Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

22 Watiwa Mbaroni kwa tuhuma za Kutaka Kuchoma Moto Ofisi za CUF Dar es Salaam

$
0
0
Ikiwa zimepita siku kadhaa tangu Kamati ya Uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kutuhumu baadhi ya viongozi wake waliosimamishwa uanachama kupanga njama za utekaji viongozi wa chama hicho, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikiliwa wanachama wa CUF 22 kwa tuhuma za kupanga njama za kufanya fujo na kuchoma mali za ofisi za chama hicho.

Ikumbukwe kuwa, Septemba 16,2016 CUF kupitia Kurugenzi yake ya Habari na Uenezi ilitoa taarifa ya jaribio la utekaji wa Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha CUF, Joran Bashange ambapo chama hicho kiliwatuhumu Magdalena Sakaya, Abdul Kambaya na Profesa Ibrahim Lipumba kuwa walinzi wao walijaribu kufanya tukio hilo.

Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Simon Sirro jana alisema wanachama hao walikamatwa na zana za kufanyia uhalifu yakiwemo mapanga, Jambia, visu na chupa za kupulizia 10 zikiwa kwenye boksi lenye maandishi ya lugha ya kichina.

Watuhumiwa hao walikamatwa Septemba 25,2016 maeneo ya Mwananyamala katika gari ya abiria ambayo ruti yake inapitia njia ya Buguruni-Mwananyamala.

Kamanda Sirro alisema watuhumiwa hao walikamatwa baada ya askari kupata taarifa kwamba wamekuja Dar es Salaam wakitokea visiwani Unguja kutoka katika matawi mbalimbali ya chama hicho kwa lengo la kufanya fujo.

Aidha, Sirro alisema baada ya watuhumiwa hao kuhojiwa, walieleza kuwa wamekuja kutokana na maelekezo ya kiongozi wa CUF Nassoro Ahmad Mazrui ambaye ni Naibu Katibu mkuu wa chama hicho aliyewataka kuungana na walinzi wenzao waliopo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Buguruni.

Hata hivyo, baada ya taarifa za watuhumiwa hao kukamatwa kuenea katika mitandao ya kijamii, baadhi ya watu walimhusisha aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya uongozi wa CUF kwa muda Julias Mtatiro kuhusika katika mipango ya njama hizo.

Lakini Kamanda Sirro alieleza kuwa hadi sasa hajapokea taarifa hiyo ya kuhusika kwa Mtatiro na kwamba taarifa hizo si za kweli.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 57 & 58 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0

Mtunzi: Eddazaria g.Msulwa


Ilioishia
Nikamkabidhi msichana hati yangu ya kusafiria cha kwanza akanitazama machoni, kisha hati yangu ya kusafiria akaiweka kwenye mashine inayotoa ripoti kwenye kioo kikubwa cha ‘computer’.Askari anaye kagua akaanza kazi yake ya kukipitisha kifaa chake kuanzia miguuni, msichana akanitazama kwa macho makali kisha akatazama tena kwenye kioo cha kumputer yake, nikatazama pembeni na kuwaona askari wawili walio shika mbwa wakubwa weusi wakianza kunisogelea, huku wakiwa na bubduki zao mikononi, kifaa cha ukaguzi kikaanza kutoa mlio wa kelele huku kikiwaka taa nyekundu kilipo fika maeneo ya shingoni

Endelea
“vua cheni yako”
Askari anaye nikagua aliniambia na kunifanya niivue cheni, niliyo ivaa shingoni mwangu.Akaendelea kukipitisha kifaa chake kwenye mgongo hadi chini kwenye miguu,
“safari njema”
Dada aliyekuwa anaikagua hati yangu ya kusafiria alizungumza huku akinikabidhi hati yangu ya kusafiria, huku usoni mwake akiwa ameachia tabasamu pana lililo pendezeshwa na mwanya wake mwembamba.
“asante na wewe pia kazi njema”

Nikapita kwenye kizuizi na kuwafanya sashah na rajiti kushusha pumzi nyingi kwani walihisi kwamba tayari nimeingia kwenye mikono ya askari, tukaingia ndani ya ndege, cha kushukuru mungu, siti zetu tatu zipo sehemu mmoja, hatukukaa hata dakika nyingi, rubani akatuomba tufunge mikanda yetu kwani ndege itajiandaa kuruka muda sio mrefu.Ndani ya dakika kadhaa tukaanza kuiacha ardhi ya nchini kenya
“eddy” rajiti aliniita
“naam”
“unajua kwamba unaonekana tofauti sana”
Alizungumza kwa sauti ndogo
“kweli?”
“ndio, umekuwa bonge la handsome”
“mmmmm”
“kweli vile”
“jamani acheni kelele watu wamelala” sashah alizungumza
“ahaaa shauri yao, bwana”

Masaa yakazidi kusongo mbele, na ndege yetu ikatua baadhi ya nchi ambapo, baadhi ya abiria walishuka na kupanda abaria wengine na safari ikaendelea.Tukafika nchini iraq, majira ya saa moja saa tisa alasiri huku sote tukiwa tumechoka kwa uchovu wa kukaa kwenye ndege takribani masaa kumi na tano, kutokana hatukuwa na mizigo tukawahi kupanga mstari wa kutokea sehemu ya kukaguliwa, huku moyoni mwangu nikiwa ni naomba sana nisiweze kushtukiwa kwa lolote, na nikafanikiwa kutoka njee ya uwanja wa ndege pasipo mtu yoyote kunistukia kwamba nimevalia sura bandia,

Sikuwa na sehemu yoyoote ninayo itambua na wenyeji wangu wakubwa ni sashah na rajit.Tukapanda kwenye taksi mojawapo iliyopo kwenye maegesho ya uwanja wa ndege na sashah akazungumza kwa lugha ya kiarabu na dereva tuliye mkuta ndani ya teksi hii, tukafika kwenye moja ya hotel kubwa iliyo andikwa kwa maandishi ya kiarabu na kila kitu ambacho wanakizungumza shasha na watu wengine, sikuweza kukifahamu kutokana siitamui lugha ya kiarabu
Sashah akamaliza kuzungumza, na wahudumu na akakabidhiwa funguo moja, akatufwata sehemu tulipo simama na rajit, tukaingia kwenye lifti iliyo tupeleka hadi ghorofa ya sita, na tukaingia kwenye chumba ambacho sashah alikodisha

“eddy utakaa hapa siku mbili, ili uyazoee mazingira kisha tutaelekea makao makuu”
Sashah alizungumza
“na nyinyi munakwenda wapi?”
“sisi, tunakwenda kufwatilia mambo muhimu, kwa ajili ya kazi zetu, kikubwa ni wewe kuwa makini katika hili eneo.Tumekulipia chakula kila mahitaji utakayo yahitaji tumegharamia”
“sasa jam….”
“eddy hapo hakuna cha sasa kikubwa ni wewe kuwa makini, usipende kujitokeza tokeza kwa watu kwani watu wa huku hawana huruma, wana roho za kinyama.Yaani ukitembea sana wewe mwisho wako ni kule chini kwenye sehemu ya chakula”
“sawa nimewaelewa, je nikihitaji hudumu ya kuwapigia wahudumu wa hii hoteli?”
“kuna kitabu pale juu ya meza kwenye ile simu basi utaweza kuitumia hiyo sawa, na kabla sijasahau chukua hizi cuppon ukienda kuchukua chakula unaonyesha, zipo za ana mbili, moja ya chakula na nyingine ya kinywaji.Ukizipoteza baba utashinda njaa hizi siku mbili”
“powa”

Robert PJN Kaseko: Salaam Za Pongezi Kwa Rais Wangu John Pombe Magufuli.

$
0
0

Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa dhati Kabisa kama Kijana &  Kada  mtiifu wa Chama Cha Mapinduzi  ninaetambua juhudi/Jitihada zako unazozionyesha kila siku iitwapo leo za kuwaletea Maendeleo Wananchi wako napenda kukupongeza kwa Kutimiza Ahadi yako ya kufufua Shirika la Ndege la Taifa " ATCL" kwa kununua Ndege Mbili Mpya na leo tumepokea Ndege ya Pili.

Sasa Watanzania Wote wamejionea wenyewe na Ulimwengu umejionea wenyewe ya Kwamba   Tanzania Mpya yaja.

Mheshimiwa Rais Hongera sana na Mungu akubariki, Akulinde na kukujaalia Afya njema ili ukatimize vyema Majukumu yako ya kuwatumikia Watanzania kwa Kuwaletea Maendeleo.

Robert PJN Kaseko
Mjumbe Baraza Kuu UVCCM Mkoa wa Arusha
September 27, 2016.

Majina Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Chuo Kikuu Ruaha University- RUCU 2016/2017

Samuel Sitta apelekwa ujerumani kutibiwa

$
0
0

HALI ya afya ya Spika mstaafu, Samuel Sitta si nzuri,baada ya Serikali kumpeleka nchini Ujerumani kwa matibabu zaidi.

Habari za uhakika  zinasema Sitta alipelekwa Ujerumani juzi kwa matibabu baada ya afya yake kubadilika ghafla.

“Nilimtembelea siku moja kabla ya kupelekwa nje ya nchi, kwa kweli hali ya afya yake ilikuwa imedhoofu, namwombea Mungu amsaidia apone haraka ili arudi kuendelea na majukumu yake.

“Nimesikitishwa mno na taarifa za kuzushiwa kifo mzee wangu huyu, Mungu ni mwema najua bado anampigania uhai wake…hii tabia ya mitandao ya kijamii kumzushia mtu kifo sijui inafaidika nini.

“Mpaka anaondoka nchini kwenda matibabu natambua amekuwa asikumbuliwa mno na tatizo la miguu, sasa mimi si daktari wake siwezi kuongeza zaidi,”kilisema chanzo chetu.

Septemba 19, mwaka huu, Rais Dk. John Magufuli alimtembelea Sitta hospitalini alikolazwa kwa muda sasa kumjulia hali, kisha kumwombea dua Mungu amsaidie.

Siku iliyofuata Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa naye alimtembelea hospitalini kumjulia hali.

Sitta ameshika  nyadhifa mbalimbali, zikiwamo za Spika wa Bunge kuanzia mwaka 2005 hadi 2010, uwaziri na ubunge kwa kipindi kirefu.

Mahakama yakana kuitambua kampuni iliyotumiwa na NHC kumtimua Mbowe

$
0
0
Mahakama Kuu imekana kuitambua kampuni ya Fosters Auctioneers and General Traders iliyohusika kuondoa vitu vya kampuni za Freeman Mbowe kwenye jengo la Shirika la Taifa la Nyumba (NHC).

Hayo yalibainishwa jana na kiongozi wa jopo la mawakili wanaomtetea Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa Chadema, Peter Kibatala wakati wa usikilizwaji wa maombi yaliyofunguliwa na mlalamikaji huyo kupitia kampuni ya Mbowe Hotels Ltd dhidi ya NHC na kampuni hiyo ya udalali.

Wakati wa usikilizwaji wa maombi hayo jana, pamoja na mambo mengine Mbowe aliiomba Mahakama iliamuru NHC na kampuni hiyo wamrejeshe katika jengo hilo pamoja na vifaa na mali zake zinazoshikiliwa na kampuni hiyo.

Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa mteja wake aliondolewa katika jengo hilo kinyume na sheria.

Alidai dalali aliyetumiwa na NHC kuziondoa kampuni za Mbowe katika jengo hilo hajasajiliwa na Mahakama kwa kuwa walimwandikia Msajili wa Mahakama barua kujua kama anatambulika, lakini alijibu kuwa haimtambui.

Kutokana na majibu ya msajilihuyo kupitia barua yake ambayo wameiwasilisha mahakamani kama kielelezo, Kibatala alidai sheria na mchakato mzima uliotumika vilikuwa ni batili.

Mawakili wa NHC, Ipilinga Panya na Aloyce Sekule walidai shirika hilo kabla ya kumtimua Mbowe lilimwandikia notisi ya siku 30 iliyokwisha kisha akaongezewa siku 30 zingine kama sheria inavyotaka ambazo ziliisha na kumpa tena siku 14, lakini hakulipa deni.

Wakili wa kampuni ya Foster Auctioneers and General Traders, Aliko Mwamanenge alidai madai ya kuwa mteja wake ni dalali wa Baraza la Usuluhishi na kwamba anayesajiliwa kama dalali ni mtu binafsi na siyo kampuni, hayana ukweli kwani upande wa mlalamikaji ulipoandika barua kuulizia uhalali wake ulipaswa kuuliza jina la mmiliki kampuni hiyo.

Hata hivyo, wakili wa mlalamikaji Kibatala alidai notisi zinazodaiwa kuandikwa na NHC zilipelekwa mahali pasipohusika kwa kampuni ya Free Media badala ya Mbowe Hotels ambayo ina mkataba na NHC. Baada ya kusikiliza hoja za pande zote, Jaji Sivangilwa Mwangesi anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Oktoba 18, mwaka huu atakapotoa uamuzi wa maombi hayo ya mlalamikaji.

Septemba Mosi, wafanyakazi wa kampuni ya udalali ya Foster Auctioneers and General Traders walifika kwenye ofisi za kampuni ya Free Media na kuondoka vifaa mbalimbali vya kazi, zikiwamo kompyuta na viti kwa madai kwamba mmiliki wake, Mbowe anadaiwa na NHC fedha nyingi za kodi ya pango.

Majaliwa Akutana Na Wawekezaji Kutoka Korea Ya Kusini.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amekutana na wawekezaji wa kampuni tisa za nchini Korea Kusini  na kumuahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwekeza katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu, afya na michezo.

Wawekezaji hao wanatoka kampuni ya Sima textile, ESM, Jusung Solar Engineering, Seongnam City FC, Yeong Yang City Korea,Ulsan Vocational Training, Egis Smart City, MBN

Akizungumza na wawekezaji hao jana jioni (Jumanne, Septemba 27, 2016) kwa niaba ya Mhe. Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu alisema kwamba Tanzania ni sehemu salama kwa uwekezaji ikiwa na fursa za uwekezaji kwenye sekta nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Licha ya mazingira mazuri ya uwekezaji pia aliwahahakishia ulinzi kwenye uwekezaji wao.

Waziri Mkuu alisema Korea ya Kusini inashirikiana vizuri na Tanzania hivyo wanatarajia mengi kutoka nchini huko kupitia wawekezaji hao.

Wawekezaji hao tayari wamefanya mazungumzo na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela jijinii Mwanza na kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) kwa ajili ya miradi minne ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya maji, kiwanda cha nguo, zana kubwa za kilimo na mafunzo ya ufundi.

Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo, Bw. Son Young Soo alisema amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza  nchini.

Naye, Bw. Jihyun Kim wa  kampuni ya Yeong Yang City Korea ambayo inashughulikia masuala ya kilimo cha mbogamboga alisema watawekeza kwenye kilimo  hususan cha zao la pilipili na watajenga kiwanda kwa ajili ya usindikaji.

Naye Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee alisema klabu yake ipo tayari kuwekeza katika shule ya michezo kwa vijana ili kuongeza kasi ya maendeleo ya soka.

LIVE: Fuatilia Matangazo ya Moja kwa Moja Rais Magufuli Akizindua Ndege Mbili Mpya za ATCL

$
0
0
Fuatilia Matangazo ya Moja kwa Moja Rais Magufuli Akizindua Ndege Mbili Mpya za ATCL

Rais Dkt Magufuli Azindua Rasmi Ndege Mbili Mpya Zilizonunuliwa Na Serikali Kwa Ajili Ya Atcl Jijini Dar Leo

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 28 Septemba, 2016 amezindua ndege mpya mbili aina ya Bombardier Dash 8 Q400 zilizonunuliwa na Serikali kwa ajili ya kutumiwa na Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Uzinduzi wa ndege hizo za kisasa zilizotengenezwa nchini Canada, umefanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiwemo Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai, Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Ian Myles, Mawaziri, Wabunge, Viongozi wa Wafanyabiashara, Taasisi mbalimbali na wadau wa usafiri wa anga.

Kabla ya kuzindua ndege hizo zenye uwezo wa kubeba abiria 76 kila moja, Rais Magufuli ameshuhudia makabidhiano ya mkataba wa ukodishaji wa ndege hizo kutoka kwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwa niaba ya Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA) kwenda kwa Katibu Mkuu Uchukuzi Dkt. Leonard Chamriho kwa niaba ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Taarifa ya ununuzi wa ndege hizo iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa ndege hizo ni mali ya Serikali na zitakodishwa kwa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) kwa lengo kutoa huduma za usafiri wa anga ndani na nje ya nchi.

Imeongeza kuwa ndege hizo zimenunuliwa kwa kuzingatia kuwa zinafaa kufanya kazi katika mazingira ya Tanzania ikilinganishwa na ndege nyingine za jamii yake, na imetaja manufaa hayo kuwa ni pamoja na uwezo wa kuruka na kutua katika viwanja vya lami na visivyo vya lami, matumizi madogo ya mafuta, kuwa na injini zenye nguvu zaidi na kubeba mzigo mkubwa.

"Ni dhairi kuwa ndege hizi zitaimarisha mtandao wa huduma za usafiri wa anga kwa soko la ndani, lakini pia zitaongeza ushindani na kuleta unafuu wa bei kwa watumiaji wa usafiri wa anga, vilevile zitaimarisha sekta za biashara na uwekezaji na kuwezesha watalii kutembelea vivutio vya ndani ya nchi" ameeleza Balozi Kijazi.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa na kutimia kwa ahadi aliyoitoa ya kununua ndege mpya ili kufufua usafiri wa anga kupitia ATCL na ameahidi kuwa Serikali imeanza mazungumzo ya kununua ndege nyingine mbili zitakazofanya safari za ndani na nje ya bara la Afrika ambapo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160, na nyingine itakuwa na uwezo wa kubeba abiria zaidi ya 240.

"Kwa sababu fedha za kununulia ndege hizo zote mbili kubwa zipo, tukinunua ndege ya kubeba watu 240 itakuwa inatoka hapa Dar es Salaam hadi Marekani bila kutua popote, itaondoka hapa Dar es Salaam mpaka China bila kutua popote ili watalii wanaotoka China, Marekani, Urusi, Ujerumani na nchi nyingine wasifikie nchi nyingine, watue hapa moja kwa moja na waangalie maliasili zetu tulizonazo, utalii wetu upande, na huo ndio mwelekeo wa nchi yetu tunaoutaka" amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika kuleta mabadiliko yenye manufaa kwa nchi na kuwapuuza watu wanaobeza juhudi hizo wakiwemo waliobeza ununuzi wa ndege hizo kwa kujenga hoja zisizo za msingi.

Aidha, Dkt. Magufuli ameitaka Bodi na Menejimenti ya ATCL kufanya kazi kwa weledi na ufanisi huku akiisisitiza kuondoa kasoro zote zilizosababisha kampuni hiyo kudorola ikiwemo kuchuja na kuwaondoa wafanyakazi watakaoshindwa kuendana na mwelekeo unaostahili, wasio waadilifu na waaminifu, wasaliti na wahujumu.

Rais Magufuli pia amewataka Watanzania wote wafanyabiashara, wakulima na wafanyakazi kusafiri kwa kutumia ndege hizo ili Kampuni ya ATCL ijiimarishe na iweze kujiendesha badala ya kutegemea ndege za Serikali.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

28 Septemba, 2016

Mti Wa Upupu Hutumika Katika Tiba Ya Tatizo La Ngiri Kwa Wanaume

$
0
0
Ngiri  ama  hernia  ni  tatizo  linalo  wakabili  wanaume  wengi  duniani. Moja  kati  ya  dalili  kuu  za  tatizo  la  ngiri  ni  pamoja  na  kusinyaa  kwa  korodani  moja  au  zote, kusinyaa  kwa  maumbile  ya  kiume.

Kama  ilivyo  kwa  magonjwa  mengine  mengi, tatizo  la  ngiri  linaweza  kutibika  kwa  kutumia  dawa  mbalimbali  za  asili.


Ganda  la  tunda  la  upupu. Ndani  yake  zinakaa  mbegu  saba.

Ipo  miti  mingi  sana  inayo  weza  kutumika  kama  tiba  ya  tatizo la  ngiri. Katika  makala  haya, nitaelezea  kuhusu   miti kumi  ambayo imefanyiwa  utafiti  wa  kisayansi na  kuthibitika kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ngiri. Kati  ya  miti  hiyo, umo pia  mti  wa  upupu  ambao  unajulikana  sana  kwa  sifa  yake  ya  kuwasha  sana.
 
Miti  hiyo  ni  kama  ifuatavyo :

1.    MULIWANIFWENGI : 


Mti  wa  Muliwanifwengi hapa  ukiwa  umetoa  matunda. Matunda  ya  mti  huu pia  ni  dawa ambayo husaidia  kusafisha  damu.
 Hili  ni  jina  la  lugha  ya  kinyamwezi. Wanyamwezi  ni  wenyeji  wa  mkoa  wa  Tabora, ambao  unapatikana  magharibi  wa  nchi  ya  Tanzania.  Mti  huu una  uwezo mkubwa  sana  wa  kutibu  na kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ngiri.
Muliwanifwengi

Jinsi  unavyo  tumika; mgonjwa  anachukua  mizizi  anachemsha   pamoja na  maji  kisha  anatumia  kunywa  mara  tatu  kwa  siku  asubuhi  mchana  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.
Mbali na  kutibu  tatizo  la  ngiri, mti  huu  pia  una  uwezo   wa  kutibu  ugonjwa  wa  kaswende  pamoja  na  kusafisha  mishipa  ya  damu.
Chipukizi  la  Muliwanifwengi  ambalo  bado halijakomaa

2.MUSISIGULU :  Kama  ilivyo  kwa  mti  wa Muliwanifwengi,  jina  la  mti  wa  Msisigulu  linatokana  na  lugha  inayo  tumiwa  na  watu  kutoka  kabila  la  wanyamwezi  wa  mkoani Tabora.
Mti  huu  umefanyiwa  utafiti  wa  kisayansi  na  kuthibitika  kuwa  na  uwezo  mkubwa  wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ngiri.

Pamoja  na  ngiri, mti  wa  Musisigulu, hutibu  pia   matatizo  ya  mapafu.

Jinsi  ya  kutumia  mti  wa  Msisigulu  katika  tiba  ya  ngiri, chemsha  mizizi  yake  kwenye  kisha  tumia  kunywa mara  tatu  kwa  siku  kwa siku  thelathini.
 

Upupu

3. MUMULIMULI :   Mumulimuli ni  jina  la  kinyamwezi. Mti  huu  umethibitishwa  kisayansi  kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  tatizo  la  ngiri, minyoo ya  tumboni, kaswende  pamoja  na  kisonono.

Jinsi ya  kutumia  mti  huu, chemsha  mizizi  yake  kisha  tumia  kunywa  mara mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  kwa  siku  thelathini.

4.Muzegezega :   Mti  huu  pia  umefanyiwa  utafiti  wa  kina  na  kuthibitika  kuwa  na  uwezo  mkubwa wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ngiri.
 
Pamoja  na  kutibu  ngiri, mti  wa  Muzegezega, una  uwezo wa  kutibu pia  magonjwa  mengineyo  kama  vile ;   Kufeli  kwa  moyo, Homa  Ya  Manjano, Kikohozi, Pumu, Mkamba ( Bronchitis ), Matatizo  katika  ubongo  pamoja  na  Degedege.

5.  Kasolanhanga  au  Sawi  au  Asparagus ; Huu  ni  mmea  uliothibitika  kisayansi  kuwa  na  uwezo  mkubwa sana  wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ngiri. Katika  lugha  ya  kinyamwezi, hujulikana  kama  Kasolanhanga  au  Sawi , lakini  katika  kiingereza, hujulikana  kama  Asparagus.
 
Mmea  huu  ambao  ni jamii  ya  mbogamboga, mbali  na  kutibu  tatizo  la  ngiri, hutumika  pia  kama  tiba  ya  ugonjwa  wa  Gono.

Jinsi  inavyo  tumika, mgonjwa   atachemsha  mizizi  ya   mti  huu  kwenye  maji, kisha  atatumia  kunywa  asubuhi  mchana  na  jioni  kwa  muda  wa  siku  thelathini.

6.  Nyanya  Chungu : Nyanya  chungu  ni  mti  wenye  faida  nyingi  sana  katika  afya  ya  mwanadamu. Karibu  kila  kiungo  kinacho  patikana  katika  mmea  wa  Nyanya  Chungu  ama  Ngogwe  hutumika  kama  tiba  kwa  mwanadamu. Kuanzia  matunda,  majani, hadi  mizizi.

Kujitibu  tatizo  la  ngiri  kwa  kutumia  mmea  wa  Nyanya  Chungu,  chukua  mizizi  yake  kisha  ichemshe  kwenye  maji , halafu  tumia  kunywa  maji hayo, mara  tatu  kwa  siku, asubuhi  na  jioni  kwa  siku  thelathini.    Tatizo lako  litapona  kabisa.

7.    Bumu  ama  Upupu ;   Bumu  ni  lugha  inayo  tumiwa  na  waluguru wenyeji  wa  mkoa  wa  Morogoro, wakimaanisha  mti  wa  Upupu.  Mti  wa  upupu  unajulikana  zaidi  kwa  sifa  yake  moja  kubwa, ambayo ni  kuwasha  sana.
 
Pamoja  na  kuwa  na  sifa  ya   kuwasha, mti  wa  upupu   una  faida  nyingi  sana za  kitabibu  pamoja  na  kiuchumi. Katika  makala  haya  ya  leo, nitaelezea  jinsi  mti  wa  upupu  unavyo  tumika  kama  tiba  ya  tatizo  la  ngiri.
 
Kutibu  tatizo  la  ngiri  kwa  kutumia  mti  wa  upupu, chukua  mizizi  au  majani  ya  mti  wa  upupu  ulio  komaa, kisha  chemsha  halafu  tumia  kunywa  mara  mbili  kwa  siku  asubuhi  na  jioni  kwa  siku  kumi  na  nne., na  tatizo  lako  litapona.  Waluguru  kutoka  mkoani  Morogoro, wanatumia  sana  mti  wa upupu  kama  tiba  ya  ngiri.  ( TAHADHARI :  WATU  WENGI  WANASHINDWA  KUTUMIA  VIZURI  MTI  VIZURI  KAMA  TIBA. HIVYO   HAUSHAURIWI  KUUTUMIA  MWENYEWE  BILA  KUPATA  USHAURI  NA  MSAADA  WA  MTAALAMU, NA  BADALA  ZINGATIA  MATUMIZI  YA  MITI  MINGINE )
Mbali  na  kutibu  ngiri, mti  wa  upupu  una uwezo pia  wa  kutibu  maradhi  ya  “Parkinson Desease”

8. Kiberuberu :  Huu  ni  mti  mwingine  ulio  fanyiwa  utafiti  na  kuthibitishwa  kitaalamu, kuwa  na  uwezo  wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la ngiri.  Kiberuberu  ni  jina  la  mti  huu katika  lugha  ya  kiluguru. Katika  lugha  hiyo  hiyo  ya  kiluguru, mti  huu  hujulikana  kama  Mguhu.
Mti  huu  hutumika  kwa  mgonjwa  kuchemsha  mizizi  yake  na  kisha  kutumia  kwa  kunywa, mara  tatu  kwa  siku  kwa  siku  thelathini.

9. Luhalamila  au  Luhambamti : Hili  ni  jina  kutoka  katika  lugha ya  Kiluguru  inayo zungumzwa  na  watu kutoka  jamii  ya  waluguru  wanao  patikana  mkoa  wa  Morogoro, nchini  Tanzania.  Mti  huu  umefanyiwa  utafiti  wa  kisayansi  na  kuthibitika  kuwa  na  uwezo wa  kutibu  na  kuponyesha  kabisa  tatizo  la  ukosefu  na  nupungufu  wa  nguvu  za  kiume
Jinsi  ya  kutumia  tiba  hii, mgonjwa  anatakiwa  kuchemsha  majani  yake  yakiwa  mabichi  na  kisha  kutumia  kunywa  mara  tatu  kwa  siku, asubuhi, mchana  na  jioni  kwa  siku  thelathini.

10.Luziwana :   Waluguru  wa  mkoani  Morogoro, wanautumia  sana  mti  huu  kama  tiba  ya  tatizo  la  ngiri. Mbali na  kutibu  ngiri,  mti  wa  Luziwana  hutibu  magonjwa  mengineyo  kama  vile  kuharisha  pamoja  na  maumivu  ya  tumbo.
Mgonjwa  anashauriwa  kuchemsha  mizizi  ya  mti  huu  na  kisha  kutumuia  kunywa  mara  tatu  kwa  siku  kwa  siku  thelathini.

KAMA  NILIVYO DOKEZA, HAPO  AWALI, TANZANIA TUMEBARIKIWA  KUWA  NA  MAELFU  YA  MITI  YENYE  UWEZO  WA  KUTIBU  MAGONJWA  NA  MATATIZO  MBALIMBALI  YA  KIAFYA  YANAYO MKABILI  MWANADAMU.  KATIKA  TATIZO  LA  NGIRI  PEKEE, KUNA  MAMIA  KWA  MAMIA  YA MITI  INAYO  TUMIKA  KUTIBU  TATIZO  HILO. KATIKA   MAKALA  HAYA  NIMEELEZEA  MITI  KUMI  TU.  KATIKA  MAKALA  ZA  USONI,  NITAELEZEA  PIA MITI  MINGINE, AMBAYO  INATIBU  TATIZO  LA  NGIRI.

MAKALA  HAYA  YAMELETWA  KWENU  KWA  HISANI  YA  DUKA  LA  NEEMA HERBALIST. DUKA  LINALO  UZA  DAWA  MBALIMBALI  ZA  ASILI.  TUNAPATIKANA  UBUNGO  JIJINI  DAR  ES SALAAM,  JIRANI  NA  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING, NYUMA  YA  JENGO  LA  UBUNGO  PLAZA.
 
Wasiliana  nasi  kwa  simu  namba  0766  53 83  84.
Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  tiba mbalimbali  za  asili, tutembelee  kila  siku  katika  blogu  yetu:

Upate  kujua  mambo  mbalimbali  kama  vile :

1.    JINSI  SUALA  LA  UPIGAJI PUNYETO  LINAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME.
2.    JINSI SUALA  LA  KITAMBI, UNENE  NA  UZIO  ULIO  ZIDI, LINAVYO  SABABISHA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA  KIUME
3.    UHUSIANO  ULIOPO  KATI  YA  TATIZO  LA  NGUVU  ZA  KIUME  NA  MAGONJWA  MBALIMBALI  KAMA  VILE : Kisukari, Presha, Shinikizo  La  Damu, Kolestrol Mbaya  Mwilini ,  Magonjwa  Ya  Moyo, Magonjwa  Ya  Figo,  Ngiri,   Msongo  wa  Mawazo, Maumivu  Ya  Mgongo, Magonjwa  Katika  Mishipa  Ya  Kusafirishia  Damu  Mwilini  na  Hitilafu  Katika  Mfumo  wa  Usafirishaji  na  Utiririshaji  wa  Damu  mwilini.
 
4.    JINSI  UNAVYO  WEZA  KUONDOA  KITAMBI  NA  KULIFANYA  TUMBO  LAKO  KUWA  FLAT  KABISA  NDANI  YA  SIKU  14
5.    JINSI  UNAVYO WEZA  KUPUNGUZA  UNENE NA  UZITO MKUBWA  NDANI  YA  SIKU  THELATHINI.
6.    KWA  MTU  ULIE  KONDA  NA  KUDHOOFIKA; JINSI  UNAVYO WEZA   KUNENEPA  NA  KUREJESHA  AFYA  YAKO  NDANI  YA  SIKU  THELATHINI.
7.    JINSI UNAVYO  WEZA  KUPONA  KABISA  TATIZO LA  BAWAZIRI NDANI  YA SIKU  THELATHINI.
8.    JINSI UNAVYO  WEZA  KUTIBU  TATIZO  LA  UVIMBE  WA  TUMBONI  PAMOJA  NA  UVIMBE  WA  KWENYE  KIZAZI  NDANI  YA SIKU  THELATHINI.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Alhamisi ya Septemba 29

Taarifa Ya Katibu Mkuu Juu Ya Upatikanaji Wa Dawa

Taarifa kutoka Ikulu: Uingereza yachangia Bilioni 6 kwa ajili ya ukarabati wa shule mkoani Kagera

$
0
0
Uingereza imetoa mchango wa Shilingi Bilioni 6 kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa miundombinu ya shule zilizopata madhara kufuatia tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera tarehe 10 Septemba, 2016.

Mchango wa fedha hizo umewasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Balozi wa Uingereza hapa nchini Mhe. Sarah Catherine Cooke, Ikulu Jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Balozi huyo kuwasilisha hati zake za utambulisho.

Balozi Sarah Catherine Cooke amemueleza Rais Magufuli kuwa pamoja na kutoa mchango wa fedha hizo Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May anatoa pole kwa Serikali ya Tanzania na kwa familia zote zilizopatwa na madhara ya tetemeko hilo na kwamba Uingereza imeona ishirikiane na Tanzania katika kukabiliana na madhara hayo.

“Uingereza imeguswa sana na maafa yaliyowakumba wananchi kufuatia tetemeko lililotokea Kagera, tunapenda kuona wananchi wanasaidiwa na wanafunzi wanaendelea na masomo” amesema Balozi Sarah Catherine Cooke.

Kwa Upande wake Rais Magufuli amemshukuru Waziri Mkuu wa Uingereza kwa mchango huo ambao utasaidia juhudi za Serikali za kuhakikisha inarejesha miundombinu iliyoharibika zikiwemo shule.

“Mhe. Balozi Sarah Catherine Cooke naomba unifikishie shukrani zangu za dhati kwa Waziri Mkuu wa Uingereza Mhe. Theresa May na umueleze kuwa kwa niaba ya watanzania hususani waliopatwa na madhara ya tetemeko la ardhi tumeguswa sana na moyo wake wa upendo kwetu” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli na Balozi Sarah Catherine Cooke pia wamezungumzia uhusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Uingereza ambapo Rais Magufuli ametoa wito kwa Balozi huyo kuendelea kuwahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Uingereza kuongeza uwekezaji wao hapa nchini na kwamba Tanzania itaendeleza na kukuza uhusiano huo.

“Uingereza ni rafiki na ndugu wa kweli na wa kihistoria kwa Tanzania, tunatambua kuwa nchi yenu ni mdau mkubwa na muhimu wa maendeleo yetu, hivyo tusingependa kupoteza rafiki na ndugu yetu, tuendelee kushirikiana kwa manufaa ya wananchi.

“Natambua kuwa Uingereza ina utaalamu mkubwa katika masuala ya gesi hivyo nawakaribisha waje wawekeze katika sekta ya gesi” amesisitiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli amesema Serikali itahakikisha fedha zote zinazotolewa kwa ajili ya kusaidia kukabiliana na madhara ya maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera zinafikishwa kwa walengwa na ameonya kuwa watakaothubutu kuiba fedha hizo watashughulikiwa.

Dkt. Magufuli amebainisha kuwa baada ya kutengua uteuzi na kuchukua hatua nyingine dhidi ya aliyekuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Bw. Amantius Msole na Mkurugenzi wa Manispaa ya Bukoba Bw. Steven Makonda pamoja na kumsimamisha kazi Mhasibu Mkuu wa Mkoa wa Kagera Bw. Simbaufoo Swai, amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei awachukulie hatua watumishi wa Benki hiyo walioshirikiana na watumishi hao kufanya njama za kuanzisha akaunti nyingine ya benki yenye jina linalofanana na akaunti rasmi ya “Kamati ya Maafa Kagera” kwa lengo la kujipatia fedha”

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

28 Septemba, 2016

Waziri Mkuu Atoa Mwezi Mmoja Kwa Watumishi Waliohamishiwa Kibiti Kuripoti Kituoni

$
0
0


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi. 
 
Amesema mtumishi yeyote aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti anatakiwa arudi na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si vinginevyo. 
 
"Tayari nimemuagiza ndugu Zuberi Samatabu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani kuhakikisha anasimamia watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya wilaya hiyo waishi Kibiti na si Ikwiriri," amesema. 
 
Kauli hiyo ya Waziri Mkuu ilifuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri Mkuu kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya 74 waliopangiwa kufanya kazi kwenye wilaya hiyo wameripoti katika kituo cha kazi 
 
 Ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi ya ujenzi wa nyumba za watumishi. 
 
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano, Septemba 28, 2016 wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo,utendaji wa serikali na kutoa msimamo wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yake ya kila siku 
 
Wakati huo huo Waziri Mkuu amewataka madiwani wa halmashauri hiyo wawe wakali katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kuomba omba kwa wakuu wa idara ili kuepuka kujishushia hadhi zao na kupelekea kuhujumiwa kwa miradi mbalimbali ya jamii 

Aidha aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kutengeneza mazingira ya kukaribisha wawekezaji na wahakikishe kwamba uwekezaji utakaofanyika hausababishi migogoro ya ardhi kwa wananchi. 
 
Waziri Mkuu amewahamasisha wananchi kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa maana Serikali imebeba mzigo wote wa gharama za ada na uendeshaji wa shule hizo. 
 
Alisisitiza kuwa njia pekee na ya haraka kuondoa umaskini ni kusomesha watoto Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameagiza halmashauri zote nchini kutumia mfumo wa kieletroniki katika ukasanyaji wa mapoto ili kuziba mianya ya uvujaji mapato haswa ya maliasili

Mpina ataka wanaosoma 'cheti' nao wapewe mikopo

$
0
0

Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira Luhaga Mpina amesema umefika wakati wa bodi ya mikopo ya elimu ya juu kuangalia upya sera ya ukopeshaji ili waweze kutoka mikopo kwa ngazi ya Astashada kwa masomo ya Sayansi ili kupata wataalam wengi wa fani hiyo
 
Mhe. Mpina amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kwenda sambamba ma mapinduzi ya maendeleo ya uchumi wa viwanda jambo ambalo litawezesha taifa kuwa na wataalam wengi wa mambo ya Sayansi na kuongeza tija katika ustawi wa maendeleo ya viwanda.

Akiongea na uongozi wa juu wa bodi ya mikopo ya elimu ya Visiwani Zanzibar, amesema Tanzania sasa inataka kuingia katika uchumi wa viwanda jambo ambalo linahitaji wataalam wengi wa masomo ya Sayansi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya Mikopo Tanzania, Abdul-Razaq Bandru, amesema kuwa bodi hiyo inafanya marekebisho mbalimbali ikiwemo kufanikisha mabadiliko ya kanzidata ili kuwafikia wadaiwa kwa urahisi zaidi kuliko ilivyokuwa hapo awali.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri Luhaga ametoa pongezi kwa tume ya taifa ya nguvu za atomic visiwani Zanzibar na kuwambia kuwa serikali ya Tanzania itaendelea kuimarisha na kuisimamia ofisi za tume hiyo visiwani Zanzibar.

Pato La Taifa Lakua Kwa Asilimia 7.9

$
0
0
Na Veronica Kazimoto

Pato la Taifa limekua kwa jumla ya thamani ya Shilingi trilioni 11.7 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ikilinganishwa na Shilingi trilioni 10.9 katika kipindi kama hicho cha mwaka 2015.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Dkt. Albina Chuwa amesema ukuaji wa pato la Taifa umetokana na shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo, mifugo, misitu na uvuvi ambapo shughuli  hizo zimekuwa  kwa asilimia 3.2 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 1.9 katika kipindi kama hicho mwaka 2015.

Kwa upande wa shughuli za uchumi za viwanda na ujenzi, Dkt. Chuwa alisema kumekua  na ongezeko la asilimia 20.5 katika kipindi hicho ukilinganisha na ukuaji wa asilimia 11.2 mwaka 2015 katika shughuli za uchimbaji madini, mawe na kokoto.

Aidha shughuli za uzalishaji bidhaa na viwanda zimeongeza kwa asilimia 9.1 katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka 2016 ukilinganisha na kasi ya asilimia 5.2 ya mwaka 2015.

Shughuli za uchukuzi na uhifadhi, Dkt. Chuwa amesema kuwa shughuli hizo zimekua kwa kiwango cha asilimia 30.6 zikisababishwa  na usafirishaji wa abiria kwa njia ya reli na barabara ikiwa ni pamoja na usafiri wa UDART.

Vilevile, shughuli za fedha na bima zimeongezeka kwa kasi ya asilimia 12.5 ikilinganishwa na asilimia 10.0 iliyopatikana katika kipindi kama hicho mwaka 2015.

Dkt. Chuwa amefafanua kuwa  huduma za elimu zimekua kwa kasi ya asilimia 8.0 katika robo hiyo ya mwaka ikilinganishwa na aslimia 7.4 ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2015 ambapo ukuaji wa shughuli hii imetokana na ongezeko la wanafunzi waliodahiliwa mwaka 2016.

Kwa upande wa Nchi za Afrika Mashariki ambazo zimeshachambua na kutoa Pato la Taifa katika kipindi kinachoishia Juni 2016 ni Rwanda ambapo Pato halisi la Nchi ya Rwanda katika kipindi cha Aprili – Juni 2016 limeendelea kukua kwa asilimia 5.4 ikilinganisha na asilimia 7.2 ya miezi kama hiyo mwaka 2015.

Takwimu za Pato la Taifa kwa robo mwaka hupimwa kwa kutumia thamani ya bidhaa na huduma zilizozalishwa nchini katika vipindi vya miezi mitatu mitatu ambavyo ni Januari – Machi, Aprili – Juni, Julai – Septemba na Oktoba – Desemba ambapo hujumuisha shughuli zote za kiuchumi, na hutumika katika kutathmini, kupanga mipango na kutayarisha sera za kiuchumi.
MWISHO.
 

Maalim Seif 'Kumshitaki' Lipumba kwa mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)

$
0
0
KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad, atatua ofisini kwa kiongozi mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Ernest Mangu, ili kumueleza mkakati wake wa kutua ofisini kwake, Buguruni jijini Dar es Salaam

Maalim anakwenda kwa IGP Mangu kumueleza adhima yake ya kufika ofisi kuu ya chama chake kesho Ijumaa, majira ya saa mbili asubuhi.

Hatua ya Maalim kutinga ofisini kwa IGP imetokana na kitendo cha jeshi la polisi kumsindikiza Prof. Lipumba kurejea ofisini; kusaidia uharibifu wa mali na kushambulia wanachama na wafuasi wa chama hicho.

Azma yake ya kwenda ofisini kwake kesho, inatokana na ofisi hiyo kuvamiwa na aliyepata kuwa mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba na genge la wafuasi wake.

Prof. Lipumba aliyejiuzulu uenyekiti wa CUF, 6 Agosti mwaka jana na miezi 11 baadaye akatangaza kurejea katika nafasi yake, amefukuzwa rasmi uanachama wa chama hicho Jumanne iliyopita na Baraza Kuu la uongozi la Taifa (BKT), lililokutana Visiwani.

Hata hivyo, Prof. Lipumba, ameendelea kung’ang’ania kuwa bado mwenyekiti halali wa chama hicho na msimamo wake huo, unadaiwa kuungwa mkono na msajili wa vyama vya siasa nchini, Jaji Francis Mutungi.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa watu waliokaribu na Maalim Seif zinasema, kiongozi huyo amekwenda kwa IGP Mangu kumtaarifu kuwa yeye na wabunge wa chama hicho, wamepanga kufika Buguruni kwa pamoja.

Anasema,“Maalim Seif anakwenda kumweleza IGP Mangu kwamba, tayari kumekuwepo na viashiria vya uvunjifu wa amani vinavyofanywa na watu wa Prof. Lipumba na kwamba chochote kitakachotokea, yeye na jeshi lake, wanapaswa kubeba msalaba.”

Prof. Lipumba alijiuzulu uenyekiti karibu na uchaguzi mkuu mwaka jana, akakimbilia nje ya nchi huku akidai hakufurahishwa na Edward Lowassa kuwa mgombea urais chini ya mwavuli wa vyama vinne ikiwamo CUF.

Ukawa unaundwa na vyama vinne; Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na National League for Democrats (NLD).

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 30

Serikali Yaridhia Utekelezaji Wa Ujenzi Wa Mradi Wa Bomba La Mafuta

$
0
0

SERIKALI ya Tanzania imeridhia rasmi utekelezaji wa mradi ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Kabaale katika Wilaya ya Hoima nchini Uganda hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania. 
 
Uamuzi huo umefikiwa katika Kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika  tarehe 29 Septemba, 2016  Ikulu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli. 
 
Taarifa ya kuridhiwa rasmi kwa mradi huo imetolewa naWaziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa ambaye amesema ujenzi wa mradi huo utakaoanza wakati wowote kuanzia sasa unatarajiwa kukamilika mwaka 2020. 
 
Amesema ujenzi wa bomba hilo unatarajiwa kugharimu dola za Marekani Bilioni 3.5 ambapo kati yake Dola Bilioni 3 zitatumika kujenga bomba upande wa Tanzania. 
 
Mradi huo mkubwa utatekelezwa kwa ubia wa ujenzi na uendeshaji kwa kushirikishaka mpuni za Total ya Ufaransa, CNOOC ya China, Tullow ya Uingereza na Serikaliza Tanzania na Uganda. 
 
Mhe. Majaliwa ameongeza kuwa bomba hilo lenye urefu wa kilometa 1,443 linatarajiwa kusafirisha mapipa 200,000 kwa siku ambapo kila pipa litaliingizia taifa Dola za Marekani 12.2. 
 
Amebainisha kuwa pamoja na kusafirisha mafuta ya kutoka nchini Uganda bomba hilo pia linatarajiwa kusafirisha mafutakutoka nchi nyingine zaJ amhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Sudani Kusini ambazo zimeonesha nia ya  kusafirisha mafuta yao kupitia bandari ya Tanga. 
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametaja faida nyingine ambazo Tanzania itazipata kutoka na namradi huo kuwa ni kupatika na kwa ajira zaidi ya 15,000 wakati wa ujenzi na ajira 2,000 baadaya ujenzi kukamilika, kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia, kukuza biashara katika ukanda wa kaskazini mwa Tanzania, kampuni za ujenziza Tanzania kupata kazi za ujenzi. 
 
Aidha, amesema Tanzania inatarajia kunufaika zaidi kwa kutumia bomba hilo kupitisha mafuta yanayotarajiwa kupatikana katika maeneo ya ziwa Tanganyika na Ziwa Eyasi.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMATANO, SEPTEMBA  28, 2016 

Waziri Mkuu kuhamia Dodoma leo

$
0
0

WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, anatarajia  kuhamia rasmi Dodoma leo.

Majaliwa anahamia mjini hapa ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ahadi ya Serikali ya awamu ya tano ya kuhamia Dodoma ambako ndiko yaliko makao makuu ya nchi.

Julai 25 mwaka huu, katika kilele cha siku ya mashujaa kilichofanyika mkoani hapa, Waziri Mkuu Majaliwa alisema ifikapo Septemba mwaka huu, Serikali itakuwa imehamia mjini hapa.

Hatua hiyo ya  waziri mkuu   ilitangazwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alipozungumza  na waandishi wa habari.

Alisema   Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili leo mchana akitokea   Dar es Salaam alikokuwa akiishi.

“Baada ya kuwasili hapa  atafanya ziara ya siku mbili katika Manispaa ya Dodoma Oktoba mosi na Oktoba 2 mwaka huu   kukagua hatua mbalimbali za maandalizi ya kupokea   Serikali mkoani hapa.

“Wakati wa ziara hiyo, atakagua majengo ya Serikali, maeneo ya kutolea huduma za afya, kituo cha umeme cha Zuzu, masoko, chanzo cha maji Mzakwe na maeneo ya viwanda.

“Kwa hiyo  maandalizi yote muhimu kwa ajili ya mapokezi ya waziri mkuu yamekamilika na uongozi wa mkoa unaendelea kuwajulisha wananchi na wadau wote katika maeneo yatakayohusika na ziara hiyo, washiriki kwa ukamilifu.

“Kwa niaba ya uongozi wa Mkoa wa Dodoma, tunampongeza Waziri Mkuu Majaliwa kwa kuitikia na kutekeleza uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli kwa kuhamia makao makuu mjini hapa,”
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images