Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Disemba 30


Francis Cheka atangaza ramsi kustaafu ngumi

0
0
Bondia maarufu nchini Tanzania Francis Cheka, jana ametangaza rasmi kustaafu mchezo wa msumbwi kwa kile alichokieleza ni ubabaishaji wa ma-promota pamoja na kutopata faida katika mchezo huo.

Cheka ambaye anakabiliwa na tuhuma za kuchukua pesa na kugoma kupanda ulingoni katika pambano lililokuwa limeandaliwa siku ya Krismasi, amesema amechoshwa na kile alichokiita kuwa ni utapeli wa mapromota, na kwamba sasa atajikita zaidi katika mapambano ya kuhamasisha vijana.

Akiwa amedumu kwenye ngumi  nchini kwa takribani miaka 19, Cheka amesema mchezo huo umetawaliwa na majungu, na fitina huku watu wengi wakifikiri kuwa kuna pesa nyingi, wakati hakuna anachokipata zaidi ya umaarufu na kuhojiwa kwenye vyombo vya habari.

"Huu mchezo una majungu na fitina, hakuna faida yoyote zaidi ya kuhojiwa na waandishi wa habari, hakuna pesa, tunapata pesa gani, watu wanadhani tunapata pesa,  nitabaki kucheza mapambano kwa ajili ya kuhamasisha vijana katika ngumi pamoja na kufanya biashara nyingine nipate pesa, nimedumu kwenye ngumi zaidi ya miaka 19, nimevumilia mengi" Alisema Cheka.

Washitakiwa Wanne Mauaji wa Dr. Mvungi Waachiwa Huru

0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya 10 waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya bila  kukusudia ya aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.

Washitakiwa walioachiwa ni Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata Darajani, Zacharia Msese (33), Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala na John Mayunga (56).

Waliachiwa kwa mujibu wa Kifungu Namba 91 Kifungu kidogo cha kwanza cha Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA). Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala alidai mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba kuwa upande wa mashitaka umeshasajili jalada hilo Mahakama Kuu.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mshitaka Nchini (DPP), hakuwa na nia ya kuendelea kuwashitaki washitakiwa hao kwa mujibu wa kifungu hicho. Awali, Shinyambala alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maelezo ya mashahidi baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.

Hakimu Simba alisema anawaachia washitakiwa hao, kama walivyoomba upande wa mashitaka. Alisema kwamba washitakiwa sita, ndio watakaosomewa maelezo hayo ya mashahidi.

Washitakiwa hao ni Longishu Losingo (29), Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Juma Kangungu (29) mkazi wa Vingunguti, Msungwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti na Masenga Mateu.

Hata hivyo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashitaka, kuhakikisha kwamba wanaleta cheti cha kifo cha mshitakiwa wa kwanza, Chibago Magozi (32), mfanyabiashara mkazi wa Vingunguti Machinjioni.

Pia alieleza kuwa kesi hiyo ikienda mahakama kuu, bila ya kupelekwa mahakamani hapo cheti cha kifo, itakwama kwa kuwa hawawezi kusoma maelezo hayo hadi kwa mtu aliyekufa.

Aliwataka kuhakikisha katika tarehe ijayo ambapo washitakiwa sita watasomewa maelezo, wawe wamewasilisha cheti cha kifo.

Hata hivyo, Wakili Shinyambala alikubaliana na maelezo hayo na kuomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa waliobaki maelezo ya mashahidi. Kesi imepangwa Januari 10, 2017.

Waziri Mkuu: Wasichana waachwe wasome

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imedhamiria kuwalinda watoto wa kike na ndiyo maana inasisitiza waachwe wasome hadi wamalize kidato cha sita.

Alitoa kauli hiyo kwa nyakati tofauti wakati akizungumza na wananchi wa vijiji mbalimbali vya wilaya ya Ruangwa, mkoani Lindi ambako anapita kuwasalimia wananchi wa jimbo lake na kuhimiza kazi za maendeleo. Waziri Mkuu yuko Ruangwa kwa siku nne kwa mapumziko ya mwisho wa mwaka.

“Tumesema mtoto wa kike aachwe asome hadi kidato cha sita, akifika chuo kikuu atakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi yake lakini kwa sasa waacheni watoto wa kike wasome. Ninyi vijana, mkibainika mmewapa mimba mabinti wanaosoma, adhabu yake ni miaka 30 jela,” alisema.

Alisema nia ya Serikali ni kupata watumishi ambao ni wataalamu wa kada tofauti kama madaktari, wanasheria, mafundi, walimu na hata Wakuu wa Wilaya ambao ni wanawake.

Aliwaonya wazazi ambao huwa wanakubali kuongea pembeni (kupewa fedha) na wanaume waliowapa mimba mabinti zao na kuwaeleza kuwa, kwa mujibu wa sheria ilivyo, nao pia wanastahili kupewa adhabu ya kifungo jela.

“Mzazi ukigundua binti yako ana ujauzito toa taarifa haraka ili mhusika akamatwe mara moja. Usikubali kuongelea jambo hili pembeni, nawe pia utawekwa ndani pamoja na huyo mhusika ambaye tayari ni mhalifu,” alisema na kuongeza:

“Mwanao akisema anataka kuoa, mzazi inabidi upeleleze kwanza anataka kumuoa nani. Asije kuwa anamuona binti ambaye bado anasoma. Akisema anaoa na wewe ukamkubalia tu, ikija kubainika kuwa ni mwanafunzi, wewe na mkeo mnakwenda jela miaka mitano mara sita,” alisema huku akionyesha ishara ya kukunja ngumi.

Akiwa kwenye baadhi ya vijiji, Waziri Mkuu alielezwa kwamba kuna shule ambazo zina walimu wa kiume watupu na akamtaka Afisa elimu asimamie suala hilo kwa kuwahamisha baadhi ya walimu kutoka Ruangwa mjini na kuwapeleka shuke za vijijini.

“Kuna shule pale Ruangwa mjini zina walimu wamerundika lakini hapa naambiwa hakuna Mwalimu wa kike hata mmoja. Hili tatizo kwa wanafunzi wa kike. Wana masuala ambayo hawawezi kuongea na walimu wa kiume, ni lazime awepo Mwalimu wa kike wa kusikiliza shida zao,” alisema na kumsisitiza afisa elimu afuatilie tatizo hilo kwenye shule zote.

Mapema, akitoa taarifa ya mkoa mbele ya Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema mkoa huo unakabiliwa na tatizo la utoro mashuleni kwani wanaoandikishwa darasa la kwanza si wote wanaomaliza darasa la saba na vivyo kwa wanaoanza kidato cha kwanza na kumaliza kidato cha nne.

“Takwimu zinaonesha mkoa wa Lindi unalo tatizo kubwa sana na ambalo tunaendelea kulipa uzito wa pekee la kudhibiti wanafunzi wanaoandikishwa kuanza shule lakini wanashindwa kukamilisha kipindi chao cha miaka saba shuleni. Idadi kubwa ya wanafunzi ni watoro,” alisema.

Takwimu za kidato cha nne zinaonyesha kuwa idadi ya watahiniwa wa shule walikuwa 4,764 (wavulana 2411 na wasichana 2,353) na watahiniwa wa kujitegemea walisajiliwa 335 na kati yao watahiniwa 290 (asilimia 86.6) walifanya mtihani na watahiniwa 45 ambao ni sawa na asilimia 13.4 hawakufanya mtihani.

Kwa upande wa masomo ya sayansi, shule zilizofanya mitihani ya sayansi ya vitendo (actual practical) zilikuwa ni 78 (Kilwa 19, Liwale 11, Lindi Manispaa 9, Ruangwa 4, Lindi vijijini 14 na Nachingwea 21) watahiniwa ambao hawakufanya mtihani baada ya kusajiliwa ni 100 (wavulana 50 wasichana 50).

DC Singida aagiza atakayeugua kipindupindu afikishwe mahakamani

0
0
Na Nathaniel Limu, Singida
Watu wawili wakazi wa jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida, wamefariki dunia baada ya kuugua ugonjwa hatari wa Kipindupindu unaotokana na uchafu.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana ofisini kwake, Mkuu wa wilaya ya Singida, Elias Tarimo, alisema Novemba, 26 mwaka huu, ugonjwa huo wa Kipundupindu ulibainika katika vijiji vya Merya na Msange jimbo la Singida kaskazini.

Hata hivyo, alisema kuwa ilichukua muda mrefu mno mamlaka zinazohusika kutoa taarifa ya ugonjwa huo, kitendo kilichochangia idadi ya wagonjwa kuongezeka na kufikia 30.

“Urasimu huu umesababisha hatua stahiki za kudhibiti ugonjwa huu, kuchelewa kuchukuliwa na hivyo kuchangia wananchi wawili kupoteza maisha. Kwa sasa tumebakiwa na wagonjwa sita kambi ya Merya na Msange wapo watatu,” alisema Tarimo.

Mkuu huyo wa wilaya, alisema baada ya kupata taarifa hizo kwa kuchelewa, hawakulala walipiga kampeni ya nguvu kuhimiza usafi wa mazingira, matumizi bora ya vyoo na kuchemsha maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

“Aidha, wataalam walipima maji ya visima 14 yanayotumiwa na wananchi wa vijiji hivyo, na 12 kubainika vina vidudu vinavyochangia ugonjwa wa kipindu pindu. Baada ya kugundua hivyo, tumepiga marufuku maji ya visima hivyo kutumika,” alisema.

Akifafanua, alisema wamewaelekeza wananchi kutumia maji ya bomba na wamechukua mashine kubwa ya kupampu maji kutoka kijiji cha Sagara.

“Mashine hii tumeisimika na itasambaza maji ya bomba katika vijiji hivyo vya Msange na Merya. Hatujaishia hapo, tunaendelea kuwahimiza wananchi kutumia vidoge vya waterguird kwa ajili ya kutibu maji yawe safi na salama. Vile vile tanawahimiza kutumia vyoo na kuacha tabia ya kujisaidia ovyo kwenye vichaka,” alisema.

Katika hatua nyingine, Tarimo alisema kuwa baada ya kufanya kampeni ya kuhimza usafi, mwananchi yoyote atakayeugua Kipindupindu, atatibiwa na akipona, mara moja atafikishwa mahakamani, kujibu tuhuma ya kutaka kujiuawa kwa makusudi.

Wakati huo huo, katika kuchukua hatua kudhibiti Kipindupindu, Manispaa ya Singida imechukua hatua mbalimbali, ikiwemo ya kupiga marufuku wafanyabiashara wa matunda, kumenya matunda. Imeagizwa kuwa matunda yote yaliwe nyumbani baada ya kuoshwa vizuri kwa maji.

Pia kila kaya imeagizwa kutumia vyoo bora na kunawa mikono kwa sabuni kabla ya kula chakula na baada ya kutoka chooni.

Mkurugenzi wa manispaa hiyo, Bravo Kizito Lyapembile, amesema mtu ye yote akikamatwa kwa kuchafua mazingira, atatozwa faini kati ya shilingi 30,000 na 300,000.


Baba Adaiwa kumlawiti mtoto wake wa kiume

0
0
Mwanamume mwenye miaka 45 Yohana Omari anatafutwa na Polisi kwa tuhuma za kumlawiti mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 16, kwa zaidi ya miaka miwili. 

Omari ametoroka baada ya kupata taarifa kuwa anatafutwa na wananchi kutokana na tukio alilokuwa akimfanyia kijana huyo (jina linahifadhiwa) tangu mwaka 2013. 

Akizungumzia tukio hilo, kijana huyo alisema kuanzia mwaka huo, akiwa darasa la nne amekuwa akifanyiwa kitendo hicho na baba yake na kukatazwa asiseme. 

Alisema siku ya kwanza alipobaini anafanyiwa ilikuwa usiku akiwa amelala, alishtuka kutokana na kuhisi maumivu makali na kumkuta baba yake amemlalia juu. 

Alifafanua kuwa kuanzia hapo hayo yakawa ndiyo maisha yake na anapolalamika hukosa baadhi ya huduma, jambo lililokuwa likimlazimu akubali kuendelea kwa shingo upande.

 “Kuna mafuta huwa ananipaka na kunifanyia kitendo hicho, nimeishi kwa tabu ikiwamo kuamka asubuhi nimechoka na sina hamu ya jambo lolote, natamani kulala. 

“Imefikia mahali natoka majimaji hadi kuogopa kujichanganya na wenzangu,” alisema kijana huyo.

Kijana huyo alisema kabla ya kuishi na baba yake, alikuwa anaishi na mama yake, lakini alipata mwanamume akaolewa kwa sharti la kutokuishi na yeye, ndipo akampeleka kwa baba yake. 

Alieleza kuwa licha ya kuwaeleza ndugu wa familia, wakiwamo bibi zake, hakuna walichomsaidia. 

“Nimemaliza darasa la saba, nimechaguliwa kujiunga sekondari, lakini sina uhakika wa kuendelea na masomo. 

“Baba amekimbia na kuna viashiria alitumia rushwa, ulinzi shirikishi badala ya kumkamata walimtorosha,” alisema. 

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kwa Mustapha Pugu, Dar es Salaam, Bahati Omari alisema baada ya kupata taarifa hizo, kwa kushirikiana na vijana wake, walifikisha taarifa polisi ili akamatwe lakini alikuwa ameshatoroka. 

Askari polisi mmoja wa eneo hilo alisema baada ya kupokea malalamiko hayo, walimpeleka hospitali kijana huyo kumfanyia vipimo ambavyo alibainisha kuwa amefanyiwa kitendo hicho mara nyingi. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema suala hilo lipo chini ya upelelezi. 

“Tumepokea hayo malalamiko, tunayachunguza kwa sababu yanachanganya, amekuwa akifanyiwa vitendo hivyo tangu mwaka 2013 na amekuja kubainisha leo, hivyo inahitaji upelelezi wa kina,” alisema Hamduni.

Jela maisha kwa kupora simu ya Sh110,000 na kujeruhi

0
0
Kesi ya wizi wa simu aina ya Tecno iliyochukua takriban miaka miwili mahakamani, imefika tamati kwa mtuhumiwa kufungwa maisha jela. 

Hukumu hiyo ilifikiwa jana katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala, baada ya mtuhumiwa Kassim Salum (18) kukutwa na hatia kwa kosa la unyang’anyi wa kutumia nguvu wa simu yenye thamani ya Sh110,000. 

Mshtakiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Januari 28, mwaka jana katika Mtaa wa Ghana Magenge eneo la Buguruni jijini Dar es Salaam. 

Ushahidi uliotolewa na mashahidi watano uliiwezesha mahakama kukubaliana na madai ya mlalamikaji Lutifia Mohamed. 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Flora Haule alisema, “Baada ya kusikiliza mashahidi wote watano wa upande wa jamhuri, mahakama inaona wamethibitisha mashtaka dhidi ya mshtakiwa.” 

Akipitia ushahidi huo, hakimu Haule alisema mshtakiwa alimsukuma mlalamikaji na kuangukia katika karai la mafuta ambalo lilikuwa jikoni. 

Mashahidi hao waliieleza jinsi mshtakiwa alivyomvamia mlalamikaji akimtaka atoe simu aliyokuwa nayo na katika purukushani hizo, alimpiga ngumi tumboni hali iliyosababisha kuishiwa nguvu. 

Ilielezwa kuwa kutokana na kupigwa, mlalamikaji aliirusha simu upande wa pili ambapo kulikuwa na muuza chipsi, hivyo Salum aliamua kumuachia mlalamikaji ili aende kuifuata. 

Hata hivyo, wakati mlalamikaji anajaribu kuokota simu yake, Salum alimsukuma akaangukia katika karai la mafuta ya moto na kumsababishia kuungua eneo lote la mgongoni. Inadaiwa baada ya hapo Salum alichukua simu hiyo na kutoweka nayo. 

Wakili wa Serikali, Sylvia Mitanto aliomba mahakama impe adhabu kali Salum ili aweze kujifunza kwa kuwa amemtia mlalamikaji ulemavu wa kudumu. 

Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mahakama ilitoa nafasi kwa mshtakiwa kujitetea na Salum aliomba isimpe adhabu kali akisema si yeye aliyechukua simu hiyo, bali ni chuki binafsi za mitaani wanakoishi. 

Viongozi Chadema Arusha Wakamatwa Na Polisi

0
0
JESHI la Polisi Mkoa wa Arusha linawashikilia watu 12, wakiwemo viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Mkoa wa Arusha.

Viongozi hao walikamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo wakituhumiwa kuhusika kuchoma moto mashine za kuvuta maji kutoka kwenye chanzo cha Kangdet wilayani Karatu kwa madai kwamba wanatekeleza agizo la Serikali, hatua ambayo imeelezwa kuwa haikufuata utaratibu.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Arusha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Karatu, Moshi Darabe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Barai, anayedaiwa kuhamasisha wananchi kuchoma moto mashine hizo zenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 16.

Wengine waliokamatwa ni Diwani wa Kata ya Mang’ola, Lazaro Emanuel, viongozi wa vijiji vya kata hizo pamoja na baadhi ya wananchi.

Kamanda Mkumbo alisema kuwa msako wa kuwakamata watuhumiwa wengine waliohusika na tukio hilo bado unaendelea na uchunguzi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Desemba 27, mwaka huu, kundi la wananchi wa vijiji vinne vya  kata hizo waliandamana, wakang’oa na  kuchoma moto mashine za kuvuta maji katika chanzo cha  maji cha Kangdet, kinachotegemewa na  vijiji vingine vya Kata ya Barai.

Kutokana na tukio hilo, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ikiongozwa na mwenyekiti wake ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Gambo, walitembelea eneo la tukio na baada ya viongozi kueleza kilichotokea, aliagiza kukamatwa kwa watu wote waliohusika na uharibifu huo.

“Sheria lazima ichukue mkondo wake kwani agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa lilikuwa wazi na halikusema wananchi wachukue sheria mkononi, jambo hili ni kinyume cha sheria,” alisema Gambo katika mkutano huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu, Jubilate Mnyenye (Chadema), amesema kuwa yeye, mbunge wa jimbo hilo, Willy Qambalo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mang’ola, Jacob Pius, wametakiwa kuripoti Kituo Kikuu cha Polisi jijini Arusha leo asubuhi kwa mahojiano kuhusu tukio hilo.

Pata Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kuondoa Michirizi, Kuongeza Unene, Kuondoa Chunusi na Zingine Nyingi Toka Beauty Cosmetics

0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS Ni wauzaji wa vipodozi aina mbali mbali na vyenye matokeo mazuri na ya haraka zaidi bila kemikali wala madhara yoyote
 
     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @90,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @120,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 120,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 90,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 100,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @100,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
12.kuotesha nywele kwenye kipara @100,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=
 
     WASILIANA NASI KWA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti ili kuhakikisha mafanikio yako
 
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Urusi Yaapa Kulipiza Kisasi Baada ya Marekani Kuwatimua Wanadiplomasia wa Urusi

0
0
Urusi imeonya kwamba italipiza kisasi hatua ya rais wa Marekani Barrack Obama ya kuwatimua wanadiplomaisa 35 wa Urusi kufuatia tuhuma kwamba Urusi iliingilia maswala ya uchaguzi wa Marekani kwa njia ya udukuzi wa mitandaoni.

Obama amesema Urusi pia imekuwa ikiwadhalilisha maafisa wa Marekani.

Kwa upande wake, rais mteule Donald Trump ambae mara kwa mara amekuwa akizipuuzilia taarifa hizo za udukuzi, sasa amesema atakutana na wakuu wa kiintellijensia wa Marekani ili kupata undani zaidi wa swala hilo.

Msemaji wa rais Vladmir Putin amesema kuwa hatua zitakazochukuliwa na Urusi zitaiathiri Marekani.

Hatahivyo amesema kuwa Urusi itasubiri hadi rais mteule Donald Trump ambaye amepinga tuhuma hizo za udukuzi atakapochukua mamlaka.

Urusi imekana madai yoyote ya udukuzi na kuvitaja vikwazo hivyo vya Marekani kama visivyo na msingi.

Siku ya Alhamisi, Idara ya maswala ya kigeni nchini Marekani ilitangaza kwamba mabalozi hao 35 kutoka Urusi pamoja na wasaidizi wao huko San Fransisco hawatakiwi  Marekani na kuwapatia wao na familia zao muda wa saa 72 kuondoka nchi humo.

Picha: Waziri Nchemba atembelea WCB, aahidi kuongeza kasi ya kulinda kazi za wasanii

0
0
Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba wiki hii alitembelea ofisi ya WCB iliyopo Sinza Mapambano jiji Dar es salaam na kujionea uwekezaji uliofanywa na label hiyo ambayo ipo chini ya Diamond Platnumz.

Waziri huyo kijana aliweza kuzungumza na viongozi wa label hiyo na kuangalia namna ambavyo serikali inaweza kudhibiti wizi wa kazi za wasanii.

Baada ya kumaliza mazungumza hayo, Waziri Nchemba kupitia instagram yake aliandika:

    #Wizi wa kazi za wasanii #Jeshi la polisi kuongeza nguvu

Pia alisema kuwa serikali haitasita kuwapa msaada pale watakapokwama na kuhitaji usaidizi wa serikali.

Diamond Atikisa Australia....Wimbo Wake Wavunja Rekodi ya Mwaka

0
0
Diamond Platnumz haishi kutuamsha na habari kubwa zinazohusiana na nyimbo zake.

Siku moja baada ya DW kuitaja ngoma aliyoshirikishwa na marehemu Papa Wemba, Chacun Pour Soi kuwa imefunga mwaka kwa kuwa namba moja katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Kidogo aliyowashirikisha P-Square nayo imefunga mwaka kwa kishindo.

Wimbo huo umekuwa wimbo wa mwaka katika kituo cha redio cha Radio Afro cha Australia, baada ya kuzishinda nyimbo za magwiji wengi wa Afrika wakiwemo Wizkid, Davido, Tiwa Savage na wengine kibao.

Diamond ameshukuru kwa nafasi hiyo kwa kusema, “Thank you AUSTRALIA thank you RADIO AFRO…. KIDOGO ft P -SQUARE Song of the Year #RADIOAFRO.”

Tamko la Zitto Kabwe kuhusu madeni anayodaiwa, mshahara na mali alizonazo

0
0
Leo December 30, 2016 Mbunge Zitto Kabwe kutoka Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo) kupitia akaunti yake facebook ametoa taarifa kuhusu madeni anayodaiwa, kiwango cha mshahara wake wa mwaka, kiasi cha pesa kilichopo benki, posho pamoja na mali zote anazomiliki.

Hiki kimeandikwa na Zitto Kabwe leo.
Ndugu Watanzania, Kama mnavyofahamu kuwa ibara ya 132(4) na (5) na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Sheria namba 13 ya mwaka 1995 inataka viongozi wote wa umma kujaza fomu za Tamko la Rasilimali na Madeni. Tamko hilo huwasilishwa Sekretariat ya Maadili ya Viongozi kabla ya mwisho wa kila mwaka. Kama nifanyavyo siku zote, nawajulisha rasmi kwamba nimetimiza matakwa hayo ya katiba na sheria kuhusu Maadili ya Viongozi.

Inafahamika kuwa Chama Cha ACT Wazalendo, kwa mujibu wa Katiba yake na Azimio la Tabora, kimeelekeza kuwa Viongozi wake wote waweke wazi kwa Umma Tamko la Mali, Madeni na Maslahi. Kwa kufuata masharti ya Katiba ya Chama Cha ACT Wazalendo natangaza rasmi fomu zangu nilizowasilisha Leo Sekretariat ya Maadili ya Viongozi wa Umma.

Ni matumaini yangu kwamba itafikia wakati Daftari la Rasilimali na Madeni la Viongozi wa Umma litakuwa linawekwa wazi kwa Umma ili wananchi waweze kujua Mali, Madeni na Maslahi ya Viongozi wao na pale ambapo kiongozi ametoa habari zisizo sahihi au kuficha mwananchi aweze kutoa Taarifa kwenye Sekretariat na Baraza la Maadili liweze kufanya kazi yake ipsavyo.

Mfumo wa kuweka wazi Rasilimali na Madeni ya Viongozi wa Umma ni mfumo endelevu na muhimu kwenye vita vita dhidi ya ubadhirifu na ufisadi. Mataifa kadhaa duniani hutumia mfumo huu ( public disclosure of leaders’ assets and liabilities) kuwezesha mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi. Nchini Uingereza na Kanada kwa mfano, daftari la matamko ya Rasilimali na Madeni ya Viongozi lipo wazi kwa kila mwananchi kuona na huuzwa kwenye duka la vitabu la Bunge.

Namsihi Sana Rais John Pombe Magufuli kusaidia kufanya mabadiliko makubwa ya Sheria ya maadili ya Viongozi ili kurejesha na kuboresha Miiko ya Viongozi katika kuimarisha vita dhidi ya ufisadi nchini. Rais aliahidi kuweka wazi Mshahara wake alipokuwa anazungumza katika kipindi cha 360 cha Clouds TV. Ninamkumbusha afanye hivyo na pia aweke wazi Mali, Madeni na Maslahi yake ya Kibiashara ili awe mfano kwa Viongozi wengine Nchini.

Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb
Kigoma Mjini
30/12/2016

Picha : Hali ya mwanamuziki Chid Benz yazidi kuwa mbaya

0
0
Watu wengi walionyesha kusikitishwa baada ya habari kuenea kuwa mwanamuziki Rashid Mkwiro maarufu Chid Benz ametoroka kwenye nyumba ya matibabu (Sober house) alipokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Kwa kadiri picha zake zinavyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii inaonyesha dhahiri kuwa mwanamuziki huyo hali yake inazidi kuwa mbaya tofauti na alivyotoka kwenye nyumba ya matibabu ambapo aliweza kurekodi wimbo na pia kutumbuiza katika matamasha kadhaa ya muziki.

Babu Tale aliyekuwa amejitolea kumsaidia awali alisema hawezi kumsaidia tena kwani alishafanya hivyo ikashindikana na kusema Chid Benz ni sikio la kufa.

Licha ya kuwa inadaiwa kuwa hataki kupatiwa matibabu lakini ni dhahiri kuwa kwa hali yake ilivyo sasa anahitaji msaada tena wa haraka zaidi kuweza kuyanusuru maisha yake.

Hapa chini ni picha za hali ya mwanamuziki huyo kwa sasa.

Kilichosababisha bondia Francis Cheka kufungiwa kucheza ngumi

0
0

Leo December 30, 2016 Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC) imetangaza kumfungia kwa miaka miwili Bondia wa ngumi za kulipwa, Francis Cheka kufuatia kitendo chake cha kugoma kupanda ulingoni kupigana na Bondia Abdallah Pazi “Dullah Mbabe”.

Pambano hilo ilikuwa lifanyike Desemba 25 mwaka huu, katika Ukumbi wa PTA Saba saba jijini Dar es salaam, lililoandaliwa na Promota Siraju Kaike kupitia kampuni yake ya Kaike Promotion.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, Katibu Msaidizi wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa nchini (TPBC), Chatta Michael amesema kuwa Kamisheni yake ilitoa kibali cha kufanyika kwa mpambano huo baada ya kujiridhisha kuwa taratibu zote zimefuatwa na mabondia wameridhia na kukubaliana na muandaaji, Ila wameshangwaza na Bondia Francis Cheka kugoma kupanda ulingoni kwa madai ya malipo wakati alishasaini mkataba na muandaaji ulioonyesha kuwa ameshachukua kiasi cha shilingi milioni tatu (3,000,000) na baada ya mpambano alitakiwa kupewa kitita chake cha milioni sita.

Amesema kitendo kilichofanywa na Cheka kinaweza kupoteza uaminifu baina ya mabondia na waandaaji wa mapambano, kujiondoa kwa waandaaji katika mchezo huo kwa kuona hakuna uaminifu na pia kinaweza sababisha uvunjifu wa amani kwa watazamaji, iwapo wataendelea kudanganywa uwepo wa mapambano hewa.

Hivyo Kamati ya utendaji ya Kamisheni hiyo iliyokaa Desemba 27, na kupitia kanuni za mchezo huo, imemkuta Bondia Francis Cheka na makosa ya kimakubaliano na kutangaza kumfungia kujihusisha kwa namna yeyote na mchezo huo na kutakiwa kupipa faini ya shilingi laki tano (500,000).

Kamanda Sirro Katoa Tathmini ya Uhalifu Dar kwa Mwaka Mmzima wa 2016

0
0
KIKOSI cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata jumla ya watuhumiwa 13,626 na kuwafikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya na ujambazi wa kutumia silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2016.

Aidha, hali ya uhalifu wa kutumia silaha katika jiji la Dar es Salaam umepungua, ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2015 na matukio yanayoongezeka kwa wingi ni ya ubakaji na ulawiti.

Akitoa tathmini ya mwaka mmoja, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yamepungua kutoka 204 mwaka jana hadi 127 mwaka huu.

Idadi hiyo ni pungufu ya matukio 77, sawa na asilimia 37.7 huku matukio ya kutumia nguvu yamepungua kutoka 1,181 mwaka jana hadi 874 sawa na asilimia 26.

Kamishna Sirro alifafanua kuwa matukio ya mauaji, yamepungua kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka jana, ambapo kulikuwa na jumla ya matukio 327 wakati kwa mwaka huu ni matukio 291 pungufu ya matukio 36.

Alisema matukio ya ubakaji, yameongezeka kutoka 972 mwaka jana hadi 1030 mwaka huu, sawa na asilimia sita wakati matukio ya ulawiti yameongezeka kutoka 310 mwaka jana hadi 383 mwaka huu sawa na asilimia 23.5.

‘’Kwa matukio ya ubakaji yaliyoongezeka ni 58 na ulawiti matukio yaliyoongezeka ni 73. Lakini wizi wa watoto umepungua kutoka 26 mwaka jana hadi matukio 19 mwaka huu sawa na asilimia 27,’’ aliongeza.

Kwa mujibu wa Sirro, matukio ya uvunjaji yamepungua kwa asilimia 5.7 ambapo kwa mwaka jana kulikuwa na matukio 5,677 na mwaka huu matukio 5,355 sawa na upungufu wa matukio 322.

Kwa upande wa wizi wa magari, umepungua kwa asilimia 18.1 kutoka matukio 392 hadi 321 mwaka huu huku wizi wa pikipiki ukipungua kutoka pikipiki 2,644 mwaka jana hadi 2,191 ambapo matukio 453 yamepungua sawa na asilimia 17.1.

Wizi wa mifugo umepungua kutoka 197 mwaka jana hadi 163 mwaka huu sawa na asilimia 17.3 ikiwa ni pungufu ya matukio 34.

“Sababu za kuongezeka au kupungua kwa matukio hayo kumetokana na juhudi za polisi wa kuzuia na kupambana na uhalifu kwa kufanya doria pamoja na misako mbalimbali iliyosaidia kukamatwa kwa wahalifu wa makosa mbalimbali pamoja na raia wema ambao wametoa taarifa za siri ili kugundua makosa hayo,’’ alieleza Sirro.

Akielezea watuhumiwa hao, Sirro alisema kuwa kati yao 52 walikutwa na silaha za kivita 67 na risasi 1,076, na watuhumiwa 126 walikutwa na dawa za kulevya aina ya mirungi kilo 75 na gramu 254.

Pia alisema kuwa watuhumiwa 7,625 walikutwa na bangi kilo 2,843 na gramu 78 huku watuhumiwa 269 walikutwa na cocaine kilo tatu na gramu 255 na heroine kilo moja na gramu 654.

‘’Watuhumiwa 5,627 walikutwa na pombe haramu ya gongo lita 8,547 na mitambo 34 na tuliwafikisha mahakamani. Pia tumekamata wahamiaji haramu 105 kutoka mataifa mbalimbali ambao hawana kibali cha kuingia na kuishi nchini,’’ alisema Sirro.

Katika hatua nyingine, Sirro alisema kuwa jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watu wanne wakiwa na gari moja aina ya Noah lenye namba za usajili T 188 CZN rangi nyeupe ambalo liliibwa mkoani Kilimanjaro.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Erasto Edward (36), mkazi wa Kawawa Moshi, Wilson Kapori (37) mkazi wa Njia Panda Himo mkoani Kilimanjaro, Hussein Issah (32) mkazi wa Chanika na David Marwa mkazi wa Pugu Kajiungeni.

Watuhumiwa hao walikamatwa Desemba 21 mwaka huu, saa 5 asubuhi katika misako maeneo ya Tabata Bima. Watuhumiwa walitumia ufunguo bandia kuiba gari hiyo.

Rose Ndauka: Sina mahusiano ya kimapenzi na MC Pilipili

0
0
Baada ya kuenea uvumi katika mitandao ya kijamii kuwa mchekeshaji MC Pilipili anatoka kimapeniz na Rose Ndauka, muigizaji huyo amekanusha uvumi huo.

Wiki chache zilizopita kupitia kipindi cha The Play List cha Times FM mchekeshaji huyo alidaiwa kukiri kutoka kimapenzi na muigizaji huyo.

Jana ijumaa muigizaji huyo amescreenshot ujumbe wa mtangazaji wa The Play List, Lilommy ambao ulidai huwenda wawili hao wakawa wanatoka kimapenzi na kuandaika

 “Jamaniii naomba niweke ili swala sawa sawa, mimi na MC Pilipili ni watu tunaofahamiana haswa kwenye kazi hatuna uhusiano wowote wa kimapenzi. NADHANI NTAKUWA NIMEELEWEKA”

Basi la National Express lapata ajali Singida....Wawili Wafariki, 26 Wajeruhiwa

0
0
Watu wawili wamefariki dunia na wengine 26 kujeruhiwa kwenye ajali iliyohusisha basi la kampuni ya National Express T.662 DEF, baada ya kuacha barabara na kupinduka zaidi ya mara tatu katika eneo la kijiji cha Tumuli, wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

Waliofariki ni dereva wa basi hilo Athumani Idd (47) mkazi wa Mabibo jijini Dares Salaam na mwalimu wa shule ya msingi Malunga aliyefahamika kwa jina moja la Janet (anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 29).

Habari zilizopatikana jana eneo la tukio, zimedai kuwa katika siku za hivi karibuni mwalimu Janet alimpeleka mama yake jijini Dar es salaam kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Imedaiwa kuwa baada ya kufika Dar es Salaam, aligundua kuwa amesahau kuchukua kadi ya bima ya afya, na hivyo akalazimika kurudi Iramba.

Jana asubuhi Janet alichelewa basi la National Express katika kituo cha Kyengenge na kuamua kukodi bodaboda kulifukuzia basi hilo na kufanikiwa kulikuta kituo cha Malunga. Baada kupanda basi hilo, dakika chake baadae, basi hilo lilipata ajali na kulaliwa na basi kichwani.

Watu hao wamefariki dunia papo hapo na miili yao ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida. Basi hilo lilikuwa linatokea New Kiomboi, likielekea jijini Dar.

Akizungumza kwenye eneo la tukio, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Singida , ACP Debora Daudi Magiligimba, alisema ajali hiyo imetokea Desemba, 30 saa 12.45 asubuhi katika eneo la kijiji cha Tumuli.

Alisema ajali hiyo pia imesababisha majeruhi 26 ambao wamelazwa katika hosipitali ya mkoa kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kamanda Magiligimba alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa ajali hiyo kwa kiwango kikubwa imesababishwa na mwendo kasi na uzembe.

“Eneo hili ilipotokea ajali hii kuna mteremko na kona kali. Kutokana na mwendo kasi, dereva alishindwa kulimudu na hivyo kuacha barabara na kuingia kwenye korogo la mto, na kuruka juu kisha kupinduka mara tatu,” alisema.

Kwa upande wake mganga mkuu mkoa wa Singida, Dk. John Mwombeki, alikiri kupokea miili ya watu wawili waliofariki dunia kwenye ajali ya basi la National Express, pamoja na majeruhi 26.

“Kati ya majeruhi hawa, mmoja dada Joyce tumempa rufaa kwenda hospitali ya taifa Muhimbili kutokana na sehemu yake ya mwili ya chini kutokufanya kazi. Majeruhi 10 wao tunaendelea kuwafanyia uchunguzi” alisema Dk. Mwombeki.

Mmoja wa majeruhi hao mfanyakazi wa shirika la TBC jijini Dar es Salaam, Victor Elia, alisema pamoja na kupoteza kila kitu, anamshukuru Mungu kwa kupona kufa kwenye ajali hiyo mbaya.

“Kilichonisaidia ni kufunga mkanda … abiria wenzangu wote ambao hawakufunga mikanda ndio walioumia zaidi wakiwemo waliopoteza maisha. Ajali hii kwa vyovyote imechangiwa na mwendo kasi,” alisema Victor ambaye ni mtayarishaji na mtangazaji wa TBC.

Kondakta wa basi hiyo, Nicolaus Apolinari (23) mkazi wa jijini Dar es Salaam, alisema ajali hiyo imechangiwa na utelezi uliosababishwa na mvua kubwa iliyonyesha katika eneo hilo.

Waziri wa Fedha na Mipango azungumzia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Julai – Disemba, 2016

0
0
Nashukuru kupata fursa ya kuzungumza nanyi  leo kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2016 na matarajio hadi Juni 2017. Nitajitahidi kutumia lugha rahisi ili wananchi wa kawaida waweze kuelewa mambo ya msingi kuhusu mwenendo wa uchumi wa nchi yetu.

Ustawi wa Uchumi Unapimwaje?
Ustawi wa uchumi wa Taifa unapimwa kwa kuangalia viashiria mbalimbali. Kwa kifupi, ustawi wa uchumi unapimwa kwa kuangalia kama shughuli mbalimbali za kiuchumi zinaongezeka au zinapungua au kama zimedumaa.
 
Shughuli  muhimu zinazoangaliwa ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi; uzalishaji wa bidhaa za viwandani na migodini; ujenzi wa miundombinu; uwekezaji; mwenendo wa bei, biashara na masoko; utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji, mawasiliano, usafiri na usafirishaji, utalii na huduma za kifedha; na kiwango cha utekelezaji wa bajeti ya Serikali.
 
Aidha, uchambuzi na tathmini ya hali ya uchumi wa Taifa inafanyika kwa kulinganisha viashiria na malengo yaliyowekwa au kwa kuangalia vigezo vinavyokubalika kimataifa au kwa kulinganisha na mwenendo wa viashiria vya kiuchumi katika nchi nyingine. Vilevile, afya ya uchumi inapimwa kwa kutumia vigezo vya jumla, vya kisekta na kimaeneo.
  • VIASHIRIA MBALIMBALI VYA MWENENDO WA UCHUMI WA TAIFA
    1. Ukuaji wa Pato la Taifa
Ukuaji wa uchumi (kasi ya kuongezeka au kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa na huduma katika nchi) ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa Taifa. Kiashiria kinachotumika kupima ukuaji wa uchumi ni ukuaji wa Pato la Taifa yaani thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa katika nchi katika kipindi kinachorejewa ikilinganishwa na kipindi kilichopita. 

Takwimu za ukuaji uchumi zinaonesha kuwa uchumi wa Taifa umeendelea kukua na Tanzania imebaki kuwa miongoni mwa nchi za bara la Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ambazo uchumi wake unakua kwa kasi kubwa zaidi. Mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa baadhi ya nchi jirani na kisekta umeoneshwa katika jedwali la 1 na la 2.
 
Jedwali1: Ukuaji wa Pato la Taifa Katika Baadhi ya Nchi za Kiafrika
NCHI2015  2016
Burundi-4.0-0.5
Kenya5.66.0
Rwanda6.96.0
Tanzania7.07.2
Uganda4.84.9
Zambia3.03.0
Malawi2.92.7
Congo DRC6.93.9
Afrika Kusini mwa Sahara3.41.4
    1. Mfumuko wa bei
Kiashiria kingine cha jumla ni mfumuko wa bei ambao unapima mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma zinazotumiwa na kaya nchini. Mfumuko wa bei ulipungua kutoka asilimia 6.5 Januari 2016 hadi asilimia 5.5 Juni 2016 na kupungua zaidi hadi asilimia 4.5 Septemba 2016 na baadaye kupanda kidogo mwezi Novemba na kufikia asilimia 4.8. Maana yake ni kuwa bei za bidhaa na huduma ziliongezeka kwa kasi ndogo zaidi ikilinganishwa na kipindi cha nyuma.
 
Mwenendo huu wa kushuka mfumuko ulichangiwa na kasi ndogo ya ongezeko la bei za chakula nchini, kushuka kwa bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia, utekelezaji madhubuti wa sera za bajeti na fedha, na utulivu wa thamani ya Shilingi. Kupanda kwa mfumuko wa Bei mwezi Novemba kulitokana na kupungua kwa upatikanaji wa bidhaa za chakula (mbogamboga, unga wa mahindi na ngano) pamoja na mkaa.
 
Mfumuko wa bei katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki: Wastani wa mfumuko wa bei uliendelea kubakia katika wigo wa tarakimu moja. 

Hata hivyo, mwezi Novemba 2016, karibu nchi zote zilikuwa na ongezeko la mfumuko wa bei kutokana na kuyumba kwa ugavi wa chakula katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na kupanda kwa bei za mafuta katika soko la dunia. 

Nchini Uganda, mfumuko wa bei uliongezeka kufikia asilimia 4.6 Novemba 2016 ikilinganishwa na asilimia 4.1 Oktoba 2016. Aidha, mfumuko wa bei nchini Kenya ulipanda na kuwa asilimia 6.68 ikilinganishwa na asilimia 6.47 katika kipindi hicho.
 
Matarajio kwa mwaka 2017 ni kubaki na mfumuko wa bei katika kiwango cha tarakimu moja. Hata hivyo upungufu wa mavuno ya mazao ya chakula uliojitokeza kwa baadhi ya nchi za ukanda wa kusini mwa Afrika unaweza kusababisha shinikizo la mfumuko wa bei katika siku za usoni.
    1. Thamani ya shilingi
Thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Kimarekani imeendelea kuimarika. Shilingi imekuwa ikibadilishwa kwa kati shilingi 2,167 hadi 2,199 kwa dola moja ya Marekani.
 
Hali hii ilitokana na kuwa sera thabiti za uchumi pamoja na mwenendo mzuri wa urari wa mapato ya fedha za kigeni hususan kutokana na mauzo ya bidhaa za viwandani, utalii na huduma mbalimbali.
    1. Mwenendo wa Sekta ya Kibenki
Tathmini ya hali ya mabenki yetu inaonesha kuwa mabenki yetu ni imara na salama, yakiwa na mitaji na ukwasi wa kutosha:
 
Kiwango cha mitaji kikilinganishwa na mali iliyowekezwa (total capital to total risk weighted assets and off-balance sheet exposures) kilikuwa asilimia 18.68 kikilinganishwa na kiwango cha chini kinachotakiwa kisheria cha asilimia 12.0.
 
Hali ya ukwasi hupimwa kwa kuangalia uwiano kati ya mali inayoweza kubadilishwa kuwa fedha taslimu na amana zinazoweza kuhitajika katika muda mfupi (liquid assets to demand liabilities). Uwiano huu ulikuwa asilimia 37.46 ukilinganishwa na uwiano wa chini unaohitajika kisheria wa asilimia 20.
 
Amana za wateja katika mabenki zilipungua kidogo kutoka shilingi trilioni 20.73 mwezi Desemba 2015 kufikia shilingi trilioni 20.57 mwezi Septemba 2016. Miongoni mwa sababu zilizochangia kupungua kwa amana kwenye mabenki ni pamoja na uamuzi wa Serikali kuhamisha sehemu ya fedha za taasisi na mashirika ya umma kutoka mabenki ya biashara kwenda Benki Kuu ya Tanzania. Hata hivyo amana za serikali kwenye mabenki ya biashara ni asilimia 3 tu ya amana zote za mabenki.
 
Upatikanaji wa huduma za kifedha kwa wananchi wasiofikiwa na mabenki umeendelea kuongezeka kutokana na ubunifu wa mipango ya utoaji wa huduma za malipo ya rejareja kupitia simu za mikononi, pamoja na huduma za uwakala wa mabenki (agent banking services).
 
Benki zilizopata msukosuko: Katika kipindi cha Julai – Septemba 2016, CRDB na TIB Development Bank zilipata hasara. Hasara ilisababishwa na tengo kwa ajili ya mikopo chechefu (provision for loan losses). Aidha, Twiga Bancorp imewekwa chini ya uangalizi wa BOT, jambo ambalo si geni. Crane Bank Ltd ya Uganda imewekwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu ya nchi hiyo Oktoba 2016 kama ilivyokuwa Imperial Bank Kenya, Oktoba 2015. 

Licha ya hali hiyo, benki nyingi zikiwamo CRDB na TIB Development Bank, zimebaki kuwa na mitaji na ukwasi wa kutosha kwa mujibu wa Sheria. Aidha ni vema kukumbuka kwamba jumla ya benki na taasisi za fedha nchini kote ni 66 na zina matawi 783. Hivyo, kwa benki tatu (3) tu kupata msukosuko katika robo moja ya mwaka si sababu ya kuzua taharuki!
 
Mwenendo wa mabenki katika nchi nyingine Afrika: Kupungua kwa mikopo kwa sekta binafsi katika miezi ya hivi karibuni siyo kwa Tanzania pekee. kwa mfano kiwango cha ukuaji cha ukuaji wa mikopo kwenda sekta binafsi katika nchi jirani ya Kenya kilipungua kutoka asilimia 19.7 kati ya Julai na Oktoba 2015 hadi kufikia asilimia 4.1 katika kipindi kama hicho katika mwaka huu 2016. 

Aidha huko Uganda mikopo kwa sekta binafsi ilipungua kutoka asilimia 25.2 mwezi September 2015 hadi asilimia -1 mwezi September 2016. 

Pia mwenendo usioridhisha ulijitokeza katika mikopo chechefu katika nchi hizo jirani na kusababisha baadhi ya mabenki hususan Crane Bank ya Uganda na Imperial Bank ya Kenya, kuwekwa chini ya uangalizi. Hali ni mbaya zaidi kwa nchi kama Nigeria na Ghana zinazouza mafuta.
 
Ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ulikua kwa asilimia 4.5 katika kipindi cha mwaka ulioishia Oktoba 2016 (au ongezeko la shilingi bilioni 547.3) ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 16.6 (au ongezeko la shilingi bilioni  3,084.6) kwa mwaka ulioishia Oktoba 2015. Ukuaji mdogo unatokana na usimamizi madhubuti wa matumizi sambamba na kupungua kwa fedha za misaada na mikopo kutoka nje.
 
Kwa upande wa mikopo kwa shughuli za biashara na za binafsi ilikuwa asilimia 39 ya mikopo yote. Mikopo kwa sekta binafsi iliongezeka kwa shilingi bilioni 1,550.5 hadi shilingi bilioni 16,654.4 katika mwaka unaoishia Oktoba 2016, sawa na ukuaji wa asilimia 10.3 ikilinganishwa ongezeko la shilingi bilioni 2,977.6 au ukuaji wa asilimia 24.6 katika kipindi kinachoishia Oktoba 2015. 

Katika kipindi cha Julai – Oktoba 2016 mwenendo wa riba za amana na za mikopo umekuwa wa kupanda na kushuka. Wastani wa riba za amana ulikuwa asilimia 9.49 ukilinganisha na wastani wa asilimia 9.08 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. Aidha, wastani wa jumla wa riba za mikopo ulikuwa asilimia 15.85 ikilinganishwa na asilimia 16.11 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. 

Mwenendo wa riba za mikopo unategemea mambo mbalimbali kama vile, gharama ya fedha (cost of funds), gharama za uendeshaji wa benki husika (bank’s operational cost), kiwango cha faida (profit margin), mfumuko wa bei na vihatarishi vinavyotokana na sifa za mkopaji (risk premium). Viwango vya riba katika masoko ya fedha vimeendelea kutegemea nguvu ya soko na hali ya ukwasi unaotokana na sera za fedha na kibajeti.
    1. Sekta ya Nje na Akiba ya Fedha za Kigeni
Hadi kufikia Novemba 2016, nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, huduma na uhamishaji mali nchi za nje (current account deficit) ilipungua kwa asilimia 52.5 na kufikia nakisi ya dola za Kimarekani milioni 1,904.2, kutoka nakisi ya dola za Kimarekani milioni 4,008.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2015. 

Kupungua huko kulitokana na ongezeko la thamani ya madini hususan dhahabu, bidhaa asilia, mapato yatokanayo na utalii, pamoja na kupungua kwa thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ya nchi hususan bidhaa za mitaji, na bidhaa za matumizi ya kawaida. Katika kipindi hicho thamani ya bidhaa na huduma zilizouzwa nje ya nchi ziliongezeka kwa asilimia 6.4 na kufikia dola za Kimarekani milioni 8,502.8 wakati thamani ya bidhaa na huduma toka nje zilipungua kwa asilimia 15.4 na kufikia dola za Kimarekani milioni 9,846.0.
 
Hadi mwezi November 2016, akiba ya fedha za kigeni ilifikia dola za Kimarekani milioni 4,254.1 ambazo zinatosheleza kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa takriban miezi 4. Wakati huo huo, rasilimali za fedha za kigeni za mabenki (gross foreign assets) zilikuwa kiasi cha dola za Kimarekani milioni 777.0 Hivyo, akiba ya fedha za kigeni imeendelea kuwa ya kuridhisha.
 
Jedwali 2: Viashiria vya Ustawi wa Uchumi
ENEOKIASHIRIAJUL – SEPT 2015OCT – DES 2015JUL – SEPT 2016OCT – DES 20162016
Ukuaji wa UchumiUkuaji wa Pato la Taifa6.3%9.1%6.2%8.0%7.2%
Sekta zenye mchango mkubwa  ktk Pato la TaifaKilimo (35.8%); Ujenzi (12.4%); Biashara (9.7%)Kilimo (28.3%); Ujenzi (11.0%); Biashara (10.7%); Viwanda (6.3%)Kilimo (24.7%); Ujenzi (14.6%); Biashara (10.3%); Viwanda (7.3%); Madini (5.2%)

Sekta zilizokua harakaUjenzi (17.6%); Usafirishaji & Uhifadhi (10.6%); Mawasiliano (9.1%); Huduma za kifedha (8.4%); Madini (8.0%)Madini (15.750; Ujenzi (13.8%); Huduma za kifedha (12.6%); Mawasiliano (10.2%); Viwanda (9.5%)Madini (19.9%); Mawasiliano (14.3%); Usafirishaji (12.2%); Nishati (11.8%); Huduma za kifedha (8.7%);

Sekta zilizokua polepoleKilimo (2.7%);
Kilimo (0.3%)

Bei, Biashara na MasokoMfumuko wa bei5.3%6.6%Jul (5.1%)Ago (4.9%) Sep (4.5%Okt (4.5%),Nov (4.8%)5.5%
Nakisi kwenye Biashara ya Nje (US$ Milioni)




Mwenendo wa Sekta ya FedhaAkiba ya fedha za Kigeni (US$ milioni)3,999.34,093.74,096.04,254.14,654.2
Kiwango cha Kubadilisha Fedha (Tshs; 1US$)2,150.02,148.52,175.322,170.97
Uwiano wa mikopo na Amana za wateja katika mabenki77.1678.88%71.16%

uwiano wa jumla ya   mitaji na mali iliyowekezwa (Total capital/Total risk weighted assets)Sept (18.68%)19.4% (Des)Sept (18.68%)
12%
uwiano wa raslimali inayoweza kubadilishwa kirahisi kuwa fedha taslim na amana zinazohitajika katika muda mfupi (Liquid assets/Demand liabilities)Sept (37.46%)Des (37.18%)Sept (37.46%)
20%
Riba za Mikopo ya mwaka mmojaSept (14.4%)Okkt (14.27%)Sept (13.4%)Okt (13.23%)
Riba za amana za mwaka mmojaSept (10.6%)Okt (10.95%)Sept (11.5%)Okt (11.46%)
Amana za watejaSept (Tshs19.892 trillion)Okt (Tshs19.995 trillion)Sept (Tshs20.73 trillion)Okt (Tshs20.98 trillion)
Mikopo chechefuSept (6.62)Des (6.64)Sept (8.26)

  • MWENENDO WA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI 2016/17
    1. Mwenendo wa Mapato
Katika mwaka wa fedha 2016/17 Serikali ilipanga kukusanya na kutumia shilingi bilioni 29.539.6.  Katika kipindi cha miezi mitano ya kwanza ya mwaka 2016/17, makusanyo ya ndani ikijumuisha mapato ya Halmashauri yalifikia shilingi bilioni 7,018.7 sawa na asilimia 96.4 ya makadirio ya shilingi bilioni 7,281.2 katika kipindi hicho
 
Mapato ya kodi
Mapato ya kodi yalifikia shilingi bilioni 5,674.7 ikiwa ni asilimia 96.6 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 5,873.3 kwa kipindi hicho. Aina za kodi zilizofanya vizuri ni pamoja na kodi ya Ongezeko la thamani ndani, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa nje. 

Hii ilitokana na usimamizi thabiti wa makusanyo kwenye malimbikizo ya kodi, ukaguzi na uchunguzi wa marejesho ya kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT returns) na kodi ya mapato uliofanyika katika kipindi hicho, kupanua wigo wa kodi kwa kusajili walipa kodi wapya, pamoja na utekelezaji wa mikakati ya kuongeza makusanyo ya kodi.
 
Mapato yasiyotokana na kodi
Mapato yasiyotokana na kodi yalifikia shilingi bilioni 1,133.4 sawa na asilimia 0.2 zaidi ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 1,130.6. Sababu za kuvuka lengo ni kutokana na kuongezeka kwa mapato yasiyo ya kodi yanayokusanywa na TRA ikijumuisha kodi ya majengo pamoja na kufanya vizuri kwa Wizara na Mikoa zinazokusanya maduhuli.
  1. Aina za kodi ambazo hazikufikia lengo
Aidha, aina za kodi ambazo hazikufikia lengo ni pamoja na ushuru wa bidhaa ndani, kodi  ya Ongezeko la Thamani (VAT) nje, kodi ya mapato  na kodi nyingine hasa ushuru wa stamp (stamp duty) na Departure fee.
 
Sababu zilizopelekea kutokufikiwa kwa malengo la ukusanyaji wa mapato ya kodi:
  1. Kushuka kwa mauzo ya bidhaa mbalimbali kama vile saruji, bia, vinywaji baridi na bidhaa nyinginezo za jumla na rejareja kumesababisha makampuni mengi kutopata faida ilivyotarajiwa na hivyo kupunguza wigo wa ukusanyaji wa kodi;
  2. Mabenki makubwa yalifanya marekebisho ya makisio yao ya kulipa kodi kutokana na kushuka kwa mapato ya riba;
  3. Kupungua kwa uchimbaji wa madini, mafuta na gesi asilia ambako kuliathiri kodi ya zuio na kodi ya mapato;
  4. Ajira kutoongeza kama ilivyotarajiwa baada ya kusitisha ajira mya ili kupisha zoezi la kubaini watumishi hewa serikalini;
  5. Baadhi ya kampuni kupunguza bei katika baadhi ya bidhaa kama vile bia ili kuongeza mauzo yao;
  6. Kuongezeka kwa malimbikizo ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kwenye sekta ya uzalishaji wa umeme hususan IPTL na Symbion Power Ltd;
  7. Matumizi hafifu ya mashine za kielektroniki (EFD);
  8. Kupunguza kwa ulaji wa bidhaa zinazotozwa kodi na ushuru wa bidhaa husuan bia, vinywaji vikali na vinywaji baridi;
  9. Matatizo ya kifedha yaliyokumba kampuni za usafirishaji wa anga pamoja na kupungua kwa idadi ya wasafiri hususan wa sekta ya umma (departure charges); na
  10. Kushuka kwa uingizaji wa bidhaa kutoka nje.
Hatua za kuimarisha ukusanyaji wa kodi ili kufikia malengo katika kipindi kilichobaki cha mwaka 2016/17:
  1. Kupanua wigo wa kodi kwa kuendelea kusajili na kuhakiki taarifa za walipakodi kwenye mifumo ya kikodi ya TRA;
  2. Kuendelea kushirikiana na Taasisi nyingine za ndani na nje ya nchi kwa kubadilishana taarifa;
  3. Kuendelea kusimamia na kuhamasisha matumizi sahihi ya mashine za kielektroniki za kutolea risiti (EFDs);
  4. Kudhibiti udanganyifu katika ukadiriaji wa kodi kwa kuendelea kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa walipakodi;
  5. Kuimarisha ukaguzi wa kodi (tax audit);
  6. Kudhibiti na kusimamia bidhaa zinazopitia hapa nchini kwenda nchi jirani (transit) kwa kutumia mfumo wa kufuatilia mizigo (electronic cargo trackin system);
  7. Kuboresha ukaguzi wa mizigo bandarini; na
  8. Kudhibiti biashara ya magendo hususan katika Bahari ya Hindi, mipaka na njia zisizo rasmi kati ya nchi yetu na nchi jirani.
  9. Misaada na Mikopo Yenye Masharti Nafuu
Katika mwaka 2016/17 Washirika wa Maendeleo waliahidi kuchangia bajeti ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 3,600.8, ambapo kati ya hizo, misaada ya Kibajeti ni shilingi bilioni 483.0, Mifuko ya Kisekta ni shilingi bilioni 372.1 na miradi ya Maendeleo ni shilingi bilioni 2,745.7. Jumla ya misaada na mikopo nafuu iliyotolewa kwa kipindi cha Julai hadi Novemba 2016 ni shilingi bilioni 603.9 sawa na asilimia 21.5 ya lengo la shilingi bilioni 2,806.3 katika kipindi hicho.
 
Misaada: Kati ya Julai hadi Novemba 30, 2016, misaada ya kiasi cha shilingi bilioni 287.5 ilitolewa, sawa na asilimia 28.4 ya lengo la shilingi bilioni 1,012.6 kwa kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho, misaada ya kibajeti (General Budget Support) ni shilingi billioni 36.1 ambazo zote zimetolewa na EU tu;  na kiasi kilichopokelewa kwa ajili ya mifuko ya kisekta (Basket Funds) ni shilingi bilioni 58.4, sawa na asilimia 61 ya lengo ya shilingi bilioni 95.5 kwa kipindi hiki cha marejeo.  Aidha, misaada kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa kipindi hicho ilifikia shilingi bilioni 193.1, ambayo ni asilimia 21 ya lengo la shilingi bilioni 917.1 kilichotarajiwa kupokewa kwa kipindi hicho.
 
Mikopo nafuu iliyopokelewa kutoka kwa washirika wa maendeleo kwa ajili ya miradi ya maendeleo kati ya Julai hadi Novemba, 2016 ni shilingi bilioni 316.4. Kiasi hiki ni sawa na asilimia 17.6 ya lengo la shilingi bilioni 1,793.7. Aidha, katika kipindi hicho, hakuna mikopo nafuu iliyopokelewa kwa ajili ya mifuko ya kisekta na programu (GBS).
 
Sababu za kutofikiwa malengo ya upatikanaji wa misaada na mikopo nafuu ni pamoja na masharti magumu yaliyowekwa na wahisani/wakopeshaji. Hata hivyo, Serikali inatarajia kukamilisha majadiliano na AfDB kati ya mwezi Desemba 2016 hadi Machi, 2017. 

Aidha, majadiliano na Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya, bado yanaendelea. Kuhusu fedha za miradi, jitihada zinafanyika katika sekta husika kukamilisha taarifa za miradi zinazohitajika na wafadhili.
 
Mikopo ya ndani
Katika kipindi cha Julai – Oktoba 2016, shilingi bilioni 1,367.2 zilikopwa katika soko la ndani. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 1,305.7 zilikopwa kwa ajili ya kulipia dhamana na hatifungani za Serikali zilizoiva na shilingi bilioni 61.5 zilikuwa ni  malipo ya marejesho (repayment). Kiasi kilichokopwa katika kipindi hiki ni sawa na asilimia 58 ya kiasi kilichopaswa kukopwa cha shilingi bilioni 2,232.5.
 
Mikopo ya Kibiashara
Katika mwaka 2016/17, Serikali ilipanga kukopa fedha kutoka kwenye vyanzo vya   kibiashara   kiasi   cha   Dola   za   Kimarekani   milioni   936   sawa   na   shilingi bilioni 2,100.9 ili kugharimia miradi mbalimbali ya maendeleo. Hata hivyo, hadi kufkia Novemba, 2016 Serikali haikukopa kutoka katika chanzo hiki kutokana na hali ya soko la fedha la kimataifa kutokuwa nzuri hasa katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2016/17.
 
Hali hii ilisababishwa na mdodoro wa kiuchumi katika bara la Ulaya na hivyo kuongezeka kwa gharama za mikopo mipya na kuathiri upatikanaji wake. Mfano, riba ilipanda kutoka wastani wa asilimia 6 hadi asilimia 9. 

Kutokana na sababu hiyo, Serikali iliahirisha kuendelea na mchakato wa kukopa kutoka kwenye masoko hayo na badala yake ikajielekeza kukopa kutoka nchi nyingine (China, India, Korea Kusini, Japan). 

Aidha, gharama za ukopaji katika masoko ya ulaya imeanza kuimarika na hivyo Serikali   imeanza majadiliano na Benki ya Credit Suissuie ya Uingereza ili tuweze kukopa   dola   za   kimarekani   milioni   300. Vilevile majadiliano na taasisi   nyingine   za   fedha kama  Kuwait Fund, Abu Dhabi Fund na OPEC  yameendelea kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali.
 
Mwenendo wa Matumizi
Sera za Bajeti ya Serikali kwa mwaka 2016/17, zililenga kusimamia nidhamu ya matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu pamoja na miongozo mbalimbali. Lengo kuu ni kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuziba mianya ya uvujaji wa fedha za umma na kuelekeza kiasi kikubwa cha fedha kwenye miradi ya maendeleo.
 
Fedha zilizotolewa  Julai – Novemba, 2016
Katika kipindi cha Julai – Novemba, 2016 jumla ya Shilingi bilioni 9,481.260 zilitolewa na Hazina kwa Wizara, Idara Zinazojitegemea, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa.
  • Shilingi bilioni 7,295.455 zilizotolewa kwa ajili ya matumizi ya Kawaida (ikijumuisha makusanyo ya Halmashauri Shilingi 61.047)
  • Mishahara ya Watumishi wa Serikali Shilingi 2,834.695,
  • Deni la Taifa Shilingi bilioni 3,552.249
  • Matumizi Mengineyo Shilingi bilioni 928.511
  • Shilingi bilioni 2,185.805 kwa ajili ya Matumizi ya Maendeleo (ikijumuisha makusanyo ya Halmashauri shilingi bilioni 91.571)
  • Fedha za ndani Shilingi bilioni 1,749.047
  • Fedha za nje Shilingi bilioni 436.758
  1. Maeneo ya Msingi ambayo fedha zimeelekezwa
Matumizi ya kawaida yaliyopewa kipaumbele zaidi katika utoaji wa fedha kwa kipindi cha Julai – Novemba 2016 ni pamoja na:
  • Uboreshaji wa huduma za afya katika ngazi zote ikiwemo ununuzi wa dawa na vifaa tiba Shilingi bilioni 69.346;
  • Mitihani ya darasa la nne na saba Shilingi bilioni 33.745;
  • Mitihani ya kidato cha pili na nne Shilingi bilioni 31.051;
  • Posho ya chakula kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama;
  • Chakula cha wafungwa Shilingi bilioni 7.5;
  • Mishahara ya watumishi wa Serikali;
  • Elimu msingi bila malipo Shilingi bilioni 93.885 (kwa kutenga shilingi bilioni 18.777 kila mwezi);
  • Malipo ya posho na stahili mbalimbali kwa maafisa katika balozi zetu nje shilingi bilioni 23.127;
  • Ruzuku ya pembejeo shilingi bilioni 10.00;
  • Ununuzi wa chakula cha Hifadhi ya Taifa shilingi biliioni 9.00.
  • Deni la kuchapisha Vitabu vya Hati za Kusafiria Shilingi 2.569;
  • Uendeshaji wa vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge, Mkutano wa Bunge, Posho ya Jimbo kwa Wabunge pamoja na shughuli za Mfuko wa Bunge Shilingi bilioni 31,137;
  • Michango ya Taasisi na Jumuiya za Kimataifa Shilingi billion 8.833;
  • Ruzuku ya Vyama vya Siasa Shilingi bilioni 7.168;
Aidha, sehemu iliyosalia ya fedha za Matumizi ya Kawaida ilielekezwa kwenye shughuli za kila siku za uendeshaji katika Mafungu mbalimbali.
Matumizi ya Maendeleo yaliyopewa kipaumbele kwa kipindi cha miezi mitano ni pamoja na:
  • Ununuzi wa ndege mbili za Serikali Shilingi bilioni 103.386 na malipo ya awali ya ununuzi wa ndege 4 shilingi bilioni 91.533;
  • Usambazaji wa umeme vijijini Shilingi bilioni 266.493;
  • Ujenzi na ukarabati wa barabara Shilingi bilioni 335.931;
  • Usambazaji wa maji vijijini na mijini Shilingi bilioni 65.2445;
  • Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Shilingi bilioni 210.758;
  • Mfuko wa Reli Shilingi bilioni 42.404;
  • Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Dodoma na Mwanza Shilingi bilioni 12.353;
  • Ujenzi wa majengo ya utawala katika Wilaya mpya na Mamlaka za Serikali za Mitaa Shilingi bilioni 11.00;
  • Ujenzi na ukarabati wa ofisi za Halmashauri Shilingi bilioni  30.10;
  • Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo Tanzania bara Shilingi bilioni 9.0; na
  • Uboreshaji wa miundombinu ya shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum Shilingi bilioni 2.5.
  1. Ulipaji wa Madai mbalimbali
Katika kipindi cha Julai – Novemba, 2016 madai yaliyohakikiwa ya jumla ya Shilingi bilioni 318.556 yalilipwa, ambapo shilingi bilioni 183.714 ni kwa ajili ya Wakandarasi na Wahandisi Washauri wa miradi ya barabara; Shilingi bilioni 42.951 kwa ajili ya ujenzi wa miradi ya maji; Shilingi bilioni 30.00 kwa ajili ya mikataba ya ulinzi na usalama; Shilingi bilioni 25.00 kwa ajili ya miradi ya umeme; Shilingi bilioni 15.439 kwa ajili ya wazabuni mbalimbali; shilingi bilioni 10.00 kwa ajili ya madai ya watumishi; Shilingi bilioni 7.00 kwa ajili ya matibabu nje ya nchi (Hospitali ya Apollo, India); Shilingi bilioni 3.150 kwa ajili ya Mtaalam Mwelekezi wa mipango miji ya jiji la Arusha na Mwanza; na shilingi bilioni 1.302  kwa ajili ya ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali.
 
Deni la Taifa
Deni la Taifa limeendelea kuongezeka na kufikia dola za Kimarekani milioni 21,087.9 mwishoni mwa mwezi October 2016, kutoka dola za Kimarekani milioni 19,861.1 mwezi Desemba 2015.
 
Deni la nje liliongezeka kwa asilimia 3.4 na kufikia dola za Kimarekani milioni 16,407.6 mwezi October 2016 (sawa na asilimia 77.8 ya deni la taifa), kutoka dola za Kimarekani milioni 15,863.9 mwezi Desemba 2015. Hii ilitokana na kuongezeka kwa mikopo mipya pamoja na malimbikizo ya malipo ya madeni. Katika deni hilo la nje, asilimia 83.0 ni deni la Serikali na taasisi za umma.
 
Deni la ndani liliongezeka kufikia shilingi bilioni 10,089.3 mwishoni mwa mwezi Octoba 2016 kutoka shilingi bilioni 8,597.0 mwezi Desemba 2015. Ongezeko hilo lilitokana na Serikali kukopa kupitia dhamana na hati fungani kwa ajili ya kugharamia bajeti ya Serikali kwa mwaka 2015/16, ikichangiwa pia na kupungua kwa misaada na mikopo kutoka nje.
 
Deni la Taifa ni himilivu: Pamoja na kuongezeka huko, deni la Taifa bado ni himilivu. Uchambuzi wa Uhimilivu wa Deni uliofanyika mwezi Novemba 2016 unaonesha kuwa viashiria vya deni la nje na deni lote la umma viataendelea kuwa chini ya ukomo wa uhimilivu katika kipindi cha muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Uchambuzi unaonesha kuwa viashiria vyote vitaendelea kuwa chini ya ukomo wa kimataifa hivyo deni la Taifa ni himilivu.
 
Changamoto
Pamoja na mafanikio hayo, changamoto kadhaa zilijitokeza zikiwemo:-
  1. Baadhi ya wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla kutokuwa na mwamko wa matumizi ya mashine za kielektroniki;
  2. Ukusanyaji usioridhisha wa maduhuli ya Serikali;
  3. Kushindwa au kuchelewa kupatikana kwa mikopo yenye masharti nafuu na ya kibiashara kutoka nje;
  4. Maombi ya misamaha ya kodi; na
  5. Mahitaji makubwa (yasiyowiana na hali halisi ya upatikanaji wa mapato) ya kuboresha miundombinu hususan ya maji, reli, bandari, viwanja vya ndege na barabara;
  • MAENEO YANAYOLALAMIKIWA NA BAADHI YA MAGAZETI NA KWENYE MITANDAO
4.1 Kupungua kwa Ukwasi Kufuatia Uamuzi wa Serikali Kuzitaka Taasisi za Umma Kufungua Akaunti za Mapato Benki Kuu
 
Uamuzi wa Serikali kuzitaka taasisi za umma kufungua akaunti ya mapato Benki Kuu utaendelea kubaki kama ulivyo. Kwa kifupi, fedha hizi za umma zilikuwa zinatumika vibaya na Bodi za mashirika lakini pia zilitumika kuikopesha Serikali fedha zake yenyewe kwa riba kubwa kupitia biashara ya dhamana na hati fungani za Serikali. Kasoro hiyo iliondoa motisha kwa mabenki ya biashara kupeleka huduma za kifedha vijijini na hata kukopesha sekta binafsi (crowding out credit to the private sector).
 
Aidha, ni vyema jamii ya Watanzania ikafahamu kwamba akaunti ambazo fedha za mashirika zimehamishiwa Benki Kuu ni akaunti za kukusanya mapato tu. Akaunti za matumizi bado ziko katika benki za biashara ili kuyawezesha mashirika kufanya malipo kupitia akaunti hizo. Hivyo, bado benki za biashara ni kiungo muhimu kati ya mashirika ya umma na watoa huduma kwa mashirika hayo. 

Hatua iliyochukuliwa na Serikali inalenga kuzisukumu benki za biashara kuchukua hatua za ziada kupanua huduma za kifedha hadi vijijini badala ya kujikita mijini zaidi kuhudumia makampuni makubwa (corporate sector) na kufanya biashara katika soko la dhamana na hati fungani za Serikali.
 
4.2 Mkikimkiki wa Ukusanyaji Kodi umekimbiza Wapangaji wa Majengo Marefu na Kusababisha Biashara Nyingi Kufungwa
 
Taarifa kutoka Mfuko wa Pensheni wa PPF zinaonesha kuwa kati ya majengo 15 inayomiliki sehemu mbalimbali nchini, mtiririko wa wastani wa wapangaji uko kama ifuatavyo:
  1. Majengo saba (7) yana wapangaji kwa asilimia 100 hadi kufikia Desemba 14, 2016;
  2. Jengo moja (DICC – PPF Tower) kwa sasa halipangishwi bali linaendeshwa na PPF wenyewe kama ukumbi wa mikutano;
  3. Jengo moja (PPF Plaza – Arusha) ni jipya na idadi ya wapangaji imeshaanza kuongezeka kutoka asilimia 34 mwezi Machi 2016 lilipofunguliwa hadi asilimia 39.1 Desemba 2016;
  4. PPF Kijitonyama ina nyumba nne (4) na kati ya hizo, mbili tu zenye wapangaji. Hatua za kutafuta wapangaji zinaendelea;
  5. PPF Kaloleni Arusha ina nyumba 20 na mwenendo wa wapangaji ulikuwa ukipanda na kushuka  na katika kipindi kilichoishia Desemba 2016 umeongezeka kufikia asilimia 75 kutoka asilimia 65 mwezi Juni 2016;
  6. Majengo manne yaliyobaki (PPF Tower and Parking Arcade, PPF Plaza Mwanza, PPF House na PPF Olerien Estate) idadi ya wapangaji ilipungua na kufikia wastani wa asilimia 78.5 kwa yote katika kipindi kilichoishia Desemba 2016 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 84.8 Juni 2016.
Aidha, taarifa kutoka PSPF zinaonesha kuwa katika majengo manne (4) inayomiliki imeweza kukodisha jumla ya futi za mraba 58,119.33 katika kipindi kilichoishia Juni 2016 ikilinganishwa na futi za mraba 57,883.5 zilizokodishwa hadi Juni 2015, sawa na ongezeko la asilimia 0.4. 

Katika kipindi hicho kilichoishia Juni 2016, eneo lililokodishwa katika majengo ya Jubilee na PSPF Plaza lilipungua kwa asilimia 4.7 na 2.7 kwa mtiririko huo wakati ambapo katika majengo ya HIP na Ubungo Plaza kulikuwa na ongezeko la eneo lililopangishwa kwa asilimia 20.9 na 1.3 mtawalia.
 
Ni dhahiri kuwa, kwa ujumla, kumekuwa na ongezeko la ushindani katika sekta ya nyumba na majengo kufuatia kuongezeka kwa ujenzi unaofanywa na mashirika na taasisi mbalimbali za umma na binafsi. 

Hali hii ilipelekea baadhi ya wamiliki wa majengo hayo kubuni mbinu mbalimbali za kibiashara ikiwa ni pamoja na kubadili matumizi ya majengo hayo na pia kuweka viwango vya kodi ya pango vinavyoendana na hali halisi ya soko. Kwa kuzingatia takwimu za hapo juu ni wazi kuwa madai kwamba mkikimkiki wa ukusanyaji kodi ndiyo umekimbiza wapangaji hayana mashiko.
 
Madai ya biashara nyingi kufungwa: Kwa upande wa madai ya biashara nyingi kufungwa katika siku za karibuni, tumefuatilia na kwa kiasi fulani kuna ukweli. Imebainika kwamba kasi ya wafanyabiashara kufunga biashara zao imeongezeka kati ya mwezi Agosti na Oktoba 2016. Mfano Ilala 1,076, Kinondoni 443, Temeke 222 na Arusha 131. Aina ya biashara nyingi zilizofungwa ni katika sekta ya ujenzi na biashara ya jumla na rejareja, na chache katika huduma za usafiri.
 
Hata hivyo, sababu hasa zilizopelekea biashara hizo kufungwa hazijabainika kutokana na ugumu wa kupata taarifa kutoka kwa wenye biashara zilizofungwa.

Sababu za mtu kufunga biashara yake zinaweza kuwa nyingi, ikiwemo, kushindwa kuingiza bidhaa nchini bila kulipa kodi stahiki, kushindwa kulipa au kulipwa madeni, kubadilisha aina ya biashara, kushindwa kusimamia biashara, gharama kubwa za uendeshaji, wabia katika biashara kutoelewana au kutapeliana, kuibuka kwa washindani wa kibiashara wenye nguvu au huduma bora zaidi n.k.
 
4.3 VAT Imekimbiza Watalii
Takwimu rasmi kuhusu wageni walioingia nchini katika mwaka 2016 kwa ujumla zinaonyesha kuwa idadi ya wageni imeongezeka ikilinganishwa na mwaka 2015 (Jedwali 4). Hivyo madai kuwa watalii wameikimbia Tanzania kwa sababu ya VAT kwenye baadhi ya huduma za utalii hayana msingi! Na kama nia ni kutolipa kodi na wakati huohuo Serikali inadaiwa fedha kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya utalii na huduma nyingine kwa wananchi, hilo halikubaliki! Nawaalika wadau wa sekta ya utalii waje wajenge hoja zenye mashiko wakati wa mapitio ya marekebisho ya kodi kwa ajili ya bajeti ya 2017/18.
 
Jedwali 4a: Idadi ya Wageni  walioingia Nchini 2015 – 2016
Mwezi20152016Badiliko %
Januari98,71099,7631
Februari88,93991,5193
March77,84193,09620
Robo ya Kwanza265,490284,3787
Aprili67,44776,67914
Mei81,53876,155-7
Juni90,23689,626-1
Robo ya Pili239,221242,4601
Julai91,896126,75538
Agosti142,885121,321-15
Septemba100,829121,27920
Robo ya Tatu335,610369,35510
Octoba84,121124,62348
Jedwali 4b: Idadi ya Wageni waliongia nchini kupitia njia mbalimbali ;
Januari – Septemba
KITUO20152016Badiliko %
JNIA238,423252,5245.91
KIA126,286137,0248.50
ZIA109,738139,28426.92
Namanga105,88381,073(23.43)
Kasumulo9,87112,00621.63
Sirari18,89924,39329.07
Zanz. Port31,99443,24235.16
Kabanga13,56516,75123.49
Manyovu17,76118,5504.44
  • MWELEKEO NA MATARAJIO HADI JUNI 2017
Kwa kuzingatia mwenendo wa ukuaji wa uchumi kwa kipindi cha Januari hadi September 2016, matarajio ni kwamba kasi ya ukuaji wa uchumi kwa mwaka 2016/17 unatarajiwa kufikia asilimia 7.2 kama ilivyokadiriwa awali.
Mfumuko wa bei unatarajiwa kuendelea kubaki kwenye tarakimu moja.
 
Thamani ya shilingi inategemea kuendelea kuimarika kutokana na hatua zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania.
Kwa upande wa mapato, Serikali inakusudia kufanya yafuatayo hususan katika kuongeza mapato ili kuweza kufikia lengo:
  1. Kusimamia dhana ya kulipa kodi kwa hiari kupitia udhibiti wa matumizi  ya  mfumo wa EFDs;
  2. Kuendelea kuboresha makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi hasa yale yanayotokana na michango ya mashirika na wakala za Serikali;
  3. Kuendelea na majadiliano baina ya serikali na wahisani ili kuhakikisha kwamba fedha za misaada na mikopo zinapatikana kama ilivyopangwa;
  4. Kuendelea kufanya uthamini wa mkupuo wa majengo ili kukusanya zaidi katika kodi ya majengo;
  5. Kuendelea kuboresha na kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na usimamizi wa maduhuli; na
  6. Kuendelea kutoa elimu juu ya umuhimu na faida za kulipa kodi kwa kutumia mitandao ya kielektroniki. Aidha, MDAs zinahimizwa kutumia mabenki katika kulipia maduhuli.
Aidha, Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kusimamia matumizi kama ifuatavyo:-
 
(i)     Kuendelea kusisitiza nidhamu katika utekelezaji wa bajeti kama         ilivyoidhinishwa kwa kuzingatia Sheria ya Bajeti ya mwaka             2015;
(ii)    Kuendelea kuwianisha mapato na matumizi kwa kuhakikisha         kuwa mgawo wa fedha utaendana na upatikanaji wa mapato; 
(iii)    Kupunguza matumizi yasiyo ya lazima kama kupunguza safari         za nje zisizo na tija, matumizi katika sherehe za kitaifa pamoja         na makongamano.
  • HITIMISHO
Ninapohitimisha maelezo yangu naomba kusisitiza yafuatayo:
 
Kwanza: napenda kuwahakikishia wafanyabiashara kuwa Serikali ya awamu ya Tano inathamini sana mchango wa Wafanyabiashara katika Maendeleo ya nchi yetu. Milango ya serikali ipo wazi kwa wale wote wenye hoja zenye maslahi kwa Taifa letu. 

Wizara ya Fedha na Mipango imekwisha toa tangazo kwa Watanzania na wadau wote wa kodi kuwasilisha mapendekezo ya marekebisho ya kodi kwa ajili ya uchambuzi na kufikiriwa kuingizwa katika mapendekezo ya mabadiliko ya kodi katika bajeti ijayo. Ninawaomba wadau wote kuitumia vizuri fursa hiyo ili tupate mapendekezo mazuri ya kuboresha mfumo wetu wa kodi na kutupatia mapato zaidi ya kuendeleza nchi yetu.
 
Pili: Napenda kutoa rai kwa Watanzania wenzangu kuhakikisha kuwa tunadai risiti za EFD kila tunaponunua bidhaa au huduma kama Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alivyokwisha kuagiza. Yeyote asiyetoa risiti na asiyedai risiti ajue anatenda kosa na anasaliti jitihada zetu za kuijenga Tanzania mpya.

 Aidha, ningependa kusisitiza kwa wale wote wenye mashine za EFD wazitumie ipasavyo kwa kila muamala wanaoufanya. Kuna tabia ambayo imezuka ya kusingizia kuwa mashine imeharibika au kutoa risiti ya EFD kwa mteja anayeidai tu. 

Wale wote wenye tabia hii wanahujumu maendeleo ya nchi yetu na ninawataka waache mara moja! Nimewaagiza TRA kufanya kaguzi za kushtukiza na kuwashughulikia ipasavyo wale wasiotaka kutii maelekezo ya Serikali kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
Napenda nisisitize kuwa Tanzania mpya ambayo wote tunaitamani iko mikononi mwetu! Lakini ili tufike huko lazima tufanye kazi kwelikweli – iwe ni kazi ya kuajiriwa au kujiajiri katika kilimo, uvuvi, ufugaji, biashara au huduma au kumiliki viwanda (vidogo, vya kati na vikubwa)!! 

Aidha, lazima kila mmoja wetu alipe kodi stahiki kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania yetu! Tuitikie wito wa Rais wetu kwa vitendo ambaye amedhamiria  kujenga Tanzania mpya ili kuwaondoa Watanzania kwenye lindi la umaskini haraka. Kulipa kodi ndiyo njia ya uhakika ya kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora zaidi (upatikanaji wa maji, elimu, afya, umeme, barabara, ulinzi & usalama) kwa wananchi wake. 

Uamuzi huu unahitaji kuachana na mazoea, kujitoa (sacrifice) na kufanya kazi kwa bidii, nidhamu na uadilifu. Tunataka uchumi ambao wananchi wengi wananufaika nao, uchumi ambao utajengwa kwa kufanya kazi siyo uchumi wa ujanja ujanja (mission town), kukwepa kodi au wizi wa mali na fedha za umma.
 
Tatu: Wanahabari kwa ujumla mnafanya kazi nzuri sana. Nawaomba mwendelee hivyo na hasa nikiwasihi mtumie weledi na mjielekeze kuwajuza Watanzania kuhusu mifano mizuri ya maendeleo hapa nchini na hata katika nchi nyingine lakini wakati huo huo mtangulize maslahi ya Taifa letu kwanza. 

Hata hivyo, yapo magazeti fulani ambayo consistently yanajielekeza kutoa taarifa za kupotosha na kuifanya jamii ihamaki! Nawaomba: Epukeni kuwa vipaaza sauti vya nyimbo za watu wachache wenye maslahi binafsi (wawe wanasiasa, wafanyabiashara, au wafanyakazi) waliozoea “upigaji”! Punguzeni uandishi wa kuuza magazeti (sensationalism) na uchambuzi wa mambo kijuujuu!  Pimeni taarifa mnazoziandika ili msiwanufaishe washindani wa nchi yetu kiuchumi (kibiashara au kiuwekezaji) au kuchafua sura nzuri ya Tanzania!!
 
Nimalizie kwa kuwahakikishia Watanzania wote kwamba madai  ya baadhi ya magazeti siku za karibuni kuwa uchumi wa Taifa una hali mbaya siyo ya kweli. Hata gazeti moja la leo limeandika kuwa “Ripoti ya Uchumi Yashtua”!! Ukweli ni kuwa kama Taifa tumeendelea kupiga hatua nzuri katika maeneo mengi ya uchumi japo yapo maeneo machache ambayo yana changamoto, na Serikali inaendelea kuyafuatilia kwa karibu ili kuyatafutia ufumbuzi. Afya ya uchumi wetu bado ni nzuri na inatarajiwa itaendelea kuwa ya kuridhisha katika mwaka ujao 2017.
 
NAWATAKIA WOTE HERI YA MWAKA MPYA 2017
UWE KWELI MWAKA WA HAPA KAZI TU!!
ASANTENI KWA KUNISIKILIZA

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 31

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images