Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CCM Zanzibar Waonyana Kuhusu Kusemana Kwenye Mitandao ya Kijamii

$
0
0
Baadhi ya Viongozi na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar wametakiwa kuacha tabia ya kutumia mitandao ya kijamii kujadili masuala yanayohusu Chama badala yake watumie vikao halali vinavyotambuliwa na Katiba ya Chama hicho.

Rai hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai wakati akifunga Mkutano wa Viongozi wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Kusini Unguja Kichama uliofanyika katika Shule ya Msingi Makunduchi Mkoani humo.

Alifafanua kwamba  tabia hiyo ya kujadili, kukosoa na kuwatuhumu baadhi ya viongozi wa ngazi mbali mbali wa Chama na Jumuiya zake kupitia Mitandao ya kijamii ni utaratibu unaokwenda kinyume na miongozo ya chama hicho.

Alisema  Katiba ya CCM inaelekeza Kwamba mambo yote yanayogusa maslahi mapana ya Chama yajadiliwe Katika Vikao halali vinavyotambuliwa na kanuni za Chama, kwani jukwaa hilo ndiyo sehemu rasmi ya kukosoana na kupeana maelekezo.

Vuai alisikitishwa na tabia hiyo na kueleza kuwa  njia pekee ya kumaliza Changamoto hiyo ni Wanachama na Viongozi kujenga utamaduni wa Kusoma na kuelewa Kanuni, Katiba na miongozo mbali mbali ya CCM ili kufahamu wajibu, majukumu, haki na maadili yanayoongoza Chama.

Alisema tabia hiyo imekuwa ikifanyika katika Magroup ya Mitandao ya kijamii zikiwemo Facebook, WhatsApp na mitandao mingine, jambo ambalo ni kosa kwa mujibu wa kanuni za Chama.

“ Wanachama, Viongozi na Watendaji naomba muelewe kwamba hiki Chama kinaendeshwa kwa utaratibu maalum ulioelezwa  Kikatiba , Kikanuni na miongozo mbali mbali, kwa nia ya kulinda hadhi na heshima  ya  Chama chetu, na hakuna jambo lolote linaloshindikana kupatiwa ufumbuzi kupitia utaratibu huo.

"Sasa panapojitokeza baadhi ya Watu miongozi mwetu wakaanza kujadili na kuwakosoa wenzao nje ya mfumo huo basi hao tunawahesabu kuwa  wana nia ya kuanzisha Majungu, Fitna na mpasuko katika taasisi yetu.”,   alieleza Vuai na Kuongeza kuwa CCM ni Chama imara na kinachoheshimu Demokrasia katika kujadili mambo yake na kuyatolea maamuzi stahiki katika Vikao rasmi na sio vichochoroni au vibarazani.

Aliongeza kuwa sio kwamba kuna viongozi na wanachama wanaogopa ama hawataki  kukosolewa lakini lazima heshima na nidhamu iwepo katika kutekeleza matakwa ya Demokrasia ndani ya Chama hicho kwa kuheshimu utaratibu uliowekwa Kikatiba.

Akizungumzia utekelezaji wa Ilani ya  Uchaguzi ya Chama hicho ya mwaka 2015/ 2020 katika Mkoa huo aliwapongeza Viongozi wa Majimbo wakiwemo wabunge, wawakilishi na Madiwani huku akiwasisitiza Viongozi wa Chama kuhakikisha wanakagua kikamilifu miradi inayotekelezwa na viongozi hao ili kujiridhisha kama inawanufaisha wananchi wote.

Aliwataka viongozi wa Chama na Jumuiya zake kuwa wa kwanza kutambua kero na changamoto za wananchi wa maeneo mbali mbali na waziwasilishe kwa Wakuu wa Wilaya (DC)  ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kudumu na Serikali.

“ Huu sio wakati wa kusubiri taarifa zinazohusu Changamoto za Chama, Jumuiya na Serikali ziletwe Ofisini, badala yake mtoke na kuzitafuta wenyewe ili kuwasaidia wanachama na wananchi kutatuliwa kero zao kwa haraka kupitia Mamlaka husika.”, alisisitiza Vuai.

Alisema Viongozi wanatakiwa kufahamu kwamba suala la kuwatumikia wananchi sio jambo la hiari bali ni lazima watekeleze kwa vitendo ahadi walizotoa wakati wa kampeni kwani wasipotekeleza Wajibu wao vizuri kwa jamii mwisho wa siku kitakacho hukumiwa ni Chama na sio kiongozi husika.

Aidha aliwakumbusha viongozi hao kwamba Chama na Jumuiya zake wanatarajia kufanya Uchaguzi mwaka 2017, hivyo waanze mapema kuwaelimisha, kuhamasisha na kuwaandaa kisaikolojia wanachama wa Chama hicho juu ya matumizi sahihi ya kanuni za UChaguzi ili kuepuka lawama zisizokuwa za lazima.

Alisema Wanachama wanatakiwa kuwachagua viongozi wenye sifa na wasiokuwa na Mukhari( kuoneana haya) katika kusimamia mambo ya msingi ya CCM na waumini wa kweli  wa Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964, Muungano wa Serikali mbili wenye vigezo hivyo ndio wanaofaa kuwa viongozi.

Hata hivyo aliwapongeza Rais wa Zanzibar, Dkt. Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli  kwa juhudi na kasi zao za kufanikisha mipango ya maendeleo ya nchi kwa ufanisi mkubwa hali inayoongeza hamasa kwa jamii kuendelea kuwaamini.

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini(NCCR) na kuhamia ACT-Wazalendo, Moses Machali ahamia CCM

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI NA WATANZANIA WOTE. ​

Kutoka mezani kwangu Moses Joseph Machali, Tarehe: 21/11/2016

Napenda kuutaarifu umma wa Watanzania kupitia kwenu waandishi wa habari kwamba ni jambo la ajabu na aibu kwa watu makini na wenye kuhitaji mabadiliko ya kweli Kuacha kuunga Mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini Uongozi wa Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli bila kusahau utendaji makini wa Waziri Mkuu wake Mhe. Majaliwa Kasim Majaliwa (Mb) pamoja na mawaziri mbalimbali wameonesha kutaka kufuata mwenendo wa Rais Magufuli na Waziri Mkuu wake.

Mimi Moses Joseph Machali niliyefanya sana siasa za Upinzani hapa nchini na niliyepiga kelele na kupinga siasa za kifisadi zilizoitawala nchi hii; niliyepinga pia ufisadi uliokuwa umeitawala serikali huko nyuma kwa nguvu na uwezo wangu wote nikishirikiana na wapinzani wenzangu, ninaamua kujiunga na watu wanaonesha dhamira safi ya kuiendeleza nchi yetu Tanzania. Watu wenye mwelekeo na dhamira ya kuijenga nchi yetu kwa maendeleo enedelevu ni jamii ya akina Magufuli, Kasim Majaliwa, nk.

Mwaka mmoja wa Uongozi wa Rais Magufuli na baadhi ya wasaidizi wake kupitia hatua mbalimbali zilizochukuliwa dhidi ya ufisadi uliokuwa umeigubika nchi yetu, inatosha kabisa kwa mtu yeyote makini kufanya uamuzi wa kumuunga mkono au kutokumuunga mkono Rais Magufuli.

Mimi nimechagua kumuunga Mkono Rais kwa vitendo, kwa sababu ninaposoma Rekodi yangu ya enzi nikiwa Mbunge (Hansard) na kabla ya kuwa mbunge ni kwamba nilipinga mnoo wizi na ufisadi wa kila aina; Nilipinga Matumizi ya fedha serikalini yasiyo ya lazima na yasiyo na tija kwa taifa (Rejeeni hotuba yangu ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi, nikiwa Waziri Kivuli wa wizara hiyo ya mwaka 2014/2015 na 2015/2016), vilevile bila kusahau hotuba zangu mbalimbali Bungeni na nje ya Bunge.

Kwa kushirikiana na wapinzania wenzangu enzi hizo tulishauri na kupinga ufisadi wa kila aina, tuliitaka serikali kufanya mambo yenye tija kwa taifa na sasa kila mwenye macho anaona hatua zinazochukuliwa na serikali ya awamu ya tano. Miradi kama ya Ujenzi wa Reli, Ununuzi wa ndege mbili na mipango ya kununua ndege zaidi kama namna ya kulifufua shirikia la ATCL ni mambo tuliyoyahitaji kuyaona wapinzani; sasa yanafanyika. Wale wenye dhamira ya dhati ya kuona nchi yetu ikipiga hatua, kamwe hatuwezi kubeza mambo hayo bali kuyaunga mkono.

Wale tuliosema na kupiga kelele kwamba Serikali ni dhaifu ktk kuwachukulia hatua watu mbalimbali wenye dhamana serikalini walioonekana kufanya vibaya serikalini ktk nafasi zao, leo tunaona kumekuwepo na kasi nzuri ktk kuwachukulia hatua watu hao. Hata hivyo leo hii upinzani umepiteza mwelekeo kwa sababu unapingana na kile ulichokihubiri nchini.

Agenda ya kupinga ufisadi siyo ya upinzani tena bali ya JPM na CCM yake au yao. Wapinzani wamegeuka kuwa watu wanaokataa yale waliyoyasimamia na kuyahubiri huko nyuma. Hakika huo siyo uungwana bali aina mpya ya ufisadi nchini na usaliti kwa agenda zao.

Kama kweli sisi tumeokuwa wapinzani na tulioonesha kupinga kwa nguvu zote ufisadi ulioiumiza nchi hii tulimaanisha yale tuliyoyahubiri na kuwaaminisha watu basi tunao wajibu wa kuacha tabia ya kuwa vigeugeu kwa mambo tuliyoyaamini na kuyahubiri. Kutofanya hivyo basi ni mwendelezo wa ufisadi kwa maslahi binafsi.

Ni nani asiyeona kwamba serikali ya awamu ya tano inafanyia kazi mambo mengi tuliyoyapigia kelele? Au tunajifanya kutokukubali ukweli unaoishi kwa ule msingi wa upinzani wa Tanzania kwamba Tukimuunga mkono Mtawala kamwe hatutapata kuaminiwa na wapiga kura nchini na hivyo tupinge tu hata kama ni ukweli? Nadhani kinachofanyika ni mwendelezo wa kupinga hata mazuri ili kutafuta fursa ya wapinzani kukubalika kisiasa zaidi hata kwa njia na mbinu haramu kama kawaida ya siasa zilizo zoeleka hapa nchini kwa miaka mingi.

Taifa hili haliwezi kuendelea kwa kuwa na siasa za kutokukubaliana na ukweli unaoishi. Kama dhamira ya kila mtanzania ikiwemo wapinzani ni kuona nchi ina move basi hatuhitaji kuwa watu wa kupingapinga hata yaliyo mema bali kuyaunga mkono yale yaliyo mema bila kujali yanafanywa na nani bali msingi mzuri unapaswa kuwa ukweli kwa kila jambo.

Serikali ya awamu ya tano imeonesha njia ktk mambo mengi na inastahili kuungwa mkono. Safari ni hatua na ninaamini kwamba hata yale yanayoonekana kutokufanyiwa kazi ndani ya mwaka mmoja uliopita na ambayo yalishindikana huko nyuma, bado yanaweza kuja kufanyiwa kazi huko mbeleni. Serikali ya JPM imejitahidi sana tukilinganisha na huko tuliko toka. Uongozi huu unafanana sana na ule wa akina Hayati EDAWARD MORINGE SOKOINE chini ya hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Daima ninaamini ktk yale ninayoyaamini pasipo kufungwa na ukada bali kuangalia ukweli ni upi. Hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma bali tukubali kwamba wapiga dili waliozoea kupiga dili na kuziingiza fedha walizopiga ktk mzunguko kwamba siyo jambo la msingi ktk kujenga uchumi imara.

Uchumi imara hauwezi kujengwa kwa kuruhusu ubadhirifu wa fedha na mali za umma au hata za mtu mmoja mmoja. Kinachoonekana hivi sasa ni kama nchi inasukwa upya na hivyo tuwaunge mkono viongozi wa serikali ya awamu ya tano kwa mema wanayoyafanya na kuwashauri kurekebisha ktk yale ambayo hayajakaa vizuri. Tuachane na siasa nyepesi za kutaka kuona kwamba mazuri ni yale yanayofanywa na wapinzani huku mambo hayohayo yakifanywa na CCM yaonekane hayafai na kutajwa kuwa ni ya hovyo. CCM ya JPM siyo ile ya 2015 kurudi nyuma kidogo. Hii ni tofauti na ninaiunga mkono.

Hivyo basi leo Tarehe 21/11/2016 ninatangaza rasmi kwamba ninajiunga na timu JPM kwa maslahi ya taifa kwa kuwa sioni sababu ya kupingana na yale niliyoyapigania na itakuwa ni sawa na mtu kupigana na kivuli chake mwenyewe. Kwaherini Upinzani nimeamua kuanza siasa mpya za masuala yale niliyoyaamini na ninayoyaamini. Imani ni Matendo Na Matendo ni imani. Piga vita ufisadi kwa imani na Matendo.

Moses Joseph Machali
X-mbunge, Kasulu Mjini 2010-2015,

Rais Magufuli akutana na kiongozi wa Jeshi la Ukombozi la China

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Novemba, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao wamezungumzia uhusiano na ushirikiano wa muda mrefu uliopo kati ya Tanzania na China katika nyanja mbalimbali ikiwemo katika masuala ya ulinzi ambapo Jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) limekuwa na ushirikiano na Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA)
 
Rais Magufuli amemueleza Jenerali Fan Changlong kuwa Tanzania inathamini ushirikiano huo ambao umechangia kufanikisha juhudi za kuimarisha JWTZ zinazolenga kuwa na Jeshi la Kisasa na vifaa bora.
 
Dkt. Magufuli amemuomba Jenerali Fan Changlong afikishe salamu na shukrani zake kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping na kumhakikishia kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na China katika kuimarisha majeshi ya ulinzi na pia katika masuala mengine ya maendeleo ya kijamii.
 
“Nimefurahishwa na ziara yako hapa nchini kwetu, ujio wako unazidi kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zetu ulioasisiwa na waasisi wa mataifa haya Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania na Hayati Mwenyekiti Mao Tse-tung wa China.
 
“Naomba unipelekee salamu zangu kwa Rais Xi Jinping na umwambie kuwa pamoja na kuendeleza uhusiano na ushirikiano wetu katika kuimarisha majeshi pia tunatarajia kuona China inakuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi zetu za maendeleo kwa kujenga viwanda na kushiriki katika miradi mingine ukiwemo ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani Standard Gauge” amesema Rais Magufuli.
 
Kwa upande wake Jenerali Fan Changlong amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi imara aliouonesha katika Awamu ya Tano na amemhakikishia kuwa China itaendeleza na kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika masuala ya usalama hasa kuimarisha JWTZ.
 
Jenerali Fan Changlong amesema Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa China na Jeshi la Wananchi Tanzania yana uhusiano wenye manufaa makubwa na kwamba hivi sasa yanafanya uboreshaji utakaoyaimarisha zaidi na kuwa majeshi ya kisasa.
 
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt. Hussein Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange na Makamanda wa Majeshi wa Tanzania na China.
1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na kumkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
2 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimtambulisha Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kwa mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
4..Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.
6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na mgeni wake wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong wakati wakelekea kwenye ukumbi wa mikutano Ikulu jijini Dar es Salaam. 
7.
7..Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na ujumbe wake akiongoza mazungumzo rasmi na Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
8
10.
12Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi la Watu wa China(PLA) pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
13
14Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na mgeni wake Makamu Mwenyekiti wa Kamisheni kuu ya Ulinzi ya Jeshi la Ukombozi la Watu wa China (PLA) Jenerali Fan Changlong Ikulu jijini Dar es Salaam.
15Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange Ikulu jijini Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Maafisa wa ngazi za juu katika Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
21 Novemba, 2016

Waziri Mkuu Atoa Miezi Miwili Kwa Wakuu wa Hifadhi Kuweka Beacons Kuzuia Migogoro ya Mipaka..........Aagiza TAMISEMI isimamishe usajili wa vijiji kuanzia sasa

$
0
0
*Ni kwa ajili ya kuzuia migogoro ya mipaka na wanavijiji

*Aagiza TAMISEMI isimamishe usajili wa vijiji kuanzia leo

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa miezi na siku tisa kwa Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu kuhakikisha wanaweka mawe ya alama (beacons) kwenye mipaka yao ili kuepusha migogoro na wanavijiji wanaowazunguka.

Ametoa agizo hilo jana jioni (Jumatatu, Novemba 21, 2016) wakati akizungumza na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii na Wakuu wa Mapori ya Hifadhi za Misitu nchini katika kikao alichokiitisha kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma.

“Tatizo la migogoro baina ya wafugaji, wakulima na kamati za ulinzi na usalama za mikoa na wilaya ni lazima lifanyiwe kazi. Mkitoka hapa rudini katika maeneo yenu mkawaambie wananchi mipaka yenu iko wapi. Ninyi mnatambua mipaka yenu iko wapi kwa hiyo waelewesheni wananchi kwa kuweka alama,” alisema.

“Wakati Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli akizindua bunge tarehe 20 Novemba, 2015 aliwapa maeneo makuu matatu ambayo ni kuanisha mipaka, kupambana na ujangili na kukusanya mapato. Alizungumzia suala la mipaka kwa sababu iliyopo haieleweki, mkiulizwa mnajibu kuna buffer zone. Hivi mwananchi wa kawaida anajua buffer zone ni nini?,” alihoji.

“Sasa ninawapa muda hadi Januari 31, 2017 kazi ya kuweka beacons kwenye hifadhi zote za misitu iwe imekamilika. Kila pori nenda mkatengeneze alama zenu kama TANROADS walivyofanya. Kaeni mpige hesabu ni kiasi gani cha saruji na kokoto kinahitajika. Tutarudi hapa Dodoma kupeana taarifa ya utekelezaji. Katibu Mkuu niletee taarifa ya kila mkoa na wilaya kuna mapori mangapi tutakutana hapahapa kupeana mrejesho,” alisisitiza.

Alisema kama TANROADS waliweza kuweka alama za barabarani kwa nchi nzima ni kwa nini Wizara ya Maliasili na Utalii imeshindwa kuchukua hatua kama hizo. “Ni lazima tuweke hizo alama kila katika pori lake, tusipofanya hivyo, migogoro hii itaendelea,” alisema.

“Nendeni mkaweke alama za mipaka mkishamaliza sasa muwaeleze wananchi ni umbali wanapaswa waache kutoka kwenye hizo alama zenu na muwaelimishe kwamba hiyo ndiyo buffer zone. Suala la beacons ni serious na ninatarajia nikute hizo beacons kwenye maeneo yenu”

“Kila mmoja anayo fursa ya kuitisha mkutano na wananchi na kuwaelimisha kuhusu umuhimu wa kuwa na mapori ya akiba. Pandeni kwenye majukwaa, muelezee mipaka hiyo mipya na wananchi watawaelewa kwa sababu mwenye dhamana ya kwanza katika kutoa elimu hii ni wewe Mkuu wa Pori,” alisistiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amesema kuanzia leo Ofisi ya Rais TAMISEMI haina budi kusitisha usajili wa vijiji hadi zoezi la kuweka alama kwenye mipaka mapori ya hifadhi za misitu litakapokalimika.

“Kuanzia leo ninasimamisha zoezi la usajili wa vijiji unaofanywa na TAMISEMI hadi wizara ya Maliasili na Utalii ikamilikshe zoezi la kuainisha na kuweka alama kwenye mipaka mapori ya hifadhi za misitu. Tusipofanya hivyo tutaendelea kuwa na Taifa la walalamikaji,” alisema huku akishangiliwa na watendaji hao.

“Wakuu wa mapori tambueni ni vijiji vingapi ambavyo Serikali ilifanya makosa na kuvisajili wakati viko ndani ya hifadhi na vijiji vingapi bado havijasajiliwa. Pia onyesheni ni vijiji vingapi ambavyo ni hatarishi,” alisema.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amemtaka Mkurugenzi wa Idara ya Utalii katika wizara hiyo, Bw. Zahoro Kimwaga pamoja na Bodi ya Utalii nchini wabadilike na kuanza kufanya kazi kibiashara zaidi.

“Mkurugenzi wa Utalii na Bodi yako ya Utalii bado hamjajitangaza vya kutosha. Promosheni ya utalii hapa nchini bado haitoshi na mgeweza kuoata mapato makubwa zaidi kwa kujitangaza. Mabango ya barabarani yamejaa matangazo ya Vodacom na Airtel badala ya kuwa na picha za wanyama ili kila mtu akiona atamani kwenda mbugani,” alisema.

“Tumieni mabango ya kieletroniki (electronic screens) kurusha picha za wanyama. Mfano pale nje ya uwanja wa Taifa, au uwanja wa ndege hata kwenye njia kuu  za mikoani wekeni mabango ya iana hiyo. Ombeni vipindi kwenye televisheni nyingine, kile cha TBC1 peke yake hakitoshi,” alisisitiza.

HAKIELIMU Yabariki Mabadiliko Katika Mafunzo Ya Ualimu Nchini

$
0
0
Kutokana na mabadiliko ya mafunzo ya  ualimu yaliyo fanywa na Wizara ya Elimu ,Sayansi, Tektinolojia na ufundi  novemba mwaka huu  kuondoa  mamlaka ya usimamizi wa ngazi ya cheti  na stashahada  kutoka  Baraza la taifa elimu ya ufundi     NACTE  na kuyarudisha wizara ya Elimu chini ya  uangalizi wa baraza la mitihani Tanzana  NECTA,   shirika lisilo la kiserikali  linalojishughulisha na Elimu nchini (HAKI ELIMU ) limeipongeza Serikali kwa hatua  hiyo kwani hapo awali kwa kushirikiana na wadau wengine wa  Elimu  lilikuwa limesha toa mapendekezo kama hayo lakini hayakufanyiwa kazi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam  jana, mkurugenzi mtendaji wa HAKI  ELIMU ,Bwana John Kalage alisema  mabadiliko hayo yatasaidia kuinua kiwango cha elimu nchini,ingawa mabadiliko ya awali yalikuwa na lengo jema la kukabiliana na upungufu  mkubwa  wa  waalimu wa kufundisha masomo ya Sayansi katika shule nyingi hapa nchini lakini yalikuwa na athari  ya kuzorotesha ubora wa Elimu.

Alisema ,utaratibu wa kuvifanya vyuo  vya elimu kujitegemea  katika kudahili wanafunzi, kutathimini na kutunza waalimu tarajali ulikuwa pia na athali ya kushusha  kiwango  mafunzo ya ualimu  kwakuwa kila taasisi iikuwa na uhuru wa kujiamulia viwango vya  ubora wa mafunzo  itakayo toa ,

Katika zama hizi za ushindani kulikuwa na hatari dhahili kuwa  kila taasisi ingeweza kudahili  na kufaulisha wanafunzi wake  hata wasio stahili  ili kuvutia wana chuo wengi zaidi  kwalengo la kujipatia ada ‘’alisema

Hatahivyo  shirika hilo limetoa baadhi ya mapendekezo na kuishauri Serikali  kuunda chombo  chenye mamlaka ya juu katika elimu (Education Reguratory Authority ) chini ya sheria  ya elimu ili  kusimamia na kulinda sera ,sheria ,kanunu na miongozo  ya elimu iliyo wekwa ili  kupunguza  maamuzi na mabadiliko ya mara kwa mara  katika secta ya Elimu

Kwa sasa ina onekana  waziri ana mamlaka makubwa  makubwa ya kutoa  maamuzi  hali inayo onekana kuwepo kwa nyaraka nyingi  zinazo badilika kia mara hata kabla hazija fanyiwa kazi kikamilifu”

Kalage alisema  nivema  mafunzo ya  ualimu ngazi zote yakaendelea kutolewa na  vyuo vikuu na vyuo vya ualimu peke yake na vyuo vingine visivyo vya ualimu visiruhusiwe kutoa mafunzo hayo kwa kuwa lengo lao sikutoa mafunzo hayo .

"Nibora kuwa na vyuo vichachache ambavyo serikali ina uhakika na uandaaji wake  ili vyuo hivi vilishe shule zote  za umma na bnafsi ,hii itasaidia kuboresha kiwango cha elimu nchini."alisema

Wakili wa Serikali Amuomba Radhi Hakimu kwa Kushindwa Kumkamata Tundu Lissu

$
0
0

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita amemuomba radhi Hakimu Mkazi Mkuu wa Kisutu kwa kushindwa kutekeleza amri ya kumkamata mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio.

Wakili Mwita alifanya hivyo jana baada ya hakimu huyo, Thomas Simba kumuhoji sababu za kushindwa kutekeleza amri hiyo wakati hati ya kumkamata ilitolewa Novemba 3, 2016 na wakili huyo kuisaini.“Kwa nini hamkumkamata” Si mlikuwa na wajibu wa kumkamata? Mnamuogopa?” alihoji hakimu huyo.

Hata hivyo, pamoja na kuomba radhi hiyo mahakama imechukua hati ya kusafiria ya Lissu ili kudhibiti safari zake nje ya nchi kwa kuwa amekuwa akisafiri bila kuitaarifu mahakama.

Katika kesi hiyo, Lissu na watu wengine watatu wameshtakiwa kwa makosa matano ya uchocheza kutokana na habari iliyochapishwa na gazeti la Mawio kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar.

Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 28, 2016 na washtakiwa wote wapo nje kwa dhamana.

Kabla ya uamuzi huo, Wakili Mwita alisema jana ilikuwa siku ya kesi hiyo kutajwa na kwamba upelelezi unakaribia kukamilika.

Kuhusu madai ya kudharau mahakama Wakili Peter Kibatala anayemwakilisha Lissu aliiambia mahakama kuwa mteja wake yupo mahakamani, hivyo ametii amri ya mahakama na kwamba jukumu la dhamana ni kuhakikisha mshtakiwa anakuwapo mahakamani wakati wa kesi yake na kwamba uwepo wake ni kutii masharti ya dhamana.

Hata hivyo, Wakili Mwita alidai kuwa kitendo cha Lissu kutofika mahakamani mara mbili mfululizo ni kama kuonyesha dharau kwa mahakama hiyo.

Mwita alidai kuwa Lissu ni mwanataaluma wa sheria na anafahamu taratibu za kufuatwa kama hafiki mahakamani na kwamba mdhamini si mbadala wa mshtakiwa mahakamani.

“Alipaswa kuandika barua kuitaarifu mahakama hii kama wakili kuwa ana kesi ya uchaguzi anayoiendesha Bunda na kuambatanisha na samansi ama orodha ya kesi. Tunaomba mahakama iheshimiwe na jukumu la kumfutia dhamana ama kutokumfutia dhamana Lissu bado lipo mikononi mwako mheshimiwa,” alieleza wakili huyo wa Serikali.

Akizungumzia hoja hizo, Hakimu Simba alisema Lissu ni wakili maarufu, msomi na anajua taratibu zote za mahakama, lakini wadhamini wake wanababaika, hivyo alimtaka aeleze sababu za kwenda Ujerumani bila kutoa taarifa mahakamani.

Lissu alijibu kuwa hakuwa na nia ya kuidharau mahakama, wala kuikimbia kesi inayomkabili bali alikwenda Ujerumani katika mazingira ya dharura.

Hakimu Simba alimwambia mahakama inafahamu kesi za uchaguzi na maelekezo yake, hivyo ikamuuliza sababu za kutotoa taarifa wakati alipokwenda kushughulikia kesi ya Bunda 

“Nilipopata taarifa ya kwenda kuiendesha kesi hiyo ilikuwa ni siku moja baada ya kutoka nchini Ujerumani na kwamba niliandika barua ya kuitaarifu mahakama na nilituma iletwe mahakamani kupitia wasaidizi wangu,”alisema Lissu.

Lakini Hakimu Simba alisema: “Hakuna barua iliyotufikia. Usituingize katika migogoro kutokana na nafasi yako katika jamii ya mwanasheria. Hatukuogopi labda upande wa mashtaka ndio wamekuogopa.

“Tunataka kufuata mfumo, hatutakuogopa na wala hatutakuonea. Hapa naona upande wa mashtaka wanapiga blaa blaa, tuelewane tunaichukua hati yako ya kusafiria ili ukitaka kusafiri tujue.”

Majambazi Dar waendelea kuangukia mikononi mwa polisi huku pombe feki na mitambo yake pia vikikamatwa.

$
0
0
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam imeendesha operesheni katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo na kuwakamata watuhumiwa 67 wakiwemo watano waliokutwa wakiuza na kusambaza pombe bandia aina ya konyagi na vifaa vya kutengeneza kinywaji hicho.

Akizunguma jana jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Kamishna wa Polisi, Simon Sirro alisema watuhumiwa hao pia walikamatwa wakiwa na chupa tupu za konyagi 175, chupa zenye kinywaji cha konyagi 17 na vifungashio vya viroba vya konyagi 111.

Aidha, alisema watuhumiwa hao walikamatwa wakiwa na vifuniko vya chupa za konyagi 200, lebo na stika za konyagi, katoni 111 za viroba vya konyagi, vimiminika vya pombe aina ya spiriti lita 20, ndoo kubwa aina ya jaba moja na koki 10, viroba original pakiti 14,916 na Victorious pakiti 1,080.

Aliwataja watuhumiwa waliokamatwa na bidhaa hizo bandia kuwa ni Ladness Kagaruki (26), mkazi wa Sinza madukani, Aloyce Emmanuel (53), mkazi wa Salasala, Leonard Arobogasti (49), mkazi wa Makongo, Godfrey Gabriel (29) na Eveline Sandole (58) wakazi wa Mwenge.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili, huku akieleza kuwa kwa suala la shisha, tayari watuhumiwa watatu wanashikiliwa na upelelezi wao utakapokamilika watafikishwa mahakamani.

Katika tukio lingine, wanamshikilia Kulwa Rajabu anayetuhumiwa kwa ujambazi akiwa na silaha aina ya Browning yenye namba A731441 yenye risasi 12 ndani ya magazine.

Alisema mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba 16, mwaka huu saa 10.00 jioni Mbande Mbagala baada ya kuwekewa mtego. Alisema silaha hiyo iliibiwa Novemba 13, saa 9.30 usiku maeneo ya Tuangoma katika tukio la uvunjaji na kuibwa kwa vifaa mbalimbali ambavyo vyote vilipatikana.

Aidha, alisema baada ya mahojiano ya kina mtuhumiwa huyo alitaja silaha nyingine ambayo ni bastola aina ya Revolver iliyofutwa namba ikiwa na risasi mbili ikiwa imefichwa maeneo ya msitu wa Dona huko Yombo.

Pia wamemkamata mtuhumiwa anayetambulika kwa jina moja la Shomari aliyekuwa akituhumiwa kwa mauaji yaliyofanyika kwenye daladala Oktoba 28, mwaka huu Tandika Tambuka.

Kwa mujibu wa Sirro, baada ya Polisi kupata taarifa na kumfuatilia, mtuhumiwa huyo alianza kukimbia na ndipo askari walifyatua risasi juu ili asimame, lakini hakutii amri na askari walimpiga risasi mbili mguuni na kudondoka chini kisha kumkamata pamoja na bastola yake aina ya Revolver ikiwa na risasi mbili ndani ya magazine.

Waliohamishiwa UDOM kutoka St Joseph kurudia mwaka

$
0
0
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknlojia Imewataka wanafunzi wa St. Joseph walioamishiwa katika chuo kikuu cha Dodoma kurudia mwaka kwa kile kilichobainika kuwa na ujuzi na maarifa usiokidhi viwango vya chuo cha Dodoma.

Wizara hiyo pia imesema kwamba watakaogomea uamuzi huo watatakiwa kurudi makwao .

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania TCU, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema, ni lazima wanafunzi hao warudie mwaka kwani wamepimwa na kubainika kuwa na uwezo mdogo hivyo hatua ya kuwataka kurudia mwaka ni nafasi ya pili kwao.

Prof. Ndalichako alisema, kwa sasa wizara yake inaandaa ripoti ya vyuo vinavyofundisha chini ya viwango ambapo amesema mara tu baada ya kukamilika ripoti hiyo, itatolewa na kwamba kwa wale wanafunzi ambao vyuo vyao vimefungwa kwa kutokidhi vigezo ni lazima wapimwe kiubora ili kupata wanafunzi watakao kidhi vigezo vya soko la ajira.

Aidha, Prof. Ndalichako ametoa onyo kwa wanafunzi ambao wamegushi nyaraka mbalimbali ikiwemo za vifo vya wazazi wao ama ugonjwa na kufanikiwa kupata mkopo wa elimu ya juu kwa njia ya udanganyifu kuwa wizara hiyo inafanya uhakiki na pindi watakapo bainika hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Makomba Asubiri Kibali cha Rais Kuwafuta Kazi wa Watumishi wa Umma Dar...

$
0
0
Serikali ya Mkoa wa Dar es Salaam imesema itawastaafisha kwa manufaa ya umma watumishi wa mkoa huo walioshindwa kutekeleza majukumu yao kikamilifu.

Hayo yalisemwa jana jijini humo na Mkuu wa Mkoa huo, Paul Makonda wakati akizungumza na watumishi wa Manispaa ya Temeke akiwa katika ziara ya siku mbili wilayani humo. Alisema watumishi wengi wamekuwa mizigo na wanasubiri kuchukua mishahara bila kuifanyia kazi hivyo ni bora kuwasimamisha kwa manufaa ya umma.

“Nafikiri kuna haja ya kuwapunguza watumishi serikalini hakuna wanachofanya zaidi ya majungu na umbea, asilimia 20 ndio wanaofanya kazi, tayari nimeongea na Rais na kuna taratibu nakamilisha na tutachukua hatua,” alisema Makonda.

Aidha Makonda alisema watumishi wengi wa umma wanaishia kula fedha za miradi na matokeo yake wanatengeneza miradi mibovu ambayo imekuwa ikichukuwa muda mfupi kuharibika.

Makonda aliwashangaa watumishi wanaoshindwa kufanya kazi na kudai hawana bajeti wakati wana uwezo wa kuzungumza na wadau na kupata fedha nyingi na kuendesha miradi.

“Tumechoka kusikia kelele za kukosa bajeti, yapo mambo hayahitaji bajeti lakini hamfanyi tangu kuteuliwa kwangu nimeweza kufanya miradi ya zaidi ya Sh bilioni 30 ambayo sio ya bajeti, lakini nyinyi mnapiga kelele za bajeti, tukiona hamuwezi kubadilika tutawastafisha tunataka watu wanaofikiria nje ya boksi,” alisema Makonda.

Godbless Lema Kujaribu Tena Bahati yake Leo Mahakamani baada ya Kusota Mahabusu kwa Siku 19

$
0
0
Jaribio jingine la maombi ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema linafanyika leo baada ya kusota mahabusu tangu akamatwe mkoani Dodoma Novemba 3. 

Lema anayekabiliwa na tuhuma ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli, ombi hilo la dhamana linakuwa la tatu baada ya kukwama mara mbili tangu alipoingizwa mahabusu. 

Lema ambaye anatetewa na mawakili sita; Peter Kibatala, John Mallya, Charles Adiel, Adam Jabir, Faraja Mangula na Sheck Mfinanga, dhamana yake licha ya kutolewa na Hakimu Mkazi, Desdery Kamugisha ilipingwa kutokana na notisi ya rufani iliyowasilishwa na mawakili wa Serikali.

Baada ya notisi hiyo, Lema aliandika barua Mahakama Kuu kuomba mapitio ya kesi hiyo kwa maelezo kuwa taratibu za kisheria zilikiukwa kutokana na hakimu kutoa dhamana lakini akashindwa kukamilisha masharti ya dhamana na kupokea hoja za Jamhuri.

Hata hivyo, wakili mwandamizi wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi jingine kupinga Mahakama Kuu kufanya marejeo ya kesi hiyo.

Kadushi aliwasilisha hoja mbili za kisheria juu ya kuweka pingamizi la ombi la mbunge huyo kuwa muombaji hakukidhi vigezo vya kuiomba mahakama irejee  maamuzi ya mahakama kwa kuwa badala ya kuiandikia mahakama barua ya kuomba ifanye mapitio ya maamuzi hayo, angetakiwa akate rufaa juu ya maamuzi ya mahakama.

Pia, alisema maombi hayo yamekinzana na Sheria ya Mahakama za Hakimu kifungu (43) (2) kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa kupokea ombi ama kukata rufaa kwa maamuzi hayo, kwa kuwa ni madogo.

Hata hivyo, mawakili wa Lema walipinga hoja hizo na kueleza sheria zinaruhusu mlalamikaji kuandika barua kuomba mapitio, na tayari suala hilo limewahi kufanyika hata kwa ofisi na mwanasheria mkuu kuomba mapitio.

Wakili Kibatala alisema Mahakama Kuu ina mamlaka ya kisheria yenyewe kufanya mapitio ya kesi hata kama hakuna aliyelalamika na tayari imewahi kufanya mapitio kwa kesi kadhaa.

Baada ya hoja za pande zote kutolewa Jaji Sekela Moshi aliomba kupewa muda, kupitia hoja zote zilizoletwa na pande zote ili kuzifanyia maamuzi leo.

Baba Wa Kambo Atiwa Mbaroni kwa Kumnajisi Hadi Kufa Mtoto wa Miaka Mitatu

$
0
0

Mtoto  mdogo mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa Kijiji cha Nyamihaga Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma amekufa baada ya kunajisiwa na baba yake wa kambo.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kwamba wamemtia mbaroni mtuhumiwa Hamimu Saidi (27) mkazi wa kijiji hicho cha Nyamihaga.

Akitoa maelekezo kuhusu mkasa huo, Kamanda Mtui alisema mtuhumiwa alitekeleza dhamira yake hiyo wakati mama wa mtoto huyo ambaye alikuwa mke wa mtuhumiwa alipokwenda kisimani kuchota maji.

Alisema baada ya mwanamke huyo kurejea nyumbani kutoka kisimani alimshuhudia mtoto wake akilalamika sana wakati akitaka kujisaidia haja ndogo na ndipo alipomchunguza akagundua kwamba mtoto huyo alikuwa ameingiliwa na kujeruhiwa kwenye sehemu zake za siri.

Kamanda Mtui alisema baada ya kugundua hilo, mama huyo wa mtoto alimchukua mtoto huyo na kumpeleka Hospitali ya Mkoa ya Maweni kwa matibabu, ambako iligunduliwa kuwa mtoto huyo alikuwa amenajisiwa na alikuwa amebanwa shingo wakati akifanyiwa kitendo hicho hivyo alikosa pumzi wakati akifanyiwa unyama huo.

Kamanda huyo alisema hata hivyo mtoto huyo alifariki katika Hospitali ya Mkoa ya Maweni alipokuwa akitibiwa na kwamba baada ya uchunguzi wa kidaktari na uchunguzi wa Polisi, mwili wa mtoto huyo ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya maziko.

“Kwa sasa mtuhumiwa Hamimu Saidi anashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Kigoma wakati upelelezi ukiendelea ili taratibu za kumfikisha mahakamani zifanyike na kwamba anatarajia kufikishwa mahakamani wakati wowote upelelezi huo utakapokamilika,” alieleza Kamanda Mtui.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 22

Godbless Lema Anyimwa Dhamana Kwa Mara Nyingine Tena

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema amekwaa kisiki kwa mara nyingine katika harakati za kuomba dhamana baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kutupilia mbali ombi la marejeo ya kesi yake na kushauri kuwa Mawakili wake wakate rufaa ya kupinga zuio la dhamana

Mawakili wa Lema leo walikuwa wakirusha karata hiyo kwa mara ya tatu baada ya mara mbili za awali mteja wao kushindwa kupata dhamana.

Lema amesota rumande tangu alipokamatwa Novemba 3, 2016 akiwa mkoani Dodoma na kusafirishwa hadi Arusha ambapo anashtakiwa kwa kosa la uchochezi dhidi ya Rais Dkt Magufuli.

Rais Magufuli Amuapisha Katibu Tawala Wa Mkoa Wa Kagera (Ras) Kamishna Diwani Athumani Leo Ikulu Dar Es Salaam

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Kamishna Diwani Athumani kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Kamishna Diwani Athumani mara baada ya kumuapisha kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAS) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
 Katibu wa Maadili ya Viongozi – Siasa,  Bw. Waziri Kipacha akimuongoza  Kamishna Diwani Athumani kula  kiapo cha uadilifu cha viongozi wa umma   baada ya kuapishwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika picha ya pamoja na  Kamishna Diwani Athumani pamoja na viongozi waandamizi wa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama umma   baada ya Kamishna Diwani kuapishwa  kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera (RAs) Ikulu jijini Dar es salaam leo Novemba 22, 2016.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 43 & 44

$
0
0
 Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  
Kwanza kijana huyo akamkumbatia raisi Praygod Makuya, nakumfanya raisi Praygod Makuya kujitahidi kuvuta kumbukumbu zake niwapi alipo muona kijana huyu anaye mwagikwa na machozi. Kumbukumbu za raisi Praygod Makuya zikagota kwenye ndege na kukumbuka kijana huyu ndio yule aliye kuwa akishirikiana na Rahab.
“We…weee si…”  
Raisi Praygod alizungumza kwa kigugumizi, kwani kama kijana huyu alimkosa kwenye ndege basi leo amekuja kumuua kwenye alaiki ya watanzania.
“Samson, Samson muheshimiwa.”
Samson alizungumza huku machozi ya uchungu yakimwagika, akazidi kumkumbatia Raisi Praygod Makuya kwa nguvu zake zote.
                                                                                        
ENDELEA
Raisi Praygod Makuya akajaribu kujitoa mikoni mwa Samson ila akajikuta akishindwa kwani Samson alizidi kumkumbata kwa nguvu
“Naoamba unisamehe muheshimiwaa”
Samson alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi. Makamu wa rais baada ya kumuona Samson, ikanyanyuka kwenye kiti chake huku macho yakiwa yamemtoka. Woga wa siri yake kuweza kufichuliwa na mjomba wake huyo ukaanza kumtawala.

“Muheshimiwa natambua kwamba nilikukosea, ila si kosa langu mimi”
“Nilitumwa niweze kukuangamiza, na mjomba wangu ili kiti chako cha uraisi kiweze kukaliwa na mjomba wangu ambaye ni makamu wa raisi wa sasa”
Maneno ya Samson yakamfanya raisi Praygod kuweza kumtazama makumu wa raisi aliye  keti kwenye jukwaa. Sura ya makamu huyo ikamuashiria raisi Praygod kwamba ina hasira dhidi yake.

“Nimekuelewa kijana, unaitwa nani?”
“Samson”
“Sawa Samson nitalifanyia kazi”
“Kabla ya hayo kuna jengine muheshimiwa nahitaji kukuambia”
Makamu wa raisi alipo zidi kumuona Samson anazungumza na Raisi Praygod, akazidi kushikwa na hasira akiamini kwamba kila kitu kimesha haribika, akaangaza macho yake huku na huku, akamuona mlinzi wake aliye simama pembeni, bastola ikiwa imechomekwa kiunoni. Kwa haraka makamu wa Raisi akaichomoa bastola hiyo bila hata yakufikiria mara mbili, akafyatua risasi ambazo kwa haraka Samson aliweza kuliona tukio hilo, alicho kifanya ni kumsukumia pembeni Raisi Praygod, na risasi hizo mbili zikaingia mwilini mwake na kumuangusha chini.

Mlio wa bastola hiyo, ukazua hali ya taharuki kwa kila aliye kuwa katika uwanja wa taifa, kila mmoja akafanya jinsi akili yake ilivyo muagiza kuweza kufanya, wapo walio weza kuchanganya miguu yao na kukimbia hovyo hovyo, wengine waliweza kupoteza fahamu, wengine waliweza kukanyagwa vibaya pale walipo zidiwa nguvu na wale walio hitaji kuokoa nafsi zao. Askari na walinzi wa viongozi waalikwa wakawa na kazi moja tu, yakuwaokoa viaongozi wao waliomo ndani ya kiwana hichi kikubwa cha mpira. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani hapakuwa na aliye weza kuvumilia. Walinzi wengi wakamzunguka Raisi Praygod, wakamtoa uwanjani huku wakiwa wanamkimbiza, baadhi ya wanajeshi wakaweza kumtia nguvuni makamu wa raisi aliye weza kufanya tukio lakinyama.

Hali ya Samson, ikazidi kuwa mbaya huku macho yake akimtizama jinsi Raisi Praygod anavyokimbizwa na askari kuyaokoa maisha yake, Samson akaachia tabasamu pana, huku taratibu macho yake yakiingiwa na ukungu ulio pelekea kuyafumba macho yake na kutulia tuli.
                                                                                         ***
     Moja kwa moja Agnes akakimbilai kwenye chumba amacho aliamini kiongozi anaye muhitaji ni lazima atakuwa amepelekwa huko baada ya milipuko hiyo ya magari kuweza kutokea. Akafanikiwa kufika kwenye kordo yakuelekea kwenye chumba hicho kilichopo chini ya ardhi. Walinzi walio valia suti nyeusi pamoja na miwani nyeusi wapatao kumi na tano, wakawa wamesimama nje ya mlango huo huku macho yao yote wakimtupia Agnes anayekuja kwa kasi huku akiwa amejiamini sana.

Kila mmoja akabaki kuwa na alama ya kujiuliza kwani mavazi aliyo yavaa Anges ni ngumu sana kumtilia mashaka kwani akafanana sana na wahudumu wa kikosi cha kuzima moto. Muonekano wa umbo dogo dogo la Agnes, likawapa imani kwamba binti huyo anaye kuja kasi huku akiwa amenyanyau mikono yake juu, hana madhara yoyote kwao.

“Naomba muwatoe viongozi nje, jengo limeanza shika moto”
Kauli ya Agnes aliyo izungumza kwa lugha ya kirasia, ikawafanya walinzi wote kuchanganyikiwa, ikawalazimu kuwasiliana na wezao waliomo ndani ya chumba kuweza kuwatoa viongozi hao haraka iwezekanavyo. Bwana Paul Henry Jr pamoja na Raisi wa Russia wakatolewa ndani ya chumba hicho kuku wakiwa wamezungukwa na walinzi wao wapatao ishirini.

“GO GO GO….!!!”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akionekana ndio mkuu wa kikosi hichi maalumu chakuwalinda viongozi hawa. Agnes akatazama jinsi walinzi hawa walivyo makini na kuwalinda viongozi hawa.
“Hapa hapa”
Agnes akawaacha viongozi hao kupiga  hatua nyingi mbele, kisha  kwa kasi akanza kukimbia na kuwafwata kwa nyuma, akamfikia mmoja aliye ishika bastola yake na kuitanguliza mbele. Kwa kasi ya ajabu Agnes akajigeuza kwenye shingo ya mlinzi huyo na kuivunja, kabla hajaanguka chini, tayari akawa ameikamata bastola ya mlinzi huyo.

Kwa mafunzo ya uharaka na umahiri wake katika kutumia silaha hizi za bunduki, Agnes, akaanza kuwaangusha chini walinzi hao, walio changanyikiwa kwani, kitendo cha mtu kujaribu kufanya shambuliza tayari umesha vamiwa na kuangushwa chini.
Agnes akafanikiwa kusimama nyuma kwa bwana Paul Henry Jr, akampiga kabali huku bastola yake akiwa ameiweka sikioni mwa kiongozi huyo. Macho yake kwa haraka aliweza kuona miili ya walinzi wapatao kumi na sita wakiwa chini wamekufa huku wanne wakiwa wamesimama huku wamenyooshea bastola zao.


Ndalichako Awalaumu Wazazi Kuwa chanzo cha kushuka kwa maadili miongoni mwa wanafunzi

$
0
0
Serikali  imewalaumu wazazi kuwa ni chanzo cha kushuka kwa maadili miongoni mwa wanafunzi, kwa kuwa kama walezi, hawana ushirikiano mzuri na walimu.

Kutokana na hali hiyo, imesema walimu wameacha  kurekebisha maadili ya wanafunzi kwani hawaungwi mkono, hivyo kuwaongezea kiburi wanafunzi.

Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa, Joyce Ndalichako kwenye ufunguzi wa mdahalo kuhusu kujenga na kukuza maadili, haki za binadamu, uwajibikaji utawala bora na mapambano dhidi ya rushwa.

Mdahalo huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya maadili na haki za binadamu ambayo yatakafikiwa kilele Desemba 10 mwaka huu.

Kuhusu maadili aliwaomba wazazi na walimu kuweka misingi bora ya malezi kwa wanafunzi kuzingatia maadili.

“Wazazi watimize wajibu wao wa kuwalea watoto ipasavyo na wanafunzi mkubali kupokea na kuzingatia mafundisho ya maadili, kamwe msikubali kuja kufunzwa na ulimwengu,” alisema Profesa Ndalichako akiwaasa vijana walioko shuleni kuwa watambue hakuna mafanikio bila nidhamu na bidii.

Aidha, alisema serikali imebaini kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya walimu kuwa Bodi za Shule zimekuwa zikipelekewa wanafunzi wakorofi na kuwatetea bila kuchukua hatua na kuwaacha wakiendelea na masomo.

“Kitendo hiki huwapa kiburi zaidi wanafunzi hao na kuamua kuwafanyia vitendo viovu vinavyodhalilisha walimu wao,” alisema na kuwaagiza wakuu wa shule na Bodi zote kuhakikisha wakati wote wanachukua hatua stahiki dhidi ya utovu wa nidhamu unaofanywa na wanafunzi wao.

Mawakili Kesi ya Godbless Lema Wagonga Mwamba Mahakamani ......Arudishwa Tena mahabusu ya Gereza la Kisongo

$
0
0
Mbunge  wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameendelea kusota katika mahabusu ya Gereza la Kisongo mjini Arusha akiingiza siku ya 22 leo baada ya jana kukwama katika azma yake ya kutaka Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kufanya marejeo ya uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha uliomnyima dhamana.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Sekela Moshi ndiye aliyetupilia mbali ombi la Lema, hivyo kumfanya arejee mahabusu huku mawakili wake wakihaha kuhakikisha wanakata rufaa ili kuomba dhamana hiyo katika ngazi nyingine ya kisheria.

Aidha, Jaji Moshi ameridhia ombi la Lema kupitia kwa mawakili wake Sheck Mfinanga na Peter Kibatala la kukata rufaa mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe na hatimaye Lema kupata dhamana baada ya kupitiwa na jaji atakayepangiwa.

Akitoa uamuzi huo mahakamani hapo, Jaji Moshi alisema kimsingi hoja ya mawakili wa Lema ya kutaka mahakama hiyo kuitisha faili na kulipitia haina msingi wowote kisheria hivyo anaitupilia mbali hoja hiyo na kutoa rai kwa mawakili hao kukata rufaa Mahakama ya Rufaa ili dhamana ya Lema isikilizwe.

“Mahakama hii haiwezi kupitia faili la kesi hii ya Lema ya kupata dhamana hivyo siwezi kupitia faili hili, bali nashauri mkate rufaa ili iweze kusikilizwa,” alisema Jaji Moshi.

Awali Wakili wa Serikali, Paul Kadushi aliwasilisha pingamizi Mahakama Kuu la kuitaka wasisikilize maombi ya Lema ya kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 kwa madai yapo makosa ya kisheria yaliyofanywa awali na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa lengo la kumnyima dhamana mbunge huyo.

Akiwasilisha hoja zake mbele ya Jaji Moshi katika Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Kadushi akisaidiana na Materu Marandu alisema anawasilisha hoja mbili za pingamizi za mahakama hiyo kuendelea kusikiliza kesi hiyo.

Alisema kimsingi maombi hayo yaliwasilishwa mahakamani hapo kutaka mahakama hiyo iitishe faili la kesi namba 440/441 yanakinzana na kifungu cha 43 (2) cha sheria ya Mahakama ya Mahakimu. Katika kesi hiyo, Lema anashitakiwa kwa kutoa maneno ya kumtusi Rais katika maeneo tofauti.

Kadushi alisema uamuzi unaopinga kufanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ya kukubali kutompa dhamana Lema ni uamuzi mdogo na haukuwa na sababu za kukataa dhamana.

“Mahakama yako inafungwa mikono na kifungu hiki kufanya mapitio au uamuzi mdogo, hivyo tunaomba mahakama itupilie mbali maombi hayo,”alisema Kadushi ambaye wakati akiwasilisha hoja zake alikuwa akinukuu mashauri mbalimbali ya kesi zinazofanana na hiyo.

Aidha, Kadushi alisisitiza kuwa wao wanatambua haki ya kukata rufaa ipo wazi kwa mleta maombi ila itakuwa jambo geni kama mahakama itawapa nafasi kusikiliza maombi yao.

 Alisema hoja ya pili ya pingamizi lake, linatokana na mleta maombi kutokidhi matakwa ya kisheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.

Katika sheria ya makosa ya jinai, kifungu cha 359(1) ya mwaka 2002 kuwa mtu asiporidhika na maamuzi ya mahakama ya chini kama ilivyo katika kesi hiyo, kamwe hawezi kuwa na mbadala wa mapitio ya rufaa.

Akijibu hoja hizo Wakili anayemtetea Lema, Peter Kibatala akiwa na jopo la mawakili wenzake, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, John Mallya, Faraji Mangula na Charles Adiel, alipinga kuwekewa pingamizi hilo na kuomba mahakama isikilize maombi yao.

Alisema wao wamefungua maombi hayo kuiomba Mahakama Kuu kuitisha jalada la kesi ya mahakama ya chini ili kuona uhalali wa kutotekelezwa kwa uamuzi wa kutoa dhamana, kwani kilichokuwa kinasubiriwa ni masharti ya dhamana.

“Huyu mshitakiwa alipewa dhamana , ila kabla ya mahakama haijatoa masharti ya dhamana, upande wa serikali ukasimama kabla mahakama haijaweka masharti ya dhamana ambayo lazima ifanye hivyo, wakasema wameonesha nia ya kukata rufaa na mahakama ikakubaliana nao bila kutekeleza amri yao,” alisema Kibatala.

Aliomba mahakama hiyo itupilie mbali pingamizi la serikali na kuiomba kuendelea na kazi iliyokusudia kuifanya ya kupitia maombi yao ili kutoa dhamana kwa mshtakiwa au iamuru mahakama ya chini kuendelea na uamuzi wake.

Wakili wa mbunge huyo baada ya maombi yao kugonga mwamba, walikuwa kwenye hekaheka ya kukamilisha kuandika rufaa ili kumnasua Lema atoke mahabusu.

Baada ya kutoka nje ya Mahakama Kuu, Wakili Mfinanga alisema wanamalizia kukamilisha taratibu za wao kukata rufaa Mahakama Kuu na wataomba rufaa hiyo isikilizwe kwa hati ya dharura ili kumnasua Lema mahabusu.

Agizo la Rais Magufuli bandarini latekelezwa

$
0
0
Mradi wa kuweka mashine mpya za kisasa za kukagua mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam ambazo zina uwezo wa kusoma na kupeleka taarifa na picha za mizigo mubashara kwenye mifumo ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) na Mamlaka ya Mapato (TRA) umekamilika.

Kukamilika kwa mradi huo kunatokana na maagizo aliyoyatoa Rais John Magufuli kuwa TPA na TRA zishirikiane kuendesha mashine za kukagua mizigo zinazotoa taarifa na picha mubashara, pamoja na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha Serikali haipotezi mapato na kupitisha mizigo haramu.

Kuwepo kwa mashine hizo kutazisaidia TPA na TRA kubaini shehena zilizoko kwenye makasha yanayofikishwa bandarini hapo kupelekwa na kutoka nje ya nchi kama inawiana na nyaraka za mzigo huo; na hivyo kutozwa ushuru sahihi kwa mzigo stahiki. Lengo la kufunga mashine hizo ni kuongeza mapato kwa serikali.

Meneja wa Mradi huo, Zhang Sheng alisema jana kuwa mradi huo umekamilika na sasa wako katika hatua ya pili ya mafunzo na skana hiyo mpya inaweza kutumika muda wowote mara baada ya kukamilisha mafunzo.

Kwa mujibu wa Meneja huyo kutoka China, skana hiyo ina uwezo wa kusoma na kupeleka taarifa na picha za mizigo mubashara kwenye mifumo ya TPA na TRA kwa wakati mmoja bila kuchelewa. Kutokana na kukamilika kwa mradi huo, TRA na TPA zimeanza kuwapa mafunzo watumishi wao namna ya kutumia mashine hizo.

Jana Watumishi 20 wa mamlaka hizo kutoka Dar es Salaam na Tanga walihudhuria mafunzo yanayolenga kuwajengea uwezo ili wamudu kutumia skana hiyo inayotumia teknolojia ya kisasa.

“Nazipongeza Serikali za Tanzania na China kwa kuwezesha mradi huu kukamilika. Tunatarajia mafunzo hayo yatawaongeza uwezo wafanyakazi, ufanisi wa bandari pamoja na kuongeza mapato ya Serikali,” alisema Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Deusdedit Kakoko wakati akifungua mafunzo hayo ya siku tano.

Aliwaagiza washiriki kuhakikisha watakapokuwa wanafanya kazi katika mashine hizo wahakikishe wanafanya tathmini ya mizigo inayoonekana katika kontena kama ina taarifa sahihi kwa kulinganisha na nyaraka za kuagizia mizigo husika.

Pia aliwataka kuhakikisha nyara za Serikali, silaha haramu, dawa za kulevya, bidhaa za mionzi na nyingine zisizofaa hazipitishwi bandarini. Mkurugenzi huyo pia aliwataka watumishi hao kujifunza kufanya matengenezo ya mashine hizo angalau kwa asilimia 50 kuliko kutegemea wataalamu kutoka nje pekee.

Alisema TPA na TRA watahakikisha waendesha skana wanajifunza kufanya matengenezo kwa asilimia 100 ili kuondokana na gharama za kutumia wataalamu kutoka nje.

Wakati alipotembelea Bandari ya Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi wa bandari hiyo, Rais alitoa miezi miwili kwa TPA kununua mashine nne za kisasa za kukagulia mizigo bandarini.

Alitoa agizo hilo baada ya kubaini kuwa kati ya mashine nne za ukaguzi wa mizigo zilizopo, ni mashine mbili tu ndizo zinafanya kazi na hazina uwezo wa kukagua mizigo yote inayotoka na kuingia nchini kupitia bandari hiyo hali inayosababisha kutokuwepo kwa udhibiti wa uhakika wa udanganyifu.

Awali baadhi ya wafanyabiashara ambao sio waaminifu walikuwa wanatumia udhaifu wa mashine za bandarini hapo kusema uwongo kuhusu shehena inayokaguliwa bandarini hapo kwa lengo la kukwepa kulipa kodi stahiki.

Chadema Kukusanya Bilioni 13.9 Kwa Mwaka Kupitia Kadi Mpya za Wanachama Zitakazoanza Kutolewa Mwakani

$
0
0

Chadema imetangaza kuwa Januari itaanza kutumia kadi mpya za uanachama za kielektroniki, zitakazoiwezesha kukusanya Sh13.9 bilioni kwa mwaka na kupunguza utegemezi wa ruzuku ya Serikali.

Mkakati huo ulitangazwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika mkoani Morogoro. Tofauti na Mbowe, viongozi wengine wa chama hicho walioko mikaoni ni Edward Lowassa aliyeko Dodoma na Frederick Sumaye ambaye yupo Singida.

Mbowe alisema mfumo huo utasaidia pia kudhibiti baadhi ya viongozi wasio waaminifu, wanaotumia mwanya wa kuuza kadi na kushindwa kuwasilisha fedha kwenye hazina ya chama.

Alisema kwa mfumo huo mpya, kama Chadema itakuwa na wastani wa wanachama 100,000 katika wilaya moja na kila mmoja kulipa ada ya Sh1,000 kwa mwaka, maana yake itaingiza Sh100 milioni.

Kwa hoja hiyo ya Mbowe, ikiwa chama hicho kitakuwa na wastani wa wanachama 100,000 katika kila wilaya za Tanzania Bara ambazo ni 139, Chadema itakuwa na uwezo wa kukusanya Sh13.9  bilioni kila mwaka.

Vyama vya siasa vinapata ruzuku kwa mujibu wa sheria na ripoti ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ilibainisha kuwa jumla ya Sh67.7 bilioni zililipwa na Serikali kwa vyama vya siasa katika mwaka kipindi cha miaka minne, kuanzia mwaka wa fedha 2009/2010 mpaka 2012/2013. Fedha ambazo kwa mujibu wa CAG zilikuwa hazijakaguliwa kisheria.

Ikilinganishwa na mkakati mpya wa Chadema, fedha hizo ni ndogo katika kuhudumia shughuli za chama nchi nzima.

Mbowe alisema Chadema imeamua kuhakiki wanachama wake ili ifikapo Januari iwe tayari imemaliza kazi hiyo na kuingia rasmi katika mfumo mpya, utakaokisaidia kuondokana na dhana ya utegemezi wa ruzuku kutoka serikalini.

Alisema ili chama kipige hatua na kuondokana na utegemezi wa ruzuku serikalini, wamekusudia kuingia katika mfumo wa kupata mapato kutoka ndani ya wanachama kupitia ulipaji wa ada.

Mbowe alizungumza na wanachama hao kutoka ngazi za vitongoji, vijiji, kata na wilaya waliohudhuria mkutano mkuu maalumu wenye lengo la kuwakumbusha mambo mbalimbali ya kuimarisha chama hicho baada ya Serikali ya Rais Magufuli kuzuia mikutano ya hadhara.

“Katika kipindi cha miaka miwili ijayo, Chadema itakuwa tayari imefanya utambuzi wa wanachama wake kwa kuwatambua katika kila mtaa, kitongoji, kijiji, kata na jimbo kupitia mfumo mpya wa kadi za eleketroniki ifikapo Januari 2017,” alisema Mbowe.

Alisema katika baadhi ya maeneo ya mikoa hapa nchini, kadi za uanachama za Chadema ni lulu na zimekuwa zikiuzwa hadi Sh5,000 badala ya 500.

Alieleza kuwa mapato ya chama lazima yatokane na ada za wanachama na siyo ruzuku ya Serikali, kwa kuwa utegemezi wa ruzuku ni hatari kwa uhai wake.

“Hii ruzuku inayotolewa na Serikali inatolewa kwa sababu ya CCM na CCM bila ruzuku hakiwezi kujiendesha,” alidai.

Mbowe alisema kila jimbo linapata fedha za ruzuku kulingana na idadi ya kura ilizopata katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 mwaka jana, akitolea mfano Jimbo la Mlimba kuwa Mbunge Suzan Kiwanga alishinda kwa kura 40,000 wakati urais Chadema ilipata kura 38,000 huku katika udiwani wakipata kata tisa kati 16.

“Kutokana na ruzuku, Mlimba itapata Sh163,688 kila mwezi. Unaweza kuona fedha za ruzuku kutoka ndani ya chama ni ndogo sana ambapo Mkoa wa Morogoro unapokea kiasi cha Sh2.2 milioni kila mwezi.

“Kufikia mwaka 2017 kupitia programu ya Chadema msingi, tumekusudia kukijikita zaidi kusaka wanachama kutoka ngazi ya mitaa, vitongoji na balozi na tutaanza uchaguzi ndani ya chama.

“Tumebaini kuwa baadhi ya maeneo Chadema tumeshindwa kupata wenyeviti wa Serikali ya vitongoji na vijiji, kukosa madiwani na wabunge kutokana na kukosa misingi imara wa wanachama,” alisema Mbowe. 

Mwenyekiti aomba kupigwa risasi mbele ya Makonda

$
0
0
Katika hali ya kushangaza, jana Mwenyekiti wa soko la Mbande Mbagala katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mokiwa Hassani aliomba kupigwa risasi mbele ya Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam, Paul Makonda baada ya kutuhumiwa kutoza kiwango kikubwa cha fedha katika upangishaji wa vizimba sokoni hapo.

Mwenyekiti huyo alitoa kauli hiyo baada ya mkuu huyo wa mkoa kufika sokoni hapo kwaajili ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake katika manispaa ya Temeke.

Kufuatia tuhuma hizo ikamlazimu mkuu wa mkoa kumsimamisha mwenyekiti wa soko hilo Hassani ili kujibu tuhuma hizo ndipo alipotoa kauli hiyo na kufafanua kuwa bei hiyo ya shilingi laki nne kwa kizimba ni makubaliano kati yao na wananchi hao, pia fedha hizo zimetumika kwa ajili ya kuendesha soko hilo, ambalo bado halijakabidhiwa kwa Halmashauri.

Kufuatia utetezi huo ikamlazimu Mkuu wa Mkoa kutumia busara ambapo aliuagiza mkuu wa wilaya ya Temeke Felix Lyaniva kusimamia uundwaji wa uongozi wa soko hilo haraka mpaka kufikia mwezi Desemba kero zinazolikabili soko hilo ziwe zimetatuliwa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images