Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Pata Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kuondoa Michirizi, Kuongeza Unene, Kuondoa Chunusi na Zingine Nyingi Toka Beauty Cosmetics

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS Ni wauzaji wa vipodozi aina mbali mbali na vyenye matokeo mazuri na ya haraka zaidi bila kemikali wala madhara yoyote
 
     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @90,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @120,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 120,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 90,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 100,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @100,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
12.kuotesha nywele kwenye kipara @100,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=
 
     WASILIANA NASI KWA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti ili kuhakikisha mafanikio yako
 
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Lowassa: Fidel Castro ni shujaa wangu wa dunia

$
0
0
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Edward Lowassa amesema kuwa aliyekuwa Rais wa Cuba na mwana mapinduzi wa nchi hiyo, Fidel Castro alimhamasisha kuingia katika uongozi.

Ameyasema hayo alipotembelea ubalozi wa Cuba hapa nchini kutoa pole na kusaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Castro kilichotokea Novemba 25 mwaka huu jijini Havana nchini Cuba.

Lowassa amesema Marehemu Castro alikuwa mwana mapinduzi na ni miongoni mwa wanasiasa waliomhamasisha kuingia kwenye uongozi kutokana na alivyokuwa akiwatetea masikini na wanyonge duniani, hali ambayo imelisababishia taifa hilo dogo kuogopwa kutokana na uimara wake.

“Castro alikuwa kiongozi imara sana,kila kiongozi makini lazima awe  kinara wa kuwatetea wanyonge na masikini popote walipo”alisema Lowassa.

Lowassa amesema kuwa Castro aliifanya Cuba pamoja na udongo wake uitikise dunia kwa kuwa kila mahali ukienda ni lazima utasikia jina la Castro.

Mzee wa Upako: Tajeni nilikunywa pombe gani na Katika Baa Gani

$
0
0
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo ‘Mzee wa Upako’ baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake ameendelea kujibu madai hayo kwa mtindo wa ‘kudonoa donoa’ na jana aliwataka wanaodai kuwa alilewa siku hiyo wataje alikunywa pombe gani na katika baa gani. 

Wiki mbili zilizopita, taarifa kwenye vyombo vya habari zilisema kwamba Mchungaji Lusekelo alikwaruzana na majirani zake huku akidaiwa kuwa alikuwa amelewa jambo ambalo lilifanya achukuliwe na kuhojiwa na polisi. 

Lakini, tangu kuibuka kwa tukio hilo alikataa kulitolea ufafanuzi licha ya kutafutwa na vyombo vya habari, hata pale alipohudhuria ibada kanisani kwake aliwaambia waumini wake hatalizungumzia na badala yake alidonoadonoa baadhi ya matukio. 

Alipokwenda kanisa kwake kwa mara ya kwanza Novemba 25, Mchungaji Lusekelo alisema; “Kuna kitu nilikuwa nataka nikiseme, lakini sitakisema ili waendelee kusema haohao waliokuwa wanasema.Wakawaulize wenyewe. Nimeyaona magazeti hapa, ooh Mzee wa Upako, ooh Mzee wa Upako, sisemi. Sasa leo yupo hapa, na kwa taarifa yao watashindana sana, lakini hawatashinda. Hii ni kama kumpiga chura teke.”

Lakini, Novemba 28, Mchungaji huyo akajibu baadhi ya hoja akisema kwanza, maneno aliyotumia ambayo ni mshenzi, mpumbavu na mjinga siyo matusi kwani yameandikwa kwenye Biblia. Pili, watu hao ndiyo walianza kumtukana yeye baada ya kuwauliza wanatafuta nini eneo la getini kwake.

 Hoja nyingine alisema watu hao hawakuwa jirani zake kama inavyodaiwa kwani mtaani kwake wanaishi kama majambazi kutokana na mazingira ya kutofahamiana. 

Jana, Mchungaji Lusekelo akiwahubiria waumini wake alidonoa tena eneo jingine linalohusiana na tukio hilo, kwamba wanaodai alikuwa amelewa pombe, waeleze alikunywa pombe gani na baa gani. 

Akikaribishwa kwa wimbo wa kuabudu uitwao, ‘Nina haja nawe’ kabla ya kuanza kumtunza kwa sadaka, Mchungaji Lusekelo alisema watu wanaotuhumu kuwa alilewa, wanatakiwa kueleza alikunywa pombe gani na alikunywa akiwa eneo gani. 

“Wiki iliyopita nilikuwa Wizara ya Mambo ya Ndani, baadhi ya maofisa wakaniona , wewe Mzee wa Upako… Mzee wa Upako, askari mmoja akaniuliza wewe Mzee wa Upako unachukua sadaka halafu unaenda kunywa pombe. Nikawauliza, hiyo pombe nilikunywa wapi, halafu pombe zipo za aina nyingi, taja ni pombe gani, ukienda mbali zaidi ungeuliza nililewa nini, maana hata upako wa roho mtakatifu ni ulevi,” alisema. 

“Lakini kuna majina ya watu, mitaani inaitwa pombe, sasa sijui ni pombe gani hiyo….watashindana sana. Lakini kushindana siyo tatizo, je, mtashinda? Eti oooh hayo maneno tu hata kwenye kanga yapo, subiri tusiandikie mate na wino upo, ukitaka kummaliza Mzee wa Upako we mpige risasi tu,” alisema huku akishangiliwa na waumini wake.

 Alisema hakuna mwanadamu atakayeweza kumwangusha kwa kipawa na kalama Mungu aliyompatia. 

“Ndiyo maana unapojiita mtume leo unakuwa unajirusha kwenye harakati ambazo zilijengwa na baba zetu, ndiyo maana kumshinda shetani ni lazima, kuna mfumo umejengwa na mfumo huu uko imara kama chuma cha pua,” alisema. 

Katika ibada ya wiki iliyopita, mchungaji huyo alisema taarifa zinazosambazwa kumchafua hazitamvunja moyo wa kuendelea kufanya kazi ya uchungaji, huku akihoji kwanini magazeti yanaandika mabaya pekee na hayaandiki habari za uponyaji anaofanya kanisani kwake.

Yusuf Manji Atii Sheria Bila Shuruti......Alipewa saa 24 kuondoka kwenye jengo la PSPF Plaza (Quality Plaza)

$
0
0
Mfanyabiashara Yusuph Manji jana alitii sheria bila shuruti kwa kuhama kwenye jengo la Quality Plaza akitekeleza amri ya Mahakama ya kumtaka kurejesha jengo hilo ambalo ni mali ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF). 

Mbali na kutekeleza amri ya kuhama baada ya kupewa notisi ya saa 24 iliyomalizika juzi, pia anatakiwa kulipa malimbikizo ya deni la pango la Dola za Marekani 6.1 milioni (zaidi ya Sh13 bilioni), ambazo kama asipozilipa mali zake zitakamatwa. 

Hatua hiyo imekuja baada ya Mahakama Kitengo cha Ardhi kutoa hukumu ya kumtaka Manji kuondoka kwenye jengo hilo pamoja na kuilipa deni la pango. 

Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo, Manji ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi. 

Viongozi wa kampuni za Manji waliokuwa wakisimamia uondoaji wa vifaa uliomalizika jana asubuhi, walikataa kuzungumza na waandishi wa habari waliofika kufuatilia tukio hilo. 

Tangu juzi chini ya usimamizi wa kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart, Manji na kampuni zake walikuwa wanaondoa vifaa mbalimbali vilivyopo kwenye jengo hilo na kuhitimisha shughuli hiyo jana.

Meneja Uendeshaji wa Yono Auction Mart, Atukuzwe Mhugo alisema kampuni ambazo walikuwa wakizisimamia kuondoa vifaa ni Quality Group Co Ltd, Gaming Managemeti Ltd, Q Consult Ltd na Quality Logistics Co Ltd.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo ya Yono, Scholastica Kenyela alisema tayari wameshaziondoa kampuni za Manji kwenye jengo hilo. 

Kenyela alisema mteja wao ambaye ni PSPF alichukua uamuzi huo baada ya Manji kushindwa kulipa kodi ya pango ya zaidi ya Sh13 bilioni. 

“Sisi tumetimiza wajibu wetu, ukienda pale utaona tayari tumeshafanya kazi yetu kwa sababu alipewa notisi ya saa 24 awe ameondoka,” alisema.

Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi alisema masuala yote yanayohusiana na jengo hilo kwa sasa yako chini ya Yono Auction Mart. “Sipo Dar es Salaam na sitazung- umzia chochote kuhusu jengo hilo wenye mamlaka ni Yono naomba uwatafute wao,” alisema.

Waziri Mkuu afanya ziara ya kushtukiza katika Hospitali ya Mount Meru.....Akerwa na Msongamano Katika Wodi ya Wazazi

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana alifanya ziara ya kushtukiza katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru ambako kulikuwa na tuhuma za kuibwa watoto, lakini alishuhudia wazazi watatu wakilala kitanda kimoja. 

Ziara hiyo ilitokana na taarifa alizolalamikiwa na wananchi juzi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, kwamba hospitali hiyo ina matukio ya wizi wa watoto wachanga. 

Hata hivyo, jana baada ya kufika katika hospitali hiyo, Majaliwa alishuhudia msongamano katika wodi ya wazazi na kuagiza kuboreshwa hospitali za pembezoni. 

Majaliwa aliagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha wanaondoa changamoto za ongezeko la wagonjwa na kuboresha huduma katika hospitali hiyo. 

Akizungumzia sakata ya kupotea kwa watoto katika hospitali ya mkoa alivitaka vyombo husika kuendelea na uchunguzi kwa kuwa suala hilo tayari lipo mikononi mwa vyombo vya dola. 

Wiki mbili zilizopita mzazi, Walda Mussa alisema kuwa alijifungua mtoto katika hospitali hiyo lakini hadi alipotoka hakumpata.

“Nilikuja hapa hospitali Oktoba 4 na Oktoba 7 nikajifungua kwa upasuaji wakamchukua mtoto na kumpeleka chumba cha joto, akaja mume wangu akaenda kumuona mtoto mzima, siku ya pili alienda kumuona mtoto pia akiwa mzima lakini siku ya tatu, tulipokwenda wote mimi na mume wangu tuliambiwa mtoto alifariki na hatujawahi kuona mwili wake,” alisema mwanamke huyo hivi karibuni. 

Mganga Mkuu mfadhiwi wa hospitali ya Mkoa Mount Meru, Dk Jackline Urio alipotakiwa kuelezea sakata hilo, alisema kuwa mtoto huyo baada ya kuzaliwa alifariki dunia na baadaye mwili ulipelekwa chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali hiyo. 

Mwanafunzi wa darasa la 5 Ajinyonga

$
0
0

Mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Kizota mjini Dodoma, Yasin Abdallah (13) amekutwa amejinyonga bafuni nyumbani kwao baada ya kuchukizwa kufanya vibaya kwenye masomo yake. 

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Ernest Kimoli alisema tukio hilo lilitokea Desemba 2 eneo la Kizota Relini Manispaa ya Dodoma. 

Kimoli alisema baba mzazi wa mtoto huyo, Hassan Juma (53) aligundua kujinyonga kwa mwanaye saa 6:00 mchana.

“Sababu ya kujinyonga ni kuchukizwa na matokeo ya mitihani yake,” alisema. 

Diwani wa Kizota, Jamary Ngalya alisema mtoto huyo ambaye alizikwa juzi jioni, alianza kwa kuwaeleza wanafunzi wenzake Ijumaa kuwa atajinyonga. 

Alisema baada ya kutamka maneno hayo, wenzake walimwambia wanakwenda kumweleza mwalimu. Hata hivyo, baada ya kuwasikia wenzake aliwaambia kuwa anatania hawezi kufanya hivyo. 

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kizota, Juma Malecela alisema mwanafunzi huyo alihamia Oktoba kutoka mkoani Kigoma. 

“Katika matokeo ya kumaliza darasa la nne alikuwa wa 129 kati ya 132, inawezekana huko alikuwa anafanya vizuri,” alisema.

Waziri Mkuu: Kampuni Za Watumishi Zisipewe Zabuni Ndani Ya Halmashauri Wanazozitumikia

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Bi. Theresia Mahongo kuhakikisha kampuni zinazomilikiwa na madiwani na watumishi wa halmashauri hiyo hazipewi  zabuni zinazotolewa katika maeneo yao kwa ajiliya  kuepusha migongano ya kimaslahi.

Ametoa agizo hilo leo (Jumatatu, Desemba 5, 2016) wakati akizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Karatu mkoani Arusha katika ukumbi bwalo la  Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Karatu akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa.

"Hauzuiliwi kufanya biashara ili mradi kampuni yako isifanye kazi katika halmashauri ambayo wewe unaitumikia na una nguvu nayo ili kuepusha migongano ya kimaslahi kwani miradi yote utajilundikia," amesema.
Pia amewataka Wakuu wa Idara katika halmashauri hiyo walisaidie Baraza la Madiwani katika kubaini vyanzo vipya vya mapato kwa lengo la kuongeza mapato ya halmashauri yao.

Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka watumishi wa halmashauri wa umma  kujitathmini na kujiridhisha kama wanafuata misingi ya utumishi katika utendaji kazi wao wa kila siku. Amewasisitiza  wawatumikie wananchi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.

"Hatuhitaji kuwa na mtumishi mvivu, asiyewajibika, mwizi, mla rushwa na asiyekuwa muadilifu mahali pa kazi.Na  atakayeona ameshindwa kutunza na kusimamia fedha za miradi ya maendeleo ya wananchi atoe taarifa hatutaki watu kufanya kazi kwa mazoea," amesema.

Waziri Mkuu ameongeza kuwa " watumishi wa umma lazima mbadilike na muwe na nidhamu ya kazi. Muache malalamiko fanyeni kazi na msitafute  sympathy (huruma) kutoka kwa watu kwani Serikali haitamuonea mtumishi yeyote ," amesema.

Amesema katika baadhi ya ofisi za Serikali kuna ugonjwa wa watumishi wanapoona wageni wamelifika kwa ajili ya kupatiwa huduma wanawapita bila ya kuwasikiliza. " sasa hatutaki watumishi wa namna hiyo, Jukumu lako ni kumtumikia Mtanzania na tunataka kuona mabadiliko. Hatutaki kuona watu wakizubaa maofisini,".

Waziri Mkuu amesema Serikali ikikuta wananchi wanalalamika kutokana na kutoridhishwa na  huduma zitolewazo na watumishi wa umma itahakikisha watumishi hao wanachukuliwa hatua. Serikali ni ya Watanzania wote hivyo lazima wahudumiwe vizuri bila ya kujali uwezo wao kifedha wala itikadi zao za kidini na kisiasa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATATU, DESEMBA 5, 2016.

Rais Magufuli akutana na Mkurugenzi wa Mauzo wa Kamupuni ya Ndege wa Boeing ....Asema Serikali itanunua ndege 4 pia aagana na Balozi wa Cuba & Mwakilishi wa AfDB

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 05 Desemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Masoko ya Afrika wa Kampuni ya utengenezaji wa ndege ya Boeing yenye makao yake nchini Marekani Bw. Jim Deboo ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kununua ndege kubwa kutoka kampuni hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Doto James.

Baada ya Mazungumzo hayo Rais Magufuli amesema Serikali yake ya Awamu ya Tano imedhamiria kununua ndege nyingine nne zikiwemo ndege kubwa 3 ambazo zitasaidia kuinua uchumi wa nchi kwa kuwezesha watalii kuja hapa nchini moja kwa moja kutoka nchi zao.

"Sisi hapa tunazungumza kuwa watalii hawajafika hata milioni 2 kwa mwaka, lakini nchi kama Morocco inapata watalii zaidi ya milioni 12 kwa mwaka, hii yote ni kwa sababu hatuna mashirika ya ndege ya kwetu, watalii wakitaka kuja hapa ni lazima waje kwa kuungaunga, wafikie nchi nyingine halafu ndipo wapate moyo wa kuja huku, licha ya kwamba sisi Tanzania ni miongoni mwa nchi 5 duniani zenye maeneo mazuri yenye utalii.

"Kwa hiyo niwaombe tu Watanzania wapende mali zao, kwa sababu wakati mwingine nikiangalia mitandao na magazeti ni ajabu huwezi kuamini kama hao ni Watanzania, unakuta wanasifia tu ndege za watu wengine na wanazibeza za kwao" amesisitiza Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli ametaja aina ya ndege mpya ambazo Serikali itazinunua kuwa ni ndege 1 aina Bombardier Q400 Dash 8 NextGen inayotarajiwa kufika nchini Mwezi Juni 2017, ndege 2 aina ya Bombardier CS300 zenye uwezo wa kuchukua kati ya abiria 137 na 150 na zinazotarajiwa kuwasili nchini kati ya Mei na Juni, 2018 na ndege moja aina ya Boeing 787 Dash 8 Dream Liner yenye uwezo wa kuchukua abiria 262 na inayotarajiwa kuwasili nchini Juni, 2018. Malipo ya awali kwa ndege hizi yameshafanyika.

Dkt. Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi hizi za Serikali zenye lengo la kuinua utalii na kuimarisha uchumi wa nchi.

"Tumeleta ndege aina ya Bombardier hapa, zimepunguza gharama za safari mfano kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza, sasa wanalipa kati ya 160,000/ hadi 200,000/- wakati nauli ilishafika Shilingi laki 8 na kitu, lakini watu wengine utakuta wanazungumzazungumza wee maneno ya hovyo kwa kutumiwa, tumeshaamua na tutafanya hivyo" amesisitiza Rais Magufuli.

Wakati huo huo, Rais Magufuli ameagana na aliyekuwa Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika hapa nchini (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero ambaye amepandishwa cheo na kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Ukanda wa Kusini mwa Afrika katika ofisi zake zilizopo Afrika Kusini.

Rais Magufuli amemshukuru Dkt. Tonia Kandiero kwa juhudi kubwa alizozifanya akiwa Mwakilishi Mkazi wa AfDB hapa nchini ambapo miradi mikubwa na muhimu katika maendeleo imetekelezwa na inaendelea kutekelezwa.

Akizungumza baada ya kuagana na Rais Magufuli Dkt. Tonia Kandiero amemshukuru Rais Magufuli na Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano alioupata katika kipindi cha miaka 6 aliyokuwa hapa nchini na amesema anaondoka akiwa ameiwezesha Tanzania kupiga hatua kubwa ya kimahusiano na AfDB ambapo miradi yenye thamani ya Dola za Kimarekani Bilioni 2 imetekelezwa hususani katika ujenzi wa miundombinu ya barabara.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Cuba hapa nchini Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo anayemaliza muda wake baada ya kuiwakilisha nchi ya Cuba kwa miaka minne.

Rais Magufuli amemshukuru Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo kwa uhusiano na ushirikiano mzuri aliouendeleza kati ya Tanzania na Cuba uliojengwa na waasisi Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Mhe. Fidel Castro wa Cuba

Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo amemshukuru Rais Magufuli na Serikali kwa kuendeleza uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Cuba na amesema anaondoka akiwa anaamini kuwa uhusiano kati ya nchi hizi utaendelea kuwanufaisha wananchi ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo na huduma za kijamii.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
05 Desemba, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitazama kitabu cha  picha ya ndege aina ya Boeing 787-8 Dream liner wakati alipokuwa akisikiliza maelezo yake kutoka kwa Mkurugenzi wa mauzo wa kampuni ya Ndege ya Boeing Jim Deboo. Ndege hiyo itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 262 na itakuwa na uwezo wa kuruka kutoka nchini Marekani hadi Tanzania bila kutua mahali popote.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Balozi wa Cuba anayemaliza muda wake hapa nchini George Luis Lopez Tormo Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo. Dkt. Tonia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ukanda wa Kusini Mwa Afrika katika Ofisi zake zilizopo Afrika ya Kusini


Unaikubali Simu Yako Ya Tecno? Shinda Safari Ya Uingereza Ukajiachie Na Supastaa

$
0
0
Kampuni ya simu ya Tecno hii leo imezindua kampeni ya Christmas ambayo inawawezesha wateja wake kujishindia tiketi za safari ya kuzuru nchini Uingereza katika kampeni inayokwenda kwa jina la #KamaMbele. 

Uzinduzi huu ni katika jitihada za Tecno kuwapatia wateja wake zawadi katika msimu huu wa Sikukuu za Christmas na Mwaka Mpya na kuwawezesha kununua simu bora kwa gharama nafuu hivyo kuwawezesha kufurahia pamoja. 

Mwadada mrembo anayeng’arisha video za mastaa wa Bongo (Video Vixen), Hamisa Mobetto na Mshindi wa Big Brother Africa – Hotshots mwaka 2014, Idris Sultan ni mabalozi wa kampeni hii ambapo mmoja wao ( Idris au Hamisa) atashinda safari ya Uingereza akiambatana na shabiki mmoja.
 
Jinsi ya kushiriki ni kwamba mteja ataingia kwenye tovuti ya shindano ambayo ni http://tecnokamambele.co.tz/ atapiga kura kwa supastaa moja kati ya Idris au Hamisa kisha ataeleza kwanini anaikubali Tecno yake akitumia hashtag #KamaMbele na shabiki mshindi atapatikana kutokana na kura zitakazopigwa na mashabiki katika hatua ya pili ya shindano. 

Mbali na kujishindia safari ya kwenda nchini Uingereza, wateja wa Tecno na Watanzania kwa ujumla wataweza kujishindia zawadi mbalimbali na kupata punguzo la bei katika simu za Tecno. 
 
Tazama video hii na ingia http://tecnokamambele.co.tz/ kumpigia kura Idris Sultan uwe kwenye nafasi ya kuibuka mshindi wa Safari. 


Endapo ungependa kusafiri na Hamisa Mobeto tazama video hii kisha ingia http://tecnokamambele.co.tz/ kumpigia kura. 
Tembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi.
 
 
 

Taarifa Ya Ufafanuzi Kutoka Tra Kuhusu Mizigo Ya Wama

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Disemba 6

Dar es Salaam Yashika Nafasi Ya 6 Barani Afrika Kwa Maambukizi Ya Ukimwi

$
0
0
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO.
Mbali na jitihada za makusudi za Serikali na wadau wa mapambano dhidi ya UKIMWI nchini bado hali siyo ya kuridhisha ambapo Jiji la Dar es Salaam linashika nafasi ya Sita barani Afrika kwa maambukizi ya ugonjwa huo.

Dar es Salaam ambalo ni Jiji kubwa kuliko yote Tanzania linakadiriwa kuwa na watu 210,000 wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambapo kati yao asilimia 58 ni wanawake, na kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 idadi ya wakazi wa jiji hilo inakadiriwa kuwa Milioni 5.
 
 Kwa mujibu wa taarifa ya hali ya UKIMWI duniani kutoka Shirika la Mpango wa UKIMWI la Umoja wa Mataifa - Tanzania (UNAIDS) kwa mwaka 2015, Jiji la Dar es Salaam limekuwa kati ya majiji Barani Afrika yenye kiwango kikubwa cha maambukizi ya UKIMWI.

Afisa wa UNAIDS Tanzania, Fredrick Macha anasema asilimia 16 ya maambukizi yote mapya Tanzania Bara yanatokea katika jiji la Dar es Salaam ambapo kwa wanawake wenye umri mdogo wa miaka 15-24 kiwango cha maambukizi kimefikia asilimia 7%,sababu kubwa ikiwa ni kujiingiza katika ngono wakiwa na umri mdogo pamoja na biashara ya ukahaba.

Anafafanua kuwa maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto Jijini Dar es Salaam ni asilimia sita (6%) licha ya jitihada kubwa za Serikali na wadau mbalimbali wa mapambano dhidi ya UKIMWI,kuelimisha na kuhamasisha wajawazito kupima na kufuata ushauri wa kitaalamu wa jinsi ya kujikinga na VVU.
 
“Takwimu za Wizara ya afya za mwaka (2011-2012), mtu mmoja kati ya watu watano jijini Dar es Salaamana mahusiano ya kimapenzi na zaidi ya mtu mmoja,na mara nyingi wanafanya ngono zisizo salama hivyo hicho ni kiashiria kikubwa cha ongezeko la maambukizi hasa kwa wana ndoa”alisema Macha.
 
 Aidha amevitaja baadhi ya vichocheo na viashiria vinavyochangia uwepo wa ongezeko kubwa la maambukizi katika jiji hilo kuwa ni ukuaji wa kasi wa shughuli za kiuchumi na kibiashara unaosababisha muingiliano wa watu kutoka Mikoa mbali mbali nchini pamoja na mataifa mengine.
 
Dar es Salaam kama yalivyo majiji mengine duniani yenye muingiliano wa tamaduni na desturi mbalimbali limeathirika pia na makundi yanayoelezwa kuchochea maambukizi mapya ya UKIMWI kama vile wafanya biashara ya ngono, wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja na watumiaji wa madawa ya kulevya na kwa kujidunga.
                                                                                     
“Kwa mujibu wa takwimu hizo, kati ya wanawake 4 wanaojihusisha na biashara ya ngono, mmoja ni mwaathirika na virusi vya UKIMWI (sawa na asilimia 26).Vile vile kati ya watu watano wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja, mtu mmoja ameathirika, sawa na asilimia 22.3) na kati ya watu sita wanaotumia madawa ya kulevya kwa njia ya kujidunga sindano, mmoja ni mwathirika wa virusi vya UKIMWI (sawa na asilimia 15.5),”alisema Macha.
 
 Aidha Macha alisema pamoja na changamoto mbalimbali, Jiji la Dar es Salaam limependekezwa kuwa moja ya majiji machache ya mfano ulimwenguni katika mkakati wa dunia wa kuimarisha udhibiti wa UKIMWI kwenye majiji (UNAIDS Fast Track Cities Initiative).
 
 Mkakati huo ni kuyafanya majiji makubwa Afrika kuwajibika zaidi katika kuongeza ufanisi kwenye mapambano dhidi ya UKIMWI katika maeneo ya mijini kwani kasi ya maambukizi na wingi wa maambukizi yapo mijini.
 
 Pamoja na majiji kuwa na rasilimali nyingi, mifumo ya utoaji huduma za afya bado inaandamwa na changamoto mbalimbali, hususani katika kuandaa na kutekeleza mipango mizuri yenye kuhakikisha ushirikishwaji wa watu wote hasa makundi maalumu katika jamii, ambayo kiwango cha maambukizi ni kikubwa.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama anasema takwimu zilizopo sasa zinaonyesha kuwa asilimia 6.2 ya wanawake  nchini wameambukizwa ugonjwa wa ukimwi ikilinganisha na asilimia 3.8 ya wanaume,jambo ambalo linahitaji jitihada zaidi kujikinga.

“Kwa mujibu wa Utafiti wa Viashiria vya Virusi vya UKIMWI (VVU) na Maralia (THMIS) wa mwaka 2011/2012 kwa upande wa Tanzania Bara vinaonyesha kuwa idadi kubwa ya wanawake wameambukizwa ugonjwa huo kuliko wanaume.

Waziri Mhagama anasema kuwa kutokana na utafiti huo, maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa upande wa Tanzania Bara ni asilimia 5.3 na inakadiriwa  kuwa  jumla ya watanzania 1,538,382 wanaishi na VVU ambapo vijana wenye umri kati ya 15-24 ni asilimia 10.6 na watoto walio chini ya miaka 15 ni 11.8.

Aliongeza kuwa UKIMWI bado ni janga kubwa nchini Tanzania kwani takwimu zinaonyesha kuwa  maambukizi mapya yanakadiriwa kufikia watu 48,000 kwa mwaka hali ambayo  inaashiria kupoteza  nguvu kazi kubwa katika nchi yetu hivyo Tanzania itendelea kushirikiana na nchi nyingine Duniani,pamoja na mashirika ya kupambana na UKIMWI kuhakikisha janga hilo linatokomezwa  ifikapo mwaka 2030.

Alisema Serikali inaendelea kuwahamisha wananchi waendelee kujitokeza kupima afya zao kwa hiari ili wajitambue na kujua namna ya kujilinda kwani Shirika la Afya Duniani (WHO) linasisitiza nchi wanachama kuwaanzishia dawa mara moja watu wote watakaopima na kugundulika kuwa na VVU,bila kusubiri hadi kinga zao zipungue.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS), Dr. Leonard Maboko alisema kuwa kwa mwaka 2015 walioambukizwa VVU walikuwa Watanzania 2,100,000 ambayo ni idadi kubwa ukilinganisha na idadi ya sasa lakini  pamoja na kushuka kwa idadi hiyo wananchi wanatakiwa kuendelea kujilinda mara dufu.

”Ingawa maambukizi ya VVU yameshuka kutoka Watanzania 2,100,000 hadi 1,538,382, Watanzania hatutakiwi kubweteka bali tunatakiwa tufanye jitihada za pamoja kuhakikisha janga hili linafikia mwisho,”alisema Dr. Maboko.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu alisema wataalam wa afya wametuambia UKIMWI unapungua nchini Tanzania, suala hilo linatokana na misaada mbalimbali tunayoipata kutoka nchi wahisani  kwahiyo ili kutokomeza kabisa suala la upungufu wa dawa na misaada kwa waathirika wa ugonjwa huo Watanzania wanahitaji kujichangia wenyewe na sio kutegemea fedha za wahisani peke yake.

Alifafanua kuwa ili kuwezesha suala hilo,Sheria Na. 5 ya mwaka 2015 imeitaka Wizara yenye dhamana kuwa na Mfuko wa Udhamini wa UKIMWI pamoja na Bodi yake hivyo, kuanzishwa kwa Mfuko huo kutaleta chachu kwa Watanzania kuungana kuzuia maambukizi mapya ya Virusi vya UKIMWI (VVU) pamoja na kuwahudumia wananchi wanaoishi na virusi hivyo.
 
 “Kwa kawaida fedha zinazotoka kwa wahisani huwa zina mwisho wake hivyo Tanzania tunazindua Bodi rasmi itakayosimamia Mfuko huo ili na sisi tuongeze nguvu pale wahisani watakapoishia,”alisema Mama Samia.
 
 Naye muathirika wa UKIMWI, (jina limehifadhiwa) ameishkuru Serikali kwa kuwasaidia kwa hali na mali watu wenye ugonjwa huo kwani sio wote wenye ugonjwa huo wameupata kwa kujitakia.
 
 “Kitendo hiki kinatufanya tusijione wanyonge wala kukata tamaa kwani Serikali yetu haitutengi inatupa ushirikiano sawa na watu wengine wasio na maambukizi ya ugonjwa huu,”alisema muathirika huyo.
 
 Tarehe 1 Disemba kila mwaka ni siku maalumu ambayo tunaadhimisha Siku ya UKIMWI duniani, siku ambayo kwa pamoja tunaungana na watu wote wanaokadiriwa kufikia milioni 78 ambao tayari wameshapata mambukizi na watu milioni 35 ambao tayari wamefariki ulimwenguni kote kutokana na athari zitokanazo na maambukizi ya UKIMWI.

Waziri Mkuu aagiza pampu za maji kuondolewa kwenye chanzo cha maji Karatu

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bi. Theresia Mahongo kuhakikisha mashine zote za kupampu maji zilizoko ndani ya mita 500 kutoka kwenye chanzo cha maji cha Qangded ziwe zimeondolewa ifikapo saa 12.00 jioni ya jana na atakayekaidi atachukuliwe hatua za kisheria.

Alisema kitendo cha kuweka mashine za kupampu maji karibu na chanzo hicho na kuvuta maji kwenda kwenye mashamba yao kinasababisha maji kushindwa kufika katika mashamba ya wakulima wengine hivyo amewataka wafuate utaratibu uliowekwa na waendeshaji wa mradi huo.

Waziri Mkuu alitoa agizo jana Jumatatu, Desemba 5, 2016 wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Jobaji kata ya Baray wilayani Karatu, ambapo alisema Serikali haitavumilia kuona mtu mmoja akivuruga mradi huo wa umwagiliaji.

Alisema ili kuhakikisha mradi huo wa umwagiliaji unakuwa endelevu lazima chanzo cha maji kilindwe na wananchi wasiruhusiwe kufanya shughuli za kijamii karibu na chanzo na badala yake wasogee umbali wa mita 500.

“Sitaki kuona mashine zikipampu maji ndani ya mita 500 kutoka kwenye chanzo na badala yake wakulima wote wafuate taratibu zilizowekwa . Lazima chanzo kilindwe kwa sababu maji yakikauka mazao nayo yatakauka, hivyo tutakosa chakula jambo ambalo hatutaki litokee. Mkuu wa wilaya kesho nenda kafanye ukaguzi katika chanzo ukikuta mashine kamata,” alisema.

Awali, Waziri Mkuu alizindua mradi wa maji safi na salama wa kijiji cha Jobaj unaotekelezwa na shirika la World Vision Tanzania uliogharimu sh. milioni 285. Mradi huo utahudumia vijiji vitatu vya Kata ya Baray ambavyo ni Mbunga Nyekundu, Jobaj na Dumbechand.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Miradi wa Wolrld Vision Tanzania, Bw. Revocutus Kamara alisema mradi huo unatokana na hitaji kubwa la maji katika vijiji hivyo vitatu na uwepo wa kisima kirefu cha maji kilichochimbwa kwa ufadhili wa Benki ya Dunia mwaka 2009.

“Mradi huu wa maji unatekelezwa kwa awamu tatu, awamu ya kwanza ilianza Machi hadi Novemba 2016, ambapo wakazi 5,272 ikiwa ni pamoja na taasisi nne za Serikali ambazo ni Zahanati, Magereza, shule ya msingi na sekondari zilizoko katika kijiji cha Jobaj wananufaika kwa kupata maji safi na salama,” alisema.

Alisema awamu ya pili na ya tatu ya mradi huo itaanza Disemba 2016 na itagharimu zaidi ya shilingi milioni 200.

Akizungumza kuhusu mradi wa umwagiliaji Mkurugenzi huyo alisema shirika lao limechangia kuboresha miundombinu ya umwagiliaji kwa kujenga kilomita 1.716 za mfereji katika kijiji cha Jobaj (kilomita moja) na Dumbechand (mita 716) ambapo umegharimu zaidi ya sh. milioni 210 na inalenga kunufaisha zaidi ya wakulima 4,450 wa vijiji hivyo.

Alisema mifereji hiyo itawezesha wakulima katika vijiji hivyo kuwa uhakika wa upatikanaji wa maji kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji kwa mazao ya chakula na biashara hivyo itasaidia kupunguza migogoro ya maji, kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji kutoka hekta 803 hadi hekta 1,203.

Rais Magufuli na mkewe Mama Janet wakabidhi msaada wa Sh mil 5 ya matibabu ya Mtoto anayeotwa na nyama kichwani

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli jana  tarehe 5 Desemba, 2016 wamekabidhi msaada wa Shilingi Milioni 5 kwa ajili ya kusaidia matibabu ya mtoto Haidari Bonge mwenye umri wa miaka 9 anayesumbuliwa na tatizo la kuota nyama kichwani, kinywani na machoni.

Fedha hizo zimekabidhiwa kwa Mama wa mtoto huyo Sauda Kassim  na Kaimu Mnikulu Ndugu Ngusa Samike kwa  niaba ya Rais Dokta Magufuli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo mtoto huyo anapatiwa matibabu.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi fedha hizo, Kaimu Mnikulu Ndugu Ngusa  Samike alisema Rais Dkt. Magufuli ameguswa baada ya kutazama kipengele cha Hadubini “Habari kwa Kina” kilichorushwa hewani katika taarifa ya habari saa 2 usiku na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) tarehe 03 Desemba, 2016.

Kwa upande wake Daktari Bingwa wa magonjwa ya ngozi Dkt. Andrew Foi alisema mtoto Haidari anayeishi Mbagala Kuu Jijini Dar es Salaam alianza kuota nyama miezi mitatu baada ya kuzaliwa na amekuwa akifanyiwa upasuaji wa kuondoa nyama hizo mara kwa mara.

Dkt. Foi alisema Hospitali ya Taifa Muhimbili inatoa matibabu ya mtoto huyo bure tangu awasili hospitalini hapo isipokuwa kwa matibabu ambayo hayapatikani hospitalini hapo ndio analazimika kuyalipia katika sehemu husika.

Alisema mtoto Haidari anahitaji eneo maalum la kuishi muda wote ambalo lina giza na kuvaa nguo nyeusi zinazomfunika mwili wote ili kujikinga na miale ya jua ambayo imekuwa ikimuathiri kwa kiasi kikubwa.

Mama wa mtoto Haidari, Ndugu  Sauda Kassim alimshukuru Rais Dkt. Magufuli na mke wake Mama Janeth Magufuli kwa moyo wa upendo waliouonesha baada ya kuguswa na shida zinazomkabili mtoto wake na kutoa msaada huo na hivyo kuomba wananchi wengine waige mfano wa Rais na Mkewe katika kumsaidia mwanawe.

Tayari mtoto Haidari  Bonge, ameshafunguliwa akaunti katika Benki ya CRDB tawi la Azikiwe yenye namba 0152236450100, ambapo benki hiyo kupitia kwa meneja Uhusiano wake Godwin Semunyu amekabidhi shilingi laki Tano ikiwa ni msaada kutoka Benki hiyo.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Slaam (UDSM) Prof. Mukandala aongezewa muda


Serikali yatengua umiliki wa Shamba la Mifugo la Manyara.....Waziri Mkuu Alikabidhi kwa Wananchi

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amemkabidhi hati ya shamba la mifugo la Manyara, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Stephen Ulaya baada ya kubadilisha umiliki wa shamba hilo.

Umiliki ulibadilishwa kutoka Taasisi ya Tanzania Land Conservation Trust (TLCT) ambayo mwenyekiti wa bodi yake ni Mbunge wa zamani wa Monduli, Edward Lowassa kwenda kwa wananchi wa vijiji viwili vya Elesilalei na Ortukai vya kata ya Elesilalei, eneo la Makuyuni, wilayani hapa.

Hatua ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi ni baada ya kilio cha muda mrefu kwa wananchi hao kudai kuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliagiza shamba hilo ligawiwe kwa wananchi lakini haikuwa hivyo, badala yake watu wachache walijimilikisha kinyemela chini ya wenyekiti wa bodi ya TLCT.

Majaliwa alitangaza kukabidhiwa hati hiyo wakati alipomtembelea mwanzilishi wa Shule ya Msingi Laibon, Leshuko ole Mapii, kata ya Elesilalei.

Alifika kujionea hali halisi ya mwamko wa elimu kwa mzee huyo ambaye wajukuu zake na watoto wake zaidi ya 102 wanasoma shuleni hapo pamoja na watoto wengine wanaotoka jirani na eneo hilo.

Alisema serikali imeamua kurudisha shamba hilo kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili baada ya Baraza la Madiwani na uongozi wa wilaya hiyo ya Monduli kuridhia kwa pamoja umiliki wa shamba hilo kurudi kwa wananchi.

Alisema shamba hilo lenye ukubwa wa ekari 44,930 lilikuwa likimilikiwa na TLCT linalofadhiliwa na Shirika la African Wildlife (AWF), hivi sasa ni mali ya wananchi na halmashauri ya Monduli ndio wataamua kupanga matumizi bora ya ardhi.

Alisema nyaraka zinazoonesha kuwa shamba hilo lililotolewa kwa wananchi wa vijiji vya Elesilalei na Ortukai na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu mwaka 1999 kwa ajili ya kilimo na ufugaji lakini hakuna kilimo chochote hapo na badala yake TLCT ikajimilikisha shamba hilo kinyume na maagizo.

"Sasa namkabidhi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli hati hii na kuanzia leo(jana) umiliki wa shamba hilo utakuwa chini ya halmashauri na wananchi mtaamua kupanga matumizi bora ya ardhi katika shamba hili mliloteseka nalo kwa muda mrefu," alisema.

Alisema serikali itawanyang'anya mashamba wale wote wanaomiliki bila ya kuyaendeleza kwa kuwapa wananchi na kuhoji ni kwa nini wenye fedha kuchukua mashamba mkubwa bila ya kuyaendeleza.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kabla ya ujio wa Waziri Mkuu, alifanya ziara katika shamba hilo na kuagiza uongozi wa wilaya ya Monduli, mkoani Arusha na baraza la madiwani la wilaya hiyo kuhakikisha wanabadilisha umiliki wa shamba hilo kwenda kwa wananchi wa vijiji husika kama Rais mstaafu, Benjamini Mkapa, alivyoagiza.

Mbunge wa Monduli, Julius Kalanga (Chadema) pamoja na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Isack Joseph kwa nyakati tofauti waliishukuru serikali kwa uamuzi huo na kuipongeza serikali kwa kujali maslahi ya wananchi wake.

Mkurugenzi wa TLCT, Boniface Ngimojiro alipopewa nafasi ya kusema neno kwa wananchi hao, alisema taasisi hiyo inaongozwa na bodi ya wadhamini yenye wajumbe wanane wakiongozwa na Mbunge wa zamani wa Monduli, Edward Lowassa kama mwenyekiti wa bodi hiyo.

Aidha alikiri kupata amri ya kubadilishwa umiliki wa shamba hilo kutoka katika taasisi hiyo kwenda kwa wananchi wa vijiji hivyo viwili na kusisitiza kuwa kwa sasa ameridhia shamba hilo kumilikiwa na wananchi.

Meneja wa AWF, Fidelis Ole Kashe, alisema wamekuwa wakifanya kazi katika mazingira magumu ndani ya shamba hilo pamoja na kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye shamba hilo ikiwemo shule, zahanati, ufugaji wa kisasa na machinjio.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, aliwasihi wananchi hao kuheshimu njia za mapito ya wanyama katika eneo hilo ambalo wanyamapori kutoka hifadhi za Tarangire, Manyara na Ngorongoro wanalitumia kwa ajili ya kupita kwenye hifadhi hizo mara kwa mara.

Serikali yatangaza adhabu mpya kwa wala rushwa

$
0
0
Serikali imeeleza dhamira yake ya kuongeza adhabu kwa watu wanaobainika kuhusika na rushwa ili wawe wanalipa fidia ya hasara iliyojitokeza mbali na kutumikia kifungo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mh. Angellah Kairuki amesema kuwa adhabu zinazotolewa kwa wala rushwa ni ndogo ikilinganishwa na hasara wanayoisababishia serikali, hivyo marekebisho ya sheria hizo itamtaka mlarushwa kulipa fidia ya hasara iliyojitokeza

Akiongea na waandishi wa habari, mara baada ya kuzinduliwa kwa wiki ya kupokea malalamiko ya wananchi, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Mhe Angella amesema serikali itahakiki mali za viongozi wa serikali wapatao 500 na kuwataka wananchi kujitokeza kuhakiki mali za viongozi wao pamoja na kutoa taarifa ambazo serikali haikufanikiwa kuzipata.

Profesa Muhongo: Tuna nishati ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo amesema Tanzania kwa sasa ina hazina ya kutosha ya makaa ya mawe na gesi itakayowawezesha wawekezaji kupata nishati ya uhakika.

Waziri Muhongo pia ameahidi kuendeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini ili kutimiza lengo la kila mtanzania kuwa na uhakika wa kupata nishati ya umeme.

Profesa Muhongo amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa kikanda wa masuala ya nishati endelevu uliwakutanisha washiriki kutoka nchi kadhaa ndani na nje ya bara la Afrika.

Katika mkutano huo, Waziri Muhongo aliwataka wadau hao kutafuta suluhisho la upungufu wa nishati kwa kuzingatia malengo ya milenia yanayotaja nishati kama moja ya sababu za kuinua uchumi.

Kwa upande wake, Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez alisema nchi za Afrika zinahitaji kutumia teknolojia, sera na uwezo walio nao katika kupambana na suala la upungufu wa nishati huku umoja huo ukiahidi kutumia jumla ya dola za Kimarekani bilioni mbili katika kuwezesha upatikanaji wa nishati endelevu.

Kipindupindu charejea kwa kasi, chatikisa mikoa 6

$
0
0

Serikali imesema kumeibuka upya kwa ugonjwa wa kipindu pindu katika mikoa sita ambapo takwimu zinaonyesha kuwa wapo wagonjwa 458 huku sita wakiwa wameshapoteza maisha kutokana na ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu aliitaja mikoa yenye wagonjwa wa kipindipindu kuwa ni pamoja na Morogoro wagonjwa 282 na Dodoma wagonjwa 96.

Aliitaja mikoa mingine kuwa ni Mara wagonjwa 31, Kigoma wagonjwa 30, Arusha 11 na katika jiji la Dar es salaam wapo wagonjwa 8 wa kipindupindu kati ya hao 6 kutoka Ubungo na 2 kutoka Ilala.

Aidha, Mh. Waziri amebaini kuwepo kwa uzembe mkubwa unaofanyika katika wilaya na mikoa kwa kushindwa kutoa taarifa za ugonjwa huo huku wagonjwa wa kipindu pindu wakilazwa pamoja na wagonjwa wa kawaida kwa kile kinachoelezwa ni viongozi kuogopa kutumbuliwa na Rais Dkt. John Magufuli.

Mbunge wa Ukonga apinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam

$
0
0

Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) amepinga amri iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya wafanyabiashara kufunga maduka yao kila siku ya Jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa nne ili wafanye usafi.

Amesema amri hiyo ni batili na haitekelezeki kwa sababu inarudisha nyuma uchumi wa wananchi hususani wafanyabiashara ndogondogo ambao wanategemea kipato chao cha siku kuendesha maisha yao.

Akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Kivule mwishoni mwa wiki, Waitara alisema yeye hapingani na watu kufanya usafi katika maeneo yao, lakini amri ya kufunga maduka kila Jumamosi inaathiri uchumi wa wananchi hivyo ni batili na haipaswi kuendelea kuwapo.

Siku chache baada ya kuteuliwa kuongoza Mkoa wa Dar es Salaam, Makonda alipiga marufuku kufungua maduka na biashara zingine kabla ya saa nne asubuhi ili muda huo utumike kufanya usafi na anayekaidi agizo hilo hutozwa faini isiyopungua Sh 50,000.

Mbunge huyo wa Ukonga alisema uchumi wa watu masikini hususani wa mjini unategemea kile wanachokizalisha kila siku, hivyo amri ya kufunga biashara kila wiki ni kurudisha nyuma juhudi za wananchi kujiletea maendeleo yao.

Katika mkutano huo aliwaambia wananchi hao kujiwekea utaratibu kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi wakati wote na kila Jumamosi wafungue biashara zao asubuhi kama kawaida na wasibughudhiwe na mtu yeyote.

“Mimi naunga mkono utaratibu wa kufanya usafi kila mwezi uliotangazwa na Rais Dk. John Magufuli ambao upo kwa mujibu wa taratibu, lakini huu wa kila Jumamosi mimi sina mwongozo nao na hizo faini za kila wiki sizitambui na ni batili.

“Ninachotaka kila mtu afanye usafi kwenye eneo lake, hizi faini zinatozwa bila utaratibu hata kama eneo la mtu ni safi sitaki kuzisikia, wananchi hawa si wanyama, waelimishwe waachwe wajiwekee utaraibu wao.

“Hivi mama, baba ntilie anayepika  maandazi, vitumbua, chapati afunge biashara tangu asubuhi mpaka saa nne halafu hiyo chai itanywewa na nani, huyu mtu unamwambia afunge biashara ili akaibe mtaani?” alihoji mbunge huyo na kuongeza:

“Watendaji lazima muwasikilize watu, nasikia kinachofanyika ni mwendo wa kuviziana, waacheni watu wafanye kazi, hapa ni kazi tu sio faini tu” alisema Waitara.

Katika hatua nyingine, Waitara ambaye pia ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kivule alivunja kikundi cha ulinzi kilichokuwa katika ofisi hiyo kwa tuhuma za kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwanyanaysa wananchi.

Badala yake, alisema uitishwe mkutano wa hadhara watu wote wanaohitaji kazi hiyo walete maombi katika ofisi hiyo na baadaye wajadiliwe na wananchi katika mkutano wa hadhara ili kuepuka kuwapa kazi watu wasiokuwa waaminifu katika jamii.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images