Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tibaijuka Ahofia ESCROW.....Akataa Zawadi ya Milioni 200

0
0
MBUNGE wa Muleba Kusini, Profesa Anna Tibaijuka (CCM), amepata tuzo ya Umoja wa Mataifa (UN) ikiwa ni mchango wa kuthamini kazi aliyoifanya, huku akikataa kupokea zawadi ya Dola 100, 000 za Marekani, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 200.

Profesa Tibaijuka alitoa taarifa hiyo jana jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo alisema tuzo hiyo ya Maendeleo Endelevu ilidhaminiwa na mwana Mfalme wa Bahrain, Khalifa bin Salman Al Khalifa.

Alisema, hatua ya kuzikataa fedha hizo, ni njia ya kukwepa mtego kama uliomkuta mwaka juzi baada ya kupokea fedha za Escrow Sh bilioni 1.6 kutoka kwa mfanyabiashara,  James Rugemalira.

Tuzo hiyo ambayo ni heshima kwa Tanzania, alikabidhiwa Septemba 24, mwaka huu na inajulikana kama ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award  for Sustainable Development’.

Profesa Tibaijuka alisema, alikabidhiwa tuzo hiyo kwa kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo duniani.

Alisema tuzo  hiyo ya heshima hutolewa kila baada ya miaka miwili na washiriki wakuu huwa ni wale waliowahi kufanya kazi na Shirika la Umoja wa Mataifa.

Mwaka huu, Waziri Mkuu wa Bahrain Khalifa bin Salman ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo, alisema.

“Tuzo hii nimepewa Marekani ikiwa kama sehemu ya kutambua mchangoa wangu katika kuhamasisha maendeleo  na nilikabidhiwa katika Makao Makuu ya UN na kushuhudiwa na viongozi mbalimbali duniani.

“Na huambatana na zawadi ya Dola za Marekani 100,000 (Sh milioni 200).    Sikuzichukua fedha hizi, kama mnavyojua maadili ya nchi yetu unaweza ukapokea  yakaibuka mambo mengine.

“Ingawa kwenye ule mkutano niliwaambia kuwa sipokei fedha kutokana na hali halisi … niliwaambia kuwa kama mnavyojua katika mkoa ninaotoka (Kagera) kuna tetemeko limetokea,” alisema Profesa Tibaijuka.

Alisema kupokea tuzo hizo si kwa ajili ya mafanikio yake binafsi bali kwa Watanzania wakiwamo wapiga kura wake wa Muleba Kusini ambao muda wote wamekuwa wakimtia moyo wa kufanyakazi kwa bidii.

Profesa Tibaijuka ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, alisema ameuachia Umoja wa Mataifa (UN)  na wadhamini wa tuzo hiyo waamue cha kufanya kuhusu fedha hizo.

Katika kupokea tuzo hiyo, mbunge huyo alisindikizwa na  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  Balozi Dk. Augustine Mahiga  na Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM).


Waziri Mkuu apokea misaada zaidi ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko Kagera

0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea zaidi ya sh. milioni 760 zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.
 
Amepokea misaada hiyo kutoka kwa taasisi na wadau mbalimbali likiwemo kundi la wanawake New Millennium linaloundwa na wake wa viongozi wa Serikali walio madarakani na waliostaafu.
 
Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika jana jioni (Alhamis, Septemba 29, 2016) kwa nyakati tofauti kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam pamoja na makazi ya Waziri.
 
Miongoni mwa waliokabidhi misaada hiyo ni pamoja Meya wa jiji la Dar es Salaam Mhe. Isaya Mwita sh. milioni 10, Kampuni ya mabati ya ALFA imekabidhi mabati yenye thamani ya sh. milioni 50 na kampuni ya Bia Tanzania (TBL) sh.milioni 100. 
 
Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu kampuni ya vinywani baridi ya Pepsi Cola, Bw. Avinash Jha amekabidhi sh.milioni 50, kampuni ya Round Table pamoja na wadau wao sh. milioni 57, kampuni ya Wool Worth  sh.milioni 20 na Jumuiya ya Waislam (FIRDAUS) imetoa viti 15 vya walemavu.

Aidha, kampuni ya Trans Ocean Supplies LTD imetoa sh. milioni 20, Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe. Amina Masenza amekabidhi sh. milioni 18.681,Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Shy-Rose Bhanji amekabishi sh. milioni tano.

Pia Chama cha Waagizaji Wakubwa wa Mafuta Tanzania kimekabidhi sh. milioni 415.8, kundi la mtanzao wa kijamii la Whatsapp la Papaso, D’jaro Arungu limekabidhi sh.520,000 na kampuni ya mafuta ya Camel iliyokabidhi mifuko 1,000 ya saruji.

Jumuia ya Wanataaluma ya Vyuo Vikuu vya Umma Tanzania (ASAs) imekabidhi sh. milioni 7.5, Umoja wa Wamiliki wa Maduka ya Dawa Muhimu Tanzania umekabidhi dawa zenye thamani ya sh. milioni tano pamoja na Eric Shigongo wa Global Publisher amekabidhi mabati 500 yenye thamani ya sh. milioni 10.

Waziri Mkuu amewashukuru wadau wote kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.
 
“Tunashukuru sana kwa michango yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa. Amesema.
 
Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye Namba. 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669(M-Pesa), au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616(Tigo Pesa).
 
Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.
 
Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
 
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Taarifa kuhusu kesi ya viongozi waliofungua akaunti bandia ya maafa Kagera

0
0
Watumishi  watatu wa Serikali akiwamo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Bukoba, wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Bukoba wakituhumiwa kutaka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu.

Watumishi hao wanadaiwa kutaka kujipatia fedha hizo baada ya kufungua akaunti feki iitwayo kamati ya maafa Kagera kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10 mwaka huu.

Watumishi waliofikishwa mahakamani hapo jana ni aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Amantus Msole, Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, Mhasibu wa Mkoa wa Kagera, Simbaufoo Swai na Meneja wa CRDB tawi la Bukoba, Carlo Sendwa.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali, Hashimu Ngole, alidai watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili.

Alilitaja shtaka la kwanza kuwa ni kula njama za kutenda kosa la kufungua akaunti feki yenye jina linalofanana na jina la akaunti iliyofunguliwa na Serikali kwa ajili ya waathirika wa tetemeko la ardhi.

Aliitaja akaunti hiyo kuwa ni yenye jina la Kamati Maafa Kagera yenye namba 015225617300.

Kwa mujibu wa wakili huyo, watuhumiwa hao badala ya kutumia akaunti ya Serikali kukusanya fedha za maafa, walifungua akaunti yao waliyoipa jina la Kamati Maafa Kagera yenye namba 0150225617300.

Alilitaja shtaka la pili kuwa ni watuhumiwa kutumia madaraka na vyeo vyao vibaya kinyume cha sheria.

Mawakili wanaowatetea watuhumiwa hao walimwomba hakimu awapatie dhamana wateja wao kwa kuwa bado ni watumishi wa Serikali na wanao uwezo wa kujidhamini wenyewe na hawawezi kutoka nje ya Kagera.

Washtakiwa hao walirejeshwa rumande ambapo kesi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo Septemba 30 na hakimu atatoa maamuzi kuhusu dhamana yao.

Chadema kutoa msimamo wa Oparesheni UKUTA Leo

0
0
Mwezi mmoja baada ya Chadema kusitisha Operesheni Ukuta kupinga inachokiita ukiukwaji wa haki za binadamu na ukandamizaji wa demokrasia, leo inatarajia kutoa mwelekeo wa mkakati huo.

Operesheni hiyo ilipangwa kuzinduliwa Septemba mosi nchini kwa maandamano na mikutano ya hadhara kama maazimio ya Kamati Kuu ya Chadema, baada ya chama hicho kukumbwa na vikwazo kadhaa kuendesha shughuli zake, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara.

Siku moja kabla ya kufanyika kwa operesheni hiyo, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alitangaza kuisitisha kwa mwezi hadi kesho, ili kutoa fursa kwa viongozi wa dini kusemezana na Rais John Magufuli na Serikali yake.

Jana, Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema: “Kuhusu Ukuta, kesho (leo) tutatoa msimamo wetu juu ya kitu tutakachofanya.”

Alisema operesheni hiyo ilisitishwa kutokana na sababu za msingi zilizoelezwa, hivyo kauli ya chama hicho leo itafafanua kwa kina kuhusu mambo yote yaliyojitokeza katika kipindi hicho cha mwezi.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano
CHADEMA, Tumain Makene alipost taarifa hii katika ukurasa wake;

Wakati viongozi hao wakieleza hayo, hadi jana hakukuwa na taarifa zozote za kufanyika kwa kikao kati ya viongozi wa dini na Serikali.

Viongozi hao waliitaka Serikali na Chadema kufikiria amani ya nchi na kutafuta njia mwafaka za kumaliza msuguano wa kisiasa hasa baada ya chama hicho kushikilia msimamo wake wa kufanya mikutano na maandamano.

Wakati Chadema wakijipanga kutoa tamko lao, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda jana alisisitiza kuwa Oktoba mosi ni Siku ya Kupanda Miti jijini humo ambapo viongozi mbalimbali watahudhuria.

Zanziar Yapitisha Marekebisho ya Katiba Yanayomzuia Rais wa Zanzibar Kushauriana na Kiongozi wa Upinzani

0
0
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewasilisha marekebisho ya Katiba ya Zanzibar ya 11 ya mwaka 1984, ambayo yatatoa nafasi na kumpa uwezo Rais wa Zanzibar, kuchagua wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani ambaye kwa sasa hayupo katika baraza hilo.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Haroun Ali Suleiman, katika marekebisho hayo vifungu viwili vinahitaji kufanyiwa marekebisho kikiwemo cha 66 kwa kufanya marekebisho na kufuta maneno ya vyama na kiongozi wa upinzani.

Akifafanua katika kifungu hicho, alisema lengo lake ni kutoa nafasi kwa Rais wa Zanzibar kuchagua nafasi mbili za wajumbe wa Baraza la Wawakilishi bila ya kushauriana na Kiongozi wa Upinzani katika Baraza ambaye kwa sasa hayupo, baada ya Chama cha Wananchi (CUF) kususia Uchaguzi Mkuu wa marudio mwaka huu, na hivyo kutopata mwakilishi yeyote na hivyo kufutika kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ambayo Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Shariff Hamad alikuwa Makamu wa Kwanza wa Rais.

Haroun alisema katika mazingira ya sasa katika Baraza la Wawakilishi, hakuna kiongozi katika Baraza hilo pamoja na vyama vilivyopata wingi wa kura, hatua ambayo imemfanya Rais kushindwa kuteua wajumbe wawili katika Baraza la Wawakilishi.

‘Katika Baraza la Wawakilishi la sasa Rais ameshindwa kuteua wajumbe wawili katika nafasi kumi ambapo anatakiwa ashauriane na kiongozi wa upinzani ambaye hayupo kwa sasa,” alifafanua na kuongeza kuwa Kifungu cha 77(2) kinafuta neno la upinzani lenye uwakilishi ndani ya Baraza la Wawakilishi.

Akifafanua, alisema marekebisho ya Katiba yanayopendekezwa mbele ya Baraza la Wawakilishi, lengo lake kubwa kuimarisha demokrasia na kumpa nafasi Rais kuchagua wajumbe wa Baraza watakaofanya kazi kwa maslahi ya taifa. 

Katiba ya Zanzibar imempa mamlaka Rais wa Zanzibar kuchagua wajumbe 10 katika Baraza la Wawakilishi, ambapo nafasi mbili kwa kushauriana na kiongozi wa upinzani ambaye hayupo kwa sasa.

Wajumbe watatu wa Baraza la Wawakilishi walioteuliwa kutoka katika vyama vya upinzani, wanatokana na nafasi 10 kwa mujibu wa uwezo aliopewa Rais na Katiba. Wajumbe hao watatu kutoka vyama vya upinzani ni Hamad Rashid Mohamed, Juma Ally Khatib na Said Soud Said.

Utafiti Twaweza: Nchi Haiongozwi Kidikteta

0
0
Asilimia 58 ya Watanzania wamepinga kauli za baadhi ya wanasiasa kuwa Rais John Magufuli anaendesha nchi kidikteta huku asilimia 31 imesema haina uhakika na jambo hilo.

Aidha, imeelezwa kuwa asilimia 80 ya wananchi wanaona kwamba baada ya uchaguzi juhudi za kimaendeleo zipewe kipaumbele na vyama vya siasa.

Akitoa taarifa za utafiti uliofanywa na Taasisi ya Utafiti ya Twaweza jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, Aidan Eyakuze alisema ni asilimia 11 pekee ya Watanzania ndiyo waliosema nchi hii inaongozwa kidikteta.

“Baadhi ya wanasiasa na wasomi walitafsiri uongozi wa Rais Magufuli kama udikteta na neno hilo likawa mojawapo ya mambo yaliyounda Ukuta, asilimia 11 wanakubaliana na wazo hilo lakini asilimia 58 wanalipinga huku asilimia 31 wanasema hawana uhakika,” alisema Eyakuze.

Alisema kundi kubwa ambalo limejibu kuwa Rais Magufuli ni dikteta ni la vijana na watu matajiri na wenye uwezo wa juu kiuchumi kuliko masikini, wazee na watu wenye elimu ya chini; huku alisema asilimia 29 ya wananchi walio karibu ya vyama vya upinzani wanamuona Rais kuwa ni dikteta na asilimia tano ni wa chama tawala yaani CCM.

Aidha, alisema wananchi wana uelewa tofauti tofauti kuhusu neno udikteta, asilimia 32 walitafsiri kama kutawala kimabavu, asilimia 15 walitafsiri kuwa mtu mmoja ndiye mwenye maamuzi ya nchi nzima, huku asilimia 34 ya watu waliohojiwa hawaelewi maana ya neno hilo.

Katika demokrasia, Eyakuze alisema asilimia 51 ya Watanzania walisema mikutano inasaidia kuiwajibisha serikali huku asilimia 49 ikisema mikutano huvuruga umakini wa serikali na wananchi kudhoofisha shughuli za kimaendeleo.

Katika suala la maandamano, asilimia 50 walisema hawawezi kushiriki maandamano yoyote, asilimia 29 wanaweza kushiriki na asilimia 20 walijibu kuwa hawajui.

“Kati ya takwimu hizo, vijana waliosema wako tayari kushiriki maandamano yoyote na siyo lazima ya ukuta ni asilimia 35, watu wazima ni asilimia 15, wafuasi wa CCM asilimia 27 na wa vyama vya upinzani ni asilimia 43,” alisema Eyakuze.

Aidha alisema kuwa miongoni mwa waliosema kuwa hawatajiunga na maandamano asilimia 45 walisema ni kwa sababu wana wasiwasi itatokea vurugu na asilimia 29 walisema kwa sababu siyo njia sahihi za kutatua matatizo.

Alisema wananchi sita kati ya kumi waliunga mkono kuzuiwa kwa mikutano ya kisiasa wakiwemo wale wa vyama vya upinzani waliunga mkono suala hilo.

“Asilimia 60 waliunga mkono maamuzi ya Rais kuzuia mikutano ya kisiasa huku wazee wengi zaidi ndio walioonekana kuunga mkono zaidi uamuzi huo ambao ni asilimia 70 na vijana asilimia 55 na asilimia 31 ya wafuasi wa vyama vya upinzani wanakubaliana na kuzuiwa kwa maandamano ya Ukuta."

Asilimia 16 wananchi wanafahamu harakati za ukuta na asilimia 79 hawafahamu harakati hizo na miongoni mwa wanaofahamu uelewa wao kuhusu harakati hizo ni asilimia 48. Na kwamba kati ya wanaofahamu ukuta asilimia 50 walijibu wanaunga mkono ukuta na asilimia hamsini hawaungi mkono.

“Asilimia tisa kati ya wanaounga mkono ukuta katika maandamano ya Septemba mosi walipanga kushiriki ambapo ni pamoja na asilimia tatu ya wale wa chama tawala,” alisema.

Katika utafiti huo umeonesha kuwa wananchi hawakubaliani na mbinu zinazotumiwa na baadhi ya vyama vya upinzani katika kuhakikisha demokrasia inalindwa. 

Mapokezi ya Maalim Seif Buguruni yaota mbawa

0
0
Mapokezi makubwa yaliyopangwa kufanyika leo  jijini Dar es salaam ya kuwapokea Wajumbe wa Baraza Kuu la CUF na  Kamati ya Uongozi ya chama na Katibu Mkuu Maalim Seif yameota mbawa kufuatia kusitishwa  kwa hofu ya kutokuwepo usalama.

Mapema jana, ilitangazwa kwamba Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, wajumbe wa baraza kuu la CUF na kamati ya uongozi ya chama wangefanyiwa mapokezi makubwa katika ofisi hizo lakini yaliahirishwa ghafla baadaye usiku kwa kuhofia kuwapo vurugu.

Kiongozi wa wabunge wa CUF waliokuwa wameandaa mapokezi hayo, Riziki Shahari alisema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa wameahirisha mapokezi hayo baada ya kujiridhisha kuwa hali ya usalama siyo nzuri.

“Tunazo taarifa kuwa yapo makundi hatari ya watu yanayoishi ndani ya ofisi huku yakilindwa na vyombo vya dola tangu ofisi hiyo iporwe na aliyewahi kuwa mwanachama na kiongozi wa juu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akishirikiana na watu wanaomuunga mkono.

 “Tunajipa muda wa kushauriana na viongozi wa juu wa chama chetu huku tukiwaomba wanachama wote walioko Dar, mikoani na Zanzibar wawe watulivu kwani chama kina viongozi makini na hawawezi kuwa tayari kuona maisha ya wanachana na viongozi yanahatarishwa kwa kuigeuza ofisi kuu kuwa uwanja wa mapambano,” alisema Shahari.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya CUF, Julius Mtatiro alisema wabunge 41 kati ya 43 wa CUF walioandaa mapokezi hayo walikuwa wamekwishafika Dar es Salaam, lakini wamechunguza na kubaini kuwa yangeleta maafa.

Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF – Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alisema pamoja na hayo, chama hicho kimeshamalizana na Profesa Lipumba na kusisitiza kuwa si mwanachama tena.

Ofa Ya Vitabu Vya Hadithi na Riwaya za Kusisimua Toka kwa Mtunzi Aliyebobea Eddazaria g.Msulwa

0
0

Ofa Ya Vitabu Ya Kufunga Mwezi Wa 9

Hard Day Sh 3500

Sex Dealers Sh 3000

My Mom's Friend Sh 4500

Vitabu Hivi Vinapatikana Kupitia Whatsapp Na Email Tu, Wasiliana Nami 0657072588  Au 0768516188

Taarifa Ya Kanusho Kuhusu Tangazo La Ajira Serikalini

0
0
Kuna tangazo ambalo linasambazwa kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii lenye kichwa cha habari ‘’Sekretarieti ya Ajira yatangaza zaidi ya nafasi za kazi 1,000’’. Likionyesha kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,101 kwa niaba ya waajiri mbalimbali Serikalini.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira anapenda kuwataafu wadau na wananchi wote kwa ujumla kuwa taarifa hiyo haina ukweli wowote na inalenga kuupotosha Umma, hivyo wananchi wote wanapaswa kuzipuuza. 

Matangazo yote ambayo hutolewa na Serikali kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni lazima yaonekane kwenye Tovuti ya Sekretarieti ya Ajira www.ajira.go.tz au portal ya Ajira ambayo ni portal.ajira.go.tz.

Kama mnavyofahamu hivi karibuni Serikali ilitoa taarifa ya kusitisha Ajira mpya Serikalini kwa ajili ya zoezi la uhakiki wa Watumishi hewa kama ambavyo taarifa ilivyotolewa hapo awali, kwa kuwa zoezi hilo bado halijakamilika tunaomba wananchi wote na wadau wa Sekretarieti ya Ajira waendelee kuvuta subira hadi pale zoezi hilo litakapokamilika na taarifa rasmi itatolewa na Mamlaka husika.

Sekretarieti ya Ajira inapenda kuomba radhi kwa wale wote waliopata usumbufu kutokana na tangazo hilo lenye nia ya kupotosha Umma. 

Aidha,tunaendelea kuwasisitiza wadau wetu wote kuwa, wanapoona matangazo ya kazi yanayodaiwa kutolewa na Sekretarieti ya Ajira katika baadhi ya mitandao ya kijamii wasiyokuwa na uhakika nayo wajiridhishe kwa kuangalia katika tovuti na portal ya Sekretarieti ya Ajira kabla ya kuyafanyia kazi.

Aidha, Sekretarieti ya Ajira inapenda kutoa taarifa kuwa haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wenye nia ya kuupotosha umma kupitia taarifa zinazosambazwa ambazo hazina ukweli.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.

Tarehe 30 Septemba, 2016

Dawa Asilia Zinazo Tibu Tatizo La Kutokwa Na Kinyama Ama Uvimbe Kwenye Sehemu Ya Haja Kubwa.

0
0
Kutokwa  na  kinyama  ama  uvimbe  kwenye sehemu  ya  haja  kubwa  ni  tatizo  linalo  wakabili  maelfu ya watu  duniani.

Tatizo  hujulikana  kwa  Kiswahili  kama  Bwaziri,  katika  lugha  ya kisukuma  na  kinyamwezi  huitwa  “Man’gondi” na  katika  lugha  ya  kiingereza  hujulikana  kama  Hemorrhoids.

AINA  ZA  BAWAZIRI : Kwa mujibu  wa  tafiti mbalimbali  za  kitaalamu, zipo  bawaziri  za  aina  mbili, bawaziri  ya  ndani  na  bawaziri  ya  nje. Kwa  kawaida  mtu  huweza  kuwa  na  moja  wapo kati  ya  aina  hizo   na  wakati  mwingine, mtu  mmoja  anaweza  kuwa  na  bawaziri  za  aina  zote  mbili  kwa  wakati  mmoja.

NINI  HUSABABISHA  BAWAZIRI ?

Mpaka   sasa  wataalamu  bado  hawaja  baini  chanzo  halisi  cha  tatizo  la  bawaziri. Hata  hivyo  tafiti  mbalimbali za  kitaalamu  zinabainisha  mambo  kadhaa  yanayo  changia  kutokea  kwa  tatizo  la  bawaziri.

Mambo  hayo  ni  pamoja  na :

i. Kukosa  choo  kwa  muda  mrefu

ii. Kuharisha  kwa  muda  mrefu

iii. Kukaa  kwenye  choo  kwa  muda  mrefu

iv.Kukaa  kwa  muda  mrefu

v. Unene  na  uzito  kupita  kiasi: Tafiti  mbalimbali  zina onyesha  kuwa, asilimia  kubwa  ya  watu wenye  tatizo  la  unene  na  uzito  ulio zidi, huwa  katika  hatari  kuu  ya  kupatwa  na  tatizo  la  bawaziri

vi. Ujauzito :  Tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu  zinaonyesha  kuwa, asilimia  kubwa  ya  wanawake  wajawazito  huwa  katika  hatari  ya  kupatwa  na  tatizo  la  bawaziri, sababu  ikiwa  ni  kuongezeka  kwa  shinikizo  ndani  ya  mfuko  wa  uzazi.

vii.  Kutofanya  mazoezi  kwa  muda  mrefu

viii. Kutotumia  vyakula  vyenye  nyuzi nyuzi

ix.Sababu za  kinasaba : Tafiti  zinaonyesha  kuwa, wapo  watu wanao  patwa  na  bawaziri, kwa  sababu  za  kijenetiki
NINI  DALILI  ZA  BAWAZIRI ?

Dalili  kuu  za  bawaziri  ni  pamoja  na  kutokwa  na  kinyama  ama  uvimbe  kwenye  sehemu  ya  haja  kubwa, kukosa  choo, kupatwa  maumivu makali  sana  wakati  wa  kujisaidia  au wakati  unatembea  na  wakati  mwingine  maumivu  huendelea  hata  ukiwa haupo katika  matendo  niliyo  yataja  hapo  juu. Dalili  nyingine  ni  pamoja na  kuhara  damu  ama  kutoa  kinyesi  chenye  damu.

JINSI  YA  KUJIKINGA  USIPATWE  NA  BAWAZIRI :

Kujikinga  usipatwe  na  bawaziri, unashauriwa

i. Kujenga  tabia  ya  kuwa  unakula  vyakula vyenye  nyuzi nyuzi ( fibre) kwa wingi

ii. kula  matunda  kwa wingi

iii.Kunywa  maji mengi

iv.Fanya  mazoezi  ya  mwili  mara  kwa  mara

v. Usikae   maliwatoni kwa  muda  mrefu

vi. Usiruhusu  unene  na  uzito  kubwa.

TIBA  ASILIA  YA  TATIZO  LA  BAWAZIRI :

Zipo  tiba  mbalimbali  za  asilia  ambazo  zina  tibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la bawaziri

Baadhi  ya  tiba  hizo  ni  kama  ifuatavyo :

i. MKATABAWAZIRI : Ni tiba  ya  asili  inayo  tibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la bawaziri ndani  ya  siku  ishirini  na  moja. Mbali  na  kutibu  bawaziri, MKATABAWAZIRI  inatibu  pia, tatizo  la kukosa  choo  (  constipation ) , kusafisha  tumbo na  kuondoa  koletsrol mbaya  mwilini.

ii. LUFAMBO  ama  UFWAMBO :   Huu  ni  mti  unato  tumika  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  bawaziri. Mti  huu  hutoa  matunda  yenye  rangi mbili, nyekundu  na  nyeusi.

Jinsi  ya  kutumia  ufwambo  katika  tiba  ya  bawaziri, chemsha  mizizi na / au majani  yake kasha  tumia  kunywa  asubuhi  mchana  na  jioni  kwa  siku  thelathini.  Shida  yako  itapona.  Mti  wa  ufwambo, mbali na  kutibu  tatizo  la  bawaziri,. Unatibu  pia  tatizo  la  kuharisha kusikokoma.

iii.MKOMAVIKALI : Huu  ni  mti mwingine  ulio fanyiwa  utafiti  na  kuthibitishwa  kitaalamu  kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo la  bawaziri.  Jinsi  ya  kutumia  mti  huu, chukua  mizizi yake   kasha  chemsha  halafu mpe mgonjwa  anywe  mara  tatu  kwa  siku  asubuhi  mcxhana  na  jioni, unaweza  pia  kuikausha  na  kuisaga  na  kasha  kuchemsha  unga unga  wake  na  kuutumia  kwa  kunywa.

iv. NUN’GANU’NGA : Huu  ni  mti  mwingine  unato tibu  tatizo  la  bawaziri. Mbali na  kutibu  bawaziri, mti  huu  unatibu  pia tatizo  la ngiri,  maumivu  ya  tumbo  pamoja  na  minyoo  ya  tumboni.   Sehemu  ya  mti  huu  inayo  tumika  kama  tiba  ya  magonjwa  ni mizizi  pamoja  na  majani  yake.

v. ZUMANGUKU : Huu  ni mti mwingine  ambao  umethibitishwa  kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la  bawaziri. Jinsi  ya  kutumia  mti  huu  kama  tiba, chemsha  majani  yake  kishe mpe  mgonjwa  anywe  mara  tatu kwa  siku  kwa  siku  thelathini.

vi. LUWAWA :  Luwawa  hutibu   tatizo  la  bawaziri  kwa mgonjwa  kuchemsha  majani  yake  ni  kasha  kutumia  kwa  kunywa  mara  tatu kwa  siku, kwa  siku  thelathini.

HIYO  NI  BAADHI  YA  MITI  INAYO  TIBU  NA  KUPONYESHA  KABISA  TATIZO  LA  BAWAZIRI. ENDELEA  KUTEMBELEA  :   www.neemaherbalist.com    KILA  SIKU  ILI  UPAT  KUFAHAMU  KUHUSU   MITI  INAYO  TIBU  MAGOINJWA  MBALIMBALI  YANAYO  MSUMBUA  MWANADAMU.

MAKALA  HAYA  YAMELETWA  KWENU  KWA  HISANI YA  DUKA  LA  NEEMA HERBALIST. DUKA  LINALO  UZA DAWA  MBALIMBALI  ZA  ASILI.  TUNAPATIKANA UBUNGO  JIJINI  DAR  ES SALAAM,  JIRANI  NA  SHULE YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, NYUMA  YA JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.

Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83  84.

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  tiba mbalimbali  za  asili, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu:


Upate  kujua  mambo  mbalimbali  kama  vile :

1.JINSI  SUALA  LA  UPIGAJI PUNYETO  LINAVYO SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.

2.JINSI SUALA  LA  KITAMBI, UNENE  NA  UZIO ULIO  ZIDI, LINAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA KIUME

3.UHUSIANO  ULIOPO  KATI  YA  TATIZO  LA NGUVU  ZA  KIUME  NA  MAGONJWA MBALIMBALI  KAMA  VILE : Kisukari, Presha, Shinikizo  La  Damu, Kolestrol Mbaya  Mwilini , Magonjwa  Ya  Moyo, Magonjwa  Ya  Figo,  Ngiri,  Msongo  wa  Mawazo, Maumivu  Ya  Mgongo, Magonjwa  Katika  Mishipa  Ya  Kusafirishia  Damu Mwilini  na  Hitilafu  Katika  Mfumo  wa  Usafirishaji  na Utiririshaji  wa  Damu  mwilini.

4.JINSI  UNAVYO  WEZA  KUONDOA  KITAMBI  NA KULIFANYA  TUMBO  LAKO  KUWA  FLAT KABISA  NDANI  YA  SIKU  14

5.JINSI  UNAVYO WEZA  KUPUNGUZA  UNENE NA UZITO MKUBWA  NDANI  YA  SIKU  THELATHINI.

6.KWA  MTU  ULIE  KONDA  NA  KUDHOOFIKA; JINSI  UNAVYO WEZA   KUNENEPA  NA KUREJESHA  AFYA  YAKO  NDANI  YA  SIKU THELATHINI.

7.JINSI UNAVYO  WEZA  KUPONA  KABISA  TATIZO LA  BAWAZIRI NDANI  YA SIKU  THELATHINI.

8.JINSI UNAVYO  WEZA  KUTIBU  TATIZO  LA UVIMBE  WA  TUMBONI  PAMOJA  NA  UVIMBE WA  KWENYE  KIZAZI  NDANI  YA SIKU THELATHINI.

Chadema Waahirisha Tena Maandamano ya Oparesheni UKUTA

0
0

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe ametangaza kuwa Operesheni UKUTA iliyokuwa ifanyike Oktoba Mosi haitofanyika tena.

Mbowe amesema hayo leo baada ya kimya cha muda mrefu tangu kuahirishwa kwa maandamano Septemba Mosi. Aidha, Mbowe amesema kuwa hawatataja tarehe ya kufanya maandamano ili kutompa adui nafasi ya kujipanga. Amesisitiza kuwa maandamano yapo, ila tarehe hawataweka hadharani.

Operesheni hii ilikuwa ifanyike Septemba Mosi mwaka huu lakini iliahirishwa ili kuwapa nafasi viongozi wa dini kuweza kukutana na kujadiliana na Rais Dkt Magufuli juu ya mustakabali wa hali ya kisiasa nchini kufuatia kuzuiwa kwa shughuli mbalimbali za kisiasa.

Hadi leo viongozi wa dini bado hawajakutana na Rais Magufuli licha ya wao kueleza kuwa Rais Magufuli hajakataa kukutana nao kama inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Octoba 1

Rais Magufuli afunga Maadhimisho ya Miaka 52 ya JWTZ ashuhudia Zoezi la Amphibious Landing Bagamoyo

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 30 Septemba, 2016 amefunga maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kwa kushuhudia zoezi la medani liitwalo ''Amphibious Landing'' lililofanyika katika Kijiji cha Baatini Wilaya ya Bagamoyo. Mkoani Pwani.

Zoezi hilo lililochukua muda wa wiki mbili, limeshirikisha kamandi zote tano za JWTZ  ambazo ni Nyika, Majini, Anga, Kamandi ya Makao Makuu na  Jeshi la Kujenga taifa limefanyika katika ufukwe wa bahari ya Hindi na limetekelezwa kwa mfano wa mapambano ya kivita yaliyohusisha kutua nchi kavu kutoka majini na kukomboa eneo lililotekwa.
 
Akizungumza baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Rais na Amiri jeshi Mkuu Dkt.John Pombe Magufuli amempongeza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange pamoja na Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ walioshiriki katika zoezi hilo ambalo limefanywa kwa umakini, uhakika na weledi wa hali ya juu.
 
''Kwa kweli nimefurahi na nimeamini tuna wapiganaji wa kutosha katika maeneo yote, hii mikakati na mipango iliyotumika inaonesha tuna jeshi imara na linaloaminika'' amesema Dkt. Magufuli.  
 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu amewahakikishia Makamanda na Wapiganaji wote wa JWTZ kuwa Serikali yake itahakikisha inaendeleza na kuongeza zaidi juhudi zilizofanywa na Marais waliopita kwa kuimarisha na kuwa na jeshi la kisasa linalotumia vifaa na teknoljia ya kisasa na pia itahakikisha maslai ya askari yanaboreshwa.
 
Aidha, Dkt. Magufuli ametaka Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuimarishwa zaidi na kujielekeza katika uzalishaji mali ikiwemo uwekezaji katika viwanda.
 
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein ambaye pamoja na kuipongeza  JWTZ amesema miaka 52 tangu kuanzishwa kwa Jeshi hilo Watanzania wanashuhudia jeshi lao likiwa imara na makini zaidi kwa ajili ya kulinda nchi.
 
Nae Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake na nia yake ya kuliimarisha Jeshi na kuboresha maslai ya Makamanda na Wapiganaji na ameongeza kuwa anajivunia kuwa kiongozi  wa Jeshi hilo.
 
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na Viongozi wengine wakiwemo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Zanzibar Abdulhamid Yahaya Mzee.
 
Rais na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. John Pombe Magufuli, amemuagiza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange kuwapa ajira za JWTZ askari mgambo wote walioshiriki zoezi la Amphibious Landing.
 
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam.
30 Septemba, 2016
Amiri  Jeshi Mkuu Rais Dkt John Pombe Magufuli, Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein na meza kuu wakipiga saluti wakati wa wimbo wa Taifa wakati wa kufunga Zoezi la medani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani  Septemba 30, 2016
Ndege vita zikipita angani katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani  Septemba 30, 2016
 Vifaru vinavyopita baharini na nchi kavu vikiwa katika zoezi la "Ambhibious Landing"  katika kilele cha maadhimisho ya miaka 52 ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Baatini, Bagamoyo mkoa wa Pwani Septemba 30, 2016.PICHA NA IKULU.

Serikali Yasogeza Mbele Field Kwa Wanafunzi Wa Afya 2016

0
0

Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia ,wazee na watoto inawatangazia wahitimu wote wa vyuo vikuu vya kada mbalimbali za afya wanaopaswa kufanywa mafunzo ya utarajali yani ‘internship’ ambao ni madaktari wa meno, wafamasia, wauguzi, wataalamu wa Radiolojia, wataalamu wa maabara na wataalamu wa afya ya mazingira kwamba pamoja na kuwa walipaswa kuanza mafunzo yao leo Oktoba 1, 2016  ambayo ilikuwa ni tarehe rasmi ya kuanza mafunzo hayo itatangazwa hapo baadae.

Wizara ya Afya imesema kuwa kuchelewa huko ni kutokana na juhudi zinazoendelea kufanywa na Wizara ili kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanaanza katika namna na mfumo uliobora zaidi.

Aidha Mganga Mkuu wa Serikali Profesa Muhammad bakari kambi  (Pichani juu) amesema kuwa mara baada ya juhudi hizo kukamilika wataalamu tajwa watafahamishwa rasmi na hivyo kuwaomba wataalamu hawa na wadau wengine kuwa na subira.

“Tunapenda kuwafahamisha wahitimu ambao walikuwa hawajapangiwa vituo vya kufanyia mafunzo kwa vitendo, kuwa utaratibu unafanywa kuhakikisha kwamba wanapangiwa vituo hivi karibuni ambapo mtandao utafunguliwa na wahusika watapewa taarifa”. Amesema Prof. Muhammad Bakari

Waziri Mkuu Atimiza Ahadi Ya Kuhamia Dodoma

0
0
Waziri MKUU Kassim Majaliwa amesema kuanzia sasa mtu yeyote mwenye shida ya kuonana naye itabidi amfuate Dodoma na kwamba atarudi Dar es Salaam pindi akiitwa na Mheshimiwa Rais au Makamu wa Rais.

Ametoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Septemba 30, 2016) wakati akizungumza na viongozi mbalimbali na wakazi wa mji wa Dodoma waliofika kumpokea mara baada ya kuwasili mjini hapa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi yake aliyoitoa Julai 25 kuwa atahamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu.

“Tukio hili la kuhamia Dodoma si la mzaha, hakuna siasa na wala si jaribio. Tumeshakeleza. Kama kuna waliokuwa wanafiria kwamba halitekelezeki watambua kwamba tayari tumeshafika. Na kuanzia sasa atakayetaka huduma ya Waziri Mkuu

Waziri Mkuu amesema Dodoma si ndogo kama baadhi ya watu wanavyodai na kwamba  huduma zilizopo zinatosha kukidhi mahitaji ya sasa. "Mkakati uliopo wa kupanua huduma za tiba, maji, umeme na masoko utawezesha watumishi wote kuishi bila bugudha yoyote."

“Awamu ya kwanza inaanzia Septemba hadi Februari mwakani. Mimi nimeshatangulia na wanaofuata ni mawaziri na manaibu wao wote, Makatibu Wakuu na Naibu Makatibu Wakuu wote. Natambua kwamba wote wana nyumba za kuishi na kama wapo ambao hawana hawazidi asilimia tano na nyumba zipo

Amewataka watumishi wote wa Serikali watambue kwamba safari imeshaanza na kila mmoja ajipange, na akarudia wito wa Mheshimiwa Rais kwamba atakayegoma kuhamia Dodoma atakuwa amejifukuza kazi.

Waziri Mkuu amewataka watendaji wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) wasifanye kazi kwa mazoea, bali wabadilike na kwa kuwa amehamia Dodoma ameahidi kuafuatilia kwa karibu zaidi.

Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Waziri wa Nchi (OWM SUBKAV), Jenista Mhagama amesema kilichofanyika leo ni uthibitisho kuwa yale ambayo Serikali ya Awamu ya Tano iliahidi sasa hivi imeanza kuyatekeleza.

"Tuliahidi kukusanya kodi, tuliahidi elimu bure, tuliahidi kupambana na mafisadi, tuliahidi kuondoa watumishi hewa, tuliahidi kuifufua ATCL na kununua ndege mpya na yote tumetekeleza,” amesema.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. George Simbachawene amesema uamuzi wa kuhamia Dodoma ni uthibitisho kuwa  viongozi wetu kweli wamedhamiria kutekeleza ahadi ya Baba wa Taifa ya kuhamishia makao makuu ya nchi hapa Dodoma.

"Dodoma imeanza kuchangamka na hii ni fursa tosha kwa mkoa wetu kubadilika. Tushirikiane na CDA kuijenga Dodoma mpya. Kitendo cha Mheshimiwa Waziri Mkuu kuingia Dodoma leo hii maana yake ni kwamba Serikali iko rasmi Dodoma," amesema.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Manaibu Waziri Anthony Mavunde na Dk. Ashatu Kijaji, Makatibu Wakuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Rais (Utumishi), Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo, wazee wa mkoa huo, viongozi wa dini, viongozi wa taasisi zilizoko mkoani na baadhi ya wananchi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA


Ofisi ya Bunge, TCRA Kuburuzwa TAKUKURU kwa tuhuma za rushwa

0
0

Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), imeifikisha Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika Taasisi ya Kudhibiti na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kutokana na harufu ya rushwa kwenye ununuzi.

Mwenyekiti wa Bodi ya PPRA, Dk Matern Lumbaga, alisema hayo jana Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu ukaguzi wa Mamlaka hiyo, kwenye ofisi, taasisi na mashirika ya umma 70 kati ya 506.

Kwa mujibu wa Dk Lumbaga, katika ukaguzi huo wa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/16, taasisi tisa za umma, ikiwamo Ofisi ya Bunge na wizara moja, zilibainika kuwa na viashiria vya rushwa.

Taasisi zingine mbali na Bunge ambazo nazo zimepelekwa Takukuru ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Makumbusho ya Taifa, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma na Wakala wa Umeme Vijijini (REA).

Zingine ni Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es Salaam (Darts), Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge na Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

“Lengo la ukaguzi huo ni kuangalia kama ununuzi ulizingatia matakwa ya Sheria ya Ununuzi ya mwaka 2011 na mikataba ya ununuzi iliyoingia katika kipindi hicho.

“Kati ya taasisi za umma 506, ni taasisi 70 pekee ndizo zilifanyiwa ukaguzi kati ya Aprili na Septemba, ambapo taasisi 15 zimewekwa kwenye kundi la wizara, idara na wakala wa Serikali, mamlaka ya Serikali za Mitaa 25 na mashirika ya umma 30,” alisema.

Alisema pia mikataba 21,313 yenye thamani ya Sh trilioni 1.05 ilifanyiwa ukaguzi na kati ya hiyo, 845 ilihusu kazi za ujenzi; 7,179 vifaa na bidhaa; 103 ushauri wa kitaalamu; 3,083 ununuzi na mikataba na 453 makubaliano maalumu.

Dk Lumbanga alisema uchambuzi wa matokeo hayo ulionesha kuwa taasisi 22 zilikidhi viwango, 38 kiwango cha kati na 10 kiwango kisichoridhisha yaani chini ya asilimia
60.

Katika ukaguzi huo, walibaini malipo tata ya Sh. bilioni 1.32 kutoka kwenye taasisi nne kwenda kwa wakandarasi kwa kazi ambazo hazijafanyika.

Alitaja taasisi hizo kuwa ni Jiji la Dar es Salaam, Rea, Taasisi ya Mifupa Muhimbili (Moi) na Mfuko wa Pensheni wa LAPF. 

Ofisa Mtendaji Mkuu wa PPRA, Dk Laurent Shirima alisema wakati wowote Bodi ya Wakurugenzi itaita wakuu wa taasisi zilizofanya vibaya, wajieleze kwa nini wasichukuliwe hatua kutokana na uzembe na kuisababishia Serikali hasara.

Alisema pia kwa taasisi zilizopata chini ya asilimia 78, Mamlaka hiyo itaandaa utaratibu wa kuwapa mafunzo ya uelewa wa matumizi ya Sheria ya Ununuzi na kanuni zake.

“Ingekuwa rahisi kubaini upungufu iwapo taasisi zote zingewasilisha taarifa zao PPRA kwa wakati,” alisema.

Mbarawa ataka ujenzi Flyover ya TAZARA uharakishwe

0
0
Serikali imeitaka Kampuni ya kikandarasi ya Sumitomo Mitsui inayojenga mradi wa ujenzi wa barabara ya juu (Flyover) katika makutano ya barabara ya Nyerere na Mandela eneo la Tazara kumaliza ujenzi huo kwa wakati

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa ndiye aliyetoa agizo hilo na kusema kuwa mradi huo ni muhimu ili kusaidia kupunguza tatizo la msongamano.

Akizungumza mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo jijini Dar es salaam, Profesa Mbarawa amesema kuwa kukamilika kwa mradi huo kutajenga historia nchini kutokana na kuwa ni wa mwanzo kujengwa.

“Nimefurahi kuona mradi huu upo katika hatua nzuri, naomba mkamilishe mradi huu unakamilika kwa ubora na kwa wakati ili tatizo la msongamano lililopo katika maeneo haya kupungua au kuisha kabisa”, amesema Waziri Mbarawa.

Aidha, Waziri Mbarawa amewataka wananchi wa maeneo hayo kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi huyo ili kurahisisha kazi za ujenzi huo kukamilika kwa wakati na kupata matokeo chanya.

“Nawaomba watanzania wenzangu kuwa wavumilivu na usumbufu wowote utakaojitokeza katika kipindi hiki chote, kwani ukamilifu wa mradi huu utasaidia kupunguza tatizo la msongamano katika barabara hizi”, amefafanua Waziri Mbarawa.

Katika hatua nyingine, Profesa Mbarawa amekagua daraja la watembea kwa miguu eneo la Buguruni Sheli na kuwataka wananchi wa maeneo hayo kulitunza daraja hilo ambalo uwepo wake umesaidia kupunguza ajali katika maeneo hayo.

“Ni matumaini yangu sasa wakazi wa maeneo haya mtavuka kwa amani kupitia daraja hili, na ajali zilizokuwa zikitokea maramara hazitakuwepo tena”’, amesema Profesa Mbarawa.

Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) Eng. Patrick Mfugale amemuahidi Waziri huyo kumaliza kwa wakati ujenzi huo na kumhaakikishia Waziri kuwa ujenzi wa barabara hiyo utakuwa na viwango vilivyo bora.

Mradi wa Tazara Flyover ni msaada kutoka Serikali ya Japan ambao umegharimu shilingi bilioni 93.4 na unatarajiwa kukamilika mwezi Oktoba mwaka 2018

Bodi Ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Yatangaza Majina Ya Wanafunzi Waliokosea Kujaza Form Za Mikopo 2016/2017

0
0

During the exercise of processing 2016/2017 loan application forms, the Board has come across loan applications which are missing some vital information such as applicant’s and guarantor’s signatures. For that reason, the Board would like to inform loan applicants with such incompleteness to visit HESLB offices in Dar es Salaam.

Loan applicants and/or their guarantors who have not signed their documents are required to physically visit HESLB offices on Plot No. 8, Block No. 46 Sam Nujoma Road, Mwenge, Dar es Salaam to append signatures to their loan applications from Monday 3rd September 2016.

Loan applicants who did not attach applicant’s photo, guarantor’s photo (to their application forms) or who attached uncertified photocopies of birth certificates, academic certificates, guarantor’s particulars such as photocopy of Passport or voter’s registration cards; should send the missing particulars with covering letters indicating their full names and form four index numbers with year of completion e.g. S0143.0012.2013 via EMS through the following address:

The Executive Director,
Higher Education Students’ Loans Board,
P. O. Box 76068,
DAR ES SALAAM.

The deadline for correction of the shortcomings is Friday 7th October 2016.

All attachments must be certified by a Commissioner of Oaths.

NB:    The Board is:
•  cautioning loan applicants to be careful with some unscrupulous individuals who might take advantage of this opportunity to make financial demands.
•Reminding loan applicants that correction of missing items is not a guarantee to be awarded loans.
• Incomplete application forms will not be considered for further processing until the missing information is provided within specified time. 

*The list of loan applicants with missing signatures and other attachments can be viewed through: http://olas.heslb.go.tz

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 59 & 60 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

0
0

 Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilioishia...
Hadi kunapambazuka sikuweza kumuona nesi phidaya, hali ya hatari ikaanza kunijia kichwani mwangu na kuhisi nesi phidaya anaweza kuwa amekutwa na matatizo, mlango ukafunguliwa na wakaingia manesi wawili pamoja na madaktari wale wawili.Wakaanza kufungua kitandana na kukishusha chini kidogo hadi kikafikia usawa mzuri wa kuweza kusukumwa.Pasipo hata ya kunisemesha wakaanza kunisukuma na kunipeleka nisipo pajua huku nyuso zao zikiwa na tabasamu ambalo sikuliewewa nini maana yeke

Endelea...
Wakazidi kukisukuma kitanda nilicho lalia hadi hadi tukafika kwenye maja ya mlango ambao juu kuna maandishi ya kiharabu ambayo sikuweza kuyaelewa, nesi mmoja akausukuma mlango na kufunguka, na wakaniingiza ndani nikiwa juu ya kitanda changu, mwanga mwekundu wa taa ulioo ndani ya chumba ukazidi kuniogoesha.Chumba kizime kimezungukwa na mashine mbalimbali ambazo sikujua zinakazi gani.Daktari mmoja akachukua mashine yenye kimviringo mbele, kisha akakiwasha na kuanza kuzunguka, akachukua moja ya miwani kubwa ambayo ni nyeupe akaivaa na kuanza kucheka kitu kilichoo zidi kuniogopesha zaidi.

Gafla taa ya mwanga mweue ikawashwa na kuwafanya madaktari na manesi, kustuka, macho yetu wote tukayaelekezea mlangoni na kumuona nesi phidaya akiwa ameshika, bastola huku jasho jingi likiwa linamwagika usoni, akaanza kuzungumza kwa kiarabu na taratibu madaktari wakanyoosha mikono juu wakitetemeka, akazungumza neno lililo wafanya  madaktari kuanza kurudi nyuma kutoka kilio kitanda changu.
“eddy, wamekufanya chochote kibaya?”
“hapana”
“powa”

Nesi phidaya akazungumza neno jengine lililowafanya madaktari na manesi kulala chini, sakafuni huku mikono yao wakiwa wameiweka juu ya vichwa vyao.Nesi phidaya akanifwata hadi kitandani na kuuitisha mkono wake mmoja kwenye, mgongo wangu na kuniomba niwe kushuka chini, japo ninajihisi maumivu ila nikajikaza kiume kwani kuendelea kukaa haoa kutahatarisha maisha yangu.
“jikaze baba yangu”

Nesi phidaya alizungumza huku akiendelea kunishusha kwenye kitanda, akanisaidia kusimama vizuri, huku muhimili wangu wote wa kusimama nikiutegemea kutoka kwake, nesi phidaya akawatazama watu madaktari walio lala chini, akazungumza neno la ukali lililo wafanya madaktari na manesi kuzidi kuzifunika sura zao chini pasipo kuzinyanyua juu.Tukafanikiwa kotoka nje ya chumba walicho niingiza, nesi phidaya akafunga mlango kwa nje na sote tukaanza kuondoka taratibu huku nesi phidaya akiificha bastola yake na baadhi ya wahudumu wakabaki wakiwa wanatushangaa.Tukatoka nje na kukuta gari aina ya taksi ikiwa inatusubiria

“ahaaaa”
Nilitoa mguno wa maumivu baada ya mguu wangu nilio vunjika kugongwa kwenye mlango nilipokuwa ninajiaandaa kuingia ndani ya gari, siti ya nyuma
“pole eddy”
“asante”

Nesi phidaya akanisaidia kuingia ndani ya gari na kufunga, kisha yeye akaingia kwenye siti ya mbele kwa dereva na kumuongelesha dereva kiarabu na akaliondoa gari lake kwa kasi.
“asante sana, nesi phidaya”
“usijali nipo kwa ajili yako, ila ningependa uniite phidaya tu na si nesi phidaya”
“sawa”

Nikaendelea kujilaza kwenye siti ya nyuma ya taksi tuiyo ipanda, ila kuna mwanga mkali wa taa ukawa unaingia kwenye gari letu, ikanilazima kunyanyua kichwa changu kutazama nyuma, nikaona gari ndogo ikija kwa kasi sana,
“phidaya kuna watu wanatufwata nyu……”

Kabla sijamalizia sentesi yangu nikastuka risasi ikipiga kwenye kioo cha nyuma na kunifanya nirudi chini, na kulala kwenye siti yangu.Dereva akaanza kulalamika, na phidaya akaanza kumuhimiza dereva kuongeza mwendo kasi wa gari,risasi zipatazo nne zikaingia kwenye kioo cha nyuma cha gari na kushangaa ragi ikiaanza kuyumba huku dereva akiwa ameulalia mskani wake,

“shit dereva amepigwa risasi ya kichwa”
Phidaya alizungumza kwa kuchanganyikiwa kiasi kwamba na mimi nikaanza kuchanganyikiwa, risasi zikaendelea kumiminika ndani ya gari na kuzidi kunichanganya
“mtoe huyo dereva”

Nilizungumza kwa sauti ya juu, phdiaya akafanya kama nilivyo muagiza, akaufungua mlango wa dereva na kumsukumia kwa nje, kisha akafunga mlango na kukaa kwenye siti ya dereva

“nipe bastola yako”
Phidaya akanirushia kwa nyuma bastola yake, nikauchukua mkanda wa siti wa siti ya nyuma na kuanza kuuvuta nikijaribu kuukata ila nikashindwa.Nikamtazama
“eddy unataka kufanyaje?”
“nataka kukata huu mkanda niufunge mguu wangu unavuta sana”

Phidaya akafungua kwenye kisanduku kilichopo pembeni ya siti ya dereva, na kuanza kutoa vituvitu, vilivyomo ndani ya kisanduku, akabahatika kupata mkasi na kunikabithi.Nikauchukua mkasi na kuukata mkanda wa siti na kuufunga mguu wangu ulio vunjika, maeneo ya mapajani, hadi nilipo hakikisha kwamba nimeunguza misuli kuvuta, nikajilaza vizuri kwenye siti na kutoa magazine ya bastola na kukuta ikiwa na risasi za kutosha.

Chadema yamtangazia vita Profesa Lipumba ..........Yeye ampa masharti Maalim kuingia ofisini

0
0
Wakati  Mwenyekiti wa CUF aliyefutiwa uanachama, Profesa Ibrahim Lipumba akitangaza masharti kwa Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad ya kuingia kwenye ofisi za chama hicho Buguruni, Dar es Salaam Chadema imetangaza kutoshirikiana naye.

Akizungumza kwenye makao makuu ya Chadema jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliwataka viongozi wa chama chake, kutotoa ushirikiano kwa Profesa Lipumba, badala yake wampuuze na wamwone kuwa msaliti wa harakati za kudai haki.

Wakati akisema hayo, Profesa Lipumba akiwa katika Ofisi Kuu za CUF, alitoa masharti kwa Seif kama anataka kufika ofisini hapo, kuwa lazima akiri kumtambua na kumkubali kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho.

Mbowe katika mkutano wake na waandishi wa habari, alisema Lipumba, Msajili wa Vyama vya Siasa na taasisi ya utafiti ya Twaweza, ni mawakala wa Serikali wa kuzia harakati za kupigania demokrasia nchini.

Alisema harakati za kuzuia wapinzani kupigania haki, hazifanywi moja kwa moja na Serikali, bali na wakala wao ambao wanakuja kwa sampuli mbalimbali.

“Kamati Maalumu ya Kamati Kuu inatambua mgogoro ndani ya CUF, hivyo chama chetu hakimtambui Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF wala Mwenyekiti Mwenza wa Ukawa.

“Kamati inalaani uamuzi wa Jaji Francis Mutungi wa kuivuruga CUF kwa kujaribu kumrudisha madarakani Lipumba ambaye alijiuzulu katika mazingira yanayoashiria kununuliwa na CCM, kwa lengo la kusaliti Ukawa kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana,” alituhumu.

Kuhusu Jaji Mutungi, Mbowe alimtangaza kama adui wa demokrasia na vyama vingi na kudai kuwa pamoja na kuwa Jaji, hana weledi wa kusimamia vyama vya siasa.

Alitumia nafasi hiyo kubainisha kuwa chama hicho hakina sababu hata moja ya kumheshimu mtu kama Jaji Mutungi ambaye alisema anaonekana kutumika na CCM.

“Mtu ambaye tunamwona msomi, ambaye hapewi mamlaka yoyote ya kisheria ya kuamua ndani ya vyama vya siasa, badala ya kusaidia vyama kumaliza migogoro, amekuwa akichangia migogoro.

“Anaona vyama vinaminywa na Serikali anakaa kimya, lakini kila akizungumza anavikandamiza zaidi, huyu mtu ni adui mkubwa sana,” alisema.

Alimhakikishia Jaji Mutungi kuwa mbinu zake za kudhoofisha vyama vya upinzani hazitafanikiwa, kwani hakuwa Msajili wa kwanza, na kwamba matendo hayo hayatafifisha vyama hivyo.

Kuhusu Twaweza, alidai kuwa imekuwa ikilipwa na Serikali itangaze mambo mbalimbali siku moja kabla ya Ukuta kwa kutoa takwimu alizoziita za kipumbavu na kwamba wamekubali kujitwisha uendawazimu.

“Hawa ni mawakala wa Serikali na wanajulikana. Ni Mtanzania mwendawazimu pekee ambaye utamwambia kwamba hali ya nchi, Serikali inakubalika kwa asilimia 96, lazima uwe mwendawazimu na utafiti huo hauwezi kulisaidia Taifa,” alisema.

Wakati Chadema ikitoa kauli hiyo, hali ya kisiasa ndani ya CUF ilizidi kuwa mbaya kutokana na pande mbili zinazosigana kutunishiana misuli.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari waliofika Ofisi Kuu zaCUF jana, Profesa Lipumba alisema alipata taarifa kwamba Maalim Seif angefika ofisini hapo juzi, hivyo alimsubiri ampangie kazi.

Alisema kama Seif angefika, kabla ya kufanya kazi na Mwenyekiti jambo la kwanza ingekuwa ni kumtambua kwa nafasi hiyo ambayo alivuliwa na kikao kisicho halali.

“Ni lazima akija hapa afanye kazi na Mwenyekiti na walinzi wetu wanamfahamu, wasingemfanya chochote kwa kuwa ni kiongozi wao pia,” alisema na kuongeza:

‘’Huwezi kuja ofisi za chama, halafu ukasema humtambui Mwenyekiti, analijua hilo kwamba akija hapa ni lazima afanye hivyo, kwani anajua kikao kilichokaa Zanzibar ni cha ujanjaujanja.’’

Profesa Lipumba alisema ndiye kiongozi wa walinzi wote wa chama, hivyo wana haki ya kumlinda wanavyotaka wao kwa maslahi ya chama.

Alisema Maalim Seif anatakiwa kujiamini na kufika kwenye ofisi hiyo ili afanye kazi na Mwenyekiti wake za kujenga chama na hakuna kikundi kilichokuwa kimeandaliwa kufanya vurugu au kugombana na kiongozi huyo.

“Anaweza akaja lakini hawezi kusema kuwa kuna kikundi, hawa ni walinzi wanaomlinda tangu anagombea nafasi hiyo mwaka 2014, hatuna kikundi ni Blue Guard na anapaswa kuwaheshimu na si kuwaita kikundi,’’ alisema Lipumba.

Alisema hakuwa na taarifa rasmi ya ugeni wa Maalim Seif, bali alisikia kwenye vyombo vya habari, kwamba atakuja na wabunge pamoja na wajumbe kutoka Zanzibar, hivyo alikuwa anasubiri ujio wake kwa kuwa ana ofisi yake.

‘’Maalim Seif ana ofisi hapa, yeye kuja ni jambo la kawaida, ila tangu nimeanza kufanya shughuli za chama sijamwona ofisini, hana haja ya kutangaza anaweza akaja ofisini kwa Mwenyekiti wake, apate miongozo ya kazi,’’ alisema.

Kuhusu ujio wa wabunge na wajumbe wa Baraza Kuu alisema atawajulisha muda wa kukutana, kwa kuwa hajawaita hawapaswi kufika katika ofisi hiyo kama kikundi.

Habari za ndani kutoka ofisi hizo, zilidai kuwa Lipumba alilala ndani ya ofisi hizo usiku wa kuamkia jana pamoja kundi la wafuasi wake waliokuwa wakihofia kwamba upande wa Maalim Seif ungefika usiku kuchukua ofisi yao.

Mmoja wa wafuasi wa Lipumba ambaye alikuwa katika ofisi hizo jana, alidai baadhi ya wafuasi wa kiongozi huyo walikesha hapo kwa lengo la kumlinda kwani alikuwa anafanya kazi zake.

‘’Lipumba hakubaki ofisini kwa kuogopa kundi la Maalim Seif ila alikuwa akifanya kazi zake kwa kuwa ni muda mrefu tangu ajiuzulu hakuwa ofisini hivyo kazi zimezidi,’’ alisema.

Hata hivyo, Lipumba alikana kulala ofisini bali alifika saa 1:45 asubuhi.Katika ofisi hizo magari ya Polisi yalikuwa hayakauki kuanzia saa moja asubuhi huku Lipumba akieleza kwamba hakuomba msaada wala ulinzi wowote wa Polisi, kwa kuwa alikuwa ofisini. 

Juu ya taarifa kwamba Maalim Seif aliomba ulinzi Polisi, wamsindikize alisema ni jambo la ajabu.

‘’Ikiwa kuna ukweli katika hilo nastaajabu, unaomba ulinzi kwenda ofisini kwako, ina maana walinzi alionao wa Serikali na wana chama hawatoshi?’’ Alihoji Lipumba.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images