Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Msajili wa Vyama Ashikilia Msimamo wake Wa Kumtambua Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF

$
0
0
Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi amesema hana hofu ya kuchafuliwa kutokana na tuhuma zinazotolewa dhidi yake, huku akisema msimamo wake uko palepale na kwamba anamtambua Profesa Ibrahim Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif ni Katibu Mkuu. 

Kauli ya Jaji Mutungi imekuja baada ya taarifa na kauli za matusi na kejeli zilizomuhusisha yeye na ofisi yake kusambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii baada ya kuidhinisha zaidi ya Sh300 milioni za ruzuku kwenda kwenye akaunti ambayo kamati ya uongozi ya CUF ilidai siyo ya chama hicho. 

Taarifa za msajili kuingiza fedha hizo kwenye akaunti hiyo na baadaye kutolewa kwa njia ambayo inaonekana kutia shaka zilitolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro ambaye alilinganisha suala hilo na uchotwaji wa zaidi ya Sh300 bilioni zilizokuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow. 

Kupitia taarifa yake jana, Jaji Mutungi alisema kuna mbinu zinazopangwa na wanaojiita Kamati ya Uongozi ya CUF ambayo ofisi yake haiitambui, huku akisisitiza kumtambua Profesa Lipumba kama mwenyekiti wa CUF na Maalim Seif kuwa Katibu Mkuu.

Jaji Mutungi ambaye mwishoni mwa mwaka jana alifunguliwa kesi Mahakama Kuu na bodi ya wadhamini wa CUF ikiiomba itoe amri ya kubatilisha barua ya mlezi huyo wa vyama vya siasa inayomtambua Profesa Lipumba kuwa mwenyekiti wa CUF, alisema kauli zinazotolewa mitandaoni zina lengo la kuchafua ofisi yake. 

“Tayari mbinu hizo zimeanza kutekelezwa na viongozi wa kamati hiyo kwa kusambaza habari za kudhalilisha katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii kama Facebook na mingineyo,” alisema. 

Msajili huyo alisema moja ya mkakati huo ni taarifa iliyosambazwa juzi na Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari wa CUF,, Mbarala Maharagande ya kejeli, matusi, tuhuma na dhihaka kwake. 

Jaji Mutungi alisema hivi karibuni, Maharagande alizungumza na waandishi wa habari huku akidai kuwa ofisi ya msajili inasababisha mpasuko ndani ya chama hicho na ndiyo maana imetoa ruzuku kwa Profesa Lipumba. 

Licha ya tuhuma hizo, Jaji Mutungi alisema kwamba haogopi kuchafuliwa akizingatia ukweli kwamba yeye ni mtumishi wa umma na anafanya kazi zake akiwatumia wananchi kwa mujibu wa sheria za nchi. 

Alisema kamwe hawezi kuyumbishwa na matusi wala kejeli zinazotolewa dhidi yake pamoja ofisi anayoiongoza. 

“Nimezipata hizo taarifa kwamba kuna baadhi ya watu wamepanga kupambana nami kwa kunichafua, japo naendelea kuzifanyia kazi lakini waache wanichafue, wala siogopi lolote,” alisema. 

Hata hivyo, Jaji Mutungi alisema mjadala wa ruzuku ya CUF aliyotoa kwa chama hicho ameshaufunga na anashangazwa na maneno yanayozidi kusambazwa na watu wanaojiita viongozi wa CUF.

Alipotafutwa  kuzungumzia tuhuma hizo, Maharagande aliendelea kusisitiza kuwa kauli iliyotolewa wakati alipofanya mkutano na vyombo vya habari ipo hivyo na kwamba waliitisha mkutano kumjibu msajili ambaye alifanya mkutano na waandishi wa habari siku moja kabla kuhusu masuala ya CUF.

Majeshi ya Senegal yaingia Gambia kumng’oa rais king’ang’anizi Yahya Jammeh

$
0
0
Viongozi wa Afrika Magharibi wamempa Yahya Jammeh nafasi ya mwisho kuachia madaraka wakati majeshi ya Senegal yakiingia nchini Gambia tayari kwa kumng’oa.

Jammeh amepewa hadi Ijumaa hii  mchana awe ameshachukua virago vyake ama kuondolewa kwa nguvu na majeshi ya Afrika Magharibi yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, Ecowas inamuunga mkono Adama Barrow, aliyeapishwa kama rais mpya wa Gambia, Alhamis hii katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal.

Ni rais halali sababu ndiye alishinda uchaguzi wa mwezi uliopita na amekuwa akitambulika kimataifa. Barrow, ambaye bado yupo nchini Senegal, amedai kuwa hatarejea kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Banjul, hadi pale operesheni ya kijeshi itakapokamilika.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya January 21

Rais Wa Gambia Akubali Kuachia Madaraka

$
0
0
Yahya Jammeh ambaye amekua madarakani na kuingoza Gambia kama Rais kwa miaka 22 hatimae amekubali kuachia madaraka hayo na sasa Adama Barrow aliyetangazwa mshindi kwenye uchaguzi mkuu ndio anatarajiwa kuchukua nafasi.

Kupitia Television ya taifa, Yahya ametangaza kuachia madaraka ambapo AlJAZEERA wameripoti kwamba taarifa kutoka IKULU zilisema baada ya kuachia madaraka alitarajiwa kuondoka kwenye nchi hiyo ndani ya siku 3 ila media nyingine zinasema amepewa saa tu za kuondoka.

TV ya habari Nigeria imesema ECOWAS walimpa hadi saa sita mchana kuondoka lakini mwenyewe akaomba muda huo usogezwe hadi saa kumi jioni na imeripotiwa atakwenda kuishi Guinea.

Barrow aliandika kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kusema ‘Yahya Jammeh amekubali kuachia madaraka na anatarajiwa kuondoka kwenye nchi ya Gambia leo’

Taarifa ya Bunge kuhusu Dkt Abdallah Possi kujiuzulu ubunge

Rais Dkt Magufuli amteua Anne Kilango Malecela kuwa mbunge

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 21 Januari, 2017 amemteua Anne Kilango Malecela kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Anne Kilango Malecela ataapishwa kwa mujibu wa taratibu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

21 Januari, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili Ya January 22

Tanzania Kujifunza Toka China Kuhusu Namna ya Kukuza Uchumi

$
0
0
Serikali imesema iko tayari kujifunza namna ambavyo China imefanikiwa katika kukuza uchumi wake, ili kutengeza mfumo utakaoleta maisha bora kwa Watanzania wote.

Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan wakati akifungua sherehe za Mwaka Mpya wa China, ambao kwa mwaka huu unajulikjana kama ‘Mwaka wa Jogoo” katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.

Samia alisema mafanikio ya China katika kuwatoa wananchi wake katika umasikini, unaendelea kuihamasisha Serikali na hasa katika kipindi hiki ambacho inaongia katika mageuzi ya kiuchumi.

“Tunaridhishwa jitihada zenu katika kumaliza tatizo la rushwa, tunafahamu mabadiliko mliyofanya ndio yametoa matokeo ya usimamizi mzuri wa uchumi. Najua mabadiliko yanaweza kuwa ajenda ya malengo yetu, lakini kuna sababu nzuri kwa sisi kuwa na nia.”

“China imeweza katika siku za nyuma, sisi pia tunaweza kufanya sasa, lakini tunahitaji kuungwa mkono,” alisema Samia.

Aidha, alisema uhusiano kati ya China na Tanzania ni wa muda mrefu na kwamba wanathamini mchango mkubwa wa China katika maendeleo ya Tanzania.

Akizungumzia nyanja ya kisiasa, alisema ubadilishanaji uzoefu baina ya nchi hizo mbili hasa katika masuala ya utawala, umeongezeka na kuzaa matunda.

Alisema ziara ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China, Wang Yi, ilikuwa si tu kwajili ya kuboresha mahusiano ya kidiplomasia pekee, bali pia kufanya kazi ya kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na mikakati ya miradi ya miundombinu, ambayo ni muhimu katika kusaidia maendeleo ya viwanda nchini.

Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing alisema sikukuu hiyo muhimu, wamefanya hivyo ili kuruhusu Watanzania kujua utamaduni wa Wachina, huku akitoa shukrani kwa Serikali kwa msaada na ushirikiano.

Alisema, mwaka uliopita ulikuwa ni muhimu kwa ajili ya mahusiano ya China na Tanzania na pia ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa matokeo ya Mkutano wa FOCAC uliofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini.

Alisema chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, Serikali ya Tanzania inasisitiza mapambano dhidi ya rushwa na uvivu, na kuhimiza uwajibikaji ili watu wote waweze kunufaika.

Alisema kwamba Rais Magufuli alianza kwa kuchukua hatua madhubuti za mfululizo, kukomesha matatizo hayo. Balozi Youqing alisema Rais Magufuli alimuandika barua Rais wa China, Xi Jingping na watu wa China, kumpongeza kwa mafanikio ya Serikali ya China iliyopata katika mapambano ya rushwa na kufanya mageuzi ya kina.

“Alisifu uhusiano wa kindugu kati ya Tanzania na China, alisisitiza kwamba ushirikiano wa Tanzania na China, na mpango wa “Belt and Road” utasaidia maendeleo ya viwanda nchini Tanzania na alisema Tanzania itaendelea kuinga mkono China katika masuala mbalimbali,” alisema Balozi Youqing.

Aliongeza kuwa China inafurahia ushirikiano wa kina katika masuala ya kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kimataifa. Kwamba katika uwanja wa ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, China imekuwa mkandarasi mkubwa na chanzo cha pili kwa uwekezaji. Alitaja baadhi ya miradi mikubwa ni reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA), Bandari ya Bagamoyo na hifadhi ya viwanda Buguruni; na mradi wa biashara ya muhogo pia uko kwenye ukuaji mzuri.

Alisema Ubalozi wa china nchini utatekeleza kikamilifu makubaliano ya mawaziri wawili ambao ni Wang Yi wa China na Dk Augustine Mahiga wa Tanzania ili kuendeleza mahusiano kwa manufaa ya nchi hizo mbili. Balozi huyo pia alisema ubalozi wake, umechangia Sh milioni 100 katika Mfuko wa Maendeleo ya Serikali, ili kusaidia sekta ya elimu nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga alisema Tanzania imepewa kipaumbele cha kipekee katika nchi za Afrika, kwakuwa China imetoa dola za Mareakni milioni 60 kwa ajili ya kusaidia nchi za Afrika na imechagua Tanzania kuwa nchi ya kwanza kati ya nne, ambazo ni Afrika Kusini, Ethiopia na Kenya.

Alisema kama ulivyo mwaka huo wa Jogoo, mahusiano ya China na Tanzania nayo yanazidi kuwika katika nyanja mbalimbali. “…Katika hili la viwanda China imeahidi kama sisi tutachangamkia fursa hizo, viwanda vingi vidogovidogo na vile ambavyo sasa hivi vinachukua ajira ya watu wachache, kwasababu wao wanajikita katika teknolojia kubwa, viwanda hivyo vitahamia Tanzania,” alisema Dk Mahiga.

Waumini Kanisa la Anglikan Wamzuia Askofu Mokiwa kufanya vikao

$
0
0
Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam wa Kanisa la Anglikana, Dk valentino Mokiwa jana alishindwa kuendesha vikao viwili baada ya kundi la waumini kufika Usharika wa Ilala kwa lengo la kuzuia.

Askofu Mokiwa, ambaye anapinga uamuzi wa Askofu Mkuu wa Anglikana, Dk Jacob Chimeledya kumvua madaraka kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha, alikuwa aendeshe vikao vya kamati ya fedha na halmashauri kuu, lakini alilazimika kuviahirisha baada ya kundi hilo kufika eneo hilo.

Wakati waumini hao wakizuia vikao hivyo kufanyika, mashemasi, mapadri, wainjilisti na waumini wa dayosisi hiyo wametoa tamko la kumuunga mkono Dk Mokiwa wakipinga uamuzi wa mkuu wa kanisa hilo kumvua madaraka.

Askofu Mokiwa anapinga uamuzi wa kumvua madaraka akisema hauwezi kufanywa na mkuu wa kanisa, bali na halmashauri kuu ya jimbo ambayo anasema haikushirikishwa zaidi ya kutaarifiwa uamuzi huo.

Tukio la jana la kumzuia Dk Mokiwa kufanya mkutano lilitokea saa mbili asubuhi katika Kanisa la Mtakatifu Nicolau wilayani Ilala, ambako kuna ofisi ya Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam.

Mmoja wa watu walioshiriki kuzuia vikao hivyo, Haule Sylvester ambaye alijitambulisha kuwa kiongozi wa waumini wa Anglikana jijini Dar es Salaam, alisema walichukua uamuzi huo kwa kuwa Dk Mokiwa ameshavuliwa uaskofu.

“Huyu (Dk Mokiwa) hapaswi kufanya shughuli zozote za kanisa kwa sababu si askofu. Lakini amekuwa akiendesha vikao vya siri na mapadri wanaomuunga mkono,” alisema Sylvester.

“Jana (juzi) alifanya kikao cha siri. Leo (jana) alikuwa aongoze vikao viwili, kikiwamo cha bodi ya fedha ya dayosisi hii, ndiyo maana tumemzuia.”

Alifafanua kuwa baada ya kikao hicho cha fedha kilichokuwa kimepangwa kuanza saa 3:00 asubuhi, kikao ambacho kingefuata ni cha halmashauri kuu ya dayosisi ambacho kingefanya uamuzi wa mambo ambayo yangejadiliwa na bodi ya fedha.

Sylvester alisema kwa mujibu wa katiba ya dayosisi hiyo, vikao hivyo vyote vinatakiwa viongozwe na mwenyekiti ambaye ni askofu wa dayosisi.

Alisema halmashauri ina wajumbe 10 akiwamo askofu wa dayosisi, wakati kikao cha bodi ya fedha kina wajumbe zaidi ya 200 na kina lengo la kupanga bajeti ya mwaka.

“Ki utaratibu ili kuendesha vikao hivi, lazima uwe askofu wa jimbo la Dar es Salaam. Tunamsihi Mokiwa aache kufanya kazi na kutumia ofisi kwa kofia ya uaskofu,” alisema.

Alisema waumini wengi walipanga kushiriki katika mchakato huo, lakini walienda 20 baada ya kutoa taarifa polisi.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Yohana Sanga ambaye ni ofisa habari wa Dk Mokiwa alisema vikao hivyo vilikuwa vya kawaida vya dayosisi hiyo na vililenga kujadili maendeleo ya kanisa.

“Tulishangaa kuona kundi lile la watu, ambalo chimbuko lake limetoka Kanisa la Magomeni linalompinga Askofu Mokiwa,” alisema. 

Mbali na kundi hilo, kilichowasikitisha zaidi ni kuona magari sita ya polisi, wakiwamo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), yaliyokuwa yameegeshwa nje ya kanisa.

Hata hivyo, Kamanda wa Polisi wa Ilala, Salum Hamduni alisema  kuwa askari hao walikuwa katika doria ya kawaida.

Sanga alisema baada ya kundi hilo kufika katika eneo hilo, liliingia moja kwa moja kanisani na walipowauliza walijibiwa kuwa wanakwenda kujadili masuala ya kanisa.

Alisema baada ya kuona hivyo, walisita kufungua ofisi iliyoandaliwa kwa ajili ya vikao na baada ya majadiliano ya muda mrefu, waliahirisha.

“Walivyoona hatufungui ofisi, waliamua kuondoka kwa mafungu.Lengo lao lilikuwa kuvunja vikao hivi,” alisema Sanga.

Taarifa ya viongozi hao wanaomuunga mkono Askofu Mokiwa, inasema bado wanaendelea kumtambua na kumuunga mkono kiongozi huyo kama askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam na kwamba uamuzi uliochukuliwa dhidi yake ni batili.

Hivi karibuni, Askofu Mkuu, Chimeledya alimtaka Dk Mokiwa ajiuzulu kwa kile alichodai kuwa anatumia vibaya madaraka yake na ubadhirifu wa fedha.

Hata hivyo, Dk Mokiwa alikanusha madai hayo na kusema mgogoro wa kanisa hilo ni wa kutengenezwa na maadui zake.

Yahya Jammeh aondoka nchini Gambia kwenda kuishi uhamishoni

$
0
0
Aliyekuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh ameondoka nchini humo baada ya mvutano wa muda kufuatia kushindwa katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Disemba Mosi mwaka jana.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ECOWAS, kiongozi huyo aliyeiongoza Gambia kwa miaka 22 alipanda ndege kuelekea nchini Guinea ambapo akifika atasafiri kwenda nchini Equatorial Guinea atakapoishi uhamishoni.

Yahya Jammeh is to go into exile in Equatorial Guinea

Jammeh alishindwa na kiongozi wa upinzani, Adama Barrow ambaye amekuwa akiishi nchini Senegal na kueleza kuwa atarudi Gambia usalama ukiimarika.

Barrow aliyeapishwa katika Ubalozi wa Gambia nchini Senegal, alisema kuwa akiingia madarakani ataunda tume kuchunguza ukiukwaji wa haki za binadamu uliofanywa na Yahya Jammeh katika kipindi cha miaka 22 ya utawala wake.

Rais wa ECOWAS, Marcel de Souza pia ameeleza kuwa wanajeshi waliokuwa wametumwa kutoka nchi wanachama kwenda kumuondoa Jammeh madarakani sasa wataondolewa japo wachache watabaki kuendelea kuimarisha usalama.

Wananchi wa Gambia wamekuwa na hisia tofauti kuhusu kuondoka kwa Jammeh ambapo wanaoaminika kuwa ni wafuasi wake walisikitika kwa majonzi alipokuwa akiwaaga katika uwanja wa ndege huku wengine wakishangilia kuamini kuwa ni mwisho wa utawala wa kidikteta uliokuwa hauheshimu haki za binadamu.

Kitu alichoahidiwa Jammeh kuweza kuachia madaraka baada ya kukutana na baadhi ya viongozi wa mataifa mengine bado hakijafahamika.

Yahya Jammeh anakuwa Rais wa kwanza wa Gambia kuondoka madarakani kwa amani tangu walipopata uhuru mwaka 1965.

Waziri Mkuu: Vijiji 53 Njombe Kupatiwa Huduma Ya Maji

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema jumla ya vijiji 53 vya mkoa wa Njombe vitapatiwa huduma ya maji safi na salama katika mwaka huu wa fedha.

Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizungumza na wananchi wa wilaya ya Wanging’ombe katika mkutano wa hadhara katika kata ya Ilembula.

Waziri Mkuu alisema zaidi ya sh. bilioni 2.4 zimetengwa kwa ajili ya kugharamia mradi huo wa maji katika miji ya Makambako, Njombe na wilaya ya Wanging’ombe.Alisema kati ya vijiji hivyo vitakavyopatiwa maji, vijiji 22 ni vya wilaya ya Wanging’ombe, hivyo aliwaomba wananchi hao kuwa na subira.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu tayari zabuni ya mradi huo imeshatangazwa, hivyo amewaagiza viongozi wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji watafute mkandarasi mzuri.Alisema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kila mwananchi anapata huduma ya maji katika umbali usiozidi mita 400 kutoka mahali anapoishi.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo baada ya Mbunge wa Wanging’ombe, Mheshimiwa Mhandisi Gerson Lwenge kumuomba awasaidie katika kutatua kero ya maji.Mbunge huyo ambaye pia ni Waziri wa Maji na Umwagiliaji alisema “Mheshimiwa Waziri Mkuu sisi tunakabiliwa na changamoto ya maji, leo tunaomba ututatulie kero hii”.

Changamoto nyingine aliyoitaja Mheshimiwa Lwenge ni pamoja na ukosefu wa hospitali ya wilaya, ambapo Waziri Mkuu aliigiza halmashauri hiyo kuanza ujenzi.Alisema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inaelekeza kuwa na hospitali katika kila wilaya, kituo cha afya kwa kila kata na zahanati kwa kila kijiji.

Katika hatua nyingine Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo Bw. Ally Kasinge kukutana na viongozi wa kata na vijiji vinavyozunguka hifadhi ya Mapanga Kipengele ili kutatua kero ya mpaka.
                  
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Waziri Mkuu :serikali Imeanza Kulipa Madeni Ya Watumishi .....Jumla Ya Sh. Bilioni 29 Zililipwa Mwaka Jana

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imelipa jumla ya sh. bilioni 29 kwa watumishi mbalimbali wa umma wakiwemo walimu ikiwa ni sehemu ya madeni yao.

Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 21, 2017) wakati akizindua vyumba vitatu vya kisasa vya madarasa katika shule ya sekondari Iwawa iliyoko wilayani Makete.

Waziri Mkuu alisema Serikali imedhamiria kumaliza madeni ya watumishi hao, ambapo hadi kufikia Novemba mwaka jana jumla sh. bilioni 29 zililipwa kwa watumishi 31,000.Alisema kwa sasa Serikali imejipanga kuhakikisha hakuna madeni mapya yanayozalishwa hivyo amewataka watumishi wa umma na wananchi kuendelea kuiunga mkono Serikali.

Hata hivyo alisema Serikali inaendelea na mikakati ya kuboresha sekta ya elimu kwa kujenga mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.“Tumeanza mradi wa ujenzi wa nyumba za walimu katika halmashauri nchini. Hapa Makete tumeleta sh. milioni 557 kwa ajili ya ujenzi huo,” alisema.

Alisema nyumba hizo za walimu zinazojengwa katika maeneo mbalimbali hususan ya vijijini ni za kisasa ambazo zinalenga kuwaondolea changamoto ya makazi.Waziri Mkuu alisema Serikali inafanya jitihada za dhati za kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu kwa kuwa elimu ni kichocheo cha maendeleo ya jamii.

“Tumedhamiria kumpatia elimu kila Mtanzania, hivyo halmashauri zihakikishe kila kijiji kinakuwa na shule ya msingi na lazima ziwe na darasa la awali,” alisema.Naye Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Novatus Msivala aliishukuru Serikali kwa kugharamia ujenzi wa vyumba hivyo vitatu vya madarasa na matundu 10 ya vyoo pamoja na uingizaji wa maji kwenye vyoo na utengenezaji wa madawati 46.

Alisema ujenzi huo umegharimu sh. milioni 95 ambao utasaidia kupunguza msongamano kwa wanafunzi. Kwa sasa Serikali na wananchi wanaendelea kukamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi ya walimu.
                       
Katika hatua nyingine jana Waziri Mkuu alitimiza ahadi yake ya kumpatia laptop mwanafunzi Ally Alijai wa Chuo kikuu cha SAUT tawi la Songea mkoani Ruvuma.Ahadi hiyo aliitoa mwanzoni mwa mwezi huu alipokuwa katika ziara yake kikazi mkoani Ruvuma, lengo likiwa ni kuendeleza kipaji cha utunzi wa vitabu kwa mwanafunzi huyo.

Alisema mwanafunzi huyo alionyesha umahiri mkubwa katika utungaji wa kitabu ambacho kinaweza kutumika kufundishia katika shule za sekondari.

Hata hivyo Waziri Mkuu alisema tayari kitabu hicho kimeshawasilishwa Taasisi ya Elimu Tanzania (TEA) kuona kama kinaweza kuanza kutumika kwa kufundishia. Mwanafunzi huyo alishukuru kwa zawadi hiyo na kuahidi kutunga vitabu vizuri zaidi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JANUARI 22, 2017.

Mbowe kitanzini tena,apewa siku 14 kulipa deni linalomkabili

$
0
0
Miezi takribani mitano iliyopita tangu aondolewe Billcanas, siku moja tangu Serikali imzuie asiendelee na shughuli za kilimo katika shamba lake, Mwenyekiti huyo wa Chadema amepewa siku 14 awe amelipa kodi inayokadiriwa kufika milioni 13.5, ya hoteli yake ya Aishi iliyoko Machame Mkoani Kilimanjaro.

Uamuzi huo mpya wa Serikali wa Wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro,umefikia hatua hiyo ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya hiyo Gellasius Byakanwa, kutangaza kusitisha shughuli za kilimo katika shamba la Veggies analomiliki Mbowe kutokana na kile kilichosema lipo ndani ya chanzo cha maji.

Byakanwa amesema kuwa Serikali ya awamu ya Tano imelenga kukusanya mapato ili iweze kutekeleza majukumu yake ikiwamo kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Hatuwezi kufikia malengo ya ukusanyaji mapato yetu ya ndani kama kuna wafanyabiashara wakubwa kama huyo wanakwepa kulipa kodi, na tena kwa kipindi chote hicho ameshindwa kuleta hali ya mauzo yake ambayo yataweza kujulikana kiasi anachostahili kulipa kodi,”amesema Byakanwa.

Hata hivyo Mkuu huyo wa Wilaya amemshutumu Mbowe kwa kufanya uharibifu wa mazingira kwa kuvuna miti ya asili bila kibali cha mkuu wa Wilaya kulingana na uamuzi wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) pamoja na kuvuta maji kwa kutumia mashine kinyume na kibali na taratibu za utumiaji wa maji mfereji.

Sakata la ruzuku CUF latua BoT,Maalim Seif ateta na Gavana

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif  Sharif Hamad, amemwandikia barua Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT), Profesa Beno Ndulu ili achukue hatua za kulishughulikia sakata la fedha za ruzuku zinazodaiwa kukwapuliwa na CUF upande wa Mwenyekiti anaetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba.

Maalim Seif ameandika barua hiyo yenye kumbukumbu namaba CUF/HQ/AKM/003/017/01 na nakala zingine kuzituma kwa mamlaka mbalimbali.

Katika barua hiyo kwa Profesa Ndulu, Maalim ameamabatanisha kumbukumbu ya miamala ya fedha ilivyofanyika, pia amesema kuwa chama hicho kinaendelea na taratibu za kukamilisha hatua za kisheria ili kuwafikisha mahakamani wahusika wote walioshiriki  katika kuchukua fedha hizo, akiwapo Msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Francis Mutungi.

Amesema kuwa, Mutungi atakuwa na kesi ya pili na atashtakiwa kutokana na madai ya kushirikiana na walalamikiwa wale wale wa kufungua akaunti mpya ili wapewe ruzuku.

Aidha, amesema Jaji Mutungi amefanya hivyo huku akifahamu fika kuwa kuna kesi ya msingi iliyopangwa kusikilizwa Februari 2, 2017 mbele ya Jaji Kihiyo.

“Gavana baada ya Muhtasari huo, kwa masikitiko makubwa leo nakuandikia barua hii kukujulisha kuwa njama za kuiba fedha za ruzuku  ya CUF Chama cha Wananchi zimefanikiwa  kwa kufanya muamala wa jumla ya shilingi 369,378,502.64 toka kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini kwenda akaunti namba 2072300456 ya NMB tawi la Temeke januari 5 mwaka huu,”amesema Maalim.

Hata hivyo, hivi karibuni CUF upande wa Maalim Seif ulilalamikia hatua iliyochukuliwa na Jaji Mutungi kuwapa CUF upande wa Profesa Lipumba zaidi ya shilingi milioni 360 za ruzuku

Rais wa Uturuki kuwasili nchini leo

$
0
0
Taarifa kuhusu ziara ya Rais wa Uturuki nchini
Rais wa Jamhuri ya Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan anatarajiwa kufanya ziara ya kitaifa ya siku mbili nchini tarehe 22 na 23 Januari 2017 kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mhe. Rais Erdogan ambaye ataambatana na Mkewe, na kuongoza ujumbe wa watu 150 wakiwemo Mawaziri, Wabunge, Maafisa kutoka Serikalini na Wafanyabiashara anatarajiwa kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere tarehe 22 Januari, 2017 jioni  na atapokelewa na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Madhumuni ya ziara hiyo ni kukuza mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Uturuki na Tanzania pamoja ‎na kupanua fursa za uwekezaji hususan katika maeneo ya biashara  na uwekezaji.

Wakati wa ziara hiyo, Mhe. Erdogan  atakutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa mazungumzo ya faragha yatakayofuatiwa  na mazungumzo rasmi yatakayowahusisha wajumbe wa pande mbili na baadaye Marais hao watashuhudia uwekwaji saini wa mikataba ya ushirikiano kwenye maeneo mbalimbali.

Siku hiyo ya tarehe 23 Januari, 2017, kutakuwa na Kongamano la Biashara kati ya Uturuki na Tanzania litakalowakutanisha Wafanyabiashara kutoka nchi hizi mbili. Kongamano hilolitahutubiwa na viongozi wa Tanzania na Uturuki.

Mhe. Rais Erdogan na ujumbe wake watashiriki Dhifa ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima yake na Mhe. Rais Magufuli.
 
Mahusiano ya Uturuki na Tanzania‎
Mahusiano ya Tanzania na Uturuki ni mazuri. Ikumbukwe kuwa, kufunguliwa kwa mara nyingine kwa Ubalozi wa Uturuki hapa nchini mnamo Mei 2009 kuliongeza kasi ya mahusiano baina ya nchi hizi mbili. Katika hatua nyingine Tanzania imetangaza kufungua Ubalozi wake nchini Uturuki na hivi leo Mhe. Rais atamwapisha Balozi Mteule, Prof. Elizabeth Kiondo atakayetuwakilisha Uturuki.
 
Pia kumekuwa na ziara za viongozi wakuu wa kitaifa wa nchi hizi mbili ikiwemo ziara ya Rais mstaafu wa Uturuki, Mhe. Abdullah Gul  nchini mwaka 2009 ; ziara ya Rais wa Awamu ya Nne wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete nchini Uturuki mwaka 2010 na ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein mwaka 2011.
 
Tume ya Pamoja ya Biashara
Tanzania na Uturuki zinashirikiana pia kupitia Tume ya Pamoja ya Biashara ambayo ilianzishwa baada ya kusainiwa kwa Mkataba wa Ushirikiano kwenye masuala ya Biashara mwaka 2010. Kikao cha kwanza cha Tume hiyo kilifanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Novemba 2012. Katika kikao hicho pande zote zilikubaliana kushirikiana kwenye maeneo mbalimbali hususan biashara na uwekezaji, elimu, Kilimo, Nishati na Madini, Maendeleo ya viwanda na mawasiliano ya simu.

Kikao cha Pili cha Tume ya Pamoja ya Biashara kati ya Tanzania na Uturuki kilifanyika tarehe 11 – 12 Januari 2017, Uturuki kwa lengo la kujadili utekelezaji wa Makubaliano ya Kikao cha Kwanza na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano kati ya pande hizi mbili. Aidha, Mkutano huu pia ulikuwa na umuhimu wa kipekee kwa kuwa ulifanyika ikiwa ni maandalizi ya ziara ya Kiserikali ya Mheshimiwa Recep Tayyip Erdoğan, Rais wa Jamhuri ya Uturuki inayotarajiwa kufanyika tarehe 23 Januari, 2017.

Pande zote mbili zimekubaliana kuongeza nguvu katika kuhamasisha uwekezaji kwenye nchi zetu. Katika kutekeleza hili, Uturuki imepanga kuandaa Mkutano wa Uwekezaji kati ya Tanzania na Uturuki ndani ya robo ya pili ya mwaka huu jijini Istanbul. Vile vile, nchi zote mbili zimekubaliana kubadilishana taarifa za fursa za uwekezaji kupitia Balozi zetu na Baraza la Biashara la Tanzania na Uturuki.

Aidha, Taasisi zetu za Uwekezaji zimeelekezwa kuanza majadiliano ya kuingia Mkataba wa Ushirikiano ili kuhamasisha uwekezaji nchini. Hali kadhalika, Uturuki imemchagua Mwambata wa Biashara katika Ubalozi wao wa Dar es Salaam na Tanzania imeahidi kuteua Afisa Maalum ndani ya mwezi mmoja kushughulikia uhamasishaji wa uwekezaji na biashara kati ya nchi hizi mbili.

Mafanikio yaliyopatikana kutokana na ushirikiano kati ya Tanzania na Uturuki

Tangu kuanzishwa kwa Tume ya pamoja ya ushirikiano ya kiuchumi mafanikio ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili yameonekana ikiwemo:- Kuimarishwa kwa ushirikiano katika masuala ya Usafiri wa Anga ambapo Shirika la Ndege la Uturuki lilianzisha safari tatu  za moja kwa moja kutoka Istanbul hadi Dar es Salaam, Kilimanjaro na hivi karibuni Zanzibar. Kuanzishwa kwa safari hizi kumekuza biashara kati ya Uturuki na Tanzania  ambapo mwaka 2009  ukubwa wa biashara ulikuwa Dola za Marekani milioni 66 sawa na shilingi bilioni 145.2 lakini hadi kufikia Februari 2016 biashara kati  ya nchi hizi mbili iliongezeka kwa Dola za Kimarekani milioni 160 sawa na shilingi bilioni 352.

Aidha, kuzinduliwa kwa Baraza la Biashara kati ya Tanzania na Uturuki mwaka 2013 ambalo kumewezesha kuimarisha ushirikiano wa sekta binafsi za nchi hizi mbili na  Kuongezeka kwa Makampuni ya Uturuki yaliyowekeza nchini ambapo hadi sasa ni Kampuni 30 zimefanya uwekezaji wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 305.08 na zinatarajiwa kutengeneza ajira 2,959.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dar es Salaam
20 Januari, 2017

Picha: Mamilioni ya wanawake duniani waandamana kupinga Urais wa Donald Trump

$
0
0
Rais Donld Trump aliapishwa Ijumaa hii kwa sherehe mjini Washington DC, lakini hiyo haimaanishi kuwa mambo yametulia – ndio yameanza.

Jumamosi hii, mamilioni ya wanawake duniani, waliandamana kupinga kuapishwa kwake kama rais wa 45 wa Marekani. Maandamano makubwa zaidi yalikuwa Marekani hususan kwenye mji mkuu, Washington.

Wanawake hao walioungwa mkono na mastaa kibao pamoja na wanaume walioependa kuwaunga mkono, walikuwa na ujumbe mmoja tu, kuwa hawatakuwa kimya kwa miaka minne yote ya uongozi wa Trump.
 
Kulikuwa na maandamano kwenye zaidi ya miji 600 duniani kote huku waandamaji wakiwa na mabango mengi yanayomdhihaki na kumlaani Trump.

Mastaa walioshiriki kwenye maandamano hayo ni pamoja na Katy Perry, Madonna, Scarlett Johansson, Jake Gyllenhaal, Emma Watson, Ashley Judd, Cher, America Ferrera, Kristen Stewart, Charlize Theron, Whoopi Goldberg, Cynthia Nixon, Charlotte Church, Yoko Ono, Helen Mirren, Julia Roberts, John Legend, Amy Schumer na wengine.

Takriban watu milioni 2.2 wanaaminika kuwa waliandamana kutetea haki zao na za binadamu.

Pamoja na miji mingi ya Marekani, miji mingine duniani iliyokuwa na maandamano makubwa ni pamoja na London, Paris, Berlin, Edinburgh, Rome, Prague, Amsterdam, Stockholm, Athens, Copenhagen, New Delhi, Brussels, Mexico City, Barcelona, Manila, Toronto, Madrid, Geneva, Cardiff na Sydney.

Bulembo amtaka Lowassa Aachane na Siasa

$
0
0
Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM, Abdallah Bulembo amemshangaa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa kuendelea kung’ang’ania siasa hadi sasa hivi, badala yake anastahili kukaa kimya kula maisha ili afaidi uzee wake vizuri.

Bulembo aliyasema hayo wakati akifunga kampeni za udiwani Kata ya Mateves iliyopo Wilaya ya Arusha juzi, ambako walitarajiwa kumchagua diwani wao katika uchaguzi mdogo. Mbunge huyo mteule wa kuteuliwa, alisema anashangaa Lowassa kung’ang’ania madaraka, badala yake anastahili kula maisha ili kufaidi uzee wake vizuri.

Alisema wapinzani wataruhusiwa kutumia barabara, maji, shule na vinginevyo, lakini kwenda Ikulu haiwezekani. 

Aidha, Bulembo alilaani kitendo cha wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuingilia msafara wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) uliokuwa ukielekea Uwanja wa Ngorbob Sokoni kwa ajili ya kufunga kampeni za chama hicho.

Alisema wafuasi wa CCM ni wastaarabu na wavumilivu, hawakufanya fujo, bali waliwapita kwa mbele na kuelekea kwenye mkutano wa kufunga kampeni.

Mgombea Udiwani wa Kata ya Mateves, Julius Saing’ore maarufu kwa jina la Sovoyo na mgombea uenyekiti wa serikali ya kijiji, Mohamed Nassoro maarufu kwa jina la Arsenal, waliomba kura kwa wananchi hao ili walete maendeleo.

Mgombea udiwani Saing’ore aliwasihi wananchi wa kata hiyo, kumpa kura ili waliokwenda mahakamani kudai uchaguzi uliokuwa na kasoro wajue kuwa CCM ndio yenyewe.

Awali, Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shabani Mdoe alisema wananchi wana imani kubwa na chama hicho na hawataki porojo, bali wanataka maendeleo.

Alisisitiza kuwa awali alipokuwa madarakani aliyekuwa diwani wa CCM kabla ya kutenguliwa na mahakama mwaka jana, Saing’ore maarufu kwa jina la Sovoyo, alifanya kazi mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama.

Alisema diwani huyo ambaye sasa anagombea tena, alikaa madarakani kwa siku 63 kama Diwani wa Kata ya Mateves kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Arusha Vijiji (Arusha DC) hivyo kurudi kwake kama diwani kutawezesha wananchi kupata maendeleo.

Hatimaye Jecha Afunguka Kuhusu Kufuta Uchaguzi Zanzibar...

$
0
0
Baada  ya kimya kirefu, hatimaye Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha amefunguka na kuelezea kuwa uamuzi aliouchukua wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar wa mwaka 2015 baada ya kubainika kuwa na dosari, ulifanyika kwa kufuata taratibu, kanuni, Sheria na Katiba ya Zanzibar.

Jecha aliyasema hayo wakati akihojiwa na kipindi cha Funguka, kinachorushwa na Kituo cha Televisheni ya Azam na kusisitiza kuwa, hana wasiwasi wala hofu yoyote kwa hatua hiyo, aliyoichukua ya kufuta uchaguzi kwa kuwa ilifuata misingi yote ya Sheria na Katiba.

Pamoja na kwamba alikataa kujibu kwa undani kuhusu hatua yake hiyo na kusisitiza kuwa mengi atayabainisha kwenye taarifa ya tume, alisisitiza kuwa hakuwahi kutumika na chama chochote wala kuwasiliana na Rais Ali Mohammed Shein kama inavyodhaniwa na wengi.

“Haya yote yataonekana kwenye taarifa ya uchaguzi, siwezi kuongea hapa sasa ila kiukweli utaratibu ulifuatwa. Matokeo yalifutwa kutokana na dosari zilizojitokeza ikiwemo baadhi ya matokeo kujulikana kabla na kusababisha baadhi ya vyama kulalamika,” alisisitiza Jecha.

Alieleza kuwa matatizo na dosari za uchaguzi huo, yalianza kujitokea katika kipindi cha kupokea matokeo ambapo matokeo yalitoka katika maeneo ya Unguja, hayakubainika kuwa na matatizo, isipokuwa kwa matokeo yalitoka katika maeneo ya Pemba.

Alisema katika kura hizo za Pemba, ilibainika kuwa utaratibu wa kiufundi ulifanyika kuharibu matokeo ya hesabu za kura baada ya kufanyika urekebishaji wa kasoro wa mambo, ambayo hayakutakiwa yafanywe nje ya sheria za uchaguzi.

Alisema baada ya kutokea kwa dosari hizo, kwa upande wa tume kupitia yeye, iliamua kufuta uchaguzi mzima ili kuepusha vurugu na mgongano wa kisiasa huku Polisi ikifanya uchunguzi kuwabaini wahusika waliosababisha dosari hizo katika matokeo ya uchaguzi.

Kuhusu kushirikisha wajumbe wengine wa tume katika kufanya maamuzi ya kuufuta uchaguzi, Jecha alibainisha kuwa tume nzima ya ZEC ilihusika katika kufutwa kwa uchaguzi huo na ndio maana baada ya kufutwa taratibu za uchaguzi mwingine zilitekelezwa vyema na tume hiyo.

Hata hivyo, alibainisha kuwa katika kutangaza uamuzi wa kufuta uchaguzi huo, alilazimika kufanya hivyo binafsi baada ya kuona hali ya matokeo hayo inazidi kuwa mbaya na kwenda kinyume cha taratibu za uchaguzi.

Alibainisha kuwa baada ya kufuta uchaguzi huo, ili kuleta usawa kwa vyama vyote, tume hiyo ilisubiria vikao vya kutafuta mustakabali wa kisiasa visiwani humo vilivyokuwa vikifanyika baina ya viongozi wa kisiasa wa vyama vyote ndipo itangaze tarehe ya uchaguzi mpya.

“Tulikaa kimya kwa takribani mwezi mmoja tukisubiri hatua zichukuliwe na viongozi kupitia hivyo vikao vyao. Tulisubiri katika ule muda bila kuvunja sheria, na baada ya kuona hakuna hatua zinachokuliwa dhidi ya maamuzi yetu tulitangaza tarehe ya uchaguzi,” alieleza Jecha.

Mwenyekiti huyo alikanusha madai kuwa ametumika kufuta uchaguzi huo kwa maslahi ya CCM na Dk Shein. “Hapana, Sijawahi hata mara moja kuitwa au kutafutwa na kiongozi yeyote wa serikali, wala Rais sijawahi kuwasiliana na hata namba yake sina,” alifafanua.

Alisema ingawa hajawahi kukutana na mtu yeyote anayemlaumu kuhusu uamuzi wa tume hiyo wa kufuta uchaguzi, endapo kuna mtu bado ana malalamiko, anaruhusiwa kuiandikia ZEC malalamiko yake na si yeye binafsi, yatafanyiwa kazi.

Pamoja na hayo, mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa hata baada ya kuufuta uchaguzi huo, kwa kuwa anaamini alifuata taratibu na sheria zote, hakujificha wala kuogopa kitu, kwani aliendelea na shughuli zake kama kawaida.

“Hadithi zilikuwa nyingi, kila mmoja alifikiri alivyotaka yeye, mie nilikuwepo Zanzibar natembea, lakini si kila mtu alikuwa ananiona. Redio za kijamii kila moja ilikuwa inazungumza vyake, mwenyekiti yuko hivi, mwenyekiti yuko wapi, mwenyekiti kesho ananyongwa mara nimepelekwa mahakama za kimataifa yote hayo yalizungumzwa lakini mie nipo,” alisema.

Bibi Akutwa amekufa Huku akiwa na vibuyu 5 na kuku mweupe

$
0
0
Bibi  mwenye umri wa miaka 60 amekutwa amekufa mkoani Tabora huku amevaa nguo nyeusi aina ya kaniki, akiwa na vibuyu vitano na kuku mweupe, katika mazingira yanayoashiria kushiriki vitendo vya kishirikina.

Aidha, mwili wa mtu mwingine umekutwa pembeni ya mti aliokuwa akichimba dawa.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamis Selemani iliwataja waliokutwa wamekufa kuwa ni Nsoma Dotto (60) mkazi wa Kijiji cha Zugimlole Wilaya ya Kaliua na Mayara Marashi (50) ambaye ni mkazi wa Igunga.

Kamanda Selemani alisema Nsoma alikutwa akiwa amekufa umbali wa mita 200 kutoka nyumbani kwake juzi.

Alisema bibi huyo alikutwa amevaa nguo nyeusi aina ya kaniki akiwa na vibuyu vitano huku pembeni yake kukiwa na kuku mweupe. Uchunguzi wa awali wa jeshi hilo, unaonesha kuwa huenda ni imani za kishirikina.

Aidha, alisema Marashi ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Mwakapinga, Kata ya Nanga, aliyekuwa mganga wa kienyeji, mwili wake uliokotwa Januari 16, mwaka huu ukiwa umeanza kuharibika.

Kwa mujibu wa Kamanda Selemani, mganga huyo wa kienyeji aliondoka nyumbani kwake Januari 8, mwaka huu kwenda porini kuchimba dawa, lakini hakurudi kijijini hadi maiti yake ilipookotwa akiwa amekufa.

Alisema Polisi wanaendelea na uchunguzi wa kifo hicho. Aliwaomba wananchi wanaoenda porini kwa ajili ya shughuli zozote zile, wawe wanatoa taarifa kwa ndugu zao ili iwe rahisi tatizo linapotokea.

Rais wa Uturuki Awasili Nchini Kwa Ziara ya Kikazi

$
0
0
RAIS wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini jana jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt Çavuşoğlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak

Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images