Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Basata yaonya disko toto, maonesho machafu

$
0
0
BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), linalosimamia sanaa na burudani nchini, limeonya wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani, kuepuka kuruhusu disko toto na kujaza watu kwenye kumbi hizo.

Aidha, Baraza hilo pia limesisitiza kuwa halitafumbia macho ukumbi utakaokiuka maelekezo yake, ikiwa ni pamoja na kuruhusu maonesho machafu yenye kudhalilisha utu hasa yanayoonesha maungo ya ndani, kwa kuwa yameshapigwa marufuku.

Hayo yamo kwenye taarifa ya Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari, kwa lengo la  kuwatakia wasanii na wadau wote wa sanaa heri ya Krismasi na Mwaka mpya.

Huku ikisisitiza kauli mbihu yake kuwa ‘Sanaa ni kazi tuikuze, tuilinde na kuithamini’, Basata iliwataka wamiliki na waendeshaji wa kumbi za burudani, kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizo kwenye vibali vyao vya uendeshaji kumbi.

“Wanaelekezwa kuhakikisha wanakuwa na vibali halali vya uendeshaji wa kumbi zao, kuzingatia muda wa matumizi wa kumbi, kuepuka kelele zinazosumbua kwenye maeneo maalumu hasa makazi ya watu na kuhakikisha ulinzi na usalama wa maisha ya watu na mali zao,” ilieleza taarifa hiyo.

Basata pia iliwakumbusha wamiliki wa kumbi za sherehe na burudani, kuwa inakatazwa kukusanya watoto kwenye kumbi hizo kupitia ‘Disko Toto’ katika msimu huu wa Sikukuu za Krismasi na Mwaka mpya, ili kuepuka maafa yanayoweza kujitokeza.

“Uzoefu unaonesha, kwamba nyakati za sikukuu kama hizi wamiliki wa kumbi hujisahau na kuandaa madisko toto hali mbayo imekuwa ikisababisha maafa ambayo yangeepukika kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu.

“Aidha, baadhi ya wamiliki na waendeshaji kumbi wamekuwa wakijisahau na kuendekeza faida bila kujali maelekezo ya vibali vyao, wamekuwa wakijaza watu kupita viwango vya madaraja waliyopangiwa na Basata,” ilieleza taarifa hiyo na kuonya kuwa hatua kali na za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka maagizo hayo.

SORRY MADAM -Sehemu ya 5 & 6 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
“Nipe namba ya mumeo”
“Eehee”  
“Nipe namba ya mumeo, hujanisikia?”
Phidaya kwa uwoga akaichukua simi yake aliyo kua ameiweka pembeni ya glasi iliyo jaa juisi ya embe, vyote kwa pamoja vikiwa juu ya meza ya kioo iliyopo ndani ya kibanda hicho. Kwa kutetemeka Phidaya akaitafuta namba ya simu ya mumewe na kumuonyesha Mzee Godwin, ambaye taratibu akainadika kwenye simu yake na kuipiga namba hiyo.                                                                     

ENDELEA
“Mwanangu Phidaya”
Mzee Godwin alijibu kwa kujiamni, jambo lililo zidi kumchanganya Eddy ambaye mapigo ya moyo yakaanza kumuenda mbio, kwani uhasama wake na Mzee Godwin ni mkubwa kupita kiasi.
“Nakuomba usifanye chochote kwa mke wangu, nakuomba baba yangu”
“Mmmm leo ndio unajua kwamba mimi ni baba yako?”

Mzee Godwin aliendelea kuzungumza kwa dharau jambo lililo zidi kumpagawisha Eddy, kwani umbali kutoka Dododma hadi Dar es Salaam, unachukua muda mwingi sana kuweza kufika mbaya zaidi bado anakipengele cha kumalizia bungeni kuweza kujibu maswali atakayo ulizwa kama waziri wa ulinzi, ambaye amechukua majukumu ya kusimamia sekta zote za jeshi kuanzia polisi hadi jeshhi la kujenga taifa, na wizara ya mambo ya ndani ikatolewa katika usimamizi wa jeshi la polisi na kubaki ikiendelea kusimamia mabo mengi na si jeshi la polisi, ambalo lilihamishiwa kwenye wizara ya ulinzi moja kwa moja

“Leo, mke wangu atanipikia chakula kizuriii, kwahiyo usiwe na wasiwasi wowote, wewe endelea kupiga kazi”
Baada ya kuzungumza hivyo mzee Godwin akakata simu, na kuizima kabiasa kisha akamtazama Phidaya ambaye bado anaendelea kutetemeka mwili wake wote kwa woga mwingi ulio mtawala. Madam Mery akatoa kitambaa cheupe kilicho kunywa vizuri ambacho walikipulizia madawa ya kulevya kisha akamkabidhi mzee Godwin.

Mzee Godwin akamsogelea Phidaya sehemu alipo na kumziba na kitambaa hicho puani mwake, Phidaya akajitahidi kushindana nguvu na mkono wa mzee Godwin ulio mziba puani ila akajikuta akishindwa, huku nguvu zikianza kumuishia taratibu taratibu hadi akalala fofofo.

Mzee Godwin akambeba Phidaya begani na kuingia naye ndani, ambapo wakamlaza kwenye moja ya sofa kubwa walilo likuta hapo sebleni, kisha akaanza kuingia chumba kimoja baada ya kingine kuweza kutafuta funguo ya gari walizo  zikuta zimewekwa sehemu maalu za maegesho. Madam Mery yeye akawa na kazi ya kuchungulia madirishani ili kuweza kuona nje kama kuna mtu anaingia aweze kumstua mzee Godwin ambaye anaendelea kuwajibika na utafutaji wa funguo hizo.

Mngurumo wa gari, ukisimama nje, ukamstua Madama Mery aliye kuwa ameketi kwenye sofa, kila mara akitazama tazama saa yake ya mkononi, akihesabu muda jinsi unavyo kwenda. Akasimama kwa haraka na kwenda kuchungulia dirishani, akamuona mtoto mdogo wa kiume akishuka kwenye gari hilo aina ya BMW Z8, huku akiwa ameongozana na mtu anaye onekana kama ni dereva.

Kwa jinsi mototo huyo anavyo fanana na Eddy moja kwa moja Madam Mery akagundua kwamba huyo ni mtoto wa Eddy. Kwa haraka Madam Mery akapandisha ngazi za kuelekea gorofani, ambapo ndipo alipo Mzee Godwin. Kwa bahati nzuri akakutana na Mzee Godwin akitoka kwenye moja ya chumba akitaka kuelekea kwenye chumba kingine.

“Vipi?”
“Kuna watu wanakuja”
Madam Mery alizungumza huku akihema kwani, alizipandisha ngazi hizo zipatzo thelathini kwa kukimbia
“Kina nani?”
Mzee Godwin alizungumza huku akitembea kuelekea sehemu ambapo ataweza kuiona seble vizuri. Mzee Godwin akamshuhudia mjukuu wake Junio  akiingia huku nyuma akiwa ameongozana na dereva wa gari aliye mleta. Junio akamkimbilia mama yake aliye lala kwenye sofa na kumrukia kwa lengo la kumstua, ila hakufanikiwa kumstua mama yeka kwani hakuweza kustuka wala kutikisika, jambo lililo mpa wasiwasi mwingi Junio na kumfanya anze kulengwa lengwa namachozi.

  ***
    Eddy akajaribu kuipiga tena namba ya Mzee Godwin iliyo toka kumpigia muda mchache ulio pita ila haikupatiokana, wasiwasi mwingi ukazidi kumsumbua Eddy, akajaribu kupiga kwa mara ya pili ila hali ikawa ni ile ile ya kuto kupatikana kwa namba hiyo. Akajaribu kuipiga namba ya mke wake, ikaita pasipo kupokelewa.
“Mungu wangu?”
Eddy alizungumza huku akizunguka zunguka ndani ya chumba huku jasho jingi likimwagika mwilini mwake, na kujikuta akifungua vifungo vyote vya shati lake. Eddy akafungua mlango na kuanza kutembea kwenye kordo ndefu, ya hoteli aliyo fikizia akielekea sehemu  ya mapokezi, kabla hajafika akakutana na askari wake anaye mlinda
“Vipi muheshimiwa”
“Nahitaji kwenda, Dar sasa hivi”
Eddy alizungumza kwa haraka huku akizidi kupiga hatua kuelekea nje ya hotel hiyo kwenda kwenye maegesho ya magari.

“Unakwenda kufanya nini muheshimiwa?”
“Mke wangu ametekwa, fanya hivi mpigie simu naibu waziri, mkabidhi mafaili yangu yote na kipindi cha pili yeye ndio atajibu maswali sawa”
“Sawa mkuu”
Eddy akafika kwenye gari lake, na kumkuta dereva akiwa amejilaza.
“Shuka nipishe niendeshe”
Eddy alizungumza na kumfanya dereva wake kustuka kutoka usingizini
“Mmmmm”
“Hujanisikia au, nimekuambia kwamba zunguka upende wapili wa gari, tunahitaji kwenda Dar es Salaam sasa hivi”
“Muheshimiwa ni jukumu langu mimi kukuendesha”
“Wewe mzee, mimi ni nani yako? Nimekuambia nipishe”
Eddy alizungumza kwa hasira na kumfanya mzee Selemani Mbogo, kutii amri ya bosi wake, akashuka kwa haraka na kuzunguka upende wapili wa gari, askari akataka kuingia kwenye gari ila Eddy akamzuia
“Wewe baki, hakikisha document zangu zote unampa naibu waziri sawa?”
“Sawa mkuu”
“Naomba bastola yako”

Hapo askari akasita kidogo kuichomoa bastola yake aliyo ichomeka kiunoni mwake, kwa ishara Waziri Eddy akamuomba amkabidhi bastola hiyo, taratibu askari huyo akaichomoa na kumpa bosi wake. Eddy akaipokea na kuifunga mlango wa gari, akaliwasha, akakanyaga mafuta pamoja na breki na kuzifanya tairi za gari hilo kuserereka, na kutoa moshi mwingi, kisha akaachia breki na kulifanya gari hilo kuchoka kwa kasi, na kuwafanya watu wlaiopo katika eneo la hoteli kushangaa.

Waziri wa Habari, Nape Nnauye atuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha mpigapicha Mpoki Bukuku kilichotea Disemba, 23.

Rais Magufuli awasili mkoani Singida kusherehekea Sikukuu ya Krismasi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 24 Desemba, 2016 amewasili mkoani Singida na kupokelewa na mkuu wa Mkoa wa huo  Dkt. Rehema Nchimbi na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Singida.

Rais Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, leo  tarehe 25 Desemba 2016 wanatarajia kuungana na waumini wengine wa dini ya Kikristo nchini  katika ibada ya Sikukuu ya Krismasi mkoani Singida.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewaomba waumini wa dini ya kikristo mkoani Singida kujitokeza kwa wingi  kuungana na Rais Magufuli katika ibada ya Krismasi kwani imekuwa ni heshima kwao kutokana na uwepo wa  Rais Mkoani hapa kwa ajili ya sikukuu ya Krimass.

Dkt. Nchimbi amewataka wananchi wa mkoa wa Singida na Tanzania kwa ujumla kuendelea kumuombea Rais Magufuli na familia yake ili aendelee kuwatumikia watanzania katika kuwaletea maendeleo.

Amesema ni bahati kubwa kwa mkoa wa Singida kwa mara nyingine tena kumpokea Kiongozi huyo Mkuu wa nchi kwa kuwa katika kipindi kifupi mkoa huo pia ulimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa alipohudhuria sherehe za Maulidi.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Singida
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaini Kitabu cha Wageni mara baada ya kuwasili mkoani Singida na kupokelewa na Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi akielezea ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mkoani humo ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki katika Ibada ya Siku ya Krismasi katika Kanisa mojawapo mkoani Singida.

Waliotafuna Fedha za TASAF Waanza Kusakwa........Zaidi ya Watu 80 Simiyu Wakamatwa na Kutupwa Selo

$
0
0
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, imeanza msako wa kuwatembelea walengwa wanaonufaika na Mfuko wa Jamii (TASAF) Awamu ya Tatu.

Zaidi ya watu 80 wamekamatwa na kufikishwa mahabusu ya Kituo cha Polisi Bariadi kwa kudaiwa kufisadi fedha hizo.

Akizungumzia hilo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jana, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Abdallah Malela alisema kuwa jumla ya kaya 80 katika halmashauri hiyo, zinatafutwa ili zirejeshe fedha zote.

Alisema imebainika kuwa kaya 80 ziliingizwa katika mradi wa TASAF III kwa njia za kinyemela na kuchukua Sh milioni 17.8.

“Ni kweli kuna msako huo, jumla ya kaya 80 hazikustahili kuwemo katika mpango huu, tulifanya ukaguzi mpya baada ya maelekezo kutoka Serikali Kuu kututaka kupitia upya walengwa, kama wanakidhi vigezo vya kuwemo kwenye mpango,” alieleza Malela. Alisema kaya hizo zilibainika kutokuwa na vigezo.

Ziliandikiwa barua tangu Agosti mwaka huu, kutaka warejeshe fedha zote za miezi sita zilizotolewa kwao. Alieleza kuwa baada ya kupatiwa barua hizo, hakuna kaya hata moja ambayo imeanza kurejesha fedha hizo.

Hali hiyo imesababisha kuwepo kwa msako huo wa nguvu. Alisisitiza kuwa wahusika hawatapewa dhamana mpaka warejeshe fedha zote.

“ Watu ambao tumewakamata hawapewi dhamana mpaka warejeshe fedha za serikali. Mpaka leo tumefanikiwa kurejeshewa kiasi cha Shilingi milioni 1.1 kati ya milioni 17.8,” alieleza Malela.

Alisema msako huo utaendelea kwa halmashauri nzima mpaka pesa zote zirejeshwe, ili kuweza kutumika kwa walengwa ambao walikusudiwa katika mpango huo.

“ Leo ni siku ya tatu tunahangaika kupata dhamana, mama yetu amekamatwa, wamesema ili kupata dhamana mpaka arejeshe kiasi chote ambacho amepokea. Tangu aanze kuchukua fedha za TASAF anadaiwa shilingi 240,000,” alisema mmoja wa mtoto wa mnufaika, ambaye hakutaka kutaja majina yake.

Mwenyekiti wa mtaa ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kuwa wao kama viongozi wa mtaa waliletewa barua kutoka TASAF wilaya, yenye majina ya watu ambao walikuwa kwenye mpango huo na wanatakiwa kurejesha fedha zote kutokana na kutokidhi vigezo.

“ Nilipokea barua ikiwa na majina ya watu wanaotakiwa kurejesha fedha zote walizochukua toka waanze kupokea, wanasema wao hawakustahili kuwemo katika mpango huo, wengi wanadaiwa zaidi ya shilingi 200,000” alisema Mwenyekiti huyo.

Waziri Mkuu Majaliwa Atinga Gereza la Ukonga .......TBA kujenga nyumba 320, askari wafungwa kufyatua matofali

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea gereza la Ukonga jijini Dar es Salaam na kukagua eneo la ujenzi wa makazi ya askari wa Magereza unaotarajiwa kuanza baada ya wiki tatu zijazo.

Akizungumza na askari wa magereza kabla ya kufanya ukaguzi huo jana Jumamosi, Desemba 24, 2016 Waziri Mkuu alisema ziara aliyoifanya , ni ufuatiliaji wa maagizo ya Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli aliyoitoa wakati alipoenda kukagua gereza hilo.

Novemba 29, mwaka huu, Rais Magufuli alifanya ziara kwenye gereza hilo na kupokea taarifa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari wa jeshi hilo zipatazo 9,500 na akaagiza zitafutwe sh. bilioni 10 haraka ili kupunguza tatizo hilo.


Akizungumzia kuhusu ujenzi huo, Waziri Mkuu alisema amefarijika kukuta Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wako eneo la kazi na wameanza kusafisha eneo hilo.


“Nimefarijika kukuta TBA wako kazini na nimeelezwa hatua inayofuata ni upimaji wa sampuli za udongo kabla hawajaanza kujenga msingi. Nawapongeza TBA kwa kazi nzuri wanazofanya za ujenzi wa nyumba zenye viwango na kwa haraka kama tulivyoona kule Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na nyumba za Magomeni Kota,” alisema.


Waziri Mkuu alisema Serikali inatambua mchango uliofanywa na Serikali ya awamu ya nne katika suala la makazi ya askari kama vile wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) na Jeshi la Polisi. 


“Nia ya Serikali ni kuhakikisha makamanda wote wanapata nyumba nzuri ili waendelee kufanya kazi zao kwa weledi mkubwa wakiwa na uhakika familia zao zimetulia kwenye makazi bora”.

Alisema katika ziara alizozifanya kwenye mikoa mbalimbali, alitembelea magereza ya Isanga, Msalato (Dodoma), Lindi, Singida na Keko (Dar es Salaam) alikuta nyumba za askari hazina viwango na kama zipo zimechakaa sana.


Mapema, akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa nyumba hizo, Kaimu Kamishna Jenerali wa Magereza, Juma Malewa alisema wanamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapatia fedha za ujenzi wa makazi ya askari na kwamba jeshi hilo litafanya kazi zote zisizo za kitaalamu ili kuokoa fedha za Serikali na badala ya kulipwa watu binafsi, fedha hizo zitatumika kuongeza nyumba zaidi.


“Tumekubaliana na TBA kazi zote zisizohitaji utalaamu kama kufyatua matofali, kubeba mizigo au kufyeka zitafanywa na askari wetu pamoja na wafungwa ili tuokoe gharama zote hizo na badala ya kulipa watu binafsi, fedha hizo zitumike kujenga nyumba nyingine 80,” alisema huku akishangiliwa.


Alisema wamejipanga kufanya kazi hizo kwa saa 24 kila siku ili kuokoa muda ambao TBA walikuwa wameuweka wa kukamilisha ujenzi ndani ya miezi minane.


Alisema wako tayari kuanzisha kambi za ujenzi kwa kutumia wafungwa na askari ili wafanye kazi zisizohitaji utaalamu na fedha zitakazopatikana, badala ya kuwalipa watu binafsi zitumike kujenga nyumba zaidi za askari.


Naye mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TBA, Bw. Baltazar Kimangano alisema wanataraji kuanza ujenzi ndani ya wiki tatu baada ya kupokea matokeo ya uchunguzi wa sampuli za udongo kutoka taasisi ya BICO ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.



Alisema wanataraji kujenga majengo (block) manne ya ghorofa sita kila moja ambayo kwa ujumla yatakuwa na nyumba 240 zenye ukubwa wa vyumba viwili vya kulala. Pia watajenga majengo (block) mengine mawili ya ghorofa sita kila moja ambayo yatakuwa na nyumba 80 zenye ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Magereza wakati alipowasili kwenye gereza la Ukonga jijini Dar es salaam kukagua maadlizi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza Desemba 24, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea heshima kutoka kwa gwaride lililoandaliwa na Jeshi la Magereza wakati alipowasili kwenye gereza la Ukonga jijini Dar es salaam kukagua maadlizi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya Askari Magereza Desemba 24, 2016.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipokwenda kwenye Gereza la Ukonga kukagua maandalizi ya ujenzi wa nyumba za makazi ya askari Magereza Desemba 24, 2016.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua maadalizi ya eneo la ujezi wa nyumba za askari magereza katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Desemba 24, 2016. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhandisi Hamad Masauni na kushoto kwake ni Kaimu Kamishina Jenerali wa Magereza, Dkt. Juma Ali Malewa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Magereza baada ya kukagua maandalizi ya eneo zitakapojengwa nyumba za makazi za Askari magereza katika gereza la Ukonga jijini Dar es salaam Desemba 24, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
 
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Majambazi Yavamia Mgodi na Kuua Watu Wawili

$
0
0
WATU wawili wamekufa huku wengine wanne wakijeruhiwa baada ya majambazi walio na silaha kuvamia mgodi wa dhahabu wa Nholi uliopo wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.

Majambazi hao wanadaiwa kupora dhahabu, fedha na mali nyingine na kuwavua watu nguo na kuondoka nazo.

Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk Charles Kiologwe alikiri kupokelewa kwa miili ya watu wawili hospitalini hapo na majeruhi wanne.

Alisema mwili mmoja upo katika hali mbaya. Waliofariki dunia katika tukio hilo, walitajwa kuwa ni Lukumale Membo na mwingine aliyefahamika kwa jina moja la Hamisi.

Kwa mujibu wa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, Melisiana Danford, maiti hao na majeruhi walipokelewa hospitalini hapo saa 6 usiku kuamkia jana mara tu baada ya kutokea kwa tukio hilo. Majeruhi katika tukio hilo ni Sunday Undi (49), Lawrence Mhagama (35) , Maila Mchele (44) na Sophia Sayuni (37).

Wakizungumza katika wodi namba moja ambako wamelazwa, majeruhi hao walisema walivamiwa na majambazi, ambao baadaye waliwapiga risasi na kusababisha vifo vya watu wawili na wengine kujeruhiwa.

Lawrence Mhagama ambaye amepigwa risasi mguu wa kushoto, alisema amekuwa akiendesha shughuli za uchimbaji mdogo kwenye mgodi huo. Alisema siku ya tukio majira ya saa mbili usiku akiwa ndani, alisikia milio ya risasi nje na alipojaribu kutoka, alipigwa risasi ambayo ilimjeruhi mguuni.

“Chanzo cha tukio kwa kweli sikijui ila majambazi walituvamia , mimi ni mgeni eneo hilo nilikwenda kwa ajili ya kazi ya mgodi, nimepigwa risasi mguuni ambapo mpaka sasa bado ninayo mwilini, wanasema wataniruhusu nikipata nafuu na baadaye wataangalia uwezekano wa kuitoa risasi hiyo,” alisema.

Alisema majambazi hao, walipora mali nyingi ambapo waliwavua watu nguo na kuondoka nazo huku wakiacha watu uchi.

Majeruhi mwingine aliyelazwa wodi namba moja, Sunday Undi, alisema walivamiwa na majambazi hao majira ya saa mbili kasorobo usiku wa kuamkia juzi, wakiwa kwenye kioski cha Maila Mchele, wakipata vinywaji na kuendelea na mazungumzo.

“Tulivamiwa tukasikia tunaambiwa tuko chini ya ulinzi, kwa vile lilikuwa ni tukio la kushtukiza tukawa tunashangaa, wakapiga risasi juu ikabidi tuingie ndani ya kibanda kile baada ya muda tukajikuta watu saba tukiwa chini ya kitanda,” alisema.

Alisema majambazi hao waliwaamrisha watoke na kuwaambia kila mtu atoe alichonacho na aliyekuwa akikataa, aliamriwa kuvua nguo.

“Walininyang’anya fedha na simu, wakatuvua na suruali wakaondoka nazo, mimi binafsi wamenipora Shilingi milioni mbili nilizokuwa nazo,” alisema.

Alisema majambazi hao walikuwa zaidi ya wanne na walikuwa wamevalia kininja. Alisema mtu aliyejaribu kuwatazama usoni, alikuwa akipigwa risasi. Majeruhi mwingine katika tukio hilo, Maila Mchele ambaye amelazwa wodi hiyo akiwa hajitambui, amejeruhiwa vibaya.

Inadaiwa alipigwa risasi tumboni na kutokea upande wa pili. Majeruhi wa nne, Sophia Sayuni (37) amelazwa wodi namba 10 hospitalini hapo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alipohojiwa kuhusu tukio hilo, alisema atalitolea ufafanuzi baadaye.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Disemba 25


Picha za Rais Magufuli na mkewe walivyoshiriki ibada ya Krismasi mkoani Singida

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli, leo tarehe 25 Desemba, 2016 wameungana na waumini wa Jimbo Katoliki la Singida kusali Misa ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Moyo Mtakatatifu wa Yesu Mjini Singida.Misa hiyo Takatifu ya Krismasi imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Singida Mhashamu Edward Mapunda.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa Misa Takatifu, Mhe. Rais Magufuli amewatakia heri ya Krismasi waumini wote wa Jimbo la Singida na Watanzania wote kwa ujumla na amewasihi kusherehekea kuzaliwa kwa Bwana Yesu kwa kuendeleza amani na upendo na kuacha vitendo vya kubaguana kwa misingi ya dini, kabila, itikadi na kanda zao.

Dkt. Magufuli amewahimiza Watanzania wote kuongeza juhudi katika kuchapa kazi kama alivyofanya Bwana Yesu na pia amesema kwa kuwa maeneo mengi ya nchi yameonekana kukabiliwa na uhaba wa mvua, ni vema wakatumia vizuri mvua chache zinazoendelea kunyesha kuzalisha mazao yanayokomaa haraka ili kuepuka upungufu wa chakula.

Kwa upande wa Mkoa wa Singida ambao ni maarufu kwa kilimo cha alizeti, Mhe. Rais Magufuli amewasisitiza kuchangamkia fursa ya ujenzi wa viwanda ambayo nchi inatoa kipaumbele kwa kuzalisha alizeti kwa wingi ili zitumike kuzalisha mafuta ya kupikia kwa wingi.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Singida
25 Desemba, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Disemba 26

Picha 15: Vodacom Wasafi Festival Ilivyofanyika Dec 25 Mkoani Iringa

$
0
0
Usiku wa Dec 25, 2016  wakali wa Bongo Fleva akiwemo Diamond Platnumz, Harmonize, Rayvanny, Queen Darleen, Q Boy, Chege pamoja na msanii kutoka Nigeria Kcee wameandika historia katika mkoa wa Iringa.

Show hiyo iliyopewa jina la Vodacom Wasafi Festival imefanyika katika uwanja wa Samora Stadium, hizi ni baadhi ya picha kutoka mahali palipofanyika tamasha hilo.

Tazama Hapa Video Mpya ya Wizkid iitwayo ‘Daddy Yo’

$
0
0
Mwimbaji staa wa Nigeria ambae alikua mgeni mualikwa wa FIESTA 2016 Mwanza na kwenye tamasha la Mombasa Rocks Music Festival 2016 ametoa video  nyingine kutoka kwenye maktaba yake

 Itazame apo  chini

Michezo: Haji Manara Amuombea Msamaha Jerry Muro Kwa Rais Wa TFF

$
0
0
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba Haji Sunday Manara amejitokeza kwa mara ya kwanza kumuombea msamaha mtani wake Jerry Muro ili kuifufua upya hamasa na kuongeza ushindani katika ulimwengu wa soka la Bongo.

Jerry Muro ambaye ni Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Yanga amefungiwa na TFF kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na soka kutokana na matumizi mabaya ya kauli zake kupitia vyombo vya habari mwezi Julai mwaka huu.

Manara katika ujumbe aliouweka kwenye mtandao wake wa Instagram akiuelekeza kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi, amesema katika kuadhimisha sikukuu ya Krismasi anaona ni wakati muafaka sasa kwa Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia Jerry kwa kuwa amekwishatumikia takriban nusu ya kifungo chake na kwamba soka la Bongo linamuhitaji sana kwa sasa.

"Nimekaa nimetafakari sana,nimeamua kumuombea msamaha mtani wangu Jerry Muro ambaye TFF mlimfungia mwaka mmoja kujihusisha na mpira wa miguu, ninafanya hivi nikijua kabisa Jerry alikosea na tayari ameshatumikia karibia nusu ya kifungo chake, ninajua kwa kufanya hivyo atakuwa keshajifunza lugha za kutumia na pia itakuwa fundisho kwetu sisi wasemaji na viongozi wa vilabu kwa ujumla. "Ameandika Manara

Manara pia hakusita kukumbushia jinsi ambavyo Jerry Muro amewahi kumtolea hata yeye mwenye lugha za kuudhi "
Nnafahamu pia Jerry aliwahi kunitolea lugha zisizostahili mimi bnafsi, lakini yale yashapita na binafasi amenihakikishia kutorudia tena, na nnaamini viongozi na washabiki wa Simba watanielewa dhamira yangu hii njema, ambayo inathibitisha uungwana tulio nao wanasimba".

manara amemaliza kwa kusema kuwa soka la Tanzania linammis sana Jerry Muro na kuomuomba Rais Malinzi kutumia mamlaka yake kumfungulia kwa kuwa Jerry bado alikuwa hajawa na uzoefu wa kutosha katika siasa za mpira.

Kwa upande wake Jerry Muro amefurahi na kushukuru kuona mtani wake Haji Manara anamkumbuka na kutumia fursa hiyo kuomba msamaha kwa shirikisho la soka Tanzania ili aendeleze hamasa ya soka aliyokuwa ameiweka nchini yeye na Haji Manara.

Michezo: TFF Yasema Mechi ya Simba na Yanga iko palepale

$
0
0
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa mechi ya ligi kuu Tanzania Bara ya mzunguko wa pili kati ya Simba na Yanga iliyokuwa imepangwa kuchezwa Februari 18 mwaka 2017 iko palepale kwa kuwa bado halijafikiria kuibadili tarehe hiyo.

Hatua hiyo inatokana na tarehe hiyo kugongana na kalenda ya CAF ya michuano ya Klabu Bingwa Barani Afrika iliyotolewa hivi karibuni na kuipanga Yanga kucheza mchezo wa marudiano kati yake na Ngaya de Mbe ya Comoro kati ya tarehe 17, 18 na 19 mwezi Februari 2017.

Afisa Habari wa TFF Alfred Lucas amesema kuwa hadi sasa shirikisho hilo kupitia Bodi ya Ligi halijafikiria kufanya mabadiliko yoyote kwenye ratiba hiyo, na kwamba ratiba itaendelea kubaki kama ilivyo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo.

"Ratiba imeshapangwa na haitabadilika, kila timu inajua itacheza lini, kuhusu ratiba ya CAF haiwezi kutuzuia kufanya mashindano yetu, kama kuna timu inacheza CAF inatakiwa ijipange, kila timu inatakiwa kuwa tayari wakati wowote ndiyo maana zinafanya matayarisho, zinaajiri makocha, zinasajili wachezaji , hiyo yote ni matayarisho kwahiyo sidhani kama watahitaji kupumzika na kutuharibia ratiba" Amesema Lucas

Jumatatu iliyopita Mtendaji Mkuu wa Bodi ya ligi Boniface Wambura akiwa kwenye kipindi cha 5Sports cha EATV, alisisitiza kuwa katika mzunguko wa pili wa ligi, ratiba haitakuwa tatizo, na kwamba haitabadilishwa badilishwa kwa kuwa katika upangaji wake kila kitu kilizingatiwa ikiwemo kalenda ya CAF.

Michezo: Ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi inayotarajiwa kuanza Disemba 30

$
0
0
Pazia la Mashindano ya Kombe la Mapinduzi linatarajiwa kuanza kutimua vumbi lake Disemba 30, 2016 katika uwanja wa Amaan saa 2:15 Usiku ambapo kutakuwa na mchezo wa Derby ya Jangombe kati ya Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys ambapo mashindano ya msimu huu yameshirikisha vilabu 9, vitano vikitokea Zanzibar, vitatu Tanzania bara na kimoja kutaka Uganda ambao ndio mabingwa watetezi timu ya URA.
 
KUNDI A: Simba, URA, KVZ, Taifa ya Jangombe na Jangombe Boys.
 
KUNDI B: Yanga, Azam, Zimamoto na Jamhuri.
 
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP
30/12/2016 Taifa ya Jang’ombe vs Jang’ombe boys saa 2:30 usiku.
 
1/1/2017 KVZ VS URA Saa 10:00 alasiri, Simba vs Taifa ya Jang’ombe saa 2:30 usiku.
 
2/1/2017 Azam vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Jamhuri saa 2:30 usiku.
 
3/1/2017 Jang’ombe boys vs URA saa 10:00 alasiri, KVZ vs Simba saa 2:30 usiku.
 
4/1/2017 Zimamoto vs Yanga saa 10:00 alasiri, Jamhuri vs Azam saa 2:30 usiku.
 
5/1/2017 KVZ vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri, Simba vs URA saa 2:30 usiku.
 
6/1/2017 Taifa ya Jang’ombe vs KVZ saa 2:30 usiku.
 
7/1/2017 Jamhuri vs Zimamoto saa 10:00 alasiri, Yanga vs Azam saa 2:30 usiku.
 
8/1/2017 Simba vs Jang’ombe boys saa 10:00 alasiri ,Taifa ya jang’ombe vs URA 2:30 usiku.
 
10/1/2017 Saa 10: 00 nusu fainali ya kwanza , Saa 2:30 nusu fainali ya pili.
 
13/1/2017 Fainali saa 2: 30 usiku.

Rais Magufuli Atoboa Siri ya Kula Christmass Mkoani Singida

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania,Dk.John Pombe Magufuli,amefichua siri ya kusali Krismasi kwenye kanisa la Parokia ya Moyo wa Yesu, mjini Singida mwaka huu.

Ametaja siri hiyo kuwa wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita, aliwahi kusali kwenye kanisa hilo na wakati akitoka, alikutana na sista mmoja (hamkumbuki jina) ambaye alimzawadia rozali, na kumwahidi kuwa itamsadia kushinda uchaguzi huo.

Rais Magufuli ametoa siri hiyo jana  wakati akizungumza kwenye sherehe ya Krismasi iliyofanyika kwenye kanisa la Porokia ya Moyo wa Yesu, na kuhudhuriwa pia na mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli.

Akifafanua, alisema kuwa rozali hiyo amezunguka nayo kwenye kampeni yake, na mwisho wa siku, alifanikiwa kupata kura za kutosha na hivyo kuwa mshindi.

“Hiyo ndio sababu kubwa au siri ya mimi kufika mjini Singida, na kuungana na wakazi wa mkoa wa Singida na Watanzania kwa ujumla, kusherehekea kuzaliwa kwa Yesu kristo,” alisema na kusababisha mamia ya waumini kushangilia kwa nguvu.

Rais Magufuli alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania wote kutumia sikukuu hii ya Krismasi kuimarisha upendo, kuvumiliana na wala wasibaguane ,na kwa njia hiyo,Tanzania itaendelea kupaa kimaendeleo.

Katika hatua nyingine, alisema kuwa Watanzania na hususani wakulima, wahakikishe wanazitumia vizuri mvua zinazonyesha kwa sasa nchini kwa kuchapa kazi ya kilimo kwa nguvu zote na kulima mazao yanayostahimili ukame.

“Ndugu zangu waumini na Watanzania kwa ujumla, acheni kulialia kuwa fedha zimepotea … fedha hazijapotea isipokuwa ninyi wenyewe hamfanyi kazi. Vitabu vyote vya madhehebu ya dini vinasisitiza wajibu wa kuchapa kazi … na vinasema asiyefanya kazi na asile,” alisisitiza.

Akiijengea nguvu hoja yake ya hapa ni kazi tu, alisema kuwa Yesu kristo amezaliwa na fundi mchapa kazi kweli kweli seremala, na hivyo tunaposherehekea Krismasi Watanzania wote wenye uwezo wa kufanya kazi, wafanye kazi huku wakijua hakuna cha bure.

Aidha, Rais Magufuli, aliwataka wakazi wa mkoa wa Singida, kuongeza uzalishaji wa zao la alizeti, ili kukiwezesha kiwanda kikubwa cha kukamua mafuta ya alizeti cha Mount Meru kupata mbegu za kikudhi mahitaji ya kiwanda.

Awali askofu wa kanisa katoliki jimbo la Singida, Edward Mapunda, alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakazi wa mkoa wa Singida, kutunza mazingira, ili yaweze kuwatunza na wao.

Alisema hivi sasa hali ni mbaya kutokana na binadamu kuongeza kasi ya kuharibu mazingira, kitendo kinachochangia madhara mengi ikiwemo uhaba wa mvua.

“Mimi nashangaa sana, watu wanaendelea kuzaa huku wakiendelea kuharibu mazingira na kutishia nchi kuwa jangwa. Tuna zaa watoto waje wateseke kutokana na uharibifu wa mazingira. Kama tunaendelea kuharibu mazingira, ni vema tuache kuzaa”, alisema Mapunda.

'Yesu nipe nyonyo‘: Wimbo Ambao Kenya Inataka Uondolewe Mtandaoni Kwa Kudhalilisha Dini

$
0
0
Gazeti la Kenya liitwalo taifa leo limeripoti kwamba bodi ya filamu kwenye nchi hiyo imehuzunishwa na Msanii wa muziki wa Injili SBJ kuimba wimbo wa Injili ambao unadhalilisha Imani.

Wimbo wenyewe unaitwa ‘Yesu nipe nyonyo‘ ambapo mkuu wa bodi hiyo Ezekiel Mutua alisema baadhi ya Waimbaji wa Kenya wamekosa maadili na kipaji cha kubuni au kutunga nyimbo nzuri zisizochafua hali ya hewa.

Alisema wimbo huo unaendelea kukaguliwa kwa sababu Wakenya wamekasirishwa: "Nashangaa sana mtu mzima anakaa chini na kuimba wimbo kama huu, Wasanii wetu wamejua kuwa kama hawaongei uchafu ama kutoa video za utata hawatasikilizwa wala kutazamwa na wanafanya hivyo ili wapate umaarufu”

Tayari bodi hiyo ilikua kwenye mipango ya kuwaandikia Youtube ambao ndio wanamiliki wa mtandao huo ili waiondoe hiyo video kwasababu bodi hiyo inayo mamlaka na katiba haitakubali Wasanii kutunga nyimbo za kudhalilisha imani.

Mpaka sasa wimbo huo bado upo kwenye mtandao na umeshatazamwa mara 93,812 mpaka sasa.

SORRY MADAM -Sehemu ya 7 & 8 (Destination of my enemies)

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  
“Unanidai shilling ngap?”  
Mzee Godwin alizungumza huku akitoa pochi yake mfukoni, huku macho yake yote yakiwa kwa mama Eddy.
“Elfu hamsini”
Akachomoa noti tano za elfu kumi kumi, nakumkabidhi dereva bodaboda pasipo kumtazama, kisha akaanza kupiga hatua kuelekea alipo Mama Eddy, huku taratibu hasira kali dhidi ya mke wake huyu ikiongezeka na kujikuta akiichomoa bastola yake tayari kwa kumpiga risasi.

ENDELEA
    Mama Eddy baada ya kuzungumza na simu, akaingia ndani ya hospitali na kumfanya Mzee Godwin kusimama kwenye moja ta gari lililo egeshwa kwenye maeneo haya huku macho yake akimsindikiza mke wake huyo, ambaye alimshuhudia akizungumza na Eddy kisha wakaondoka
“Eddy Eddy Eddy”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwa amekasirika, tukio kubwa linalo muuliza kichani mwake ni pale anapovuta picha jinsi pacha mwenzake alivyo kuwa akifanya mapenzi na mke wake huyo, jambo linalomfanya kuzidi kumchukia Eddy

“Nitakuua kwa mkono wangu mimi mwenyewe”
Mzee Godwin alizungumza huku akiwashuhudia Eddy na mama yake wakitoka tena nje ya hospitali huku wakiwa na Junio, aliye bebwa mikononi mwa Eddy akionekana kupitiwa na usingizi. Gari la mama Eddy likafika sehemu walipo simama huku kukiwa na dereva ndani yake.

“Nitakuja basi asubuhi, kumuona mgonjwa. Ngoja nikamlaze huyu chekbud wako”
“Sawa mama, usisahau kuja na chakula”
“Sawa nitakiandaa mimi mwenyewe”
Mama Eddy akaingia siti ya nyuma alipo lazwa Junio aliye jichokea kwa usingizi.
“Mama kumbuka hajala huyo akifika ale”
Eddy alizungumza huku gari la mama yake likiondoka taratibu, Eddy akalisindikiza kwa macho gari hilo hadi linatoka kwenye geti, Macho ya Eddy yakashuhudia mtu akiwa amejibanza kwenye moja ya gari huku akionekana kama anachunguza kitu fulani, kutokana na mwanga hafifu ya eneo la maegesho hakuweza kumuona sura yake.
Eddy akataka kwenda ndani ila roho yake ikasita kabisa na kujikuta akianza kupiga hatua za taratibu kwenda sehemu lilipo gari hilo. Mzee Godwin akatabasamu, alipo kua anamuona Eddy akija katika eneo alipo jificha yeye. Akaishika bastola yake huku akimsubiria kwa hamu kubwa, Eddy afike ili amuulie mbali
Gafla simu ya Eddy ikaita na kumfanya asimame na kuitoa mfukoni mwake, na kukuta ni namba ya spika wa bunge, akaitazama kwa sekunde kadhaa, kisha akaipokea

“Ndio kiongozi habari”
Eddy akuzungumza huku akitazama pembeni upande ambapo hayupo mtu aliye hitaji kumuona ni nani na kwanini anajificha
“Salama vipi, mbona umekimbia bila taarifa?”
“Kuna matatizo yakifamilia ilinibidi niwahi kuyatatua”
“Kwema lakini?”
“Hapana si kwema kiongozi, kwani mke wangu alivamiwa na majambazi na kumuwekea sumu, pia nikakuta mwili mwengine wa rafiki wa karibu ukiwa ndani ya nyumba yangu, naye akiwa amepigwa risasi”
“Aisee, basi mimi nilijua kwamba umekimbia maswali”
“Hapana kiongozi”

“Pole sana, vipi polisi umewataarifu?”
“Bado, ila hili swala nitalimaliza kimya kimya”
“Basi kama ni hivyo, ila nikusifie kwa vidonge vyako vya leo, Umeniburudisha japo nilikuwa ninajikaza”
“Ni moja ya kazi yangu”
“Basi endelea na majukumu ukiwa saswa utaniambia”
“Sawa kiongozi”
Eddy akakata simu na kuzunguka sehemu alipo hisi kuna mtu, ila hakukuta mtu yoyote aliyepo kwenye eneo hilo. Kumbe kitendo cha Eddy kuzungumza na simu, ikawa ni nafasi kubwa sana kwa Mzee Godwin kutembea kwa hatua za haraka na kuingia kwenye jembo moja la kuhifadhia nguo, ikiwemo mashuka, neti, na mavazi ya kidaktari

“Kumbe huyu mwanamke hajafaa, nilazima nimuue”
Mzee Godwin alizungumza baada ya kumsikia Eddy akidai kwamba Madam Mery hajafa. Mzee Godwin akavaa moja ya koti la kidaktari akachukua na kipimo cha kupimia mapigo ya moyo, kisha kwa haraka akaanza kupita wodi moja baada ya nyingine ya wagonjwa mahututi

    Halikuwa ni jambo la kustukiwa mara moja kwamba yeye sio dokta, hii nikutokana na wingi wa wafanya kazi katika hospitali hii, huku wengine wakiwa wameingia zamu ya usiku wakiwapokeza wezao walio fanya kazi kutwa nzima. Eddy akapiga namba za Mzee Seleman aliye kuwa akisimamia ufanyiwaji wa oparesheni wa Madam Mery kutolewa risasi
“Ndio bosi”
“Hali ya mgonjwa inaendeleaje?”
Eddy alizungumza huku akiingia ndani, kuelekea kwenye chumba alicho lazwa mke wake
“Bado madaktari wanaendelea kuzitoa risasi, nipo kwa nje hapa ninachungulia kwenye kioo cha mlangi
“Sawa hakikisha haumruhusu mtu kuwa karibu ya mgonjwa zaidi ya madaktari, au nikuongezee nguvu ya ziada?”

“Hapana”
“Sawa fanya hivyo”
Eddy baada ya kumaliza kuzungumza na mzee Selemani Mbogo, simu yake ikazima chaji kabisa na kujikuta akiidumbukiza mfukoni mwake. Eddy akafika kwenye chumba alicholazwa Phidaya, akaingia na kukaa pembeni ya kitanda cha mke wake na kuanza kumtazama usoni mwake, na kuanza kufikiria ni kitu gani ambacho anaweza kumfanya Mzee Godwin pale atakapo mtia mikononi
“Sasa huyu mzee amevuka mipaka kwa sasa, nitamuua kimya kimya”
Eddy alizungumza kwa sauti ya chini kabisa huku akiendelea kumtaza mke wake kwa macho ya masikitiko. Taratibu akamshika mkono mke wake ambao haujachomwa sindano ya dripu, taratibu akaubusu kisha akakanyanyuka na kuanza kupiga hatua taratibu za kuelelea kwenye mlango

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 27

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Gharama Za Matibabu Ya Dawa Ya Sumu Ya Nyoka Nchini

$
0
0
Kama tunavyofahamu, nchi yetu ina aina mbalimbali za nyoka ambao pindi wakimuuma mtu huleta madhara mbalimbali ya kiafya. Aidha tunafahamu kwamba tatizo hili lipo zaidi katika maeneo ya vijijini ambako uwezo wa wananchi kumudu gharama za matibabu ni mdogo.

Dawa za kutibu sumu ya nyoka huagizwa kutoka nje ya nchi. Dawa hizo siyo tu hazipatikani kwa urahisi, bali pia zinapatikana kwa gharama kubwa. Bei ya kununulia dawa hizi ni kati ya dola za kimarekani 55 hadi 85 (yaani shilingi za kiTanzania 118,250 hadi 182,750) kwa kichupa kidogo (vial) kimoja. Kichupa hicho huweza kutumika kwa wagonjwa wanne, lakini mara tu baada ya kufunguliwa dawa hiyo huwa haifai tena kutumika ndani ya mwezi mmoja tu.
 
Pamoja na changamoto hizo, Serikali kupitia MSD kila mwaka huagiza dawa hizi kwa ajili ya mahitaji hayo ya kutibu wagonjwa walioumwa na nyoka, ambapo bei ya kuinunua kutoka MSD ni TZS 200,000/= kwa kichupa kimoja. Hospitali zetu mbalimbali zimekuwa zikiagiza dawa hizi kutoka MSD na kwa washitiri wengine kwa bei hii au zaidi na kuwatibu waathirika wanaohitaji dawa za sumu za nyoka mara zinapohitajika. 
 
Napenda kuwakumbusha kwamba kwa mujibu wa Sera ya Afya ya mwaka 2007, huduma za tiba hutolewa bure kwa makundi maalum, au kwa kuchangiwa kwa sehemu ya gharama, au kwa kupitia mfumo wa Bima mbalimbali za Afya kama vile CHF. Kwa wale wasio na uwezo na wanaothibitishwa kuwa hawana uwezo, utaratibu wa msamaha hutumika.
 
Katika kuhakikisha kwamba wananchi wanaohitaji dawa ya  sumu ya nyoka wanahudumiwa ipasavyo, Mhe. Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto anatoa maelekezo yafuatayo:-

Waganga Wakuu wa Mikoa na Viongozi wa Hospitali zote nchini wahakikishe kuwa Hospitali zote za umma zinaingiza dawa hii katika dawa za dharura ili iweze kununuliwa kama dawa zingine za dharura kupitia kifungu cha fedha za dawa za dharura.  
 
Kwa wagonjwa ambao watakuwa na Bima ya Afya, basi gharama za matibabu hayo zitalipwa kwa kupitia utaratibu huo wa Bima. Wananchi wanahimizwa kujiunga na Bima za Afya (CHF/NHIF) ili kupata unafuu wa matibabu haya na mengine. Mfano CHF - gharama ya kujiunga katika Halmashauri mbalimbali kwa kaya ni kati ya shilingi 5,000/= hadi shilingi 30,000/= kwa mwaka.
 
Kwa wagonjwa ambao watakuwa hawana Bima ya Afya, hao watatakiwa kuchangia gharama hiyo kwa nusu ya bei ya gharama ya dawa hizi au kwa kiwango kingine kitakachoamuliwa na Mganga Mkuu wa Serikali kadri itavyohitajika. 

Hii ni kutokana na ukweli kwamba kung'atwa na nyoka ni ajali na wananchi wengi wanaopatwa na ajali hii wapo maeneo ya vijijini ambao kimsingi uwezo wao wa kumudu gharama hizi kubwa za matibabu ya dawa ya sumu ya nyoka ni mdogo.
 
Wagonjwa watakaothibitika kuwa hawana fedha za kuchangia gharama hiyo, basi hospitali husika kwa kupitia mpango wa msamaha wa kulipia huduma za afya wahakikishe kwamba wanampatia mgonjwa huduma hizo kwa utaratibu wa msamaha wa gharama hizo.

Aidha, kwa kuwa nchi yetu ni kubwa na ina nyoka wengi, Mhe Waziri wa Afya anawaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kupitia kwa uangalifu takwimu za wagonjwa walioumwa na nyoka katika kipindi cha kuanzia mwaka 2013 hadi 2016 na kuziwasilisha Wizarani kabla  ya tarehe 31 Januari 2017 ili  kupata takwimu za mahitaji halisi ya dawa ya sumu ya nyoka nchini. Hii itasaidia  kuboresha upangaji, uagizaji na upatikanaji wa dawa hizo nchini. 
 
Vile vile, Waziri wa Afya ameiagiza Bohari ya Dawa (MSD)  kuweka utaratibu wa haraka wa kununua dawa hizo moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji ili kupata unafuu wa bei.

Imetolewa na:-
Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikalini  - Afya
26/12/2016
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images