Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Viza za Israel zaanza kutolewa hapa nchini, faida zake zabainishwa

$
0
0
Serikali ya Israel imeanza kutoa huduma za viza moja kwa moja kutokea jijini Dar es Salaam ambapo kwa mujibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii Profesa Jumanne Maghembe, hatua hiyo itachochea ukuaji wa biashara pamoja na ushirikiano wa kidiplomasia.

Awali, viza zilikuwa zikitolewa jijini Nairobi nchini Kenya lakini hivi sasa huduma hiyo itakuwa ikipatikana jijini Dar es Salaam ambapo Waziri Maghembe ametaja baadhi ya faida chache za utolewaji wa huduma hizo hapa nchini kuwa ni kupungua kwa urasimu na gharama za kutafuta viza, kukua kwa ushirikiano katika nyanja zote za uchumi, elimu ulinzi pamoja na usalama.

Balozi wa Israel nchini Kenya Bw. Yahel Vilan amesema hatua hiyo itakuza uhusiano wa kidiplomasia hususani kwenye eneo la uchumi, kutokana na uzoefu mkubwa iliyonao taifa hilo ambalo hivi sasa limepiga hatua kubwa kwenye uchumi na teknolojia.

Kwa upande wake, Bi. Pooja Lalji amesema wamejipanga kuhakikisha wafanyabiashara wanaokwenda Israel wanapata viza zao mapema na hivyo kuchochea biashara baina ya Tanzania na taifa hilo la Mashariki ya Kati

Marekebisho saba Yafanyika Muswada wa sheria ya huduma za habari

$
0
0
Serikali jana imewasilisha bungeni muswada wa sheria ya huduma za habari mwaka 2016, huku ikitaja marekebisho saba katika muswada huo.

Marekebisho hayo ni pamoja na kuainisha haki na wajibu wa wanahabari, kuainisha haki ya chombo cha habari kukata rufaa, uwakilishi wa wanahabari katika bodi ya ithibati, Jaji Mkuu kuweka utaratibu wa kusikilizwa haraka kesi za kashfa.

Mengine ni kuviondolea vyombo vya habari adhabu kwa baadhi ya makosa ya mwandishi, vyombo vya dola kukamata mitambo na vifaa vya wanahabari na mitambo kutohusika moja kwa moja kwa kosa la gazeti.

Akiwasilisha bungeni muswada huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, alisema marekebisho hayo yamefanyika baada ya mashauriano na wadau wa habari wakiwamo wananchi, wanataaluma ya habari, wanasheria na kamati nyingine za bunge.

Alisema katika eneo la kuainisha haki na wajibu wa wanahabari, muswada wa awali kwa kiasi kikubwa uliainisha zaidi wajibu wa wanahabari lakini kwa kuzingatia mikataba ya kimataifa ambayo nchi imesaini na kuridhia na matakwa ya katiba.

Nnauye alisema kwa sasa eneo hilo limerekebishwa katika kifungu cha saba kwa kuainisha pia haki za wanahabari kama vile uhuru wa kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza habari.

Alisema kuhusu kuainisha haki ya chombo cha habari katika kukata rufaa, katika kifungu cha 10 kuhusu utoaji wa leseni za vyombo vya habari , muswada wa awali haukuwa umeweka haki ya kukata rufaa kwa atakayekataliwa kupewa leseni na Mkurugenzi wa Idara ya Habari.

Alibainisha kuwa chombo husika kinaweza kukata rufaa kwa waziri wa habari na pia mwishowe kisiporidhika na uamuzi wa waziri sasa kinaweza kupinga suala hilo mahakamani.

Kuhusu uwakilishi wa wanahabari katika bodi ya ithibati, Nnauye amesema eneo hilo limeboreshwa ni uwakilishi wa vyombo vya habari katika bodi hiyo, na kwa mujibu wa mapendekezo ya awali, bodi hiyo itakayokuwa na wajumbe saba sasa itakuwa na wanahabari wanne akiwemo mwenyekiti.

Alisema suala la Jaji Mkuu kuweka utaratibu kusikilizwa haraka kesi za kashfa, moja ya malalamiko makubwa ya wadau katika utoaji wa haki zinapokuja kesi za habari hasa za masuala hayo ni kuchukua muda mrefu kwa kesi hizo.

Katika maboresho ya kipengele hicho, alisema hivi sasa jaji huyo kwa kuzingatia tathmini ya uwezo wa Mahakama na rasilimali zilizopo na kama ilivyowekwa kwa kesi nyingine kama za uchaguzi atatunga kanuni zitakazoweka muda wa kumalizika kwa kesi za aina hiyo.

Kadhalika, Nnauye alisema kuhusu vyombo vya dola kukamata mitambo na vifaa vya wanahabari, maboresho yamefanywa kwa kulenga kumuondoa mkurugenzi wa idara ya habari kuwa na mamlaka ya kukamata mitambo hiyo.

Tundu Lissu Akataa Kujisalimisha Mahakamani Bila Barua ya Witoi

$
0
0

Siku moja baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kuagiza Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akamatwe kwa kushindwa kuhudhuria kortini, mbunge huyo amedai hana taarifa hizo hivyo hawezi kujisalimisha popote.

Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, alidai atajisalimisha tu kwenye vyombo vya dola au kwenda mahakamni ikiwa atapelekewa barua aliyoandikiwa na mahakama na kutiwa saini na kugongwa muhuri na hakimu. 

“Kaka, mimi siwezi kufanyia kazi za magazeti katika masuala ya kisheria, nipo hapa ninaendelea na shughuli zangu kama kawaida na kama mnavyoniona niko katika kuwawakilisha wananchi wa jimbo langu,” alieleza Lissu. 

Mwanasheria huyo mkuu wa Chadema alitoa maelezo hayo jana alipohojiwa kuhusiana na habari zilizoandikwa na vyombo vya habari, kwamba Mahakama ya Kisutu juzi iliagiza mbunge huyo akamatwe baada ya kushindwa kuhudhuria katika kesi inayomkabili. 

Mbali ya mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa kwa Lissu, pia iliagiza iandaliwe hati ya kuitwa mahakamani kwa wadhamini wake ili wajieleze kwa nini wasilipe fungu la dhamana walilotia saini ambalo ni Sh10 milioni.

Kwa mujibu wa Hakimu Mkazi wa Kisutu, Thomas Simba, Lissu amekuwa hahudhuri kortini kusikiliza kesi ya uchochezi inayomkabili pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob. 

Katika kesi hiyo, inadaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14 mwaka huu, Dar es Salaam, Lissu na wenzake walikula njama za kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari: “Machafuko yaja Zanzibar”.

Juzi, siku ambayo kesi hiyo ilipangwa kutajwa tena, Lissu hakuwapo mahakamani kutokana na kile mdhamini wake Robert Katula alichodai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza hivyo asingeweza kuhudhuria.

Kutokana na maelezo hayo wakili wa upande wa Jamhuri, Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa jambo ambalo Hakimu Simba alikubali pamoja na wito kwa wadhamini kufika mahakamani Novemba 21, mwaka huu.

Alipoulizwa kuhusu hatua hiyo, Lissu alisema kuwa wito wa kwenda mahakamani ni lazima barua iwe imeandikwa na kugongwa muhuri na kutiwa saini ya hakimu wa mahakama na siyo kusikia na kwenda bila ya kuwepo kwa wito kamili.

Bodi ya Mikopo Elimu Ya Elimu ya Juu Yaagizwa Kuwapa Wanafunzi Fedha Zao ifikapo Leo

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HELSB), imeagizwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo zinapelekwa vyuoni ifikapo leo. 

Agizo hilo lilitolewa bungeni jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wabunge mbalimbali kuomba miongozo kwa Spika kuhusu kuwapo kwa wanafunzi wengi waliokosa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17. 

Mwongozo kwa Spika ulitiliwa mkazo na Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwan Kikwete aliyeeleza kuwapo taarifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa wanafunzi wanataka kugoma kwa kukosa fedha za mikopo. 

Kutokana na miongozo hiyo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga aliitaka Serikali kutoa maelezo. 

Akitoa kauli ya Serikali, Profesa Ndalichako alisema fedha za mikopo kwa ajili ya wanafunzi zilikwenda vyuoni wiki moja iliyopita. 

“Tatizo lililotokea kwa UDSM sijui kama walidanganyana au la lakini hawakujaza fomu. Serikali haitatoa mkopo kwa mwanafunzi ambaye hajajaza fomu. Na waliosaini leo wataingiziwa fedha zao kwenye akaunti na vyuo,”alisema. 

Kuhusu wanaoendelea na masomo, Profesa Ndalichako alisema wanafunzi wote wanufaika na wanaoendelea na masomo wataendelea kupatiwa mikopo kama ilivyokuwa mwaka uliopita. 

Alisema wanafunzi ambao vyuo vyao vimewasilisha HELSB taarifa za matokeo, Bodi imekwishawatumia fedha vyuoni kwa ajili ya kuwapa mikopo wanafunzi hao. 

Hata hivyo, alisema taratibu za kuwabaini wanafunzi wenye sifa zinaendelea na wasio na sifa wataendelea kuondolewa kupata mikopo. 

Pia, alikiri kuwa ucheleweshaji wa matokeo ya wanafunzi wanaoendelea na masomo umeathiri kasi ya kutuma fedha vyuoni. 

“Wizara yangu imekwishaagiza vyuo vyote ambavyo havijawasilisha matokeo ya mitihani ya wanafunzi wao kwa mwaka wa masomo uliopita, kufanya hivyo mara moja,”alisema. 

Ndalichako alisema hadi kufikia Novemba 3 mwaka huu, Sh71.042 bilioni zilikwishatumwa vyuoni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.

Akizungumzia utoaji wa mikopo kwa mwaka wa fedha 2016/17, Ndalichako alisema katika mwaka huo, Sh483 bilioni zimetengwa na zimelenga kutoa mikopo kwa wanafunzi 119,012, wanafunzi 93,295 wanaoendelea na masomo na wa mwaka wa kwanza 25,717.

Ndalichako alisema katika mwaka wa fedha 2016/17 wanafunzi 58,010 walidahiliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na orodha yao iliwasilishwa HELSB na hadi Novemba 2, mwaka huu, wanafunzi 21,190 wa mwaka wa kwanza wamepewa fedha. Kati yao 4,321 ni yatima, 118 wenye ulemavu na 87 ni waliosoma sekondari kwa ufadhili wa taasisi mbalimbali.

Mwaka Mmoja Wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli.

$
0
0
Leo na mimi nipaze sauti yangu imfikie Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa Mafanikio Makubwa aliyoyapata ktk kipindi cha Mwaka mmoja wa utawala wake tangu aingie madarakani mnano Novemba 05, 2015.

Rais Magufuli kwa kiasi kikubwa amerudisha nidhamu kwa watumishi wa umma. Leo ofisi nyingi za utumishi wa umma zina nidhamu ya hali ya juu sana, watu wanatambua vizuri nini wanapaswa kufanya na nini hawapaswi kufanya ktk Utumishi wao. Huduma zenye kukidhi matakwa ya wananchi zimerejea.

Rais Magufuli amefanikiwa  kwa kiasi kikubwa  kudhibiti matumizi ya fedha za Serikali kwa kuzuia na kufuta matumizi yasiyokuwa ya lazima kama safari za nje ambapo ktk kila safari kwa sasa ni lazima Ikulu ibariki kwa kutoa Kibali na kuruhusu idadi ndogo tu ya watu na mara nyingine mabalozi kuiwakilisha Tanzania, kuondoa posho zisizo za lazima n.k

Rais Magufuli  alielekeza fedha mbalimbali ambazo zilitengwa kwa matumizi Maalum Mfano Fedha kwa ajili ya Semina kwa Baraza la Mawaziri, Fedha kwa ajili Sherehe ya Kitaifa ya Maadhimisho ya Uhuru - 09 Desemba 2015 n.k  Mh. Rais alielekeza  zikafanye Shughuli za Kimaendeleo ikiwemo kununua Vitanda vya Hospitali ya Taifa Muhimbili na kutengeneza Madawati kwa ajili ya Shule za msingi  ili kuboresha Elimu.

Rais Magufuli alituahidi endapo atachaguliwa   Elimu ya msingi na Sekondari itakuwa ni BURE ambapo ametimiza sasa Elimu kwa Shule za Msingi na Sekondari ni BURE kabisa.

Rais Magufuli aliahidi atafufua Shirika la Serikali la Ndege la ATCL kwa kununua Ndege Mpya ambapo tayari Mheshimiwa Rais ametimiza Ahadi yake kwa Kununua Ndege Mbili Mpya  na leo ameahidi kutuletea Ndege Kubwa aina ya Boeing yenye uwezo wa Kubeba abiria zaidi ya 240 ili kukuza uchumi wa Nchi kupitia  Sekta ya Utalii.

Rais Magufuli amefanikiwa kusimamia ipasavyo Ukusanyaji wa Mapato ya serikali na Kudhibiti Matumizi yake. Hongera pia Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kumsaidia Mheshimiwa Rais ktk hili.

Rais Magufuli alituahidi kupambana na Ufisadi na Kuendeleza Vita dhidi ya Wala Rushwa kwa Kuanzisha Mahakama ya Kushughulikia Ufisadi na Rushwa na tayari mahakama ya Kushughulikia Ufisadi & Rushwa inaishi na leo naamini imesikiliza Kesi moja.

Rais Magufuli ameendelea kuboresha barabara kwa Kukijenga kwa Kiwango cha lami mfano kama ile ya Mwenge Dar es Salaam & Mwanza.

Mheshimiwa Rais aliahidi kuhamishia Serikali yake Makao Makuu ya Tanzania Mjini Dodoma na tayari amekwisha anza kutekeleza kwa kuhamisha Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara mbalimbali.

Rais Magufuli aliahidi kukuza Uchumi wa Nchi yetu kwa kuifanya Tanzania ya Viwanda na wote tumeshuhudia Juhudi za Mheshimiwa Rais za Kutafuta wawekezaji kutoka Mataifa mbalimbali duniani ili yawekeze nchini.

Ndugu zangu yako Mengi sana aliyofanya Rais Magufuli  mwenye macho haambiwi tazama ila naomba niishie hapo.  Ijapokuwa Bado Changamoto ni nyingi na watu wataona Maisha yamekuwa magumu lakini tutambue na kuelewa hali hiyo haina budi kuja kwani  Nchi iko katika kipindi cha Mabadiriko ya kiuchumi kitaalamu tunaita " TRANSITION PERIOD " ambapo kutokana na Juhudi za Mheshimiwa Rais kuujenga uchumi wa Nchi yetu ni lazima mwanzoni tutaona Mabadiriko fulani fulani hivyo Watanzania wenzangu tuvute subira kwa maisha Mazuri yaja. Tumpe nafasi Mh. Rais apambane kwa ajili ya Maendeleo ya Nchi yetu na sisi kwa nafasi zetu tumpe ushirikiano wa kutosha kwa kufanya kazi kwa Bidii sana.

Ama Kwa Hakika Rais wetu anastahili pongezi nyingi sana na Mimi Robert PJN Kaseko Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha nichukue nafasi hii kukupongeza Rais wangu na Mwenyekiti wangu CCM Taifa Mh. DKT. John Pombe Magufuli kwa kutuletea Maendeleo makubwa na Mabadiriko ya kweli kwa kipindi cha Mwaka mmoja tunashirikiana toka tukuchague utuongoze, Mabadiriko  ambayo kiukweli sisi Wananchi wa Tanzania tulisubiri kwa Muda mrefu sana na nizidi kukutia moyo Mh. Rais usirudi nyuma endelea mbele tunatambua vikwazo ni vingi na Kazi ni ngumu lakini namuomba Mwenyezi Mungu azidi kukutia nguvu, akupe afya njema na ulinzi wake ili uendelee vyema kuwaletea Maendeleo Wananchi wako maana wewe ni Mchapa Kazi Kwelikweli tunakufahamu vizuri. HAPA KAZI TU. CCM Hoyeeeeeee. 

Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
November 04, 2016.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 35 & 36

$
0
0
Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA  
“Asante sana Fred”
Wakiwa juu angani, wakaendelea kupata vinywaji mbalimbali, huku wakitazama baadhi ya chanel, za tv ndogo iliyopo kwenye kila meza ya safa lililopo ndani ya ndege hiyo ya kifahari. Gafla Rahab akaanza kujihisi vaibaya vibaya, huku mara kadhaa, akawa anajikaza ili Praygod asijue ni kitu gani kinacho endelea, ila gafla akajikuta akianza kutapika na kulichafua gauni lake alilo livaa

ENDELEA  
Furaha ikabadilika na kuwa mshike mshike ndani ya ndege kwani kadri muda ulivyo zidi kwenda hali ya Rahab ikaanza kubadilika na kujikuta mwili mzima ukianza kumtetemeka, na kutoa mapuvu mdomoni mwake. Frednando akawaamuru marubani wairudishe ndege haraka kwenye kiwanja cha nyumba kwake ili kumuwahisha Rahab, aweze kuonana na madktari.

Macho ya Rahab yakabadilika na mboni zake nyeusi zikapotea na kubaki weupe kwenye macho yake jambo lililozidi kumchanganya raisi Praygod pamoja na Frednando ambaye hakujua ni ugonjwa gani ambao bibi harusi ameweza kuupata.
Haikuchukua muda mwingi, matairi ya ndege yakawa yanaserereka kwenye ardhi ya uwanja wa nyumbani kwa Frednando, ambapo Alisha waeleza madaktari wake wawe tayari kwa kumpokea mgonjwa.

Kwa kushirikia na Frednando, wakambeba Rahab na kumtoa nje ya ndege na kumuingiza kwenye gari maalumu la wagonjwa lililokuwa likiwasubiri. Moja kwa moja Rahab akakimbizwa kwenye jingo linalo tumiwa na Fredando kama hospitali inayo mtibu yeye na familia yake pale wanapo patwa, na hali yoyote ya kuumwa. Uzuri wa eneo lilipo jumba la Frednando, aliweza kuwekeza pesa nyingi kujijengea vitu muhimu kwa mahitaji yake, ikiwemo jengo la hospitali, lenye madaktari bingwa ambao Fredinando anawaamini sana

“Kaka hivi mke wangu atapona kweli?”
Raisi Praygod alizungumza huku machozi yakimlenga lenga, akamshuhudia mke wake akipakizwa kwenye kitanda cha matairi baada ya kushushwa ndani ya gari, na moja kwa moja akaingizwa kwenye chumba kilicho jaa vifaa muhimu kwa kumuhudumia mgonjwa mahututi

“Atapona tu, usijali rafiki yangu”
Fredinando alimfariji raisi Praygod, lakini yeye mwenye amechanganyikiwa kwani hakuamini kama siku kama hiyo kutajitokeza jambo kama hilo la kuhuzunisha. Wakiwa wamesimama kwenye nje ya mlango wenye kioo kikubwa, wakawashuhudia madaktari wakitumia mashine za kustulia mapigo ya moyo wakiziweka kwenye kifua cha rahabu ambaye amezima kabisa mapigo yake ya moyo.
Machozi taratibu yakaanza kumtoka raisi Praygod, hakuamini uzuri wote wa Rahab, unaweza kupotea muda wowote kuanzia sasa.

“Kaka jikaze”
Frednando alizungumza huku, naye machozi yakiwa yanamtiririka, uchungu anao upata rafiki yake, nao unaugusa moyo wake, kwani ni dakika chacha tu wametoka kucheka na kufurahi na shemeji yake ambaye muda mwingi anapenda kumtania kwa jina la ‘AFRICAN QUEEN’. Mashine zakupulia zinazo soma mapigo ya moyo jinsi yanavyo kwenda yakazidi kuwachanganya madaktari hawa wane, kwani ni mstari mmoja ulio nyooka ndio unakatiza kwenye mashine hiyo, huku kukisomeka sifuri mbili za rangi nyekundu zikiashiria kwamba Rahab mapigi ya moyo hayafanyi kazi, moja inawezekana amesha fariki au moyo wake upepata mstuko mkubwa
                                                                                           ***
Si Fetty wala mwenzake yoyote aliye weza kujinyanyua kutoka kwenye sakafu walipo kaa, kila mmoja macho yake yaliyo jaa machozi, wakawa wanaitazama sura ya kipande cha mwanaume, aliye fura kwa hasira na si mwingine bali ni bwana Rusev, aliye simama huku bastola yake ikiwa mkononi mwake. Kila mmoja akatamani kujitetea, ila nguvu hakuwa nazo za kutosha kusema anaweza kupambana na bwana Rusev, anaye onekana kuchukia baada ya mapiganaji yake matatu kuuliwa kinyama
“Hatuna tulicho kibakisha tena duniani, tumekuwa ni watu waovu. Hatuna pa kwenda zaidi ya kaburini. Tuue sisi yupo tayari”
Anna alizungumza huku machozi yakimwagika usoni mwake, huku mikono yake yenye kufungwa pingu akiendelea kumshika Halima, aliye kwenye hali ngumu sana.
“Ehee Mungu zipokee roho zetu, na utusamee makosa yetu tuliyo yafanya. Amen”

Anna alizungumza kwa sauti ya unyonge iliyo wafanya wezake kuendelea kulia kwa uchungu, kwani hakuna aliye tarajia kwamba maisha yake yatakuwa hivyo. Maneno ya Anna, yakamfanya bwana Rusev, kumwagikwa na chozi lililo washangaza askari wake waliopo nje wakiwatazama.
Bwana Rusev akawamrisha askari wake kuingia ndani na kuwechukua Fetty na wezake, ambapo akawaamrisha wavalinye vipande vya vigunia vyuesi kwenye vichwa vyao wasijue ni wapi wanapelekwa.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumapili ya Novemba 6

Bunge Lapitisha Rasmi Muswada Wa Sheria Ya Huduma Za Habari Wa 2016

$
0
0

Na Jacquiline Mrisho na Eleuteri Mangi – MAELEZO, Dodoma.
Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania umepitisha rasmi Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ambapo hatua inayofuata ni kuridhiwa na kusainiwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili uwe Sheria kamili ya nchi.

Muswada huo umepitishwa jana Bungeni mjini Dodoma ambapo mkutano huo uliongozwa na Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Andrew Chenge.

Wabunge walijadili Muswada huo kifungu kwa kifungu na kuunga mkono upitishwaji wake baada ya Waziri mwenye dhamana na habari kutoa hoja ili Muswada huo uweze kujadiliwa.

Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kupitishwa Muswada huo, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye aliwashukuru wadau wote walioshiriki katika kutoa maoni juu ya Muswada huo kwani ndiyo yamepelekea kukamilisha mchakato mzima wa Muswada huo.

“Kwa niaba ya Serikali napenda kuwashukuru wadau wote walioshiriki kwa namna moja au nyingine katika kuhakikisha tunatimiza malengo ya takribani miaka 20 iliyopita ya kuifanya taaluma hii ya habari kuheshimika kama zilivyo taaluma zingine”, alisema Waziri Nape.

Waziri Nape aliongeza kuwa kwa sasa Muswada huo umeshapitishwa hivyo kilichobaki ni utungaji wa Kanuni ambapo ameomba wadau wa tasnia ya habari kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kutoa maoni yatakayopelekea kuwa na kanuni zenye tija kwa wanahabari na taifa kwa ujumla.

Aidha, Mhe. Nape aliwaasa wadau wa habari kuunganisha nguvu kwa pamoja hasa katika kipindi hiki ambacho Muswada huo umepitishwa pia amewataka wadau hao wasiruhusu mgawanyiko utokee kati yao bali washirikiane na Serikali katika kutekeleza wajibu wao wa kihabari kwa jamii.

Kwa upande wake Mwanasheria Mkuu wa Serikali George Masaju alisema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa mwaka 2016 ni mwanzo mpya wa tasnia ya habari nchini ambapo aliwaasa wadau wa habari wakiwemo waandishi wa habari kutambua kuwa haki mara zote huendana na wajibu, hivyo hakuna haki isiyo na wajibu.

Muswada huo uliopitishwa jana umejadiliwa na Bunge hilo kwa siku mbili ambapo kwa mara ya pili ulisomwa mbele ya Kamati ya Bunge zima na hatimaye kusomwa kwa mara ya tatu ili kukidhi hatua za utungwaji wa Sheria nchini.

Godbless Lema Aamua Kufunga Kula Akiwa Rumande

$
0
0
Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema ameamua kufunga ili kuwa karibu na Mungu wakati akiendelea kushikiliwa na polisi mkoani Arusha. 

Wakati Lema akiamua kufanya hivyo, taarifa zilizopatikana mjini Arusha zinaeleza kuwa polisi walikwenda naye nyumbani kwake kwa ajili ya upekuzi lakini hawakufanikiwa kupata chochote. 

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo na hata alipotafutwa kwa simu, hakupokea. 

Suala la Lema kuacha kula ili awe karibu zaidi na Mungu lilielezwa na mwenyekiti wa Chadema wa mkoa, Amani Golugwa ambaye alisema ameelezwa na mke wa mbunge huyo. 

Lema, ambaye alikamatwa Jumatano iliyopita mkoani Dodoma na kuletwa mjini hapa Alhamisi, bado hajafikishwa mahakamani. Imeelezwa kuwa viongozi wa chama chake wameshindwa kumuona kutokana na kuzuiwa na polisi. 

Akizungumzia suala hilo jana, Golugwa alisema alipokea ujumbe kutoka kwa mke wa mbunge huyo, Neema Lema kuwa mumewe ameamua kufunga na kuomba kwa ajili ya Taifa kuhusu mambo yanayoendelea na kuwa ameona kipindi hiki ambacho yupo rumande ni cha kuwa karibu zaidi na Mungu. 

“Kama tunavyomjua Lema ni mtu anayempenda sana Mungu, ameamua kujinyenyekeza mbele za Mungu. Anafunga na kuomba jioni mke wake anampelekea chakula na amesema yupo katika hali nzuri,” alisema Golugwa. 

Golugwa alisema wamejitahidi kutaka kumuona Lema, lakini wamegonga mwamba na wameshindwa kumwekea dhamana mbunge huyo. 

Alisema alizungumza na ofisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani hapa na Kamanda Mkumbo, wote walisisitiza kuwa Lema ataendelea kuhojiwa hadi watakapojiridhisha. 

“Ni jambo la kushangaza kama mtuhumiwa anaweza kukaa rumande zaidi ya saa 48 kama sheria inavyotaka, nadhani hapa siyo sheria tena, labda ni kwa mujibu wa maelekezo ambayo hatujui yametoka wapi na kwa malengo yapi,” alisema Golugwa.

 Alisema baada ya kuwasili kutoka Dodoma alifanikiwa kuonana naye mara moja tu na baadaye hakuna mtu aliyeruhusiwa kuonana naye; iwe viongozi wa Chadema au wakili wa chama hicho, John Mallya ambaye ameshawasili kwa ajili ya mambo ya kisheria . 

Juzi, Kamanda Mkumbo alisema Lema hataachiwa hadi upelelezi ukamilike na mwanasheria wa Serikali atakapokuwa amemaliza kuandaa mashtaka kwa kuwa amekuwa akirudia makosa yaleyale ya uchochezi. 

Lowassa Atikisa Bunge Kwa Mara Nyingine

$
0
0
Edward Lowassa bado  angali vinywani mwa wabunge japokuwa hayupo tena Bungeni .Jina lake jana limeibua mjadala bungeni wakati wabunge walipotoleana maneno makali kuhusu waziri huyo mkuu wa zamani.

Sakata hilo limetokea wakati Bunge la Jamhuri ya Muungano lilipokuwa likijadili Muswada wa Huduma ya Habari ambao ulipitishwa jana licha ya kupingwa vikali na kambi ya upinzani na wadau wa habari.

Lowassa amelizua tafrani bungeni baada ya wabunge wawili kurushiana maneno kuhusu taarifa zake tofauti zilizokuwa zikiandikwa na vyombo vya habari kiasi cha kusababisha mwenyekiti wa Bunge aingilie kati.

Akichangia muswada huo, mbunge wa viti maalumu (CCM), Amina Mollel amerejea sakata la zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura iliyopewa kampuni ya Richmond Development ya Marekani ambayo ilibainika baadaye kuwa haikuwa na uwezo. Sakata hilo lilitokea wakati Lowassa akiwa Waziri Mkuu.

“Mimi naomba ninukuu baadhi ya vichwa vya habari ambavyo vilitumiwa katika magazeti,” amesema Mollel, ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.

Mollel ametaja mfano wa gazeti lililoandika“Lowassa anajua uzalendo au ni machozi ya mamba” na kichwa kingine cha habari cha gazeti hilo kilichosema “Lowassa Hasafishiki” na kingine kilichosema“Lowassa karibu Chadema”.

“Kuna haja ya kuwa na waandishi ambao leo hii wanaandika habari kwamba mtu huyo ni mbaya lakini kesho hiyo hiyo uongo huo unabadilika na kuwa ukweli?”amehoji Mollel.

Amesema Taifa linahitaji kuwa na sheria kama hiyo ambayo inaweza kulinda taaluma ya waandishi wa habari, hivyo kupitishwa muswada huo ni kwa manufaa ya wanahabari.

Maneno hayo kuhusu Lowassa yakamfanya mbunge wa Konde (CUF), Khatib Said Haji kusimama na kutumia methali inayosema “ukienda kwa wenye chongo, ufumbe macho ili ufanane nao japokuwa unaona”.

“Leo kituko cha karne hii ni pale anaponyanyuka mbunge wa CCM ndani ya Bunge akatulaumu eti sisi (wabunge wa kambi ya upinzani) kwa sababu tunampenda Lowassa. Hiki ni kituko cha karne,” amesema.

“Rudini kwenye kumbukumbu ya Mkutano Mkuu wa CCM kuhusu kale kawimbo katamu. Kweli?” amesema na kufanya wabunge wengine wa upinzani kuanza na kuimba “tuna imani na Lowassa”.

Jina la Lowassa limekuwa likiibuka kwenye vikao mbalimbali na katikati ya mwaka lilikuwa gumzo kwenye Mkutano Mkuu Maalumu wa CCM ulioitishwa kwa ajili ya uchaguzi wa mwenyekiti mpya wa chama hicho,

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 85 & 86 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0

MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
Baada ya dakika moja, simu akakabidhiwa Phidaya
"Eddy usitoe chochote"
Sauti ya Phidaya ilisikika, ikiambatana na mlio wa risasi kisha simu ikakatwa, nikajaribu kupiga tena huku mwili mzima ukinitetemeka ila haikupatikana tena, na saa yangu ya mkononi ikinionyesha yamesalia masaa kumi na tano tu.

ENDELEA
Nikabaki nikiwa nimeizhik simu yangu nisijue nini cha kufanya. Nikapata wazo la kumpigia mmoja wa waongozaji wa tangazo la magari ya Ford, ambaye alitokea kuwa rafiki yangu sana
"Smith, mimi Eddy"
"Vipi kaka, mbona unahema sana?"
"Nahitaji msaada wako"
"Upo wapi?"

"Nipo Dar es Salaam, umesha rudi Marekani?"
"Hapana, bado nipo Dar, labda kesho kutwa naweza kuondoka kuna vipande vya lile tangazo, vinamapungufu, tumeamua kuvitengeneza upya"
"Ahaa mupo wapi?"
Smith akanielekeza walipo, nikakodi tena pikipiki hadi walipo kwenye moja ya godauni, ambapo wamepafanya kama studio, wakitumia 'blue screen' wakitengeneza mazingira kama ya Arusha.
"Vipi Eddy mbona kama una wasiwasi?"
"Kaka nina matatizo makubwa sana"
Nikanza kumuadisia Smith, tukio moja baada ya jengine, sikumficha kitu cha aina yoyote.
"Eddy nakuahidi hakuna kitakacho haribika, nitakusaidia kaka yangu"

"Pesa yote hiyo utaitoa wapi Smith, wakati bado upo Tanzania?"
"Njoo uone"
Tukaingia ña Smith kwenye moja ya chumba, ambapo tukakuta Mtu anaye fanana na mimi kila kitu.
"Huyu nane ni nani?"
"Tumemtafuta mtu wa kufanana na wewe, ili aweze kurekebisha baadhi ya vipande, tulijaribu kukupigia simu ila hatukukupata"
Hapa ndipo nilipo amini duniani watu ni wawili wawili, Jamaa hadi kuzungumza anafanana na mimi.
"Umaitwa nani?"
"Fred"
"Duuu jamaa anafanana na mimi"
Nilizungumza huku nikiwa ninacheka kwani sikuamini kukutana na mtu anaye fanana na mimi, kwa asilimia zaidi ya tisini.
"Eddy huyu umnaonaje kakakusaidia katika swala zima la wewe kuoa"

"Apo Smith umenena jambo la maana"
"Alafu una bahati kwa maana ndio amemaliza kushooti vipande tulivyo vikosea"
Nikaanza kumuelezea fredy historia yangu yote kuanzia mwanzo hadi mwisho, nikamuelezea mazingira yate ya nyumbani, pamoja na mtafaruku uliopo kati yangu na mama
"Nimekuelewa Eddy, ila huoni kwamba itakua hatati siku wakigundua kwamba mimi sio wewe?"
"Hawawezi kugundua, kikubwa ni weww kuwa karibu sana na mimi, kila jambo ambalo utaona linakutatiza nijulishe kwa njia ya meseji"
"Ila kuna kitu kingine ambacho ni kigumu"
"Kitu gani?"
"Na mimi nina mke, ila bado sijamuoa"
"Ahaaaa Fredy, hii ni ishu kati yangu mimi na wewe, pia nitakupa kiasi chochote cha pesa"
"Utachukua muda gani kurudi, kutoka kuko Somalia?"
"Haitazidi mwezi mmoja"
"Ahaa kaka, huoni nitampoteza mke wangu"
"Mkeo anaishi wapi?"
"Mbagala rangi tatu"
"Ndipo ulipo kua ukiishi wewe?"
"Ndio ninapo ishi"

"Fanya hivi, mimi ninakupeleka nyumbani kwetu, mimi nielekeze kwako, nitazungumza na mkeo"
Fredy akajifikiria kwa dakika kadhaa, akakakubali kuufanya mchezo wa hatari, uliopo mbele yetu. Ikanilazimu kumnunulia Fredy kama nilizo vaa, pamoja na simu inayo fanana na mimi. Nikatafuta laini mpya ya kuwasiliana na Fredy tu, kwani ya kwangu imeunganishwa na namba ya mama.
"Bado nini hapa"
"Sweta ulilo vaa wewe"
"Twende nitakupa mbele ya safari"
  Tukaingia kwenye gari ya Smith, tukaelekea nyumbani kwetu, ambapo nikakuta basi kubwa, lililo toka kuwachukua ndugu kutoka stendi ya ubungo, walio toka mikoa tofauti kuja kushuhudia harusi yangu, wakishuka na kuingia ndani, huku wengine wakicheza kwa furaha.

Nikampa Fredy sweta langu na kujifunika kichwa chake, akajichanganya na wanandugu hao, walio landuka kwa kucheza kwa furaha, wengine wakionekana kulewa chakari. Fredy akafanikiwa kuingia ndani pasipo kustukiwa. Nikampigia simu
"Sasa chumba chako ni kipi?"
"Si umeona kuna nyumba tatu?"
"Ndio"
"Sasa wewe, pandisha kwenye hilo gorofa lenye rangi ya pinki, achana na hayo majengo mawili yenye ghorofa mbili mbili"
"Mbona zote zina rangi sawa"
"Hilo jengo la katikati, ndio upande, si umeliona?"
"Ndio naelekea"
Smith akawasha gari, tukaondoka, huku simu yangu ikiwa hewani

"Nipo ndani"
"Pandisha ngazi hizo utakuta kirdo ndefu, nyoosha hadi mwisho chumba cha mwisho kushoto ndio changu"
Japo ni jambo la hatari tunalo lifanya mimi na Fredy ila hapakuwa na njia nyingine zaidi ya kufanya hivyo.
"Nimesha ingia chumbani kaka, nipazuri sana"
"Sasa kazi kwako, ila hakikisha huwi muongeaji sana, usije ukachapia baadhi ya vitu"
"Nimekupata, demu anaitwa Sheila?"
"Ndio"
"Poa, kaka kukiwa na shida nitakueleza"

"Sawa"
Moja kwa moja tukaelekea Mbagala, hadi nyumbani kwa Fredy, kutokana Smith anapafahamu haikuwa shida kwangu kupajua. Tayari yaamekatika masaa manne yamesalia masaa kumi na moja kabla sijapeleka pesa ya kumkomboa Phidaya na mwanangu Junio.
Kitendo cha kushuka kwenye gari, nakastukia nikiguswa kwa nyuma, kugeuka nikakutana na Manaka akiwa amejitanda kanga mbili mwilini mwake

Benki ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) itaanza kutoa baadhi ya huduma za kibenki Novemba 8, 2016.

$
0
0

Kwa mamlaka iliyopewa kisheria kupitia kifungu namba 58(2) (a) na (b) cha Sheria ya Mabenki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, Benki Kuu inapenda kuutarifu umma kwamba zoezi la tathmini ya hali ya kifedha ya Twiga Bancorp Ltd (Twiga) limekamilika; kwa mantiki hiyo, Twiga itaanza kutoa baadhi ya huduma za kibenki kwa umma kuanzia Jumanne tarehe 8 Novemba 2016. 

Huduma hizo ni pamoja na ukusanyaji wa marejesho ya mikopo ya wateja. Meneja Msimamizi wa benki hiyo atawajulisha wateja huduma zitakazotolewa na taratibu za kuzingatia.

Benki Kuu ipo katika mchakato wa kupitia na kuchambua njia mbadala za kutatua tatizo la mtaji linaloikabili Twiga Bancorp. Njia inayopewa kipaumbele ni kutafuta mtaji kutoka kwa wawekezaji wapya, mchakato utakaowahitaji kuchambua hali halisi ya taarifa za hesabu za Twiga (due diligence).

 Zoezi hili linatarajiwa kuchukua takribani wiki tatu na litakapokamilika, Benki Kuu itaingia makubaliano na wawekezaji wapya kuhakikisha wanaingiza mtaji unaohitajika haraka iwezekanavyo ili shughuli za kawaida za kibenki ziweze kuendelea.

Benki ya Twiga itaendelea kuwa chini ya usimamizi wa Benki Kuu hadi hapo utaratibu wa kuwamilikisha wawekezaji wapya utakapokamilika.

Benki Kuu ya Tanzania ilitangaza kuiweka Twiga Bancorp Ltd chini ya usimamizi wake kuanzia tarehe 28 Oktoba 2016 kutoka na upungufu mkubwa wa mtaji unaoikabili.

Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuuhakikishia umma kuwa itaendelea kulinda maslahi ya wenye amana katika mabenki kwa lengo la kuleta ustahimilivu katika sekta ya fedha.

BENKI KUU YA TANZANIA
6 Novemba, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya No vemba 7

Ajali Mbaya ya Noah na Lori la Mizigo Yaua watu 17 Mkoani Shinyanya

$
0
0
Watu 17 wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha lori la mizigo aina ya Scania lenye namba za usajili T198CBQ na Noah ya abiria yenye namba za usajili T232BQR iliyotokea jana usiku katika kijiji cha Nsalala mkoani Shinyanga.

Waliokula Fedha za Mikopo Elimu ya Juu Kitanzini....Sheria Yarekebishwa Kuwabana Zaidi

$
0
0

Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Sheria Mbalimbali Namba 3 wa Mwaka 2016 unatarajiwa kuwasilishwa bungeni leo, ukigusa sheria tisa ikiwemo ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu ambapo sasa mnufaika wa mkopo aliyejiajiri atalipa kiasi kisichopungua Sh 120,000 au asilimia 15 ya kipato chake, huku taasisi za umma, bodi, wakala na tume zimebanwa zisirekebishe au kuwianisha mishahara, posho na marupurupu kwa watumishi.

Kwa mujibu wa muswada huo, kwenye Sheria ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, waajiri wanaoshindwa kuwasilisha marejesho ya mwezi baada ya makato wataadhibiwa, ambapo mwajiri atawajibika kuitaarifu Bodi ya Mikopo kuhusu ajira ya mtu yeyote ambaye ana shahada au stashahada na kukata makato ya mwezi kutoka kwenye mshahara wa mnufaika wa mkopo.

Kifungu hicho kinapendekeza kufanya marejesho ya mkopo kuwa ya kisheria na kupewa nafasi ya awali katika orodha ya makato na kinapendekeza kupunguzwa idadi ya wajumbe wa Bodi ya Mikopo na kufikia saba kwa lengo la kupunguza gharama za uendeshaji.

Kwenye marekebisho ya Sheria ya Utumishi wa Umma, Kifungu cha 8 kinapendekeza kufanyiwa marekebisho ili kumpa mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi) kurekebisha na kuwianisha mishahara, posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma.

Inapendekezwa kumuondolea Katibu mamlaka ya kuteua watumishi wa umma wanaounda baraza la majadiliano ya pamoja ya watumishi wa umma na sasa waziri atateua katibu kutoka wizara yenye dhamana na kada husika ya watumishi.

Pia inapendekezwa kufuta kifungu cha 11 ili kuondoa masharti yanayokataza Baraza la majadiliano ya pamoja ya watumishi na baraza la pamoja la watumishi wa umma kutoa mapendekezo kuhusu ujira.

Kwa upande wa marekebisho ya Sheria ya Leseni na Usafirishaji, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kutaongezwa kifungu ili kuweka masharti yanayoruhusu ulipwaji wa faini pale mkosaji anapokiri kosa, badala ya kila kosa kufuata taratibu za kimahakama.

Muswada huo una marekebisho kwenye Sheria ya Mazingira ambako kutawekwa mwongozo wa namna ya kupima urefu wa mita 60 kwenye kingo za bahari, ziwa, mto au bwawa la maji kinachozuiliwa kufanyia shughuli zozote za binadamu. Upimaji utapimwa kuanzia kwenye kingo za maeneo hayo.

Sheria nyingine zitakazofanyiwa marekebisho kwenye Mkutano wa Tano wa Bunge la 11 ni ya Usafiri wa Anga, Sheria ya Msajili wa Hazina na Sheria ya Vipimo.

Spika Job Ndugai wakati akizungumza na waandishi wa habari kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge wiki iliyopita, alieleza kuwa kwa wiki hii Bunge litapokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali(CAG) ya mwaka 2014/2015 kisha kujadili na kuishauri serikali kuhusu Mkataba wa Ushirikiano wa Kiuchumi kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) na Afrika Mashariki (EPA-EU) na kisha taarifa ya kamati ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi Kufuatia Kifo cha Spika Mstaafu Mhe. Samwel Sitta.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kufuatia kifo cha Spika Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Urambo lililopo Mkoani Tabora Mhe. Samwel Sitta.

Mhe. Samwel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Technical University of Munich nchini Ujerumani alikokuwa akipatiwa matibabu tangu mwezi uliopita.

Katika salamu hizo, Rais Magufuli amesema amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mhe. Samwel Sitta na kwamba Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.

“Nitamkumbuka Mzee Sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na Serikali.

“Kupitia kwako Mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa Mke wa Marehemu Mhe. Magreth Sitta ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo Mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.

Dkt. Magufuli amesema anaungana na wafiwa wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo na amewaombea moyo wa uvumilivu na ustahimilivu.

“Namuomba Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi, Ameni”

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
07 Novemba, 2016

Breaking News: Samwel Sitta Afariki Dunia

$
0
0

Spika wa Bunge Mstaafu, Samuel Sitta (74) amefariki dunia usiku wa kuamkia leo wakati akipatiwa matibabu nchini Ujerumani.

Mtoto wa marehemu, Benjamin Sitta amesema baba yake amefariki saa 10:00 usiku wa kuamkia leo.

‘’Nikweli mzee amefariki nchini Ujerumani akiwa anapatiwa matibabu, alipelekwa Alhamisi iliyopita na alikuwa anasumbulia na saratani ya tezi dume ambayo ilisambaa na kuathiri miguu na mwili mzima."

Benjamin amesema kuwa taarifa za mipango ya kusafirisha mwili zitatolewa baadaye.

Sitta alikuwa Spika wa Bunge tangu mwaka 2005 hadi mwaka 2010 na pia mbunge wa Urambo Mashariki.

Pia, alikuwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na aliwahi kuwa waziri katika wizara mbalimbali kwa vipindi tofauti.

Alikuwa miongoni mwa wanachama zaidi ya 42 wa CCM waliochukua fomu za kugombea urais mwaka jana.

Msimamo wa Rais Magufuli Kuhusu Katiba Mpya Wamtesa Tundu Lissu

$
0
0
Siku tatu baada ya Rais John Magufuli kueleza bayana kwamba suala la Katiba Mpya si kipaumbele chake kwa sasa akitaka aachwe ili ainyooshe nchi kwanza, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amesema kiongozi huyo hawezi kunyoosha nchi bila kuwa na Katiba Mpya iliyotokana na maoni ya wananchi.

Wakati Lissu akisema hayo, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damiani Lubuva amesema atatolea ufafanuzi suala hilo siku za karibuni.

Lubuva na Lissu walieleza hayo walipotakiwa kuzungumzia kauli ya Rais Magufuli kwamba kipaumbele chake ni kuchapa kazi ili kuinyoosha nchi na mengine yafuate ikiwamo Katiba Mpya.

Magufuli alitoa kauli hiyo Novemba nne, alipozungumza na Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari siku moja kabla ya kutimiza mwaka mmoja tangu aingie madarakani.

Lakini, Lissu alisema nchi haiwezi kunyooka bila kunyoosha kwanza Katiba inayoiongoza ambapo alipendekeza uwepo wa Katiba Mpya badala ya kuifanyia marekebisho iliyopo sasa.

“Tulishaondoka kwenye mjadala wa kuziba viraka kwenye Katiba, tumeshakubaliana kwamba tunahitaji mabadiliko ya Katiba yote si sehemu tu. Rais asidhani mtu akikalia kiti hicho basi neno lake ni sheria ya nchi. Haiwezekani,” alisema.

Alisema mchakato wa Katiba Mpya hautakiwi kuendelea ulipoishia kwa maelezo kuwa ikiwa hivyo nchi haiwezi kufika popote.

“Katiba Inayopendekezwa ni kama imepakwa rangi ya Katiba ya sasa. Inaonekana mpya lakini misingi yake ni ya Katiba ya sasa…, kama Rais Magufuli anataka kunyoosha nchi, anapaswa kuirejea Rasimu ya Jaji Warioba. Tuanzie hapo, zaidi ya hivyo atajidanganya na kuwadanganya Watanzania,” alisema.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki alisema nchi haiwezi kuongozwa kwa matamko ya kiongozi mkuu pekee bila kuangalia matatizo ya kisheria.

“Anafikiri akiamua yeye kama Rais unafuata utekelezaji? Kuna matatizo mengine ya kikatiba…, hayawezi kubadilika bila kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba. Kuna mambo ili yanyooke ni lazima uwe na Katiba nzuri. Usipoyashughulikia hayo mengine yote hayatawezekana,” alisema Lissu.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ,Jaji Lubuva alipoulizwa kuhusu mchakato wa Katiba Mpya na kauli ya Rais Magufuli alisema suala hilo linahitaji kukaa na kulizungumza vizuri.

“Naomba upokee kuwa nimekuelewa ila kwa sasa ninachoweza kusema nitatoa ufafanuzi mzuri kuhusu suala hilo kwani ni jukumu la ofisi yangu,” alisema.

Alisema ni kweli baada ya Katiba Inayopendekezwa kupigiwa kura na Bunge hatua iliyokuwa inafuata ilikuwa ni kuitisha Kura ya Maoni, lakini ilishindikana kutokana na kuingiliana na Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Kabla ya Rais Magufuli kutoa kauli yake kuhusu Katiba Mpya, siku za karibuni NEC iliwahi kueleza kwamba ipo katika hatua mbalimbali za kuhakikisha mchakato huo unafanyika kwa mujibu wa sheria.

Katika kauli yake ya Novemba nne, Rais Magufuli alisema wakati anaomba kura hakuweza kuzungumzia Katiba hivyo kwa sasa kilichopo mbele yake ni kunyoosha nchi kwanza na Katiba mpya itakuja baadaye.

TAKUKURU Yajitosa Kuchunguza Tuhuma za Wabunge wa CCM Kuhongwa Milioni 10

$
0
0
Taasisi ya Kuzuia na Kupambanana Rushwa (Takukuru) imeanza kuchunguza tuhuma zilizoibuliwa Bungeni kuwa Wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) walipewa rushwa ya shilingi milioni 10.
 
Tuhuma hizo zilitolewa wiki iliyopita Bungeni na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani, Freeman Mbowe alipomuuliza swali Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa. 

Hata hivyo, swali lake halikupata jibu ndani ya jengo hilo baada ya kuwekewa zuio na Naibu Spika, Dk. Tulia Ackson alieleza kuwa halikuwa swali la kisera.
 
Mbowe alitaka kufahamu kutoka kwa Waziri Mkuu kama tuhuma hizo ni za kweli au la, akidai fedha hizo zilitolewa kwa lengo la kuwashawishi kupitisha muswada wa sheria ya huduma za habari na mpango wa maendeleo ya taifa.
 
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola amesema kuwa taasisi hiyo imeanza uchunguzi kama alivyosema Rais John Magufuli alipokuwa akijibu swali katika mkutano wake na vyombo vya habari mwishoni mwa juma lililopita, Ikulu jijini Dar es Salaa.
 
“Ndiyo, tumeanza kuchunguza, Takukuru ni chombo chake na tumeanza kazi hiyo,” Mlowola anakaririwa .
 
Mkuu huyo wa Takukuru alifungua mlango kwa yeyote mwenye ushahidi kuhusu tuhuma hizo aziwasilishe ili kukisaidia chombo hicho.

Mkataba wa EPA pasua kichwa....Wabunge Kuamua Hatima Yake

$
0
0
MKATABA wa Uhusiano wa Uchumi na Biashara Kati ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na Ulaya (EPA), umegeuka kaa la moto baada ya mtalaamu wa sheria wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Palamagamba Kabudi, kuainisha vifungu visivyofaa vinavyoweza kuiumiza nchi kama itaukubali.

Kutokana na hali hiyo wabunge wameitaka Serikali isiingie kwa haraka kwenye mkataba huo kwa kuwa hauna maslahi kwa Taifa.

Mkataba huo ambao hadi sasa  Tanzania haijausaini, unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Alhamisi wiki hii kwa ajili ya kujadiliwa ingawa Kenya na Rwanda zimekwisha kuusaini.

Akiuchambua mkataba huo    kwenye semina ya wabunge mjini hapa jana, Profesa Kabudi, alisema mkataba huo haifai kwa kuwa una ahadi nyingi zisizotekelezwa.

Kwa mujibu wa mkataba huo, Profesa Kabudi alisema nchi za Ulaya hazitapata hasara yoyote ila nchi za EAC ndiyo itaathirika kwa sababu  hazitaruhusiwa tena kuongeza ushuru wa bidhaa zinazoingia katika nchi husika.

“EPA itasababisha wananchi wa nchi za Afrika Mashariki kukosa ajira kutokana na ukanda huo kugeuka ukanda huru wa bidhaa za Ulaya.

“Kama tutausaini kisha tukataka kuingia kwenye ushirikiano wa uchumi na nchi nyingine zilizo nje ya EPA, mkataba hauturuhusu kwa sababu unalazimisha nchi za EAC  kupeleka kwao bidhaa zenye kuzingatia afya na usalama kwa kukidhi viwango vya nchi zao.

“Kwa mujibu wa mkataba huo, kuna uwezekano bidhaa zetu zikakosa soko kwa kutokidhi vigezo vyao pamoja na kutakiwa kuthibitisha usalama huo kisayansi ambako kwa bidhaa za nchini ni vigumu kupata uthibitisho huo kama asali inayotoka  Tabora.

“Pia, ibara ya 99 ya mkataba huo inakwenda kuua ajira kwa vijana kwa vile  inachagua ni maeneo gani ya kufanyia kazi.

“Uchumi wa nchi yetu sasa tunaelekeza kwenye mkakati wa viwanda, lakini mkataba wa EPA una mtego kwa sababu hausemi ni mazao gani ya biashara yanatakiwa kwao.

“Kwa hiyo, pamoja na Kenya na Rwanda kuusaini, bado katika jumuiya kama kuna mwenzenu mmoja hajasaini, hautasainiwa katika jumuiya husika,” alisema Profesa Kabudi.

Mmoja wa wachambuzi wa mkataba huo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk. John Jingu, alisema Tanzania ikisaini mkataba huo, itapoteza mapato kwa sababu inategemea ushuru wa forodha ambao asilimia 10 ya ushuru huo, hutoka kwenye bidhaa zinazoingia kutoka Ulaya.

“EPA itaiathiri Tanzania katika biashara kwa sababu nchi inazofanya nazo biashara si za Umoja wa Ulaya kama vile Saudi Arabia, China, India, Falme za Kiarabu, Afrika Kusini, Uswisi, Marekani, Korea Kusini, Kenya na Andorra.

Awali, Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Adolf Mkenda, alisema Tanzania ikisaini mkataba huo, haitaweza kuongeza kodi na badala yake itabaki na tozo inazotoza.

Akichangia mjadala huo, Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu (CCM), alisema  anaunga mkono uchambuzi wa watoa mada kwa sababu  hatua ya kukimbilia kusaini huo ni kuendelea kuumia.

Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msingwa (Chadema), alisema pamoja na hoja za uzalendo za wachambuzi hao, bado kuna haja ya kuelezwa pia na faida zake badala ya kutajwa hasara peke yake.

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo), aliitaka Kamati ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, ihakikishe inakutana na timu ya wataalamu wakiwamo wafanyabishara kujadili kwa kina mkataba huo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images