Quantcast
Channel: MPEKUZI
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live

UVCCM Waitisha Maandamano Nchi Nzima Agosti 31

$
0
0

Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wanatarajia kufanya maandamano ya Amani nchi nzima Agosti 31 kwa ajili ya kueleza utendaji kazi wa Rais Dk.John Pombe Magufuli kwa Watanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Shaka Hamdu Shaka amesema kuwa wameshamwandikia barua mkuu wa jeshi la Polisi kwa ajili ya kupata ulinzi siku hiyo

Amesema kuwa wasipopata ulinzi watafanya kwa kujilinda wenyewe ikiwa ni lengo la kufikisha ujumbe kwa wananchi juu ya utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli.

Shaka amesema kuwa Rais Dk.John Pombe Magufuli amefanya watendaji kuwa na utii pamoja na maadili katika utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aidha amesema kuwa katika maandamano hayo wanaawalika na vijana wa vyama vingine kushiriki kwa lengo moja tuu,la kuunga mkono utendaji wa Rais Dkt.John Pombe Magufuli.


Jeshi la Polisi Lamkamata Kijana akiuza fulana za UKUTA.......Latoa Onyo Kali Kwa Waliojipanga Kuandamana Septemba 1

$
0
0

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema limejiandaa kudhibiti maandamano ya Umoja wa Kupambana na Udikteta Tanzania (Ukuta) yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) yanayotarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amewatoa hofu wakazi wa mkoa huo kuwa hakuna mtu na au kikundi chochote cha watu kitakachofanya maandamano siku hiyo.

“Habari ya Ukuta haipo,umeshabomoka na kama haujabomoka utabomoka, wakazi wa Dar es Salaam msiwe na hofu, fanyeni kazi na hata siku hiyo hakuna mtu atakayejitokeza barabarani kuandamana,” amesema.

Kamanda Sirro amedai kuwa siasa zinatakiwa kufanywa kwa amani na utulivu na kwamba wanasiasa wanaoitumia siasa kufanya vurugu hawatafanikiwa.

“Mimi niwahakikishie kwamba tunajiandaa kwelikweli kuhakikisha watu wanafuata sheria , anayetaka kuvunja sheria kwa kufanya maandamano aanze yeye ili nasi tuanze naye,” amesema.

Ameongeza kuwa ” Suala la utii wa sheria ni la msingi,kama kuna watu au kikundi cha watu kinataka kuitumia siasa kufanya uvunjifu wa amani wajue kwamba nafasi hiyo kwa Dar es Salaam haipo.”

Aidha,Kamanda Sirro amesema August 20 2016 Jeshi la Polisi lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya Kinondoni kuna duka linauza flana zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ , ‘UKUTA’ ‘
 
Amesema  Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa aitwaye YORAM SETHY MBYELLAH miaka 42, mfanyabiashara na mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake


Picha: Jeshi la polisi mkoa wa Singida likifanya majaribio ya silaha

$
0
0
Baadhi ya askari polisi mkoani Singida, wametembeza silaha zao kwenye mitaa mbalimbali Singida mjini, kwa ajili ya kuwaonyesha wananchi silaha zilizonunuliwa kwa kodi zao. 

Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SSP Mayalla Towo, alisema zoezi hilo ni la kawaida na halina uhusiano na jambo lolote.(Picha na Nathaniel Limu).
Baadhi ya askari polisi mkoa wa Singida wakiwa kwenye paredi muda mfupi kabla hawajaanza kuonyesha silaha zao kwa wakazi wa mji wa Singida.

Taarifa Ya Awali Ya Chama Cha CUF Juu Ya Vurugu Zilizotokea Jana Wakati wa Mkutano wa Kumchagua Mwenyekiti Mpya wa Chama Hicho

$
0
0

Jana tarehe 21/8/2016 chama cha wananchi cuf kilifanya mkutano mkuu maalumu wa taifa katika ukumbi wa hotel ya blue pearl –ubungo plaza, dar es salaam.

Chama cha cuf kinapenda kutoa taarifa rasmi za awali juu ya kilichotokea. Baraza kuu la uongozi la taifa la chama cha cuf liliitisha mkutano mkuu huo kwa madhumuni ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi wazi ikiwemo ya mwenyekiti wa chama taifa kutokana na aliyekuwa mwenyekiti wa chama taifa prof. Ibrahimu lipumba kujiuzulu katika nafasi hiyo tarehe 5/8/2016.

Mkutano mkuu maalum wa taifa ulitimiza akidi ya wajumbe halali waliopaswa kuhudhuria katika mkutano huo. Kwa mujibu wa katiba ya chama (1992) ibara ya 79(3) toleo la mwaka 2014 wajumbe wa mkutano mkuu walimchagua mheshimiwa julius mtatiro kuwa mwenyekiti wa kuongoza kikao hicho cha mkutano mkuu kutokana na nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chama taifa kuwa wazi .

Wajumbe wa mkutano mkuu walizikubali na kuzithibitisha ajenda mbili za mkutano huo zilizoandaliwa na kuwasilishwa na baraza kuu la uongozi taifa ambazo ni;
Ajenda ya kwanza kupokea taarifa ya barua ya kujiuzulu kwa prof. Ibrahim lipumba, na ajenda ya pili ni kujaza nafasi wazi ya mwenyekiti wa chama taifa, makamu mwenyekiti taifa na wajumbe wanne wa baraza kuu la uongozi taifa.

Baada ya kuwasilishwa ajenda ya kwanza na wajumbe kupata nafasi za kuijadili ajenda hiyo kwa uwazi na kina, huku kukiwa na mitazamo tofauti, ghafla aliyekuwa mwenyekiti wa chama taifa prof. Ibrahimu lipumba alilazimisha kwa nguvu kuingia ndani ya ukumbi akifuatana watu ambao si wajumbe wa mkutano mkuu huo na kuanzisha vurugu ndani ya ukumbi wa mkutano. 

Viongozi wa chama na mwenyekiti wa mkutano huo waliweza kuwatuliza wajumbe na kuendelea na kikao.

Kuhusu hitimisho la mjadala wa ajenda ya kwanza juu ya taarifa ya barua ya kujiuzulu kwa Prof. Ibrahim Lipumba.
Kwa mujibu wa katiba ya chama (1992) ibara ya 117 (2) baada ya mjadala wajumbe walikubaliana kufanya maamuzi juu ya kukubali na au kukataa kujiuzulu kwa prof. Ibrahimu lipumba. 

Wajumbe wa mkutano mkuu walipiga kura na matokeo ni kuwa wajumbe walioafiki maamuzi ya kujiuzuru kwa prof. Ibrahimu lipumba walikuwa wajumbe 476 na waliokataa kujiuzulu kwake walikuwa wajumbe 14 na wajumbe wengine hawakupiga kura ya kukubali au kukataa.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa na wajumbe kurejea katika ukumbi kuendelea na ajenda ya pili, huku mheshimiwa prof. Ibrahimu lipumba wakati wote akiwa ndani ya ukumbi akishuhudia maamuzi hayo ya wajumbe, wajumbe wachache waliokuwa wakikataa kujiuzulu kwa prof ibrahimu lipumba wakishirikiana na wale alioingia nao walianzisha vurugu za kutotaka kuendelea kwa ajenda ya pili ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizowazi.

Kutokana na hali hiyo ya kufanya vurugu ndani ya mkutano mkuu, viongozi wa chama taifa walishauriana na kuona kuwa busara ni kuahirisha zoezi hilo la kujaza nafasi, na mwenyekiti wa kikao cha mkutano mkuu maalumu wa taifa mheshimiwa julius mtatiro alifunga mkutano huo mpaka hapo wajumbe watakapoarifiwa tena.

Baraza kuu la uongozi taifa lilifanya mchujo wa wagombea tisa waliojaza fomu na kupitisha majina matatu ya wagombea wa nafasi hiyo ya mwenyekiti wa chama taifa ambao ni mheshimiwa twaha taslima, riziki shaali mngwali na juma mkumbi.

Kwa nafasi ya makamu mwenyekiti waliopitishwa kugombea ni mheshimiwa salim biman na mheshimiwa mussa haji kombo.

Msimamo wa chama juu ya kadhia
Chama cha wananchi-cuf kinapenda kuwataarifu na kuwahakikishia wanachama, wapenzi wa chama chetu na marafiki zetu wote kuwa cuf ni taasisi kubwa ya kisiasa nchini iliyo na viongozi makini na mahiri. 

Tunawaomba wajumbe wote wa mkutano mkuu wa taifa na wanachama wetu wote na watanzania kwa ujumla kuwa watulivu katika kipindi hichi, na kuzipuuza taarifa zote zenye lengo la kupotosha usahihi wa suala hili.

Mchakato wa kukamilisha zoezi la kujaza nafasi wazi za uongozi wa chama taifa upo palepale na baada ya kukamilisha taratibu za ndani ya chama tutatoa taarifa kwenu na kwa watanzania wote.

Ni muhimu kukumbukwa kwamba ajenda ya kwanza ya msingi katika mkutano mkuu huu imekamilika kwa wajumbe wengi wa mkutano mkuu wa chama taifa kukubali kujiuzulu kwa mheshimiwa prof. Ibrahimu lipumba.

HAKI SAWA KWA WOTE
SALIM BIMAN
MKURUGENZI WA HABARI, UENEZI NA MAWASILIANO KWA UMMA.

Rais Magufuli apokea taarifa ya maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha kusindika gesi asilia (LNG) Ambacho Kitagharimu trilion 65 za kitanzania

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 22 Agosti, 2016 amepokea taarifa ya maendeleo ya mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kusindika gesi asili (LNG Plant) kinachotarajiwa kujengwa katika eneo la Likon'go, Mchinga Mkoani Lindi.

Mwakilishi Mkazi wa Kampuni ya Statoil ya Nchini Norway ambayo ni moja ya Kampuni zitakazowekeza katika mradi huo Bw. Oystein Michelsen amemueleza Rais Magufuli kuwa ujenzi wa kiwanda hicho unatarajiwa kugharimu Dola za Kimarekani Bilioni 30 sawa na zaidi ya Shilingi Trilion 65 za Kitanzania na kwamba uzalishaji unatarajiwa kuchukua muda wa zaidi ya miaka 40 baada ya kuanza.

Bw. Oystein Michelsen amebainisha kuwa Serikali ya Norway ina dhamira ya dhati ya kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa manufaa ya pande zote na ameomba Serikali ya Tanzania iendelee kutoa ushirikiano ili kufanikisha ujenzi wa kiwanda hicho.

Kwa upande wake Rais Magufuli amemuhakikishia Mwakilishi huyo wa kampuni ya Statoil kuwa Serikali ya Tanzania ipo tayari kuhakikisha mradi unafanikiwa na ameitaka Wizara ya Nishati na Madini kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC) kushirikiana na wadau kutoka Wizara nyingine kuharakisha mchakato wa kuanza kwa ujenzi wa kiwanda hicho.

"Nataka kuona mradi huu unaanza kujengwa, tunachukua muda mrefu mno, kamilisheni mambo yaliyobaki ili wawekezaji waanze kazi mara moja" Amesema Rais Magufuli.

Dkt. Magufuli amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha ajira kwa idadi kubwa ya watanzania na utaiwezesha serikali kupata mapato kupitia tozo mbalimbali, na hivyo kutumika kuimaisha huduma za kijamii zikiwemo elimu, afya, maji na miundombinu.

Pamoja na Statoil kampuni nyingine zinazoshiriki katika uwekezaji wa mradi huu ni Shell, Exxon Mobil, Pavillion na Ophir.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
22 Agosti, 2016

Lowassa Apigilia Msumari Oparesheni UKUTA......Asema Haiwezekani Mtu Mmoja Azuie Kila Kitu

$
0
0
Leo nimezunguka katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma nikiwaeleza kuhusu Operation UKUTA,

UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki ya kidemokrasia na katiba ya nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya tano .

CHADEMA ni nani wakapambane na polisi ,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani . 

Najua polisi watapiga watu ,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie wao na walio na mamlaka wataishia katika mahakama ya Kimataifa .

Siasa ni mazungumzo ,lazima tuzungumze milango yetu iko wazi kufanya mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi hatutorudi nyuma September Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko ngazi ya kaya na wajumbe wetu wanakamilisha kazi katika kaya ili tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe kwa maandamano na mikutano kama tulivyokubaliana katika kata zetu na majimbo nchi nzima .

Haiwezekani hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote na inaongozwa na Katiba na sheria.

Kamati kuu ilipoamua katika suala la UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi wa kada mbalimbali ,wazee wenye busara na vijana machachari kamwe hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki ya watanzania wote.

Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020 ndugu zangu na wanachama wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020 kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia
Kwanza; Umoja ndani ya Chama na wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu
"chama ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma "- LOWASSA

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumanne ya Agosti 23

Namba za Simu za Utoaji Wa Malalamiko Na Kero Juu Ya Huduma Za Afya Nchini Pamoja Na Masuala Ya Jinsia, Wazee Na Watoto

$
0
0
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inayo dhamana ya kusimamia na kuratibu Mipango, Sera, Sheria na Mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha utoaji wa huduma za afya nchini pamoja na kujenga jamii ya watanzania inayojali na kuheshimu Usawa wa Jinsia, Haki za Wazee na Watoto.

Katika utekelezaji huu, yapo mafanikio kadhaa yaliyopatikana lakini pia zipo changamoto mbalimbali zinazojitokeza katika utoaji wa huduma za afya hapa nchini. Baadhi ya changomoto hizo ni za kiutendaji zaidi ambazo zinaweza kutatuliwa kwa haraka endapo tutaimarisha usimamizi na uwajibikaji katika kila ngazi kuanzia ngazi ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Vituo vya kutolea huduma za afya. Changamoto hizi ni pamoja na wagonjwa kutopatiwa huduma haraka na sahihi, lugha na kauli mbaya kutoka kwa watoa huduma na makundi yanayotakiwa kupata matibabu bure (yaani Wazee, Wajawazito na Watoto wa umri wa chini ya miaka 5) kutozwa fedha kinyume na Sera ya Afya ya 2007)

Takribani kila siku vyombo vya habari vimekuwa vikiripoti matukio kadhaa kuhusu malalamiko na kero mbalimbali wanazokumbana nazo wananchi katika kupata huduma za afya.

Wasimamizi wa Wakuu wa Utekelezaji wa Sera na Miongozo ya Afya katika ngazi ya Mikoa ni Waganga Wakuu wa Mikoa. Ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya pamoja na kuhakikisha malalamiko na kero zao zinashughuhulikiwa kwa haraka, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Ummy Mwalimu (Mb) ameamua kuweka wazi namba za simu za Waganga Wakuu wa Mikoa (RMO) wote nchini ili wananchi wanapokuwa na malalamiko/kero waweze kuwasiliana nao moja kwa moja. 


Mhe Waziri amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa kuyafanyia kazi masuala yote yanayoletwa na wananchi katika Mikoa yao na kuyapatia ufumbuzi haraka. Hivyo, wananchi wasisite kuwasiliana nao kupitia namba zao zifuatazo pamoja na kwa barua pepe.

Katika muktadha mzima wa kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Sheria na Sera za Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, mwananchi yoyote ambae ana malalamiko, maoni au ushauri kuhusu sekta husika unaweza kuwasiliana moja kwa moja na Mheshimiwa Waziri, Ummy Mwalimu (Mb) kupitia simu namba 0746 – 505030 (kwa njia ya ujumbe) pamoja na kueleza mkoa uliopo, twitter @wamjw na email: waziri@moh.go.tz

  
“Uwazi na Uwajibikaji ni chachu ya kuleta mabadiliko katika sekta ya afya, sambamba na kulinda Haki za Watoto, Wazee na Wanawake”.

MAWASILIANO NA WAGANGA WAKUU WA MIKOA (RMOs)

IMETOLEWA TAREHE 22/08/2016

Wezi fedha za TASAF kikaangoni

$
0
0
SERIKALI imetoa siku 30 kukamatwa kwa watumishi waliosababisha matumizi mabaya ya fedha za Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) III, kwa kuingiza majina ya watu masikini wasiostahili ili kujipatia fedha za mradi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene akizungumza na baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi, jana alisema ni lazima watumishi wa umma waliohusika katika kuisababishia hasara Serikali wawajibishwe.

Februari mwaka huu, TASAF ilitekeleza maagizo ya Serikali na kufanya uhakiki wa kaya masikini ziliopo kwenye mpango wa kupata fedha na kuziondoa zile zilizokosa sifa na kuziondoa kaya 32,456.

“Katika msako huo tulibaini, waliokufa ni 7,819, viongozi waliojipachika 2,999, waliohama sehemu ambapo mpango haujaanza 3,948, wasiojitokeza au wasiofahamika 9,342 na wasiokuwa na sifa 8, 348,” alisema Simbachawene.

Aidha alisema kuwa, zoezi hilo ni endelevu na kwamba utaratibu wa kutoa taarifa za walengwa waliofariki au kuhama unapaswa kufanyika ili fedha za serikali zisitumike ovyo nje ya malengo yaliyokusudiwa.

Simbachawene alisema, kuingizwa kaya zisizo na sifa katika mpango huo na kuachwa kwa kaya ambazo ni maskini zaidi, kumetokana na baadhi ya watumishi wasio waadilifu ambao pia wamekuwa wakipunguza malipo ya walengwa.

Watu 6.5 milioni, katika kaya maskini na zinazoishi katika mazingira hatarishi wanatarajiwa kunufaika na mradi wa fedha za TASAF katika awamu ya sasa.

Hata hivyo, Simbachawene aliwashauri wakurugenzi wa halmashauri zote nchini pamoja na wakuu wa wilaya, kutoogopa kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo kwani suala hilo litaepusha hasara na mianya ya wizi.

Mhandisi Evarist Ndikilo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, alimuahidi waziri Simbacahwene kuwa, hawatofumbia macho ubadhirifu katika halmashauri na kusema watazishauri, kuzikumbusha na hata kuingilia kati pale mambo yanapoenda ndivyo sivyo katika halmashauri.

Polisi Wamzuia Lowassa Kuingia Rukwa

$
0
0

Msafara wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa umekwama kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi  baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea mikoa hiyo.

Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake  mkoani Mbeya tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake  mkoani  Songwe wakati leo asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.

Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya  Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.

Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, Frank Mwaisumbe  alisema  kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa 1.00 jioni akiwa Tunduma  wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.

Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa  kwa njia ya simu alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara kwa sababu  mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.

Taarifa Kwa Umma Kuhusu Hali Ya Mbunge Joseph Michael Baada Ya Kupata Ajali

Rais Magufuli Apokea Hati Za Utambulisho Kutoka Kwa Mabalozi Wa Nchi Mbalimbali Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 23 Agosti, 2016 amepokea hati za utambulisho kutoka Mabalozi wanne wanaowakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi hao ni Mhe. Roberto Mengoni - Balozi wa Italia hapa nchini, Mhe. Kim Yong Su - Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Korea hapa nchini, Mhe. Mohamed Hassan Abdi - Balozi wa Jamhuri ya Somalia hapa nchini na Mhe. Paul Sherlock - Balozi wa Ireland hapa nchini.

Akizungumza kwa nyakati tofauti baada ya kupokea hati za utambulizo za Mabalozi hao Rais Magufuli amewapongeza Mabalozi hao kwa kuteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini na amewahakikishia kuwa Serikali yake itawapa ushirikiano wa kutosha ili kuendeleza na kuuimarisha zaidi uhusiano ulipo kati ya nchi hizo na Tanzania.

Dkt. Magufuli amewaambia Mabalozi hao kuwa katika kipindi cha kuanzia Mwaka 2016/2017 hadi 2020/2012 Tanzania imedhamiria kutekeleza mpango wa ujenzi wa viwanda, hivyo amezialika nchi zao na sekta binafsi katika nchi hizo kuungana na Tanzania katika uwekezaji kwenye sekta ya viwanda na biashara.

"Naomba kukuhakikishia kuwa Wafanyabiashara watakaokuja kuwekeza ama kufanya biashara, mitaji yao itakuwa salama na Serikali yangu itatoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha uwekezaji huo unafanikiwa na unanufaisha pande zote mbili" Amesisitiza Rais Magufuli alipokuwa akizungumza na Balozi wa Ireland Mhe. Paul Sherlock.

Aidha, Rais Magufuli amewashukuru Marais wa nchi zote nne ambazo Mabalozi wake wamewasilisha hati za utambulisho kwake hii leo na amewahakikishia kuwa uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na nchi hizo utadumishwa na kuimarishwa zaidi kwa manufaa ya wananchi wa pande zote.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
23 Agosti, 2016

Taarifa kutoka ubalozi wa Marekani nchini Tanzania kuhusu operesheni UKUTA

$
0
0
Ubalozi wa Marekani kwa Tanzania umewatahadharisha raia wa Marekani waishio nchini kuhusiana na Operesheni UKUTA iliyopangwa kufanyika septemba.

Taarifa kutoka ofisi za ubalozi huo zinaeleza kuwa kuna hofu ya maandamano hayo kudumu hata baada ya september mosi hivyo kuwataka raia wake kuwa makini na usalama wao.

Ubalozi umeeleza kuwa raia wa Marekani hawajawai kuwa wahanga wa maandamano yaliyopita ila umewataka raia wake kuwa makini juu ya usalama pamoja na kufuatilia vyombo vya habari vya ndani ili kujua kinachoendelea.

Ubalozi huo umesema ingawa maandamano yamedhamiriwa kuwa ya amani, kuna uwezekano wa kutotokea makabiliano yatakayoweza kusababisha machafuko hivyo kuwataka raia wake kuepuka maeneo yatakayokuwa na maandamano. 


**************
Security Message: Nationwide Protests Scheduled for September 1, 2016

The U.S. Embassy in Dar es Salaam alerts U.S. citizens that opposition political leaders have called for a nationwide day of protest currently scheduled for September 1, 2016, but may continue for more than one day.

While U.S. citizens have not been specifically targeted in past demonstrations, we urge you to exercise caution and stay current with media coverage of local events.

Even demonstrations intended to be peaceful can turn confrontational and escalate into violence.  Avoid areas where demonstrations are taking place and exercise caution when in the vicinity of any large gatherings, protests, or demonstrations.

For further information:
  • Contact the U.S. Embassy in Tanzania, located at 646 Old Bagamoyo Rd, Msasani, Dar es Salaam, at+255-22-229-4000 or e-mail at drsacs@state.gov, and is open Monday-Thursday, 7:30 a.m.-5:00 p.m and Friday 7:30 – 11:30 a.m. For after-hours emergencies, U.S. citizens should call +255-22-229-4000 and ask to speak with the duty officer.
  • Call 1-888-407-4747 toll-free in the United States and Canada or 1-202-501-4444 from other countries from 8:00 a.m. to 8:00 p.m. Eastern Standard Time, Monday through Friday (except U.S. federal holidays).
Follow us on Twitter and Facebook.

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumatano ya Agosti 24

Majambazi Yaua Polisi 4 Mbande Dar es Salaam usiku wa Kuamkia Leo

$
0
0
Jeshi la Polisi limethibitisha kuwa jumla ya askari wake wanne wameuawa usiku wa kuamkia leo baada ya majambazi kuvamia tawi la benki ya CRDB lililopo Mbande, wilayani Temeke, Dar es Salaam.

Akizungumza moja kwa moja kupitia kituo cha Redio One Stereo leo asubuhi, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro, amesema watu kadhaa wamekamatawa na msako unaendelea ili kuwapata waliotekeleza unyama huo.

Sirro amesema taarifa kutoka eneo la tukio zinaonesha kuwa majambazi hao walikuwa 14 na baada ya kufanya mauaji hao, walivamia kituo cha polisi cha Mbande kisha wakavunja stoo na kuchukua sare ya askari na silaha.


Akielezea namna tukio hilo lilivyotokea, Kamanda Sirro amesema wahalifu hao walitumia mwanya wakati askari wakibadilishana lindo katika taasisi hiyo ya fedha na kuibuka ghafla na kuanza kurusha risasi.

Kwa mujibu wa Sirro, gari la polisi limechakazwa kwa risasi na askari mmoja aliyekuwa lindo alifanikiwa kukimbia na ndiye aliyeweza kutoa taarifa na maelezo ya namna tukio lilivyofanyika.

“Watu kadhaa wamekamatwa na tunaendelea na msako. Tunawataka wakiwa hai au wafu,” amesema Kamanda Sirro huku akiwataka watu kujihadhari na yeyote anayejitambulisha kwao kuwa ni askari bila kuonesha kitambulisho.

Ameendelea kusema kuwa baada ya operesheni ya kukomesha mtandao wa wahalifu kama hao na wengine kukimbilia nchi jirani, masalia wameanza kujikusanya na kutekeleza matukio ya mauaji huku askari wakilengwa.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba  akimjulia hali  aliyejeruhiwa
Waziri Nchemba na Kamanda Sirro wakiwa eneo la tukio
Gari ya Polisi ikiwa imezagaa Risasi


Mke wa bilionea Msuya kortini Kwa Mauaji ya Wifi Yake

$
0
0

MKE wa bilionea Erasto Msuya, Miriam Elisaria Msuya (41) amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za mauaji ya dada wa wa bilionea huyo, Aneth Msuya.

Mshtakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana jijini Dar es Salaam na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali, Diana Lukondo mbele ya Hakimu Mkazi, Margareth Bankika.

Akisoma mashtaka hayo, Lukondo alidai mshtakiwa huyo ambaye ni mkazi wa maeneo ya Sakina kwa Iddi, jijini Arusha anadaiwa Mei 25, mwaka huu katika maeneo ya Kibada Kigamboni jijini Dar es Salaam alimuua Aneth Elisaria Msuya.

Mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji, mbapo Jamhuri ilidai upelelezi haujakamilika na kuomba kesi hiyo ipangwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Bankika, alikubali kuahirisha kesi hiyo hadi Septemba 9, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na mshtakiwa alirudishwa rumande.

Habari zilizopatikana baada ya tukio hilo zilidai kwamba, marehemu Aneth aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia Mei 25, mwaka huu Dar es Salaam. 

Mauaji hayo yalitokea nyumbani kwake eneo la Kibada block 16, Kigamboni ambako inaelezwa wauaji hao hawakuchukua kitu chochote ndani ya nyumba yake.

Marehemu Erasto Msuya, aliyekuwa mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite aliuawa kwa kufyatuliwa risasi Julai 7, mwaka 2013 katika eneo la Mijohoroni,  kando ya barabara ya Arusha – Moshi wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, akiwa ameitika wito wa kwenda kununua madini ya Tanzanite baada ya kupigiwa simu na vijana wawili  waliomtaka wakutane maeneo hayo.

Inaelezwa kuwa alifika katika eneo hilo akiwa na gari lake aina ya Range Rover T 800 CKF na kuwakuta vijana hao wakimsubiri, baada ya kuteremka Msuya alielekea kumsalimia mmoja wa vijana hao.

Hata hivyo kabla hajamfikia kijana huyo aliitoa bunduki ya SMG namba KJ 10520 aliyokuwa ameificha kwenye koti na kumfyatulia risasi takribani 22 mwilini.

CHADEMA Wamwalika Kamanda Sirro Katika Maandamano yao ya UKUTA

$
0
0

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Dar es Salaam, kimemkaribisha Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, Kamishna Simon Sirro kujitokeza na kuwa mstari wa mbele kwenye maandamano ya Operesheni Ukuta yatakayofanyika Septemba Mosi.

Kimesema kinamkaribisha kamanda huyo ili kuondoa uwezekano wa kupelekewa taarifa za uongo na askari wake kuhusu maandamano hayo.

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Dar es Salaam, Benard Mwakyembe, alisema jana kuwa hakuna haja ya kamanda huyo kukaa ofisini bali ajitokeze katika Operesheni Ukuta na awe mstari wa mbele kuwapiga wananchi ambao watatumia muda huo kumuuliza maswala ya sheria kuhusu maandamano hayo.

“Lengo la Operesheni Ukuta ni kuwaeleza wananchi kuwa nchi yetu haifuati sheria bali inafuata mawazo ya mtu mmoja.

“Tumwambie tu kwamba Kamanda Sirro ngoma hii ya Ukuta si ya kitoto, vitisho na mbwembwe zake anazozionyesha barabarani hazitutishi, tupo tayari kwa lolote.

“Tumejiandaa kisaikolojia kwa namna yoyote, tupo tayari kufa kwa ajili ya kuwatetea wananchi, na Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita, atakuwa mstari wa mbele pamoja na viongozi wengine,” alisema Mwakyembe.

Aidha alisema maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia 99.5 katika mitaa 582 na kata 102 ya jiji zima la Dar es Salaam.

“Niwashukuru Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) kwa kutuunga mkono kuandaa maandamano yao, tunaamini haya ya kwetu yamewapa motisha na kuamua kufanya ya kwao.

“Ninaliomba Jeshi la Polisi liwape ulinzi wa kutosha ingawaje sisi tunajua kwamba huo ni mtego walioufanya kisiasa ili kuleta mabishano ambayo hayana nafasi kwetu,” alisema.

Alisema haki za vyama vya siasa ni kutoa maoni ya kisiasa  kadiri vitakavyoona inafaa, ili kutekeleza sera zake kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Katiba ya Zanzibar.

Wenye Virusi Vya Ukimwi (VVU) sasa kuwahishiwa ARVs

$
0
0

WATU watakaogundulika kuwa na Virusi Vya Ukimwi (VVU) wataanza kupewa na kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa (ARVs) bila kusubiri kinga zao za mwili kupungua kama ilivyozoeleka.

Wakati utaratibu huo mpya ukitarajiwa kuanza Oktoba mwaka huu, kwa upande wake, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya Ukimwi kupitia kwa Mwenyekiti wake, Constantine Kanyasu, imeshauri serikali kuangalia namna ya kuruhusu dawa ziingizwe na kuuzwa madukani kwa bei nafuu kwa ajili ya watu ambao hawako chini ya mpango wa serikali.

Hayo yalielezwa jana mjini Dodoma kwenye kikao cha kamati hiyo ya Bunge ambayo ilipokea taarifa iliyofikiwa katika utafiti wa upatikanaji wa chanjo ya Ukimwi.

Katibu Mkuu, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Mpoki Ulusubisya aliieleza kamati juu ya mabadiliko katika tiba na kusema mtu yeyote anayepima na kugundulika kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, ataanza kupatiwa ARVs mara moja.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi, Dk Angela Ramadhani, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa (WHO) yaliyotolewa mwaka jana baada ya tafiti kubainisha kuwa zipo faida za kuwahi kupata dawa husika.

Dk Ramadhani alisema maagizo hayo ya WHO yanatokana na tafiti zilizofanyika katika nchi mbalimbali na kubainisha kuwa kutumia ARVs kabla ya kinga ya mwili kushuka, kuna faida kutokana na kuonesha kuwa kunakuwa na usalama zaidi.

Kwa mujibu wa Dk Ramadhani, baada ya mwongozo kutolewa mwaka jana, Aprili mwaka huu, shirika hilo liliita nchi wanachama na kusambaza taarifa hizo kwa ajili ya kuziwezesha kujipanga kiutekelezaji.

“WHO wakishatoa mwongozo, huita wataalamu na kuwaeleza ili nchi zijiendae. Kwa mfano, kama zina uwezo wa kutoa dawa hizo,” alisema Dk Ramadhani na kusema pia hapa nchini, wameanza wiki hii kupitia miongozo ya zamani kabla ya utaratibu huo mpya kuanza Oktoba mwaka huu.

Wakati huo huo, wakati wa kikao na Kamati ya Bunge baada ya wizara kuonesha kuwa uwezo wa serikali wa kutoa dawa hizo unaishia kwa watu milioni 1.3 licha ya kuwa na watu 2.4 wenye VVU, Mwenyekiti wa Kamati, Kanyasu alishauri suala hilo liangaliwe kwa umakini.

“Kama uwezo wa serikali unaishia kwa watu milioni 1.3, ni kwa nini serikali isijikite hawa wanaopata free (bure) halafu hawa private (binafsi) wakaruhusiwa kuingiza dawa zikauzwa kwenye maduka kwa bei nafuu ili mtu akishajiona ana Ukimwi aende akanunue ili kuziba pengo hilo la watu milioni 2.4,”alihoji Kanyasu wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Katika kikao hicho cha kamati na watendaji kutoka wizara, taarifa zilibainishwa kwamba wafadhili wamepunguza na wanaendelea kupunguza bajeti katika masuala ya Ukimwi.

Kuhusu chanjo, ilielezwa na Katibu Mkuu kwamba, shughuli zote zilizopangwa awali kuhusu chanjo zilisitishwa Juni, 2015 baada ya fedha kutoka kwa wafadhili kwisha jambo ambalo serikali imechagizwa kutoa fedha uendelee.

Ilisisitizwa kwamba Tanzania inapaswa ijikite kwenye chanjo ikizingatiwa kwamba haiwezi kutegemea tafiti za mataifa mengine kutokana na wadudu kutofautiana.

Wakati huo huo, kamati ilielezwa changamoto zilizopo kwenye utafiti juu ya suala la Ukimwi kwamba Watanzania wengi wanaogopa kuwekewa vimelea vya kupambana na Ukimwi wakidhani wakipandikiziwa watakuwa wameambukizwa. Katibu Mkuu alisema hali hiyo inasababisha watafiti kupata shida ya kupata watu wa kufanyia utafiti.

Awali, katika taarifa yake kuhusu utafiti wa chanjo ya Ukimwi, Katibu Mkuu alisema wizara yake kupitia Chuo Kikuu cha Afya Muhimbili na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Kituo cha Mbeya zilifanya utafiti mwaka 2014.

Alisema kati ya Februari 2007 na Februari 2008, watu 162 miongoni mwa 177 walifanyiwa uchunguzi na chanjo kuonesha usalama mzuri na hakukuwa na madhara makubwa yanayohusiana moja kwa moja na chanjo.

Aidha, asilimia 100 ya washiriki waliopata chanjo halisi waliweza kutengeneza kinga zinazohusisha seli za kinga ya mwili na protini zilizoko kwenye damu dhidi ya VVU. Kutokana na mafanikio ya awamu ya kwanza, mradi wa awamu ya pili ulifanyika Tanzania na Msumbiji.

Wabunge Wataka Rais Magufuli Atoe Kibali cha Ajira Kwa Walimu Wapya ili Kukabili Uhaba Wa Walimu Uliopo Hivi sasa

$
0
0

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa imeomba Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imuombe Rais atoe kibali cha ajira kwa walimu kukabili uhaba unaoikabili nchi.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza alitoa ushauri huo jana mjini Dodoma kwenye kikao kati ya wajumbe wa kamati hiyo na viongozi na watendaji wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wakiongozwa na Naibu Waziri, Selemani Jafo.

Kikao hicho kilikuwa ni cha kamati kupokea na kujadili taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa mpango wa ofisi hiyo wa utoaji elimu bila malipo katika kipindi cha Januari hadi Juni mwaka huu ambako suala la uhaba wa walimu liliibuliwa na wajumbe.

“Walimu waajiriwe...ni vyema mumuone rais, angalau afungulie kibali cha walimu pekee...wanafunzi wanaongezeka mara mbili, lakini walimu hakuna,” alisema Rweikiza.

Awali, akijibu hoja za wajumbe juu ya changamoto ya uhaba wa walimu, hususan wa Sayansi na Hisabati, Jafo alikiri hali hiyo kuikumba serikali na kusema ndiyo maana walilenga kutoa ajira 35,000 kabla ya rais kusimamisha vibali vya ajira kwa watumishi wote.

Hata hivyo, alisema uamuzi wa Rais ni wa nia njema kuwezesha uhakiki wa watumishi hewa.

Alisema katika kauli ya hivi karibuni ya Rais John Magufuli, alisema wakati wowote kibali kitatolewa.

Jafo alisisitiza kuwa kibali kitakapotolewa, kipaumbele itakuwa ni ajira kwa walimu wa Sayansi ya Hisabati.

Akielezea namna ya kuziba mapengo ya walimu wa masomo hayo, Jafo alisema serikali itafikiria pia watu wengine wanaoweza kufaa katika kufundisha masomo hayo wakiwemo walimu wastaafu na wahitimu wa fani nyingine.

JKT yatoa siku 7 wabunge wachukue madawati yao

$
0
0

JESHI la Kujenga Taifa (JKT), limetoa siku saba kwa wabunge wa majimbo 18 yaliyopo ndani ya mikoa saba nchini kuhakikisha wanachukua madawati yao yaliyotengenezwa na jeshi hilo kabla ya Agosti 30, mwaka huu.

Madawati hayo 9,666 ni kati ya 30,000 ya awamu ya kwanza yaliyotengenezwa na jeshi hilo baada ya Ofisi ya Bunge kulipa zabuni ya kutengeneza madawati 60,000 kwa Sh bilioni tatu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JWTZ), Dk Hussein Mwinyi, alisema jeshi hilo limelikabidhi Bunge madawati 30,000, lakini madawati 9,666 kati ya hayo hayajachuliwa.

Hata hivyo, alisema kulingana na mgawo ambao jeshi hilo lilikabidhiwa na Kamati ya Bunge, madawati hayo yaligawanywa katika majimbo ya mikoa tisa, lakini hadi sasa majimbo 18 katika mikoa saba hayajachukua madawati hayo.

Aliitaja mikoa iliyopo kwenye mgawo huo na idadi ya madawati kwenye mabano kuwa ni Tanga ( 6,444), Njombe (3,222), Iringa (3,790), Mbeya (3,759), Mbeya Songwe (3,222), Rukwa (1,611), Ruvuma (4,833), Unguja (3,200) na Pemba (1,800).

“Mpaka sasa madawati yaliyokwishachukuliwa ni 22,721, madawati 9,666 kati ya 30,000 yaliyokwishakamilika sawa na asilimia 30 hayajachukuliwa na majimbo husika. Tunawaomba wabunge husika waje kuyachukua kabla ya Agosti 30, vinginevyo tutaziomba mamlaka husika ziyagawe kwenye maeneo yenye mahitaji,” alisema.

Dk Mwinyi aliyataja majimbo na mikoa ambayo hadi sasa hayajachukua madawati hayo kuwa ni Tanga katika majimbo ya Kilindi na Pangani (1,611) na Njombe majimbo ya Makambako, Ludewa, Wanging’ombe na Makete (2,148).

Maeneo mengine ni Iringa katika majimbo ya Iringa Mjini, Mbeya Mjini na Mbeya Vijijini (91,611), Ruvuma Jimbo la Tunduru Kaskazini ( 537) na Mbeya katika majimbo ya Ileje, Kyela, Rungwe na Busokelo ( 2,148).

Mengine ni Songwe ( 537) na Kwela, Nkasi Kaskazini na Nkasi Kusini (Rukwa) (1,611). Kwa mujibu wa Dk Mwinyi, kutochukuliwa kwa madawati hayo kunasababisha kukosekana kwa nafasi ya kuweka madawati mengine yanayotengenezwa kwenye vituo mbalimbali vya JKT.

Pia, alisema yanapoendelea kubaki mahali hapo yanapigwa jua, kunyeshwa na kupungua ubora. Pamoja na hayo, alisema kuwa awamu ya pili ya madawati 30,000 inaendelea vyema kwa kuwa tayari madawati 20,000 yamekamilika na yanaweza kuchukuliwa na kugawanywa panapohusika.

Alisema, “madawati 10,000 yaliyobaki yatakamilika kabla ya Oktoba 30,000 kama ilivyopangwa na yatagawanywa katika majimbo 51”.

Aprili 11, mwaka huu, Bunge lilimkabidhi Dk Magufuli Sh bilioni sita ilizoziokoa kwa kubana matumizi katika maeneo mbalimbali kuanzia Julai hadi Desemba mwaka jana, ikiwemo posho, safari za nje na viburudisho, ambazo Rais aliagiza zitumike kununua madawati kwa kila jimbo.
Viewing all 45270 articles
Browse latest View live




Latest Images