Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Video: Rais Dk Magufuli akitembea kama mwanajeshi baada ya kukagua gwaride

0
0
Leo Desemba 9 Tanzania Bara imeazimisha miaka 55 tangu ilipopata uhuru wake kutoka kwa wakoloni mwaka 1961. 

Maadhimisho hayo yamepambwa na shughuli mbalimbali za kijeshi lakini pia ngoma za asili kutoka kwa makundi mbalimbali.

Mbali na mambo hayo yaliyoonekana kuwavutia wengi, jambo lingine lililowafurahisha ni pale Rais Dk Magufuli alipoamua kutembea kiukakamavu kama mwanajeshi mara baada ya kumaliza kukagua gwaride katika maadhimisho haya ya 55 ya uhuru.

Hapa chini ni video ra Rais Dk Magufuli akitembea kiukakamavu baada ya kukagua gwaride katika sherehe za uhuru.

Rais Magufuli ataja mambo yanayoikwamisha Tanzania

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitaja rushwa kama changamoto sugu ambayo bado inaendelea kulitafuna taifa la Tanzania katika miaka yake 55 ya Uhuru.

Rais Magufuli ameitaja changamoto hiyo leo akati akiwaongoza watanzania katika maadhimisho ya miaka 55 ya uhuru wa Tanzania Bara ikiwa ni mara ya kwanza tangu aingie madarakani na kutaja changamoto nyingine kuwa ni tatizo la ajira pamoja na umasikini.

Akizungumza katika hotuba yake ya shukrani katika maadhimisho hayo ambayo yamefanyika katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam, Dkt. Magufuli, amesema kuwa serikali yake itaendelea kupambana na vitendo na rushwa na ufisadi, kwa ajili ya kuliletea taifa maendeleo.

Aidha Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa serikali itahikisha kuwa inaondoa uonevu hasa kwa wananchi wanyonge ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili ili kila mtanzania aweze kufaidika na matunda ya nchi yake.

Maadhimisho hayo ambayo kwa mujibu wa Rais Magufuli ndio ya mwisho kufanyika Jijini Dar es Salaam na kuanzia mwakani yataadhimishwa Dodoma, yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wastaafu na serikali pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali zenye uwakilishi hapa nchini.

Sherehe za Uhuru kuhamia Mkoani Dodoma....Leo Ilikuwa Mara ya Mwisho Kufanyika Dar es Salaam

0
0

Sherehe za Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara zitakuwa zikifanyika mjini Dodoma kuanzia mwaka 2017 badala ya Jijini Dar es Salaam kama ilivyozoeleka.
 
Uamuzi huo umetangazwa leo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Magufuli, wakati akitoa salamu zake za maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara, kwenye sherehe zilizofanyika leo katika uwanja wa Uhuru dar es Salaam.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, ameeleza sababu za kufuta sherehe hizo mwaka jana na kuruhusu mwaka huu zifanyike ambapo amesema sababu moja wapo iliyomfanya afute sherehe hizo mwaka jana ni kubana matumizi.

"Mwaka jana nilipouliza gharama za sherehe zile nikaambiwa ni shilingi bilioni 4, nikashangaa, bilioni 4 zote ni za nini?" Amesema Rais Magufuli.

Kuhusu sababu za kuruhusu mwaka huu sherehe hizo zifanyike, Rais Magufuli ametaja sababu mbili ambazo ni pamoja na kutumia gharama ndogo huku  sababu ya pili akiitaja kuwa ni kutokana na kwamba hizi ni sherehe za mwisho za Uhuru kufanyika Jijini Dar es Salaam huku akieleza kuwa kuanzia mwaka 2017, sherehe hizo zitakuwa zikifanyika katika makao makuu ya nchi Dodoma.

"Mwaka huu gharama ni ndogo, hata kula wala kunywa hakuna, baada ya hapa hakuna kula wala kunywa"

Rais Magufuli pia ametumia nafasi hiyo kuelezea mafanikio ya Tanzania katika miaka yake 55 ya Uhuru, huku akieleza mikakati ya serikali yake ya awamu ya tano katika kuifikisha nchi kwenye kipato cha kati na kuwashukuru viongozi wakuu wa awamu zilizopita.

Kaulimbiu ya sherehe hizo kwa mwaka huu ni: Tuunge mkono jitihada za kupinga rushwa na ufisadi na tuimarishe uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu.

Picha 16 za Maadhimisho ya Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara Yaliyofanyika Jijini Dar

Mabweni ya shule ya Secondary ya Ufundi ya Mtwara Yateketea Kwa Moto

0
0

Bweni la wasichana wa shule ya sekondari ya Mtwara ufundi iliyoko katika Manispaa ya Mtwara Mikindani limeteketea kwa moto leo majira ya saa moja asubuhi.

Akizungumza katika eneo la tukio kamanda polisi Mkoani hapa Thobias Sedoyeka amesema kwamba majira ya saa moja katika shule ya sekondari ufundi kulitokea moto ambao ulianza kuwaka katika mabweni ya wasichana ambapo mpaka sasa chanzo hakijajulikana na kuongeza kuwa hakuna madhara yoyote yaliyotokea kwa binadamu na makadirio ya hasara ya thamani ya jengo na mali zilikuwemo  bado haijajulikana.
 
Naye mwalimu wa shule hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Nanyalika amesema kwamba alikuwepo eneo la tukio wakati bweni hilo la wasichana wa shule ya sekondari ya ufundi linaanza kuteketea ambapo kwa upande wake hajui chanzo cha moto huo hali ambayo imepelekea walimu ambao wanaishi ndani ya shule hiyo kuwa na hali ya sintofahamu kwa kuhofia usalama wao.
 
kwa upande wake mwalimu wa shule ya sekondari Sululu Sekondari iliyoko Mjini Masasi ambae yupo shuleni hapo kwa ajili ya kusahihisha mitihani ya kidato cha pili na alikuwa akitumia moja ya chumba cha bweni hilo amesema kwamba kipindi ambacho wapo katika maeneo yao ya kazi ndipo walipoona moshi unatokea kwenye bweni.
 
Naye mwalimu Masele Francis kutokea shule ya sekondari ya Namwombe iliyoko katika Halmashauri ya Masasi ameeleza kuwa kipindi ambacho anatoka bwenini aliona moshi mkubwa hali ambayo ilimpelekea kurudi ndani ili kuwapa wenzake taarifa.
 
Aidha  Afisa Habari wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Bi.Jamad Omary amewatoa hofu walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo na kuwaomba kuwa wavumilivu katika kipindi hiki kigumu mbali na hayo amewataka wananchi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani kuwa na ushirikiano wa kutosha pindi kunapotokea tatizo kama hilo na si kuishia kutoa lawama.
 
Hata hivyo Kamanda amesema kwamba taarifa kamili kuhusiana na tukio hilo ikiwemo chanzo cha moto huo itatolewa baada ya taratibu zote kukamilika.

Video: Makomando wa JWTZ walivyoonyesha uwezo wao mbele ya Rais Magufuli

0
0

Leo  zimefanyika sherehe za maadhimisho ya 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara katika uwanja wa Uhuru Dar es salaam, ambapo Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli alikuwa mgeni Rasmi. 

Mbele ya Rais Magufuli Makomando wa JWTZ walipata nafasi ya kuonyesha uwezo wao ikiwamo namna ya kukabiliana na adui. 

Tazama hapo chini

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 10

Rais Magufuli Atoa Msamaha Kwa Wafungwa 5,678 Katika Maadhimisho Ya Miaka 55 Ya Uhuru Wa Tanzania Bara

0
0
Katika kuadhimisha miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe  9 Disemba, 2016 Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutumia madaraka aliyopewa chini ya Ibara ya 45(1)(d) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa msamaha kwa wafungwa wafuatao:-
(i)Wafungwa wote wamepunguziwa moja ya sita (1/6) ya vifungo vyao zaidi ya punguzo la kawaida linalotolewa chini ya kifungu 49(1) cha Sheria ya Magereza Sura ya 58 isipokuwa wafungwa walioorodheshwa katika Ibara ya 2 (i-xx).

(ii)Wafungwa wagonjwa wenye magonjwa kama UKIMWI, KIFUA KIKUU (TB) na SARATANI (CANCER) ambao wako kwenye “terminal stage”. Wafungwa ambao wamethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

(iii)Wafungwa wazee wenye umri wa miaka sabini (70) au zaidi ambao umri huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

(iv)Wafungwa wa kike walioingia na mimba gerezani, pamoja na wale walioingia na watoto wanaonyonya na wasionyonya.

(v)Wafungwa wenye ulemavu wa mwili na akili (Physical disability and mental disability) ambao ulemavu huo umethibitishwa na Jopo la Waganga chini ya Uenyekiti wa Mganga Mkuu wa Mkoa/Mganga Mkuu wa Wilaya.

2.Aidha, Msamaha huu wa Mheshimiwa Rais hautawahusu wafungwa wafuatao:-

(i)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa.
(ii)Wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kunyongwa na adhabu hiyo kubadilishwa kuwa kifungo cha maisha au kifungo gerezani.
(iii)Wafungwa waliohukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

(iv)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na usafirishaji na matumizi ya madawa ya kulevya kama vile cocaine, heroin, bhangi n.k.

(v)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kujihusisha na uombaji, upokeaji au utoaji rushwa.

(vi)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya unyang’anyi na unyang’anyi wa kutumia silaha au kujaribu kutenda makosa hayo (robbery with violence, armed robbery and attempt robbery).

(vii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya kupatikana na silaha, risasi au milipuko isivyo halali (firearms, ammunitions and explosives).

(viii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya shambulio la aibu, kunajisi, kubaka na kulawiti, au kujaribu kutenda makosa hayo.

(ix)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa kosa la kuwapa mimba wanafunzi wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari na ambao walitenda kosa hilo wakiwa na umri wa miaka kumi na nane (18) na kuendelea.

(x)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya wizi wa magari na pikipiki au kujaribu kutenda makosa hayo.

(xi)Wafungwa wanaotumikia kifungo chini ya Sheria ya Bodi ya Parole (Act. No. 25/1994) na Sheria ya Huduma kwa Jamii (Act. No. 6/2002).

(xii)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo kwa makosa ya kutumia vibaya madaraka yao.

(xiii)Wafungwa waliowahi kupunguziwa kifungo na Msamaha wa Mheshimiwa Rais na bado wangali wanaendelea kutumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.

(xiv)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kuzuia watoto kupata masomo.

(xv)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la utekaji wa watoto, kupoka na kufanya biashara ya binadamu (Human Trafficking).

(xvi)Wafungwa waliopatikana na hatia na kuhukumiwa kwa kosa la kukutwa na viungo vya binadamu.

(xvii)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kujihusisha na  usafirishaji wa nyara za Serikali na ujangili (Poachers).

(xviii)Wafungwa wanaotumikia kifungo kwa makosa ya        wizi/ubadhirifu wa fedha za Serikali.

(xix)Wafungwa wanaotumikia vifungo kwa makosa ya kutoroka au kujaribu kutoroka chini ya ulinzi halali.

(xx)Wafungwa walioingia gerezani baada ya tarehe 9/10/2016.

3.Wafungwa wapatao 5,678 watafaidika na msamaha huu baada ya kupunguziwa 1/6 ya vifungo vyao ambapo 1,340 wataachiliwa huru na wafungwa 4,338 watanufaika na kubaki gerezani wakitumikia sehemu ya kifungo kilichobaki.
 
 Ni mategemeo ya Serikali kwamba watakaoachiliwa huru watarejea tena katika jamii kushirikiana na wenzao katika ujenzi wa Taifa na kwamba watajiepusha kutenda makosa ili wasirejee tena gerezani.

Imesainiwa na;
Meja Jenerali  Projest  Rwegasira
KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
9/12/2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Disemba 11

Picha: Rais Magufuli alivyokutana na kufanya mazungumzo na muwekezaji Aliko Dangote Ikulu Dar es Salaam

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 10 Desemba 2016, amekutana na kufanya mazungumzo na Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara, Alhaji Aliko Dangote.

Katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli alimhakikishia mfanyabiashara huyo kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wote nchini katika kutimiza lengo lake la kuwa na Tanzania ya Viwanda.
 
Rais Magufuli alisema kuhusu kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote kilichopo Mkoani Mtwara hapakuwa na tatizo lolote ila kulikuwa na watu ambao walitaka kujinufaisha binafsi kupitia mradi huo kwa kufanya biashara za ujanja kitu ambacho serikali yake haikiruhusu.
 
Alimtaka Dangote kununua gesi moja kwa moja kutoka TPDC ambacho ni chombo cha serikali badala ya kutumia watu ambao wamekuwa na nia ya kutengeneza faida tu.
 
”Iwapo unataka maelezo yoyote ama lolote linalokukwamisha uwasiliane na viongozi wa serikali badala ya kuwasiliana na watu ambao wako kwa ajili ya kufanya biashara ya ujanja ujanja kwa lengo la kupiga dili ” alisema Rais Magufuli.
 
Dokta Magufuli alisema Dangote ametaka eneo dogo ambalo angelitumia kusafirishia saruji yake wakajitokeza watu ambao wametaka kumuuzia kwa shilingi bilioni 43 kitu ambacho hakina uhalisia wowote bali ni watu ambao wanataka kutengeneza faida kitu ambacho hakiwezekani.
 
Kwa upande wake mmiliki wa Kiwanda cha kuzalisha Saruji cha Dangote, Alhaji Aliko Dangote alishangazwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa amefunga kiwanda kwa sababu amekatazwa kuagiza makaa ya mawe toka nje ya Tanzania kitu ambacho amesema hakiingii akilini kwa sababu makaa ya mawe ya Tanzania ni rahisi na yana ubora kuliko kuagiza nje.
 
Katika kuthibitisha hilo, tayari Mfanyabiashara huyo ameingiza malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake. 

Aliongeza kuwa lengo la kufanya biashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
 
Alhaji Dangote alimuhakikishia Rais magufuli kuwa ataendelea kufanyakazi na Serikali ya Tanzania na kamwe hana nia yoyote ya kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa na baadhi ya vyombo vya habari bali ana mpango wa kuangalia fursa nyingine zaidi za uwekezaji hapa nchini kutokana na uwepo wa sera nzuri za uwekezaji chini ya Serikali ya Awamu ya Tano.

Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mmiliki wa Kiwanda cha Saruji cha Dangote kilichopo Mtwara Alhaji Aliko Dangote akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.




Picha 5: Meli yenye malori 600 ya Kiwanda cha Dangote yawasili Mtwara

0
0

Mfanyabiashara Alhaji Aliko Dangote jana alipokuwatana na kufanya mazungumzo na Rais Dk Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam alimthibitishia kuwa hana lengo la kufunga kiwanda chake kama inavyodaiwa badala yake anatafuta fursa nyingine za kuwekeza hapa nchini.

Katika kuthibitisha hilo, Mfanyabiashara huyo alisema jana meli yenye malori mapya 600 kwa ajili ya kusambazia saruji yake itawasili nchini. 

Aliongeza kuwa lengo la kufanyabiashara hapa nchini mbali na kutengeneza faida pia ana lengo la kuisaidia serikali ya Tanzania kutengeneza ajira hivyo hana sababu ya kuagiza mali ghafi toka nje ya nchi ambazo zinapatikana nchini.
 
Baada ya kufanya mazungumzo hayo, meli yenye magari hayo 600 ilitia nanga katika bandari ya Mtwara ambapo ndipo kiwanda cha Saruji cha Dangote kilipo.
 
Aidha, imeelezwa kuwa wiki ijayo meli nyingine kutoka Korea Kusini yenye malori 451 inatrajiwa kuwasili katika bandari ya mkoani Mtwara.
 
Hapa chini ni picha ya meli hiyo ikiwa bandarini Mtwara.

Picha 8: Christopher Ole Sendeka na viongozi wengine walivyoapishwa na Rais IKulu

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Christopher Olonyokie Ole -Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano), Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha  Balozi Grace Alfred Martin kuwa Mkuu wa Itifaki kutoka Wizara ya mambo ya Nje Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole-Sendeka.
 Viongozi walioapishwa waki weka saini katika viapo vya maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wakwanza kutoka kushoto ni Mkuu wa Itifaki Balozi Grace Alfred Martin, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mali asili na utalii Dkt. Aloyce Kashindye Nzuki, Katibu Mkuu Mawasiliano Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu Kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe pamoja na Mkuu wa mkoa wa Njombe Christopher Olonyokie Ole Sendeka.



Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) zitakazofanyika kitaifa mkoani Singida.

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Siku ya Maulid ya kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (S.A.W) ambayo kitaifa itaadhimishwa mkoani Singida.

Katibu wa Bakwata Mkoa wa Singida, Alhaji Buruhani Mlau alisema sherehe za Kitaifa za Maulid ya Mtume Mohammad (SAW) kwa mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Mkoani Singida katika Kijiji cha Shelui, wilayani Iramba, Singida.

Wiki iliyopita, akitangaza utaratibu wa sherehe hizo, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir alisema kwa mwaka huu, Maulid itasomwa usiku wa Desemba 11 na mapumziko yatakuwa siku inayofuata yaani Desemba 12. 

Mufti wa Tanzania aliwataka Waislamu wote nchini waadhimishe Siku ya Maulid kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu.

“Waislamu wanatakiwa kutumia siku hiyo kwa kufanya matendo mema na yenye kumpendeza Mwenyezi Mungu ikiwa ni pamoja na kufanya usafi kwenye mitaa yao na kuchangia damu ili kusaidia wenye uhitaji huo,” alisema.

Washindi wa EATV AWARDS 2016 hawa hapa

0
0

Historia imeandikwa kwenye tasnia ya sanaa nchini ambapo kwa mara ya kwanza tukio la utoaji wa tuzo za #EATVAwards kwa wasanii wa muziki na filamu Afrika Mashariki, limefanyika usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam. 
 
Tuzo hizo zilizoandaliwa na East Africa Television Ltd, zimekuwa za kwanza Afrika Mashariki, ambapo wasanii mbali mbali wamefanikiwa kujinyakulia tuzo zao.
 
Tazama orodha nzima ya washindi hapa chini..
 
Kipengele cha mwanamuziki bora wa kiume
G Nako – 'Original'
Sheta –'Namjua'
Mwana FA – 'Ahsanteni kwa Kuja'
Alikiba – 'Aje' --- MSHINDI
Ben Pol – 'Moyo Mashine'
 
Mwana muziki bora wa kike
Lilian Mbabazi – 'Yoola'
Ruby – 'Forever'
Lady Jay dee – 'Ndindindi' --- MSHINDI
Linah – 'No stress'
Vanessa Mdee – 'Niroge'
 
Mwanamuziki bora chipukizi
Manfongo – 'Hainaga ushemeji' --- MSHINDI
Feza Kessy – 'Sanuka'
Rukia Jumbe (Ruky Baby) – 'Mpasuo'
Bright – 'Nitunzie'
Mayunga – 'Nice couple'
 
Kundi bora la mwaka
Navy kenzo – 'Kamatia chini'--- MSHINDI
Mashauzi Clasic - 'Kismat'
Team Mistari – 'Tuzidi'
Sauti Sol – 'Unconditional bae'
Wakali wao – 'Chozi langu utalilipa'
 
Video bora ya mwaka
Njogereza – Navio
Namjua – Shetta
Aje – Alikiba -- MSHINDI
Don't Bother – Joh Makini
Ndindindi – Lady Jaydee
 
Wimbo bora wa mwaka
Don't bother – Joh Makini
Ndindindi - Lady Jayedee
Kamatia chini - Navy Kenzo
Moyo mashine – Ben Pol
Aje – Alikiba --- MSHINDI 
 
Filamu bora ya mwaka
Facebook profile
 
Safari ya Gwalu --- MSHINDI
Mfadhili wangu
Hii ni laana
Nimekosea wapi
 
Muigizaji bora wa kiume
Meya Shabani Khamisi
 
Salim Ahmed (Gabo) --- MSHINDI
Daudi Machael (Duma)
Doto Hussein Matotola
Said Mkukila
 
Muigizaji bora wa kike
Chuchu Hansy --- MSHINDI
Rachel Bithulo
Frida Kajala Masanja
Khadija Ally
 
TUZO YA HESHIMA
DJ Maarufu bongo Boniventure Kilossa (Dj Bonny Love) ndiye mtu aliyepewa tuzo maalum ya heshima, akitambuliwa kutokana na mchango wake kwenye tasnia ya sanaa hapa nchini

Mchungaji Awanywesha waumini dawa ya kuua bakteria “Dettol” ili Wapone Matatizo Yao

0
0
Mchungaji  maarufu kwa jina la Rufus Phala kutoka kanisa la AK Spiritual Christian lililopo Makgodu, Limpopo, Afrika Kusini amewashangaza watu kwa kitendo cha kuwanywesha  Dettol waumini wake ilihali ina madhara kwa binadamu.

Kwa mujibu wa Daily Sun SA, mchungaji huyo alifanya kitendo hicho kwenye ibada za kawaida kanisani kwake akiwataka waumini wenye matatizo na wanaohitaji maombi wanywe Dettol aliyokuwa ameishika mkononi mwake huku akiwambia watapona shida zao ikiwemo magonjwa.

“Nafahamu kuwa Dettol ni sumu, lakini Mungu ameniagiza niwape na muitumie. Mimi nilikuwa wa kwanza kuinywa,”  – Mchungaji.

Pia alisema kuwa amepokea meseji za WhatsApp kutoka kwa watu waliokunywa na wamethibitisha kupona. Baada ya kuwepo kwa taarifa hizo, amehojiwa Daktari kutoka Afrika Kusini, Dr Mabowa Makhomisane, ambaye amekiri kuwa Dettol ina madhara inapotumika tofauti na maelekezo ikiwemo kuinywa

“Mtu akinywa Dettol na ikafika tumboni, kimsingi hupunguza mzunguko wa hewa ya Oxygen mwilini. Hali hiyo ikitokea mtu anaweza kupoteza fahamu na kufariki.

 “Na kama mtu atatapika na bahati mbaya maji maji yakaingia kwenye mapafu yake, Detto itamsababishia ugonjwa wa Nimonia. Mapafu yatajikunja na mtu atashindwa kupumua”

Dr Makhomisane amewashauri watu waliokunywa dawa hizo waende Hospitali kupata vipimo ili kujua madhara waliyopata..

Watu 40 Wafariki kufuatia gari la kubebea mafuta kulipuka Nchini Kenya

0
0
Lori la mafuta limelipuka nje ya mji wa Nivasha nchini Kenya usiku wa Jumamosi December 10 2016 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40.

Taarifa iliyotolewa mapema leo December 11 2016 asubuhi na msemaji wa idara ya taifa ya mambo ya dharura nchini Kenya Pius Masai amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kwamba magari zaidi ya 11 yameteketezwa kwa moto katika barabara ya Nairobi-Naivasha.

Maafisa kutoka wizara ya usafirishaji wakiongozwa na Katibu mkuu wa wizara hiyo Irungu Nyakera wamewasili katika eneo la tukio na Taarifa zaidi zinaeleza kuwa watu wengi wamejeruhiwa na miongoni mwao ni watu waliokuwa wakirejea nyumbani kutoka harusini subukia.

Katibu mkuu  Irungu amesema kuwa kwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa ajali hiyo imetokana na dereva kutokufahamu vizuri barabara hiyo kutokana na kwamba lori hilo la mafuta ni la nchini Uganda.

TRA yamwadhibu mtumishi aliyemtolea mteja lugha chafu

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 101 & 102 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"John rafiki yangu, Sheila mke wangu, niwakate kate, kate vipande vigogo vidogo kama nyana. Au mufe kwa bomu hili, litakalo wachangua vipande vidogo vidogo"
Sheila badala ya kujibu, akaangua kilio likubwa kilichonifanya nimtandike ngumi nzito ya shavu, hadi taya ikapinda, huku meno baadhi yakianguka chini.

ENDELEA
"Ahaaaaa fu**"
John alijikuta akitukana kwa kitendo nilicho mfanyia mke wake. Sheila akaendelea kuangua kilio cha majuto sana.
"Nipe kisu"
Pretty akanipatia kisu chenye makali, John akabaki akiwa amenitumbulia mimacho, huku hakiema kwa woga. Nikamkita John kisu cha kwenye paja, la mguu wake wa kulia.

"Mamaaaa.."
John alilia kwa uchungu, ulio changanyika na maumivu makali.
"Ahaa kuna kitu nahitaji ukifanye kabla haujakufa"
Nilizungumza huku, nikikizungusha kusu kilicho zama kwenye paja lake, John akazidi kutoa mlio wa machozi.
"Kuna mali zangu, ulizo zichukua wewe na ulivyo mjinga ukaamua kumdhulumu Madam Merry. Sasa nazihitaji zote zirudi kwangu"

"Na....ru..disha"
"Sawa kama utazirudisha"
"E...ddy tusa...mehe"
Sheila alizungumza kwa sauti iliyo legea, kutokana na ukosefu wa meno yake mdomoni na kuvunjika kwa taya yake.
"Tena wewe usizungunze. Ni mwanamke gani usiye na huruma katika maisha yangu. Ulipanga kuniua mimi ili muchukue mali za mama yangu. Kwa bahati mbaya ukamuua Fredy. Mtu niliye fanana naye. Leo hii unasema kwamba niwasamehe"
Nilizungumza kwa hasira huku nikimtazama Sheila jinsi anavyo vuja damu.
"Nimezaliwa na roho ya kiatili, na sijawahi kumsamehe mtu abaye kwenda kinyume na mimi."
Nikachukua mkasi mkubwa kiasi. Nikashika kidole kimoja cha John na kukichomeka katikati ya mkasi.

"Ngoja ngoja usinikate nikuambie ukweli"
John alizungumza huku akiendelea kulia hadi makamasi yakaanza kumwagika puani mwake.
"Mali zote nilizo zichukua, kuma mtu ndio mmiliki kabisa na mimi ndio nilikua ninamsimamia"
"Nani?"
"Mzee Godwin na.....na yupo Oman, ndipo yalipo makazi yake"
Ikawa ni taarifa nyingine mpya kwani mzee Godwini ninavyo fahamu mimi amefungwa. Ila gereza alilo fungu ndio sikulifahamu.
"Mmmm kwahiyo, hajafumgwa yeye?"
"Haa....hajafumgwa na mtu aliye kua akishirikiana naye ni madam Mery"

Nikakaa kimya huku nikimtazama John usoni mwake. Sikuhitaji kumuonea huruma John hata kidogo. Nikakikata kidole chake kwa kutumia mkasi na lukitenganisha na vidole vinne vilivyo bakia kwenye mkono wake.
"Nahitaji namba za akaunti zako zote za benki"
"Ehee tena ngoja nichukue laptop"
Pretty alizungumza huku akitoka kwenye chumba tulichopo. Ptetty akarudi akiwa na laptop yake.
"Tunaweza kuzihamisha hizo popote pale kwenye akaunti ya benki"
Pretty alizungumza huku akiminya minya batani za laptop yake.

"Kwanza una akaunti ngapi?"
"Eheeee?"
"Hujanisikia eheee"
Nikachukua koleo, nikalichomeka kwenye sikio la John, la upande wa kushoto na kuanza kulibana taratibu.
"Nakuambia hiviiii, una akaunti ngapi za benki"
Nilizungumza kwa sauti ya kumnong'oneza John
"Tano tano"
John alijibu kwa sauti ya juu.
"Kumbe unanisikia vuzuri. Ila una ihakika ni tano?"
Nilizungumza huku nikiminya zaidi sikio lake
"Zipo saba, nyimgine ni....ni ni...."
"Ni..ni ni sizihitaji kuzisikia, una akaunti ngapi?"
"Kumi"
Nikajikuta nikicheka kwa maana kili ninavyo zidi kulibana sikio lake ndivyo kila alivyo zidisha kutaja idadi ya akaunti zake za benki.
"Tutajie namba ya akaunti na beki"
John akataja namba ya kwanza, huku akimwagikwa na machozi.

"Ni ya benki gani?"
Pretty alimuuliza, huku akiendea kuminya batani za laptop yake.
"Co-operative"
"Ya London?"
"Ndio"
"Yes Eddy, imesoma, tunaomba namba ya siri"
John akataja, Pretty akaiingiza na kusubiria kwa muda kidogo.
"Ohoo My God, Eddy njoo uone"
Nikaliachi sikio la John na kwenda alipo Pretty. Akanionyesha kiasi cha pesa kilichopo kwenye akaunti hiyo. Ambacho dola za limarekani bilioni kumi.
"Eheeee, John mwanangu, kumbe wewe nintajiri hivi. Ukiambiwa utakufa na kuziacha hizi"
   Nilizumgumza huku nikimcheka John, ambaye uhai wake upo mikononi mwangu. Nikamtajia Ptetty namba za akaunti yangu ambayo nahitaji wazihamishe pesa hiyo.

"Ohoo wanataja alama ya dole gumba la John ili waweze kudhibitisha kuzihamisha kwenda kwenye akaunti yako"
"Wanataka la upande gani, hilo dolr gumba?"
"Kulia"
Nikachukua mkasi wangu na kumfwata John alipo.
"Nina kazi na kidole chako"
"Eddy kikatie chini chini kidogo ili kifiti hapa"
Pretty aliniambia, John akanitumbulia mimacho akihisi kwamba sinto fanya hilo swala. Nikalikamata dole gumba la kulia na kulikata kwa nguvu. Sheila akatoa ukelele, kama yeye ndio aliye katwa.

"Kinacho kuliza na wewe? Nahisi hili tukio si geni kwako, kwani Derick yule malaya wako naye alikufa kama huyu"
  Nikakichukua kidole cha John na kwenda sehemu alipo kaa, Pretty.
"Kisuuze kwanza bwana, si unaona kimejaa damu"
Nikakisuuza vizuri kidole cha John kwa kutumia maji, nikampa Pretty akakiweka kwenye kifaa kingine, alicho chomeka waya wake kwenye laptop. Mwanga mwekundu ukapita kwenye kidole cha John,
"Hapo kinafanyaje?"
"Nina kiscan. Yes kimesoma"
Pretty akanionyesha, kidole kimefanana na alama ya dole gumba iliyopo kwenye benki hiyo.
"Sasa pesa hapa tunaweza kuihamisha"

Pretty akaanza kufanya, kazi ya kuhamisha pesa hiyo kwenye akaunti yangu.
"Asilimia zinakwenda taratibu?"
"Kwa nini?"
"Pesa nyingii hii"
Kama robo saa, pesa, yote ikawa imekamilika luhamishiwa kwenye akaunti yangu. John akaendelea kututajia akaunti zote anazo zimiliki na zote zina pesa nyinhi tu. Pesa nyingine nilimpa ruhusa, Pretty akazihamishia kwenye akauti yake.

Hadi inafika majira ya saa kumi jioni, tukawa tumelikamilisha zoezi zima la kumfilisi John kwenye maakaunti yake ya benki.
"Vifo vyenu nahitaji viwe vya taratibu mno"
Nilizungumza huku nikinywa juisi, aliyo nipa Pretty, hii ni baada ya kukaa kwa muda mrefu pasipo kula chocho.
"Eddy nisamehe kaka, kwani haya yote niliyafanya kwa tamaa"
"Ahaaa tamaaa?"
"Pretty ile video ya mauaji ya Victoria iweke mtandaoni, kila mtu ajionee ukatili wa huyu mjinga"

"Sawa bosi"
Pretty akamuonyesha John, ile vodeo jinsi alivyo muua Voctoria, John akabaki akitokwa na machozi mengi. Sheila naye akabaki akikodoa mimacho, hata kuzungumza alishindwa kutokana na taya kuvunjika.
"Una jengine la kuzungumza?"
John akatingisja kichwa kwamba hana la kuzungumza. Nikachomoa bastola, kiunoni mwangu. Nikaifunga kiwambo cha kuzuia sauti.
"Yupi awe wa kwanza kufa?"
Hakuna aliye nijibu zaidi ya woye kukaa kimya. Nikampiga John risasi za miguu, kwenye magoti, kisha nikachukua kishoka kidogo cha kukatia nyama. Nikakata viganja vyake vya mikono yote miwili.

  Yote niliyo yafanya Pretty na Sheila waliyashuhudia kwa macho yao mawili. John alilia kwa uchungu mkubwa huku akiniomba nisimuue ila sikumpatia msamaha wa aina yoyote. Nikamgeukia Sheila na kumtazama kwa macho yaloyo jaa chuki na hasira kali.

"Ed.."
Sheila aliniita, kabla hajamaliza kuliita jina langu, nikampiga risasi tano za kifuani mwake, nikachukua bomu, lakutega. Nikaliweka mbele ya John huku nikiwa nimelitega dakika tano lilipuke.
"Kifo hichi ndicho unacho stahili John"
Nikamaliza kumpiga John risasi za miguu yake yote, hadi nilipo hakilisja hatoweza kusimama wala kulishika bomu hilo, kwani hana tena viganja vya mikono.

Tukatoka na Pretty hadi nje, Pretty akachukua gari lake jengine na tukaliacha gari tulilo kuja nalo, kuepuka kukamatwa na polisi. Tukaondoka eneo la nyumbani, hatukufika mbali sana nyumba nzima ikalipuka huku John na mwili wa Sheila vikiwa ndani.
"Eddy inabidi ukatubu kwa Mungu wako"
Pretty alizungumza huku akiendelea kuendesha gari kwa kasi. Tukaingia kwenye barabara ile tuliyo pita jana, iliyo nyooka. Tukaingia mjini majira ya saa mbili usiku, ambapo tukaelekea moja kwa moja hotelini.
Nikafika chumbani kwangu na kuchukua kila kilicho changu, nikarudisha funguo kwa wahusika
Nikatoka nje na kumkuta Ptetty akinisubiri ili anisindikize uwanja wa ndege. Nikaingia ndani ya gari na tukaondoka eneo la hotelini.

Habari Zilizopo Katika Magazet ya Leo Jumatatu ya Disemba 12

Maalim Seif Aivaa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)

0
0

Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amesema uamuzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wa kutaka pande zinazovutana ndani ya chama hicho kuteua kwa pamoja jina la mgombea ubunge katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Dimani kuwa ni wa kukurupuka. 

Desemba 8, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Ramadhani Kailima alisema fomu za wagombea wa CUF katika uchaguzi huo zitapaswa kusainiwa na pande mbili zilizo na mgogoro wa uongozi.

“Kipengele cha 4 (5) (iii) cha Sheria ya Uchaguzi kinataka fomu za wagombea kwenye chama chenye mgogoro zisainiwe na viongozi wakuu wote wawili kwa vile wamethibitishwa na Msajili wa Vyama Siasa,” alinukuliwa Kailima.

Lakini juzi, Maalim Seif alizungumzia uamuzi huo wa NEC na kusema kila chama cha siasa kina kanuni na taratibu zake za kuwapata wagombea wa nafasi mbalimbali.

“NEC wamenishangaza kwa sababu nchi inaendeshwa kwa sheria na kanuni labda nimuulize Kailima ameitazama Katiba ya CUF inasema nini kuhusu mchakato wa wagombea? Tume inatoa uamuzi wa kisiasa ambao haukupaswa kutolewa na chombo hiki muhimu,” alisema Maalim Seif.

Hata hivyo, licha ya kushangazwa na hatua hiyo, Maalim Seif hakuwa tayari kutoa msimamo wa CUF juu ya suala hilo akisema: “Ni mapema mno kusema tutafanya nini?”

Tayari Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui amesema lengo la NEC ni kutaka chama hicho kikose mgombea. 

Wakati Maalim Seif akieleza hayo, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa alisema:

“Tutaweka utaratibu na watu wajitokeze ili tuweze kufanya uteuzi wa mgombea. Ingawa kulikuwa na mgombea wa mwaka jana, nina imani watajitokeza wengine na Baraza Kuu ndilo litamteua.”

Alisema uchaguzi kwa ngazi udiwani hakuna tatizo kwa sababu mchakato wake unaishia wilayani, lakini kwa ubunge lazima wakae pamoja.

CUF imekuwa katika mgogoro baada ya Profesa Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti mwaka jana kuibuka na kutaka kurejea kwenye nafasi hiyo, lakini viongozi wengine wakamuwekea ngumu na kuibua mgogoro uliopo mahakamani.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images