Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

CHADEMA Waijibu CCM.......Wadai Lowassa ni Tishio Ndo Maana Wanamwandama, Waitaka CCM Ijiandae Kuachia Madaraka 2020

0
0

Baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia msemaji wake Christopher Ole Sendeka kusema kuwa aliyekuwa mgombea wa kiti cha urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Edward Lowassa, kuwa si tishio kwa CCM.

Jumamosi ya Oktoba, 29 Chadema imejibu kuwa Lowassa pamoja na Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) utaendelea kuwa tishio kwa chama hicho na kwamba CCM ijiandae kuachia madaraka mwaka 2020 kwa kuwa imejipanga kuchukua dola.

Mkuu wa Idara ya Uenezi Chadema Taifa, Hemed Ali wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya chama hicho, jijini Dar es Salaam amesema Lowassa ni tishio kwa kuwa alipokihama chama hicho aliacha mpasuko na kudai kuwa aliondoka na nguvu ya chama hicho.

“CCM wana homa kubwa iitwayo Lowassaphobia na ndio maana imeacha kuendelea na shughuli zao na kumuandama Mjumbe wa kamati kuu wa chama chetu Lowassa. Kimsingi mchakato wa kumpata Mgombea Urais na Mgombea mwenza wa chama chetu ulikuwa wa kidemokrasia kwa mujibu wa katiba yetu ambapo ibara (7.7.16 (a) kamati kuu inapewa mamlaka ya kuwafanyia utafiti wagombea Urais wa chama chetu na kupeleka ripoti Baraza kuu,

“Baraza kuu la chama kwa mujibu wa katiba ( 7.7. 13 (a)) inapendekeza majina ya wagombea au mgombea aliejitokeza na hatimae kwa mujibu wa katiba (7.7.10 (c)) Mkutano mkuu wa chama utachagua mgombea Urais na Mgombea Mwenza,” amesema na kuongeza.

” Lowassa alipitia hatua zote kama mwanachama halali wa CHADEMA mwenye haki sawa na mwanachama yeyote kwa mujibu wa katiba (5.1) na (5.2) kimatendo na kiimani kwa kufuata katiba , nilitaraji Sendeka aeleze kile kiini macho cha kumchagua Ndugu Magufuli Dodoma kuwa Mgombea wao huku wenyewe kwa wenyewe wakipinga mchakato wa kumpata usiofuata katiba na kanuni za chama hicho kama walivyojitenga na uamuzi huo baadhi ya wajumbe wa kamati kuu ile kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wa maamuzi ndani ya vikao.”

Amedai kuwa, Kamati Kuu yao ilipasuka katikati baina ya wajumbe wake na kudai kuwa wajumbe waliokuwa wanamuunga mkono Lowassa, wengi wao hawakuchaguliwa kushika nyadhifa serikalini .

“Ni kawaida ya CCM kuchafua mtu ambae atakua na msimamo na nia ya kulivusha taifa , Wamefanya hivyo kwa viongozi wetu wa chama na watu binafsi hivyo hatushangai walivyo mshambulia Lowassa akiwa ndani ya CCM na hata Sasa CHADEMA. Sendeka amesema kuwa yupo kiongozi ndani ya chama chetu aliyepata dola milioni 15 takribani bilioni 33 eti apangesafu ya uongozi ndani ya chama,

“Kiuhalisia na kwa hesabu ndogo tu ni kuwa pesa hiyo si tuu kuwa inatosha kwa ajili ya kupanga uongozi ndani ya chama bali ni inatosha kwa ushindi wa mitaa, kata na halmashauri , ubunge na urais hivyo wakati anataja tarakimu hizo ajue na michanganuo ya kimahesabu badala ya kuwa mkurupukaji na ningemuelewa kama angekuja hadharani kuaga rasmi kwa niaba ya chama chake na kutupisha kuwatumikia watanzania kuliko kuongea uongo,” amesema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Octoba 30

Sumaye adai Amepata taarifa ya Kutimuliwa Nyumbani kwake pia

0
0
Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye amesema kuwa baada ya kutangazwa mchakato wa kunyang’anywa shamba lake la Mwabwepande, amepata taarifa ya kutaka kuondolewa anapoishi pia.

Sumaye ametoa kauli hiyo ikiwa ni siku chache baada ya Waziri Wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kueleza kuhusu kuanza rasmi kwa mchakato wa kumnyang’anya mwanasiasa huyo shamba la Mwabwepande kwa madai ya kutoliendeleza kwa muda mrefu.

“Hapa ninapoishi naambiwa kuna maelekezo yametoka juu kuwa sijapaendeleza. Sasa kama sijapaendeleza mbona ninaishi hapahapa,” Sumaye amekaririwa na gazeti la Nipashe.

Aidha Sumaye amesema kuwa ingawa alimsikia Waziri Lukuvi akieleza kuwa tayari wameshampa notisi ya siku 90 kuhusu kunyang’anywa shamba lake la Mwambwepande, hadi jana hajaipata notisi hiyo licha ya kufanya jitihada za kuifuatilia.

Alisema kuwa anashangazwa na uamuzi huo wa Waziri kwani kesi inayolihusu shamba hilo bado inaendelea mahakamani kutokana na uvamizi wa wananchi na kwamba Mahakama imezitaka pande zote mbili kutofanya chochote kwenye ardhi hiyo.

Mwanasiasa huyo ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chadema alisema kuwa anachokifahamu ni kwamba alipokea notisi ya kuondolewa katika shamba lake la Mvomelo kwa madai ya kushindwa kuliendeleza kwa muda mrefu.

“Ninachokijua ninaandamwa kisiasa. Shamba langu la Mvumelo naambiwa sijaliendeleza. Kwenye hilo shamba nimejenga nyumba ya kuishi, ghala, kuna trekta na vifaa vingine. Ninalima mazao na nimefuga zaidi ya ng’ombe 200, nina kondoo 300 na nimechimba visima viwili vya maji halafu serikali inasema sijaliendeleza,” alisema Sumaye.

Alisisitiza kuwa ingawa anaamini anaandamwa kisiasa kwa kunyang’anywa mashamba yake, hatarejea CCM hata akinyang’anywa mashamba yote aliyoanayo.

Sumaye alihama CCM mwaka jana, miezi michache kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu na kujiunga na harakati za kumpigia kampeni mgombea urais kwa tiketi ya Chadema, Edward Lowassa. Baada ya uchaguzi huo alitangaza kujiunga rasmi na Chadema.

Polisi Wazuia Mkutano wa Maalim Seif........Wamlinda Profesa Lipumba

0
0
Wakati polisi ikizuia mkutano mkuu maalumu wa CUF uliopangwa kuhudhuriwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad mjini Tanga jana, mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba alifanya usafi soko la Buguruni, huku akilindwa na jeshi hilo. 

Lipumba alifanya kazi hiyo akitekeleza agizo la Rais John Magufuli la kufanya usafi Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi. Msemaji wa CUF, Abdul Kambaya alisema haoni kama ni jambo la ajabu kwa Lipumba kufanya usafi wakati akilindwa.

“Sioni mantiki ya swali hilo, suala la kulindwa Lipumba siyo wa kwanza,” alisema 

Mapema jana, polisi mjini Tanga ilizuia mkutano uliopangwa kuhudhuriwa na Maalim Seif ambao ulipaswa kuwajadili madiwani 12 waliopigana wiki iliyopita katika ofisi za chama hicho wilayani humo, baada ya kugawanyika kuhusu uamuzi wa wenzao waliohudhuria baraza la madiwani wa jiji hilo Oktoba 12.

Taarifa ya jeshi hilo ilidai kuzuiwa kwa mkutano huo ni kutokana na tisho la uvunjifu wa amani na kuwapo kwa makundi mawili yanayozozana. Mkutano huo ulipangwa kufanyika katika Hoteli ya Mkonge mjini hapa.

Pia, taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga, Idd Abdallah ilisema ukumbi ambao mkutano huo ungefanyika ni mdogo kutokana na wingi wa wanachama.

 “Ukumbi uliopangwa kufanyika kwa mkutano huo ni mdogo na ikumbukwe kuwa wiki iliyopita mkutano wa chama hicho ngazi ya wilaya ulivunjika kutokana na vurugu,” alisema

Akizungumzia sakata hilo, Mwenyekiti wa CUF wa wilaya hiyo, Rashid Jumbe alisema hata kama jeshi hilo limezuia mkutano huo, lengo la chama kuwajadili madiwani hao liko palepale. 
Alisema kamati ya utendaji imependekeza madiwani saba kati ya 12 wafukuzwe uanachama kutokana na kukiuka msimamo wa chama na watano watabaki chini ya uchunguzi.

“Katika fagio hili mbunge (Mussa Mbaruku) pia yumo kwani naye alishiriki kikamilifu pamoja na naibu meya (Mohamed Aniu), kwa sasa tunafanya utaratibu na jeshi la polisi kutekeleza masharti na vigezo wanavyotaka ili kuufanya mkutano huo tena,” alisema.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatatu ya Octoba 31

Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 30 Oktoba, 2016 amemteua Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA).

Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi huo umeanza tarehe 29 Oktoba, 2016.

Jenerali Mstaafu George Marwa Waitara ni Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Mstaafu.

WAKATI HUO HUO,Rais Dkt. Magufuli amemteua Dkt. Eligy Mussa Shirima kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Mifugo Tanzania (TALIRI)

Uteuzi wa Dkt.Shirima umeanza tarehe 29 Oktoba 2016.

Kabla ya uteuzi huu Dkt. Eligy Mussa Shirima alikuwa Mtafiti Mkuu na Msimamizi wa Utafiti wa Nyama ya Ng'ombe Makao Makuu ya TALIRI. 

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Rais Magufuli kufanya ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya Kuanzia Kesho

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 31 Oktoba, 2016 ataanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini Kenya kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais Magufuli anatarajiwa kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Jijini Nairobi majira ya saa nne asubuhi na baadaye kupokelewa rasmi na mwenyeji wake Rais Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi ambako viongozi hao watafanya mazungumzo rasmi.

Pamoja na kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, Rais Magufuli atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta Ikulu Jijini Nairobi

Katika ziara hii Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na pia anatarajiwa kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Barabara hiyo mchepuko ya Southern By-pass ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inaunganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini na imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika Jiji hilo.

Rais Magufuli anatarajiwa kumaliza ziara yake tarehe 01 Novemba, 2016 na kurejea Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Basi La Abiria Lateketea Kwa Moto Kimara Stop Over Jijini Dar......Mtu mmoja Afariki, 16 Wajeruhiwa

0
0
Basi  la abiria kutoka mkoani Dodoma, Safari Njema na lori lenye tela lililokuwa limebeba mifuko ya saruji, yameteketea kwa moto na kusababisha kifo cha mtu na msongamano wa magari kwenye Barabara Kuu ya Dar – Morogoro. Magari hayo yameungua baada ya kugongana jana mchana.

Ajali hiyo ilitokea saa nane mchana.baada ya lori kupoteza mwelekeo na kuligonga basi ambalo lilijaribu kulikwepa, lakini likagongwa ubavuni na kusababisha mlipuko na kuwaka moto magari yote mawili.

Basi hilo lina namba za usajili T 990 AQF wakati lori liliteketea kabisa kichwa chake, lakini tela lake lenye namba za usajili T 534 BYJ limebaki.

Ajali hiyo ilitokea katika eneo la Garage, Kimara kati ya Suka na Stop Over wilaya mpya ya Ubungo katika Barabara Kuu ya Dar – Morogoro, na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye ameungua moto kiasi cha kutotambulika.

Watoto watano na wadada wanne wameripotiwa kuokolewa dakika 15 baada ya magari hayo kuwaka moto, huku abiria wengine wa basi hilo wakiruka kwa nia ya kuokoa maisha yao katika ajali hiyo mbaya.

Hadi jana saa 12.30 jioni, bado magari hayo yalikuwa eneo la ajali na kulikuwa na msururu mrefu wa magari kutoka eneo la Mbezi kwenda jijini Dar es Salaam pamoja na kutoka jijini Dar es Salaam kwenda nje ya Jiji na mikoani na abiria walikuwa wakitembea kwa miguu.

Wakati huo askari wa trafiki ndio walifika eneo la tukio.

Akizungumza katika eneo la ajali jana saa 12.45 jioni, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Suzan Kaganda alithibitisha kifo cha mtu mmoja ambaye anaelezwa kuwa ni mtoto, na amehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa utambuzi zaidi.

Kamanda Kaganda alieleza kuwa ajali hiyo imesababisha majeruhi 16 ambao kati yao, 10 hali zao ni mbaya na wamelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wakati sita waliruhusiwa kurejea makwao baada ya kutibiwa kwani walipata mshtuko tu.


HESLB Yafafanua vigezo Utoaji mikopo.........Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa

0
0
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017.

Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu.

Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na 25,717 wa mwaka wa kwanza.

Katika mkutano na waandishi wa habari jana (Jumapili, Oktoba 30, 2016), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru alisema vigezo vikuu vinavyotumika mwongozo uliotangazwa na Bodi hiyo wakati ilipotangaza kuanza kupokea maombi mwezi Juni mwaka huu ambao unataja makundi makuu matatu ya watakaopata mikopo.

Vigezo vilivyotumika kutoa mikopo
Kwa mujibu wa Bw. Badru, kundi la kwanza linajumuisha wanafunzi waombaji wa mikopo wenye uhitaji maalum kama wenye ulemavu uliothibitishwa na Waganga Wakuu wa Wilaya na yatima ambao katika maombi yao waliwasilisha nakala za vyeti vya vifo zilizothibitishwa na makamishna wa viapo.

“Kundi la pili linajumuisha waombaji wa mikopo ambao baada ya uchambuzi wa taarifa zao walizowasilisha na baada ya kulinganisha na gharama za jumla za masomo yao ya sekondari, wamebainika kuwa wana uwezo mdogo wa kugharamia masomo yao ya elimu ya juu na hivyo kuwa na uhitaji zaidi wa mikopo,”
alisema Bw. Badru.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Badru alitaja kundi la tatu na la mwisho kuwa linajumuisha waombaji wa mikopo ambao wenye ufaulu wa juu katika matokeo yao ya kidato cha sita na wamechaguliwa kujiunga na fani za kipaumbele kwa taifa.

Fani hizo ni Sayansi za Tiba, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi wa Kilimo, Mafuta na Gesi na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

Makundi ya wanafunzi waliopata mikopo
“Hivyo basi, hadi sasa tumetoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 wakiwemo wanafunzi yatima 4,321, wenye ulemavu 118, wanafunzi wenye uhitaji waliosomeshwa na taasisi mbalimbali katika masomo ya sekondari (87), wanafunzi wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na wanafunzi wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele lakini wanaotoka kwenye familia duni 9,498,” alifafanua Bw. Badru. 

Sababu za kukosa mikopo
Katika mkutano huo, kiongozi huyo wa HESLB pia alieleza kwa kina sababu nyingine za waombaji 27,053 ambao hawajapangiwa mikopo.

Ametaja sababu hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya waombaji (90) kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30, waombaji mikopo waliopata udahili kwa sifa linganishi (equivalent qualifications) na waombaji waliomaliza masomo ya kidato cha sita zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Kundi jingine la waombaji waliokosa mikopo katika awamu ya kwanza ni waombaji waliopata nafasi katika vyuo kwa ufaulu wa mitihani waliyofanya kama watahiniwa binafsi (Private Candidates) na waombaji ambao hawakurekebisha fomu zao za maombi ingawa waliitwa kufanya hivyo.

Nafasi ya rufaa na uhakiki wa wanafunzi wanaoendelea na masomo
Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo pia amewataka waombaji ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo unaotangazwa, kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao utakaofunguliwa kuanzia katikati ya wiki hii.

“Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamekosa mkopo kwa kutowasilisha baadhi ya nyaraka ingawa tuliwaomba kufanya hivyo, hawa na wengine wenye sababu za msingi, watapata fursa ya kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao na nakala kuzituma kwa utaratibu tutakaoutangaza wiki inayoanza kesho(leo),”
alisema Bw. Badru.

Aidha, katika mkutano huo, Bw. Badru alisema bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kazi kuhakiki taarifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wanapata mikopo ya elimu ya juu kwa lengo la kubaini kama ni wana uhitaji wa mikopo hiyo kwa mujibu wa vigezo au hapana.

Katika zoezi hili linalotarajiwa kufanyika kwa siku 30 kuanzia mwezi ujao (Novemba, 2016), wanafunzi wote ambao ni wanufaika watalazimika kujaza dodoso maalum litakalokusanya tarifa za kiuchumi za wazazi na walezi wao ili kuweza kupata uhalisia wa sasa.

“Wanafunzi watakutana na dodoso katika akaunti zao katika mtandao wetu wa maombi ya mikopo (OLAMS) na watapaswa kujaza. Wale ambao hawatajaza dodoso hili kwa njia ya mtandao tutasitisha mikopo yao na wale ambao baada ya uchambuzi tutabaini hawana uhitaji, nao tutasitisha mikopo yao na watapaswa kuanza kurejesha fedha walizokopokea,’ alifafanua.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka 2005 kwa lengo la kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji waliopata nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wadaiwa walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994.

Polisi azua GUMZO baada ya kumpigia saluti Profesa Lipumba

0
0
Kitendo cha askari polisi kumpigia saluti Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa, Profesa Ibrahim Lipumba imezua gumzo la kuhoji uhalali wake.

Askari huyo alionekana juzi akimpigia saluti Profesa Lipumba katika eneo la Buguruni ambapo mwanasiasa huyo alienda kushiriki zoezi la usafi.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alipoulizwa kuhusu usahihi wa askari polisi kuwapigia saluti viongozi wa vyama vya siasa wasio wabunge alijibu kwa ufupi, “sio sawa.”

Kwa mujibu wa Kanuni za Jeshi la Polisi (PGO) namba 102, haiwataji viongozi wa vyama vya siasa wasio wabunge kati ya watu wanaopaswa kupewa salamu hiyo ya jeshi yenye kuonesha heshima.

Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Kapteni John Chiligati aliwahi kueleza Bungeni kuwa saluti ni ishara ya kuonesha heshima kwa kiongozi mkuu kwenye asasi za kijeshi.

Kapteni Chiligati alisema kuwa mbali na viongozi wa kijeshi, viongozi wengine wanaopaswa kupewa saluti ni wa mihimili ya Serikali, Bunge na Mahakama.

Wengine ni majaji wote, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mahakimu wa mikoa na wilaya wakiwa kwenye mahakama zao.

Katibu Mkuu wa Chama Cha CCK, Renatus Muabhi alisema kuwa huenda askari huyo alipiga saluti kwa kupaniki kutokana na maagizo aliyopewa ya kumlinda Profesa Lipumba katika zoezi hilo.

Serikali yakanusha kuuza Kisiwa Shungi Mbili

0
0
Serikali  imewahakikishia wakazi wa Wilaya ya Mafia na Watanzania wote kuwa Kisiwa cha Shungi Mbili kilichopo wilayani humo mkoani Pwani, hakijakodishwa wala kuuzwa kwa mtu yeyote kama inavyodaiwa na baadhi.

Badala yake, serikali imeingia mkataba na mwekezaji kwa ajili ya kufanya biashara ya hoteli ya kitalii ya hadhi ya nyota tano katika kisiwa hicho kwa kipindi cha miaka 20, uwekezaji ambao una manufaa zaidi kwa wananchi na serikali kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa hoteli hiyo iliyopewa jina la Thanda, Meneja Mkuu wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu nchini, Dk Milali Machumu alisema mwekezaji huyo ameingia mkataba huo na serikali kufanya biashara hiyo ikiwa ni sehemu ya kukiendeleza Kisiwa cha Shungi Mbili ambacho kilikuwa hakikaliwi na watu.

“Mimi niwahakikishie tu Watanzania kwamba serikali iliyoko madarakani chini ya Rais John Pombe Magufuli ipo makini na hizo tetesi za kuuzwa kwa kisiwa hiki mzipuuze, kwani kama mnavyoona pamejengwa hoteli ya kitalii kwa makubaliano na serikali na sio kuuzwa wala kukodishwa,” alisema Dk Machumu.

Alisema kufunguliwa kwa hoteli hiyo kutainufaisha serikali kwa kupata mapato kupitia kodi na kutengeneza ajira kwa wakazi wa Mafia pamoja na kuchochea maendeleo na pia wamezingatia sheria ya utunzani wa mazingira ya baharini.

Mkuu wa Wilaya ya Mafia, Shaibu Nunduma alisema kufunguliwa kwa hoteli hiyo kumetoa fursa nzuri ya ajira kwa wakazi wake na pia kutachochea kasi ya maendeleo kwa wilaya hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa hoteli hiyo, Pierre Delvaux aliishukuru serikali kupitia kwa Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu, Dk Machumu kwa kuwezesha uwekezaji huo, ambao machakato wake ulianza miaka 10 iliyopita.

Delvaux alisema hoteli hiyo ina vyumba vitano vya kulala, bwawa la kuogelea, maeneo ya michezo kama tenisi pamoja na vitu vyote vya kufurahisha na gharama yake ni Dola za Marekani 10,000 (sawa na zaidi ya milioni 20) kwa usiku mmoja.

Pia alisema wamezingatia manufaa kwa wakazi wa Mafia na hivyo kwa upande wa ajira asilimia 65 itakuwa ni kwa wakazi wa kisiwa hicho.

“Leo tumeizindua rasmi hoteli hii, lakini itaanza kufanya kazi katikati ya Novemba mwaka huu,” alisema Delvaux.

Kisiwa cha Shungi Mbili ambacho ni sehemu ya Wilaya ya Mafia mkoani Pwani ni miongoni mwa visiwa 15 ambavyo ni maeneo tegefu vilivyopo katika Bahari ya Hindi na hairuhusiwa kufanya shughuli yoyote ya uvuaji wa samaki.

Serikali Yazuia Mpango wa Mchungaji Lwakatare na Mrema Kuwalipia Faini Wafungwa

0
0
Serikali imesitisha shughuli iliyokuwa ikiendeshwa na Mchungaji Getrude Lwakatare ya kuwalipia faini wafungwa walioko magerezani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotolewa.

Mpango huo unaofanywa na Lwakatare kwa kushirikiana na Mwenyekiti wa Taifa wa Bodi ya Parole, Augustine Mrema tayari umewezesha wafungwa 78 kutoka magerezani baada ya kuwalipia faini inayofikia Sh25 milioni. 

Mkuu wa Magereza Mkoa wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema amepata maelekezo ya kusitishwa kwa mpango huo kutoka ngazi ya juu ya jeshi hilo. 

Alisema wananchi wengine bado wanaweza kuwalipia faini hiyo ndugu zao. Mrema alisema jana kuwa mpango huo ulilenga kupunguza msongamano magerezani na kuipunguzia Serikali gharama za kuwahudumia wafungwa.

Lowassa, Sumaye Wapiga Kambi Dodoma Ili Kuteta na Wabunge wa UKAWA

0
0

Mawaziri Wakuu wa zamani ambao ni wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na Frederick Sumaye wameweka kambi mjini Dodoma ili kuteta na wabunge wa Ukawa.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema kuwa wanasiasa hao wako mjini humo kwa ajili ya kufanya vikao na wabunge wa Ukawa ili kuweka mkakati na msimamo dhidi ya hoja mbalimbali zinazotarajiwa kuibuliwa katika vikao vya Bunge vinavyoanza kesho.

Moja kati ya hoja zinazotarajiwa kuwekewa msimamo ni pamoja na kuupinga muswada wa huduma za habari unaotarajiwa kujadiliwa na kupitishwa kuwa sheria.

“Tutakuwa na kikao cha kuweka msimamo wetu dhidi ya muswada hatari wa huduma za habari,” Mrema anakaririwa. “Vikao vimeshaanza na vitaendelea kesho (leo),”aliongeza.

Kwa mujibu wa Mrema, mbali na Lowassa, Sumaye na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, vigogo wengine wa Ukawa waliohudhuria vikao hivyo ni pamoja na Profesa Mwesiga Baregu, Profesa Abdallah Safari na Arcado Ntagazwa.

Picha: : Rais Magufuli aondoka Nchini Kwenda Kenya Kwa Ziara ya Kiserikali ya Siku Mbili

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 31 Oktoba, 2016 ameondoka nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini humo kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Rais Magufuli ameagwa na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es salaam, Paul Makonda na viongozi mbalimbali wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Mara baada ya kuwasili nchini Kenya, Rais Magufuli atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, na baadae atakwenda kutoa heshima katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta.

Mheshimiwa Rais pia anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa atakayoandaliwa na mwenyeji wake Ikulu Jijini  Nairobi.

Katika ziara hiyo Rais Magufuli anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi na pia kuzindua barabara mchepuko (Southern By-pass) iliyopo Jijini humo. Barabara hiyo ni moja kati ya miradi mikubwa ya barabara nchini Kenya, inayounganisha maeneo mbalimbali ya Jiji la Nairobi kwa barabara za juu na chini.

Jaffar Haniu
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar Es Salaam

31Oktoba, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisindikizwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. Hii ni safari yake rasmi ya tatu kwenda nje ya nchi toka aingie madarakani mwaka mmoja uliopita. Alisafiri kwa mara ya kwanza alikwenda Rwanda, kisha akaenda Uganda.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Naibu Balozi wa  Kenya nchini Mhe Boniface Muhia katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili  leo Oktoba 31, 2016
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea saluti toka kwa Inspekta jenerali wa Polisi (IGP) Ernest Mangu  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa tayari kwa safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi,  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda na viongozi wengine wakipunga mikono kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere wakati akianza  safari ya kwenda Nairobi, Kenya kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili leo Oktoba 31, 2016. PICHA NA IKULU

Bondia maarufu Tanzania Thomas Mashali afariki Dunia

0
0

Bondia maarufu wa ngumi za kulipwa nchini, Thomas Mashali amefariki dunia usiku wa kuamkia leo October 31 2016 maeneo ya Kimara DSM, 

Taarifa zinadai kuwa alishambuliwa na wananchi baada ya madai ya kuitiwa mwizi.

Taarifa kutoka kwa Promota wake, Siraji Kaike amesema watu aliokuwa anagombana nao walimwitia mwizi na wakawa wamemshambulia na kumtupa baadaye bodaboda waliokuwa wanamjua Thomas Mashali walimuokota na kumpeleka hospitali ambapo baadaye zilitolewa taarifa kuwa amefariki.

SMZ yatoa onyo kwa watakaoleta vurumai za kidini visiwani humo

0
0

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Ussi Gavu amesema Zanzibar inahistoria ndefu ya uvumilivu wa kidini na kuonya kwamba Serikali itawakuchulia hatua wale wote watakaolete chokochoko za kidini.

Akizindua jimbo mpya za ibada za Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania, Waziri Gavu alisema kwamba tofauti za imani ya dini kamwe isiwe chanzo cha kuigawa jamii na mifarakano.

“Ndugu zangu waumini, tofauti za dini isiwe chanzo cha mifarakano katika jamii, tujiepushe na aina yoyote ya uchokozi au mgawanyiko, daima tuwe wamoja wenye kuheshimu imani za dini nyengine” Alisema Waziri Issa Gavu.

Waziri Gavu alisema kwamba ni jambo la aibu kuona watu wanagombana kwa sababu ya tofauti za imani za kidini. Aliwataka wananchi kuendelea kutunza amani na kuongeza upendo miongoni mwao.

Alisema Serikali itaendelea kuheshimu imani za dini na kwamba kila mwananchi anawajibu wa kufuata sheria na taratibu za nchi na kuonya kuwa Serikali haitochelea kuwachukulia hatua za kisheria wale wote watakaovunja sheria za nchi.

Waziri Issa Gavu alisema kwamba Zanzibar ina historia ndefu ya uvumilivu wa kidini ambapo pia ina historia kongwe ya dini ya Uislamu na Ukristo.

Amewataka waumini wa kanisa hilo kuungana na waumini wengine katika kuhimiza umoja na mshikamano katika jamii na kusisitiza kwamba Watanzania wanawajibu wa kuishi kwa kuheshimiana, lakini pia kuvumiliana.

Katika hatua nyengine, Waziri huyo alisema Zanzibar imendelea kuwa sehemu tulivu na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kuitunza amani iliyopo.

Waziri Gavu alisema kwamba Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Machi mwaka huu ulifanyika katika mazingira tulivu huku waumini wa dini mbalimbali wakiendelea na shughuli za ibada zao bila kusumbuliwa.

Katika uzinduzi huo, Waziri Issa Gavu amewahakikishia waumini wa kanisa hilo kwamba Serikali itanedelea kushirikiana nao ili kuona kwmaba kila muumini wa dini anatekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi.

Na Dk. Juma Mohammed, Zanzibar

MWISHO

Picha 6: Rais Magufuli alivyowasili Nairobi nchini Kenya

0
0
Leo October 31 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliondoka nchini kuelekea Nairobi nchini Kenya kwa ziara ya Kiserikali ya siku mbili nchini humo kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Uhuru Kenyatta.

Rais  Magufuli  amewasili Nairobi kenya kwa ziara hiyo na amelakiwa na mwenyeji wake Rais uhuru kenyatta.

Taarifa kutoka Ikulu Kuhusu Siku ya kwanza ya ziara ya Rais Magufuli nchini Kenya

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema Kenya ni nchi inayoongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania ikilinganishwa na nchi nyingine za Bara la Afrika.

Rais Magufuli amesema hayo leo tarehe 31 Oktoba, 2016 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika Ikulu ya Nairobi nchini Kenya ambako ameanza ziara ya Kiserikali ya siku mbili kwa mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta.

Rais Magufuli ambaye kabla ya Mkutano huo na waandishi wa habari amepokelewa rasmi kwa kupigiwa mizinga 21 na kukagua gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima yake na baadaye kufanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta, amesema takwimu za kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC) zinaonesha kuwa Kenya ina jumla ya kampuni 529 zinazoendesha shughuli zake nchini Tanzania ambapo zimewekeza Dola za Marekani Bilioni 1.7 na zimeajiri watu 56,260.

Pia, Rais Magufuli amebainisha kuwa biashara kati ya Tanzania na Kenya imeongezeka kutoka Shilingi za Kitanzania Bilioni 652.9 hadi Shilingi za Kitanzania Trilioni 2.044.

“Naomba niwahakikishie kuwa uhusiano na ushirikiano wetu ni mzuri na utaendelea kuwa mzuri zaidi, na kwetu sisi Tanzania, Kenya ndio nchi ya kwanza kwa uwekezaji kuliko nchi zote za Afrika.

“Tunashirikiana vizuri katika uchumi, watu wetu wanafanya kazi pamoja, yapo makabila yetu ambayo yanaingiliana kwa shughuli zao za kila siku na hata wanyamapori wetu wanazunguka katika nchi zote mbili bila kujali mipaka” amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesisitiza kuwa Serikali yake itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na Kenya ulioasisiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais wa Kwanza wa Kenya Hayati Mzee Jomo Kenyatta na amewakaribisha wafanyabiashara wengi zaidi wa Kenya kuwekeza nchini Tanzania.

“Kabla ya kuja hapa nimekwenda kutoa heshima katika kaburi la Mzee Jomo Kenyatta, kwa kweli nimeguswa sana na kazi kubwa iliyofanywa na wazee wetu, naomba niwahakikishie kuwa tunawathamini sana ndugu zetu Wakenya na tutaendelea kufanya hivyo” amesisitiza Dkt. Magufuli.

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Uhuru Kenyatta amemshukuru Rais Magufuli kwa kukubali mwaliko wake na amemhakikishia kuwa Kenya itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Tanzania.

“Kwetu sisi Tanzania ni ndugu zetu, ni kaka na dada zetu tunao ushirikiano wa siku nyingi na wa kidugu na tutahakikisha tunauendeleza ushirikiano na uhusiano huu mzuri ulioasisiwa na wazee wetu” amesema Mhe. Kenyatta.

Rais Kenyatta amesema Tanzania na Kenya ni nchi zinazofanana kwa mambo mengi muhimu ikiwemo kubadilishana uongozi wa Serikali kwa njia ya amani na ameongeza kuwa katika mazungumzo yao wamekubaliana kuwa nchi hizi zitaendelea kuzisaidia nchi nyingine za Afrika Mashariki zinazokabiliwa na matatizo mbalimbali.

Aidha, Rais Kenyatta amesema Kenya itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kutekeleza miradi ya ushirikiano ikiwemo ujenzi wa miundombinu kama vile barabara ya Bagamoyo (Tanzania) hadi Malindi (Kenya) pamoja na mambo mengine ambayo Tume ya pamoja ya ushirikiano kati ya nchi hizi mbili (Joint Commission Cooperation) itayaainisha.

Baadaye leo, Rais Magufuli anatarajiwa kuhudhuria dhifa ya kitaifa katika Ikulu ya Nairobi aliyoandaliwa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta na Kesho anatarajiwa kutembelea kiwanda cha maziwa cha  Eldoville kilichopo Karen Jijini Nairobi, na  kuzindua barabara mchepuko ya Southern By-pass iliyopo Jijini Nairobi.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Nairobi

31 Oktoba, 2016

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Yatoa Siku 90 Kwa Waliokosa Mikopo Kukata Rufaa

0
0

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.

Serikali imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017.

“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kuingia katika mtandao wetu wahttp://olas.heslb.go.tzna kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.

ANGALIZO: Ada ya Maombi ya Tshs 10,000/- iliyopaswa kulipwa na waombaji mikopo kwa MPesa kwa ajili ya malipo ya Rufaa (HESLB) imefutwa.Taratibu nyingine zinabaki palepale

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Novemba 1

Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images