Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sehemu ya Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere(JNIA) Yateketea kwa moto usiku wa kuamkia leo.

$
0
0
Moto mkubwa umezuka kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA) usiku wa leo na kusababisha taharuki kubwa kwa wasafiri na watumiaji wa uwanja huo, ambapo imelazimu shughuli zote uwanjani hapo kusitishwa kwa muda wakati vikosi vya zimamoto vikiendelea na kazi yao kwenye uwanja huo mkubwa zaidi nchini Tanzania.

Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Martin Otieno amesema kuwa wamefanikiwa kuudhibiti moto huo na kwamba uchunguzi wa kina juu ya chanzo cha moto huo na hasara iliyosababisha, unaendelea kufanyika na kwamba tayari shughuli zote za kawaida zinaendelea kama kawaida.

Aidha Meneja wa Uwanja huo ameeleza kuwa kwa sasa shughuli zote za usafirishaji zimeamishiwa Terminal One na zinaendelea kama kawaida huku wakiweka sawa maeneo yalioathirika.

“Kwanza naomba niwatoe hofu Watanzania na wasafiri wote wanaotumia Uwanja wetu, ni kweli moto umezuka kuanzia majira ya saa 6 hadi saa 7 usiku wa kuamkia leo.

“Lakini madhara kidogo yametokea kwenye jengo la kuhifadhia mizigo pekee, hakuna mtu aliyepoteza maisha wala kujeruhiwa kutokana na moto, mashine zote zipo salama na sasa shughuli zote za usafirishaji tumezihamishia kule terminal one (Uwanja wa zamani) zinaendelea kama kawaida”. Amesema Meneja huyo.

“Baada ya kuudhibiti moto huo tumerudi kuangalia chanzo tukakuta, mfumo wa umeme uko sawa, hivyo hatujajua chanzo hasa cha moto huo ila tunajitahidi kufanya utafiti ili tujue.” Aliongeza Meneja na kusema taarifa zaidi, zitatolewa baadaye.

 Chanzo: GPL


Lowassa Akerwa na Gazeti Lililoandika Uongo Dhidi Yake.......Adai ni Mbinu Chafu Zinazofanywa na CCM

$
0
0
Waziri  Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amesema kasi ya kuimarika kwa umoja na mshikamano miongoni mwa vyama vya upinzani nchini, kunaitia kiwewe CCM kiasi cha kuanzisha mbinu chafu za kisiasa.

Kauli hiyo aliitoa jana mjini Kahama katika Hoteli ya Gaprina ambapo alifikia kabla ya kuanza safari ya kuelekea mkoani Kagera katika ziara ya kuimarisha chama chake.

Alisema kuimarika kwa mshikamano huo chini ya mwavuli wa Vyama Vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi  (Ukawa) ni hatua kubwa katika kuelekea kuing’oa CCM.

“Wameanza mbinu zao za kutaka kutuondoa katika umoja wetu, wameanza kuwalisha viongozi wetu maneno, mfano  gazeti (nalitaja jina) la leo (jana) wamenilisha maneno ya kwamba eti nimeitabiria CCM ushindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani kule Arumeru.

“… mambo ya ajabu kabisa hili  gazeti linaishi kwa kodi zetu sisi wananchi leo linaamua kutumika kuvunja demokrasia inasikitisha sana.

“Wanaandika uongo mchana kweupe kuwa nilikuwa katika kampeni kwenye kitongoji Ematasia..mimi sikwenda huko..lakini mbinu zao hizi wananchi wameshazijua na hawako tayari kuona hamu yao ya kupata mabadiliko inapotea,” alisisitiza.

Wakati huo huo mamia ya wakaazi wa mji wa Kahama waliizingira Hoteli ya Gaprina alikofikia Lowassa, wakiwa na nia ya kutaka kumwona.

Akiwa njiani kuelekea Bukoba, Lowassa na msafara wake alipata nafasi ya kusalimiana na wananchi katika mnada wa Lusaunga wilayani Biharamlo, ambako wananchi hao walimwambia kuwa hali yao ya maisha ni ngumu pamoja na hali mbaya ya ukame inayowakabili.

Hata hivyo Lowassa hakutoa kauli yoyote kwao zaidi ya kusema kwa sasa mikutano ya hadhara imepigwa marufuku na asingependa kuvuja sheria kwa kile alichodai amri kandamizi.

Mzee Majuto : Ntaendelea Kuigiza Hadi Siku Yangu ya Kifo Changu

$
0
0
Mkongwe wa Filamu za Kibongo nchini, aliyejipatia umaarufu kwa kuigiza vichekesho, Amri Athumani ‘Mzee Majuto’, aliyeanza kuagiza mwaka 1958 akiwa na miaka 10, ambaye mwaka jana aliwahi kutangaza kuacha uigizaji na kumrudia Mungu, amesema ataendelea kuigiza hadi anakufa kwa sababu uigizaji upo kwenye damu na hii inadhihirishwa wazi kwani ni miaka 58 sasa ya uigizaji wake na fani hii ameianza akiwa darasa la pili.

Majuto alizungumza hayo Dar es salaam Jana.Alisema hawezi kukubali kuona fani inachezewa na watoto, hivyo ataendelea kuigiza hadi siku atakayokufa kwa sababu uwezo wake ni wa hali ya juu kwenye kuandika na kuigiza.

”Kuigiza kwangu ni kama maradhi vile, hivyo sidhani kama naweza kuacha, siwezi kukaa pembeni  sanaa ikawa inachezewa na watoto sitaki kabisa,  nitaendelea kuigiza hadi nakufa,” alisema Majuto.

Mzee Majuto aliongeza ataendelea kuigiza  ili kuhakikisha anapata chipukizi ambaye anaweza kufanya kile alichokuwa anakifanya yeye hapo baadae.

Alisema bado hajapata mtu wa kurithi mambo yake katika tasnia hiyo, hivyo hawezi akakurupuka kuachana na kazi hiyo bila ya faida ambayo kwa upande wake ni kupata mrithi.

Mapinduzi Cup Fainali leo ni Simba au Azam FC?

$
0
0
Fainali za 11 za michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup zinatarajiwa kupigwa leo kwenye dimba la Amaan Visiwani Zanzibar kwa kuzikutanisha timu za Simba na Azam zote za Dar es Salaam.

Mchezo huo unaotarajiwa kuanza Saa 2:15 usiku wa leo, utakuwa ni wa pili kuzikutanisha timu hizo katika fainali ya michuano hiyo.

Awali zilikutana katika fainali ya mwaka 2012 na Azam FC ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kutwaa taji lake la kwanza kati ya mawili ya Kombe la Mapinduzi, linguine likija mwaka 2013 baada ya kuifunga Tusker katika fainali.

Simba ndiyo mabingwa mara nyingi wa taji hilo, mara tatu baada ya kulitwaa katika miaka ya 2008 ikiifunga Mtibwa Sugar katika fainali, 2011 ikiwafunga mahasimu, Yanga na 2015 wakiwafunga Mtibwa Sugar.

Kocha wa Simba Joseph Omog, amepania kulitwaa taji hilo, kwa lengo la kuondoa ukame wa makombe ambayo umeikumba klabu hiyo kwa misimu minne iliyopita pasipo kubeba ubingwa wowote

Azam mara zote ilizoingia fainali ilitwaa taji hilo, wakati Simba mwaka 2012 na 2014 ilicheza mechi ya mwisho na kufungwa na kukosa Kombe hilo.

Kuelekea mchezo wa leo, kila timu iko vizuri baada ya rekodi nzuri katika mechi zilizopita, Simba wakiwatoa wapinzani wa jadi, Yanga kwa penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 kwenye Nusu Fainali na Azam wakiitoa Taifa Jang’ombe kwa bao 1-0.

Timu zote ziliongoza makundi yao, Simba A lilikuwa na timu tano kwa pointi zake 10 na Azam B lililokuwa na timu nne kwa pointi zake saba.

Mganga Auawa Kwa Kuchomwa Visu........Kisa ni Kuwatapeli Watu Kwamba Atawapa Utajiri

$
0
0
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la DOTTO MWAIPOPO mkazi wa Kafundo – Ipinda wilayani Kyela Mbeya ameuawa kwa kuchomwa kisu ubavu wa kulia na BONIPHACE KISWAGA Mfanyabiashara na Mkazi Chaugingi Mkoani Njombe kwa madai ya kufanya utapeli.

Taarifa ya Polisi Mkoa wa Mbeya imesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 11.01.2017 majira ya saa 4 usiku katika Kitongoji cha Ipinda – Chini, Kijiji na Kata ya Ipinda, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya.

Inadaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni kulipiza kisasi baada ya marehemu kuwatapeli watuhumiwa pesa ambazo kiasi halisi bado hakijafahamika kwa madai kuwa yeye ni mganga wa kienyeji na atawasaidia kuwa matajiri.

Aidha katika tukio hilo mtuhumiwa huyo BONIPHACE KISWAGA alijeruhiwa kwa kupigwa na wananchi na amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kyela kwa matibabu. Watuhumiwa wengine wawili ambao walikuwa pamoja na mtuhumiwa aliyekamatwa walikimbia na msako mkali unaendelea.

Insta inayotumika kumtusi Diamond yaendelea kutoa matusi wakati mtuhumiwa mwenye akaunti yupo Selo

$
0
0
November 18, 2016 kijana mmoja ambaye jina lake halikutambulika mara moja alikamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kutumia akaunti ya ‘Shilolekiuno_official’ kuwatukana watu mbalimbali akiwemo Diamond pamoja na familia yake.

Lakini cha kushangaza akaunti hiyo bado inaendelea kutukana watu wakati mtuhumiwa yupo ndani.

Sallam ambaye ni meneja wa Diamond ndiye aliyetoa taarifa za kukamatwa kwa kijana huyo mwezi Disemba mwaka jana.

“Kwa watu wote kama ulitukanwa na huyu ambae anaejiita @shilolekiuno_official kwa sasa yupo chini ya mikono ya sheria, Kama una mashitaka yoyote fika Oyster Bay Polisi, Vizuri ametaja watu wanaemtuma afanye hivyo! Na kuwasaidia wale ambao wanajiamini kuwa hawawezi kujulikana basi kwa taarifa yenu Serikali ina mkono mrefu sana! Eti Jana alikuwa anamuita Diamond “Simba” 😂😂😂.” aliandika Sallam Insta baada ya kukamatwa kwa jina hiyo.
Hata hivyo kamanda wa polisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa hakuna kijana kama hiyo aliyekamatwa.

“Hatujamkamata na hatuna mtu kama huyo kituoni kwetu. Tuna vijana wengi ambao wamekamatwa wanamakosa kama hayo, jina kama hilo uliloniuliza halipo hapa kituoni kwetu labda kwenye kituo kingine.”
Hii ni baadhi kati ya post mpya za kwenye akaunti hiyo.

Rais Magufuli Atishia Kuyatumbua Magazeti Mawili

$
0
0
Rais wa Jamhri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 13 Januari, 2017 ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini.

Rais Magufuli ametoa onyo hilo wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli amesema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo.

''Serikali ya kutumbua majipu haiwezi kuacha kutumbua magazeti yanayofanya mambo ya uchochezi hatuwezi kuiacha Tanzania ikawa dampo la eneo la kuweka maneno ya uchochezi chini ya utawala wangu hilo halitakuwepo kuna magazeti mawili tu kila ukisoma wao ni kuchochea tu ikizungumzwa habari hii wao wanageuza hii nasema na nataka wanisikie siku zao zimeshafika kama wanasikia wasikie wasiposikia  wasisikie lakini magazeti mengine na vyombo vyote vingine vinatoa uchambuzi mzuri sana''.

Rais Magufuli amesema Serikali yake haiwezi kuvumilia kuona amani ya nchi inahatarishwa na magazeti mawili kwani amani ndio chimbuko la maendeleo ya taifa lolote duniani.

Amesema bila kuwepo kwa amani hakuna mwekezaji atakayeweza kuja kuwekeza nchi, hata wawekezaji wa ndani watashindwa na hivyo kurudisha nyuma maendeleo ya nchi.

Rais Magufuli amesema uwepo wa amani nchini ndio uliowezesha wawekezaji wa Kiwanda cha Fresho cha kutengenezea mifuko ya kubebea bidhaa za chakula nchini na kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga kujengwa mkoani hapo kwani bila amani visingeweza kujengwa.

Aidha ameitaka Benki ya Uwekezaji Nchini TIB na Taasisi nyingine za fedha kutoa mikopo kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza katika viwanda badala ya kuwakopesha wanasiasa ambao hutumia fedha wanazokopa kwa matumizi yasiyowanufaisha watanzania waliowengi

Rais Magufuli ameupongeza uongozi wa mkoa wa Shinyanga kwa kuanza kutekeleza kwa vitendo azma ya Serikali ya kutaka Tanzania ya viwanda kwa kujenga viwanda vingi mkoani humo ikiwa ni pamoja na viwanda hivyo viwili alivyovizindua katika siku yake ya mwisho ya ziara mkoani Shinyanga.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, Ikulu
Shinyanga

13 Januari 2017.

Taarifa Kwa Umma Toka Ofisi Ya Makamu wa Rais


Jipatie Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kutoa Michirizi, Kuondoa Chunusi, Kuongeza Maumbilie na Nguvu za Kiume

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS ni kampuni inayoongoza kwa kutoa bidhaa original za asili zenye matokeo mazuri bila kemiko wala madhara yoyote pia tunatoa punguzo la bei la %10 kwa ajili ya Xmas and new year pata bidhaa kwetu uweze kufurahia matokeo mazuri kwa bidhaa original.

     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
 
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
 
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @10,000/= vidonge maalum @150,000
 
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @130,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 130,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
 
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 100,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 120,000
 
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @120,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @90,000/=
 
12.kuotesha nywele kwenye kipara @120,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=

     WASILIANA NASI KWA NAMBA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma zetu. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti unapewa ili kuhakikisha mafanikio yako
           Follow us 
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya January 14

NEC yaijibu ACT Wazalendo kuhusu chaguzi ndogo

$
0
0
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekishauri Chama cha ACT – Wazalendo na Vyama vingine vyenye wagombea wa Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani na Udiwani katika Kata Ishirini (20) za Tanzania Bara ,kuwasilisha malalamiko ya ukiukwaji wa Maadili ya Uchaguzi kwenye Kamati za Maadili zilizo katika maeneo yao.
 
Akizungumza na vyombo vya habari jana  jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan alisema NEC imepata taarifa kupitia Vyombo mbalimbali juu ya malalamiko ya Chama Cha ACT-Wazalendo kuvilalamikia Vyombo vya Dola pamoja na Watendaji wa Umma kufanya vitendo vyenye muelekeo wa kukipendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM).
 
Bw. Kailima alisema taarifa ya Chama hicho iliyotolewa kwenye Vyombo vya Habari Januari, 12 2017, imeeleza kuwa Watendaji wa Halmashauri ya Geita waliwakusanya Wazee katika Kata ya Nkoma waje na Vitambulisho vyao vya kupigia Kura kwa lengo la kuwapatia huduma ya afya bure jambo linalolalamikiwa na ACT- Wazalendo kwa madai kwamba Watendaji hao wana lengo la kuwahadaa Wazee hao ili wakipigie Kura Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Wizara ya Elimu Yatoa ONYO Kali......Ni Kuhusu Kuwatimua Wanafunzi Vilaza

$
0
0
Serikali imezionya shule zote za sekondari na msingi nchini hususani za mashirika ya dini ambazo bado zinakaririsha wanafunzi darasa kwa kigezo cha kutofikia alama za ufaulu zilizowekwa na shule, kuacha kufanya hivyo kwa kuwa ni kinyume na sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Kamishna wa Elimu nchini Nicolas Burreta imesema kuwa serikali kupitia wizara ya elimu imebaini kuwa bado kuna shule ambazo mbali na kukaririsha wanafunzi darasa, zimekuwa pia zikiwafukuza wanafunzi shule, na nyingine zikiwahamishia katika shule nyingine.

Kamishna Burreta katika taarifa hiyo ameziagiza shule hizo kufuta maagizo yao ya ama kuwakaririsha darasa, kuwafukuza wanafunzi hao, au kuwahamisha huku akiwataka wazazi ambao watoto wao wamefukuzwa au kuhamishwa, wawarudishe watoto wao katika shule hizo waendelee na masomo.

Pia amewataka wathibiti ubora wa shule, kanda wilaya na maafisa elimu wa wilaya na mikoa kusimamia agizo hilo na kwamba shule yoyote itakayokiuka maagizo hayo itachukuliwa hatua kali za kisheria.

Ufafanuzi wa Wizara ya Nishati Kuhusu Tuhuma za Profesa Muhongo Kushiriki Kupandisha Bei ya Umeme

$
0
0

Wizara ya Nishati na Madini inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu kikao cha Waziri wa Nishati na Madini na Ujumbe wa Benki ya Dunia kilichofanyika tarehe 28.09.2016 kikihusishwa na kupandishwa kwa bei ya umeme kama ilivyoripotiwa na magazeti ya Mwananchi ya tarehe 12.01.2017 lenye kichwa cha habari “Prof. Muhongo alivyoshiriki kupandisha bei ya umeme” na la tarehe 13.01.2017 lenye kichwa cha habari“Prof. Muhongo awekwa mtu kati”.

Wizara inapenda kuutaarifu Umma kuwa, imekuwa ikifanya vikao na wadau mbalimbali wakiwemo Taasisi za Umma, Binafsi na Washirika wa Maendeleo yakiwemo Mashirika ya Kifedha ya Kimataifa. Lengo la vikao hivyo ni pamoja na kuhamasisha uwekezaji katika Sekta za Nishati na Madini nchini.

Aidha, tarehe 28/9/2016 Wizara ilifanya kikao na Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ikiwa ni mwendelezo wa vikao vya majadiliano kuhusu upatikanaji wa mkopo wa Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya kuboresha uendeshaji wa Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO). 

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na taasisi nyingine zikiwemo Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Katika kikao hicho masuala yaliyojadiliwa yalikuwa ni;

1.  Upatikanaji wa umeme wa kutosha, uhakika na  bei nafuu kwa ajili ya kuchochea shughuli za maendeleo ya kukuza uchumi wa nchi ikiwemo viwanda, biashara, kilimo na huduma za jamii;
2.  Kuongeza ufanisi wa utendaji wa Shirika la Umeme (TANESCO); na
3.  Kupunguza deni la TANESCO.

Katika kulipunguza deni la TANESCO ambalo linakaribia Shilingi Bilioni 800 (takriban Dola za Marekani Milioni 363) na kuboresha shughuli za utendaji za TANESCO, Benki ya Dunia ilijadiliana na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Madini ili kupata mkopo wa Dola za Marekani Milioni 200. Hivyo, katika kikao hicho, hakukuwa na makubaliano ya kupandisha bei ya Umeme kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo.

Vile vile, tunaomba kuutaarifu Umma kwamba Wizara ya Nishati na Madini kwa niaba ya Serikali inafanya majadiliano na Benki ya Maendeleo ya Africa (AfDB), Umoja wa Ulaya (EU), JICA (Japan), na Mashirika mengine ya fedha kwa lengo la kutafuta fedha za kuboresha Sekta ya Nishati.

Imetolewa na;
WIZARA YA NISHATI NA MADINI
13.01.2017

Tangazo Kwa Umma Kuhusu Wahitimu Wa Shahada Na Stashahada Za Ualimu (Sayansi) Waliotakiwa Kuwasilisha Vyeti

Mhadhiri Chuo Kikuu Akamatwa na TAKUKURU Kwa Kuomba Rushwa ya Ngono ili Ampatie matokeo mazuri ya mtihani wake wa Supplementary

$
0
0
Mhadhiri Msaidizi wa Chuo cha Taifa cha Usifirishaji (NIT) amekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Konondoni baada ya kunaswa katika mtego wa rushwa ya ngono.

Mhadhiri huyo anayefahamika kwa jina la Samson Jovin Mahimbo (66) mkazi wa Makongo Juu, Dar es Salaam alikamatwa  Januari 12, 2017 katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kama Camp David iliyopo eneo la Mlalakua, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Samson Mahimbo alikamatwa baada ya kuwekewa mtego kufuatia taarifa iliyotolewa na mwanafunzi huyo aliyeombwa rushwa ili aweze kumpatia alama (marks) nzuri  katika mtihani wake wa marudio (supplementary examination) alioufanya tarehe 5 Januari 2017.

Mtuhumiwa huyo amekamatwa kwa tuhuma za kufanya kosa hilo kinyume na kifungu cha 25 cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2017.

Video: Joti alivyoirudia Muziki ya Darassa kwa kuifanyia hii video

$
0
0
Msanii wa vichekesho Bongo, Joti ameurudia wimbo wa Darassa ‘Muziki’ ambao kwa sasa unafanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga. Tazama video hiyo hapa chini

Azam Fc Yatwaa Ubingwa wa Mapinduzi Cup 2017 Kwa Kuitandika Simba 1-0

$
0
0
Shuti la ‘mwendokasi’ la umbali usiopungua mita 25 la kiungo Himid Mao limetosha kuamua matokeo ya mchezo wa Fainali ya Mapinduzi uliofanyika mjni Zanzibar.

Miamba hiyo ya Ligi Kuu Tanzania Bara iliichapa Simba bao 1-0 na kutosha kutangazwa mabingwa wapya wa Kombe la Mapinduzi.

Wakinolewa na kocha wa vijana wa Azam, Idd Cheche aliyechukua kwa muda mikoba ya Zeben Hernandez aliyetimuliwa kwa matokeo mabaya, Azam FC iliibuka na ushindi wa bao la dakika ya 13 lililofungwa na kiungo huyo wa Taifa Stars, Himid.

Ushindi huo pia umeifanya Azam FC kutwaa taji la tatu la Kombe la Mapinduzi baada ya awali kulitwaa miaka ya 2011 na 2012.

Katika mashindano hayo, beki wa Simba, Method Mwanjali amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Mapinduzi Cup, tuzo ya kipa bora imekwenda kwa Aishi Manula wa Azam FC, timu bora ya vijana ni Taifa Jang’ombe.

Mfungaji bora ni kiungo wa Yanga, Saimon Msuva, aliyeweka kimiani mabao manne, wakati mwamuzi bora wa mashindano hayo akichaguliwa kuwa Mfaume Ali.

Ratiba ya kufuzu AFCON2019, Tanzania yapangwa kundi moja na Uganda

$
0
0
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetoa ratiba ya makundi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 (AFCON2019) michuano ambayo itafanyika nchini Cameroon.

Tanzania imepangwa katika kundi L ikiwa pamoja na Uganda, Lesotho na Cape Verde.

Michuano hii hufanyika kila baada ya miaka miwili ambapo mwaka 2017 inafanyikia nchi Gabon ambapo inatarajiwa kuanza leo  Januari 14, 2017.

Bodi ya Mikopo yaongeza kiwango cha makato kwenye mishahara ya watumishi

Video: Msikilize Rais Magufuli Akitoa ONYO Kali Kwa Magazeti

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameyaonya magazeti mawili yanayoandika habari za uchochezi na kupotosha wananchi kwa kuwa vinahatarisha amani ya nchini. 

Ametoa onyo hilo jana wakati akikagua na kufungua Kiwanda cha Jambo cha kuzalisha vinywaji baridi mkoani Shinyanga.

Rais Magufuli alisema Serikali haitayavumilia magazeti hayo mawili kwa kuandika habari za uchochezi ambazo zinaweza kuhatarisha amani ya nchi kama ilivyotokea katika nchini ya Rwanda na kupelekea mauaji ya kimbari nchini humo. 

==> Mtazame na kumsikiliza hapo chini akitoa onyo hilo
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images