Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Waziri Mkuu aziagiza shule na majeshi kuachana na kuni.........Waziri Maghembe Aahidi Kupandisha Kodi ya Mkaa Maradufu

$
0
0
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka taasisi za serikali zinazotumia kuni na mkaa kwa wingi kama vile shule na majeshi kuanza mikakati madhubuti ya kubadili mfumo wa kupikia na kuweka majiko ya gesi ili kupunguza matumizi ya mkaa ambayo yamekuwa chanzo cha uharibifu wa mazingira.

Alisema hayo jana Dar es Salaam katika hotuba iliyosomwa kwa niaba yake na Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kujadili namna na njia bora ya kupunguza matumizi ya mkaa kwa usimamizi endelevu wa mazingira nchini.

“Nimeelezwa kuwa makampuni yanayouza majiko na gesi ya kupikia aina ya LPG yameonesha nia ya kuweka majiko haya bila gharama yoyote. Tutumie vyombo vyetu vya habari na majukwaa ya mikutano kuhamasisha wananchi kutumia fursa hii ya LPG,” alisema Waziri Mkuu.

Aidha, alisema nchi inakabiliwa na changamoto kubwa za uharibifu wa mazingira kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ufugaji wa kuhamahama, mifugo kuvamia misitu na kuiharibu pamoja na vyanzo vya maji na watu kukata miti katika vyanzo hivyo.

Alisema mabadiliko ya tabianchi yamesababisha mabadiliko ya vipindi vya mvua, mtawanyiko wa kiwango cha mvua na hivyo kutishia usalama wa chakula na ukosefu wa malighafi kwa viwanda ambavyo ndiyo njia ya kuivusha nchi kuingia katika uchumi wa kati.

Alisema takwimu zinaonesha asilimia 90 ya nishati ya kupikia hasa mijini ni mkaa na kwa vijijini asilimia kubwa na wananchi wanatumia kuni ambapo takwimu hizo pia zinaonesha ili kuzalisha tani moja ya mkaa sawa na magunia 30 zinahitajika tani 12 za kuni na hali hiyo imesababisha nchi kupoteza zaidi ya hekta 370,000 kila mwaka.

Alisema utafiti pia umebainisha kwamba matumizi ya mkaa yanaongezeka kutokana na ongezeko la watu na kama haitaanza kutumika nishati mbadala, mahitaji ya mkaa yatafikia takribani tani milioni tano kwa mwaka ifikapo mwaka 2030 kutoka tani milioni 2.4 zilizotumika mwaka 2015.

Hata hivyo, Profesa Maghembe alisema wizara yake inatarajia kupandisha ushuru na kodi ya mkaa ili uuzwe kwa bei ya juu lengo likiwa ni kuwafanya wasafirishaji na wanunuzi washindwe kumudu gharama na hatimaye matumizi ya mkaa kupungua.

Video mpya ya Navy Kenzo – Feel Good Ft. Wildad (Official Music Video)

$
0
0
Kundi la muziki kutoka nchini Tanzania, Navy Kenzo linaloundwa na wasanii wawili Aika na NahReel jana Novemba 29 wameachia video ya wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina la Feel Good. Itazame video hiyo hapa chini.

Makada Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Wazuru Tanzania Kujifunza toka CCM

$
0
0
UJUMBE wa watu sita kutoka Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) uko nchini kwa ziara ya siku saba kujifunza shughuli zinazofanywa na CCM.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema ujumbe huo unaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Uhusiano wa Kimataifa, Maendeleo na Mafunzo wa Chuo cha Viongozi wa Chama hicho, Jia Bo.

Madabida alisema lengo la ziara hiyo ni kudumisha ushirikiano baina ya Tanzania na China ulioasisiwa na marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na Baba wa Taifa la China, marehemu Mao Tse-Tung.

Alisema ujumbe huo ambao utatembelea Temeke na Zanzibar uliwasili nchini baada ya ziara ya baadhi ya makada wa CCM waliokwenda China na kujifunza mambo mbalimbali ambayo ujumbe huo utapenda kujua kama wameyafanyia kazi.

Mratibu wa Masuala ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Dk Pindi Chana alisema ujio wa viongozi wa chama hicho ni matunda ya ushirikiano wa Tanzania na nchi mbalimbali duniani.

"Ujio wa wenzetu hawa kutoka China ni matunda ya ushirikiano kati yetu na nchi zingine kama Zimbabwe, Afrika Kusini, Angola, Cuba na zinginje za  Ulaya hasa katika siasa za kijamaa," alisema Chana.

Alisema China wako karibu bilioni moja na wamepiga hatua katika maeneo mbalimbali hivyo ujio wao nchini ni fursa kwao kujifunza mambo yetu na sisi kujifunza kwao kutokana na hatua ya kiuchumi waliyopiga..

VIDEO: Masikilize Rais Magufuli Akipiga Marufuku Watu Binafsi Kuuza Sare za Majeshi

$
0
0

Rais Magufuli akizungumza na watumishi wa gereza la ukonga alipotembelea kwa kushtukiza jana. Kapiga marufuku watu binafsi kuuza sare za majeshi

Selfie ya Diamond akiwa na BOXER Yazua Balaa Mitandaoni

$
0
0
Diamond Platnumz amezua balaa mtandaoni baada ya Jumanne hii kupost selfie akiwa amevalia kiboxer cheusi.

Kwenye picha hiyo, Diamond aliandika: Straight from the Changing room!…I think i need to go back to the gym so that i can be more flexible on m 24th Pre-XMass Parformance in Dar Es Salaam.

Licha ya kufunika kwa emoji kwenye eneo la sehemu zake za siri, selfie hiyo imesababisha hisia tofauti huku wengi wakimponda staa huyo kwa kukosa staha.

Hizi ni baadhi ya comments:

isaac_siame: @diamondplatnumz sitaki kuamini kama mawaziri kama nape au makamba watatamani kuja tena wcb kuonana namsanii wa namna hii, hii itakucost au imekucost tayari @babutale busara zako azijatumika kushauri hii naanza kuona misingi ya heshima ulioitunza kwa mda mrefu ikipotea

tausizehemasaleh: You ‘ve a beautiful soul but I think sometimes you go over board,remember to much is given .much is expected,I respect the path Mom Tee is taking,don’t neglect her advices,you may need them sometimes,Big love small bro

yahyakiwera8646: Nduguyangu nakuusia usidanganyike nahizi like nacomment kumbuka weweni muislamu nautazikwa kiislamu kuogope mungu kwanza niharamuvhizo tatoo ukiswali swalazako haziswihii ukiogajanaba halitoki nduguyangu unapotea HAWA wanao like wote kaburini hatakuwepo utakua pekeyako namatendoyako iwemazuri au mabaya je utaponaa? Ilahuu WANGU niukumbushotu kwako nikutakie mabadiliko usijekusema hukuambiwa buree miminisha kuambia

swaum1140: Mmmm jaman mm hapo hapan nasibu sio nzuri hyo pic kwa kweli kumbuka wew ni baba now sio pich nzur kumbuka IPO cku tifa ataiona alaf itakua aibu kubwa uxifany hvy bhana hapo mm sijapenda kabisaaa

ommie_latino26: Bro huo ni ujinga una familia sasa ina maana hapo tiffah aje aone dudu ya baba au

RC Paul Makonda Atuhumiwa Kuwadhalilisha Watumishi wa Umma kwa Kuwaita VICHAA........Tazama Video

$
0
0

KAULI mbalimbali zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa ziara zake zimezua taharuki jijini humo.

Kwa nyakati mbalimbali wakati wa ziara zake,  Makonda anadaiwa kutoa kauli za vitisho hasa kwa watumishi wa umma.

Kutokana na hali hiyo, Chama cha ACT-Wazalendo kimemshtaki mkuu huyo wa mkoa katika Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Utawala Bora ili imuwajibishe.

Katika taarifa yake iliyotumwa jana kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam na Katibu wa Ngome ya Wanawake wa chama hicho, Esther Kyamba alisema kauli alizozitoa Makonda zimewadhalilisha watumishi hao.

“Tumesikitishwa na kuhuzunishwa na kauli zisizo za kiuongozi na zisizozingatia kanuni za maadili ya utumishi wa umma zinazoendelea kutolewa na RC Makonda.

“Jana (juzi), katika mkutano anaouita wa kutatua kero kwa wakazi wa Dar es Salaam aliendelea kushindwa kutatua kero na badala yake kuongeza kero ya kudhihaki, kudhalilisha kukejeli na kutukana hadharani wananchi anaowaongoza na watumishi anaowasimamia kitendo ambacho ni kinyume na maadili ya Watanzania,” alisema.

Kyamba alisema kitendo cha Makonda kumtolea lugha ya udhalilishaji Ofisa Ardhi wa Manispaa ya Kinondoni, Rehema Mwinuka akiwa Mabwepande kwa kumtamkia kwamba “Hawa ndio vichaa tunaohangaika nao, toka hapa”. Hakikubaliki.

“Kauli hiyo imetushtua sana,tunalaani kwa nguvu zetu zote, kauli kama hii si tu haikupaswa kutolewa na kiongozi mkubwa katika ngazi ya mkoa lakini pia ni kauli mbaya ambayo ililenga kumdhalilisha Rehema na kumvunjia heshima yake mbele ya umma,” alisisitiza.

Alisema kutokana na udhalilishaji huo uliofanywa na Makonda, wameshawasilisha mashtaka yao dhidi yake mbele ya Tume, wakiitaka imwajibishe kwa kitendo chake hicho cha utovu wa nidhamu na maadili ya utumishi wa umma.

“Ngome inamtaka mkuu huyo wa mkoa kutambua kuwa kwa kuzingatia Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 pamoja na Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma, kanuni ya 65(1) inamtaka mtumishi wa umma, “kuepuka kufanya vitendo viovu au kutamka maneno yanayolenga kuwaaibisha watumishi wa ngazi moja, za chini yao au wa vyeo vya juu,” alisema.

Alisema kitendo alichofanya, kumwaibisha na kumtolea lugha ya udhalilishaji, Mwinuka ni kinyume cha Sheria na Kanuni za Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Tunaitaka Tume ifanye uchunguzi na kuchukua hatua dhidi ya matamshi mbalimbali yaliyotolewa na Makonda ambayo yalikiuka sheria ya Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma.

“Tunayataka mashirika na asasi mbalimbali zinazosimamia haki za binadamu, haki za jinsia na utawala bora kupaza sauti dhidi ya kauli isiyo ya kiuongozi ya  Makonda, Ngome na Chama kwa ujumla tutaendelea kuwasemea wanyonge wote popote walipo kwa kadri ya uwezo wetu,” alisema.

Chadema: Hatutakubali tena kudhulumiwa 2020

$
0
0
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) ,Vincent Mashinji amesema hawatakubali tena kudhulumiwa kwa namna yoyote  katika uchaguzi wa mwaka 2020.

Dk. Mashinji amesema hayo huku akimtolea mfano wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha, na kuongeza kuwa kuna mambo hutokea bila kutarajia lakini watapambana kwa kila hali,

“Huu ni uchaguzi kuna mtu alitarajia haya yaliyofanywa na Jecha? hii inaonyesha kwenye nchi yetu bado kuna tatizo la utendaji haki, wewe umefanya mara ya kwanza tukanyamaza,ukafanya tena mara ya pili kibabe,tukalalamika, badala ya kutuita tuongee, unasema nendeni mkaseme kokote kule”alisema Mashinji.

Aidha, akiongelea utawala wa Rais Magufuli ,Mashinji amesema kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa utawala bora na matokeo yake yeye ndio amekuwa kila kitu, ameongeza kuwa wakati anaanza  mapambano na rushwa aliamini kwamba angeweza kuliondoa tatizo hilo lakini imekuwa tofauti.

Hata hivyo, Mashinji ameongeza kuwa katika mwaka mmoja wa Rais Magufuli, amesema ameshindwa kusimamia utawala bora baada ya kupiga marufuku mikutano ya hadhara pamoja na shughuli zote za kisiasa nchini kwa kile alichosema kuwa muda wa siasa umekwisha.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 47 & 48

$
0
0
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA      
Akaminya honi zake kwa nguvu ili mtu uyo kuweza kupisha njiani, na mbaya zaidi dokta Maliki aligundua amasimama katikati ya daraja la Sarenda. Kwa haraka akilini mwake akahisi ni majini ambao mara kwa mara inasadikika yanaonekana kwenye daraja hilo. Akawasha gari yake ila haikuwaka akajaribu kuliwasha gari lake ila halikuwaka kabisa. Mtu aliye simama mbele ya gari lake taratibu akaanza kugeuka huku sura yake akiwa ameiinamisha chini. Alipo inyanyua sura yake, macho ya Dokta Maliki yakamuona vizuri Samson akiwa amsimama mbele yake, huku akiwa tumbo wazi, mikononi mwake akiwa amshika bastola mbili zilizo elekea chini.
  
ENDELEA
Samson hakuhitaji kumuacha hai dokta Maliki, akafyatua risasi zipatazo ishirini, zilizo vunja kioo cha gari ya dokta Maliki, na nyingi zikatua kifuani kwake na huo ndio ukawa mwisho wa maisha ya dokta Maliki. Samson akapiga hatua hadi kwenye gari la Dokta Maliki, akafungua mlango wa gari hilo ili kuhakikisha kwamba adui yake amesha poteza maisha. Alipo hakikisha dokta Maliki tayari amekuifa, akarudi kwenye gari walipo raisi Praygod pamoja na Rahab.

“Tayari Madam Rahab”
“Kazi nzuri”
Wakaondoka katika eneo la daraja ili kuto kuweza kuingia mikononi mwa askari ambao hawakujilikana watafika muda gani kwenye eneo hilo, kwani ni tayari askari wa nchi nzima walipewa jukumu la kuimarisha ulinzi masaa ishirini na nne, kwani usalama wa nchi bado ni hali tete.
                                                                                              ***
Agnes akiwa katika wazo la kufikiria kutoka nje ya treni hiyo inayo kwenda kwa kasi, binti huyo akavunja kioo kimoja kwa kutumia kishikizo cha jambia lake. Upepo mwingi ukaanza kuingia ndani ya treni hiyo

“Tunatoka sasa”
Binti huyo alizungumzakwa sauti ya juu kutokana na upepo huo mwingi. Binti huyo akachungulia nje, alipo ona kuna usalana, hakuhitaji kupoteza muda akapanda kwenye dirisha hilo huku akiwa ameshikilia vizuri kwa ndani. Kabla ya kupanda juu, akamtazama Agnes ambaye anaonekana kuhofia kitendo hicho.
“Hei jikaze, unahitaji kukamatwa?”
Binti huyo alizungumza huku akimtazma Agnes. Hapakuwa na jinsi yoyote ya kuweza kufanya, binti huyo akatoka ndani ya behewa hilo na kwautaalamu mkubwa alio nao akapanda juu ya behewa hilo. Agnes akashusha pumzi kuuondoa woga, akafanya kama alivyo fanya binti huyo, chakushukuru Mungu akafanikiwa kupanda juu ya behewa hilo alipo mwenzake.

“Tunafanyaje sasa?”
Agnes aliuliza kwani hakuelewa ni kitu gani ambacho kinakwenda kutokea kwa wakati huo, na jinsi akitazama mwendo kasi wa treni hilo akajikuta akizidi kuchanganyikiwa.
“Tunaruka”
“TUNARUKAAA…..!!”
“Ndioo”
“Ahaaa siwezi kufanya hivyo, nitakufaaa”
“Tunafanyaa jiamini, pale mbele kuna daraja chini kuna mto mkubwa”
“Ndio turuke………?”
Wakiwa katika kujadiliana ni nini cha kufanya, kwa mbali wakaiona helcoptar ikija kwa kasi ikitokea nyuma, kwao treni inapo tokea. Katika kuitazama vizuri binti huyo akagundua kwamba ni helcoptar ya jeshi la Marekani.

“Shitii…..”
Akamkumbatia Agnes, kisha kwakutumia nguvu, akajirusha naye kuelekea kwenye mto mkubwa unao pitisha maji mengi. Agnes akawa na kazi ya kupiga makelele kwani hakujua watakapo fika chini watakuwa hai au laa. Kila mwanajeshi aliye kuwa kwenye helcoptar hiyo, walio pata habari juu ya uvamizi wa mabinti hao, alijikuta akishangaa kitendi hicho, kwani kuruka kutoka juu ya treni hadi kwenye mto huu kuna urefu mkubwa sana, ambao kama mtu akiruka ni lazima atakutana na mauti yake ndani ya mtu huo.
Wakawashuhudia mabinti hao wakidumbukia ndani ya maji hayo mengi yanayo kwenda kwa kasi sana.
“Sir tunafanyaje?”
Mwanajeshi mmoja alimuuliza mkuu wao wa kikosi waliye kuwa naye ndani ya helcoptar hiyo.
“Peleka helcoptar karibu na mtu huo”
“Sawa mkuu”
Rubani huyo akafanya kama alivyo agizwa na mkuu wake, kutokana na uwezo wa helcoptar hiyo aliweza kuishusha karibu sana na mtu huo kuangalia kama mabinti hao wapo hai au wamesha kufa. Hawakufanikiwa kuwaona wasichana hao ambao hakuna aliye weza kujua kama wamechukuliwa na maji au kufia ndani ya mto huo.

“Wasiliana na kikosi cha maji waje kutoa msaada”
Mkuu huyo alimuagiza msaidizi wake, akafanya kama alivyo agizwa, kwani hawakuhitaji kuweza kuwapoteza wasichana hao, haswa Agnes aliye weza kufanya mauaji ya kiongozi wao, jambo lililo zua simanzi kubwa sana kwa wamarekani wengi, ukiachilia simanzi iliyo wakumba pia ni aibu kubwa sana kwa nchi kubwa iliyo endelea kama hiyo, kiongozi wao mapoja na askari walio aminika kumlinda kiongozi wao nao pia waliuawa kikatili
“Hawa malaya nilazima tuwakamate”
Mkuu huyo wakikosi alizungumza huku akiwa amekunja ngumi ya mkono wake wa kulia akiwa na hasira kali, kwani masaa ishirini na nne waliyo pewa na raisi wao ya kumkamata binti huyo yanazidi kuteketea pasipo mafanikio ya aina yoyote.
Baada ya muda mchache, wanajeshi wa majini wakafika katika sehemu walipo ingia mabinti wanao watafuta, kazi ya kuwasaka ikaanzia hapo, huku  kila mmoja akijitahidi kufanya anacho weza kuwatia nguvuni wasichana hao.
                                                                                                 ***
“Muheshimiwa kuna barua ujumbe wako”
Msemaji  wa ikulu alimfwata raisi Praygod Makuya, mara baada ya kufuki ikulu wakiwa wameongozana na mke wake pamoja na Samson.
“Umetoka wapi?”
“Whait House Marekani”
Raisi Praygod hakuwa na wasiwasi mkubwa, kwani Tanzania inaushirika mzuri sana na nchi hiyo kubwa duniani na alicho weza kukiamini, ujumbe huo utakuwa ni wapole kwa yale yaliyo weza kujitokeza.

“Baby muangalie mtu wako”
“Sawa”
Raisi Praygod akaondoka na kumuacha Rahab na Samson wakipelekwa kwenye chumba kingine kwa kuweza kuzungumza. Raisi Praygod alicho weza kukifanya ni kuweza kuivua sura ya bandia aliyo weza kuivaa, moja kwa moja akaongozana na msemaji wa ikulu, hadi ndani ya ofisi maalumu ya mawasiliano. Tv kubwa zote zilizomo ndani ya chumba hicho zikawashwa, ili kuweza kufanya mawasiliano na kiongozi mwenzake wa nchi hiyo kubwa. Kutokana na urafiki wao wakaribu, wakasalimiana kwa furaha, huku raisi wa Marekani akimpa pole raisi Praygod kwa yale yaliyo weza kujitokeza.
“Ila ninatatizo kubwa kuliko hata hilo lakwako”
Raisi wa Marekani alizungumza, huku wakitazama Raisi Pragod Makuya kwa kupitia Tv hizo kubwa


Rwanda yashtumiwa kupanga shambulizi la kutaka kumuua msaidizi wa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

$
0
0
Nchi ya Burundi imeishutumu Rwanda kwa madai ya kupanga kufanya majaribio ya kutaka kumuua msaidizi wa Rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe.

Msemaji wa jeshi la polisi kutoka Burundi, Pierre Nkurukiye amesema maagizo ya kufanywa kwa jaribio hilo lililofeli, yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa wapangaji waliotoka kwenye jeshi la Burundi.

Nyamitwe alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko Burundi lakini si mara ya kwanza kupatwa na tukio kama hilo. 

Mwezi Julai mwaka huu Burundi iliishtumu Rwanda kwa mauaji ya Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Hafsa Mossi aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.

Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Singida Afariki Dunia, Mwili Kuagwa Leo Saa 11 Jioni Muhimbili

$
0
0
Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) EX Peter Kakamba amefariki dunia alfajiri ya tarehe 30/11/2016 katika hospital ya taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Kakamba alizaliwa mwaka 1963 katika kijiji cha Kawajense Wilayani Mpanda, mkoa wa Katavi. Alisoma shule ya msingi Shanwe Kawajense  mwaka 1973 hadi 1980, Kidato cha kwanza hadi cha nne katika shule ya Sekondari Kantalamba mwaka 1981 hadi 1984 ambapo kidato cha tano na sita alisoma katika shule ya Sekondari Umbwe mkoani Kilimanjaro mwaka 1985 hadi 1987. Mwaka 1992 hadi 1994 alisoma Astashahada ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Marehemu alijiunga na Jeshi la Polisi mwaka 1988 ambapo katika utumishi wake alipandishwa vyeo mbalimbali ikiwemo Konstable wa Polisi (1989), Sagenti wa Polisi (1991), Mkaguzi Msaidizi wa Polisi (1997), Mkaguzi wa Polisi (2003), Mrakibu Msaidizi wa Polisi (2006), Mrakibu wa Polisi (2008), Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (2011), Kamishna Msaidizi wa Polisi (2015) na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (2016).
 
Baadhi ya nafasi alizowahi kushika ni pamoja na kuwa  Mwendesha Mashtaka wa Polisi katika mkoa wa Iringa, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi, Afisa mnadhimu wa Polisi katika Mikoa ya Iringa na Geita, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa na mpaka anafariki alikuwa Kamanda wa Polisi katika mkoa wa Singida.
 
Kufuatia kifo hicho Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Ernest Mangu anatoa pole kwa Maofisa, Wakaguzi,Askari, ndugu, jamaa na marafiki kwa Msiba huo.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa,
Jina la Bwana lihimidiwe - Amen.

Imetolewa na:
Advera John Bulimba - ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Polisi.        

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Kufanya Ziara Ya Kikazi Mkoani Arusha

$
0
0
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MHE. Kassim Majaliwa  anatarajiwa kutembelea Jiji la Arusha kuanzia kesho tarehe 01 hadi 03/12/2016 na kukagua miradi ya maendeleo, kuongea na watumishi wa Jiji, kukutana na wafanyabiashara pamoja na kuzungumza na wananchi.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa Jiji la Arusha Nteghenjwa Hosseah, kesho tarehe 01/12/2016 Waziri mkuu MHE. KASSIMU MAJALIWA atatembelea National Milling Company (NMC) na pia atakagua ujenzi wa barabara ya Friends Corner - Muriet yenye urefu wa Km 7 inayojengwa kwa kiwango cha Lami kupitia mradi wa Mpango Mji Mkakati (TSCP) na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi.

Hosseah amesema siku ya tarehe 02/12/2016 Waziri Mkuu atakutana na kuzungumza na watumishi pamoja walimu katika Ukumbi wa AICC Arusha na baadae atakutana na wafanyabiashara katika Ukumbi huo.

"Katika nsiku ya tatu ya ziara yake Mhe Majaliwa  atatembelea na kukagua viwanda vya Lodhia pamoja na Hans Paul vilivyoko mtaa wa Viwanda – Njiro na baadae atakutana na wanachi wote kwenye Mkutano wa hadahara utakaofanyika kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid kuanzia saa nane mchana."

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Disemba 1

TPDC Yakanusha Taarifa Kuwa Imeshindwa Kukiuzia Kiwanda Cha Dangote Gesi Asilia Kwa Bei Nafuu

Msajili wa Hazina Atoa Ufafanuzi kuhusu fedha kukauka mifukoni mwa watu Pamoja na Sababu za benki kulalamika kufilisika

$
0
0
Msajili  wa Hazina nchini, Lawrence Mafuru amesema benki nchini zinashindwa kueleza ukweli juu ya kuyumba kwao na kwamba madai ya kuwa hali zao ni mbaya kutokana na agizo la serikali la kutaka fedha zake zitunzwe Benki Kuu ya Tanzania (BoT), hazina ukweli.

Mafuru amesema taarifa ambazo serikali wanazo ni kwamba benki hizo zaidi ya 50 zimekopesha fedha nyingi kwa watu mbalimbali, lakini marejesho ya madeni hayo yamekwama kiasi cha kusababisha benki hizo ziwe katika hali hiyo.

Akizungumza jana Dar es Salaam, Msajili wa Hazina licha ya kukiri kuwa mzunguko wa fedha umepungua kutokana na Tanzania kuchagua kwamba fedha inazozipata zitumike katika miradi ya maendeleo badala ya matumizi ya kawaida, benki zinazolalamika zimeshindwa kurejesha fedha ilizokopesha watu na taasisi mbalimbali.

Akizungumzia taarifa zinazoenezwa kwamba benki zimekosa fedha za kujiendesha, Mafuru alisema taarifa walizozipata ni kwamba Septemba mwaka huu, benki hizo zaidi ya 50 nchini zimekopesha zaidi ya Sh trilioni 16.3 kwa watu mbalimbali.

Hata hivyo, alisema kati ya fedha hizo, Sh trilioni 1.43 zimekopeshwa bila ya kurudishwa katika benki husika na kwamba benki hizo zinashindwa kueleza ukweli uliopo badala yake wanalalamika kwamba hatua ya serikali kuamua fedha zake zitunzwe BoT badala ya katika benki za kibiashara, ndio sababu ya hali yao (benki) mbaya.

Kwa mujibu wa Mafuru, serikali imeamua kuchukua uamuzi huo wa kuzitoa fedha zake kutoka katika benki mbalimbali za kibiashara nchini kwa ajili ya kuwezesha serikali kujua mapato wanayopata kutoka katika taasisi zake.

Msajili wa Hazina amesema zaidi ya Sh bilioni 515 zimeingizwa BoT baada ya uamuzi huo wa Serikali ya Awamu ya Tano ambao ulitangazwa na Rais John Magufuli baada ya kushika madaraka mwaka mmoja sasa. 

Mafuru alikiri kuwa ni kweli kwamba mzunguko wa fedha umekuwa mdogo na kueleza kuwa chanzo chake si kwamba benki zimekosa fedha kwa ajili ya kujiendesha.

Alifafanua kuwa awali watu wengi walitegemea safari na posho ambazo baada ya chenji kubaki, walikuwa wakitumia bila ya malengo, lakini sio kwamba mzunguko huo wa fedha unawaathiri watu wote.

“Tumeona tusitegemee wahisani badala yake tujiwekeze katika miradi mikubwa ya maendeleo ambayo kwa sasa haitaonekana, lakini baadaye itasaidia kuondoa nafasi iliyopo sasa,’’ alisema Mafuru.

“Tayari shilingi bilioni 515 zimeingizwa BoT na mpaka Septemba mwaka huu fedha hizo zilikuwa kwenye akaunti hiyo. BoT ni sehemu ya mfumo wa benki, kwani itakuwa inafanya kazi ya kukopesha kama zilivyo benki nyingine,” alifafanua Mafuru ambaye ofisi yake inasimamia mashirika na taasisi za umma.

Alifafanua kuwa ofisi yake ambayo ina jukumu la kusimamia mapato na matumizi, awali walikuwa wanapata shida kupata taarifa za mapato na matumizi katika benki hizo zilizopo kila kona nchini na kwamba baada ya BoT kuchukua dhamana hiyo, imewasaidia, kwani wanaandika barua na kupatiwa taarifa hizo kwa muda mfupi.

Alisema serikali inategemea mapato yake kutoka katika makundi matatu ambayo ni Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na kupitia mashirika na taasisi mbalimbali.

Alisisitiza kuwa itasaidia kujua mashirika hayo zaidi ya 260 namna wanavyotumia fedha zake katika miradi mbalimbali na kwamba suala la kuchukua fedha bila ya kuzitumia lisiwepo.

Mganga wa Kienyeji Auawa Akitaka Kumbaka Mgonjwa

$
0
0
Mganga wa kienyeji aliyejulikana kwa jina la Kashinje Kashinje (55), mkazi wa kijiji cha Singita kilichopo Kata ya Usanda wilayani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa na wananchi ikielezwa alijaribu kutaka kumbaka mteja wake.

Mteja huyo ambaye ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 (jina linahifadhiwa) alikwenda kutibiwa kwa lengo la kupata mtoto.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Muliro Jumanne, tukio hilo ni la Novemba 29 mwaka huu, akisema lilitokea majira ya saa tano asubuhi.

Alisema Kashinje alifariki dunia alipokuwa anakimbizwa hospitali baada ya kujeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali katika jicho la kulia na kupigwa kwa fimbo mgongoni na watu waliojichukulia sheria mkononi.

“Watu hao walijichukulia sheria mkononi baada ya mganga huyo kujaribu kumbaka mwanamke (jina linahifadhiwa), mkazi wa kijiji cha Ishinabulandi wilaya ya Shinyanga ambaye alikuwa akimtibu kwa tiba za asili ili aweze kupata mtoto”, alieleza kamanda Muliro.

Alisema tatizo lililompeleka mwanamke huyo kwa mganga ni kupata tiba ili aweze kupata mtoto.

Kamanda Muliro alibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo ni tamaa za kimwili na uongo wa kimatibabu wa kutaka kumuingilia kimwili mgonjwa wake baada ya kumlewesha kwa dawa za kienyeji, lakini alifanikiwa kupiga kelele na ndipo wananchi walipomvamia mganga huyo.

Scorpion Akana Hoja 6 . . . . Akiri Hoja 3 Ikiwemo Kupata Mafunzo ya Kareti

$
0
0
MSHITAKIWA katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, Salum Njwete (34) ‘Scorpion’, amekiri kupata mafunzo ya kareti kutoka chuo cha mafunzo cha Ifakara aliyoyafanya mwaka 1989 hadi 1995.

Aidha, upande wa mashitaka katika kesi hiyo umemuongezea mashitaka ya shambulio kupitia kifungu namba 234 cha Sheria ya Makosa ya Jinai ambacho kinaruhusu kuongeza au kubadilisha mashitaka.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga alidai jana mbele ya Hakimu Mkazi, Flora Haule kwamba kesi hiyo imekuja kwa ajili ya mshitakiwa kusomewa maelezo ya awali ambapo katika maelezo ya zaidi ya saa nane, alikiri kuhusu jina lake, sehemu anayoishi ya Machimbo Yombo na mafunzo hayo.

Hata hivyo, alikana kuhusu jina la Scorpion, mashitaka yake na kwamba hakukamatwa wala kuhojiwa na Polisi kuhusu mashitaka hayo.

Katuga alidai kuwa Septemba 6, mwaka huu, mshitakiwa alikuwa maeneo ya Buguruni Sheli na kwamba Septemba 12, alihojiwa na kukamatwa na polisi maelezo ambayo aliyakana.

“Mashahidi watakaotoa ushahidi katika kesi hii wapo sita ambapo upande wetu wa mashitaka utawasilisha vielelezo viwili ikiwemo Fomu namba tatu ya Polisi (PF3) na ripoti ya daktari kwa ajili ya kuthibitisha mashitaka hayo,’’ alidai Katuga.

Hakimu Haule aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 14 mwaka huu, kesi hiyo itakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa. Katika mashitaka yake, mtuhumiwa inadaiwa alitenda kosa hilo Septemba 6, mwaka huu katika maeneo ya Buguruni Sheli, wilaya ya Ilala.

Inadaiwa, Njwete aliiba mkufu rangi ya fedha wenye uzito wa gramu 34 wenye thamani ya Sh 60,000, bangili ya mkononi na fedha taslimu Sh 331,000, vyote vikiwa na thamani ya Sh 476,000 mali ya Said Mrisho.

Inadaiwa kabla na baada ya wizi huo, alimchoma kisu machoni, tumboni na mabegani mlalamikaji ili ajipatie mali hizo.

Majaliwa aongoza waombolezaji kuaga mwili wa Pinda

$
0
0
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana aliongoza mamia ya waombolezaji kuaga mwili wa marehemu Mzee Xavery Pinda ambaye ni baba mzazi wa Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda.

Akizungumza wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwa Mheshimiwa Pinda kijijini Zuzu, Manispaa ya Dodoma  jana  Waziri Mkuu alitoa pole kwa wanafamilia na kuwaomba waendelee kumuombea marehemu apumzike mahala pema peponi.

Mzee Xavery alifariki dunia Novemba 27, 2016 saa 9.30 alasiri katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Alisema msiba huo ni mzito, hivyo anawaomba wanafamilia wawe watulivu na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.

Wakati huo huo Waziri Mkuu alimuhakikishia Mheshimiwa Pinda kwamba Serikali iko pamoja naye katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mzazi wake.

Naye Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk. Jakaya Kikwete alisema marehemu Mzee Xavery alikuwa mwema sana na alikuwa na upendo kwa watu wote.

“Baba yake Pinda alikuwa baba yangu pia. Alitambua ugumu wa kazi tulizokuwa tunazifanya na alitutaka tuwe wavumilivu,” alisema.

Kwa upande wake Mheshimiwa Pinda aliwashukuru viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na wananchi kwa kutenga muda wao na kwenda kumfariji kufuatia msiba huo mzito. “Kuondokewa na baba mzazi au mwanafamilia yeyote si jambo dogo”.

Awali akisoma wasifu wa marehemu, Edward Kyungu ambaye ni mjukuu alisema Mzee Xavery alizaliwa mwaka 1926 katika kitongoji cha Mbede akiwa ni mtoto wa pekee wa Mzee Mizengo Pinda na Mama yake Wakalyate (Umartina).

Mzee Xavery alikuwa Katekista kazi ambayo aliifanya kuanzia mwaka 1951 hadi 1972 alipoamua kustaafu.

“Kazi ya pili ambayo alianza kuifanya kabla na hata wakati wa Ukatekista ni ukulima, jambo ambalo amewarithisha  watoto wake wote na ndio maana wameachiwa sifa moja ya kuitwa watoto wa mkulima,” alisema.

Mzee Xavery anatarajiwa kuzikwa leo Alhamisi, Desemba Mosi, 2016 katika kijiji cha Kibaoni wilaya ya Mlele mkoani Katavi. Marehemu ameacha mke, watoto wanane, wajukuu 54 na vitukuu 40.

Wafanyabiashara Wawili wa Madini Wafikishwa Mahakamani kwa Tuhuma za Kulawiti na Kubaka Watoto

$
0
0

Wafanyabiashara wawili mashuhuri wa madini katika miji ya Mererani na jiji la Arusha jana walifikishwa mahakamani mjini Moshi kwa wakikabiliwa na makosa ya ulawiti na ubakaji watoto. 

Mmoja wao, Welaufoo Munisi (38) anashtakiwa kwa kosa la kumlawiti mtoto wa kiume wa mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), mwenye umri wa miaka 16. 

Mtoto anayedaiwa kufanyiwa kitendo hicho ni mwanafunzi wa shule moja ya sekondari wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, baba yake ni mchungaji katika usharika ambao tunauhifadhi kwa sababu za kimaadili. 

Akimsomea mashtaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa Kilimanjaro, Joachim Tiganga, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Tamari Mndeme alidai kuwa Munisi alitenda kosa hilo Novemba 21, 2016. 

Wakili huyo alidai kuwa siku hiyo katika nyumba za wafanyakazi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), mshtakiwa alimlawiti kijana huyo mwenye umri wa miaka 16. 

Kabla ya kufikishwa kortini jana, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Koka Moita alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo baada ya kumnyeshwa kijana huyo dawa za kulevya. 

Hata hivyo, Munisi alikana mashtaka hayo na kesi hiyo imepangwa kutajwa Desemba 14 mwaka huu baada ya wakili Mndeme kuiambia Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo ulikuwa haujakamilika. 

Dhamana yake ilikuwa wazi na alitakiwa kuwa na wadhamini wawili na hadi saa 8:00 mchana alikuwa hajatimiza masharti hayo.

Wakati Munisi akikabiliwa na shtaka hilo, mfanyabiashara mwingine wa Mererani, Benedict Kimario (42) jana alipandishwa kizimbani mjini Moshi, akikabiliwa na mashtaka ya kumlawiti na kumbaka mtoto wa miaka minane. 

Wakili Mndeme alidai mbele ya Hakimu Mkazi, Idan Mwilapo kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo Mei 10 mwaka huu katika Kijiji cha Mrau, Wilaya ya Rombo, Kilimanjaro.

Mshtakiwa huyo anayetetewa na wakili wa kujitegemea, Joseph Peter, alikana tuhuma hizo na kesi hiyo imepangwa kutajwa kesho ili kuangalia kama ametimiza masharti ya dhamana au la baada ya jana kukwama. 

Alikwama baada ya Hakimu Mwilapo kumtaka kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja angesaini hati ya dhamana ya Sh5 milioni, lakini wakajitokeza wadhamini ambao si wakazi wa Mkoa wa Kilimanjaro. 

Wadhamini hao walikuwa na barua kutoka Mererani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, ambazo kiutaratibu zilipaswa kwanza kuidhinishwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro.

Pata Dawa za Asili za Kupunguza Maziwa, Kuondoa Michirizi, Kuongeza Unene, Kuondoa Chunusi na Zingine Nyingi Toka Beauty Cosmetics

$
0
0
NATURAL BEAUTY COSMETICS Ni wauzaji wa vipodozi aina mbali mbali na vyenye matokeo mazuri na ya haraka zaidi bila kemikali wala madhara yoyote
 
     Tunazo za:👇👇👇👇
1. Kutengeneza shepu hipsi na makalio kwa:- (a) Dawa ya kunywa au Botcho yakupaka @ 150,000/= (b)Vidonge maalum @ 150,000/=
2. Kupunguza au kuongeza maziwa @ 90,000
3. Kushepu miguu kuwa (Chupa ya bia) @ 100,000
( Kuludisha bikra (@) 100,000/=
4. Kuondoa mipasuko au michirizi @90,000/=
5.Kuwa softi na mweupe mwili mzima kwa mafuta @90,000/= vidonge maalum @150,000
6.Kuongeza unene wa mwili mzima @120,000/=
7.kupunguza tumbo na manyama uzembe kwa:-
(a)Dawa ya kunywa au kupaka @ 120,000/=
(b) Mkanda original wa MICRO COMPUTER @200,000/=
8.Kuondoa chunusi na madoa sugu (@) 90,000/=
9.Kuondoa mvi milele na zisiludi tena @ 100,000
10.Kuongeza maumbile kwa:- (a)Gel ya kupaka @100,000/= Mashine original ya HANDSOME UP @170,000/=
11.Kuondoa vinyweleo @80,000/=
12.kuotesha nywele kwenye kipara @100,000/=
13.Kuongeza nguvu za kiume na hamu ya tendo @100,000/=
14.Kuondoa makovu sehemu yoyote @90,000/=
 
     WASILIANA NASI KWA :-
          065 9618585 au
             0759029968.
 
Popote ulipo utapata huduma. BIDHAA  zetu zote ni GARANTII  na risiti ili kuhakikisha mafanikio yako
 
           Follow us
   👇👇👇👇👇👇
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
@natural2162
      👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻👆🏻

Wadaiwa Sugu NHC Washitakiwa kwa Rais Magufuli

$
0
0
Shirika  la Nyumba la Taifa (NHC), limewasilisha ripoti ya wadaiwa sugu wa shirika hilo, zikiwamo wizara, taasisi za Serikali na watu binafsi kwa Rais Dk. John Magufuli, huku wizara mbili zikiwa na deni kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mikoa na Utawala wa NHC, Raymond Mndolwa, alisema uamuzi huo umekuja baada ya Rais Magufuli kuwataka kukusanya madeni hayo na kuwasilisha taarifa hiyo ofisini kwake ili aweze kuipitia.

Mndolwa alisema NHC ilitoa notisi ya siku 90 ambayo ilianza  Septemba, mwaka huu, huku wadaiwa hao wakitakiwa kulipa madeni  ndani ya muda uliopangwa.

Alisema kuwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo bado zinadaiwa kiasi kikubwa cha fedha, licha ya kuwapo kwa mazungumzo ya kulipa madeni yao.

“Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto inadaiwa Sh bilioni 1.4, huku wakilipa Sh milioni 300, wakati Wizara ya Habari, inadaiwa Sh bilioni 1.14, lakini imelipa Sh milioni 700,” alisema Mndolwa.

Mndolwa alisema shirika hilo hadi sasa limekusanya Sh bilioni 5.9 kati ya Sh bilioni 9.3 ambalo ni deni la Serikali kupitia wizara na taasisi mbalimbali, huku Sh bilioni 2.5 zikikusanywa kutoka kwa wadaiwa binafsi ambao awali walikuwa wanadaiwa Sh bilioni 4.

Alisema lengo la shirika hilo ni kuhakikisha madeni yanalipwa ili fedha hizo ziweze kutumika kwenye shughuli nyingine za maendeleo, ikiwamo ujenzi wa nyumba za kisasa 300 mkoani Dodoma.

Alizitaja wizara zinazodaiwa ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Fedha na Uchumi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na iliyokuwa Wizara ya Ujenzi.

Wadaiwa wengine ni Ofisi ya Waziri Mkuu, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC)
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images