ni lazima miguu ndio itangulie kutoka na sio kichwa, vinginevyo roho au mzimu wa marehemu huyo, utatazama katika jengo hilo na kumuita mtu mwingine wa kufuatana nae.

30. Marehemu azikwe mahali alipo pachagua wakati wa uhai wake, au la sivyo endapo mtaenda kinyume chake, vifo vitatokea katika familia hiyo. Na kama mtalazimisha kusafirisha mwili wa marehemu, basi msafara huo lazima utapata ajali njiani, na mtu mmoja lazima atakufa.

31. Ukiugusa mwili wa marehemu, utakuwa na uhakika kwamba, roho ya marehemu haitakusumbua. Na endapo utaugusa mwili wa marehemu usoni, hutoota ndoto mbaya kuhusu marehemu huyo.

32. Usipeleke mwili malaloni kwa kutumia gari lako binafsi. Ni nuksi kubwa sana kufanya hivyo. Mwili wa marehemu unapelekwa malaloni kwa kutumia gari maalumu.

33. Endapo mtasafirisha mwili wa marehemu kwa basi, kichwa kitazame anapotoka na miguu itazame anapoelekea.

34. Usi hesabu magari kwenye maziko (makaburini), ukifanya hivyo unakuwa unahesabu siku zako mwenyewe za kuishi.

35. Kuwa muangalifu usione taswira yako kwenye gari lililo beba mwili wa marehemu, vinginevyo wewe ndio utakae fuatia kubebwa kwenye gari hilo.

36. Usiende na mtoto mchanga kwenye msiba, vinginevyo atakufa kabla hajatimiza mwaka mmoja.

37. Ni nuksi kubwa sana kutangulia makaburini ( kwenye maziko)  au kupita bila kushiriki kwenye maziko . Kama utafanya hivyo, utakufa ndani ya muda si mrefu.

38.  Kama paka mweusi atakatisha mbele wakati wa maziko (makaburini ) mwanafamilia mmoja katika familia ya marehemu atakufa ndani ya siku tatu.

39.  Kama ndugu yenu amekufa, kwa kuuwawa au mna wasiwasi kwamba ndugu yenu ameuwawa, basi mzikeni huku kichwa kikiwa kinatazama chini. Mtu aliye muua ndugu yenu, kama atakuwa kwenye eneo la maziko, basi hatoondoka eneo hilo hadi atakapo kamatwa. Watu wote wataondoka, lakini yeye atabaki, hapo hapo, atakuwa kama amepagawa  na kupigwa na bumbuwazi. Kama msiporudi kutazama hapo kaburini, basi hata siku tatu mtamkuta, na atakapo waona, basi ata tubu na mtafikisha kwenye vyombo vya dola.

Miaka ya sabini kushuka chini, babu zetu ilikuwa kama ndugu yao amekufa kwa kuuwawa ama kama wanahisi ndugu yao amekufa kwa kuuwawa, mfano amewekewa sumu, amenyongwa n.k,. basi walikuwa wanafanya hivi, wanatoa ini la marehemu, halafu wanazika ini sehemu tofauti na mwili wa marehemu, kwa kufanya tambiko maalumu. Ndani ya siku saba, mtu aliye muua marehemu, atapatikana katika eneo lililozikwa ini.

40.  Kaburi lilisale wazi, likilala wazi, basi mwanafamilia mwingine katika familia ya marehemu atafariki ndani ya mwaka huo huo. Kaburi lizikwe siku liliyo chimbwa.

41. Kaburi likilala wazi  siku ya Jumapili, basi jumapili itakayo fuata, mwanafamilia mwingine kutoka kwenye familia ya marehemu na yeye atamfuata marehemu.

42. Vifaa vilivyo tumika kuchimba kaburi, vinatakiwa vibakie kaburini kwa siku nyingine saba. Kuvipeleka nyumbani vifaa hivyo siku hiyo hiyo aun kabla ya siku saba, ni nuksi kubwa sana.

43. Kuondoka makaburini kabla kaburi lote halijafukiwa, kutasababisha msiba kwenye familia yako wewe uliye ondoka kabla watu hawajamaliza kuzika. Mvua ikinyesha kwenye kaburi ambalo bado halijafukiwa, ni ishara mbaya sana kwa familia ya wafiwa.  Ili  kuepukana  na  nuksi  hiyo, inabidi  kuwe  na  mtaalamu  wa  kuzuia  mvua.

44. Ni nuksi  kubwa  sana  kusonta  kaburi

45. Ni  nuksi  kubwa  sana kurukia  kwenye  kaburi

46. Ni  nuksi  kutembelea  makaburini  baada  ya  jua  kuzama

47. Wafiwa  wasiondoke  nyumbani  wala  kujichanganya  mtaani na watu  wengine, hadi  matanga  yatakapo  inuliwa. Kwa  mfano  watu wengine, unakuta  mtu  amefiwa, lakini  kabla  hata  matanga  hayajainuliwa, anakwenda  bar kunywa  na  kurudi  msibani. Hayo ni makosa  makubwa  sana.

48. Wafiwa wote  wakuu, yaani  ndugu  wa  karibu  wa  marehemu, wasioge  hadi  baada  ya  siku  tatu, ambayo  ndio  siku  ya  kuanua  matanga, na  maji  watakayo  oga  yawe  maji  ya  moto.

49. Wafiwa  wasishiriki  ngono  hadi  matanga  yatakapo  inuliwa.

50. Waombolezaji  msibani, wasiongee  kwa  nguvu  wala  kucheka  kwa  nguvu. Ni makosa  makubwa  sana  kufanya  hivyo.

Leo  tumekomea  miiko  50. Kama  kichwa  cha  maya  kinavyo  jieleza, MIIKO  ELFU MOJA  NA  MOJA YA  WAFU. Hivyo  basi, ili  kufahamu  kuhusu  miiko  mingine  iliyo  baki, tembelea  kila  siku:  www.mungwakabili.blogspot.com

Imesimuliwa  na   Dokta. mungu  wa  kabili. Anapatikana  kwa  simu  namba  0744 000  473

Agizo la Rais Magufuli latekelezwa, pikipiki 16 zatolewa matari kwa kupita barabara za mwendokasi

$
0
0
Agizo la Rais wa Jamuhuri ya Muungano Dr. John Pombe Magufuli la kulitaka jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani kung’oa matairi vyombo vyote vya moto vitakavyopita katika barabara za mabasi yaendayo haraka limeanza kutekelezwa kwa vitendo ambapo pikipiki kumi na sita zimeng’olewa matairi na wahusika wakitarajiwa kufikishwa mahakamani tarehe 2 Febuari mwaka huu.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alisema kuwa pikipiki hizo 16 zilizotolewa matairi ni sehemu tu ya nyingi zilizokamatwa huku akisema kuwa mkakati huo ni endelevu ambapo wote watakamatwa na kufikishwa mahakamani.

Rais Dkt Magufuli alitoa maagizo kwa askari kukamata magari na pikipiki zinazotumia barabara za mabasi yaendayo haraka na kisha kuzitoa matairi na madereva hao wafikishwe mahakamani. Rais Magufuli alisema madereva hao wakiuliza matairi yao yalipo, wajibiwe kuwa askari hawajaajiriwa kulinda matairi.

Waziri Mkuu: Rais Hajatangaza Kufutwa Kwa Vyama Vya Upinzani

$
0
0
 WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais, Dkt. John Magufuli hajawahi kutangaza ama kutoa kauli ya kufutwa kwa vyama vya siasa nchini.

Ametoa kauli hiyo leo (Februari, 2, 2017) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Freeman Mbowe  katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu.

Katika swali lake Mheshimiwa Mbowe alisema Rais Dkt.  Magufuli alinukuliwa akisema atahakikisha anafuta vyama vyama vya upinzani na ifikapo mwaka 2020 hakuna upinzani nchini.

Pia Mheshimiwa Mbowe alitaka kujua nini kauli ya Serikali kuhusu kunyimwa dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Mheshimiwa Godbless Lema ambaye anashikiliwa kwa muda miezi mitatu.

Mbali na Mheshimiwa Lema, pia kiongozi huyo alitaka kujua kuhusiana na kufungwa kwa Mbunge wa Kilombelo, Mheshimiwa Peter Lijualikali pamoja na madiwani sita wa chama hicho ambao wamefungwa na viongozi wengine 215 wanakabiliwa na kesi mbalimbali.

“Kwanza nataka nikanushe kwamba Mheshimiwa Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani. Pia Watanzania wote wanajua nchi hii inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu i,” amesema Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa “tunajua katika kuendesha nchi tunaendesha kwa mihimili mitatu ipo Serikali, Mahakama na Bunge na hakuna mhimili unaoweza kuuingilia mhimili mwingine,”.

“Pia Watanzania wote wanajua kwamba jambo lolote ambalo lipo Mahakamani haliwezi kuzungumzwa mahali pengine popote, hivyo siwezi kutumia nafasi hii kuzungumzia mambo yote yanayoendelea chini ya sheria na yaliyo mahakamani,” amesema.
Wakati huo huo; Waziri Mkuu amewahakikishia Watanzania kwamba suala la upungufu wa sukari halitatokea nchini kwa sababu viwanda vya ndani vinaendelea kuzalisha na hadi mwishoni mwa Januari vilifikia asilimia 86 ya uzalishaji.

“Hadi kufikia mwishoni mwa msimu wa uzalishaji ambao ni mwezi Machi, tunaweza kuwa tumefikia malengo na kama itajitokeza upungufu Serikali itatafuta namna nzuri ya kupata sukari kwa kushirikiana na wenye viwanda nchini,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akijibu swali la Mbunge wa Mvomero, Mheshimiwa Suleiman Sadiq aliyetaka kujua hali ya sukari ilivyo nchini kwa sasa na hatua gani zinazochukuliwa na Serikali ili kunusuru hali ya uhaba wa sukari isijitokeze.

Wema atajwa kuhusika na dawa za kulevya.....Mkuu wa Mkoa wa Dar Amtaka Aripoti Polisi. Pia Wamo Askari 9

$
0
0

Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ametajwa kuwa ni kati ya wasanii ambao wanatumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kesho kukutana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda katika kituo cha polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaama amewataja wasanii wengine akiwepo TID, Chid Benz, pamoja na Recho na kusema anahitaji kesho wafike makao makuu ya kituo cha polisi.

"Naomba tukutane kesho pale polisi Central akiwepo TID, akiwemo Wema Sepetu, wakiwepo wakina Junior Sniper, wakina Ditto, Titoo, kuna Ally Denya, kuna wakina Chacha, kuna kina Mecky wengine hawa wakina Petit Man tayari nishawatia mikononi mwa sheria, kuna watu kama kina Recho, Chid Benz wote hawa nawahitaji ni vijana wenzangu nafikiri tutaelewana vizuri" alisema Paul Makonda

Taarifa Ya Serikali Kutoka Bungeni Leo 02/02/2017

$
0
0
Dodoma, Alhamisi, 2 Februari, 2017: Serikali imetoa ufafanzi kuhusu masuala mbalimbali kuhusu utawala wa Sheria na kuainisha mikakati yake katika kuzuia au kupunguza athari za matetemeko ya ardhi nchini. Ufafanuzi huo umetolewa mjini hapa leo.

Serikali Kutoingilia Mihimili ya Dola
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesisitiza kuwa Serikali inaheshimu mgawanyo wa mihimili mitatu ya dola nchini. Waziri Mkuu alikuwa akifafanua kuhusu malalamiko kuwa baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa kesi zao zinachukua muda mrefu.

Aidha, Waziri Mkuu amekanusha vikali madai kuwa Serikali inakusudia au imetangaza kufuta vyama vya siasa hasa vya upinzani nchini madai yaliyotolewa na Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Bw. Freeman Mbowe.

 Mkakati Kuzuia Majanga Ya Asili
Akijibu hoja kuhusu mikakati ya kupambana na athari za majanga ya asili, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira), Anthony Mavunde, amesema Serikali tayari inao mkakati wa kitaifa wa kupambana na majanga ya asili yakiwemo matetemeko.

Aidha, Serikali imeandaa Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ambayo imeainisha aina mbalimbali za maafa ikiwemo tetemeko la ardhi pamoja na majukumu ya kila mdau katika kushughulikia maafa. Aliongeza kuwa, Serikali pia imeandaa Mwongozo wa Taifa wa Kukabiliana na Maafa ambao unaelekeza Taasisi kiongozi na wajibu wao wakati wa kukabiliana na majanga.

Liganga, Mchuchuma Kuzalisha Megawati 350
Serikali imesema kuwa, miradi unganishi ya Mchuchuma na Liganga itakayotekelezwa kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) na Kampuni ya Sichuan Hongda Group (SHG) Limited ya China kupitia ubia wa pamoja wa Tanzania China International Mineral Resources Limited (TCIMRL) itazalisha zaidi ya ajira 33,000 na kuipatia nchi umeme wa megawati 350.

Akitoa ufafanuzi huo, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani amesema kuwa kampuni hiyo imeshapewa leseni  na vibali vingine muhimu na sasa inakamilisha ulipaji wa fidia ili kuanza kazi. “Miradi hiyo unganishi itawezesha kuchimbwa makaa ya mawe kiasi cha tani milioni (3) na chuma ghafi tani milioni 2.9 kwa mwaka,” alisema.

Usalama wa Raia Mipakani
Serikali kupitia vyombo vya ulinzi na usalama katika maeneo ya mipaka inachukua hatua za pamoja na vyombo vya nchi jirani kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao katika maeneo hayo.

Akijibu hoja kuhusu suala la usalama wa raia wanaoishi pembezoni mwa mipaka ya Tanzania, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amefafanua kuwa operesheni za pamoja zinafanyika katika mipaka ya nchi na vikao vya ujirani mwema ili kuhakikisha usalama. Wananchi wameombwa kutoa taarifa wanapowaona wageni wasioeleweka katika maeneo yao ili kuimarisha usalama.

Wanahabari Waendeleze Kiswahili
Serikali imewapa changamoto wanahabari nchini kuwa chachu ya kuendeleza lugha ya Kiswahili. Wakijibu maswali mbalimbali ya wabunge kuhusu matumizi ya Kiswahili fasaha katika vyombo vya habari, Waziri na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wameliambia Bunge kuwa, ni vyema sasa hata wamiliki wa vyombo vya habari wakaanza kuzingatia ufaulu kwa somo la Kiswahili kabla ya kuwaajiri waandishi.

Kwa upande wake Waziri Nape akitoa majibu ya nyongeza, alisema kuenziwa kwa Kiswahili nchini kumeipa Tanzania hadhi ya kuwa makao makuu ya taasisi mbalimbali za Afrika zinazojihusisha na maendeleo ya lugha ya Kiswahili.

Imetolewa na:

Idara ya Habari-MAELEZO.

PICHA: Rais Magufuli Azindua Mwaka Mpya Wa Kimahakama Jijini Dar Es Salaam

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongea  na Kaimu Jaji Mkuu wa  Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma  wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017

Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma  akihutubia wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017 wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wakati  wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akipokea ripoti ya mahakama kuhusu kesi za uchaguzi kutoka kwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma  wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli  akikabidhi kwa Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai  ripoti ya mahakama kuhusu kesi za  uchaguzi wakati wa uzinduzi wa Mwaka Mpya wa Kimahakama katika viwanja vya Mahakama vya Mtaaa wa Chimala Ocean Road jijini Dar es salaam leo February 2, 2017. Kulia ni Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai

Video: Mwanamke azua tafrani mbele ya Rais Dkt Magufuli

$
0
0
Leo katika uzinduzi wa mwaka mpya wa kimahakama jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Rais Dkt John Pombe Magufuli. Rais Magufuli alizungumza mambo mengi ambapo alipongeza Mahakama kwa kufanya kazi nzuri ya kutatua kesi mbalimbali kwa mwaka mmoja uliopita.

Aidha, Rais Dkt Magufuli alielezea baadhi ya changamoto zinazokabili muhimili wa mahakama ambapo alisema kuwa tatizo la rushwa limekuwa likisababisha kukosekana kwa haki kwa atu wanyonge huku kesi nyingine zikicheleweshwa kwa makusudi. Rais Dkt Magufuli amewataka watumishi wa mahakama kuhakikisha wanatoa huduma bila upendeleo.

Baada ya kuzungumza huko, tafrani kubwa ilizuka baada ya mama mmoja kunyanyuka akiwa na kitambaa kilichoandikwa jumbe mbalimbali kuelekea kwa Rais akionyesha kudhulumiwa haki yake huku mahakama na polisi wakihusika.

Hapa chini ni video ya tukio hilo;

Breaking NewsR: ais Magufuli Ateua Mkuu mpya wa Majeshi Tanzania anaechukua nafasi ya Mwamunyange

Rais Dkt Magufuli aeleza kusikitishwa kwake na namna mahakama inavyoshughulikia kesi za ukwepaji kodi.


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaaa ya January 3

Rais Magufuli aitaka Mahakama kufuatilia madeni ya kesi serikali ilizoshinda

$
0
0
Na Beatrice Lyimo - MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa TANZANIA Dkt. John Pombe Magufuli ametoa wito kwa Mahakama kukusanya Shilingi Trillioni 7.3 ambazo ni matokeo ya serikali kushinda kesi mbalimbali za ukwepaji kodi.
 
Rais Magufuli ameyasema hayo jana  jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Sheria na Mwaka mpya wa Mahakama iliyobeba kauli Mbiu isemayo Utoaji haki kwa wakati kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Alisema  kuwa Takwimu zinaonesha kuwa kumekuwa na baadhi ya kesi za pingamizi za kodi ambapo  Serikali imeshinda kesi hizo japo  fedha hizo hazijakusanywa mpaka sasa.“Kukwepa au kutolipa kodi ni kosa kubwa sana, kila mtu anawajibu wa kulipa kodi nchini kwa maendeleo ya nchi” nalifafanua Dkt Magufuli.
 
Aidha, Rais Magufuli alisema kuwa katika kuelekea ukuaji wa uchumi, Mahakama iwe sehemu ya chanzo cha pato la taifa kwa kwa kuhakikisha wale wanaotakiwa kulipa fidia baada ya kushindwa kesi wanafanya hivyo pamoja na kuwabana wakwepa kodi kwani kutimiza hilo kutaleta mabadiliko katika uchumi wa nchi.
 
Katika hatua nyingine Rais Magufuli alisema kuwa Maendeleo ya nchi hayaangalii chama chochote, hivyo amevitaka vyombo vya utoaji haki kutoa haki kwa usawa.Kwa upande wake Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma alisema kuwa Mahakama imeandaa Mpango mkakati uliolenga kufanya maboresho ndani ya Mahakama.
 
Alisema kuwa mpango mkakati huo umelenga masuala makuu matatu ikiwemo Utawala bora, uwajibikaji na usimamizi wa rasilimali, upatikanaji wa haki na kwa wakati, uimarishaji wa amani kwa wananchi na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za mahakama.
 
Aidha Kaimu Jaji Mkuu alisema kuwa Mahakama imefanikiwa kusikiliza mashauri ya kesi za uchaguzi kwa asilimia 100.“kati ya mashauri ya kesi 249 ikiwemo 53 za ubunge na 196 za madiwani ya waliopinga uchaguzi kati ya kesi hizo, kesi 52 za ubunge zilikamilishwa na kesi zote za madiwani zilikamilishwa” alifafanua Kaimu Jaji Mkuu.
 
Naye Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju amesema kuwa Katiba imeanisha bayana Kanuni ambazo zinapaswa kuzingatiwa na Mahakama wakati ikitekeleza mamlaka yake ya utoaji haki.“utoaji haki mapema ipasavyo ni moja ya Kanuni ambazo Mahakama inapaswa kuzingatia katika utekelezaji wa majukumu yake kama inavyoelekezwa katika Katiba” alifafanua Mwanasheria Mkuu.

Alisema kuwa Serikali imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara katika nchi ya Tanzania hivyo kuchochea maendeleo ya kiuchumi.Siku ya Sheria nchini ilioanzishwa mwaka 1996 ikiwa ni siku muhimu ya kuombea Majaji na Mahakimu ili kuweza kusikiliza kesi.

Mbowe na Naibu Spika Dr Tulia Ndani ya BIFU Jipya

$
0
0
Mvutano  umeibuka bungeni kati ya Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson baada ya Mbunge huyo wa Hai kumwuliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa swali lililopingwa na Naibu Spika kwa maelezo kuwa ni la kisheria si la kisera.

Sakata hilo liliibuka asubuhi katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu, baada ya Mbowe kuhoji sababu za Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kusota rumande kwa kukosa dhamana, Peter Lijualikali wa Kilombero anayetumikia kifungo cha miezi sita gerezani na wanachama wengine wa Chadema wanaokabiliwa na mashitaka mbalimbali.

Mbowe alimtaka kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni, aeleze kama ni sera ya Serikali kuua vyama vya upinzani, huku akisema Rais John Magufuli alipata kutamka kuwa atavimaliza vyama vya upinzani kabla ya mwaka 2020.

Kwa maswali hayo, Dk Tulia alimtaka Waziri Mkuu kujibu swali linalohusu sera na kuachana na yanayogusa masuala ya kisheria.

Jambo hilo liliwafanya wabunge wa Upinzani huku wakipiga meza kwa takribani dakika tano kupinga, wakimtaka Naibu Spika aache Waziri Mkuu ajibu swali hilo.

Katika swali lake la msingi, Mbowe alisema wakati jana ikiwa ni Siku ya Haki Duniani, imepita miezi mitatu tangu Lema aanze kusota rumande huku akinyimwa dhamana licha ya kuwa iko wazi.

Pia alisema Lijualikali anatumikia kifungo cha miezi sita jela kwa kosa la kisiasa sambamba na mwenyekiti wa chama hicho wa mkoa wa Lindi, Suleiman Mathew aliyefungwa miezi minane na madiwani zaidi ya sita na viongozi wengine 215 nao wakifungwa au kuendelea na mashitaka huku zikifanyika hila za kuidhoofisha CUF.

“Haya yanayoendelea katika Serikali ambayo ni kinyume na utamaduni na mazoea yetu kama Taifa, je ni utekelezaji wa sera ya kuua upinzani chini ya Rais Magufuli?” Alihoji Mbowe.

Kabla ya Waziri Mkuu kujibu swali hilo, Dk Tulia aliingilia kati na hali kuwa hivi:

Dk Tulia: Katika swali lako kuna masuala ya kisera na kisheria. Maswali yanayomhusu Lema na Lijualikali na madiwani sita ni ya kisheria, hayo kuhusu leo (jana) kuwa siku ya haki duniani, Waziri Mkuu anaweza kuyajibu.

Majaliwa: Nakanusha, Rais hajawahi kutangaza kuvifuta vyama vya upinzani, nchi inaongozwa kwa sheria, kanuni na taratibu na kuna Bunge, Serikali na Mahakama. Hakuna mhimili unaoingilia mhimili mwingine. Jambo lililopo mahakamani halizungumzwi kokote, siwezi kuzungumzia hilo.

Mbowe: Kwa kuwa Rais anaonekana kuvunja Katiba ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa, je tukileta ushahidi kuwa Rais amekusudia kuumaliza upinzani kabla ya 2020, Waziri Mkuu utakuwa tayari kuwajibika kwa kujiuzulu?

Dk Tulia: Mbowe swali lako la maelezo ya jumla, yako sawasawa ila la kumtaka Waziri Mkuu kuwajibika si la kisera, kuwajibika si sera uliza swali la kisera.

Mbowe: Labda swali langu nilielekeze kwa Naibu Spika (Dk Tulia). Swali langu lilikuwa la mwendelezo ambalo hutokana na majibu ya msingi yaliyotokea. Kama kulikuwa na msingi wa kisera kwenye swali la msingi, swali la mwendelezo linakwenda kutokana na majibu yaliyotolewa. Waziri Mkuu aseme tu kama yupo tayari kujiuzulu tukileta ushahidi.

Katika maelezo yake, Dk Tulia alitaka Mbowe ajikite katika swali la kisera jambo ambalo Mwenyekiti huyo wa Chadema alipinga na kusisitiza kuwa huenda mambo yanayofanyiwa wapinzani, wabunge, mawaziri Serikali inayafurahia.

Taarifa Ya JWTZ Kuhusu Mauaji Ya Kondakta Mkoani Tanga

$
0
0
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4438 la tarehe 28 Januari 2017, Habari leo   la tarehe 29 Januari 2017 na baadhi ya vyombo vya habari vikihusisha mauaji ya kondakta wa daladala na Wanajeshi Mkoani Tanga.

Tunapenda  kuwataarifu wananchi kwamba kwa mujibu wa jeshi la polisi watuhumiwa wanaoshikiliwa na Jeshi hilo ni wanne (4),mmoja kati yao ni Mwanajeshi ambaye ni mzazi wa msichana anayetuhumiwa kusababisha tukio hilo.

Hivyo Mwanajeshi huyo anashikiliwa kwa ajili ya kulisaidia Jeshi la Polisi katika uchunguzi kwa kuwa tukio hilo lilifanyika nyumbani kwake. 

Hakuna Wanajeshi waliohusika katika tukio hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari, kambi za Jeshi wanaishi Wanajeshi pamoja na familia zao hivyo kuhusisha moja kwa moja mauaji hayo na Wanajeshi  mkoani Tanga ni kuupotosha umma.

Wito unatolewa kwa vyombo vya habari kuripoti habari zenye ukweli.Habari zisizo za kweli zinapotosha umma na kujenga taswira potofu kwa wananchi dhidi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania. 

Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   
Dar es Salaam,  
Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

==> Tazama video hapo chini kama tukio hilo lilikupita

Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS ni kampuni inayoongoza kwa kutoa bidhaa original za asili zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote pia tunatoa punguzo la bei la %10 kwa ajili ya Xmas and new year pata bidhaa kwetu uweze kufurahia matokeo mazuri kwa bidhaa original.

     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
 
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
 
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @10,000/= vidonge maalum @150,000
 
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @130,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
 
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
 
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @90,000/=
 
12.kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=

     WASILIANA NASI KWA NAMBA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma zetu. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti unapewa ili kuhakikisha mafanikio yako
           Follow us 
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images