Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Hatuhusiki kumtafutia mtu ajira - Bodi ya Mikopo

$
0
0
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imesema kuwa haihusiki kumtafutia mnufaika wa mkopo ajira badala yake inahusika kumpatia mwanafunzi mkopo na akishamaliza muda wa masomo atatakiwa kurejesha mkopo wake.

Hayo yamesemwa jana Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Cosmas Mwaisobwa wakati akijibu maswali ya wananchi kupitia kipengele cha Kikaango cha EATV.

“Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatoa mikopo suala la kutafuta ajira halituhusu hivyo mnufaika yoyote asiwe na kigezo kwamba hajapata kazi , hiyo siyo kazi yetu, kazi yetu ni kuwawezesha kupata elimu basi” Alisema Mwaisobwa.

Aidha Mwaisobwa alisema wanufaika wote ambao walipata mikopo wanatakiwa kukatwa asilimia 8% ya pato la mwezi, na kama mtu anafanya kazi binafsi na hakatwi popote atatakiwa kutoa kiwango cha 120,000/= na kwa ambao wamenufaika na hawataki kuanza kulipa mkopo watapigwa penati ya 10% ya mkopo kwa mwaka.

Pamoja na hayo Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu imewataka walioomba mikopo kuvuta subira kwani Bodi inasubiri majina kutoka Tume ya Vyuo Vikuu ili Bodi ya Mikopo iweze kufahamu vyuo walivyopangiwa na kiwango cha ada ili haki iweze kutendeka kwa waombaji.

Gavana BOT afichua siri ya kilio cha fedha kupotea mtaani

$
0
0

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Profesa Benno Ndulu jana alitolea ufafanuzi hali ya kiuchumi nchini huku akieleza siri ya kilio kinachovuma cha fedha kupotea mtaani na nyingine zikidaiwa kufichwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Profesa Ndulu alisema kuwa kwakuwa taasisi hiyo ndiyo inayofahamu fedha zote zilizopo benki na zilizopo mtaani, inafahamu kuwa hakuna fedha iliyopotea bali fedha zimepotea kwa watu waliokuwa wanazipata kwa njia ya udanganyifu kwakuwa sasa Serikali imebana mianya hiyo.

“Hakuna fedha iliyopotea, Serikali imebana shughuli za watu na ‘mission town’ sasa shughuli zote zinafanywa na Serikali. Hivyo, kwao fedha zimepotea, lakini kwetu hazijapotea,” alisema Profesa Ndulu.

Hata hivyo, Profesa Ndulu alikiri kupungua kwa fedha katika mabenki nchini hali iliyopelekea kupunguza kasi ya utoaji mikopo kwa wananchi. Alisema hali hiyo ilitokana na kuhamishwa fedha za mashirika ya umma na taasisi kutoka benki za biashara kwenda BoT.

“Fedha hizo zitarudi katika benki hizo wakati zitakapopelekwa kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali,” Profesa Ndulu aliahidi.

Katika hatua nyingine, Gavana huyo wa Benki Kuu alisema kuwa uchumi unatarajiwa kukuwa kwa asilimia 7.2 mwaka huu, huku akibainisha kuwa moja kati ya sababu zinazopelekea ukuaji huo ni  ongezeko la uzalishaji wa umeme na saraju.

Akizungumzia hali ya deni la taifa, alisema kuwa deni la taifa la ndani limeongezeka kutoka shilingi  trilioni 8.6 Mwezi Desemba mwaka jana hadi shilingi trilioni 10 mwezi Juni mwaka huu.

Profesa Ndulu alibainisha kuwa wakati deni linalotokana na kukopa ndani likipaa, deni linatokana na ukopaji wa limepungua baada ya Serikali kupunguza ukopaji nje ya nchi.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 47 & 48 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...
Alizungumza kwa sauti ya ukali kidogo.Nikiwa ninavua kofia,mkuu wa shule ambaye tunawindana kama paka na panya naye akawa anaingia ndani ya ukumbi huku akiwa ameongozana na mkuu wa shule.Akabaki akinitazama kwa hasira na kuanza kupiga hatua za haraka kunifwa huku mikononi mwake akiwa amekunja ngumi

Endelea...
Nikaanza kurudi nyuma huku nikimtazama mkuu wa shule,akazidi kuja kwa kasi ikanilazimu kusimama nikimtazama kwa umakini.Wanafunzi wote wakawa na hamu ya kuangalia ni nini ambacho atakifanya mkuu wa shule.Hatua chache kabla hajanifikia nikaifunua tisheti yangu sehemu ya kiunoni na kumuonyesha bastola niliyo ichomeka kiunoni.Kidogo akapunguza kasi hadi ananifikia munkari wote ulimuishia.

“toka katika shule yangu”
Alizungumza huku meno yake ameyang’ata kwa hasira.Nikamtizama na macho makali na ukumbi mzima wa shule upo kimya hata kijiko kikianguka mlio wake utasikika vizuri.
“sitoki”

Wanafunzi wote wakashangilia,mkuu wa shule akawatizama wanafunzi na wakakaa kimya
“walinzi mupo wapi?”
Mkuu wa shule alizungumza kwa sauti kubwa,hapakuwa na mlinzi hata mmoja aliye nifwata kila mlinzi aliye niona kuwa ni mimi aliishia mlangoni na kusimama.Mmiliki wa shule akatufwata sehemu tulipo simama na mkuu wa shule
“jamani,kuweni wapole.Mkuu unaniambisha bwana”

Mkuu wa shule akajifanya kama hamsikii muajiri wake,kitu kinacho niumiza kichwa ni kwanini mkuu wa shule hadi leo yupo wakati amafanya mambo ya ajabu hadi muda huu hajachukuliwa hatua zozote.Akanisogea katibu yangu,nikastukia kibao kikali kikitua kwenye shavu langu.Nikataka kulipiza nikaisikia sauti ya john ikiniita jina langu na nilipo mtizama nikamkuta john akitingisha kichwa akiniashiria nisifanye chochote

Mkuu wa shule akanitandika kibao cha pili,ila john akawa na kazi moja ya kuniomba hadi machozi yakawa yanamwagika,nisilipize chochote kwa mkuu wa shule.Machozi ya hasira yakaanza kunimwagika,huku kifua changu kikianza kutanuka kwa hasira kali,akataka kunitandika kofi la tatu nikamdaka mkono wake.
“nitakuua”

Nilizungumza kwa sauti ya ukakamavu,huku macho yangu yakimtazama mkuu wa shule.Akajaribu kuuchomoa mkono wake kutoka kwenye mkono wangu ila akashindwa.John kwa haraka akaja na kuingia katikati yetu na kuniachanisha mkono wangu na mkuu wa shule na kunishika mkono na kuanza kunitoa nje
“eddy achana naye huyo mzee”
Machozi yakazidi kunimwagika,pasipo kuzungumza kitu cha aina yoyote

“john niachie,tafadhali”
“eddy siwezi kukuachia,nakujua.Tuliza kwanza hasira”
“john,yule mzee ananitafuta nini mimi?”
“mpotezee bwana,hajui atendalo”
“john,mama yangu hata siku moja hajawahi kunizalilisha mbele ya watu kwa kunipiga.Sembuse yeye kikaragosi”
“ndio,naelewa hilo eddy ila punguza jazba”

Tukaingia kwenye moja ya darasa lililopo chini ya ukumbi kwani ukumbi upo gorofani.John akanikalisha kwenye moja ya kiti na yeye akakaa mbele yangu juu ya meza.Moyo na mwili wangu vyote vikawa vinajisikia vibaya sana kwa kitendo cha kuzalilishwa.Kwani katika maisha yangu tangu nikiwa mtoto sikupenda mtu kunizalilisha wala kunionea.

Hata awe ni mkubwa vipi nilijitahidi kwa uwezo wangu wote kupambana naye hata akinipiga basi ipo siku nitamvizia hata kwa mawe nimpige,ndio maana hadi hapa nimekua bondia mzuri tuu.Nikaichomoa bastola yangu kwa haraka john akanibeta na kunipokonya
“eddy,unataka kufanya nini?”
“lete hiyo bastola”
“ahaa eddy sikupi”

John alikimbia nyuma ya darasa,huku bastola akiwa ameishika mkononi.Nikamtazama kwa macho makali sana yasiyo pepeseka hata kidogo.Kwa haraka nikatoka mlangoni na kumfungia john kwa nje.Nikakimbia na kuanza kupandisha ngazi za kuelekea kwenye ukumbi.Kitendo cha mguu wangu wa kwanza kukanyaga sakafu ya ukumbini nikatazama wapi alipo mkuu wa shule.

Nikamuona akiwa amekaa kwenye meza ya wageni waalikwa akiwa katikati ya waalimu wengine na mmiliki wa shule.Kwa kasi ya ajabu nikakimbia hadi alipo kaa na kujirusha na sote wawili tukaanguka na kiti,mbaya zaidi yeye akangukia mgongo na kunipa mimi nafasi nzuri ya kumkalia kwenye kifua chake na kuanza kumshambulia kwa ngumi zisizi na idadi kwenye uso wake

Kelele za wanafunzi kushangilia zikazidi kuongezaka,waalimu walio karibu yetu wakaanza kunivuta,kuniachanisha na mkuu wa shule.Wakanisimamisha na kunipeleka pembeni.Mkuu wa shule akasimaa huku akitaka kunifwata ila waalimu wezake wakanizuia.Ukumbi mzima wanafunzi kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita wakawa na kazi ya kunishangilia huku wakilitaja jina langu na kupiga makofi.

“eddy......Eddy........Eddy........Eddy”
Mkuu wa shule akawazidi nguvu,waalimu walio mshika na kuja kutuvaa na waalimu ambao wamenishika mimi.Sote tukaanguka chini,kabla mkuu wa shule hajafanya chochote nikamuwahi kumdaka  shingo na kumpiga kabali.Akaanza kunishindilia ngumi za mbavu,nikamuachia shingo yake na kumsukuma pembeni na kunyanyuka juu kidogo.Akanyanyuka kwa kasi na kunifwata,kabla hajanifikia nikaruka juu kwa kutumia mguu wangu wa kulia,nikautulisha kwenye kifua chake na kumuangusha chini.Waalimu wakaendelea kutushika,kelele za wanafunzi wezangu zikazidi kuongezeka.Hata ambao wawanijui vuzuri,nao pia wakawa katika mkombo wa kushangilia
“nitakuua wewe kijana”

Mkuu wa shule alizungumza huku akiwa ameshikwa na wezake kwa nguvu.Nikabaki nikitabasamu kwa dharau zaidi nikamnyooshea kidole cha kati kama tusi.Ndio nikawa nimemfungulia hasira zake zote.Akajibabadua mikononi mwa waalimu wengine na kunifwata.Nikasikia mwalimu mmoja aliye nishika akiwaambia wezeke
“hembu muachieni tuone atakacho kifanya,mzee mgomvi kama nini”

Watano kortini kwa kumdhalilisha Rais Magufuli

$
0
0
VIJANA watano wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumdhalilisha Rais Dk. John Magufuli na Jeshi la Polisi kutokana na mauaji ya askari polisi wanne waliouawa na majambazi katika eneo la Mbande na Vikindu, Dar es Salaam hivi karibuni.

Washtakiwa hao walifikishwa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam mbele ya mahakimu watano tofauti na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Salum Mohammed.

Walisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Emmilius Mchauru, Huruma Shahidi, Margareth Bankika, Dk. Yohana Yongolo na Respicius Mwijage.

Akisomewa mashtaka, mshtakiwa Dennis Mtegwa anadaiwa Agosti 24, mwaka huu eneo la Ubungo External kupitia mtandao wa WhatsApp, aliweka maoni katika group linaloitwa Dsm 11 4u Movement, akisema ‘JPM sijui anawaza nini kichwani… hata samahani hajui au nilikosea hajui’, ‘nchi imefika hapa kwa sababu ya mtu mmoja aliyeamua kujilipua ufahamu wake’, ‘sijaona tatizo kwa hilo, ila kwa huyu bwana misimamo ambaye amesema msinijaribu na ilhali kajaribiwa na ubwabwa wa jubilee kusema yote’.

‘Siasa si chuki wala upinzani si uadui, ajifunze kushindana kwa hoja sio mitutu ya bunduki na mazoezi yasiyo na kichwa wala miguu ya polisi’.

Mshtakiwa Suleiman Saidi anadaiwa Agosti 25, mwaka huu maeneo ya Kigogo, kwa kutumia mtandao wa Facebook, aliandika ‘Safi sana aisee, mi naona wangekufa kama 20 hivi halafu Simon Sirro tumuulize mazoezi wanafanyia wake zao au’.

Katika kesi nyingine, mshtakiwa Juma Mtatuu akiwa eneo la Ocean Road, Agosti 24, mwaka huu anadaiwa kuwa alituma ujumbe katika Facebook akisema ‘Huyu hata akifa ataenda peponi, na kufanya mazoezi kote kule wamekufa Mbagala, mimi nitakuwa wa kwanza kuandamana  kule Kahama, tarehe moja naelekea Kahama kwa Ukuta, mimi nitakuwa namba moja kushika bendera ya Ukuta, kifo kipo tuu, usiogope kwani mawe na mapanga yameisha’

Rais Magufuli ateua Mwenyekiti wa Bodi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ndege ATCL

$
0
0


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  tarehe 15 Septemba, 2016 amemteua Mhandisi Emmanuel Korosso kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, imeeleza kuwa uteuzi wa Mhandisi Emmanuel Korosso unaanza mara moja.

Mhandisi Emmanuel Korosso anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Salim Msoma ambaye alimaliza muda wake.

Wakati huo huo, Rais Magufuli amemteua Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL).

Kabla ya uteuzi huu Mhandisi Ladislaus Ernest Matindi alikuwa Mkurugenzi katika Shirika linaloshughulikia masuala ya usafiri wa anga Barani Afrika (EGNOS-Africa Joint Programme Office) lenye makao yake nchini Senegal.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

15 Septemba, 2016

Serikali Yakataa Kuongeza fedha za kujikimu kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Wanaopatiwa mikopo

$
0
0
Serikali imekataa kuongeza fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa elimu ya juu wanaopatiwa mikopo na Serikali kutoka Sh8,500 hadi kufikia Sh10,000 kwa siku.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya amelieleza Bunge kuwa kiwango hicho kitaendelea hadi utakapofanyika utafiti baada ya miaka miwili.

Manyanya alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,  Zainabu Katimba (CCM), aliyetaka kujua kama Serikali itakuwa tayari kuongeza fedha kwa wanafunzi hadi kufikia Sh 10,000 kwa madai gharama za maisha zimepanda.

Amesema bodi ya mikopo ilifanya ongezeko la fedha za kujikimu kwa wanafunzi wa vyuo vikuu kwa Sh1,000 kutoka Sh7,500 hadi kufikia 8,500 katika mwaka 2015/16.

“Ongezeko hilo haliendani na kasi ya mfumuko wa bei uliorekodiwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kutoka asilimia 4.2 Februari 2015 hadi kufikia asilimia 5.6 Februari 2016,” amesema Katimba.

Naibu waziri amesema Serikali imekuwa ikifanya utafiti wa gharama halisi za maisha kwa wanafunzi ambazo hujumuisha malazi na chakula.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2014/15 Serikali kupitia bodi hiyo ilifanya utafiti katika vyuo vyote nchini ili kujua gharama halisi za chakula na malazi na kuonyesha kuwa gharama halisi ilikuwa ni kati ya Sh8,000 hadi 8,500.

Naibu waziri amesema wizara itafanya utafiti mwingine ili kubaini gharama halisi za chakula na malazi kwa wanafunzi hao na matokeo yake yatatumika kupanga viwango vya fedha zitazolipwa kwa wanafunzi.

UTAFITI: Asilimia 96 ya watanzania wamkubali Rais Magufuli

$
0
0

Asilimia 96 ya watanania wanamkubali Rais Magufuli, na asilimia 88 ya wananchi Tanzania wameonesha imani ya kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo katika uwajibikaji.

Wananchi hao pia wamevutiwa na uondoaji wa wafanyakazi hewa, utoaji wa elimu bure pamoja na usimamishaji watumishi wa serikali kwa makosa mbalimbali.

Takwimu zilizotolewa kwa vyombo vya habari na shirika la TWAWEZA jana  jijini Dar es salaam kupitia kwa mkurugenzi mtendaji wa wa shirika hilo Aidan Eyakuze, zimebainisha kuwa asilimia 69 ya watanzania wamefurahishwa na uondoaji wa wafanyakazi hewa uliotajwa, asilimia 67 wamefurahishwa na elimu bure huku asilimia 61 wakipendezwa na utumbuaji majipu.

“Kwa ujumla kiwango cha kukubalika kwa Rais Magufuli anakubalika na asilimia 96 ya wananchi. Kiwango hiki kinaendana na viwango vya kukubalika kwa marais wa Tanzania waliopita. Pamoja na hayo, asilimia 88 ya wananchi wana imani kuwa Rais Magufuli ataendelea na kasi aliyoanza nayo, mpaka mwisho wa awamu yake ya uongozi”

Aidha wananchi pia wameonesha viwango vya kukubalika kwa viongozi wao wa kijiji na serikali za mitaa ambapo wenyeviti na watendaji wa vijini wanakubalika kwa asilimia 78, diwani kwa asilimia 74 na mbunge kwa asilimia 68.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye utafiti uitwao "Rais wa Watu. Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano". 

Muhtasari huo umetokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, ambapo wahojiwa 1,813 kutoka maeneo yote Tanzania Bara kati ya tarehe 4 Juni na tarehe 20 Juni 2016 walihojiwa.

Aidha Wananchi wengi wanasema serikali ya awamu ya tano imeleta maboresho kwenye huduma nyingi za umma, huku Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiongoza kwa asilimia 85 .

Wananchi pia wamesema huduma ni nzuri mashuleni kwa asilimia 75, vituo vya polisi kwa asilimia 74, mahakamani kwa asilimia 73, vituo vya afya asilimia 72 na mamlaka za maji asilimia 67.

Pamoja na kiwango kikubwa cha kukubalika kwa serikali ya awamu ya tano na Rais John Pombe Magufuli, wananchi wapo makini na kanuni za demokrasia na haki na wanataka zifuatwe.

Wananchi nane kati ya kumi (au 80%) wanasema watendaji wa umma waondolewe pale tu panapokuwepo udhibitisho wa vitendo viovu.

Asilimia 75 wanasema kuwa watendaji waondolewe pale wanaposhindwa kufanya kazi zao na siyo wanaposhindwa kufuata maagizo ya Rais.

Revised Decision On Minimum Admission Entry Qualifications For Undergraduate Students

$
0
0

RE: REVISED DECISION ON MINIMUM ADMISSION ENTRY QUALIFICATIONS FOR UNDERGRADUATE STUDENTS

The Tanzania Commission for Universities (TCU) through the earlier public notice issued on 11th July, 2016 notified the General Public and all Prospective applicants for admission into various undergraduate degree programmes of the Government’s decision to change the Procedures, Requirements and Minimum Admission Entry Qualifications for Undergraduate Students for all categories of applicants.

According to that notice, the Minimum Admission Entry Qualifications for applicants with Ordinary Diploma (NTA Level 6) qualifications is at least four O’-Level passes (Ds and above) or NVA Level III with less than four O’-Level passes or equivalent foreign qualifications as established by either NECTA or VETA; AND at least a GPA of 3.5. Whereas the Minimum Admission Entry Qualifications for applicants with Full Technician Certificate (FTC) qualifications is at least four O’-Level passes (Ds and above) or NVA Level III with less than four O’-Level passes or equivalent foreign qualifications as established by either NECTA or VETA; AND Average of B.

By this notice, the General Public and all applicants with Ordinary Diploma and Full Technician Certificate (FTC) qualifications are hereby informed that the earlier decision on the Minimum Admission Entry Qualifications for applicants is hereby revised from GPA of 3.5 to 3.0 for holders of Ordinary Diploma (NTA Level 6) and for FTC holders from an average of “B” to “C”.

In this context, TCU informs all applicants with Ordinary Diploma qualifications with at least a GPA of 3.0 and holders of Full Technician Certificate (FTC) with an average score of at least “C” that, they are now eligible to apply for admission into various undergraduate degree programmes through the Central Admission System (CAS).

Please note the following instructions:

   1. Applicants who had previously applied through the National Council for Technical Education (NACTE) and who meet the revised Minimum Admission Entry Qualifications stated herein are not required to re-apply.

  2.  Applicants who were yet to apply and who meet the revised Minimum Admission Entry Qualifications stated herein are required to apply upon payment of the prescribed admission fee through the prescribed procedures spelt out in the Admissions Guidebook. The new applicants are strongly advised to carefully read the Admissions Guidebook for Holders of Ordinary Diploma or Equivalent Qualifications only.

  3.  The deadline for applications is 23rd September, 2016.

For further information or clarification please contact the Tanzania Commission for Universities through the following:


Phone:+255 (0) 22 2772657
 Hotlines:    +255(0) 683 921 928
                  +255 (0) 675 077 673 

Fax: +255 (0) 22 277289 
Email: es@tcu.go.tz


Issued by
The Executive Secretary
Tanzania Commission for Universities 
15th September, 2016

Wabunge wote wa CUF Wamkataa Profesa Ibrahim Lipumba

$
0
0

Wabunge wote wa Chama cha Wananchi (CUF) wametangaza rasmi kutomtambua aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba.

Wamemtaka Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi kutomkumbatia mwanasiasa huyo aliyebobea katika uchumi, ikielezwa kwa sasa hana sifa za kuwa mwenyekiti wa chama hicho, labda aanze upya mchakato.

Wameeleza msimamo huo jana mjini Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu, Riziki Mngwali ambaye pia ni Kiongozi wa Wabunge wa CUF katika mkutano baina ya waandishi wa habari za Bunge na wabunge wa CUF isipokuwa Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Magdalena Sakaya aliyesimamishwa uanachama, ingawa anaendelea kutimiza majukumu yake bungeni.

Mngwali alisema Profesa Lipumba amekuwa akijaribu kukiyumbisha chama na hivi karibuni kudai amekaririwa akisema anasubiri barua ya Msajili wa Vyama vya Siasa ya kuthibitishiwa kuendelea na uenyekiti wake.

“Wakati anajiuzulu uenyekiti Agosti 5, mwaka jana aliutangazia umma na kudai anakwenda Rwanda kwa kazi aliyodai ya utafiti ili aje kuisaidia serikali, lakini inashangaza sasa anataka kujirejeshea uenyekiti. Hilo hatukubali kwa kuwa chama kina taratibu zake,” alisema.

Aliongeza kuwa, alikiacha chama katika wakati mgumu kuelekea Uchaguzi Mkuu, lakini kikaimarika zaidi kwa kupata wabunge 43, madiwani 287, kuongoza manispaa mbili na halmashauri za wilaya tatu, hivyo wanashangazwa kuona akitaka kurejea, tena kwa kutumia nguvu.

“Tunataka ifahamike kwa dhati kuwa, sisi wabunge, hatumtambui tena Profesa Lipumba kama Mwenyekiti wa CUF,” alisema Mngwali na kumtaka Msajili kutomuidhinisha Lipumba, kitendo alichodai kitachochea mgogoro ndani ya chama.

Aliongeza kuwa badala ya kutumia mabavu kutaka kurejea madarakani, ni vyema akabaki na heshima yake, kwani amekitendea mambo mengi chama hicho na kwamba wanamheshimu, hivyo afuate taratibu za kichama kutaka kuwania tena uenyekiti.

Mngwali alisema wamekubaliana na uamuzi wa Baraza Kuu la Uongozi wa CUF wa kuwasimamisha uanachama Lipumba na wenzake tangu Agosti 28, 2016 kutokana na kile kinachodaiwa kukiuka Katiba ya chama hicho. 

Miongoni mwa tuhuma zao ni kusababisha vurugu wakati wa Mkutano Mkuu Maalumu wa Uchaguzi Agosti 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam uliokuwa unalenga kumthibitisha Juma Duni Haji kuwa Mwenyekiti mpya.

Hata hivyo, kutokana na vurugu zilizoibuka, mkutano huo ulivunjika. Mbali ya Lipumba na Sakaya, wengine waliositishiwa uanachama ni Abdul Kambaya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Ashura Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.

Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa wabunge kipindi cha 2010/2015, Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na Kombo Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

Kutokana na kusimamishwa kwa viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alimtangaza Julius Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara kuwa kiongozi wa Kamati ya Uongozi wa muda inayowajumuisha pia wabunge Katani Ahmed Katani na Savelina Mwijage ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Augustino Lyatonga Mrema na Mama Lwakatare Waunganisha Nguvu Kuwatoa Wafungwa Magerezani

$
0
0
Kukosekana kwa fedha ya kukamilisha mchakato wa sheria ya Parole kwa wafungwa mbalimbali nchini waliomaliza nusu ya kifungo chao gerezani ni miongoni mwa sababu yakuwepo mrundakano wa wafungwa katika magereza Tanzania.

Akiongea na waandishi wa habari hii jana jijini Dar es salaam wakati akimpongeza na kisha kumteua Mchungaji Dkt. Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa harambee ya kuchangisha fedha kwaajili ya kuwalipia wafungwa wanaotakiwa kutoka gerezani chini ya sheria ya Parole, Mwenyekiti wa bodi ya Parole Taifa Augustino Lyatonga Mrema alisema ili mfungwa atolewe gerezani ni lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu.

“Ni lazima maofisa wa parole wafuatilie nakala ya hukumu kwenye mahakama iliyomukuhumu na waende kuonana na uongozi wa kijiji au mtaa ambapo mfungwa atenda kuishi anapotoka gerezani ikiwa ni pamoja na kuonana na familia yake na pia kuonana na watu waliowakosea ili jamii ya eneo hilo itambue kuwa ataachiwa huru” alisema

Aidha, Mrema aliwataka maofisa wa parole kote nchini kuwatembelea wafungwa waliopata Parole ili wafungwa wengi wenye sifa za kutolewa kwa sheria ya Parole wasiendelee kuteseka magerezani bali waende kuungana na familia zao sambamba na kuongeza nguvu kazi.

Kutokana na kutotengwa fedha kwaajili ya kushugulikia suala hilo, Mwenyekiti huyo wa Parole Taifa, amemteua Mama Getrude Lwakatare kuwa mratibu wa kuchangisha fedha kwa kushirikisha viongozi wote wa dini nchini kushiriki harambee kwaajili ya kuchangisha fedha za kuwatoa wafungwa magerezani na kupunguza msongamano katika magereza nchini.

“Napendekeza kufanyike harambee kwenye makanisa yote nchini, siku ya Jumapili moja ili sadaka zote zikatumike kuwalipia faini wafungwa waliopo magerezani” alisema

Mrema alisisitiza kuwa wanaolengwa na Parole siyo wanye makosa ya ubakaji, mauaji, wizi kwa kutumia silaha na makosa mengine.

Naye Mchungaji Dkt. Getrude Lwakatare aliwataka watanzania kuangalia taifa kwanza kwani kina baba wengi wenye nguvu watarudi katika jamii na kusaidia katika uzalishaji mali sambamba na kutatua matatizo ya kiuchumi na kimaendeleo katika familia zao.

“Tutaunganisha familia zilizo sambaratika na kutaabika baada ya mzazi mmoja kufungwa miaka 6 pengine kwa kukosa faini ya milioni moja tuu, tutaondoa msongamano wa wafungwa na kulinda afya zao kutokana na magonjwa wanayopata wakiwa gerezani” alisema

Mchungaji Gutrude Lwakatare alisema anaunga mkono jitihada za bodi ya Parole Taifa na siyo kuwalinda waalifu kama ambavyo wengine watatafsiri kwani kurejesha familia ni miongoni mwa kustawisha jamii huku akinukuu maneno ya kidini yanayolenga kuwakomboa walioko kwenye vifungo na taabu mbalimbali ndani ya jamii.

Wasanii na viongozi wa WCB waalikwa nyumbani kwa rais mtaafu Jakaya Kikwete

$
0
0

Jumatano ya Sept 14, 2016 Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete aliwaalika wasanii na viongozi kutoka kwenye lebel ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz nyumbani kwake kula chakula cha mchana na kuzungumza kuhusu kazi za muziki na maisha.
Rais mstaafu JK, mwimbaji Harmonize na mama Salma Kikwete
Rich Mavoko na Rais mstaafu JK
Diamond Platnumz na JK
Rayvanny na JK

Meneja Sallam SK kwenye picha ya pamoja

Kauli ya serikali kuhusu Wanaohusika na mauaji ya wakulima na wafugaji

$
0
0

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Lameck Nchemba amesema hakuna shamba lenye thamani ya maisha ya binadamu na kuwataka wakulima na wafugaji kutatua migogoro yao kwa kufuata sheria na kuacha kujichukulia sheria mkononi.

Mwigulu ameyasema hayo Bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Mikumi kupitia (CHADEMA) Joseph Haule aliyetaka kujua hatua za serikali katika kudhibiti mauaji ya wakulima na wafugaji yanayotokea mara kwa mara katika jimbo lake na maeneo mengine nchini.

Katika swali lake Mbunge Haule ametaja baadhi ya mifano ya mauaji katika jimbo lake hususani eneo la Tindiga ambapo mauaji yamekuwa yakifanyika mara kwa mara huku serikali ikitoa matamko ambayo hayajazaa matunda.

Waziri Mwigulu Nchemba amesema katika kijiji ambacho mauaji yatafanyika jeshi la polisi litakamata vijana wote wenye nguvu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria ili wahusika waweze kubainika.

“Naliagiza Jeshi la Polisi kuwakamata vijana wote wenye nguvu katika kijiji ambacho mauaji yatafanyika ili wahusika wapatikane na kama magereza zikijaa vibaka walioiba vitu vidogovidogo waachiwe ili hao ambao wamesababisha mauaji wawekwe humo hatuwezi kufananisha maisha ya binadamu na mifugo au shamba” Alisema Waziri Mwingulu.

Awali katika swali hilo Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Dkt. William Ole Nasha aliwataka wafugaji na wakulima kuepuka kutumia hasira ambazo zinapelekea kugharimu maisha ya watu kwani serikali haitasita kuwachukulia hatua kali za kisheria.

UVCCM Arusha kwazidi kuwaka moto

$
0
0

Jeshi la Polisi mkoani Arusha jana asubuhi  lilituliza vurugu za viongozi na wanachama wa Jumuiya ya Vijana ya CCM (UVCCM) mkoani hapa, waliokuwa wakigombea ofisi. 

Vurugu hizo ziliibuka hadharani jana baada ya kuwapo taarifa za mgogoro wa chini kwa chini uliodumu kwa kwa miezi miwili, kati ya makundi mawili yanayokinzana kiuongozi. 

Mgogoro huo ulielezwa kukolezwa na uhamisho wa Katibu wa UVCCM Mkoa, Ezekiel Mollel kwenda makao makuu, huku katibu mpya aliyepelekwa kuchukua nafasi hiyo akikwama kukabidhiwa kwa siku tatu sasa. 

Katibu huyo mpya Saidi Goha, jana alitaka kuingia ofisini lakini alikumbana na kigingi cha kundi linalomuunga mkono Mollel lililofunga mlango kwa mnyororo. Kutokana na vurugu za jana, polisi wanamshikilia mwenyekiti wa miradi ya jumuiya hiyo, Phillemon Ammo pamoja  na  Mollel

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo alisema: “Ni kweli tumemkamata lakini nina ugeni wa Serikali (wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan), naomba nitoe taarifa baadaye,” alisema Mkumbo. 

Lengai Ole Sabaya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha,  alisema anapinga na kulaani kitendo cha baadhi ya wanachama wa umoja huo kufunga ofisi hizo kinyume na taratibu. 

Mollel anadai  uhamisho wake ni njama za kupoteza ushahidi wa baadhi ya tuhuma za ufisadi na matumizi mabaya ya fedha kwenye jumuiya hiyo, hivyo hatokwenda popote.

Anasema yeye anatekeleza maagizo ya kamati ya utekelezaji ya kusimamia mali za chama, kwani katika kipindi cha miezi miwili ameokoa zaidi ya Sh30 milioni ambazo zilikuwa zinaingia mifukoni mwa watu wachache.

“Tuna maduka hapa, waliopangishwa wanalipa zaidi ya Sh300,000 lakini chama kinapata chini ya Sh50,000 kwa duka kama kodi ya mwezi sasa tumetaka wenye maduka kulipa moja kwa moja UVCCM na siyo kwa watu wa kati na hapa ndipo chanzo cha mgogoro,” alisema. 

Kutokana na vurugu hizo zilizoibuka jana asubuhi,  Sekretarieti ya UVCCM imeamua kumsimamisha kazi bwana  Ezekiel Mollel. 

Kaimu Katibu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alitangaza uamuzi huo jana jioni muda mfupi baada ya Mollel  kukabidhi ofisi kwa katibu mpya wa UVCCM mkoa, Saidi Goha ambaye amehamishiwa Arusha akitokea Lindi, akiwa chini ya ulinzi wa polisi. 

Baada ya makabidhiano hayo polisi walimrejesha kituo kikuu cha polisi anakoshikiliwa. Shaka alisema, Mollel aliandikiwa barua ya uhamisho kwenda makao makuu tangu Agosti 25, na alitakiwa kukabidhi ofisi ndani ya siku 14 lakini aligoma. 

Alisema Mollel amekiuka kanuni za utumishi za UVCCM, hivyo Baraza Kuu na Kamati ya Utekelezaji Taifa watatoa uamuzi zaidi kwa mujibu wa kanuni kwa kuwa ukomo wa sekretarieti ni kumsimamisha. 

Hata hivyo, Mollel akizungumza akiwa chini ya ulinzi, alisema makabidhiano hayo ni batili kwa kuwa hakuyasaini.

Hukumu Rufani ya Mauaji Inayowakabili Abdallah Zombe na Wenzake Kutolewa Leo

$
0
0

Baada ya kimya kirefu, Mahakama ya Rufani leo inatarajia kutoa uamuzi wa rufaa ya aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi Abdallah Zombe na maofisa wenzake watatu. 

Hukumu hiyo itahitimisha mvutano wa muda mrefu wa kisheria kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na maofisa hao. 

Wajibu rufani wengine ni Mrakibu wa Polisi (SP) Christopher Bageni, aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi Wilaya ya Kinondoni (OC-CID); aliyekuwa Mkuu wa Upelelezi wa Kituo cha Polisi Urafiki, Mrakibu Msaidizi wa Polisi (ASP) Ahmed Makelle na Rajabu Bakari. 

Habari  kutoka mahakamani hapo  zilizothibitishwa  na Msajili wa Mahakamahiyo, John Kahyoza hukumu inatarajiwa kusomwa leo saa sita mchana. 

Hukumu hiyo ambayo imekuwa ikisubiriwa na wadau, wakiwamo ndugu wa marehemu hao, wanasheria na jamii kwa jumla inatolewa leo baada ya miezi minne, majuma mawili na siku mbili, tangu rufaa iliposikilizwa. 

DPP alikata rufaa akipinga hukumu ya Mahakama Kuu iliyowaachia huru Zombe na wenzake wanane katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara wawili wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teksi, mkazi wa Dar es Salaam.

Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake walidaiwa kuwaua kwa kukusudia wafanyabiashara Sabinus Chigumbi, maarufu Jongo na ndugu yake, Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na Juma Ndugu, aliyekuwa dereva wa teksi wa Manzese. 

Walidaiwa kutenda makosa hayo Januari 14, mwaka 2006, katika msitu wa Pande, uliopo wilayani Kinondoni baada ya kuwakamata wafanyabiashara hao Sinza, walipokuja Dar es Salaam kuuza madini. 

Agosti 17, 2009, Mahakama Kuu iliwaachia huru washtakiwa hao ikisema baada ya kusikiliza ushahidi na hoja za mawakili wa pande zote iliridhika kuwa hawakuwa na hatia ya mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili. 

Badala ya kosa la mauaji ambalo adhabu yake ni kunyongwa hadi kufaa, DPP aliiomba Mahakama imtie hatiani Zombe kwa kosa la kuwalinda wahalifu (wanaodaiwa kutenda kosa la mauaji hayo), ambalo adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka saba jela.

Wakili wa Serikali Mkuu (PSA), Timon Vitalis alidai DPP alifikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa hakuna ushahidi wa kumtia hatiani Zombe kwa kosa la mauaji. 


Kabla ya kubadili msimamo huo dhidi ya Zombe, DPP aliwafutia rufaa wajibu rufani watano, Jane Andrew, Emmanuel Mabula, Michael Shonza, Abineth Salo na Festus Gwabisabi.

Kijana Anyofolewa Ulimi na Mwanamke Wakati Wakipigana Denda

$
0
0

Mkazi wa Mandewa, Manispaa ya Singida, Said Mamba (24), amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida baada ya kung’atwa theluthi tatu ya ulimi wake na mwanamke waliyekuwa wakinyonyana ndimi. 

Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, saa 3:30 usiku wa sikukuu ya Idd el Hajj. 

Mamba, ambaye hawezi kuzungumza ametoa maelezo ya tukio hilo kwa njia ya maandishi. 

Alisema siku ya tukio alikutana na mwanamke huyo kwenye grosari iliyopo eneo la Mandewa na baadaye mwanamama huyo alimwomba amsindikize nyumbani kwake. 

“Nilikubali kumsindikiza, tukiwa njiani aliniomba tufanye mapenzi. Nilipokataa alinilazimisha na baada ya kuona sitaki aliomba tuagane kwa kunyonyana ndimi, nilikubali ombi hilo,” alisema. 

Mamba alisema wakati wakiendelea, mwanamke huyo alianza kumvua mkanda wa suruali lakini alimzuia ndipo alipomng’ata ulimi na kuondoka na kipande. 

Mzazi wa Mamba, Fatuma Alli alisema alipata taarifa ya tukio hilo baada ya siku tatu na kwamba, siku hiyo hiyo mume wa mwanamke aliyetenda kitendo hicho alikwenda kwake akieleza kijana huyo alijaribu kumbaka mkewe. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Peter Kakamba, alisema hana taarifa za tukio hilo. 

Daktari wa meno wa hospitali hiyo, Dk Hamisi Kakandilo alisema ulimi wa kijana huyo hauwezi kutibika isipokuwa kuusafisha ili asipate maambukizi. 

“Hata kama kipande kilichotolewa kingepatikana kisingeweza kushonwa,” alisema.

Madereva kutoka Tanzania watekwa nchini DRC.

$
0
0


Serikali imepokea taarifa za kutekwa kwa malori 12 katika eneo la Namoyo Jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, jana tarehe 14 Septemba 2016. Kati ya malori hayo nane yanamilikiwa na mfanyabiashara wa Kitanzania, Bw. Azim Dewji na mengine yanamilikiwa na wafanyabiashara kutoka Kenya.

Kwa taarifa zilizopatikana watekaji ni kikundi cha waasi cha MaiMai ambao baada ya kuyateka magari hayo, waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Bw. Dewji. Waasi hao wametoa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia. 


Wametishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha wanachokitaka itakapofika saa 10 jioni leo. Katika tukio hilo, madereva wawili wa Kitanzania wamefanikiwa kutoroka ambao ndio waliosaidia kutoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo.

Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imeshachukua hatua za awali za kuwasiliana na Serikali ya DRC ili kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa haraka iwezekanavyo wakiwa salama kabisa.

Tukio hili ni la pili kutokea katika miaka ya hivi karibuni ambapo mwaka 2015 Mashekhe kutoka Tanzania walitekwa nchini DRC lakini kwa ushirikiano wa Serikali hizi mbili zilifanikisha mashekhe hao kuachiwa huru bila madhara yoyote.

Serikali ingependa kuushauri Umma wa Watanzania hususan wafanyabiashara kuomba taarifa ya hali ya usalama kwa maeneo yenye matatizo ya kiusalama kama Mashariki ya Congo hususan Kivu ya Kusini kabla ya kusafiri kwenda maeneo hayo.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

Dar es Salaam, 15 Septemba 2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 16

Update: Watanzania Wenzetu Waliokuwa Wametekwa huko DRC Congo Wameokolewa

$
0
0
Madereva wa malori kutoka Tanzania waliokuwa wametekwa katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hatimaye wameokolewa na vikosi vya jeshi la nchi hiyo.

Waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo amezungumza na shirika la utangazaji la BBC na kusema wote wameokolewa   na wako salama

Taarifa iliyotolewa jana  na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ilieleza kuwa watekaji hao ni kikundi cha waasi cha MaiMai ambao baada ya kuyateka magari 8 toka Tanzania , waliwashusha madereva na kuwapeleka porini na kisha kuteketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Bw. Dewji. 

Waasi hao walioa saa 24 kuanzia jana saa 10 jioni walipwe fedha kiasi cha Dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia.

Teketeke : Dawa Asilia Ya Kulainisha Ngozi Ya Makalio.

$
0
0
Kuwa   na  makalio  magumu  ama  yaliyo kakamaa  ni  jambo  linalo  wakabili  wanawake  wengi  duniani.

Miongoni  mwao  wapo  wanawake  wanao kabiliwa  na tatizo la  kuwa  na  chunusi, mabaka, michirizi, madoa  na  vipele  kwenye  sehemu  za  makalio.

Hata  hivyo  unaweza  kumaliza  tatizo  hili  kwa  kutumia  dawa   asilia  iitwayo  Teketeke.

Dawa  hii  hufanya  kazi  zifuatazo :

i. Hulainisha  ngozi  ya  kwenye  makalio  na  kuifanya  kuwa  laini  sana

ii.Huondoa  chunusi  na  vipele  vya kwenye makalio

iii. Huondoa mabaka , madoa na michirizi  ya  kwenye  makalio.

iv.Hutumika  pia  kulainisha  ngozi  ya  kwenye  sehemu nyinginezo  za  mwili  kama vile  Hips, mapaja, miguu  nakadhalika.

Vile  vile, tunazo  dawa  mbalimbali  za  asili  kama  vile :

1.   Dawa  asilia  ya  kurefusha  nywele, kuzuia  kukatika kwa  nywele  na  kuzifanya   kuwa  nyeusi na zenye  afya.

2.   Dawa  asilia  ya  kuondoa  harufu  mbaya  ya  kinywa

3.   Dawa  asilia  ya kuondoa  harufu  mbaya  ya  kwenye  kikwapa

4.   Dawa  asilia ya  kutibu  tatizo  la  fangasi  za  ukeni

5.   Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  kutokwa  na  harufu  mbaya  ukeni

6.   Dawa  asilia  ya  kutibu  tatizo  la  fangasi  za  kwenye  miguu

7.   Dawa  asilia  ya kutibu  tatizo  la  chunusi  na  vipele  usoni.

8.   Pamoja  na  dawa  nyingine  nyingi.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM,  jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jen go  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa  wateja  wa jijini  Dar  Es  Salaam, wasio weza  kufika  ofisini  kwetu, tunayo  huduma  ya  kuwapelekea  dawa  mahali  popote  walipo  jijini  Dar  Es  Salaam  ( Home & Office Delivery )

Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  magari.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  boti.

Kwa wateja  wetu  wa  Mombasa, watasafirishiwa  dawa  kwa   bus  la  TAHMEED.

Kwa  wateja  waliopo  NAIROBI, watasafirishiwa  dawa  kwa  bus   la  DAR  EXPRESS

Na  kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI, watasafirishiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

TUNAPATIKANA  KWA  SIMU  NAMBA  0766  53 83 84.

Kwa  taarifa  zaidi kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku   kwenye  blogu yetu:

Tecno Phantom 6 Inaweza Kuwa Simu Nyembamba Kuliko Zote....Wamewezaje?? Bofya Hapa

$
0
0
UNAFIKIRI TECNO MPYA INAYOTARAJIWA KUTOKA HIVI KARIBUNI INAWEZA KUWA SIMU NYEMBAMBA KUSHINDA ZOTE?
 
Mwezi wa 9 (Septemba) ukiwa ukingoni kuelekea mwezi wa 10 (Oktoba) hali imekuwa ikipamba moto huku TECNO Phantom mpya ikiwa mbioni kuzinduliwa.
 
Wakati tangazo rasmi likitarajiwa kutolewa mwezi Septemba mwaka huu (2016), yote yamebaki kuwa fununu tu kama ushahidi ikifananishwa sawa na kupigilia msumari kichwani. Swali lililobaki ni, TECNO Phantom 6 au 6+ itabaki kuwa smartphone nyembamba kushinda zote? 
Tukiwa bado hatuna picha kamili juu ya muonekano wake halisi, makisio yamebaki kuwa ya kubahatisha tu. Binafsi, nasubiri kwa hamu uzinduzi rasmi wa toleo hili. Kwa fununu na uvumi unaosambaa kuna uwezekano Tecno Phantom 6 ikawa ndio smartphone nyembamba kutengenezwa?

Kama fununu hizi ni za kweli, swali linabaki kuwa, ni vipi wameweza kufanya hivyo?
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images