Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Ommy Dimpoz Na Alikiba Wamekuletea “KAJIANDAE” Inapatikana Mkitodotcom

$
0
0
Mkali wa wa Bongofleva Ommy Dimpoz aliyetamba na kibao chake cha“Baadae” ametuletea burudani mpya akiwa na Alikiba inaitwa ‘Kajiandae’ ambayo imefanywa na muongozaji mwenye kipaji kutoka Afrika Kusini, Justin Campus wa Gorilla Films ambayo unaweza kuipakua kutoka Mkito kwa kubofya hapa http://bit.ly/Kajiandae
Hii inakuwa kolabo ya pili kati ya Ommy Dimpoz na Alikiba baada ya miaka minne. Alikiba yuko chini ya usimamizi wa Studio ya Kimataifa ya ROCKSTAR4000 na Rockstar Publishing wakati Ommy Dimpoz yuko chini ya PKP Management.

Wimbo huu uliobeba ujumbe wa mapenzi unazungumzia mwanamke wa ndoto zao uliandikwa na Ommy Dimpoz pamoja na Alikiba na kufanyiwa kazi na mtayarishaji Emmma The Boy. Video pia iko tayari katika chaneli ya YouTube ya AliKiba na unaweza kuitizama hapo chini. Pakua : http://bit.ly/Kajiandae kisha tupe mrejesho wako.


Una Tatizo Lolote Kuhusu Simu Yako? .....TECNO Wamekujibu Hapa

$
0
0
Kampuni inayoongoza kwa kuuza simu bora kwa gharama nafuu ambayo kila Mtanzania anaimudu, Tecno imefanya “kujiongeza” katika kukusaidia mteja wake kuhakikisha kwamba haupati tatizo lolote unapotumia simu zao na kupatiwa msaada wa haraka endapo utakuwa na tatizo. 

Timu ya Tecno imefanya mahojiano ya moja kwa moja na mashabiki wa mtandao wa kijamii wa Facebook maarufu kama “Facebook Live” ambapo ilijibu changamoto mbalimbali kutoka kwa watumiaji wa simu za Tecno.

Akizungumza katika mahojiano hayo mtaalamu wa masuala ya ufundi kutoka Tecno John G. Ndazi alisema “Tumekuwa tukipokea baadhi ya maswali kupitia kurasa zetu za mitandao ya kijamii kutoka kwa wateja wetu na bila shaka nyote mnafahamu kwamba hivi karibuni tumezindua simu mbili kali, kuna Phantom 6 na Phantom 6 Plus ambazo zimepokelewa vizuri na tukaamua kutumia Phantom 6 kujibu maswali kupitia Facebook Live ambapo tumejibu maswali kutoka kwa wateja wetu.” 

Pamoja nae alikuwepo Gilbert Asumwisye ambaye ni Mhandisi wa Programu.


Unaweza kutembelea kurasa za mitandao ya kijamii ya Tecno kufahamu zaidi kuhusiana na Tecno Phantom 6 na Phantom 6 Plus.
 
 
 


CCM Yatuma Salamu Za Rambi Rambi Kifo Cha Mzee Samwel Sitta

$
0
0
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa majonzi na simanzi kubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samuel John Sitta, Spika mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kilichotokea usiku wa jana tarehe 6/11/2016 katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akitibiwa.

Mhe. Samuel John Sitta, amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za utumishi katika Chama na Serikali. Alikuwa Katibu wa CCM na Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha uwekezaji, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Mjumbe wa Kamati Kuu, Mbunge, Waziri na Spika.

Mhe. Sitta alikuwa ni Kiongozi mchapakazi, mwadilifu na aliyejitambulisha kwa utendaji wenye kufuata falsafa yake ya “kasi na viwango”. Ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Chama na Serikali.

Katibu Mkuu wa CCM Ndg Abdulrahman Kinana amemtumia salamu za rambi rambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, familia ya Mhe. Sitta pamoja na Wananchi wa Jimbo la Urambo kufuatia kifo cha Kiongozi huyu. Tunaungana nao katika msiba huu ambao pia ni msiba wetu

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Ameni

Imetolewa na:-
CHRISTOPHER OLE SENDEKA (MNEC)
MSEMAJI WA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

07 – 11 – 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 8

Bodi Ya Pamba Kuhamia Mwanza.

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi imejipanga kuhamishia Bodi ya Pamba katika Mkoa wa Mwanza kabla ya Novemba 10 mwaka huu ili kuhakikisha wakulima wa pamba waliopo katika mkoa huo wanapata huduma zilizo bora kwa ukaribu na haraka.

Hayo yamesemwa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe.  William Ole Nasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Bukombe Mhe. Doto Biteko lililohoji juu ya hatua ya Serikali kwa wakulima walioathirika na pembejeo zilizotolewa ambazo hazikuwa na ubora pamoja na kuhamishia Bodi ya Pamba katika mkoa huo.

”ili kuwafikia kirahisi wakulima wa pamba waliopo mkoani Mwanza, Wizara imeamua kuhamishia Bodi hiyo katika mkoa huo na kwa taarifa zilizopo Bodi hiyo inatakiwa kuhama haraka iwezekanavyo kabla ya Novemba 10 mwaka huu”, alisema Mhe.Ole Nasha.

Kwa upande wa matatizo ya pembejeo, Mhe. Ole Nasha alisema kuwa Serikali tayari ina taarifa kuhusu tatizo lililowapata wakulima wa pamba katika maeneo mbalimbali kwa kusambaziwa viuatilifu pamoja na mbegu ambazo hazikuwa na ubora unaotakiwa hivyo kuathiri wakulima nchini.

“Serikali iliiagiza Tropical Pesticides Research Institute (TPRI) kufanya uchunguzi wa malalamiko ya wakulima ambao ulibaini kuwa viuatilifu hivyo vilikuwa na utendaji hafifu hivyo Serikali itaanza kuzalisha mbegu bora za pamba za UK08 ili kuhakikisha tatizo hili halijirudii tena”, alisema Mhe. Ole Nasha.

Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa kufuatia changamoto hizo za uotaji wa mbegu, Serikali iliamua kufanya majaribio ya utoaji wa mbegu ambazo zilikuwa zikisambazwa hapo awali bila kujua ufanisi katika uotaji wake.

Alithibitisha kuwa, matokeo ya jaribio hilo yamewezesha kutoa maelekezo kuhusu aina za mbegu za pamba zenye sifa za msingi ambazo zitasambazwa kwa wakulima katika msimu wa kilimo wa mwaka 2016/2017.

Tanzia: Mwenyekiti wa Klabu ya Azam, Said Mohammed afariki dunia

$
0
0
Uongozi wa Klabu ya Azam FC kwa masikitiko makubwa, unatangaza kifo cha mwenyekiti wake, Mzee Said Mohamed Abeid, kilichotokea alasir ya  Novemba 7, 2016, katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar es Salaam.

Mzee Said Mohamed, atakumbukwa kama mmoja wa nguzo muhimu kwenye mafanikio ya klabu ya Azam FC tangu kuanzishwa kwake miaka takribani nane iliyopita.

Chini ya uongozi wake kama mwenyekiti wa Azam FC, aliiongoza klabu hii kunyakuwa mataji mbalimbali makubwa na kwa mafanikio, ikiwemo taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la Mapinduzi mara mbili pamoja na Ngao ya Jamii.

Si hivyo tu, mchango wake Mzee Said Mohamed hauku-ishia nyumbani kwake Azam FC tu, bali hata kwenye familia ya soka la Tanzania kwa ujumla wake ambapo hadi umauti unamkuta alikuwa ni makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu Tanzania bara na mjumbe wa kamati mbalimbali za shirikisho la soka Tanzania, TFF.

Sisi Azam FC, tutamkumbuka Mzee Said Mohamed kwa ucheshi wake, ukarimu na uchapakazi wake kwa ujumla.

Marehemu alizaliwa tarehe 20 Machi 1940 visiwani Zanzibar na anatarajiwa kuzikwa Jumanne leo  tarehe 8 Novemba, 2016 kwenye makaburi ya Kisutu baada ya swala ya Alasir, mwili wake utaswaliwa kwenye msikiti wa Maamour Upanga.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake Said Mohamed Abeid mahali pema peponi, Amiin,

Innalilah Wa-inna-ilaih Rajioun.

Nassor Idrissa,

Makamu Mwenyekiti,

Azam Football Club.

Hospitali Ya Taifa Muhimbili Yapokea Msaada Wa Mashine Kubwa Ya Utrasound Yenye Uwezo Mkubwa Wa Kung’amua Magonjwa Ya Figo.

$
0
0
Hospitali ya Taifa Muhimbili imepokea  msaada wa mashine kubwa na ya kisasa  ya Utra Sound maalum  kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye matatizo ya Figo.

Msaada huo umetolewa  jana na Hospitali ya Chuo Kikuu cha Haukeland cha nchini Norway ambapo pamoja na mambo mengine wameahidi kuendelea kutoa ushirikiano  katika maeneo ya elimu , utafiti pamoja na vifaa tiba.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya Figo ambaye pia Mhadhiri kutoka MUHAS Paschal Ruggajo  amesema mashine hiyo itasaidia kuchukua sampuli ya figo kwa ajili ya kugundua  magonjwa  ya Figo , kuweka vifaa kwenye mishipa damu kwa wagonjwa wanaoanzishiwa matibabu ya uchujaji wa damu na kugundua matatizo mbalimbali ya Figo.

“ Kwa muda mrefu sasa tumekua na ushirikiano wa karibu kati ya Hospitali hiyo , MUHAS na MNH  na wametusaidia kufundisha Madaktari sita wa Figo , wameshatoa mashine za kusafisha Figo na sasa wametupatia mashine hii kubwa ya Utra Sound kwakweli tunawashukuru kwa msaada wao.” Amesema Dk. Ruggajo.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili , Dk . Hedwiga Swai ambaye ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba ameishukuru Hospitali hiyo ya Haukeland  na kusisitiza kuwa msaada huo umekuja wakati muafaka kwakua  mashine hiyo itasaidia sana katika kitengo cha Figo
Profesa Einar Svastard ( kulia)   akimkabidhi  msaada wa mashine kubwa ya kisasa ya Utrasound  Mkurugenzi wa huduma za tiba  MNH Dk. Hedwiga Swai  .
Profesa Einar Svastard akimfanyia uchunguzi mgonjwa kwa kutumia mashine hiyo

Tanzania yachaguliwa kuongoza mkutano wa kimataifa wa wamiliki wa kampuni

$
0
0
Kufuatia uchumi wa Tanzania kuzidi kukua na kushika nafasi ya kwanza kwa ukuaji uchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki, pamoja na jitihada zake za kuifanya nchi kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.

Imechaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa tatu wa kimataifa wa Chama cha Kampuni Ndogo na za Kati Ulimwenguni unaotarajiwa kufanyika kuanzia Disemba 5 hadi 7, 2016 katika Ukumbi wa Mikutano wa Mwalimu Julias Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Taasisi ya Sekta Binafsi nchini (TPSF), Godfrey Simbeye amesema chama hicho huchagua nchi yenye uchumi mkubwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo na kwamba kuchaguliwa kwa Tanzania kuwa mwenyeji wake, kunaashiria kuwa miongoni mwa nchi inayokuwa kiuchumi kwa kasi barani Afrika.

“Tanzania sasa inaanza kuonekana kuwa na hadhi, hali hii huenda inachangiwa na utendaji kazi wa Rais John Magufuli, na itakuwa nchi ya tatu kufanyika mkutano huo unaokutanisha wadau na wamiliki wa kampuni ndogo na za kati duniani,” amesema.

Amesema mkutano huo utasaidia kampuni za ndani kujifunza namna ya kutoka katika kampuni ndogo kwenda za kati na za kati kuwa kubwa.

Amesema pia TPSF itaitumia fursa hiyo kutangaza kwa wageni fursa za uwekezaji zilizopo nchini.

“Mkutano huo pia utafungua milango ya biashara sababu tunatarajia wageni zaidi ya 200 kutoka nje, watahitaji malazi, chakula na hata bidhaa nyingine za ndani. Pia tutawaomba wahudhurie katika maonyesho ya bidhaa za Tanzania yatakayoanza Disemba 7 hadi 11, 2016 ili wajionee bidhaa zinazozalishwa nchini,” amesema.

Simbeye amesema kuwa, tafiti iliyofanywa na serikali mwaka 2013 na kuchapishwa mwaka huu inaonyesha kuwa kuna viwanda 49,000 ambapo 20,000 ni viwanda vikubwa.

“Uchumi wa Tanzania utajengwa na viwanda hasa vidogo ambavyo vitaongeza idadi ya kampuni ndogo nchini, nchi inapokuwa na kampuni nyingi fursa za kiuchumi pia huongezeka sababu zinaajiri watu. Taasisi ya Sekta Binafsi itaendelea kutangaza fursa za biashara na uwekezaji zilizomo nchini,” amesema.

Askari 152 Wafukuzwa Kazi.

$
0
0
Jumla ya askari 152 wamefukuzwa kazi mwaka huu na Jeshi la Polisi kwa sababu ya kukiuka Sheria, Taratibu na Kanuni ya Jeshi hilo kama zilivyoainishwa katika Kanuni za Kudumu za Polisi (PGO) namba 103.

Idadi ya askari hao waliofukuzwa kazi imetolewa jana mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Maryam Msabaha aliyehitaji kufahamu juu ya idadi ya askari waliochukuliwa hatua kwa sababu ya utovu wa nidhamu.

Mhandisi Masauni alisema kuwa kazi ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni kulinda raia, mali zao pamoja na mipaka ya nchi lakini kuna baadhi ya askari hao wanakwenda kinyume na Sheria kwa kuwapiga wananchi na kuwasababishia ulemavu pamoja na vifo hivyo Jeshi hilo limewachukulia hatua za kinidhamu.

“Jeshi la Polisi hufanya kazi kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo lakini kuna baadhi ya askari wamekuwa wakikiuka maadili na mwenendo mwema wa Jeshi letu hivyo kuanzia Januari 2015 hadi Juni 2016 tuliwachukulia hatua za kinidhamu askari 200”, alisema Mhandisi Masauni.

Naibu Waziri huyo alifafanua kuwa baada ya askari hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu, walifanyiwa uchunguzi wa kina na jumla ya askari 152 kati ya 200 walikutwa na hatia hivyo hatua iliyofata ni kuwafukuza kazi.

Akizungumzia kuhusu mpango wa Serikali juu ya kujenga nyumba za askari Polisi, Mhandisi Masauni alisema kuwa wanatambua tatizo la makazi ya Askari Polisi katika maeneo mbalimbali nchini hususani kwenye mikoa mipya hivyo Serikali ina nia ya kutatua tatizo hilo kwa kuanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya askari hao.

“Serikali imedhamiria kupunguza tatizo la upungufu wa makazi ya askari polisi kwa kujenga nyumba kwa awamu kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba 4,136 nchi nzima ambao utaanza kutekelezwa baada ya taratibu za mkopo wa kuwezesha ujenzi huu kukamilika”, aliongeza Mhandisi Masauni.

Kauli Ya mwisho ya Samwel Sitta Baada ya Daktari kumueleza kuwa Asingeweza Kupona

$
0
0

Kufuatia kifo cha aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanza nia (2005-2010), Samuel Sitta, mwanae wa kiume ameweka wazi maneno matatu ya mwisho aliyoyatamka, yenye maana nzito katika maisha.

Akizungumza nyumbani kwa marehemu, Meya wa Kinondoni, Benjamini Sitta ambaye ni mtoto wa kiume wa marehemu, alisema kuwa baba yake alitoa maneno matatu ya kuukubali ukweli wa maisha baada ya Daktari kumueleza kuwa asingeweza kupona.

“That’s life (hayo ndiyo maisha),” Benjamin alikariri maneno ya baba yake. Alisema hayo yalikuwa maneno yake ya mwisho baada ya kuelezwa ukweli na daktari wa hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Maneo ya Sitta ni funzo kubwa kwa watu wote kuwa maisha huanza na huisha, hiyo ndiyo maana ya maisha na hakuna aishie milele hivyo tuishi kwa kuzingatia maana hiyo ya maisha na kuikubali.

Sitta ambaye anakumbukwa kwa kauli mbiu yake na matendo ya kusimamia ‘kasi na viwango’, alifariki kutokana na ugonjwa wa tezi dume uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu.

Alitangaza kustaafu siasa muda mfupi baada ya kukamilika kwa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo yeye alikuwa mmoja kati ya waliokuwa msitari wa mbele kumnadi mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi, Dkt. John Magufuli aliyeshinda uchaguzi huo.

Benjamini alieleza kuwa marehemu atazikwa Urambo Mkoani Tabora na kwamba ratiba ya mazishi itatolewa na Ofisi ya Bunge ambayo ndiyo inayoratibu mazishi

“Tumempoteza baba na kiongozi ambaye tulikuwa tunamtegemea kwa ushauri na masuala mbalimbali, tutafuata yale aliyokuwa akituelekeza,” alisema Benjamini.

Hakika Taifa limempoteza mtu muhimu, pengo lake halitazibika kamwe. Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe!

Chadema watinga Mahakama Kuu kutaka Lema ashtakiwe

$
0
0

Chama Cha Demokrasia na Meendeleo (Chadema), jana kilifungua kesi Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, wakipinga kitendo cha Jeshi la Polisi kumuweka rumande mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kwa zaidi ya saa 175 bila kumpeleka Mahakamani.

Mwanasheria wa chama hicho, John Mallya jana aliwaambia waandishi wa habari katika viwanja vya mahakama hiyo kuwa wamefungua kesi hiyo kwakuwa sheria inaelekeza mtuhumiwa kutozidi saa 24 mahabusu bila kufikishwa mahakamani, hivyo kitendo cha kumshikilia Lema kwa zaidi ya muda huo ni kinyume cha sheria.

Katika kesi hiyo, chama hicho kimeiomba Mahakama kuwaamuru Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Polisi wa Arusha na Mkuu wa kituo cha Arusha (Central) kumpeleka mahakamani mbunge huyo.

Mallya aliongeza kuwa anakamilisha mchakato wa kukusanya hati ya wito wa kuitwa mahakamani kwa vigogo wa Polisi pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili waweze kueleza ni kwanini wamekiuka masharti ya kisheria ya kutomshikilia mtu kwa zaidi ya saa 24 bila kumfikisha mahakamani.

“Tunataka hawa tuliowashtaki kumleta Lema mahakamani na dhamana yake ifanyiwe mchakato Mahakama Kuu na waiambie mahakama kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria, pia tumeomba gharama zote za hii kesi zilipwe na Serikali,” Mallya aliwaambia waandishi wa habari.

Lema alikamatwa Jumatano iliyopita akiwa Bungeni mjini Dodoma na kusafirishwa hadi jijini Arusha kwa tuhuma za kutoa maneno ya kichochezi dhidi ya Rais John Magufuli.

Tanesco yaomba kupandisha bei ya umeme kwa Asilimia 18

$
0
0

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imepokea maombi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) ya kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 18.19 kuanzia mwaka ujao.

Taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) imeeleza kuwa Oktoba 4, mamlaka hiyo ilipokea ombi la mabadiliko ya bei ya umeme, hivyo unaandaliwa mkakati wa kukusanya maoni ya wadau wa nishati hiyo.

“Mikutano ya ukusanyaji maoni kuhusu bei inayopendekezwa na Tanesco itaanza Novemba 16 katika mikoa ya Mwanza, Mbeya, Arusha, Dodoma  na kwa Dar es Salaam ni Novemba 23,” inaeleza taarifa hiyo.

Aprili mwaka huu, Tanesco ilituma maombi kwa Ewura ya kupunguza gharama za umeme kwa asilimia 1.1, lakini baada ya mamlaka hiyo kupitia maombi hayo, ilipunguza gharama hizo kwa asilimia 1.5 hadi 2.4.

Bei ya sasa baada ya punguzo hilo la Ewura kwa wateja wa shirika hilo, kutoka kundi la D1 wanaotumia kiasi cha umeme kuanzia kilowati 0 hadi 75 ni Sh 100 na zaidi ya kilowati 75 kwa mwezi wanatozwa Sh 350 kwa uniti moja.

Aidha, kwa wateja wa kundi la T1 ambao ni kuanzia majumbani, viwandani na biashara ndogo ndogo hutozwa kiasi cha Sh 292 kwa uniti moja na kwa wateja wa kundi T2 ambalo ni kundi linalotumia umeme kuanzia kilowati 7,500 hutozwa kwa wastani wa Sh 15,004 kwa mwezi kwa uniti moja.

Kwa makundi ya T3 na T4 wanaotumia umeme mkubwa kama vile kwenye machimbo, viwanda vikubwa na Mamlaka ya Umeme Zanzibar (ZECO) yenyewe hutozwa kiasi cha Sh 13,200 hadi 16,550 kwa mwezi kwa uniti moja.

Hata hivyo, kutokana na ombi hilo la ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, sasa wateja wa kawaida wanaotumia umeme kuanzia kilowati hadi 75 watakuwa na ongezeko la Sh 18 ambapo endapo ombi hilo likiridhiwa watatozwa Sh 118 kwa uniti moja.

Aidha, kwa wateja wanaonunua umeme zaidi ya kilowati 75 ambao kwa sasa wanatozwa Sh 350 kwa uniti moja, endapo ombi hilo likipitishwa watakuwa na ongezeko la bei la Sh 63 hivyo watatozwa kiasi cha Sh 413 kwa uniti moja.

Kwa upande wa wateja wa kundi la T1 ambao ni kuanzia majumbani, viwandani na biashara ndogo ndogo wanaotozwa kwa sasa kiasi cha Sh 292, watakuwa na ongezeko la Sh 52.56 hivyo endapo ombi hilo litaridhiwa bei hiyo itapanda na kufikia Sh 344.56 kwa uniti moja.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Ewura, Titus Kaguo pamoja na kuthibitisha mamlaka hiyo kupokea maombi hayo, alisisitiza kuwa bado ombi hilo linachambuliwa na kufanyiwa tathmini na mamlaka hiyo kabla ya kuidhinishwa.

Taarifa Muhimu toka Benki ya Twiga Bancorp

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 37 & 38

$
0
0

Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA      
“Detener inmediatemente”(Simamisha hapo hapo)
Frednando alizungumza kwa sauti ya juu na kumfanya muongozaji wa video hiyo kusimamisha sehemu inayo muoenyesha Mercy akimkumbatia Rahab kwa furaha. Mercy akajikuta akiitumbualia macho sehemu hiyo iliyo simamishwa huku mapigo ya moyo yakimuenda kasi sana.

ENDELEA  
Kila mmoja aliweza kulishuhudia tendo la Mercy kumimini kiasi cha unga unga mweupe kwenye kinywaji alicho kishika Rahab, pasipo watu wengine kuweza kumuona wakati wa sherehe hiyo kuweza kufanyika. Walio na roho nyepesi wakajikuta wakimaka kwa sauti ya juu, Mercy baada ya kuona kwamba ameweza kugundulika kwa haraka, akapandisha juu gorofani na kuingia chumbani kwake kwani anagundua kinacho kwenda kutokea ndani ya masaa machache mbeleni hakitakuwa ni kizuri kwani anautambua vizuri ukatili wa bosi wake.

Mercy akafungua kabati lake na kutoa begi dogo la mgongoni na kuanza kuingiza kiasi cha pesa alicho kuwa amekihifadho ndani ya kabati hilo kisha kwa haraka akafungua dirisha na kusimama, kabla hajafanuya chochote mlango wake ukapigwa na teke wakaingia walinzi wawili wa Frednando wakiwa na bunduki mikononi mwao

                                                                                           ***
Hali ya Fetty na wezake, zikazzidi kushuhulikiwa na madaktari bingwa waliomo ndnai ya ngome ya bwana Rusev, komandoo wa nchi ya Rusev aliye weza kuisaliti nchi yake na kuunda kikosi chake alicho kipa jina la R.U.P.P(Rusev United Power of People). Kikundi hichi aliweza kukianzisha kwa siri kubwa tangu akiwa ndani ya jeshi pasipo watu wengine kuweza kukifahamu kwa haraka.

Akaweza kutengeneza kambi yake chini ya bahari kaskazini mwa nchi yake ya Urusi, haya yote aliweza kutafanya kwa siri kubwa akishirikia na baadhi ya viongozi wa juu serikalini walio kuwa na uchu mkubwa wa madaraka. Mbaya zaidi ni kwamba viongozi hao walitaka kumgeuka, ila kwa kutumia umahiri wake aliweza kuwaangamiza kwa mkono wake mwenyewe kuhakikisha kwamba siri yake haiwezi kuvuja kwa mtu wa ina yoyote kwamba yeye anamiliki jeshi kubwa la vijana kinyume na sheria za nchi yake..

R.U.P.P, ikazidi kukua miaka kwa miaka na kuzidi kupata wataalamu wakubwa wa mitambo na kuanza kutengeneza silaha za nyuklia kisiri sana.
Ndani ya miaka ishirini ya usiri, siku moja bwana Rusev aliweza kuja kujikuta siri yake ya kuwa ni muasi ndani ya nchi yake ikagundulika, hii ni baada ya siku hiyo kunywa kiasi kikubwa sana cha pombe na kujikuta akilala ma malaya mmoja aliye weza kumpa penzi tamu, hadi akajikuta akianza kumuambia mambo yake ya ndani huku akimuahidi kumpa nafasi ya kuweza kufanya naye kazi.

Binti huyo pasipo kuwa mvumilivu akajikuta akijinadi kwa rafiki zake, juu ya kupata nafasi ya kuajiriwa na bwana Rusev katika kikosi chake cha siri cha R.U.P.P, hii ni mara baada ya binti huyo kutoka kulala na bwana Rusev ambaye kwa kipindi hicho bado alikuwa ndani ya jeshi la nchi ya Rusia.     

     Bwana rusev hakuwa na jinsi zaidi ya kuamua kuiasi nchi yake mara baada ya serikali kuanza kumfwatilia na kumuwekea vikwazo vingia hadi kutaka kumuhukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa, ila haikuwa ni rahisi  kwa serikali, kwnai watu wa bwana Rusev waliweza kumtorosha kiongozi wao huyo walio muabudu kama Mungu wao, na kuweza kumuweka katika mazingira salama ambayo ni ngumu sana kwa mtu yoyote kuweza kumfikia na kumdhuru.
“Jamani tupo wapi?”

Anna alikuwa wa kwanza kuzungumza mara baada ya kuzinduka kutoka usingizini. Akashangaa eneo zima la chumba kikubwa walicho lazwa na kilicho tawaliwa na rangi nyeupe kwenye kuta zake kuanzia chini, pembeni hadi juu. Akawatazama wezake na kuwakuta bado wakiwa wamejilaza kitandani, huku wakiwa na madripu ya maji. Anna akajitazama na yeye na kujikuta akiwa na dripu kwenye mkono wake wa kushoto, nguo walizo kuwa wamezivaa mara ya mwisho hawakujikuta nazo, alijishuhudia akiwa amevishwa mavazi meupe yanayo fanana na wezake.
Baada ya muda kila mmoja akazinduka na wote wanne wakajikuta wakipiwa katika hali ya kuto fahamu ni kitu gani ambacho kinaendelea katika eneo walilo kumbuka.

“Jamani hapa tulipo tunaonekana kila kona”
Fetty alizungumza baada ya kuzitazama kamera za ulinzi zilizo kuwa katika kona nne za chumba walichomo.
“Sasa kamani tutafanyaje, kwa mana hapa mimi sielewi?”
Halima aliuliza akiendelea kuyapepesa macho yake
“Kikubwa tuweni wapole, kwa maana kama hawa watu wangekuwa ni wabaya kwetu wanegesha tuu, ila wemeweza kutuhudumia hadi hapa”
Fetty aliwasisitiza wezake, kabla Agnes hajazungumza, bwana Rusev akaingia huku akiwa ameongozana na walinzi wake wawili pamoja na daktari mmoja, mwenye umri mkubwa kiasi.

“Munaendeleaje mabinti”
Bwana Rusev alizungumza kiswahili fasaha kilicho wafanya wote wanne kushangaa na kumtumbilia macho kwani siku zote walikuwa wanajua kwamba mzee huyo atambui kishwahili
“Munanishangaa mimi kuzungumza kishwahili? Ok tuachane na hayo, kama munavyo weza kujionea mupo katika mikono salama sana, na kwaupande mwingine pia si salama”
Fetty na wezake wakatazama kwa macho yakujiiuliza ni kwanini Bwana Rusev anasema sehemu hiyo ni salama ama si Salama, hapakuwa na aliye kuwa na jibu la kuzungumza kwa mwenzake zaidi ya kukaa kimya kusubiri ni kitu gani ambacho bwana Rusev atazungumza.

“Natambua kwamba nyinyi ni miongoni mwa mabinti mahiri mulio weza kufanya matukio kadhaa kwenye nchi ya Tanzania, na pia hadi sasa hivi bado munaendelea kutafutwa si ndio?”
Anna akajibu kwa kutingisha kichwa akikubali kwamba ni kweli bado wanatafutwa
“Sawa sasa ni hivi, nawapa uchaguzi wa haya nitakayo kwenda kuyazungumza. Kwanza mukikubali kuwa na mimi nitawapa nafasi kubwa ya kuyatambua mambo mengi ambayo hamjawahi kuyajua. Pili mukikataa kuwa na mimi miili yenu itakuwa ni chakula cha papa walio zunguka eneo hili.”

Zitto Kabwe: Sitasahau maneno aliyoniambia Samwel Sitta

$
0
0
Alfajiri ya tarehe 7 Novemba 2016, tunaamka na kukutana na habari za kusikitisha kuwa Mzee Samwel John Sitta, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangulia mbele ya haki. Babu alikuwa mgonjwa kwa kitambo kidogo akisumbuliwa na saratani ya tezi dume.

Majonzi ni makubwa kwa Taifa kutokana na sababu kubwa kwamba Samwel John Sitta alitumikia nchi yetu kwa muda mrefu na kwa uadilifu mkubwa.

Sisi wengine pia kwa kiasi fulani kukua kwetu kisiasa kumetokana na utumishi wake uliotukuka kwa nchi yetu alipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika tanzia hii ninamkumbuka Mzee Sitta Kwa namna nilivyofahamiana naye binafsi na namna nilivyomshuhudia katika kazi zake.

Sitta ananigusa mimi binafsi moja kwa moja. Alikuwa babu yangu. Tukiwa bungeni akiniandikia kitu alikuwa akitumia neno hilo “babu” kwa mwandiko wake mzuri usiotoka kwenye kumbukumbu zangu kabisa.

Aliniapisha kiapo cha ubunge Desemba 29, 2005. Maneno ambayo aliniambia baada ya kunikabidhi Kanuni za Bunge na Katiba ya Nchi niliyaandika kwenye daftari langu la kumbukumbu siku hiyo hiyo jioni.

Baada ya kula kiapo cha utii na cha uaminifu kawaida wabunge hupewa mkono na mwapishaji na kupewa nyaraka za kazi. Kwa upande wangu Mzee Sitta alinikumbatia na kuniambia, “utakuwa kiongozi muhimu sana kwa nchi yetu. You have a bright future.”

Maneno haya hayajawahi kutoka katika kumbukumbu zangu na kila nikipata misukosuko yangu kisiasa huyakumbuka na wakati mwingine yeye mwenyewe alikuwa akinipigia na kunikumbusha na kunitia moyo. Babu alikuwa mlezi wa wanasiasa vijana.

Sitta pia amenilea kwa kunisomesha. Mwaka 1996 nilikuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Galanos jijini Tanga nikisomea mchepuo wa Historia, Jiografia na Uchumi (HGE).

Hali ya hewa ya Tanga haikunipenda, hivyo nikawa naumwaumwa sana. Pia nilitaka kusoma Hesabu badala ya Historia. Wakati wa likizo ya Desemba mwaka 1996, nilitoka Tanga nikaenda Dar es Salaam, Wizara ya Elimu kuomba uhamisho kwenda shule yenye Somo la Hesabu, kidato cha Tano na Sita. Nikakataliwa. Lakini nikaambiwa kuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari wakati huo Bwana Ndeki alisoma na Samwel Sitta.

Kipindi hicho Mzee Sitta akiwa Mkurugenzi wa Investments Promotion Centre (IPC) kabla haijabadilishwa jina kuwa Tanzania Investments Centre (TIC). Nikaenda Ofisi za IPC mahali ambapo leo ni CRDB Tawi la Azikiwe.

Nilipofika Katibu Muhtasi wake akaniuliza kama nina miadi na bosi wake, nikasema hapana. Akaniambia hawezi kukuona. Nikasisitiza sana na kumlilia dada yule aniruhusu dakika chache tu. Akaniruhusu.

Nilipofika Mzee Sitta aliniuliza shida zangu kwa heshima kubwa. Nikamwambia kwamba ninataka kuhama shule. Akaniomba matokeo yangu ya Kidato cha Nne, nikampa maana nilikuwa natembea nayo. Alipoyasoma akaniambia, “wewe hupaswi kuhangaika kutafuta shule maana kwa matokeo yako unaweza kusoma shule yoyote nchini ya chaguo lako”. Akainua simu akampigia Bwana Ndeki. Kisha akaniandikia kikaratasi niende wizarani muda uleule. Nilipofika wizarani nikapewa uhamisho kwenda Shule ya Sekondari Mazengo.

Nilipotoka nje ya wizara nikakutana na kijana mwingine anaomba uhamisho, yeye anatoka Mazengo anataka kwenda Tosamaganga, Iringa. Akaniambia, achana na Mazengo hakuna mwalimu wa Uchumi na hali ya vyoo ni mbaya sana. Nikarudi kwa Mkurugenzi. Mzee aliyenipa uhamisho aliponiona narudi na kumwambia sitaki Mazengo akachukua fomu zangu za uhamisho na akachukua ‘whiteout’ akafuta Mazengo na kuweka Tosamaganga huku akisema kwa hasira “ nyie watoto wa wakubwa bwana”. Sikujali nikaenda zangu Tosamaganga kusoma Economics, Geography na Mathematics (EGM).

Sitta akaendelea kufuatilia maendeleo yangu shuleni na baadaye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Taasisi ya InWent nchini Ujerumani.

Nilipotoka Ujerumani kusoma masomo ya Juu ya Biashara ya Kimataifa mwaka 2004 ilipaswa niwe na mradi wa kitaaluma. Nikachagua kuunganisha kampuni za Kijerumani na Tanzania kwa kuandika mradi wa kuchukua wafanyabiashiara 20 kutoka Tanzania na kuwaunganisha na wengine 20 kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya.

Ilibidi kupata Taasisi ya Tanzania kwa ajili mradi huo na Mzee Sitta akawa mstari wa mbele kuhakikisha mradi unafanikiwa na tukautekeleza kwa umakini kwa msaada wa ofisa wa TIC aitwaye Phina Lyimo.

Mwaka mmoja baadaye tukakutana na Mzee Sitta bungeni, yeye akiwa Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki na mimi nikiwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Ulezi wake ukaendelea mpaka mauti yalipomkuta leo mapema asubuhi (jana). Nimempoteza babu mlezi.

Sitta alikuwa mwana mageuzi (reformer) na kupitia uanamageuzi wake alifanya mabadiliko makubwa sana katika uendeshaji wa shughuli za Bunge. Sisi tuliohudumu kwenye Bunge la Tisa, tukimwita Spika wa Viwango na Kasi, tuliona wenyewe juhudi zake za kuliweka Bunge katika nafasi yake ya Kikatiba. Licha ya kuhakikisha kuwa maslahi ya Wabunge yanalingana na hadhi ya Bunge, alihakikisha pia kuwa Bunge linaisimamia Serikali sawa sawa. Haikuwa kazi rahisi sana kwani kulikuwa na mvutano mkubwa sana kati ya Spika Sitta na Waziri Mkuu Edward Lowasa katika kuleta mabadiliko hayo.

Tulikuwa tunaambiwa kuwa mvutano huo ulitokana na tetesi kwamba Sitta ndiye alipaswa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na hivyo kuwa na msuguano na aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo. Si Sitta wala Lowasa ambaye alithibitisha ama kukanusha tetesi hizo. Sitta ametangulia mbele ya haki, labda Edward Lowasa ataweza kusemea hili siku za usoni.

Sitta alitumia fursa ya msuguano huo kufanya mabadiliko makubwa ya kanuni za Bunge na kutoa uhuru mpana wa mawazo ndani ya Bunge na kuhakikisha kuwa taarifa za Kamati za Bunge na hususani Kamati za Usimamizi wa Serikali zinasomwa na kujadiliwa ndani ya Bunge kwa mujibu wa Kanuni.

Wakati wa Bunge la Nane, Taarifa za CAG hazikuwahi kusomwa hata mara moja. Ni kutokana na mabadiliko haya ya kanuni ndipo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (Poac ) ilianzishwa Machi, mwaka 2008.

Nilichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa kwanza wa kamati hiyo na kuingia kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge ambayo kipindi hicho tuliiona kama kamati ya wabunge wazee. Namna nilivyoingia kuwa Mwenyekiti wa Poac nayo ni hadithi nyingine ya namna ya malezi ya kiuongozi yaliyofanywa na Spika Sitta.

Sikuwa nimejaza fomu kuomba Kamati ya Poac. Wakati huo ulikuwa ni wakati wa vuguvugu la Buzwagi (Mkataba wa Madini uliosainiwa na Waziri wa Nishati hotelini nchini Uingereza kwa siri ). Nilikuwa mjini Bagamoyo kwenye kazi za Kamati ya Bomani nikiwa na Harrison Mwakyembe na Ezekiel Maige.

Spika wa Bunge akanipigia simu, akaniambia “Babu, kesho kuna uchaguzi wa Kamati za Bunge. Nimekuteua Kamati ya Poac ambayo ni kamati mpya itakayokuwa chini ya Kambi ya Upinzani. Najua hukuomba kuwa mjumbe wa kamati hii, lakini nahitaji damu changa kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge. Naomba unikubalie na kesho uwepo Dar es Salaam kwa ajili ya uchaguzi na ugombee. Utashinda maana nimeshafanya kazi yangu”. Sikuwa na namna ya kukataa japo nilitaka sana kuendelea kuwa Kamati ya Fedha na Uchumi chini ya Abdallah Kigoda, ama Kamati ya Nishati na Madini chini ya Mzee William Shelukindo.

Ombi la Mzee ni amri. Nikawa Mwenyektii wa Poac na kuwa mmoja wa washauri wakuu wa Spika wa Bunge. Kamati ya PAC ikawa chini ya Mzee John Cheyo na Kamati ya Laac ikawa chini ya Dk Wilibrod Slaa. Ilikuwa ni Bunge lenye meno kweli kweli.

Spika Sitta alikuwa mbabe. Ubabe wake ulimsababisha kufanya maamuzi ambayo wakati mwingine yalimweka kwenye matatizo na wananchi. Mfano mzuri ni suala la Hoja Binafsi ya Buzwagi na Hoja ya Wizi wa Fedha Benki Kuu ( Epa). Mwanzoni, Spika alikuwa upande wa wabunge wenye hoja hiyo yaani mimi na Dk Slaa kiasi cha kuziboresha hoja zile kwa kalamu yake mwenyewe. Wabunge wa chama chake hawakuwa wanapenda hoja hizi na hivyo Waziri Mkuu Lowasa akamweka kwenye wakati mgumu sana wa kuegemea upande wa Serikali. Hoja ya Dk Slaa akaitupa kuwa ‘ ni makaratasi ya kuokoteza’. Hoja yangu akaiingiza bungeni na akasimamia kusimamishwa kwangu bungeni. Wananchi walimkasirikia sana.

Siku moja usiku, nikiwa nyumbani kwa Freeman Mbowe Mikocheni, Sitta akanipigia simu kulalamika kuwa wafuasi wangu wanamtukana kwa meseji. Akaniambia niwakataze. Nilimkubalia tu, lakini sikuwa na uwezo huo. Nchi ilikuwa imevimba. Ilikuwa Oktoba 2007, Sitta alijua namna ya kusoma nchi na kuwapa watakacho, wakati mwingine. Mwezi Novemba, katika kujibu kiu ya wananchi kuhusu uwajibikaji na kufuta makosa ya Buzwagi na Epa, Spika alisimamia kuundwa kwa Kamati Teule kuchunguza suala la Mkataba wa Richmond. Yaliyofuata yalikuwa historia. Taarifa ya Kamati Teule ilisababisha ‘kuanguka’ kwa Serikali kwa mara ya kwanza katika hsitoria ya Tanzania, Waziri Mkuu Lowasa alilazimika kujiuzulu ndani ya Bunge, Baraza la Mawaziri likavunjika na Serikali mpya kuundwa chini ya Mizengo Kayanza Pinda.

Spika Samwel Sitta akawa ni Spika pekee wa nchi yetu aliyeshuhudia uundwaji wa Serikali mbili ndani ya miaka mitano ya uspika wake. Mzee Msekwa yeye alikaa miaka 10 na Waziri Mkuu mmoja, ingawa mwaka 1993-1995 naye aliona mabadiliko ya mawaziri wakuu, kutoka John Malecela kwenda kwa Cleopa Msuya. Baada ya kujiuzulu kwa Lowasa, Samwel Sitta hakurudi nyuma tena. Aliendelea kuwa Spika wa Viwango mpaka alipomaliza muda wake katika Bunge la Tisa.

Spika Sitta alikuwa mwepesi kuomba msamaha alipokosea. Nakumbuka siku moja mwaka 2009 alimfukuza bungeni mzee mwenzake John Cheyo kwa makosa ambayo Cheyo hakufanya. Baadhi yetu tukakasirishwa sana na kitendo kile. Nikaenda kumwona Mzee Sitta ofisini kumwuliza kulikoni amdhalilishe mwenzake namna ile. Akanieleza kuwa hakuwa sawa na atamwomba radhi John Cheyo. Tukiwa kwenye Kamati ya Uongozi ya Bunge kwa ajenda za kawaida tu, Mzee Sitta akamwomba radhi Mzee Cheyo.

Nikikumbuka kisa hiki nacheka sana maana Jaji Werema aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali alicheka mpaka kuanguka chini. Sababu? Mzee Sitta aliketi kwenye kiti chake, wenyeviti wote wa kamati tukiwa tumetulia tuanze kikao. Mzee Sitta akasema, “John, naomba radhi kwa tukio lililotokea bungeni wiki iliyopita. Sijui nilikuwa nina nini siku hiyo, nadhani nilisumbuliwa na watu wanaopitapita jimboni kutaka kunitoa, nisamehe mzee mwenzangu”. Kicheko ukumbi mzima na Cheyo akamkubalia radhi yake huku naye akicheka na yakaishia hapo. Wazee hawa wawili wameandika pamoja kitabu, ‘Bunge lenye Meno.’

Nimwelezeje zaidi Babu? Nimwelezeje zaidi Spika wa Kasi na Viwango Samwel Sitta? Mwanasiasa shupavu, jasiri, mwenye ngozi ngumu, mbabe, mnyeyekevu inapobidi na mwenye uthubutu. Tangulia Babu. Tangulia Mtemi wa Unyanyembe Samwel John Sitta. Umeondoka duniani lakini bado unaishi kupitia kazi zako kwa nchi yetu.

Mwandishi wa makala haya ni Kiongozi wa ACT- Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini.

Godbless Lema Afikishwa Mahakamani.......Arudishwa Rumande Baada ya Kunyimwa Dhamana

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema leo amefikishwa mahakamani mkoani Arusha na kusomewa shtaka la uchochezi kwa viongozi wa serikali.

Lema amefikishwa leo mahakamani akiwa tayari amekaa rumande takribani siku 7 tangu alipokamatwa.

Lema anakabiliwa na shtaka la uchochezi ambapo ni pamoja na kumtishia Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo na kauli yake aliyoitoa dhidi ya Rais Dkt Magufuli kuwa Mungu amemuonyesha asipojirekebisha atafariki.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Lema amerejeshwa rumande baada ya kukosa dhamana kufuatia pingamizi lililowekwa na upande wa Jamhuri.

Mahakama imeeleza kuwa itatoa uamuzi kuhusu dhamana ya Lema Novemba 11 mwaka huu.

Rais Magufuli atuma salamu za Rambirambi vifo vya watu 18 Shinyanga na Vifo vya viongozi Zanzibar

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bi. Zainabu Telack kufuatia vifo vya watu 18 vilivyosababishwa na ajali ya barabarani katika kijiji cha Salala Kilichopo katika Wilaya ya Shinyanga Vijijini Mkoani Shinyanga tarehe 06 Novemba, 2016.
 
Ajali hiyo ilitokea Majira ya saa moja jioni baada ya gari dogo aina ya Noah lililokuwa limebeba abiria 21 kugongana uso kwa uso na lori na kusababisha vifo vya watu 18 na wengine 3 kujeruhiwa.
 
Katika salamu hizo Rais Magufuli ameelezea kusikitishwa na ajali za barabarani zinazoendelea kutokea na ametaka vyombo vinavyohusika na wadau wa usalama barabarani kushirikiana kukabiliana na ajali hizo.
 
"Ni jambo linaloumiza na kusikitisha sana kupoteza idadi kubwa ya watu namna hii, nakuomba Ndugu Mkuu wa Mkoa Shinyanga Bi. Zainab Telack unifikishie pole nyingi kwa familia za Marehemu wote, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza jamaa zao na uwaambie tupo pamoja katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo" amesema Rais Magufuli.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kufuatia kifo cha Mwenyekiti Mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jaji Zubeir Juma Mzee kilichotokea jana tarehe 07 Novemba, 2016 Mjini Unguja.
 
Sambamba na salamu hizo, Rais Magufuli pia amemtumia salamu za rambirambi Dkt. Shein ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kufuatia kifo cha Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndugu Saleh Ramadhan Ferouz kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 08 Novemba, 2016 Mjini Unguja.
 
"Mhe. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein, nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za viongozi wetu wastaafu waliotangulia mbele za haki hapo jana, tutawakumbuka kwa mchango wao mkubwa kwa Zanzibar na Taifa letu kwa ujumla kwa kuwa katika kipindi chao cha uongozi walijitahidi kutimiza wajibu wao na kuleta manufaa kwa Taifa" amesema Rais Magufuli.
 
Rais Magufuli amewaombea marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi. Amina

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
08 Novemba, 2016

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya Lawafukuza Kazi Askari Wawili Kwa Kuwadhalilisha Wanafunzi wa Kike

$
0
0
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linaendelea na shughuli zake za kila siku ili kuhakikisha mkoa unakuwa salama hii ni kutokana na wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili kuweza kuwabaini wahalifu wanaofanya vitendo vya uhalifu ili mkoa wetu uwe salama. 

Hata kuanzia tarehe 01.11.2016 Jeshi la Polisi lilianza zoezi la ulinzi wa Mitihani ya Kitaifa ya kuhitimu kidato cha nne 2016 katika Shule mbalimbali za mkoa wa mbeya. Hata hivyo katika zoezi hilo linaloendelea la ulinzi wa mitihani kuna changamoto zilijitokeza:-

KUFANYA KITENDO KIBAYA KINYUME NA MAADILI.
Mnamo tarehe 04.11.2016 majira ya saa 23:30 usiku huko katika Shule ya Sekondari Isuto iliyopo Kijiji na Kata ya Isuto, Tarafa ya Isangati, Wilaya ya Kipolisi Mbalizi, Mkoa wa Mbeya, askari wawili wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya waliofahamika kwa majina ya 1. H.4925 PC PETRO OSCAR MAGANA wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya na 2. J.1422 PC LUKAS JOSEPH NG’WEINA wa Wilaya ya Kipolisi Mbalizi walituhumiwa kuwafanyia vitendo vibaya kinyume na maadili wanafunzi wa kike wa kidato cha nne wa Shule hiyo.

Inadaiwa kuwa, askari hao kwa pamoja wakiwa kwenye ulinzi wa mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne 2016 waliwatoa kwenye Hostel wanafunzi wa kike kwa kile walichodai kupiga kelele.

Baada ya kuwatoa wanafunzi hao, waliwapeleka eneo la kufoleni na kuanza kuwapa adhabu mbalimbali ambazo ni kupiga push up, kuruka kichura, kushika masikio na kuwachapa viboko sehemu za makalio vitendo vilivyowasababishia maumivu makali na kupelekea baadhi ya wanafunzi hao wa kike kuondoa na kuelekea nyumbani kwao.

Kufuatia vitendo hivyo, Mkuu wa Shule hiyo aitwaye ROSE MZEE DIHEMBE alitoa taarifa kwa uongozi wa Wilaya ambapo taarifa zilifika kwa uongozi wa Mkoa ambao mara moja walifika eneo la tukio na kuchukua hatua za awali ikiwemo kusikiliza malalamikio hayo ya tukio na kuwaondoa askari waliolalamikiwa na mwisho kuchukua hatua za kinidhamu zilizopelekea kufukuzwa kazi askari hao.

Hata hivyo, kutokana na vitendo walivyovifanya askari hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya uchunguzi kukamilika.

WITO:
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Naibu Kamishna wa Polisi DHAHIRI A. KIDAVASHARI anatoa wito wananchi waendelee kuliamini Jeshi la Polisi kwamba halitafumbia macho vitendo vya askari vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi yao. Pia vitendo vinavyokwenda kinyume na sheria za nchi. 

Aidha Kamanda KIDAVASHARI anaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa ya vitendo vyote vya uhalifu vinavyotendwa bila kujali vinatendwa na askari au wananchi wa kawaida ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.

Imesainiwa na:

[DHAHIRI A. KIDAVASHARI – DCP]

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

BUNGENI: Serikali Yaitaka sekta binafsi kuwekeza katika kinywaji aina Gongo ili kurasimisha kinywaji hicho

$
0
0

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amezishauri kampuni zinazotengeneza vilevi kutengeneza pombe yenye ladha ya gongo, kwa kuwa  baadhi ya wateja wanavutiwa na ladha hiyo wana wanakipenda kinywaji hicho.

Mwijage ameyasema hayo leo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Gimbi Masaba (Chadema) aliyehoji mpango wa serikali wa kuanzisha na kuhalalisha viwanda vya kutengeneza pombe aina ya gongo ili kuchochea uchumi wa nchi na kubainisha kuwa, gongo ikitengenezwa kiwandani itafuata ubora unaotakiwa kisheria.

“Moja ya kigezo muhimu cha kuanzisha kiwanda ni uwepo wa soko, kutokana na wananchi kupenda kinywaji hiki(gongo) nawashauri wadau wa sekta hii kuwasiliana na ofisi za Sido ambazo zinapatikana mikoa yote ili kupata muongozo juu ya uanzishaji wa viwanda bora na salama vya aina hii,” alisema Mwijage.

Amesema haiwezekani Serikali kuhalalisha gongo, ila inaishauri sekta binafsi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi zinazotengeneza kinywaji hicho kwa lengo la kuzalisha kinywaji kinachokidhi viwango vya usalama na ubora wa chakula.

Katika swali la nyongeza, Masaba amehoji kama serikali ipo tayari kufanya utafiti kujua faida zilizo kwenye gongo.

Mwijage amesema faida zinafahamika, lakini atawaelekeza wataalamu wake waendele maeneo yenye gongo na pombe nyingine za kienyeji ili kuzifanyia utafiti na zitengenezwe kwa kufuata ubora na viwango.

Wabunge waridhia msimamo wa Serikali wa kutokusaini mkataba wa EPA

$
0
0
Wabunge wameridhia rasmi msimamo wa serikali wa kutokusaini mkataba wa ubia wa uchumi ' EPA' baina ya nchi za jumuia ya Afrika Mashariki na umoja wa ulaya.

 ==>Sikia michango ya baadhi ya wabunge hapo chini
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images