Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Orodha ya vyuo 26 vilivyofutiwa usajili na NACTE leo

0
0

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limevifungia vyuo vya ufundi 26 kutokana na makosa mbalimbali, ikiwamo kushindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika cheti cha usajili wa vyuo hivyo, huku likisimamsisha utoaji wa programu zilizokuwa zikitolewa katika vyuo 20 ambazo hazijasajiliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam, Kaimu Katibu mtendaji wa NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga, alisema kuwa wamekuwa wakifuatilia vyuo vya ufundi ili kutathmini kama vinafuata viwango vya ubora wa kitaaluma vilivyowekwa na NACTE katika kutoa mafunzo.
 
Katibu huyo amesema kuwa baada ya kufanya uchunguzi huo, wamebaini vyuo 26 vilishindwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na NACTE katika cheti cha usajili, huku vyuo 20 vikitoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa chini ya idara isiyotambulika,wakati vyuo viwili vikiwa na vituo vya satellite/Kampasi ambavyo navyo havijathibitishwa na chombo husika.

NACTE ni bodi iliyoanzishwa kisheria chini ya Sheria ya Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi, kifungu cha 129, kusimamia na kuratibu utoaji wa elimu ya ufundi na mafunzo nchini Tanzania.  Chini ya sheria hiyo, ili kufikia na kudumisha hali ya mtoa mafunzo, vyuo vyote vinatakiwa viwe vimesajiliwa, vibali na kuwa mitaala iliyopitishwa na baraza. Vyuo haviruhusiwi kuanza kutoa kuanza kutoa huduma yoyote ya mafunzo bila idhini ya baraza.
 
Hapa chini ni mgwanyo wa vyuo katika makundi matatu na hatua zilizochokuliwa dhidi ya kila kundi
 
Jedwali 1: Vyuo vya Ufundi vilivyofutiwa usajili
S/NCHUO
1Institute of Management and Development Studies – Iringa
2Green Hill Institute – Mbeya
3Institute of Business and Social Studies – Mbeya
4Loyal College of Africa – Mbeya
5Mbeya Training College – Mbeya
6Mbengwenya College of Business and Information Technology –Mbinga
7New Focus College – Mbeya
8Shukrani International College of Business and Administration –  Mbeya
9Majority Teachers College – Mbeya
10Rukwa College of Health Sciences – Sumbawanga
11MAM Institute of Education – Mbeya
12Belvedere Business and Technology College – Mwanza
13Geita Medical Laboratory Sciences and Nursing Training College – Geita
14Global Community College – Geita
15Muleba Academy Institute – Muleba
16St. Bernard Health Training Institute – Katoro, Geita
17Victoria Institute of Tourism and Hotel Management – Mwanza
18Gisan Institute of Health Sciences – Mwanza
19Dar es Salaam Institute of Business Management – Dar es Salaam
20SAMFELIS College of Business Studies – Dar es Salaam
21Ellys Institute of Technology – Bunda, Mara
22Tanzania Institute of Chartered Secretaries and Administrators – Arusha
23Emmanuel Community College – Kibaha
24Modern Commercial Institute – Dar es Salaam
25Marian College of Law – Dar es Salaam
Jedwali 2: Vyuo vya Ufundi vinavyotoa mafunzo ambayo hayajathibitishwa
S/NCHUOMAFUNZO
1MISO Teachers College – MafingaCompetence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
2Tusaale Teachers College – MafingaCompetence Building Network (CBN) – a Certificate in Early Childhood Education
3The St. Joseph’s College Institute of Business and Management (SJCIBM) – Morogoro
4The Golden Training Institute – Dar es Salaam
5Nkrumah Mkoka Teachers College – Kongwa, Dodoma
6National Institute of Agriculture (Chuo cha Kilimo cha Taifa) – Arusha
7Musoma Utalii Training College – Musoma
8Mwanza Polytechnic Institute – Mwanza
9Mwanza Polytechnic Institute – Maswa
10Ruter Institute of Financial Management – Mwanza
11Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Mwanza
12Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Geita
13Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Bukoba
14Singni International Training Institute – Bukoba
15Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Kahama
16Dar es Salaam Institute of Journalism and Mass Communication – Simiyu
17Richrise Teachers College – Geita
18Twiga Training Institute – Musoma
19Zoom Polytechnic Institute – Bukoba
20St. Thomas Training College – Shinyanga
Jedwali 3: Vyuo vya Ufundi vyenye Vituo vya Satellite / Kampasi
S/NCHUO
1MISO Teachers College – Mafinga
2Rungemba Teachers College – Mafinga

Kesi ya Godbless Lema na mkewe kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha yakwama kusikilizwa..

0
0
Kesi ya kumtukana Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, inayomkabili Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless lema na mke wake Neema Lema (33), imeshindwa kusikilizwa maelezo ya awali.

Hatua hiyo ni baada ya Mbunge huyo kukwama kuletwa Mahakamani toka Mahabusu kwa sababu zisizojulikana.

Kukosekana kwa Mbunge huyo kuonekana Mahakamani, kulimlazimu Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha Agustino Rwezile kutoa amri ya kutolewa hati ya kumtoa Mahabusu mshitakiwa huyo na kumleta mahakamani hapo ili kesi hiyo isikilizwe maelezo ya awali.

Hata hivyo tangu amri hiyo itolewe saa nne asubuhi hadi saa saba mchana mshitakiwa hakuweza kuletwa mahakamani hapo, licha ya mke wake kuwepo mahakamani hapo.

Rwezile alimtaka wakili wa serikali kueleza sababu za kushindwa kumleta Lema Mahakamani wakati Mahakama imetoa amri.

Wakili wa serikali Fotunatus Mhalila alisema mshitakiwa ameshindwa kuletwa Mahakamani kutokana na sababu zisizozuilika , ila kwa sababu upelelezi umekamilika aliomba Mahakama ipange tarehe ya usikilizaji wa hoja za awali.

Majibu hayo yalipingwa vikali na Wakili wa utetezi, John Mallya ambaye alitaka kufahamu sababu za kutomleta Lema anazodai hazikuweza kuzuilika ni zipi na kwa nini zisitajwe  mahakamani. 

“Mheshimia hakimu hizo sababu zisizoweza kuzuilika ni zipi, Wakili wa seriali atueleze, tujue kama siyo amedharau mahakama licha ya kutakiwa kumleta mshitakiwa,” alisema.

Baada ya hoja hizo kutolewa Hakimu Rwezile aliendelea kusisitiza hati ya kumtoa Mahabusu itolewe ili aletwe Mahakamani leo katika kesi hiyo, ambayo itasikilizwa hoja za awali.

Awali katika kesi hiyo Godbless Lema na mke wake Neema, alisomewa mahitaka kuwa kati ya Agosti 20 Mwaka huu ndani ya Arusha,walimtumia ujumbe wa simu ya kiganjani Mkuu huyo wenye lugha ya matusi , huku wakijua ni kosa kisheria. 

Ilidaiwa kuwa ujumbe huo ulitumwa kutoka 076415**47 namba 075655**18 kwenda namba 0766-75**75 ukidai, “Karibu, tutakuthibiti kama Uarabuni wanavyothibiti mashoga.” Washitakiwa walikana shitaka hilo na walipatiwa dhamana

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Novemba 16

Mgonjwa ashindikana kutibiwa Muhimbili kwa kuwa mrefu kuliko binadamu wa kawaida

0
0
Kijana Baraka Elias Mashauri mwenye umri wa miaka 35 mkazi wa Musoma mkoani Mara ameshindwa kupata matibabu katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) kutokana na urefu wake usio wa kawaida.

Baraka anayesumbuliwa na tatizo ya nyonga ana kimo kirefu cha zaidi ya  futi 7 na hii kufanya kushindwa kupatiwa matibabu kufuatia vifaa katika taasisi hiyo ikiwemo mashine za X- ray vitanda vya kufanyia upasuaji kuwa vifupi ukilinganisha na urefu wake.

Tatizo hilo la nyonga linalomsumbua Baraka limemfanya ashindwe kutembea na kulazimika kutumia magongo ambayo anasema yanamtesa kutokana na urefu alionao.

Akizingumzia jinsi watu wanavyomshangaa kutokana na urefu wake alisema kuwa kwake anaona fahari kwani ni maisha ambayo ameyazoea kila anapokwenda. Amesema kuwa hiyo haimpi shinda kwani anajua wanamshangaa kutokana na urefu wake kitu ambacho si kibaya.

Kuhusu ugonjwa unaomsumbua na baada ya kushindikana kupatiwa matibabu nchini, Baraka ameomba wasamaria wema waweze kumsaida ili apatiwe matibabu nje ya nchi ili arudie  kwenye hali  yake ya kawaida kwani magongo anayotumia kutembelea yanamtesa.

Hapa chini ni video yake alipokuwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mifupa.

Naibu Waziri wa Afya Anasa Kiwanda cha Viroba FEKI

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam  na kufanikiwa kukama shehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye maeneo  hayo.

Katika operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya Sinza Jijini Dar  es Salaam. 

Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo, chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.

Kwa hatua hiyo Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili ambao inasemekana wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla  akiwa ameshika vifuniko vya bidhaa za pombe feki katika moja ya kiwanda bubu cha kutengeneza pombe hizo aina ya Konyagi. katika zoezi hilo eneo la Sinza

TIC Yazindua Kitengo Cha Huduma Za Mahala Pamoja Ambapo Huduma zote za uwekezaji Zitapatikana sehemu moja

0
0
Idadi ya siku na utaratibu unaotumika kuomba vibali vya uwekezaji nchini Itapungua baada ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kufungua huduma ya mahala pa kutolea huduma za pamoja.

Katika huduma hiyo vibali kutoka taasisi zote zinazohusika na uwekezaji nchini zitapatikana katika sehemu moja.

Waziri ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ndiye aliyefungua kituo hicho jijini Dar es Salaam jana ambapo katika maelezo yake alizitaka taasisi za umma kufanya kazi kwa ushirikiano ili kupunguza urasimu usio wa lazima na kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Clifford Tandari alisema wao kama kioo cha wafanyabiashara wanaokuja kuwekeza nchini wamejipanga kuhakikisha kuwa huduma wanazotoa zinachochea ukuaji wa uchumi kama yalivyo matarajio ya serikali.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Bw. Godfrey Simbeye aliipongeza hatua hiyo ya serikali na kwamba inaonesha matumaini ya kufikia uwekezaji wenye thamani ya dola bilioni 25 katika kipindi cha miaka mitano ijayo.
Waziri wa Viwanda na Biashara ,Charles Mwijage, akizungumza na baadhi ya watoa huduma katika Kitengo hicho mara baada ya uzinduzi wake.

Mwigulu Afanya Ziara Makao Makuu Uhamiaji.......Aagiza Wahamiaji Haramu Warudishwe Nchini Kwao

0
0
Serikali imeagiza idara ya uhamiaji nchini kufanya uhakiki upya wa vibali vya wahamiaji wote walioko nchini na kwa wale ambao hawana sifa zinazostahili warudishwe kwenye nchi zao kwakuwa wanaishi nchini kinyume na sheria za nchi zinavyoelekeza.

Agizo hilo limetolewa jana na waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na viongozi wa idara ya uhamiaji nchini kwaajili ya kujadili na kutatua kero mbalimbali katika idara hiyo.

Kwa upande wa mifumo ya utoaji vibali Mhe. Mwigulu ameiagiza idara hiyo iunde tume maalum ya kujadili nakuangalia namna ya kuweka mifumo maalum ya kutoa vibali vya uraia kwa urahisi ili kupunguza malalamiko na ufisadi ambao kama hautatatuliwa mapema utasababisha hasara kwa taifa.

Aidha aliwaagiza watawala katika idara hiyo kutenda haki kwa watumishi wake na watanzania kwa ujumla sambamba na kuwalipa madeni yao watumishi wapya walioajiriwa na idara ya uamiaji nchini.

Lowassa aeleza kwanini hakuhudhuria misiba ya Samwel Sitta na Mungai

0
0
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu mjadala ulioibuka kwenye mitandao ya kijamii baada ya kutoonekana kwenye misiba ya aliyekuwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta na waziri wa Elimu wa zamani, Joseph Mungai.

Sitta alifariki Novemba 7 mwaka huu nchini Ujerumani alipokuwa ameenda kutibiwa maradhi ya tezi dume ambapo siku iliyofuata alifariki Mungai.

Lowassa amesema kuwa hakuweza kuhudhuria kwakuwa alikuwa nchini Afrika Kusini akimuuguza mdogo wake, Bahati Lowassa.

“Mdogo wangu Bahati Lowassa ni ofisa ubalozi nchini Afrika Kusini, alikuwa anaumwa na alikuwa amelazwa. Kwa siku zote nilikuwa huko kumuangalia. Nisingeacha kuhudhuria misiba hiyo,” Lowassa 
 
Mwanasiasa huyo ameongeza kuwa alikuwa pamoja na waombolezaji kwa kutuma salamu zake za rambirambi kwa familia ya Sitta kupitia vyombo vya habari pamoja na kumtumia mwanasheria wake kuwasilisha salamu zake za rambirambi kwa familia ya Mungai.

Makamu Wa Rais Mhe.samia Azindua Kampeni Ya Uchunguzi Wa Saratani Ya Matiti........Asema 50% ya Vifo vya Wanawake Husababishwa na Saratani Hiyo

0
0

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahakikishia wananchi kuwa serikali imeweka mipango na mikakati thabiti ya kukabiliana na idadi kubwa ya vifo vinasababishwa na saratani  hasa saratani ya matiti na mlango wa kizazi kote nchini.

Ametoa kauli hiyo jana  katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza wakati akizundua kampeni ya uchunguzi wa saratani ya matiti na mabadiliko ya awali ya saratani ya mlango wa kizazi mkoani Mwanza.

Samia alisema Tanzania ikiwa ni nchi mojawapo Kusini mwa Jangwa la Sahara ina kiwango cha juu cha vifo vya saratani ya matiti na mlango wa kizazi ambapo asilimia 60 ya vifo vyote   vinavyotokea Kusini mwa jangwa la Sahara vinasababishwa na saratani hiyo.

Makamu wa Rais alisema kuwa vifo vingi vinatokana na uelewa mdogo, imani potofu, gharama kubwa za matibabu, unyanyapaa na kuwepo kwa vituo vichache wa kufanyia uchunguzi  hapa nchini ambapo kwa sasa tiba ya mionzi inapatikana katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Dar es Salaam.

Katika kukabiliana na tatizo hilo, Makamu wa Rais alisema kuwa Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imepokea kiasi cha shilingi bilioni Tano kutoka Benki ya Dunia fedha ambazo zitawezesha vituo Vitatu kwa kila Halmashauri ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za uchunguzi na matibabu ya mapema ili wanawake kote nchini hasa wale wale wa vijijini waweze kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa ukaribu kwenye maeneo wanayoishi.

“Wote ni mashuhuda kwa namna saratani ya mlango wa kizazi inavyosababisha vifo vingi hali ambayo hutokana  na magonjwa wanaogundulika na ugonjwa kuwa tayari wamefikia hatua isiyotibika na kwa pamoja saratani hizi mbili husababisha zaidi ya asilimia 50 ya vifo vyote vya akinamama”

Makamu wa Rais alisisitiza kuwa kwa sasa tayari kuna vituo takribani 300 vinavyotoa huduma za upimaji wa dalili za awali katika vituo vya afya kote nchini na hivyo vituo vipya vitaongeza huduma endelevu ili kupunguza vifo vitokanavyo na saratani.

Kwa upande wake, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa Tanzania  ni miongoni mwa nchi zenye wagonjwa wengi wa saratani ya mlango wa kizazi na pia ndiyo inaongoza katika nchi za Afrika Mashariki.

Alisema kuwa idadi ya wanawake 6,241 hugundulika kuwa na saratani kila mwaka  na kati yao zaidi ya nusu yaani 4,355 hufariki dunia.

Rais wa Congo Joseph Kabila atangaza kutokuwania Urais tena

0
0

Rais wa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo Joseph Kabila, amelihutubia Bunge la Taifa jana na kuwahkikishia wananchi kuwa hatogombea tena Urais katika uchaguzi mkuu ujao.

Rai Kabila amesema anaiheshimu katiba ya nchi yake na kwamba ataifuata huku akisisitiza kuwepo kwa amani na utulivu.

“Jahmuri ya Kidemorisia ya Congo ni nchi inayoongozwa na katiba, hatujakiuka katiba na tutaendelea kuiheshimu. Kwa mda huu kilicho muhimu ni kuangalia maisha ya wakongo,” alisema Kabila.

Hata hivyo, juzi waziri mkuu Augustina Matata Ponyoa alijiuzulu kutoa nafasi wadhifa huo kuchukuliwa na upinzani kwenye utawala wa mpito.

Hatua hii ni ya kutuliza vurugu za kisiasa nchini humo baada ya vyama vikuu vya kisiasa kususia mazungumzo ya kitaifa.

Awali Kamisheni ya Uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo iliahirisha uchaguzi wa rais uliokuwa umepangwa kufanyika mwaka huu hadi mwezi Julai mwakani.

Pia, Mahakama ya juu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza kuwa iwapo serikali ya Rais Joseph Kabila haitaweza kuandaa uchaguzi wa rais katika wakati ulioainishwa basi kiongozi huyo anaweza kubakia madarakani.

Kabila alishika hatamu za kuiongoza Congo mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba yake, Laurent Kabila, na kisha akashinda uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka 2006.

Vyeti FEKI vya vifo Vyatumika Kupata mikopo Elimu ya Juu

0
0
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imebaini kuwepo kwa baadhi ya wanafunzi ambao wamewasilisha vyeti feki vya vifo vya wazazi wao ili waonekane kama ni watoto yatima; hivyo wapewe kipaumbele cha kupatiwa mkopo.

Kuwepo kwa vyeti hivyo vya bandia kumegunduliwa na bodi hiyo baada ya kupeleka nakala za vyeti vyote vya vifo ofisi ya Msajili wa Vizazi na Vifo (Rita) kwa ajili ya uthibitisho ndipo ikagundulika kuwepo kwa kasoro hizo.

Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul- Razaq Badru, amesema  kuwa wahusika wote ambao wamewasilisha vyeti hivyo feki suala lao limekabidhiwa kwa mamlaka zinazoshughulika na makosa ya jinai.

Hata hivyo, Badru hakutaka kuingia kwa undani kuhusu suala hilo kwa maelezo kuwa bado wanaendelea na ukaguzi.

“Bado tunaendelea kuchunguza na idadi yao hapa sina, tukikamilisha tutawaita kuwaambia idadi yao,” alisema Badru na kuongeza kuwa kutokana na kasoro hizo, ndio maana kuna baadhi ya watu wanaolalamika kuwa ni yatima, lakini hawakupata mkopo. 

“Hayo malalamiko ya kwamba kuna yatima wamekosa mikopo tumeyasikia, lakini na sisi tunajiridhisha kuwa huyu ni yatima baada ya kupata uthibitisho wa vyeti vya vifo kutoka Rita,” alisema Badru.

Aliongeza kuwa hata wale ambao ni wanafunzi wenye ulemavu, bodi hiyo haiwezi kuwaamini kama ni walemavu, bali hadi wapate uthibitisho kutoka kwa daktari wa wilaya (DMO) kuthibitisha ulemavu wa mwombaji.

Alisema baadhi ya wanafunzi ambao wanalalamika kuwa wamekosa mikopo ni wale ambao maombi yao yalikaguliwa na kukutwa na dosari kadhaa, na wakaombwa wazirekebishe kasoro hizo, lakini baadhi yao hawakufanya hivyo.

Badru alisema bodi yake baada ya kuchambua maombi ya waombaji wote; hadi sasa imeshatoa mikopo kwa wanafunzi wote wanaostahili wakiwemo yatima, walemavu, wanafunzi wanaosoma kozi za kipaumbele na wahitaji wanaosoma kozi zingine.

Akizungumzia suala la baadhi ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambao wamekosa mikopo na kulazimika kurudi makwao, Badru alisema wanafunzi hao yawezekana ni miongoni mwa wale ambao hawakukidhi vigezo vya kuweza kupewa mkopo.

“Pale Dodoma tumetoa mkopo kwa wanafunzi wapya takribani 3,000, hivyo hao wanaoondoka kurudi nyumbani yawezekana wako kwenye kundi la wanafunzi ambao hawakukidhi vigezo vya kupewa mkopo,” alisema Badru.

Alisema sio rahisi kutoa mkopo kwa wanafunzi wote, kwani Serikal inaendeshwa kwa bajeti na mwaka huu wamechagua kusomesha wanafunzi 25,000 kulingana na bajeti iliyopo pamoja na kulingana na mahitaji ya wataalamu wanaotakiwa na kutokana na vipaumbele vyake.

Alisema anatambua kuna wanafunzi zaidi ya 10,000 ambao wamekosa mikopo na kuongeza; “lakini bajeti ya mwaka huu imeishia hapo, mwaka kesho tunaweza kuishauri Serikali iongeze fedha baada ya kuwa tumefanya tathmini uhitaji wa mikopo hiyo.”

Hata hivyo, Badru alisema kuna wanafunzi ambao wanasoma kozi za kipaumbele, lakini wazazi wao wana uwezo, hao nao hawakupatiwa mikopo licha ya kuwa kwenye kundi la wanaostahili mkopo.

“Kuna mtu anasomea udaktari, lakini wazazi wake wana uwezo, na kuna mwanafunzi anasomea sayansi ya jamii na wazazi wake ni watu wasio na uwezo, hapo lazima tuangalie mhitaji ni yupi kati ya hao wawili na ndiye tunampatia mkopo,” alisema Badru.

Alisema kuna wanafunzi wanasoma kozi za kipaumbele baadhi yao hawakupata mkopo kabisa na baadhi yao wamepatiwa mkopo kidogo baada ya bodi hiyo kufanya tathmini ya hali ya uchumi ya wazazi au walezi wa mwombaji.

Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa atoa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mkuu wa ATCL kufanya mabadiliko ya menejimenti ya Shirika hilo

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa ametoa muda wa mwezi mmoja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), kufanya mabadiliko katika menejimenti ya Shirika hilo ili kuongeza ufanisi na kuboresha utendaji kazi.

Ametoa agizo hilo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza katika mkutano wa Menejimenti pamoja na wafanyakazi wa Shirika hilo na kuwataka kutoa huduma bora ili kulifanya Shirika hilo kuwa miongoni mwa mashirika bora ya ndege barani Afrika.

“Nataka ndani ya mwezi mmoja uwe umeshafanya mabadiliko katika menejimenti, mabadiliko lazima yaanzie juu kwanza kwa watoa maamuzi na ishuke hadi kwa wafanyakazi wazembe na wasio waadilifu,” amesema Waziri Prof. Mbarawa.

Waziri Mbarawa amepinga nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi wa Shirika hilo hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali ipo katika juhudi za kulifufua na kuliimarisha Shirika hilo.

Aidha Waziri Mbarawa ameitaka Idara ya Masoko ya shirika hilo kuzunguka katika taasisi zote zilizo chini ya Wizara yake na kuzishawishi kuweza kutumia huduma za usafiri wa anga wa ATCL.

“Serikali imekamilisha upande wake wa ununuzi wa ndege, sasa kazi inabaki kwenu, sitaki watu wa masoko kukaa ofisini”, amesema Prof. Mbarawa.

Ameongeza kuwa wafanyakazi wa ATC wanatakiwa kujipanga kutoa huduma iliyotukuka kwa wateja wake ili kuweza kuhimili ushindani uliopo katika mashirika ya ndege nchini.

“Inabidi tofauti kubwa ionekane kati yenu na mashirika mengine, yeyote ambaye anaona hawezi kutoa huduma bora kwa mteja atafute sehemu nyingine kwani hapa hatufai ”, amesisitiza Waziri Mbarawa.

Profesa Mbarawa amelitaka shirika hilo kutumia mfumo wa kisasa wa kukata tiketi kwa njia ya simu na kompyuta ili kuwarahishia watumiaji wa shirika hilo kuweza kupata tiketi kwa haraka na urahisi.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo Eng. Ladislaus Matindi amemhakikishia Waziri Mbarawa kufanyia kazi maagizo aliyotoa na kuahidi kuboresha utendaji kazi wa shirika hilo kwa lengo la kuteka soko la ushindani wa usafiri wa anga nchini.

“Kwa sasa tumeanza vizuri na naamini uwezo wa kuzalisha faida zaidi tunao, tunaahidi kuboresha utendaji kazi ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya Serikali ya Awamu ya Tano,” amesema Eng. Matindi.

Dr. Shein Atia Saini Sheria ya Gesi na Mafuta.....Asema Wanaoikosoa ni Wachoyo na Hawana Nia Njema na Zanzibar

0
0
Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, jana amesaini sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia ya Zanzibar.

Mbali ya kusaini sheria hiyo, amewapiga kijembe wanaoikosoa sheria hiyo kuwa ni wachoyo na wasioitakia mema Zanzibar.

Dk. Shein aliwaambia viongozi na waandishi wa habari kuwa sheria hiyo namba 6 ya mwaka 2016, inaipa Zanzibar mamlaka ya kisheria ya kuendeleza rasilimali ya mafuta na gesi asilia.

Alisema kitendo cha kutia saini sheria hiyo, hakijavunja Katiba ya Jamhuri ya Muungano kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hakuna aliyevunja sheria, anayevunja sheria wala atakayevunja sheria. Lakini kama wao wanadai kutia saini sheria hii ni kuvunja sheria, basi watafute suluhisho la kisheria,” alisema.

Aliwashauri wenye mawazo hayo wakasome vizuri Sheria ya Mafuta Namba 21 ya 2015 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo imeweka msingi imara wa kisheria wa kutambua rasilimali ya mafuta na gesi asilia ni miongoni mwa mambo yaliyoorodheshwa kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo yanahitaji usimamizi bora na imara wa kisheria.

Alisema sheria hiyo imeainisha mambo makuu matatu ambayo kwanza ni kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Bara zitasimamiwa na taasisi zilizoanzishwa ndani ya sheria namba 21 ya 2015.

Sheria hiyo inatamka pia kuwa shughuli zote za mafuta na gesi asilia kwa upande wa Tanzania Zanzibar zitafanywa na taasisi zitakazoanzishwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania Zanzibar.

Kuhusu mapato yatokanayo na shughuli hizo, Dk. Shein alisema sheria inatamka upande wa Tanzania Bara mapato yatatumiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa faida ya Tanzania Bara wakati kwa upande wa Tanzania Zanzibar yatatumiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa faida ya Zanzibar.

“Kila upande ulishiriki kikamilifu katika mchakato huu. Tulishauriana kwa kina viongozi na tukapata ushauri wa kutosha kutoka kwa wanasheria wetu wakuu hadi kufika bungeni,” alisema Dk. Shein.

Alisema anatambua sheria hiyo ni mpya na anaelewa changamoto ambazo zinaweza kutokea, lakini akatoa wito kwa wananchi kuiunga mkono na kushirikiana na Serikali.

“Mafuta ni jambo kubwa katika maendeleo, pia yasipotumika vyema yanaweza kuitikisa nchi,” alisema Dk. Shein.

Aliwatahadharisha wananchi kutegemea mafanikio ya haraka kutoka sekta hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla iliyofanyika jana ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.]
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa jana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja jana.

Meya wa West Virginia ajiuzulu baada ya kufurahia andiko lililomfananisha mke wa Obama na Nyani

0
0
Meya wa mji wa Clay nchini Marekani, Beverly Whaling amejiuzulu wadhifa huo  baada ya kuunga mkono maandishi yenye ubaguzi wa rangi kwenye facebook dhidi ya mke wa Rais Barack Obama, Michelle Obama.

Meya huyo aliingia matatani na kuamua kujiuzulu nafasi yake baada ya kuonesha kufurahishwa na ‘post’ ya kibaguzi iliyoandikwa na Mkurugenzi wa shirika moja la kutoa misaada, Pamela Taylor aliyelenga kubainisha tofauti kati ya mke wa Rais Mteule wa Marekani, Donald Trump, Melania na mama Michelle Obama.

Taylor alimtusi Michelle akimfananisha na sokwe huku akimpamba Melania kuwa ni mrembo.

Meya huyo aliandika chini ya ujumbe huo wa kibaguzi,“Just made my day Pam.”

Zaidi ya watu 200,000 wamejiandikisha mtandaoni ndani ya muda mfupi kupinga ubaguzi huo na kuwataka Whaling na Taylor kujiwajibisha haraka.

Vitendo vya kibaguzi vimeripotiwa kuongezeka nchini humo tangu Trump alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais.

Ingawa kauli zake wakati wa kampeni zilikuwa na matamko tata, Trump amewataka wafuasi wake kuacha mara moja vitendo vyovyote vya kibaguzi akisisitiza kuwa yeye atakuwa rais wa Wamarekani wote.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 41 & 42

0
0
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Agnes akaingia ndani ya choo alicho elekezwa, akavua koti lake dogo alilo livaa kutokana na baridi kali, kisha akavua na gloves nyeusi alizo zivaa. Akaminya kitufe kwenye choo cha kukalia na kuyafanya maji kuweza kuzunguka, ili kumdanganya dada huyo kwamba amemaliza haja yake ya kujisaidia.

Kabla hajatoka akasikia mlango ukigongwa, jambo lililo mfanya kujiandaa na kujiweka tayari kwa lolote kisha akamruhusu mtu anaye gonga kuweza kuingia ndani. Akaingia dada mfanyakazi huku akiwa na vifaa vyake, gafla Agnes akampiga ngumi nzito shingoni dada huyo na kumfanya aanguke mzima mzima kama mzoga.

ENDELEA
Akamvuta dada huyo na kumuingiza ndani ya choo. Akatoka ndani ya choo na kuufunga mlango kwa ndani wa kuingilia ofisini hapo, kisha akasimama kwenye moja ya dirisha na kuangalia nje. Kwa bahati nzuri katika sehemu alipo simama anaweza kuona vizuri kwenye mlango wa hotel atakayo ingilia kiongozi huyo, ambapo kumejaa wananchi wengi wakiwa wamejipanga kwa kumpokea kiongozi huyo. Akachukua darubin yake, akatazama kila sehemu ya magorofa ya pembeni ili kuhakikisha usalama wake kama upo.

Alipo ridhika hakuna walenga shabaha wa serikali ambao mara nyingi hujitegega kwenye magorofa makubwa kama hayo. Akafungua kabki kake na kuanza kuchomoa kipande kimoja baada ya kingine cha silaha yake. Akaanza kuiunga kwa utaalamu mkubwa hadi ikakamilika. Akaweka magazine yenye risasi  ishirini, kisha akafunga kiwambo cha kuzuia sauti.

Akasimasa kwenye moja ya sehemu ambapo si rahisi kwa mtu wa nje kuweza kumuona. Saa yake ya mkononi akaiweka vizuri, huku ikionyesha zimesalia dakika kumi kabla ya kiongozi huyo kuweza kufika katika eneno hilo.

“Mmmmmmmm”
Agnes aliguna badaa ya kuanza kuona magari meusi yakianza kusimama katika eneo alipo ielekezea bunduki yake, kwa kutumia lensi iliyopo juu ya bunduki yake, akaona baadhi ya walinzi wa waziri huyo wakishuka kwenye magari hayo aina ya GVC. Walinzi hao wakaendelea kuwa macho huku wakijipanga mstati mmoja kuhakikisha kwamba waziri wao anakuwa salama. Kajasho kembamba kakaanza kumchuruzika Agnes, huku mapigo ya moyo yakinza kumpiga kwa mbali jambo lililo anza kumpa wasiwasi kwani katika kazi kama hiyo mtu hutakiwi kuwa na wasiwasi wa aina yoyote.

“Shitiiii!!!!”
Agnes alizungumza huku akitingisha kichwa chake, akijitahidi kutoa wasiwasi mwingi alio kuwa nao. Gari ndefu yene milango sita, ikasimama kwenye zulia jekundu la kuingialia kwenye hoteli hiyo. Walinzi wanne walio valia suti nyeusi wakaufwata mlango wa nyuma wa gari hiyo, mmoja akashika kitasa na kuufungua.

Agnes akashuhudia mguu mmoja ukitangulia kutoka kwenye gari hiyo, akatulia kidogo kutazama vizuri. Akamuona kiongozi Bwana Paul Henry Jr, akitoka kwenye gari hilo, huku akizungukwa na askari hao wanne. Mapigo ya moyo yakazidi kumuenda mbio Agnes baada ya kumuona mtoto mdogo wa kike mwenye umri wa miaka kama nane akitoka ndani ya gari hilo, na mtoto huyo anafanana sana na bwana Paul Henry Jr.
Agnes akataka kufyatua risasi ila akajihisi vibaya sana huku pumzi akiihisi inakwenda kumuishia, kila allipo jaribu kuiweka sawa bunduki yake, mikono yote ikamtetemeka, akajikuta akiwa ameduwaa akimtazama mtoo huyo aliye nyanyuliwa na bwana Paul Henry Jr na kumbeba kifuani mwake.

Bwana Paul Herny Jr akaendelea kuwasalimia wananchi walijitokeza kumpokea, huku akiwa amembeba mwanaye anaye mpenda kuliko kitu chochote na mara nyingi huwa anapenda kwenda naye kwenye dhiara kubwa kama hii ya hapa nchini Russia.
Mlio wa simu ukamstua Agnes, kwa haraka akachukua ear phone na kuiweka sikioni kisa akaminya kitufe kilichopo kwenye hiyo earphone na kuipokea simu hiyo.

“Unafanya nini wewe, muue huyo”
Sauti ya bwana Rusev alisikika kwenye simu hiyo akizungumza kwa kufoka. Agnes hakujibu kitu chochote zaidi ya kuishika bunduki yake vizuri, akayang’ata meno yake kwa nguvu na kuikaza misuli yake, ili kuuzuia wasiwasi mwingi ulio mtawala.
“Uaaaaaa”
Sauti ya bwana Rusev ikaendelea kumshawishi Agnes kufanya tukio alilo tumwa kuweza kulifanya, mshale wa msalaba uliopo kwenye lensi ya bunduki yake, ukatua kichwani bwana Paul Henry Jr, tayari kwa kufyatua risasi.


Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya novemba 17

Waziri Mkuu Majaliwa azindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme Dar es Salaam

0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Jiji la Dar es Salaam watumie fursa ya uwepo wa umeme wa uhakika kwa kuanzisha viwanda vidogo na vikubwa ili waweze kujiongzea kipato.

Ametoa wito huo jana (Jumatano, Novemba 16, 2016) wakati akizungumza na wananchi na viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa mradi wa uboreshaji miundombinu ya umeme jijini Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ofisi za TANESCO zilizoko Mikocheni jijini humo.
 
Akizungumza kabla ya kubonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi huo, Waziri Mkuu alisema:“Umeme ni mhimili mkubwa sana kwa maendeleo ya nchi yoyote ile. Tumepata umeme wa uhakika, tumieni fursa hii ya uwepo wa umeme wa uhakika kujiongezea kipato.”
 
“Hivi sasa tumepata umeme wa uhakika, fanyeni kazi kwa bidii ili mfaidi matunda ya kuwepo kwa umeme huo. Serikali inategemea kwamba sasa wananchi mtaanzisha na kukuza viwanda vidogo vidogo na vikubwa, biashara zitapanuka na kilimo bora huko vijijini kitaongezeka,” alisema.
 
Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kujenga uchumi wa viwanda na moja ya nyenzo kuu ya kuendesha uchumi wa viwanda kwa tija na ufanisi ni upatikanaji wa nishati ya umeme ya uhakika, na ndiyo maana kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo Serikali imefanya jitihada kubwa kuhakikisha miundombinu ya umeme inaboreshwa ili kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme.
 
“Wataalam wamenieleza kuwa mradi huu ulihusisha ujenzi wa kituo kikubwa cha kupozea umeme cha MVA 100, ujenzi wa njia za usafirishaji umeme wa msongo wa kilovoti 132 katika maeneo mbalimbali ya Jiji kupitia chini ya ardhi, ujenzi wa njia za usambazaji umeme wa msongo wa kilovoti 33, pamoja na ujenzi wa ujenzi kituo cha udhibiti mifumo ya usambazaji umeme (Distribution SCADA System) katika msongo wa kilovoti 33 na 11.”
 
“Kukamilika kwa mradi huu kunaondoa adha zilizokuwepo awali kutokana na kukatika umeme mara kwa mara. Jiji la Dar es Salaam ni kitovu cha shughuli za biashara katika kuleta maendeleo ya Taifa ambapo upatikanaji wa umeme wa uhakika ni wa lazima,” aliongeza.
 
Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na hadhira iliyokuwepo, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisema Wakala wa Jiolojia Tanzania kwa kushirikiana na Wakala wa Jiolojia wa Finland wanaunda mpango wa pamoja wa kuibua madini ya kisasa ambayo yanatafutwa zaidi duniani kukidhi mahitaji ya kiteknolojia.
 
“Hivi sasa madini kama graphite na lithium yanahitajika zaidi kwenye teknolojia za kisasa kama za utengenezaji wa simu, tuachane na madini yaliyozoeleka kama vile dhahabu na Tanzanite,” alisisitiza.
 
Alitumia fursa kuuagiza uongozi wa TANESCO uhakikishe kuwa hakuna mgao wa umeme nchi nzima kwani Watanzania wamechoshwa na tabia ya kukatiwa umeme mara kwa mara. 

“Ili tujenge nchi ya viwanda, tunahitaji umeme wa uhakika, umeme unaotabirika na zaidi ya yote umeme wa bei nafuu,” alisema huku akishangiliwa.
 
Naye Waziri wa Biashara za Nje na Maendeleo wa Finland, Bw. Kai Mykkanen alisema Serikali yake imedhamini ujenzi wa mradi huo kwa vile inaamini kuwa umeme wa uhakika ni suluhisho la kuondoa umaskini kwa hiyo kukamilika kwa mradi huo kutaondoa adha ya kukatika umeme kila mara.
 
Aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika eneo la nishati ya umeme na nishati mbadala.
 
Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Eng. Felchesmi Mramba alisema ujenzi wa mradi huo umegahirimu sh. bilioni 74.6 ambapo kati ya hizo, sh. bilioni 63.56 zimetolewa na Serikali ya Finland na sh. bilioni 11.03 zimetolewa na Serikali ya Tanzania.
 
Alisema kukamilika kwa mradi huo kumewezesha sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam kuwa na njia za mzunguko (ring circuit) zinaoingizaa umeme. 

“Teknolojia hii iliyotumika itawezesha vituo vya kupozea umeme kuwa na njia mbadala ya kupata umeme endapo njia mojawapo inayopeleka umeme itapata hitilafu,” alisema.
 
Naye Meneja wa Kituo cha Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji, Eng. Alex Kalanje alimweleza Waziri Mkuu kwamba kwa kutumia mifumo ya kisasa ya kompyta, (distribution SCADA SYSTEM) kituo hicho cha udhibiti wa mifumo ya usambazaji umeme katika jiji la Dar es Salaam kitawasaidia watoa huduma wao waweze kufuatilia kwa haraka zaidi pale matatizo yanapotokea.
 
“Baada ya kukamilika kwa kituo hiki, lengo letu ni kujenga kituo kama hiki kwenye mjai ya Arusha, Mbeya, Dodoma na Mwanza,” alisema.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Biashara na maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen wakatizama moja ya mitambo ya umeme katika Kituo cha TANESCO cha Mikocheni kabla ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam, Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) wakitazama mfumo wa usambazaji umeme kabla ya Waziri Mkuu kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen akizungumza katika Uzindunduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akizungumza katika Uzindunduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya umeme katika jiji la Dar es salaam uliofanywa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni jijini Dar es salaam Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen na kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia baada ya kukata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen na kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na watalaam kutoka Finland baada ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme jijini Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. Kushoto kwake ni Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen na kulia kwake ni Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Waziri wa Biashara na Maendeleo wa Finland, Kai Mykkanen baada ya kuzindua Mradi wa Uboreshaji Miundombinu ya Umeme katika jiji la Dar es salaam kwenye Kituo cha TANESCO cha Mikocheni Novemba 16, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
IMETOLEWA NA: 
 OFISI YA WAZIRI MKUU,

Makonda Amkaanga Kamanda Sirro....Adai anakula Rushwa za Wauza Shisha, Waziri Mkuu Atishia Kumtumbua Jipu

0
0
Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa amesema atamwajibisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda iwapo hatasimamia ipasavyo kukomesha matumizi ya dawa za kulevya, aina ya shisha.

Hatua hiyo inatokana na kauli ya Makonda kuwatuhumu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Simon Sirro na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi Suzan Kaganda, kulegalega kusimamia suala hilo huku akihofia wanaweza kuwa wamehongwa na watu waliotaka kumhonga lakini akakataa.

Waziri Mkuu Majaliwa alisema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu ya Umeme katika Jiji la Dar es Salaam.

Alisema katika udhibiti wa suala la shisha, mkuu huyo wa mkoa amefanya kazi nzuri, na kwamba kwa kuwa ameshatoa maelekezo, akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, Makonda hana budi kuyatekeleza.

Alisema alivyosikia anawaagiza wakuu wake wa wilaya wote kusimamia maagizo yake na kama hawakusimamia atachukua hatua, basi naye atachukua hatua kwake (Makonda) asipotekeleza suala hilo ambalo kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni tatizo kubwa.

“Sasa mimi nasema nakuagiza wewe usimamie na kama hutasimamia suala hilo nitakuchukulia hatua, hivyo hangaika na shisha kwa wanaopuliza wakiwa wamelala hakikisha unawadhibiti,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa wakati akijibu sehemu ya salamu za Makonda alipopewa fursa ya kusalimia wananchi katika hafla hiyo.

Katika salamu zake, Makonda alisema Waziri Mkuu alipiga marufuku matumizi ya shisha, hivyo alimwagiza Kamanda Sirro kuhakikisha suala hilo linatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

“Lakini Waziri Mkuu nimeshangaa kupita katika baadhi ya maeneo na kuona watu wameanza tena kuvuta shisha na nilipouliza wakasema wewe ndiyo umetoa kibali cha shisha,” alieleza Makonda na kuongeza alishangaa Waziri Mkuu alipiga marufuku shisha, ni lini ametoa kibali kuanza kutumika.

Lakini mkuu huyo wa mkoa alienda mbali zaidi na kudai kuna kikundi cha watu 10 waliokwenda kwake ambao anawatambua kama “maajenti wa shetani” ambao wanapata faida kati ya Sh milioni 35 mpaka Sh milioni 45 kwa mwezi kutokana na dawa hizo za kulevya.

Alidai watu hao walipanga mikakati ya kumshawishi kupokea Sh milioni tano kwa kila mmoja kwa mwezi yaani Sh milioni 50 ili asipige kelele kuhusu shisha na wao waendelee kupata faida. 

“Shisha imerudi katika Mkoa wa Dar es Salaam na nimeshamuagiza Kamishna Sirro, lakini nimeona kama ana kigugumizi… lakini sijajua kama hizi tano tano zimepita kwake na pia RPC wa Kinondoni nimemuona hapa, lakini hawa wana kigugumizi sijui kama hizi tano tano zimepita kwao,” alisema Makonda.

Alisema aliamua kufanya ziara mwenyewe na kushuhudia watoto wadogo wanavuta shisha, hivyo uwezekano miaka 10 ijayo vijana wengi kuwa matatizo ya afya, hivyo kumwomba Waziri Mkuu kutochoka kusimamia suala hilo na taasisi zote ili likome katika mikoa yote.

Kuhusu wafanyabiashara wadogo, alisema suala hilo linamnyima usingizi na kutoa rai kwa wakuu wa wilaya kuwa, kama kuna mkuu wa wilaya atachelewa kutekeleza yale aliyoagiza kuwapeleka machinga katika maeneo yaliyoruhusiwa atachukua hatua kabla ya Waziri Mkuu kufanya hivyo.

Aidha, alishukuru kwa mradi wa umeme akisema ukatikaji umeme una madhara sana na hasa kwa wajasiriamali wadogo wanaojishughulisha na biashara ndogo kama saluni na shughuli nyingine ndogo zinazojenga uchumi wa kati.

NIDA kuanza kutoa namba za utambulisho Desemba

0
0
Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imesema kuanzia Desemba mwaka huu mpaka Januari 2017 itaanza kutoa namba maalum za utambuzi kwa wananchi.

Mkakati huo umetangazwa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mwigulu Nchemba alipokutana na uongozi na wafanyakazi wa NIDA, kwa lengo la kujadili mikakati mbalimbali ya kuboresha utendaji wa mamlaka hiyo.

Alisema tayari serikali imekamilisha kanzidata ya wananchi walizozipata kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC na kwamba, tayari taasisi zaidi ya 35 zimeanza kutumia taarifa za NIDA katika kufanya utambuzi wa wafanyakazi wao sawia na kupunguza usumbufu kwa wananchi kuhusu taarifa zinazowahusu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NIDA Bw. Andrew Massawe alisema kwa zoezi la awali lililofanyika nchi nzima tayari wamefanya uhakiki wa kuwatambua watumishi wa serikali takribani laki tano na elfu sitini na tano.

‘Mpemba’ wa meno ya Tembo na Wenzake Watano Wafikishwa Mahakamani

0
0
WATU sita akiwemo mfanyabiashara Yusuf Yusuf (34) aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli kwa jina la ‘Mpemba’ kuwa ni kinara wa ujangili, wamefikishwa mahakamani wakikabiliwa na mashtaka ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6.

Washtakiwa hao walipandishwa kizimbani jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, huku baadhi wakiwa hawajavaa viatu, wakitembea kwa kuchechemea.

Baada ya kusomewa mashtaka, upande wa Jamhuri ulidai unatarajia kuwapeleka washtakiwa hao katika Mahakama Kuu Kitengo cha Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, maarufu kama “Mahakama ya Mafisadi” kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Washtakiwa hao watapelekwa katika mahakama hiyo baada ya upande wa Jamhuri kuandaa maelezo ya mashahidi pamoja na vielelezo ili kesi hiyo ianze kusikilizwa.

Yusuf pamoja na wenzake Charles Mrutu (37) mkazi wa Mlimba, Morogoro, Benedict Kungwa (40) mkazi wa Mbagala Chamazi, Jumanne Chima (30) mkazi wa Mbezi, Ahmed Nyagongo (33) dereva na Pius Kulagwa (46) walisomewa mashtaka manne mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Thomas Simba.

Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali Paul Kadushi alidai katika tarehe tofauti kati ya Januari, 2014 na Oktoba, mwaka huu wakiwa Dar es Salaam, Tanga, Iringa na Mtwara walijihusisha na mtandao wa ujangili kwa kukusanya na kuuza nyara za serikali ambazo ni vipande 50 vya meno ya tembo vyenye thamani ya Dola za Marekani 180,000 sawa na Sh milioni 392.8 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori.

Aliendelea kudai kuwa katika shtaka la pili kuwa, Oktoba 26, mwaka huu, washtakiwa wakiwa Mbagala Zakhem, walikutwa na vipande 10 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 13.85 vyenye thamani ya dola za Marekani 30,000 sawa na Sh milioni 65.4.

Katika mashtaka mengine, inadaiwa Oktoba 27, mwaka huu, washtakiwa wakiwa Tabata Kisukuru walikutwa na vipande vinne vya meno hayo vyenye uzito wa kilo 11.1 na thamani ya dola za Marekani 15,000 sawa na Sh milioni 32.7.

Aidha, Oktoba 29, mwaka huu walikutwa na vipande 36 vyenye thamani ya Sh milioni 294.6 bila kuwa na kibali cha Mkurugenzi wa Wanyamapori. 

Hakimu Simba alisema washtakiwa hawatakiwi kujibu mashtaka yao kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo aliiahirisha hadi Desemba mosi mwaka huu.

Kabla ya kutoka kwenye chumba cha mahakama, washtakiwa walimuomba hakimu awape muda waeleze jinsi walivyokamatwa kwa kuwa walipigwa sana. Mpemba alidai siku aliyokamatwa, alipigwa sana hadi sasa hawezi kusikia vizuri na viungo vyake vya mwili havina nguvu hivyo aliomba PF3 ili akatibiwe.

Mrutu alidai kuwa alipigwa hadi wakamng’oa kidole kimoja cha mkononi na washtakiwa wengine walidai walipigwa mpaka sasa wanashindwa kutembea vizuri hivyo waliomba wapewe msaada wa kutibiwa.

Hakimu Simba alisema hawezi kutoa amri ya kutolewa kwa PF3 kwa sababu Magereza wana zahanati zao na kuna taratibu wanazifuata hivyo wasiwe na wasiwasi na kama watashindwa kuwatibia, watatafuta utaratibu mwingine wa kuwapeleka katika hospitali za nje ya Magereza.

Baadhi ya washtakiwa, waliingia mahakamani hapo wakiwa wanachechemea huku wakificha sura zao kukwepa kupigwa picha. Washtakiwa wawili hawakuwa na viatu.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images