Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

NEC yatangaza ratiba ya chaguzi ndogo za Ubunge na Madiwani

$
0
0
Na Eliphace Marwa – MAELEZO
TUME ya Taifa ya Uchaguzi imetangaza ratiba ya uchukuaji wa fomu za kujaza nafasi zilizo wazi ya Mbunge na Madiwani katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Imesema kuwa inatarajia kuendesha Uchaguzi Mdogo katika Jimbo la Dimani , Mkoa wa Mjini Magharibi ,Tanzania Zanzibar kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Tume hiyo, hatua hiyo itanatokana na vifungu vya 37(1)(b) na 46(2) vya sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 na Vifungu vya 13(3) na 48(2) vya Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura 292.

Aidha ,Tume hiyo pia itaendesha Uchaguzi Mdogo wa kujaza nafasi za wazi za Udiwani katika kata 22 kwenye baadhi ya Halmashauri za Tanzania Bara zilizokuwa wazi kutokana na sababu mbalimbali.

Imezitaja Kata hizo Ng’hambi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Ihumwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma, Kiwanja cha Ndege ya Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Igombavanu na Ikweha za Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa pamoja na Ngarenanyuki iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mkoani Arusha.

Kata nyingine ni Kijichi ya Halmashauri ya Manispaa ya Temeke Mkoani Dar es Salaam, Kata ya Kinampundu ya Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida, Isegehe ya Halmashauri ya Mji wa Kahama Mkoani Shinyanga, Kasansa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi, Malya na Kahumulo Mkoani Mwanza, Maguu na Tanga Mkoani Ruvuma pamoja na Kata ya Kimwani Mkoani Kagera.

Imeongeza kuwa Kata nyingine ni pamoja na Nkome Mkoani Geita, Kata ya Lembeni Mkoani Kilimanjaro, Mkoma ya Mkoani Mara, Duru ya Mkoani Manyara, Mwamtani ya Mkoani Simiyu, Misugusugu ya Mkoani Pwani pamoja na Mateves ya Mkoani Arusha.

Tume hiyo imesema kuwa zoezi la kutoa fomu za uteuzi litaanza Desemba 10 hadi 22 na kufuatia kwa zoezi la uteuzi wa wagombea siku ya tarehe 22 mwezi Desemba na Desemba 23 hadi Januari 21 mwakani itakuwa ni kipindi cha kampeni ambapo Januari 22 mwakani itakuwa siku ya kupiga kura.

Picha: Machinga Waanza Kurudisha Vibanda Vyao Makoroboi Mwanza

$
0
0
Jana Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli alitoa agizo kwa watendaji wa Mkoa wa Mwanza kusitisha mara moja zoezi la kuwaondoa wafanyabiashara wadogo Machinga katikati ya mji.

 Baada ya agizo la Rais tayari kwenye eneo la Makoroboi Mwanza machinga wameanza ujenzi wa vibanda kwenye maeneo yao ya biashara

Rais Magufuli Aongoza Kikao cha Barazs la Mawaziri Ikulu Dar es Salaam

$
0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika leo tarehe 07 Desemba Ikulu jijini Dar es Salaam. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. PICHA NA IKULU

Mameja Jenerali Wapya Wavishwa Vyeo Vyao Makao Makiu ya JWTZ

$
0
0
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (kushoto) akimvisha cheo cha Meja Jenerali Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa Brigedia Jenerali Michael Isamuhyo, Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (Kushoto), akimvisha cheo cha Meja Jenerali,Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali George William Ingram,Makao Makuu JWTZ Upanga Dar es Salaam.

Rais Magufuli afanya mabadiliko kwenye Mikoa na Wizara......Amteua Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 07 Desemba, 2016 amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja na Mkuu wa Mkoa mmoja na pia amefanya mabadiliko madogo katika Wizara na Mikoa kama ifuatavyo;

Dkt. Magufuli amemteua Prof. Faustin Kamuzora kuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.Kabla ya uteuzi huo, Prof. Kamuzora alikuwa Katibu Mkuu Mawasiliano.

Rais Magufuli amemteua Mhandisi Mathew Mtigumwe kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo. Mhandisi Mathew Mtigumwe anachukua nafasi ya Dkt. Frolence Turuka ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Frolence Turuka alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi aliyekuwa akishughulikia Kilimo. Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Job Masima ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Rais Magufuli amemteua Dkt. Maria Sasabo kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na atakuwa akishughulikia Mawasiliano. Dkt. Maria Sasabo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Faustin Kamuzora ambaye ameteuliwa Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais.

Pia Rais Magufuli amemteua Mhandisi Angelina Madete kuwa Naibu Katibu Mkuu Katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Mhandisi Angelina Madete anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Maria Sasabo aliyeteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Mawasiliano.

Aidha, Rais Magufuli amemteua Dkt. Aloyce K. Nzuki kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Christopher Ole Sendeka kuwa Mkuu wa Mkoa wa Njombe.Bw. Christopher Ole Sendeka anachukua nafasi ya Dkt. Rehema Nchimbi ambaye amehamishwa kituo cha kazi na kuwa Mkuu wa Mkoa wa Singida.

Dkt. Rehema Nchimbi anajaza nafasi iliyoachwa na Mhandisi Mathew Mtigumwe ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Uvuvi na Mifugo anayeshughulikia Kilimo.


Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Dkt. Osward J. Mashindano kuwa Msajili wa Hazina.

Dkt. Osward J. Mashindano anachukuwa nafasi ya  Bw. Lawrence Mafuru ambaye atapangiwa kazi nyingine

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasilino ya Rais, IKULU
Dar es Salaam


07 Desemba, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 8

Taarifa kutoka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuhusu wanafunzi wanaotakiwa kujiunga na Operesheni Magufuli Awamu ya Pili.

Taarifa kuhusu sherehe ya maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9, Desemba 2016.


Ufafanuzi Wa Taarifa Zilizoandikwa Na Baadhi Ya Magazeti Juu Ya Mgogoro Wa Tanzania Na Malawi Kwenye Ziwa Nyasa

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UFAFANUZI WA TAARIFA ZILIZOANDIKWA NA BAADHI YA MAGAZETI JUU YA MGOGORO WA TANZANIA NA MALAWI KWENYE ZIWA NYASA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Afrika Mashariki inapenda kufafanua na kuweka sawa taarifa zilizoandikwa kwenye baadhi ya Magazeti ya tarehe 07 Desemba, 2016 kuwa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwenye Ziwa Nyasa unakaribia kuiva na kwamba Mgogoro huo unatarajiwa kumalizwa na washauri wa kimataifa.

Taarifa hiyo haikuwa sahihi. Ukweli ni kuwa, mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kwa sasa upo chini ya Jopo la Viongozi Wastaafu wa Afrika wanaotokea kwenye nchi za Ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo  Kusini mwa Afrika (SADC). Jopo hilo linaongozwa na Mhe. Joachim Chissano, Rais Mstaafu wa Msumbiji akisaidiwa na Mhe. Festus Mogae, Rais Mstaafu wa Botswana na Mhe. Thabo Mbeki, Rais Mstaafu wa Afrika Kusini.

Aidha, Jopo hili ambalo liliundwa na Umoja wa Afrika kupitia Jukwaa la Viongozi Wastaafu wa Afrika (Forum for Former African Heads of State and Government) kwa ajili ya kusuluhisha mgogoro huu, linaendelea na kazi hiyo kwa kupitia taarifa mbalimbali na maandiko yaliyowasilishwa kwao na Tanzania na Malawi. Vile vile, Jopo lilikwisha zikutanisha pande zote mbili katika mashauriano ya awali yaliyofanyika nchini Msumbiji

Wizara inapenda kuujulisha umma kuwa licha ya kuwepo kwa mgogoro wa mpaka wa Tanzania na Malawi katika Ziwa Nyasa, mahusiano ya nchi hizi mbili yamezidi kuimarika siku hadi siku katika Nyanja zote za kiuchumi, kisiasa na kijamii. Hata wananchi wa pande zote mbili za Ziwa wameendelea kuishi kwa amani na ushirikiano wa karibu.

Aidha, katika kuimarisha uhusiano huu, Tanzania na Malawi zinatarajia kuwa na mkutano wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano mapema mwakani. Mkutano huu utawaleta watalaam wa nchi hizi mbili kutoka Sekta mbalimbali kwa lengo la kujadili changamoto za ushirikiano katika sekta hizo, kubaini maeneo mapya ya ushirikiano pamoja na kuweka mikakati ya kutekeleza miradi ya pamoja itakayokubaliwa baina ya pande hizi mbili.

Pamoja na mambo mengine, Mkutano huo unatarajiwa kujadili masuala ya ushirikiano katika sekta za biashara na uwekezaji, usafirishaji, fedha, nishati, utalii, ulinzi na usalama uhamiaji, uvuvi na ardhi.

Hivyo, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inawaomba Waandishi wa Habari, Wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla inapohitajika kupata taarifa sahihi za suala hili kwenda kwenye Mamlaka husika na kuziandika kwa usahihi kwa ustawi wa nchi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 07 Desemba, 2016.

Mawakili Wajitosa Tena Kumtoa God bless Lema Gerezani

$
0
0
Licha ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), kuwataka mawakili wake wasijihusishe na chochote baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kufuta rufaa yake, mawakili hao wamepeleka maombi kuiomba mahakama hiyo kumpa mteja wao muda wa kupeleka notisi ya kusudio la kukata rufaa.

Kutokana na hali hiyo, Lema anatarajiwa kufikishwa mahakamani hapo ili kujua hatima ya maombi ya rufaa yake.

Desemba 2, mwaka huu, mahakama hiyo ilifuta rufaa ya mbunge huyo kutokana na kukatwa nje ya muda, huku mawakili wake wakitakiwa kuwasilisha kusudio la kukata rufaa ndani ya siku 10.

Hatua hiyo ilikuja baada ya uamuzi wa maombi ya marejeo ya mwenendo na uamuzi wa mahakama ya chini kutupwa na Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha na Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Sekela Moshi, Novemba 11, mwaka huu.

Wakili wa Lema, Sheck Mfinanga, jana alisema wamepeleka maombi mahakamani hapo wakiiomba impe mteja wao muda wa kupeleka notisi ya kusudio la kukata rufaa na kusikiliza rufaa hiyo ya maombi ya dhamana.

“Tumepeleka maombi mahakamani ili impe Lema muda wa kupeleka notisi ya kusudio la kukata rufaa na kusikiliza rufaa yake. Maombi hayo yanatarajiwa kusikilizwa na Jaji Dk. Modesta Opiyo,” alisema Mfinanga.

Lema ambaye anashikiliwa kwa zaidi ya mwezi mmoja katika Gereza Kuu la Kisongo, mjini Arusha, alikamatwa Novemba 2, mwaka huu, nje ya viwanja vya Bunge mjini Dodoma na kufikishwa mahakamani mjini Arusha, Novemba 8, mwaka huu, akikabiliwa na mashtaka ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, Angero Rumisha, alisema mahakama hiyo imeifuta rufaa hiyo kwa sababu wakata rufaa waliikata nje ya muda.

Kutokana na sababu hizo, mahakama hiyo ilikubaliana na pingamizi la awali lililowasilishwa na mawakili wa Serikali, Paul Kadushi na Matenus Marandu, walioomba mahakama hiyo isisikilize rufaa hiyo kwa sababu imekiuka matakwa ya sheria, yanayotaka kutolewa kwa kusudio la kukata rufaa kabla ya rufaa yenyewe.

Novemba 28, mwaka huu, rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa kwa Jaji Mfawidhi wa mahakama hiyo, Fatuma Masengi, lakini ilishindikana baada ya mawakili wa Serikali kuweka pingamizi.

Kwa mujibu wa mawakili hao, mawakili wa Lema walikuwa wamekiuka matakwa ya sheria yanayowataka kutoa notisi ya nia ya kukata rufaa badala ya kukata rufaa yenyewe.

Katika shauri hilo, Lema anawakilishwa na mawakili Adam Jabir, John Mallya, Sheck Mfinanga na Faraji Mangula wakati upande wa Jamhuri unawakilishwa na Kadushi na Marandu.

Mzee wa Miaka 76 Aja na Sharti Jipya la Mke Anayemtaka ........Kazi Kwenu Wanawake!

$
0
0
MZEE Athuman Mchambua (76), ambaye ameweka tangazo nyumbani kwake la kutafuta mke, ameongeza sharti jipya kwa mke anayemuhitaji.

Amesema licha ya kupokea simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali nchini, lakini amewataka wanawake ambao atawafanyia usaili, hasa kwa yule ambaye atakuwa ameshinda, kutobweteka kwani atakuwa katika kipindi cha mpito cha ndoa yake.

Mzee huyo amelieleza gazeti la Mtanzania  kuwa amefikia hatua hiyo ili kuanza kupitia majina ya wanawake zaidi ya 30 ambao tayari wamejaribu bahati ya kuolewa naye.

Alisema kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuweka tangazo hilo kwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaojitokeza hushindwa kukidhi vigezo anavyovihitaji.

Alivitaja vigezo sita muhimu vya mwanamke anayemuhitaji kuwa ni awe mcha Mungu na mwenye kutunza watoto wake.

“Vigezo vingine awe na sifa ya ndoa, awe na sifa ya mume, awe na sifa ya kilimo, awe na sifa ya kutunza watoto na awe na sifa ya usafi wa hali ya juu.

“Tangu kuanza nimepata wanawake zaidi ya 30 ambao wanne kati yao wamefika hapa nyumbani kwangu, lakini wengine wamekuwa wakiona aibu kuja hapa moja kwa moja na hivyo wamekuwa wakitumia simu. Leo (jana) nimewafanyia usaili wanawake watano kwa simu, lakini hakuna hata aliyefuzu nusu ya vigezo, wengi wamekuwa wakiteleza sifa ya kilimo,” alisema.

Magari zaidi ya mawili likiwepo basi la New Force yamegongana leo asubuhi jijini Mbeya

$
0
0
Ajali ya barabarani imetokea leo asubuhi eneo la Igurusi mkoani Mbeya ikiwa imehusisha basi la abiria mali ya Kampuni ya New Force, malori mawili ya mizigo na gari jingine dogo.Basi hilo la abiria hufanya safari zake kati ta Tunduma na Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi bado halijatoa taarifa kuhusu chanzo cha ajali hiyo na kama kuna watu waliofariki  kutokana na ajal hiyo.

CHADEMA wataka Rais Mkapa anyang’anywe shamba kama Sumaye

$
0
0
Meya wa Manispaa ya Ubungo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (CHADEMA), Boniface Jacob amemtaka Rais Dk Magufuli kulichukuwa shamba linalomilikiwa na Rais Mstafuu Mzee Benjamin Mkapa kama alivyofanya kwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye.

Meya huyo alisema kuwa kiongozi huyo wa zamani na familia yake wanamiliki shamba kubwa katika wilaya ya Ubungo ambalo halijaendelezwa kwa muda mrefu sasa.

Meya huyo ambaye amekuwa Diwani wa Ubungo kwa muda mrefu ametaa shamba hilo lililopo Mbezi, Dar es Salaam lirejeshwe kwenye halmashauri ili liweze kufanyiwa shughuli nyingine.

Hoja hiyo ya Meya wa Kinondoni imekuja siku chache tangu aliyekuwa Waziri Mkuu katika serikali ya awamu ya tatu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Frederick Sumaye aliponyang’anywa shamba lake eneo la Mabwepande ambalo hajaliendeleza kwa muda.

Meya alitoa maelezo hayo alipokuwa akizungumza na gazeti la mwananchi ambapo alisema kuwa watamuandikia Rais Magufuli barua wakimuomba abatilishe umiliki wa shamba hilo aipe Manispaa ya Ubungo ambayo ndiyo kwanza imeanzishwa.

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Afanya Mazungumzo Na Waziri Mkuu Wa Ethiopia

$
0
0
Rais Mstaafu na Kamishna wa Kamisheni ya Umoja wa Mataifa ya Kugharamia Fursa ya Elimu Duniani (UN Education Commission on Financing Global Education Opportunity) amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mheshimiwa Haile Mariam Desale alipomtembelea ofisini kwake jijini Addis Ababa, Ethiopia.
 
Katika nafasi yake ya Mjumbe Maalum wa Kamisheni hiyo, Rais Mstaafu amemkabidhi Waziri Mkuu wa Ethiopia Ripoti ya Kamisheni hiyo yenye mapendekezo ya namna Dunia inavyoweza kukabili janga la Elimu kwa kuwekeza katika Mpango wa Kizazi cha Elimu (A Learning Generation). 

Mpango huo unalenga kuleta mapinduzi makubwa ya Elimu katika nchi zinazoendelea ndani ya Kizazi Kimoja (miaka 30). Azma kuu ya Mpongo huo ni kuwezesha ifikapo mwaka 2040, watoto wote kote duniani wawe wanaopata elimu iliyo bora na kwa kiwango kinachofanana dunia nzima.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kwa sasa, hali ya elimu katika nchi zinazoendelea inalingana na ile ambayo nchi zinazoendelea zilikuwapo miaka 70 iliyopita. Aidha, ripoti inasisitiza kuwa, ikiwa nchi zinazoendelea zitaendelea kwa kasi ya sasa, itazichukua nchi hizo kati ya miaka 90 na 110 kufikia viwango vya sasa vya nchi zilizoendelea.
 
Kwa ajili hiyo, Kamisheni inapendekeza njia mpya na bora za kufanya mageuzi katika elimu ikiwemo kuongeza usimamizi, kupanua fursa, kuingiza ubinifu na teknolojia na kuongeza uwekezaji katika elimu kwa kushawishi ushiriki wa Jumuiya ya Kimataifa na Sekta Binafsi. Iwapo mapendekezo hayo yatatekelezwa, nchi zinazoendelea zinaweza kufikida pengo hilo ndani ya miaka 30 ijayo.
 
Rais Mstaafu ameiomba Ethiopia kujiunga na Mpango huo ambapo Waziri Mkuu wa Ethiopia ameelezea nia ya nchi yake kujiunga na Mpango huo. 

Ethiopia ni moja kati ya nchi za Afrika ambayo imepiga hatua kubwa katika utoaji wa fursa ya elimu kwa watoto na vijana wake. Pamoja na mafanikio makubwa bado zipo changamoto zinazohitaji hatua madhubuti ili kufikia lengo la kizazi cha elimu ifikapo 2040.
 
Ziara ya Rais Mstaafu itamfikisha katika nchi 14 barani Afrika ambapo zimechaguliwa katika awamu ya kwanza ya mpango huo. Tayari amekwishazitembelea nchi za Uganda na Malawi na kufanya mazungumzo na viongozi wakuu wa nchi hizo.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 99 & 100 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"Yes mpango umekwenda vizuri kama nilivyo panga"
John alionekana akiwa amefurahi sana kwa habari hiyo. Iliyo onyeshwa kwenye kituo hichi cha habari. Hii ni baada ya muandishi huyo kudai kwamba ndege hiyo ilikuwa ikitokea nchini Brazili, kwenda bara la Afrika. Abiria wote waliomo ndani ya ndege hiyo wamekufa kwenye mlipuko huo wa ndege ulio tokea majira ya mida hii ya mchana, jambo lililo nipa wasiwasi mwingi, hadi nikajihisi mwili mzima kuishiwa na nguvu.

ENDELEA
  Pretty akamtazama John kwa umakini huku akionekana kuwa na mshangao mkubwa.
"Unafurahia nini?"
"Kuna mpango niliupanga na vijana wangu, kuhusiana hiyo ndege"
"Unataka kusema wewe umehusika kwenye mpango wa hiyo ndege kulipuka?"
Pretty alimuuliza John huku akimkodolea macho ya wasiwasi. Mimi hata nguvu ya kunyanyuka kwenye kochi sikuwa nayo hii yote ni kwakuiwazia familia yangu.

"Ndio"
"Kwanini?"
Kuna mjinga nilimuua, sasa ulikua muda wakuiteketeza famia yake"
Nikastukia kumuona Pretty akinyanyuka kwa hasira na kumrukia John, hadi sofa alilo likalia wakaaanguka nalo. Sheila akasimama kwa haraka na kumchomoa Pretty aliyekuwa akimshambulia mumewe kwa kumpiga kwa makofi mfululizo.
"Wewe ni gaidi"
Pretty alizungumza kwa hasira, huku mimi nikiwa nimepigwa na bumbuazi lililo nifanya nishindwe kufanya kitu cha aina yoyote.
"No no nakudanganya Pretty"
John alizungumza huku akicheka.
"Muongo wewe"
"Kweli Pretty siwezi kufanya kitu kama hicho. Kwanza nitaanzia wapi. Eti Henry kweli ninaweza kufanya jambo hili?"
Nilitabasamu tu, hata kinywa changu kikashindwa kufunguka. Tangu nizaliwe sijawahi kukumbana na hali ya mshangao kama hii, iliyo nimaliza nguvu zote.

Pretty akafungua mlango na kutoka huku akiubamiza kwanguvu. Jambo lililo nistua na kurudi kwenye hali yangu yakawaida. Nikanyanyuka kwa haraka na kumfwata Pretty ndani kwake
"Nilazima nimpeleke polisi nikamstaki"
Pretty alizungumza kwa hasira huku akiingia chumbani kwake. Nikamfwata na kumkuta akiwa amekaa kwenye kitanda huku akilia.
"Pretty nisikilize, kitu kimoja"
"Nahitaji zile video mbili kama una flash zihifadhi sawa"
Pretty alibaki akiwa amenikodolea macho. Nikatoa simu mfukoni na kuingiza namba za Blanka. Ikaita kwa muda mrefu, kisha ilapokelewa.
"Blanka wamefika?"
"Hawajafika"
Jibu la Blanka likanifanya nizidi kuchanganyiliwa, hadi mwili ukawa unanitetemeka kwa woga kwani swala la akufiwa nafamilia tena kwa wakati mmoja, sikuliwazia kichwani mwangu.
"Hawajakupigia?"
"Hapana hawajanipigia"

Nikakata simu nakushusha pumzi kubwa, nikabaki nimesimma pasipo kuzungumza kitu chochote na Pretty. Nikamshika mkono Pretty na kumnyanyua juu.

"Twende kwangu"
"Kufanya nini?"
"Twende tu"
Tukatoka sebleni, Petty akaziingiza video zote mbili kwenye flash, kisha akachukua begi lake lenye laptop.
Tukaondo hadi nyumbani mwangu. Kitu cha kwanza nikaifwata simu ya chumbani kwangu. Nikamiinya kitufe cha kusikiliza ujumbe wa sauti, ili kutambua kama kuna ujumbe wowote wa suti ulio ingia nikiwa sipo.
"Eddy mume wangu, mbona hupokei simu?"
Ilikuwa nisauti ya Phidaya, kwenye ujumbe wa kwanza wasauti
"Tumeamua kubadilisha safari, tupo Marekani kwa sasa. Shamsa ndio alitoa pendekezo la sisi kubadilisha safari. Ukipata ujumbe huu usiwe na wasiwasi, tupo salama na kesho tunakwenda Tanzania. Nakuupenda mume wangu"

Ujumbe wasauti, ukawa umekwisha. Nikashusha pumzi nyingi, huku tabasamu pana likiwa usoni mwangu. Nikatoka sebleni na kumkuta Pretty akiwa anaminya minya batani za laptop yake.
"Unafanya nini?"
"Nachapisha habari za kumchafua John kwenye mtandao na kuituma hii video ya mauaji"
"Hapana usifanye hivyo"
"Kwanini?"
"Nataka kumuua John taratibu"
"Kumuua taratibu!?"
"Ndio"
Nikaanza kumuadisia historia nzima ya maisha yangu. Kuanzia nilivyokua shule na John hadi leo ni adui yangu.
"Sasa kwanini hutaki tumuue sasa hivi?"
"Pretty mpango wangu ni mrahisi sana. Nataka kumuua kwa kifo chakumzalilisha na kumtesa sana."
"Ila familia yangu ipo salama"
"Kweli?"
"Ndio"
Pretty akanikumbatia kwa furaha, huku machozi yakimwagika kwani historia yangu ilimuuzunisha sana.

Siku ya pili, tukakutana na John na Sheila wakiwa kwenye maandalizi. Ikamlazimu Pretty kuwaomba msamaha kwa kile kilicho jitokeza jana mchana. Hii ikiwa ni moja ya mpango wetu wa kumteketeza John na Sheila, pasipo wao kujua chochote.
"Nilijua tu nihasira, mimi nimemsamehe"
John alizungumza huku akimpa mkono Pretty.
Ikawa ni furaha kubwa sana kwa John, na Sheila wake. Wakiamini urafiki wetu utaendelea kama kawaida na laiti wangejua wasinge ruhusu kujipendekeza kwetu.
               ***
  Siku ya harusi ya John ikawadia, mimi na Pretty tukawa nimiongoni mwa waalikwa kwenye sherehe hii ndani ya kanisa hili kubwa la Roman katolic.
"Kila kitu umekipanga sawa?"
Nilimuuliza Pretty mara baada ya kufika kanisani, tukishuka kwenye gari yetu aina ya BMW, tulilo linunua jana kwa kazi moja tu iliyopo mbele yetu.
"Kila kitu kipo powa mpenzi"
Kabla sijazunguza chochote simu yangu ikaita kwa namba ya Blanka, ndio inayo nipigia.
"Nipigie bwana"
Blanka alizungumza kwa furaha, ikanibidi nikate simu na kumpigia.
"Ndio kaka Eddy. Kweli wewe nikiboko"
"Kwanin?"
"Yaaani toto lako nikopi na wewe yaani umefanya kazi kubwa kulitafuta"
"Kwani wamefika?"
"Ahaaa ndio nipo hapa uwanja wa ndege nimewapokea yaani weee acha tuu. Ninafuraha yakufa mtu"
"Hembu mpe Junio simu nizungumze naye"

"Dady tumefika Tanzania"
"Umemuona antie?"
"Ndio, ila kuna joto kali"
"Poleni mwanangu, mpe mama simu"
Nikasikia sauti ya Junio ikimuita Phidaya, furaha ikazidi kuongezeka moyoni mwangu, nakujiamini zaidi kwamba kazi yangu inazidi kuwa nyepesi zaidi.
"Mume"
"Niambie mke wangu"
"Safi, tumesha fika Tz yaani hapa nijoto"
"Sasa hivi nisangapi?"
"Saa.....saa tano inakwenda saa sita usiku"
"Poleni kwa uchovu"
"Yàani wee acha tu, yaani tumetoka Marekani jana alfajiri, tunashukuru Mungu ndege tuliyo panda haikupita kwenye nchi nyingi"
"Ilikuwaje mukaenda Marekani?"
"Hilo swali muulize mwanao Shamsa"
"Mpe simu"
"Vipi wewe"
"Ahaaa safi baba"
"Hembu sogea pembeni uniambie nini kilitokea?"
"Wee acha baba, kipindi tupo uwanja wa ndege kuna jamaa nilikua ninamtilia mashaka, sasa tulipo maliza kukaguliwa. Kipindi sasa tunaelekea kupanda basi lile linalo wapeleka watu kwenye ndege"


Rais Magufuli akutana na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan Kusini

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuia ya Afrika ya Mashariki na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  Alhamisi ya tarehe 08 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mke wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Nyandeng Garang de Mabior.

Baaada ya mazungumzo hayo,Mke huyo wa Mwanzilishi wa Taifa la Sudan ya Kusini Rebecca Mabior amesema yeye pamoja na ujumbe wake wamelazimika kufika nchini Tanzania kuonana na Rais Dkt Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuia ya afrika ya Mashariki kwa lengo la kumfahamisha hali halisi ya nchi ya Sudan ya Kusini.

Amemuomba Rais Dkt Magufuli na viongozi wenzake wajumuia ya Afrika ya Mashariki kulisaidia Taifa la Sudan ya Kusini kutafuta suluhisho la mgogoro unaolikabili taifa hilo na kurejesha amani.

"Tumefarijika kuwa hapa katika ikulu ya Tanzania na tuko hapa kumsihi Rais Dkt Magufuli kama Mwenyekiti wa jumuia ya Afrika ya Mashariki akishirikiana na viongozi wenzake wa jumuia hiyo kuona namna gani wanaweza kutusaidia ili Taifa la Sudani ya Kusini liwe Taifa lenye amani,hivyo hapa tunawakilisha vilio vya watu wa nchi yetu na kikubwa tunachokitaka ni Amani katika nchi yetu na hiki ndio kilio chetu"

Rais Magufuli kwa upande wake amewasihi viongozi na wananchi wa Sudan ya Kusini kutafuta njia muafaka ya kumaliza tofauti zao kwa njia ya amani na ili kuepuka machafuko yanayosababisha mateso kwa wananchi wa Taifa hilo.

"Mama Rebecca hata mimi binafsi naumizwa na kile kinachoendelea katika nchi ya Sudani ya Kusini hivyo,ningezisihi pande zote zinazotofautiana kumaliza tofauti zao kwa amani kwa mustakabali wa maendeleo ya Taifa la Sudani ya Kusini"

Emmanuel Buhohela
Kaimu Mwandishi wa habari Msaidizi wa Rais.
Dar es Salaam

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Ijumaa ya Disemba 9

Serikali Yaweka Pingamizi Tena Maombi ya Godbless Lema Kupewa Dhamana

$
0
0

Jana, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, ilishindwa kusikiliza maombi ya kuongezewa muda wa kuwasilisha notisi ya kukata rufaa ya kupinga kuzuiwa kwa dhamana ya Lema. 

Mawakili wa Serikali waliomba muda wa kuwasilisha hoja za kupinga maombi hayo. 

Maombi hayo, yaliyotarajiwa kusikilizwa jana na Jaji Dk Modesta Opiyo yalikwama kutokana na kusudio la pingamizi lililowekwa na mawakili waandamizi wa Jamhuri katika shauri hilo, Paul Kadushi na Maternus Marandu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya Jaji Opiyo kuahirisha kusikiliza maombi hayo, Wakili wa Lema, Sheck Mfinanga alisema mawakili wa Serikali, wameomba wapewe muda kuwasilisha kiapo kinzani dhidi ya maombi hayo.

 Alisema Jaji Opiyo alitumia busara kutoa uamuzi kuwa mawakili wa Jamhuri wawasilishe hoja hizo, Desemba 13 na upande wa utetezi utazijibu siku hiyo hiyo na uamuzi utatolewa Desemba 14, saa 6.00 mchana.

Jana Lema hakufika mahakamani, kwa kile kilichoelezwa kuchelewa kupelekewa hati ya kufikishwa mahakamani.

Lema anaendelea kushikiliwa baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kupinga uamuzi wa hakimu mkazi, Desdery Kamugisha aliyempa dhamana Lema katika kesi namba 440 na 441/2016 ya kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Lema anatuhumiwa kuwa kati ya Oktoba 23 hadi 26, mwaka huu alitoa kauli za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli katika maeneo tofauti katika mikutano yake ya hadhara.

Miongoni mwa kauli za Lema ni: “Nchi itaingia katika machafuko kama haitafuata misingi ya katiba na sheria na pia Rais Magufuli asipobadilika” 

Lema pia akiwa katika uwanja wa shule ya Sekondari Baraa alitoa kauli kuwa: “Kiburi cha Rais akiendeea kujiona yeye ni Mungu, hatafika 2020, Mungu atakuwa amechukua maisha yake, Rais ni mbabe…”

Sakata la Kuuawa kwa Faru John Lachukua Sura Mpya.......Watumishi Watano Watiwa Mbaroni

$
0
0

Maofisa watano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) wanaotuhumiwa kushiriki kumwondoa faru John kutoka katika Creta hiyo walikamatwa juzi kwa mahojiano ili kujua ukweli kuhusu mazingira ya kupotea kwake. 

Hatua ya maofisa hao kukamatwa imekuja siku tatu baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuituhumu menejimenti, wafanyakazi wa NCAA na Baraza la Wafugaji (NPC) kuwa imejaa vitendo vya rushwa na wizi na asingeweza kuvumilia sakata la faru John ambaye alisema kuwa aliuzwa kwa Sh200 milioni kwenye Hoteli ya Grumet iliyo Hifadhi ya Serengeti na kuwa walipokea fedha za awali Sh100 milioni. 

Waziri Mkuu alisema anataka kumwona faru huyo, nyaraka za kumhamisha na kama amekufa basi apelekewe hata pembe ofisini kwa kuwa anajua pa kuzipeleka. 

Alisisitiza kuwa ikibainika kuna ambao wamekiuka taratibu watawajibika. 

Habari za uhakika kutoka Ngorongoro, ambazo zimethibitishwa na Jeshi la Polisi zinasema kuwa maofisa hao watano wanashikiliwa katika kituo chao cha Ngorongoro kutokana na ushiriki wao kwa njia moja au nyingine. 

Wanaoshikiliwa ni pamoja na Israel Naman ambaye alikuwa Kaimu mkuu wa idara ya uhifadhi wakati faru huyo akiondolewa. 

Wengine ni Cuthbert Lemanya, ambaye alikuwa Mkuu wa Kanda ya Creta, Dk Athanas Nyaki ambaye anadaiwa kumdunga sindano ya usingizi ili aweze kubebwa. 

Maofisa wengine waliokamatwa ni aliyekuwa Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka ya Ngorongoro, Kuya Sayaleli na aliyekuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Ikolojia, Patrice Mattey. 

Ofisa mmoja wa NCAA, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina lake jana alisema maofisa hao walikamatwa juzi jioni na jana walikuwa wanaendelea kuhojiwa. 

“Tuiache serikali ifanye kazi kwani ni muhimu sana kujulikana ukweli wa tukio hili,” alisema ofisa huyo. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakupatikana jana kuelezea tukio la kukamatwa maofisa hao, baada ya simu yake kupokelewa na msaidizi wake ambaye alieleza yupo kwenye kikao. 

Lakini, ofisa wa mmoja wa polisi, ambaye aliomba kuhifadhiwa jina kwa kuwa si msemaji alikiri kukamatwa maofisa hao kwa mahojiano. 

Chanzo cha sakata 
Akiwa katika ziara ya kikazi Ngorongoro, Waziri Majaliwa aliibua sakata la kuhamishwa kinyemela faru huyo na kudaiwa kupelekwa Grumet. 

Waziri mkuu alitaka ukweli kuhusu upotevu wa John aliyeondolewa Creta na kupelekwa Grumet na kudaiwa kufa huku taarifa za kifo hicho zikifanywa siri. 

Waziri Mkuu alitaka kupewa nyaraka zote zilizotumika kujadili kumuondoa faru na kuamua kumpeleka Grumet. 

Waziri Mkuu alitoa hadi Desemba 8 (jana) awe amepata taarifa zote, ikiwamo ya daktari inayothibitisha kifo hicho na kwamba pembe za faru huyo zifikishwe ofisini kwake. Pia, Majaliwa alisema ikibainika wapo waliokiuka taratibu watawajibika. 

==>Msikilize Waziri Mkuu Alipokuwa  akiongea
 

LIVE: Tazama Hapa Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru Kutoka Uwanja wa Uhuru Jijini Dar. Mgeni Rasmi ni Rais Magufuli

$
0
0

Tazama  Hapa  Sherehe za Miaka 55 ya Uhuru  Kutoka Uwanja wa Uhuru Jijini Dar. Mgeni Rasmi ni Rais Magufuli
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images