Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya January 19


PICHA: Rais Magufuli Alivyomuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma Kuwa Kaimu Jaji Mkuu Wa Tanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatano Januari 18, 2018.  Anayeshuhudia kushoto ni Jaji Mkuu mstaafu Mohamed Chande Othman. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatano Januari 18, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Januari 18, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan  na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Katibu Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Profesa Sifuni Mchome na Naibu wake Mhe. Amon Mpanju wakiwa katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa, Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatano Januari 18, 2018. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na majaji wa mahakama ya Rufaa na Majaji wa Mahakama kuu baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatano Januari 18, 2018. 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, katika picha ya pamoja na watendaji wa Mahakama baada ya kumuapisha Profesa  Ibrahim Hamisi Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Ikulu jijini Dar es salaam  Jumatano Januari 18, 2018.

Waziri Mkuu Amaliza Mgogoro Wa Mpaka Kilindi Na Kiteto.........Awaonya viongozi wa siasa wasiwavuruge wananchi

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameumaliza mgogoro wa mpaka wa ardhi baina ya vijiji vya wilaya za Kiteto na Kilindi uliodumu kwa muda mrefu.

Mgogoro huo ambao ulianza kusuluhishwa tangu mwaka 1997, umepata suluhu kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu na kuwajumuisha Wakuu wa Mikoa hiyo miwili, Wabunge wa Kiteto na Kilindi, wenyeviti wa Halmashauri na madiwani wa kata mbili za mpakani pamoja na wananchi wa kata hizo.

Waziri Mkuu pia amewataka wanasiasa na viongozi wengine kutowavuruga wananchi na badala yake wawaongoze vizuri na kutoa maelekezo kwa mujibu wa sheria za nchi.

Ametoa agizo hilo jana (Jumatano, Januari 18, 2017)  wakati akizungumza na wananchi wa wilaya za Kiteto na Kilindi katika kijiji cha Lembapili wilayani Kiteto, mkoani Manyara ambako ni kuna mpaka wa  wilaya hizo mbili alipokwenda kutatua mgogoro huo.

Alisema viongozi wa wilaya hizo lazima wafuate sheria na wawaelekeze wananchi umuhimu wa kuzingatia sheria za nchi ikiwa ni pamoja na kuheshimu mipaka iliyowekwa kwa mujibu wa sheria ili kuepusha migogoro.

Akizungumzia kuhusu mgogoro huo wa mpaka, Waziri Mkuu alisema nchi ilishaweka mipaka ya mikoa na wilaya zake yote tangu zamani na kumbukumbu zipo zikiwemo za mpaka wa  wilaya hizo tangu mwaka 1961 kwa  tangazo la Serikali namba 65 na hakuna mabadiliko. Hivyo, aliwasisitiza wauheshimu na kuufuata.

Alisema Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi itakwenda kuweka alama vizuri na viongozi wa wilaya hizo watashirikishwa. Alama hizo zitawekwa na kifaa maalumu, hivyo amewataka wahusika watoe ushirikiano.

Waziri Mkuu alisema katika kipindi ambacho Serikali itakuwa ikiweka alama hizo, wananchi waendelee na shughuli zao hadi hapo zoezi litakapokamilika na wala wasibughudhiwe.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ametoa siku nane kwa watu wote wanaomiliki silaha katika wilaya za Kilindi na Kiteto wazipeleke kwenye vituo vya Polisi ili zisajiliwe upya na kisha Wakuu wa Mikoa wafanye operesheni maalum na atakayekutwa anamiliki silaha kinyume cha sheria achukuliwe hatua.

“Wakuu wa Mikoa fanyeni ukaguzi maalum na atakayekutwa anamiliki silaha kinyume na utaratibu achukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. Pia kuna watu wana mitambo ya kutengenezea bunduki hapa, nao pia waisalimishe haraka,” alisisitiza.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. William Lukuvi alisema mwanzoni mwa Februari wataalamu wake watakwenda katika mpaka huo ili kuanza kuweka alama vizuri.

Alisema baadhi ya viongozi huwa wana tabia ya kuzuia watendaji kutekeleza majukumu yao, hivyo ametumia gursa hiyo kuwaomba viongozi wa wilaya hizo watoe ushirikiano.

Alisema moja ya majukumu aliyopewa na Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ni kuhakikisha ndani ya miaka hii mitano anamaliza migogoro ya ardhi nchini ukiwemo huo wa Kilindi na Kiteto.

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU

Maiti iliyozikwa na Kisha Baadae Kukutwa Iko Nyumbani Kitandani Yazikwa Tena Chini Ya Ulinzi Mkali wa Polisi

$
0
0
Maiti ya mtoto Haruna Kyando (9) ambayo ilikutwa nyumbani muda mfupi baada ya wananchi kutoka makaburini kumzika, imezikwa kwenye makaburi ya Isanga chini ya ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi nchini, huku waombolezaji wakiaga mwili huo kwa kufunuliwa jeneza eneo la kichwani makaburini hapo.

Aidha, Mchungaji wa Kanisa la Bonde la Baraka, ameingizwa lawamani kwa kupotosha umma.

Haruna aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifafa tangu udogo wake, alikutwa na wazazi wake Jailo Kyando (36) ambaye ni muosha magari na mkewe, Anna Elieza (32) akiwa amefia usingizini Jumatatu wiki hii nyumbani kwao Mtaa wa Igoma A, Kata ya Isanga jijini Mbeya.

Kilichowapa taharuki wakazi wengi jijini hapa ni baada ya ndugu, jamaa na marafiki wa familia ya Haruna walipotoka makaburini siku hiyo walikokwenda kuzika, waliporejea nyumbani waliukuta mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye godoro, pale pale ulipowekwa wakati walipokuwa wakiuandaa kuuweka kwenye jeneza.

Hatua hiyo ilizua taharuki kubwa kiasi cha wananchi kutaka kufahamu ni kitu gani kilichozikwa ndani ya jeneza na ndipo Jeshi la Polisi lilipoingilia kati, kuzuia kufukuliwa kwa kaburi husika.

Hatua hiyo ilisababisha vurugu na hatimaye saa tatu za usiku siku hiyo hiyo ya maziko ya awali, Polisi wakalazimika kutumia mabomu ya machozi, kutawanya watu waliofurika katika makaburi ya Isanga wakishinikiza kaburi lifukuliwe.

Lakini juzi baada ya kukamilishwa kwa taratibu husika, ikiwemo kupatikana kwa kibali kutoka mahakamani, saa nne na nusu asubuhi, Polisi Mkoa wa Mbeya walifika eneo la makaburi alipozikwa marehemu na kusimamia shughuli nzima ya kufukua kaburi hilo.

Shughuli hiyo iliyodumu kwa muda wa nusu saa kama ilivyokuwa siku ya kwanza, ilihudhuriwa na mamia ya wakazi jijini hapa waliotaka kujua nini kilichozikwa ilhali mwili ukiwa umehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa wakati huo.

Nusu saa baadaye jeneza la mtoto huyo lilitolewa nje ya kaburi na ndipo Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma A, Fredy Mwaiswelo alipofunua jeneza na kukuta ndani kukiwa tupu, hali iliyoashiria mwili wa marehemu haukuwekwa ndani ya jeneza wakati wanakwenda kuzika.

Kutokana na hali hiyo, Polisi kwa kushirikiana na baadhi ya vijana, walibeba jeneza hilo na kuelekea nalo katika Kituo cha Polisi kwa ajili ya uchunguzi zaidi kabla ya kuwakabidhi tena wanandugu mwili ili kuendelea na taratibu za maziko kwa mara nyingine.

Baada ya ndugu kukabidhiwa mwili, jeshi hilo pia lilisimamia maziko yaliyofanyika upya saa 10 jioni katika kaburi lile lile la awali, lakini tofauti na awali, kabla ya kuzika ulifanyika utaratibu wa ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria, kuuaga mwili wa marehemu uliokuwa ndani ya jeneza lililofunuliwa upande wa kichwani.

Kutokana na mkanganyiko uliojitokeza, baadhi ya ndugu na majirani wa Mtaa wa Igoma, walisema tukio hilo linaweza kuwa na sura mbili kwa maana ya hujuma iliyofanywa kwa makusudi, ikilenga maslahi binafsi ya mtu inayohusishwa na imani za kishirikina au bahati mbaya ya kuusahau mwili wa marehemu.

Walisema inaweza kuwa hujuma kutokana na kawaida ya misiba kabla ya maziko, lazima ndugu watoe heshima za mwisho kwa marehemu, lakini kwa msiba huu haikufanyika pamoja na baadhi ya ndugu kutohudhuria mazishi.

Akizungumza  nyumbani kwake jana pamoja na kukanusha tuhuma za kuhusisha tukio hilo na imani za kishirikina, baba wa marehemu alisema mkanganyiko uliojitokeza wakati taratibu za kuuandaa mwili zikifanyika pamoja na uzushi uliofanywa na mchungaji, ambaye alisema hamjui kwa jina, ndiyo vilivyokuza jambo hilo.

Alisema kama ilivyo kawaida baada ya majirani kupata taarifa za msiba wakiwa nyumbani hapo, walichanga fedha na kutuma watu kwenda kununua jeneza.

“Wananchi walichanga hela wakanunua jeneza likaletwa nyumbani. Waliobeba jeneza walilisukumiza tu kwenye chumba wakatoka, sisi tukaendelea na taratibu nyingine za mazishi. Baadaye akaja mwenyekiti akasema toeni mwili wa marehemu nje, wakatoa meza nje wakatuma vijana waende kuchukua mwili wa marehemu ndani. Waliopeleka jeneza ndani na waliokwenda kulichukua ni watu wengine. Jeneza likawekwa juu ya meza tukaendelea na mahubiri,” alisema Kyando.

Alisema baadaye walikwenda kuzika na baada ya kuzika walirudi nyumbani kisha wakala chakula na kunawa maji, kama ilivyo desturi ya misiba mingi mkoani hapa.

“Tumenawa maji tukakaa. Baada ya kukaa kuna mgeni akaingia katika chumba tunacholala ambapo awali ndipo tulimlaza mtoto kwenye kigodoro, alipoweka begi akakuta kuna blanketi. 

"Alipolifunua akashtuka akasema kuna nyoka watu wakaanza kukimbia ndani. Baadhi ya watu wenye roho yenye hasira wakaamua kuingia ndani wakahakikishe kuna nini,” alisimulia. 

“Walipoingia ndani ndipo wakakuta ni mwili wa mtoto yaani marehemu. Waliposema ni mtoto wakipaza sauti watu wakajaa ndani. Ndipo waumini wa yule mchungaji wakaanza kumpigia simu yule mchungaji baadaye akarudi.”

Alisema baada ya mchungaji huyo kufika, aliingia ndani na waumini wake na kuanza kuomba.

“Walipoomba kwa muda mrefu ndipo mchungaji huyo alipotoka nje na kushika MIC na kuuambia umati kuwa mtoto baada ya kuombewa amehema mara mbili na ndipo watu wakaanza kulumbana,” alieleza.

“Kama siyo mchungaji kuzusha yale wala yasingekuzwa mpaka kwenye mitandao kiasi hiki. Sisi tunaamini walioagizwa kuchukua mwili walichukua jeneza tupu pasipo kuwekwa mwili ndani yake na kwa kuwa baada ya kutolewa jeneza hatukuingia ndani hivyo tuliuacha mwili nyumbani tukaenda kuzika jeneza peke yake,” alibainisha.

Akizungumzia suala la imani ya familia hiyo, Kyando alisema awali yeye na familia yake yenye watoto wawili, walikuwa wakisali katika Kanisa Katoliki, lakini kutokana na matatizo ya degedege yaliyokuwa yakimsumbua mwanawe wa kwanza, mkewe aliamua kumpeleka mtoto huyo kwa mchungaji wa Kanisa la Bonde la Baraka ili aombewe ikiwa ni sehemu ya kuhangaikia afya ya mtoto.

“Tulikuwa tunasali Roma, lakini kutokana na matatizo ya mtoto, mama yake akaamua aanze kusali Kanisa la Bonde la Baraka ili aombewe. Hapo mimi nikaacha kusali na ndiyo sababu hata katika ibada ya maziko ya mtoto ikabidi tulishirikishe kanisa walikokuwa wanasali mama na mtoto,” alisema Kyando na kuongeza: 

“Watu wamezungumza maneno mengi sana, siwezi kubisha japo ni ya uzushi ila wameongea kutokana na walivyosikia, ila ukweli naujua mimi na namwachia Mungu.”

Naye baba mkubwa wa marehemu, Saulo Kyando alisema jambo lililotokea lilikuwa la kawaida na kilichotokea ni kukosekana kwa uratibu makini wa msiba huo.

“Hili jambo lilikuwa la kawaida sema kilichokosekana ni mtu ambaye angeliweka jambo sawa, angekuwepo mtu wa kusimamia kila hatua yasingefikia hapa,” alisema Saulo.
Jeneza baada ya kufukuliwa kutoka kaburini
Mwenyekiti wa Mtaa wa Igoma pamoja na Baba wa Marehemu wakifunua jeneza kuhakikisha kama kulikuwa na mwili wa marehemu 
Jeneza lililofukuliwa likiwa halina kitu ndani yake 
Vijana wakiwa wanaondoa jeneza makaburini na kulipeleka kituo cha Polisi kwa ajili ya taratibu zingine

Jeshi la Senegal, Nigeria Kuivamia Gambia Usiku wa Kuamkia Leo Ili Kumng'oa Rais Yayha Jammeh Aliyegoma Kuachia Madaraka

$
0
0
Jeshi la Senegal limesema kuwa majeshi ya Afrika Magharibi yataingilia suala la Gambia usiku wa kuamkia tarehe ya mwisho wa madaraka ya Rais Yayha Jammeh ambayo ni leo  ili akabidhi madaraka kwa mshindi wa uchaguzi mkuu uliofanywa mwezi uliopita ,Adama Barrow ambaye kwa sasa yuko nchini Senegal..

Vikosi kutoka Senegal vimesogea katika mipaka ya Gambia, Nigeria pia imetuma vikosi vya anga katika eneo hilo.

Senegali imeomba Jumuiya ya Usalama ya Umoja wa Mataifa kushinikiza Umoja wa nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) kuchukua hatua za msingi katika kuhakikisha Rais mteule wa Gambia anakabidhiwa madaraka.

Kwa nini Senegal inaongoza Mpango wa Kumng'oa?
Ecowas, Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, iliipa Senegal jukumu hilo kwa sababu taifa hilo linaizunguka Gambia.

Kanali Abdou Ndiaye, msemaji wa jeshi la Senegal, amesema Ecowas iliamua kumuwekea Jammeh mkakati huo ili kujaribu kupata suluhu ya kidiplomasia.

"Mambo yote yako tayari na wanajeshi wa Ecowas wako tayari kuingilia kati baada ya saa sita iwapo hatutapata suluhu ya kidiplomasia kwa mzozo huu wa Gambia," alisema.

Wanajeshi hao wa Ecowas wanasubiri Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lipitishe azimio la kutumiwa kwa "hatua zozote zile" kusaidia kuondolewa madarakani kwa Be Jammeh. Wanajeshi wote wa Gambia ni takriban 2,500.

Nigeria imesema imetuma ndege za kivita na ndege nyingine za kawaida, pamoja na wanajeshi 200 nchini Senegal. Wanajeshi hao walienda Senegal Jumatano asubuhi.

Meli za kivita za Nigeria pia zimewekwa tayari baharini.Manowari moja iliondoka Lagos Jumanne na itakuwa na jukumu la kuwaokoa raia wa Nigeria walio nchini Gambia.Ghana pia inachangia wanajeshi


Credit: BBC

Mwenyekiti wa CHADEMA Ambaya Alikuwa Mpinzani wa Nape Nnauye Atupwa Jela Miezi 8 Kwa Kufanya Mikusanyiko Bila Kibali...

$
0
0
Mahakama ya Mkoa wa Lindi, imemuhukumu kwenda jela miezi nane, Suleiman Mathew ambaye alikuwa mpinzani wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika Jimbo la Mtama.

Mathew ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Lindi na kiongozi mwenzake wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.

Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha shaka.

Waliotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi, Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Mhina alisema, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali Juma Maige uliwafikisha mahakamani hapo mashahidi sita.

Alisema kutokana na ushahidi ulitolewa na mashahidi hao, mahakama imeona upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao bila kuacha shaka yoyote na kuwatia hatiani.

Baada ya kuwatia hatiani mahakama iliwapa nafasi washtakiwa ili waweze kujitetea ambapo waliomba  wapunguziwe adhabu.

Akiwasilisha hoja za upande wa utetezi Wakili wa washtakiwa hao,  Deusdet Kamalamo aliiomba mahakama isiwape adhabu kali kwa madai kwamba wanafamilia inawategemea, hivyo iwapo watapewa adhabu kubwa kutaifanya ikose huduma zao.

Baada ya utetezi huo, Wakili wa Serikali Juma Maige aliiomba mahakama hiyo iwape washtakiwa hao adhabu kwa mujibu wa sheria inavyoelekeza ili iwe fundisho kwao na wengine.

Hakimu Mhina akitoa adhabu katika kesi hiyo namba 36/2016, chini ya kifungu cha 74 (1) na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16, alisema mahakama inawapa adhabu, kila mshtakiwa  atatumikia kifungo cha miezi minane gerezani na kusema nafasi ipo wazi ya kukata rufaa iwapo wataona hawakuridhishwa na hukumu hiyo.

Baada ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mathew alisikika akiguna na baadae aliketi sakafuni, huku katibu wake wa tawi, Ismail  ambaye alionekana kuchoka kutokana na hukumu hiyo akiwa amelowa kwa jasho.

Mahakama hiyo pia iliwaachia huru washtakiwa wanne ambao ni wanachama waliokuwa wameshtakiwa pamoja na viongozi hao, baada ya ushahidi uliokuwa umetolewa na upande wa mashtaka kutokuwa na mashiko ya kuishawishi mahakama kuwatia hatiani.

Washtakiwa hao ni Bashiru Rashid, Hassani Mchihima, Abdallah Masikini na Mohamedi Makolela ambao wote ni wakazi na wakulima wa Kata ya Nyangamala.

Awali washtakiwa hao walidaiwa kutenda makosa hayo Aprili 3,  mwaka jana, maeneo ya Kata ya Nyangamala, mkoa Lindi, washtakiwa walifanya mkusanyiko usio halali.

Akizungumza nje ya mahakama hiyo, Wakili wa upande wa utetezi,  Deusde Kamalamo alisema wanajiandaa kukata rufaa kupinga uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo.

“Tutakata rufaa kupinga uamuzi huu, leo naandaa barua ya kuomba nakala ya hukumu ili tuanze kuandaa rufaa ya wateja wangu,” alisema Wakili Kamalamo.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Methew alikuwa akipambana na Nape ndani ya CCM lakini alishindwa kufurukuta katika kura za maoni na baadae alijiengua na kujiunga na Chadema na kuwa mgombea ubunge kupitia chama hicho.

Katika hatua nyingine jana Diwani wa Kata ya Kyangasaga, wilayani Rorya, Christopher Kichinda maarufu ‘Protocol’ amehukumiwa kwenda jela miaka mitano.

Akizungumzia hukumu hiyo Katibu wa Chadema Mkoa wa Mara, Chacha Heche, alisema diwani huyo alikuwa anakabiliwa na kesi ya Katiba iliyokuwa inamkabili kuwa alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Katiba la Wilaya lakini alijitoa ambapo mahakama ilimtia hatiani kwa makosa yaliyokuwa yanamkabili.

“Ni kilio kingine kwa demokrasia ya nchi yetu na ufanisi kwa siasa za CCM,” alisema Heche.

Mbowe Alaani
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumzia hatua ya Methew kuhukumiwa kwenda jela, alisema huo ni
mkakati ulioandaliwa Serikali ya CCM kudhohofisha upinzani na kuwatisha wasifanye siasa.

Hata hivyo, Mbowe aliwagiza viongozi wa chama hicho nchi zima kuandaa orodha ya kesi walizonazo ili kuziwasilisha jumuiya za kimataifa kuonyesha jinsi upinzani unavyokandamizwa na kupokonywa haki yao ya kufanya siasa.

Alisema Methew amehukumiwa wakati tayari Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali akiwa ameshahukumiwa kwenda jela miezi sita.

Serikali Yatoa Tahadhari Kuhusu Mafua Ya Ndege

$
0
0
Wizara  ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imewatahadharisha Watanzania juu ya kuwapo kwa virusi vya ugonjwa wa mafua ya ndege.

Ugonjwa huo umegundulika kuwapo katika nchi jirani ya Uganda ambako taarifa zinaeleza kuwa maeneo yaliyoathirika ni yale yanayozunguka Ziwa Victoria.

Tahadhari hiyo imetolewa jana na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kupitia taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari na Kurugenzi ya Mawasiliano Serikalini- Afya.

“Ugonjwa huu umegundulika baada ya kuwapo kwa vifo vingi vya ndege pori katika maeneo ya Lutembe Beach, Masaka, Kachanga, Bukibanga na Bukakata nchini Uganda.

“Vilevile, vifo hivi vimetokea kwa baadhi ya ndege wafugwao (kuku na bata) na inahisiwa kuwa ndege hao wamepata virusi vya ugonjwa huo kutoka kwa ndege pori wanaohama kutoka nchi za Ulaya,” alisema.

Waziri Ummy alisema vifo hivyo vya ndege pori vilianza kuonekana tangu Januari 2, mwaka huu na vimeonekana kuendelea hadi sasa.

“Kwa hapa nchini hakuna vifo vya ndege vilivyoripotiwa hadi sasa,” alisisitiza.

Alisema ingawa hadi sasa hakuna binadamu aliyeonekana kuwa na dalili za ugonjwa huo nchini Uganda, tahadhari inatolewa kwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kusambaa kwa binadamu ikiwa hatua madhubuti za kujikinga hazitazingatiwa.

Waziri Ummy alisema ugonjwa huo unasababishwa na virusi aina ya Influenza na huenezwa na ndege pori wanaohama hama.

Alisema ndege hao hubeba virusi vya ugonjwa huu bila ya kuonesha dalili za ugonjwa.

“Hivyo huweza kuambukiza ndege wanaofugwa majumbani mfano kuku na bata wakati wanapokutana nao. Aidha ndege hao huweza kuambukiza ugonjwa kupitia njia ya kinyesi ambacho hudondoshwa ardhini au kwenye mabwawa na madimbwi ya maji,” alisema.

Aliongeza: “Kwa kuwa binadamu huwezaa kuambukizwa ugonjwa huu kwa kugusana na ndege au kinyesi cha ndege aliyeathirika na ugonjwa huu. Ni muhimu kutokugusa mizoga ya ndege pori au kinyesi chake.”

Alisema kuwa binadamu anaweza pia kupata maambukizi wakati wa kuchinja kuku, kunyonyoa manyoya, na wakati wa kutayarisha kabla ya kumpika.

Waziri Ummy aliwataka wananchi watoe taarifa iwapo wataona dalili zozote za ugonjwa na vifo katika jamii ya ndege wa kufugwa na ndege pori.

“Kuna uwezekano wa virusi hivi kuambukizwa kutoka kwa binadamu mwenye uambukizo kwenda kwa binadamu mwingine, na hii ikitokea inaweza kusababisha mlipuko mkubwa unaoweza kusambaa pande zote za dunia,” alisema.

Lema na Mkewe Wakana Mashitaka Dhidi Yao......Mawakili Wake Waomba Kesi Ipelekwe Mahakama ya Katiba

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) jana alikana tuhuma za makosa ya jinai kwa pamoja na mkewe, Neema, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Mbele ya Hakimu Mkazi, Nestory Barro, Lema na Neema walikana mashtaka ya kutuma ujumbe mfupi wa simu ya mkononi wenye matusi kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Awali akiwasomea maelezo ya kesi hiyo Wakili wa Serikali Alice Mtenga alidai kuwa Lema na Neema, Agosti 20 mwaka jana, ndani ya Jiji la Arusha, walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani kwa mkuu huyo wenye lugha ya matusi, huku wakijua ni kosa kisheria.

Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka simu namba 0764-150747 kwenda namba 0766-757575 uliokuwa ukidai, “Karibu, tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga.”

Baada ya kuwasomea maelezo hayo ya awali, washtakiwa hao kwa pamoja walikiri kuwa ni wakazi wa Arusha na Lema ni Mbunge wa Arusha Mjini ila walikataa kusambaza ujumbe huo wa kumtukana Gambo na tarehe ya kukamatwa kwao.

Hakimu Barro aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 3, ambapo upande wa Jamhuri utaanza kuwasilisha ushahidi wake Gambo akiwa wa kwanza.

Baada ya kesi hiyo kuahirishwa, wakili wa Lema, John Mallya aliiambia mahakama wanatoa notisi ya kuwasilisha pingamizi la mdomo kwa kuwa hati ya mashtaka ina mapungufu, na baadaye wataomba mahakama iitupilie mbali hati hiyo.

Hata hivyo, Hakimu huyo alisema hoja za awali za pingamizi hilo zitasikilizwa Februari 3 pia.

Mbali na Mkuu wa Mkoa, Jamhuri inakusudia kuita mashahidi wengine wanne, ilielezwa.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mtenga upande wake pia utakuwa na vielelezo vitatu vitakavyotolewa
mahakamani hapo.

Alisema mashahidi watano watakaotoa ushahidi wao ni Gambo, Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Arusha (RCO), George Katabazi, (ASP) Damasi Massawe, mhusika kutoka kampuni ya simu ya Vodacom pamoja na mtaalamu wa picha.

Pia alivitaja vielelezo watakavyovitoa katika kesi hiyo kuwa ni nakala ya taarifa za mawasiliano ya simu kutoka kampuni ya Vodacom, simu ya mshtakiwa mke wa Lema na taarifa ya uchunguzi kutoka kitengo kinachoshughulikia masuala ya kiuchunguzi (Forensic Bureau).

Wakati huo huo, wakili wa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, John Mallya amemuomba Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Bernard Nganga kutoanza kusikiliza kesi ya kuhamasisha maandamano Septemba Mosi (Ukuta) inayomkabili Lema peke yake.

Akitoa ombi hilo jana, Mallya alidai kuwa kesi hiyo ya kuhamasisha maandamano kwa njia ya mtandao wa kijamii kisha kuusambaza Agosti Mosi hadi Agosti 26 mwaka jana, haifai kusikilizwa katika mahakama hiyo sababu kuna hoja za Kikatiba.

Alisema shahidi aliyeandaliwa kwa ajili ya kutoa ushahidi wake ambaye ni RCO, George Katabazi hapaswi kutoa ushahidi mahakamani hapo, sababu kesi hiyo ina hoja za kikatiba.

“Mheshimiwa kesi hii ukiiangalia ipo kikatiba zaidi na kwasababu ipo kikatiba basi sisi tunaenda Mahakama Kuu ikasikilizwe na majaji watatu ili tupewe tafsiri ya vifungu vya sheria," alisema Mallya.

Alisema kwa Katiba ya Jamhuri ya mwaka 1977 inampa haki kiongozi au mwanasiasa kufanya shughuli za kisiasa.

"Kuwakataza au kuingilia kati tunataka kujua huko Mahakama Kuu ya Katiba, nani ana mamlaka ya kuzuia maandamano."

Naye wakili wa Serikali Mtenga alimuomba hakimu kutupa pingamizi la Mallya alilolitoa mahakamani hapo, badala yake kesi hiyo iendelee kusikilizwa kwani upande wa Jamhuri tayari ulishamuandaa
shahidi wake.

Hakimu Nganga alisema amesikia hoja za mawakili hao wa pande zote mbili na yeye anaendelea na kesi hiyo baada ya aliyekuwa
 
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Augutino Rwezile kupanda cheo na kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kitengo cha biashara.

Alisema atatoa uamuzi wa kesi hiyo, kusikilizwa au kwenda kwa majaji watatu Februari 8.


Kajala Masanja akanusha binti yake kuharibikiwa kimaadili, ni baada ya video ya Ngono kusambaa mtandaoni

$
0
0
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii ipo video iliyosambaa ambayo inamuhusu binti mdogo wa chini ya miaka 18 akifanya mapenzi na mtu mzima ndani ya Gari.

Awali ilisemekana kuwa katika video hiyo binti aliyeonekana ni Paula Paul ambaye ni mtoto wa staa wa filamu Kajala Masanja hali ambayo ilimfanya muigizaji huyo kukanusha uvumi huyo.

Muigizaji huyo kupitia instagram ameandika:
"Hey everyone….jamani mimi sina shida na mtu kama akinichukia au akinisema mimi kwa kitu chochote kile…kwasababu najua binadamu kuongea mmezoea..ila katika kuongea kwenu,kuingilia na kujudge my life naomba msimuingize mtoto wangu…

"Sijawahi kumuomba mtu anisaidie kulea hata siku moja…mimi nimeona kuna video insambaa mnasema ni mwanangu na mnajua kabisa sie paula huyo ila ilimradi tu mfurahishe roho zenu…nilinyamaza…ila sasa naona mnakoelekea ni pabaya..mnahisi yeye hana moyo? Au mnahisi haumii?.

"Mwanangu anasoma na sitaki mumchanganye na mambo yenu ya kipuuzi…vitu vibaya mnavyo muombea mwanangu viwarudie wenyewe…leave my daughter alone jamani…give us a break..fanyani tu mambo yenu yatakayofanya mpate faida katika maisha”,
Hey everyone....jamani mimi sina shida na mtu kama akinichukia au akinisema mimi kwa kitu chochote kile...kwasababu najua binadamu kuongea mmezoea..ila katika kuongea kwenu,kuingilia na kujudge my life naomba msimuingize mtoto wangu...sijawahi kumuomba mtu anisaidie kulea hata siku moja...mimi nimeona kuna video insambaa mnasema ni mwanangu na mnajua kabisa sie paula huyo ila ilimradi tu mfurahishe roho zenu...nilinyamaza...ila sasa naona mnakoelekea ni pabaya..mnahisi yeye hana moyo? Au mnahisi haumii?.mwanangu anasoma na sitaki mumchanganye na mambo yenu ya kipuuzi...vitu vibaya mnavyo muombea mwanangu viwarudie wenyewe...leave my daughter alone jamani...give us a break..fanyani tu mambo yenu yatakayofanya mpate faida katika maisha yenu na sio mwanangu....na pia mjue kua mnamdhalilisha huyo binti na sio paula tena...na huyo binti ana wazazi na familia pia...hope tumeelewana
A photo posted by Kajala Masanja (@new_kajala) on

Mpenzi wa Ray Kigosi, Chuchu Hans ajifungua mtoto wa kiume

$
0
0
Mpenzi wa msanii mkongwe wa filamu Ray Kigosi, Chuchu Hans amejifungua mtoto wa kiume wiki hii, Ray amethibitisha.
 
Muigizaji huyo ameonyesha furaha yake kwa kuwa huyo ni mtoto wake wa kwanza.

“Asante mungu kwa kuniletea pacha wangu asante my lovely mzungu kwa kunipa heshima kubwa kunifanya niitwe baba, mungu wangu wa haki asiyeshindwa na jambo akubariki sana,” muigizaji huyo aliandika Instagram.

Aliongeza,“Sasa msianze maneno yenu kwamba mwanangu amekunnywa maji, mtoto bado ni mchanga maana watu wa Insta kiboko lakini hawaishi mtoni,”

Kwa upande wa Chuchu Hans huyo ni mtoto wake wa pili, mtoto wake wa kwanza alizaa na mume wake wa zamani.

Rais Magufuli Ateua Mabalozi Sita Kuwakilisha Tanzania Nchi Mbalimbali

Mkapa Amfuata Tena Rais Magufuli IKULU

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa katika mazungumzi na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman na Balozi wa Denmark Nchini Mhe. Einar Jensen Hebogard na ujumbe wao pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiagana na Waziri wa Maendeleo wa Denmark Mhe. Martin Bille Herman na Balozi wa Denmark Nchini Mhe. Einar Jensen Hebogard wakiwa pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango (kuhoto) na Katibu Mkuu Wizara hiyo Mhe. Dotto James (kulia) Ikulu jijini Dar es salaam leo Alhamisi Januari 19, 2017

Wizara zote zatakiwa Kuhamia Dodoma kabla ya Feb. 28

$
0
0
Serikali imezipa msisitizo wizara mbalimbali kuhakikisha zinahamishia makazi yake Makao Makuu ya nchi mkoani Dodoma kabla ya Februari 28, mwaka huu, kama ilivyotangazwa na Rais John Magufuli mwaka jana.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Ulemavu, Jenista Mhagama, alisema agizo la serikali lazima liwe limetekelezwa ifikapo Februari 28, mwaka huu.

“Kama agizo lilivyotolewa na Rais Magufuli kuhusu wizara na watumishi wake kuhamia Makao Makuu Dodoma, ndivyo wanavyotakiwa manaibu makatibu wakuu, makatibu, manaibu mawaziri na mawaziri kutakiwa kuwapo Dodoma mwishoni mwa Februari,” alisema Mhagama.

Waziri Mhagama alisema ofisi yake imeweza kukagua miundombinu na ujenzi wa majengo mbalimbali ya serikali yanayoendelea kujengwa na mengine yakiwa yamekamilika kwa ajili ya matumizi ya wizara hizo.

“Hakuna tatizo la ofisi za watumishi wa wizara zote, kwani majengo yamekamilika na yapo katika hali nzuri tayari kwa ajili ya kuanza kutumiwa, hivyo wakuu husika wakiwamo mawaziri wahakikishe wanatakiwa kuhamia Dodoma,” alisema.

Mbowe Amkabidhi David Kafulia Kadi ya CHADEMA

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amempongeza aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila kwa kujiunga na chama hicho kwa mara nyingine huku akisema kuwa kilichompata ni ajali ya kisiasa.

Mbowe alitoa kauli hiyo wakati akimkabidhi kadi ya uanachama Mhe. David Kafulila ambaye amehama kutoka NCCR Mageuzi katika Mkutano Mkuu wa Kanda ya Victoria uliofanyika jana Jijini Mwanza.

Alisema David Kafulila amerudi katika chama ambacho alikuwa amekizoea na ambacho ameshiriki katika kukijenga.

Tazama video hapo chini.....

Rais Magufuli amvua ubunge na Uwaziri Dkt. Possi......Amteua Kuwa Balozi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Januari, 2017 amemteua Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi.

Kituo cha kazi na tarehe ya kuapishwa kwa Dkt. Abdallah Possi itatangazwa baadaye.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Abdallah Possi alikuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu aliyekuwa akishughulikia Ulemavu.

Kufuatia uteuzi wa Dkt. Abdallah Possi kuwa Balozi, nafasi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu (Ulemavu) itajazwa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
19 Januari, 2017

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya January 20

Donald Trump Kukabidhiwa Leo IKULU Ya Marekani

$
0
0
Mshindi wa uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba Donald Trump leo anatarajiwa kuapishwa kuwa rais wa 45 wa Marekani.

Bw Trump wa Chama cha Republican anatarajiwa kuapishwa mbele ya watu 750,000 mbele ya majengo makuu ya bunge la Marekani, Capitol Building, Washington D.C.

Kisheria, rais anafaa kuapishwa kabla ya saa sita mchana saa za Amerika Mashariki ambazo Afrika Mashariki ni saa mbili usiku.

Hii hapa ni ratiba fupi ya matukio yanayotarajiwa siku hiyo.

Saa 17:30 (Saa za Afrika Mashariki) Wanamuziki walioalikwa wataanza kutumbuiza.

19:30 Hotuba za kufungua sherehe zitaanza kutolewa.

20:00 Muda mfupi kabla ya saa Mbili Afrika Mashariki Donald Trump atalishwa kiapo cha kuwa rais wa Marekani na Jaji wa Mahakama ya Juu John Roberts.

Baadaye, kutakuwa na msafara baada ya sherehe ya kuapishwa ambao utaanza katika vidato vya jumba la Capitol Building kuelekea ikulu ya White House kupitia barabara maarufu ya Pennsylvania Avenue.

Bw Trump na mkewe Melania baadaye watacheza dansi katika matamasha matatu, mawili katika ukumbi wa mikutano wa Walter E Washington na jingine katika ukumbi wa Jengo la Makumbusho ya Taifa.

Miaka minane iliyopita, Rais Obama alipokuwa anaapishwa kura rais, waliohudhuria walikuwa watu 1.8 milioni.
 
Siku moja baada ya kuapishwa kwa Bw Trump, wanawake takriban 200,000 wanatarajiwa kuandamana Washington DC na miji mingine kumpinga Bw Donald Trump.

Hillary Clinton na mumewe Bill wamethibitisha kwamba watahudhuria sherehe hiyo, sawa na George W Bush na mkewe Laura.

Wamesema wanataka “kushuhudia kukabidhiwa madaraka kwa rasi mwingine kwa njia ya amani.”

Rais mwingine wa zamani Jimmy Carter atahudhuria pia, lakini George HW Bush, 92, na mkewe Barbara hawataweza kwa sababu za kiafya.

Chanzo: bbcswahili

Wanaosoma Diploma Sasa Kupewa Mikopo na Bodi ya Mikopo (HESLB)

$
0
0
Serikali imewasilisha pendekezo la mabadiliko ya Sheria ya Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ili kuwezesha wanafunzi wanaochukua Stashahada katika vipaumbele vya kitaifa, kupewa mikopo ya kuwawezesha kuchukua elimu husika.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako alisema mabadiliko hayo, yamelenga kuwezesha kasi katika uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako alisema mabadiliko katika Sheria Namba 4 ya Mwaka 2016 ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), yamelenga kutoa nafasi ya kada ya Stashahada inayohitajika ambao wamekuwa hawapati mikopo.

“Kwa lengo la kupata balance (mizania) na kwa kuwa Diploma nayo iko kwenye elimu ya juu, watoto ni wale wale. Kuna wengine nao wanashindwa kumudu gharama na ili serikali ipate uwiano mzuri tumeona ni vizuri kuwe na marekebisho ya sheria,” alieleza Profesa Ndalichako.

Profesa Ndalichako alisema kuna umuhimu mkubwa wa kada ya Stashahada, hasa wanaokwenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa kwenye msukumo wa Serikali ya Awamu ya Tano wa ujenzi wa taifa la vijana, kama ilivyo kwa wenye Shahada.

“Kama taifa tunazungumzia uchumi wa viwanda,wadau wote hata wale wa ngazi ya kati ni muhimu katika kuhakikisha kwamba ajenda hii inafanikiwa kama vile ambavyo wale wa digrii wangelifanya,” aliongeza waziri huyo.

Mwaka 2004, kulikuwepo na mabadiliko katika sheria hiyo iliyowezesha wanaochukua masomo ya sayansi, hisabati na elimu ya msingi (kwenye msisitizo wa sayansi na hisabati), kupata mikopo ya elimu, nafasi iliyoanza kutumika mwaka 2014, lakini hatua hiyo ilisimamishwa wakati wa muhula wa masomo wa mwaka 2016/17.

Hata hivyo, HESLB ilikaririwa ikisema kwamba maamuzi ya kusitisha utoaji wa mikopo, ililenga kutekeleza maagizo ya serikali. 

Hata hivyo, jana Profesa Ndalichako alisema kwamba uamuzi wa kusimamisha mikopo hiyo,ulitokana na nia ya serikali kufanya mabadiliko katika sheria hiyo ili kuipa wigo mpana zaidi kuliko kujikita katika eneo la sayansi pekee.

“Mwaka 2004 tuliingiza diploma, lakini kwa masomo ya sayansi pekee sasa, tunataka kuwa na kipengele kinachopanua wigo ili tuweze kuhusisha kozi nyingine za diploma ambazo zinaenda sanjari na vipaumbele vya kitaifa,” alifafanua waziri huyo.

Kwa mwaka wa masomo 2016/17, serikali ilipanga bajeti ya Sh bilioni 483 ambazo zitakopeshwa kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wale wanaoendelea. Katika mwaka huo, wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo walikuwa ni 25,715.

Mume Amuua Mkewe kwa Kipigo Kisa Kachumbari

$
0
0
Mkazi  wa mtaa wa Mageuzi, kata ya Ngokolo, manispaa ya Shinyanga, Ibrahimu Daniel (42) amemuua mke wake, kwa kushindwa kuhifadhi vizuri kachumbari na kupika mboga isiyo na kiwango.

Aidha mauaji hayo yaliyofanyika kwa kumporomoshea kipigo yalifanyika kwa kuwa alipika chakula kingine wakati kilichobaki mchana kilikuwepo.

Aliyeuawa ni Stella Ibrahimu (39) na alipigwa baada ya mumewe Daniel kurudi nyumbani na kuuliza kachumbari ambayo alikula jana yake ndipo mtoto aliyekuwa akimlea Elizabeth Ibrahimu (13) alipomuonesha, lakini hakuridhika nayo na kuanza kuuliza maswali kwa nini haikuhifadhiwa vizuri.

Baadhi ya waandishi wa habari waliofika eneo la tukio walielezwa na mtoto wa marehemu, Daniel Ibrahimu (12) kuwa baba yake alipofika nyumbani saa moja usiku alimkuta yeye akiwa na Elizabeth ndipo alipoanza kumhoji Eliza akimuuliza kachumbari yake iko wapi.

Daniel alisema baada ya Eliza kumuonesha baba yake kachumbari hiyo aliyoila na kuibakisha Jumatatu wiki hii, aliiona imechacha na kuonekana na uchafu, ndipo alitoka nje na kuchukua fimbo anayoihifadhi juu ya nyumba na kutaka kuanza kumpiga lakini kabla ya kumpiga mtoto huyo alichoropoka na kukimbia nje.

Aliendelea kusimulia kuwa baada ya kukimbia na binti huyo, mama yake ambaye alikuwa kazini alifika nyumbani wakati huo mfarakano ukiendelea na alimkuta baba yao akifoka na baada ya kuuliza kuna nini, aliambiwa kwa nini hakupika mboga yenye kiwango na kwa nini alipika ugali mwingine wakati kulikuwa na ugali uliobaki mchana.

“Mama alifika na kuanza kunywa chai lakini baba aliendelea kufoka ndipo mama alimjibu kwa hasira ndipo alipomuuliza baba uliacha fedha ya matumizi ya kuweza kupika mboga yenye kiwango, alianza kumpiga baadaye alimpiga na kikombe na mateke akaanguka ndipo mimi nilikimbia kwa majirani kuwataarifu mama anapigwa, walikuja na kukuta mama ameanguka chini baba akiwa anamruka ruka,” alisema Daniel.

Baadhi ya majirani waliofika katika tukio hilo, Gloria Shija na Retisia Mashalah, walisema kwa nyakati tofauti kuwa, walikuta baba huyo amefunga mlango na walipomgongea afungue, alikataa na kusema kuwa kuna kazi kidogo anaifanya wasubiri, lakini baada ya kuchungulia dirishani walimuona anampuliza puani na masikioni huku akimmwagia maji ili azinduke, baada ya kuona hazinduki.

Shija alisema kuwa waliingia ndani na kumkuta akiwa amemkalisha chini huku akiwa ameinamisha shingo ambapo walimbeba na kumtoa nje, walijaribu kummwagia maji tena lakini ilishindikana ndipo walichukua uamuzi wa kumpeleka hospitalini walifika na kuanza kupimwa, lakini alionekana tayari alishafariki muda mrefu.

Kwa mujibu wa majirani, waliporudi nyumbani, mwanaume huyo alionekana kumtuma mara kwa mara mwanawe wa kiume na wakaingiwa na hofu na kutoa taarifa polisi ambapo walifika na kuwachukua watoto wawili; Daniel na Eliza kwa mahojiano.

Shangazi wa marehemu, Getruda Vitalis alisema ugomvi huo ulikuwa ukitokea mara kwa mara. Mwenyekiti wa mtaa wa Mageuzi, Emmanuel Sama alisema yeye alikuwa amelala nyumbani kwake aligongewa mlango na kuambiwa kuna tukio la mwanamke kupigwa na mume wake na ana hali mbaya ndipo aliamka na kwenda katika tukio.

Baada ya kuuliza aliambiwa chanzo ni kachumbari iliyobaki jana haikuhifadhiwa vizuri na mtoto waliokuwa wakimlea, Elizabeth.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Elias Mwita, alithibitisha na kueleza kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi. Alisema uchunguzi wa awali katika mwili wa marehemu umeonesha kuwa na jeraha katikati ya kichwa na waliruhusu usafirishwe kesho wilayani Ngara, Kagera kwa maziko.

Kiongozi wa CHADEMA Apewa Kipigo na Vijana wa CCM Kwa Kuingilia Mkutano wao

$
0
0
Katibu wa Chadema Jimbo la Sengerema, Deusdeth Mwigala juzi, alipata kipigo kutoka kwa vijana wa CCM kilichosababisha apoteze fahamu baada ya kutuhumiwa kutaka kuvuruga mkutano wa hadhara. 

Kiongozi huyo wa Chadema alikuwa akipita karibu na eneo ambalo CCM walikuwa wakiendelea na mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani wa Kata ya Kahumulo, akiwa na vipaza sauti alivyotumia kutangaza mkutano wa chama chake, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kuvuruga usikivu.

Hata hivyo, katibu huyo alikana kuvuruga mkutano wa chama hicho akidai alikuwa umbali wa zaidi ya mita 200 kutoka eneo ambalo CCM ilikuwa ikiendesha mkutano.

“Wakati naendelea na kazi ya kutangaza mkutano wa Chadema nikiwa nimeongozana na makada wengine wanne na dereva, ghafla tulivamiwa na watu wa CCM na wakaanza kutushambulia,” alisema Mwigala akizungumzia tukio hilo lililotokea Kijiji cha Lubanda.

Alisema wenzake pamoja na dereva walifanikiwa kukimbia, lakini yeye alinaswa na wafuasi hao walioendelea kumshambulia kwa kipigo. 

Hata hivyo, mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, James Kisinza alimtupia lawama katibu huyo wa Chadema kwa kitendo cha kupita karibu na eneo la mkutano wa CCM akitangaza mkutano wa chama chake kwa kutumia vipaza sauti na hivyo kuvuruga usikivu. 

Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wilayani Sengerema, Hassan Moshi alisema wafuasi wao walichukizwa na kitendo hicho na kuamua kumuadhibu kiongozi huyo kwa madai kuwa alikuwa anavuruga mkutano wao kwa makusudi. 

“Viongozi tulilazimika kuingilia kati kumwokoa asiendelee kuadhibiwa na vijana wenye hasira, lakini ukweli ni kwamba mwenzetu alifanya kosa kwa kuingilia mkutano wa chama kingine kinyume cha sheria,” alisema Moshi. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema ofisi yake haijapokea taarifa hizo na kuahidi kuzitolea ufafanuzi baada ya kuzipokea kutoka Sengerema.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images