Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Rais Museveni Wa Uganda Awasili Dar Es Salaam Tayari Kwa Mkutano Wa Viongozi Wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki

$
0
0
Mwenyekiti wa Jumuya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akitambulisha wasaidizi wake kwa Mgeni wake, Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni, alipowasili Ikulu Dar es salaam leo jioni Septemba 7, 2017   tayari kwa mkutano wa Viongozi wa jumuiya hiyo hapo kesho.

Mwenyekiti wa Jumuya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli akipeana mkono na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni  alipowasili Ikulu Dar es salaam leo jioni Septemba 7, 2017 tayari kwa mkutano wa Viongozi wa jumuiya hiyo hapo kesho.
Mwenyekiti wa Jumuya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni wakiwa na Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki, Kikanda na Kimataifa Dkt Augustine Mahiga na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Plilip Mpango mara mgeni wake huyo alipowasili Ikulu Dar es salaam leo, tayari kwa mkutano wa Viongozi wa jumuiya hiyo hapo kesho.
Mwenyekiti wa Jumuya ya Afrika Mashariki Rais Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo na Rais wa Uganda Mhe Yoweri Kaguta Museveni mgeni wake huyo alipowasili Ikulu Dar es salaam leo jioni  tayari kwa mkutano wa Viongozi wa jumuiya hiyo hapo kesho.PICHA NA IKULU

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Alhamisi ya Septemba 8

Mahakimu 11 Wafukuzwa Kazi......Wengine 30 Kikaangoni

$
0
0
Watumishi 34 wa mahakama wakiwemo mahakimu 11, wamefukuzwa kazi kutokana na makosa mbalimbali ya kinidhamu.

Aidha, Tume ya Utumishi wa Mahakama inaendelea kujadili hatma ya mahakimu 30, waliokuwa wanatuhumiwa kuhusika na rushwa na kushinda zao mahakamani ili kuangalia kama walifanya makosa ya kinidhamu.

Jaji Mkuu, Mohammed Chande Othman alisema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea taarifa za ukaguzi wa mahakama pamoja na uendeshwaji wa mashauri.

Othman alisema watumishi hao, wamefukuzwa kutokana na uamuzi wa kikao cha Tume ya Mahakama, kilichofanyika Agosti 18, mwaka huu baada ya kushughulikia masuala mbalimbali ya kinidhamu.

“Tumewafukuza mahakimu wakazi wafawidhi, mahakimu wa mahakama za Mwanzo za Rombo, Temeke, Bahi na Chamwino na watumishi wengine 23. Hii ni idadi ndogo ambayo ni sawa na asilimia 0.005 ya wafanyakazi wote lakini kwa mahakama ni doa kubwa,” alisema Jaji Mkuu.

Alisema mahakimu hao wamefukuzwa kwa makosa mbalimbali ya kinidhamu, ikiwemo kutumia muhuri wa mahakama kinyume cha taratibu, kuathiri utendaji wa haki kwa kumsaidia mtu kufungua kesi moja katika mahakama mbili pamoja na kufungua kesi ya mirathi bila kuwa na hati ya kifo.

Aliongeza kuwa kuna makosa ya kisheria ambayo jaji au hakimu akikosea kutumia kifungu cha sheria hawajibishwi, lakini kuna makosa ya kinidhamu ambayo yanaondoa sifa ya kuwa hakimu au jaji.

Kuhusu mahakimu walioshinda kesi za rushwa mahakamani, Jaji Chande alisema mahakama inaweza isiwakute na hatia, lakini Tume itaangalia kama walifanya vitendo vya ukosefu wa nidhamu na kuwawajibisha.

Aidha, alisema mahakimu wengine 32 waliokuwa wanakabiliwa na kesi za jinai na kushinda kesi mahakamani, wanafunguliwa mashitaka ya kinidhamu katika Kamati ya Maadili ya Maofisa wa Mahakama kwa sababu inawezekana hawajapatikana na hatia ya kosa la jinai, lakini kama kuna vitendo vya ukosefu wa maadili watawawajibisha kimaadili.

Mahakama Maalumu ya Ufisadi
Katika hatua nyingine, Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi imeanza rasmi na wiki ijayo Kanuni za Uendeshaji wa mahakama hiyo, zinatarajiwa kuchapishwa. 

Jaji Mkuu Othman alisema mahakama hiyo, imeanza rasmi Julai 18 mwaka huu baada ya Rais John Magufuli kusaini sheria ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.

“Wiki ijayo tutachapisha kanuni mbalimbali za uendeshwaji wa mahakama hiyo, ikiwemo jinsi ya kulinda mashahidi pamoja na taratibu za ufunguaji wa kesi,” alisema Othman.

Alisema mahakama hiyo itakuwa na majaji wa kutosha ili kufanya kazi kwa uadilifu na kumaliza kesi kwa wakati, pia haitakuwa ikiahirisha kesi mara kwa mara.

Kuhusu utendaji kazi wa mahakama, Jaji Mkuu alisema mahakama haiwezi kutoa haki kama itakuwa inajificha au kuendeshwa kwa siri, ndiyo maana kwenye maboresho ya mahakama, wameamua kuwapa fursa wananchi kutoa mapendekezo au kero zao kupitia namba za simu pamoja na barua pepe.

Kesi za uchaguzi 
Awali akiwasilisha taarifa za utendaji wa Mahakama Kuu, Mahakama za Hakimu Mkazi, Wilaya na za Mwanzo, Msajili wa Mahakama Kuu, Ilvin Mugeta alisema baada ya uchaguzi, walipokea kesi 247 za uchaguzi, 53 za kupinga matokeo ya ubunge na 194 za udiwani.

Mugeta alisema tayari wameshamaliza kesi 234, zimebaki 13, lakini hadi kufikia Desemba mwaka huu kesi zote zitakuwa zimemalizika.

Aidha, alisema tathmini waliyoifanya inaonesha kesi zilizopo zinawiana na mahakimu, na kama watawezeshwa kwa vifaa vya kutendea kazi hadi Desemba mwaka huu watamaliza kesi zote zilizofunguliwa mwaka huu.

Mahakama ya Rufaa 
Kwa upande wake, Msajili wa Mahakama ya Rufaa, John Kahyoza alisema kiwango cha kumaliza mashauri katika Mahakama ya Rufaa kimeongezeka, pia wana lengo la kuhakikisha nakala za hukumu zinapatikana siku hukumu na ndani ya siku tatu zitapatikana kwenye tovuti ya Mahakama ya Tanzania.

Aidha, aliwaomba wananchi watoe ushirikiano ili rufaa zisikilizwe na kuisha mapema, kwa sababu kuna watu wanashindwa kufika mahakamani bila sababu za msingi au kutoa visingizio jambo linalosababisha rufaa zao kuchelewa.

Umuhimu wa mahakama
Katika hotuba yake kwenye Maadhimisho ya Siku ya Sheria Februari 4, mwaka huu, Rais Magufuli alisema anaitegemea sana Mahakama na aliwaambia majaji na mahakimu nchini kuwa:

“Nawaomba waheshimiwa majaji na waheshimiwa mahakimu, muitangulize Tanzania kwanza. Mkiitanguliza Tanzania kwanza tutaweza kufika mbali na tutaweza kuwasaidia watanzania wengi. 

"Nimeamua nchi iende, na itaenda. Anayefikiri ataikwamisha, atakwama yeye kwa sababu Mungu yuko pamoja na mimi. Na watu ninaowategemea sana ni Mahakama. Mahakama unafunga kila mmoja. Hata Rais nikitaka kufungwa na Mahakama, nafungwa. Mbunge anafungwa, nani anafungwa, nyinyi ndio wenyewe”.

Marais EAC Kukutana kwa Dharura Jijini Dar es Salaam chini ya Mwenyeji wao Rais Magufuli

$
0
0
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanyika Jijini Dar es Salaam

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameitisha Mkutano wa 17 wa Dharura wa Wakuu wa Nchi Wanachama Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) utakaofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Septemba, 2016.

Mkutano huo ambao ulitanguliwa na vikao vya maandalizi vya Makatibu Wakuu na Mawaziri vilivyofanyika Jijini Arusha utajadili agenda kuu nne ambazo ni:- Mahusiano ya kibiashara na uwekezaji kati ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Umoja wa Ulaya (EU) kupitia Mkataba wa Ushirikiano wa Kibiashara (EPA).

Agenda zingine ni Kupokea Taarifa ya Mwezeshaji wa mazungumzo ya Amani nchini Burundi, Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais Mstaafu wa Tanzania; Kupata taarifa ya hatua za kukamilisha uanachama wa Sudan Kusini kwenye EAC; na Kuapishwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Rwanda.

Akizungumzia mkutano huo kwa Waandishi wa Habari, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga amesema kuwa mkutano huu umeitishwa kwa dharura ili kuzungumzia agenda hizo muhimu hususan ile ya nchi wanachama kukubaliana kwa pamoja kusaini au kutosaini Mkataba wa EPA ifikapo tarehe 1 Oktoba, 2016.

Kuhusu Mkataba wa EPA, Mhe. Waziri Mahiga alisema kuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ilianza mazungumzo na Jumuiya ya Ulaya ya kushirikiana kibiashara kupitia EPA miaka 14 iliyopita na kuingia makubaliano ya awali mwaka 2014. 

Alieleza kuwa kwa mujibu wa makubaliano hayo ya awali EU na EAC zilikubaliana Mkataba huo usainiwe kwa pamoja na nchi zote za Jumuiya mwezi Julai 2016 kabla ya kuanza utekelezaji wake.

Hata hivyo Tanzania ilitangaza kutosaini makubaliano hayo kwa sababu mkataba huo unaweza kukwamisha juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano ya kuifanya Tanzania nchi ya Viwanda na Uchumi wa kati ifikapo 2025.

Aidha, Tanzania inahitaji kujadiliana zaidi na nchi wanachama ili kujiridhisha kuwa mkataba huo hautoathiri Mkataba ulioanzisha Jumuiya ya Afrika Mashariki hususan hatua ya mwanzo ya mkataba ambayo ni Umoja wa Forodha.

Kuhusu nchi nyingine wanachama Mhe. Mahiga alieleza kwamba, tayari Kenya na Rwanda zimesaini mkataba huo huku Uganda ikisubiri majadiliano ya nchi wanachama kabla ya kusaini na Burundi ikijitoa kusaini mkataba huo kwa vile tayari nchi za Ulaya zimeiwekea vikwazo vya kiuchumi.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dar es Salaam, 07 Septemba 2016.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Akagua makazi yake mapya Dodoma.

$
0
0
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa makazi mapya ya Waziri Mkuu katika eneo la Mlimwa na kuagiza umalizike kwa wakati ili aweze kuhamia kama alivyoahidi.

Katika ziara hiyo aliyoifanya jana mchana (Jumatano, Septemba 7, 2016) Waziri Mkuu alisema ameridhishwa na namna kazi ya ujenzi inavyofanyika.

“Nimekuja kukagua makazi mapya na mahali pa kufanyia kazi. Kazi ya ujenzi inaendelea vizuri, nimejionea mwenyewe na naamini katika kipindi kifupi watakuwa wamekamilisha,” alisema.

Alisema kutokamilika kwa ujenzi huo hauwezi kukwamisha azma yake ya kuhamia Dodoma kwa sababu tayari inafahamika kuwa Makao Makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu yako Dodoma.

Alisema uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma hautokani na shinikizo la kisiasa bali ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ambao chimbuko lake ni agizo lililotolewa Oktoba Mosi, 1973 kwenye Mkutano Mkuu wa 16 wa chama cha TANU.

“Tangu wakati huo Serikali zote ziliendelea kufanya juhudi mbalimbali za kuandaa miundombinu na hata awamu ya nne ilisimamia kwa kiwango kikubwa uwekaji wa miundombinu hiyo,” alisema.

“Pia tukumbuke kauli ya Mheshimiwa Rais aliyotoa kwenye hotuba yake ya Julai 23, 2016 alipochaguliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM, na akairudia tena Julai 25, kwenye maadhimisho ya kumbukumbu ya Mashujaa na mimi siku hiyo hiyo nikaweka msisitizo,” alisema.

Alisema uamuzi wa Serikali ya awamu ya tano wa kuhamia Dodoma unakuja baada ya kuridhishwa na ujenzi wa miundombinu na maeneo ya kutolea huduma za kijamii kwa wageni na wenyeji ikiwemo Hospitali ya Benjamini Mkapa iliyopo katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) yenye uwezo wa kutibu magonjwa makubwa kama ya moyo na figo.

Waziri Mkuu alisema tayari Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ina mpango kamambe (master plan) na ina viwanja vya kutosha kujenga makazi na ofisi mbalimbali.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU

Wazee wa CHADEMA Wamtuhumu Msajili wa Vyama Kwa Kuandaa Mitego Haramu ya Kukifuta Chama Hicho

$
0
0
Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limetoa pongezi kwa Kamati Kuu ya chama hicho kuahirisha maandamano na mikutano ya nchi nzima iliyopewa jina la Ukuta.

Maandamano hayo ambayo yalipangwa kufanyika kuanzia Septemba Mosi, mwaka huu yaliahirishwa na Kamati Kuu ya chama hicho kwa madai ya kuombwa na viongozi wakuu wa madhehebu ya dini.

Akizungumza katika Makao Makuu ya chama hicho jana, Katibu Mkuu wa Baraza hilo, Roderick Lutembeka alisema, hatua ya kamati hiyo kuahirisha maandamano hayo ni muhimu na inaonesha jinsi chama hicho kina viongozi wavumilivu.

“Kwa kutambua moyo wa kiuongozi waliouonesha na dhamira ya dhati ya kuwatumikia Watanzania wote, tunapenda kuwapongeza viongozi wetu wakuu kwa uamuzi huu wa busara ambao umeuthibitishia umma kuwa chama kina viongozi imara,” alisema Lutembeka

Katika hatua nyingine, baraza hilo limesema limebaini kuwepo kwa njama zinazopikwa dhidi ya chama hicho kupitia Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa na Baraza la Vyama vya Siasa nchini, kukifuta chama hicho.

“Taarifa zinaonesha njama hizo zinalenga kukihujumu Chadema kwa kuandaa mitego haramu ya kisiasa ili hatimaye yatolewe mapendekezo ya kukifuta katika orodha ya vyama vya siasa,” alisema Lutembeka  na kuongeza;

“Tarehe 15 Agosti mwaka huu Jaji Mtungi alitangaza kuwa, Baraza la Vyama vya Siasa lilikuwa limeitisha kikao ambacho kingefanyika tarehe 29-30 Agosti kujadili masuala ya hali ya kisiasa nchini. Siku mbili kabla ya kikao Mwenyekiti wa baraza akatangaza kukiahirisha hadi tarehe 3-4 mwezi huu.

“Jambo la kushangaza baada ya busara kutumika kupitia viongozi wa dini kushawishi Chadema kuahirisha kwa kutoa mwanya wa mazungumzo hadi tarehe 1 mwezi ujao, Kamati ya Uongozi wa Baraza la Vyama vya Siasa ikaibuka tena na kutangaza kuahirisha kikao cha baraza hadi itakapotangazwa tena.

“Wakati taarifa zote hizo zikitolewa na viongozi wa baraza, ofisini hapa (Chadema) hakuna hata barua moja kutoka kwa msajili ya kutuita katika kikao chochote kati ya hivyo. Kuanzia kile cha tarehe 29-30 Agosti, tarehe 3-4 Septemba wala hiyo ya kuahirisha.

“Katika mazingira haya nani ambaye hatashawishika kuamini ofisi ya msajili inatii maagizo ya watawala,”

Profesa Lipumba Aendelea Kupingwa Kila Kona.

$
0
0

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba ameendelea kupingwa ndani ya chama hicho, na safari hii jumuiya ya wanawake wa chama hicho ikiibuka na kumtaka ajiweke kando ili kuepusha mpasuko zaidi.

Aidha, wamewataka wanawake wafuasi wa chama hicho kote nchini, kuunga mkono uongozi wa muda uliowekwa na Baraza Kuu la Uongozi wa CUF hivi karibuni, ambao ulimtangaza Julius Mtatiro kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Muda ya Uongozi ndani ya chama hicho kilichowahi kuwa kikuu cha upinzani Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma jana, Makamu Mwenyekiti wa Taifa wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF, Savelina Mwijage ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu, alisema kauli yao imelenga kuunga mkono hatua iliyochukuliwa na Baraza la Uongozi dhidi ya wanaotajwa kukiuka Katiba.

Baraza hilo lilikutana Agosti 28, mwaka huu mjini Zanzibar ikiwa ni hatua ya kukabiliana na hali ya hewa iliyochafuka baada ya kundi la wanachama kuvamia Mkutano Mkuu Maalumu wa uchaguzi Agosti 21, mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Mwijage aliyefuatana na wabunge wengine wanne wa viti maalumu, amesema wanawake ndani ya CUF wamefedheheshwa na wafuasi wa Profesa Lipumba kwa kufanya vurugu, kudhalilisha wanawake wakati wa mkutano wa Dar es Salaam na pia kukisababishia chama hasara ya Sh milioni 600 zilitozumika kugharamia mkutano huo.

“Tunalaani kwa nguvu zote vitendo vya baadhi ya watu wanaotaka kukivuruga chama, lakini pia kuiingiza nchi katika migogoro ya udini, ukabili, ubara na Uzanzibari. Mbinu hiyo imepitwa na wakati, tunawaomba Watanzania wote wapuuze siasa hizo za uchochezi,” alisema.

Akizungumza hatua ya kusimamishwa kwa baadhi ya viongozi 11 wa juu wa chama hicho, wanaodaiwa kushiriki kukivuruga chama, alisema ni hatua sahihi na kwamba hata Profesa Lipumba hapaswi kuwa nyuma ya vurugu hizo, kwani aliachia madaraka kwa hiyari yake wakati chama kikielekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Kauli ya wanawake hao wa CUF ilikuja saa chache baada ya Mbunge wa Kaliua, Magdalena Sakaya ambaye ni mbunge pekee wa kike mwenye jimbo kutoka chama hicho, kuliambia Bunge kuwa hajatikiswa na uamuzi wa kumsimamisha uanachama na kwamba anaendelea kutimiza majukumu yake ndani ya chama, ambacho kabla ya mpasuko wa hivi karibuni, ndiye aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara.

Mbali ya Lipumba na Sakaya, wengine waliositishiwa uanachama ni Abdul Kambaya ambaye alikuwa Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Ashura Mustapha, Omar Mhina, Thomas Malima, Kapasha M. Kapasha, Mohamed Habib Mnyaa, Haroub Shamis na Mussa Haji Kombo.

Ashura ni mjumbe wa Baraza Kuu na aliwahi kuwa Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano ya Umma CUF wakati Mnyaa na Kombo, walikuwa wabunge kipindi cha 2010-2015; Mnyaa akiwakilisha Jimbo la Mkanyageni na Kombo Jimbo la Chake Chake, kisiwani Pemba.

Kutokana na kusimamishwa kwa viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Nassor Ahmed Mazrui alimtangaza Mtatiro aliyewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu Bara kuwa kiongozi wa kamati ya uongozi wa muda, inayowajumuisha pia Ahmed Katani na Mwijage ambao ni wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa.

Katani ni Mbunge wa Tandahimba, Mtwara wakati Severina alikuwa mjumbe wa kamati kama hiyo ilipoteuliwa Agosti mwaka jana baada ya Profesa Lipumba kujiuzulu uenyekiti kwa barua ya Agosti 5, mwaka jana.

Baraza hilo lilimteua pia Joram Bashange kukaimu nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara na Mbaraka Maharagande kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma hadi hapo nafasi hizo zitakapojazwa rasmi kwa mujibu wa masharti ya Katiba ya Chama hicho.

Afariki Kisimani Akimuokoa mbuzi

$
0
0
MKAZI wa Kijiji cha Kazibizyo Kata ya Ng’anzo, Wilayani Bukombe, Sebastian Lumbe (36), amefariki dunia kisimani alimoingia   kumuokoa mbuzi kwa ujira wa Sh 6,000.

Tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana katika Mtaa wa Misheni   baada ya mbuzi huyo kutumbukia kwenye kisima kinachodaiwa kuwa na urefu wa futi 30.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Misheni, Antony Kuya alithibitisha kutokea   tukio hilo.

Alisema baada ya mbuzi huyo kutumbukia kisimani, mmiliki wake, Marco Sylvester alitangaza ujira wa Sh 6,000 kwa mtu ambaye angefanikiwa kumtoa   na ndipo Lumbe alipojitolea kuingia kisimani humo.

Alisema kabla ya Lumbe kuingia kisimani humo na kukutwa na mauti, walijitokeza watu wawili tofauti lakini kila walipoingia waligundua kisima hicho kilikuwa kirefu.

Kwa sababu hiyo  walighairi  hadi alipofika yeye na kujitosa.

“Baada ya kuingia kisimani alianza kupiga kelele za kuomba msaada.

“Watu waliokuwa karibu na kisima hicho walimtupia kamba lakini wakati anajaribu kuivuta kupanda ilikatika na akaanguka kurudi kisimani.

“Baadaye kijana mmoja, Leonard Mathayo aliingia kujaribu kumuokoa lakini wakati akiwa humo ndani alisema baada ya kukaribia kufika mwisho wa shimo alimkuta akitupa miguu.

“Alipoanza kumfunga kamba ili wamvute  aliishiwa nguvu na kukosa hewa na hivyo ilimlazimu kuomba msaada kutoka nje,” alisema Kuya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo aliwaonya wananchi kuwa waangalifu na visima virefu kama hivyo kwa sababu  ni hatari.

Profesa Lipumba Asema Hana mpango wa kuhama CUF wala kuanzisha chama Kingine ........Ataja Sababu Zilizomfanya Amkatae Lowassa

$
0
0
Aliyekuwa mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amesema hana mpango wa kuhamia chama chochote.

Aidha amesema hana mpango wa kuanzisha chama chake kwa kuwa yeye bado ni Mwenyekiti halali wa CUF kwa mujibu wa Katiba ya chama hicho.

Akiongea katika kipindi cha Powerbreakfast cha Clouds FM Alhamisi hii, Profesa Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF anataka kukiua chama cha CUF Tanzania bara.

“Mimi nipo CUF bado, na ni Mwenyekiti halali kwa mujibu wa Katiba na sina mpango wa kuhamia chama kingine,”

“Katibu Mkuu wetu anataka chama hiki upande wa bara kife kabisa na ibaki CHADEMA pekee yake ndio maana anafukuza wabunge.,”

Pia Lipumba amesema Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif alikosea kumnyima mkono Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein kwa kuwa unapoenda kwenye msiba jambo la msiba lilipaswa kutawala.

“Hata mimi nilipokutana na Maalim baada ya kunikatalia kurudi kwenye uenyekiti tulisalimiana.” Alisema Lipumba.

Katika hatua nyingine Lipumba alizungumzia sababu ya kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA.

“Sababu za msingi za kutomkubali Mh. Edward Lowassa kuingia UKAWA, ni kwamba ukiwa katika siasa unahitaji uongozwe na misingi na ‘principals’ na hoja kwamba mnagombea kitu gani, na sisi tulianzisha UKAWA kwa kusema kwamba tutafute nchi, serikali na dola inayowajibika ambayo inatengeneza mambo vizuri, inatumia rasilimali vizuri itapambana na ufisadi na itajenga demokrasia ya kweli katika nchi yetu, ukiwa na misingi hiyo kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na tulikuwa wote kwenye bunge la katiba na Mh. Edward Lowassa alikuwepo kwenye bunge hilo hakuwa mmoja ya wabunge aliyeunga mkono rasimu ya Katiba,” alisema Lipumba.

Alioongeza,“Kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha kwamba utataka kiongozi ambaye anaunga mkono misingi hiyo na ukumbuke Mh. Edward Lowassa alikuwepo katika bunge la katiba ya rasimu ya Jaji Warioba na hakuunga mkono rasimu hiyo kwahiyo ilikuwa ni kinyume kabisa na ile misingi iliyotuunganisha na kuanzisha UKAWA kuja kumchukua Edward Lowassa ndiye awe mgombea urais wa watu wanaounga mkono rasimu ya Jaji Warioba,”

Ray C aonyesha muonekano wake mpya.........Mashabiki Wampa Ushauri Mzito

$
0
0
Msanii wa muziki Rehema Chalamila ‘Ray C’ ameonyesha picha yake ya kwanza toka asaidiwe na jeshi la polisi miezi michache iliyopita baada ya kudaiwa kuzidiwa na matumizi ya Madawa ya kulevya

Jumatano muimbaji huyo aliwaonyesha mashabiki wake muonekano wake mpya hali ambayo imewafanya mashabiki kumtaka kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya kwa kuwa amekuwa akisaidiwa mara kadhaa kuachana na matumizi ya Madawa ya kulevya lakini yeye amekuwa akirudia.

Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki wake.

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 41 & 42 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0
Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Kwa kupitia kwenye kiio nikazishuhudia gari sita za polisi zikija katika eneo ilipo ndege na kuizuia isiondoke na katika kuchungulia vizuri nikamuona askari lawrance akizungumza na waongozaji wa ndege wa chini akiwaomba ndege isiondoke na wakihitaji kumshusha mmoja wa abairia wa ndege hii na kwa haraka nikajua ni mimi ndio wamenifwata na kuyafanya mapigo yangu ya moyo kuanza kwenda kasi na amani ikanitoweka moyoni mwangu

Endelea...
Kutokana tayari injini za ndege zilishaanza kuata moto haikuwa rahisi kwa kuisimamisha ndege ambayo taratibu ilishaanza kuondoka kuzipisha ndege nyingine ambazo zinasubiri kutua na kila kitu katika uwanjwa huu wa ndege vinakwenda na muda wanao jipangia.Macho yangu yakashuhudia jinsi tunavyo ziacha gari za polisi na ndege inavyo ongeza mwenza na kuitafuta njia ya kurukia
“ehee mola niokoe mimi mja wako kwa maana mmmm”

Nilijizungumza kimoyo moyo na kweli ndege ikakaanza kunyanyuka taratibua na kuiacha ardhi ya afrika kusini hadi ndege inakaa sawa angani ndio nikapata amani na kajasho taratibu kakanishuka huku kwa mbali nikijasikilizia jinsi mapigo ya moyo yanavyo punguza kasi yake,safari ikaendelea kwa amani na kutokana na uchovu mwingi nikajikuta nikilala fofofo pasipo na kitu kilicho nistua ni kipaza sauti cha rubani akituomba tufunge mikanda yetu vizuri kwani ndege inajiandaa kutua katika uwanja wa jomo kenyata nchini kenya
“mmmmmmm”

Nikajikuta nikiguna kwani sijazoea kuziona ndege zinazo toka nchini afrika kusini kutua kenya ili kwenda tanzania na isitoshe kwa maelezo niliyo yasikia wakizungumza mama na balozi wa tanzania ni kwamba ndege inakwenda moja kwa moja tanzania.Moyo wangu ukaanza kupoteza amani tena ikanilazimu kumiya muhudumu wa ndege na hakusita kunifwata sehemu nilipo na kunisikiliza haja yangu niliyo muitia

“sijui nimesikia vibaya au....? Ni kweli tutatu kenya?”
“ndio kuna mzigo tunaishusha kwanza na pia kuna mmoja wa abiria nanhitajika kurudisha afrika kusini kwahiyo tunaiwahi ndege ya shirika letu inayo ondoka kenya saa sita usiku na tutamkabidhi abiria huyo kwa askari.”
Moyo ukawa kama umelipuliwa na bomo,kuzungumza nikajikuta nikishindwa na kubaki nikimtazama muhudumu kama sanamu la kushangaza

“halloo mr”
Nikastuka na kumtazama muhudumu wa ndege ambaye alikuwa akinipungia mkono mbele ya uso wangu baada ya kuniona nikiwa nimegandishwa kama sanamu
“umesema kuna mtu anashushwa?”
“ndio hiyo ni taarifa tuliyo powa tukiwa njiani”
“ni mwanume au mwanamke”
“kusema kweli hatujatajiwa ni jinsia gani?”
“nashukuru”
“na wewe pia”

Muhudumu akaondoka na kuniacha nikitawaliwa na mawazo na laiti ingekuwa nipo kwenye gari nigeweza kuruka na kufilia mali.Kitu cha ndege ni ngumu sana kujirusha,rubani akatutangazia kuwa zimesalia dakika tano kwa ndege kutua na kila mto ahakikishe kuwa amejifunga vizuri  mkanda wake hapo ndipo nikakumbuka na mimi kujifunga mkanda.

Ndani ya dakika tano ambazo rubadi alisema ndivyo jinsi iliyo kuwa na ndege nikaanza kushuka chini kwa kasi na matairi yake yakaanza kukanyaga ardhi ila gafla tukasikia mlio wa ‘kwaaa’ kama kitu kilicho katika na kuifanya ndege kuegemea upande wangu niliopo na wezangu tulio kaa upande huu.Milio ya vyuma kukatika katika tukazidi kuisikia na si mimi mwenye niliye anza kupiga kelele za kumuomba mungu ila hadi wezangu nao wakafanya hivyo huku kila mmoja akiomba kwa lugha anayo ijua yeye mwenyewe

Ndege ikazidi kulala upande wetu na kazidi kuserereka na mbaya zaidi moto mwingi ukaanza kuwaka sehemu ya nyuma mita chache kutoka ilipo siti yangu na kunilazimu kuufungua mkanda ili kuyaokoa maisha yangu kama wanavyofanya wezangu.

Nikawahi kuishika siti ya mbele yangu ili kujizuia na upepo mwingi unao nivuta nyuma kutoka katika sehemu ulipo moto ambao umepasua sehemu nzima ya nyuma.Nikajikaza kwenda mbele na watu walio shidwa kujishikilia walivutwa nyuma kwenye moto.Kelele na vilio vikazidi kutawala na kila sehemu na watu wengi wakawa wamebanwa na siti zao kiaisi kwamba baadhi yao walijigonga vibaya kwenye vyuma na vichwa vyao kupasuka vibaya na wengine kukatika viungo vya miili yao.

Ndege ikagonga sehemu na kusababisha mtikisiko mkubwa na kupinduka kichwa chini miguu juu jambo lililosababisha mikono yangu kushindwa kuhimili kuishikilia siti niliyo kuwa nimeishika na nikajikuta nikiachia na kuanza kuvutwa nyuma na upepo mkali uliochanganyika na moto ambao ni mkali sana,gafla nikastukia nikidakwa mkono na kuangalia vizuri nikamkuta ni sheila ambaye amenishika mkono huku na yeye akiwa amekaa kwenye siti yake na kuzuiwa na mkanda alio jifunga na huku mkono mmoja akiwa ameushika kwenye siti iliyopo pembeni.

Nikamtazama kwa macho ya huzuni na kumuona akishindwa kuhimili uzito wangu kwani tegemezi lote la mwili wangu ni mkono wake na sikuwa na sehemu yingine ya kushikilia
“sheila niachie nife”
“eddy unasemaje?”
“niachie.”

Nilizungumza huku nikimtazama sheila machoni ambaye anatumia nguvu nyingi kunizuia nisichomolewe nje ya ndege na mbaya zaidi pembeni yangu hakuna kitu ambacho ninaweza kusema kuwa nitakishika ili kinizuie nisichomolewe nje kwani siti zote za nyuma zimechomoka na watu wake.

Ndege ikaendelea kugonga majengo yaliyopo ya hapa uwanja wa ndege hadi ikasimama ndipo sheila akaniachia mkono na mimi nikaanguka chini na kujigonga mkono wangu wa kushoto kwenye upande wa pili wa ndege.Sheila akaaanza kupata shida ya kujifungua mkanda wa siti yake na mbaya zaidi kwa jinsi ndege ilivyo anguka imemfanya awe kichwa chini miguu juu

Nikaanza kusikia ving’ora vya gari za zimamoto zikija katika eneo la tukio na kuazna kuuzima moto  unaoendelea kuiteketeza ndege,moshi mwingi ulio tawala ndani ya ndege ukanifanya nianza kukohoa na taratibu nikaanza kujivuta nje ya ndege huku mkono wangu ukitawaliwa na maumivu makali.Niavutwa nje na waokoaji na gafla mlipuko mkubwa wa ndege ukatokea na kuturusha mbali mimi pamoja na waokoaji na nikajzidi kuuegemea mkono wangu ambao ninahisi unamaumivu

Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa Leo Bungeni kuhusu wahusika wa mauaji ya askari na Swala la Uchumi wa Nchi

$
0
0
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na masuala ya uchumi katika kuhakikisha uchumi wa nchi unaendelea kukua.

Hayo yamesemwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Hai Mhe. Freeman Mbowe mijini Dodoma aliyetaka kujua hali ya uchumi ilivyo kwa sasa hapa nchini.

Waziri Mkuu  amesema kuwa lengo kuu la Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha uchumi wa nchi unaongezeka kupitia nyanja tofauti kwa kushirikiana na taasisi za fedha zilizopo ili kufikia uchumi wa kati kama ilivyoanishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza kuhusu suala la midororo wa upokeaji wa mizigo katika bandari nchini, Waziri Mkuu amesema kuwa mdororo huo umetokana na kupungua kwa kiasi cha mizigo na  kushuka kwa uchumi duniani.

Katika suala ya mauaji yaliyotokea Tanga, Mwanza na Vikindu, Waziri Mkuu amesema kuwa usalama wa wananchi utaendelea kuimarishwa huku serikali ikiahidi kupambana vitendo vya mauaji kwa raia na askari katika maeneo mbali mbali nchini.

“Serikali imesikitika sana na jambo hili la mauaji hivyo itahakikisha wauaji hao wanawekwa katika mikono ya Sheria na kuongeza ulinzi kwa maeneo yote nchini kwa kuanzia ngazi ya vitongoji” alifafanua Waziri Mkuu.

Mbali na hayo Waziri Majaliwa ametoa wito kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya dola katika kuthibiti matukio hayo.

Kuhusu suala la uwepo wa tozo katika zao la korosho swali limeibuliwa na Mbunge wa viti maalumu Mhe.Riziki Lulida (CUF), Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa Serikali imeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na Wilaya kusimamia uondoaji wa Tozo zisizo na maana katika zao la korosho.

Waziri Mkuu: Serikali Haijashindwa Kuongoza Nchi

$
0
0

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo macho, haijalala na haijashindwa kuongoza nchi bali imejipanga  kuliongoza Taifa kwa mafanikio makubwa.
 
"Serikali haijashindwa kuongoza nchi. Nataka niwahakikishie waheshimiwa Wabunge na wananchi wote kwamba tutaongoza nchi hii kwa mafanikio makubwa na kazi hiyo imeanza kwa marekebisho makubwa kwa maeneo ambayo tunadhani yatafanya Taifa hili liweze kupata mafanikio makubwa,” amesema.
 
Ametoa kauli hiyo leo (Alhamisi, Septemba 8, 2016) Bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali lililoulizwa na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe, ambaye alitaka kufahamu Serikali ina mkakati gani wa kunusuru mdororo wa uchumi uliopo nchini.
 
Bw. Mbowe alidai kwamba hali ya uchumi imeshuka na kwa mujibu wa taarifa za Benki Kuu ya Tanzania (BOT) uagizaji wa bidhaa kutoka nje umepungua, uuzaji wa bidhaa nje ya nchi na sekta ya ujenzi imesimama hali inayoashiria kudorora kwa uchumi.
 
Kuhusu suala la kupungua kwa mizigo katika bandari na vituo vya forodha, Waziri Mkuu amesema usafirishaji wa mizigo kwa njia ya bahari umeshuka duniani kote kwa sababu ya kushuka kwa hali ya uchumi kutokana na kuporomoka kwa bei ya mafuta na gesi.
 
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema tayari wafanyabiashara wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) wameihakikishia Serikali kwamba mizigo yao yote itakuwa inapitia Bandari ya Dar es Salaam hasa kwa mkakati wa pamoja wa ujenzi wa reli ya standard gauge inayoanzia Dar es Salaam-Tabora - Isaka.
 
Wakati huo huo Waziri Mkuu amesema Serikali itahakikisha inaendelea kuimarisha amani na ulinzi kwenye maeneo yote nchini na kwamba vyombo vya dola viko macho. “Watu wote wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu yakiwemo mauaji watakamatwa popote walipo na kuchukuliwa hatua za kisheria,; amesema.

Amesema hatua hiyo inatokana na matukio ya mauaji yaliyotokea hivi karibuni ambapo raia wasiokuwa na hatia na askari waliuawa katika maeneo ya Vikindu mkoani Pwani, Tanga na Mwanza. Waziri Mkuu ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Korogwe Vijijini, Bw. Stephen Ngonyani

Katika swali lake, Bw. Ngonyani alitaka kujua ya Serikali kuhusu  kukomesha mauaji hayo, yanayotokea kwa watu wasio na hatia pamoja na askari, ambapo Waziri Mkuu, alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa wananchi na familia, ambazo ndugu zao walipoteza maisha katika mauaji hayo.

Pia ametoa wito kwa Watanzania wote kuhakikisha wanawafichua watu ambao wanawatilia shaka na kutoa taarifa kwa vyombo vya dola ili waweze kuchunguzwa na kuchukuliwa hatua

Habari na Ofisi ya Waziri Mkuu

Jeshi La Polisi Latolea Ufafanuzi Taarifa Inayosambazwa Kwenye Mitandao Juu Ya Kukamatwa Watu Wanaokuwa Kwenye Nyumba Za Wageni Mchana

$
0
0
Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar Es Salaam anatoa rai kwa wakazi wa Jiji la Dar Es salaam na wageni wanaoingia jijini wakitokea mikoani  kupuuza  taarifa za sauti  zinazozagaa katika mitandao ya kijamii kuwa Polisi wanawakamata ovyo watu wanaolala kwenye nyumba za kulala wageni.

Taarifa hizo za uvumi  zinazoendelea kuzagaa  kwenye mitandao ya Kijamii kama WHATSAPP, TELEGRAM na pia zimechapishwa kwenye baadhi ya magazeti kwamba Askari Polisi wanawakamata watu  ovyo mchana wakiwa kwenye nyumba za kulala wageni  kwa madai ya kukamata kwa makosa ya uzembe na uzururaji na pia kutimiza kauli ya Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania ‘HAPA NI KAZI TU’.

Kimsingi niwatoe hofu raia wema kuwa tunaendelea na oparesheni za kuwasaka watuhumiwa wa makosa mbalimbali yakiwemo wanaofanya biashara ya nyumba za kulala wageni kinyume cha sheria (guest bubu), majambazi na wahalifu wengine wa makosa mbalimbali.

Aidha taarifa za kuaminika zimebaini kuwa baadhi ya nyumba za kulala wageni zimekuwa zikitumika kuhifadhi magenge ya wahalifu, dada poa na kaka poa, hivyo Jeshi la Polisi tunawajibika kufuatilia na kuwakamata wahalifu.
 
Niwajibu wa Polisi kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwenye nyumba za kulala wageni, Hoteli, migahawa, Vilabu vya vileo,  kumbi za starehe zinazokesha na zisizokesha na watakaobainika kuvunja sheria, hatua kali za kisheria dhidi yao zitachukuliwa. 

Sheria ya Mwenendo ya makosa ya jinai kifungu cha 60(1) (sura ya 77 iliyofanyiwa marekebisho 2002) kinampa nguvu askari kufanya ukaguzi wa maeneo yote yaliyotajwa hapo juu na kumkamata mtu yeyote anayetiliwa shaka akienda kinyume na utaratibu wa biashara hizo.

Sambamba na hayo nawatahadharisha wafanyabiashara wote wa nyumba za kulala wageni wafuate taratibu za kupokea wageni kwa kuandika kwenye vitabu, kuandika namba za vitambulisho vyao na sehemu wanayotoka, na pale watakapomtilia mashaka mteja yeyote watoe taarifa kituo chochote cha polisi.

Pia wenyeviti wa serikali za mitaa na wajumbe wa nyumba kumi wanawajibika kuwatambua wageni wote wanaoingia kwenye himaya zao na kuwachukulia hatua stahiki ili kuimarisha usalama katika jiji letu la  Dar Es salaam.

DAR ES SALAAM BILA UHALIFU INAWEZEKANA, TUSHIRIKIANE KUISAFISHA JIJI LETU

S.N.SIRRO - CP
 KAMISHNA WA POLISI
KANDA MAALUM
DAR ES SALAAM

Makamu wa Rais: Viongozi Na Watumishi Wa Umma Kuchukuliwa Hatua Kali Iwapo Watabainika Kukiuka Taratibu Za Kazi

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Nchi kuchunguza na kuwachukulia hatua kisheria na za kinidhamu viongozi na watumishi wa umma ambao wanakiuka taratibu za kazi kwa ajili ya maslahi yao binafsi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo 8-Sep-2016 mjini Mtwara wakati anafungua jengo la sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini ambalo ujenzi wake umegharimu takribani shilingi bilioni MBILI.

Makamu wa Rais amesema iwapo kama hatua hizo zitachukuliwa haraka zitakomesha na kupunguza kasi ya mmomonyoko wa maadili kwa viongozi na watumishi wa umma hali ambayo itaongeza uwajibikaji katika utendaji wa kazi miongoni watendaji hao.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuiimarisha sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma nchini kwa kuijengea uwezo wa rasilimali watu na fedha kwa kadri hali ya uchumi itakavyo ruhusu ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Makamu wa Rais amewahimiza viongozi na watumishi wa umma kuthamini na wahakikishe walinda maslahi ya umma wakati wote wa utendaji wao wa kazi ili kuondoa malalamiko kwa wananchi.

Makamu wa Rais amesema ni jambo la muhimu kwa sekretarieti hiyo kufutilia mienendo ya viongozi wa umma na kuwabaini wale wanaokwenda kinyume na misingi ya uadilifu na wachukuliwe hatua ipasavyo kabla hawaleta madhara kwa serikali na jamii kwa ujumla.

Makamu wa Rais pia ametoa rai maalum kwa wananchi wa mkoa wa Mtwara kuitumia ofisi hiyo mpya ya sekretarieti ya maadili ya viongozi wa umma Kanda ya Kusini kwa kutoa taarifa kuhusu mienendo ya viongozi wanaokiuka maadili ya umma katika utendaji wao wa kazi ili waweze kuchukuliwa hatua.

Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala bora Angela Kairuki amesisitiza kuwa kazi ya kuhakiki mali na madeni ya viongozi wa umma itaendelea kwa kasi nchini na mwaka huu sekretarieti hiyo itahakiki mali za viongozi wapatao 500 kote nchini.

Naye Jaji Mstaafu na Kamishna wa Maadili Nchini Salome Kaganda akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa jengo hilo ameiomba serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya kufanikisha zoezi la uhakiki wa mali na madeni ya viongozi kwa nchi nzima.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Mtwara.
8-Sep-2016.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya Septemba 9

Polisi Wamhoji Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob

$
0
0

Maofisa wa Polisi wamemhoji Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob kabla ya hajakutana na waandishi wa habari kwa madai kuwa wamepata taarifa mkutano wake huo ulilenga kumkashifu Rais John Magufuli.

Maofisa hao waliovalia kiraia walionana na Jacob ofisini kwake na walimruhusu kuendelea na mkutano huo baada ya meya huyo kuwahakikishia kwamba hana nia hiyo bali alitaka kutoa ufafanuzi wa baadhi ya masuala baada ya ujio wa Rais, Kinondoni Jumanne iliyopita.

“Kwa mara ya kwanza meya anahojiwa, lakini niliwaambia wana usalama lengo langu ni nini na sipo kwa ajili ya kumkashifu Rais, ila nafahamu vita iliyopo kati yetu na baadhi ya viongozi,” alisema Jacob.

Pamoja na ufafanuzi huo, Jacob aliwataka baadhi yao (askari) kushiriki kwenye mkutano huo wa wanahabari kufuatilia alichotaka kuwaeleza wanahabari na polisi mmoja alibaki kusikiliza bila kutambulishwa.

Kamanda wa Polisi wa Kinondoni, Suzan Kaganda alisema hakukuwa na tatizo lolote polisi kuwapo eneo  hilo, kwani wanafanya shughuli zao za ulinzi na usalama wa raia na hasa ikizingatiwa kuwa kuna Ofisi ya Mkuu wa Wilaya.

Katika mkutano huo, meya Jacob alitoa ufafanuzi wa yaliyojiri Jumanne iliyopita wakati Rais Magufuli alipofanya ziara katika manispaa hiyo na kubatilisha umiliki wa eneo la Magomeni Kota lililokuwa mali ya halmashauri kuwa ya Serikali Kuu.

Meya Jacob aliwaambia wanahabari kuwa uamuzi wa Serikali kuchukua eneo hilo umeisababishia halmashauri yake hasara ya zaidi Sh4.5 bilioni kutokana na gharama walizoingia. 

Katika eneo hilo, nyumba 644 zilivunjwa mwaka 2011 kwa miadi ya kwamba zikijengwa upya, wananchi waliokuwa wakiishi hapo wakiwa wapangaji wangerejeshwa, lakini mradi huo ulichelewa kuanza.

Akiwa ameambatana na baadhi ya madiwani, Jacob alisema hasara hiyo imetokana na halmashauri kutumia Sh2 bilioni kumlipa mkandarasi kwa ajili ya michoro ya eneo litakavyokuwa. 

Alisema pia manispaa hiyo imetoa Sh1 bilioni kwa mkandarasi Gulf kwa ajili ya kuchora ramani ya ofisi mpya za halmashauri na kusimamia ujenzi wa mradi huo na kutumia Sh700 milioni kuwalipia kodi wapangaji hao baada ya kuwahamisha.

“Faida tuliyoipata ni kwamba wananchi tuliopanga kuwahudumia tayari Rais amewahudumia. Hatupingi maamuzi ya Serikali, lakini wananchi watambue kwamba manispaa haina chochote itakachokipata, bali kila kitu kitakuwa kinafanywa na Serikali Kuu,” alisema Jacob.

Meya alisisitiza kuwa madiwani wa Ukawa hawapingi uamuzi huo ila baadhi ya viongozi wanaomzunguka Rais hawamwambii ukweli wa mambo kuhusu mradi wa Magomeni Kota na kwamba baadhi ya watumishi wa Serikali ndiyo waliosababisha kufikia hatua hiyo.

“Siku ile ningepata nafasi hata dakika tatu, ningemweleza Rais Magufuli ukweli wa mambo wa mradi huu. Lakini kuna baadhi ya viongozi waliomzunguka waliamua kuninyima nafasi hiyo. "

Hata hivyo, Jacob alimwomba Rais Magufuli kukutana naye ili amweleze kwa undani jambo linalomuumiza kuhusiana na masuala ya ardhi yanayoikumbuka Kinondoni.

Alifafanua kwamba, Serikali iliyopita na manispaa hiyo ilishaingia mkataba na kampuni ya Blue Marine ya Romania kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Magomeni Kota ambao ulifikia katika hatua nzuri lakini baadhi ya watumishi wa Serikali waliamua kuweka ‘kauzibe’ na kuipa sifa mbaya Kinondoni.

“Tulikuwa tunasubiri utiaji wa saini kutoka Serikali Kuu, lakini baada ya kuona Kinondoni inaongozwa na Ukawa wameamua kuleta ‘figisufigisu’ za kuukwamisha,” alisema Jacob.

Katika ziara hiyo, Rais Magufuli alielezea kusikitishwa kwake na namna tatizo la wakazi hao lilivyoshughulikiwa na kuwaahidi kuwa Serikali yake itahakikisha hawasumbuliwi.

Mahakama Yaizuia NHC Kupiga Mnada Mali za Freeman Mbowe

$
0
0
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kitengo cha Ardhi imeliamuru Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutouza au kupiga mnada mali za Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), mpaka kesi ya msingi itakapomalizika.

Shirika hilo lilizichukua mali mbalimbali za kampuni za Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, wiki iliyopita kupitia mawakala wa kampuni ya Fosters Auctioneers katika jengo lililopo makutano ya mitaa ya Mkwepu na Indira Gandhi (Makunganya) jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya NHC ilitokana na mgogoro wa muda mrefu, wakimtuhumu Mbowe kushindwa kulipa deni la zaidi ya Sh. 1.3 bilioni, ikiwa jumla ya fedha za kodi ya kupangishwa kwenye jengo hilo.

Kutokana na mvutano huo, Mbowe alifungua kesi katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Ardhi, kupinga hatua ya NHC kumuondoa katika jengo hilo, pamoja na kuchukua mali zake huku wakitangaza kuzipiga mnada baada ya siku 14 tangu kuzichukua.

Jana, Jaji Siyovelwa Mwangasi alitoa zuio na kuiamuru NHC kutouza wala kupiga mnada mali hizo za Mbowe mpaka mahakama hiyo itakapotolea uamuzi katika kesi ya msingi.

Katika kesi hiyo namba 722 ya mwaka 2016, Mbowe anawakilishwa na Mawakili  Peter Kibatala na Omary Msemo.

Jaji Mwangasi amesema kuwa, anakubaliana na maombi ya mlalamikaji na kutaka mali hizo zisiuzwe hadi hapo mahakama itakapofanyia uamuzi kesi ya msingi.

Hatua hiyo inakuja baada ya upande wa NHC kupitia mawakili wake Aloyce Sekule na Miriam Mungula kushindwa kuwasilisha hoja za msingi kueleza, ni kwanini zuio hilo lisitolewe hadi hapo kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Awali, mawakili wa NHC, walidai kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza maombi ya Mbowe kwa kuwa hakuna kesi ya msingi ambayo imefunguliwa, hivyo maombi hayo yatupiliwe mbali.

Wakili Kibatala alijibu hoja hiyo kwa kusema, hatua ya kuwasilisha maombi hayo inalenga kubaini kama kweli Mbowe anadaiwa kodi ama la.

Kibatala alidai kuwa mahakama hiyo ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, hivyo inaweza ikatoa uamuzi wowote, na ndiyo maana wamewasilisha maombi hayo ili itolewe amri ya muda ya kuzuia mchakato huo.

Miongoni mwa hoja za Mbowe alizoziwalisha mahakamani hapo, ni pamoja na hoja kuwa, yeye (Mbowe) na shirika hilo walikubaliana kwamba atalikarabati na kulipanua jengo hilo kwa asilimia 100. Makubaliano ambayo yaliingiwa mwaka 1997.

Amedai kuwa katika makubaliano hayo yeye na NHC walikubaliana watamiliki jengo hilo kwa pamoja kwa muda wa miaka 99, huku Mbowe katika mgawanyo wa mapato akitakiwa kupata asilimia 75 na NHC ikitakiwa kupata asilimia 25.

Pia alieleza kuwa katika makubaliano hayo, licha ya mwenendo wa kibiashara kutokuwa mzuri, muda wote alikuwa akilipa asilimia hiyo 25, kwa mujibu wa makubaliano yao.

Hivyo kutokana na hatua ya NHC kuvunja mkataba huo kwa kumtoa kwenye jengo na kuchukua mali zake, anaiomba mahakama iliamuru shirika hilo limlipe fidia.

Mbowe aliondolewa kwenye jengo husika mnamo Septemba mosi kwa madai ya kushindwa kulipa deni la zaidi ya Sh. bilioni 1.3.

Mawakala wa NHC walifika katika jengo hilo saa 12:30 asubuhi na wafanyakazi zaidi ya 50 na kwenda moja kwa moja katika kampuni ya Free media pamoja na ukumbi wa Bilcanas na kuchukua vifaa mbalimbali ikiwemo, meza, viti na kompyuta.

Siku chache baada ya kuondolewa kwa Mbowe katika jengo hilo, Rais John Magufuli alilisifu shirika hilo kwa hatua hiyo na kulitaka lichukue hatua kama hizo kwa wadaiwa wengine zikiwemo taasisi za umma

Ambari Nyeupe Ni Tiba Ya Kuongeza Ukubwa Wa Maumbile Ya Kiume Yaliyo Sinyaa.

$
0
0
Ipo  idadi  kubwa  ya  wanaume  wanao  kabiliwa na  changamoto  ya  kuwa  na  maumbile  madogo  ya  kiume.  

Kama  wewe  ni  mwanaume  ulie  katika  kundi  hili, unaweza  kujitibu  tatizo  lako  kwa  kutumia dawa  asilia  itokanyo  na  AMBARI  NYEUPE.

Ambari  nyeupe  nyeupe  ikichanganywa  na  dawa  nyingine  tatu  za  asili,  hutumika  kama  tiba  ya  kuongeza  ukubwa  wa  maumbile  ya  kiume  yaliyo  sinyaa.

Kwa  mahitaji  yako  ya  dawa  hii, fika  katika  duka  la  kuuza  dawa  asilia  la  NEEMA  HERBALIST & NUTRITIONAL  FOODS  CLINIC.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini Dar  Es  Salaam, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo la  UBUNGO  PLAZA.

Wasiliana  nasi  kwa  SIMU  NAMBA  0766  53  83  84

Na kwa  taarifa  Zaidi  kuhusu  huduma  zetu,  tutembelee  katika  blogu  yetu :

Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.

$
0
0
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao ulikuwa unaelekea Wilayani Tandahimba ukitokea Ikulu ndogo ya Rais ,mkoani Mtwara, umepata ajali na kusababisha majeruhi ambao wamekimbizwa hospitali ya rufaa Ligula.

Ajali imetokea mbele kidogo ya kijiji cha Nanguruwe kilichopo halmashauri ya wilaya ya Mtwara .Majeruhi walioumia ni dereva  pamoja na wasaidizi wanne wa Makamu wa Rais.
 
Awali kabla ya gari hilo lililobeba wasaidizi wa Makamu wa Rais kuacha njia na kupinduka, gari liliokuwa limebeba waandishi wa habari wa channel ten, startv na clouds tv liliacha njia na nusura kupinduka.

Barabara ya kutoka Mtwara kuelekea Tandahimba si ya kiwango cha kuridhisha na kuruhusu magari kwenda mwendokasi hali iliyosababisha magari hayo kuacha njia na moja kupinduka kabisa na kusababisha majeruhi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images