Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatatu ya Septemba 19


Kufuatia Tetemeko La Ardhi Mkoani Kagera Waziri Mwigulu Aamuru Wafugwa 280 Wahimishwe Gereza

0
0
Serikali imeagiza wafungwa 280 katika gereza la Kitengule wilayani Karagwe, wahamishwe katika kipindi cha wiki moja kupelekwa gereza la Mwisa.

Watahamishwa baada ya mabweni yao kuharibiwa kwa tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera wiki iliyopita.

Agizo hilo lilitolewa jana na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Kagera, Jeremiah Nkonda.

Mwigulu aliagiza hilo baada ya kufanya ziara mkoani hapa na kutembelea taasisi zilizo chini ya wizara yake kwa lengo la kuona uharibifu uliojitokeza kutokana na tetemeko hilo, lililoripotiwa kusababisha vifo vya watu 17, majeruhi, nyumba kubomoka na uharibifu mkubwa wa majengo na miundombinu ya barabara.

“Nimetembelea magereza yetu, lakini gereza la Kitengule limeharibika sana, kuta zimeanguka, mabweni yameharibika kwa kiwango kikubwa kiasi kwamba hawapaswi kuishi watu. Kwa hiyo, naagiza mkuu wa magereza hapa kuwahamishia wafungwa hawa katika gereza la Mwisa lenye mabweni manne yaliyo wazi,” aliagiza Mwigulu.

Alisema katika kipindi cha wiki moja, kazi hiyo iwe imekamilika kwa sababu wakiendelea kuwaacha wafungwa hao katika gereza hilo lililoharibika ni hatari, kwani wanaweza kudondokewa na kuta zinazoning’inia na kusababisha maafa mengine.

Mwigulu alisema kutokana na tukio hilo, Wizara inaandaa mpango wa muda mrefu wa kujenga bweni kubwa, litakalokuwa na uwezo wa kubeba wafungwa 400 kwa wakati mmoja kwa kuwa hilo ni gereza la kikazi linalobeba watu wengi.

Kwa upande wake, Nkonda alisema kilichochangia zaidi kushuka kwa kuta hizo ni kwamba matofali yaliyojenga kuta hizo yanaonekana yalikuwa mabichi.

Alisema kwa hali hiyo haitawezekana kufanya ukarabati, bali ni kuhakikisha wanabomoa mabweni hayo na kujenga upya.

Alisema gereza hilo, lilikuwa na uwezo wa kubeba wafungwa 380 kati ya hao 100 wako kwenye kambi ndogo na 280 ndio watakaohamishiwa kupelekwa katika gereza la Mwisa.

Familia ya Aliyeuawa kesi ya Zombe na wenzake Yamuomba Rais Magufuli Awasaidie

0
0


Aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kinondoni, SP Christopher Bageni akisindikizwa kupanda gari la askari baada ya kuhukumiwa kunyongwa hadi kufa.
***
 
Baada ya Mahakama ya Rufani kutoa hukumu dhidi ya vigogo wa polisi katika mauaji wafanyabiashara wa madini, familia ya mmoja wa marehemu amemuomba Rais John Magufuli kuwasaidia yatima walioachwa. 

Akizungumza jana, Martha Martine ambaye alikuwa mke wa marehemu Mathias Lunkombe alisema kwa kuwa mahakama imeshatoa hukumu hiyo, hawezi kupingana nayo, badala yake akaeleza namna kifo cha mumewe kilivyoiathiri familia, hususan watoto wawili alioachiwa. 

Katika hukumu hiyo iliyotolewa juzi, aliyekuwa mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai Wilaya ya Kinondoni, Christopher Bageni alihukumiwa kunyongwa hadi kufa huku Abdallah Zombe na wenzake wawili wakiachiwa huru. 

Hukumu hiyo ilitolewa baada ya rufani ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ambaye hakuridhishwa na hukumu ya Mahakama Kuu ambayo iliwaachia huru washtakiwa hao. 

Bageni alikuwa ni miongoni mwa washtakiwa kwenye kesi hiyo iliyokuwa inawakabili askari polisi tisa akiwamo Zombe ambaye alikuwa Mkuu wa upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam. 

Wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, ndugu yake Eprahim Chigumbi na Mathias Lunkombe na dereva teksi, Juma Ndugu waliuawa Januari 14, 2006 kwenye Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis, Dar es Salaam. 

Kutokana na hukumu hiyo, Martha alisema kwa sasa anaishi maisha magumu kwa kuwa anatumia fedha nyingi kuwasomesha watoto wake Grace anayesoma kidato cha nne na Fulmes anayesoma kidato cha pili. 

Alisema Serikali ilimuahidi kumsaidia kutunza watoto lakini hakuna msaada wowote alioupata kutoka serikalini wala kwa kiongozi yeyote. 

Kutokana na hali hiyo, Martha alimwomba Rais Magufuli kuwasaidia watoto hao kupata elimu na mahitaji mengine muhimu ili waweze kuja kujitegemea kimaisha. 

Mdogo wa marehemu Protas, Mathias Lunkombe alisema tangu kaka yake alipofariki amekuwa akihudumia familia mbili, ya kwake na ya marehemu kaka yake. 

Kuhusu hukumu iliyotolewa, alisema haki imetendeka kwa kumhukumu Bageni kunyongwa hadi kufa japokuwa hakuna hukumu ambayo ingeweza kupoza au kuondoa machungu waliyonayo kwa ndugu yao aliyeuawa. 

“Pamoja na kumuua kaka yangu lakini kifo chake ni cha kumdhalilisha kwa sababu walimsingizia kuwa ni jambazi ilhali ni mfanyabiashara wa madini. "

Mke wa Bageni asita 
Wakati familia ya Lunkombe ikisema hayo, mke wa Bageni amekataa kuzungumzia hukumu kifo iliyotolewa kwa mumewe. 

“Mimi ni askari, nipo chini ya Kamishina (wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon) Sirro, siwezi kuongea na waandishi wa habari siruhusiwi kuongea chochote,” alisema mke wa Bageni, Stella Saria na kuongeza: 

“Kijeshi sisi tuna miiko ya kazi, kama mume wangu amepata matatizo hayo ni mambo ya kawaida, mimi nina viongozi wangu wa kazi, nilivyofundishwa kama ni kitu cha familia yangu, Christopher alikuwa ofisa wa polisi watajibu viongozi wake wapo. 

“Mimi nina amani ya kutosha, ni Mkristo nimempokea Yesu, tatizo haliwezi kunitokea nikadharau miiko ya kazi. Mimi ni kiongozi askari, naelewa miiko ya kazi lazima niiheshimu, samahani sana.” 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni Aagiza Magari yanayokamatwa yakisafirisha wahamiaji haramu yataifishwe

0
0

Serikali imeiagiza Idara ya Uhamiaji kuhakikisha inasimamia sheria kwa kuyakamata na kuyataifisha magari yote yanayotumika kusafirisha wahamiaji haramu kutoka nje ya nchi.

Pia, serikali imewaonya wanaojihusisha na mtandao wa kusafirisha wahamiaji haramu kuacha mara moja na kutafuta kazi nyingine za kufanya kwani serikali iko makini kudhibiti wahamiaji haramu.

Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuf Masauni, alipotembelea mpaka wa Tanzania na Kenya eneo la Namanga mwishoni mwa wiki, ili kujionea changamoto zilizopo mpakani na kuelewa hali halisi.

Masauni aliwatahadharisha watumishi wa Idara hiyo kuwa endapo gari litakamatwa katika eneo lolote nchini likiwa na wahamiaji haramu kupitia mpaka huo, watakuwa wameidanganya Serikali na kuidhihirishia kuwa majukumu yao yatakuwa yamewashinda.

Alisema pamoja na kuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na idara hiyo ya uhamiaji Namanga kudhibiti wahamiaji haramu, bado zipo njia za panya zinazotumiwa na wahamiaji hao mmoja mmoja kwa kushirikiana na Watanzania wachache wanaofanya kazi ya kuwavusha kwa kulipwa ujira kinyume cha sheria.

Aliitaka idara hiyo kutumia vitendea kazi vichache ilivyonavyo pamoja na waumishi wachache waliopo ili kudhibiti mianya inayotumiwa na wahamiaji hao. Pia, aliagiza doria za mara kwa mara na kuimarisha ukaguzi ndani ya magari ili kubaini wahamiaji haramu.

Alisema idara hiyo inafanya kazi kwenye mazingira magumu kutokana na uhaba wa vitendea kazi, ukubwa wa eneo la mpaka hivyo akatoa wito kwa wananchi kusaidia kuwafichua wahamiaji haramu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo alisema idara hiyo inakabiliwa na changamoto zilizopo mpakani hapo kutokana na ukubwa wa eneo la mpaka hivyo inashindwa kudhibiti eneo hilo kikamilifu.

Awali, Mkuu wa idara hiyo katika eneo hilo la Namanga, Abdalah Katimba, alisema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo upungufu wa watumishi na vitendea kazi.

Serikali Kuwasaidia Watanzania Kushiriki Katika Ujenzi wa Tanzania ya Viwanda

0
0
Serikali imeahidi kuwasaidia wazalishaji wadogo wa bidhaa mbalimbali zikiwemo bidhaa za ngozi kwa kuwajengea uwezo wa kuzalisha bidhaa nyingi na bidhaa bora, ili wazalishaji hao wageuke ni viwanda vidogo, ili uchumi wa Tanzania ya Viwanda, viwanda hivyoviwe vinamilikiwa na Watanzania wakiwemo wazalishaji wadogo wa bidhaa mbalimbali.

Ahadi hiyo imetolewa jana na Katibu Mkuu, Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Prof Adolf Mkenda kwenye mkutano wa wazalishaji wa bidhaa za ngozi  uliokwenda sambamba na maonyesho ya siku moja ya bidhaa za ngozi nchini yaliofanyika jana kwenye Viwanja wa Maonyesho ya Saba Saba, vya Mwl. J.K.Nyerere, Barabara ya Kilwa, Dar es Salaam.
 
Prof. Mkenda alisema , serikali ya awamu ya tano ina nia ya dhati ya kuwawezesha Watanzania kuumiliki uchumi wa taifa kwa kuweka mazingira wezeshi na vivutio mbalimbali na masharti nafuu kwa Watanzania kushiriki katika Tanzania ya Viwanda, ila ametoa changamoto kwa wazalishaji hao kuunganisha nguvu zao kwa pamoja na kuunda viwanda vidogo vidogo hivyo kuwa rahisi kusaidiwa kwa pamoja kuliko mmoja mmoja.
 
Prof. Mkenda alisema“Serikali inavipaumbele vya kuwawezesha wazawa kuanzisha viwanda ili kukuza bidhaa za Tanzania ikiwemo bidhaa za sekta za ngozi, hivyo mnapaswa kuwa na ujasiri wa kuzalisha na kutumia fursa hiyo kwa ajili ya ushindani”
 
Pia alitumia muda huo kuwahamasisha wazalishaji hao kutumia soko la pamoja la jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) pamoja na soko la SADC maana wanahaki ya kuuza kwenye kanda hizo.

 Na aliwaasa kutumia taasisi zingine za serikali zinazoweza kuwainua kwenye sekta hiyo ili kuondokana na changamoto mbalimbali watambue kuwa serikali inajipanga kukomesha bidhaa za mtumba nchini ili kuboresha soko la bidhaa bora zinazozalishwa katika nchi yetu.
 
Prof. Mkenda alimalizia kwa kutoa changamoto kwa Mamlaka ya Biashara Tanzania, kuandaa maonyesho mbalimbali yakiwemo maonyesho ya kisekta, ili viwanja vya maonyesho vya Saba Saba vitumike wakati wote wa mwaka mzima kwa maonyesho mbalimbali, na sio kipindi cha Saba Saba tuu mpaka Saba Saba nyingine, na kutoa vito kwa Tantrade kutoa maeneo ya kudumu kwa wajasiliamali na wazalishaji wadogo wadogo wapate maeneo rasmi ya kuonyesha bidhaa zao wakati wote.
 
Naye kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Edwin Rutageruka akijibu changamoto za Katibu Mkuu, alisema kwa kuanzia,  TanTrade ipo tayari kuwapa mafunzo ya ujasiliamali ya namna watakavyoweza kupenya kwenye masoko mbalimbali ili kukuza sekta hiyo ya ngozi, na kutenga eneo maalum kwa wazalishaji wadogo wadogo wa bidhaa mbalimbali na wajasiliamali kuonyesha bidhaa zao na pia kuanza mchakato wa kuutumia uwanja wa maoyesho ya Saba Saba kuendeshea magulio ya masoko ya Jumamosi na Jumapili, (Saturday Market na Sunday Market).

Mwenyekiti wa chama cha wazalishaji wa bidhaa za ngozi (TALEPPA)Dedan Munisi, alisisitiza sasa umefika wakati kwa Watanzania sio tuu kwa kuonyesha uzalendo wa kuthamini bidhaa za ndani, bali kuzinunua na kuzitumia bidhaa zinazozalishwa na Watanzania wenyewe, na kuwataka kuacha kasumba ya kudharau chako na kuthamini cha mwenzio kwa kutukuza bidhaa za nje kwa kudhani zina ubora zaidi kuliko zile zinazolishwa nchini, na kusisitiza bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini zina ubora wa hali ya juu kuliko bidhaa za nje.

Kwa upande wao, Wazalishaji hao wakiongozwa na Denis D. Kileo mzalishaji wa bidhaa za ngozi kutoka Woiso Original Products alisema changamoto kubwa ni watanzania kutoweza kutofautisha viatu vya ngozi bandia kutoka nje ya nchi vyenye ufanano na bei kuwa chini hivyo sekta hiyo  kudumaa  ni wakati sasa wauzaji wa maduka mbalimbali nchini kuwaamini wazalishaji na bidhaa za sekta ya ngozi na kuvipeleka mbele sokoni bidhaa zao ili kupanua masoko.

Naye Bi. Cecilia China mtafiti kutoka TIRDO aliwashauri wazalishaji wa bidhaa za ngozi kutumia taasisi za serikali za kisayansi nchini ili kuondokana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwenye sekta hiyo ili kupunguza gharama kwenye uzalishaji wa bidhaa zao na waweze kushauriwa kitaalam njia bora ya uzalishaji wenye kukidhi soko la ndani na nje ya nchi. 
 
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade) (TanTrade) ikishirikiana na na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wameandaa mkutano huo wa wazalishaji wa bidhaa za ngozi kwa lengo la kuwakutanisha wadau wa serikali na sekta binafsi ili kujadili fursa, changamoto na mikakati ya kuendeleza sekta hiyo ambayo inamchango mkubwa uchumi wa taifa kuelekea kenye Tanzania ya viwanda.

Aliyeng’atwa ulimi Wakati Akipigana Denda na Mwanamke Ahofia Kuachwa na Mchumba Wake

0
0

Kijana Saidi Mnyambi (26) anayedaiwa kung’atwa 1/3 ya ulimi wake wakati wakinyonyana ulimi na mwanamke mmoja, ameingiwa na hofu kuwa mchumba wake anaweza kumwacha kutokana na kitendo hicho.

Kijana huyo mkazi wa Unyankhae, Manispaa ya Singida, aliyasema hayo juzi hospitalini alikolazwa .

Alisema hofu aliyonayo inachangiwa kwa kiasi kikubwa na tukio hilo kuwa gumzo kubwa ndani na nje ya Singida. 

“Kabla ya tukio hilo, uchumba wangu ulikuwa unaendelea vizuri na mambo yalikuwa yanaelekea kwenye kufunga ndoa lakini sasa nina hofu mwenzangu anaweza akapotoshwa na mambo yakaharibika. Nikitoka hospitalini nitalifuatilia jambo hili kwa ukaribu zaidi ili kuweka mambo sawa,” alisema Mnyambi. 

Kuhusu matibabu, Mnyambi alisema anaendelea vizuri na kwamba sasa anaongea vizuri kama binadamu wengine na maumivu yamepungua. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba alisema wanamshikilia mwanamke huyo (jina hajalitaja) aliyemng’ata ulimi Saidi na wanaendelea na upelelezi kabla sheria hazijachukua mkondo. 

Alisema mkuu wa upelelezi makosa ya jinai Mkoa wa Singida anakamilisha uchunguzi lakini akabainisha kuwa taarifa zilizoenea awali kuhusu tukio hilo ni tofauti na hali halisi. 

“Baada ya kumpata mwanamke anayetuhumiwa kumng’ata ulimi Mnyambi, zimepatikana taarifa mpya. Waandishi kuweni na subira tutawapatia taarifa zenye mashiko wakati wowote kuanzia sasa,” alisema Kakamba.

Tetemeko la Kagera Laibua Tuhuma......UVCCM Waituhumu CHADEMA Kufanya Siasa Potofu, Wataka Uhakiki wa Misaada Ufanywe na JWTZ

0
0
Umoja  wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Kagera umelalamikia kitendo kinachofanywa na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutumia janga la tetemeko la ardhi mjini hapa kufanya siasa na propaganda potofu.

Pia umoja huo umeitaka na kuishauri Serikali kuacha kazi ya uhakiki, ugawaji wa misaada yote kwa waathirika ifanywe na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alimueleza suala hilo Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Salum Kijuu, alipomtembelea ofisini kwake.

Alimweleza kuwa kinachofanywa na Chadema ni kituko na fedheha ya kisiasa. Alisema baadhi ya viongozi wa chama hicho wanatumia tetemeko hilo kujaribu kujijenga kisiasa huku wakiwabagua wanachama wa CCM kwa itikadi za kisiasa.

Alisema uhakiki na utoaji wa msaada katika awamu ya kwanza ulifanyika kukiwa na ubaguzi na upendeleo huku baadhi ya shehena za mizigo ya misaada na vifaa vya ujenzi ikiandikwa maneno “ukawa pamoja”.

Wakati huo huo umoja huo umekikabidhi msaada wa mifuko 100 ya saruji kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali mstaafu Salimu Kijuu.

ACT-Wazalendo Wambipu Magufuli......Watangaza kufanya kongamano la kidemokrasia Septemba, 24

0
0
Chama cha ACT – Wazalendo kimetangaza azma yake ya kufanya mkutano mkuu wa kidemokrasia Jumamosi ijayo licha ya kuwapo kwa amri ya Polisi iliyokataza kufanyika kwa mikutano yote ya kisiasa nchini. 

Jeshi la Polisi lilipiga marufuku maandamano na mikutano yote ya hadhara tangu Juni 7 hadi pale hali ya usalama itakapotengemaa. 

Jeshi hilo lilisema limefikia hatua hiyo baada ya kupokea taarifa kutoka kwa vyama vya siasa vikitaka kufanya mikutano na maandamano kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kutotii sheria za nchi.

Lakini jana, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT – Wazalendo, Ado Shaibu alisema wamepanga kufanya mkutano huo kwa sababu Katiba inawaruhusu.

“ACT kimekusudia kuitisha mkutano mkuu wa kidemokrasia, hii ni haki yetu kikatiba na hata kwa dunia nzima si ajabu kwa kuwa vyama vya siasa hufanya hivyo. Kongamano hili litawaleta pamoja wanachama, wadau na wafadhili wa ACT ambao watajadili hali ya maendeleo ya nchi,” alisema na kuongeza.

“Hatutaji mahali na ukumbi tutakaoufanyia kwa sasa, wakati ukifika tutawajulisha.Na hatutaomba kibali kwa kuwa katiba haisemi vyama vya siasa viombe  kibali vinapotaka kufanya mikutano ya ndani.

Shaibu alisema kuwa endapo serikali itazuia kufanyika kongamano hilo watachukua hatua za kisheria kupinga maamuzi hayo kwa madai kuwa katiba ya nchi na ya vyama vya siasa inarushusu kufanyika.

“Serikali ilituzia kufanya mikutano na vikao vya ndani, tulikaa kimya awali tukiamini kuwa tutaishawishi kwa hoja na itajirekebisa lakini haikufanya hivyo.Tunaamini serikali itarudi nyuma na kuamini haina mamlaka ya kuzuia mikutano na vikao vya ndani kwa sababu kuizuia inamaana unafuta shughuli za siasa na sisi tutakuwa wa mwisho kukubali vyama kufutwa ,” alisema.

Alisema ACT haitokuwa nyuma kuiunga mkono serikali inapofanya vyema na kwamba endapo chama hicho kitakosoa utendaji kazi wake, serikali isikichukie kwa kuwa kinatekeleza wajibu wajibu wake.

Kwa upande mwingine, Shaibu alisema Kamati Kuu ya Uongozi wa Chama cha ACT imefanya baadhi ya marekebisho ya muundo wa uendeshaji kwa kuteua baadhi ya makatibu wa kamati za chama hicho.

“Kikao cha tatu cha kamati kuu kilichoketi Septemba 5,2016 kilifanya teuzi mbalimbali za makatibu, sambamba na kugawa baadhi ya kamati ikiwemo iliyokuwa kamati ya Ulinzi, Usalama na Uadilifu ambapo kwa sasa imegawanyika na kuwa kamati ya Usalama na Ulinzi na mpya ni Kamati ya Uadilifu, ” alisema.

Aliwataja makatibu wapya wa kamati walioteuliwa akiwemo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana Chama cha Wananchi CUF (JUVICUF) Mohamed Babu ambaye kwa sasa ni Katibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, Ally Kifu ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati ya Fedha na Miradi ya Kujitegemea. Katibu mwingine aliyeteuliwa ni Sabrah Mohamed ambaye ameshikilia Kitengo cha Kushughulikia Maendeleo ya Zanzibar.

Jipatie Kitabu cha HARD DAY Toka kwa Mtunzi Aliyebobea Eddazaria g.Msulwa

0
0

Jipatie  nakala ya  Kitabu  cha  HARD  DAY  Toka  kwa  Mtunzi  Aliyebobea  Eddazaria g.Msulwa....

Ni simulizi kali na ya kusimumua kama zilivyo Sorry Madam na She is My wife ambazo umekuwa ukizishuhudua  kupitia mtandao huu.

Bei ya kitabu ni 4000  tu, mcheki Whatsapp kwa  namba: 0657072588

Miti Ya Msyenene Na Mpambawake Huwasaidia Wanawake Wenye Tatizo La Kutobeba Ujauzito.

0
0

Kutokubeba  ujauzito  ni  tatizo  linalo  wakabili  wanawake  wengi  duniani.  Zipo  tiba  mbalimbali  za  asili  ambazo  zina  uwezo  wa  kuwasaidia  wanawake  wenye  tatizo  la kutokubeba  ujauzito    na  wale  wenye  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  mimba  ama  miscarriage.

Miongoni  mwa  dawa  asilia  zilizo  na  uwezo  wa  kuwasaidia  wanawake  wenye  matatizo  ya  uzazi  ni mti  wa  Msyenene  pamoja  na  mti  mwingine  ujulikanao  kama  Mpambawake.
 
Miti  hii  inapochanganywa  pamoja, huwa  na  msaada  mkubwa  wa kitabibu sana kwa  wanawake  wanao kabilliwa  na  tatizo  la  uzazi.
 
Tiba  hii  husaidia  katika  mambo  yafutayo :
i. Husaidia  kusafisha  mirija  ya  uzazi
ii. Husaidia  kurutubisha  mayai ya  uzazi
iii.Husaidia  kutibu  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  mimba
iv. Husaidia  kutibu  tatizo  la kutokwa  na  hedhi  mfululizo
v. Husaidia  kutibu  tatizo  la  kupatwa  na  maumivu  wakati  wa  tendo  la  ndoa pamoja  na  maumivu  wakati  wa  hedhi
vi. Husaidia  kutibu  matatizo  ya  homoni  kwa  wanawake
vii. Husaidia  kuboresha  na  kuimarisha  afya  ya  mtoto  awapo  tumboni
viii. Husaidia kutibu  tatizo  la  maumivu  chini  ya  kitovu.
Kama wewe  ni  mwanamke  unae  sumbuliwa  na  tatizo  la kutobeba  ujauzito na/au  tatizo  la  kuchoropoka  kwa  mimba, jaribu  kutumia  tiba  hii  ili  upate  faida  ambazo  wanawake  walio  itumia  wamezipata.
 
JINSI  YA  KUPATA  TIBA  HII
Kupata  dawa  hii  fika  katika  duka  la kuuza  dawa  za  asili  la  Neema  Herbalist.
 
Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO   NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo la  UBUNGO  PLAZA.
 
WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  NAMBA
0766  53  83  84.
Kwa  wateja  wa jijini  Dar  Es  Salaam, wasio weza  kufika  ofisini  kwetu, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  Dar  Es  Salaam  ( Home & Office Delivery )
 
Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  magari.
Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  boti.
 
Kwa wateja  wetu  wa  Mombasa, watasafirishiwa  dawa  kwa   bus  la  TAHMEED.
 
Kwa  taarifa  Zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  kupitia  tovuti  yetu:www.neemaherbalist.com

Waziri Mbarawa Amteua Dr Musa Mgwatu Kuwa Mtendaji Mkuu wa TEMESA

0
0

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame M. Mbarawa(Mb), amemteua Dkt. Musa Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA).

Dkt. Mgwatu amechukua nafasi ya Mhandisi Marcellin Magesa  ambaye amepangiwa majukumu mengine  Wizarani.

Kabla ya Uteuzi huo Dkt. Mgwatu alikuwa  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika Hodhi la Rasilimali za Reli (RAHCO).

Katika hatua nyingine Profesa Mbarawa amemteua Bw. Masanja Kadogosa ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) Kukaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa RAHCO.

Uteuzi huo unaanza mara moja.
Imetolewa na
Eng. Joseph M. Nyamhanga
Katibu Mkuu (Ujenzi)
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Mwenyekiti wa UVCCM afikishwa mahakamani kwa kujifanya Afisa Usalama wa Taifa

0
0


Na Woinde Shizza,Arusha-Maelezo

Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha imemsomea mashtaka mawili Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) Lengai Ole Sabaya ambaye pia ni diwani wa kata ya Sambasha Wilaya ya Arusha vijijini .

Miongoni mwa makosa hayo aliyosomewa mahakamani hapo kosa la kwanza alituhumiwa kujifanya Afisa mtumishi wa serekali (TISS)huku kosa la pili ikiwa kugushi moja ya nyaraka za serekali(kitambulisho ).

Akisoma mashtaka hayo mahakamani hapo Wakili wa serekali Lilian Mmasi alisema kuwa Mnamo May 18 katika hotel ya Skyway iliopo makao mapya jijini Arusha Mshitakiwa alijitambulisha kama Afisa utumishi wa idara ya usalama wa taifa na kufanya Utapeli .

Wakili Mmasi alitaja kosa la pili ambalo Mshitakiwa Lengai Ole Sabaya alisomewa kuwa ni kugushi kitambulisho cha idara ya usalama wa Taifa kilichokuwa kikisomeka jamuhuri ya muungano wa Tanzania idara ya usalama wa Taifa (TISS) Lengai Ole Sabaya kikosi maalumu Agent (undercover)chenye code no MT 86117 huku akitambua kuwa ni kinyume cha kisheria .

Hata hivyo mara baada ya kusomewa mashtaka hayo mahakamani hapo mtuhumiwa alikana mashtaka ndipo Hakimu Mkazi aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo Gwantwa Mwamkuga Alisema dhamana ipo wazi iwapo wathamini watakithi vigezo vinavyotakiwa na mahakama hiyo.

Hata hivyo Mshitakiwa alipata dhamana baada ya kukithi vigezo vilivyowekwa na mahakama ambapo ilikuwa ni wadhamini wawili wenye sifa ambapo kwanza awe mtumishi wa serikali pili awe na mali isiyohamishika yenye thamani ya shilingi milioni tatu kwa kila mmoja.


Kesi imeaihishwa na hakimu mkazi hadi itakapotajwa tena October 5 ambapo uchunguzi unatarajiwa kukamilika na kesi hiyo kuanza kusikilizwa.

Mara baada ya kupata dhamana mahakamani hapo wakili wa mtuhumiwa Yoyo Asubui alisema kuwa mshtakiwa amesomewa mashtaka yote mawili na kukana mashtaka ambapo wanatarajia uchunguzi ukikamilika kesi itaanza kusikilizwa mapema na haki kutendeka ,huku akimtaka mteja wake kuendelea na majukumu ya mandeleo kwa wananchi wa kata ya Sambasha.

“kwakweli kesi hii sio ya kweli na naweza kusema ipo kisiasa na nashukuru jeshi la polisi kwa kunishikilia na kukaa na mimi vyema hadi kunileta mahakamani ambapo naamini haki itatendeka na ukweli utabainika “Alisema Sabaya mara baada ya kupata dhamana

Alisema kuwa hili limetokea mara baada ya kuwatoa wabadhilifu wa mali za umoja wa vijana (UVCCM) ambapo kwa muda mrefu wamekuw a mali za umoja huo kujinufaisha wenyewe na vijana kukosa maendeleo kupitia miradi ya umoja huo.

Ndege moja kati ya mbili za ATCL Alizonunua Rais Magufuli Itatua Kesho Nchini

0
0

Ndege ya kwanza kati ya mbili zilizonunuliwa na Serikali za Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL), inatarajiwa kuingia  nchini kesho ikitokea Canada.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam jana na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL, Patrick Itule alisema ndege hiyo aina ya Bombardier Q400 inatarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7:00 mchana.

Itule alisema ndege hiyo yenye uwezo wa kubeba abiria 76, tayari imeanza safari ya kuja nchini tangu mwishoni mwa wiki iliyopita ikipitia miji ya Reykjavík, Southampton, Malta, Luxor, Addis Ababa Ethiopia kabla ya kutua nchini ikiwa na timu ya marubani wanne kutoka Canada.

“Ndege ya pili inatarajiwa kukabidhiwa Septemba 22 na kuanza safari ya kuja Tanzania Septemba 23,’’ alibainisha.

Rais Dkt. Magufuli Amjulia Hali Spika Mstaafu Samuel Sitta Pia Atembelea Kwa Kushtukiza Ofisi Za Magazeti Ya Uhuru Na Mzalendo Jijini Dar Es Salaam

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 19 Septemba, 2016 amefanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Gazeti la Uhuru zilizopo Mtaa wa Lumumba Jijini Dar es Salaam na kuzungumza na wafanyakazi.

Katika Mazungumzo hayo, wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru linalomilikiwa na CCM wamelalamikia kutolipwa mishahara yao kwa miezi saba, kutotolewa kwa michango ya wafanyakazi kwa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti katika hali ya kutatanisha, kutotambuliwa katika ajira kwa baadhi ya wafanyakazi, kutolipwa kwa madeni wanayozidai taasisi za Serikali na wanaostaafu kutolipwa mafao yao.

Wafanyakazi hao pia wamemueleza Dkt. Magufuli kuwa Bodi na Menejimenti ya kampuni ya vyombo vya habari vya chama inayoendesha Gazeti la Uhuru na Redio Uhuru zimeshindwa kuendesha vyombo hivyo na wamemuomba aingilie kati ili kuvinusuru vyombo hivyo ambavyo kwa sasa vina hali mbaya kutokana na kukabiliwa na madeni makubwa, na biashara yake imeshuka kwa kiasi kikubwa.

Akijibu malalamiko hayo Rais Magufuli aliyetembelea ofisi za Gazeti la Uhuru akitokea Ofisini kwake katika jengo la Makao Makuu ya chama, Ofisi Ndogo ya Lumumba Jijini Dar es Salaam amemuagiza Katibu Mkuu wa CCM Ndg. Abdulrahaman Kinana kuhakikisha mishahara yote wanayodai wafanyakazi inayofikia Shilingi Milioni 609 inalipwa ndani ya Mwezi huu wa Tisa, ameagiza kupatiwa orodha ya taasisi za Serikali zinazodaiwa na Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, na pia ameagiza deni linalodaiwa na NSSF kutokana na kutowasilishwa kwa makato ya wafanyakazi lilipwe.

Kuhusu malalamiko dhidi ya Bodi na Menejimenti ya Kampuni hiyo, ajira za wafanyakazi, mafao kwa wastaafu, kuuzwa kwa mtambo wa kuchapisha magazeti na mazingira magumu ya kazi Dkt. Magufuli ameahidi kuyafanyia kazi.

Aidha, Dkt. Magufuli amewapongeza wafanyakazi wa Gazeti la Uhuru kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya licha ya kukabiliwa na changamoto kubwa na amewakikishia kuwa anatambua umuhimu wao na kwamba atahakikishia anaboresha hali ya chombo hicho muhimu.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemjulia hali Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samwel Sitta ambaye anaendelea kupata matibabu Jijini Dar es Salaam na hali yake inaendelea vizuri.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

19 Septemba, 2016 

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Septemba 20


Japan yaahidi kukarabati shule zote zilizoathiriwa na tetemeko mkoani Kagera

0
0
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Japan nchini, Mheshimiwa Masaharu Yoshinda ambaye amemueleza kwamba Serikali yake ipo tayari kukarabati shule zilizoharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.

Pia imeomba kupatiwa orodha ya mahitaji ya dharura yakiwemo mahema, mablanketi, dawa na vifaa tiba kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko hilo.
 
Balozi Yoshinda ameyasema hayo leo (Jumatatu, Septemba 19, 2016) wakati alipokutana na Waziri Mkuu ofisini kwake Magogoni Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya maafa yalitokea Kagera.
 
Kwa upande wake Waziri Mkuu ameishukuru Serikali ya Japan kwa hatua hiyo na kukiagiza Kitengo cha Maafa kilicho chini ya Ofisi yake kuwasiliana na Ubalozi wa Japan nchini na kuwasilisha orodha ya shule zilizoharibika pamoja na mahitaji ya dharura.
 
Wakati huo huo Waziri Mkuu amepokea msaada wa tani 2.5 za mchele, magodoro 200, mablanketi 100 na fedha taslimu sh. milioni 10 ili kusaidia wananchi waliothirika na tetemeko hilo.
 
Msaada huo umetolewa na wadau mbalimbali akiwemo Ofisa Utumishi wa Kampuni ya Chang Qing Inernational Investiment Limited ya nchini, Bi. Anna Jiang aliyetoa magodoro 200 yenye thamani ya sh. milioni sita.
 
Wengine ni Mkuu wa Kitengo cha Fedha wa Benki ya Exim, George Shumbusho aliyetooa sh. milioni 10 pamoja na Katibu Mkuu wa Chama cha Urafiki kati ya Serikali ya Tanzania na China, Bw. Joseph Kahama aliyetoa mchele tani 2.5 pamoja na mabllanketi 100 vyote vikiwa na thamani y ash. milioni 10.
 
Waziri Mkuu amewashukuru kwa misaada hiyo na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kwa wingi ili kuwasaidia watu walioathirika na tetemeko hilo ambalo ni kubwa na halijawahi kutokea nchini.
 
Tetemeko hilo lilitokea Jumamosi, Septemba 10, 2016 na kusababisha vifo vya watu 17 na wengine 440 walijeruhiwa kati yao watu 253 walifikishwa Hospitali ya Mkoa, 153 walilazwa, 113 wametibiwa na kuruhusiwa na wengine 38 wanaendelea na matibabu ambapo kati yao watu 23 wamefanyiwa upasuaji mkubwa na wanaendelea vizuri.
 
Pia tetemeko hilo limesababisha nyumba 2,063 kuanguka huku nyingine 14,081 zikiwa katika hali hatarishi baada ya kupata nyufa na 9,471 zimepata uharibifu mdogo huku wananchi 126,315 wakiiitaji misaada mbalimbali.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa Japan nchini, Masaharu Yoshida kuhusu namna ambavyo Japan inaweza kusaidia waathika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Mazungumzo yao yalifanyika Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dares salaam Septemba 19, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

IMETOLEWA NA: 
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
2 MTAA WA MAGOGONI, 
S. L. P. 3021, 
11410 DAR ES SALAAM. 
JUMATATU, SEPTEMBA 19, 2016

Rais Magufuli ateua Wenyeviti wa Bodi na Meneja Mkuu Masoko Kariakoo

0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;

Kwanza, Rais Magufuli amemteua Prof. Jacob Philip Mtabaji kuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) kuanzia tarehe 15 Septemba, 2016.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi mbalimbali kama ifuatavyo;

Prof. Jacob Philip Mtabaji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Awadhi Mawenya ambaye uteuzi wake ulitenguliwa baada ya Kamisheni ya TCU kuvunjwa.

Pili, Rais Magufuli amemteua Prof. Mathew L. Luhanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe (MU) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.

Prof. Mathew L. Luhanga anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Daniel Mkude ambaye amemaliza muda wake.

Tatu, Rais Magufuli amemteua Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kuanzia tarehe 29 Agosti, 2016.

Dkt. Maurice Chakusaga Yohana Mbago anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Naomi Katunzi ambaye amemaliza muda wake.

Nne, Rais Magufuli amemteua Bi. Gaudensia M. Kabaka kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Dodoma (UDOM) kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Bi. Gaudensia M. Kabaka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. Augustine Mahiga ambaye kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Tano, Rais Magufuli amemteua Bi. Mariam Mwafisi kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kuanzia 05 Septemba, 2016.

Bi. Mariam Mwafisi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Deogratias Ntukamazina ambaye amemaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Bw. Hetson Msalale Kipsi kuwa Meneja Mkuu wa Shirika la Masoko ya Kariakoo kuanzia tarehe 05 Septemba, 2016.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

19 Septemba, 2016

Ujumbe wa Zitto Kabwe kwa Rais Magufuli kuhusu sakata la ESCROW

0
0
Kwanini Rais Magufuli hafanyii Kazi suala la IPTL?

Matapeli hawa wataendelea kuipa hasara Nchi yetu mpaka lini? Sasa mahakama ya ICSID imeamua kuwa Benki ya Standard Chartered ilipwe Shilingi za Kitanzania Bilioni 300 na riba. TANESCO wanaingia Hasara hii Kwa sababu ya wizi wa Fedha za TEGETA Escrow, na Rais bado anavuta miguu kuchukua hatua dhidi ya suala hili. Nini kimemkuta Rais Magufuli? Rais anataka tuamini kuwa IPTL/PAP Ni kweli waligharamia Mkutano Mkuu wa CCM uliompa yeye Uenyekiti ?

Tanzania hapo ni hasara tupu:

1) Mmelipa matapeli Fedha zilizokuwa kwenye TEGETA escrow account

2) Mmewapa mtambo wa kuzalisha umeme matapeli hao na mnaendelea kuwalipa capacity charges mpaka sasa

3) Mnawalipa standard chartered Fedha zao Kwa mtambo ambao sio wenu na Kwa Fedha ambazo mngezitoa escrow a/c lakini sasa mtazitoa hazina

Rais achukue hatua zifuatazo

– Awafikishe mahakamani watu wote waliohusika na kuitia Nchi hasara katika sakata la TEGETA Escrow
– Aitwae mitambo ya IPTL kisheria na kuimilikisha Kwa TANESCO
– Amkamate Bwana Harbinder Singh Seth na wafuasi wake wote na kuwafikisha mahakamani Kwa makosa ya utapeli, wizi, uhujumu uchumi, utakatishaji wa Fedha nk
– Benki iliyotumika kupitisha Fedha za TEGETA escrow ndio ilipe Hilo deni tunalotakiwa kulipa

Rais aamue kusimama na watanzania au kusimama na matapeli wa TEGETA escrow

Diwani wa CHADEMA Temeke afukuzwa uanachama kwa tuhuma za rushwa

0
0
September 19, 2016 Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA jimbo la Temeke kimemfukuza uanachama Diwani na Mwenyekiti wake kutoka kata ya Kurasini, Matiti Claudian Togocho kutokana na kashfa ya ufisadi wa zaidi ya shilingi milioni 400 alizozipata kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa iliyotolewa na Benard Mwakyembe ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wilaya ya Temeke imeeleza kuwa mnamo November 23 2015, Diwani huyo akiwa na wenzake wanadaiwa walitengeneza hati feki ya nyumba tano za James Makundi aliyekuwa mpangaji kwenye nyumba zake kisha kufanya hujuma ya kuvunja nyumba hizo kwa amri ya uongo ilitolewa na wakili kishoka wa Samora Avenue badala ya amri ya mahakama ikiwa ni kwa lengo la kujipatia pesa kutoka kwa mwekezaji ambazo ni zaidi ya shilingi milioni 200.

Diwani huyu pia anahusishwa na matukio mengine mawili ya udhulumaji wa zaidi ya shilingi milioni 140 za mirathi ya marehemu Peter Christian Kijeni wakati kesi ikiwa mahakamani pamoja na fedha za fidia za Paulina Shaban na wajukuu zake ambao Diwani huyo alisimamia nyumba zao kubomolewa.

"Kutokana na maamuzi ya chama baada ya kujiridhisha na makosa yake na kwa mujibu wa katiba ya chama chetu, mamlaka za mwisho zimefikia maamuzi ya kumvua uanachama wake hivyo atakuwa amepoteza sifa za kuwa Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mivinjeni pamoja na nafasi yake ya Udiwani kata ya Kurasini." Alisema Benard Mwakyembe

Wataalam wa maabara waagizwa kujisajili

0
0
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ameagiza waajili wote nchini kutoajili wataalamu wasio sajiliwa na wataalamu wa Baraza la Maabara za Afya nchini ili kuepuka kuajili wataalam hewa.

Dk. Kigwangalla ameyasema hayo jana wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wataalamu wa Huduma za Maabara za Afya tukio lililofanyika Jijini Dar es Salaam ambapo Naibu Waziri alikuwa mgeni rasmi huku akitoa vyeti kwa wajumbe wa Baraza hilo waliomaliza muda wao pamoja na wajumbe wapya.

Akipongeza Baraza hilo la Maabara, alisema kuwa licha ya kuwa ni la siku nyingi,  amelitaka kuhakikisha wanashirikiana na Mamlaka zingine husika kusimamia ubora wa wataalamu kusimamia vyuo husika katika kuwapata wataalam hao.

Pia aliwataka wataalamu wa Maabara waliosajiliwa kwa sheria ya 12 ya 1997, wajisajili tena upya kwa sheria mpya ya namba 22 ya mwaka 2007 kama ilivyoelekezwa ili wapate vyeti vipya.

Mwisho aliwaagiza wataalamu woye wa maabara waliosajiliwa wahakikishe wanalipia ada ya usajili kila mwaka ili kuendelea kupata kibali cha kuendelea kutoa huduma cha maabara kwa mwaka mzima ili baraza hilo liweze kujiendesha.

“Ili muwe wataalam, lazima muwe na chombo kama hichi. Hivyo katika msingi huo nyie wataalum wenyewe mutakiwa kujiongeza katika kuhakikisha munapata fedha kwa kuchangia/kuchangishana muweze kujindesha kama yalivyo mabaraza mengine” alisema Dk.Kigwangalla.

Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya, ni chombo cha kisheria kilichowekwa na Serikali ili kuwatambua na kuwasajili Wataalamu wa Maabara za Afya ya Binadamu, kusimamia ubora wa utoaji wa huduma za uchunguzi wa magonjwa ya binadamu, kuchukua hatua za kisheria kwa wakiukaji wa sheria, na kushauri Serikali katika kuboresha huduma za maabara kwa wagonjwa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images