Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Mahakama yaiamuru Serikali kurekebisha kifungu Sheria ya Mtandao

$
0
0
Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ameondolewa mamlaka ya kutoa adhabu isiyokatiwa rufaa kwa mshtakiwa anayekiri makosa ya kimtandao.

Uamuzi huo umetolewa na Mahakama Kuu,umeipa Serikali miezi 12 kukifanyia marekebisho kifungu cha 50 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kilichobatilishwa.

Hata hivyo, mahakama hiyo imehalalisha vifungu vingine vyote vya sheria hiyo, ambavyo pia vimekuwa vikilalamikiwa na wadau wa matumizi ya mitandao na teknolojia ya habari.

Uamuzi huo umetokana na kesi ya kikatiba, iliyofunguliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Kituo cha Msaada wa Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)na mashirika mengine.

Katika hukumu iliyotolewa na majaji Profesa John Ruhangisa, Winfrida Korosso na Lugano Mwandambo, Mahakama ilibatilisha Kifungu cha 50 cha sheria hiyo, lakini ikaridhia vingine kuwa ni halali.

Serikali yatoa kauli uhaba wa chanjo ya pepopunda

$
0
0
Baada ya kuripotiwa taarifa kwamba kuna uhaba wa kinga za ugonjwa wa Pepopunda kwenye Hospitali za Dar es salaam, Leo January 2, 2017 Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, jinsia, wazee na watoto imetoa ufafanuzi kuhusu chanjo hiyo na kueleza kuwa ipo akiba ya kutosha tofauti na ilivyoandikwa na gazeti la Tanzania Daima leo Jumatatu ya  tarehe  02/01/2017.

Wizara ya Afya imesema kuwa habari iliyotolewa na gazeti hili sio sahihi, na hata majina ya watu waliohojiwa kuhusu kuadimika kwa chanjo hiyo hawapo wizarani, na wengine wapo masomoni, hii ni taarifa yazamani sana kimsingi imepitwa na wakati ambayo haikupaswa kutolewa kama wahariri wa habari wangekuwa makini katika kufanyia kazi taarifa hii.

Kwenye taarifa hiyo ametajwa Daktari kiongozi wa hospitali ya Amana, Stanley Dinagi, ambaye sasa hivi hayupo nchini, yupo masomoni. Pia katajwa Mganga mkuu wa serikali Donald Mmbando ambaye hayupo katika wadhifa huo sasa imepita takribani miaka mitatu iliyopita.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkuu wa  kitengo  cha  Mawasiliano Serikalini-Afya, Nsachris B. Mwamaja imefafanua uwepo wa kinga hiyo katika wilaya kuu tatu za Dar es salaam.

Mkoa wa Dar Es Salaam una chanjo za Pepopunda zakutosha katika manispaa  zake zote na umesambaza mgao wake kama ifuatavyo,
  1.  ILALA– Dozi 35,300 zilisambazwa Tarehe 06/12/2016 na mahitaji yao kwa mwezi Dozi 7,110.
  2. TEMEKE– Dozi 33,000 zilisambazwa Tarehe 06/12/2016, mahitaji yao kwa mwezi ni Dozi 7,620.
  3. KINONDONI – Dozi 11,000 zilisambazwa Tarehe 07/12/2016, mahitaji yao kwa mwezi ni dozi 9,210.
“Kwa hivi sasa hakuna upungufu wowote wa chanjo ya pepopunda nchini, Tuna jumla ya dozi 599,000 katika bohari ya taifa, na tunatarajia kupokea shehena nyingine ya dozi 1,200,000 wakati wowote ili kuhakikisha kwamba hatuna uhaba wa chanjo hii.”– Mwamaja

Rais Magufuli Atembelea Maeneo Yalioathirika Na Tetemeko Na Kuweka Jiwe La Msingi Ujenzi Wa Shule Ya Sekondari Ihungo Mkoani Kagera

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke (kushoto) wakiweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Shule hiyo inajengwa upya kufatia kuathirika na tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama wakati Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke alipokuwa akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Joyce Ndalichako.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Balozi wa uingereza hapa nchi Sarah Cooke wakikagua ujenzi wa majengo ya Shule ya Sekondari ya Wavulana Ihungo mkoani Kagera.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini (TBA) Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo nchini Elius Mwakalinga akitoa maelezo ya mradi huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa ukaguzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Charles Masinde mmoja wa wanachi mkoani Kagera aliyeamua kujenga nyumba yake mwenyewe mara baada ya tetemeko. Rais Dkt. Magufuli amemuahidi mwananchi huyo kuwa atampatia mabati 30 kwa ajili ya kuezekea nyumba yake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifafanua jambo wakati alipokuwa akikagua majengo ya shule ya Sekonadri ya Wavulana Ihungo ambayo yanajengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Rais Magufuli Amaliza Ziara ya Siku Mbili Mkoani Kagera

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu  Januari mbili, 2017 amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kuwatembelea baadhi ya wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi pamoja na kukagua baadhi ya miundo mbinu iliyoathiriwa na tetemeko hilo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo  Omumwani iliyobomolewa na tetemeko la ardhi la Septemba 10,2016.

Mara baada ya ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli akazungumza na wananchi wa Mkoa huo wa Kagera katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ihungo na kuagiza kuvunjwa kwa kamati ya maafa ya Mkoa huo iliyokuwa ikiratibu utoaji wa misaaada na kufanya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.

”Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho wake ukiwa na harusi huwa kuna kamati ya harusi,ukishamaliza kufunga ndoa kamati ya harusi huwa inavunjwa,na ukiwa kwenye msiba huwa kuna kamati ya msiba na msiba  mkishazika kamati ya mazishi huvunjwa,kamati ya maafa ya Kagera huu ni mwezi wa tano na inawezekana hata kwenye kamati huwa wanalipana posho,sasa nataka hii kamati nayo iishe,yalishapita yamepita”

Aidha Dkt Magufuli amewataka wote walioahidi kuchangia katika kamati ya tetemeko la ardhi ya mkoa wa Kagera ambao bado hawajatekeleza ahadi zao ambazo ni jumla ya shilingi bilioni nne nukta tano wakamilishe ahadi hizo ili ziweze kumalizia miundombinu ya Serikali iliyoathiriwa na tetemeko hilo.

Ameongeza kuwa wale wote wanaoendelea kuguswa kusaidia wapeleke michango yao moja kwa moja kwa wananchi badala ya kuipeleka serikalini kwa kuwa hakuna mchango mwingine utakaopokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Pia Rais Dkt Magufuli ameagiza shule ya Sekondari ya Omumwani iliyokuwa inamilikiwa na Jumuia ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM imilikiwe na Serikali kutaka wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo kutolipa ada kama zilivyo shule nyingine za serikali.

Dkt Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kagera kupunguza utitiri wa kodi katika zao la kahawa ili bei ya zao hilo ipande na kuwanufaisha wakulima

Balozi wa Uingereza hapa Nchini Bi Sarah Cooke ambaye nchi yake imechangia kiasi cha shilingi bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ihungo, amempongeza Rais Dkt Magufuli na serikali yake kwa jitihada za kupambana na rushwa suala ambalo nchi yake ya Uingereza inalipa kipaumbele sambamba na kutoa elimu bila malipo jambo linalowawezesha watoto wengi wa kitanzania kupata elimu bure

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Kagera.
02 Januari, 2017

Waziri Mkuu Akemea Uharibifu Wa Mazingira

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaonya wakazi wa Ruangwa wanaokata miti kwenye misitu waache kufanya hivyo mara moja ili kuokoa ardhi chepechepe waliyokuwa nayo.

Amesema ukataji miti huo unafanywa zaidi na watu wanaoanzisha mashamba ya ufuta na wapo walioamua kulima karibu na vyanzo vya maji hali iliyosababisha maji yakauke kwenye maeneo mengi.

“Zamani kuna maeneo ulikuwa haupiti hadi ukunje suruali, na kama una gari napo pia ilikuwa ni taabu kupita kwenye maeneo hayo. Lakini sasa hivi, hakuna tena maeneo hayo ndiyo maana kila unakopita unakuta akinamama wanatembea mwendo mrefu na ndoo huku vijana wakibeba madumu kwenye baiskeli nao wakitafuta maji,” alisema Waziri Mkuu ambaye ni mbunge wa jimbo la Ruangwa.

Ametoa onyo hilo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wakazi wa vijiji mbalimbali vya  wilaya hiyo ambao walifika Ruangwa mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya CCM kusikiliza taarifa ya mambo aliyoyafanya jimboni humo katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

“Kilimo cha ufuta kimekuwa balaa, sasa hivi hakuna maji sababu ya ukataji miti ovyo. Mfano mzuri ni mto Mbwemkuru ambao ulikuwa ukitiririsha maji mwaka mzima, angalia sasa hivi, umegeuka kuwa mto wa msimu na chanzo ni ukataji wa miti,” alisisitiza.

“Tusipobadilika na kuacha hiyo tabia tutamlaumu mbunge na Serikali kuwa hawaleti maji wakati sisi wenyewe tumechangia hali hiyo kwa kuharibu vyanzo vya maji,” alionya na kuongeza kuwa amelazimika kutafuta mashine ya kuchimba maji ili kupunguza tatizo la maji.

Alisema mapema mwaka huu, wataalamu wataanza kufanya utafiti ili kubaini maji yako umbali gani kwenda ardhini kabla ya kuanza kuchimba visima hivyo. “Ikibidi tutaaza na visima vifupi na vya kati ili maji yapatikane haraka,” alisema.

Akielezea mipango ya mwaka huu kwenye sekta ya afya, Waziri Mkuu aliwaeleza wakazi wa jimbo hilo kwamba anatamani kuona kila kijiji kinakuwa na zahanati ili kupunguza umbali wa upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa vijijini.

“Kila nilikopita vijijini nimewahamasisha wananchi waanze kufyatua mafotali ili ujenzi wa boma ya zahanati uanze. Na mimi nimeahidi kuchangia mabati kwa kila zahanati, na kuna baadhi ya maeneo nimechangia hata mabati ya nyumba ya mganga na muuguzi,” alisema.

Alisema mwaka uliopita, alifanikiwa kukamilisha ujenzi wa wodi ya akinababa, ya akinamama na kukarabati wodi ya magonjwa mchanganyiko katika hospitali ya wilaya ambapo fedha taslimu milioni 100 zilitumika. Pia aliwezesha kufunga umeme wa jua kwenye zahanati zote zinazotoa huduma za afya ndani ya jimbo na kazi hiyo itaendelea kwa awamu ya pili.

“Pia niliweza kulipia kaya 10 zisizokuwa na uwezo kwa kila kijiji ili zijiunge na mfuko wa afya ya Jamii (CHF) kwa gharama za shilingi milioni 9. Jumla ya vijiji 92 vimefikiwa. Ninawasihi wana-Ruangwa kila mmoja ajiunge na mfuko huu ili muweze kupatiwa huduma za afya bila matatizo,” aliongeza.

Akielezea kuhusu sekta ya elimu, Waziri Mkuu alisema ameweza kufadhili ujenzi wa matundu ya vyoo 70 Katika shule za msingi saba ambapo kila shule imejengewa matundu 10 (manne wavulana, manne wasichana na mawili kwa walimu) ambapo jumla ya sh. milioni 63 zimetumika. Alisema kazi hiyo itaendelea awamu ya pili.

“Zaidi ya hayo, nimefanikisha ufungaji wa umeme jua kwenye shule za sekondari nne za Chunyu, Makanjiro, Narungombe na Nambilanje. Katika awamu ya kwanza tumekamilisha kuweka umemejua kwenye sekondari za tarafa ya Mandawa, na tarafa ya Ruangwa imefikiwa nusu tu. Katika awamu ya pili, tutamalizia tarafa ya Ruangwa na kukamilisha tarafa nzima ya Mnacho,” alisema.


IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, JANUARI 2, 2017.

Waziri Mkuu Amjulia Hali Majimarefu Kairuki Hospitali

$
0
0
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimpa pole mbunge wa Korogwe Vijijini, Steven Ngonyani ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es salaam akitibiwa Januari 2, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
**
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mhe. Steven Ngonyani (Profesa Majimarefu) aliyelazwa katika Hospitali ya Kairuki akipatiwa matibabu.
 
Akiwa hospitalini hapo leo (Jumatatu, Januari 2, 2017), Waziri Mkuu amesema amefurahi baada ya kumkuta Mbunge huyo anaendelea vizuri na kwamba afya yake inaridhisha.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumtakia afya njema Mhe. Ngonyani. Amesema anaamini hivi karibuni atapona na kuruhusiwa kutoka hospitali.
Kwa upande wake Mbunge huyo ambaye amelazwa katika hospitali ya Kairuki iliyoko Mikocheni jijini  Dar es Salaam, amemshukuru Waziri Mkuu kwa kwenda kumjulia hali.

Pia amesema anaendelea vizuri na anatarajia kwenda nchini India kwa matibabu zaidi mara taratibu zitakapokamilika.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,

Madawa ya kulevya yamwathiri aliyekuwa mshiriki wa Big Brother -Nando

$
0
0
Ni kijana aliyeshiriki big brother mwaka 2013, kama mwakilishi wa Tanzania, kutokana na hali ngumu ya maisha kijana huyu alijidumbukiza kwenye janga kubwa la matumizi ya madawa ya kulevya

Kwa sasa hali ya Afya ya Nando si nzuri imezorota kutoakana na matumizi ya madawa ya kulevya yaliyo kithiri,

Hii iwe kama kengele kwa vijana wa kisasa kuwa dawa za kulevya sio “ujanja” ni majanga. Unaweza kuanza na kuvuta kisirisiri, lakini majibu ya madhara yake yakawa hadharani na unapotoka hadharani basi muda unakuwa umekwisha kwenda.

Askari wa wanyama pori mbaroni kwa kuua na kuficha maiti

$
0
0
Jeshi la polisi mkoani Dodoma, linawashikilia askari watatu wa wanyamapori wa pori la akiba Swagaswaga wilayani Kondoa, wakituhumiwa kumuua mkazi wa kijiji cha Olimba wilaya ya Chemba kwa kumpiga risasi mgongoni wakimtuhumu kubeba nyama pori.

Akizungumza ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Lazaro Mambosasa, alisema tukio hilo lilitokea Disemba 31,mwaka jana saa 7:30 mchana katika kijiji cha Selya kata ya Selya wilayani humo.

“Marehemu ambaye hakufahamika jina lake lakini mkazi wa kijiji hicho, alikuwa akiendesha pikipiki huku akiwa amepakia kiroba kilichokuwa na sukari guru ndani yake, lakini askari wanyamapori hao walimhisi amebeba nyama pori na bila kumsimamisha na kumhoji waliamua kutumia bunduki zao kumuua papo hapo,” alisema Kamanda Mambosasa.

Aidha Kamanda huyo amesema baada ya kufanya mauaji hayo, askari hao waliubeba mwili huo kwenye gari walilokuwa nalo pamoja na pikipiki ya marehemu na kiroba cha sukari guru, kisha kwenda kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo la Swagaswaga.

“Baada ya kuutelekeza mwili huo ndani ya pori hilo, walichukua pia pikipiki na kiroba na kuvificha kila kimoja mahali pake kwa lengo la kupoteza ushahidi wa tukio hilo”.

Kamanda Mambosasa alisema wakati askari hao wanafanya tukio hilo, walishuhudiwa na mwananchi mmoja wa kijiji hicho ambaye alijificha porini ambaye aliamua kutoa taarifa kituo cha polisi Kondoa.

Wahusika wa tukio hilo ambao  wanaendelea kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani ni George Grefee (26), Chini Paulo (40) na Christopher Waunko (36).

Feza Kessy awalilia Chidi Benz na Nando baada ya kudhoofu kwa Madawa ya Kulevya

$
0
0
Feza Kessy ana mdogo wake ambaye naye ni muathirika wa madawa ya kulevya hivyo anaelewa kinagaubaga changamoto ya kuwa na mtu wa karibu anayepambana na janga hilo.

Na sasa amewaomba Watanzania kuwaombea wote walioingia kwenye tatizo hilo wakiwemo Chidi Benz na Nando ambao hali zao za hivi karibuni zinasikitisha.

Ameandika kwenye Instagram:
"Let’s pray for our brothers and sisters who are caught up in drug addiction. Chidi ni rafiki yangu for many years Na Nando mdogo wangu, I will Not Post how they look like Now cos kwangu haijakaa sawa. #MadawaYaKulevya sio mchezo it’s time tuache kunong’ona Na tuwe wazi! Hashtags Na Repost won’t help jamaniiiii A plan is needed as a society to fight this devil. Kwa wale ambao wanasema “wakafie mbali” mara “wameyataka wenyewe” let me tell you something;

"Kuna watu wamezaliwa Na addictive personality, wanajaribu Mara moja na ndo mwanzo wa kujiuwa, wengine wanajaribu na wanaacha tu so muache kuhukumu watu kama vile nyie ni Mungu. There is nothing fair about addiction wao wenyewe wanakata tamaa. We need to stop this drug business “Sisi” kama society, we need to teach about it and make our kids fear these drugs, and we also need to love the ones affected, pray for them because huijui Kesho it might come to your house. Ni hayo tu for now."
Let's pray for our brothers and sisters who are caught up in drug addiction. Chidi ni rafiki yangu for many years Na Nando mdogo wangu, I will Not Post how they look like Now cos kwangu haijakaa sawa. #MadawaYaKulevya sio mchezo it's time tuache kunong'ona Na tuwe wazi! Hashtags Na Repost won't help jamaniiiii A plan is needed as a society to fight this devil. Kwa wale ambao wanasema "wakafie mbali" mara "wameyataka wenyewe" let me tell you something; Kuna watu wamezaliwa Na addictive personality, wanajaribu Mara moja na ndo mwanzo wa kujiuwa, wengine wanajaribu na wanaacha tu so muache kuhukumu watu kama vile nyie ni Mungu. There is nothing fair about addiction wao wenyewe wanakata tamaa. We need to stop this drug business "Sisi" kama society, we need to teach about it and make our kids fear these drugs, and we also need to love the ones affected, pray for them because huijui Kesho it might come to your house. Ni hayo tu for now.
A photo posted by Feza (@fezakessy) on

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya January 3

Mwenyekiti wa Chadema na Wenzake 7 Wafikishwa Mahakamani

$
0
0
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Thomas Darabe na wenzake saba wamepandishwa kizimbani kujibu shitaka la kuharibu mali ya thamani ya zaidi ya sh milioni 75.4 na vitunguu.

Pamoja na Darabe, waliopandishwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha/ Arumeru ni Charles Lameck ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia maji ya ya vijiji saba vilivyoko katika wilaya ya Karatu na George Pius.

Wengine ni Baridi John, Christopher Lameck, Florian Tiofil, Daniel Ninida na Lazaro Emmanuel.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya watumia maji alishitakiwa na mashitaka manne pekee yake ya thamani ya zaidi ya sh milioni 60 katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha na Mahakama ya Wilaya ya Arumeru.

Akisomewa shitaka la kwanza na Mwendesha mashitaka wa serikali, Charles Gakirwa mbele ya Hakimu Mkazi Patricia Kisinda, alidai kuwa Desemba 28 mwaka huu mtuhumiwa alifanya uharibifu wa mali aina ya pampu ya maji ya thamani ya sh milioni tatu na bomba la maji la sh 448,000.

Shitaka la pili lililosomwa wakili wa serikali Gakirwa mbele ya hakimu mkazi wa wilaya ya Arusha , Devotha Msofe ilidaiwa kuwa Lameck alifanya uharibifu katika wa mfumo wa maji katika kijiji cha Quandet Karatu wa thamani ya zaidi ya sh milioni 1.6.

Mtuhumiwa alikana mashitaka yote na alipewa dhamana ya mtu mmoja na wadhamini wakifanikiwa kukidhi vigezo vyote katika mashitaka hayo. 

Katika mashitaka yaliyowahusu washitakiwa wote, akiwemo Darabe pamoja na Lameck ilidaiwa kuwa wote kwa pamoja walitenda kosa la uharibifu wa mali kwa kuchoma pampu ya maji ya thamani ya zaidi ya sh milioni tatu na injini ya maji ya thamani ya sh milioni 12.

Shitaka la tatu lililokuwa likiwakabili washitakiwa wote ni kuharibu mazao aina ya vitunguu ya thamani ya zaidi ya sh milioni 49 na pampu mbili za sh milioni sita. 

Washitakiwa wote walikana mashitaka hayo na dhamana zao zilikuwa wazi na upelelezi wa kesi hiyo ulikuwa bado haujakamilika na kesi hiyo itatajwa tena januari 16 mwaka huu.

Majambazi yapora mamilioni mbele ya askari polisi Dar

$
0
0
Watu  wanaodaiwa majambazi wamepora kiasi cha fedha kinachokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi milioni 25 katika makutano ya barabara ya Mandela na Nyerere, eneo la Tazara, Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea  jana saa 4 asubuhi wakati gari hilo likiwa kwenye foleni ya magari eneo hilo la taa za Tazara.

Watu hao wameporwa katika eneo ambalo huwa askari doria wametanda, lakini wakikamata pikipiki zinazotokea eneo la Buguruni.

Aidha taa za Tazara yaliko makutano ya barabara kutokea Buguruni, Temeke, Kariakoo/Posta na Gongo la Mboto ndilo eneo lenye askari wengi wakiwemo wa usalama barabarani.

Wakati tukio likifanyika kulikuwepo askari wenye magwanda maalumu ya askari doria zaidi ya watano wakivurumushana na waendesha pikipiki upande wa Barabara ya Mandela kutokesa Buguruni. Hata hivyo imeelezwa kuwa watu hao waliokuwa wakipeleka benki hawakuwa na ulinzi kama inavyoshauriwa na Jeshi la Polisi.

Majambazi hao waliokuwa watatu, walipora fedha hizo katika gari ndogo aina ya Toyota Rav4 yenye namba za usajili T 455 DFN mali ya kampuni ya kutengeneza mabati ya Sun Share iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwa jina la Richard Charles.

Kwenye gari pia alikuwepo mfanyakazi mwingine wa kampuni hiyo, mwenye asili ya China, aliyetambulika kwa jina la Cheng Deng.

Kwa mujibu wa dereva wa gari hiyo, Charles, walikuwa wakizipeleka fedha hizo benki eneo la Quality Centre na ndipo walipovamiwa na watu hao wakiwa na pikipiki aina ya boxer wakati magari yakiwa kwenye foleni wakisubiri taa ziwaruhusu kupita kutoka barabara ya Mandela.

Charles alisema majambazi hao walimwamrisha kufungua mlango na kuwapatia begi la fedha lililokuwa limewekwa katika kiti cha nyuma huku wakimtishia kwa bastola kabla ya kuvunja kioo cha nyuma cha gari hilo na kubeba fedha hizo na kutokomea nazo.

“Kwa kweli hata sielewi mpaka sasa hivi kilichotokea. Walikuja watu wawili mmoja upande wangu mwingine wa bosi wangu wakinitishia kwa bastola nifungue mlango niwape begi la fedha. Ghafla mtu mwingine akavunja kioo cha nyuma kwa kutumia kitako cha bastola na kubeba begi la fedha na kutokomea” alisema Richard.

Askari wenye silaha walifika katika eneo la tukio dakika 20 baada ya tukio hilo wakaishia kuhoji. Hata hivyo askari mmoja ambaye hakutaka kujitambulisha jina lake alilaumu tabia ya baadhi ya watu kusafirisha kiasi kikubwa cha fedha pasipo kuomba ulinzi wa polisi jambo linalohatarisha usalama wao na mali zao.

“Kama walijua wanasafirisha kiasi kikubwa hicho cha fedha kwa nini wasingeomba hata ‘escort’ (kusindikizwa kwa ulinzi) ya polisi? Hili ni tatizo, hasa katika kipindi hiki kigumu cha upatikanaji wa fedha, watu wanatakiwa kuchukua tahadhari mapema.” alisema askari huyo.

Credit: Habari Leo

Moto Wateketeza Maduka 14 Arusha

$
0
0
Maduka 14 katika eneo la Mianzini jijini Arusha yameteketea kwa moto jana asubuhi na kusababisha hasara mbalimbali huku jeshi la polisi likiimarisha ulinzi na kusimamia shughuli za uokoaji wa mali zilizosalimika. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema chanzo cha moto huo ni hitilafu ya umeme iliyoanzia kwenye baadhi ya majokofu yaliyokuwa katika baadhi ya maduka hayo. 

Kamanda Mkumbo alisema mara baada ya hitilafu hiyo, moto huo ulishika mitungi ya gesi iliyolipuka na kuanza kusambaa kwa kasi na kuunguza maduka hayo. 

Alisema wamefanikiwa kuokoa baadhi ya mali katika maduka tisa kati ya 14 kwa msaada wa wananchi na wasamaria wema waliokuwa katika eneo la tukio lakini ukubwa wa hasara bado haujajulikana.

 Mmiliki wa moja ya maduka yaliyoteketea, Zena Athuman alisema kabla ya kufungua biashara yake, alifika katika eneo la tukio na kukuta moto huo umeshaanza na hakufanikiwa kuokoa mali yoyote kwa kuwa moto huo ulikuwa ukisambaa kwa kasi ya ajabu. 

Shuhuda wa tukio hilo, Julius Sangeti alisema alifika katika eneo hilo saa 11:30 asubuhi na kushuhudia moto ukiwaka katika duka kubwa la Mianzini na kadri muda ulivyokuwa ukisonga, ndivyo ulivyokuwa ukihamia kwenye maduka mengine na kuteketeza mali.

Mkulima afunga safari kutoka Urambo mpaka Bukoba kumuona Rais Magufuli

$
0
0
Mkulima wa tumbaku aliyesafiri kutoka Wilaya ya Urambo mkoani Tabora, Moshi Rubibi akitafuta upenyo wa kumfikishia Rais John Magufuli kilio cha wakulima, alifanikiwa kufanya hivyo mjini Bukoba  wa kutumia staili iliyomvuta Rais kumsikiliza. 

Awali, mkulima huyo anayewakilisha wenzake zaidi ya 60 alikwama kufanya hivyo wakati Rais Magufuli alipokuwa kwenye mapumziko wilayani Chato mkoani Geita baada ya kuzuiwa na walinzi lakini bila kukata tamaa alimfuata Rais mjini Bukoba baada ya kusikia anafanya ziara. 

Utaratibu wa Rais Magufuli kutaka kusalimiana na wananchi baada ya mkutano ndiyo uliofanikisha mpango wa mkulima huyo kwani aliamua kupiga kelele mfululizo kwa mbali akilitaja jina la Rais huku akipunga hewani mkono uliokuwa na bahasha ya kaki. 

Pamoja na kudhibitiwa na walinzi, sauti ya mkulima huyo ilizidi kuchomoza kwa nguvu hali iliyomfanya Rais Magufuli aliyekuwa anaondoka kwenye eneo la mkutano kupiga hatua kadhaa nyuma na kuwaambia walinzi wake wamuache amsikilize. 

Huku akitweta na kuhema kwa nguvu baada ya kuruhusiwa kumfikia Rais Magufuli, mkulima huyo alimwambia kuwa yeye ni mwenyeji wa Urambo, Tabora na amemtafuta ili kumfikishia malalamiko ya wakulima wa tumbaku wanaopigwa chenga kulipwa mafao yao. 

Alisema wakulima hao wanadai zaidi ya dola za Marekani 98,000 (zaidi ya Sh200 milioni) za mauzo ya tumbaku waliyouza kupitia Bodi ya Tumbaku tangu Septemba, 2015 na kuwa wanashawishiwa kutoa rushwa ili wapewe haki yao. 

Alimwambia Rais kuwa wameambiwa watoe dola 10,983 ili waweze kulipwa fedha zao kupitia tawi la Benki ya CRDB Urambo na kuwa kati ya kiwango wanachodai cha mauzo ya tumbaku wakubali kulipwa dola 87,017 tu. 

Mkulima huyo alisema wamefikisha suala hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Urambo na kukosa ufumbuzi na kuwa walilipeleka pia kwa aliyekuwa Waziri wa Kilimo na Mifugo, Mwigulu Nchemba ambaye alionyesha kuwa tayari kulishughulikia lakini kabla ya kufanya hivyo, alihamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

Baada ya kumsikiliza takribani kwa dakika nne, Rais Magufuli alimkabidhi mkulima huyo kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu), Jenista Mhagama na kuagiza apewe taarifa baada ya siku tano jinsi walivyoshughulikia suala hilo.

Mtoto Amuua Baba Yake Na Kutaka Kumfukia

$
0
0
Jeshi  la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Patrick Malindisa (29) mkazi wa Mtaa wa Namanyigu Manispaa ya Songea kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi Athanasi Malindisa (70) kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kidevuni na kisha kutaka kuufukia kwenye shimo alilochimba ndani ya nyumba yao.

Mmoja wa wanafamilia ambaye ni mdogo wa marehemu Pius Malindisa jana  alisema walipata taarifa ya kifo cha ndugu yao Januari Mosi mwaka huu saa 1:30 jioni  kutoka kwa mtoto wa marehemu Patrick Malindisa.

Alisema marehemu alikuwa akiishi na mtoto wake huyo ambapo baada ya kufanya mauji hayo alianza kuwaarifu ndugu kuwa amefariki kwa ugonjwa wa tumbo.

Kutokana na taarifa hizo ndugu walikusanyika nyumbani kwa marehemu ambapo baada ya kuingia ndani walikuta akiwa amelala ndipo walipowaita viongozi wa mtaa na baada ya kufunua walibaini marehemu ameuawa kwa kupinga na kitu chenye ncha kali kichwani na kidevuni.

“Baada ya kufanyika kwa uchunguzi wa awali tulitoa taarifa polisi ambapo walifika na kuuchukua mwili kwa uchunguzi zaidi. Na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma huku mtoto wake akishikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.

“Tulipofika hapa tulikuta shimo limechimbwa ndani ya nyumba na inaelekea lilimshinda na kuamua kuanza kutoa taarifa kwetu ambapo alidai alikuwa anaumwa ugonjwa wa tumbo,” alisema Pius

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji amethibitisha kutokea kwa mauaji hayo ambapo kwa sasa wanamshikilia mtoto wa marehemu, Patrick Malindisa kwa uchunguzi zaidi.

Mbunge Lwakatare wa CHADEMA Ammwagia Sifa Rais Magufuli

Serikali Yafuta Posho Za Vitafunwa, Mazingira Magumu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya posho mbalimbali zisizokuwa za kisheria zinaelekezwa katika miradi ya maendeleo.

Ametia agizo hilo leo (Jumanne, Januari 3, 20017) wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Kigamboni akiwa katika ziara yake ya kikazi.

“Kuanzia sasa marufuku Wakurugenzi kutoa posho zisizotambulika kisheria zikiwemo za mazingira magumu, kujenga uwezo na vitafunwa katika halmashauri zenu na badala yake fedha hizo zitumike kwenye miradi ya maendeleo,” amesema.

Agizo hilo litawezesha Jiji la Dar es Salaam kuokoa sh bilioni 130 zilizokuwa zitumike na Halmashauri na Manispaa za jiji hilo, ambazo kwa sasa zitaingizwa kwenye miradi na shughuli za maendeleo.

Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma nchini kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kuacha kutumia fedha kinyume cha utaratibu na watakaobainika Serikali haitosita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

“Katika halmashauri zetu kila mtumishi anashiriki katika ukusanyaji wa mapato hadi walinzi, lakini mwisho wa siku vitafunwa huliwa na wachache wanaojiita wakubwa huku wengine wakisikilizia kwa nje. Jambo hili haliwezekani,” amesisitiza.

Waziri Mkuu amesisitiza kwamba Mkurugenzi yeyote atakayebainika kulipa posho hizo baada ya siku ya leo atakuwa amejifukuzisha kazi.

Aidha, ameagiza fedha zilizokuwa zikitolewa kwa madiwani kwa ajili ya kuhamasisha maendeleo zisitolewe moja kwa moja kwa madiwani na badala yake zipelekwe kwenye kata husika na zifuatiliwe matumizi yake.

Hata hivyo, Waziri Mkuu amezionya halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa kila fedha zinayopelekwa kwenye halmashauri hizo inatumika kama ilivyokusudiwa na atakayebainika kutumia kinyume hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

Pia amewataka watumishi wote wa umma nchini kuwajibika ipasavyo na kuhakikisha wanawatumikia vyema mwananchi ikiwa ni pamoja na kuepuka vishawishi na kujiingiza kwenye vitendo vya rushwa na ufisadi.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ametoa siku tatu kwa watumishi 10 wa halmashauri hiyo ambao wamehamishiwa kutoka wilaya ya Temeke wawe wameripoti katika Manispaa hiyo, vinginevyo watakuwa wamejifukuzisha kazi.

Awali Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Bw. Hashim Mgandilwa wakati akiwasilisha taarifa ya wilaya hiyo kwa Waziri Mkuu, alisema hadi sasa asilimia 98 ya watumishi waliotakiwa kuhamia kwenye halmashauri hiyo wameripoti isipokuwa 10 na hakuna taarifa zozote juu yao.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

EWURA yatangaza bei mpya za mafuta

$
0
0
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA)  imetangaza bei mpya za nishati ya mafuta zitakazoanza kutumika kesho Jumatano huku bei ya mafuta ya taa na dizeli ikiwa imeshuka kwa wastani wa shilingi 66 kwa lita.

Taarifa iliyotolewa na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Felix Ngamlagosi inaonesha kuwa kwa wastani kumekuwa na ongezeko dogo sana la bei ya mafuta ya petroli ambayo kwa jiji la Dar es Salaam bado itauzwa kwa bei ile ile ilivyokuwa mwezi uliopita.

Hata hivyo, taarifa hiyo imetoa ruhusa kwa wauzaji wa jumla na rejareja wa mafuta nchini kuuza bidhaa hiyo kwa bei ndogo chini ya bei elekezi iliyotangazwa na mamlaka hiyo kama njia ya kuchochea ushindani baina ya wauzaji wa mafuta nchini.

Utata Wagubika Mauaji ya Afisa Mtendaji Mbeya

$
0
0
Mwili wa ofisa mtendaji wa mtaa wa Kabwe, katika kata ya Iyela jijini Mbeya Clementine Enock (34) umekutwa ukiwa umetelekezwa katika eneo la Airport ya zamani baada ya kuuawa na watu wasiofahamika kwa kubanwa pumzi.

Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Dhahiri Kidavashari alisema jana kuwa walibaini kuwepo kwa mwili huo Januari mbili, mwaka huu majira ya saa moja asubuhi baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Kidavashari alifafanua kuwa kabla ya tukio hilo marehemu aliondoka nyumbani kwao siku ya Mwaka mpya  na kuaga kuwa anakwenda Airport kwenye sherehe ya rafiki yake huku akiwa na gari yenye namba za usajili T234 DJM aina ya Toyota Spacio.

Alisema kuwa ndugu wa marehemu walipata hofu mara baada ya ndugu yao kuchelewa kurudi nyumbani na ndipo wakaanza kumpigia simu bila mafanikio mpaka usiku wa manane.

“Marehemu aliaga nyumbani kwao Uyole ya Kati alikokuwa akiishi majira ya saa kumi jioni siku ya tarehe moja kwa madai anaenda kwenye sherehe ya rafiki yake akiwa na usafiri wa gari lake, ambapo mpaka kufika usiku wa manane hakukuwa na taarifa yeyote ndipo hofu ikatanda kwa familia ambapo walipiga simu kwa ndugu jamaa na marafiki na kueleza kuwa hawajui alipo,” alisema Kidavashari.

Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari siku iliyofuata majira ya saa moja asubuhi mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa umetupwa katika eneo la wazi jirani na Shule ya Sekondari ya Samora ambapo uchunguzi wa awali unaonesha kifo chake kilitokana na kubanwa pumzi na watu wasiofahamika.

Alisema mazingira ya kifo yanaonyesha wazi kuwa marehemu aliuawa na mtu wa karibu yake huku akisema tukio hilo lilifanywa ndani ya nyumba ya mtu.

TCRA Yatishia Kuzifutia Leseni Kampuni za Simu

$
0
0

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetishia kusitisha kwa muda au kufuta kabisa leseni ya biashara kwa kampuni zote za mawasiliano nchini, zitakazoshindwa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)

Hatua hiyo ni kulingana na sheria mpya ya fedha ambayo imetoa ukomo wa hadi Desemba 31 mwaka jana kampuni hizo ziwe zimejisajili katika soko hilo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam hii leo; Mkurugenzi Mkuu wa TCRA Mhandisi James Kilaba amesema kwa sasa wanasubiri maelezo kutoka Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana  (CMSA) kuhusu idadi ya kampuni za mawasiliano zilizokidhi sifa za kusajiliwa katika soko la hisa kwa ajili ya kuchukua hatua kwa zile zilizokaidi kutekeleza agizo hilo la kisheria.

Mhandisi Kilaba amesema TCRA imeikabidhi CMSA orodha ya kampuni zaidi ya 80 za mawasiliano, orodha ambayo CMSA itaipitia kwa lengo la kuchuja na kupata kampuni ambazo zinastahili kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.

Kauli ya Mhandisi Kilaba imekuja huku taarifa kutoka soko la Hisa la Dar es Salaam zikionesha kuwa ni kampuni tatu pekee ndizo zimejisajili katika soko hilo, licha ya muda wa kufanya hivyo kufikia ukomo wake Jumamosi ya Desemba 31 mwaka jana.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images