Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Kamati za Bunge kuanza vikao vyake wiki ijayo Mjini Dodoma

$
0
0

Vikao vya Kamati za Kudumu za Bunge vitaanza tarehe 17 Oktoba hadi tarehe 30 Oktoba 2016, Mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Tano wa Bunge uliopangwa kuanza tarehe 1 Novemba 2016. Kufuatia Ratiba hiyo ya shughuli za Kamati, Waheshimiwa Wabunge wote wanapaswa kuwa wamewasili Mjini Dodoma ifikapo Jumapili tarehe 16 Oktoba, 2016 kwa ajili ya kushiriki vikao hivyo.
 
Katika Vikao hivyo, shughuli zilizopangwa kutekelezwa na Kamati ni kama ifuatavyo:
  1. a) KUPOKEA MAONI YA WADAU WA MISWADA MBALIMBALI
Kamati mbili (2) za Kisekta zitajadili Miswada miwili ya Sheria ambapo Kamati ya Katiba na Sheria itajadili Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali, Na. 3 wa Mwaka 2016 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments)Bill, 2016] na itakuwa na vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya tarehe 21 Oktoba, 2016 katika Ukumbi wa Serengeti, Ofisi ya Hazina Mjini Dodoma kuanzia saa tano (5:00) Asubuhi ambapo Sheria hiyo ina jumla ya Sheria 9 zitakazofanyiwa marekebisho na Muswada huu.
 
Kamati nyingine ni Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii ambayo itajadili Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa Mwaka 2016 [The Media Services Bill, 2016] na itakuwa na vikao vya kupokea maoni ya wadau kuhusu Muswada huo siku ya tarehe 19 Oktoba, 2016 Katika ukumbi ulipo katikaJengo la Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mjini Dodoma kuanzia saa tatu kamili (3:00) asubuhi hadi saa Tisa(9:000) Alasiri.
 
Pamoja na kamati hizo mbili za kisekta, pia Kamati ya Sekta Mtambuka ambayo ni Kamati ya Bunge ya Sheria Ndogo nayo imepanga kufanya mikutano ya kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing)kuhusiana na Sheria Ndogo zilizowasilishwa na Serikali katika Mkutano wa Nne wa Bunge. Mikutano hiyo inatarajiwa kufanyika kati ya Jumanne tarehe 18 Oktoba, 2016 na Alhamisi tarehe27 Oktoba, 2016 katika Jengo la Hazina (Treasury Square) Mjini Dodoma.
 
Wadau wote katika Miswada tajwa hapo juu wanakaribishwa kufika mbele ya Kamati kutoa maoni yao katika tarehe na muda uliotajwa.
  1. b) KUPOKEA TAARIFA ZA KIUTENDAJI WA WIZARA
Kamati tisa (9) za kisekta zitapokea Taarifa za utendaji wa Wizara zinazosimamiwa na Kamati hizo kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (c) na (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo Januari, 2016.
  1. i) Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama itapokea na kujadili Taarifa za wawakilishi wa Bunge katika SADC – PF, ACP – EU na CPA kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (2) (iii) na (iv) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Januari, 2016.
  2. ii) Kamati ya Utawala na Serikali za Mitaa itafanya ziara mbili Mkoani Dodoma kwa lengo la kufuatilia utekelezaji wa majukumu ya Wizara inazozisimamia kwa mujibu wa Kifungu cha 7 (1) (d) cha Nyongeza ya Nane ya Kanuni za Kudumu za Bunge
iii) Kamati ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) itapokea na kujadili Taarifa za Uwekezaji unaofanywa na Mashirika/Taasisi za Umma tisa (9).
  1. c) UCHAMBUZI WA TAARIFA KUHUSU HESABU ZILIZOKAGULIWA
Kamati mbili za usimamzi wa Fedha za Umma zitafanya uchambuzi wa taarifa kuhusu Hesabu zilizokaguliwa kwa Mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2015 ambapo Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) itachambua taarifa kuhusu Hesabu zilizokaguliwa kwa Mwaka unaoishia tarehe 30 Juni, 2015. Katika kipindi hicho, jumla ya Mashirika/Taasisi tisa (9) na Maafisa Masuuli wa Mafungu (Votes) tatu (3) watakutana na Kamati kwa madhumuni hayo.
 
Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) itachambua Hesabu zilizokaguliwa za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2015, na Katika kipindi hicho, Hesabu za Halmashauri kumi na sita (16) zitajadiliwa.
 
Ratiba zote za Shughuli za Kamati za Bunge pamoja na Miswada itakayoshughulikiwa na Kamati katika kipindi hiki inapatikana kupitia tovuti hii ya Bunge.

Profesa Anna Tibaijuka amwakilisha Amwakilisha Rais Magufuli mkutanoni UN

$
0
0

Rais  Dk. John Magufuli, amemteua aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka kumwakilisha katika mkutano wa makazi wa Habitat III unaofanyika katika mji wa Quito,   Ecuador.

Taarifa iliyoituma kwenye mitandao ya  jamii na Profesa Tibaijuka jana, ilisema katika msafara huo amefuatana  na Katibu  Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Mandeleo ya Makazi, Dk. Yamungu Kayandabila.

“Hivi sasa niko Geneva, Uswisi kwa matayarisho nikielekea Quito Ecuador mkutano wa makazi duniani wa HABITAT III  kumwakilisha Rais wetu nikiwa pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi,namshukuru Rais kwa heshima hii kubwa, Sitamuangusha.

Habitat III,ni mkutano wa uamuzi na  mustakabali wa Shirika la Makazi Duniani na agenda ya maendeleo endelevu ya miji.

“Kama tunavyojua mkutano wa Habita I ulifanyika Vancouver,Canada mwaka 1976, Habitat II ulifanyika Istanbul, Uturuki mwaka 1996 na huu Ecuador Marekani ya Kusini 2016,”alisema.

Alisema kila baada ya miaka 20 wakuu wa nchi hukutana kukubaliana namna ya kuendeleza makazi kupitia Shirika la UNHABITAT ambalo aliwahi kuliongoza kwa miaka 10.

“Rais Magufuli alichaguliwa na kuongoza Baraza la Uongozi wa shirika hilo (Governing Council) kwa muhula wa mwaka 2006/2008 alipokuwa Waziri wa Ardhi.

“Wafanyakazi walimpenda kiasi kwamba alipobadilishwa wizara na kupelekwa  Mifugo na Uvuvi karibu iwe zogo ofisini kwangu wakidai tutayumba.

“Niliwatuliza na kuwaambia kumbadilisha wizara hakumuondolei uenyekiti wake na kweli aliendelea nao na kumaliza,”alisema Tibaijuka.

Alisema katika mkutano huo, jambo kubwa atakalolipigania ni utaratibu wa shirika hilo kuzisaidia nchi zinazoendelea kama sisi kwa kuzikopesha halmashauri zao fedha za miundombinu, bila kuilazimisha Serikali kuu kutoa dhamana kwa mikopo hiyo.

Alisema jambo hilo ni la msingi  kwa vile   huleta kasi ya maendeleo ingawa huwa linapingwa na wakubwa wanaotaka kukopa  kupitia Serikali kuu ili waibane kwa kutumia  Benki ya Dunia, kitendo  ambacho kinachelewesha kasi ya maendeleo.

“Tutajitahidi kulingana na maelekezo ya Rais tunayemwakilisha kuhusu msimamo wa nchi yetu na washirika wake ambao ni nchi za Afrika na za G77 na China,” alisema.

Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi kufuatia kifo cha Meya Mstaafu wa Jiji la Dar Dkt. Masaburi

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameitumia salamu za rambirambi familia ya Meya Mstaafu wa Jiji la Dar es Salaam Dkt. Didas Masaburi aliyefariki dunia jana tarehe 12 Oktoba, 2016 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

Katika salamu hizo Rais Magufuli amesema amepokea taarifa ya kifo cha Dkt. Didas Masaburi kwa mshituko na masikitiko makubwa na kwamba anaungana na familia ya marehemu, ndugu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu cha huzuni ya kuondokewa na mpendwa wao.

“Poleni sana familia ya Dkt. Didas Masaburi, najua huu ni wakati mgumu sana kwenu, lakini niwahakikishie kuwa sote tumeguswa sana na msiba huu kwa kuwa tumempoteza mtu muhimu, msomi mzuri, kiongozi aliyelitumikia Taifa kwa moyo wake wote na aliyesimamia kile alichokiamini” amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.

Aidha, Dkt. Magufuli amewapa pole wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wamempoteza Mwana CCM mwenzao pamoja na Viongozi na watumishi wa Jiji la Dar es Salaam ambao walifanya nae kazi alipokuwa Meya wa Jiji.

Amemuombea kwa Mwenyezi Mungu ampumzishe mahali pema peponi.

“Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amina” amemalizia Rais Magufuli.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

13 Oktoba, 2016

Nauli za ATCL zitakazotumika kuanzia Oktoba 14 hadi 28

$
0
0
Ndege mbili mpya za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q400 zinatarajia kuanza kazi wakazi  wa mikoa ya Mwanza, Arusha na Zanzibar watakuwa wa kwanza kupata ofa.

Ofisa Habari wa shirika hilo, Lilian Fungamtama amesema  safari  mpya za ndege hizo  ikiwamo ya Dar es Salaam - Mwanza, nauli iliyopangwa ni Sh160,000.

Amesema safari za  Dar es Salaam - Arusha nauli yake itakuwa Sh180,00 na Zanzibar - Dar es Salaam ni Sh85,000.

“Ofa hii imetolewa na ATCL kwa safari mpya za ndege hizo,” alisema Fungamtama.

Amesema hakutakuwa na safari ya moja kwa moja kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, lakini itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam -Arusha hadi Zanzibar.

 “Ndege ya kutoka Dar es Salaam kwenda Arusha ndiyo itakayokwenda kuchukua abiria Zanzibar haitatokea Dar es Salaam moja kwa moja,” alisema.

 Akifafanua kuhusu nauli hizo, Fungamtama alisema nauli  ya kutoka Dar kwenda Kigoma itakuwa katika madaraja mawili ambayo ilikuwapo tangu awali.

Amesema bado ndege hizo hazijaanza safari katika mikoa yote hadi hapo watakapotangaza.

Akizungumzia safari za nje ya nchi, alisema itakuwapo ya kutoka Dar es Salaam - Hahaya hadi Comorro ambayo nauli yake ni Sh543,950 kwenda na Sh926,650 kwa kwenda na kurudi.

 “Lengo letu ni kutoa huduma nzuri itakayomridhisha kila mteja,” alisema Fungamtama.

Kampuni ya Moladi Yaahidi kujenga nyumba za watumishi Dodoma......Nyumba ya Vyumba Viwili ni Milioni 20, Vyumba Vitatu Milioni 35

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameikaribisha kampuni ya ujenzi ya Moladi Tanzania ielekeze nguvu zake Dodoma ambako kuna mahitaji makubwa ya nyumba za watumishi.

“Natambua kuwa mnatumia teknolojia ya kisasa na ujenzi wa nyumba zenu unachukua siku chache sana. Ninawaencourage mje Dodoma ambako kuanzia Machi mwakani, watumishi wengi wataanza kuhamia huko,” amesema.

Waziri Mkuu ametoa wito huo jana mchana (Jumatano, Oktoba 12, 2016) wakati akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Bw. Abeid Abdallah ambaye alifika ofisini kwake Magogoni, jijini Dar es Salaam na kumuonyesha ramani ya nyumba za watumishi ambazo wanazitumia.

Waziri Mkuu alisema Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina maeneo ambayo imeyatenga rasmi kwa ajili ya viwanja vya makazi na anaamini katika muda wa miezi miwili wanaweza kujenga nyumba za kutosha watumishi wanaotarajiwa kuhamia katika awamu ya pili.

“Nimeangalia michoro yenu, nyumba za vyumba vitatu vya kulala zina hadhi ya kukaa hata wakurugenzi; na watumishi wa kawaida wanaweza kumudu zile za vyumba viwili vya kulala… ninawatia moyo mwende haraka Dodoma na wale ambao wako serious wataleta maombi yao mara moja,” alisema.

Waziri Mkuu alisema amefarijika kuona kuwa size ya ramani zao inatosha kwenye kiwanja cha ukubwa wa mita za mraba 550 ambacho ni high density na watumishi wengi wanaweza kumudu kuvinunua.

Kwa upande wake, Mkurugenzi huyo, Bw. Abdalla alimweleza Waziri Mkuu kwamba nyumba ya ukubwa wa vyumba vitatu vya kulala, yenye sebule, jiko, stoo na choo inatosha eneo la mita za mraba 94 tu.

“Kati ya vyumba hivyo vitatu, kimoja ni master, pia kuna sebule, chumba cha kulia na kibaraza. Hii inaanzia shilingi milioni 35 hadi milioni 41 kutegemea na aina ya vifaa unavyoweka kwenye umaliziaji. Lakini tukiongeza na servant quarter utalazimika kulipia shilingi milioni 7 ambapo unapata vyumba viwili na choo na bafu ndani,” alisema.

“Kimsingi, ni lazima tutaweka madirisha, milango, vyoo, masinki ya bafuni na jikoni, tiles (na mtu anaruhusiwa kuchagua za China, Italy au Spain),” aliongeza.

Akifafanua kuhusu nyumba yenye vyumba viwili vya kulala, Bw. Abdalla alisema nayo pia ina sebule, jiko, stoo na choo kimoja na inatosha eneo la mita za mraba 54. Alisema nyumba hizo zinaanzia sh. milioni 20 hadi 25 kutegemeana na aina ya vifaa vinavyowekwa kwenye umaliziaji.

Alisema ujenzi wa nyumba moja unachukua wiki sita na kama viwanja viko eneo moja au jirani, wanaokoa muda wa siku tatu hadi tano kwa kila nyumba.

 “Tunajenga ukuta kwa kumwaga theluji isiyochanganywa na kokoto ambayo ni mchanganyiko wa saruji, mchanga na kemikali. Inakauka baada ya saa saba na ukuta wetu ni imara mara nne zaidi ya ukuta uliojengwa na tofali la zege.”

Teknolojia yetu inawezesha ukuta wa nyumba nzima kukamilika ndani ya siku sita, nyumba zetu zinastahimili matetemeko, vimbunga na ujenzi wake unapunguza gharama za ujenzi kwa asilimia 40.

Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa nyumba hizo, Bw. Abdalla alisema wana mikataba na mabenki kwa hiyo wanaweza kujenga nyumba na kuziuza mara moja lakini pia wananchi wanaweza kuingia mikataba na mabenki na kulipia kidogo kidogo katika muda maalum (mortgage).

Mashahidi 16 Kujenga Kesi ya Akina Halima Mdee na Saed Kubenea

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imewasomea maelezo ya awali (PH) washtakiwa wanane wakiwamo, wabunge watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) katika kesi ya kumpiga na kumjeruhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam(RAS),Theresia Mmbando.

Akisoma maelezo hayo mbele ya Hakimu, Huruma Shaidi, Wakili wa Jamhuri, Frola Massawe aliwataja washtakiwa hao kuwa ni pamoja na Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga), Saed Kubenea (Ubungo), aliyekuwa Diwani wa Kata ya Saranga, Ephreim Kinyafu, Diwani wa Kata ya Kimanga, Manase Njema na mfanyabiashara Rafii Juma.

Wakili Massawe alidai mahakamani hapo kuwa, washtakiwa hao kwa pamoja wanadaiwa kutenda kosa hilo Februari 27, mwaka huu katika ukumbi wa Karimjee, ulioko wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam ambako kulikuwa na uchaguzi wa meya na msadizi wake.

Alidai kuwa,katika ukumbi huo,kulitolewa taarifa ya kutokuwepo kwa uchaguzi huo kutokana na kuwepo kwa zuio kutoka Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo liliwataka kutofanya uchaguzi huo mpaka zuio hilo litakapomalizika ndipo uchaguzi ufanyike.

Alidai kuwa, mshtakiwa wa kwanza ambaye si mbunge (Rafii Juma), hakuridhishwa na taarifa hiyo  ndipo aliposhirikiana na washtakiwa wengine kwa kumvamia, kumpiga na kumchania nguo RAS Mmbando hali iliyosababishia majeraha.

Alidai, baada ya kutokea kwa vurugu hizo, polisi waliingilia kati na kumuuliza kama aliweza kuwafahamu waliompiga, baada ya kuulizwa hivyo, alidai kumfahamu mshtakiwa wa pili, ambaye ni Halima Mdee.

Alidai kuwa, baada ya hapo, polisi walilazimika kuchukua daftari la mahudhurio ya siku hiyo na kuanza kuita majina mmoja baada ya mwingine na kupiga gwaride la utambulisho ambalo lilimsaidia kuwatambua washtakiwa wote na kukamatwa na kuwafikisha polisi na mahakamani.

Baada ya kusomewa maelezo hayo, washtakiwa hao walikubali taarifa zao binafsi lakini walikana shtaka linalowakabili.

Hata hivyo, upande wa mashtaka ulidai kuleta mashaidi 16 ambao watatoa ushaidi kwenye kesi hiyo.

Kutokana na hali hiyo, Hakimu Shaidi alihairisha kesi hiyo hadi Novemba 14 mwaka huu kwa ajili ya kuanza kusikiliza ushaidi.

Jaji Kuamua Hatima ya Ester Bulaya Leo....Ni Baada ya Kuwekewa Pingamizi Jana Wakati Akijieleza Mahakamani Jinsi Alivyomshinda Wasirra

$
0
0

MBUNGE wa Bunda Mjini, Ester Bulaya (Chadema), ameiambia Mahakama Kuu  Kanda ya Mwanza, kwamba alishinda uchaguzi wa ubunge uliofanyika mwaka jana.

Bulaya aliyasema hayo mahakamani hapo jana mjini Musoma kupitia kwa wakili wake, Tundu Lissu, mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Kanda ya Sumbawanga, Noel Chocha, anayesikiliza kesi ya kupinga matokeo yake iliyofunguliwa na aliyekuwa mgombea wa CCM, Stephen Wassira.

Katika utetezi wake baada ya kuapa, Bulaya alisema alitangazwa na msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo baada ya taratibu zote ikiwamo kuhesabu kura, kukamilika.

Baada ya utetezi huo, malumbano ya sheria baina ya mawakili wa upande wa waleta maombi na wajibu maombi yaliibuka na kudumu kwa zaidi ya saa tatu.

Malumbano hayo yalianza baada ya Wakili wa Waleta maombi, Costantine Mutalemwa, kuiomba mahakama hiyo iondoe aya saba kati ya 11 zilizokuwa kwenye utetezi wa Bulaya kwa kile alichodai hazimo kwenye utaratibu wa awali uliowasilishwa mahakamani hapo.
 
Aya ya saba ya utetezi wa Bulaya inadai kasoro ya kura 164,794 zilizotangazwa awali na msimamizi wa uchaguzi badala ya kura 69,369 za wapiga kura halali, hazikuathiri matokeo.

Wakili Mutalemwa alidai kwamba, madai yaliyotokea kwenye utetezi wa mbunge huyo ni mapya na suala la idadi ya wapiga kura ni moja ya kipengele ambacho wateja wake wanakipinga.

“Naomba mheshimiwa jaji aya ya pili, tatu, nne, tano, sita, saba na nane, ziondolewe kwenye utetezi wa Bulaya na zibaki aya ya kwanza, ya tisa, ya 10 na aya ya 11.

“Naomba aya hizo ziondolewe kwa sababu ni mpya na hazipo kwenye utaratibu wa awali,” alidai Wakili Mutalemwa.

Kutokana na maombi hayo, Lissu alisema hakubaliani na pingamizi la wakili huyo.

Alisema amekumbuka kauli ya aliyekuwa Rais wa iliyokuwa Mahakama ya Afrika Mashariki, Sir Charz Nyubon aliyewataka mawakili wasiweke mapingamizi yasiyo na msingi.

“Kitendo cha mawakili kuweka mapingamizi yasiyo na msingi ni kupoteza muda wa mahakama kwa mujibu wa kauli ya rais huyo na nakuomba mheshimiwa jaji uendelee na ushahidi wa mtoa ushahidi kwa kuwa muda wa kupoteza kwenye ushahidi haupo,” alisema Lissu.
 
Naye Wakili wa Serikali, Angela Lushagamba, alisema hana pingamizi lolote kwenye kiapo cha utetezi wa Bulaya uliotolewa mahakamani hapo na kuiomba mahakama iendelee kusikiliza ushahidi.

Akitoa uamuzi juu ya hoja zilizoibuka mahakamani hapo, Jaji Chocha, alisema anaona dalili za shauri hilo kusikilizwa kwa muda mrefu kutokana na hoja mpya zilizoibuka mahakamani.

“Kuna vitu vipya ambavyo vimeibuka kwa siku ya leo na nahitaji nipate muda zaidi ya saa tano kuvifanyia kazi,” alisema Jaji Chocha huku akiahirisha kesi hiyo hadi leo saa saba mchana.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 69 & 70 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

 Ilipoishia
Nilimuuliza victoria baada ya yeye kushindwa kuzungumza kitu kinacho mfanya asimame nje ya mlango wetu, akaanza kuvunja vinja vidole vyake kwa aibu, akamtazama john, ambaye hakuwa amezungumza kitu cha aina yoyote, akamshika john shati lake, kisha akamvuta karibu yake na kumpiga busu la mdomo na kunifanya nibaki nikiwa ninamshangao

“I need you john”(john, ninakuhitaji)

Victoria alizungumza huku akimsukumia john ndani ya chumba, changu, kama simba mwenye njaa victoria akamsukumiza john kitandani na kuanza kumvua shati, lake, kwa aibu ikanilazimu mimi kutoka ndani ya chumba nikawaacha waendelee na mambo yao

Endelea
Nikaelekea moja kwa moja jikoni, nikachukua maji ya kunywa kwenye friji lililopo humu jikoni, kisha nikakaa kwenye kiti kirefu ambacho nacho kipo humu ndani ya chumba.Mawazo yakaanza kurudi upa juu ya mtu aliye mteka mke wangu na kumuua kinyama kwa kumlipua kwa bomu

“nilazima nilipize kisasi kwa yoyote aliye husika katika hili”

Nilijiapiza kimya kimya huku nikiyatazama maji yaliyopo kwenye glasi niliyo ishika mkononi mwangu, nikaitazama saa ya ukutani na kukuta ikionyesha ni saa sita kasoro dakika ishirini, usiku

“hawamalizi na sasa hivi”

Nilizungumza huku nikinyanyuka kwenye kiti na kutoka nje, na kuwakuta walinzi wakizunguka zunguka kaimarisha ulinzi wa jumba hili la baba yangu, sikutaka kuzungumza na mtu wa aina yoyote zaidi ya kubatazama mandhari mazuri yalipomo kwenye eneo hili

“hei”
Nilimuita mlinzi mmoja aliye kuwa anakatiza karibu yangu
“ndio bosi”
Kwa bahati nzuri mlinzi huyu alinijibu kwa kiswahili
“ninaweza pata usafiri muda huu”
“kivipi?”

“nina maanisha ninaweza kupata gari, lolote lenye funguo”
“unataka kwenda wapi usiku huu?”
“kuna sehemu ninahitaji kwenda”
“kwa hapo, ndugu siwezi kukusaidia kwani bosi hajatoa ruhusa ya mtu yoyote kutoka na usafiri, tena muda huu wa usiku”

“ahaa powa asante”

Nikaachana na mlinzi na kurudi ndani, nikafika hadi mlango wa kuingilia chumbani kwangu, nikaweka sikio la upande wa kulia, nikasikia miguno ya mahaba ikiwa inaendelea ndani ya chumba change.
“mmmm kazi kweli kweli”

Nikapata wazo la kwenda chumbani kwa victoria japo kuegesha kichwa change kidogo, hii ni kutokana na uchovu mwingi.Nikaingia na kuwasha taa, kitu cha kwanza nikakutana na mwanga wa simu ya victoria, ikionyesha ni muda mfupi kuna meseji au simu ilipigwa.Nikapiga hatua hadi kitandani ilipo, nikaichukua na kutazama, na kukuta missed call na namba ambayo haikuwa na jina lolote.Nikafungua kipochi chake kilicho kuwa pembezoni mwa simu, nikakuta noti kumi za dola mia mia

“yess, kazi yangu imeanza kukamilika”

Nikazichomoa noti hizo, na kuzidumbukiza kwenye mfuko wa jinzi langu, ambapo kuna simu ya john, aliyo nikabidhi muda wa mchana.

Nikatazama salio kwenye simu ya victoria nikakuta lipo lakutosha, nikaiweka mfukoni, nikafungua kabatini kwake na kukuta makoti mengi makubwa ya baridi.Nikachukua koti jeusi na kulivaa, nikachukua kofia ya kuzuia baridi na kuivaa, nikatoka nje ya chumba cha victoria.Kutokana ni mzoefu sana wa jumba hili la baba haikuwa, ngumu sana kwangu kutoroka pasipo walinzi kunioa, nikatoka nje ya ukuta wa jumba hili, kwa kuuruka, nikaanza kutembea kuelekea barabara kuu, kwa bahati nzuri nikapata taksi

“nipeleke kwenye uwanja wa ndege, wa ‘johannesburg’, itakuwa ni bei gani?”
“dola mia”
“sawa”
Kutokana nina kiasi cha kutosha cha pesa, sikuwa na haja ya kumbembeleza dereva huyu, japo ninatambua amenipiga kizinga, kutokana na ugeni wangu, tukatumia dakika ishirini kufika uwanja wa ndege.

“unaweza kunisubiri?”

“bili shaka”

Nikampa dereva taksi pesa yake, nikaelekea sehemu ya huduma kwa wateja, na kuwakuta dada kadhaa wakiwa wamejipanga wakizungumza na baadhi ya abiria waliopo kwenye eneo hili
“samahani dada”
“bila samahani, nikusaidie nini?”

“juzi usiku, kuamkia jana nilifika hapa na ndege ya shirika la nchini philipines, kuna kitu ninahitaji kukipata kwenye kwenye safari ile”

“kitu gani?”


Mbio Za Kilimanjaro Marathon 2017 Zazinduliwa Dar Es Salaam.....Kufanyika Februari 26, 2017

$
0
0
Mbio za Kilimanjaro Premium Lager Marathon 2017 ambazo ni za 15 tangu Kuanzishwa kwake, zimezinduliwa rasmi  leo jijini Dar es Salaam katika mkutano na wanahabari, wadhamini na Chama Cha Riadha Tanzania.

“Tumeona matunda ya udhamini huu kwa mfano mwaka huu tumeshuhudia mshiriki wa Kili Marathon akishiriki katika michezo ya Olimpiki kule Brazil na kumaliza katika nafasi ya tano katika mbio za kilomita 42. Tunaweza kuwapata akina Simbu wengi kutoka kili Marathon na ndicho hasa wadhamini wengi wanakitafuta,” alisema Mkurugenzi wa Masoko wa TBL Group, Kushilla Thomas

Aidha Mkurugenzi huyo alisema  wadhamini wengine wa mashindano hayo ni Tigo ambao wanadhamini 21km, Gapco kwa 10 km-viti vya magurudumu na baiskeli ya kunyonga kwa mkono na Grand Malt-5km. Wadhamini wengine ni pamoja na KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile,Keys Hotel, Air Rwanda na Anglo Gold Ashanti.
 
Aliishukuru pia  wizara yenye dhamana ya michezo kwa kuhakikisha miaka yote kwamba tukio hili linafanikiwa,pia amewapongeza waandaaji, Wild Frontiers, waratibu wa kitaifa-Executive Solutions, Chama cha Riadha Tanzania (RT), Kilimanjaro Marathon Club, Mkoa wa Kilimanjaro na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo.
 
Kwa upande wake, Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli zawadi kwa 42km Kilimanjaro Premium Lager Marathon ni pamoja na – jumla ya Tsh milioni 20 kwa washindani wanaume na wanawake watakaoshika nafasi 10 za juu. Mshindi wa kwanza kutoka kila kundi atapata Tsh milioni 4 kila mmoja.

 “Hatuwezi kuwasahau wanariadha wote wa hapa nchini walioshiriki kwenye mashindano haya na kuipa fahari nchi yetu na kuwa watashinda zawadi zote hizi tunazozitoa. Tunaamini kwamba mashindano haya ya marathon pia yatafungua milango kwa wanariadha wetu kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kimataifa ya marathon nje ya nchi yenye zawadi kubwa,” alisema Pamela Kikuli.

Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Muhongo amteua Charles Sabuni kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania.

AUDIO: Wachina wakamatwa Mtwara, wakutwa wakibadili Expire date kwenye dawa

$
0
0

Watu watano wakiwemo raia wawili wa China na Watanzania watatu wamekamatwa Mtwara kwa kutuhumiwa kubadili tarehe zilizokwisha muda wa matumizi kwenye dawa za kilimo (expire date) ili dawa hizo ziingizwe tena sokoni na kuonekana bado zinafaa kwa matumizi.

Inadaiwa watuhumiwa hawa wamefanikiwa kubadilisha dawa hizo kwenye mabox zaidi ya mia sita ( 600) na kuzifanya zionekane mpya ambapo Kamanda wa Polisi Mtwara amesema Watuhumiwa hao walikamatiwa Nangwanda.

Makachero wa Polisi baada ya kupewa taarifa waliwahi kwenye eneo la tukio na kukuta watu wanne wakikwangua chupa kuondoa nembo iliyoonyesha dawa hiyo ilitengenezwa tarehe 28 February 2013 na muda wake wa matumizi umekwisha tarehe 27 February 2016.

Nembo mpya feki waliyoitengeneza Wachina hawa inasomeka dawa imetengenezwa tarehe 20 February 2016 na inamaliza muda wa matumizi tarehe 19 February 2019.

==> Msikilize Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara Acp Thobias Sedoyeka  akisimulia
==>Apo chini kuna sauti ya Mkuu wa Wilaya akiongelea Sakata hili

RC Arusha Mrisho Gambo Arejesha fedha zaidi ya shilingi milioni 1.3 alizokuwa amelipwa kwa ajili ya kuhudhuria kilele cha Mwenge.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo leo ametekeleza agizo la Rais Magufuli la kusitisha safari ya kwenda Mkoani Simiyu kwenye sherehe za kuhitimisha kilele cha mbio za mwenge wa Uhuru kwa kurejesha kiasi cha Jumla ya Shilingi 1,389,300.

Fedha hizo yalikuwa ni malipo kwa ajili ya Mkuu wa Mkoa, Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa , Dereva wa Mkuu wa Mkoa na gharama za mafuta.

Akiongea na mwandishi huyu ofisini kwake leo, mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha amesema wakati agizo hilo linatolewa yeye alikuwa bado hajaanza safari ya kuelekea mkoani Simiyu, na kwamba amelipokea bila kinyongo na mara moja akaamua kurejesha posho hiyo, akionesha stakabadhi ya kuthibitisha hilo.

Kwa mujibu wa mchakato wa malipo ya posho kwa safari hiyo ya kwenda mkoani Simiyu kwa siku tatu, posho ya RC ilikuwa ni Sh 360,000, Msaidizi wa RC Sh 240,000, posho ya dereva 24,000 na Sh 549,300 kwa ajili ya Mafuta ya gari.

Pia RC Gambo ameahidi kusimamia zoezi hilo kwa wahusika wote mkoani Arusha na kuhakikisha wanatekeleza agizo hilo kwa wakati na fedha hizo zielekezwe kwenye ujenzi wa madarasa kama sehemu ya maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wa kidato cha kwanza, darasa la kwanza na darasa la awali kwa mwaka 2017.

Polisi Dar yaua majambazi wanne wanaodaiwa kuwaua askari wanne waliokuwa lindo Mbagala DSM mwezi Agosti, yakamata 'Panya Road' 10.

$
0
0
Kikosi Maalumu cha Kupambana na Ujambazi wa Kutumia Silaha cha Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kilifanikiwa kukamata watuhumiwa wanne wa ujambazi waliohusika katika mauaji ya askari polisi 4 katika benki ya CRDB iliyopo maeneo ya Mbande, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Kamishna wa Kanda hiyo, Kamanda Simon Sirro wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, amesema watuhumiwa hao walikamatwa wakati wa majibizano ya risasi yaliyotokea Oktoba 11, 2016 katika pori la Dondwe lililopo Chanika.

“Kikosi kilifanikiwa kumkamata mtuhumiwa mmoja, baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia wema kuwa ni jambazi na ndiye aliyehusika katika mauaji ya askari polisi huko Mbande,” amesema.

Kamanda Sirro ameongeza kuwa “Baada ya kumkamata mtuhumiwa huyo alikiri kuhusika na tukio hilo akiwa na wenzie saba, alitupeleka mahala walipo wenzake, ila alikimbia, wenzie walipojua polisi wapo maeneo hayo, walianza kurusha risasi ndipo polisi nao wakaanza kurusha risasi.”

Kamanda Sirro amesema kuwa, watuhumiwa hao walizidiwa na mashambulizi ya risasi ambapo walijeruhiwa vibaya na kwamba walifariki dunia wakiwa wanapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Amesema askari polisi walifanikiwa kuipata bunduki ya kijeshi aina ya SMG iliyofutwa usajili ambayo watuhumiwa hao waliipora kutoka mikononi mwa polisi waliowaua mbande ikiwa na risasi 22 ndani ya magazine.

Katika tukio lingine, Kamanda Sirro amesema mnamo Oktoba 11, 2016 maeneo ya magomeni polisi wakiwa doria walifanikiwa kukamata bastola moja aina ya bereta baada ya kutelekezwa na kundi la vijana.

Pia amesema Jeshi la Polisi limekamata watuhumiwa watatu wakiwa na bomu moja la kienyeji, mapanga manne, visu viwili, na bisibisi moja.

Vilevile Jeshi la Polisi Dar es Salaam Oktoba 12, 2016 walikamata panya road zaidi ya 10 maeneo ya Mbagala.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Octoba 14

Rais Magufuli Alivyoagana Na Kiongozi Mkuu Wa Bohora Duniani, Ikulu Jijini Dar

$
0
0
Jumuiya ya Madhehebu ya Dawoodi Bohra imetoa mchango wa Dola za Marekani laki mbili na nusu (Usd. 250,000) sawa na Shilingi Milioni Mia Tano Arobaini na Tano za Kitanzania (Ths. 545,000,000) kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lilitokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.

Kiongozi Mkuu  wa Madhehebu ya Bohra Duniani Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin amekabidhi mchango huo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, jana walipokutana na kufanya Mazungumzo leo tarehe 13 Oktoba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Kati ya fedha hizo Dola za Marekani laki moja (Usd. 100,000) zimetolewa na Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mwenyewe, Dola za Marekani laki moja (Usd. 100,000) zimetolewa na Viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohra na Dola za Marekani Elfu Hamsini (Usd. 50,000) zimetolewa na wana Jumuiya ya Bohra wa Tanzania.

Pamoja na kutoa mchango huo, Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin ameahidi kuwa Jumuiya hiyo ambayo inamiliki hospitali kubwa zilizopo maeneo mbalimbali duniani ikiwemo India, itajenga hospitali hapa nchini kwa ajili ya kutoa huduma za matibabu.

Pia Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin ameahidi kuwa Jumuiya ya Bohra itatoa udhamini wa masomo ya udaktari kwa vijana wa Tanzania na pia itadhamini matibabu kwa wagonjwa 20 watakaopelekwa nchini India kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Kwa Upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemshukuru Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin na Jumuiya nzima ya Dawoodi Bohra kwa mchango walioutoa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera na pia kwa kufanyia mkutano wao wa mwaka hapa nchini uliowaleta wageni takribani 31,000 kutoka mataifa mbalimbali duniani.

“Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin nakushukuru sana kwa kuja hapa nchini kwetu na kutuletea mkutano huu mkubwa, ujio wenu umeimarisha uhusiano kati ya Bohra na Tanzania na pia umechangia uchumi wa nchi yetu.

“Nakushukuru pia kwa nia yenu ya kujenga hospitali hapa nchini, kuwasomesha madaktari na kudhamini matibabu ya wagonjwa huko India, naomba nikuhakikishie kuwa mchango mlioutoa utatusaidia sana na pia mkijenga hospitali na kufundisha madaktari mtakuwa mmesaidia kuokoa fedha nyingi ambazo Serikali ingetumia” amesema Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amewaalika wanajumuiya ya Dawoodi Bohra kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, kilimo, usafirishaji, madini na uvuvi na amewahakikishia kuwa Serikali itawaunga mkono wote watakaokuwa tayari kuja kuwekeza Tanzania.

Jumuiya ya Madhehebu ya Dawoodi Bohra Duniani imeadhimisha mwaka mpya wa Kiislam na kumbukumbu ya kifo cha Mjukuu wa Mtume Muhammad (S.A.W) aitwaye Imamu Hussein ambapo maadhimisho yake ya kidunia yaliyoambatana na tamasha la zaidi ya wiki mbili yamefanyika hapa nchini kuanzia tarehe 01 Oktoba, 2016 hadi tarehe 11 Oktoba, 2016.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
13 Oktoba, 2016

Taarifa Ya Jeshi La Polisi Kwa Umma Kutoka Mkoa Wa Mwanza

$
0
0

Tarehe 12.10.2016 majira ya saa 16:35 katika eneo la Busenga “A” kata ya Buswelu wilaya ya Ilemela jiji na mkoa wa Mwanza, askari walifanikiwa kumkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Juma Biria miaka 42, mfanya biashara na mkazi wa mtaa wa Busenga akiwa na vifaa vya kutengeneza noti bandia ambavyo ni kemikali ikiwa ndani chupa kubwa, sabuni ya maji iliyowekwa ndani ya chupa ndogo, karatasi zilizokatwa mfano wa noti ya shilingi elfu kumi pamoja na unga ambao bado haujafahamika ni wa kitu gani, kitendo ambacho ni kinyume na sheria na taratibu za nchi .

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa tajwa hapo juu akishirikiana na wenzake amekuwa akifanya shughuli hiyo ya uhalifu, ndipo zilipatikana taarifa za kiintelejensia kuhusiana na uhalifu huo, ndipo askari waliweza kufuatilia na kufanikiwa kumtia nguvuni mtuhumiwa huyo.

Aidha kwa sasa jeshi la polisi lipo katika mahojiano na mtuhumiwa, pindi uchunguzi ukikamilika atafikishwa mahakamani ili hatua  stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yake. Aidha jitihada za kuwasaka wenzake wanaodaiwa kushirikiana na mtuhumiwa huyu katika uhalifu huo bado zinaendelea.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza naibu kamishina wa polisi Ahmed Msangi anatoa rai kwa wakazi wa jiji na mkoa wa Mwanza, akiwataka kushirikiana na jeshi la polisi katika kupambana na wahalifu wa aina kama hii, ili waweze kufikshwa katika vyombo vya sheria, kwani jeshi la polisi linaamini endapo wananchi wataendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi lao, tutaweza kukomesha uhalifu katika mkoa wetu.

imetolewa na:

DCP: Ahmed Msangi
Kamanda wa polisi (m) Mwanza

Makontena 100 Yapitishwa Kinyemela Bandarini Bila Kukaguliwa .....Waziri Mwijage Atoa Siku 4 Wahusiku Wajisalimishe

$
0
0
WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage ametoa siku nne kwa wafanyabiashara waliopitisha makontena 100 bandarini bila kukaguliwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), wakatoe taarifa katika shirika.

Mwijage alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupata taarifa kuwepo kwa makontena 100, yaliyotolewa bandarini kwa siku zilizopita bila kukaguliwa na TBS.

“Nawataka wafanyabiashara wote waliochukua kontena hizo, wajisalimishe haraka TBS kabla ya kufika Jumanne ili wakaguliwe. Najua kuanzia kesho (leo) ni mapumziko, lakini TBS itaweka dawati la kuwasikiliza mpaka Jumatatu na ikifika Jumanne hatua zitachukuliwa kwa wahusika wote,” amesema Mwijage.

Alisema wafanyabiashara ambao hawatajisalimisha baada ya kumalizika kwa siku hizo, hatua stahiki zitachukuliwa ikiwemo kulipa faini ya asilimia 15.

Aidha, alisema kwa mawakala wa forodha wote, waliohusika kutoa kontena hizo wizara yake itawasiliana na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango ili kuona hatua za kuchukua kwa kuwa serikali haiwezi kukubali mchezo huo.

“Tayari tulishafunga michezo ya namna hii na tumeanza maisha mapya kwa hiyo mawakala na wote mliohusika kutoa kontena hizo sababu hazijafika mbali tunaomba mtueleze zilipo ili tukazikague,” aliongeza.

Pia alisema kontena hizo zilipaswa kukaguliwa na TBS, lakini baada ya tukio hilo kontena hizo zitakaguliwa na shirika hilo wakishirikiana na Tume ya Ushindani Tanzania (FCC).

 Aidha, amewaagiza TBS na FCC wafuatilie watu wao na kuziona bidhaa hizo, kwani watakaoshindwa hawatapewa cheti cha ubora bila kuona bidhaa na kukaguliwa.

“Sisi hatutaki mje mtueleze ni mzigo kiasi gani ili tupige penati hapana tunataka hilo kontena mlione na hiyo bidhaa muione na mkague,” aliongeza waziri huyo.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dk Egid Mubofu alisema ni vyema wafanyabiashara hao wakafuata maagizo hayo na kujitokeza kukaguliwa ilikuepuka faini hiyo ya asilimia 15. 

Alisema upitishaji wa bidhaa bila kukaguliwa na shirika hilo unaweza kuleta madhara makubwa kwa watumiaji ambao hawajui kama bidhaa yako imekaguliwa ubora.

“Najua wafanyabiashara wengine watasema hatuendi kukaguliwa sababu hataitumia bidhaa hiyo, lakini anasahau kama anaweza siku moja na yeye akatumia bidhaa hiyo ambayo haijakaguliwa ni vyema wakawa wazalendo na kufuata maagizo waliyopewa,” alisema Mubofu.

TBS imeanzisha utaratibu mpya wa kulipisha faini mizigo inayoingia hapa nchini, ambayo haikukaguliwa wakati iko nchini China. Faini ni asilimia 15 ya thamani ya mzigo ulioingia.

Serikali Yaiamuru Bodi ya Mikopo Istishe Makato na Imlipe Pesa Zake Mstaafu Aliyekuwa Akikatwa Kimakosa

$
0
0
Serikali  imeiagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kusitisha mara moja makato ya fedha yaliyokuwa yakifanywa kwenye malipo ya pensheni ya mstaafu Ernest Lameck, katika Chuo cha Ualimu cha Tukuyu kilichopo wilayani Rungwe.

Agizo la kusitishwa kwa makato hayo limetolewa baada ya kubainika kuwa deni hilo ni hewa kwa kuwa mtumishi huyo mstaafu hakuwahi kusoma katika chuo cha Elimu ya Juu.

Amesema Bodi ya Mikopo imekuwa ikitoa mikopo na kwamba kinachofanywa na taasisi hiyo ya Serikali ni wizi.

Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, ametoa agizo hilo jana alipofanya ziara katika Chuo cha Ualimu Tukuyu na kuelezwa juu ya uwepo wa mstaafu huyo ambaye amekuwa akikatwa fedha wakati si mnufaika wa mkopo.

Mkuu wa chuo hicho, Ubaya Salumu, amemweleza Waziri kuwa Lameck aliyekuwa mtumishi chuoni hapo alianza kukatwa fedha kwenye pensheni yake na alipofuatilia alibaini kuwa makato yamekuwa yakifanywa na Bodi ya Mikopo.

Amesema jambo la kushangaza ni kuwa kabla na wakati wa utumishi wake, Lameck hakuwahi kusoma elimu ya juu ambayo angeweza kuomba mkopo kutoka katika bodi hiyo.

Lameck amebainisha kuwa baada ya kufuatilia alibaini kuwa Bodi ya Mikopo inamdai Sh milioni tisa na ni kwa muda mrefu amejaribu kufuatilia jambo hilo pasipo mafanikio.

Kutokana na hali hiyo, Profesa Ndalichako mbali na kuiagiza bodi kusitisha makato hayo mara moja, pia aliagiza fedha zote alizokatwa mtumishi huyo zirejeshwe ili anufaike na stahili zake.

“Haiwezekani mtu haukukopeshwa halafu waanze kumkata. Hili nataka lifanyike haraka na si tu kusitisha makato, bali lazima Bodi wakulipe fedha zako zote walizokukata,” alisisitiza.

Mbowe kuiburuza Serikali mahakamani

$
0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema ataiburuza Serikaliya Awamu ya Tano mahakamani ili chombo hicho cha haki kitoe tafsiri ya vitendo vya ukandamizaji wa demokrasia vinavyofanywa na viongozi wa Serikali hasa Mkoani Arusha.

Mbowe ameyasema hayo alipokuwa akilaani kitendo cha Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, kuwasweka selo madiwani wanne wa chama hicho akisema kuwa hiyo ni ishara ya kwamba utawala wa awamu ya tano hauheshimu sheria.

“Nimewaagiza wanasheria wangu kwenda mahakamani ili kupata tafsiri sahihi kuhusu vitendo hivyo,” amesema.

Ameongeza kuwa viongozi hao wamekuwa wakifanya vitendo vya udhalilishaji kwa baadhi ya wabunge, madiwani, mameya na wenyeviti wa halmashauri kinyume na sheria.

“Nawashangaa sana Wakuu wa Mikoa na Wilaya wamekuwa wakiwadhalilisha wawakilishi wa wananchi ilhali wao wakiwa ni waajiriwa ambao hawajaomba kura kwa wananchi. Jambo hili limeanza mwaka huu, nah ii ni nafasi mbaya sana kwa Rais Magufuli kuchagua makada badala ya watumishi,” amefunguka Mbowe.

Diwani Chadema anaswa na dawa za kulevya, bunduki

$
0
0

Jeshi la Polisi Mkoani Rukwa linamshikilia Diwani wa kata ya Izira, Paschael Silimba (Chadema) baada ya kumkamata akiwa na dawa za kulevya aina ya bangi na bunduki moja aina ya gobole.

Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, George Kyando amesema kuwa jeshi hilo lilimkamata Kyando katika eneo la soko kuu ambalo hufanyia biashara yake ya kuuza mifuko ya salfeti, baada ya kupata taarifa na kuamua kumfuatilia.

Alisema kuwa baada ya kumpekua katika vifurushi vya bidhaa hiyo anayoiuza kwa kushirikiana na mkewe, walibaini uwepo wa bangi kiasi cha robo kilo.

“Baada ya kufanya upekuzi kwenye duka la diwani huyo, tumefanikiwa kukamata bangi kiasi cha robo kilo. Ni bangi kavu ambayo imeshaandaliwa tayari kwa ajili ya kufanya packing na kuuzwa,” alisema Kamanda Kyando.

Akizungumzia silaha aina ya gobole waliyoikuta nyumbani kwa diwani huyo anayodaiwa kuimiliki kinyume cha sheria, alisema ingawa ni silaha ya kizamani ina nguvu ya kuua tembo.

“Silaha hii ina nguvu sana, ina uwezo wa kuua tembo na ni hatari sana akipigwa binadamu kwa silaha hii. Kwahiyo msiione hapa mkaidharau, ina nguvu sana,” aliongeza.

Kamanda Kyando aliwataka viongozi wote waliopewa dhamana na wananchi kutotumia nyadhifa zao kufanya uhalifu. Alitoa wito wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo kufichua uhalifu bila kujali waliofanya uhalifu huo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live


Latest Images