Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Gari la wizi lamponza Padri wa Kanisa Katoliki Sumbawanga 0

$
0
0
Kikosi Kazi cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam cha kuzuia wizi wa magari kimeendelea na kazi ya kudhibiti vitendo hivyo kwa kumkamata Padri wa Kanisa Katoliki Sumbawanga Demestrious Apolinary kwa tuhuma za kuhusika na ununuzi wa gari ya wizi.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro amesema mnamo Novemba, 11 baada ya padri huyo kununua gari aina ya Toyota L/cruiser T616 DCH mali ya Joseph Kayawaya lililoripotiwa kuibiwa Dar es Salaam na nyaraka za kughushi na kuuzwa jijini Arusha.

Amesema padri huyo anafanyiwa mahojiano na kwamba upelelezi utakapokamilika atapelekwa mahakamani ili kuona kama ni mnunuzi asiye na hatia au alishiriki kwa namna moja au nyingine katika wizi huo.

Kamanda Sirro amesema pia Jeshi la Polisi linashikilia watuhumiwa wengine wanne aliowataja kwa majina ya Aman Dickson, Exaud Martin, Rashid Haruna na Mzee Nasibu kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa magari katika matukio mawili tofauti.

Katika tukio lingine, Kamanda Sirro amesema Jeshi la Polisi linashikilia majambazi watano na vifaa mbalimbali walivyopora maeneo ya Tuwangoma mtaa wa Masaki, Mbagala.

Wanahabari Watimuliwa kwa Bunduki Kesi ya Lema....Mahakama Yatoa Onyo Kali kwa Jeshi la Polisi

$
0
0
Wakati askari polisi saba watatoa ushahidi mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, Mahakama imetoa onyo kwa askari Polisi na Magereza wanaowasumbua waandishi wa habari na wananchi.

Onyo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Mfa- widhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile baada ya askari Magereza kuwafukuza kwa mbio huku wakiwa na silaha waandishi wa habari waliotaka kuchukua kumbukumbu za Lema kufikishwa mahakamani.

Pia, aliwaonya Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwazuia wananchi wanapokwenda kusikiliza kesi ya mbunge wao. 

Waandishi wa habari jana waliwahi asubuhi kusikiliza kesi ya Lema na kutaka kumpiga picha wakati akifikishwa mahakamani, lakini walipata wakati mgumu baada ya kukimbizwa na askari Magereza wenye silaha ambao hawakutaka mtu yeyote kupiga picha ya mtuhumiwa huyo.

Waandishi hao, Lilian Joel (Uhuru) na Janet Mushi (Mtanzania) waliokolewa na Hakimu Mkazi, Nestory Baro ambaye walimshika huku wakipiga kelele kuomba msaada hatua ambayo ilizua tafrani mahakamani.

Hata hivyo, baada ya tukio hilo, waandishi hao walipelekwa na hakimu Baro kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi, Rwezile ambaye alishuhudia pia tukio hilo.

Hakimu Rwezile aliwaita maofisa wa Polisi, waliokuwa mahakamani hapo na kuwaonya kuacha tabia ya kuwakamata na kuwabughudhi wananchi na wanahabari wanaofika mahakamani hapo kusikiliza kesi.

Hakimu Rwezile, pia alilitoa agizo hilo la kuwaonya askari Magereza na Polisi baada ya wakili wa Lema, John Mallya kuomba tamko la mahakama kutokana na wananchi kuzuiwa kuingia mahakamani, kukamatwa na kunyanyaswa waandishi wa habari.

Hakimu Rwezile alitoa agizo tena kwa askari Magereza na Polisi wanaofika mahakamani kuacha kuwasumbua wananchi na kueleza pamoja na wanahabari wana uhuru wa kufika mahakamani na kusikiliza kesi.

“Hakuna usiri mahakamani hatutarajii tena kuona misuguano hapa, tayari nimezungumza na waandishi na askari Magereza kuhusiana na suala hili, eneo hili lipo chini ya Mahakama hivyo watu wanapaswa kuingia na kutoka salama,” alisema 

Jana saa mbili asubuhi, Lema alifikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha kwa basi la Magereza, akiwa chini ya ulinzi mkali na haikuruhusiwa kumpiga picha.

Mbele ya Hakimu Rwezile, wakili wa Serikali, Fortunatus Mhalila alisoma maelezo ya awali ya kesi hiyo na kudai upelelezi umekamilika na upande wa Jamhuri una mashahidi saba.

Aliwataja mashahidi hao kuwa ni Ofisa Upelelezi wa Polisi Mkoa wa Arusha (RCO), SSP George Katabazi, Mkuu wa Upelelezi wa Polisi Wilaya ya Arusha (OSCID), ASP Damas Masawe, Mkaguzi wa Polisi, Adam Nyamiti, WP 6826 Ester Yohana na Ofisa wa Kitengo cha Upelelezi Makosa ya Mtandao Makao Makuu ya Polisi, Ezekiel Kway.

Alidai katika kesi hiyo, Lema anatuhumiwa kuhamamisisha watu kutenda kosa ikiwa ni kinyume na kifungu 390 (35) cha Kanuni za Adhabu, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.

Mhalila alidai Lema kati ya Agosti Mosi hadi 26, alitengeneza na kusambaza ujumbe mfupi wa sauti kupitia WhatsApp kuhamasisha watu kutenda kosa, ikiwapo kuwataka kufanya maandamano kuanzia Septemba Mosi mwaka huu. Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rwezile alimtaka Lema kueleza kama maelezo hayo ni sahihi au la.

Lema alikanusha kutuma ujumbe wa kuhamamisha uvunjaji wa sheria. Wakili Mallya alisema upande wa utetezi upo tayari kupangwa kwa siku ya kuanza kuwasikiliza mashahidi. Kutokana na maelezo hao, Hakimu Rwezile aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 2, ushahidi utakapoanza kutolewa.

Lema na mkewe, pia wana kesi nyingine ya kutoa lugha ya uchochezi dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambayo nayo iliahirishwa hadi Desemba 21 kutokana na mtuhumiwa wa pili, Neema Lema (33) kutokuwapo mahakamani.

Wakili Mallya alisema Neema ameitwa jijini Dar es Salaam katika kesi nyingine. Baada ya maelezo hayo, Hakimu Rwezile aliahirisha kesi hiyo na Lema kurejeshwa magereza hadi leo, Mahakama Kuu Kanda ya Arusha itakapoanza kusikiliza maombi ya dhamana.

Mwenyekiti wa Parole Augustine Mrema kumshtaki Mkuu wa Magereza Dodoma kwa Waziri Mkuu

$
0
0

Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole,Dkt. Augustine Mrema  amemwandikia barua Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Kasim Majaliwa kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango wake wa kuwatoa wafungwa ambao tayari wameshalipiwa fedha na wasamalia wema baada ya kukidhi vigezo.

Dkt. Mrema ameyasema hayo mchana huu wakati wa kutoa taarifa yake hiyo kwa waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuzungumzia suala lake hilo la Maafisa wa Magereza kusitisha hatua ya kukatisha mpango wake licha ya kuwalipia wafungwa waliokidhi vigezo.

“Mimi nimeona nisinyamaze. Napaza sauti nataka Rais aone, ajue kama magereza yetu yanashida na tunalotatizo kwa nini mpango huu umesimamishwa na umesitishwa tumekosea wapi?.

"Nimesha muandikia barua Waziri Mkuu kulalamikia jeshi la Magereza kukwamisha mpango huu na watu 43 tayari tumesha walipia faini hiyo lakini bado wapo magerezani wanasota. Mrema amefanya kosa lipi? Ama Mama Mchungaji Getrude Rwakatare amekosa nini? Mpaka wamesitisha zoezi hili” amesema Mrema kwa waandishi wa habari.

Dkt. Mrema ameweza kuonyesha nyaraka ikiwemo risiti mbalimbali walizofanya malipo kwa ajili ya kuwatoa wafungwa hao ambapo amesema haki ya kuzuia mpango huo imeweza kumuumiza vibaya kwani wasamalia wema walioweza kujitolea fedha za mpango huo imewagusa pia.

Pia ameongeza kuwa,  mpaka sasa magereza mbalimbali kuna msongamano wa wafungwa ambao wanahitaji msaada wa kutoka ila hawajapata fedha za kulipiwa hivyo pindi wasamalia wema kama Mchungaji Mama Rwakatare wanapojitokeza wanatakiwa kupongeza na wala si kupinda kona kona.Hivi karibuni Jeshi la Magereza lilisitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.

Awali ilidaiwa kuwa Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni.

Kwa mujibu taarifa zilizonukuliwa katika moja ya vyombo vya habari hapa nchini vilieleza kuwa, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo na  kuongeza kuwa, wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao.

Hata hivyo Mrema alisema  mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa hivyo kusitisha unarudisha nyuma juhudi za Bodi hiyo ya Parole katika kuwasaidia wafungwa waliokizi vigezo

Lipumba Atishia Kumpiga Marufuku Maalim Seif Kufanya Mikutano Tanzania Bara

$
0
0
Mwenyekiti    wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, amesema atampiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara kama hatamtambua kuwa mwenyekiti halali wa chama hicho.

Lipumba alisema hayo juzi alipokuwa akizungumza na viongozi wa CUF kwenye mkutano wa ndani mkoani Geita.

Ziara ya Lipumba imefanyika wakati Maalim Seif akiwa amesambaza barua kwa viongozi wa CUF wa wilaya zote nchini akiwataka wasishirikiane na Profesa Lipumba huku akionya atakayekaidi atachukuliwa hatua.

“Kama Maalim Seif hatambui kuwa mimi ni mwenyekiti wake, huku mimi nikimtambua kuwa Katibu Mkuu wangu, basi naye tutamzuia kufanya mikutano ya kisiasa Tanzania Bara,” alisema Lipumba.

Profesa Lipumba alisema hana tatizo na wananchi wa Zanzibar wala kiongozi wa upinzani atakayetetea watu hao na kuongeza kuwa yeye amekuwa mstari wa mbele kutetea Wazanzibari.

“Mimi natambua kuwa ndiye mwenyekiti halali wa chama hiki na mwenye mamlaka ya kumwondoa mwenyekiti au katibu ni mkutano mkuu wa chama na lazima theluthi moja ya wajumbe watoke Bara na theluthi nyingine Zanzibar, lakini mkutano huo haukufanyika wala muhtasari haupo,” alisema Profesa Lipumba.

Alieleza kwamba kwa sasa yeye na wana CUF wengine wamejipanga kukijenga chama hicho.

Mwenyekiti huyo pia alizungumzia suala la Muungano akisema ni muhimu kwa usalama wa nchi na Taifa kwa ujumla.

Alisema ili kulinda Muungano kuna mahitaji muhimu ya kuwa na vyama vyenye nguvu vitakavyokuwa mstari wa mbele kupigania maslahi ya wananchi wa pande hizo mbili.

Lipumba alisema amefika wilayani hapa akitoka Urambo kwenye msiba wa Spika wa Bunge la Tisa, marehemu Samuel Sitta ambapo pia aliongea na baadhi ya viongozi wa chama hicho.

“Tumeifika Kahama kuzungumza na viongozi wa hapa na wa wilaya jirani, dunia ina changamoto kubwa katika masuala ya demokrasia na kujenga utawala bora kwa baadhi ya viongozi,” alisema Lipumba.

Rais Magufuli asaini Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Novemba 18

TRA Yaongeza Muda Wa Kuboresha Taarifa Za Walipakodi Hadi Januari 2017

$
0
0

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapenda kuwashukuru wakazi wa Dar es Salaam kwa  kushiriki katika zoezi la kuhakiki Namba ya Utambulisho Mlipakodi (TIN).

Kutokana na mwitikio mkubwa wa wananchi kutaka kuhakiki taarifa zao, Mamlaka imeamua kuongeza muda wa uhakiki hadi tarehe 31 Januari, 2017. Pamoja na kuongeza muda wa uhakiki, Mamlaka pia imeongeza vituo vya kuhakiki.

TRA pia inawakumbusha wananchi kuwa wale wenye TIN za biashara wanatakiwa kuhakiki katika ofisi za kodi Mkoa husika na wenye TIN zisizo za biashara (yaani TIN iliyotokana na maombi ya leseni ya udereva au ya kuingiza mzigo bandarini) wanaweza kuhakiki katika kituo chochote hapa Dar es Salaam.

Vituo vya uhakiki vilivyopo ni kama  ifuatavyo:
Pamoja na vituo hivyo, Mamlaka imeanzisha kituo kinachohama (Mobile Office) ambacho kinatoa huduma sehemu mbalimbali.  Ili kuongeza ufanisi, Mamlaka itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuongeza vitendea kazi na vituo vingine vya kuhakiki.

Mwisho, Mamlaka inawasihi  wananchi kuepuka kutumia  Matapeli (Vishoka) kwani zoezi hili linamtaka mlengwa kufika mwenyewe kwenye kituo husika.

Kwa ufafanuzi zaidi tafadhali wasiliana na kituo cha huduma kwa walipakodi kwa kupiga simu za bure: 0800 780078 / 0800 750075 barua pepe: huduma@tra.go.tz


Pamoja Tunajenga Taifa Letu

Limetolewa na:
Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi
TRA- Makao Makuu

Wadau Wapinga TANESCO Kupandisha Bei ya Umeme

$
0
0

Wakati wadau wa umeme wa jijini Dar es salaam wakisubiri wiki ijayo kutoa maoni kuhusu pendekezo la Tanesco kuongeza bei ya umeme kwa asilimia 18.19, wenzao katika kanda nne wamepiga hatua hiyo.

Msimamo huo umetolea katika mikoa ya Arusha, Mwanza, Dodoma na Mbeya ambako vikao vya kukusanya maoni ya wadau vimefanyika chini ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Maji na Nishati (Ewura). 

Jijini Mwanza.
Maofisa wa Tanesco, juzi walijikuta kwenye wakati mgumu kujibu hoja za wadau wa Kanda ya Ziwa kuhusu kutaka kupandisha bei, miezi michache tangu ipunguze kwa asilimia 1.1.

Pia, wadau waliwabana maofisa hao kueleza ni kwa nini shirika hilo halikusanyi madeni sugu kutoka serikalini na taasisi za umma, badala yake inawabebesha mzigo watumiaji wa chini ambao hulipia huduma kabla.

Mwenyekiti wa Kamati ya Walaji wa Bidhaa zinazodhibitiwa na Ewura Mkoa wa Mwanza, Jerry Mwasa alisema Tanesco imekosa ubunifu kiutendaji licha ya taifa kujaliwa vyanzo vingi vya umeme ikiwamo gesi asilia, makaa ya mawe, upepo na joto ardhi.

“Ni aibu maofisa wa Tanesco kuja hapa kudai eti bei za umeme Tanzania ni nafuu kulinganisha na Kenya, Uganda na Rwanda ambao hawana gesi wala makaa ya mawe kama Tanzania,” alisema Mwasa.

Akiwasilisha maoni ya Baraza la Ushauri la Walaji (Ewura CCC), Kaimu Mwenyekiti wa baraza hilo, Thomas Mnunguli alihoji ukinyonga wa Tanesco ambayo Machi 4 iliahidi kupunguza bei ya umeme kwa asilimia 7.9 ifikapo mwakani, lakini ghafla imebadilika na kutaka kuipandisha kwa asilimia 18.19.

“Kwa maoni yetu, Ewura ikatae maombi haya, badala yake Tanesco waagizwe kutekeleza agizo la kuwasilisha mpango mkakati wa kuboresha huduma, kupunguza bei na kukusanya madeni kutoka kwa wadaiwa sugu ikiwamo serikali na taasisi za umma,” alisema Mnunguli.

Kaimu Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Serikali (GCC), Amani Mafura alishauri upandishaji wa bei ya umeme ufanyike kwa awamu ili isiathiri mpango wa Serikali wa kujenga “Tanzania ya viwanda” wala juhudi za wananchi kujikwamua kiuchumi.

Mmoja wa wadau, Frank Zekenuka alisema:“Wakati wateja tunalipia nguzo ambayo hata hivyo inasalia kuwa mali ya Tanesco, bado shirika hili linadai kuelemewa gharama za usambazaji. Hiki ni kiini macho cha kutulainisha tukubali ombi la kupandisha bei.”

Katika kikao cha Kanda ya Kati kilichofanyika Dodoma, wadau walisema kiasi kinachotakiwa kupandishwa ni kikubwa na mwananchi wa kawaida hataweza kukimudu.

Mwakilishi wa Ewura-CCC, Erasto Kishe alisema badala ya shirika hilo kupandisha bei ya umeme, linatakiwa kushusha kwa kuwa shughuli zote za maendeleo zinahitaji nishati hiyo hivyo hatua hiyo itapandisha gharama za maisha.

“Baraza linashauri Tanesco ianze kuwakatia umeme wadaiwa wake sugu ili kulazimisha kulipa madeni yao pamoja na riba kama zilivyo kanuni zake.

Mjumbe wa GCC, Ezamo Mponde aliitaka Ewura iitake Tanesco kutoa maelezo ya kina kwa nini inataka kupandisha bei kwa kipindi cha mwaka mmoja tu tofauti na utaratibu uliopo wa kufanya hivyo kwa kipindi cha miaka mitatu.

“Ukipandisha gharama za umeme ni wazi kila kitu kitapanda bei na kama sababu ni kupanda kwa gharama za uzalishaji pamoja na madeni mliyonayo ni bora kama mngeirudisha ile asilimia 1.1 ambayo mliipunguza Aprili kuliko kuongeza bei kwa asilimia 18.19 baada ya miezi saba tu,” alisema Mponde.

Huko Mbeya, Ewura CCC imeitaka Tanesco kuweka mipango madhubuti ya kukusanya mapato kutoka kwa wadaiwa sugu walipe pamoja na riba badala ya kutaka kuongeza bei.

Mjumbe wa baraza hilo, Julius Mwambeso alisema Tanesco inaweza kupata fedha nyingi kama itakuwa makini kukusanya madeni ya wateja 4,036 wanaodaiwa Sh3.2 bilioni na kubana matumizi ya vikao vya bodi ambavyo vinafanyika mara 49.

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Paul Ntinika alisema Serikali inatoa mchango wake kwa Tanesco ili iweze kuwapunguzia makali wananchi.

Alisema hategemei kuona ongezeko lolote la bei ya umeme kutokana na ukweli kwamba Serikali ingependa wananchi wapate unafuu zaidi.

Maoni ya Tanesco 
Naibu Mkurugenzi Mkuu (Usafirishaji Umeme) wa Tanesco, Kahitwa Bishaija alisema shirika hilo limelazimika kuwasilisha ombi la kupandisha bei ili kumudu gharama za uzalishaji, usafirishaji, usambazaji na kuboresha huduma kwa wateja. 

Alisema licha ya uzalishaji kwa kutumia gesi asilia kuongezeka kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi asilimia 58 mwaka huu, huku matumizi ya mafuta mazito kuzalisha umeme yakibakia asilimia tano pekee kulinganisha na asilimia 19 ya zamani, bado shirika hilo linakabiliwa na hali ngumu kiuendeshaji kutokana na madeni.

Alisema deni la Tanesco limeongezeka kutoka Sh699.57 bilioni Desemba mwaka jana hadi Sh794.48 Septemba na kwamba licha ya kuongeza mapato hadi kufikia Sh1,042.5 bilioni kulinganisha na Sh995.3 bilioni za mwaka jana, inalazimika kutumia wastani ya asilimia 13 ya mapato yake kwa mwezi kununulia mafuta ya kuzalisha umeme.

Bishaija aliwaeleza wadau kuwa ukokotoaji wa bei mpya inayoombwa umezingatia gharama ya ufuaji umeme, usafirishaji, usambazaji, uchakavu na uendeshaji.

Mhandisi kutoka Tanesco, Sophia Mgonja alisema ongezeko hilo la bei linatokana na ukame ulioikumba nchi kutokana na mvua kutonyesha kwa kiwango kinachotakiwa na kwamba kina cha maji katika Bwawa la Mtera ni kidogo hivyo wasipofanya juhudi za kutafuta vyanzo vingine vya kuzalishia umeme, kutakuwa na mgawo.

“Pia kama mnavyofahamu kuwa mamlaka ya utabiri wa hali ya hewa umeshatabiri kuwa mwaka huu hakutakuwa na mvua za kutosha hivyo kama tusipofanya juhudi za kutafuta vyanzo vingine vya kuzalishia umeme tunaweza kukwama huko mbeleni,” alisema Mgonja.

Ziara Ya Makamu Wa Rais Mhe.samia Yawa Na Mafanikio Ukerewe

$
0
0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.

Makamu wa Rais ambaye jana  alisafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika Ziwa Victoria kwenda kisiwa hicho kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa huo,aliwahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.
 
Mradi huo ambao unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.
 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliwaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano inamikakati mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini  ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji. 
 
Akihutubia mamia ya wananchi  wa kisiwa cha ukerewe kwenye kijiji cha Kagunguli mkoani Mwanza mara baada ya kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili  ukiwemo mradi wa maji na ujenzi wa chumba cha upasuaji katika kituo cha afya cha Kagunguli, Makamu wa Rais aliwapa pole wananchi wa kisiwa hicho baada ya kukumbwa na tufani ya kimbunga cha upepo iliyotokea tarehe 04 Novemba 2016 na kusababisha uharibifu mkubwa ikiwemo nyumba za watu kubomoka.

Anne Makinda Azitaka Hospitali Za Serikali Ziboreshe Huduma Ili Zipate Wateja Wengi Wa Bima Ya Afya.

$
0
0
Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Anne Makinda amezishauri hospitali, vituo vya afya na zahanati za serikali kuboresha huduma za afya ili wananchi waliojiunga katika mifuko ya afya ya jamii (CHF) na mfuko wa bima ya afya washawishike kutumia huduma katika hospitali zao.

Makinda ametoa rai hiyo jana alipotembelea hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida kujionea huduma za Bima ya afya zinavyotolewa na changamoto zilizopo ili kwa ushirikiano wa mfuko wa bima ya afya na wadau wake waweze kuzitatua.

Alisema hospitali na vituo binafsi au vya mashirika mbalimbali wamekuwa wanufaikaji wakubwa wa kupata wateja wengi wa bima ya afya na mifuko ya afya ya jamii kutokana na kusifiwa kuwa wanatoa huduma bora tofauti na hospitali za serikali ambazo hupata wateja wachache na hivyo kupata faida kidogo.

Makinda alisema hamasa anayoitoa ya kuboresha huduma kwa vituo vya serikali haimaanishi mfuko wa taifa wa bima ya afya hauthamini vituo na hospitali binafsi bali inataka hospitali za serikali kuboresha huduma na kuingia katika ushindani.

Aliongeza kuwa changamoto ya ukosefu wa dawa na vifaa tiba inawakatisha tamaa watumiaji wa bima ya afya pamoja na watu wengine kujiunga hata hivyo mfuko wa bima ya afya na hospitali za serikali zimejipanga kuziondoa changamoto hizo.

Aidha Makinda aliupongeza Mkoa wa Singida kwa kufanya vizuri katika mfuko wa afya jamii na bima ya afya huku akisisitiza kuendelea kuboresha ili Mkoa wa Singida uwe mfano kwa mikoa mingine ya Tanzania.

Akitembelea majengo mapya ya hospitali rufaa iliyopo eneo la Mandewa Makinda alivutiwa sana na majengo hayo huku akiutaka uongozi wa Mkoa kwa kushirikia na wadau wengine hasa mfuko wa bima ya afya kutafuta pesa za ukamilishaji wa majengo muhimu ili huduma zianze kutolewa katika hospitali hiyo kwakuwa itakuwa msaada hata kwa kanda nzima ya kati.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Mhandisi Mathew J Mtigumwe alimshukuru Anne Makinda kwa kuutembelea mkoa wa Singida ili kujionea huduma za Bima ya afya zinavyotolewa.

Mheshimiwa Mhandisi Mtigumwe alimuahidi Makinda kuwa Mkoa utaendeleza ushirikiano mzuri na Mfuko huo na kuomba waendelee kutoa ushirikiano wa vifaa tiba na ukarabati wa miundombinu ya hospitali na vituo vya afya vya serikali ili kuboresha huduma za afya Mkoani Singida.

Aliongeza kuwa Mkoa utaendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii na bima ya afya ili wapate huduma bora hata wakati wakiwa na upungufu wa fedha kwani bima huokoa maisha.

Umoja wa Ulaya (EU) Wasema Tanzania ina haki kutosaini Mkataba EPA kama Haijaridhika Nao

$
0
0

BALOZI wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Roeland Van de Geer amesema Tanzania ina haki ya kuamua kutosaini Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara na Jumuiya ya Ulaya (EPA) hadi itakapojiridhisha manufaa yake.

Alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo mbalimbali vya habari kuhusu masuala mbalimbali pamoja na kujibu maswali ya wanahabari hao.

Akizungumzia suala la Tanzania kutosaini mkataba huo wa EPA, ambao nchi wanachama waliosaini hufanya biashara bila kutoza kodi, Balozi Van de Geer alisema ingawa wasiwasi wa Tanzania kuwa mkataba huo utadhoofisha juhudi za nchi za kufufua viwanda vyake, haoni kama kuna ushindani kwenye hilo.

“Ingawa sioni ushindani unaohofiwa na Tanzania kwenye soko la EPA, lakini uamuzi wake wa kutosaini ni haki yao na nisisitize kuwa ni vyema Tanzania isisaini mkataba wowote ambao wana mashaka nao hadi pale watakapojiridhisha umuhimu wake,” alisema Balozi Van de Geer.

Aliongeza ni vyema nchi ikachukua muda kujiridhisha badala ya kukimbilia kusaini, kwa sababu endapo baadaye wataona mkataba huo hauna manufaa na huku wameusaini, watasononeka hivyo ni vyema wakaupitia na kuona kama una maslahi kwao.

Awali, Septemba mwaka huu, Mwenyekiti wa EAC, Rais John Magufuli alisema viongozi wote kwa pamoja walikubaliana kupewa muda wa miezi mitatu ili Sekretarieti ya EAC iangalie na kupitia masharti ya EPA kabla ya kusaini ili kila mmoja afaidike.

Hata hivyo, katika jumuiya hiyo ya EAC, nchi ambazo tayari zimesaini mkataba huo ni Kenya, Rwanda na Uganda na nchi zilizobaki ni Tanzania na Burundi.

 Rais Magufuli alisema katika kikao hicho, walibaini mambo 10 ambayo yanapaswa kuangaliwa kabla ya kufikia uamuzi kwa maslahi ya nchi na wananchi.

Mwenyekiti alitaja mambo ya kuangaliwa kuwa ni kwa namna gani nchi za EAC zitafaidika, njia gani itatumika kuzuia bidhaa za kilimo na kulinda wakulima, usawa, makusanyo yatokanayo na bidhaa zitakazoingizwa, Burundi itasainije huku ikiwa imewekewa vikwazo na EU, kujitoa kwa Uingereza EU na athari zake, kukosekana kipengele cha kuruhusu nchi nyingine kujihusisha na nchi za EAC kibiashara, kukosekana ushuru wa forodha na kipengele cha nchi kujitoa pale inapoona haijaridhika na mkataba.

Rais Magufuli alisema mkataba huo ukisainiwa kwa wakati huu, nchi wanachama zinaweza kuingia kwenye mtego mbaya.

Akizungumzia kujiondoa kwa Uingereza kwenye EU, Balozi Van de Geer alisema EU bado iko imara na umoja huo utaendelea kuwa miongoni mwa mataifa yenye uchumi imara duniani.

Kuhusu kiwango cha biashara baina ya Umoja wa Ulaya na Tanzania kwa mwaka, Balozi Van de Geer alisema hivi sasa mauzo yamefikia dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka huku akimsifu Rais Magufuli kwa sera yake ya viwanda na kusema umoja huo unamuunga mkono.

Aidha, aliisifu Serikali ya Awamu ya Tano kwa kujitahidi kuendesha nchi kwa kutumia vyanzo vya mapato vya ndani kwa wingi, badala ya bajeti kutegemea wahisani wa nje.

“Tumeona juhudi za serikali kwenye suala la bajeti ya sasa utegemezi wa wahisani kutoka nje ni chini ya asilimia 15 ya bajeti, ukilinganisha na awali ambapo bajeti kwa asilimia 40 ilikuwa tegemezi kwa wahisani, tunaona mabadiliko, na hii inaifanya Tanzania kuondoka kwenye nchi za kundi masikini zaidi duniani,” alieleza.

Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili UDOM afikishwa kizimbani akidaiwa kufadhili Ugaidi

$
0
0
Mtu mmoja anayehusishwa na vitendo vya ugaidi, Azan Abubakary amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini na kusomewa mashtaka yake.

Akiwa amevalia fulana ya rangi ya bluu na kijani na suruali nyeusi na viatu vya matairi (maarufu kama katambuga), alisomewa shtaka lake mbele ya Hakimu Mwajuma Lukindo.

Mshtakiwa huyo anashtakiwa kwa makosa ya kufadhili ugaidi chini ya kifungu cha 13 cha sheria ya makosa ya kuzuia ugaidi namba 21 ya mwaka 2002. 

Ilidaiwa kuwa Mei 15, 2016 alimtumia fedha Mohamed Ibrahim kwa njia ya M-Pesa kiasi cha Sh 265,000 katika namba +254 708104109 kwa ajili ya kufanyia ugaidi nchini.

Aidha Julai 22, 2016 Abubakary alionekana eneo la Dodoma akituma fedha kwa njia ya M-Pesa kwa Mohamed Ibrahim Sh 148,000 kwa ajili ya kufanya vitendo vya ugaidi. 

Hakimu Lukindo alisema mshtakiwa hatakiwi kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma katika taarifa yake kwa vyombo vya habari imesema kwamba mtuhumiwa huyo aliyefikishwa mahakamani ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Kitivo cha Afya na yupo mwaka wa pili.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa, mtuhumiwa alikamatwa Nzega mkoa wa Tabora baada ya kugundulika kuwa anajihusisha na mtandao wa ugaidi wa kundi la ‘Al Shabaab’ kutoka Somalia.

Kamanda alisema mtuhumiwa alikamatwa kutokana na taarifa za Intelijensia ya Polisi katika masuala ya ugaidi.

Daktari FEKI anaswa Hospitali ya Rufaa Dodoma

$
0
0

Mkazi wa Area C mjini hapa, Boniface Kigomba amekamatwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma akiwa katika harakati za kuwaonyesha wagonjwa kliniki ya wajawazito. 

Tukio hilo lilitokea jana na kusababisha wagonjwa, madaktari na wauguzi kukusanyika katika ofisi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo kumshuhudia. 

Hata hivyo, Polisi aliyekuwa amevalia kiraia alifika hospitalini hapo saa 8:00 mchana na kumfunga pingu Kigomba na kumpeleka kituoni. 

Kigomba alikamatwa akiwa na kitambulisho cha uanafunzi cha Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) chenye namba za usajili T/DOM/2014, muhuri wa hospitali hiyo na kitambulisho kinachoonyesha ni muajiriwa wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF. 

Vitambulisho vingine alivyokutwa navyo ni cha mpigakura, uanachama wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na karatasi zilizokuwa zimeandikwa gharama za matibabu. 

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Caroline Damian alisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipata malalamiko kutoka kwa wagonjwa juu ya ukiukwaji wa maadili unaofanywa na mmoja wa madaktari hospitalini hapo. 

“Tulimuwekea mtego siku nyingi lakini leo (jana) tuliambiwa ameonekana akiwa eneo hili ndipo tulipomkamata na kumhoji na ameonekana hakuna anachokijua kuhusiana na taaluma ya udaktari ingawa alisema yeye ni mwanafunzi wa udaktari Udom,” alisema. 

Dk Caroline alisema Kagomba alipohojiwa alidai kuwa alikuwa akiwaelekeza wagonjwa eneo zinakotolewa huduma hospitalini hapo. 

Alisema mbali na wagonjwa kutapeliwa fedha, hivi karibuni kumekuwa na matukio ya wizi wa vifaa. 

Mwanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Tawi la Dodoma, Pafect Kadawele ambaye anaishi naye katika nyumba ya wazazi wake Area C, alisema alikutana na Kigomba miaka miwili iliyopita katika Kanisa la Upendo na baada ya kumueleza kuwa hana mahali pa kuishi aliamua kumchukua na kuishi naye. 

Alisema kila siku amekuwa akimueleza kuwa anakwenda Udom anakosomea shahada ya udaktari. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema wameanza kushughulikia tatizo hilo na atatoa taarifa leo. 

Makamu Mkuu wa Udom, Profesa Idrisa Kikula alisema katika orodha ya wanafunzi chuoni hapo hakuna jina linalofanana na la Kagomba. 

Mamlaka ya Bandari Bandari yapokea boti mbili za kuegesha meli

$
0
0
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imepokea boti mbili za kisasa za kuhudumia meli kutoka China zitakazotumika katika Bandari za Dar es Salaam na Tanga.

 Meneja Mawasiliano wa TPA, Janeth Ruzangi alisema ujio wa boti hizo zilizopolewa jana utasaidia kuongeza kasi ya utendaji kazi na ufanisi katika bandari hizo. 

Alisema ujio wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa TPA kuongeza vitendea kazi kwa upande wa majini na nchi kavu ili kuongeza kasi ya upakuaji na upakiaji wa mizigo kwa kiwango cha kimataifa na hivyo kuvutia wateja wengi. 

Nahodha Mkuu wa TPA, Kapteni Abdullah Mwingamno alisema boti ya tani 70 iliyopewa jina la Valeria Rugaihuruza itabaki Dar es Salaam kwa ajili ya kuhudumia meli zinazoshusha mafuta katika Boya la SPM lililopo Mji Mwema, wakati nyingine inayoitwa Mwambani itapelekwa Bandari ya Tanga kwa ajili ya kuhudumia matishari. 

Boti ya MV Valeria Rugaihuruza imeundwa na ‘crane’ yake pamoja na boti nyingine ndogo mbili ndani yake kwa ajili ya kusaidia utendaji kazi kwenye boya la mafuta. Boti ya MV Mwambani ina uwezo wa kuvuta tishari lenye uwezo wa kubeba tani 3,500 za mizigo.

Polisi Dodoma Waanza Uchunguzi wa kifo chenye Utata cha kigogo mstaafu Jeshi la Magereza

$
0
0

Naibu Kamishna mstaafu wa Magereza nchini (DCP), Luhusa Chiza (62) amefariki dunia katika mazingira ya utata kwenye Hoteli ya Kitemba mjini Dodoma

Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo, mwili wa Chiza uligunduliwa juzi mchana na mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo alipotaka kufanya usafi. 

Taarifa zaidi kutoka ndani ya hoteli hiyo iliyopo Barabara ya Sita katikati ya mji, zilidai Chiza aliingia Novemba 15 usiku na msichana ambaye alitoroka baadaye. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alisema mwili wa Chiza ulikutwa ukiwa na damu puani na kwamba, aliingia chumbani akiwa na msichana ambaye wanamtafuta. 

Alisema kamishna huyo alifika mjini hapa akitokea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kukagua viwanja vyake na kwamba, alikuwa akielekea mkoani Kigoma. 

Meneja wa Hoteli ya Kitemba, Crispin Daniel alisema mteja huyo aliingia Novemba 15.

“Mhudumu alikuja kuniambia kuna mteja hajisikii vizuri chumbani, anatapika si kwamba alifariki dunia akiwa hapa. Ingekuwa hivyo usingekuta hivi,” alisema. 

Alisema baada ya kupokea maelezo hayo, alipiga simu polisi na walifika na kumchukua na hafahamu kilichoendelea. 

“Watu wanasema alifia hapa kwa sababu waliona polisi wamejaa, ukweli alitoka akiwa anaumwa ndicho ninachofahamu,” alisema. 

Kaimu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Caroline Damian alithibitisha kupokewa kwa mwili huo juzi mchana. 

“Tayari tumeshamfanyia postmortem (uchunguzi) na tumechukuwa sampuli ya chakula, kwa ajili ya kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,” alisema. 

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema mwili wa ofisa huyo ulisafirishwa jana kwenda Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa mazishi.

“Alikuwa akitokea Dar es Salaam kuchunguza afya yake maana anapressure (shinikizo la damu) na alishawahi kuzimia mara nyingi tu,” alisema Kilumbi.

Wito Wa Kujiunga Na JKT Kwa Mujibu Wa Sheria Na Vijana Kujitolea

Godbless Lema Akwama Tena Kupata Dhamana.......Arudishwa Gereza la Kisongo, Hatima Yake Kujulikana Wiki Ijayo

$
0
0

Hatma ya dhamana ya Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), ilishindwa kujulikana jana baada ya mawakili wa Serikali kuweka pingamizi, wakipinga Mahakama Kuu, Kanda ya Arusha kusikiliza maombi ya dhamana yaliyowasilishwa na mawakili wa mshtakiwa.

Kaimu Jaji Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Jaji Sekela Moshi, alisema   kutokana na pingamizi hiyo, atasikiliza hoja za sheria zilizowasilishwa mahakamani hapo kabla hajatoa uamuzi wowote juu ya dhamana ya mshtakiwa.

Aliwaelekeza mawakili wa pande zote mbili kuwasilisha hoja za sheria kabla mahakama haijaendelea na hatua yoyote.

Jaji Moshi alisema atatoa uamuzi kuhusu mvutano huo wa sheria,  Novemba 22, mwaka huu

Katika maombi hayo namba sita ya mwaka 2016, Jamhuri iliwakilishwa na mawakili, Matenus Marandu na Paul Kadushi wakati Lema anatetewa na jopo la mawakili sita ambao ni Peter Kibatala, John Mallya, Adam Jabir, Sheck Mfinanga, Faraji Mangula na Charles Adiel.

Katika shauri hilo jana, hoja za sheria za pingamizi zilianza kusikilizwa saa 4:54 asubuhi hadi saa 7:25 mchana ambako mawakili wa Serikali na wale wa upande wa utetezi, walichuana vikali kujenga hoja.

Akiwasilisha pingamizi hilo, wakili Kadushi, aliiomba mahakama iwaruhusu kuwasilisha pingamizi moja na kama mahakama ikishindwa kuridhia pingamizi hilo, wawasilishe pingamizi la pili.

Alidai   maombi hayo yaliyosainiwa na wakili Kibatala yanalenga katika kifungu cha 372 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinachoipa Mahakama Kuu kufanya mapitio ya mashauri ya kesi za mahakama za chini.

Alidai   hoja ya sheria inasema   mabadiliko ya sheria yaliyofanyika mwaka 2002 yaliondosha haki za pande zote katika kesi za jinai kuomba rufaa au mapitio ya uamuzi mdogo uliofanywa katika mahakama zinazoongozwa na mahakimu nchini.

“Kwa mujibu wa kifungu cha 43 (2) cha sheria ya mahakama za mahakimu, maombi hayo yanakinzana na kifungu hicho kwani uamuzi huo mdogo unaopingwa na mawakili wa mshtakiwa, haujamaliza shauri la jinai.

“Lakini pia, uamuzi huo unaobishaniwa na mawakili wa mshtakiwa, uko katika ukurasa wa 17 hadi 19, hivyo mahakama inafungwa na sheria kusikiliza rufaa au mapitio katika uamuzi mdogo.

“Kwa kuwa uamuzi ni mdogo mahakama inakuwa na uamuzi wa kutupilia mbali maombi haya na kusubiri tuendelee na mwenendo wa kesi. Lakini, kama mahakama haitavutiwa au kushawishiwa  na hoja hii, tunaomba kutoa hoja ya pili,”alidai wakili Kadushi

Baada ya hatua hiyo, hoja ya pili iliwasilishwa ikisema maombi ya Lema hayajakidhi matakwa ya sheria, kifungu cha 359 (1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, sura ya 20 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2,002.

Kwa mujibu wa wakili Kadushi, kifungu hicho kinaelekeza namna mtu asiporidhika na uamuzi uliotolewa na mahakama ya chini, anavyotakiwa kukata rufaa mahakama kuu.

“Msingi wa sheria umeshawekwa na mahakama kuwa maombi ya kufanya mapitio kamwe siyo mbadala wa rufaa na uamuzi mwingi umetamka hivyo,” alidai wakili Kadushi.

Katika maelezo yake, wakili huyo alirejea mashauri mbalimbali ya Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa yenye kesi za namna hiyo na kudai kuwa kulikuwa na haki ya waleta maombi kukata rufaa na haki hiyo ipo mpaka sasa.

Wakili Kibatala
Kibatala ambaye alikuwa akiwawakilisha mawakili wenzake watano, alidai   hoja za sheria zilizowasilishwa mahakamani hapo na upande wa Jamhuri hazina msingi katika sheria na akaiomba mahakama izitupilie mbali.

Aliiambia mahakama   kwamba hakimu aliyeruhusu wakili wa Serikali kusimama kabla hajafikia mwisho wa uamuzi aliokuwa akiusoma ni ishara kuwa mahakama hiyo haikuongozwa vizuri jambo ambalo linaifanya Mahakama Kuu iingilie kati na kutoa maelekezo.

“Hoja walizoleta Serikali hazijakidhi matakwa ya sheria. Kwanza kabisa, pingamizi lao halijasema linakuja kwetu au linakwenda kwa mahakama kwa sababu sisi na Serikali tumeitwa hapa mahakamani na hii ni kama mwananchi wa kawaida kwenda kwa msajili kulalamika kisha jaji akaziiita pande zote mahakamani,” alisema Kibatala.

Alisema  wanaishangaa Serikali kuzungumzia kifungu cha 43 ambacho barua ya maombi yao haijakizungumza na pia mahakama kuitisha majalada na kupitia yaliyotokea mahakama za chini, inajenga mamlaka na kuruhusu mahakama kuu kuitisha majalada hayo kupitia mwenendo au uamuzi.

“Kifungu cha 373 cha sheria hiyo ya makosa ya jinai, kinaelezea jinsi Mahakama Kuu inavyoweza kupata taarifa ya upungufu wa mwenendo katika mashauri yanayoendelea mahakama za chini.

“Mfano mahakama za chini zinaruhusiwa zenyewe kupeleka majalada mahakama kuu ili kupitia mwenendo au kupata taarifa yoyote au kuomba namna ya kurekebisha  wanapokosea na hata mwanasheria mkuu wa Serikali amewahi kutumia mfumo huu katika kesi mbalimbali,” alisema Kibatala.

Alisema mahakama kuu ina mamlaka ya kupokea malalamiko na kuyafanyia kazi na ina uhuru wa kuitisha majalada na kusikiliza maombi ya upande wowote kati ya Serikali au utetezi.

Katika maelezo yake, Kibatala alisema kifungu cha 148 (3) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kinasema rufaa inaweza kukatwa kama mtu amenyimwa dhamana ila uamuzi wa mtu kunyimwa dhamana haukatazi mshitakiwa kuomba mapitio ya uamuzi huo.

“Mahakama ilijivua mamlaka ambayo inayo ikiwa ni pamoja na kazi yake ya sheria. Katika hili, hakimu alikosea kumruhusu wakili wa Serikali kusimama katikati ya uamuzi.

“Nasema hivyo kwa sababu kifungu cha 148 (6) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai kinasema mahakama ikitoa dhamana kwa mshitakiwa ni lazima ifikie mwisho wa hatua ya uamuzi wake kwa kuweka  masharti ya dhamana.

“Lakini katika suala hili, mahakama iliishia njiani baada ya wakili wa Serikali kuingilia kati na kueleza kusudio la kukata rufaa.

“Jukumu letu ni kuiongoza mahakama na siyo kuviziana ili tushinde. Hapa Kadushi amedai haturuhusiwi kuomba mapitio au rufaa ila akasema tulipaswa kukata rufaa na siyo kuomba mapitio ya mwenendo wa uamuzi ule.

“Kwa misingi hiyo, ndiyo maana tunasisitiza kwamba pingamizi la Jamhuri halina mashiko yoyote ya sheria, tunaomba litupiliwe mbali na mahakama isikilize maombi yetu,” alisema Wakili Kibatala.

Katika maombi hayo, Lema kupitia mawakili wake, anaiomba mahakama hiyo ifanye mapitio ya majalada ya kesi za jinai namba 440 na 441 ya mwaka huu ambako anakabiliwa na makosa ya uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli

Mawakili hao wa Lema wanaomba ombi hilo kwa sababu wakati Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Desderi Kamugisha akisoma mwenendo wa uamuzi huo uliokuwa na kurasa 22 hivi karibuni, alisema mahakama hiyo inamwachia Lema kwa dhamana kwa masharti atakayopewa na mahakama hiyo.

Hata hivyo, kabla hajakamilisha uamuzi huo akiwa katika ukurasa wa 21 kati ya kurasa 22, mawakili wa Serikali walisema Serikali inakusudia kukata rufaa juu ya uamuzi huo.

Wakati hayo yakiendelea, jana nje ya mahakama kuu, kulikuwa na ulinzi mkali wa   polisi na askari magereza waliokuwa na silaha za moto.

Wakuu 7 wa Mikoa Hatarini Kutumbuliwa kwa Kushindwa Kutekeleza Agizo la Rais Magufuli

$
0
0
Wakuu wa mikoa saba wako hatarini kutumbuliwa kutokana na kushindwa kutekeleza agizo la Rais John Magufuli kumaliza tatizo la madawati katika mikoa yao. 

Akizungumza jana alipokuwa akipokea madawati 3,500 yenye thamani ya milioni  300  kutoka benki ya NMB, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, George Simbachawene alisema mikoa ya wakuu hao saba inaoongoza kwa upungufu wa madawati. 

Aliwataja kuwa ni wa Geita, Mwanza, Kigoma, Mara, Rukwa, Simiyu na Dodoma. 

Simbachawene alisema kutokana na kushindwa kutekeleza ahadi hiyo ametoa siku 43 na wasipotekeleza watakuwa wameshindwa kwenda na kasi ya Dk Magufuli. 

Wakuu wa mikoa hiyo ni John Mongella (Mwanza), Brigedia Jenerali Emanuel Maganga (Kigoma), Dk Charles Mlingwa (Mara), Zelothe Steven (Rukwa), Anthony Mataka (Simiyu), Jordan Rugimbana (Dodoma) na Ezekiel Kyunga (Geita).

“Hii mikoa ambayo haijatekeleza agizo la Rais John Magufuli kumaliza tatizo la madawati,ninawaomba hadi kufikia Januari 2017 wawe wameshatekeleza, wasipofanya hivyo watakuwa wameshindwa kasi yetu,” alisema Simbachawene.

Alisema Mkoa wa Geita unaongoza kwa upungufu wa madawati 68,306 ya shule ya msingi na 15,669 ya sekondari, Mwanza kuna upungufu wa madawati 41,438 ya shule za msingi, Kigoma 31,171 ya shule za msingi na Mara kuna upungufu wa madawati 15,843 shule za msingi na 1,135 shule za sekondari. 

Rukwa ina upungufu wa madawati 9,634 ya shule za msingi na 1,340 shule za sekondari, Simiyu ina upungufu 10,209 shule za msingi na 647 ya shule za sekondari na Dodoma ina upungufu 10,592 shule za msingi na 4,281 shule za sekondari. 

Simbachawene aliitaja mikoa iliyomaliza tatizo la madawati kuwa ni Mtwara, Lindi, Dar es Salaam, Arusha, Iringa, Kilimanjaro, Mbeya, Manyara, Njombe, Pwani, Ruvuma, Shinyanga, Singida na Tabora.

“Mikoa ambayo sijaitaja wamebakiza kidogo utekelezaji wa madawati, naamini watakamilisha hivyo naishukuru Benki ya NMB kwa kutuunga mkono kuchangia madawati,” alisema Simbachawene. 

Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Ineke Bussemaker alisema walitenga Sh1.5 bilioni kwa ajili ya kununulia madawati. 

Alisema mwaka huu wamenunua madawati 10,000 yenye thamani ya Sh900 milioni. 

TECNO Hawa Hapa Tena…....uko Tayari Kwa #Thenextbigthing?

$
0
0
Kampuni inayoongozwa kwa kuuza simu bora na imara kwa bei nafuu, Tecno kila siku wanaumiza vichwa kuhakikisha kwamba una sababu kibao za kuendelea kufurahia bidhaa za huduma zao. 

Baada ya kukuletea simu kali mbili zilizotoka kwa mpigo, Phantom 6 na Phantom 6 Plus ambazo zimekuja kuteka soko la simu zikiwa na prosesa kali, kuchaji kwa haraka na moja ikiwa na Kamera mbili. 


Sasa Tecno wanachokuletea kingine kipya cha aina yake, tetesi zilizopo ni kwamba hili ni dili litakalowawezesha wateja wake kukwea pipa kwenda majuu.

Kwenye soka kuna nyakati mbili, kuna msimu wa mpira na wakati wa kusubiri msimu wa mpira. JE, UKO TAYARI KWA JAMBO KUBWA KUTOKA TECNO? #TheNextBigThing
Endelea kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno Mobile Tanzania kufahamu jambo hili kubwa ambalo linakujia ndani ya siku chache zijazo.
 

Mwanamke Afariki akiombewa kwa ‘Nabii’ Jijini Arusha.....Dada Yake Amkuta Bila Nguo huku akiwa amenyolewa Nywele na Nyusi

$
0
0
Mwanamke  mkazi wa Unga-Limited jijini Arusha , Lightness Kivuyo ameripotiwa kufa wakati akifanyiwa maombi nyumbani kwa mchungaji aliyejulikana kama ‘Nabii Rajabu’ eneo la Kwa-Mrombo pia jijini hapa.

Kwa mujibu wa dada wa marehemu, Juliana Kivuyo, Lightness alikuwa amesindikizwa nyumbani kwa nabii huyo nyakati za usiku na mumewe aliyemtambulisha kama Shafii Mohammed na kwamba wakati akifanyiwa ibada ya maombi, alianguka na kufariki miguuni mwa ‘Mtume,’ huyo.

“Baadaye shemeji alikuja nyumbani akihema, huku anadai kuwa dada alikuwa kwenye hali mbaya kule kwenye maombi,” alisema Juliana na kuongeza kuwa alitoka mbio kwenda Kwa-Mrombo nyumbani kwa Nabii Rajab na kumkuta dada yake amelazwa kwenye kochi, akiwa bila nguo isipokuwa tu khanga alizofunikwa nazo.

Nabii huyo pia anadaiwa kumnyoa nywele zote pamoja na nyusi za macho wakati akimfanyia ‘huduma,’ hiyo.

Polisi jijini hapa wamethibitisha tukio hilo wakiongeza kuwa tayari watu wawili wamekamatwa kutokana na kifo hicho cha ‘maombi tatanishi.’

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo ameongeza kuwa atatoa taarifa kamili mara baada ya kikao chake na Mkuu wa Mkoa.

Mganga Mkuu katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, Jacqueline Uriwo amekiri kupokea mwili wa marehemu, lakini akasema, “Kwanza walijaribu kutudanganya kuwa huyo mama alikuwa hai na kwamba aliletwa kwa ajili ya matibabu, lakini tukagundua kuwa walichokileta ni mwili mfu, hivyo tukampeleka kwenye chumba cha kuhifadhi maiti!.”

Mkurugenzi wa Huduma ya Mazishi katika hospitali hiyo ya mkoa, Dk Francis Coster alisema mwili ulipelekwa hapo na mume wa marehemu ambaye alisisitiza kuwa mkewe hajafa, bali kazimia tu na kwamba mara nyingi huzimia kwa saa nyingi.

Dk Coster aliongeza kuwa ilibidi na wao wasiweke mwili kwenye jokofu na kuulaza kwenye machela kwa saa sita na ndipo wakaamua kuuweka kwenye droo za maiti, kwani ilikuwa wazi sasa kwamba asingeamka tena asilani.

Waganga hospitalini hapo wamekiri kuwa mwili wa marehemu uliletwa hospitalini hapo ukiwa umenyolewa upara, lakini ukiwa na mikwaruzo pamoja na uvimbe hususan maeneo ya mikono na kifua.

Baba mkubwa wa marehemu, Ally Kivuyo ambaye ndiye mlezi wa Lightness, alisema mume wa marehemu alimtaarifu juu ya kifo hicho na kuongeza; “Lakini baadaye nikaletewa taarifa nyingine kuwa Lightness kumbe alikufa wakati akifanyiwa maombi au vitu vingine, nyumbani kwa mtu anayeitwa ‘Nabii Rajabu,’ hapo basi ikabidi niwataarifu polisi ambao walikuja kumkamata mumewe pamoja na huyo anayejiita nabii au mtabiri.”
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images