Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Magufuli alivyompigia simu Makonda katikati ya mkutano wa Hadhara

$
0
0

Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt John  Pombe Magufuli jana  alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa  Dar  es Salaam, Paul Makonda kwa juhudi anazofanya katika ziara yake kwa kusikiliza kero za wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

Rais Dkt Magufuli alitoa pongezi hizo alipompigia simu Mkuu wa Mkoa wakati akiwa katika ziara yake ya kusikiliza kero za wananchi katika maeneno ya Ubungo jijini Dar es Salaam.

“Endelea hivyo kutembelea wananchi na kutoa ufafanuzi kwa sababu nyingine ufafanuzi huu kama ungetolewa mapema wala wananchi wasingekuwa na sababu ya kuja kuuliza maswali kui kwa hiyo endeleeni hivyo hivyo na juhudi za Dar es Salaam na wakuu wa Wilaya yako na watendaji wote kwa kazi nzuri mnazozifanya kwa kusikiliza kero zao bila kujali vyama vyao bila kujali makabila yao na uendelee kutumbua huko huko” alisema Rais Magufuli.

Hapa chini ni sauti ya Rais Magufuli akitolea ufafanuzi suala la upanuzi wa barabara


Gavana wa BoT asema akaunti maalumu ( “fixed deposit account”) si kosa

$
0
0
Sakata la Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuweka fedha katika akaunti maalumu kwenye benki za biashara limechukua sura mpya baada ya Gavana wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Profesa Benno Ndulu kusema si kosa kisheria.

Profesa Ndulu, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Bodi ya TRA iliyovunjwa na Rais John Magufuli Jumapili iliyopita, alisema mjini Arusa jana kuwa hakuna hasara kiuchumi kuweka fedha kwenye akaunti maalum isipokuwa hilo suala lilikuwa na hali nyingine.

Japokuwa Profesa Ndulu hakutaka kufafanua zaidi kwa maelezo lilichomekewa tu katika mkutano na waandishi wa habari wa kuelezea hali ya uchumi, alisema hali hiyo ndiyo suala lililozungumzwa na siyo kusema “fixed deposit account” ni mbaya.

“Kwani amesema fixed account zote ni mbaya, pamoja na za watu binafsi? Ndo hivyo sasa. Nilijua mtachomekea hilo kwa hiyo nilikuwa tayari,” alisema mhadhiri huyo wa zamani wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Ndulu alisema hayo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari walipotaka kujua athari za kiuchumi kwa taasisi za umma kuweka fedha kwenye akaunti maalumu tena benki binafsi.

Kauli hii ya Profesa Ndulu imekuja siku moja baada ya Rais Magufuli kueleza kilichochangia kuchukua uamuzi wa kutengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi, Bernard Mchomvu na pia kuivunja bodi yake iliyokuwa na wajumbe tisa. Kati ya wajumbe hao tisa, watano wanaingia kwa mujibu wa sheria na wanne ni wa kuteuliwa.

Wajumbe wanaoingia kwenye Bodi kwa mujibu wa sheria ni Gavana wa BoT, Profesa Beno Ndulu; Kamishna Mkuu wa TRA, Alphayo Kidata; Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wa Jamhuri ya Muungano, Doto James; Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Zanzibar, Khamis Mussa Khamis; na Katibu Mkuu Mipango. Bodi hiyo ilivunjwa Jumapili iliyopita.

Rais Magufuli alisema juzi kuwa Bodi ya TRA iliyokuwa na watendaji hao wakuu wa idara na taasisi za Serikali ilifanya dhambi ya kuidhinisha uamuzi wa menejimenti kuweka mabilioni ya shilingi katika benki za binafsi.

“Juzi hapa tumekuta Sh26 bilioni zilizokuwa zimetolewa TRA kwa ajili ya matumizi ya TRA zikapelekwa kwenye mabenki matatu kama ‘fixed deposit account’ na bodi ikapitisha. Ndiyo maana nilipozipata hizo hela; hela nikazichukua na bodi kwaheri,” alisema Rais Magufuli alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 31 ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) yaliyofanyika mjini Kibaha mkoani Pwani ambako jumla ya watu 4038 walihitimu shahada mbalimbali 

Ukwasi wa mabenki 
Katika hatua nyingine Profesa Ndulu amesema ukwasi wa fedha katika mabenki umeshuka ikilinganishwa na kipindi cha nyuma hatua inayotatiza utoaji wa mikopo ya muda mrefu kwa ajili ya uwekezaji nchini.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mara baada ya kufungwa mkutano wa 18 wa taasisi za fedha uliofanyika kwa siku mbili jijini Arusha alisema hali hiyo inafanyiwa kazi na wadau wa taasisi hizo ili kuja na mbinu kufanya kuwa endelevu kwani uchumi unategemea uwekezaji unaotegemea mikopo ya muda mrefu.

Profesa Ndulu alisema BoT itahakikisha inaziwezesha benki kuendelea na jukumu lao la kutoa mikopo pia kuwa wabunifu wa kutafuta pesa kwa ajli ya amana badala ya kutegemea Serikali pekee.

“Benki zinaweza kukusanya amana kwa kiwango kikubwa lakini kama nilivyosema jana (juzi) kuwa katika kila Sh60 kati ya Sh100 zipo kwenye mikono ya watu badala ya kuwekwa akiba benki hivyo ni muhimu zikawekwa mbinu ya kuzipata kwa ajili ya kuwawezesha wawekezaji kuzitumia kwenye uzalishaji,” alisema.

Alisema katika kufanikisha mpango huo lazima kuvutia mitaji kutoka nje kwani hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kupiga hatua kwa kutegemea fedha za maendeleo na uwekezaji zitokane na mapato ya ndani pekee akitolea mfano wa China kuwa ni mfano uchumi wake kutegemea mitaji inayotoka nje ya nchi hiyo.

Katika hatua nyingine Profesa Ndulu alisema amekubaliana na wadau wa sekta ya fedha kuongeza nguvu katika kutoa mikopo na kuboresha mifumo ya taarifa kwa wale wanaotaka mikopo kwa ajili ya kilimo katika mnyororo mzima wa thamani kuanzia uzalishaji hadi kufika kwenye soko.

Profesa Ndulu alisema Tanzania imekaa vizuri kijiografia kufanya biashara na nchi zisizo na bahari zikiwemo Malawi, Uganda, DRC na Zambia katika kuwezesha sekta ya fedha kusaidia eneo la usafirishaji, bandari kufanya kazi na huduma kutolewa inavyotakiwa.

Mwenyekiti wa wenye mabenki ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei amesema waendeshaji wa mabenki wamenufaika na kuelewa mikakati na fursa za Serikali ambayo itawawezesha wao kutoa fedha kwa wafanyabishara.

Alisema wao kama CRDB wameweza kukusanya amana za Sh500 bilioni zinazokopeshwa kwa wafanyabiashara katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na kufungua matawi madogo madogo 100 nchi nzima.

Dk Kimei alisema serikali inapobanwa kifedha kutokana na kutegemea mashirika ya umma inawapa fursa sekta binafsi kupanua wigo wao kuwafikia wananchi wengi.

Wakurugenzi Na Mameneja Atcl Wapanguliwa

$
0
0
Bodi  ya Wakurugenzi ya Shirika la Ndege nchini (ATCL) imewaondoa katika nyadhifa zao wakurugenzi wote waliopo katika menejimenti na baadhi ya mameneja, baada ya kubainika kuwa na kasoro za kiutendaji na kielimu.

Uamuzi huo, ambao hautamhusisha  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Ladislaus Matindi, ulitolewa katika kikao kilichofanyika Novemba 18, lengo likiwa ni kuboresha muundo wa ATCL, ili kukidhi matakwa ya muda mfupi wakati muundo wa kudumu ukiandaliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya shirika hilo, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL, Mhandisi Emmanuel Korosso, alisema katika kikao hicho bodi iliamua kuwaengua wakurugenzi watano waliokuwa katika idara mbalimbali, ikiwamo ya biashara, ambayo ilikuwa na kaimu.

Mhandisi Korroso alitaja idara nyingine ambazo wakurugenzi wameondolewa  kuwa ni fedha, usalama, ufundi na uendeshaji, ambayo mkurugenzi wake alikuwa anaelekea kustaafu.

“Kwakuwa wakurugenzi wengi walikuwa wanakaimu  nafasi hizo, tumeamua wakurugenzi wanaokaimu warudishwe katika nafasi zao  za chini, ambazo si menejimenti au wahamishiwe katika vituo vya mikoani,” alisema Mhadishi Korosso.

Alisema bodi pia imeagiza  kuondolewa kabisa katika shirika hilo wakurugenzi na mameneja waliothibitishwa ili waweze kupangiwa majukumu mengine yatakayoendana na sifa walizonazo.

Alisema kikao hicho pia kimemuagiza Mtendaji Mkuu kutangaza mara moja nafasi za wakurugenzi na mameneja zilizo wazi kwa kufuata muundo uliopitishwa.

Mbali na hilo, Mhandisi Korosso alisema kwa sasa shirika hilo limeweza kuongeza nidhamu katika mapato na matumizi, jambo ambalo limechangia kuanza kulipa baadhi ya madeni wakati Serikali ikisubiri uhakiki umalizike ili iweze kuyachukua.

“Tumeweza kudhibiti mapato na matumizi vizuri, kumekuwa na ongezeko la mapato ya uzito wa ziada wa mizigo kutokana na usimamizi mzuri, ukusanyaji wa mapato kutoka vituoni na mawakala umeboreshwa sana kutokana na ufuatiliaji wa karibu wa mauzo,” alisema Mhandisi Korosso.

Aliongeza kuwa, bodi pia imetoa ruhusa kwa wafanyakazi na familia zao kupewa tiketi bure mara moja kwa mwaka kama stahiki ya likizo na tiketi yenye punguzo mara moja kwa mwaka.

Kampuni ya ATCL, ambayo awali ilikuwa haina ndege hata moja, ilianza kufanya  kazi za safari za ndege Oktoba 14, mwaka huu, baada ya Serikali kununua ndege mbili mpya aina ya Bombardier Q400.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Novemba 27

Mkapa Ampongeza Jk Kwa Ujenzi Wa Chuo Cha Udom.

$
0
0
RAIS mstaafu katika serikali ya Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amempongeza Rais wa Awamu iliyopita, Jakaya Kikwete, kwa kuthubutu na kuwezesha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom). 

Akizungumza katika mahafali ya saba ya chuo hicho, alisema Maono ya chuo hicho yalianza na serikali zote tatu ikiwamo aliyoiongoza lakini hakuweza kuthubutu.

“Nampongeza mzee Kikwete kwa kuweza kuthubutu na kufanikisha ujenzi wake na leo tupo hapa.Mradi wa ujenzi wa chuo hichi, uliafikiwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) tangu utawala wa Rais wa Awamu ya Kwanza, Hayati Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi (awamu ya pili) na kisha mimi lakini wote hatukuweza kuthubutu,”alisema Mkapa.

Kadhalika, Rais Mkapa alishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikutane na kufanya mazungumzo na Vyuo Vikuu vinavyomilikiwa na Serikali ili kuchambua matatizo yanayotokea mara kwa mara. 


Alisema ni vyema uwepo mkutano wa wenyeviti wa vyuo hivyo ili kufahamu gharama wanzotumia kwa ajili ya uendeshaji wake.

Hata hivyo alibainisha idadi ya wanachuo kila kukicha inaongezeka na nakusababisha vyuo hivyo kushindwa kujiendesha, hivyo jambo bora ni kukutana kwa wenyeviti hao na kujadiliana kuhusu gharama za uendeshaji wake.


 Hata hivyo alisema kutoa amri na maagizo kwa wanachuo kila wakati, si suluhisho la kumaliza migogoro vyuoni, lakini pale wenyeviti wa Vyuo Vikuu vyote wakikutana pamoja na kufahamu gharama zao za uendeshaji, kuna uwezekano wa kutatua kero zote.

Naye makamu Mkuu wa Chuo hicho, Prof, Idris Kikula, alisema wahitimu hao wanakabiliwa na changamoto ya upatikanaji ajira ambayo kwa sasa imekuwa tishio duniani huku akiwashauri kujiajiri na kuacha kutegemea ajira serikalini kutokana na tatizo hilo kuwa la kidunia.
 Mkuu wa Chuo UDOM ambaye ni Rais Mstaafu Benjamin Mkapa akitunuku Shahada mbalimbali katika mahafali ya saba ya chuo hicho.
 Wahitimu wa Mahafali ya saba ya Chuo cha Udom.
Wahitimu wa Shahada ya Uzamili katika Chuo cha Udom wakiwa katika nyuso za furaha baada ya kuhitimu.

Waziri Mkuu: Tumetoa Kipaumbele Kikubwa Katika Sekta Ya Elimu

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema  Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli imetoa  kipaumbele kikubwa katika kuboresha sekta ya elimu nchini.

Amesema hatua imejidhihirisha kwenye bajeti ya mwaka 2016/2017 ambapo Serikali imetenga sh. trilioni 1.3 kwa ajili ya Sekta hiyo.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo Ijumaa, Novemba 25,2016 kwenye harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya uboreshaji wa shule nchini iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Saalam.

Akizungumza katika harambee hiyo iliyoandaliwa na Taasisi ya Hassan Maajar Trust,  Waziri Mkuu aliwahakikishia wananchi kwamba bajeti ya Sekta ya elimu itaendelea kuongezeka kadri uwezo wa Serikali utakavyokuwa unaimarika.

“Kama mnavyofahamu, Serikali iliamua kuanza mara moja, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 ambayo inaelekeza Serikali kutoa elimu bure kwa watanzania wote kuanzia shule ya Msingi hadi Sekondari,” alisema.

Alisema uamuzi huo ulikuja na changamoto mbalimbali, ikiwemo upungufu wa madawati kufuatia ongezeko kubwa la wanafunzi waliodahiliwa.

Alisema kufuatia hali hiyo, tarehe 15 Machi, 2016 Serikali iliwaagiza Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuhakikisha tatizo la madawati linatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa kuwashirikisha wananchi na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi.

“Napenda kuwaarifu kwamba, jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda kwani baadhi ya mikoa tayari imemaliza tatizo hilo kwa shule za msingi na sekondari, wakati Mikoa mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji,”.

“Hadi sasa Mikoa ambayo imekamilisha zoezi hilo kwa shule za msingi na sekondari na kubaki na madawati ya ziada ni Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Manyara, Mbeya, Mtwara, Njombe, Pwani, Shinyanga, Singida na Tabora,” alisema.

Waziri mkuu alitumia fursa hiyo kuwapongeza viongozi na wananchi wa Mikoa hiyo kwa kushiriki kikamilifu katika kumaliza kadhia hiyo kwa wanafunzi ambao walikuwa wanakaa chini. “Huo ndio uongozi tunaoutaka, uongozi wa kusimama bega kwa bega na wananchi na kutatua kero zao”,.

Wakati huo huo aliipongeza taasisi hiyo kwa kutoa mchango mkubwa katika kumaliza upungufu wa madawati katika baadhi ya Mikoa nchini  kupitia harambee mbalimbali.

Alisema kati ya mikoa 13 iliyopata ufadhili kutoka ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust, mikoa 10 kati yake imefanikiwa kumaliza tatizo la madawati kwa shule zote za msingi na sekondari.

Mikoa hiyo ni pamoja na Njombe, Rukwa, Singida, Pwani, Shinyanga, Lindi, Mbeya, Iringa, Mtwara, na Kilimanjaro.

“Hii inathibitisha kwamba jitihada za pamoja kati ya Serikali na asasi zisizokuwa za Kiserikali zinaweza kuleta ufumbuzi wa changamoto nyingi zinazolikabili Taifa letu,” alisema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa taasisi ya Hassan Maajar Trust Fund,    Balozi Mwanaidi Maajar, alisema tangu kuanzishwa kwa taasisi hiyo miaka mitano iliyopita  imefanikiwa kuwainua watoto takribani 30,000 kutoka sakafuni kufuatia kampeni ya Dawati kwa Kila Mtoto.

Salamu za Rambirambi za Rais Magufuli Kufuatia Kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba, Fidel Castro

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt, John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Raul Castro kufuatia kifo cha Rais Mstaafu wa Cuba Mhe. Fidel Castro kilichotokea tarehe 25 Novemba, 2016. Katika Salamu hizo Rais Magufuli amesema;

"Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Cuba Mhe. Fidel Castro. Kwa niaba ya Serikali, Wananchi wa Tanzania na kwa niaba yangu mwenyewe natoa pole nyingi kwako, familia, Serikali ya Cuba na wananchi wa Cuba kwa kumpoteza mtu muhimu.

Fidel Castro alikuwa kiongozi shupavu wa karne, atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa katika ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika na pia kwa misaada mikubwa aliyoitoa katika kuboresha huduma za kijamii kwa wananchi.

Alikuwa rafiki wa Tanzania na Afrika nzima, historia ya Tanzania na Afrika haziwezi kukamilika bila kumtaja Fidel Castro, hakika kifo chake sio tu ni pigo kwa Cuba bali pia kwa Tanzania na Afrika.
 
Naungana nawe na wananchi wa Cuba katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, na pia nakuombea kwa Mwenyezi Mungu wewe, familia na wananchi wote wa Cuba muwe na nguvu, subira na ustahimilivu kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu."

Pia Rais Magufuli amemuombea marehemu Fidel Castro apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Rais Magufuli atunuku Kamisheni kwa Maafisa Wapya wa JWTZ Ikulu Dar es Salaam

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, jana tarehe 26 Novemba, 2016 ametunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi 194 wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)  kundi la 59/15 katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Hii ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni nje ya Chuo Cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kilichopo mkoani Arusha, na ni mara ya kwanza kwa Maafisa Wanafunzi wa JWTZ kutunukiwa Kamisheni ndani ya  Ikulu.



Maafisa hao ambao 168 ni wanaume na 26 ni wanawake, wametunukiwa Kamisheni katika cheo cha Luteni Usu na sasa wamekuwa Maafisa Wapya wa JWTZ.



Kabla ya kutunuku Kamisheni, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na Maafisa wanafunzi wa JWTZ na baadaye akashuhudia uhodari wa askari kutoka kikosi cha maadhimisho cha JWTZ waliofanya onesho la gwaride la kimyakimya.



Akizungumza baada ya chakula cha mchana katika ukumbi wa Ikulu, Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli alimpongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange, Makamanda na Askari wote wa JWTZ kwa jukumu kubwa wanalolitekeleza la kuhakikisha nchi ipo salama na amesema Serikali itahakikisha inaboresha zaidi maslai na mazingira ya kazi kwa Jeshi hilo na vyombo vingine vya ulinzi na usalama.



Aidha, Rais Magufuli alisema ameamua tukio hili la kutunuku Kamisheni lifanyike Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa heshima kwa Maafisa wa JWTZ kama ambavyo Viongozi wengine Serikalini wamekuwa wakipata heshima ya kuapishiwa Ikulu.



"Kwamba Mawaziri tunapotaka kuwaapisha tunawaapishia hapa, Wakuu wa Mikoa tunawaapishia hapahapa, Makatibu Wakuu tunawaapishia hapahapa, kwa nini hawa Maafisa wa Jeshi tusiwaapishie hapahapa kwenye nyumba yao? Nyinyi ndio mnalinda nchi, nyinyi ndio mnasimamia usalama wa nchi hii, lakini nikiuliza hapa inawezekana wengine mpaka wamekuwa Mabrigedia Jenerali hawajawahi kukanyaga Ikulu, wakati hapa ni kwenu"alisema Rais Magufuli.



Sherehe za kutunuku Kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi hao zilihudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi na Wakuu wa Jeshi la Ulinzi wastaafu na Majenerali wastaafu wa JWTZ.



Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam


Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitunuku kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam  Novemba 26, 2016

Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akikagua gwaride la heshima linaloundwa na Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku kamisheni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es  salaam  Novemba 26, 201.


 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 201


Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiweka saini kwenye hati  ya  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) kabla hajawatunuku katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 201


 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam  Novemba 26, 201.


 Amiri Jeshi Mkuu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea baada ya kutunuku  kamisheni kwa Maafisa Wanafunzi wa Kundi la 59/15 wa Jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) katika ukumbi wa mikutano wa Ikulu jijini Dar es salaam Novemba 26, 201



PICHA NA IKULU

Serikali yampokonya Sumaye shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33

$
0
0

Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye amepokonywa na Serikali shamba lake lenye ukubwa wa hekta 33 kwa kile kilichoelezwa kushindwa kuliendeleza.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi amesema kuwa Serikali imefikia uamuzi huo baada ya Sumaye kushindwa kuliendeleza kama notisi ya siku 90 ilivyoeleza.

“Oktoba 28, mwaka huu. Rais John Magufuli alibatilisha hati ya kumiliki ardhi ya shamba namba 3074 lililopo Mabwepande. Shamba hili lilikuwa na hati namba 53086. Jina la mmiliki lililoandikwa katika hati ni Frankline Sumaye,” amesema Hapi.

Sumaye ambaye alikuwa ni mmoja wa wasemaji tegemeo katika mikutano ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu uliopita ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), anamiliki mashamba makubwa yaliyoko Morogoro na Mabwepande Dar es Salaam.

Baada ya Rais Magufuli kubatilisha hati hiyo, Hapi amesema kuanzia sasa ni marufuku kwa Sumaye kujihusisha na shamba hilo.

Kwa sababu hati yake imeshabatilishwa na akibainika kufanya chochote vyombo vya dola vitachukua nafasi yake.

“Vyombo vya ulinzi na usalama watakuwapo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba shamba hili halitafanyiwa shughuli zozote, isipokuwa baada ya taratibu za manispaa zitakapofanyika,” amesisitiza Hapi.

Amesema amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli kupima viwanja vya shamba hilo na kwamba wananchi waliokuwa na mgogoro wa shamba hilo wafikiriwe.

Februari 5 mwaka huu, akiwa Morogoro, Rais John Magufuli aliwataka watu wote waliotelekeza mashamba kuyaendeleza, la sivyo atawanyang’anya na kuwapa wananchi.

Lowassa Awajibu wanasiasa waliodai ni mgonjwa na atakufa

$
0
0
Aliyekuwa  mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, amewashukuru wananchi kwa kumpigia kura kwa wingi licha ya baadhi kumsema vibaya kwa kumwita mgonjwa na kwamba angekufa.

Lowassa ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, alitoa kauli hiyo mjini Mbinga mkoani Ruvuma ambako chama hicho kipo katika ziara ya kufanya mikutano ya ndani.

Akizungumza ndani ya vikao hivyo, Lowassa pasipo kutaja jina la mtu yeyote alisema: “Mwacheni Mungu aitwe Mungu, kwa sababu wote hata walionisema mabaya baadhi yao wameshatangulia mbele ya haki.”

Alisema kitendo cha wananchi kumpigia kura kwa wingi pamoja na kwamba alikuwa akizungumziwa vibaya juu ya afya yake, ni wazi kuwa walikubali kubeba lawama juu yake.

“Bila ujasiri na umoja wa dhati, hawa jamaa wataendelea kutupiku… lakini niwashukuru vile vile kwa kukubali kubeba lawama juu yangu, wapo waliosema huyu ni mgonjwa atakufa, bado mlinipigia kura nyingi ila Mungu ndiye hupanga yote,” alisema.

Pamoja na hayo, Lowassa aliwataka wanachama wa Chadema kuendelea kuwa na ujasiri na kudumisha umoja kwa kuendelea kujipanga kwa uchaguzi wa mwaka 2020.

Hii ni mara ya kwanza kwa Lowassa kuzungumza juu ya watu ambao walihoji kuhusu mwenendo wa afya yake wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Baadhi ya wanasiasa, hususani wale waliokuwa wakimpinga, walijaribu kuionyesha na hata kuiaminisha jamii kwamba mwanasiasa huyo ni mgonjwa na hafai kuongoza nchi.

Wapo ambao walidiriki kusema kwamba Ikulu si hospitali na wala hakuna gari la kubebea wagonjwa.

Miongoni mwa wapinzani wake ni baadhi ya wanasiasa wakubwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiwamo viongozi waliosikika katika majukwaa ya kampeni  mwaka jana wakiwashawishi wananchi kutomchagua Lowassa kwakuwa hata akipata urais hatotawala muda mrefu atakufa.

Wapo waliokwenda mbali na kusikika wakimwambia Lowassa Ikulu si wodi ya wagonjwa, hivyo hafai kupatiwa nafasi ya urais kulingana na afya aliyonayo.

Mikutano ambayo Lowassa ameitumia kuzungumzia suala hilo, inafanyika nchi nzima pamoja na kuwahusisha wajumbe wa ngazi mbalimbali za chama.

Uwepo wa Lowassa katika mikutano hiyo imesababisha watu wengi kukusanyika wakitaka kumuona.

Hata Lowassa anapokuwa anaondoka katika eneo hilo kuelekea mahali kupumzika, wananchi wamekuwa wakiunga msafara kwa kumfuata nyuma.

Mikutano hiyo inatajwa kuwa sehemu ya operesheni ya siku 40 inayofanyika nchi nzima iliyopewa jina la ‘Amsha Amsha’.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatanu ya Novemba 28

Rais Magufuli Apokea Marais Wawili Ikulu Jijini Dar es Salaam

$
0
0
RAIS John Magufuli jana aliwapokea marais wawili, Edgar Lungu wa Zambia aliyewasili kwa ziara ya kiserikali na Idriss Deby wa Chad aliyekuja kikazi.

Tofauti na Lungu ambaye ziara yake ilifahamika tangu wiki iliyopita, ujio wa Rais wa Chad ulikuwa wa ghafla na hata serikali ilitoa taarifa ya ujio wake jana saa chache kabla ya kuwasili nchini kiongozi huyo ambaye kwa sasa ndiye Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU).

Wote wawili baada ya kuwasili nchini walipigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride na ngoma za asili.

Licha ya kupokelewa na Rais Magufuli, viongozi wengine waandamizi wa Serikali pia walishiriki kwenye mapokezi ya viongozi hao. Rais Deby aliwasili saa 8 mchana na kulakiwa na Rais Magufuli na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, mwenzake Lungu aliwasili saa 11.20 alasiri na kulakiwa na Rais Magufuli na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan.

Ratiba ya ziara yao inaonesha kuwa kila mmoja atafanya mazungumzo Rais Magufuli katika Ikulu ya Dar es Salaam. 

Shughuli za Lungu 
Ratiba ya Rais Lungu inaonesha leo asubuhi atatembelea ofisi za Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na shirika hilo la ubia baina ya nchi hizo.

Baadaye atazuru pia Shirika la Bomba la Mafuta la Tazama, ambapo atatembelea mitambo ya kusukuma mafuta, pamoja na matangi ya kuhifadhi mafuta ya Tazama vyote vilivyopo eneo la Kigamboni. 

Baada ya ziara hizo za asubuhi, Lungu na ujumbe wake watafanya mazungumzo rasmi na Rais Magufuli, pamoja na Viongozi Waandamizi wa Serikali ya Tanzania.

Mazungumzo hayo yatafanyikia Ikulu kuanzia saa 5:00. Marais hao wawili pia watashuhudia utiaji saini wa Makubaliano na Mikataba mbalimbali minne (4) ya ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania kwa upande mmoja na Serikali ya Zambia.

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilifafanua kuwa mikataba hiyo inahusu kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano uliopo baina ya nchi hizo. Katika ratiba hiyo, leo jioni Rais Lungu atahudhuria dhifa ya kitaifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais Magufuli. Dhifa hiyo itafanyika Ikulu kuanzia saa 12;30 jioni.

Aidha, kesho Rais Lungu atatembelea Bandari ya Dar es Salaam ambapo atajionea shughuli mbalimbali za upokeaji na upitishwaji wa mizigo bandarini hapo.

Baadaye atafanya ziara fupi kwenye Kampuni ya kusafirisha mizigo inayomilikiwa na Serikali ya Zambia inayojulikana kama Zamcargo, kisha ataelekea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ambako ataagwa rasmi na mwenyeji wake Rais Magufuli kurejea nchini kwake Zambia.

Katika taarifa hiyo ya Mambo ya Nje inaeleza kuwa ziara ya Rais Lungu inatarajiwa kutoa fursa ya kuzidisha uhusiano na kukuza ushirikiano ili kuongeza ufanisi wa Reli ya Tazara ambayo ni mhimili na kiungo muhimu katika ukuzaji wa uchumi wa Tanzania na Zambia, lakini pia na kwa nchi nyingine majirani za ukanda wa kusini na kati mwa Afrika za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zimbabwe na Malawi.

Pia eneo lingine litakuwa ni kukuza ushirikiano katika matumizi ya bomba la Tazama ambalo lilijengwa mwaka 1968 kwa lengo la kutoa njia nafuu ya kusafirisha mafuta ghafi kwenda nchini Zambia na hivyo kuiepusha nchi hiyo na athari za kupanda kwa bei ya mafuta. Hata sasa umuhimu wa bomba hilo bado upo.

Eneo lingine litakuwa ni ushirikiano katika matumizi ya Bandari ya Dar es Salaam ambayo kwa muda mrefu Zambia kama nchi ambayo haina bandari imekuwa ikitumia Bandari ya Dar es Salaam kupitisha mizigo yake. Kwa sababu za kiuchumi na za kihistoria, nchi hiyo imeendelea kuwa mdau mkubwa katika matumizi ya bandari hiyo.

Rais Deby
 Taarifa iliyotolewa na serikali inaonesha Rais Deby ambaye ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, atafanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na watapata fursa ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Ukanda wa Afrika Mashariki na Umoja wa Afrika kwa ujumla.

Deby amefuatana na mkewe, Hinda Deby, Moussa Faki Mahamat ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje, Mtangamano wa Afrika, na Ushirikiano wa Kimataifa wa Chad na viongozi wengine waandamizi wa Serikali ya Chad.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake  Rais wa Jamhuri ya Chad Mhe Idriss Deby Itno mara  baada ya kiongozi huyo kuwasili katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam  Novemba 27, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Zambia Mhe. Edgar Chagwa Lungu akisalimiana na mabalozi wanaowakilisha nchi mbalimbali za Afrika nchini mara tu baada ya kupokewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Magufuli katika uwanja wa  ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Novemba 27, 2016.

Mchungaji Anthony Lusekelo maarufu 'Mzee wa Upako' Afunguka Kuhusu Sakata la Kuwatukana Majirani Zake

$
0
0
Siku tatu baada ya kudaiwa kumfanyia fujo jirani yake, Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo maarufu Mzee wa Upako, amejibu tuhuma hizo akisema anaishi kana kwamba hana jirani.“...Tunaishi kama majambazi tu, hujui jirani yako ni nani,” amesema.

Lusekelo amesema Yesu ambaye ni  mwana wa Mungu alikubali kudhalilishwa na baadaye kufa bila hatia hivyo na yeye alikubali kula kiapo katika nafasi ya utumishi wake.

Amesema magazeti wa  mitandao ya kijamii hayawezi kumshusha kwa kuwa hayakumpasha ila Mungu pekee.

Katika mahubiri yake yaliyohudhuriwa na waumini wengi kama ilivyo kwa Jumapili nyingine za karibuni kanisani kwake, Ubungo Kibangu, mchungaji huyo aliingia kwa mapokezi ya wimbo wa kuabudu uitwao ‘Angalia Bwana’ kabla ya waumini kuanza kumtunza kwa sadaka kama ilivyo kawaida ya ibada zake.

Katika mahubiri hayo alisema haiogopi jela, bali anaogopa kuvunja sheria za nchi na wala alipokamatwa na Polisi haikumtisha wala kumvunja moyo, kwani viongozi wa dini wamekula kiapo hadi kufa. 

Aidha, alisema wapo waliosema kuwa Mzee wa Upako alikuwa anatukana, alidai kuwa matusi yake yote ni maandiko na anayetaka ufafanuzi wowote akipata nafasi amuulize yameandikwa katika vitabu gani li apate kuelewa.

Alisema mpumbavu sio tusi hayo ni maelezo na Yesu alitukanwa sana, na hata ushenzi si tusi lina maana pana ya kwamba huna hofu ya Mungu, mjinga ana dhambi ya mauti, inayomsubiri kwenda peponi.

Hata hivyo, aliwausia waumini wa kanisa hilo kuwa kamwe wasimtukane mtu kwa umbo ama rangi yake kwa kuwa hakupenda kuzaliwa hivyo na waishi hivyo kwa kutenda mema kwa kuwa ufalme wa Mungu watauona.

Alisema tangu kutokea kwa tukio amekuwa akipigiwa simu na watu ambao hakuwategemea huku waandishi wakimtaka kuzungumzia chochote wakiwamo waandishi wa habari ambao alisema walikuwamo ndani ya kanisa hilo jana.

Akifafanua kilichotokea siku hiyo, alieleza kuwa alitoka saa 11 alifajiri bila kufafanua alikuwa akitokea wapi, ndipo alipokutana na watu wawili akiwemo Mmasai na dada mmoja alipowauliza wanatokea wapi katika eneo hilo ambalo wakazi wengi wa huko hutoka na magari yao, ndipo ugomvi ulipoanzia.

“Hawa watu wa magazeti wanataka kuuza magazeti, barabara hiyo nimeijenga mimi hivyo nilikuwa na haki ya kuwauliza maana ni kibarabara... washenzi wakubwa wanaandika tu, halafu wanasema nimewatukana majirani kule hakuna jirani hajui wanaingia saa ngapi na wanatoka saa ngapi na hakuna hata habari za asubuhi. Kila mmoja anatumia gari lake,” alieleza Mzee wa Upako.

“Kwanza waliandika habari kwamba waumini hawatakuja kanisani badala yake wamejitokeza bila kukatishwa tamaa. Wakati mnajitokeza hapa mbele (kutoa sadaka), alipita mama mmoja amebeba mtoto, nilimwombea mwaka jana hapa kwamba atapata mtoto na leo amepata mtoto, sasa mbona magazeti yasiandike habari hizo?”

“Kwa nini wasiandike hayo mazuri ‘front page’ (ukurasa wa mbele)?, halafu mnaandika Mzee wa Upako matatani, matatani babu yako.”

“Najua na leo mmekuja mpo humu mnasubiri niseme, nasubiri mmalize kwanza nyinyi halafu na mimi ndiyo nitasema, baada ya mwezi mmoja najua mtakuwa mmemaliza,”alisema.

Hatima ya dhamana ya Godbless Lema kujulikana leo

$
0
0

Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, leo, anatarajia kujua hatima ya dhamana ya kesi ya uchochezi inayomkabili.

Lema anashikiliwa katika mahabusu ya Magereza ya Kisongo mjini Arusha.

Wakili wake, Peter Kibatala amesema walikata rufaa chini ya hati ya dharura kuomba Mahakama isikilize kesi hiyo mapema.

Amesema waliamua kufuata maelekezo ya Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Mosha ya kuwataka kukata rufaa.

Katibu wa mbunge huyo, Innocent Kisanyage amesema rufaa hiyo itasikilizwa leo saa tatu asubuhi baada ya kukamilisha mambo yanayotakiwa.

Lema alirudishwa mahabusu kutokana na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kukataa kupokea ombi lake la kufanya marejeo ya uamuzi wa kunyimwa dhamana.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mosha alisema uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi umeegemea kifungu cha Sheria cha Makosa ya Jinai CPA 148, hivyo kilimtaka mshtakiwa kukata rufaa siyo kuomba Mahakama hiyo kufanye rejea,

Rufaa hiyo itasikilizwa na Jaji Fatuma Massengi, huku Lema akitimiza siku ya 26 tangu apelekwe Gereza la Kisongo.


CUF Yanyimwa Ruzuku....Maalim Seif Ataja Hujuma 9 Zinazofanywa na Profesa Lipumba

$
0
0
Katibu  Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, ameibuka na kutaja utatu unaojumuisha mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi na Jeshi la Polisi akieleza ndio unaoshirikiana kukihujumu chama hicho, huku akibainisha mambo tisa anayoeleza kuwa ‘ushahidi wa ushirikiano’ na hujuma hizo.

Akizungumza katika mkutano na wahariri na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu kuibuka kwa mgogoro ndani ya chama hicho baada ya Jaji Mutungi kumtambua profesa Lipumba kuwa  mwenyekiti wa CUF, Maalim Seif alitumia dakika 95 kueleza hujuma hizo na kudai zinalenga kukifanya chama hicho kutodai haki ya kunyang’anywa ushindi wa Uchaguzi Mkuu Zanzibar.

Akiwa sambamba na viongozi mbalimbali wa chama hicho, alisema hana ugomvi na Profesa Lipumba na yupo tayari kukaa naye meza moja kueleza uongo wa mtaalamu huyo wa uchumi, ikiwa ni pamoja na ukweli anaouficha kuhusu kujiuzulu kwake uenyekiti wa CUF Agosti mwaka jana na uamuzi wake wa kutaka kurejea katika chama hicho.

Mbali na kukiri CUF kupitia katika wakati mgumu kwa sasa, Maalim Seif alisema hujuma hizo zilizotokana na ‘wakubwa’ kuchukizwa na kitendo cha chama hicho kuwasilisha vielelezo Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa (ICC) vinavyowatuhumu viongozi wa Serikali kutumia mamlaka yao vibaya katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana,  zimesababisha chama hicho kutopata ruzuku ya Sh milioni 117 kila mwezi, tangu Agosti mwaka huu.

“Mtiririko wa matukio haya (tisa) yanaonesha wazi  hujuma hizi…, ni  mambo yanayoratibiwa kwa suhirikiano wa  makusudi  kati ya msajili, polisi na Lipumba,“ alisema Maalim Seif.

Aliyataja mambo hayo kuwa ni kuvamiwa kwa Mkutano Mkuu wa CUF iliofanyika Agosti 21, utekaji wa wanachama na viongozi wa chama hicho, kuvamiwa kwa ofisi kuu iliyopo Buguruni, kuvunjwa kwa ofisi za wilaya ya Bagamoyo na Mkuranga, wabunge na wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho kuzuiwa kufanya kikao cha ndani.

Mengine ni kuzuiwa kufanyika kwa mkutano mkuu maalumu wilaya ya Tanga, utekaji wa mlinzi wa chama hicho uliofanyika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, kuzuiwa kwa kikao cha ndani mkoani Mtwara pamoja na walinzi wa Profesa Lipumba kutaka kuzuia viongozi wa CUF kuingia chumba cha mahakama kuu hiyo.

Agosti 8 mwaka jana Profesa Lipumba alitangaza kuachana na uongozi wa chama hicho, baada ya CUF kukubaliana na Ukawa kumsimamisha Edward Lowassa kuwania urais.

Hata hivyo, Juni mwaka huu Profesa huyo aliomba kwa barua kurejea kwenye wadhifa wake, ambao kwa sasa unashikiliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro aliyechaguliwa katika mkutano wa  Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho.

Uamuzi wake huo ulizua  sintofahamu ndani ya CUF  huku mkutano mkuu wa dharura wa chama hicho uliofanyika Agosti 21 mwaka huu kumchagua mwenyekiti mpya ukivunjika baada ya kundi la wafuasi wa chama hicho kuvamia na kufanikiwa kuzima mchakato wa kupiga kura kumchagua mwenyekiti mpya, wakishinikiza Profesa Lipumba aruhusiwe kurejea katika wadhifa huo.

Baada ya sakata hilo Baraza Kuu la Uongozi la chama hicho lilimvua uanachama Profesa Lipumba na kuwasimamisha uanachama makada kadhaa wa CUF, jambo ambalo liliingiliwa kati na Msajili wa Vyama vya Siasa aliyetoa waraka wa kumtambua Lipumba kuwa mwenyekiti.

Kitendo cha Lipumba kutambuliwa na kurejea katika chama hicho kilisababisha Baraza la Wadhamini la CUF kufungua kesi Mahakama Kuu na kumshtaki profesa huyo  Jaji Mutungi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju.

Katika ufafanuzi wake, Maalim Seif alisema Lipumba alivamia Mkutano Mkuu wa chama hicho akiongozwa na polisi na kusababisha vurugu kubwa sambamba na uharibifu wa mali lakini polisi haikuchukua hatua yoyote.

“Kumekuwa na matukio kadha aya utekaji wa viongozi na wanachama wa CUF…, mkurugenzi wetu wa fedha Joram Bashange alitekwa akiwa anatoka nyumbani kwake na walinzi wa Lipumba, licha ya kukamatwa na kufikishwa polisi waliachiwa na gari walilotumia nalo halipo kituo cha polisi buguruni,” alisema.

Alisema Septemba 24 mwaka huu, Lipumba na wafuasi wake walivamia ofisi kuu ya CUF iliyopo Buguruni na kufanya uharibifu huku akipewa ulinzi mkali wa polisi.

“Polisi kazi yao ni ulinzi wa raia na mali zao pamoja na kupambana na wahalifu lakini hivi sasa wao ndio wanatetea wahalifu. Tunamuomba Mwigulu (Nchemba-Waziri wa Mambo ya Ndani) kuingilia kati na kutizama watendaji walio chini ya wizara yake,” alisema Maalim Seif.

Alisema tukio la nne ambalo polisi imeshindwa kukamata wahusika licha ya kuwajua ni uvamizi uliofanywa na wafuasi wa Lipumba wa kuvunja ofisi za chama hicho wilayani Bagamoyo na Mkuranga.

“Wabunge na wajumbe wa Baraza Kuu la uongozi la chama walizuiwa kufanya kikao cha ndani Newala na kukamatwa walipokuwa Nachingwea,” alisema na kubainisha kuwa wakati viongozi hao wakikamatwa, Lipumba anafanya vikao kama hivyo bila kukamatwa.

“Polisi walizuia kufanyika kwa mkutano mkuu maalum wa wilaya ya Tanga kwa madai kuna pande mbili zinavutana. Pia Novemba 10 mwaka huu mlinzi wa chama, Mohamed Said alitekwa akiwa mahakama kuu na kupigwa sana na kunyang’anywa fedha na kupelekwa kuhojiwa na Lipumba. Tukio hilo lilitokea mbele ya polisi,” alisema.

Alisema jeshi hilo pia lilizuia kufanyika kwa kikao cha ndani mkoani Mtwara pamoja na walinzi wa Lipumba kutaka kuzuia viongozi wa CUF kuingia ndani ya chumba cha mahakama kufuatilia shauri lao, huku akimtaja mmoja wa walinzi hao kuwa ni Hassan Kingwele.

Akijibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa na Lipumba, Maalim alisema msomi huyo anatumiwa na dola  na kubainisha kuwa anaficha ukweli juu ya uamuzi wake wa kujiondoa CUF.

“Lipumba bado hajasema sababu za kweli juu ya kujiuzulu kwake, yeye ndio alikuwa mwanzilishi wa Ukawa katika Bunge Maalum la Katiba na ndio aliyemtafuta Lowassa na kumshawishi awanie urais kupitia Ukawa,” alisema.

“Lowassa ilikuwa ajiunge na NCCR kwa sababu ni chama kidogo ili CUF na Chadema tumuunge mkono kwa mantiki hiyo iweje Lipumba aseme mimi sikumshirikisha ujio wa Lowassa ndani ya Ukawa?”

Alisema yeye hana ugomvi na Lipumba bali mtaalam huyo wa uchumi ana ugomvi na CUF, huku akidai kuwa hivi sasa anatumia udini, ukabila na uzanzibari kukigawa chama hicho.

“Hizi ni jitihada za dola kunifanya nisidai haki kwa yaliyotokea Zanzibar…, hilo halitawezekana nitaidai tu mpaka mwisho,” alisema.

Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.

$
0
0
Jiji la Mbeya ni la pili kwa wingi wa madhehebu barani Afrika likiongozwa na Lagos lililopo Nigeria.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika, jiji hilo lina makanisa 450  na Mtaa wa Sae pekee una madhehebu tisa huku Mtaa wa Simike ukitajwa kuongoza kwa vituo vya maombezi.

Meya wa Jiji la Mbeya, Mchungaji David Mwashilindi ambaye ni kiongozi wa Kanisa la International Evangerism Assemblies  of God, amesema migogoro ndani ya madhehebu, uroho wa madaraka na utapeli ni miongoni mwa sababu ya watu kuamua kuanzisha madhehebu kila kukicha.

Meya huyo ambaye pia ni msimamizi wa kanisa hilo katika mikoa ya Ruvuma, Iringa, Njombe na Rukwa, amesema hakuna ubaya wa kuwa na madhebu mengi kama yanaanzishwa kwa kufuata utaratibu, sheria na misingi ya Mungu.

Amesema madhehebu mengi ya kilokole jijini humo yaliibuka baada waamini kuamua kujitenga madhehebu yao ya awali kutokana na migogoro.

“Kuna madhehebu yanamiliki vyuo vya wachungaji wanaosomea kwa mujibu wa maadili ya Mungu, kama Lutherani, Wakatoliki, Moravian, Wasabato na la kwangu, lakini tatizo wapo wachungaji wa kujipachika ambao mara nyingi wanatiliwa shaka kwa vitendo vyao,” amesema meya huyo.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 95 & 96 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"Ndio hivyo, dokta wake amesema tunaweza kumpoteza mama muda wowote kuanzia leo. Hapa nilipo nimechanganyikiwa"
Nikakata simu, mwili mzima nikawa kama umezizima, picha ya Jonh na Sheila zikanijia kichwani jinsi walivyo kua na furaha, nilipo waona kwenye mgahawa.
"John nilazima ulipe kwa hili. Nikatuua kwa mkono wangu mwenyewe, ole mama yangu afe, nitakufanya kama Derick"

ENDELEA
Kila nilicho kifikiria juu ya adhabu nitakayo mpa John, sikupata jibu la uhakika. Nikazima kila kitu na kurudi chumbani kwetu. Nikajilaza kitandani taratibu huku mawazo yakiendelea kuniandama. Kikubwa nikawa ninamfikiria sana mama yangu. Sikulala hadi kunapambazuka.
"Umeamkaje baby?"
Phidaya alinisalimia mara baada ya yeye kuamka.
"Safi vipi?"
"Ahaaa poa, alafu nimeota ndoto mbaya kama nini?"
"Ndoto gani?"
"Nimeota John amekuja hapa tulipo, akiwa na wale watu wake, akatufunga kamba, sote wanne, kisha wakatuweka hapo sebleni. Wakamwaga mafuta ya petroli kila sehemu, na kuwasha moto wao wakaondoka. Ndio nikastuka"

"Mmmm hakuna kitu kama hicho"
Niliamua kumfariji Phidaya, kwani sikupenda apoteze amani asubuhi hii, ambayo tunaendelea kujiandaa na maandalizi ya sherehe ya kuzaliwa kwa Junio wetu.
"Hapa nilipo mapigo ya moyo yananienda mbio."
  Nikamvuta karibu yangu na kumlaza kifuani mwangu, taratibu nikaanza kuzichezea nywele zake ndefu na laini.
"Tulia mke wangu"
"Eddy naogopa"
"Umaogopa nini mke wangu"
"Nahisi familia yangu, itapata shida tena. Tena hii itakua kubwa kuliko ya kwanza"
"No baby usiyape nguvu, mawazo hayo mimi nipo. Nitahakikisha hakuna kitakacho haribika wala mtu kunyanyua mkono wake juu ya familia yangu nipo tayari kwa lolote hata kufa ili mradi familia yangu iishi kwa amani"
"Kweli baby?"

"Ndio kama aliweza ile mara ya kwanza basi hii ya pili, hato weza kamwe"
Nilizungumza huku nikiwa na jazba ya hasira, kwani hadi hapa ninavyo zidi kumfariji mke wangu, tayari John amesha yaweka maisha ya mama yangu mashakani. Taratibu Phidaya akaanza uchokozi wa kitandani, sikuwa na hiyana zaidi ya kumpa haki yake anayo stahili kama mke wangu. Hadi tunamaliza kila mmoja akawa kwenye furaha isiyo simulika, kwani wote tulifika kwa wakati mmoja mwisho wa mechi yetu.

"Ngoja nikaandae kifungua kinywa"
"Sawa"
Phidaya akanyanyuka na kuingia bafuni, akaoga na kutoka. Akavaa nguo alizo amua kuvaa kwa siku hii yaleo na kwenda nje. Nikachukua simu ya mezani, nikaziingiza namba za Blanka na kumpigia. Simu ikaita baada ya muda ikapokelewa.
"Vipi hali ya mama?"
"Kuna mabadiliko kidogo?"
"Mazuri au mabaya?"
"Mazuri, nilimuonyesha mama picha yako ukiwa na mkeo na mwanao. Kidogo mama alianza kufungua kinywa huku akitabasamu"

"Hakusema chochote?"
"Hapana, alitabasamu tu na kutingisha kichwa kama mtu aliye furahi kwa kuiona hiyo picha"
"Poa nitakuja"
"Kwani upo wapi?"
"Nitakuambia siku nyingine. Kwaheri"
Nikakata simu, baada ya kumuona Junio akiingia chumbani huku akilia jambo lililo nistua sana.
"Mona unalia?"
"Mamy kanipiga"
Kidogo mapigo ya moyo yakanitulia.
"Kisa nini?"
"Eti hataki nimsaidie kupika chai"
"Ni hilo au kuna jengine"
"Nihilo dady"
"Mwanao ni muongo"
Phidaya aliingia huku akionekanana kukasirika.
"Amefanyaje?"
"Nimemuambia asicheze mpira ndani, likawa halinielewi. Mpaka akaipiha Tv ya ukutani ikaanguka"

"Imevunjika?"
"Hapana, haijavunjika. Tena huku nje usitoke ubaki humu humu na huyo baba yako. Sitaki kukuona huku nje sawa?"
Phidaya alizunguilmza na kutoka nje, nikamnyanyua Junio na kumtupia kitandani nilipo na kumfanya aanze kucheka na kufurahi.
"Huo uronaldo wako, uwe unaufanyia nje sawa mwangu?"
"Sawa dady, twende tukacheze nje"
Junio alizungumza huku akinivuta mkono, nikatizama saa ya ukutani inaonyesha ni saa tatu asubuhi.
"Nenda ukaningoje sebleni nioge mara moja"
"Ok dady"
Junio akatoka nikaingia bafuni na kuoga, kisha, nikavaa nguo za mazoezi na kutoka nje.
"Munaenda wapi?"
Phidaya alutuuliza baada ya kutuona tukitoka mlangoni bila ya kuaga.
"Ufukweni"
"Kifungua kinywa tayari"
"Anzeni tu sisi tunakuja"
"Eddy mbona unapenda kumuendekeza huyo mwanao, kila anacho taka unamfanyia"
Nikamfwata Phidaya na kumbusu mdomoni.
"Tunakuja baby, Shamsa yupo wapi?"
"Yupo jikoni anamalizia kupika"
"Ok tunakuja"

Tukatoka na Junio, tukaingia kwenye lifti na kushuka hadi chini, tukitokea gorofa ya saba, yalipo makazi yetu. Tukaelekea kwenye fukwe zilizopo pembezoni mwa hotel hii. Kitu kilicho nishangaza ni jinsi Junio alivyo maarufu kwa watoto wezake ambao tuliwakuta hapa ufweki. Wakaunda timu mbili huku nami nikiwa timu pinzani na Junio. Wakanichagua kua goli kipa na sikuwa na jinsi. Magoli ya viayu tuliyo yaweka hayakuzuia mechi kuanza, huku golikipa wa timu ya Junio, akiwa mzee mwenye mjukuu wake kwenye timu yangu.

Hapa ndipo nilipo pata fursa ya kumtazama Junio vizuri, nakugundua anakipaji kikubwa cha kucheza mpira. Mara kadhaa akawa anapiga mashuti mazito golini mwangu, ambayo niliweza kuyanyaka vizuri. Huku wachezaji wa timu yangu wakinisifia kwamba ninaweza kazi ya kulinda goli. Kitendo cha kuinyaka mipira, ndivyo jinsi Junio alivyo ongeza juhudi ya kucheza na kupiga mashuti mazito golini.
"Kumbe na wewe ni kipa mzuri?"
Mzee wa timu ya Junio ambayo hadi sasa hivi hakuna goli alilo fungwa, aliniuliza tulipokua tukibadilishana magoli, baada ya dakika kumi na tano alizo tuwekea refa wetu kuisha.

"Najaribu tuu"
"Hapana, kuna kitu nimekiona ndani yako na huyo mwanao"
"Kitu gani?"
"Muna vipaji vikubwa sana, hakikisha unamuendeleza mwanao katika fani hii, atafanikiwa sana na atakuwa mchezaji mkubwa sana duniani"
Sauti ya filimbi ikatustua mimi na huyu mzee, huki refa akituomba kila mmoja akakae kwenye goli lake, tukafanya kama alivyo tuelekeza.
Mpira ukaanza, japo kuna tifutifu jingi kwenye hii fukwe, ila Junio, anakimbia kuliko watoto wezake ambao mara kadhaa, walikua wakianguka anguka.
Shuti kali alilo lipiga Junio, akiwa karibu yangu, likanipita katikati ya miguu yangu na kwenda mbali kidogo na sehemu tunayo chezea mpira. Nakuwafanya Junio na timu yake kushangilia ushindi wa goli hilo walilo kua wakilitafuta kwa juhudi mara baada ya kipindi cha pili kuanza.
"Hahaaaa haaaaaa"
Nilimuona Phidaya akicheka, huku akiwa na kamera yetu. Nikatambua moja kwa moja anacheka goli, nililo fungwa na Junio.

"Junio kachukue mpira sijui umeenda wapi"
Nilimuambia Junio aufwate mpira wake ambao yeye ndio aliuona sehemu ulipo elekea. Junio akaongozana na wezake wawili kwenda kuutafuta.
"Unacheka nini?"
"Nakucheka wewe, ulivyo fungwa na huyo mwanao, njoo uone hili goli lilivyo ingia"
Nikamfwata Phidaya alipo, akanionyesha video aliyo rekodi, goli lililo pita katikati ya miguu yangu
"Mwanao amekupiga tobo"
"Huyu mtoto, ananguvu za miguu kama hadi ananiogopesha, skija golini"
"Ndio hivyo tumepata mchezaji, mzuri tusubirie atakaye kuja sijui atakuwaje"
"Huyo naomba awe wa kike"
"Kweli ehee"
"Au wewe unataka aweje?"
"Vyovyote Mungu atakavyo tubariki, nenda uwanjani wamesha rudi na mpira"

Mechi ikaendelea huku mipira mingi ikielekezewa golini kwetu, baada ya wachezaji wangu kuchoka sana. Ikanikazimu mara kadhaa nikaiokote mipira inayotoka nje ya goli letu. Mpira mmoja ukapigwa na mchezaji wa timu ya Junio, ukaenda mbali kidogo. Nikaanza kuukimbiza kwa bahati mbaya ukagonga glasi mbili za juisi zilizo wekwa kwenye kijimkeja, huku pembeni yake akiwa amelala, kifudifudi msichana mmoja, aliye valia chupi na sidiri, akiota jua na juisi zikamwagikia ubavunini.

RC Makonda atembelea Uwanja wa Fisi wanapofanya biashara ya ngono....Aahidi Kupavunja na Kujenga Viwanda Vidogovidogo

$
0
0
Jumapili Novemba 27 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda aliendelea na ziara yake katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam akiwa na lengo la kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Akiwa katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alipita katika viunga vya Kata ya Manzese na kutokea sehemu ambapo kula kilabu kinachouza pombe za kienyeji huku watu waliokuwa eneo hilo wakionekana kuwa wamelewa kiasi cha kutotambuana.

“Hii achana nayo kabisa ni moto wa kuotea mbali. Hebu niikate kidogo uone,” Mzee aliyefahamika kwa jina la Mandela alisikika akimtambia Paul Makonda huku akipiga funda la pomne hiyo ya kienyeji hali inayoonyesha kuwa hakuwa akifahamu kuwa anayezungumza naye ni Mkuu wa Mkoa.

Baadaye alienda eneo lenye vibanda vya chumba kimoja kimoja, amabavyo inaelezwa kuwa ni madanguro ambayo hutumika kufanyika biashara ya ukahaba hadi kwa wasichana wenye umri mdogo. Hata hivyo kila mlango aliojaribu kugonga ulikuwa umefungwa na hakuna aliyeitika na kufungua mlango.

“Hawa wakijua watu wa serikali wanakuja hapa basi hufunga biashara zote, sasa na hapa wamefunga, si rahisi kumpata mtu,” alisikika kijana mmoja mwenyeji wa eneo hilo akisema.

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Shule ya Msingi Tandale, Mkuu wa Mkoa Paul Makonda alisema serikali inafanya mipango ya kupata wawekezaji ili kununua eneo hilo la Uwanja wa Fisi na kuwalipa fidia wakazi wa eneo hilo ili vibanda vyote vivunjwe na kujengwa vitegauchumi badala ya kuliacha eneo hilo liharibu maisha ya vijana.

Vodacom Tanzania Yapeleka Maombi Ya Kujiunga Na Soko La Hisa (DSE)

$
0
0

Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imetangaza dhamira yake ya kuuza hisa kwa umma itakayofuatiwa na   kujiunga kwenye   Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya Elektroniki na Mawasiliano ya Posta (EPOCA) na sheria ya Fedha ya mwaka 2016 ambayo inaelekeza makampuni ya simu kumilikisha asilimia 25 ya hisa zake kwa wananchi kwa kujiunga na Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).

Akizungumzia hatua hiyo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom, Bwana Ian Ferrao alisema “Tunayo furaha kutangaza kuwa tumeanza rasmi mchakato wa kuuza hisa kwa umma kwa mujibu wa matakwa ya sheria na tumewasilisha maombi na utaratibu mzima utakaotumika kuuza hisa zetu na ratiba yetu nzima kuhusiana mchakato huu kwenye Mamlaka ya Usimamiaji wa Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) na Soko la Hisa (DSE).   

Hatua hii ni kubwa na inadhihirisha kuwa Vodacom ipo mstari wa mbele katika kutekeleza agizo la kuuza hisa zake kwa umma  na inadhihirisha jinsi ilivyojipanga  kuendelea kuboresha na kukuza sekta ya mawasiliano nchini Tanzania katika siku za usoni”.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(kulia) akimkabidhi hati ya maombi ya kujiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE)  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana (CMSA) Nicodemus Mkama(wapili kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki katika ofisi za CMSA jijini Dar es Saalaam,Kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima.
 
Uuzaji wa hisa kwa umma  na kujiunga na Soko la Hisa kunapitia  hatua mbalimbali za  kupata vibali kutoka taasisi za serikali zenye mamlaka ya kupitia maombi na kutoa  vibali vya utekelezaji wake.Ferrao aliendelea kueleza “Tunaamini uuzaji wa hisa zetu kwa umma utazidi kukuza shughuli za Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE),kunufaisha watanzania kiuchumi na kukuza uchumi wa nchi kwa ujumla. Kampuni yetu haitajulikana kwa jina la mwanzo la Vodacom Tanzania Limited bali imekuwa na jina la Vodacom Tanzania Public Limited Company (Plc) ikiwa ni hatua ya awali ya kujiandaa kuingia sokoni. 

Tunawahakikishia kuwa mchakato wa kuingia kwenye hatua hii umeanza vizuri kwa mafanikio na tunaendelea kuwashirikisha wadau mbalimbali kutoka serikalini kuhakikisha tunatimiza dhamira ya kuanza  kuuza hisa kwa wananchi yenye dira ya kuleta manufaa kwa wote.”
 
Ferrao alitoa msisitizo kuwa Vodacom inalo jukumu kubwa kuhakikisha hatua hii inaleta manufaa kwa pande zote zinatazohusika kuanzia  wanunuaji wa hisa, kuendelea kuwekeza , kuendelea kuleta mapinduzi ya ubunifu wa kiteknolojia na kuimarisha ubora wa huduma za kampuni kwa wateja wake “Tutaendelea kutoa mchango mkubwa wa ufanikishaji wa sera ya nchi ya miaka 5 ya kukuza sekta ya mawasiliano.Tutaendelea pia kuwaletea taarifa mbalimbali kuhusiana na mchakato wa kuuza hisa kwa umma unavyoendelea”Alisema Ferrao.
Mkurugenzi wa  Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha(kushoto)Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao, Mkurugenzi Mtendaji wa DSE,Moremi Marwa, Mkuu wa masuala ya kifedha  wa Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia,wakionyesha hati za maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE) mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi  Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Ian Ferrao,(watatu kushoto) akimkabidhi hati ya maombi ya kuijiunga na soko la hisa la Dar es Salaam,(DSE)  Mkurugenzi wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji na Dhamana(CMSA) Nicodemus Mkama wapili (kushoto) wakati wa hafla fupi iliyofanyike mwishoni mwa wiki  katika ofisi za CMSA jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima , wanaoshuhudia kutoka Kulia ni Mkurugenzi wa  Ushauri wa kutoka huduma za Orbit Securities Company Ltd. Gerase Kamugisha, Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (wapili kulia) na Mkuu wa fedha  wa kampuni ya Orbit Securities Company Ltd, Godfrey Gabriel (watatu kutoka kulia)

Diamond, Ali Kiba, Vanessa Mdee na Navy Kenzo kuwania tuzo Nigeria. Tazama wanaochuana nao

$
0
0
Kituo cha runinga cha Sound City (Sound City Tv) kimetoa orodha ya wasanii na vipingele watakavyowani katika tuzo za Sound City MVP.
 
Kwa upande wa Tanzania, katika tuzo hizo tutawakilishwa na Diamond Platnumz, Ali Kiba, Vanessa Mdee, Navy Kenzo. 

Diamond yeye anawania tuzo ya Msanii Bora wa Afrika (Best African Of The Year) na Msanii Bora wa Kiume (Best Male), Ali Kiba atawania tuzo ya Video Bora ya Mwaka (Video Of The Year) ambayo ni video ya wimbo wa aje, Vanessa Mdee yeye akitupa karata yake katika kipengele cha Msanii Bora wa Kike (Best Female) huku Navy Kenzo wao wakichuana kwenye Kundi Bora la Muziki (Best Group).
 
Hapa chini ni orodha kamili ya wasanii na vipengele watakavyowania;-
Best Male
  1. Diamond Platnumz (Tanzania)
  2. Emtee (South Africa)
  3. Wizkid (Nigeria)
  4. Falz (Nigeria)
  5. Olamide (Nigeria)
  6. Patoranking (Nigeria)
  7. Phyno (Nigeria)
Best Female
  1. Tiwa Savage (Nigeria)
  2. Victoria Kimani (Kenya)
  3. Yemi Alade (Nigeria)
  4. Vanessa Mdee (Tanzania)
  5. Cynthia Morgan (Nigeria)
  6. Ms Vee (Ghana)
  7. Simi (Nigeria)
Best Hip Hop
  1. Cassper Nyovest (South Africa)
  2. Olamide (Nigeria)
  3. Cdq (Nigeria)
  4. Emtee (South Africa)
  5. El (Ghana)
  6. Riky Rick (South Africa)
  7. Stanley Enow (Cameroon)
  8. Phyno (Nigeria)
Best Pop
  1. Wizkid (Nigeria)
  2. Kiss Daniel (Nigeria)
  3. Tekno (Nigeria)
  4. Yemi Alade (Nigeria)
  5. Adekunle Gold (Nigeria)
  6. Timaya (Nigeria)
  7. Tiwa Savage (Nigeria)
Digital Artiste Of The Year
  1. Psquare (Nigeria)
  2. Wizkid (Nigeria)
  3. A.K.A (South Africa)
  4. Tiwa Savage (Nigeria)
  5. Davido (Nigeria)
  6. Cassper Nyovest (South Africa)
  7. Tekno (Nigeria)
Best Collaboration
  1. Mr Eazi Ft Efya – Skintight (Nigeria / Ghana)
  2. Patoranking Ft Sarkodie – No Kissing (Nigeria / Ghana)
  3. Eddy Kenzo Ft Niniola – Mbilo Mbilo Remix (Uganda / Nigeria)
  4. Emtee Ft Wizkid & Aka – Roll Up (South Africa / Nigeria)
  5. Dj Maphorisa Ft Wizkid & Dj Buckz – Soweto Baby (South Africa / Nigeria)
  6. Phyno Ft Olamide – Fada Fada (Nigeria)
  7. Olamide Ft Wande Coal – Who You Epp (Nigeria)
  8. Harry Song Ft Olamide, Kcee – Raggae Blues (Nigeria)
  9. Masterkraft Ft Flavour & Sarkodie – Finally (Nigeria / Ghana)
Video Of The Year
  1. Pana By Tekno Directed By Clarence Peters (Nigeria)
  2. Aje By Alikiba, Directed By Meji (Nigeria)
  3. Babanla By Wizkid Directed By Sesan (Nigeria)
  4. One Time By A.K.A Directed By Aka & Alessio
  5. Sin City By Kiss Daniel Directed By H2g Films (Nigeria)
  6. Emmergency By D’banj Directed By Unlimited L.A (Nigeria)
  7. Made For You By Banky W Directed By Banky W (Nigeria)
  8. Gbagbe Oshi By Davido Directed By Slash (Nigeria)
  9. Pray For Me By Darey Directed By Mex (Nigeria)
Best Group Or Duo
  1. Sauti Sol (Kenya)
  2. Mafikizolo (South Africa)
  3. Micasa (South Africa)
  4. Navy Kenzo (Tanzania)
  5. R2bees (Ghana)
  6. Toofan (Togo)
  7. Psquare (Nigeria)
  8. Vvip (Ghana)
Song Of The Year
  1. Kwesta Ft Cassper Nyovest – Ngud (South Africa)
  2. Mr Eazi – Hol Up (Nigeria)
  3. Patoranking Ft Sarkodie – No Kissing (Nigeria)
  4. Wizkid – Babanla (Nigeria)
  5. Tekno – Pana (Nigeria)
  6. Emtee Ft Wizkid – Roll Up (South Africa / Nigeria)
  7. Dj Maphorisa Ft Wizkid & Dj Buckz – Soweto Baby (South Africa / Nigeria)
  8. Olamide Ft Wande Coal – Who You Epp (Nigeria)
  9. D’banj – Emmergency (Nigeria)
Best New Artiste
  1. Koker (Nigeria)
  2. Ycee (Nigeria)
  3. Mr Eazi (Nigeria)
  4. Emtee (South Africa)
  5. Simi (Nigeria)
  6. Niniola (Nigeria)
  7. Tekno (Nigeria)
  8. Nasty C (South Africa)
Viewers Choice
  1. Mr Soldier – Falz Ft. Simi (Nigeria)
  2. Babanla – Wizkid (Nigeria)
  3. Osinachi By Humblesmith Ft Davido (Nigeria)
  4. Pana By Tekno (Nigeria)
  5. Hollup By Mr Eazi (Nigeria)
  6. Pick Up – Adekunle Gold (Nigeria)
  7. Mama – Kiss Daniel (Nigeria)
Listeners Choice
  1. Lagos To Kampala – Runtown Ft Wizkid (Nigeria)
  2. Babanla – Wizkid (Nigeria)
  3. Omo Alhaji – Ycee (Nigeria)
  4. Pana By Tekno (Nigeria)
  5. Who You Epp – Olamide Ft Wande Coal (Nigeria)
  6. Oluwa Ni – Reekado Banks (Nigeria)
  7. Pick Up – Adekunle Gold (Nigeria)
  8. Skintight – Mr Eazi Ft Efya (Nigeria / Ghana)
African Artiste Of The Year
  1. Wizkid (Nigeria)
  2. Vannessa Mdee (Tanzania)
  3. Diamond Platinumz (Tanzania)
  4. Sarkodie (Ghana)
  5. Yemi Alade (Nigeria)
  6. Olamide (Nigeria)
African Producer Of The Year
  1. Dj Maphorisa (South Africa)
  2. Gospel On The Beat (Nigeria)
  3. Masterkraft (Nigeria)
  4. Young John (Nigeria)
  5. Legendury Beats (Nigeria)
  6. Sess The Problem Kid (Nigeria)
Mwisho wa kupiga kura kwenye tuzo za Soundcity MVP ni tarehe 27 Disemba mwaka huu. Unaweza kupiga kura kwa msanii  au kundi la muziki kwa kuingia hapa soundcitymvp.com.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images