Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Bunduki 11 za Ujangili zakutwa nyumbani kwa Mbunge

0
0
Kasi ya kupambana na ujangili iliyoongezwa na Rais John Magufuli imeendelea kuzaa matunda huku Kikosi Kazi Maalum kilichoundwa kikiripotiwa kukamata bunduki 11 nyumbani kwa mbunge.

Kwa mujibu wa chanzo cha gazeti la Mwananchi, Bunduki hizo zinazosadikika kutumika katika matukio ya ujangili zilikutwa nyumbani kwa mbunge wa CCM ambaye jina lake limehifadhiwa kwa sababu za kutoingilia unyeti wa oparesheni hiyo.

Taarifa hizo zimekuja ikiwa ni siku chache baada ya Rais Magufuli kufanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Maliasili na Utalii na kukipa nguvu zaidi kikosi kazi hicho ambacho kilidaiwa kuanza kuzimwa.

Rais Magufuli alimtaja mtu mmoja kwa jina la ’Mpemba’ anayehusishwa na biashara haramu ya pembe za ndovu kwa muda mrefu na kueleza kuwa angeshangaa kama asingekamatwa. Alishuhudia meno 50 ya Tembo ambayo yalikamatwa kutokana na oparesheni hiyo, hali inayoonesha kuna tembo 25 waliuawa.

Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe juzi alieleza kuwa tayari wameshamtia nguvuni Mpemba na kwamba wanaendelea na msako wa wengine ambao wakikamatwa nchi itatikisika kutokana na majina yao.

”Hilo ni jina lake analolitumia katika harakati zake za biashara ya ujangili ili asitambulike. Yuko mwingine pia anajiita ’Mangi wa Kabila fulani’ lakini sio majina yao halisi,” alisema Profesa Maghembe na kuongeza kuwa hawaweki hadharani majina yao ili kutoharibu uchunguzi.

Profesa Maghembe aliwahakikishia Watanzania kuwa mtandao wote wa majangili utavurugwa na hakuna jangili atakayesalimika bila kujali jina lake.

Hivi karibuni, Rais Magufuli alimteua Mkuu wa Majeshi wa zamani, Jenerali George Waitara kuwa Mwenyekiti wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), ambaye ameahidi kuwakomesha wafanyabiashara hao haramu.

Godbless Lema Ahojiwa Polisi Kwa Kumkashfu Rais Magufuli..........Mkewe Afikishwa Mahakamani Kwa Kumtumia Ujumbe wa Matusi RC Gambo

0
0
Neema Lema (33), mke wa Mbunge wa   Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha.

Alifikishwa  mahakamani hapo jana na kuunganishwa katika kesi ya tuhuma za kusambaza ujumbe unaomkashifu Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.

Katika kesi hiyo ya jinai namba 351 ya mwaka huu, mshitakiwa mwingine ni Lema ambaye alifikishwa mahakamani hapo Agosti 20 mwaka huu.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Agustine Rwizile, Wakili wa Serikali, Blandina Msawa, aliiomba mahakama   kufanya marekebisho kwenye hati ya mashtaka kwa kumuongeza Neema.
 
Akisoma mashtaka yanayomkabili Neema, wakili huyo alidai   Agosti 20 mwaka huu, jijini Arusha, mshtakiwa alituma ujumbe kwa simu ya mkononi uliosema, ‘karibu tutakudhibiti kama Uarabuni wanavyodhibiti mashoga’.
 
Neema anayetetewa na Wakili Sheck Mfinanga, alikana kutenda kosa hilo na kupewa dhamana hadi Novemba 15, mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
 
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi mkoani Arusha, lilimkamata na kumhoji Lema kwa tuhuma za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais Dk. John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo, alisema Lema alitoa lugha hiyo wiki iliyopita katika mikutano halali aliyoifanya jimboni kwake.

“Tumemkamata Lema kwa kutoa lugha ya uchochezi ambayo ni kinyume cha sheria.

“Baadhi ya maneno aliyotoa yenye uchochezi ni pamoja na kusemaRais Magufuli akiendelea kugandamiza demokrasia, taifa litaingia katika umwagaji wa damu, nchi hii inaandaliwa kwenda  katika utawala wa udikteta pamoja na kuwataka wananchi wawe tayari kwa lolote na waache   uoga kwa vile uoga ni dhambi mbaya kuliko dhambi zote duniani.

“Baada ya kumhoji kuhusu maneno hayo, tulimwachia kwa dhamana na sasa jalada lale liko kwa Mwanasheria wa Serikali kwa ajili ya kuandaa hati ya mashitaka  afikishwe mahakamani,” alisema Kamanda Mkumbo.

Mwaka Mmoja Wa Rais Magufuli: TRA Yavuka Lengo La Makusanyo Ya Mapato.

0
0
Na JOVINA BUJULU- MAELEZO
Novemba Tano mwaka huu ni mwaka mmoja tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipoapishwa kuwa kiongozi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama wa Nchi hii.

Katika kipindi cha mwaka mmoja wa uongozi wake, Watanzania wameshuhudia  mafanikio makubwa katika katika sekta ya ukusanyaji kodi kupitia vyanzo mbali mbali vya mapato. 

Hatua hii inatokana na kuwa Rais Magufuli alipoingia madarakani amekuwa mstari wa mbele kuhakikisha hakuna mfanyabiashara anayekwepa ulipaji kodi na kuwahimiza wananchi kuhakikisha wanadai risiti kwa kila bidhaa au huduma wanayolipia.

Hivyo Serikali hii tangu ianze kazi rasmi imekuwa ikitilia mkazo ukusanyaji wa mapato ya Serikali kwa kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kubuni vyanzo vipya ili kuongeza makusanyo ya Serikali.

Juhudi hizi za Rais Magufuli za kuongeza mapato na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali zimejionyesha katika mikutano yake mingi ambapo mara nyingi amekuwa akisema “Ukinunua bidhaa dai risiti na ukiuza bidhaa toa risiti”.

Jitihada hizo za wa ukusanyaji wa kodi kwa ajili ya kuongeza mapato ya Serikali kwa manufaa zitatekelezwa na uongozi wa Rais Magufuli zinaunga mkono wosia aliwahi kuutoa Baba wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo alisema kuwa “Serikali yeyote isiyokusanya kodi ni “corrupt”.

Hatua hiyo ya kutoa na kudai risiti ina mchango mkubwa kwa serikali katika  kukusanya kodi ambazo zitasaidia katika kuboresha huduma za jamii kama vile elimu, afya, maji, umeme, usafirishaji, ujenzi na uendeshaji wa serikali kwa ujumla kutokana na mapato yanayopatikana.

Hapa nchini, Mamlaka ya Mapato (TRA) ndicho chombo chenye jukumu la kusimamia ukusanyaji wa mapato ya Taifa na imekuwa ikitimiza lengo hilo kwa kutekeleza mikakati mbalimbali kama ilivyoainishwa katika mpango mkuu wa miaka mitano.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi Bw. Richard Kayombo, katika kipindi cha mwaka mmoja wa utawala wa Rais Magufuli kumekuwepo na ongezeko la makusanyo ya mapato ya serikali yatokanayo na kodi.

Anasema kuwa katika kipindi hiki, TRA inakusanya wastani wa trillion 1.1 kila mwezi kuanzia mwezi Novemba, 2015 hadi Septemba 2016.
 
“Hili ni ongezeko la asilimia 28.1 kutoka kwenye kukusanya wastani wa shilingi bilioni 867 kwa mwezi katika kipindi cha mwezi Novemba, 2014 hadi Septemba 2015” anasema Bw. Kayombo.

Makusanyo ya mapato katika kipindi cha utawala wa Rais Magufuli kuanzia mwezi Novemba 2015 yamekuwa yakiongezeka ikilinganishwa na miaka iliyotangulia kwa mfano mwaka wa fedha 2015/2016 mapato yaliyokusanywa yalikuwa shillingi trilioni 12.5 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26.4 ya makusanyo ya mwaka 2014/2015. 

Aidha TRA imekwisha kusanya kodi kiasi cha shilingi trilioni 3.5 kufikia mwezi Septemba 2016, ikiwa ni ongezeko la asilimia 23.4 ikilinganishwa na kipindi kama hiki cha robo mwaka 2015/16.

Bw. Kayombo anaongeza kuwa kwa sasa TRA inatekeleza mpango mkakati wa nne wa ukusanyaji kodi wenye dhamira ya kuongeza makusanyo ya kodi za ndani kwa kuongeza ulipaji kodi wa hiari.

“Jitihada mojawapo zinazofanywa na TRA ni pamoja na kuboresha mifumo ya makusanyo inayoendana na mazingira ya sasa ya ukuaji wa teknolojia ili kuhakikisha walipa kodi wanalipa kwa urahisi kama ilivyo dhamira yake ya kurahisisha ulipaji kodi na kufanya mazingira yawe bora” anasema Bw. Kayombo. 

Katika kipindi cha mwaka mmoja ambao Rais Magufuli amekuwa madarakani, juhudi mbalimbali zimefanyika ili kuhakikisha matarajio ya Rais ya kuimarisha makusanyo ya kodi na kudhibiti mianya ya rushwa yanafanikiwa.

Mafanikio hayo yatamuwezesha Rais Magufuli kutimiza ahadi zake alizozitoa wakati wa kampeni zikiwemo kuboresha afya, upatikanaji wa maji, umeme, kutoa elimu bure, ujenzi wa miundombinu kama vile viwanja vya ndege, reli na barabara. 

Aidha makusanyo hayo yatawezesha uwekezaji katika ujenzi wa viwanda ambavyo vitatoa ajira kwa wananchi na serikali kuweza kujitegemea na hivyo kupunguza utegemezi wa misaada kutoka kwa wafadhili.

Bw.Kayombo anataja kiini cha ongezeko la kukusanya kodi kuwa ni matumizi ya mashine za kielektroniki (EFD) ambazo zinatumika zaidi badala ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono. 

“Matumizi ya stakabadhi zinazoandikwa kwa mkono hayakuwa na ubora mzuri wa kukusanya na kuongeza mapato na kutunza kumbukumbu sahihi ambayo yaliifanya serikali ipoteze mapato mengi” anaongeza.

Katika hatua nyingine TRA ilitoa mashine za EFDs 130 bure kwa makatibu wakuu wa Wizara mbali mbali kwa ajili ya taasisi za serikali ambazo zinakusanya maduhuli ya serikali kwa nia ya kudhibiti upotevu wa mapato ya serikali.

Katika kuhakikisha makusanyo ya kodi yanaongezeka TRA imeendelea kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi, kufichua wakwepa kodi, kupambana na rushwa na kupanua wigo wa kodi kwa kusajili wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa sambamba na kuendesha zoezi la kuhakiki namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) linaloendelea jijini Dar es Salaam kwa sasa ili kuboresha daftari la walipa kodi.

Pamoja na mafanikio hayo Kayombo alizitaja changamoto wanazokutana nazo katika ukusanyaji kodi kuwa ni pamoja na taarifa za kodi kutowafikia wananchi wote ili kujenga uhiari wa kulipa kodi na uwepo wa ukanda mrefu wa Pwani unaosababisha kuwepo mianya mingi ya ukwepaji kodi ambapo bidhaa huingizwa nchini kwa njia za panya.

Pamoja na changamoto hizo, Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) imeendelea kubuni mikakati mbali mbali ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “HAPA KAZI TU” ili kutimiza na kuvuka lengo la kukusanya shilingi trilioni 15.1 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17.

LIVE: Bofya Hapa Kutazama Kikao cha Bunge la 11 Leo Novemba 2, 2016

0
0
Bofya  Hapa  Kutazama   Kikao  cha  Bunge  la 11  Leo  Novemba 2, 2016

Mahakama Yamtia Hatiani Lady Jaydee.......Yamwamuru Amuombe Radhi Ruge wa Clouds Media

0
0
Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni imemkuta na hatia mwanamuziki Judith Wambura maarufu Lady Jaydee kumkashifu Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph Kusaga pamoja na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Hukumu hiyo imesomwa mahakamani hapo kufuatia kesi iliyokuwa imefunguliwa na viongozi hao wawili wa Clouds Media Group wakimtuhumi Judith Wambura kuwakashifu na kuwaharibia taswira zao na kampuni yao katika jamii.

Awali mahakama hiyo ilipanga kusoma hukumu ya kesi hiyo ya madai Oktoba 13 mwaka huu lakini Hakimu Lyamwike aliiahirisha hadi Novemba 2 mwaka huu kwa maelezo kuwa hakuwa amemaliza kuiandikia hukumu.

Katika kesi ya msingi, Joseph Kusaga na Ruge Mutahaba waliiomba mahakama itamke kuwa maneno yaliyotolewa na Judith Wambura kubitia blog yake ni kashfa na yanaathiri taswira yao katika jamii, pia mahakama imuamuru aombe radhi kupitia vyombo vya habari na alipe fidia kutokana na madhara ya jumla kwa jinsi mahakama itakavyoona inafaa.

Judith Wambura aliandika waraka katika blog yake na kwenye baadhi ya magazeti uliokuwa na kichwa cha habari “Wosia wangu ikitokea nimetangulia kufa kabla ya Ruge na Kusaga.”

Wakati akijibu shtaka hilo, Wambura ambaye alikuwa mtetezi pekee wa upande wake alikiri kuandika waraka huo, hivyo mahakama imemtaka aombe radhi kwenye chombo cha habari chenye coverage kubwa hapa  nchini na ikiwezekana duniani pia

Mali za Kampuni ya Mohamed Trans (yakiwemo mabasi) kupigwa mnada na TRA

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Novemba 3

Shirikisho la vyuo Vikuu lataja Hujuma bodi ya Mikopo- (HESLB)

0
0
Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini limemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa hesabu za Sh bilioni 1.74 za ada ya uombaji mikopo kwa mwaka huu katika Bodi ya Mikopo (HESLB) ili kujua matumizi ya fedha hizo kwa kuwa kuna mapungufu.

Aidha, shirikisho hilo limedai kubaini hujuma katika bodi hiyo zinazofanywa kwa makusudi ili kuchafua utendaji wa serikali iliyopo madarakani.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa shirikisho hilo, Daniel Zenda alipokuwa anazungumzia tuhuma za hujuma hizo, akidai zinafanywa kwa makusudi ili kurudisha nyuma jitihada njema za serikali.

Alisema ofisi ya CAG inapaswa kufanya ukaguzi wa Sh bilioni 1.74 fedha ambazo zilitokana na ada ya uombaji wa mikopo kwa mwaka huu ambapo kila mwanafunzi alitoa Sh 30,000 kwa waombaji 54,000.

Alisema ni muhimu kujua matumizi ya fedha hizo kutokana na upungufu uliojitokeza katika upitiaji wa sifa na vigezo vya wanaostahili kupata mkopo.

Alifafanua kuwa wanatambua hatua ya serikali katika kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanapata mikopo kwa wakati ambapo takribani Sh bilioni 80 zimeongezwa kwenye bajeti ya bodi hiyo ili kuwezesha mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa.

Zenda alisema Sh bilioni 487 zimepitishwa katika bajeti ya mwaka huu na mwaka jana ilikuwa chini ya makadirio ya Sh bilioni 350, lakini pamoja na kuongezeka kwa fedha hizo idadi ya wanafunzi walionufaika na mikopo imekuwa pungufu.

“Mwaka uliopita wanufaika wa mikopo walikuwa 53,000 na mwaka huu wanufaika wanafunzi 25,700 pamoja na ongezeko la makadirio ya zaidi ya Sh bilioni 137 kwenye bajeti ya Mikopo bado wanafunzi wengi hawajafikiwa,” alisema.

Ufisadi Wagubika Shirika la Posta.....Bodi Yabaini Mikataba Mibofu, Rushwa na Upendeleo katika Ajira

0
0

Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Posta Tanzania (TPC) imebaini madudu lukuki, ikiwamo mikataba mibovu, idadi kubwa ya wafanyakazi wenye elimu ya chini, rushwa na kuajiri kwa upendeleo. 

Akizungumza na wanahabari jana, mwenyekiti wa bodi hiyo, Dk Haruni Ramadhani alisema shirika linakabiliwa na “maradhi” mengi ambayo kama hayatashughulikiwa ipasavyo yanaweza kusababisha malengo kutotekelezwa kwa ufanisi. 

Kutokana na madudu hayo, bodi imeipa miezi sita menejimenti ya TPC kurekebisha kasoro hizo na kinyume na hapo, hatua kali za kisheria zitachukuliwa. 

“Tumebaini Shirika la Posta lina uwezo na fursa kubwa kama tutaitumia vizuri kuchangia Pato la Taifa. Ni shirika ambalo limesambaza huduma zake toka ngazi ya Taifa, kata na vijiji. Posta ina mizizi mingi mikubwa na imara,” alisema. 

“Kinachokosekana ni utashi na kujituma, ubunifu na utendaji kazi kwa weledi na umakini. Lazima sasa tubadilike, tuache kufanya kazi kwa mazoea, uzembe, ubinafsi, ufisadi, wizi na rushwa. Vitu hivi lazima tuambizane ukweli bila kuoneana aibu. Havina nafasi tena Posta,” alisema. 

Mikataba Mibovu 
Dk Ramadhani alisema wakati bodi hiyo ikiendelea na uchunguzi, imebainika shirika hilo liliingia mikataba mibovu ukiwamo ule wa kati ya TPC na kampuni ya Wande Printing and Packaging. 

Katika mkataba huu, bodi ilibaini kuwa Wande Printing and Packaging walipangisha jengo la ghorofa tatu (mali ya shirika) kwa Sh1.8 milioni kwa mwezi, kwa muda wa miaka mitatu ambayo ni sawa na Sh64.8 milioni. 

Alisema baadaye, mwekezaji alifanya ukarabati wa jengo kwa Sh398 milioni, hivyo ili kufidia fedha hizo, mkataba huo ulieleza Wande Printing and Packaging itakaa kwenye jengo hilo bila kulipa kwa miaka 20 ili kufidia fedha zake. 

Mwenyekiti huyo alisema mkataba mwingine ni kati ya TPC na kampuni ya Universal G & G ambao ulihusisha upangishaji wa jengo lililopo kitalu namba 416 Block G, Ubungo. Alisema katika mkataba huo Universal G & G na TPC waliingia mkataba wa kudumu na TPC ina hisa asilimia 25 na Universal asilimia 75. 

Kaimu Posta Masta wa TPC, Fortunatus Kapinga alisema waliingia kimakosa mkataba wa jengo la Posta lililo karibu na Mawasiliano Tower, na sasa wapo kwenye utaratibu wa kuzungumza na mwanasheria wa kampuni.

Pamoja na mikataba mibovu, Dk Ramadhani alisema baadhi ya watumishi wa shirika hilo wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya rushwa kwa kufanya malipo hewa kwa wastaafu wa Shirika la Mifuko ya Hifadhi ya Jamii wakitumia mfumo wa Post Giro. 

Post Giro ni mfumo wa kizamani wa malipo kutoka benki moja kwenda benki nyingine na mlipaji ndiye huidhinisha malipo yote. 

Mwenyekiti huyo aliyataja madudu mengine waliyobaini ndani ya shirika hilo kuwa ni kuwepo na tabia ya kupeana ajira kwa upendeleo, kupandishwa vyeo kwa rushwa, fedha au rushwa ya ngono. 

“Kwa mfano vijana walioteuliwa na ofisi ya General Manager, Corperate Resource Management baadhi yao wana dalili za kujihusisha na rushwa. Mfano watumishi waliokuwa na vyeti feki wengi wao walisaidiwa kuviondoa katika majalada yao,” alisema.

Pamoja na madudu hayo mwenyekiti huyo alisema wamebaini ufanisi unadorora kwa kuwa zaidi ya wafanyakazi 120 wana elimu ya darasa la saba na zaidi ya 1,000 wameishia kidato cha nne. 

“Wale wote wenye tabia ya wizi, umangimeza, rushwa, ubadhilifu na ufisadi hawana nafasi,” alisema. 

Dk Ramadhani alisema shirika hilo linasuasua kutokana na wingi wa madeni na hadi Juni, 2016 lilikuwa linadaiwa Sh20.5 bilioni. Kati ya fedha hizo, Sh16 bilioni ni makato ya wafanyakazi yanayotakiwa kwenda Mamlaka ya Mapato (TRA). 

Pia, alisema TPC inaidai Serikali Sh5.5 bilioni, taasisi za umma Sh1.9 bilioni, watu binafsi Sh1.8 bilioni na hivyo kulitaka kuongeza juhudi katika kukusanya madeni.

Watiwa Mbaroni Kwa kuvujisha mtihani FEKI wa kidato cha nne

0
0
Walimu wa Shule ya Sekondari Hasanga, iliyopo wilayani Mbozi mkoani Songwe na wafanyabiashara wawili, wanahojiwa na vyombo vya usalama mkoani Mbeya kwa tuhuma za kuhusika na utengenezaji wa mitihani feki ya kidato cha nne.

Watuhumiwa hao, James Kapinga (36) ambaye anadaiwa kufanya kazi Shule ya Sekondari ya Hasanga pia anajitolea kufundisha Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Sangu, Baraka Mwazambe (28), mfanyabiashara na mkazi wa Tunduma na mtaalamu wa masuala ya Tehama (IT), Alex Mochi.

Watu hao kwa pamoja inadaiwa walikamatwa juzi usiku baada ya mwanafunzi mmoja ambaye jina lake na la shule vimehifadhiwa kukutwa na mtihani wa somo la Kiingereza na alipobanwa, inadaiwa aliwataja wahusika hao.

“Mwanafunzi huyu ni wa shule nyingine tena si ya Mbeya, alikutwa na mtihani feki wa somo la Kiingereza, alipohojiwa alieleza mtihani huo ulitoka Mbeya na Serikali ilipofuatilia iliwabaini wahusika ambao walikuwa wanasambaza mitihani feki,” kilisema chanzo kimoja cha habari hii.

Akizungumzia sakata hilo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya, Mariamu Mtunguja, alikiri ofisi yake kupokea taarifa juu ya uvujaji wa mitihani na walipofuatilia walibaini mitihani hiyo ni feki.

“Mbeya hakuna mitihani iliyovuja kama inavyoelezwa katika mitandao, ukweli ni kwamba suala hilo lilifuatiliwa ilibainika mitihani inayosambazwa si ile iliyochapishwa na Baraza la Mitihani la Taifa, ni feki na baadhi ya wahusika wanahojiwa na vyombo vya dola,” alisema.

Naye Kaimu Ofisa Elimu Mkoa wa Mbeya, Benedict Sandy, alisema hakuna mitihani iliyovuja.

“Mitandao imekuwa ikitoa taarifa za upotoshaji eti mitihani imevuja, mitihani iliyosambaa na kukutwa na baadhi ya wanafunzi tena si wa Mkoa wa Mbeya ni feki na wahusika wanaodaiwa kuisambaza wamekamatwa.

“Nawaomba wanafunzi wazingatie yale waliyofundishwa, mitihani hiyo inakuja kwa lengo baya la kuwapotezea muda wao na mwisho wa siku kuishia kufeli, watu wanaofanya kazi hiyo wapo kimasilahi,” alisema.

Askari watatu wafukuzwa kazi mkoani Mwanza

0
0

Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza limewafukuza kazi askari watatu kwa tuhuma za kukiuka maadili ya kazi ikiwemo kujihusisha na vitendo vya utovu wa nidhamu pamoja na upokeaji wa rushwa.

Akizungumza na askari hao Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema kuwa hatua imechukuliwa ili iwe fundisho kwa askari wengine wanaokwenda kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Amesema askari mmoja kati ya hao alikutwa akiwa amelewa na kulala lindoni, huku wengine wawili wakituhumiwa kujipatia pesa kwa njia ya udanganyifu.

Kamanda Msanga amesema ukiukwaji wa maadili ni chanzo cha ongezeko la uhalifu hivyo hatamvumilia askari yoyote atakaye kwenda kinyume kwa kuwa kwa kufanya hivyo kunalichafulia hadhi jeshi la polisi kwa sababu ya makosa ya askari wachache.

Kamanda Msingi ametumia nafasi hiyo kuwakumbusha askari kufuata weledi wa kazi zao na kusema askari wanaotumia vyeo vyao kwa ajili ya kujipatia pesa kutoka kwa wananchi atawatumbua kabla kasi hiyo ya utumbuaji haijamfikia kwa kushindwa kuwasimamia.

Wapakistani Wahukumiwa Miaka Minne Jela Kwa Kuingiza Vifaa vya Mawasiliano Bila Leseni

0
0

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu raia watatu wa Pakistan, kifungo cha miaka minne jela au kulipa faini ya Sh milioni 125 baada ya kupatikana na hatia ya kuingilia mtandao wa mawasiliano na kuisababishia serikali hasara ya Sh milioni 145.

Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage, alitoa hukumu hiyo baada ya washtakiwa, Hafees Irfan, Mirza Irfan Baig na Mirza Rizwani Baig, kukiri makosa yao.

Akitoa adhabu hiyo, Hakimu Mwijage alisema, washtakiwa wamepatikana na hatia ya makosa manne na katika kila kosa watalipa faini ya Sh milioni tano au kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, ambayo ni sawa na faini ya Sh milioni 20 au kifungo cha miaka minne jela.

Aidha, alisema kwa sababu mashtaka yanahusisha kuisababishia hasara Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh milioni 35, pia washtakiwa wakimaliza kutumikia vifungo vyao, warud ishwe nchini kwao na vifaa walivyokutwa navyo vitakuwa mali ya serikali.

Awali, kabla ya hukumu hiyo, Wakili wa Serikali Esther Martin aliwasomea washtakiwa hao maelezo ya awali na kudai kuwa katika tarehe tofauti, Dar es Salaam, washtakiwa walikutwa na vifaa vya kuunganishia mawasiliano ya kimataifa bila kuwa na kibali cha TCRA.

Alidai, washtakiwa walitoka Pakistan na kwenda maeneo mbalimbali ikiwemo Arab Emirates, Malaysia, Msumbiji kwa ajili ya kutumia vifaa hivyo, pia waliingia nchini katika tarehe tofauti na kufikia kwenye chumba namba 905 katika Hoteli ya Butterfly iliyopo Kariakoo, Dar es Salaam.

Inadaiwa wakiwa kwenye chumba hicho, waliunganisha mawasiliano kwa kutumia vifaa vya kimataifa bila kuwa na kibali cha TCRA, lakini wakati wakiendelea na kazi zao ilibainika kuwa, kuna watu katika maeneo hayo wanatoa huduma ya mawasiliano, kinyume cha sheria.

Aliendelea kudai kuwa, Oktoba 5, mwaka jana, maofisa wa Polisi wakiambatana na TCRA walifika maeneo hayo na kufanya upelelezi, kisha wakawakamata washtakiwa hao katika hoteli wakiwa na vifaa mbalimbali vya mawasiliano, ambavyo ni kadi za simu 273, CPU 18, Laptop saba, Moderm ya Huawei na vocha zilizokwishatumika.

Washtakiwa walifikishwa kituo cha Polisi Kijitonyama na baada ya kufanya upelelezi, ilibainika kuwa wameisababishia serikali na TCRA hasara ya Sh milioni 140.

Baada ya kusomewa maelezo yao, washtakiwa walikiri makosa. Wakili Esther aliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa washtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine na makosa hayo, yasiwe yanajirudia rudia, adhabu itolewe kwa kuzingatia hasara walioisababisha washtakiwa, pia alidai makosa hayo yanahatarisha usalama wa taifa.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi, Shadrack Ishengoma aliiomba mahakama hiyo kuwapunguzia adhabu hiyo washtakiwa kwa sababu wamekiri makosa yao, pia wanategemewa na familia zao, na kuongeza kuwa washtakiwa wameshakaa rumande kwa miezi 13 yaani zaidi ya mwaka mmoja.

Hakimu Mwijage alisema ametoa adhabu hiyo kwa kuzingatia hoja za pande zote mbili na washtakiwa walilipa faini na kuachiwa.

Mawaziri Wasulubiwa Bungeni

0
0
Bunge la Jamhuri ya Muungano jana liliweka kando tofauti zao za kisiasa wakati lilipowaweka kwenye kibano mawaziri watano kutokana na utendaji wao.

 Wabunge wa chama tawala na upinzani walionyesha makali yao wakijadili Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2017/18 na Mwongozo wa Kuandaa Mpango wa Bajeti ya Serikali kwa mwaka ujao, ikiwa ni mwaka mmoja tangu Serikali ya Rais John Magufuli iingie madarakani.

 Mbali na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango, mawaziri wengine waliowekwa kwenye hali ngumu ni Ummy Mwalimu, ambaye ni Waziri wa Afya, Angellah Kairuki (Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi), Charles Mwijage (Viwanda, Biashara na Uwezeshaji) na Profesa Joyce Ndalichako (Elimu, Sayansi na Teknolojia). 

Mwongozo huo wa mpango wa kuandaa bajeti unaonyesha Serikali itatumia Sh32.9 trilioni kwa mwaka ujao wa fedha, ikiwa ni ongezeko la Sh3.4 trilioni kulinganisha na bajeti ya mwaka huu. 

Mjadala wa wabunge hao ulijielekeza katika kuchambua utendaji wa mawaziri hao na hali ilivyo kwenye wizara zao, hasa kiuchumi ambayo inaelezwa kuwa ngumu kutokana na wananchi kudai fedha zimepotea kwenye mzunguko.

Aliyefungua mashambulizi hayo ni mbunge wa Busega (CCM), Dk Raphael Chegeni aliyesema Dk Mpango ni msomi, lakini ana “kiburi, si msikivu na hataki kushauriwa”. 

Dk Chegeni alisema wabunge walimshauri mambo mengi waziri huyo katika Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa mwaka 2016/17, lakini hakutaka kusikiliza na ndiyo maana hali imekuwa ngumu kila eneo. 

‘’Dk Mpango unapaswa kuwa msikivu na kuacha kiburi. Tunayokushauri yachukue (kwa kuwa) tunakusaidia ufanye kazi.Tulikuambia mambo mengi, ukatudharau sasa yanatokea, kila kona hakuna unafuu,’’ alisema.

Dk Chegeni alisema uchumi ambao anauzungumziwa kwenye mpango wake hauendani na hali halisi ya maisha ya wananchi, akisema hata halmashauri hazijapewa fedha hadi sasa. 

“Wananchi hawana fedha, wabunge hawana fedha. Fedha ambazo Mamlaka ya Mapato (TRA) inaeleza kuwa inakusanya, ziko wapi wakati madeni yameongezeka?”

Alimtaka waziri huyo kutimiza wajibu wake kwa unyenyekevu na kwa kusikiliza ushauri wa wabunge kuhusu wizara yake.

“Umekuwa ni tatizo sana. Hata ukiitwa na jumuiya za wafanyabiashara huendi, ukiitwa na kamati ya Bunge ya Bajeti huendi.Umekuwa mgumu kupatikana, dhamana uliyopewa ni kubwa, usitumie vibaya mamlaka yako,” alisema Dk Chegeni. 

Mbunge mwingine aliyechangia alikuwa John Heche (Tarime Vijijini-Chadema), ambaye alisema mtu wa pili kutumbuliwa na Rais John Magufuli baada ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga atakuwa Dk Mpango. 

“Kwa sababu gani utakuwa ni wa pili kutumbuliwa? Kwa sababu mambo yanapokwama, mipango yote mliyopanga inapokwama, wewe ndiye unabebeshwa zigo hilo ili yeye aonekane yuko sawa wakati mnakosea wote,” alisema. 

Heche alisema wamesimamisha ajira kutafuta watumishi hewa kwa mwaka mzima, lakini wako vijana waliosomeshwa na baba zao wako mitaani kwa kukosa ajira. 

“Dada zetu wanajiuza, mikopo nayo hakuna, mnatafuta wanafunzi hewa. Kilimo nako mnatafuta wakulima hewa. Cha msingi mseme kuwa Serikali yenu imefilisika na hamuwezi kutekeleza kitu chochote, msaidiwe,” alisema. 

Mbunge wa Solwa (CCM), Ahmed Salum aliwataka wabunge wa CCM kumwambia ukweli Dk Mpango kuwa wanakwenda kugonga mwamba katika uchumi.

“Unajiuliza fedha zimekwenda wapi? Unakuja hapa unasema kuwa uchumi umekua, how (kwa vipi)? Twiga imeshakuwa taken over (imeshachukuliwa), CRDB imetangaza hasara na TIB hasara,” alisema. 

Alisema hali hiyo inaonyesha kuwa baada ya miaka miwili benki hizo zinakwenda kufungwa na huo utakuwa ni mgogoro wa kiuchumi nchini. 

Alisema hilo huenda linatokana na mawaziri kutokwenda kuomba kura na hivyo hawafahamu joto la maisha lililopo kwa wananchi majimboni. 

“Mimi natoka Jimbo la Solwa, unaahidi, unadanganya hadi unachoka. Alikuwa JK ameondoka, anakuja Magufuli ataondoka hakuna lililofanyika,” alisema. 

Aliitaka Serikali kurejesha fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii ilizoziweka “kabatini” Benki Kuu na mifuko hiyo iziweke fedha hizo kwenye benki za biashara ili fedha zianze kuzunguka.

Aliitaka Serikali kulipa madeni ya ndani ili fedha zianze kuzunguka na kwamba kumekuwa na joto hata ndani ya Bunge, akisema kuna ukata.

Salum alisema makusanyo ya kodi yanayotangazwa na kuonekana kuwa makubwa yanatokana na watu kulipa madeni ya nyuma na mara baada ya kuisha kwa malimbikizo hayo, makusanyo yatabaki kama ilivyokuwa wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne. 

“Watalipa itafika mahali itakwisha na kubaki na makusanyo ya siku hiyo, cash revenue (fedha taslimu). Hapo ndipo itashuka kutoka Sh1.5 trilioni hadi Sh800 bilioni iliyoachwa na Rais Jakaya Kikwete,” alisema. 

“Haya madeni yakiisha tutarudi kukusanya bilioni. Hatuwezi kufika trilioni hizo za leo. Tuna matatizo. Kipindi cha Kikwete, TRA ilikuwa inakusanya Sh850 bilioni, lakini nchi ilikuwa nzuri na mambo mengi yalienda vizuri kuliko sasa.” 

Alisema Rais Magufuli amekuwa na maono mazuri ya kuifanya nchi kufikia mafanikio ya Thailand, lakini tatizo wasaidizi wake hawamwambii ukweli ama wanaogopa kufukuzwa. 

“Magufuli tulikuwa naye hapa kwa zaidi ya miaka 10, namfahamu. Ukienda na data (takwimu) ukamueleza kukimbiwa na wafanyabiashara bandarini, atakuelewa,” alisema. 

Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussen Bashe alisema mipango ya Dk Mpango haifanani na ahadi walizozitoa kwa wananchi kuwa watawaboreshea hali ya uchumi watakapowachagua. 

“Kwa sababu kaka yangu (Dk Mpango) hujaenda kuomba kura? Dunia imebadilika tunaenda kufa tunapaswa kubadilika,” alisema Bashe. 

Alisema miradi mingine kama wa chuma wa Liganga na makaa ya mawe wa Mchuchuma ameanza kuisikia muda mrefu, lakini hajaona utekelezaji. 

Bashe alisema Waziri Dk Mpango anazungumzia bajeti ya Sh33 trilioni na kwamba eneo la kwanza ni makusanyo ya kodi kuongezeka kwa asilimia 16, wakati siyo mazuri. 

Alisema wabunge waliwahi kuwaambia wasiweke kodi kwenye uhamishaji wa fedha, utalii na maeneo mengine, lakini hawakuwasikia. 
 
Ndalichako 
Wakizungumzia hali ya elimu, wabunge walimkosoa Waziri Ndalichako kutokana na hali inavyoendelea, hasa suala la mikopo ya wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu. 

Akichangia eneo hilo, Heche alianza kwa kukosoa kitendo cha Profesa Ndalichako kwenda kupiga kura katika uchaguzi wa meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni uliofanyika wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam. 

“Leo elimu ni majanga. Mimi nilikuwa nakuheshimu sana Profesa Ndalichako ukiwa Katibu wa Baraza (la Mitihani la TaifaNecta). Umewahi kuonyesha watu wamechora mazombi kwenye mitihani,” alisema. 

“Wewe umepewa wizara hii, umechora Zombie kubwa kuliko wale waliochora kwenye mitihani, sijui hata wizi wa mitihani utazuiaje kama wewe Profesa ulitoka hapa kwenda kuiba kura Kinondoni.” 

 Alisema hivi sasa Bunge wamelifanya kama idara fulani ya Ikulu inayohusika na umwagiliaji maji katika maua. 

Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Wataira alisema Ndalichako alipiga kura za kuwachagua mameya wa halmashauri za manispaa za Kinondoni na Ilala. 

“Ulikuwapo juzi kwenye uchaguzi wa meya Kinondoni wakati ulishapiga kura katika umeya wa Ilala, Profesa mzima unahusika katika wizi wa kura,” alisema. 

Mwijage
Pia Waziri Mwijage alikuwa kwe- nye kikaangio hicho. Akichangia suala la mpango wa Serikali kuifanya Tanzania iwe nchi ya viwanda, Dk Chegeni alisema Mwijage ni “mzee wa sound” ambaye anafanya porojo. 

“Waziri wetu anajulikana kamamzee wa porojo, sijui hiyo Tanzania ya viwanda tutafika lini. Acheni maneno maneno na kusigana wenyewe kwa wenyewe. Mnatofautiana kauli, kila mmoja anaongea lake.  Fanyeni kazi kwa pamoja kila wizara itoe maoni yake katika huo Mpango,” alisema Dk Chegeni. 

Naye Heche alisema hata kwa Watanzania wanamjua Mwijage kwa jina la “Mzee wa Sound”. “Ukikutana naye hapo nje ukamsimamisha waziri, anauliza ‘vipi unataka nikupe kiwanda’ na kutoa mkono mfukoni. 

Anataka kuchomoa kiwanda mfukoni? Mpango wenu hamjajenga kiwanda hata kimoja,” alisema. 

Alisema kiwanda ndicho kitaajiri watu wengi wakiwemo mamantilie, wahasibu wahandisi na wengine wengi, lakini hadi sasa hakuna kiwanda hata kimoja. 

Kairuki 
Akizungumzia suala la watumishi hewa, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo) Zitto Kabwe alionyesha kushangazwa na kitendo cha mawaziri kutoa taarifa zinazotofautiana. 

 “Monthly Economic Review (taarifa ya uchumi ya mwezi) ya Agosti 2015 inaonyesha kwamba wages and salaries (mishahara) ambazo Serikali ililipa Juni mwaka 2015 zilikuwa Sh456 bilioni. 

"Monthly Economic Review ya Agosti 2016 inaonyesha kwamba wages and salaries ambazo Serikali imelipa kwa mwezi Juni 2016 ni Sh534 bilioni,” alisema Zitto.

“Kwamba kuna nyongeza ya gharama za mishahara ya kila mwezi ya Sh78 bilioni. Waziri wa Utumishi jana ameeleza wanaokoa Sh19 bilioni kila mwezi kwa kuondoa watumishi hewa. Taarifa ya Benki Kuu inaonyesha kuwa tangu Serikali hii iingie madarakani, gharama za watumishi kwa mwezi zimeongezeka kwa Sh78 bilioni.”

 Zito alisema pamoja na watumishi hewa kuondolewa, ajira mpya kuzuiwa na nyongeza ya mishahara kusimamishwa, gharama za mishahara zimeongezeka kwa Sh78 bilioni. “Haiekeweki. 

Kuna mmojawapo kati ya hawa wawili (Waziri Kairuki na BOT) anadanganya umma. Ama zoezi la watumishi hewa ni publicity stunt (la kujitafutia umaarufu) au Serikali inatumia fedha kwa matumizi mengine, halafu BOT inasema ni mishahara,”alisema Zitto.

Zuku TV Yaboresha Chaneli Ya Zuku Swahili, Yaja Na Sura Mpya

0
0
Pichani ni mwakilishi kutoka bodi ya filamu Tanzania Ndg. Aboubakar Kimario, akizungumza na waandishi wageni waliohudhuria uzinduzi wa chaneli ya Zuku Swahili

**
Zuku TV imezindua kwa upya chaneli ya Zuku Swahili ambayo itakuwa na vipindi vipya vya kusisimua vilivyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa Tanzania.

Zuku Swahili  inalenga kuwa chaneli bora zaidi ya burudani kwa Watanzania na itaonyesha vipindi vipya mbalimbali vya burudani kama vile  Bongo Movies, Bongo Swahili Series, Bongo Star Search, Bongo Secular Music (muziki wa bongo), Bongo Taarab, Bongo Comedies, Bongo Weekly Gossip, Bongo Gospel,  Bongo Cooking Shows pamoja na vipindi vingine vingi. Chaneli ya Zuku Swahili Movies itabadilishwa kuwa Zuku Swahili namba 210, chaneli yenye vipindi mbalimbali za burudani kuanzia Novemba 13, 2016

Akizungumza katika uzinduzi, Meneja Mkuu wa Zuku TV Tanzania Bw. Omari Zuberi alisema, "Tunafurahia kuzindua kwa watanzania na wateja wetu muonekano mpya wa chaneli ya Zuku Swahili ambayo itatoa burudani bora zaidi za kibongo. Chaneli hii ni ushahidi wa dhamira yetu kwa watanzania na tumejipanga kukidhi mahitaji ya watazamaji na kujenga maudhui kwa wakati na  kuvutia" alisema.

Chaneli ya Zuku Swahili  inapatikana kwenye vifurushi vyote vya Zuku kuanzia  kifurushi cha  Zuku Smart kwa Tsh. 8,999, kifurushi chetu cha  bei nafuu zaidi chenye chaneli zaidi ya  36 za bure ikiwa na chaneli za kitanzania na kimataifa na kupatia kipaumbele  chaneli na mahudhui ya asili ya kiafrika.

Pia, Zuku TV itazindua filamu tatu mpya kupitia chaneli ya Zuku Swahili namba 210, filamu hizo ni Task Force Unit - (filamu ya upelelezi), Najifunga - (filamu ya hatma ya Albino)   - na Wakoloni Weusi - (filamu ya rushwa katika Ofisi Kubwa ) na zinatarajiwa kuoneshwa mwezi wa Desemba 2016. Zuku imewekeza kwa asilimia kubwa na kuchangia ukuwaji wa sekta ya burudani na uzalishaji wa maudhui ya ndani Afrika Mashariki. 

Kwa Tanzania, Zuku imewekeza zaidi ya TZS 21bn katika upatikanaji filamu za ndani ya nchi ambazo zimeonyeshwa katika nchi za Tanzania, Kenya, Zambia,Uganda na Malawi.


Wasanii nguli wa Filamu nchini Tanzania wakiongozwa na Chick Mchoma na JB walihudhuria uzinduzi huo. Chaneli ya Zuku Swahili itakuwa ni kituo chako cha burudani kwa filamu zote za Bongo.
Pichani ni Raisi wa TAFF ndg. Simon Mwakifamba akizungumza na wageni waliohudhuria uzinduzi wa chaneli ya Zuku Swahili jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Zuku Tanzania, Ndg. Omari Zuberi akiongea jambo na Meneja msaidizi Zuku Tanzania, Bi. Veneranda Raphael katika uzinduzi wa Chaneli ya Zuku Swahili.

Kesi ya SCORPION Yapigwa Kalenda

0
0
Upande wa Jamhuri kwenye kesi ya Salim Njwete  maarufu kama 'Scorpion' anayetuhumiwa kumwibia Saidi Mrisho na kumtoboa macho kwa kisu umedai mahakamani hapo kwamba upelelezi haujakamilika na kuomba siku nyingine ya kukamilisha.

Mshitakiwa Njwete 34,  anashitakiwa kwa kumwibia Mrisho na kumjeruhi kwa kumchoma tumboni, mabegani na machoni.

Taarifa ya upelelezi kutokamilika ilielezwa jana na Mwendesha Mashitaka Chensensi Gavyole mbele ya Hakimu Mkazi Flora Haule kesi hiyo ilipotajwa na kuangaliwa kama upelelezi umekamilika.

“Mshitakiwa yuko mbele ya Mahakama hii lakini upelelezi haujakamilika, tunaomba Mahakama itupangie siku nyingine ya kutajwa kutokana na upelelezi kuendelea,” alisema Gavyole.

Kutokana na sababu hizo, Hakimu Haule aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 16 itakapotajwa tena.

Mshitakiwa huyo maarufu kama Scorpion alifikishwa mahakamani hapo akiwa kwenye gari dogo la mizigo tofauti na siku za nyuma ambapo alikuwa akiletwa akiwa kwenye basi la Magereza.

Awali ilidaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 9 Buguruni Sheli alipomwibia Mrisho fedha na vitu vyenye thamani ya Sh 476,000 na kumjeruhi kwa kumchoma kisu tumboni, mabegani na machoni.

Live: Maswali na majibu kwa Waziri Mkuu Bungeni Dodoma

0
0
Tazama hapa moja kwa moja kutoka Bungeni, Bunge la kumi na moja, kipindi cha maswali na majibu kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, kisha maswali ya kawaida kwa Serikali. Bofya hapa kutazama

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 83 & 84 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

0
0
MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA

ILIPOISHIA
"KAMA MIMI SIJAKUWEKA, TUMBONI MWAÑGU MIEZI TISA, HUTO MUOA SHEILA, ILA KAMA NILIKUZA KWA UCHUNGU, BASI UTAMUOÀ SHEILA."
"HICHO KIBESI CHAKO WAPANDISHIE HAO WASICHANA WAKO, ILA SI MIMI MAMA YAKO. USIPO ANGALIA NITAMPOTEZA HUYO MBWA WAKO NA KITOTO CHAKE"
Mama alizungumza na kupiga hatua tatu mbele akanigeukia na kwaishara ya kidole chake, akaniamrisha nitangulie kwenye gari, huku yeye na mlinzi wake wakifwatia nyuma.

ENDELEA
   Katika siku ambayo nimejisikia vibaya ndani ya moyo wangu ni siku ya leo, sikutegemea kama mama yangu anaweza kumkataa mwanangu mbele yangu japo sijamuona, ila muonekano wa kwenye picha una dhihirisha kwamba Junio ni mwanangu wa damu. Kila nilipo mtazama aliye keti, pembeni ya siti yangu. Moyo ukazidi kuniuma, kiasi cha kutamani nishuke ndani ya gari, nitembee hata kwa miguu kurudi nyumbani.

Tukaafika nyumbani nikawa wa kwanza kushuka ndani ya gari. Sikuelea chumbani kwangu kuepusha kelele za Sheila, ambaye muda wote, mama anamchukulia Sheila kama mtoto mdogo. Chochote anacho kihitaji anakipata.
"Shem, mbona umekaa huku bustanini, peke yako”
Sauti ya ndugu wa Sheila anaye itwa Blanka, niliisikia ikinisemesha, nyuma yangu

"Hapana nina punga punga upepo"
"Ahaaa, basi nilijua kwamba hjarudi na mama"
"Nimerudi"
Blanka akakaa pembeni yangu, huku akivua viatu vyake na kuvisogeza pembeni
"Shem mbona kama, haupo sawa, unaumwa?"
Nikatingisha kichwa kumjibu Blanka
"Sasa n nini tatizo shem wangu? Sasa hivi ulitakiwa uwe ndani unafuraha"
"Hapana, nina furaha"
"Shem huna furaha, au dada amekudhi?"
"Hapana, kuna maswala yangu yakibiashara kidogo ndio ninayafikiria"
"Ahaaaa, ila shem kuna kitu nahitaji kukuuliza"
"Kitu gani?"
"Unampenda kweli dada Sheila?"
Ikabidi nimtazame Blank vizuri machoni mwake.
"Mbona umeniuliza hivyo?"
"Yaa nàhitaji kujua, kwa maana kuna vitu hapa nyuma vilikua vinaendelea"
"Sijakuelewa, vitu gani vilikua vinaendelea?"
"Kuna mambo alikua anayafanya dada Sheila, kwa upande wangu sijayapenda isitoshe anakwenda kufunga ndoa na wewe, sizani kama anastahili kua mkeo"
Moyo ukaanza kunienda mbio, nikamgeukia vizuri Blanka, kabla sijamuuliza kitu, nikamuona mama akija sehemu tulipo.

"Ina bidi uongeze juhudi kwenye masomo, isitoshe unasoma masomo ya udaktari, ujitahidi sana"
Ilinibidi kubadilisha mada, ili mama asielewe ni kitu gani tunazungumza. Chakumshukuru Mungu Blanka alinielewa maana yangu ya kubadili mada tuliyo kua tukiizungumza.
"B wezako wanakutafuta kule ndani"
"Ahaa sawa mama"
Blanka akanyanyuka na kuondoka, mama akakaa sehemu nilipo. Ukimya wa sekunde kadhaa ukakatiza, sikua na kitu cha kuzungumza.
"Hivi Eddy, ni nani aliye kuroga?"
"Hakuna"
"Nimempigia mchungaji simu, aje kukuombea"
"Ili iweje"
"Eddy wewe si bure, utakua umerogwa"
"Mama na elimu yako hiyo yote yaani una amini kwamba mimi nimerogwa?"
"Tena sana, na aliye kuroga amesha fariki"
Laiti kama añgekua si mama yangu, aliye nibeba tumboni mwake miezi tisa, ningemtandika ngumi, ambayo asinge isahau maisha yake yote.

"Na kama nilivyo kuambia, mtoto uliye naye mimi simtambui, na huyo mama yake naye simtambui. Sasa ole wako unidhalilishe kwa wageni nilio waalika. Haki ya Mungu naapa nitakuachia laana."
Mamà akanyanyuka, nakujifunga tenge lake vizuri.
"Na sitaki siku hata moja huyo mwanangu Sheila ajue, kwamba unamtoto. Akijua na kuchukua maamuzi mabaya utajuta"
Mama àkaondoka na kuniacha nikibaki nikimsindikiza kwa macho, yaliyo jaa hasira.
Kitu kilicho anza kuniumiza kichwa, nikuhitaji kujua ni mambo gani aliyo kua akiyafanya Sheila, kipindi ambacho mimi sikuwwepo. Nikaanza kuamini kwamba Blanka atakua ni msaada mkubwa sana kwangu.

Usiku sikuamini kumuona mchungaji akiwa ameketi kwenye sofa za sebleni, akizungumza na mama. Wakaniita, nikajumuika nao kwenye mazungumzo, mimi na mchungaji tukaingia kwenye chumba cha maombi, kilichopo ndani ya hili jumba jipya la mama.
  Bila hata mchungaji kuniuliza swali, lolote akaanza kuniombea huku akiuweka mkono wake juu ya kichwa changu
"Pepo mchafu uliyopo ndani ya kichwa cha huyu kijana toka kwà jina la Yesu kristo"
Mchungaji aliendelea kuniombea huku akinisukuma sukuma kichwa changu. Zaidi ya nusu saa mchungaji aliendelea kunisalia
”Mchungaji, nimechoka kupiga magoti kama mapepo sina si tuachane na hii biashara bwana"
"Ohhhh shagara bagharaa, pepo wewe mchafu huwezi jibizana na mimi mtu wa Mungu, hapo ulipo toka kwa jina la Yesu"

Walichosema ACT kuhusu ahadi za Rais Magufuli katika uchaguzi wa mwaka jana

0
0
Na Regina Mkonde
Chama cha ACT-Wazalendo kimemkumbusha Rais John Magufuli kutekeleza ahadi yake aliyoitoa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka jana, kuwa serikali yake haitaruhusu mwanafunzi atakayefaulu kwenda chuo kikuu ambaye atashindwa kujiunga na elimu hiyo kwa kukosa ada ama mkopo.

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu leo amesema chama hicho kimetoa tamko hilo, baada ya takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kuthibitisha kuwa takribani wanafunzi 65,000 wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu, wanafunzi 20,000 ndiyo waliopata mikopo.

“Kwenye mikutano yake ya kampeni Rais Magufuli alitamba kuwa serikali yake hakuna mwanafunzi ambaye atafaulu kwenda chuo kikuu ambaye atashindwa kujiunga na elimu hiyo kwa kukosa mkopo. tunamtaka kutekeleza ahadi yake kwa vitendo.”

Ameongeza kuwa “Kwenye mikoa mingi iliyotembelewa viongozi wa chama wamepinga vikali utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao kama ukiachwa bila kupingwa utafanya watoto wengi kutoka familia masikini washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo,”

Shaibu amedai kuwa, kisingizio kinachotolewa na serikali cha kutilia mkazo kwenye kozi za kipaumbele hakistahili kutumiwa kwa kuwa ni kigezo cha kuwanyima watoto wa masikini haki ya kujiunga na elimu ya juu.

“Katika ilani ya ACT ya mwaka 2015 suluhisho la mikopo ya elimu ya juu limepambanuliwa vyema. kifungu 5.4.2 (v)(d) ya ilani yetu inapendekeza kuanzishwa kwa utaratibu wa scholarship kwa kozi za kipaumbele ili mkopo utumike kusomesha wanafunzi wengi zaidi wa kozi zinazosalia,” amesema.


Mahakama Yatoa kibali Tundu Lissu Akamatwe

0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, imetoa amri ya  kukamatwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu na kuamuru wadhamini wake kufika mahakamani hapo kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kutokana na mshtakiwa huyo kushindwa kufika kusikiliza kesi yake bila ruhusa.

Lissu na wenzake watatu wanakabiliwa na mashtaka ya uchochezi kupitia gazeti la Mawio.

Amri hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa kesi hiyo ilipangwa jana kutajwa lakini mshtakiwa wa nne Lissu hakuwepo mahakamani.

Hata hivyo, alijitokeza mdhamini wake mmoja kati ya wawili Robart Katula kudai kuwa mshtakiwa huyo anaendesha kesi ya uchaguzi Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Mwanza.

Hakimu alihoji kwa nini mshtakiwa amesafiri na kuacha kuhudhuria kesi yake bila kuomba kibali cha mahakama yake.

"Mshtakiwa Lissu anafanya dharau  kila wakati inapopangwa kesi yake mahakamani anashindwa kuhudhuria bila kutoa sababu ama kuomba ruhusa ya mahakama... kama asingekuwa nje kwa dhamana angefanyaje? angetumia busara kuomba ruhusa" alihoji na kuongeza kuwa.

"Wadhamini wa mshtakiwa wapelekewe wito wa mahakama waje kujieleza kwanini wasilipe fungu la dhamana kama walivyoahidi kwenye hati ya dhamana ya maneno ya Sh. milioni 10 kila mmoja" alisema Hakimu Simba.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Patrick Mwita aliomba mahakama hiyo kutoa hati ya kukamatwa mshtakiwa.

Hakimu Simba alikubali ombi la Jamhuri na kutoa amri ya kukamatwa mshtakiwa na wito kwa wadhamini kufika mahakamani Novemba 21, mwaka huu kujieleza kwa nini wasilipe fungu la dhamana dhidi ya mshtakiwa kwa kushindwa kuhudhuria kesi yake.
 
Mbali na Lissu, washtakiwa wengine ni, Wahariri wa gazeti la Mawio, Simon Mkina na Jabir Idrisa na mchapaji wa magazeti, Ismail Mehboob.

Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa kati ya Januari 12 hadi 14, mwaka huu,  Dar es Salaam, Lisu na wenzake  walikula njama ya kuchapisha chapisho la uchochezi katika gazeti la Mawio lenye kichwa cha habari kisemacho, ‘Machafuko yaja Zanzibar’.

Pia Lissu na wenzake walidaiwa  Januari 14, mwaka huu, Dar es Salaam, kwa nia ya kuleta chuki na uchochezi  kati ya wananchi na mamlaka halali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, walichapisha chapisho hilo lenye uchochezi.

Aidha, Lissu alidaiwa siku hiyo kinyume cha sheria na bila ya mamlaka waliwatishia na kuwatia hofu wananchi wa Zanzibar   wasiweze kuingia kwenye marudio ya Uchaguzi Mkuu.

Washtakiwa walikana mashtaka hayo kwa nyakati tofauti na wako nje kwa dhamana.

TANESCO Yaanza Mchakato Wa Kupeleka Umeme Kiwanda Cha Bakhressa Kama Ilivyoagizwa Na Rais Magufuli.

0
0

Na: Frank Shija & Daud Manongi, MAELEZO.
SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limeanza kutekeleza agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufu la kufikisha umeme kwenye kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Product kilichopo Mwandege mkoani Pwani.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco Makao Makuu, Leila Muhaji amesema kuwa agizo hilo limeshaanza kutekelezwa katika hatua mbalimbali na kuahidi kuwa litakamilika kwa wakati.

Muhaji amaesema kuwa agizo linapotolewa na Mhe. Rais kinachobaki ni utekelezaji tu, hivyo kufuatia agizo hilo Tanesco wameanza kufanya utekelezaji kwa kuchukua hatua kadhaa ili kuhakikisha wanakamilisha kulingana na wakati kama agizo linavyosema.

“Utekelezaji wa agizo la Mhe. Rais unaendelea na hadi kufikia mwezi Desemba tutakuwa tumefikisha umeme katika kiwanda hicho”. Alisema Bi. Muhaja.

Aidha alitumia fursa kutoa rai kwa uongozi wa kiwanda hicho kuanza uzalishaji punde umeme utakapofika kiwandani hapo ili kuongeza uzalishaji.

Kwa upande wake Meneja Ushirikiano wa Jamii wa Kiwanda cha Bakhressa Food Product Hussein Sufian Ally amesema kuwa wanamshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kuona umuhimu wa kupelekewa umeme kiwandani hapo.

Aliongeza kuwa utekelezwaji wa agizo hilo utakapo kamilika utasaidia kuongeza uzalishaji na kupunguza gharama ambazo kwa sasa zinachangiwa na matumizi ya Jenereta katika kuendeshea uzalishaji wa Kiwanda hicho.

Utekelezaji huu umefutia agizo la Rais alilolitoa tarehe 06/10/2016 wakati wa uzinduzi wa Kiwanda cha kusindika matunda cha Bakhressa Food Product ambapo alimuagiza meneja wa Tanesco Mkoa wa Pwani kuhakikisha ndani ya miezi miwili umeme uwe umefika kiwandani hapo
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images