Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Tanzania yaongoza duniani kwa utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia simu

$
0
0

Tanzania imetajwa kuwa nchi ya kwanza duniani kufanikiwa katika utoaji wa huduma za kifedha kwa kutumia mitandao ya simu.

Hayo yameelezwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) Eng. James Kilaba katika mkutano wa kimataifa wa wadau wa mawasiliano ulioandaliwa na Shirika la Kimataifa la Mawasiliano (ITU) kwa kushirikiana na TCRA pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

“Huduma za kifedha kwa mfumo wa digitali nchini Tanzania imepiga hatua kubwa ,ni nchi ya kwanza tuseme ulimwenguni kwa kutuma fedha na kutoa kwa njia ya simu bila matatizo yoyote, pia kuna mfumo wa kutuma fedha benki kwa kutumia mitandao ya simu,” alisema.

Kuhusu mkutano huo wa kimataifa ulioshirikisha washiriki zaidi ya 150 kutoka nchi mbalimbali duniani ambazo ni wanachama wa ITU, alisema umelenga kujadili namna ya kufikisha huduma za kifedha kwa njia ya simu katika sehemu ambazo hazifikiwi na huduma hiyo.

“Mkutano huu unasimamiwa na shirika la mawasiliano duniani ITC ambao umelenga kujadili namna ya kutumia mitandao ya simu kupeleka huduma za kifedha katika maeneo yasiyofikiwa na huduma za kifedha hasa ambako hakuna mabenki. Mkutano huu nchi imeamua kuuanda kwa ushirikiano wa TCRA na BOT, ” alisema.

Naye Gavana Mkuu wa BOT Profesa Benno Ndulu alisema hadi mwisho wa mwezi Julai mwaka huu takribani watanzania milioni 21.5 nchi nzima wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu.

“Hadi kufikia Julai, 2016 watanzania 21.5 milioni wanatumia mitandao ya simu walau mara 1 kwa mwezi idadi hii ni kubwa na kwamba inaonesha sekta hii inakua kwa kasi,” alisema.

Profesa Ndulu alisema kuwa huduma za kifedha kwa njia ya mitandao ya simu imesaidia kukuza uchumi wa nchi.

“Malipo ya fedha kwa njia ya simu yanasaidia kupunguza gharama hivyo na kuwa kichochea cha maendeleo, sasa hivi wafanyakazi, wakulima, wanaotumia huduma za bima, wanaonunua bidhaa hulipa kwa Kutumia simu za mkononi hususani kwamba muda ndio muhimu,” alisema.

Aliongeza kuwa “Mitandao ya simu haiathiri huduma za kibenki, na benki wamechangamkia kutumia mitandao kufikia wateja wao, hutumia mawakala kufungulia account, mitandao hii husaidia benki kufikia wateja kote nchini, woga huo umepungua kwa sasa,”

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 51 & 52 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
Nikafanya kama dorecy anavyo niagiza, gafla tukaiona gari moja mbele yetu, aina ya pick up ikiwa na watu wenye bunduki zao huku mmoja wao akiwa ameshika bomo aina ya rocket ambalo upigaji wake analiweka begani na kulifyatulia.Sote tukafunga breki za magari yetu na majamaa wakaanza kushuka huku mwenye bomo akiwa ametuelekezea kwetu akijiandaa kutufyatulia

Endelea....
Macho yangu yangu yakawatazama jamaa walio shika bunduki mikononi mwao, wote wanaonekana wapo makini katika kutushambuli sisi.Kwa kupitia kioo pembeni, nikaangalia nyuma na kuona kuna kona ambayo ipo karibu na sehemu tulipo simama, nikakanyaga mafuta na gari kuanza kuirudisha nyuma kwa kasi kubwa, jamaa wakaana kutushambulia kwa risasi ambazo kwa bahati nzuri hazikuingia kwenye gari, kitendo cha kukunja tu, bomu alilo lifyatua jamaa likapita mita chache kutoka sehemu gari letu lilipo na kwenda kugongwa kwenye miamba na kusababisha mlipuko mkubwa na mawe yakaziba barabara kwa nyuma na kushindwa kurudi nyuma.

Nikafunga breki na kulisimisha gari, sote tuakashuka kwenye gari huku bastola zetu zikiwa mikononi,tukaifungua milango ya gari na kujificha nyuma ya milango kwani uzuri wake haipitishi risasi.Bastola zetu zikawa zimeelekea kwenye kona ambapo tunatarajia majambazi kutokea.Ukimya wa kama dakika tatu ukatawala, hatukuona watu ambao wanajitokeza kwenye kona, nikataka kunyanyuka
“eddy kaa chini”

Dorecy alizungumza kwa sauti ya ukali, nikatii kwa haraka na risasi ikapiga kwenye kioo cha gari katika mlango ambao nipo mimi.Dorecy akaanza kufyatua risasi zilizo elekea walipo majambazi, kila risasi ambayo ninaipiga mimi haikumpata mtu yoyote zaidi ya kupiga pembeni, hata kama mtu nimemlenga vizuri ila haikumpata

“nakosea wapi?”
Nilizungumza kwa sauti ya juu
“kaza mkono”
Dorecy alizungumza, huku akiendelea kufyatua risasi kwa majambazi ambao wanatoa vilio vya maumivu kila aliye pigwa na risasi.Nikaingia ndani ya mlango na kuufunga mlango wa upande ambao nipo
“unafanya nini?”
“ngoja nikuonyeshe”

Nikaiwasha gari na screen(kioo), kilichopo pembeni yangu kikawaka na kuniandikia maneno yaiyo nichosha
‘system weapon empty’ ikimaanisha hakuna silaha yoyote inayoweza kufanya kazi kwani zimeisha.
“shitiii”
Nilizungumza huku nikiupiga mskani kwa kitako cha bastola
“vipi?”
“kuna, ishu nilikuwa ninaicheki kwenye hii gari.Imeisha”
“ni nini?”
“silaha, naomba hilo jaketi lako la kuzuia risasi”

Dorecy alinitazama kwa muda kisha akavua bullet proof yake na kunirushia upande niliopo,  nilalivaa vizuri na mara nyingi nilikuwa nikimuona mzee godwin akilivaa jinsi nilivyo livaa nikiwa mtoto mdogo.Kwani kuna siku nyumbani tulivamiwa na majambazia nyumbani, akatuvalisha sote kisha yeye alielekea kupambana nao na siri moja aliyo niambia ni kwamba jaketi hili linamionzi ambayo hata ukiwa umelengwa kupigwa risasi ya kichwa basi inaivuta na kukimbilia kifuani.
“vipi huku, mbele mimi ngoja nipande hapo juu”

Nilimuambia dorecy, nikapanda kwenye gemo ambalo lipo pembeni yetu, nikapanda hadi pasipo majambazi kuniona, nikatafuta sehemu nzuri ya kusimama ambayo nikawa ninawaona kwa chini, nikawahesabu kwa haraka na kuwaona wakiwa wamebaki wanne wamejibanza kwenye gari lao wakimsubiria dorecy kujitokeza, dorecy naye akawa amejibanza kwenye gari akiwasubiri wajitokeze

Nikaishika bastola vizuri, nikafumba jicho langu moja huku nikiitazama sehemu yenye mfuniko wa tanki la mafuta kwenye gari, nikameza mate mengi kisha nikafyatua risasi tatu mfululizo huku nikiwa nimeikaza mikono yangu, risasi mbili zikapiga pembeni, jambo lililo wachanganya jamaa.Risasi ya tatu ikapiga kwenye tanki la mafuta na kulifanya gari kulipuka, huku likinyanyuliwa juu na jamaa wote wakarushwa pembeni.Hadi gari linatua chini milango na matairi yake yalichanguka vibaya.

Nikashuka kwenye gemo kupitia njia niliyo pandia na kumkuta dorecy akiwa bado ameshika bastola yake akiielekezea walipo majambazi, nikatembea kwa mwendo wa tahadhari hadi ilipo gari ya majambazi, nikaanza kuhakikisha jambazi mmoja baada ya mwengine kama amekufa, ambaye ninamkuta kwenye hatua za mwisho za maisha yake nilampiga risasi ya kumsindikiza kuzimu

Nikageuka nyuma na kumkuta dorecy akiwa ananitazama kwa macho ya mshangao, kwani haamini kama nitaweza kuwapiga risasi wezake ambao amewasaliti, nikarudi lilipo gari na kuingia, nikaliwasha hadi sehemu alipo, akafungua mlango na kuingia.Nilalipitisha pembeni gari langu taratibu kulikwepa gari linalo teketea na kuandelea na safari.Dorecy akaendelea kunielekeza njia hadi tukatokea barabara inayotokea tanga kuelekea moshi

“eddy, ulisha wahi kuua?” dorecy aliniuliza
“swali gani sasa hilo?”
“hapana, kwa mtu ambaye hazifanyi hizi kazi hawezi kuwa kufanya kama ulivyo fanya wewe”
“nimefanyaje?”
“ulivyo wapiga wale, risasi waliokuwa wakikaribia kufa”
“kawaida”

Nilimjibu huku nikendelea kuendesha gari kwa umakini, macho yangu yote yakawa ni barabarani kuangali kama polisi wa usalama barabarani wapo au hakuna.Tukaingia kwenye motel iitwayo mombo motel iliyopo kwenye barabara ya mombo

“una pesa?”
Nilimuuliza dorecy
“ndio”
“kachukue chakula basi”
“utakula nini?”
“bufee,nyama chukua na soda za take way”

Dorecy akalivua shati lake na kubaki na vest ya kiume, akaziweka vizuri nywele zake ndefu, akaichomeka bastola yake kwenye buti la jeshi, mguu wa kulia na kushuka ndani ya gari.Kwa kupitia kioo cha pembeni nikawaona askari wa usalala barabarani, wakiingia kwenye geti la motel wakiwa na pikipiki.

Wakaisimamisha pikipiki nyuma ya gari langu na kunifanya nianze kupata wasiwasi, kwani sihitaji kumwaga damu tena katika eneo hili.Mmoja akaanza kulitazama gari langu vizuri, akaanza kulizunguka taratibu huku akilitazama kadi zake za usajili zilizo bandikwa kwenye kii cha mbele
“anataka nini huyu?”
Nilijizungumzia kimya kimya, akanionyesha ishara ya kufungua kioo cha gari langu, akanitazama kwa sekunde kadhaa

“habari yako afande?” nilianza kumsalimia
“salama, gari yako ilipata nini?”
“kivipi?”
“imebonyea  pembeni huku?”
“ilipata ajali, afande”
Nilizungumza huku mkono wangu wa kulia ukiwa umeishika bastola, huku nikiwa nimeficha pembeni ya siti yangu
“unatakiwa ukaiyooshe, kwa maana gari ya kifahari inakuwa haileti picha nzuri”

“sawa afande”
“insuarence yako nayo ipo katika siku za ukingoni”
“yote nitayafanya, nikifika ikulu”
Niliingiza swala la ikulu kwa maana askari, anahisi kama mimi ni miongoni mwa askari, hii nikutoka na bullet proof niliyo ivaa
“ahaaa, upo ikulu wewe?”
“yaaa”

“wezetu nyinyi wa ikulu muna kula kula pesa”
“tunakua pesa wapi kaka, kazi nyingi kama hizi unazo ziona”
“ila si kwa kila kazi unapata mkwanja mrefu?”
“inategemea, na kazi”
“ahaa sisi wa barabarani huku ni shida”
“shida gani?”
“ahaaa, madereva wenyewe wabishi kama nini”
“wabaneni”

Kizimbani kwa kutangaza kuoa askari mwenye mafuta ya kilainishi cha KY JELLY

$
0
0
Mfanyabiashara Christon Mbalamula, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kudai anatangaza ndoa na askari watakaomhudumia kama mume, huku akihoji kama wameshanunua mafuta ya kilainishi maarufu KY.

Mshtakiwa huyo alifikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana akikabiliwa na shtaka la kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’ kulidhalilisha jeshi hilo.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk. Yohana Yongolo, Wakili wa Serikali, Winifrida Sumawe alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Agosti 26 mwaka huu katika eneo la Vijibweni Kigamboni.

Alidai siku ya tukio, mshtakiwa alilidhalilisha  Jeshi la Polisi  baada ya kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp kusambaza ujumbe unaosema.“Natangaza ndoa na askari yoyote atakayejipendekeza kwangu siku hiyo ataolewa bila mahari.

“Ataishi kwangu bila nguo hadi operation Ukuta  itakapoisha atapika na kupakua na kunikidhi haja km mume wake, Note KY JELLY mmeishanunua so msiogope nyie mapolice uchwara” alisema katika ujumbe huo.

Mshtakiwa huyo alikana shitaka hilo na upande wa mashtaka ulidai upelelezi haujakamilika.

Hakimu Yongolo alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika, kila mmoja asaini dhamana ya maandishi ya Sh milioni moja na mmoja kati ya wadhamini hao awe na mali isiyohamishika yenye thamani isiyo chini ya Sh milioni mbili. Mshtakiwa awe anaripoti kila baada ya wiki mbili kwa msimamizi wa mawakili wa serikali.

Basi la New Force Lapata Ajali na Kuua Watu 12

$
0
0
Watu 12 wamefariki dunia papo hapo na wengine tisa kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya New Force kupinduka katika eneo la Ilongwe kata ya Kifanya, Mkoani Njombe na kupelekea vifo hivyo pamoja na majeruhi.

Basi hilo linalofanya safari zake kati ya Mkoa wa Njombe na Dar es Salaam lilipinduka majira ya saa moja na dakika 40 usiku wa kumakia leo wakati likitokea jijini Dar es Salaam kuelekea mkoani Njombe.

Kwa mujibu wa habari iliyotolewa na shirika la habari la taifa kutoka mkoani Njombe zinasema kati ya watu hao 12 wanawake ni nane akiwemo mtoto mmoja wa kike pamoja na wanaume wanne akiwemo mtoto mmoja wa kiume.

Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo amesema kuwa chanzo cha ajili hiyo ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo amesema kabla ya ajali kutokea tayari basi hilo lilikuwa limeyumba karibu mara tatu na baadaye kupinduka kabisa.

Katika tukio lingine la ajali iliyotokea mkoani Kilimanjaro katika msafara wa ziara ya mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Said Meck Sadiki imesababisha majeruhi wawili akiwemo afisa wa polisi pamoja na mwandishi wa habari wa shirika la habari la taifa ambao wote wamelazwa kwa ajili ya matibabu.

Rais Magufuli awalilia waliokufa kwa ajali ya Basi la New Force

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 9 & 10

$
0
0
Muandishi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
Dokta Williama aliendelea kuwasikiliza wakuu hawa wa polisi ambao vyeo vyao vinawatambulisha kama ma RPC kwenye mikoa yao.Lifti ikafunguka na wote wakatoka ndani ya lifti.Askari hao wakaendelea kwa mwendo wa kasi na kuingia kwenye ukumbi wa mikutano.Dokta William akajiweka sawa nguo zake na kuingia ndani ya ukumbi huu.Gafla macho yake yakatazamana na midomo ya bastola alizo elekezewa na wakuu wa polisi waliokaa kwenye viti vyao huku wakioneka kukasirishwa sana na uwepo wake

ENDELEA....
IGP bwana Gudluck Nyangoi akwaamuru wezake kuziweka silaha zao chini na wakati
“Karibu dokra Willian”
Bwana G.Nyangoi alizungumza huku akitabasamu na kumfanya dokta William kushusha pumzi nyingi,kidogo wasiwasi ukaanza kumpungua.

“Jamani huyu ni miongoni mwa wanajeshi wa umoja wa matiafa,yupo hapa nchini kwa ajili ya mafunzo wa madaktari wa jeshi letu juu ya jinsi gani wanaweza kumtengeneza sura bandia”

“Dokta,kwanza samahani kwa kukuvunjia ratiba zako kwa maana haikuwa katika ratiba zako leo kama nitakuitaji hapa”
“Bila samahani mkuu”
“Karibu ukae”

Dokta William akaka kwenye kiti alicho onyeshwa na bwana Nyangoi,akawaytizama makamanda wote waliopo ndani ya ofisi na hapakuwa na hata mmoja anaye mfahamu zaidi ya IGP Gudluck Nyangoi.

“Jamani kama munavyo jua,sisi kama jeshi la polisi tumekubwa na msiba mkubwa sana wakupoteza vijana wetu katika tukio la jana usiku,Pia ni aibu kubwa kwetu sisi kama jeshi la polisi kwa kushindwa kupambana na majambazi ambao,sijajua ni vipi tulishindwa kuwazuia na kusababisha maafa makubwa kama haya”

Ukimya ukatawala,huku akili ya Dokta William ikiwa inajaribu kupanga kitu cha kuzungumza kabla hajaulizwa kwani ametambua umuhimu wake wa yeye kuwa hapa ni kuwashauri viongozi waliopo humu ndani

“Jamani ninawasililiza,nasubiri maoni yenu.Nini tufanye ili kuwakamata hawa watu na ninavyo sikia wao ni wasichana sasa sijajua inakuwaje wasichana kama hawa wanatushinda kirahisi rahisi?”

“Mkuu mimi ninaona,kwanza tudhibiti mipaka yote ya nchi jirani kwa maana kumbukeni kulikuwa na tishio la kundi la Al-Shabab kuivamia mlimani city.Sasa isije ikwa ndio hao wameanza kutekeleza mipango yao”

“Asante bwana Shaban Mbago,mwengine?”
“Mkuu mimi kuna swala ambalo bado silipatii picha,haiwezekani mpango ule wa kumsafirisha yele binti katika njia ya ardhini ulibumburuka.Swali ni je,ni nani aliye toa siri ile?”

Mapigo ya moyo ya dokta William yakaanza kwenda kasi,ila hakutaka kuiruhusu hali hii kuendelea kuundama moyo wake,akawatazama wakuu wa polisi waliopo eneo hili na kuwaona wengi wapo kimya kila mmoja akikosa cha kuzungumza.Dokta William akanyoosha kidole na bwana G.Nyangoi akampa ruhusa ya kuzungumza
“Wakuu wangu mimi ninajambo moja ninaomba nizungumze”
“Zungumza tuu,kwani ushauri wako ni mkubwa sana”

“Kuna hali ambayo inaendelea ndani ya jeshi lenu,kwa kipindi kifupi nilicho kaa katika nchi hii na kushirikiana na jeshi lenu nikagundua kuna hali amayo sio nzuri na endapo mukiacha ikikua na kukomaa,Siku hadi siku jeshi lenu litazidi kuzalilisha na kuteketea mwisho wa siku ile imani ya kusema kuwa Tanzania ni nchi ya amani itafutika katika vichwa vya watu wengi”

“Viongozi kwa viongozi hamuaminiani,hilo ni la kwanza.Pili viongozi mumekuwa ni watu wakuunda vikundi vikundi vya watu ambao munawatumia kwa maslai yenu binafsi na si ya taifa.Kwa mfano kuna magaidi ambao jeshi la polisi mulikuwa munawatafuta kwa kipindi kirefu sana.

Kutokana na uaminifu finyu wa baadhi ya viongozi magaidi wale wakaendelea kudumu na kuishi kwa kipindi kirefu pasipo serikali kuzungumza kitu cha aina yoyote.Kila mulipo kuwa munajaribu kwenda kuwakama walikuwa wanawakwepa na kubaki mukijiuliza mutafanya nini?”

“Kabla ya hichi kikao kuendelea,jiulizeni je hakuna wasaliti watako vujisha siri juu ya watu muna watafuta? Na kama wapo je kuna haja gani ya hichi kikao kuendelea kuwepo hapa?”

Ukumbi mzima ukakaa kimya,sura za makamanda wote wapolisi zikawa zikimtazama Dokta William ambaye amezungumza maneno ambayo wengi wao hawakuwa wanayafikiria kuyazungumza

“Musikalie kuunda tume kuchunguza vitu ambavyo munajua majibu yake kabla ya kuzungumza.Nyinyi ni jeshi,munatakiwa kuwa kitu kimoja na si kuwa katika mgawanyiko ambao utawakost garama ambazo si za msingi.Jaribuni kuiga baadhi ya mbinu za kijeshi katika mataifa makubwa yaliyo endelea,mfano Marekani na kadhalika.Nitatolea mfano mdogo tuu wa wa wale wanejeshi walio tumwa kwenda kumuua Osama Bin Laden,Gaidi ambaye sisi kama Israel alituumiza pia vichwa jinsi ya kumpata”

“Ila kikosi cha wanajeshi wachache walio tumwa kuumuua Osama,kilikuwa ni cha siri kubwa hata makamu wa raisi wa Marekani hakuwa analifahamu hilo,zidi ya raisi Obama na wasadizi wake,Na tukio zima lilipokuwa linaendelea walikaa kwenye chumba maalumu pasipo na mtu yoyote kuwa na mawasiliano ya simu ya mkononi,hata raisi mwenyewe alizuiwa kuwa na simu.

Huo ni mfano mdogo ila hapa hapa ninashanga muheshimiwa unaendeleza kikao ila kuna huyo bwana hapo anachati na simu chini ya meza,Je kuna umuhimu gani wa hichi kikao?”
Bwana Noel Muro akastuka na kuuingiza simu yake mfukoni baada ya kunyooshewa kidole na Dokta William.
“Muro ninaomba uzime simu yako”

Bwana G.Nyangoi alizungumza huku akimtazama bwana Muro
“Mkuu cha mwisho kukizungumza ninawaomba,muunde kikosi maaalumu cha siri kitakacho wa pambana na hili swala.Asanteni”
Dokta William akakaa kwenye kiti na viongozi wote wakampigia makofi wakimpongeza kwa ushauri wake alio utoa.

“Dokta Willim asante sana kwa ushauri wako mzuri sana.Mimi ningekuomba usaidiane na mimi kuunda kikosi kitakacho weza kuwasaka hawa majambazi.Nipo radhi kuwaishawishi serikali kuongezea mshahara”
Laiti IGP bwana G.Nyangoi angegundua mtu anaye muomba juu ya huo mpango ndio muhusika nambari moja wala asinge zungumza hayo maneno


Ndege mpya ya aina ya Bombardier Q400 NextGen iliyonunuliwa na Serikali yawasili Jijii Dar es Salaam

$
0
0
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakisubiri kuwasili kwa Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016
Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikipata saluti ya maji (Water Canon Salutation) toka kwa magari ya Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mara tu bada ya kuwasili  katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akisalimiana na Rubani aliyerusha Ndege mpya moja kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) ikiwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  saa sita na robo juu alama leo Septemba 20, 2016.
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu, na maofisa wengine wakiwa kwenye  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016
Katibu Mkuu wa Uchukuzi Dkt Leonard Chamriho akipeana mikono kwa furaha na Mkurugenzi wa Kampuni ya Bombadier Commercial Aircraft Bw. Pardeep Sandhu mara baada ya  Moja ya Ndege mpya mbili zilizonunuliwa na serikali kwa ajili ya kampuni ya ndege Tanzania (ATCL) kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius leo Septemba 20, 2016, Wengine ni marubani wa ndege hiyo.PICHA NA IKULU

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Amjulia Hali Spika Mstaafu Samweli Sitta

$
0
0

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Spika Mstaafu, Samwel Sitta na mkewe Margaret wakati alipomjulia hali jijini Dar  es salaam Septemba 20, 2016.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Rais Magufulia ateua Wenyeviti wengine watatu

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhan Kondo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Posta Tanzania.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 20 Septemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo umeanza tarehe 05 Septemba, 2016.Luteni Kanali Mstaafu Haroun Ramadhani Kondo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Yamungu Kayandabila ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Dkt. Hedwiga Francis Swai kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Dkt. Hedwiga Francis Swai ni Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Balozi Ladislaus Columban Komba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Balozi Ladislaus Columbas Komba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Christopher Celestine Liundi ambaye amemaliza muda wake.

Halikadhalika, Rais Magufuli amemteua Bw. Fidelis Mutakyamilwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Tume ya Taifa ya Matumizi ya ardhi kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.Bw. Fidelis Mutakyamilwa ni Mwanasheria Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii wa LAPF


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
20 Septemba, 2016

Waziri Mkuu Apokea Mchango wa Watumishi wa Serikali wa Tetemeko la Ardhi Kagera

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amepokea jumla ya sh. bilioni 1.040 kutoka kwa watumishi na wadau mbalimbali zikiwa ni misaada kwa wananchi walioathirika na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Septemba 10, mwaka huu.

Makabidhiano ya michango hiyo, yamefanyika leo mchana (Jumanne, Septemba 20, 2016) kwenye ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam.

Akikabidhi hundi kwa Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi alisema kiasi cha sh. 1,000,030,100 kimekusanywa kutoka kwa watumishi wa idara na Wizara zote  za Serikali na kwamba michango zaidi bado inaendelea kukusanywa.

“Tunaamini michango hii itasaidia kuwafuta machozi wenzetu waliopatwa na maafa japokuwa tunajua haitatosha kurudisha kile walichopoteza. Tuna imani itasaidia kupunguza makali ya machungu waliyoyapata,” amesema.

Hata hicyo, Balozi Kijazi amemhakikishia Waziri Mkuu kwamba bado wanaendelea kukusanya michango kutoka kwenye nyingine ambazo zilichelewa kupata taarifa na kwamba wakikamilisha wataiwasilisha mapema iwezekanavyo.
              
Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amepokea michango ya sh. milioni 40 na kati ya hizo, sh. milioni 20 zimetolewa na kampuni ya ujenzi ya CHICO ya China na sh. milioni 20 nyingine zimetoka kwa Umoja wa Wafanyabiashara na Wenye Viwanda wa India waliopo nchini (India Business Forum).

Akiwasilisha mchango wake, Mwakilishi Mkuu wa kampuni ya CHICO hapa nchini, Bw. Guo Zhijian alisema wamesikitishwa na maafa yaliyotokea mkoani Kagera. “Tumefanya miradi mingi mkoani Kagera ikiwemo ujenzi wa barabara za urefu kilometa 300, kwa hiyo mkoa huu tunaujua zaidi. Tunatoa pole kwa wote waliopatwa na maafa  hayo,” amesema.

Naye Mwenyekiti wa umoja wa wafanyabiashara na wenye viwanda kutoka India (IBF), Bw. Gagan Gupta alimweleza Waziri Mkuu kwamba wameshtushwa na tukio hilo na kwamba wametanguliza kiasi hicho ili kisaidie juhudi za Serikali katika kukabiliana na maafa hayo.

“Bado tunaendelea kuwasiliana na wenzetu wengine na tukipata michango zaidi tutaiwasilisha mapema iwezekanavyo,” amesema.

Akitoa shukrani kwa waliotoa michango yote hiyo, Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuahidi kuwa Serikali itahakikisha michango hiyo inafikishwa Kagera kwa walengwa.

“Tunashukuru sana kwa michango yote. Michango hii ni muhimu na inaonyesha mshikamano wa dhati uliopo. Michango hii inaonyesha kuguswa na mapenzi ya dhati kwa waliopatwa na maafa. Napenda niwahakikishie kuwa Kamati za Maafa za Mkoa, Ofisi ya Waziri Mkuu na kamati za wilaya, ziko pale kuhakikisha walengwa wanafikiwa,” ameongeza.

Waziri Mkuu amesema Serikali inakamilisha tathmini ya maafa hayo na kuahidi kutoa taarifa ya kiasi kilichokusanywa na kiasi kilichotumika. Amewaomba wananchi waliotoa ahadi zao za michango wakamilishe ahadi zao.

“Ninawaomba wale walioahidi kutoa michango wakamilishe ahadi zao na wale walio mbali na benki watumie namba za simu zilizotolewa mahsusi kwa ajili ya kuchangia maafa hayo,” amesisitiza.
Akaunti ya maafa imefunguliwa katika Benki ya CRDB yenye namba 015 222 561 7300 kwa jina la KAMATI MAAFA KAGERA – Swiftcode: CORUtztz na namba za simu za mkononi zinazotumika kupokea michango hiyo ni 0768-196-669 (M-Pesa) au 0682-950-009 (Airtel Money) au 0718-069-616 (Tigo Pesa).

Tetemeko hilo lililotokea Jumamosi, Septemba 10, mwaka huu, lilisababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 kujeruhiwa. Kati yao, watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 walitibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.

Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S.  L. P. 3021,
11410 - DAR ES SALAAM.

JUMANNE, SEPTEMBA 20, 2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Septemba 21

Aliyemuua Trafiki Afikishwa Mahakamani

$
0
0

Mkazi wa Mbezi Africana Dar es Salaam, Amani Elikana (32), amefikishwa   katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akituhumiwa kumuua Askari wa Usalama Barabarani, Sajenti Mensali wa Kituo cha Polisi Mabatini – Kijitonyama.

Akisoma hati ya mashtaka jana mbele ya Hakimu, Caroline Kiliwa, Wakili wa Serikali, Amani Mghamba alidai  mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 22 mwaka huu eneo la Kijitonyama.

“Mtuhumiwa inadaiwa kwamba siku hiyo kwa makusudi  ulimuua askari mwenye namba D. 8254 Sajenti Mensali kinyume cha sheria ya Jamhuri ya Muungano,” alidai Mghamba.

Hakimu Kiliwa alisema mtuhumiwa hapaswi kujibu kitu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo hivyo shtaka hilo liliahirishwa  hadi Oktoba 4 mwaka huu litakapotajwa tena.

CUF kugharamia matibabu ya Maalim Seif

$
0
0
Wanachama wa Chama cha Wananchi (CUF)  wamesema wapo tayari kugharamia matibabu ya Katibu Mkuu wa chama chao, Maalim Seif Sharif Hamad.

Tamko hilo limetolewa siku chache baada ya kuibuka taarifa kuwa  kiongozi huyo amesusa gharama za matibabu zinazotolewa na Serikali ingawa ni haki yake kwa mujibu wa sheria kama kiongozi mstaafu.

Akizungumza   kwa niaba ya wanachama wenzake kisiwani Unguja jana, mmoja wa wanachama wa CUF, Ali Abdallah Issa, alisema wanashangazwa na baadhi ya watu kumpiga na kumsema kiongozi huyo ambaye alidai ni kiungo muhimu katika kuwaunganisha Wazanzibari.

“Maaalim ana haki zote za kuhudumiwa na Serikali na si vinginevyo. Lakini kwa manyanyaso na kusimangwa  kila kukicha sisi wanachama wa CUF tupo tayari kugharamia matibabu ya kiongozi wetu.

“Na hili si jambo geni, Maalim alikamatwa na kuwekwa kuzuizini.  Je, alipotoka  alikuwa akitibiwa na SMZ? Jibu ni hapana ni fedha zake mwenyewe binafsi pamoja na wana CUF ambao walikuwa mstari wa mbele kumhudumia kiongozi wetu nasi sasa tutafaya hivyo ikiwa SMZ imeshindwa,” alisema Ali.

Alisema kitendo cha Maalim Seif kusafiri nje ya nchi kwa matibabu bila ya huduma za Serikali hakileti picha nzuri.

Kuna hatari visiwa vya Zanzibar vikaingia katika mgogoro na kujengeka   chuki hasa kati ya CUF na CCM, alisema.

‘’Iwapo Maalim Seif amekwenda kwenye matibabu kwa gharama zake binafsi basi inasikitisha sana kuona ni jinsi gani Katiba inavyoanza kukiukwa na kwa kweli si jambo jema na halifai,” alisema.

Naye Is-hak Said Makame, alisema   Zanzibar imepita katika wakati mgumu hasa baada ya kutokea   migogoro ya siasa iliyotokana na Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba mwaka jana  na ule wa marudio uliofanyika Machi 20, mwaka huu.

“Maalim hawezi kusemwa na hata kuonekana ni kiongozi anayetibiwa kwa fadhila kama alivyotaka Rais Magufuli alipokuja hapa Unguja kwenye mikutano yake. Sasa tunasema sisi CUF tutamlinda kiongozi wetu kwa hali na mali,”alisema Makame.

Alipotafutwa  Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Uhusiano wa Umma wa CUF, Salim Biman  kujua  Maalim Seif  amepata wapi fedha kwa ajili ya safari ya nje ya nchi kutibiwa.

Alisema  hajui ni wapi kiongozi huyo alipopata fedha za matibabu.

“Katibu Mkuu amekwenda India kwa ajili ya uchunguzi wa kawaida wa afya yake lakini nasi hatujui ni wapi amepata fedha. Ila atakaporejea nchini itatolewa taarifa kwa kina kuhusu suala hili,” alisema Biman.

Maalim Seif yuko   India na anatarajiwa kujerea nchini siku chache zijazo.

Rais Magufuli atengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPFi na kuvunja Bodi yote

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 21 Septemba, 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Prof. Hasa Mlawa kuanzia leo.

Pamoja na kutengua uteuzi wa Prof. Hasa Mlawa, Rais Magufuli amevunja Bodi ya Udhamini ya Mfuko huo.

Uteuzi wa Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Udhamini ya LAPF utafanywa baadaye.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

21 Septemba, 2016

Mahakama ya Kisutu yamtaka Mhe.Tundu Lissu kufika mahakamani kujieleza kwa nini asifutiwe dhamana.

$
0
0

Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam imemtaka mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Mhe.Tundu Lissu anayekabiliwa na kesi ya uchochezi pamoja na wahariri wa gazeti la Mawio kufika mahakamani kujieleza kwa nini asifutiwe dhamana.

Hakimu Simba ametoa agizo hilo jana baada ya Lissu pamoja na mdhamini wake kutokuwepo mahakamani hapo kama sheria inavyotaka na hatua hiyo ilifikiwa baada ya wakili wa serikali kuomba itolewe hati ya kumkamata lakini hakimu Simba akamtaka Lissu aende kujieleza kwanini asifutiwe dhamana.

Katika kesi hiyo ya uchochezi, hakimu Simba alitoa uamuzi ambao umeuruhusu upande wa mashtaka kuyaleta upya mashtaka yanayofanana na yale yaliyoondolewa awali mahakamani hapo kutokana na kutokuwa na kibali cha mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kwa kuwa ya sasa yanakibali na kuyatupilia mbali maombi ya Kibatala.

Hakimu Simba alisema upande wa mashtaka walikuwa na haki ya kurekebisha mapungufu na kuyaleta tena mashtaka hayo mahakamani.

Baada ya uamuzi huo kutolewa wakili Peter Kibatala alidai kuwa hawajaridhika na uamuzi huo watakata rufaa kuupinga kwa sababu wanaamini mashtaka hayo yalivyofutwa ilikuwa na maana ya kuwa yamekufa na akaiomba mahakama kutoyasoma mashtaka hayo mapya hadi rufaa yao itakaposikilizwa na mahakama kuu na kutolewa uamuzi.

Wakili wa serikali mwandamizi, Mutalemwa Kishenyi alidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekwisha kamilika.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhariri wa gazeti hilo, Simon Mkina, Jabir Idrisa na mchapishaji wa kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob ambao awali walikuwa wakikabiliwa na mashtaka matano likiwamo la kuandika habari za uchochezi kinyume na sheria ya magazeti ya mwaka 2002.

Chanzo: ITV

Uamuzi wa CCM kuhusu Mwenyekiti wa UVCCM anayetuhumiwa kughushi nyaraka za Usalama wa Taifa

M-PAWA Inazidi Kuwatajirisha Watanzania .....Mshindi Wa Pili Wa Milioni 20 Apatikana

$
0
0
Vodacom Tanzania wakishirikiana na Benki ya CBA, ilizindua promosheni kubwa inayojulikana kama "Jiongeze na M-Pawa" ambayo inawawezesha watumiaji wa huduma ya M-Pawa kujishindia zawadi ya fedha taslimu. 

Jumla ya shilingi milioni 300 zimetengwa kwa ajili ya promosheni hiyo na mshindi mmoja wa droo kubwa atajishindia kitita cha shilingi milioni 100. 

Washindi wa wiki watazawadiwa shilingi milioni 20 na washindi wa siku watazawadiwa shilingi milioni moja. 

Promosheni hiyo ambayo ilianza mwanzoni mwa mwezi wa 9 itadumu kwa kipindi cha wiki sita na itafikia kilele mwishoni mwa Mwezi Oktoba, 2016.
Meneja masoko Huduma  za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiongea na mmoja wa  mshindi  wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa  wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. Wanaoshuhudia kutoka  kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-Pawa wa Benki ya CBA Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.
Meneja masoko Huduma  za kifedha wa Vodacom Tanzania ,Noel Mazoya (katikati) akiwaonyesha waandishi wa habari namba ya  mshindi  wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20. 

Wanaoshuhudia kutoka  kushoto ni Meneja  wa Huduma za M-pawa wa Benki ya CBA  Eric Luyangi  na Msimamizi wa bodi ya michezo ya Kubahatisha nchini Bakari Maggid.  Hadi sasa  washindi 2,800 wameongezea mara mbili ya akiba zao za M-Pawa washindi 14 wameshinda milioni 1 kila mmoja na washindi 2 wamejishindia milioni 20  mshindi wa jumla washilingi milioni 100 atapatikana mwezi wa kumi.
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio la kuchezesha  wa droo ya  promosheni ya Jiongeza na M-Pawa   wakati wa hafla ya kuchezesha droo ya pili ya wiki iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ambapo mkazi wa Arusha  Isaack Pilemon alijishindia kitita cha shilingi Milioni 20.

Basi la Super Shem Lapata Ajali na Kuua watu 11 Jijini Mwanza Leo

$
0
0

Basi la Super Shem linalofanya safari za Mwanza kwenda  Mbeya limepata ajari ya kugongana na hiace katika kijiji cha Hungumalwa Mwanza na kusababisha vifo vya watu  wanaodaiwa kufika 11 asubuhi hii.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, wanaeleza kuwa Basi hilo liliigonga gari hiyo ndogo ambayo iliingia kwenye barabara kubwa bila ya kuwa na tahadhali, Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza zinaendelea kufanyika ili kuthibitisha tukio hilo.

Jipatie Kitabu cha My mom's friend Toka kwa Mtunzi Aliyebobea Eddazaria g.Msulwa

$
0
0


Mwandishi mahiri wa SORRY MADAM na SHE IS MY WIFE anakuletea  Kitabu cha My mom's friend kwa sh 5000 tu. 

Kinapatikana kupitia WhatsApp au Email, ni njia rahisi kukufikia msomaji .

 Wasiliana nae kwa simu; 0657072588(WhatsApp) au 0768516188. Wahi sasa upate uhondo wa hadithi hii ya kusisimua na kuburudisha

Rais Magufuli aipongeza Kilimanjaro Queens kwa Ubingwa wa CECAFA Chalenji

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amewapongeza wachezaji wa Timu ya soka ya Wanawake ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Queens) kwa kuandika historia ya kuwa Mabingwa wa kwanza wa Michuano ya kugombea kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Challenge) iliyofanyika katika Mji wa Jinja nchini Uganda.


Kilimanjaro Queens imefanikiwa kutwaa Ubingwa huo baada ya kuibwaga Kenya (Harambee Starlets) kwa mabao 2-1 katika mchezo wa fainali uliofanyika jana tarehe 20 Septemba, 2016.

Katika pongezi hizo alizozitoa kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, Rais Magufuli amesema Timu ya Kilimanjaro Queens imeandika historia ambayo inalipa heshima Taifa na inaamsha morali kwa wanamichezo kufanya vizuri katika mashindano.

“Mhe. Waziri Nape Nnauye naomba unifikishie pongezi nyingi kwa Wachezaji wa Kilimanjaro Queens, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Walimu na Viongozi wa Timu pamoja na wadau wote waliochangia kuiandaa Timu yetu ya Taifa ya wanawake ambayo hatimaye imepata ubingwa katika michuano hii mikubwa.

“Nimefurahishwa sana na ubingwa huu na nawaomba wachezaji wa Kilimanjaro Queens na wanamichezo wengine hapa nchini kuuchukua ushindi huu kama changamoto ya kuongeza juhudi katika michezo yetu ili nchi isiishie kupata ubingwa wa Chalenji bali pia ipate ushindi katika michezo na michuano mingine mingi ambayo hushiriki” Amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amewaomba Watanzania wote kuendelea kuwaunga mkono wanamichezo na kuwatia moyo wachezaji kwa kuwa mafanikio yao yanaitangaza nchi na yana mchango mkubwa katika maendeleo.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

21 Septemba, 2016
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images