Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Sheikh Ponda Amtembelea Godbless Lema Gerezani........Lema Aandika Barua Nzito Akiwa Gerezani

$
0
0

Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu, Sheikh Ponda Issa Ponda amemtembelea Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema katika Gereza Kuu la Mkoa wa Arusha la Kisongo. 

Kwa mujibu wa Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Vijana la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Noel Olevaroya, Sheikh Ponda alizungumza na Lema kwa muda usiopungua saa moja. 

“Sheikh Ponda amekutana na Mbunge wetu Lema na amekuja mahususi kumjulia hali na amemuambia hampi pole bali anampongeza kwa kukaa mahabusu muda wote licha ya kuamini anastahili kupata dhamana,” alisema Olevaroya. 

Alisema katika mazungumzo yake alimtaka Lema kuwa sauti ya wanyonge kwa kuzungumza hata kama itamfanya awe sehemu alipo hivi sasa, kwani kuna mambo mengi yanayohitaji kusemwa na hakuna wa kuyasema. 

Pia, alimsihi kutokuona kama ametengwa bali hiyo ndiyo njia ya wapigania haki na demokrasia wanayopitia, akijitolea mfano yeye binafsi.

 Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Amani Golugwa alipotafutwa kwa njia ya simu hakupokea na alipotumiwa ujumbe mfupi hakuweza kujibu iwapo chama chake kilikuwa na taarifa ya ugeni wa Sheikh Ponda au ilikuwa ni safari binafsi. 

Atuma salamu za harusi 
Katika hatua nyingine Lema aliandika barua yenye kumbukumbu namba 76/AR/I/I/36 akimtakia heri ya ndoa, Wakili wa chama hicho, John Malya. 

Katika barua hiyo iliyowekwa muhuri na Ofisa wa gereza hilo, Lema alimtumia Malya salamu hizo katika ndoa yake iliyofungwa juzi, Jumamosi. 

“Harusi yenu ni Jumamosi tarehe 10/12/2016 na kwamba nadhani sitaweza kuhudhuria, ningependa sana kuwepo, nimeshindwa kusimamia na hata keki sili? Niko gerezani Arusha,” ilinukuliwa sehemu ya barua hiyo. 

Barua hiyo iliendelea: “Natamani kuona jinsi mlivyovaa kwani nilikuwa nimepania sana, lakini najua mtakuwa mmependeza sana ninawaombea kwani huku jela nina nafasi sana ya kuomba kwa kweli, naomba hadi Mungu anafurahi.”

Lema ambaye alikamatwa Novemba 2, akiwa Dodoma, hadi sasa anashikiliwa katika gereza hilo kutokana na kusudio na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) la kupinga uamuzi wa hakimu mkazi, Desdery Kamugisha aliyempa dhamana Lema katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli. 

Katika kesi hiyo, ambayo huvuta umati, Lema anatuhumiwa kati ya Oktoba 23 hadi 26 kutoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais Magufuli katika maeneo tofauti na mikutano yake ya hadhara. 

Lema anadaiwa katika maeneo matatu tofauti alitoa maeneo ya uchochezi kuwa: “Nchi itaingia katika machafuko kama haitafuata misingi ya katiba na sheria na pia Rais Magufuli asipobadilika.” 

Lema pia akiwa katika Uwanja wa Shule ya Sekondari Baraa anadaiwa kutoa kauli kuwa: “Kiburi cha Rais akiendeea kujiona yeye ni Mungu, hatafika 2020, Mungu atakuwa amechukua maisha yake, Rais ni mbabe na watu anawaonea, wafanyakazi wa Serikali hawana amani, wafanyabiashara hawana amani.” 

Alisema Lema akiwa katika Uwanja wa Kambi ya Fisi Kata ya Ngarenaro alitoa kauli kuwa: “Rais akiendelea tabia ya kud- halilisha demokrasia na uongozi wa upinzani ipo siku taifa litaingia kwenye umwagaji wa damu, Rais yoyote ambaye haheshimu mipaka ya sheria, katiba, atakuwa ameliingiza taifa katika majanga na umwagaji wa damu, watu wamejaa vifua wakiamua kulipuka polisi hawana uwezo na jeshi halitaweza kudhibiti uhalifu utakapotea.”

18 Wanaswa Ufisadi Wa Bil. 2.6/-

$
0
0

Taasisi  ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Kilimanjaro, imebaini ufisadi wa zaidi ya Sh bilioni 2.6 katika tuhuma 18 zilizohusisha viongozi waandamizi wa Serikali, vyama vya ushirika, viongozi wa kisiasa na mawakili.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Kilimanjaro, Alex Kuhanda, taasisi hiyo ilipokea jumla ya tuhuma 72, ambazo baada ya kuchunguzwa, 41 zilithibitika.

Kuhanda alisema uchunguzi huo ni kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Desemba mwaka huu, na kwamba maeneo makubwa yaliyolalamikiwa ni vyama vya ushirika, Saccos, rushwa na udhalilishaji kwenye mikopo ya kibenki, watumishi hewa na ufisadi wa fedha za Uchaguzi Mkuu ulifanyika Oktoba mwaka jana.

Kuhanda alisema tuhuma hizo zilihusisha viongozi 18 waandamizi wa Serikali, vyama vya ushirika, viongozi wa kisiasa, wafanyabiashara na wafanyakazi wasio waadilifu katika benki.

Alisema kuwa katika kipindi hicho, taasisi hiyo imeweza kuokoa zaidi ya Sh milioni 31 kutokana na malipo ya mishahara hewa pamoja na miamala mingine.

Kuhanda alisema kwamba muda mwafaka ukifika watuhumiwa watapandishwa kizimbani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Leo ni mapumziko ya Maulid ya Mtume Muhammad.....Waziri Mkuu ni Mgeni Rasmi

$
0
0
Leo ni mapumziko ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambapo Waislamu nchini wanaungana na wenzao duniani kuadhimisha siku hii muhimu katika imani ya dini ya Kiislamu.

Maulid ilisomwa usiku wa jana kuamkia leo na leo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza la Maulid.Maadhimisho ya Maulid kitaifa yanafanyika mkoani Singida.

Katibu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) Mkoa wa Singida, Alhaji Buruhani Mlau alisema jana kuwa maandalizi yako vizuri na kuwataka waumini wa dini hiyo kuwa watulivu na kusherehekea kwa amani.

Awali Alhaji Mlau alisema sherehe hizo za Kitaifa za Maulid zinafanyika katika kijiji cha Shelui, wilayani Iramba, mkoani hapa na kwa utaratibu sherehe hii mapumziko ni siku moja.

Wiki iliyopita, akitangaza utaratibu wa sherehe hizo, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir alisema kwa mwaka huu, Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11 na mapumziko yatakuwa siku inayofuata yaani Desemba 12.

Mufti wa Tanzania aliwataka Waislamu wote nchini waadhimishe Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu.

“Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kwa kufanya matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo,” alisema Mufti.

Zitto Kabwe Apata Zigo....Mchage Ajivua Uanachama, Aachana na Siasa

$
0
0


Aliyekuwa Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange, amejiondoa uanachama wa chama hicho na kujiweka kando na siasa.

Taarifa ya uamuzi huo wa Mchange ilisambazwa jana katika mitandao ya kijamii, ikionyesha kuandikwa naye huku ikiambatanishwa na namba yake ya simu.

Katika andiko hilo, Mchange aliyewahi kuwa mwanachama wa Chadema kabla hajahamia ACT Wazalendo, alisema aliamua kujitoa rasmi katika ushiriki wa aina yoyote ya siasa ili apate muda zaidi wa kusimamia shughuli zake za kijasiriamali.

Mchange alisema ameamua kujiengua na siasa ili kutoa fursa na huduma sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa.

“Kwa moyo mkunjufu kabisa na kwa mapenzi mema na taifa langu, ninathibitisha kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali zinazonitaka nitoe fursa na huduma sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa,” alisema Mchange.

Alisema kutokana na uamuzi huo ambao aliomba uheshimiwe, lolote atakalolifanya lisihusishwe na chama bali iwe ni msimamo wake mwenyewe kama mtu huru asiye na chama.

“Ninafahamu kuwa mwanachama wa chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba, lakini nimeamua kuihifadhi kwa sasa mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanya vinginevyo. Ninawatakia kila la heri waliokuwa wanachama wenzangu wa ACT Wazalendo katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa chama hicho,” alisema Mchange.

Mchange alisema kujiondoa kwake kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya chama hicho bali ichukuliwe kama chachu ya kufika mbali.

“Msivunjike moyo, msirumbane, pendaneni, heshimianeni na shikamaneni ili mfikie lengo. Nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na swahiba. Zaidi Mtanzania mwenzenu. Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa,” alisema Mchange.

Mchange alishika nafasi mbalimbali katika chama hicho ikiwamo Katibu wa Mipango na Mikakati, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mjumbe wa Mkutano Mkuu.

Mchange anakuwa mwanasiasa wa tatu kuondoka ACT-Wazalendo mwaka huu baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba kuachia nafasi yake na kwenda masomoni nchini Kenya, Aprili mwaka huu.

Miezi michache baadaye, Novemba mwaka huu mwanasiasa Moses Machali naye alitangaza kujiondoa rasmi chama hicho na kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli.

Machali aliwahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi kabla ya mwaka jana kushindwa kutetea jimbo lake kupitia ACT-Wazalendo.

Watoto Watatu Wafa Wakiogelea Bwawani

$
0
0
Watoto watatu wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 wamekufa maji baada ya kuzama katika bwawa lililopo eneo la Ziwamboga, Mombasa wilaya ya Magharibi B, mjini Unguja.

Taarifa ya vifo hivyo imetolewa na daktari wa uchunguzi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Msafiri Marijani.

Daktari huyo alisema watoto hao walikufa baada ya kukosa hewa ya oksijeni baada ya kuzama katika bwawa hilo.

Miili ya watoto hao wanaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 12 ilifikishwa katika hospitali kuu wa Mnazi Mmoja mjini Unguja majira ya saa sita na nusu mchana.

Kwa mujibu wa taarifa ya polisi kutoka mkoa wa Mjini Magharibi, watoto waliokufa ni Ahmed Mjaka Kombo, Fessal Abrazak Mjaka na Mundhir Sheha Khamis wote wakazi wa Ziwamboga, Mombasa Mjini Unguja.

Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema watoto hao walifika katika bwawa hilo kwa lengo la kuogelea ambapo wawili walizidiwa maji na kuanza kuzama ambapo yule wa tatu aliwafuata wenziwe kwa lengo la kuwaokoa na yeye kuzama.

Imeelezwa kuwa ni kawaida ya watoto kuogolea kwenye bwawa hilo, japo huzuiwa.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Silima Haji amewataka wananchi kuacha shughuli za uchimbaji mchanga katika maeneo yasiyo rasmi ili kuepusha matukio yanayozuilika huku diwani wa wadi ya Mombasa akitoa mwito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwazuia watoto wao kucheza katika madimbwi ya maji.

Steven Wasira: Sijateuliwa kuwa msemaji wa CCM

$
0
0

Aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira, amesema kuwa taarifa zilizozagaa  kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa ameteuliwa kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio za kweli.

Taarifa hiyo imedai kuwa Wasira ameteuliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Christopher Ole Sendeka aliyeteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe huku nafasi ya mweka hazina na Naibu Katibu Zanzibar zikidaiwa kupata viongozi wapya.

Wasira amesema kuwa taarifa hizo sio za kweli na ni uzushi tu wa watu ambao wana nia mbaya na hawamtakii mema.Pia CCM kupitia ukurasa wao wa Twitter alikanusha taarifa hizo

“Zipuuzeni hizo taarifa, hakuna kitu kama hicho, nmepigiwa simu na watu wengi sana wanaulizia suala hili. Na sijui kuna ajenda gani nyuma ya hawa waliozusha” Amesema Wasira.

Wasira amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda mrefu huku akishika nyadhifa mbali mbali, ingawa mwaka 1995,alikihama chanma hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni za ndani ya CCM na Jaji Joseph Sinde Warioba.

Magufuli aanza mchakato wa kuwanyoosha Wasaliti Ndani ya CCM

$
0
0

CCM imeanza mchakato wa kuwashughulikia wasaliti ndani ya chama hicho, walioisumbua kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. 

Hatua hiyo ni miongoni mwa mambo ambayo Kamati Kuu ya CCM iliyoketi jana jijini Dar es Salaam ikiongozwa na mwenyekiti wake, Rais John Magufuli ilijadili ikiwa ni sehemu ya tathmini ya uchaguzi huo. 

Tangu uchaguzi huo umalizike ambapo mgombea wa CCM, Rais Magufuli aliibuka na ushindi wa asilimia 58.46 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa aliyepata asilimia 39.97, madai ya kuwapo wasaliti waliomuunga mkono yalitawala na kuwekwa mikakati ya kuwashughulikia kupitia vikao. 

Mbali na kusababisha ushindani mkali dhidi ya CCM, Lowassa aliyehama chama hicho baada ya kuenguliwa katika mchakato wa urais na kwenda Chadema, aliviwezesha vyama vinavyounda Ukawa kupata wabunge 116, idadi kubwa kuwahi kufikiwa tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe. 

Pamoja na Lowassa kuhamia upinzani, mwanasiasa huyo aliendelea kuungwa mkono ndani ya CCM na mara kadhaa ametoa kauli zinazoonyesha kuwa bado ana wafuasi ndani ya chama hicho. 

Wakati akikabidhi chama kwa Rais Magufuli, mwenyekiti aliyemaliza muda wake na Rais mstaafu, Jakaya Kikwete alimkabidhi pamoja na ripoti ya uchaguzi ikiwa na orodha ya wanaodaiwa kukisaliti chama kutoka maeneo mbalimbali nchini wakisubiri hatua za vikao vya juu.

 Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema tathmini hiyo inafanyika kwa lengo la kukiimarisha chama kwa chaguzi zijazo. 

“Agenda iliyozungumzwa leo ni tathmini ya uchaguzi wa mwaka 2015. CCM iliagiza ngazi zake za mashina, kata wilaya na mikoa, wafanye tathmini ya uchaguzi wa mwaka 2015 wa madiwani, wabunge na rais. 

“Tathmini hiyo ilikuwa ni pana, imefanyika kwa kipindi cha mwaka mzima. Mikoa na wilaya zake na kata zao na matawi yake na mashina yake, wameagizwa wakaleta Kamati Kuu ya chama,” alisema Nape ambaye pia ni waziri wa habari, utamaduni, michezo na sanaa. 

Alisema tathmini hiyo ilipitiwa na sekretarieti ya chama kabla ya kupelekwa kwenye Kamati Kuu ambako nako itapelekwa kwenye Halmashauri Kuu kwa maamuzi zaidi. 

“Baada ya kujadiliwa na Kamati Kuu itapelekwa kwenye kikao cha NEC ambacho ndicho kikao cha maamuzi , kitatoa maelekezo ya mambo ya kufanya na hatua za kuchukua,” alisema Nape. 

“Nisingependa kuzungumzia sana nisije ku-pre empty NEC, ninachoweza kusema ni kwamba chama kimepokea tathmini, wanachama wametoa mawazo yao, maoni yao wameleta kwenye vikao, tusubiri maamuzi ya vikao. Ndiyo siri ya uimara wa CCM,” alisema bila kuzungumzia ajenda nyingine zilizojadiliwa. 

Hatua ya CCM kufanya tathmini hiyo imekuja wakati wakiwapo baadhi ya makada ambao hawakuridhishwa na uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kukata jina la Lowassa. 

Katika mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM uliofanyika Julai 2015, baadhi ya wajumbe akiwamo Dk Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Adam Kimbisa ambaye ni mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma, walipinga hadharani hatua ya kukata majina ya wagombea kinyume cha kanuni za chama hicho, hali iliyoelezwa kuwakera viongozi wakuu wa chama hicho. 

 Akihutubia mkutano wa kumkabidhi uenyekiti wa CCM Julai 23, 2016 mjini Dodoma, Mwenyekiti mstaafu Jakaya Kikwete alisema mchakato wa kumpata mgombea urais wakati huo ulikuwa mtihani mgumu uliotishia kukigawa chama hicho. 

“Mi nadhani katika historia ya CCM hakuna wakati kulikuwa na tishio la kugawanyika kama mwaka jana. 

“Tumeingia kwenye NEC haijapata kutokea ya namna ile. Lakini tukasema hatutayumba, maadamu sisi viongozi juu tumeshikamana, tutashinda,” alisema Rais Kikwete. 

Lakini akihutubia mkutano huo baada ya kukabidhiwa uenyekiti Julai mwaka huu, Rais Magufuli aliwataka wanachama wanaokisaliti chama hicho kutubu au  waondoke mara moja. 

“Tunataka tukomeshe usaliti ndani ya chama. Katika uongozi wangu na ninaomba Mungu anisaidie na mnisaidie tushikamane ndugu zangu, nitahakikisha usaliti unakomeshwa,” alisema Rais Magufuli na kuongeza:

 “Ndani ya chama chetu pamekuwa na tabia ya baadhi ya wanachama kusaliti chama. Asubuhi anakuwa CCM usiku yuko Chadema, au yuko chama kingine. Wasaliti wa namna hii hawatakuwa na nafasi katika uongozi wangu. Kama wapo wenye tabia hiyo, ni vema wakajirekebisha na kutubu kuanzia leo. 

“La sivyo watupishe ikiwezekana hata leo, waondoke. Ni vema kuishi na mchawi kuliko kukaa na msaliti. Na hili lazima niliseme na ninalisema kwa dhati. Narudia tena, kama wapo watubu kuanzia leo.” 

Alisema katika uongozi wake anataka wanachama waadilifu wanaofuata Katiba na maadili ya chama chetu, siyo ndumilakuwili.

 “Hatuhitaji CCM pandikizi na wana CCM masilahi ambao wapo CCM kwa sababu wanamwabudu mtu fulani kwa masilahi yao binafsi. Ninahitaji wana CCM ambao siku zote, usiku, mchana, mvua ikinyesha, jua likichoma, njaa ikiuma, shibe wameshiba, watabaki CCM bila kuyumba.” 

 Akizungumzia baadhi ya wanachama waliokihama chama hicho wakati wa uchaguzi na kurejea, Rais Magufuli aliwafananisha na ng’ombe waliokatika mikia. 

“Sisi wachunga ng’ombe, nafahamu hata mzee wetu Kikwete kwa sababu ana ng’ombe. Ng’ombe akikatika mkia humzuii kuingia zizini, japo wenzake watajua huyu hana mkia,” alisema Rais Magufuli ambaye pia alisema yeye hana uvumiliku wa Kikwete, na kuwa kama angekuwa yeye wale walioimba wana imani na fulani (Lowassa), nusu au robo wangepotea. 

Alikuwa anamaanisha wajumbe wa Halmashauri Kuu walioimba wimbo wa “Tuna imani na Lowassa” mara baada ya Kamati Kuu kukata jina la mwanasiasa huyo. 

Salaam Za Lowassa Katika Sikukuu Ya Maulid

$
0
0
Nachukua nafasi hii kuwatakia kheri na baraka waislam wote nchini katika kuadhimisha siku hii ya kuzaliwa kwa kiongozi wao Mtume Muhammad SAW.

Waislam kama walivyo watanzania wa dini nyingine wamekuwa nguzo muhimu katika kujenga amani, upendo na utulivu nchini kwetu, na hii yote ni kutokana na mafundisho ya kiongozi wao huyo.

Ni rai yangu kwa watanzania wote wakiwemo watawala kuwa tunapo sherehekea siku hii tutimize kwa vitendo mafundisho ya bwana Mtume ambaye ni mmoja wa mitume wa mwenyezi mungu kwa kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana.

Edward Lowassa
Waziri mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu - Chadema.

Mzee wa Upako: Wote Walionichafua WATAKUFA Mwakani......Wasipokufa Ntaanza Kuuza Gongo

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo, maarufu kwa jina la Mzee wa Upako jana amesema waandishi wote wa habari wanaoandika habari za kumchafua, watakufa kabla ya kufika Machi 2017.

Kauli hiyo ameitoa ikiwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo, akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu kumfanyia fujo jirani yake na kulewa. 

“Kila mwandishi aliyeniandika vibaya, ikifika mwezi wa tatu akiwa hai, mimi naacha kuhubiri, nafunga virago nakwenda kuuza gongo, sasa Mungu ndiye ataamua kwamba ama niache kuhubiri mimi au wewe ufe …najua hata leo mko humu mmekuja na mnasikiliza tu,” alisema.

“Akisema Mungu uishi wewe basi, nakuwa sina namna, lakini sijawahi kumtumikia Mungu ambaye ananyamaza. Nilishakubaliana mimi na Mungu, mpango wa Mungu ndiyo mpango wangu, sasa wajiandae, mimi siyo Sheikh Yahaya, mmeingia choo cha kike, nasema ‘Mama yangu mzazi’ nitaacha kuhubiri, nitaacha kuhubiri ….mimi nina nguvu saaana,”alisema.

Hata hivyo baadaye mchungaji huo alishuka na kusema anamuachia Mungu wake ambaye atawahukumu kwa wakati wake.

“Lakini Mungu anasema tusihukumu, namuachia Mungu atawahukumu kwa wakati wake, haleluya, haleluya, Mungu awabariki sana."

Novemba 24, mitandao ya kijamii ilikuwa na picha zinazomuonyesha Mzee wa Upako akirushiana maneno makali na jirani huyo ambaye anasikika sauti.

Taarifa za kukamatwa kwa kiongozi huyo wa kiroho zilisambaa baada ya mwandishi wa habari, Happiness Katabazi aliyeshuhudia tukio hilo, kuandika kwa urefu kisa hicho na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii.

Novemba 26, Mzee wa Upako kwa mara ya kwanza alisita kuzungumzia sakata hilo na badala yake akasema wanaomtuhumu waendelee kusema:“Sisemi, lakini siogopi kwenda jela mimi na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”

Novemba 28, pia Mchungaji huyo akajibu akisema maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye biblia na kwamba watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.

Jana, mchungaji huyo aliwahakikishia waumini wake akisema waandishi walioandika kwa lengo la kumchafua watakufa kabla ya kufika Machi mwakani.

Katika mahubiri yake yaliyojengwa na msingi wa Biblia kutoka kitabu cha Samweli wa kwanza, sura ya 16, mstari wa saba, Mzee wa Upako aliyekaribishwa kwa nyimbo kadhaa ikiwamo ‘kusanya kusanya’ alisema yeye siyo mchungaji anayejikweza, lakini baadhi ya wachungaji wakubwa kutoka nje wamekuwa wakienda kuomba upako.

Pia, alisema hata Rais John Magufuli hakumuita yeye bali aliona kitu ndani yake na kubarikiwa kabla ya kumtembelea.

Sherehe za Maulid: Waziri Mkuu Asema Serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali dini Zao

$
0
0
Katika kusherekea siku ya Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammed (S.A.W), Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali imani zao za kidini.

Majaliwa ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida na kusema kuwa kuna matukio ambayo yamekuwa yakijitokeza katika jamii na katika kuyachukulia hatua za kisheria vitendo hivyo Serikali haitakuwa ikibagua mtu kutokana na imani yake ya kidini kama jinsi inavyofanya kwa shughuli za maendeleo.

“Serikali inawashukuru sana kwa kuendelea kuunga mkono jitihada ya Serikali ya Rais Magufuli, tunaamini juhudi tunazofanya za kuweka nidhamu kwa watumishi wa umma na taasisi binafsi mtaendelea kutuunga mkono, tutaendelea kuruhusu uhuru wa kuabudu na kushirikiana na viongozi wa dini lakini tu mafundisho yanayotolewa yasikiuke sheria na kanuni za nchi,

“Serikali ipo macho kupambana na tukio lolote lenye nia ya kupoteza amani ya nchi yetu, Watanzania tushirikiane kutoa taarifa ili hatua zichukuliwe, ni vyema mtambue ninyi kama viongozi na waumini ndiyo walinzi wa nchi yetu, niwambie tu kuwa Serikali itaendelea kuwatumikia Watanzania wote bila kujali dini ya mtu wala kabila,” amesema Majaliwa.

Nae Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeiry amesema“Jambo ambalo Waislamu tunatakiwa kuwa nayo ni kupendana, tufanye kama Mtume wetu, yeye alikuwa akijenga mshikamano, akijenga upendo akijenga umoja na kama tunataka kumfata tumwige Mtume katika kupendana, tuache majungu, fitna na tuache kila kitu kisicho na faida,

“Kwanini mnagombana Waislamu na nyie ni watu wa Mungu, Waislamu tuwe na mshikamano kama tuliokuwa nao, pia tunao undugu wa Tanzania, tupendane kama Watanzania na mwenyezi Mungu ametwambia tusibague hata kama sio Waislamu, Mungu hakatazi mtu kumtendea wema mtu mwingine kama tu hakufanyi mabaya na hayo ndiyo mafunzo ya Uislamu.”

Sherehe za Maulid: Waziri Nchemba awataka Watanzania kuwafichua watu wanaotumia dini kufanya vurugu

$
0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Lameck Nchemba amewataka Watanzania wote nchini kuungana kwa pamoja na kuwataja watu ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya vurugu kwa kuhusisha vitendo hivyo na dini kwani watu hao wanaweza kusababisha nchi kupoteza amani.

Waziri Nchemba ameyasema hayo katika sherehe za kitaifa za Maulid ambazo zimefanyika mkoani Singida ambapo alisema mtu ambaye anamcha Mungu hawezi kuwa akijihusisha na vitendo hivyo na Serikali ya awamu ya tano itakuwa ikimchukulia hatua mhusika bila kuhusisha dini.

“Wizara yangu inahusika na taasisi zote zinazohusika na ibada, niwambie jambo moja tutofautishe udini na kumcha Mungu, mtu anaposhika sana dini ni mshika dini na mtu unanayemcha Mungu ni mchaMungu sio mdini, makosa yote katika nchi yanafanywa na makundi mawili ya watu wenye dini na wasio na dini,

“Kosa lolote ambalo likifanywa liwe kosa la ambae alifanya kosa, sio kosa la dini, akifanya Mkristo kosa la mtu sio la dini, akifanya Mwislamu kosa ni lake si la dini, na hata kama hana dini kosa ni lake yeye, na tusaidiane kuwa tunawafichua wanaosababisha vurugu,” amesema Nchemba.

Pia Nchemba ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa amekabidhi msaada wa mabati 1,000 kwa ajili ya kutumika kujenga misikiti na kuahidi kuwa baada ya wiki moja atawapatia gari aina ya Noah.

'Dume Suruali' ya Mwana FA na ‘Muziki’ ya Darassa Zachuana Vikali Youtube

$
0
0

Video ya ‘Dume Suruali’ ya Mwana FA akiwa na Vanessa Mdee pamoja na video ya ‘Muziki’ ya Darassa akiwa na Ben Pol ndizo video za muziki wa rap Tanzania zinazoongoza kwa kuangaliwa zaidi kwenye mtandao wa YouTube kwa muda mfupi hivi sasa.
 
Video hizo zimeonekana kutoana nduki kwa mashabiki wao kuziangalia mara nyingi zaidi zikigusa rekodi ya kuangaliwa zaidi ya mara milioni moja ndani ya kipindi kisichozidi wiki mbili tangu zilipopandishwa mtandaoni.
 
Muziki ya Darassa imeshaangaliwa zaidi ya mara milioni 1.43 tangu ilipopandishwa kwenye mtandao huo Novemba 23 mwaka huu huku ‘Dume Suruali’ ikiangaliwa zaidi ya mara milioni 1.13 tangu ilipowekwa YouTube Novemba 25 mwaka huu. 
 
Hii inaonesha kuwa hivi sasa wasanii wanaungwa mkono zaidi na mashabiki wao kwa kuangalia video zao kwenye mtandao kutokana na uwepo wa mapinduzi ya kiteknlojia, ambapo mamilioni ya Watanzania sasa wanaweza kupata ‘internet’ kwenye simu zao.


Miss World Diana Edward aingia fainali za Beauty With A Purpose

$
0
0

Miss Tanzania 2016, Diana Edward, ameingia kwenye fainali za shindano la Beauty With A Purpose ambalo ni sehemu ya mashindano mbalimbali kwenye Miss World.

Beauty With A Purpose huhusisha miradi mbalimbali ya kijamii ambayo hufanywa na washiriki wa Miss World. Diana amewasilisha documentary ya masuala ya ukeketaji kwenye jamii ya watu wa Masai.

Fainali za Miss World mwaka  huu zitafanyika December 18, nchini Marekani.

Pamoja na Diana kuonesha kufanya vizuri, tangu atawazwe kuwa Miss Tanzania mwaka huu, amekuwa akipokea maneno hasi.
“I’m not beautiful Yes,I’m not focused Yes,I’m in a vacation Yes,I’m dumb Yes,I’m not up todate Yes. Who knows tomorrow ONLY God can determine your future.Thanks for those who have been and still voting for me and supporting me no matter how much Haters are pushing me back you guys are still holding my hand and lift me up,” ameandika kwenye Instagram.

“Good News My Beauty with a Purpose Documentary for Masai Dondosha Wembe has shined again to TOP 20 waiting for the TOP position and has been said ever since there has never been such a wonderful message to the beauty pageant history of Miss World.Please Keep on voting for your Tanzania’s Best Kept Secret Princess Diana,I love myself though. One rule I was born to shade tears to fight and to become a champion,” ameongeza.

Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Haki za Kiraia na Kisiasa Tanzania.........LHRC Wametaja Mikoa 8 hatari kwa kukiuka haki za binadamu

$
0
0

Kituo cha Sheria na Haki za BInadamu (LHRC) kimetoa Ripoti ya Mtazamo wa Hali ya Kisiasa Tanzania kwa mwaka 2016 ambayo miongoni mwa mambo mengi yaliyoonyeshwa katika ripo hiyo ni pamoja na mikoa iliyokumbwa na matukio mengi ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Hapa chini ni orodha ya mikoa yenye hatari kwa wakazi wake kutokana na kukiuka haki za binadamu.

Simiyu na Kaskazini Unguja:

Mikoa hii miwili kwa mwaka 2016 imekumbwa na changamoto kubwa katika uhuru wa kujieleza, uhuru wa kukusanyika na haki ya kupiga kura. Lakini kwa upande mwingine mikoa hii imepata alama za juu zaidi katika matokeo ya mtazamo kuhusu haki za kiraia na kisiasa, hasa kwa upande wa haki ya kuishi.

Songwe, Tabora na Shinyanga:

Mikoa hii ilipata alama za chini zaidi ukilinganisha na mikoa mingine yote. Mikoa yote ilikuwa na alama za chini sana kwenye uhuru ya Kukusanyika na haki ya kuishi-mauaji na ukatili mikononi mwa vyombo vya dola. Kama serikali za mikoa zitaendelea kuminya uhuru wa kukusanyika, kushughulikia mauaji yanayotokana na imani za kishirikina na matukio ya kujichukulia sheria mikononi, basi itakua ngumu kupata mwenendo chanya katika mikoa hii.

Morogoro, Arusha na Manyara:

Katika mikoa hii kuna ongezeko kubwa la migogoro ya ardhi ambayo inaweza kupelekea watu kujichukulia sheria mkononi au mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola. Migogoro hii hasa husababishwa na mvutano kati ya wakulima na wafugaji ambapo mara nyingi hupelekea vifo vya raia.
Mbali na mokoa hayo, kituo cha haki za binadamu pia kilitaja haki za raia zilizoongozwa kukiukwa kwa mwaka 2016 ambazo ni pamoja na;

Haki ya Kuishi-Kujichukulia Sheria Mkononi:

Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro, ambayo kwa sehemu kubwa ni mijini, iliongoza kwa kiasi kikubwa kwenye ukiukwaji wa haki hii. Kuna haja ya polisi na viongozi kurudisha imani ya wananchi juu yao ili kupunguza matuko ya kujichukulia sheria mkononi.

Uhuru wa Kutoa Maoni:

Athari ya Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari zitakuwa ni za muhimu sana kufanyiwa uchambuzi kwa mwaka 2017 hasa kwa kuwa uhuru wa vyombo vya habari umeelezwa kuwa miongoni mwa matatizo katika mikoa iliyopata alama za chini. 

Ukizingatia shinikizo ndani nan je ya nchi, itakuwa muhimu kuangalia kama Serikali itayafanyia kazi mapendekezo ya watetezi wa haki za 21 Matukio Makubwa yaliyotokea Mwaka 2016 Mtazamo wa Haki za Kiraia na Kisiasa 2016 Mikoa na Haki za Kuangalia mwaka 2017 Methodologia na Alama binadamu ya kurekebisha vipengele vya sheria hiyo vinavyominya haki.

Uhuru wa Kukusanyika:

Tumeshuhudia zuio la mikutano na mikusanyiko ya kisiasa kwa mwaka 2016, kitendo ambacho kimepelekea mtazamo kwamba uhuru wa kukusanyika imeminywa. Japokuwa Jeshi la Polisi baadae liliondoa zuio hilo, kitendo hicho kiliendelea kuathiri mtazamo kuhusu uhuru wa kukusanyika.

Haki ya Kuishi – Mauaji na Ukatili Mikononi mwa na Vyombo vya Dola:

Matukio ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yamechangia kwa kiasi kikubwa kushusha alama za haki katika mikoa mingi. 

Japokuwa kumekuwa na ongezeko la mashtaka ya mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola, ikiwemo askari polisi wawili kukutwa na hatia ya mauaji hivi karibuni, kauli na matamko mbalimbali za viongozi wa serikali ambayo yanaweza kuchochea mauaji yanayofanywa na vyombo vya dola yanaweza kuwa chanzo cha mauaji pia.
Unaweza kupakua ripoti nzima hapa chini;
 
 

VIDEO: Tazama Hapa Video ya Sherehe za Maulid Zilivyofanyika Kitaifa Singida. Mgeni Rasmi Alikuwa Waziri Mkuu

$
0
0
Tazama  Hapa  Video  ya Sherehe  za  Maulid  Zilivyofanyika  Kitaifa  Singida. Mgeni   Rasmi  Alikuwa  Waziri Mkuu

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumanne ya Disemba 13

Pata Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kuondoa Michirizi, Kuongeza Unene, Kuondoa Chunusi na Zingine Nyingi Toka Beauty Cosmetics

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS Ni wauzaji wa vipodozi aina mbali mbali na vyenye matokeo mazuri na ya haraka zaidi bila kemikali wala madhara yoyote
 
     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @90,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @120,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 120,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 90,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 100,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @100,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
12.kuotesha nywele kwenye kipara @100,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=
 
     WASILIANA NASI KWA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti ili kuhakikisha mafanikio yako
 
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Magufuli kuongoza kikao cha NEC leo

$
0
0
KIKAO cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinakutana leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni kikao cha kwanza kuongozwa na Rais John Magufuli tangu achaguliwe kukiongoza chama hicho tawala Julai mwaka huu.

Juzi, Rais Magufuli aliongoza kikao cha Kamati Kuu ambacho kilipaswa kuwa cha siku mbili, lakini kikamaliza kazi zake juzi.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye aliwaambia waandishi wa habari juzi baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Kuu kwamba mapendekezo au hoja zote zilizoibuliwa na wajumbe katika kikao hicho zitawasilishwa katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ambacho kitafanyika jijini Dar es Salaam.

Nape hakueleza hoja na mapendekezo hayo yanayopelekwa NEC, lakini kwa ujumla kikao hicho ndicho chenye uamuzi wa kubariki mapendekezo yanayotoka katika kikao cha Kamati Kuu hivyo inatarajiwa kuwa itafanya maamuzi mbalimbali.

Miongoni mwa hayo ni uteuzi wa mgombea wa ubunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar, lakini pia huenda NEC ikabariki uteuzi wa wajumbe wa Sekretarieti ya chama hicho kama yatawasilishwa kwao na Mwenyekiti kutokana na nafasi mbalimbali kuwa wazi.

Naibu Katibu Mkuu Bara, Rajab Luhavi na aliyekuwa Kaimu Katibu wa NEC wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk Pindi Chana hivi karibuni wameteuliwa kuwa mabalozi wakati Nape pia anashikilia wadhifa wa uwaziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Aidha, aliyekuwa Msemaji wa chama, Christopher ole Sendeka mwishoni mwa wiki aliteuliwa na kuapishwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe, hali inayoashiria kuwa mabadiliko katika Sekretarieti hayaepukiki. 

Aidha, Nape aliwaambia waandishi juzi kuwa ajenda kuu katika kikao hicho cha Kamati Kuu ilikuwa ni tathimini ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Alisema tathimini hiyo ilikuwa ni pana na imefanyika kwa kipindi cha karibu mwaka mmoja ambayo ilifanyika kwa ngazi ya mikoa, wilaya na kata na wamemaliza tathimini na kuipeleka makao makuu ya chama ili kupitiwa na vikao vya maandalizi vya sekretarieti na vikao vingine kisha ikawasilishwa kamati kuu kwa ajili ya kujadiliwa.

Alisema baada ya tathimini hiyo kujadiliwa Kamati Kuu itapelekwa katika kikao cha Halmashauri Kuu leo ambacho ndio chenye maamuzi na kitapitia na kuangalia endapo kuna mambo yaliyopendekezwa na hatua za kuchukua kama mabadiliko na vitu vingine.

“Huu ni utaratibu wa kawaida katika chama chetu kila uchaguzi huwa inafanyika tathimini ambazo hutusaidia sana, kujua wapi tulifanya vizuri na wapi hatukufanya vizuri na mengineyo yote yaliyokuwa sehemu ya ushiriki wa chama katika Uchaguzi Mkuu, na tumekuwa tukifanya hivi katika chaguzi zote hali ambayo imeifanya CCM kuimarika zaidi,” alieleza Nape.

Jeshi la Polisi Kutoa Msimamo wake Leo Kuhusu Kauli za Mzee wa Upako Kwamba Waliomchafua Watakufa Mwakani

$
0
0

Siku moja baada ya Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako kusema waandishi waliomuandika vibaya watakufa kabla ya Machi 2017, Jeshi la Polisi linatarajia kutoa msimamo wake dhidi ya kauli hiyo leo. 

Kauli hiyo ya Mzee wa Upako aliyoitoa juzi kanisani kwake, ilikuwa ni mwendelezo wa mahubiri yake ya nne katika wiki ya tatu mfululizo akijibu yale yaliyoandikwa katika vyombo vya habari kuhusu madai ya kulewa na kumfanyia fujo jirani. 

Kamanda wa Kanda Maalumu ya Kipolisi ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro jana  alisema ni mapema kuzungumzia sakata hilo kwa sababu jana ilikuwa sikukuu na atatolea ufafanuzi leo. 

“Anasema hao waandishi watakufa kabla ya Machi 2017 kwani yeye Mungu? Hilo ni suala zito, tumeandaa mkutano na waandishi wa habari tutalizungumzia suala hilo kesho (leo),” alisema Kamanda Sirro.

 Katika kauli hiyo, Mzee wa Upako alisema kila mwandishi aliyemuandika vibaya ikifika Machi mwakani hatakuwa hai na kama wataendelea kuishi, ataacha kazi ya kuhubiri injili na kwenda kuuza gongo.

Serikali Yacharuka Suala la Maiti 7 Kuokotwa Mto Ruvu........Waziri Mkuu Atoa Maagizi Mazito kwa Jeshi la Polisi

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa ameiagiza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Jeshi la Polisi kufanya upelelezi kuwabaini waliohusika na mauaji ya watu saba ambao miili yao iliokotwa pembezoni mwa mto Ruvu wilayani Bagamoyo, mkoa wa Pwani, ikiwa kwenye mifuko ya sandarusi, ili hatua kali zichukuliwe dhidi yao.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema serikali imepokea kwa huzuni kubwa taarifa ya kuokotwa kwa miili hiyo Desemba 8, mwaka huu na kueleza kuwa matukio kama hayo, likiwemo la mjasiriamali kuuawa baada ya kutekwa mkoani Tabora, hayavumiliki wala kukubalika.

Alitoa maagizo hayo jana katika Baraza la Maulid ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) lililofanyika kitaifa kijijini Shelui wilayani Iramba mkoani Singida. Waziri Mkuu Majaliwa alikuwa mgeni rasmi.

Alisema, “Serikali kwa kushirikiana na Polisi, tena Waziri wa Mambo ya Ndani uko hapa (akimzungumzia Mwigulu Nchemba aliyekuwepo katika baraza hilo), tutaendelea na upelelezi ili wahusika wachukuliwe hatua kali.”

Jana akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Star TV, Mwigulu alisema uchunguzi umebaini kuwa miili saba iliyookotwa Bagamoyo ni ya wahamiaji haramu.

Miili ya watu sita ilikutwa Desemba 7, mwaka huu kando ya mto Ruvu wilayani Bagamoyo ndani ya mifuko ya sandarusi na ikiwa imewekwa mawe ili isielee kisha mifuko hiyo kushonwa kama mzigo wa mazao na kutupwa mtoni.

Mwili mwingine uliokotwa Desemba 9, eneo hilo hilo na pamoja na kutokuwa katika mfuko wa sarandusi, ulikuwa umevuliwa shati na kuonekana na majeraha mgongoni na kwenye ubavu umekatwa na kitu chenye ncha kali.

Mwishoni mwa wiki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Boniventure Mushongi alisema miili yote ilizikwa kwa kuwa ilikuwa vigumu kuwatambua kutokana na kuharibika vibaya huku kukiwa hakuna kitambulisho chochote kinachoashiria watu hao ni nani na wametoka wapi na kwamba Polisi inaendelea na upelelezi kubaini waliohusika na mauaji hayo na atakayebainika sheria itachukua mkondo wake.

Aidha, Waziri Mkuu alisema serikali ipo macho kukabiliana na tishio lolote la usalama na vyombo vya usalama vipo tayari muda na wakati wote. 

Aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama kutoa taarifa wanapoona kuna hatari kwani viongozi wa dini na waumini wa dini hizo ndio walinzi wa Taifa.

Alisema uwepo wa vikundi vya uhalifu kama ‘panya road’ cha jijini Dar es Salaam ni hatari kwa jamii, kwani vinadhuru na kuvuruga amani na kueleza kuwa ni vijana na watoto wanaoishi katika jamii, walioko misikitini na makanisani na kutaka waripotiwe katika vyombo vya usalama ili washughulikiwe.

Alizungumzia ugaidi na kubambikizwa kesi, na kusema serikali itaendelea kusimamia mtu kupata haki zake na anayestahili adhabu, kuipata vile vile.

“Ni heri kuwa na watu 10 waliotoroka mahabusu kuliko mtu mmoja kukaa mahabusu kwa kesi ya kuonewa,” alisema Majaliwa.

Mwigulu anena kuhusu miili 7, Saanane
Akizungumza jana kwa simu kuhusu vifo hivyo vya Bagamoyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba alisema serikali baada ya tukio hilo ilichukua hatua kupitia vyombo vya usalama na tayari Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu amemhakikishia wanalifanyia kazi.

“Kama nilivyosema awali, hatujajua asilimia mia kwa mia kama watu hao waliouawa wana connection (uhusiano) na wahamiaji haramu waliookotwa wamechoka sana hivi karibuni (juzi). 

“Kuna wahamiaji 81 waliokotwa hawajitambui, wameishiwa nguvu kabisa, ni eneo hilo hilo kulikookotwa miili hiyo, tumehisi watu waliowabeba wahamiaji hao inawezekana wengine walikufa na kwa vile hawana utu, wakawafunga katika viroba (sarandusi) na kuwatupa, Polisi wanachunguza hili kwa kina,” alieleza Mwigulu.

Aidha, alisema pia Polisi inachunguza ikiwa miili hiyo ilitupwa kikatili na wasafirishaji wa binadamu ambao nao hawana utu.

Alipoulizwa kwa nini wazikwe haraka bila vipimo vya vinasaba, Mwigulu alisema kuwa alizungumza na IGP na kuelezwa kuwa miili hiyo ilikuwa katika hali mbaya sana, lakini pia kuzikwa hakuzuii uchunguzi kufanyika kujua chanzo cha vifo hivyo.

Kuhusu kupotea katika mazingira ya kutatanisha Ofisa wa Ofisi ya Chadema, Makao Makuu Dar es Salaam, Bernard Saanane Novemba 18, mwaka huu, Mwigulu alisema aliona taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na kwa kuwa alikuwa akimfahamu, alimpigia simu na kubaini simu haipatikani.

“Nilishtuka kuona hizi habari, binafsi ni rafiki yangu wa karibu, nilipoona hizi habari nilimpigia na sikumpata, baada ya kuona simpati nilimpigia Mbowe (Freeman- Mwenyekiti wa Chadema Taifa), lakini simu yake iliita kama vile mtu yupo nje ya nchi,” alifafanua Mwigulu.

Hata hivyo, alisema amemuagiza IGP awaagize polisi kumtafuta Saanane na kuhakikisha ufumbuzi wa kupotea kwake unapatikana na kujulikana alipo.

Juzi, Mwenyekiti wa Umoja wa Kizazi cha Kuhoji Tanzania (UTG), Malisa Godlisten akizungumza na waandishi wa habari, aliipa Chadema na taasisi za umma zenye dhamana ya usalama wa raia saa 72 kuanzia jana kuhakikisha Saanane anapatikana na kueleza umma chanzo cha vifo vya watu hao saba ambao miili yao ilikutwa kando ya mto Ruvu, Bagamoyo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images