Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

Salum Mwalimu na Wafuasi 18 wa Chadema wapata dhamana

$
0
0
Mahakama ya Hakimu Mkazi Simiyu imewaachia kwa dhamana Naibu Katibu Mkuu wa Chadema (Zanzibar), Salum Mwalimu na wafuasi wengine 18 wa chama hicho baada ya kukaa mahabusu kwa zaidi ya siku 12.

Kiongozi huyo wa Chadema na wafuasi hao 18 walikuwa wakishikiliwa katika mahabusu za jeshi la polisi kwa tuhuma za kuandaa na kuhamasisha maandamano na mikutano ya Oparesheni ya chama hicho iliyopewa jina la UKUTA, ambayo ilipigwa marufuku na jeshi hilo.

Walifanikiwa kupata dhamana baada ya Hakimu wa Mahakama hiyo kueleza kuwa ameridhia hoja za upande wa utetezi baada ya kusikiliza pande zote mbili na kubaini mapungufu kwenye maombi ya upande wa mashtaka.

Awali, Mwendesha mashtaka aliitaka Mahakama hiyo kuwanyima dhamana washtakiwa hao kwa madai kuwa endapo wataachiwa wataendelea kufanya kosa hilo.

Hata hivyo, Hakimu alitupilia mbali maombi hayo akieleza kuwa wameshindwa kuthibitisha pasipo shaka kuwa endapo washtakiwa hao wataachiwa watafanya tena kosa hilo.

Pia, Hakimu alieleza kukubaliana na hoja ya washtakiwa hao kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa mahakamani hapo na mwendesha mashtaka ilikuwa na mapungufu ya kisheria.

“Ninakubaliana na upande wa utetezi kuwa hati ya kiapo iliyowasilishwa ina mapungufu ya kisheria,” alisema Hakimu baada kupitia na kugundua kuwa aliyesaini hati hiyo sio anayeonekana kuitoa.

Washtakiwa wote walitimiza masharti ya dhamana kwa kuwasilisha wadhamini wawili kila mmoja ambaye ataweka dhamana ya shilingi milioni 3.

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria mahakamani hapo na kuondoka na Salum na wafuasi hao ambao walifikishwa mahakamani hapo awali chini ya ulinzi mkali. Kesi imeahirishwa hadi Oktoba 4 mwaka huu

Anthony Diallo Atoa Ufafanuzi Baada ya TRA Kuzifunga Akaunti Zake

$
0
0

Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imekamata akaunti za Kampuni ya Sahara Media Group kwa kushindwa kulipa deni la Sh4 bilioni kama kodi iliyopaswa kulipwa na kampuni hiyo.

Taarifa zilizosambaa kupitia mitandao ya kijamii zimeeleza kuwa akaunti zote za kampuni hiyo zimefungiwa mpaka pale watakapolipa deni hilo, lakini kampuni hiyo imetoa ufafanuzi.

Ujumbe huo uliongeza kuwa kampuni hiyo imefikishwa mahakamani na benki moja hapa nchini  kwa madai ya kutaka kulipwa Sh600 milioni, baada ya kuingia makubaliano ya kulipa wafanyakazi wake mishahara pamoja na mikopo lakini mpaka sasa imeshindwa kurejesha fedha hizo.

Hata hivyo, akizungumzia suala hilo mwenyekiti mtendaji wa  kampuni ya Sahara, Anthony Diallo alikiri mamlaka hiyo kufungia akaunti ya kampuni yake.

Diallo ambaye ndiye mmiliki wa kampuni hiyo alisema ni akaunti moja tu iliyofungiwa na kwamba anaamini baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na mamlaka hiyo watafikia muafaka ili biashara ziendelee kama kawaida.

“Tutalimaliza hakuna kitakachoenda mrama,” alisisitiza Diallo ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo nafasi ya Waziri wa Maliasili na Utalii na Naibu Waziri wa Maji, Maendeleo ya Mifugo katika Awamu ya Nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Amesema deni la TRA linatokana na kodi iliyopatikana baada ya ukaguzi wa vitabu kwa miaka mitatu. 

“Ni ukaguzi wa kawaida hufanyika kama taratibu. Sasa kwa sababu ya kuhamisha matangazo yetu kutoka analojia kwenda digitali ilibidi tukope benki,  ujenzi na kumaliza mradi imechukua miaka mitatu. Wakati wote tumekuwa tukilipa riba benki na zinazobaki toka mauzo ya matangazo tunalipa mishahara, umeme na malipo ya kodi za kawaida,”alisema.

“Ni kawaida ila wamefanya hatua za kutuaibisha tu. Kampuni yetu ya ving’amuzi ni ya Kitanzania na mapato yote yanaingia nchini wakati kampuni nyingine kubwa zote ni za kigeni kutoka China, Afrika Kusini, Mauritius na Kenya! Ukweli sisi tunahitaji kusaidia nchi kiuchumi na kutuharibia ni hasara kwa nchi.”                       

Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu

$
0
0
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio mbalimbali ya kihalifu katika mkoa wa Dar es Salaam, wameuawa na majambazi wenzao katika eneo la Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

Licha ya kuuawa kwa majambazi hao, Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwakamatwa watu zaidi ya saba, wanaosadikiwa kuhusika na tukio la majibizano ya risasi na polisi, lililotokeo Vikindu lililosababisha kifo cha askari mmoja.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu, Simon Sirro alisema kabla ya kuuawa watuhumiwa hao walikamatwa katika maeneo tofauti ya Mbagala, Keko na Kawe jijini humo.

Alisema watu hao walikamatwa kufuatia tukio la ujambazi, lililotokea Agosti 29, mwaka huu katika Jengo la Sophia House maeneo ya Veta Changombe, ambapo majambazi hao walidaiwa kupora Sh milioni 35 na kutoweka kwa kutumia gari aina ya Toyota Noah lenye namba bandia T 549 BPK.

Aliongeza kuwa uchunguzi wa tukio hilo, uliendelea kufanyika na Septemba 3, timu ya upelelezi kutoka Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, iliweka mtego na kufanikiwa kuwakamata majambazi hao watatu na walipohojiwa walikiri kufanya matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha na kuweza kutaja silaha mbalimbali walizonazo.

Kamanda Sirro alisema majambazi hao, waliwapeleka askari eneo la Mbezi Chini katika nyumba waliyokuwa wamekodi na askari walifanya upekuzi na walifanikiwa kupata silaha mbalimbali, zikiwemo bunduki 23 na risasi zaidi ya 800 na vitu vinginevyo.

Alitaja silaha hizo kuwa ni bunduki za kijeshi tatu aina ya SMG zikiwa na magazini nane na risasi 120, bastola 16, magazini tatu za bastola na risasi moja, Shot gun pump action tatu na risasi 130, bastola 16 magazini na risasi 548 na bunduki tatu aina ya Shot gun na risasi zake 130.

Aidha alisema walikuta redio za mawasiliano 12 na chaja zake tatu, darubini za kuonea mbali tatu, pingu za plastiki 45, majaketi ya kuzuia risasi matatu, mkasi mmoja wa kukatia vyuma, mtarimbo mmoja, risasi baridi za kutishia 37, boksi moja la kusafishia silaha, nyundo kubwa moja, pingu za chuma tatu, mashine moja ya kuhifadhia kumbukumbu na magari mawili.

Alisema uchunguzi wao ulibaini kuwa majambazi hao Septemba 6, mwaka huu walipora bunduki aina ya Shot gun yenye namba 006091830, ikiwa na risasi moja katika barabara ya Mbozi Chang’ombe.

Sambamaba na hayo, majambazi hao walikiri kuhusika na wizi wa mamilioni ya fedha katika Benki ya Habib African ya Kariakoo mwaka 2014 na Benki ya Stanbic mwaka 2014, wakitumia gari aina ya Toyota Noah.

Kamanda Sirro alisema baada ya mahojiano zaidi, majambazi hao walisema wanazo silaha nyingine ambazo wamezificha Vikindu wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani. Ndipo askari walifuatana na watuhumiwa hao hadi kwenye msitu wa Vikindu.

Alisema askari walipofika eneo hilo, walilodai ni karibu na zilipo silaha hizo, walishuka kwenye gari na kuingia porini wakiwa wamewatanguliza watuhumiwa mbele majira ya usiku.

Aliongeza kuwa wakiwa msituni humo na askari wakiwa wenye tahadhari kubwa, ghafla walisikia milio ya risasi ikitokea mbele, ambapo askari walilala chini na baadaye zikisikika sauti zikisema ‘mmetuua sisi’.

Alisema baada ya risasi za mfululizo kutulia, askari walishuhudia majambazi hao ambao walichelewa kulala chini wakati risasi zikipigwa wakiwa wamejeruhiwa sehemu za kifuani na tumboni huku wakivuja damu nyingi.

Alisema askari walipiga risasi kuelekeza eneo zilikotokea risasi na walipoendelea kusonga mbele, walikuta silaha aina ya SMG ikiwa imetelekezwa na haikuwa na risasi ndani ya magazine, hivyo kufanya idadi ya silaha za SMG kufikia nne.

Aidha alisema askari waliwabeba majambazi hao na kuwapeleka kwenye gari kuelekea hospitalini, lakini wote walifariki dunia wakiwa njiani kutokana na kutoka damu nyingi. 

Akizungumzia tukio la Vikindu, Sirro alisema wamefanikiwa kuwakamata watu hao wanaosadikiwa kuhusika na tukio ambalo lilisababisha kifo cha askari mmoja.

“Majambazi hao walikuwa ni kundi la kama watu 14 na tayari tumewakamata zaidi ya saba ambao mpaka sasa tunawashikilia kwa mahojiano zaidi ili kufanikisha upelelezi,” alisema Kamanda Sirro.

Pia alisema kumekuwa na taarifa mbalimbali, zikisambazwa katika vyombo vya habari zikidai kuwa katika tukio la Vikindu, kuna askari anahusika na tukio hilo na kudai taarifa hizo si za kweli na hakuna askari aliyehusika katika tukio hilo.

Katika tukio lingine, jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wanne kwa makosa ya wizi wa magari manane, likiwemo gari moja la kibalozi. 

Kamanda Sirro alisema magari hayo yaliibwa jijini Dar es Salaam na kuuzwa kwa watu mbalimbali jijini hapo na mikoani na watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Sirro alisema katika tukio lingine jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa sita wanaodaiwa kuhusika na kuvunja nyumba usiku na kuiba. 

Alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa na mara upelelezi utakapokamilika watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili.

Mkurugenzi Ileje Haji Mnasi Atoa Onyo Kali Kwa Wasimamizi Wa Mitihani Ya Darasa La Saba

$
0
0
Na fredy mgunda,ileje
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi, amewaasa wasimamizi wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi kutofanya kazi kwa mazoea ili kutoruhusu mianya itakayowafanya wanafunzi wasiokuwa na uelewa kufaulu mitihani hiyo.
 
Alisema kumekuwa na baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika wanafaulu mithani hiyo kitendo kinachotia mashaka kwa wasimamizi hao kushindwa kunyakazi waliyopewa kwa makini.

Mnasi aliyasema hayo jana, wakati akitoa semina ya mafunzo kwa wasimamizi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje ambapo alisema usimamizi hafifu wa mitihani umesababisha kuwepo kwa watumishi wasiokuwa na uwezo kitaaluma.

Aidha kabla ya uteuzi wa Rais wa jamhuri ya muungazo wa tanzania Dr John Pombe Magufuli mkurugenzi huyo ambaye kitaaluma ni mwalimu alikuwa afisa elimu shule ya msingi manispaa ya iringa alisema iwapo ikibainika kufaulu kwa wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika mtuhumiwa wa kwanza kwenye uzembe huo atakuwa msimamizi wa mitihani na hatua kali zitachukuliwa zidi yake.
 
“Nawatahadharisha kwamba mnaweza mkarubuniwa kuwawezesha wanafunzi wasiokuwa na sifa wafaulu mitihani hiyo,kufanya hivyo ni kukiuka kanuni za usimamizi na uendeshaji wa mtihani na kuwaambia hayupo tayari kutumbuliwa na rais kwasababu za wasimamizi”alisisitiza Mnasi.
 
Hata hivyo Mnasi aliwataka wasimamizi hao kuwa makini katika kufanyakazi hiyo na kama kuna jambo lolote ambalo hawajalielewa kuhusu kazi hiyo ni vyema wakauliza ili kupewa majibu.
 
“hakikisheni kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo na kuwataka wasimamizi wote kufanya kazi yao kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.“Nawaasa wasimamizi  wa mitihani kujiepusha na vitendo vya udanganyifu kwani serikali itachukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani,” alisema Mnasi.

Mnasi alibainisha kuwa, serikali imezingatia uwezo wa kitaaluma, uadilifu na uaminifu hivyo wasimamizi hao kupewa jukumu la kusimamia mitihani hiyo muhimu ya kitaifa.

Aliongeza kuwa mitihani hiyo ni muhimu ili kuliwezesha taifa kupima kiwango cha elimu kilichpo nchini na kuwapata wasomi wa kiwango cha juu.

Nao wasimamizi wa mitihani hiyo wamemuahidi mkurugenzi huyo kuwa watasimamia mitihani hiyo kwa kufuata sheria na kanuni za usimamizi wa mitihani walizopewa.
 
Mitihani hiyo ya kuhitimu darasa la saba inatarajiwa kufanyika siku ya jumatano tarehe 07 /09 /2016 na alhamisi tarehe 08 /09 /2016.

Serikali Yakanusha Taarifa Inayosambazwa Katika Mitandao ya Kijamii Kwamba Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan Ameomba Kujiuzulu

$
0
0

Ofisi ya Makamu wa Rais inakanusha taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kwamba Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan, ameomba kujiuzulu nafasi yake na kwamba taarifa hiyo ni ya uzushi na uongo haina ukweli wowote.

Taarifa hiyo ni ya uchochezi inayolenga kuliweka Taifa kwenye taharuki.  Mhe. Makamu wa Rais yuko bega kwa bega na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya kazi zao kwa mujibu wa Katiba ya nchi ili kuwaletea wananchi maendeleo.

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka wananchi na Watanzania kwa ujumla kupuuza taarifa hiyo ambayo inalenga kupotosha umma kuhusu ushirikiano mzuri uliopo baina ya Viongozi wetu.

Mwisho, Ofisi ya Makamu wa Rais inawasihi Watanzania kufanya kazi kwa bidii na wajiepushe na vitendo vinavyolenga kuvuruga amani na utulivu nchini.

Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es Salaam

Tamko Rasmi la Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo kuhusu Hali ya Nchi kwa Sasa

$
0
0

1. Utangulizi

Jana Jumatatu, 5 Septemba 2016, Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo ilikutana katika kikao chake cha kawaida. Pamoja na mambo mengine, Kamati Kuu ilipokea, kujadili na kuidhinisha Taarifa kuhusu HALI YA NCHI. Taarifa hii sasa inatolewa rasmi kwa umma. Taarifa ipo katika maeneo makubwa manne: Hali ya kisiasa, hali ya kiuchumi, umoja wa kitaifa na hitimisho.

2. Hali ya Kisiasa
Kamati Kuu imezingatia kuwa Kikatiba, nchi yetu inafuata mfumo wa demokrasia ya vyama vingi. Katiba na Sheria mbalimbali zimeanisha utaratibu wa kazi na shughuli za vyama vya siasa. Ili kuhakikisha kwamba kazi na shughuli za vyama vya siasa zinakuwa endelevu, vyama vyenye kukidhi vigezo hupewa ruzuku kupitia Bajeti ya Serikali inayopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania.
 
Hata hivyo, katika awamu hii ya tano, Serikali ya Chama cha Mapinduzi imeamua kuzuia shughuli za siasa kwa kutumia nguvu ya Jeshi la Polisi na hata Jeshi la Wananchi. Kwa mujibu wa serikali ya CCM, shughuli za kiuenezi za vyama vya siasa kama vile mikutano ya hadhara, maandamano, makongamano, mijadala na hata mikutano ya ndani inapaswa kukoma mapema baada ya uchaguzi. 

Kisheria, huu ni uvunjifu wa Katiba na Sheria za nchi. Kisiasa, tunatambua kwamba Viongozi wa CCM wamepoteza mvuto kwa wananchi na sasa wanamsukuma Mwenyekiti wao Rais Magufuli kutumia jeshi katika kuokoa taswira ya Chama cha Mapinduzi mbele ya umma.
 
Kwa kuzingatia hali ya kisiasa nchini kwa sasa, Kamati Kuu ya chama chetu:
i) Tunalaani na kupinga kwa nguvu zetu zote hatua za Serikali ya Chama cha Mapinduzi za kuvunja Katiba na kujaribu kuweka pembeni utawala wa sheria.
ii) Tunapinga vitendo vinavyozidi kushamiri katika serikali hii ya CCM ya kujaribu kuendesha nchi kwa ubabe na matamko ya viongozi badala ya utawala wa sharia.
iii) Tutasimama imara, na tutaungana na vyama vingine vya siasa pamoja na taasisi zingine za kiraia katika kulinda mfumo wa demokrasia ya vyama vingi, uhuru wa maoni, na utawala wa sheria katika nchi yetu

3. Hali ya Kiuchumi​
Katika miaka 10-15 iliyopita, nchi yetu imejenga uchumi ambao umekuwa ukikua kwa kiwango cha asilimia 6-7 kwa mwaka katika kipindi chote hiki. Ukuaji huu wa uchumi ulitokana na juhudi za nchi katika kuvutia wawekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji mali kwa wananchi wenye kipata cha chini. Awamu ya tano ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi imerithi changamoto ya uchumi unaokua bila kuwafaidisha wananchi wa kawaida. Hili ndilo tulitegemea Serikali mpya ishughulike nalo.
 
Kamati Kuu imeshtushwa na hali ya kuanza kudorora kwa shughuli za uchumi katika kipindi cha miezi kumi ya utawala wa awamu ya tano. Kwa mfano:
a) Taarifa za Benki Kuu zilizopo kwenye tovuti yake (Quarterly Economic Review na Monthly Economic Review) kwa robo ya mwisho ya mwaka 2015 (Oktoba - Desemba 2015 ) zinaonesha kuwa kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa 9%. Katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 (Januari - Machi 2016) kasi ya ukuaji wa Pato la Taifa ilishuka hadi kufikia 5.5%. Kiuchumi, hii inamaanisha kuwa ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo ya utawala wa awamu ya tano chini ya Rais Magufuli umepungua kwa 4%.
 
b) Shughuli za uchumi zinazohusu wananchi masikini zimeshuka kutoka kasi ya ukuaji ya 10.20% robo ya mwisho ya mwaka 2015 mpaka 2.7% katika robo ya kwanza ya mwaka 2016, ikiwa ni punguzo la 8% ndani ya kipindi kisichozidi miezi sita. Hii ina maanisha kwamba Wananchi wetu wanazidi kudumbukia kwenye ufukara kwa kasi tangu awamu ya tano ya Serikali ya Chama Mapinduzi iingie madarakani
 
c) Ukuaji wa sekta ya ujenzi katika robo ya mwisho ya mwaka 2015 ilikuwa 13.8% lakini ukuaji wa sekta hii katika robo ya kwanza ya mwaka 2016 ilikuwa ni 4.30%, ikiwa ni tofauti ya takribani -10%. Hii ni kwa sababu uwekezaji katika sekta hii umeanza kushuka.
 
d) Kasi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji imeporomoka kutoka kukua kwa 14.50% robo ya mwisho ya 2015 mpaka kukua kwa 7.9% robo ya kwanza ya 2016, ikiwa ni kuporoka kwa 7% katika kipindi cha miezi 6 tu ya kwanza ya utawala wa Rais Magufuli. Kuporomoka kwa sekta ya usafirishaji itaathiri watu wengi, wakiwemo madereva, matingo, pamoja na mama Ntilie wanaowauzia chakula. .
 
Kwa kuzingatia mwenendo wa hali ya uchumi katika nchi, Kamati Kuu:
a) Tunaitaka serikali izingatie sayansi ya uchumi katika kuendesha uchumi wa nchi. Uamuzi wa CCM wa kuitelekeza serikali yake kwa mwanasiasa mmoja anayedhani ndiye anayejua kila kitu na yeye kugeuka kuwa mshauri wa washauri wa uchumi itasambaratisha uwekezaji nchini na kuua kabisa juhudi za miaka 20 za kuvutia wawekezaji na kujenga uchumi shirikishi.

b) Inahimiza wananchi kuzingatia kuwa msingi wa uchumi wetu ni uwekezaji kutoka ndani na nje ya nchi. Msingi wa kuvutia wawekezaji ni utawala wa sheria. Juhudi za serikali ya CCM za kuua utawala wa sheria zitaua uwekezaji na kuangamiza uchumi wa nchi. Tusirihusu CCM iue uchumi wa nchi kwa maslahi yake ya kisiasa na viongozi wake.

4. Umoja wa Kitaifa
Nchi yetu imefanya juhudi kubwa katika miaka 50 iliyopita katika kujenga umoja na mshikamano wa kitaifa kwa kuhakikisha kuwa makabila, dini na baadaye vyama vya siasa tunaishi bila kukamiana. Juhudi za dhati za kupambana na ubaguzi ndiyo umekuwa msingi imara wa kujenga Umoja wa Kitaifa na amani tunayojivunia.
 
Hata hivyo, Kamati Kuu imezingatia kuwa utawala mpya wa Serikali ya CCM, kupitia Mwenyekiti wake mpya na Rais wa Jamhuri wa Muungo, umeanza kwa juhudi na kasi kubwa kuchokonoa na kumomonyoa misingi ya utaifa na umoja wetu. Sasa tunaye Rais asiyechagua maneno na asiyejua aongee nini na wapi. Vijana waliosoma kwa bidii katika mazingira ya shule zilizotelekezwa na serikali ya CCM anawaita VILAZA. 

Katikati ya uhasama mkubwa wa kisiasa na kijamii huko Zanzibar Rais wetu amefunga safari, sio kujaribu kutibu majeraha yaliyosababishwa na kuchezewa kwa sanduku la kura, bali kuchochea uhasama chini ya ulinzi wa vyombo vyetu vya dola vyenye jukumu la kulinda na kudumisha amani. Sasa Rais wetu, kupitia kauli zake, ameanza kuubomoa muungano wetu uliojengwa kwa unyenyekevu na katika mazingira magumu. 

Kila asimamapo kuhutubia, jambo moja la kutarajiwa kutoka katika kinywa cha Rais wetu ni matamshi yanayodhoofisha nguzo fulani ya umoja, mshikamano na undugu wetu kama taifa. Yote haya yakitokea chama chake cha CCM ama kimekaa kimya au kinachekelea. 

Inasikitikitisha kwamba Chama kilichoasisiwa na Mwalimu Nyerere kinamruhusu kiongozi wake kubomoa misingi ya umoja wa kitaifa na kuchochea chuki katika jamii ya watanzania.
 
Kwa kuzingatia mtikisiko mkubwa katika umoja na mshikamano wa kitaifa unaoendelea nchini, Kamati Kuu:
a) Tunalaani juhudi zinazofanywa na Serikali ya CCM kupitia Mwenyekiti wao za kuchochea chuki katika jamii ya watanzania na kubomoa misingi ya umoja wa kitaifa na amani ya nchi
b) Tunatoa wito kwa watanzania wote waipendayo nchi yao kusimama kidete katika kulinda misingi ya nchi yetu na kukataa chuki inayoanza kujengwa na utawala wa CCM
c) Tunatoa wito wa kipekee kwa viongozi wetu wa dini na wakuu wa nchi waliopita, hususani Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na Mzee Jakaya Mrisho Kikwete, pamoja na wazee wengine wanaoheshimika katika nchi yetu wavae ujasiri wa kumuonya Mwenyekiti wa CCM kuwa juhudi zake za kuchochea chuki katika jamii yetu ya watanzania zitasambaratisha Taifa letu.

5. Hitimisho

i) Sisi kama chama cha siasa, tunaendelea kusisitiza kuwa tutaunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kupambana na ufisadi na kujenga uwajibikaji nchini.
ii) Tunaamini kwa dhati kabisa kuwa kuheshimu na kulinda demokrasia na kuzingatia utawala wa sheria nidyo msingi wa mapambano dhidi ya ufisadi. Tunasisitiza kuwa mtu yeyote, wa kawaida au kiongozi, anayesema kwamba anaweza akapambana na ufisadi kwa kukanyaga misingi ya demokrasia na utawala wa sheria mtu huyo ni mwomgo na kwa kweli ni fisadi na anataka kujenga himaya mpya ya ufisadi. Mtu huyo, pamoja na mambo yake yote, yafaa akataliwe na kudharauliwa haraka!
 
iii) Tunasisitiza kuwa msingi wa uchumi wetu ni kuvutia uwekezaji wa ndani nan je ya nchi. Kuzingatia utawala wa sheria ndiyo msingi wa kuvutia uwekezaji. Juhuzi za hivi karibuni za serikali ya CCM za kujaribu kuua utawala wa sharia ni juhudi ovu za kuua uchumi wa nchi yetu. TUZIKATAE juhudi za kuua utawala wa sheria kwa kuwa zitaangamiza taifa letu kiuchumi, kisiasa na kijamii.


Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto, Mb

Kiongozi wa Chama
Dar es Salaam, 
Jumanne 6 Septemba 2016.

Rais Magufuli atoa siku 7 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kumaliza deni wanalodaiwa na NHC

$
0
0


Na: Lilian Lundo- Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa siku 7 kwa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kulipa deni la bilioni 2 ambalo wanadaiwa na Shirika la nyumba la Taifa (NHC).

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo kwa Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Injinia Joseph Nyamhanga leo jijini Dar es Salaam katika ziara ya kushtukiza ya kuangalia ujenzi wa hosteli za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Nawapa siku 7 muwe mmelilipa hilo deni huku mkiendelea na utaratibu wa kuhamia Dodoma, kama hamtalilipa kwa wakati nitawaagiza NHC kuwatolea vitu vyenu nje kama wanavyofanya kwa wengine,” alisema Dkt. Magufuli.

Amesema kuwa kiwango hicho cha bilioni 2 kingeiwezesha wizara hiyo kujenga ofisi za wizara kwa kuwatumia Wakala wa Majengo (TBA) ambao wako chini ya wizara hiyo badala ya kutumika kama kodi ya pango.

Aidha, ameitaka wizara hiyo kuhamia Mjini Dodoma mara tu watakapokamilisha deni hilo na kutoendelea kupanga jijini Dar es Salaam, kwani hakuna sababu ya kuendelea kupanga majengo ya ofisi Dar es Salaam wakati Serikali yote inahamia Dodoma.

Wakati huohuo, Rais Dkt. Magufuli ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Tecknolojia, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano pamoja na  Wakala wa Majengo (TBA) na uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kusimamia  vizuri mradi wa ujenzi wa hosteli za chuo kikuu ambao Rais mwenyewe aliahidi shilingi bilioni 10 katika ujenzi huo, bilioni 5 imekwishatolewa na bilioni nyingine 5 itatolewa ndani ya wiki hii.

Hosteli hizo zinategemea kuchukua wanafunzi 4000 ambapo itapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la wanafunzi kukaa nje ya maeneo ya chuo.

Wakazi wa Magome Kota kuishi miaka 5 kwenye nyumba za kupanga bila kulipa kodi .....Wanaodaiwa na NHC Wapewa Siku 7

$
0
0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota kukaa kwenye nyumba za Serikali miaka mitano bure na baadaye kuzinunua kwa bei nafuu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia wakazi wa Magomeni na kuagiza ujenzi wa nyumba hizo kuanza ndani ya miezi miwili.

“Nasema wakandarasi ndani ya miezi miwili waanze kujenga nyumba 644 kwa ajili ya wazee ambao wameteseka sana baada ya nyumba zao kuvunjwa, nitatoa fedha Serikalini mwezi huu kwa ajili ya kuanza kwa shughuli hiyo” alisema Dkt. Magufuli.

Ameongeza kusema kuwa ujenzi huu anataka ukamilike ndani ya mwaka mmoja au miezi sita kama ulivyokuwa kwa hosteli za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Rais Magufuli amesema atafurahi kukabidhi hati kwa wakazi wa Magomeni Kota pindi nyumba hizo zitakapokuwa zimekamilika.

“Namuomba Mwenyezi Mungu anipe uzima ili nyumba hizo zikiwa tayari hati nizikabidhi mwenyewe,”alisema Magufuli.

Rais Magufuli ameonyesha kukerwa na vitendo vya baadhi ya watumishi wa Serikali wasio waaminifu kuwanyima haki wanyonge. Amesema vitendo hivyo vya unyanyasaji viishe mara moja na watanzania wakae kwenye nchi yao kwa amani.

Aidha, Rais Magufuli amemwagiza Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Mchechu kukusanya madeni yote ya kodi kwa wanaodaiwa na shirika hilo bila kujali chama, serikali au mtu yeyote.

Ameagiza kuwa wanaodaiwa inabidi walipe deni lao ndani ya siku 7 (saba) vinginevyo waondolewe kwenye nyumba hizo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Lukuvi amemshukuru Rais Magufuli kwa kuwajali wanyonge hasa kwa kutatua mgogoro wa makazi kwa wakazi wa Magomeni Kota.

“Mheshimiwa Rais ninakushukuru kwa kuwajali wazee hawa wa Magomeni, nami nilitekeleza maagizo yako na kufuatilia mgogoro huu hadi kupata ufumbuzi”, alisema Lukuvi.

Lukuvi amesema kuwa mgogoro wa Magomeni ulivyokuwa mkubwa ulistahili nguvu ya Mhe. Rais Magufuli, lakini kwa migogoro mingine ambayo ni midogo, hiyo ameishughulikia na ataendelea kuishughulikia ili kero za wananchi kuhusu ardhi ziishe kama alivyoagizwa na Rais.

Nyumba zilizokuwa Magomeni Kota zilivunjwa mwaka 2009 na wananchi wakaahidiwa kujengewa nyumba ambazo wangeuziwa kwa bei nafuu. Lakini kwa takribani miaka mitano nyumba hizo hazikujengwa hali ambayo iliwafanya wakazi hao waishi maisha ya kuangaika.

Hivi karibuni Mhe. Rais John Pombe Magufuli alifuta hati zote za umiliki eneo la Magomeni Kota na kuondoa usimamizi wa Nyumba TAMISEMI na kuupeleka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili ya kuanza kusimamia ujenzi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Mwenyekiti wa waliokuwa wakaazi wa  nyumba za Magomeni Kota  Bw. George Abdi wakati alipotembelea na kuongea na wakaazi hao wa  Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli  akimfariji  Bi. Mwajuma  Sama  kwa taabu walizopata  yeye kiongozi na wakaazi wenzie  wa   Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimshukuru wakili Twaha Taslima wa Law Chambers kwa kusimamia vyema maswala ya mgogoro wa eneo iliyokuwa Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo Septemba 6, 2016. PICHA NA IKULU

Taarifa ya spika Job Ndugai kuhusu Rais Magufuli kupitisha miswada mitano

$
0
0

Na Eleuteri Mangi-Maelezo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia na kusaini Miswada mitano kutumika kama Sheria kamili za nchi.

Hayo yamesemwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai mara baada ya kufungua Mkutano wa nne wa Bunge la 11 leo mjini Dodoma.

Miswada iliyoidhinishwa na Rais ni pamoja Sheria ya Fedha na Matumizi ya mwaka 2016, Sheria ya Fedha namba 2 ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali ya mwaka 2016, Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbambali namba 2 na 4 ya mwaka 2016 na Sheria ya Marekebisho ya Ununuzi ya Umma namba 5 ya mwaka 2016.

Aidha, Mhe. Spika amewakumbusha Wabunge kusoma na kuelewa kila kinachokuja Bungeni ili waweze kutekeleza majukumu yao ya kibunge ipasavyo kwa niaba ya wananchi waliowatuma kufanya kazi hiyo ili kuwaletea maendeleo.

Wabunge wametakiwa kutekeleza majukumu hayo ya uwakilishi wa wananchi ili waweze kujadili masuala mbalimbali kwa kuzingatia haki, ustahimilivu, busara, hekima na kutumia lugha ya staha katika mijadala ya Bunge.

Vile vile Mhe. Spika amempongeza Naibu Spika Dkt. Tulia Akson kuongoza vema mkutano wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19 na kumalizika Juni 30 mwaka huu kwa kushirikiana na wenyeviti wa Bunge Andrew Chenge, Mussa A. Zungu na Najima Giga.

Katika hatua nyingine Mhe. Spika amemshukuru Rais Dkt. Magufuli, Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watanzania wote walimuombea alipokuwa kwenye matibabu nje ya nchi pamoja na Madaktari waliomhudumia akiwa kwenye matibabu na kumshukuru Mungu kwa kumwonesha upendo alipokuwa kwenye mapito ya kuugua.

Katika mkutano huo wa Bunge yameulizwa maswali 14 ambayo yalielekezwa kwenye Wizara mbalimbali na kujibiwa kwa llengo la kutolea ufafanuzi masuala yanayotekelezwa kwa Serikali.

Jeshi la Magereza lawasilisha taarifa za utekelezaji wa sheria ya Bodi za Parole kwa Agustino Lyatonga Mrema

$
0
0
Jeshi la Magereza nchini limekabidhi rasmi ripoti ya taarifa ya utekelezaji wa sheria ya bodi za Parole kwa Mwenyekiti wa bodi hiyo Taifa, Agustino Lyatonga Mrema ikihusisha uelewa na elimu juu ya mambo ya Parole.

Tukio hilo limefanyika mapema leo Septemba 6.2016 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi hilo la Magereza Jijini Dar es Salaam.

Kamishna Jenerali wa Magereza ambaye pia ni Katibu wa Bodi ya Parole ya Taifa, Bwana John Casmir Minja aliwasilisha taarifa hiyo ambapo imebeba maudhui mbalimbali ikiwemo ya kujenga uelewa juu ya Parole kama sheria  ya Parole na utekelezaji wake.

Hii ni pamoja na sifa za mfungwa wa Parole, muundo wa bodi ya taifa, kitaifa na bodi za ngazi ya mikoa. Utendaji wa kazi kwa bodi ya Taifa ya Parole na bodi za ngazi ya mikoa, mafanikio na changamoto ya bodi ya Parole kitaifa na katika ngazi ya mikoa.

“Nimeipokea taarifa yenu ya bodi ya Parole na mimi kama Mwenyekiti nitahakikisha panapo tatizo tunasaidiana. Na yale magumu kama tatizo la bajeti ya kuhakikisha Parole haikwami nitaiwasilisha mimi mwenyewe kwa Rais John Pombe Magufuli” amesema Mrema

Ameongeza kuwa: “Kama hakuna pesa tusitegemee miujiza kwa Parole kufanya kazi na hii ni kutokana na ufinyu wa bajeti. Lakini labda tu nieleweshe jamii kwamba nilipopewa kazi ya kuwa mwenyekiti wa bodi ya Parole ya Taifa watu walidhani kwamba nakwenda magereza halafu nifungue milango wafungwa watoke, Hapana si hivyo, hili jambo lina mchakato mkubwa na mrefu,” ameongeza Mrema

Aidha Dkt.Mrema ametoa rai kwa jamii kuepuka kufanya uhalifu na kusema kuwa Magereza si mahala pazuri kupeleka nguvu kazi ya Taifa

“Magereza si mahala pazuri  kwakweli, ni sehemu mbaya amabyo mtu anatakiwa aende kwa bahati mbaya tu.la muhimu ni kuwa jamii iepukane na vitendo vya uhalifu kwani nguvu kazi ya Taifa inapotelea jela”

Katika suala lingine Dkt. Mrema amewataka wananchi hususani vijana kuachana na makundi yanayohamasisha migomo na maandamano yasiyo na tija kwenye Taifa

“Labda tu niseme kwamba kufanya maandamano ya Lazima ni uhaini. Wenyewe wanayaita maandamano yasiyo na kikomo, hayo ni uhaini niwaombe wananchi wote hususani vijana waache kutumika na makundi yanayohamasisha maandamano dhidi ya serikali na uongozi uliopo madarakani” amesema Mrema

..hivi sasa mitaani kwetu kuna wafungwa watarajiwa wengi na mahabusu watarajiwa wengi hvyo wazazi wakanyeni vijana wenu wasijihusishe na vitendo vya uhalifu vitakavyowapelekea kwenda gerezani” amemalizia Dkt. Mrema.
Afisa wa Jeshi la Magereza (aliyesimama kushoto) akisoma taarifa ya utekelezaji wa sheria ya bodi ya parole kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema (wa kwanza kulia) wakati Mwenyekiti wa Bodi alipomtembelea Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja (katikati) mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja akimkaribisha Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipomtembelea ofini kwake ili kujua matatizo mbalimbali yanayoikabili bodi hiyo mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akiagana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini ambaye pia ni Katibu wa bodi ya Parole John Casmir Minja wakati Dkt. Mrema alipomtembelea ofisini kwake mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Picha na Eliphace Marwa

Habari Zilizopo Katika Magazeti Ya Leo Jumatano ya Septemba 7

Rais Magufuli apokea ujumbe kutoka kwa Rais Salva Kiir na Rais Nkurunziza

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit amemtumia ujumbe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimuarifu kuwa hali ya usalama katika nchi hiyo imeanza kutengemaa.

Rais Salva Kiir Mayardit amewasilisha ujumbe huo kupitia kwa Mjumbe wake Maalum Mhe. Aggrey Tisa Sabuni ambaye pamoja na kuwasilisha ujumbe huo amesema Sudani Kusini imekamilisha nyaraka za azimio la kuridia mkataba wa kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki ambao umewasilishwa jana tarehe 05 Septemba, 2016 katika makao makuu ya Jumuiya Jijini Arusha.

Mhe. Aggrey Tisa Sabuni amesema Sudan Kusini ipo tayari kushirikiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika masuala mbalimbali yenye manufaa kwa wananchi ikiwemo biashara na uwekezaji na kwamba ni matumaini yake kuwa itapata ushirikiano mzuri.

Kwa upande wake Rais Magufuli ameelezea kufurahishwa kwake na taarifa za kutengemaa kwa hali ya amani nchini humo na kwamba ni matarajio yake kuwa Sudan Kusini itajikita katika maendeleo ya wananchi wananchi wake.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amepokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Pierre Nkurunziza ulioletwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo Mhe. Aime Laurentine Kanyana.

Katika ujumbe huo Rais Nkurunziza amesema hali ya Burundi ni shwari na kwamba wananchi wa Burundi wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.

Kwa upande wake Rais Magufuli amesema Tanzania yenye wakimbizi takribani 200,000 wa kutoka Burundi inafurahishwa na taarifa za kuwepo hali ya amani nchini humo.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

06 Septemba, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais wa Burudi uliowasilishwa kwake na Aime Laurentine Kanyana Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU

Serikali Yaendelea Kutatua Changamoto Mbalimbali Za Wananchi

UVCCM Wamtetea Rais Magufuli........Wasema Hotuba Yake Aliyoitoa Zanzibar Imezika upotoshaji wa siasa uchwara

$
0
0
UMOJA wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umesema Rais John Magufuli, hana baya alilolitamka katika mikutano yake ya Unguja na Pemba, bali amezika upotoshaji wa siasa uchwara, kusafisha upepo mchafu na kufumba vinywa vya wanasiasa wakorofi na wazushi.

Pia umetoa mwito kwa Wazanzibari kwa nguvu zote kupinga siasa chafu au zenye lengo la kuwagawa, kuwatenganisha au kuwahasimisha badala yake watambue umuhimu wa kuendeleza umoja, amani na maendeleo ya kiuchumi na kijamii.

Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, Shaka Hamdu Shaka alisema hayo ofisini kwake Makao Makuu ya CCM, Dodoma, alipotakiwa kueleza maoni yake kuhusu shutuma anazotupiwa Rais Magufuli ikidaiwa na baadhi ya wanasiasa kwamba alilenga kuamsha joto la mtafaruku wa kisiasa visiwani humo.

Shaka alisema hotuba ya Rais Dk Magufuli imezima siasa za uzushi na dhidi ya viongozi wanaowadanganya wafuasi wao kwamba utafanyika Uchaguzi Mkuu mwingine kabla ya mwaka 2020 na Rais Ali Mohamed Shein ataondoka madarakani ili kumpisha Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.

Shaka alisema hotuba ya Rais ilikuwa yenye mashiko na maudhui, makatazo, maonyo, maelezo na wosia uliojiegemeza katika kudumisha amani nchini.

“Kuhubiri amani ni dhamana yake kiutawala, kuwaonya wananchi wanaokata mikarafuu, kutoboa mitumbwi, kufyeka mazao mashambani na wengine kukataa kuwauzia bidhaa wenzao halikuwa kosa na si jambo baya kama inavyoelezwa na wazushi wa kisiasa,” alisema Shaka.

Aidha, alisema ikiwa kuna mwanasiasa asiyemtii Rais aliye madarakani Zanzibar na hata kukataa hata mkono wake, hakuna sababu kwa kiongozi huyo kutaka msaada kwenye serikali asiyoitambua.

“Iweje baniani mbaya kiatu chake dawa, unajigamba humtambui Rais aliyeshinda na kuunda serikali ila unadoea fedha zinazokusanywa na serikali usioitambua ili usaidiwe na kulipwa marupurupu. UVCCM inaunga mkono SMZ kumnyima stahili zote hadi atakaipomtambua Rais,” alisema Shaka.

Kaimu Katibu Mkuu huyo alisema wakati wa utawala wa Dk Salmin Amour Juma, Maalim Seif aliposema hamtambui kama mshindi halali hakuwa akilipwa chochote, Rais mstaafu Amani Abeid Karume hakumlipa kitu hadi alipojipeleka Ikulu Novemba 5, 2009 akatangaza kuitambua serikali yake.

Alisema matamshi ya Dk Magufuli katika hotuba zake zote, ameweka bayana kila kitu, amewakanya wanasiasa wachochezi na hatarishi kwa amani, amewaonya viongozi katika serikali zote huku akikataa uzembe, urasimu, ubadhirifu wa mali za umma na kusema wote wasiotosha, wajipime iwapo bado wanafaa au la.

Afikishwa Mahakamani kwa Kumtisha Rais Magufuli Kupitia Mtandao wa Watsapp

$
0
0
Mfanyabiasha  Leonard Materu (31) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashitaka ya kutuma ujumbe wa kumtishia Rais John Magufuli kupitia mtandao wa WhatsApp.

Materu ambaye ni mkazi wa Moshi Bar Kwadiwani, alifikishwa mahakamani hapo jana na kusomewa mashitaka yake na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi Magreth Bankika.

Akisoma mashitaka Wakili Diana alidai, mshitakiwa huyo amefunguliwa kesi hiyo ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa WhatsApp chini ya Sheria ya Mtandao ya mwaka 2015.

Ilidaiwa kuwa, Julai 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam, Materu aliandika ujumbe wenye lengo la kudanganya umma kupitia WhatsApp ukisomeka; “Magu ajiandae tunaenda kupindua mpaka Ikulu.”

Inadaiwa kuwa maneno hayo yalikuwa na lengo la kumtishia Rais John Magufuli. Baada ya kusomewa mashitaka, mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo, na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika na kuomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Mshitakiwa aliachiwa kwa dhamana baada ya kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja alisaini hati ya Sh milioni tano. Kesi itatajwa tena Septemba 20, mwaka huu.

Tecno Phantom 6 Mpya Kuja Na Saizi Tofauti

$
0
0
Watumiaji wa smartphone au maarufu Simu-Janja ni watu makini sana linapokuja suala la ukubwa wa simu, mwenendo wa masoko kwa sasa unaonyesha wanunuaji wengi wa simu wanavutiwa sana simu zenye kioo kipana.
 
Lakini sio wapenzi wote wa simu wanatamani simu zenye kioo kipana, watumiaji wengine wanapenda simu zenye ukubwa wa wastani. Fununu zilizotapakaa ni kuwa TECNO wanakuletea simu mpya Phantom 6 ambayo pia itakuja na matoleo mengine kama Phantom 6 Plus na Phantom 6 mini.

Fununu hizi zinaweka wazi kwamba watengenezaji hawa wakubwa wa simu za mkononi wana mkakati kabambe wa kuwavutia watumiaji wakubwa wa simu kununua matoleo haya mapya yanayotarajiwa kutoka Septemba hii pindi TECNO Phantom 6 itakapazinduliwa.

HAKUNA SHAKA JUU YA UKUBWA WAKE
Jambo hili linatia moyo huku TECNO ikiwekwa bayana katika uvumi unaosambaa angalau kwa vidokezo na muonekano ambao unasemekana ni rasmi Tecno Phantom 6 itaboreshwa zaidi na wala haitopunguziwa sifa zake kuu. 

Nafikiri hili ni jambo la kufurahisha sana kwa sababu mara nyingi tumekuwa tukiona makampuni mengi ya simu yakiwauzia wateja wao simu zenye uwezo mdogo katika maduka yao makubwa wakitumia jina la makampuni yanayobamba kwa kuuza simu. Watumiaji wengi wa simu siku hizi wako makini sana na hawadanganyiki kirahisi.

PHANTOM 6 NA MATOLEO MAPYA YA TECNO YATAKUWA NI GUMZO?
Watengenezaji hawa wakubwa wa simu za TECNO wamekuwa wakipambana kuweka toleo lao bora kabisa kwenye mauzo kuanzia Phantom A+ mpaka Phantom Z au Z mini, Phantom 5 na sasa Phantom 6. Swali linalobaki ni je, phantom 6 itabadilisha mtazamo wa baadhi ya wananuaji wa simu?
 
Unadhani wpenzi wa Smartphones wataanza kuiona Phantom 6 kama moja ya toleo la kipekee kama inavyotarajiwa na wengi? Na inasemekana kuwa Phantom 6 ama 6 + itakamata soko kubwa kipindi hiki endapo toleo zitambulishwa kwa upekee kwa wakati muafaka.

Mbali na fununu zote hizi tunasubirri kuona toleo rasmi la Phantom 6 kuzinduliwa ifikapo Septemba.  Endapo unahitaji taarifa zaidi unaweza kutembelea mitandao ya kijamii ya Tecno kama ilivyoorodheshwa hapa chini.
 
 
 

RIWAYA: Sorry Madam - Sehemu ya 39 & 40 (Riwaya inawafaa kuanzia miaka 18 na kuendelea )

$
0
0

Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa

Ilipoishia...

Na jinsi ninavyo ogelea kwenda mbele ndivyo jinsi papa aliyozidi kunikaribia na safari hii akajitokeza vizuri na kuhakikisha kweli ni papa samaki mwenye meno makali ya kumrarua binadamu anaye ingia kwenye kumi na nane zake ndio anaye nifwata kwa mwendo wa kasi na kujikuta nikipiga picha ya jinsi atakavyo nirarua pamoja na huyu msichana mdogo

Endelea...

....Gafla nikasikia milio mingi ya risasi iliyoanza kunichanganya hata mfumo wa kuogelea ukabadilika nikatamani maji ya bahari yabadilike na kuwa mchanga ili miguu yangu ipate uwezo wa kukimbia ila hikuwa hivyo zaidi ya milio kuzidi kuongezeka kwa kasi ya ajabu na kwakiweza sikujua hata ni wapi inapo tokea,maji yakabadilika na kuanza kuwa na rangi nyekundu nikageuka nyuma na kukutana na boti iliyo wabeba watu wapatao wanne wenye bunduki na pembeni nikamuona papa aliyekuwa akinifwata akielea elea juu ya maji akiwa amekufa.

Jamaa wenye boti yao wakaisogeza hadi pembeni na kunitazama kwa muda kisha wakanipa mkono na kunivuta kwa nguvu huku buinti mdogo akuwa mgongoni,wakanipa kitaulo cha kujifunga na kunza kumfwata mama ambaye tayari alisha fika mbali kutoka sehemu ambayo nilikuwepo mimi.Jamaa mmoja alizungumza na simu na sikuielewa luga yake kutokana anazungumza kikabila kisha akakata simu.Wakaisogeza boti yao hadi alipo mama na wakamvutia ndani ya maji.Nikawaona jamaa wakinong’onezana na kisha wakagongeana mikono ikatubidi mimi na mama tutazamane.

“asanteni ka masaada wenu”
Mama alizungumza huku akiwatazama usoni
“musijali kwa hilo”
Jamaa wakaonekana kutawaliwa na furaha ambayo hadi wakati huu sikujua ni ya nini
“mbona munafurahi?”
“tunafurahi kwa maana tumesha kuwa ni matajiri”
“matajiri wa nini?”

“kuna tangazo lilikuwa linatolewa kwa mtu atakaye fanikisha kukupata wewe atapewa dola milioni mbili za kimarekani na baba yako na sasa ni mwezi wa tatu ndio sisi tumekupata”
Nikatabasamu ila ikawa ni tofauti kwa mama ambaye nahisi kuwa anajua ni mume wake mzee godwin
“eddy waambie wanipige risasi ili nife sipi tayari kurudi tena mikononi mwa baba yako”
“mama sio baba wa tanzania?”

“unataka kusema wewe baba yako yupi huyo mwenye roho ya kibinadamu atakaye toa pesa yake ili amzawadie mtu?”
“mama sio baba unaye mjua wewe…tambua kuwa ukweli wote ninauju na ninamshukuru mungu kuwa nimempata baba yangu ambaye yeye ndio damu yeke japo amepitia yaliyo mengi ila ninamshukuru mungu yupo hai”

Mama akabaki kimya huku macho yake yakiwa chini akimtazama mtoto tuliye mlaza chini,tukaona boti nyingine kubwa ikija na kusimama karibu na sehemu ilipo boti hii ndogo,wakatuwekea kingazi na tukaanza kupanda na kuingia kwenye boti kubwa iliyo kuja na jamaa watatu wakingia na kumuacha mwezao mmoja kwenye boti ndogo.Ndani ya boti wakatupa makoti makubwa kwa ajili ya kuzui baridi kali iliyo kuwa ikitukung’uta.

Wakampa msichana mdogo huduma ya kwanza na sisi wakatupatia vyakula na chai ya moto kutoa njaaa tumboni.Mimi wakanihudumia kwenye sehemu niliyo jeruhiwa na jiwe kisha wakanipa suruali mpaya,nikavua kitaulo nilicho pewa na kuivaa suruali hii.Boti ikazidi kusonga mbele huku moyoni mwangu nikijawa na amani tele ya kuweza kumpata mama yangu na kilicho salia ni kuwaunganisha baba mzazi na mama.

“samahani kaka nyinyi ni kina nani?”
“sisi ni wavuvi wa samaki wakubwa sasa yule papa tuliye muua tulikuwa tunamkimbiza alitusumbua sana na pale tumemuacha yule mwezetu akilinda sisi tutamrudia kumchukua na boti nyingine”
“sawa”

Tukafika ufukweni na jamaa wakatupeleka kwenye moja ya hotel isiyo mbali sana na bahari na kutuchukulia chumba,wakamchukua daktari maalumu na kuja kutuhudumia.Tukakaa hotelini kwa wiki moja tukijitahidi kuirudisha miili yetu katika afya zake za kawaida kwani kwa muonekano tulio nao ninaweza kujifananisha na misukule.Mudu wa wiki moja kukatika afya yangu ikarejea kama awali japo sio sana ila kidogo niliweza kusimama mbele ya mtu au watu na kujiona ni mtu.

Gharama zote zikalipwa na mama kutokana na kuwa na akaunti yake ya siri iliyopo huku afrika kusini na kwakipindi chote hatukuwasiliana na mtu yoyote zaidi ya jamaa walio tuokoa ambao nao mama aliwakanya wasizungumze ummbea wa aina yoyote kwa mtu yoyote ili waweze kupata donge lao nono wanalo lisubiria kwa hamu kubwa kutoka kwa baba yangu mzazi

Msichana mdogo alilazwa kwenye moja ya hospitali na madaktari wanaendelea na juhudi za kuweza kumtibu kama ataweza kuzungumza tena ili awe miongoni mwa mashaidi wa kumuhukumu baba mzee godwin katika kesi ya kuwatumikisha watu kikatili na kuwakatili katika kuzungumza nao.

“mama unampango gani na baba?”
”nitahakikisha ninamfunga hadi magereza yanabomoka”
“sawa mama je baba yangu mzazi naye una mpango gani naye?”
“mmmm sijui hata ni wapi nitaanzia kwa maana kwa niliyo mfanyia baba yako kidogo yananipa hata ugumu wa kusema ninaanzi wapi”

“ninafurahi kusikia hivyo mama ila kwa hilo ninaomba uniachie mimi kwa maana baba ananipenda sana”
“ila eddy roho yangu imejawa na dukuduku kubwa ambalo sielewi siku ninamkamata godwin nitamfanya kitu gani?”
“hilo mama wala lisikutie mawazo sana cha msingi ni kuweza kumuomba msamaha baba yangu ili kama ni maisha yaweze kuendelea kwa amani”

“sawa mwanangu nitafanya hivyo”
“je umewasiliana na serikali ya tanzania?”
“mmmm siwezi kufanya hivyo kwanza kutokana huwezi jua baba yako ana mtandao mkubwa kiasi gani ila nitarudi kimya kimya”
“hapo umesema ila yule daktari wako ni mnoko sana na kama unaweza awe miongoni mwa watu wa kushuhulikiwa”
“kwa nini?”

“ana vitu vingi sana ambavyo wewe ukimuambia humuambia baba,kwa mfano swala la kuwa mimi sio mwanaye wewe siku ulipokuwa unamwambia pale sebleni kama sisi.Yeye kaenda kuyang’aza kwa lile jijambazi ndio maana likatumia uwezo wake wa kijeshi kufanya mambo ya ajabu kama haya”
“kumbee hapa ndio ninaanza kupata picha kwa maana siku ambayo waliniteka hospitali baba yako akawa analalamika kuwa nimemdhalilisha na lazima na mimi anidhalilishe”

“ndio hivyo mama je ile siku walikupeleka wapi?”
“walinipeleka sehemu moja hivi wala sikujua ni wapi ila nikaja kukutana na binti mmoja aliniambia anaitwa nani vileee…..”
“nani…..?”
“jina lake limenitoka mara moja alisema na yeye anatokea tanzania na anakufahamua sana wewe na mumeshirikiana sana kwenye mambo mengi”
“sheila”

“eheee huyo huyo….Yule binti alinisaidia sana kipindi nipo matesoni kweni baba yako alinipeleka kwenye jijumba chakavu msituni huko wakanifungia…cha kushukuru mungu yule binti alikuwa akiniletea chakula kila siku usiku kwani wao walikuwa wakinipa vyakula vibaya?”
“kina nani?”
“si hilo jibaba lako na watu wake”
“ahaaa ila sio baba yangu”

“basi siku kama mbili zilipita sikumuona sheila sasa sikujua ni wapi walimpeleka binti wa watu sijui walimuua au”
“hawakumuua….Nilikutana naye hapa kipindi cha katikati akiwa amelishwa makaa ya mawe hawezi kuzungumza”
“weeee ndio maana baba yako akaamua kunipeleka kwenye lile jipango na kuniambia kuwa nitalisha keki za moto”
“ndio”

“basi nakumbuka kipindi ninaingizwa mule sikubahatika kulishwa hayo makaa na walinipiga na kuninyanyasa sana hadi ikafikia kipindi wakanitenga na wezanu na kunifungia kwenye kile kijichumba”

“unajua siku ya mwisho unapigwa mimi ndio niliye kusadia kuuziba mwili wako ili nipigwe mimi badala yako”
Mama akabaki akiwa mdomo wazi na taratibu chozi likamtoka na akanivuta na kunikumbatia kwa uchungu na machozi yakaendelea kumtoka hadi akalowanisha bega langu alilo pitishia bega

Niambembeleza mama hadi akanyamaza na akaniaga na kuingia chumbani kwake kulala na mimi nikabaki nikitazama tv na nikapitiwa na usingizi kwenye sofa nililo kaa.Asubuhi kama ilivyo kawaida daktari maalumu anayetuhudumia akaja kututembelea na kutupa maelezo ya nini tuweze kufanya ili afya zetu ziweze kuhimarika.Nikwasiliana na jamaa walio tuokoa kili waje kutuchukua na watupeleke nyumbani kwa baba.

Baada ya nusu saa jamaa wakawa wamefika na sisi tukawa tayari kwa safri,njia nzima ndani ya gari mama akawa amenishika mkono huku akiwa na futaha sana.Tukafika kwenye jumba la baba na nikamuona mama akitazama tazama kila sehemu
“mama mbona unashangaa?”
“hili jumba lote ni la kwake?”
“ndio”
“amejitahidi”

Je umedhoofika mwili na kukonda? Unahitaji kunenepa na kurejesha afya ya mwili wako?....BOFYA Hapa

$
0
0
Je umedhoofika mwili   na  kukonda? Unahitaji  kunenepa  na  kurejesha  afya  ya mwili wako?

Kama  jibu  lako  ni  NDIO  basi  hii  ni  HABARI   NJEMA  SANA  KWAKO.

Neema Herbalist  ni  wauzaji  wa  dawa mbalimbali  za  asili.

Tunapenda  kukufahamisha  kuwa, tunayo  dawa  nzuri  ya asili  itakayo  saidia  kuufanya  mwili  wako KUNENEPA  na  KUONGEZEKA  ndani  ya  SIKU  THELATHINI.

Tunapatikana  UBUNGO  jijini  DAR  ES  SALAAM, jirani  na  SHULE  YA  MSINGI  UBUNGO  NATIONAL  HOUSING  nyuma  ya  jengo  la  UBUNGO  PLAZA.

Kwa mkaazi  wa   jijini  DAR  ES  SALAAM, usiye na  nafasi  ya  kufika  ofisini  kwetu, utaletewa  dawa  mahali  ulipo  ( HOME & OFFICE  DELIVERY )

Kwa  wateja  waliopo  mikoani, watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  usafiri  wa  mabasi.

Kwa  wateja  waliopo  Zanzibar  watatumiwa  dawa kwa  njia  ya  usafiri  wa  boti.

Kwa  wateja  waliopo  Mombasa  watasafirishiwa  dawa  kupitia  bus  la  TAHMEED.

Kwa  wateja  wa   Nairobi watasafirishiwa  dawa  kupitia  bus  la  DAR EXPRESS.

Kwa  wateja  waliopo  UGHAIBUNI  watatumiwa  dawa  kwa  njia  ya  POSTA  au  DHL.

WASILIANA  NASI  KWA  SIMU  0766  53  83  84.

Na  kwa  taarifa  zaidi  kuhusu  huduma  zetu, tutembelee  kila  siku  kupitia  tovuti  yetu :

TACAIDS yawataka wadau wa Mapambano dhidi ya Ukimwi kufuata Sheria za nchi na kuepuka kuwa wanaharakati.

$
0
0
 Na. Aron Msigwa –  Maelezo
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imeyataka mashirika, wadau na taasisi zilizo katika mapambano dhidi Ukimwi kuzingatia malengo ya awali ya kuanzishwa kwa taasisi hizo  na kuepuka kujiingiza katika shughuli za uanaharakati ambazo ni kinyume cha sheria.

Akizungumza katika kikao chake cha kwanza na wadau mbalimbali walio katika mapambano dhidi ya Ukimwi leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS Dkt. Leonard Maboko amesema kuwa baadhi ya wadau, mashirika na taasisi zimekuwa zikifanya shughuli nje ya malengo ya awali ya kuanzishwa hali inayosababisha mgongano katika jamii.

"Zipo baadhi ya taasisi zinazofanya shughuli nje ya malengo, tunatambua Serikali haijakataa jitihada za makundi mbalimbali ya kupambana na UKIMWI, sisi kama TACAIDS tutaendelea kuungana na Serikali kuhakikisha kuwa zile taasisi zilizo kwenye mapambano zinasimamia malengo ya kuanzishwa kwake na si vinginevyo"  Amesisitiza Dkt. Maboko.

Amewataka wadau na mashirika hayo kuendelea kujikita na kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ,uhamasishaji wa wananchi kupima kwa hiari VVU kwa lengo la kujua hali zao  ili waweze kujikinga na maambukizi  mapya ya  ugonjwa huo.

Pia amewata wadau hao kuangalia namna bora ya kuwafikia, kuwaelimisha na kuwafuatilia wananchi walio katika makundi maalum kwenye mazingira hatarishi pia kuongeza shughuli za utafiti zitakazoisaidia nchi kufikia lengo la maabukizi sifuri.

Amesema hali ya uelewa wa wananchi juu ugonjwa wa Ukimwi imefikia asilimia 90 kwa kuwa watanzania sasa wanauelewa kuhusu ugonjwa huo na hali zao . Aidha, wengi wana uelewa iwapo wamepata maambukizi au la kutokana na kuongezeka kwa kampeni za uhamasishaji na elimu ya kujikinga na maambukizi.

Kwa upende wake Mkurugenzi wa Chama cha Uzazi na Malezi Bora Tanzania (UMATI), Lulu Ng’wanakilala amesema Taasisi zinazosajiliwa kutoa huduma za kuzuia na kupunguza maambukizi dhidi ya Ukimwi nchini Tanzania na kuanza kujiingiza kwenye shughuli za uanaharakati zinakwamisha na kupunguza juhudi za Serikali na wadau wengine wenye mapenzi mema walio kwenye mapambano dhidi ya Ukimwi.

‘Sisi kama wadau wa hizi taasisi tunaongea lugha moja, NGOs zinazosajiliwa kutoa huduma na kuanza kufanya uanaharakati kupitia masuala ya Ukimwi zinakwenda kinyume cha malengo, sisi tupo kwa lengo moja kuhakikisha maambukizi yanafikia sifuri kuhakikisha wote wanaotakiwa kupata huduma wanafikiwa na huduma zetu hasa makundi yanayochangia kwa kiasi kikubwa maambukizi ya Ukimwi’ Amesisitiza.

Naye Afisa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi Tanzania (NACOFA) Bw. Deogratius Peter, akizungumzia hatua ya baadhi ya taasisi kuenenda kinyume na malengo ya kuanzishwa kwake amesema

‘Serikali imeshatoa Sera na miongozo mbalimbali inayosimamia shughuli za utoaji wa huduma za mapambano dhidhi ya Ukimwi kwa taasisi, makundi na wadau mbalimbali,  Sisi pamoja na Serikali tunakubali na kuheshimu juhudi za makundi haya katika mapambano dhidi ya Ukimwi, suala la uanaharakati halikubaliki maadili lazima yazingatiwe katika utoaji wa huduma zetu tufuate sheria za nchi ile kuepusha migongano isiyo ya lazima’ Amesisitiza.

Ameongeza kuwa taasisi zote zilizo katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi lazima zikajikite katifa tafiti pia kuyafuatilia makundi yote yaliyo katika mazingira hatarishi ambayo yanachangia  kwa kiwango kikubwa kueneza maambukizi ya VVU.

Serikali Imejipanga Kudhibiti Ongezeko la Deni la Taifa.

$
0
0


Na Eleuteri Mangi- Maelezo
Serikali imewahakikishia Watanzania kuwa inaendelea na mikakati ya makusudi katika kudhibiti ongezeko la deni la taifa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji alipokuwa akijibu swali la Saed Kubenea Mbunge wa Ubungo lililouulizwa kwa niaba yake na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai Freeman Mbowe lililohusu deni la taifa.

Naibu Waziri huyo aliitaja mikakati inayosaidia kupunguza deni la taifa ambayo ni pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuendelea kutafuta misaada na mikopo nafuu na kukopa mikopo michache ya kibiashara ya miradi yenye kuchochea kwa haraka ukuaji wa pato la taifa.
 
Mikakati mingine ni kudhibiti ulimbikizaji wa madai ya kimkataba kwa wakandarasi na watoa huduma na kudhibiti madeni yatokanayo na dhamana za Serikali kwenye mashirika ya umma kwa kufanya ufuatiliaji wa karibu wa mikataba inayoweza kusababisha mzigo wa madeni kwa Serikali.

Naibu Waziri Dkt. Ashatu alisema hadi kufikia Juni 2016 deni la taifa lilikuwa dola za kimarekani bilioni 23.2 ikilinganishwa na dola bilioni 19.69 kwa mwezi Juni 2015 ikiwa ni sawa na ongezeko la asilimia 18.

Dkt. Ashatu alifafanua kuwa kati ya kiasi hicho, deni la Serikali ni dola za Kimarekani bilioni 20.5 na deni la sekta binafsi ni dola za Kimarekani   bilioni 2.7 na kuongeza kuwa deni la Serikali linatokana na mikopo ya ndani na nje kwa ajili ya kugharimia miradi ya maendeleo.

Baadhi ya miradi ya maendeleo iliyoainishwa ambayo imetumia fedha za maendeleo ni pamoja na ujenzi wa barabara na madaraja, mradi ya kimakakati wa kuboresha majiji, ujenzi wa njia ya umeme wa msongo wa kv 400 kutoka Iringa hadi Shinyanga na mabasi yaendayo haraka.

Miradi mingine ni ujenzi wa bomba la gesi na mitambo ya kusafisha gesi, upanuzi wa uwanja wa ndege wa Dar es salaam na mradi wa maji wa Ruvu Juu na Ruvu Chini.

Aidha, Dkt. Ashatu amesema kuwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011, Serikali ilipokea mikopo yenye masharti nafuu na ya biashara kiasi cha sh trilioni 1.3 na mwaka 2014/2015 Serikali ilipokea mikopo ya kiasi cha Sh. trilioni 2.3 mikopo ambayo haikufikia trilioni 15 kwa mwaka 2011 na trilioni 9 kabla ya mwaka 2015.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi alipokuwa akichangia hoja hiyo amewatoa hofu Watanzania na kusema kuwa haitatokea hata siku moja wagongewe milango kwa kudaiwa deni la taifa na kuongeza kuwa deni la taifa linapimwa kutokana na ukusanyaji wa mapato hatua ambayo Serikali inaendelea kuitekeleza kwa vitendo.

Waziri Mwigulu aliongeza kuwa Serikali haikopi kwa ajili ya miradi ya kawaida isipokuwa inakopa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa lengo la kuwahudumia wananchi.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images