Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Timbulo: 'Usisahau' ingebuma nisingefanya muziki Tena

$
0
0
Msanii wa kizazi kipya, Ally Timbulo ambaye kwa muda mrefu  hajaonekana kwenye fani, hivi karibuni  baada ya kutoa kibao chake kipya, alifunguka kwa kutaja mambo ambayo angefanya  endapo kichupa chake kipya kisingefanya vizuri sokoni.

Amefunguka kuwa kama wimbo wake mpya ‘Usisahau’ aliomshirikisha baraka the Prince usingefanya vizuri ingekuwa sababu ya yeye  kuachana na muziki na kufanya kilimo kama ajira yake.

Akizungumza katika kipindi cha Dj Show Radio one, Timbulo, alisema kuwa waliwekeza zaidi kwenye wimbo huo na ulikuwa ukitegemewa na menejimenti yake pamoja na yeye mwenyewe kufanya vizuri kabla haujatoka.

”Kwa jinsi nilivyokuwa ‘nimeinvest’ kwenye hii ngoma na jinsi tulivyokuwa tunaitegemea na menejiment, pengine tungekuwa tunaongelea vitu vingine kama ngoma isingefanya poa, kwa kuwa ‘investment’ yake ilikuwa kubwa sana, pengine ingekuwa sababu ya mimi kutokuwepo tena kwenye muziki ambao naendelea kuufanya” alisema Timbulo.

Timbulo alisema kuna uwezekano mkubwa angerudi darasani au hata shamba kulima, kama wimbo huo usingeenda na matarajio yake.

Baadhi ya nyimbo ambazo amewahi kufanya Timbulo ni pamoja na Sina makosa, Samson Delila na Niende zangu’.

Breaking News:Mbunge wa Kilombero Morogoro (CHADEMA ) ahukumiwa miezi 6 jela Bila Faini

$
0
0
Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemuhukumu kifungo cha miezi sita jela Mbunge Wa jimbo la Kilombero Peter Lijualikali (30)   kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero

Mwendesha mashtaka inspekta Wa Polisi Dotto Ngimbwa aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi mosi mwaka 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

Ngimbwa alisema washtakiwa hao kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha shtaka bila kuacha shaka.

Hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya ya Kilombero Timothy Lyon alisema mahakama imewatia hatiani kwa kosa hilo na kwa kuwa mshtakiwa Wa kwanza ni Mbunge ambaye alikuwa na kesi tatu huko nyuma na kutiwa hatiani amehukumuwa jela miezi sita.

Lyon alizitaja kesi za nyuma ambazo mbunge huyo alitiwa hatiani na kuhukumiwa ni kesi namba 338 ya mwaka 2014, kesi namba 220 ya mwaka 2014 na kesi namba 340 ya mwaka 2014, hivyo kutokana na mshtakiwa ni mzoefu katika kesi zote, mahakama imemkuta na hatia ya kwenda jela miezi sita.

Hata hivyo mahakama hiyo imeona kwa kuwa mshtakiwa wa pili Stephano Mgata (35), hii ni Mara yake ya kwanza amehukumiwa kifungo cha miezi sita nje ambapo ndani ya kipindi hicho cha miezi sita hatotakiwa kutenda kosa lolote la jinai.

Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida hali katika mahakama hiyo ilikuwa tulivu tofauti na kesi nyingine dhidi ya Mbunge Lijualikali, ambapo wafuasi wachache wanaodhaniwa kuwa ni wa Chadema ndiyo walijitokeza na baada ya hukumu kutolewa Mbunge huyo alipelekwa haraka gerezani kwenda kuanza kutumikia kifungo chake

Kutokana na jambo hili mwanasiasa Julius Mtatiro anasema kuwa licha ya Lijualikali kufungwa jela lakini hali hiyo haiwezi kupoteza ubunge wake na kusema kama akikata rufaa huenda akapata haki.

"Hawezi kupoteza ubunge kwa kifungo hicho na kama akikata rufaa anaweza kupata haki, Kumfunga Lijuakali kwa sababu alihoji na kupinga kunyimwa haki yake ni kuzalisha Lijualikali wengi zaidi" alisema Julius Mtatiro

Diamond akabidhiwa bendera ya taifa kuliwakilisha taifa AFCON 2017 nchini Gabon

$
0
0
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (kushoto) akimkabidhi bendera ya Taifa Mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz kwa ajili ya kwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akiongea na wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakati wa hafla ya kumkabidhi bendera ya Taifa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon. Hafla hiyo imefanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Wageni waalikwa pamoja na Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri Nape Nnauye wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum akiongea na Waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Balozi wa DSTV Bomba Bw. Lucas Mhuvile maarufu kama Joti akiongea na Waandishi wa Habari pamoja na wageni waalikwa wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye, Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum pamoja na mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati)  akimpongeza mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kushiriki katika Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon. Anayeshuhudia kushoto ni Mkurugenzi wa DSTV Multi Choice Tanzania Bw. Salum Salum
Mwanamuziki wa bongo fleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond Platinumz akimshukuru Waziri Nape Nnauye pamoja na Serikali kwa ujumla kwa mchango mkubwa inaotoa katika kukuza sekta ya Sanaa nchini wakati wa hafla ya kukabidhi bendera ya Taifa kwa mwanamuziki huyo anayekwenda kuiwakilisha Tanzania kwenye Ufunguzi wa Mashindano ya AFCON 2017 yanayotarajiwa kufanyika nchini Gabon.iliyofanyika leo 11 Januari, 2017 Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Picha: Rais Magufuli asafiri kwa gari toka Chato hadi Simiyu kwenye ziara ya kikazi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Nyamikoma Wilayani Busega wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Kisesa mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli akiwasalimia wakazi wa Magu mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita.

Picha: Rais Magufuli Awasili Bariadi Mkoani Simiyu, Aweka Jiwe La Msingi Hospitali Ya Rufaa Ya Simiyu .......Pia Afungua Barabara Ya Bariadi-lamadi (Km 71.8)

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za asili pamoja na kikundi cha Ngoma za asili Baseki cha Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga ngoma za asili pamoja na kikundi cha Ngoma za asili Baseki cha Bariadi mkoani Simiyu mara baada ya kuwasili mkoani humo kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kabla ya kufungua rasmi barabara hiyo la Bariadi-Lamadi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka kabla ya kufungua barabara ya Bariadi-Lamadi na kuwahutubia wananchi wa mkoa huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga makofi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka wakati vikundi vya kwaya mbalimbali vilipokuwa vikitumbuza Bariadi mkoani Simiyu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikagua moja ya nguzo katika ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Simiyu.

Rais Magufuli Akerwa Na Wanasiasa Wanaodai Tanzania Kuna Njaa

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza  watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kazi

Dakta Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mara baada ya kuweka jiwe la Msingi katika  Hospitali ya Mkoa wa Simiyu na kufungua barabara ya Lamadi hadi Bariadi yenye urefu wa kilomita 71.8 iliyogharimu zaidi ya shilingi Bilioni 90.

Amesema kumekuwepo na baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara ambao wamekuwa wakiwahamisisha wananchi na kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza baa la njaa wakati wanasiasa hao hao ndio waliopitisha Bungeni kutaka nchi iuze chakula nje ya nchi na sasa hao hao wanatangaza baa la njaa.

'' Baadhi ya wanasisa walizungumza Bungeni kutaka wananchi waruhusiwe kuuza chakula nje ya nchi kwa kuwa kuna chakula cha kutosha leo hii hao hao wanatumia baadhi ya vyombo vya habari kutanga baa la njaa'' 

Akizungumzia gharama za  ujenzi wa Hospitali ya mkoa wa Simiyu, Rais Magufuli ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu, Wizara ya Ujenzi na Wakala wa majengo nchini TBA kukaa na kurejea gharama za ujenzi wa Hospitali hiyo wa Shilingi Bilioni 46 kuwa hauendani na hali halisi ya aina ya jengo linalotakiwa kujengwa.Rais Magufuli ametoa Shilingi bilioni 10 ili kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo.

''Haiwezekani  majengo ya ghorofa ishirini lijengwe kwa shilingi Bilioni Kumi wakati jengo la ghorofa moja moja lijengwe kwa gharama ya shilingi Bilioni 46''

Rais Magufuli pia ameutaka uongozi wa mkoa wa Simiyu kuendelea na ujenzi wa mradi wa tenki la maji katika mlima Ngasamo ili wananchi wa mkoa wa Simiyu ikiwemo wilaya ya Bariadi kupata huduma ya maji badala ya kukwama kutokana na mwekezaji mmoja kutaka kuchimba madini ya Nikeli katika mlima huo.

Amesema haiwezekani wananchi zaidi ya milioni moja wakose maji kutokana na mwekezaji mmoja ni kukosa muelekeo na kumkosea Mwenyezi Mungu kitu kisichokubalika hivyo Waziri wa Nishati na Madini afute leseni ya mwekezaji huyo ili wananchi wa Simiyu wapate huduma ya maji.

Rais Magufuli amewataka wananchi wa Mkoa wa Simiyu na Watanzania kwa ujumla kutumia mvua chache zinazonyesha kulima mazao yanayostahamili ukame kama vile Mtama,viazi na Uwele ili kuweza kujikimu kwa chakula badala ya kutegemea chakula cha msaada kutoka Serikali.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Simiyu
11 Januari, 2017

NEC: Mbunge Peter Lijualikali kuendelea kuwa mbunge licha ya kuhukumiwa kifungo cha miezi sita jela

$
0
0
Mjadala umeshika kasi mitaani, mitandaoni na kila mahali baada ya Mahakama ya wilaya ya Kilombero kumhukumu kutumikia kifungo cha miezi sita jela bila faini Mbunge Wa jimbo la Kilombero Mhe. Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Mbunge huyo, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo Machi 1, 2016 saa 4 asubuhi Kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Kilombero, mkoani Morogoro.

Imeelezwa  kuwa kwa pamoja walifanya fujo kinyume na kifungu namba 89 kifungu kidogo cha kwanza B, cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2002, ambapo washtakiwa walikana mashtaka na hivyo kufanya kesi kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Kailima Ramadhan ameibuka na kukata kiu ya wananchi ya kutaka kujua endapo  baada ya hukumu hiyo Mhe. Lijualikali ataendelea kuwa mbunge.

Akihojiwa na TBC One wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili jana usiku,  Bw. Kailima aliweka bayana kwamba mbunge huyo ataendelea na wadhifa wake kwa kuwa sheria inasema ili kupoteza kiti ni lazima uwe umepewa adhabu ya kifungo cha ZAIDI ya miezi sita jela.

"Ibara ya 67(2)(c) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaeleza mambo yanayotoa sifa ya kuwa Mbunge kutoka  madarakani ni kifungo cha zaidi ya miezi sita jela. Huyu bwana kafungwa miezi sita kwa hiyo bado hajapoteza sifa za kuendelea kuwa mbunge akiwa gerezani na baada ya kumaliza kifungo chake", alisema Bw. Kailima.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi Ya January 12


Dr. Shein: Sina Ugomvi na Maalim Seif na wala Sikushinikiza ZEC Ifute Matokeo

$
0
0
Wakati Wazanzibari leo wakiadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein (pichani), amebainisha kuwa mapinduzi hayo ndio alama, sifa, ukombozi na uhuru wa raia hao wa visiwa vya Zanzibar.

Dk Shein amesema hana ugomvi na Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ambaye alikuwa mgombea urais kwa tiketi ya CUF katika uchaguzi mkuu wa mwaka juzi na kubainisha kuwa wanatofautiana kisiasa, ni jambo la kawaida na mazungumzo ya muafaka yalishafanyika.

Pamoja na hayo, Rais huyo amebainisha kuwa anaamini amechaguliwa kihalali na Wanzanzibari, ambapo kufutwa na kurudiwa kwa uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2015, hakukuwa na shinikizo lolote kutoka serikalini bali ni maamuzi ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) baada ya kubaini mchezo mchafu kwenye uchaguzi huo.

Akizungumza katika kipindi cha Funguka kilichorushwa na Azam TV jana usiku, Dk Shein alisema kilichohitajika ni mazungumzo ya pande mbili ambayo yalifanyika baina yao na mwelekeo ulikuwa mzuri lakini Maalim Seif hakutaka kurudia uchaguzi. 

Mvutano huo ulijitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, 2015 baada ya Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha kufuta matokeo hayo na kusababisha mvutano wa kisiasa kabla ya kutangaza kurudiwa Machi 20, 2016, ambao CUF iligoma kushiriki.

Katika mahojiano hayo, Dk Shein alisema, “Mimi nilikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yale na Maalim upande wa pili huku wajumbe wakiwa marais wastaafu, Ally Hassan Mwinyi, Aman Karume na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd. 

“ZEC ni tume huru na inayojisimamia kwa mujibu wa sheria na Katiba ya Zanzibar, taasisi yoyote haiwezi kuiingilia hata kama ni Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), ndiyo maana wao (NEC) hawakuona dosari katika uchaguzi lakini ZEC waliziona na kutoa sababu tisa za kufuta uchaguzi,” alisema Dk Shein.

 Alisema uchaguzi wa Zanzibar umekuwa na matatizo tangu mwaka 1957 na wa awamu hii, Tume ilikuwa na hoja za msingi kuurudia huku akisema mwenyekiti wa Tume anateuliwa na Rais kwa mujibu wa Katiba na si kwa ajili ya kumpendelea. 

Changamoto za Muungano 
Dk Shein alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizofanikiwa katika kudumisha Muungano na changamoto zake pekee anazozitambua ni tume ya pamoja ya fedha na suala la mafuta ambalo limepatiwa ufumbuzi. 

“Kabla ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa kelele za Muungano na muundo wa Serikali hazikuwahi kusikika lakini baada ya baadhi ya wanaCCM kuenguliwa na kuhamia upande wa pili, ndiyo walioanza kuwalisha watu sumu. Lakini anayeupinga Muungano haijui asili yake,” alisema Dk Shein. 

Mchakato wa Katiba 
Alipoulizwa kuhusu Katiba mpya baada ya Rais John Magufuli kusema hicho si kipaumbele chake, Dk Shein alisema hayo ni masuala ya kushauriana baina ya viongozi hao wawili.

“Mchakato wa Katiba tuliuanza mimi na Jakaya Kikwete (Rais mstaafu) na ile Katiba ni ya Muungano, hivyo jambo lolote ni lazima viongozi wa Serikali mbili washauriane. Mambo haya si ya kulazimisha...,” alisema.

 Uongozi wa Magufuli
 Rais huyo alisema anamfahamu Rais Magufuli tangu akiwa waziri na anajua uwezo wake, “Majipu anayoyatumbua Rais habahatishi kwani anafanya vile kwa mujibu wa katiba na sheria za nchi, na si kwamba mimi situmbui, natumbua sana, sema mimi staili yangu siyo ya kusema kila kitu na waandishi wa huku (Zanzibar) si wafuatiliaji sana kama wa Bara,” alisema Dk Shein. 

Aliongeza kuwa watu hawawezi kujua utumbuaji wake kama waandishi wa habari si wafuatiliaji, vilevile hawezi kuyajua majipu zaidi kama waandishi wa habari hawajayaibua, “Waandishi wa habari wa Zanzibar ni tofauti sana na wa Bara.” 

Akizungumzia kauli ya Rais Magufuli kuwa awe mkali, Dk Shein alisema, “Kwa kuzungumza mimi ni mpole lakini mtu akikosea, mimi ni mkali kwelikweli, sema mimi siyo mtu wa kukasirika ovyo, busara zinaniongoza sana, japokuwa ukikosea sikuachi hata kidogo,” alisema Dk Shein. 

Alisema katika kipindi chote ambacho amekaa madarakani, anajivunia kuifanyia Zanzibar mambo mengi na bado anaendelea. 

“Katika utawala wangu nimeanzisha mpango wa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari, sasa wazazi wanachangia ada ya mitihani tu ya kidato cha nne na cha sita na yenyewe muda si mrefu nitaiondoa,” alisema Dk Shein. 

Kuhusu afya, alisema licha ya Wazanzibari wengi kutibiwa nje ya visiwa hivyo kwa madai ya kukosekana kwa huduma bora, Serikali yake imeongeza vituo vya afya kutoka 31 hadi 154, ingawa bado kuna changamoto ya wataalamu.

 Dk Shein aligusia suala la mrithi wake akisema yeyote atakayeonesha nia kupitia CCM kwa wakati huu, atakuwa anakosea licha ya kwamba huu ndiyo muhula wake wa mwisho. 

“Hata kama namfahamu mtu ambaye naona anafaa, siwezi hata kumnong’oneza mpaka pale atakapopitishwa na chama,” alisema Dk Shein

Daktari Akwamisha Kesi Ya Scorpion

$
0
0
Ushahidi katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha na kujeruhi  inayomkabili, Salum Njwete (34) maarufu Scorpion, umeshindwa kuendelea baada ya upande wa Jamhuri kudai shahidi  hakufika.

Sababu za kutofika kwa shahidi huyo ambaye  ni  daktari kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) ni kutokana na kuwa nje ya kituo chake cha kazi hivyo hakupatikana   jana.

Mshitakiwa Scorpion alipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi upande wa Jamhuri.

Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga, alidai upande wa Jamhuri ulipanga kumhoji  shahidi ambaye ni daktari lakini kwa vile alikuwa  na dharura ingefaa mahakama impangie tarehe nyingine.

“Mheshimiwa hakimu shauri lilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na upande wa Jamhuri ulipanga kumleta shahidi ambaye ni daktari lakini ameshindwa kufika leo, ana dharura ambayo inaweza ikachukua wiki tatu.

“Hivyo kwa mujibu wa kifungu namba 225 cha Sheria ya Mwenendo wa Kesi ya Makosa ya Jinai ambayo inataka kesi isiahirishwe zaidi ya wiki mbili kama mshitakiwa yuko mahabusu,   tunaomba mahakama itaje hapa  tupange tarehe ya kusikilizwa,’’alisema.

Mkono Wa Mtoto A.k.a Pesa Haiendi Bure Ni Dawa Asilia Ya Kuongeza Ukubwa Wa Maumbile Ya Kiume.

$
0
0
Wanaume  wengi  wanakosa  raha  ya  kuwa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  kwa sababu  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Ndoa  nyingi  zimevunjia, mahusiano mengi  yameharibika, huku  chanzo  kikuu  kikiwa  ni  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume.

Uzoefu  wangu katika  tiba  asilia, umeniwezesha  kugundua kuwa,  wanawake  wengi  hulazimika  kutoka  nje  ya  mahusiano  au  kwenda  nje  ya  ndoa , pale  wanapo gundua  kuwa  wameangukia  kwenye  mikono  ya  mwanaume  mwenye  maumbile  madogo  ya  kiume.

Kitu  kikubwa  kinacho weza  kumfanya  mwanamke , kuendelea  kukaa  katika  mahusiano  ya  kimapenzi  na  mwanaume  mwenye  tatizo  la  maumbile  madogo  ya  kiume, ni  pesa. 

Hapa  mwanamke  husika, hulazimika  kuendelea  kuwa  katika  mahusiano  au  ndoa  na  mwanaume  huyo  kwa  sababu  mwanaume  huyo  ana  pesa, lakini  hulazimika  kutoka  nje  ya  ndoa  pindi  anapo hitaji kufurahia  mapenzi.

Ama  kwa  upande  wa  wanaume  wenye  tatizo  la  udogo  wa  maumbile  ya  kiume. Hofu  na  mashaka  hutawala  katika  maisha  yao yote  ya  kimahusiano.

Huwa  hawajiamini  kama  mwanamke  anaweza  kuwapenda  kwa  jinsi  walivyo.

 Wivu  na  gubu  hutawala  katika  maisha  yao yote  kimahusiano. 

 Karibu  kila  kosa  linalo   fanywa  na  wenzi  wao hulihusisha  na  udogo  wa  maumbile  yao.

Kwa  mfano :  Wamekwaruzana kidogo, mke  kamnunia  au  labda  kamsonya, wao  hufikiri  wamenuniwa  au  kusonywa  kwa  sababu ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.

Amempigia  simu  mpenzi  wake  au  mke  wake, halafu  bahati  mbaya  simu  haijapokelewa zaidi ya  mara  tatu, basi  moja  kwa  moja  huhisi  mke au  mpenzi  anamsaliti kwa  sababu  ya  udogo  wa  maumbile  yake  ya  kiume .  Wakati  ukweli  unaweza  kuwa  tu  labda  simu  ilikuwa  silence  kwenye  pochi.

Wakiwa  wanafanya  tendo  la  ndoa, halafu  baada  ya  kumaliza  mshindo  mmoja,  halafu  baada  ya  dakika  kadhaa, mwanamke  akawa  anataka  waendelee tena, basi  mwanaume  huhisi  kama  vile  mwanamke  huyo  anamkejeli  kwa  sababu  ana  maumbile  madogo na  yasiyo  na  nguvu  za  kutosha.

Vile vile, wakifanya  tendo moja  tu  halafu  mwanamke  akasema  amechoka, basi  jamaa  atachukulia  hiyo  kama  amedharauliwa  na  mwanamke  huyo, kwamba  mwanamke  hafurahii tendo la ndoa  kwa  sababu  ya  maumbile  yake  madogo.

Maumbile  huwa  madogo  na  husinyaa  zaidi  mara  baada  ya  kumaliza  tendo la  ndoa. Hali  hii humfanya  mwanaume huyo  kutokujiamini zaidi  na  kuvaa  taulo  ama  kaptula  haraka, ili  mwanamke  wake  asimuone  katika  hali  hiyo.

Wanapokuwa  faragha  na  wanawake  wao  huwa  hawapendi  kushikwa  maumbile  yao, hasa  yanapokuwa  bado  hayajasimama.

Kwa  ufupi  wanaume  wenye  maumbile  madogo  ya kiume, wanaishi  maisha  ya  tabu  sana  katika  mahusiano  yao.

NINI  TIBA  YA  TATIZO   LA  MAUMBILE  MADOGO  YA  KIUME ?

Kama  una  tatizo  la  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume, liwe  limetokana  na  kusinyaa  kwa  sababu  ya  kujichua  kwa  muda  mrefu, kuugua  chango  la  kiume  au  kurithi  kwa  wazazi  wako, tumia  tiba  ya  asili  iitwayo  MKONO  WA  MTOTO  au  PESA  HAIENDI BURE.

Ni  tiba  ya  asili  ambayo  imekuwa  ikitumika  toka  enzi  za  mababu  na  mababu  wa  mababu. 

Itasaidia  kuimarisha, kurefusha  na  kunenepesha  maumbile  yako  ya  kiume  na  kukufanya  kufurahia   tendo la  ndoa.

Tiba  hii  haitakufanya  kufurahia  tendo la  ndoa  tu, bali  hata  mke  wako au  mpenzi  wako, itamfanya  pia  afurahie  tendo la ndoa  na  kuongeza  upendo  na  uaminifu  kwako.

Unapokuwa  na  uwezo  wa  kufurahia  tendo  la  ndoa  pamoja  na  kumfanya  mke  au  mpenzi  wako  kufurahia  tendo  la  ndoa, unakuwa  pia  unajiepusha  na  uwezekano  wa  kupatwa  na  maradhi  ya  kuambukizwa  kwa  njia  ya  kujamiiana  kama  vile  Kaswende, Kisonono  na  hata  V.V.U  .

JINSI  YA  KUPATA  TIBA  HII: Kupata  tiba  hii, wasiliana  na  DOKTA.  MUNGWA  KABILI  KWA  SIMU  NAMBA  :   

0744  000  473.     www.mungwakabili.blogspot.com

Picha: Rais Magufuli Ahutubia Wananchi Wa Shinyanga Katika Kilele Cha Maadhimisho Ya Sherehe Za Miaka 53 Mapinduzi Ya Zanzibar

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono kuwasalimia wananchi wa Shinyanga waliofika katika uwanja wa mpira wa Kambarage katika kilele cha Maadhimisho ya Sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kuwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha Maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Kambarage mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Kwaya ya KKKT Shinyanga mara baada ya kuwasili katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
PICHA NA IKULU

Rais Magufuli Auagiza Uongozi Wa Mkoa Wa Shinyanga Kufuta Usajili Wa Mradi Wa Triple S.

$
0
0
 Na: Frank Shija - MAELEZO.
Rais wa Jmamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Shinyanga kumfutia usajili mwekezaji wa Kiwanda cha Nyama, Kampuni ya Triple S na badala yake watafute mwekezaji mwingine.

Agizo hilo limetolewa leo Mjini Shinyanga wakati akiwahutubia wananchi wa mji wa huo ambapo yupo mkoani humo kwa ziara ya kikazi iliyoambatana na sherehe ya kuadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

“Futeni usajili wa mradi wa Triple S, haiwezekani mwekezaji akashindwa kuendesha kiwanda kwa zaidi ya miaka 10 sasa afu tuendelee kumkumbatia, tafuteni mwekezaji mwingine, mkishindwa semeni Serikali iweke hela, ili uzalishaji uendelee,” alisisitiza Rais Magufuli.

Aliongeza kuwa mwekezaji huyo amekuwa mbabaishaji kwani tangu kipindi yeye (Rais Magufuli) alipokuwa Waziri wa Uvuvi na Mifugo alimfahamu na alimpa maelekezo cha kusikitisha hakuna jambo aliloendeleza ikiwemo kuanza kwa uzalishaji.

Akizungumzia sababu ya kufanya maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar katika upande huu wa Bara Rais Magufuli amesema kuwa Tanzania ni moja, na kuongeza kuwa chimbuko halisi la uwepo wa Taifa la Tanzania ni Mapinduzi ya Zanzibara mabapo miezi michache tu baada ya kufanyika kwa mapinduzi hayo Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaliwa kwa Taifa la Tanzania.

Kwa upande wake Waziri wa TAMISEMI na Kazi maalumu kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Haji Omari Heri amesema wao kama Wazanzibar wamefarijika sana kwa kitendo cha Serikali ya Awamu ya Tano kuamua kushiriki maadhimisho ya Mapinduzi Matukufu kwa kusherehekea katika upande wa Bara kitu ambacho akijawahi kufanyika kabla.

Aliongeza kuwa ujio wake umetokana na ukweli kwamba Tanzania ni nchi moja hivyo Rais Magufuli alivyoeleza nia yake ya kuadhimisha Maapinduzi huku Bara, Rais Dkt. Shein alimteua aje kumwakilisha na kueleza kuwa maefarijika sana na kusema Tanzania ni yetu sote na tutaendelea kuwa wamoja.

Rais Dkt. Magufuli yuko ziarani Mkoani Shinyanga ambapo kesho anatarajiwa kufungua viwanda kadhaa vilivyopo mkoani hapo, baadhi ya viwanda hivyo ni pamoja na Kiwanda cha Vinywaji Baridi (maji) cha Jambo, Kiwanda cha Mafuta na vingene.

OFA: Jipatie Kibatu cha Riwaya ya Kusisimua MY MOM'S FRIEND Toka Kwa Mtunzi Aliyebobea Eddazaria

$
0
0
Leo katika sikukuu ya MAPINDUZI yamiaka 53 ya Uhuru Zanzibar. Jipatie ofa ya kitabu *MY MOM'S FRIEND* kupitia WhatsApp 0657072588, email:eddazariaM@gmail.com au Facebook inbox, *Story* *Za* *Eddy**Genius* *Story* . Bei yake ya OFA leo ni sh 5000 Tu. 
 
Wahi sasa ofa hii ni kwa siku ya leo tu.

Alichokizungumza Tundu Lissu kuhusu mbunge wa kilombero kufungwa miezi 6

$
0
0
HATUA ya Mahakama ya Wilaya ya Kilombero, Morogoro kumfunga Peter Lijualikali, Mbunge wa Jimbo la Kilombero miezi sita jela, inatokana na visa vya kisiasa

Ni kauli ya Tundu Lissu, Mwanasheria wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) leo mbele ya waandishi wa habari aliokutana nao kwenye Makao Makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki amesema kuwa, vita kati ya upinzani na Chama Cha Mapinduzi (CCM) vimesababisha Lijuakali (Chadema) kupata hukumu hiyo ya kisiasa.

Mbele ya waandishi wa habari Lissu amesema kuwa,“hiyo ni hukumu ya kisiasa” na kwamba, Jeshi la Polisi nalo limeingizwa kwenye vita hivyo.

Lissu amesema, chanzo cha hukumu hiyo kinatokana na mgogoro wa uongozi ndani ya Halmashauri ya Kiliombero ambapo Chadema na washirika wake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) walishinda madiwani wengi.

Hivyo, kwa mujibu wa Lissu, Halmashauri ya Kilombero ilipaswa kuongozwa na mwenyekiti anayetoka na Ukawa na awe Chadema.

“Ili hilo lisiwezekane, na ili CCM wachukue Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero licha ya kushidwa kwenye udiwani, ilibidi wamfanyie Lijualikali mambo ya ajabu,” amesema Lissu.

Lijualikali (30) amehukumiwa jana kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki. Huku Stephano Mgata (35), Dereva wake ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo akifungwa kifungo cha miezi sita nje.

“Kifungo cha Mh. Lijualikali ni adhabu ya kisiasa. Mh Lijualikali ni mfugwa wa kisiasa. Amefugwa kwa sababu ya siasa.

“Adhabu ya kisisa ni vita ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) dhidi ya Chadema na wanatumia Jeshi la Polisi, wanatumia mahakama na kwingineko. Vita hii hii wanawatumia akina Lipumba (Profesa Ibrahim Lipumba,” amesema Lissu na kuongeza;

“Kwingine wamemweka Lema (Godbless Lema, Mbunge wa Arusha Mjini) mahabusu kwa miezi mitatu. Hakuna jinai yoyote. Tuliwashinda kwenye uchaguzi.

“Sasa baada ya uchaguzi walimfungulia Lijualikali kesi ya kupinga matokeo mahakama kuu, tukawapiga chini. Wamefungua rufaa na tunawatandika.”

Mwanasheria huyo amesema kuwa, nchi hii ina wafungwa wa kisiasa na kwamba, pamoja na CCM kudhani kwamba, kumfungulia kesi Lijuakali kutawapa afueni. Wasahau.

“Tuna wafungwa wa kisiasa nchi hii. Wale wanaofikiria kwamba kumfunga Lijualikali CCM itapendwa na wananchi wa kilombelo wasahau hilo.

“Huwezi kuwatesa wananchi, ukatesa viongozi waliowachagua kwa mapenzi yao halafu ukategemea wakupende. Wasahau,” amesema Lissu.

Aidha, Lissu ametoa ufafanuzi kuwa Ibara ya 67 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inamlinda Lijualikali hivyo hawezi kupoteza ubunge wake kutokana na hukumu hiyo.

Amesema Chadema hakijaridhika na hukumu hiyo, hivyo kwa sasa wanaandaa utaratibu wa kisheria ili kukata rufaa kuipinga ambapo hatua hiyo inaweza kuchukua siku mbili kukamilika.

Timothy Lyon, Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo alisema, amemhukumu Lijualikali baada ya kumtia hatiani kwa kosa yeye na dereva wake na kwa kuwa, mbunge huyo alipatikana na hatia katika kesi tatu huko nyuma na kuhukumiwa kulipa faini hivyo alistahili kutumikia adhabu hiyo.

Kesi zilkizotajwa na Lyon zinazomuhusu Lijualikali ni namba 338, namba 220 na namba 340 zote za mwaka 2014.

Katika kesi hiyo, Dotto Ngimbwa, Inspekta wa Polisi aliiambia mahakama kuwa, Lijuakali akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na Mgata walitenda kosa hilo Machi Mosi mwaka 2016 eneo la Kibaoni katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kialombero na kwamba, walifanya fujo kinyume cha sheria.

Alisema tukio hilo lilitokea Machi Mosi mwaka huo saa 4 asubuhi ambapo washtakiwa walikana mashtaka lakini upande wa mashtaka ukathibitisha bila kuacha shaka kwamba, walitenda kosa.

Rais Magufuli: Marufuku kumpangia mkulima bei ya mazao

$
0
0
Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amepiga marufuku viongozi wa serikali wenye tabia ya kuwapangia bei ya mazao wakulima na kuwataka wawaache wakulima wauze mazao yao kwa bei itakayowanufaisha wakulima kutokana na mazao yao

Ameonya juu ya tabia hali ilivyo sasa ambapo mkulima amekuwa akipunjwa kutokana na bei ndogo anayolipwa pindi anapouza mazao yake.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo wakati ambapo amemaliza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu na kuanza rasmi ziara ya siku mbili mkoani Shinyanga na kuahidi kuendelea kuulinda Muungano wa Tanzania Bara na  Zanzibar kwa nguvu zake zote

Rais Magufuli amesema Mapinduzi matukufu ya Januari 12,1964 ndio yaliyosababisha kuwepo kwa Muungano kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na hivyo kuzaliwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo kuna umuhimu mkubwa kwa  Watanzania kuuenzi na kuulinda kwa manufaa ya wananchi wote.

'' leo ni siku muhimu sana kwetu Watanzania kwa kuwa siku hii ya Januari 12,1964  miaka 53 iliyopita  ndio siku yalipofanyika Mapinduzi matukufu ya Zanzibar yaliyopelekea kuondolewa kwa utawala dhalimu wa kikoloni na kupelekea kuzaliwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Tanzania Bara na  Zanzibara kuungana,hivyo tuna kila sababu ya kuienzi siku hii muhimu'' amesema Rais Magufuli.

Akiwa Wilayani Maswa mkoani Simiyu mara baada ya kutembelea kiwanda cha kutengenezea chaki na kuweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa barabara ya Mwigumbi hadi Maswa yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami, Rais Magufuli amewataka wananchi wa mkoa wa Simiyu kutumia barabara hiyo kujiletea maendeleo.

Rais Magufuli ameupongeza mkoa wa Simiyu kwa kutekeleza kwa vitendo Sera ya Serikali ya awamu ya Tano ya Tanzania ya viwanda kwa ujenzi wa kiwanda cha Chaki na  kutoa wito kwa uongozi wa kiwanda hicho kuongeza uzalishaji wa chaki ili ziweze kukidhi soko la nchi nzima badala ya mikoa kumi ya sasa inayotumia chaki zinazozalishwa na kiwanda hicho.

Rais Magufuli apigilia msumari kwa wapiga dili nchini

$
0
0
Rais John Magufuli ameendelea kupigilia msumari kwa watanzania na viongozi wasiopenda kujishughulisha na kuwajibika na kutegemea zaidi fedha za bure za umma.

Amehakikishia kuwa hali zao zitaendelea kuwa mbaya, isipokuwa kwa wale watakaowajibika na kujishughulisha.

Amesema wale wote wanaolalamika kuwa hawana fedha mfukoni kwa hivi sasa, walizokuwa nazo hazikuwa zao, ndio maana wanalalamika.

Katika hotuba zake mwaka jana katika sehemu mbalimbali nchini, Rais alisema wanaolalamika hawana hela mfukoni ni ‘wapiga dili’.

Rais alibainisha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, itahakikisha inamaliza hali mbaya iliyokuwa inalikumba taifa la watanzania, ambapo watu wachache ndio waliokuwa wakinufaika na fedha za umma huku wananchi wengi wakiendelea kuumia na umasikini.

Alisema hayo mkoani Shinyanga jana wakati akizungumza na wananchi kuhusu maendeleo ya mkoa huo na kumbukumbu ya maadhimisho ya Miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. 

“Nimejitoa sadaka kwa ajili ya nchi hii, mimi sikuwa na urais ila mmenipa nyie, sasa nawaahidi mimi na serikali yangu tutawatetea kwa nguvu zote dhidi ya mafisadi.

"Nasikia kuna watu wanalalamika kuwa eti fedha hamna, kwani zilikuwa zinauzwa sokoni?" alihoji. 

Alisema watu wote wanaolalamika kuwa fedha zimepotea mitaani, ni wale waliokuwa wamezoea kupata fedha za bure bila kuzitolea jasho.

Aliwahakikishia kuwa wataendelea hivyo hivyo kutaabika, huku wale waliokuwa wakijishughulisha wakineemeka. Alisema fedha zilizotumiwa na mafisadi kipindi cha nyuma ni nyingi mno, kwani kila serikali ikitenga na kutoa fedha za maendeleo, zimekuwa zikiishia mikononi mwa mafisadi.

“Watu walikuwa wanajipatia tu fedha bila kuzitolea jasho, unakuta mtu anaenda nje kila siku, wapo waliofikia kufanyia mikutano ya taasisi zao za ndani nje ya nchi, mfano pale Muhimbili (hospitali ya taifa) nilipoenda nilikuta akinamama wanajifungulia chini huku fedha zipo lakini zimetengwa kwa ajili ya starehe,” alifafanua.

Alisema wakati serikali yake inaingia madarakani ilikuta nchi ina hali mbaya hali iliyoilazimu asafishe kila kona ya idara, ndipo walipopatikana watumishi hewa zaidi ya 18,000, wanafunzi hewa 65,000, mikopo ya elimu ya juu hewa yenye thamani ya Sh bilioni 3.5.

Alisema hata fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), zinazotolewa kwa kaya maskini, zilitolewa kwa kaya hewa 55,000.

Rais alisema ni wakati sasa Watanzania na serikali kwa ujumla wakashirikiana kuijenga Tanzania mpya, itakayomkomboa kila mwananchi akiwemo masikini, kwani kutokana na utajiri ambao Tanzania inayo, imekuwa ikichekwa kwa kuendelea kuwa masikini.

Utumbuaji majipu
Alisema pamoja na kwamba wapo baadhi ya watu wanachukizwa na hatua ya utumbuaji majipu kwa watumishi wasiowajibika, serikali yake itaendelea kuwatumbua watumishi na viongozi wanaokwenda kinyume na maadili yao.

“Ni bora nichukiwe na watu wachache kuliko kupendwa na wengi huku mambo yakienda mrama. Wale wote wanaodai mtindo wangu wa kutumbua ni mbaya hawa ndio majipu. Kabla ya utumbuaji watanzania walikuwa wanaishi maisha ya ajabu, na kusisitiza kuwa alikuwa mtumishi wa serikali kwa kipindi cha miaka 10 anajua anachoongea,” alisisitiza.

Aliomba Watanzania wamuombee ili aweze kuendeleza jitihada zake za kupambana na mafisadi kwani serikali yake ya awamu ya tano imejipanga kuendelea kuongoza kwa ukali kwa faida ya watanzania wote wakiwemo wanyonge na masikini.

“Lengo langu ni kuhakikisha wale wote waliokuwa wakila na kuchekelea kipindi cha nyuma wakati wenzao wanataabika, sasa waishi kama mashetani na wale waliotaabika waishi kama wafalme,” alisema.

Hatua za maendeleo
Dk Magufuli alisema kutokana na kutambua adha wanayoipata watanzania kutokana na huduma mbovu, serikali yake imejitahidi kupambana na kuboresha maendeleo mengi ikiwemo sekta za elimu, miundombinu usafiri na afya.

Alitolea mfano namna serikali hiyo ilivyofanikiwa kukusanya mapato kwa kubana maeneo yote yenye ubadhirifu na kufanikiwa kuongeza mapato kutoka Sh bilioni 31 hadi Sh trilioni moja, hali iliyosaidia serikali hiyo kununua ndege sita, mbili zikiwa tayari zimewasili.

Pia alisema serikali imefanikisha kusimamia elimu bure kwa kutenga kiasi cha Sh bilioni 18.77 kila mwezi, zinazokwenda moja kwa moja shuleni kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kusokma bure katika shule za msingi na sekondari.

Alisema pia serikali yake kwa kipindi kifupi, imefanikiwa kuongeza bajeti ya afya na kufikia Sh trilioni 1.99 na kati ya fedha hizo bajeti ununuzi wa dawa imeongezeka kutoka Sh bilioni 31 hadi Sh bilioni 250.

Mikakati
Aidha, kiongozi huyo alisema serikali yake imejipanga kuendelea kuwaletea maendeleo wananchi, ambapo pamoja na kununua meli mbili katika Ziwa Victoria na Tanganyika, pia imeanza mchakato wa kujenga reli ya kisasa ambayo imetengewa jumla ya Sh trilioni moja katika bajeti ya mwaka 2016/17.

Alisema Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali za kutosha ikiwemo bahari, mito, maziwa, madini kama vile dhahabu na wanyama, lakini bado imeendelea kuwa na umasikini.

Alisema kutokana na hali hiyo, serikali yake imejipanga kuijenga Tanzania mpya ikiwemo viwanda ili kuweza kutimiza lengo la kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye kipato cha kati.

“Hapa Shinyanga kuna mwekezaji ambaye ana takribani miaka 10 sasa tangu nikiwa waziri wa mifugo na uvuvi na baadaye ujenzi, hajaendeleza kiwanda cha nyama, naagiza uongozi wa mkoa wawekezaji kama hawa waondolewe wapewe wengine tusonge mbele,” alisisitiza.

Pamoja na mwekezaji huyo, pia alipotembelea mgodi wa Maganzo alipatiwa taarifa za kuwepo kwa migogoro ya ardhi na kuwataka mawaziri wa ardhi na mazingira, kushughulikia suala hilo haraka iwezekanavyo.

Maji
Akizungumzia kero ya maji iliyowasilishwa mbele yake na Mbunge wa Shinyanga Mjini, Steven Masele, Dk Magufuli alibainisha kuwa atamtuma Waziri wa Maji kufuatilia bei inayotozwa kwa wakazi hao, ili kuwaondolea mzigo wa kutozwa bei kubwa ya maji.

Hata hivyo, Rais huyo aliweka wazi kuwa endapo atabaini bei inayotozwa kwa wakazi hao, haiendani na bei zinazotozwa katika miji mingine, atahakikisha ama anaipunguza au kuiongeza ili iendane na miji mingine.

Mapinduzi
Pamoja na hayo, Dk Magufuli alizungumzia maadhimisho ya siku ya mapinduzi ya Zanzibar na kubainisha kuwa kuanzia sasa serikali itakuwa inaadhimisha sikukuu za kitaifa katika mikoa mbalimbali ili kila mtanzania afaidike na sherehe hizo.

Alisema yeye na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein walipanga kila mmoja aadhimishe sherehe hizo katika maeneo tofauti, ambapo Dk Shein alikuwa visiwani Zanzibar yeye akiwa Shinyanga.

“Watu wamezoea wakisikia sherehe za kitaifa basi viongozi ni kulundikana sehemu moja. Sasa hili hatutolifanya, hizi ni sherehe za kitaifa kila mtanzania ana haki ya kuziadhimisha akiwa na viongozi wa kitaifa” alisema.

Rais Shein Apandisha Mshahara Kwa Asilimia 100

$
0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ametangaza neema mpya kwa wafanyakazi visiwani humo baada ya kuwakikishia kupandisha kima cha chini cha mshahara kuanzia mwaka huu (2017).

Dkt. Shein ametoa hakikisho hilo jana wakati akiwaongoza watanzania kuadhimisha Miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani visiwani humo.

Alisema kuanzia mwaka huu kima cha chini cha mshahara kitaongezeka kutoka Tsh. 150,000 hadi Tsh. 300,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 100.

Dkt. Shein alitoa tathmini yake ya mwaka mmoja tangu achanguliwe tena kuiongoza Zanzibar, ambapo alisema mwaka 2016 umekuwa ni wa mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, kilimo, viwanda, huduma za jamii ikiwemo afya na huduma za maji, miundombinu n.k.

Akihutubia kwenye uwanja wa Amani Dkt. Shein alisema, serikali yake itaendelea kudumisha na kuenzi umoja na mshikamano ambao uliasisiwa na viongozi wa mapinduzi hayo.

Alisema, mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kukuza pato la taifa hadi kufikia 6.6% licha ya kuongezeka kwa mfumuko wa bei kutoka 5.7% katika mwaka 2015 hadi kufikia 6.7% mwaka 2016.

Pia Dkt. Shein alieleza utekelezaji wa sera ya kulipa pensheni kwa wazee, ambapo amesema hadi mwezi Desemba mwaka 2016, jumla ya shilingi bilioni 4.3 zimetumika kuwalipa wazee 25,259 waliosajiliwa kiasi cha shilingi 20,000 kila mwezi, zoezi ambalo litaendelea kutekelezwa.

Katika hatua nyingine, Dkt Shein alitangaza rasmi kuwa matangazo yote ya TV yatahama kutoka mfumo wa 'Analogue' na kuhamia mfumo wa 'kidigitali' kuanzia mwezi April mwaka huu.

Taarifa Kwa Umma Na Wateja Kwa Ujumla Toka Benki ya NMB

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya January 13

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images