Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 5 & 6

0
0

Mwandishi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia....
.....Rahabu akapunguza mwendo wa pikipiki na agnes akaruka na kukimbilia njia aliyo kwenda kibopa,rahab akapita njia aliyo kwenda muntar.Muntar akajibanza kwenye mti na kuokota gongo kubwa na kulishika kwa umakini.Gafla rahab akajikuta akiichia pikipiki na kuanguka chini hii ni baada ya kupigwa gongo la kifua na muntar akajitokeza mbele yake huku akiwa na gongo mkononi....

Edndelea....
.....Rahab akanyanyuka haraka,akamtazama muntar ambaye alianza kucheka kwa dharau akimtazama rahab kuanzia juu hadi chini.Muntar akarusha gongo kwa kutumia nguvu nyingi,rahab akalikwepa na kurusha teke lililotua shingoni mwa muntar na akaayumba,kabla hajajiweka sawa rahab akampiga muntar ngumi kadhaa za kifua na kuzidi kumfanya muntar kuyumba mithili ya mtu aliyelewa kwa pombe za kienyeji.(mataputapu).

Muntar akajaribu kurusha ngumi ila rahab akafanya maamuzi ya haraka katika kuudaka mkono wake wa kulia,akajigeuza na kwakutumia bega lake akauvunja mkono wa muntar.Kilio cha maumivu makali kikamkumba muntar.Pasipo kuwa na huruma rahab akampiga mtama muntar na kumfanya aliachie gongo alilolishika.Rahab akaliokota gongo na kuanza kumpiga muntar gongo la kichwa hadi damu nyingi zikaanza kutoka nje kwa kasi kama bomba la maji lililo pasuka sehemu ndogo.

 Kibopa akafunga breki za miguu yake baada ya kukutana uso kwa uso na agnes.Kibopa akameza funda kubwa la mate huku mwili wake ukimtetemeka kiasi kwamba akabaki akiwa hajajua nini la kufanya.Agnes akaachia tabasamu pana baada ya kuiona surulia ya kibopa ikianza kuchora ramani ya kutota kwa mikojo aliyo shindwa kuizuia.
“ni....Iisssa...Mehe”

Kibopa alizungumza kwa kigugumizi kikali,agnes akapiga hatua hadi alipo simama kibopa na akamtisha kama anampiga ngumi ya uso,kwa woga uliokithiri ukammdondosha kibopa chini kama mzigo na akaanza kulia kama mtoto mdogo
“khaa wewe si jambazi,mbona unalia sasa?”

“mimi ni nilikuwa kibaraka waoo tuu,sioooo jambaazzziiii” kibopa alizungumza kwa kuyavuta vuta maneno kama amemeza fumba la uji wa moto na anashindwa kuumeza.Agnes akamtazama kwa huruma kipopa ambaye taratibu alianza kupiga magoti akimuomba msamaha.Agnes akampiga kofi la shavu kipopa na kumuamuru kusimama
“wenzenu wapo wapi?”
“wameshakufaa”
“changanya mbaliga zako,kabla sijabadilika”
“eheee....!!”

Agnes akampiga kibopa teke la makalio huku akimsindikiza na kofi la mgongoni na kumfanya kibopa aanze kukimbia kwa kasi kubwa.Agnes akabaki kucheka kwani hakutarajia kama ataweza kukutana na mwanaume muoga kama kibopa.

                                          *****

Jackson luther mpelelezi anaye sifika kwa kazi yake nzuri akaanza kupandisha ngazi kwenda juu alipo anna kwa lengo la kumtia nguvuni kwa kosa la mauaji.Anna akaanza kukimbia akipandisha ngazi kwa kasi hadi akafika alipo waacha wezake.
“tuondokeni kimenuka”

Wakasaidiana kumkokota fety ambaye amechoka sana kwa kazi ya kupambana na karim pamoja na shamsa.Wakaingia ndani ya lifti na kushuka hadi gorofa ya kwanza,jackson akaitoa bastola yeka na kuwa makini zaidi,taratibu akaanza kuuunguza mwili wa muntar na kuhakikisha kwamba uhai wa mwili huo umesharudi kwa Mungu baba.

Kitu ambacho kinamchanganya jackson luther ni juu ya nani aliyeweza kumuua karim kwani ni miongoni mwa majambazi ambao alijaribu kuwafuatilia kwa kipindi kirefu pasipo kupata mafanikio ya aina yoyote katika kazi ya uchunguzi wake.Akapandisha hadi gorofa ya tano alipomuona anna akimalizikia na akakuta korido ikiwa haina mtu hata mmoja.

Akachunguza sehemu yote na kumkuta mtu aliye anguka chini akiugulia maumivu na mlango wa kuingilia chumbani kwake ukiwa upo wazi, akamsogelea na kumpa mkono na kumuinua kutoka alipokuwa.

“umepatwa na nini?”
“kuna wadada bwana hapa,walikuwa wakipigana na kuniangusha”
“umeumia?”
“ndio nimepiga kiuno chini.”
“wameelekea wapi?”
“hata sijui wametoka vipi humu ndani kwangu”
“sawa”

Anna,fetty na halima wakaingia kwenye jiko kuu la kupikia vyakula kwa kutumia mlango wa chini wakashuka kwenye ngazi na kutokezea upande wenye maswimcming pool katika hotel,wakawatizama watu waliomo ndani ya hotel na kuona hakuna anayewatilia mashaka kwa mwendo wa umakini wakaanza kuelekea kwenye sehemu lilipo gati la kuingilia hotelini.Kabla ya kutoka nje ya geti walinzi wakawasimamisha,kwa jicho la kuiba fetty kwa kupitia kioo cha dirisha la kijumba cha walinzi akaona video inayomuonyesha akipambana na shamsa kupitia kwenye tv ndogo iliyopo kwenye kijumba cha walinzi


Kutoka Mahakamani: Zombe Aachiwa Huru, Mwenzake Ahukumiwa Kunyongwa Hadi Kufa

0
0

Mahakama ya Rufani imemhukumu kunyongwa hadi kufa aliyekuwa Mkuu wa upelelezi wilaya ya Kinondoni (OC-CID), Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, baada ya kumtia hatiani kwa kosa ka mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge mkoani Morogoro.

Wakati Bageni akihukumiwa kitanzi, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi mkoa wa Dar (RCO), Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Abdallah Zombe na maafisa wengine wawili wa Polisi, Ahmed Makelle na Rajabu Bakari wameachiwa huru, baada ya mahakama kuwaona kuwa hawana hatia.

Bageni amehukumiwa adhabu hiyo leo baada ya mahakama ya Rufani kukubaliana na rufaa ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu kuwaachia huru katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara hao.

Wafanyabiashara hao, Savings Chigumbi, Ephraim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi wa Manzese, Juma Ndugu, waliuawa Januari 14,2006, kwa kupigwa risasi Mbezi Luis, Dar.

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumamosi ya Septemba 17

Mbowe Aibwaga NHC Kortini

0
0

Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Ardhi, imetupilia mbali pingamizi lililowekwa na mawakili wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), katika kesi iliyofunguliwa na Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

Awali, mawakili wa NHC walidai kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza shauri hilo na kwamba mkataba baina ya Mbowe na NHC juu ya umiliki wa jengo la Bilcanas lililopo mtaa wa Makunganya jijini Dar es Salaam umeisha.

Upande wa utetezi ukiongozwa na wakili Peter kibatala ulidai kuwa, mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo inaweza ikatoa uamuzi wowote na ndiyo maana wamewasilisha maombi hayo ili yatolewe uamuzi.

Akitoa uamuzi wa pingamizi la mawakili wa NHC jana, baada ya kuwa amesikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili, Jaji Siyovelwa Mwangasi alisema kuwa hoja za Mawakili wa NHC hazina mashiko kisheria kwani suala la mkataba wa umiliki Jengo hilo linahitaji ushahidi.

Jaji Mwangasi alisisitiza kuwa zuio la NHC kutopiga mnada mali za Mbowe, lilizozichukua wiki mbili zilizopita kupitia  mawakala wa kampuni ya Fosters Auctioneers katika ukumbi wa Bilcanas na katika ofisi za kampuni ya Free Media lipo pale pele.

Shirika hilo linamtuhumu Mbowe kutolipa deni la Sh. 1.3 bilioni, ikiwa ni jumla ya fedha za kodi ya kupangishwa kwenye jengo hilo huku Mbowe akifungua kesi katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, kupinga madai hayo ya NHC.

Katika kesi hiyo namba 722 ya mwaka 2016, Mbowe anawakilishwa na Mawakili na Peter Kibatala na Omary Msemo ilihali NHC ikiwakilishwa na mawakili wake Aloyce Sekule na Miriam Mungula.

Katika hoja zake Mbowe anadai kuwa, yeye na shirika hilo walikubaliana kwamba alikarabati na kulipanua jengo hilo kwa gharama zake kwa asilimia 100, makubaliano ambayo waliyaingia mwaka 1997.

Katika makubaliano hayo, Mbowe amedai kuwa walikubaliana kumiliki jengo hilo kwa pamoja kwa muda wa miaka 99, huku yeye akitakiwa kupata asilimia 75 katika mgawanyo wa mapato na NHC ikitakiwa kupata asilimia 25.

Hivyo amedai kuwa hatua ya NHC kumtoa kwenye jengo na kuchukua mali zake ni kuvunja mkataba huo. Mbowe aliondolewa kwenye jengo hilo mnamo Septemba Mosi mwaka huu.

Baada ya mahakama kufanyia uamuzi pingamizi lililowekwa na mawakili wa NHC, kesi hiyo imeahirishwa mpaka tarehe 27 Septemba, mwaka huu ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.  

Lipumba, Sakaya, Kambaya watuhumiwa kupanga njama za utekaji viongozi wa CUF

0
0
Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange

Chama cha Wananchi (CUF) kinawatuhumu waliokuwa viongozi wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho na Magdalena Sakaya aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Bara kufanya jaribio la kumteka Mkurugenzi wa Uchumi na Fedha ambaye pia ni Kaimu Naibu Mkuu CUF, Bara Joran Bashange.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma CUF inadai kuwa jana majira ya 2:30 asubuhi vijana wanaosadikiwa kuwa wa Prof Lipumba wamefanya jaribio la kutaka kumteka Bashange wakati akitoka nyumbani kwake eneo la Buguruni.

Na kwamba watekeji hao wakiwa na gari aina ya Noah yenye namba ya Usajili T 760 CEX  baada ya jaribio la kumteka, walifanikiwa kumuingiza katika gari hiyo ya NOAH iliyokuwa na vioo vyeusi (tinted).

Taarifa hiyo ilieleza kuwa Bashange alipambana na kuomba msaada kwa kuita watu waliojirani kwa yowee la kuita “Majambazi” ndipo wananchi wakalizingira gari hilo na kuweka mawe na magogo na kuita Polisi.

Baada ya Polisi kufika waliwakagua vijana hao na kuwakuta na pingu, silaha kadhaa na kitambulisho feki cha polisi.

Baada ya ukaguzi kufanyika vijana watatu walikamatwa na mmoja alifanikiwa kukimbia.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa mmoja kati ya vijana waliokamatwa ni mlinzi wa karibu wa Prof. Lipumba aitwaye HAJI “Mrangi” ambaye ni maarufu na anadaiwa kujulikana kwa ushiriki wake wa vitendo vya kihuni na kiharamia kama hivyo.

Hata hivyo, katika mahojiano ya awali mmoja wa vijana hao alitoa ushirikiano na kueleza kuwa wametumwa na Abdul Kambaya na kwamba anayeongoza oparesheni yao hiyo ni mtu aitwaye Athumani (Mganga wa Kienyeji na Mwalimu wa mafunzo ya Kareti) aishiye Ilala akisaidiwa na watu wengine wanaojulikana Abubakar Fambo, Mohamed Ibrahim na Hassan Kingwele ( Mlinzi wa Magdalena Sakaya (MB).

Vijana hao waliokamatwa wanakiri kuwa mipango yote hiyo Prof. Lipumba anaijua kama vile walivyoongoza mpango wa kuhujumu Mkutano Mkuu Maalumu wa CUF ulioahirishwa pale Blue Pearl Hotel, Ubungo Plaza.

Joran Bashange ameumizwa maeneo kadhaa ya mwili na anaendelea na matibabu na taarifa za ndani zinaonesha kuwa wahusika walielekezwa kumshambulia vibaya na kumuua ikiwa wangelifanikiwa kuondoka naye.

Vijana waliohusika na utekaji huo na gari lao wanashikiliwa na Polisi katika Kituo cha Polisi Buguruni.

Chama cha CUF kimelaani kitendo hicho na kimesema kinachukua hatua stahiki.

Pia Chama hicho kimesema kinaamini kuwa kwa sasa Prof. Lipumba na watu wake wamekusudia kuendesha hujuma za wazi na kuvuka mipaka ya ushindani wa kisiasa za ndani ya Chama na kujivika joho la ‘Uintarahamwe na Umungiki’ wa wazi dhidi ya Chama na kuhatarisha na kutishia usalama wa maisha ya viongozi wa Chama.

Wanaowapigia simu polisi bila sababu Kuchukuliwa Hatua za Kisheria

0
0
JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, limeahidi kuwachukulia hatua kali wananchi wanaotumia vibaya simu za dharura, zenye namba 111 na 112.

Simon Sirro, Kamishina wa Jeshi la Polisi amesema kuwa watu wamekuwa wakipiga simu hizo na kutoa taarifa za uongo au kupiga simu na kisha kuwapa watoto wadogo waongee.

“Polisi tutawafuatilia wote kupitia mitandao yetu General Packet Radio Service (GPRS),inayoonyesha maeneo walipo na simu wanazotumia ili kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria. Haiwezekani mtu apige simu halafu baada ya simu kopokelewa anaweka muziki,” amesema.

Kamanda Sirro amesema ni vyema wananchi wakaacha mzaha na matumizi ya namba hiyo ya Jeshi la Polisi kwani kwa kufanya hivyo inapunguza morali ya askari wa jeshi hilo kufanya kazi kwa kujituma.

“Wananchi wote watumie simu zetu kutoa taarifa zenye ukweli na zitafanyiwa kazi kwa wakati, wawasiliane na sisi pale wanapoona viashiria vya uhalifu ama tukio lolote linaloleta uvunjifu wa amani na siyo kupiga simu na kufanya mzaha,” amesema Sirro.

UKUTA Waiponza Redio ya Lowassa....Yafungwa Kwa Miezi 3 na Faini ya Milioni 5

0
0

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kupitia Kamati yake ya Maudhui imekifungia kituo cha Redio 5 Arusha kwa kipindi cha miezi mitatu pamoja na kukitoza faini ya sh. Milioni 5 kwa kosa la kukiuka baadhi ya Kanuni za Huduma za Utangazaji (maudhui) kupitia kipindi chake cha Matukio kilichorushwa Agosti 25, 2016.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamati hiyo, katika kipindi hicho Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Mh. Godbless Lema alitamka maneno ya kashfa yaliyolenga kumdhslilisha Rais John Magufuli na serikali kwa ujumla.

Wakati akisoma maamuzi ya kamati hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui Joseph Mapunda, aliongeza kuwa kituo hicho pia kilirusha maneno yaliyo tamkwa na Lema ambayo yalikuwa yakihamasisha wananchi kushiriki katika maandamano ya Ukuta yaliyopigwa marufuku na Jeshi la Polisi.

“Maneno ya Lema yalilenga kuhamasisha wananchi kupambana na jeshi la polisi na hivyo kusababisha uvunjifu wa amani na kuhatarisha usalama wa Taifa,” alisema.

Mapunda alisema uamuzi huo umetolewa na kamati hiyo baada ya kamati hiyo kusikiliza maelezo ya utetezi yaliyotolewa na wa Uongozi wa Redio 5 Arusha.

“Baada ya kusikiliza maelezo ya utetezi kamati imeridhia kuwa kipindi cha matukio kilikiuka baadhi ya kanuni za maudhui namba 5(a,b,c,d,f,h) 6(2) (b, c) na 18 (1) (b),” alisema.

Aliongeza kuwa ” kituo hicho kinatozwa faini ya sh. Milioni 5 ambazo zitatakiwa kulipwa ndani ya siku 30 kuanzia leo, kinafungiwa kwa miezi 3 na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa muda wa Mwaka 1 baada ya kipindi cha kufungiwa kumalizika, “

Hata hivyo, Mapunda alisema haki ya wahusika kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo iko wazi ndani ya siku 30 kuanzia leo.

Kwa upande wa kituo cha redio cha Magic Fm ambacho nacho pia kwa mujibu wa kamati hiyo kinadaiwa kukiuka kanuni za maudhui kupitia kipindi chake cha Morning Magic kipengele cha Paka Rangi ambapo kilirusha maneno yanayodaiwa kumkejeli rais na wananchi, kimepewa onyo kali pamoja na kutakiwa kuomba radhi kwa muda wa siku tatu mfululizo.

“Baada ya kusikiliza na kutafakari kwa kina maelezo ya utetezi yaliyotolewa na Uongozi wa Magic Fm Redio, Kamati ya Maudhui imeridhika kuwa kipindi cha Morning Magic kilikiuka baadhi ya kanuni za huduma za utangazaji 2005. Kamati ya maudhui inaamua kutoa onyo kali kwa Magic Radio, ” alisema na kuongeza.

“Pia inatakiwa kumuomba radhi Rais John Magufuli, wasikilizaji na wananchi kwa ujumla. Tangazo la kuomba radhi litolewe kwa siku tatu mfululizo katika taarifa za habari za saa 10.00 alasriri, na 3.00 usiku kuanzia tarehe 17,9,2016.”

Matembezi Dar yakusanya Sh1.5 bilioni za waathirika wa tetemeko Kagera

0
0

Na: Frank Shija, MAELEZO

TAKRIBANI shilingi bilioni 1.5 zimechangwa kufuatia matembezi ya hisani yaliyopewa jina la “Walk for Kagera” yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kusaidia wahanga wa Tetemeko la Ardhi lililotokea tarehe 10 septemba mwaka huu mjini Bukoba Mkoani Kagera.

Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.

“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya, mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na kwa wakati.

Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.

“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili, sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.

Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni 1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.

Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.

Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.


Rais Magufuli Apokea Taarifa Ya Tetemeko La Ardhi Mkoani Kagera, Akabidhiwa Msaada Wa Dola Laki Mbili Utoka Kwa Rais Museveni Wa Uganda

0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Magufuli amepokea taarifa ya maafa yaliyosababishwa na tetemeko la ardhi lililotokea katika Mkoa wa Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Tetemeko hilo limetokea Kagera na mikoa jirani ya Mwanza, Geita na Kigoma.

Pamoja na kupokea taarifa hiyo Rais Magufuli amepokea mchango wa fedha taslimu kiasi cha Dola za Kimarekani laki mbili (USD-200,000/-) sawa na shs 437 milioni kutoka kwa Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.

Pia amepokea taarifa ya mchango wa mabati, blanketi na magodoro vyenye thamani ya Shilingi za Kitanzania milioni 115 kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kenya Mh Uhuru Kenyatta kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tetemeko la ardhi Mkoani Kagera.

Katika taarifa yake  Majaliwa amesema tetemeko hilo limesababisha vifo vya watu 17, majeruhi 440, nyumba 2063 zimeanguka, nyumba 14,081 zipo katika hali hatarishi na nyumba 9,471 zimepata uharibifu mdogo, huku watu 126,315 wakihitaji misaada mbalimbali.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi mchango wa fedha  cha dola za Kimarekani laki mbili (USD 200,000) taslimu uliotolewa na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kwa ajili ya kusaidia waathirika watetemeko la ardhi mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisoma taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kusoma taarifa kuhusu Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Naibu Balozi wa Kenya hapa nchini Mhe. Boniface Muhia mara baada ya kupokea salamu za pole kutoka kwa Rais  Uhuru Kenyatta  wa Kenya na kwa misaada mbalimbali ya mabati 4,000 na vifaa vya majumbani ikiwemo magodoro na mashuka ambayo inatarajiwa kuwasili mkoani Kagera kutoka Kenya muda wowote kuanzia sasa. Katikati ni Balozi wa Uganda hapa nchini Mhe. Doroth Samali Hyuha
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa fedha taslimu kutoka Uganda pamoja na taarifa ya Tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kutoka kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Ikulu jijini Dar es Salaam.
PICHA NA IKULU

Taarifa Muhimu Iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Jioni Hii

0
0
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuwatahadharisha kuwa kuna watu wametumia nembo ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na jina la Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu kuchapisha na kusambaza barua kwa Kampuni Binafsi na Wakurugenzi Watendaji wakiwataka kuchangia fedha kwa ajili ya kile kinachodaiwa kuwa ni "Mkutano Mkuu wa Rekebisho la Bajeti za Miundombinu na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii utakaofanyika katika kumbi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 21/09/2016 hadi 23/09/2016"

Mnataarifiwa kuwa barua hizo zilizotiwa saini na muhuri wa kughushi na ambazo hata maelezo yake hayaeleweki vizuri hazijaandikwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na kwa maana hiyo zimeandikwa na watu wenye nia mbaya na wanaolenga kujipatia fedha kwa utapeli.

Yeyote aliyepokea barua hizo azipuuze na achukue hatua mara moja kwa kutoa taarifa katika vyombo vya dola kwa kuwa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu haijaandika barua hizo na haitambui Mkutano huo.

Aidha, Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu inapenda kuueleza umma kuwa uendelee kupokea taarifa sahihi zinazotolewa kupitia vyombo vya habari na pale ambapo kuna mashaka juu ya taarifa zenye nembo ya Ikulu wasisite kuwasiliana moja kwa moja kwa njia ya simu zilizotajwa katika anuani ya mawasiliano hapo juu.

Tafadhari atakayepata ujumbe huu umtaarifu na mwenzake.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

17 Septemba, 2016

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumapili ya Septemba 18

Aliyebaka na kulawiti kwenye kaburi afungwa miaka 30 jela

0
0
Mahakama ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu Ally Rashid maarufu kwa jina la Ally Mwizi kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti msichana mwenye umri wa miaka 25, makaburini.

Hukumu hiyo iliyovuta hisia za watu wengi wa Manispaa ya Mpanda ilitolewa jana na Hakimu wa mahakama hiyo, Chiganga Ntengwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka pasipo kutia shaka, ukiongozwa na Mwanasheria wa Serikali wa Mkoa wa Katavi, Jamila Mziray.

Awali Mwendesha Mashtaka Mziray alidai mahakamani hapo kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 17, mwaka huu, saa 2:00 usiku katika makaburi ya Kashaulili yaliyoko katika Mtaa wa Kotazi, Manispaa ya Mpanda.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa kabla ya kutenda kosa hilo alimfuata msichana huyo ambaye alikuwa ameibiwa vitu vyake vya ndani ya nyumba ambapo alimdanganya kuwa ana uwezo wa kumsaidia kuvipata vitu vyote alivyoibiwa.

Mziray alidai kuwa baada ya msichana huyo kuahidiwa na mshtakiwa kuwa vitu vyake alivyoibiwa vitapatikana alimlipa mshtakiwa Sh 30,000 ili akamwoneshe vitu vyake alivyoibiwa.

Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa siku hiyo ya tukio mshtakiwa alimpigia simu msichana huyo saa 2:00 usiku akimtaka waonane ili akamwonesha vitu vyake vilivyoibiwa.

Mziray alieleza mshtakiwa alikwenda nyumbani kwa msichana huyo na wakaongozana hadi kwenye makaburi ya Kashaulili ambako alidai ndiko vilipo vitu vilivyoibwa lakini ghafla mshtakiwa alimpiga ngwala msichana huyo na kumbaka  na kumlawiti huku akimtishia maisha iwapo akijaribu kupiga kelele.

“Baada ya kumtendea unyama msichana huyo, mshtakiwa alimwomba dada huyo waende kwenye nyumba ya kulala wageni inayoitwa Kingi Paris ili wakaendelee kufanya mapenzi zaidi kwa kile alichodai kuwa nyumba hiyo ya wageni inafaa zaidi kufanyia tendo la ndoa kuliko juu ya kaburi,” alidai.

Mwenyekiti UVCCM mbaroni kwa kughushi kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa.

0
0
Siku tatu baada ya kutuliza vurugu baina ya viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM), polisi inamshikilia mwenyekiti wa umoja huo, Lengai Ole Sabaya kwa tuhuma za kughushi kitambulisho cha Idara ya Usalama wa Taifa. 

Viongozi hao walipambana Alhamisi wiki hii wakati wakigombea ofisi ya umoja huo ya mkoa, vurugu zinazodaiwa kusababishwa na mgogoro wa chini kwa chini uliodumu kwa miezi miwili kati ya makundi mawili yanayokinzana. 

Wakati hali hiyo haijatulia, juzi saa 6.00 usiku, Sabaya alikamatwa katika baa ya Mile Stone akiwa na wenzake. 

Habari zilizopatikana jijini Arusha zinasema kitambulisho hicho kilipelekwa kituo kikuu cha polisi ambako kulifunguliwa jadala la kesi ya madai namba RB 5055/2016. Ilifunguliwa na hoteli ya Sky Way aliyokwenda kulala na kuondoka bila kulipa gharama za malazi. 

Awali, ilidaiwa kwamba mwenyekiti huyo aliweka rehani kitambulisho hicho na simu yake ili kupewa muda wa kulipa deni la hoteli hiyo. 

Meneja wa hoteli hiyo, Filipo John alisema kiongozi huyo alikuwa akidaiwa Sh309,400 za siku sita alizolala hotelini hapo. 

Pia, John alikiri kupokea kitambulisho hicho na simu ambavyo alisema baada ya kiongozi huyo kuondoka bila kulipa, alipeleka malalamiko kwa uongozi wa mtaa na baadaye alipeleka kesi hiyo polisi. 

“Nilipeleka kesi kwa balozi na mwenyekiti wa mtaa, lakini walishauri vitu vyake vipelekwe polisi. Baada ya kunilipa nilifuta kesi,” alisema meneja huyo. 

Kamanda wa polisi wa Mkoa, Charles Mkumbo alisema wanaendelea kumshikilia Ole Sabaya kwa ajili ya upelelezi na atafikishwa mahakamani kesho.

Lowassa Kumwanika Profesa Lipumba

0
0
Aliyekuwa mgombea urais wa Chadema akiungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, anajiandaa kuweka wazi ushiriki wa aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba katika mchakato wake wa kuhamia Chadema mpaka kuwa mgombea urais.

Akizungumza kwa simu na mwandishi wa habari hii akiwa Nairobi nchini Kenya jana, Lowassa ambaye pia alikuwa Waziri Mkuu, wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Rais Jakaya Kikwete, alisema akirudi kutoka safari hiyo, atafafanua mbele ya vyombo vya habari, tuhuma dhidi yake zilizotolewa na Profesa Lipumba.

“Kwa sasa naomba uniache kwanza maana nipo safarini Nairobi, nikija Dar es Salaam nitazungumzia suala hilo kwa undani kupitia vyombo vya habari, hivyo subirini nirudi,” alisema Lowassa.

Madai ya Lipumba
Hivi karibuni Profesa Lipumba alitupa lawama moja kwa moja kwa Lowassa, kwamba ujio wake ndani ya Ukawa, unaoundwa na Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD, ndiyo ulisababisha matatizo katika vyama hivyo kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa Profesa Lipumba, kabla ya kujiunga kwa Lowassa Ukawa, vyama hivyo walikaa kikao ambacho aliwashauri viongozi wenzake wa Ukawa kutazama mtu anayeweza kuendana na mahitaji yao awe ndani au nje ya umoja huo.

Alisema ni kweli aliona wangeweza kupata ushindi kupitia Lowassa, lakini hata ushindi huo ungepatikana, wangeenda kusimamia mambo gani? Maana suala ni kusimamia katika eneo fulani.

Alifafanua kuwa suala lililopo katika siasa ni baada ya kuchaguliwa, uunde serikali ili usimamie misingi fulani ambayo itakidhi mahitaji ya wananchi. 

“Sisi tulisema tunahitaji serikali inayowajibika, itakayopambana na rushwa, itakayotumia rasilimali za nchi vizuri, na itakayohakikisha mali ya asili ya Tanzania inawasaidia Watanzania wote,” alisema na kuongeza kuwa hayo Lowassa asingeweza.

Baada ya kikao hicho cha kumjadili Lowassa, Profesa Lipumba alisema walifanya kingine wakiwa na Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Chadema); Mbatia (James, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na Lowassa kujadili suala hilo kwa mara ya pili kuwa ni vyema CUF, wakaribishwe kwanza ambapo walikuwa hatua za mwisho.

Alisema baada ya mchakato huo kwisha, Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad, alianza vikao vingine visivyomshirikisha yeye Lipumba, kwa kumwalika Mbowe ili wafanye mazungumzo. 

Lipumba alidai kuwa Mbowe alipoitwa na Maalim Seif kwenda Zanzibar, alimfuata na kumweleza kuwa ameitwa na Makamu wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar.

“Mbowe alinipigia simu akaniambia kuwa ameitwa kwenye kikao na kwamba ndio kulikuwa na hoja ya Lowassa kuingia Ukawa, wakati Chadema walikuwa na msimamo kuwa kwenye Ukawa asikaribishwe mtu wa nje,”alifafanua.

Alisema Mbowe aliendelea kumweleza kuwa, baada ya kikao kile ndipo Chadema waligundua kuwa kuna sintofahamu ndani ya CUF, jambo lililowafanya wao Chadema watoe hoja ya kuwa na mgombea wao, kwakuwa watakuwa na wabunge wengi basi hata Waziri Mkuu atatoka huko na CUF itatoa mgombea mwenza.

Lipumba alisema baada ya hali hiyo kutokea; ya Maalim Seif kufanya vikao vingine bila kumshirikisha, alikuwa katika wakati mgumu maana hata mazungumzo yale hakushirikishwa, ilihali yeye ndio Mwenyekiti wa CUF na yalikuwa yanafanywa na Katibu kimnya kimnya.

Sheria zote Nchini kuwa kwa Kiswahili

0
0

Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Profesa Sifuni Mchome amesema kuanzia sasa sheria zote zitakazotungwa nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo, kuzielewa.

Uamuzi huo unakwenda sambamba na kuzitafsiri sheria zote zinazotumika nchini ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza ili kutimiza lengo hilo la kuwafanya wananchi wengi wazielewe.

“Kwa sasa serikali imeamua kuwa sheria zote nchini zitakuwa katika lugha ya Kiswahili na zile ambazo ziko katika lugha ya Kiingereza zitatafsiriwa ili kuwawezesha Watanzania wengi ambao ndio walengwa wa sheria hizo kuzielewa,” alisema.

Pia alisema serikali itazifanyia marekebisho sheria zote ambazo zimekuwa zikilalamikiwa na wadau mbalimbali kuwa hazikidhi mahitaji au haja, haziendani na wakati uliopo sasa ili kutekeleza azma yake ya kuwahudumia wananchi wake kwa ukamilifu.

Profesa Mchome ameyasema hayo jijini Dar es Salaam jana baada ya kupokea mapendekezo yaliyowasilishwa na Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WILDAF), ambayo yanataka kufutwa kwa sheria mbalimbali za kimila zinazosimamia masuala ya mirathi ambazo zinalalamikiwa kuwakandamiza wanawake nchini.

Profesa Mchome amewashukuru WILDAF kwa kazi waliyoifanya na kuwaahidi kuwa wataalamu wake wizarani watayafanyia kazi mapendekezo yao ili kuhakikisha gurudumu la sheria nchini linasonga mbele na kuwasaidia wananchi wengi.

Akizungumza katika makabidhiano hayo Mkurugenzi wa WILDAF, Judith Odunga alisema mapendekezo hayo yanataka kufutwa kwa sheria za kimila ambazo kwa kiasi kikubwa zimekuwa zikiwakandamiza wanawake, kuwanyima haki ya kumiliki mali na kufanyiwa vitendo vya kidhalilishaji pale wanapofiwa na waume zao.

Alisema katika mapendekezo hayo WILDAF inaiomba serikali itunge sheria moja ambayo pamoja na zile za kidini itashughulikia masuala ya mirathi na kuweka usawa wa kisheria katika urithi wa mali kati ya mwanamke na mwanamume, ikiwa ni pamoja na watoto wa kiume na wa kike kuwa na usawa katika kurithi mali inapotokea mzazi wa kiume amefariki dunia.

Manispaa ya Kinondoni Yavunjwa Rasmi....Meya Boniface Kapoteza Nafasi Yake

0
0

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurumjuli amevunja Baraza la Madiwani rasmi baada ya serikali kuigawa manispaa hiyo kuwa mbili. Kagurumjuli alilivunja juzi saa 11:00 baada ya kumalizika kwa Baraza la Madiwani la kawaida.

Alipokuwa akitangaza kulivunja baraza hilo, Kagurumjuli alisema amevunja baraza hilo kwa kuwa serikali imegawanya manispaa hiyo kuwa wilaya mbili, ya Kinondoni na Ubungo hivyo kwa kuwa wilaya zote tayari zina wakurugenzi, wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa wilaya imempasa kufanya hivyo.

“Baraza la madiwani limevunjwa, kuvunjwa kwa baraza hili ni ukomo wa meya pia,” alisema.

Aliongeza kuwa wiki ijayo kutakuwa na uchaguzi wa meya katika manispaa hizo.

Meya wa Manispaa ya Kinondoni alikuwepo kabla ya kuvunjwa kwa baraza hilo ni Boniface Yakob ambaye amebaki nafasi yake ya udiwani.

Kuvunjwa kwa baraza hilo kulikuwa kunatarajiwa baada ya serikali kugawanya manispaa ya Kinondoni kuwa mbili.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 49 & 50 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa


Ilipoishia....
Nikaachia msunyo mkali na kuirudiisha gari yangu upande wa kushoto nilipo toka na jamaa akanifwata nilipo,sikuwa na budi zaidi ya kutoka nje ya barabara kuepika kugongana uso kwa uso na gari hilo.Gari ikaanza kunishinda nguvu badala ya kufunga breki kwa kuchangunyikiwa nikawa na kazi ya kuongeza kasi.Nikastukia gari ikaanza kupiaga kubingiria kwa kasi ya ajaba.Jinsi inavyobingiria ndivyo jinsi ninavyo jigonga ndani ya gari hadi giza jingi likayavaa macho yangu na kutulia kimya...

Endelea...
....Kwa mbali nikaanza kusikia milio ya ndege,nikajaribu kuyafumbua macho yangu ila kichwa changu nikakuta kinaniuma sana.Nikakajikaza sana na kuyafumbua macho yangu yakakutana na mwanga mkali  wa juu unao ingi kwenye kioo cha mbele cha gari langu.Nikajaribu kujichunguza kwa umakini na kugundua mikono yangu imefungwa pamoja na mskani wa gari langu.Kila nanapovuta taswira ya sehemu nilipo,sijawahi kuiona siku hata moja.Miti mirefu iliyopo kwenye eneo zima lililo gari langu likazidia kunichanganya.

Baada ya muda kiogo nikastukia mlango ukifunguliwa na akasimama jamaa mwenye bunduki mbele yangu,huku akiwa amevalia mavazi meusi kuanzia juu hasi chini.Akanitazama kwa umakini kisha akaifungua mikono yangu na kunitoa ndani ya gari na kunitupa chini.Akaninyanyua na kuniweka begani,tukaanza kuondoka pasipo kuwezakujua ni wapi tunapo elekea,hatua kadhaa mbele nikaona jumba kubwa lililo zungukwa na miti mingi ambayo kwa mbali huwezi kugundua kama kuna jumba kubwa kama hili

Tukaingia ndani na jamaa akanibwa mbele ya watu wapatao ishirini walio shika bunduki zao.Mapigo ya moyo yakaanza kunienda kasi baada ya macho yangu kutazamana na mzee godwin ambaya jicho lake moja ameliziba na kitambaa cheusi.Mzee godwin akatabasamua na kumuamuru mtu aliye nilete katika sehemu hii kunifungua mikono yangu.
“eddy.....Eddy......Eddy my x-son”

Mzee godwin alizungumza kwa dharau kubwa huku akinizunguaka taratibu katika sehmu ambayo nimesimama.Kila niliye jaribu kumtazama sura yake haikuonyesha huruma hata kidogo japo kuna wasichana watatu ila nao sura zao zinaonekana zimejaa ukatili mkubwa.Kitu mabacho kinaniumiza
“usishangae sana kwa maana vita yangu mimi na wewe bado inaendelea”

Kwa haraka ninakumbuka kwamba huyu mzee niliambiwa kuwa amechanganyikiwa sasa sijajua imekuwaje hadi leo anamiliki kundi kubwa la watu kiasi hichi,gafla mzee godwin akanipiga mtama ulio niangusha chini vibaya sana na kunifanya niaanze kutoa miguno ya maumivu

“wewe ndio,chanzo cha kuipoteza mali yangu.Wewe ndio mtu uliye mteka mwangua.Wewe sio mwanangu niambie yupo wapi mwanangu?”
Maswali ya mzee godwin yanakizidi kunichanganya kwani sikujua mwanaye anaye mzungumzia ambaye anadai nimemteka ni nani

“mi...Mi mbona sikuelewi?”
“ahaa hunielewi?”
Mzee godwin akanipiga teke la kifua na kunifanya nijikunje huku maumivu yakizidi kunitawala kwenye kifua changu.Machozi mengi yakaendelea kunitoka
“ninakwenda kumuua mama yako?”

“hapana baba.Kumbuka kuwa mama ni mke wako wa ndoa.Mtu wa kuniua ni mimi hapa na wala si mama yangu.Nipo chini ya miguu yako”
Nilizungumaza huku nikiwa nimeishika miguu ya mzee godwin,akarudi nyuma na kunipiga teke lililo ifanya mikono yangu kuuiachia miguu yake

“yupo wapi,manka mwanangu?”
“manka,yupo arusha”
“arusha,arusha.Ndipo ulip kwenda kumficha si ndio?”
“hapana baba,mbona manka yeye ndio aliye watoroka nyinyi?”
“mimi sio baba yako na manka mwangu hawezi kunikimbia mimi”

Mzee godwin alizungumza kwa hasira huku akinitazama,akamuomba mwenzake mmoja waya wa umeme ambao unene wake  ni 1.5,akaukunja mara mbili na kuanza kunichapa nao kwa fujo huku akinitukana mimi na mama yangu.Nikazidi kulia kwa uchungu mkubwa,maumivu mengi yakazidi kuusonga mwili wangu.
Kila ninapojaribu kuizuia sehemu moja ya mwili wangu isichape basi sehemu nyingine ni lazima ichapwe kwa waya huu.Mzee godwin bila ya huruma akachukua pakti mbili zenye unga mwekundu na kuanza kunimwagia mwilini mwangu,hapa ndipo nikagunda ni unga wa pilipili ndio anao nimwagia.

Mauimivu ninayo yapata hayana mfano,kikubwa ambacho ninakilinda ni macho yangu yasiingie pilipili hii.Mzee godwin akawaamrisha watu wake wakamtafute manka na kumleta hapa mara moja.Mimi wakaniburura na kuniingiaza kwenye chumba kimoja ambacho kina giza nene.Baada ya dakika kama mbili nikastukia taa tatu kubwa zikiwaka zenye mwanga mkali ambao ukaanza kuniungaza mwili wangu,jasho ambalo linanimwagika kutokana na mwanga mkali,likazidi kunichoma kwenye vidonda vyangu.
Sehemu zote za majeraha ya mwili wangu,zikazidi kuniuma kiasi kwamba maumivu makali yakazidi kunitwala.Taa zikaendelea kuwa zaidi ya dakika kama kumi kisha zikazimwa.Nikabaki nikiwa nimekaa chini nimejikinyata mwili mzima huku nikiwa ninatetemeka kma nimepigwa na shoti.

Nikaendelea kukaa ndani ya chumba kwa muda mrefu,sikujua jinsi masaa yanavyo kwenda,mlango ukafunguliwa na ikawasha taa ya kawaida,mbele yangu akasimama mwanamke mrefu mwenye mwili mmnene kiasi.Mikononi akiwa ameshika sahani yenye chakua kingi,akachuchumaa na kuniwekea

“kama unaweza kula sawa,kama hutoweza kula acha”
Alizungumza na kutoka ndani ya chumba na kukifunga,nikaivuta sahani yenye chakula taratibu.Nikaanza kula wali uliopikwa vibaya kwani wala haukuiva vizuri,sikuwa na jinsi zaidi ya kuendelea kuula huku nikiwa nimejikaza.Mwili mzima unanitetemeka kwa maumivu makali,chakula kingi kinamwagika chini kutokana na mikono yangu kutetemeka sana kiasi kwamba hata kukishika chakula ninashindwa.Sikumaliza kukila chakula kutokana na kutetemeka sana mwili wangu,

Masaa yakazidi kwenda pasipo kujua nini muafaka wangu wa kukaa ndani ya hili jumba.Nikaanza kukichunguza chumba sehemu yote na kugundua kimefungwa taa nyingi zenye ukubwa mbali mbali,nyengine zinaukubwa kama taa zinazo fungwa kwenye viwanja vya mpira ndio maana zina mwanga mkali sana.
Nikauchunguza mwili wangu na sehemu kubwa imeujeruhiwa.Nikiwa nimesimama nikastukia mlango ukifunguliwa,nikakaa kwa muda ila sikuona mtu akiingia ndani ya chumba.Taratibu nikaanza kupiga hatua za kwenda nje,nikachungulia wala sikumuona mtu wa aina yoyote.Nikapiga  hatu na kwenda nje kabisa na sikuona mtu wa aina yoyote katika eneo hili

Nikazidi kwenda mbele na yumba nzima inavyumba vingi sana,nikaendelea kuchunguza hadi nikafika sebleni.Nikachungulia dirishani na kumuona mzee godwin akiwa amesimama na watu wake wakilitazama gari linalo simama,baada ya gari kusimama wakashuka watu wawili walio valia mavazi meusi kish mmoja akafungua mlango wa nyuma akashuka manka akiwa na madam mery.Mzee godwin akamkumatia manka kwa furaha ila manka hakuonekana kuwa na furaha ya aina yoyote

“mama yangu mbona huna furaha?”
“baba kwa nini siku zote ulinificha?”
“nilikuficha na nini mwanangu?”
“baba kumbe eddy ni ndugu yangu.Umecha hadi nimefanya naye vitendo vya ajabu nikidhani ni mtu wa kaiwada kama wengine”
Maneno ya manka yakaibadilisha kabisa sura ya mzee godwin,akikunja kana kwamba amepigwa na mshale wa mgongo
“ina maana eddy amekubaka?”

“sio amenibaka,eddy alikuwa ni mpenzi wangu na hadi amenipatia ujauzito ila kwa bahati mbaya mimba ikatoka”
Mzee godwin akajishika kichwa na kuzunguka mara mbili huku akisunya misunyo mkali

“nitamuua eddy leo mbele yako”
Mzee godwin alizunguza na kuanza kupiga hatua za kuingilia kwenye mlango wa sebleni.Kabla sijafanya kitu chochote nikastukia nikishikwa kwa nyuma na kuzibwa mdomo
“shiii”

Ilikuwa ni sauti ya kike,mwanamke aliye nishika kwa nyuma akaanza kunivuta kwa nyuma huku tukielekea gizani.Tukatokea upande wa pili wa nyumba kwenye miti mingi,ndipo nikagundua mtu aliye nishika ni yule dada aliyekuwa ameniletea chakula

“kimbia kabla kifo hakija kukuta hapa”
Msichana alizungumza,huku akiwa amenitazama kwa macho makali,
“asante”
“amina ninaitwa”
“eddy”
“ninakujua,haya nenda”

Rais Mstaafu Jakaya Kikwete avutiwa na wimbo ‘Matatizo’ wa Harmonize

0
0

Wimbo ‘Matatizo’ wa msanii wa muziki Harmonize, ni moja kati ya nyimbo ambazo zinapendwa na Rais Mtaafu, Jakaya Mrisho Kikwete.

Wiki moja iliyopita Mh.Rais Mstaafu Jakaya Kikwete aliwaalika viongozi wa WCB pamoja na wasanii wake nyumbani kwake na kula nao chakula cha mchana.

“Unajua wakati Mh Jakaya Kikwete anatoka madarakani Diamond Platnumz bado alikuwa hajasaini wasanii wengine chini la WCB Wasafi, hivyo tulikwenda kuwatambulisha kina Harmonize, Raymond pamoja na Rich Mavoko pia na kukabidhi kazi zao, lakini uzuri wakati tunakabidhi kazi Mh Jakaya Kikwete alikuwa amevutiwa na wimbo wa Harmonize wa matatizo, akawa anasema alikuwa kwenye gari aliisikiliza kazi hiyo na kusema kuwa kijana ameimba sana,” Sallam alikimbia kipindi cha Enewz cha EATV.

Sallam alisema hatua ya kukutana na JK wanaimani itawasaidia kuwapa connection katika muziki wao.

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 7 & 8

0
0
Muandishi : Eddazaria g.Msulwa


Ilipoishia
Askari mmoja mwenye mwili mkubwa akamnyanyua Fetty na kumuweka begani mwake na safari ikaendelea.Fetty akayafumbua macho yake na kuona askari aliye mbebe ndio wa mwisho katika mstari wanao tembea,Kwa ustani wa hali ya juu Fetty akaichomeka mikono yeke katikati ya shingo ya askati,kwakutumia pigu akaanza kumnyonga askari huku akiwa amening'inia kwa nyuma.Mikoromo ya asakri ikawastua wenzake waliopo mbele kitendo cha wao kugeuka wakamkuta mwenzo ndio yupo kwenye hatua za mwisho huku macho yake akiwa ameyatoa njee

ENDELEA
Askari mmoja akataka kufyatua risasi ila mkuu wa masafara akamzuia,Fetty akaiachia shingo ya askari huku akiwa amehakikisha kwamba askari huyo yupo kwenye hali mbaya sana.Askari mmoja akampiga Fetty kwa kutumia kitako cha bunduki na kumfanya  Fetty ajikunje huku akitoa mguno mkali wa maumivu
“Kumbukeni kuwa,anahitajika akiwa hai”
Mkuu wao alizungumza

“Sawa mkuu,ila anahitaji kupata kibano kidogo”
Wakaendelea kumtazama mwenzo,ambaye hadi hapa alipo hali yake haipo vizuri sana.Vichwa vya askar vikaanza kupata moto kwani mwenzao ambaye alikuwa anakaribia kunyongwa ndio anaye fahamu njia ya bombo hilo japo imenyooka ila kuna sehemu mbele imegawanyika katika njia nne.Mwenzao anayejulikana kama inspector Julio hawezi kuendelea mbele na safari

“Mkuu kuna tatizo jengine limejitokea,Over”
“Nini tena inspector John? Over”
“Huyu binti alimkaba Inspector Julio,Over”
“Nyinyi mulikuwa wa hadi mwenzetu akabwe?”
Sauti ya mkuu wao ilizungumza huku akiwa anafoka,
“Mkuu alizimia,ndipo inspector Julio alipo amua kumbeba”
“Pumbavu zenu.Hakikisheni anatoka huyo binti,akiwa hai na Julio naye akiwa hai”

Fetty akatabasamu huku akiwatazama askari,kwani kwake kazi yake imeshaanza kuwa nyepesi kwani mtu ambaye anamuhofia ni huyu Inspector Julio,ambaye kwa mtazamo wake tu anaonekana ni mtu hatari sana katika swala zima la kutumia silaha.Askari mmoja akasimama mbele ya Fetty huku akiwa amempa mgongo akisaidiana na wezake katika kumpa huduma Inspector Julio,huku kazi yake ikiwa ni kuzifungua kamba za viatu vya Julio

Kwa umakini wa hali ya juu,Fetty akazichomoa funguo nyingi zinazo ning’inia kiunoni mwa askari huyo pasipo yeye mwenyewe kujua.Kwa bahati nzuri katika wingi wa funguo hizo zipatazo kumi na mbili,mbili ni funguo za pingu.

Macho ya Fetty yakawa na kazi ya kuwatazama askari jinsi wanavyo pata shida katika kumsaidi mwenzao ambaye hali yake inazidi kuwa mbaya.

Hakuna askari aliye kuwa na muda wa kumtazama Fetty kwani wanaamini kile kitako cha bunduki alicho pigwa kwenye tumbo,bado anaendelea kukisikilizia maumivu yake.Fetty akafanikiwa kufungua pingu za mikono pasipo askari yoyote kugundua.Akajaribisha kufungu mnyororo wa miguni ila akashindwa kwani hakuna funguo inayo ingiliana na kufuli alilo fungwa miguuni.

“Ja............ama..ani mmmim...i siwezi ku...pona.Ila,njia uki...oony......sha utaku...nja kulia...kwenye shimo lenye mlang....o wa....”
Inspector Julio alizungumza kwa shida na hakuweza kumalizia sentesi yake,mauti yakamchukua.

Inspector John akanyanyuka kwa hasira na kumfwata Fetty sehemu aliyo kaa.Kufumba na kufumbua akajikuta akirushwa juu kimo cha mbuzi  tena beberu na kutua chini kama mzigo.

Hii ni baada ya Fetty kuikutanisha miguu yake kwa pamoja,Kisha mikono yake aliikita chini na kujizungusha kwa kasi kubwa.Askari walio salia wakiwa wanamtizama mkuu wao.Fetty akajinyanyua kwa haraka na kumvaa askari aliye mchomolea funguo,akaichomoa bastola ya askari huyo ambaye alijitahii kumpiga ngumi  za mbavu Fetty

Bila ya huruma Fetty akafyatua risasi iliyo penya kwenye kichwa cha akari anayepambana naye na kumtuliza kimya.Askari watatu wa kiume wakazikoki kwa haraka bunduki zao na kuanza kuzifyatua risasi,ila kwa haraka sana kama tairi la gari liendalo kwa kasi sana,akawa na kazi ya kubiringika huku akiwafwata askari kwenye miguu yao mita chache kutoka alipo.

Akiwa anabiringika, bastola iliyopo mkononi mwake ikawa na kazi ya kufyatua risasi zilizo waangusha askari watatu chini na akabaki Inspector John na askari wa kike aliyetengenezwa kama yeye,na wakati wote tukio  la wezake kuangamizwa lilimpa kiwewe hadi akawa na kazi ya kuyaziba masikio yake akiziba asisikie milio ya risasi.Fetty akalala katikati ya miguu ya Inspector John huku mdomo bastola yake akiwa ameuweka kwenye sehemu za siri za Inspector John.Bunduki ya inspector John akawa ameilekezea kwenye kichwa cha Fetty ambaye macho yake yanatazamana na macho ya Inspector  John
“Shoot ni kushooti”
Fetty alizungumza huku akitabasama,na bastola yake akawa na kazi ya kuigusisha gusisha kwenye vitenesi vya Inspector John

Itizame hapa video mpya ya Diamond Platnumz ft. Rayvanny – Salome

0
0
Staa wa muziki nchini, Diamond Platnumz ameachia nyimbo ambayo amemshirikisha msanii mwenzake ambaye yupo katika lebo yake ya WCB Wasafi, Rayvanny ambayo ameipa jina la Salome. Video ameshoot, Nicorux kutoka Afrika Kusini Aprili, 10 mwaka huu, itizamehapa.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images